Rais Jakaya Kikwete (kulia) akibadilishana mawazo na Balozi wa Vatican, Francisco Montecillo Padilla wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya aliyowaandaliwa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini. Hafla hiyo ilifanyika ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe akizungumza na balozi wa Vatican, Francisco Montecillo Padilla.
Rais Kikwete akizungumza na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini wakati wa hafla ya kuukaribisha mwaka mpya.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao wakati wa hafla aliyowaandalia ya kuukaribisha mwaka mpya.
Rais Kikwete akizungumza na balozi wa China, Lu Youqip (kushoto).