Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

P FUNK MAJANI ASAKA NYOTA WAPYA

$
0
0

NA ELIZABETH JOHN
STUDIO ya Bongo Rekord iliyo chini ya mtayarishaji mkongwe nchini, P Funk Majani natafuta wasanii wapya wenye vipaji ikiwa ni pamoja na wale wanaojijua kama wanabahati.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Majani alisema anatafuta wasanii watano ambao watafanya kazi chini ya label ya Bongo rekodi kwa upade wa wanawake na wanaume.

Alisema, anataka kuchanganya pamoja ili atengeneze kundi ambalo atatangaza nia yake hapo baadae, kwa wasanii wa bongo fleva, hip hop na watayarishaji.

“Hao wote watakuwa kwa label ya bongo rekodi ambayo ilikuwepo zamani ikijengwa na wasanii mbalimbali sasa hivi tumerudi tena kwa lengo la kukuza muziki wetu,” alisema.

Majani alisema kwa yeyote ambaye anataka kuwa chini ya label hiyo anatakiwa kutuma kazi zake kwenye bongo_recordz@yahoo.com ili kumuwezesha yeye kuona kazi za msanii huyo.
Mwisho.
 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>