Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

DULLY SYKES: MIAKA MIWILI SIJAITWA NA PROMOTA

$
0
0

NA ELIZABETH JOHN
MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’ amesema  imepita miaka miwili hajawahi kupigiwa simu na promota yeyote nchini kwaajili ya kufanya shoo.

Akizungumza na mtandao wa Bongo5, jijini Dar es Salaam jana, Dully alisema hiyo imetokana nay eye mwenyewe kutojiweka sokoni na kuamua kufanya kazi za utayarishaji wa muziki huo.

Alisema kuwa, hawezi kufanya shoo kwa bei ambayo yeye haitaki ila shoo yake yeyote anataka aingize zaidi ya milioni kumi.

“Shoo zangu nyingi sifanyi chini ya milioni kumi, hivyo anaenihitaji ajue nataka nini sio kuniita kwa bei za mtaani na kupotezeana muda, kila msanii anamalengo yake hivyo siwezi kukurypuka na kutaka shoo kwa bei ambayo itaniumiza mwenyewe,” alisema.

Dully alishawahi kutamba na vibao vyake kama, Salome, Kabinti Special, Mtoto wa Kariakoo, Dhahabu na nyinginezo nyingi ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>