Na Elizabeth John

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Chege alisema wasanii wengi hawathamini vya kwao na ndio maana wengi wanaenda kufanya video nje ya nchi na kuacha studio za nyumbani.
“Hivi hatuwezi kuendelea hata kidogo kama tunashindwa kuthamini vya kwetu hatuwezi kupiga hatua, hivyo nawashauri wasanii wenzangu tuvikulai na kuvipenda vya kwetu,” alisema Chege msanii kutoka kundi la Temeke Wanaume Family.
Chege kwasasa anatamba na ngoma yake ya 'Wauwe' ambayo inafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio kutoakana na maudhui ya wimbo wenyewe kuiteka jamii iliyomzunguka.