$ 0 0 UONGOZI mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wilaya ya kichama Ubungo unatarajiwa kujulikana Agosti 3 mwaka huu baada ya uchaguzi wa ngazi za chini katika wilaya hiyo kukamilika. Mbali na viongozi wa wilaya hiyo kujulikana siku hiyo, pia chama hicho kimeeleza kuwa, kimejiandaa vema kuwadhibiti mamluki wasijipenyeze katika uongozi huo. Hayo yalibainishwa na Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Ubungo, Goodluck Justine, wakati akielezea mafanikio yaliyopatikana katika uchaguzi wa ngazi za msingi, matawi na kata.Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Ubungo, Goodluck Justine (wa kanza kushoto) akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.