Quantcast
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

KITALE: SINA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA PENNY


Na Elizabeth John
MSANII wa filamu na vichekesho, Mussa Kitale ‘Kitale’ au ‘Mkude Simba’ amekanusha uvumi kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwanadada, Penny kama inavyodaiwa.

Kitale alikanusha kauli hiyo baada ya vyombo mbalimbali vya habari kuonesha picha na kuzungumzia mahusiano hayo.

“Sina mahusiano ya kimapenzi na Penny huyo ni kama dada yangu, mimi nimeoa na naheshimu ndoa yangu, siwezi kufanya uchafu huo na hizo picha wanazosema nipo nae ni kama rafiki tu,” alisema.

Kitale kwasasa anatamba na vichekesho mbalimbali vya Mkude Simba ambavyo vinarushwa katika kituo cha E Redio iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>