Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Article 2

$
0
0
DMI KUKARABATI SHULE YA MSINGI SARANGA

Na Mwandishi Wetu

UMOJA wa Wanawake unaosimamiwa na Shirika la Masista Tanzania (DMI), umechukua jukumu la kukarabati chumba cha darasa kwenye  Shule ya Msingi Saranga iliyoko Kimara wilayani Kinondoni, Dar es Salaam.

Ukarabati huo umekuja siku chache baada ya shule hiyo kujikuta miongoni mwa zile zinazokabiliwa na changamoto lukuki ikiwemo ya uchakavu wa madarasa.

Akizungumza na wandhishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki Mwenyekiti wa umoja huo, Angela Mkemwa, alisema umoja huo unaundwa na vikundi vidogo vidogo katika Kata ya Saranga, na kusema umoja huo umekusudia kuisaidia shule hiyo baada ya kusaahulika na seriakali.

Alisema wamefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto lukuki, ambako zoezi hilo ni endelevu na limekusudia kuisaidia jamii inayowazunguka kulingana na uhitaji wa tatizo lenyewe.

“Shule ya Saranga inajiendesha katika mazingira hatarishi, ambayo yanaonekana wazi wazi, taswira ya mazingira hayo ni kitendawili cha ufaulu wa wanafunzi wake, hivyo serikali ifanye haraka kuisaidia” alisema Angela.

 Mkufunzi wa wanawake hao , Mohamed Msoffe  kutoka (DMI), alisema  muungano wa wanawake katika jamii unaweza kuleta chachu ya maendeleo baina ya mtu mmoja mmoja.

Pia alizitaka taasisi zisizo za seriakli kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto zinazoikabili jamii wanayoizunguka kwa manufaa ya maendeleo ya nchi.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Sizya Daniel, amesema msaada huo umekuja kwa wakati muafaka kwasababu shule hiyo inakabiliwa na uhaba wa vifaa muhimu vya elimu, jambo ambalo linaweza kuchangia kuanguka kwa taauma kwa wanafunzi.

Alittoa wito kwa wadau, taasisi za kidini, binafsi, kampuni pamoja mashirika mbalimbali kujitokeza katika kuisaidia shule hiyo kwa sababu bado inahitaji msaada ili iweze kujikwamua na changamoto zinazo ikabili shule hiyo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>