Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Article 3

$
0
0
Meya Kapunga ajipalia mkaa Iyela 
Na Christopher Nyenyembe,Mbeya

 MSTAHIKI meya wa jiji la Mbeya,Athanas Kapunga(CCM) amejipalia mkaa wa moto baada ya kutembelea kata ya Iyela kinyemela na kudai kuwa kata hiyo haiendelei kutokana na migogoro ya kisiasa hali ambayo imepigwa vikali na diwani wa kata hiyo,Charles Mkella.  (CHADEMA).

Mkella alitua jana katika ofisi za Tanzania Daima na kudai kuwa kauli iliyotolewa na mstahiki meya wa jiji hilo,Kapunga ambaye pia ni diwani wa kata ya Itiji  na kutamka kuwa  Iyela ni kata inayosakamwa na migogoro ya kisiasa huo si uzalendo ni uchochezi.

“Haiwezekani diwani mwenzangu kutoka Itiji atue kinyemela kwenye kata yetu bila kiongozi yoyote kufahamishwa na kufanya mkutano wa kuwachafua viongozi wenzake huku akijua kata yake ina changamoto nyingi na kero za wananchi ambazo meya huyo ameshindwa kuzimaliza miongo kadhaa tangu alipochaguliwa” alisema Mkella.

Alisem kauli hiyo  ni  ya kushangaza kwani Meya huyo anapoamua kusasafiri na wanahabari na kuwaambia kuwa kata ya Iyela ina migogoro ya kisiasa wakati wananchi wa kata hiyo walioichagua Chadema kwa kishindo kikubwa hawana migogoro inayoelezwa na diwani kutoka kata nyingine kwa lengo la kuchafua upepo wa kisiasa anachangia kudumaza maendeleo.

Mkellla aliyechaguliwa mwaka jana kuwa diwani wa kata hiyo kupitia Chadema baada ya kuibwaga CCM ,alisema kuwa amekuta matatizo mengi yaliyokuwa yakiwakabili wananchi wa kata hiyo likiwemo tatizo la vyoo katika shule ya msingi Mapambano na Nero ambalo CCM kwa muda mrefu wameshindwa kulitatua na kuahidi kuwa tatizo hilo watalimaliza wananchi wenyewe.

Alisema kuwa Meya huyo bila kujielewa ameamua kuwasha moto wa kisiasa ili kuweza kufanikisha malengo yake huku akijua wazi kuwa kwenye kata yake ya Itiji ameshindwa kabisa kusimamia na kuboresha miundombinu ya barabara,ujenzi holela na ukosefu wa huduma muhimu za kijamii na kukimbilia kwenye kata nyingine kugawa misaada ambayo hajaainisha mahali alikoipa.

“Kata ya Iyela tuna changamoto nyingi ikiwemo kupata kiungo muhimu kama daraja kwa ajili ya mazishi na tunajua Mbunge wa jimbo hilo anahangaikia suala hilo,kama Meya anakuja na misaada hatuikatai ni vyema uongozi husika ukajulishwa kuliko kuja kimya kimya na kuchochea fikra za wapenda maendeleo.sijui kimbelembele cha kuja kwenye vyoo kinatoka wapi ? ” alihoji diwani Mkella.

 “Athanas anapaswa kujibu tuhuma nyingi zinazomsakama za kuchota fedha za jiji na kuzitumia kwa ziara nchini China huku ikijulikana wazi kuwa safari hizo zimelipiwa fedha na kugharimiwa na benki ya dunia,huku anachota na kule anatafuna,angeanza na tatizo la daraja kata ya Iyela kuliko kuzuka wakati kata yake ina matatizo kibao” aliongeza Mkella.

Wakati Diwani huyo akilalama,alisema kuwa Kapunga ambaye ni diwani kata ya Itiji amekaa muda mrefu madarakani na kumfanya awe na ndoto za kuiangamiza Chadema bila kujua kuwa nguvu ya umma ni kubwa jijini Mbeya na kwamba hofu aliyonayo inaonyesha wazi ukomo wake wa kisiasa kutokana na tuhuma(hakuzitaja) nyingi  anazodai  zinazomuondolea sifa ya kuwa kiongozi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>