Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Viti Maalum (CHADEMA), Sophia Mwakagenda amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuunga mkono kampeni yake ya kuchangia fedha kwa ajili ya kuwapatia bima ya afya zaidi ya watu 2,000 kutoka familia masikini nchini.
Mwakagenda ametoa ombi hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mapambano ya hisani yanayotarajiwa kufanyika mkoani Geita Julai 28 mwaka huu.
Mapambano hayo yatashirikisha mabondia marufu Karim Mandonga, Mada Maugo, Ibrahim Class na wengine ambapo fedha zitakazopatikana zitatumika kulipia bima ya afya kwa watu 2,000 wanaotoka familia masikini.
Mbunge huyo amesema kampeni hiyo inaenda kugusa jamii ya Kitanzania, hivyo anamuomba Rais Samia kumuunga mkono kwa kulipia bima za Watanzania 300 wanaishi katika umaskini.
“Pamoja na Rais Samia, pia namuomba Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Naibu Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko, Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, taasisi za umma na binafsi kuniunga mkono katika kampeni hii muhimu kwa jamii ya Kitanzania.
Amesema fedha ambazo zitapatikana zitakabidhiwa na Mfuko Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) ambayo inatambua kaya maskini nchini kote.
Mwakagenda amesema kwa anavyomfuatilia Rais Samia na wasaidizi wake ana imani watachangia kampeni hiyo ili kuwezesha Watanzania wengi kupata bima ya afya.
Amasema Taasisi yake ya Lady in Red imejipanga kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali kuhakikisha inatatua changamoto ya bima kwa wananchi hasa maskini.
Mkurugenzi huyo wa Lady in Red amesema yeye ameamua kuwapa mabondia kipaumbele na ndio maana kila akifikiria kufanikisha jambo la hisani kundi hilo ndio la kwanza.
“Julai 28 tukutane Geita ambapo Mandonga anatarajia kupanda ulingoni kulipiza kisasi kwa Mada, lakini pia kwa mara ya kwanza Ibrahim Class ataonesha umwamba wake Geita na wengi ila yote hayo ni kuniunga mkono katika kusaidia jamii inayoishi kwenye umasikini,” amesema.
Mwakagenda amesema Mandonga na Mada watapigana kwa raundi sita huku Class akipambana kwa raundi 10.
Aidha, amesema Bondia Mkongwe, Japhet Kasseba anatarajiwa kupanda ulingoni, hivyo kuwataka wananchi wa Geita na mikoa ya jirani wasithubutu kukosa.
Mbunge huyo amesema kinachoenda kupatikana Geita kinaenda kufasiri bima za afya kwa wote, hivyo anaomba kila mwenye uwezo kujitolea ili kufanikisha.
Amesema ngumi hizo za hisani katika kuchangia bima ya afya zitanufaisha mikoani Geita, Dodoma, Mbeya, na Pwani ikiwa ni kuendelea mpango wao ulioanza mwaka 2016 kusaidia jamii.
Mbunge huyo amesema pia siku hiyo kutakuwa na mapambano ya wabunge mbalimbali akiwemo Mbunge wa Geita Constantine Kanyasu dhidi Vuma Augustino wa Kasulu Vijijini, Stanslaus Mabula wa Nyamagana dhidi Seif Gulamali wa Manonga.
Wabunge wengine watakaopambana ni Santiel Kilumba na Sylivia Sigula, Salome Makamba na Ngwasi Kamani wote wa viti maalum.
Akizungumzia pambano hilo la hisani Bondia Mandonga amesema amefurahi kuwa sehemu ya mabondi ambao watashiriki kusaidia kaya masikini ambapo ameahidi kumpiga Maugo kwa ngumi inayoitwa ‘Mbeku’.
“Baada ya Maugo kukimbia ghetto Morogoro, sasa naenda Geita kumpiga kwa ngumi inayoitwa ‘Mbeku’ ambayo ilihusika kuleta Uhuru wa Tanzania. Mada Maugo atake tunampiga, asitake tunampiga. Ila kusema kweli nimefurahi sana kushiriki pambano hili la hisani, naomba waheshiwa wengine waunge mkono juhudi,” amesema.
Kwa upande wake, Maugo alisema safari hii itakuwa mwisho kwa Mandonga kucheza ngumi, kwani amepanga kumpiga aina ya ngumi iitwayo 'Pikitieli'.
Naye bondia Ibrahim Class amesema amepata faraja kushirikishwa katika pambano hilo la hisani na kuahidi kuonesha mchezo mzuri kwani mikono inawasha.
Bondia Kaseba amesema juhudi anazofanya Mbunge Mwakagenda zinapaswa kuungwa mkono na wapenda maendeleo wote, ili kuweza kusaidia jamii ya Tanzania.
Mandonga, Maugo kumaliza ubishi
CRDB yatumia Maonesho ya Sabasaba kuwaunganisha W’biashara wa Kitaifa, kimataifa
NA MWANDISHI WETU
KATIKA kuhakikisha inaharakisha ustawi na maendeleo yao kiuchumi, Benki ya CRDB imejielekeza katika kuunganisha wafanyabiashara wa kitaifa na kimataifa kupitia Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Tanzania, sambamba kutoa huduma za kifedha na bima kwa wananchi wanaohudhuria.
Hayo yamesemwa na Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa CRDB, ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo, Bruce Mwile, baada ya kuzinduliwa na Rais waMsumbiji, Philipe Nyusi na mwenyeji wake Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, katika Viwanja vya Sabasaba, Kilwa Road jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika banda la benki hiyo, Mwile CRDB wako katika viwanja hivyo sio tu kuhudumia makundi mbalimbali ya wahuidhuriaji wa maonesho hayo, bali pia kuhakikisha wanawaunganisha wafanyabiashara wa kitaifa na kimataifa kama yalivyo maonesho yenyewe.
“Maelfu ya washiriki kutoka Tanzania na nje ya Tanzania wako hapa, wanahitaji taasisi ya kuwaunganisha pamoja na hiki ndio kipaumbele chetu, kuhakimkisha kila mmoja aliyekuja kutoka nje ananufaika na fursa zilizopo, na wafanyabiashara wenyeji nao wanatumia fursa hiyo kujitanua.
“Kwa ujumla wake, CRDB inafanya kazi kubwa hapa kuhakikisha inawaunganisha wafanyabiashara wote wa kitaifa na kimataifa, sambamba na kuwaunganisha na jamii za Kitanzania pia kupitia huduma zetu za kibenki tunazotoa hapa tawini kwetu,” alisisitiza.
“Haya ni maonesho ya kimataifa, kwa hiyo kuna waoneshaji bidhaa kutoka mataifa mbalimbali duniani, wakiwamo wale wanaotoka katika nchi ambazo tuna matawi yetu kama vile Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (DRC) na Burundi, furaha yao hapa ni kuona tupo kuwatimizia mahitaji yao ya kipesa,” alisema.
Mwile alitoa wito kwa wananchi wote wa Tanzania na waoneshaji kutoka mataifa yote kuhakikisha wanafika kwenye tawi lao kupata huduma za kibenki, na kwamba hawapaswi kutembea na pesa taslimu mkononi, badala yake watumie huduma za kidigitali za benki hiyo ambazo zipo kwa ajili yao.
Aliongeza ya kwamba mwitikio wa wananchi tawini hapo ni mkubwa, ambako kila huduma inapatikana, ikiwemo ufunguzi wa akaunti, utoaji pesa kwa ATM, utumaji pesa, huduma za uwakala, SIM Banking, na nyinginezo nyingi ikiwempo mikopo ya kilimo, ujsariamali na biashara.
“Pia CRDB Foundation iko hapa kuhakikisha makundi yote ya wanancjhi yanahudumiwa ipasavyo, hasa kwa ajili ya mitaji wezeshi kwa kina mama na vijana ili kuwawezesha kuendesha biashara zao kwa ufanisi kulingana na levo zao. Pia tuna CRDB Insurance kwa ajili ya bima mbalimbali,” alibainisha.
‘MKONGE HAUTEGEMEI MSIMU’
Afisa Kilimo wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Emmanuel Lutego akitoa elimu ya kilimo bora, masoko na fursa zilizopo kwenye Sekta ya Mkonge katika banda la bodi hiyo lililopo kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (Sabasaba).
Na Mwandishi Wetu
MKONGE umetajwa kuwa ni zao ambalo soko lake halitegemei msimu kulinganisha na mazao mengine ambapo mkulima au mfanyabiashara anaweza kuvuna na kuuza wakati wowote katika mwaka.
Akizungumza kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (Sabasaba), Afisa kilimo wa TSB, Emmanuel Lutego amesema kutokana na hali hiyo, wadau wanaotaka kuingia kwenye sekta ya Mkonge hawatakiwi kuhofia masoko kwamba watauza wapi au wakati gani kwani moja ya jukumu la Bodi ya Mkonge ni kuwaunganisha wakulima na masoko ya mkonge.
Pamoja na mambo mengine amesema; "kama nchi tuna mkakati wa kufikisha tani 120,000 ifikapo 2025 kwa hiyo tunahitaji wakulima zaidi na mashine za uchakataji ili kufikia malengo hayo.”
Aidha, ametaja mikakati ya kufanikisha malengo hayo ni kuongeza ukubwa wa mashamba na idadi ya wakulima wa mkonge kwa kuhamisisha na kutoa elimu ya kilimo bora cha mkonge katika mikoa yote inayofaa kwa kilimo cha mkonge.
“Lakini pia tumejipanga kuongeza tija ya uzalishaji, kuongeza uzalishaji wa mbegu bora za mkonge, kuanzisha vituo vya uchakataji wa mkonge(decortication centres) kwa wakulima wadogo,” amesema Lutego.
Benki ya NMB yaipiga tafu Shule mbili za Sekondari mkoani Dar es Salaam, yakabidhi meza 90 na viti 90 vyenye thamani ya shilingi milioni 10
Mkuu
wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda (katikati) akipokea sehemu ya msaada wa
meza na viti 40 kutoka kwa Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam,
Ferdinand Mpona (wa pili kulia) kwa ajili ya Shule ya Sekondari Uhamiaji
iliyopo Kurasini jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari
Uhamiaji, Christopher Mtabutu, Meneja Mahusiano wa NMB Kanda ya Dar es Salaam,
Melinda Kamukara (kushoto) na wa pili kushoto ni Meneja wa NMB Tawi la
Kurasini, Jane Mubezi. (Na Mpiga Picha Wetu).
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo (wa pili kushoto) akipokea sehemu ya msaada wa meza na viti 50 kutoka kwa Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Ferdinand Mpona (wa pili kulia) kwa ajili ya Shule ya Sekondari Mchikichini. Kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Mchikichini, Nelson Nestory na kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ilala, Christine Lifiga. (Na Mpiga Picha Wetu).
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo (wa pili kushoto) akipmkabidhi sehemu ya msaada wa meza na viti 50 Mkuu wa Shule ya Sekondari Mchikichini, Nelson Nestory vilivyotolewa na Benki ya NMB kwa ajili ya shule hiyo. Katikati anayeshuhudia ni Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Ferdinand Mpona, Diwani wa Kata hiyo, Azim Khan (kushoto) na kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ilala, Christine Lifiga.
Na Mwandishi Wetu
Benki ya NMB imekabidhi meza 90 na viti 90 venye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10 kwa mbili mkoani Dar es Salaam zikiwa ni Shule ya Sekondari ya Uhamiaji iliyopo Wilaya ya Temeke na Shule ya Sekondari iliyopo wilaya ya Temeke ikiwa ni utekelezaji wa azma ya benki hiyo kuboresha ya elimu .
Samani hizo zitapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la upungufu wa madawati kwa walimu na wanafunzi na ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa Uwekezaji kwa Kijamii (CSI) unaolenga kusaidia jamii ambapo benki hiyo inafanya kazi.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi meza na viti hivyo Jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Ferdinand Mpona alisema uboreshaji wa sekta ya elimu ni miongoni mwa vipambule muhimu kwa benki yake huku alisisitiza dhamira ya benki hiyo kuendelea kufanya kazi kwa karibu na wadau wote ikiwemo Serikali katika kuinua maendeleo ya sekta ya elimu nchini kote.
"Kama benki, tunatambua kuwa elimu ndio ufunguo wa maisha ndiyo maana kwa miaka mingi tumewekeza kwa kiasi kikubwa katika kuinua ukuaji wa sekta ya elimu. Kwa hakika, sekta ya elimu ni moja ya maeneo ya kipaumbele katika mkakati wetu wa CSI. Tumekuwa tukitenga asilimia moja ya Faida Baada ya Kodi (PAT) kila mwaka ili kuchangia mipango mbalimbali ya maendeleo,” alisema.
Mpona aliongeza, “Tunaamini samani tunazotoa leo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha mazingira ya kazi kwa walimu,”
Naye Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo aliipongeza benki hiyo kwa moyo wake wa ukarimu na kusisitiza dhamira ya Serikali ya awamu ya sita ya kuendeleza maendeleo ya sekta ya elimu.
“Tunafahamu kuwa shule nyingi za Wilaya ya Temeke bado zinakabiliwa na changamoto nyingi na zinahitaji msaada zaidi kutoka kwa wadau wa elimu kwa kuwa tuna bajeti ndogo. Naishukuru Benki ya NMB kwa kuunga mkono jambo hili zuri na nachukua fursa hii kutoa wito kwa wadau wengine wa ushirika kuungana na azma yetu ya kusaidia maendeleo ya sekta ya elimu,” Mapunda alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo wakati wa hafla ya kukabidhi meza 50 na viti 50 vilivyotolewa na benki ya NMB kwa Shule ya Sekondari Mchikichini alishukuru benki ya NMB kwa kuendelea kuunga juhudi za serikali za kuboresha sekta ya elimu.
“Tunashikia faraja kwa benki yetu kwa kuendele kuwa karibu na wananchi. Mheshimiwa rais ameshaleta fedha za kujenga ghorofa katika shule hii ya Mchikichini na matundu ya vyoo. Kitendo cha benki ya NMB kutoa meza na vitu ni jitihada njema za kuunga mkono serikali na siku zote wamekuwa wakituunga mkono kwa vitendo,” alisema.
Awali, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Uhamiaji, Christopher Mtabutu alibainisha kuwa shule yake ilikuwa inakabiliwa na upungufu mkubwa wa madawati ya walimu akionyesha matumaini kuwa madawati yaliyotolewa na benki ya NMB kwa kiasi kikubwa yatasaidia kukabiliana na upungufu huo.
“Mchango huu umekuja wakati muafaka kwani tumekuwa tukikabiliwa na upungufu wa madawati ya walimu. Ninaamini kuwa madawati na meza ambazo benki ya NMB imetupatia leo vivitasaidia tu kuboresha mazingira ya kazi kwa walimu mbali na kuboresha usalama wa mali zao pia,” aliongeza.
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mchikichini Nelson Nestory alisema, “Msaada wa meza 50 na viti 50 utasaidia sana. Kabla ya kuomba msaada huu tulikuwa na upungufu wa meza na viti 150 na meza 50 ambapo Mkurugenzi alituletea viti 100 na meza 100. Tulikuw ba upungufu wa meza 50 na viti 50. Tunaishukuri benki ya NMB kwa kutupatia meza 50 na viti 50 na kwa sasa tumemaliza tatizo la wanafunzi kukosa meza na viti.
Aliahidi shule yake kuendelea kutunza msaada huo vyema ilikusaidia vizazi vijavyo.
Kusherehekea Uhuru na Ushiriki wa Raia: Ujumbe kwa Marafiki wa Kitanzania katika Siku ya Uhuru wa Marekani
Na Balozi Michael Battle, 4 Julai 2024
Katika kuadhimisha miaka 248 ya uhuru wa Marekani, tulifanya sherehe kubwa nyumbani kwangu, ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania January Makamba alikuwa mgeni rasmi na mamia ya marafiki wa Kitanzania wa Marekani walihudhuria. Tarehe 4 Julai ni siku ya kuzaliwa kwa Marekani kama tunavyoijua sasa – ni siku ya kutambua na kuenzi ushindi wa kujitawala uliopiganiwa vikali na waasisi wa taifa la Marekani. Siku ya Uhuru wa Marekani ni wakati wa kurusha fataki na fashi fashi, kuchoma nyama na kujumuika pamoja kama jamii, lakini pia ni wakati wa kutafakari juu ya maadili na amali zetu za pamoja – uhuru, demokrasia, na ushiriki wa kiraia.
Uhuru wa kujieleza ni nguzo muhimu ya demokrasia. Inawawezesha watu kutoa maoni yao, kuchangia Mawazo yao, na kuwawajibisha viongozi wao. Nchini Marekani, haki hii ya msingi inathaminiwa na kulindwa, hivyo kuruhusu kuwa na jamii yenye nguvu na yenye kupenda na kuhimili mabadiliko ambapo mitazamo tofauti mbalimbali inaweza kustawi. Hali kadhalika, nchini Tanzania, sauti za raia ni muhimu katika kuunda mustakabali wa taifa. Kuhimiza mazungumzo ya wazi na kuheshimu mitazamo tofauti kutaimarisha mshikamano wa jamii na kukuza utamaduni wa maelewano na maendeleo. Ni muhimu kutambua kuwa uhuru huu, japokuwa ni wa msingi, si mara zote raia wanahakikishiwa kuupata, hivyo ni lazima utetewe na ulindwe – hususan wakati unapokabiliwa na changamoto mbalimbali duniani kote.
Kama Rais Joe Biden alivyopata kusema, “Demokrasia haitokei tu kama ajali. Tunapaswa kuilinda, kuipigania, kuimarisha na kuihuisha.” Maneno haya yanagusa vizazi vyote vya Wamarekani, tangu wale waliopigana kwa ujasiri kuanzisha taifa huru. Kwa miaka mingi, kupitia enzi ya harakati za kupigania ya haki za kiraia na kuendelea hadi leo, tumekuwa tukipigania kupanua na kuimarisha demokrasia kwa Wamarekani wote. Tunatambua kuwa kazi ya kujenga demokrasia nchini Marekani, kama ilivyo kwa Tanzania, inaendelea kuwa kazi inayoendelea tunapojitahidi kujenga “muungano mkamilifu zaidi.” Tamanio hili kuu na la kudumu la kuwa watu huru na wanaojiamulia mambo yao wenyewe ndilo lililomhamasisha Mwalimu Julius Nyerere kupigania uhuru wa Tanzania zaidi ya miongo sita iliyopita. Tunaungana na watu wa Tanzania kuunga mkono juhudi za utekelezaji kamili wa maadili yetu ya pamoja ya kidemokrasia.
Kufanya kazi kwa kujitolea ni nguzo nyingine ya jamii yenye afya na inayoshiriki kikamilifu katika masula yanayoihusu. Nchini Marekani, utamaduni wa kujitolea umekita mizizi, ambapo Wamarekani wengi hujitolea muda na ujuzi wao kusaidia wahitaji. Ninajivunia sana kazi inayofanywa na wafanyakazi wa kujitolea wa Peace Corps kwa kushirikiana na jamii za wenyeji wao huko Kilimanjaro, Tanga, Zanzibar na Dodoma. Na ninajivunia zaidi ushirikiano wa timu ya Peace Corps na Wizara ya Afya kuanzisha Mpango wa Kujitolea wa Nchi Mwenyeji (Host Country Volunteerism Program) katika sekta ya afya, unaowaunganisha wafanyakazi wa kujitolea wa Kitanzania na wale wa Peace Corps katika kuleta mabadiliko katika jamii zao.
Kipekee kabisa nimeguswa na jitihada zisizo na ubinafsi za madaktari na wauguzi wa Kimarekani wanaojitolea kuwahudumia Watanzania bila malipo. Watu kama Dk. na Bi. Irving Williams ambao kwa miaka hamsini wamekuwa wakiwaleta watoa huduma za afya na waelimishaji nchini Tanzania kupitia Ahead Inc., shirika lisilo tengeneza faida lililosajiliwa nchini Tanzania, ambalo litarejea mkoani Kagera wiki ijayo na madaktari na wauguzi kutoka jimbo kuu la New York ili kuendesha kliniki maalumu ya afya bila malipo. Shule za sekondari na vyuo vya Marekani vinazidi kujitolea kudhamini mafunzo ya utoaji huduma nchini Tanzania. Vijana hawa na wataalamu wanaonyesha roho ya kujitoa, kujitolea na huruma, wakithibitisha kuwa huduma ya kweli haina mipaka. Kazi yao haiboresha tu afya ya jamii wanazozihudumia bali pia hujenga madaraja ya urafiki na ushirikiano kati ya mataifa yetu.
Ushiriki kamilifu wa raia ni muhimu sana katika kulinda na kuendeleza demokrasia. Raia wanaoshiriki kikamilifu ni roho ya demokrasia, wakishiriki katika mchakato wa uchaguzi, kutetea jamii zao, na kuhakikisha kwamba serikali zao zinawajibika kikamilifu na kuendeshwa kwa uwazi. Nchini Marekani na hata Tanzania, raia wanaoshiriki kikamilifu wana nafasi na jukumu muhimu la kulinda maadili ya kidemokrasia na kukuza haki za kijamii. Tunapoingia kipindi muhimu cha uchaguzi mwishoni mwa mwaka huu katika nchi zote mbili, ni muhimu kwamba raia wachukue jukumu hili kwa uzito unaostahili, na washiriki kikamilifu katika kuchagua viongozi wa kesho. Hii si muhimu tu katika uchaguzi wa urais, bali ni muhimu pia, ikiwa sio zaidi, katika ngazi ya mitaa, ambapo viongozi waliochaguliwa wanajukumu kubwa katika kuboresha maisha ya raia wa kawaida.
Tunaposherehekea Siku hii ya Uhuru wa Marekani, ninawahimiza Watanzania wote kuzingatia na kuheshimu uhuru wa kujieleza, kujitolea, na ushiriki kamilifu wa kiraia. Kwa kufanya hivyo, mtakuwa mnachangia katika kuliimarisha na kulipa uhai taifa lenu, mkihakikisha kwamba demokrasia inastawi na kwamba sauti za raia wote zinasikika na kuheshimiwa. Pamoja, kwa kuheshimiana, kuelewana na kushirikiana, tunaweza kujenga mustakabali mzuri kwa wote.
Heri ya Uhuru wa Marekani!
Balozi Michael Battle
CHAMA AAGA KIUME UNYAMANI
Na Mwandishi Wetu
Matanga yameanuliwa kila mmoja na kwake, ila nyakati zitakumbukwa kwa washirika wa juzi na jana ndivyo unaweza kuelezea katika kile kinachoendelea kwa Wekundu wa Msimbazi Simba baada ya kuachana na Mwamba wao Clatous Chota Chama.
Baada ya Clatous Chota Chama kumaliza mkataba wake wa kuichezea Simba SC June 30, 2024 na kisha July 01,2024 akatambulishwa rasmi kama Mchezaji mpya wa Yanga SC, leo July 03,2024 Chama amewaaga rasmi Simba na kuwashukuru kwa kumfanya kuwa bora zaidi.
Chama anaondoka Simba SC baada ya kuitumikia kwa miaka 6 katika vipindi viwili tofauti ambapo alijiunga Simba SC kwa mara ya kwanza 2018 akitokea Lusaka Dynamos ya Zambia na kisha 2021 kuondoka Simba SC na kujiunga na RS Berkane aliyodumu kwa msimu mmoja na kurejea Simba SC 2022.
Kwenye taarifa aliyoitoa leo Chama amesema miaka sita iliyopita alifika Simba kama Mgeni na Club hiyo ikamfanya kuwa bora zaidi ya alivyokuwa kabla na akawa sehemu ya Watu walioitawala ardhi na kuifanya Simba kupanua zaidi himaya yake hadi sehemu nyingine za Afrika.
Chama amesema baada ya miaka sita ya furaha, fahari na kusudi ameamua kuondoka Simba huku akitoa heshima kwa kila mmoja ndani ya Simba kwa upendo na ushirikiamo aliopewa kwa miaka yote “Hakuna Mtu anayeweza kubadilisha historia tuliyotengeneza pamoja”
“Wanasema shoo haijaisha mpaka Mwanamke mnene aimbe na ninaamini huu wimbo utawapatia thamani ya muda wenu, nawatakia kila la kheri, tutaendelea kuonana, nguvu moja”
TANZANIA, QATAR KUSHIRIKIANA SEKTA YA UTALII
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza na Balozi wa Qatar nchini Tanzania, Mhe. Fahad Rashid Al Marekhi katika kikao kilichofanyika Makao Makuu ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) jijini Dar es Salaam leo Julai 4,2024.
Na Happiness Shayo- Dar es Salaam
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nchi ya Qatar ziko mbioni kusaini Hati ya Makubaliano (Memorandum of Understanding-MOU) kushirikiana katika nyanja mbalimbali za Sekta ya Maliasili na Utalii.
Hayo yamebainika leo Julai 4,2024 wakati wa kikao kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki (Mb) na Balozi wa Qatar nchini Tanzania, Mhe. Fahad Rashid Al Marekhi kilichofanyika Makao Makuu ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) jijini Dar es Salaam ambapo wamekubaliana kukamilisha Hati hiyo.
Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Kairuki amesema kuwa kupitia mkataba huo Tanzania na Qatar zitafaidika na hivyo kutoa wito kwa nchi zote mbili kutumia fursa hiyo katika kuimarisha utalii.
“Tunaamini tutapata fursa ya kuonesha vivutio vyetu vya utalii wakati wa hafla mbalimbali zilitakazofanyika nchini Qatar ikizingatiwa kwamba Qatar ni mojawapo ya soko la kimkakati la utalii kwa Tanzania lakini pia kwa kuzingatia uhusiano, umbali kati ya nchi zetu mbili, tofauti za kiutamaduni na mengi tunayofanana” Mhe. Kairuki amesisitiza.
Ametaja maeneo mengine ambayo nchi hizo mbili zitanufaika ni uhusiano kati ya Bodi yetu ya Utalii Tanzania na Qatar Tourism, kuuunganisha wadau wa utalii kama vile Wakala wa Biashara za Utalii wa Tanzania na Qatar, vyama vya wasafiri, vyama vya hoteli n.k.
Aidha, Mhe. Kairuki ametumia fursa hiyo kuomba ushirikiano kati ya Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) na vyuo vya elimu vya nchini Qatar katika kutoa mafunzo mbalimbali na kubadilishana uzoefu.
Katika hatua nyingine, Waziri Kairuki amekubaliana na wazo la kuanzishwa kwa wiki ya Qatar na Tanzania katika kukuza utalii na utamaduni katika pande zote za nchi hizo mbili.
Pia, Waziri Kairuki ameomba ushirikiano katika kutangaza utalii kupitia vyombo vya habari na mashirika ya ndege ikiwemo Aljazeera na Qatar Airways.
Amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini Qatar kuwekeza katika huduma ya malazi kwa kujenga hoteli kwenye baadhi ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji ndani ya hifadhi yaliyo chini ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) pamoja na maeneo mengine nje ya ardhi inayomilikiwa na Serikali.
Kwa upande wake na Balozi wa Qatar nchini Tanzania, Mhe. Fahad Rashid Al Marekhi amesema atahakikisha ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Qatar unaendelezwa.
“Tunashirikiana na Tanzania na nitahakikisha tunakamilisha na kusaini mikataba yote ya makubaliano kwa faida ya nchi zetu ” Mhe. Marekhi amesema.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Ephraim B. Mafuru, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Mhe. Abdalah A. Kilima na Maafisa Waandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Maliasili na Utalii.
TANZANIA KUWA NCHI YA KWANZA AFRIKA KUFANYA FILAMU KOREA KUSINI
Na Mwandishi Wetu
RAIS wa Filamu Korea Kusini Yang Jongkon amesema Tanzania imechaguliwa kuwa nchi ya kwanza Africa kufanya movie na nchi hiyo huku akiahidi kuja nchini akiwa kuonana na waigizaj wa filamu.
Akizungumza na baada ya waigizaji katika mji unaoongoza kwa filamu duniani ujulikanao kama Busan amesema Rais huyo wa filamu Korea kusini YANG Jongkon amesema Rais Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya kuunganisha soko la filamu la Tanzania na Korea.
"Hivyo basi nami sina budi kueleza kuwa Tanzania ndio nchi ya kwanza tutakayoshirikiana nayo tutakapoingia Afrika. Kwa sasa tunamalizia kuimarisha bara la Asia kwenye tasnia hii ya filamu,"amesema.
Waigizaji hao ambao wapo katika ziara ya kujifunza makubwa zaidi katika soko la filamu nchini Korea kusini wameahidiwa na wameahidiwa makubwa na Rais Jongkon.
Rais Yang Jongkon ameahidi kuja Tanzania kuonana na wasanii wa Tanzania akiongozana na baadhi ya watengeneza filamu wa Korea.
Wasanii kutoka Tanzania wamefanikiwa kutembelea Studio kubwa za Busan na kuona jinsi filamu za kikorea ambazo zimetokea kupendwa sana na watanzania zinavyotengenezwa.
Filamu hizo maarufu zinazotambulika kama Kdrama(Korean drama) zimetokea kuiteka dunia na kuiweka Korea juu kabisa katika masoko ya filamu kimataifa.
Wakati Rais YANG Jongkon akizungumza hayo mjini Busan aliendelea kwa kukazia kuwa atahakikisha anaendelea kuudumisha na kuimarisha uhusiano mzuri sana uliopo kati ya Tanzania na Korea Kusini.
Ameshukuru sana kwa zawadi kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambayo ilikabidhiwa na kiongozi wa msafara huo wa wasanii Steve Nyerere.
DL Group yajipanga kulipa wafanyakazi ndani siku saba
Na Mwandishi Wetu, Njombe
MWEKEZAJI wa viwanda na mashamba ya Chai yaliyopo Mkoani Iringa na Njombe amesema Kampuni ya DL Group ipo mbioni kulipa mishahara ya miezi miwili kwa wafanyakazi wake wote viwandani na mashambani ndani ya siku saba kuanzia leo.
Akizunzungumza na waandishi wa habari leo, miongoni mwa wakurugezi wa Kampuni ya DL Group inayomiliki viwanda vya kuchakata chai vya Itona, Kibena, Ikanga na Luponde Bw Colins Otieno amesema kuporomoka kwa soko la chai duniani na kuadimika kwa dola kumechangia ucheleweshwaji wa malipo ya mishahara kwa wafanyakazi.
“Soko la chai Afrika Mashariki limezidi kudorora kutokana na vita vinavyoendelea kati ya Ukraine na Urusi, Israel na Palestina ambapo mataifa hayo nimiongoni mwa wanunuzi wakubwa wa chai inayozalishwa Afrika Mashariki ikiwemo nchi ya Tanzania,” alisema Otieno na kuongeza kuwa kuadimika kwa dola kumechochea kushuka kwa soko la chai duniani.
Amesema wamekuwa wakipata dola ya Kimarekani 0.6 kwa kilo kwenye mapato ya hisa ya chai ambayo haiendani na gharama wanayoitumia kwenye uzalishaji na hivyo imechangia kwa kiasi kikubwa kampuni kushindwa kulipa mishahara kwa wakati na kwamba wapo katika hatua za mwisho za kupata utatuzi
“DL Group imejipanga kufanya kazi na serikali na vilevile tunatambua mchango wa Waziri wake wa Kilimo, Hussein Bashe, Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka na Bodi ya Chai Tanzania,” alisema Otieno na kuongeza kuwa kampuni yake inaendelea na mazungumzo na serikali kuona namna itakavyo wajengea uwezo wakulima wadogo wadogo na wafanyakazi wake ili kuinua sekta ya chai nchini.
Otieno amesema DL Group kwa kushirikiana na serikali wanakusudia kuboresha maisha ya wakulima wadogo wadogo, ambapo itanarajia kuiuzia serikali mashamba yake matatu ili kuwapa wakulima wadogo ambao ni miongoni mwa wale watakao nufaika na mafunzo yatakayo tolewa na kampuni ya Kenya Tanzania Development Authority (KTDA)
“Tupo kwenye mazungumzo na kampuni ya Kenya Tanzania Development Authority (KTDA ambayo ina viwanda 70 na wakulima zaidi ya laki saba (700,000) hivyo wakulima wadogo wadogo watajengewa uwezo wakuzalisha zaidi na kuwa na soko la uhakika,” alisema
Otieno amepongeza hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dk Samia Suluhu Hassani katika kuendeleza sekta ya kilimo ambayo inamchango mkubwa katika kukuza sekta ya utalii hapa nchini.
Amesema kuyumba kwa soko la chai sio Tanzania pekee bali ni Afrika Mashariki na dunia kwa ujumla hivyo kuwata wanasiasa wasitumie changamoto hiyo kujinufaisha kisiasa.
Naye Michael Mwenda ambaye ni mafanyakazi wa kiwanda cha Kibena akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wenzake, amempongeza muwekezaji wa kiwanda kwa kuchukua hatua madhubuti na kuwahakikishia wafanyakazi kulipwa stahiki zao ndani ya kipindi cha siku kumi.
“Pamoja na matatizo mbalimbali yanayoikabili sekta ya chai, DL Group imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inaboresha maslahi ya wafanyakazi. hiki kilichotokea hapa katikati ni kitu ambacho atukutarajia lakini huko mbele dalili ni njema,” amesema Mwenda.
Kampuni ya DL Group mpaka sasa hivi ishawekeza zaidi ya Sh bilioni 25 inamiliki mashamba tisa katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Iringa na Njombe sambamba na kumiliki viwanda vya kuchakata chai cha Itona kilichopo Mufindi, kiwanda cha Kibena (Njombe) na Ikanga ( Lupembe)
TUME YA MADINI YAENDELEA KUTOA HUDUMA ZA UPIMAJI MADINI KWENYE MAONESHO YA SABASABA
WANANCHI mbalimbali wamejitokeza kupata elimu kuhusu aina ya miamba na namna ya kupima sampuli za madini ya Metallic kwenye mashine ya XRF kwenye Banda la Tume ya Madini katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ‘Sabasaba’
Mashine hiyo ni maalum inayotumika kupima madini ya metallic kwa njia ya MIONZI /X-RAY na kisha kutoa majibu kwa kuonyesha madini hayo yaliyopimwa yana mchanganyiko wa madini gani, pamoja na madini yote yaliyomo ndani ya metali hiyo kwa asilimia tofauti tofauti.
Akitoa elimu hiyo kwa wananchi, Afisa Maabara kutoka Tume ya Madini, Zuwena Mtoo amesema Madini yapo ya aina nyingi duniani lakini huwa hayakai yenyewe, lazima yanakuwa yamechanganyikana na aina mbalimbali nyingine za madini katika miamba
Amesema, watu wanaonunua dhahabu ambao wanaogopa kutapeliwa kwa kuuziwa dhahabu feki wafike kwenye banda la Tume ya Madini kupata elimu ya namna ya kutambua miamba na madini mbalimbali pia wanaweza kupima Hereni, Mikufu ya Dhahabu na Silva katika banda na kushauri wananchi kuitumia fursa hii kufika katika Maabara ya Tume ya Madini iliyopo Msasani jijini Dar es Salaam ili kubaini aina ya miamba.
" Hii mashine ina kioo maalum itakuonyesha kwenye kioo madini yaliyomo ndani mfano ukipima dhahabu baada ya mionzi kuscan itakuonyesha dhahabu ipo asilimia 11 na Silver ipo asilimia 89 sasa wewe ukiona hivi unajua moja kwa moja ulichouziwa ni feki ama si feki," amesema Zuwena.
Amesema pia kuna mashine ya kupima sampuli za miamba kwa njia ya mionzi ambayo inatoa majibu ya ‘elements’ zote zilizomo kwenye huo mwamba na majina yake na wingi wake kwa kukuwekea asilimia yaani kama ni shaba utaona itaandika "CU"....%, kama ni madini ya chuma itaandika "Fe"....% kama ni dhahabu ipo itaandika "Au"....%.
.
Aidha, Zuwena ametoa wito kwa wananchi wanaokuja kwenye maonesho ya Sabasaba kutembelea banda la Tume ya Madini ili pia kujionea madini ya vito mbalimbali na kujifunza fursa zilizopo katika Sekta ya Madini.
Kauli mbiu ya mwaka 2024 katika Maonesho ya Sabasaba ni ‘Tanzania Mahali Sahihi pa Biashara na Uwekezaji’
MISA-TAN yaomba kupunguza ada leseni mitandao ya kijamii
Mwandishi Wetu
TAASISI ya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA-TAN), imeiomba serikali kupunguza viwango vya ada ya kuendesha mitandao ya kijamii (Blogs, Online Tv na YouTube ili kuvutia vijana kumiliki mitandao kisheria na kujiajiri.
Aidha MISA-TAN imeomba serikali kuharakisha kuunda baraza huru la habari na mfuko wa kusaidia wanahabari nchini kujiendeleza kielimu.
Ombi hilo limetolewa na Mjumbe wa Bodi ya MISA-TAN, Mussa Juma leo June 26, jijini Dar es Salaam, wakati akifunga warsha ya siku moja kwa wanachama zaidi ya 33 wa taasisi hiyo na waandishi waandishi wengine kutoka katika vyombo vya habari.
Warsha hiyo iliandaliwa na MISA-Tan kwa ushirikiano na Shirika la Protection International Afrika na kudhamiwa na Serikali ya Finland.
Juma amesema, gharama ya sh 500,000 ya leseni ua kumiliki blogs na millioni moja kumiliki luninga za mtandaoni ni kubwa kwa vijana na watu wenye ulemavu.
"Kama ada ya leseni ikiwa ndogo vijana wengi wenye taaluma ya habari na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), watamiliki mitandao ya kijamii kisheria na kutoa habari" amesema.
Amesema kwa sasa kutokana gharama kubwa za leseni karibu robo tatu ya mitandao inaendeshwa bila leseni .
Amesema muhimu serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kugawa mitandao ya jamii ambayo inamilikiwa kibiashara na ambayo inafanya kazi ya kutoa elimu na kupashanahabari pekee.
Juma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi katika Vyombo vya Habari (JOWUTA) na Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanahabari ya MAIPAC, pia ameomba serikali kuharakisha kuudwa baraza huru la habari, bodi ya ithibati na mfuko wa kusaidia wanahabari.
Akizungumza kwa niaba ya Msemaji Mkuu wa Serikali, Mkurugenzi Msaidizi wa Maelezo, Patrick Kipangula amesema serikali kupitia TCRA bado inaendelea na utafiti juu ya masuala ya leseni na ada mbalimbali na wakikamilisha watatoa taarifa.
Kipangula hata hivyo aliwataka wanahabari na wadau wa habari kuheshimu sheria na kanuni za masuala ya habari .
Awali wakitoa mada katika warsha hiyo, Mawakili Gedion Mandes , Ofisa Programu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Raymond Kanegene na Deus Kibamba walitaka wanahabari kusoma kanuni za maudhui ya mitandaoni ili kutovunja sheria.
Wakili Mandes licha ya kushauri kupunguzwa ada za leseni alitaka elimu zaidi kutolewa juu ya kanuni hizo na kuzingatia haki za makundi ya walemavu.
Naye Wakili Kanegene akichambua kanuni hizo amesema zinamapungufu lakini lazima kwa sasa zifuatw.
Alibainisha baadhi ya mapungufu kanuni kukataza kuandika habari za kuchochea biashara ya kamari mitandaoni huku serikali ikipokea kodi.
Kwa upande wake Kibamba amesema lengo la kanuni za maudhui mtandaoni ni kudhibiti usambazaji holela wa habari na taarifa.
"Katika kanuni hii kuna mambo mazuri na mabaya hivyo ni muhimu kuzijua kanuni, ili wakati ukitaka kuzipinga uwe na uelewa," amesema.
Akizungumza katika kongamano hilo Mkurugenzi wa MISA-TAN, Elizabeth Riziki amesema taasisi hiyo itatumia njia ya majadiliano na serikali na wadau katika kudai kanuni nzuri za maudhui ya mitandaoni lakini pia sheria bora.
Amesema anaishukuru serikali ya awamu ya sita walau imeboresha baadhi ya sheria na kanuni na imefungua milango ya majadiliano zaidi ili kuboresha uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza.
WAZIRI MKUU AZINDUA KAMATI YA KITAIFA YA AFCON 2027
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Julai 05, 2024 amezindua Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) na kuahidi kuwa Serikali itafanya nayo kazi kwa karibu ili iweze kufanikisha malengo ya Tanzania kufanya vizuri kwenye michuano hiyo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kamati hiyo kwenye hafla iliyofanyika katika hotel ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam, Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali ina imani kubwa na kamati hiyo kwamba itapata mafanikio.
“Tuambieni tufanye nini ili tuwe mabingwa, kusanyiko hili liibue nini tufanye sasa na tuanze leo kufanya maandalizi. Tumeunda kamati yenye weledi na wataalamu kwenye sekta ya michezo, tunategemea itupeleke kwenye mafanikio makubwa. Uwepo wenu ni imani ya Serikali kwamba mnaweza kusimamia suala hili.”
Amesema kuwa Serikali imeendelea kufanya maandalizi ikiwemo maboresho ya miundombinu ya viwanja, barabara, reli, anga na usafiri wa maji. “Serikali tumejiweka vizuri kuwa mwenyeji wa mashindano haya; sifa, uwezo na dhamira ya kufanikisha mashindano haya tunayo,” amesisitiza.
Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa mashindano hayo yataongeza idadi ya wageni na watalii hapa nchini, ambao watakuja kwa ajili ya kutazama mashindano na matukio yanayohusiana na AFCON 2027. “Hii itasaidia kuongeza mapato ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.”

Kwa upande wake, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro amesema kuwa uzalendo na utashi wa kisiasa wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan umeifanya sekta ya michezo kusonga mbele na hatimaye kuiheshimisha sekta ya michezo nchini.
Amesema kuwa Kamati hiyo itakuwa na kamati ndogo 13 za wataalamu na watu waliobobea katika maeneo mbalimbali. “Kamati zitakuwa za miundombinu, mawasiliano, fedha, tiba na kinga, usafiri, ulinzi na usalama, sheria, masoko, matangazo, uendeshaji matukio, usimamizi wa timu, mashabiki na watazamaji.
Katika hatua nyingine, Dkt. Ndumbaro amesema kuwa Serikali imeweka mpango wa kushiriki michuano ya AFCON kwa miaka mitatu mfululizo na ametoa wito kwa kamati inayoongozwa na Bw. Leodgar Tenga isaidie Tanzania kufuzu michuano ya AFCON 2025 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango huo.
Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya AFCON 2027, Leodgar Tenga amesema kuwa kamati hiyo itafanya kile kinachostahili ili nchi iweze kufanikiwa na kufanya vizuri katika michuano ya AFCON 2027. “Tunaipongeza Serikali kwa kutuletea watu makini kwa ajili ya kufanikisha AFCON 2027.”
Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Walace Karia ameishukuru Serikali kwa kuendelea mdau ikiwemo kuweka mazingira rafiki ya kuendesha shughuli za michezo nchini. “Kwetu sisi kipaumbele ni suala la AFCON.”
Pia ameishukuru Serikali kwa kuwa na wazo la muda mrefu la kuandaa michuano ya AFCON. “Hatimaye tumeweza kufanikiwa, tunashukuru, leo tupo hapa tunazindua kamati na itakabidhiwa majukumu.”

OSHA yapima wananchi 300 Sabasaba
Na Mwandishi Wetu
WAKALA wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) umesema Maonesho ya 48 ya Biasahara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) maarufu Sabasaba yanafanyika katika Viwanja vya Julius Nyerere yamekuwa ya manufa ambapo hadi leo wamepima zaidi ya watu 300.
Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda wakati akizungumza na waandishi wa habari leo, ambapo amesema wananchi wameonesha uhitaji wa kujua majukumu ya wakala huo muhimu kwa maendeleo ya nchi.
Mwenda amesema katika maonesho hayo wamekuwa wakitoa huduma ya usajili, kupima afya na kuonesha vifaa ambavyo wanatumia vyenye ubora wa kimataifa.
“OSHA tumeshiriki kwenye maonesho haya ya 48, yamekuwa na mafanikio makubwa sana ndani hizi siku saba hadi nane za mwanzo, ambapo tunaendelea kusajili waajiri, kupima afya kwa zaidi ya watu 300 na kuonesha vifaa vyenye ubora, hali ambayo inavutia wawekezaji,” amesema.
Aidha, Mwenda amesema OSHA ipo katika hatua za mwisho za kuhakikisha mifumo yake inasomana na hWakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), hiyo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Deogratius Ndejembi ambalo alitoa alipotembelea banda la wakala huo.
Pia amesema OSHA inatumia mbinu ya majadiliano na waajiri katika utendaji huo, hali ambayo imewezeha kusajili sehemu nyingi za kazi.
Mtendaji mkuu huyo amesema hadi sasa wameweza kusajili sehemu za kazi 45,000, huku takribani sehemu za kazi 40,000 zikisajiliwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande mwingine Mwenda amesema katika mwaka huu wa 2024/25 OSHA itaongeza kasi ya kusajili na kukagua sehemu za kazi ikiwemo kwenye vyombo vya habari ambavyo ni wadau wa kubwa kwenye jamii.
Awali akizngumza na waandishi wa habari Waziri Ndejembi aliitaka OSHA na BRELA kuhakisha mifumo yao inasomana, ili kuleta tija zaidi katika utekelezaji wa majukumu.
Waziri Ndejembi amesema OSHA na BRELA zote ni taasisi za Serikali, hivyo katika keleta tija zinapaswa kusomana kwenye mifumo hali ambayo itapunguza mlolongo mrefu kwa wawekezaji.
“Napenda kutumia nafasi hii, kuwaelekeza OSHA kuwa mifumo yao inapaswa kusomana na BRELA, ili kurahisisha wawekezaji lakini pia kuokoa muda,” amesema.
Amesema hakuna haja ya OSHA kufika katika eneo la uwekezaji dakika za mwisho, bali inatakiwa kujua mapemba ili kuleta ufanisi katika kazi.
Ndejembi amesema iwapo taasisi hizi zitafanya kazi kwa pamoja ni wazi mafanikio ambayo Serikali inahitaji hasa katika huduma kwa wawekezaji yatafanikiwa.
Aidha, Waziri Ndejembi amewataka waajiri kujisajili OSHA, ili kuhakikisha wakala huyo anafanya ukaguzi ambao unahitajika kwenye sehemu za kazi na biashara kama sheria inavyotaka.
“Kusema kweli utendaji wa OSHA chini ya Mkurugenzi Khadija Mwenda na wasaidizi wake unaridhisha ndio maana unaona kasi ya usajili imeongezeka, endeleeni kukaza buti,” amesema.
Pia Waziri Ndejembi ameipongeza OSHA kwa kuzingatia weledi mkubwa katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku, huku akiitaka isifanye uaskari na kuwa marafiki wa waajiri, hasa kwa kuwekeza kwenye elimu hasa faida ya waajiri kujisajili kwao.
Amesema OSHA imekuwa na mchango mkubwa katika utoaji wa huduma za kijamii na kuchochea ukaaji wa uchumi na kuitaka iongeze nguvu zaidi.
KIBAHA TC YAFANYA KWELI YAVISAIDIA VITUO TISA VYA KULELEA WATOTO YATIMA
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Halmashauri ya mji Kibaha katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalumu imetoa msaada wa mahitaji mbali kwa vituo tisa ambavyo vinalea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.
Msaada huo ambao umetolewa leo na kukabidhiwa kwa viongozi wa vituo uliambata na halfa ya kula chakula cha pamoja kati ya watoto hao pamoja na viongozi mbali mbali wa serikali,viongozi wa chama pamoja na viongozi wa dini.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kibaha mji Rogers Shemwelekwa akikabidhi msaada wa mahitaji hayo kwa viongozi wa vituo hivyo amesema kwamba wameamua kufanya hivyo kwa lengo la kuweza kuwasaidia kwa pamoja watoto mahitaji mbali mbali ambayo itakuwa ni muhimu katika mazingira wanayoishi.
Mkurugenzi huyo alibainisha kwamba misaada ambayo imetolewa ni zaidi ya mahitaji 19 ambayo yamegharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 40.
"Sisi kama Halmashauri tumeamua kuvisaidia vituo hivi tisa vya watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu lakini pia jambo ili tumeweza kushirikiana na wadau wa maendeleo ikiwemo shirika la elimu kibaha,benki ya CRDB pamoja na wadau wa maendeleo,"alisema Mkurugenzi.
Mkurugenzi alivitaja vituo hivyo ni Shaloom,Buloma Foundation,Sifa Foundation, Fadhila Faundation,Madina,Haven of Peace,Kibaha Children,pamoja na Karibu nyumbani.
Kadhalika Mkurugenzi huyo alivitaja baadhi ya misaada ambayo wameitoa ni pamoja na magodoro,mafuta ya kula,miswaki,pipi,sabuni za unga,stamina kwa ajili ya watoto,dawa ya miswaki,pamoja na vifaa mbali mbali vya mashuleni.
Aidha mkurugenzi huyo katika hatua nyingine aliwashukuru kwa dhati wadau wa maendeleo ambao wameweza kujitokeza na kuweza kusaidia kuwachangia kwa hali na mali mahitaji mbali mbali.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri yaKibaha mji Mussa Ndomba amesema kwamba lengo ni kuweka mipango madhubuti ya kuwasaidia watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu pamoja yatima.
Ndomba alibainisha kuwa wataendelea kushirikiana na wadau mbali mbali wa maendeleo ili kuhakikisha wanaendelea kusapoti vituo vyote ambavyo vinalea watoto wenye mahitaji maalumu.
Pia Ndomba aliongeza kuwa pia Halmashauri itaendelea kupambana katika kutatua kero na changamoto za wananchi ili kuwaletea maendeleo.
Naye Afisa ustawi wa Jamii katika halmashauri ya mji Kibaha Faustina Kayomba alisema kwamba katika vituo hivyo tisa kuna jumla ya watoto wapatao 601 ambao wengi wao ni watoto yatima na wengine wanaoishi katika mazingira magumu.
Alibainisha kwamba watoto hao wamekuwa wanakutana na changamoto mbali mbali ikiwemo kuwepo kwa mahusiano mabaya ya wazazi na walezi wao.
Nao baadhi ya viongozi kutoka vituo hivyo vilivyopatiwa msaada walimpongeza Mkurugenzi wa halmashauri ya mji Kibaha pamoja na timu yake kwa kuona umuhimu wa kutoa wazo hilo la kuwasaidia mahitaji mbali mbali kwa ajili ya watoto hao.
Baadhi ya watoto wanaolelewa katika vituo hivyo wametoa pongezi na shukrani kwa uongozi wa halmashauri ya Kibaha mji pamoja na wadau wengine wa maendeleo kwa kuwasaidia mahitaji yao muhimu.
RC PWANI,DC KIBAHA WAMPA HEKO KOKA KWA KUWAPAMBANIA WANACHI MATIBABU YA MASIKIO
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Wananchi zaidi ya mia 400 katika Jimbo la Kibaha mjini mkoani Pwani pamoja na maeneo ya jirani wamepatiwa huduma ya matibabu ya masikio bila malipo ambapo baadhi yao wamepatiwa vifaa vya maalumu kwa ajili ya kuongeza usikivu vilivyogharimu kiasi cha shilingi milioni 250.
Vifaa hivyo vya usikivu wa masikio vimetolewa na kufadhiliwa na kwa kampuni ya Starkey cares ya nchini Marekani chini ya mmiliki wake William Haston ambaye ni daktari bingwani.
Kambi hiyo ya Matibabu ya siku moja imefanyika katika hosptali teule ya Rufaa ya mkoa wa Pwani Tumbi kwa ushirikiano wa Ofisi ya mbunge Jimbo la Kibaha mjini na Kampuni ya Selous Biotechnology ya Jijini Dar na kuwezesha ujio wa daktari bingwa Kutoka Marekani
Akizungumza katika kambi hiyo Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amesema kwamba aliwasiliana na daktari bingwa kutoka marekani William Austin kwa ajili ya kusaidia vifaa kwa watu wenye matatizo ya masikio.
"Tunashukuru hawa rafiki zetu kutoka marekani kwa ajili ya kuweza kuwasaidia watu wenye matatizo ya usikivu na kwamba zoezi letu limekwenda vizuri na tulipanga kuwafikia watu 250 lkn tumevuka lengo na kuwafikia watu zaidi ya 400,"alisema Mbunge Koka.
Aidha Koka alibainisha kwamba aliamua kutafuta marafiki kutoka marekani kutokana na kubaini kuwepo kwa wananchi wengi kukabiliwa.na tatizo la masikio na wengine kushindwa kusikia.
Koka alibainisha kuwa lengo lake kubwa ni kuendelea kuwasaidia kwa hali na mali wananchi mbali mbali ambao wamekuwa wana shida hiyo na kuongeza kwamba wananchi wamepatiwa vifaa hivyo bila malipo.
Pia Mbunge huyo alibaisha kuwa vifaa hivyo ambavyo wamepatiwa wagonjwa wa masikio vimegharimu kiasi cha shilingi milioni 250 ambazo zimetolewa na daktari bingwa huyo kutoka marekani.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickosin Simon alisema vifaa ambavyo wananchi wamepatiwa katka kambi la kliniki vitaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa.
Aidha Mkuu huyo alimpongeza kwa dhati Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini kwa juhudi zake za kuweza kuwezesha ujio wa daktari huyo bingwa kutoka marekani.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge amempongeza Rais Samia kwa kuweka mazingira mazuri ya kushirikiana na sekta binafsi katika kuboresha sekta ya afya.
I
Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge amemshukuru Mbunge Koka kwa kuweza kuwajali na kuwasaidia wananchi kupata huduma hiyo ya matibabu ya masikio.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani Amani Halima
Mganga amesema kwamba huduma hiyo imekuja wakati wa muafaka kutokana na uhitaji kuwa ni mkubwa.
Nao Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwa ajili ya kupatiwa huduma katika kambi hiyo ya kliniki wamesema kwamba ujio wa daktari huyo bingwa umekuwa ni msaada mkubwa kwani wameweza kupata matibabu pamoja na kupewa vifaa vya usikivu.
Wananchi hao akiwemo Mariam Salumu na Richard Mkanza hawakusita kutoa pongeza na shukrani kwa kuwasaidia upatikanaji wa huduma ya matibabu ya masikio.
Matumaini Mapya yawakumbuka wajane Kanisa la Elbethel
Mwenyekiti wa kikundi cha Matumaini Mapya, Theresia Kibona (wa pili kushoto) akikabidhi viti kwa Mchungaji wa Kanisa la Elbethel Raphael Mhagama (wa kwanza kushoto) jijini Dar es Salaam jana wakati wa ibada ya shukrani kwa kikundi hicho.
Na Mwandishi Wetu
KIKUNDI cha Huduma ya Matumaini Mapya, kimetoa msaada wa viti 120 vyenye thamani ya sh. milioni 8.4 pamoja na zawadi kwa wajane na watoto yatima katika kanisa la Elbethel Pentecostal Church for all Nations lilipo Kivule Majohe na Kipunguni jiji ni Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Theresia Kibona akiwa na wanachama wenzake wamekabidhi msaada huo kwenye Ibada maalum ya shukrani kanisani hapo.
Amesema msaada huo ni miongoni mwa malengo yao katika kuisaidia jamii kwa sababu wamejikita kutoa huduma ya kufundisha neno la Mungu, kuwashauri mabinti na wanawake wanaopitia changamoto mbalimbali za maisha kusimama imara ili kutimiza ndoto zao.
“Tunayofuraha kubwa kupata kibali katika kanisa hili, tunamshukuru Mungu wanachama tumetoa fedha kwa ajili ya kununua viti hivi ambavyo vitasaidia huduma ya Mungu kusonga mbele, ikiwa leo nasherehekea siku yangu ya kuzaliwa nimefarijika kuwa sehemu ya barakz hizi ambazo naamini zimepata kibali kwa Mungu,”amesema Theresia.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi, Suzana Kimambo amesema wametoa msaada wa viti 120 vyenye thamani ya sh. milioni 8.4 pamoja na zawadi nyingine kwa wajane na watoto yatima kanisani hapo.
Katibu wa Kikundi hicho, Loveness Kibona, amesema walianza huduma wakiwa watu 12 na kwamba hadi sasa wamefikia 40, malengo yao ni kuhakikisha wanakuwa sehemu salama ya watu kupata huduma ya neno la Mungu na kupata ushauri nasaha kukabiliana na changamoto za maisha.
Ameongeza wamepanga kuendelea kuisaidia jamii kuwa kuyafikia makundi yote yenye mahitaji kama walivyofanya mwaka 2023 kwa kukitembea kituo cha waraibu wa dawa za kulevya, kilichopo Pugu ambapo walitoa misaada wa mavazi, chakula na mahitaji mengine.
Akipokea msaada huo Mchungaji wa Kanisa la Elbethel Pentecostal Church, Raphael Mhagama, amewashukuru wanakikundi kwa msaada huo kwa madai walikuwa na uhaba wa viti na tayari walianza kuchangishana ili kuvinunua.
Amesema msaada huo ni muujiza kwao kwani hawakutegemea na kwamba wameweka alama kwa kanisa, kila siku wataendelea kuwaombea ili wabarikiwe kimwili na kiroho kupitia sadaka hiyo walizozitoa kanisani hapo.
WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI IRAMBA SEC
*Akagua uboreshaji miundombinu ya Hospitali ya Mji Mafinga
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Iramba wilayani Mufindi ambayo inatarajiwa kugharimu sh. bilioni 1.78 hadi kukamilika kwake.
Gharama za ujenzi wa shule hiyo zinahusisha jengo la utawala moja, madarasa nane, ofisi nne, maabara tatu, chumba cha TEHAMA kimoja, nyumba za walimu tani za 2-in-1, bwalo la chakula moja na mabweni manne.
Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi wa shule hiyo iliyopo katika kijiji cha Iramba, kata ya Itandula, wilayani Mufindi, mkoani Iringa, leo mchana (Jumapili, Julai 07, 2024), Waziri Mkuu amewapongeza madiwani kwa wazo lao la kutenga fedha na kujenga mradi huo.
Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Iringa kwa ziara ya kikazi ya siku nne, ameitaka Halmashauri hiyo iendelee kubaini vyanzo vitakavyoongeza fedha ili waweze kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo. “Moja kati ya mapungufu ya baadhi ya Halmashauri ni kutotumia fedha za ndani kujenga miradi inayoonekana, ujenzi wa shule hii ni mfano wa kuigwa na Halmashauri zote, ongezeni kasi ya mkamilishe mradi huu kwa wakati.”
Pia amewataka watumie vizuri fedha iliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo ili miundombinu yote itakayojengwa iendane na fedha iliyotolewa. “Fanyeni mapitio ya fedha mliyopanga kutumia kwa ajili ya kujenga nyumba za walimu, shilingi milioni 100 ni nyingi kwa nyumba moja.”
Pia ameagiza madawati yote ambayo hayana eneo la kuweka daftari kwa ajili ya wanafunzi yaondolewe na kurudishwa kwa fundi kwa sababu hayakidhi viwango vya madawati ya shule za msingi na sekondari.
Akitoa taarifa ya ujenzi mbele ya Waziri Mkuu, Mkuu wa Divisheni ya Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Daniele Mapillya, alisema hadi sasa shilingi milioni 363.8 kimepokelewa zikijumuisha shilingi milioni 2.2 ambazo ni nguvu za wananchi na shilingi milioni 361.6 za kutoka kwenye Halmashauri hiyo.
Alisema wameanza utaratibu wa kuisajili shule hiyo ili iweze kutumika kama ya kutwa na isaidie kupunguza umbali kwa wanafunzi wanaosoma kwenye shule mama ya Itandula ambayo ina wanafunzi 1,015.
Wakati huohuo, Waziri Mkuu amekagua ujenzi wa miundombinu kwenye hospitali ya Mji wa Mafinga ambao unahusisha wodi ya wagonjwa wa daraja la kwanza, jengo la kuhifadhia maiti, wodi ya wazazi, jengo la wagonjwa mahututi (ICU) na jengo la kufulia ambavyo vyote vitagharimu sh. bilioni 1.24.
WAZIRI MKUU: WATANZANIA LIMENI MAPARACHICHI
*Silinde asema sh. bilioni 3.4 kujenga kiwanda, ahimiza wananchi wauze mahindi NFRA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wana-Iringa na Watanzania kwa ujumla waingie kwenye kilimo cha Parachichi kwa kuwa zao hilo linachochea ukuaji wa uchumi.
Amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu, Serikali ilikuwa ikitafuta masoko kwa ajili ya maparachichi yanayozalishwa nchini badala ya kutegemea nchi jirani pekee. “Tumeshapata soko la moja kwa moja kwa ajili ya maparachichi yetu nchini China na India na tumegundua ya kwetu yana thamani kubwa na ubora wa hali ya juu ukilinganisha na maparachichi kutoka nchi nyingine.”
Ametoa wito huo jana jioni (Jumapili, Julai 7, 2024) wakati akizungumza na wananchi na viongozi mbalimbali mara baada ya kukagua mradi wa kitalu cha miche bora ya parachichi unaomilikiwa na kikundi cha vijana cha Chilongola, kilichopo kata ya Upendo, Mafinga Mjini, mkoani Iringa.
Mheshimiwa Majaliwa amewataka Watanzania waingie kwenye mpango wa kuzalisha miche ya zao hilo ili kuongeza idadi ya uzalishaji wa maparachichi. “Maparachichi yetu yana ubora mkubwa. Na hii ni baada ya kupima udongo nchini kote na kubaini kuwa tuna maeneo yenye udongo unaofaa kwa kilimo hiki,” amesema.
Akizungumzia suala la barabara kama lilivyowasilishwa na wana kikundi hao, Waziri Mkuu amesema miundombinu ya barabara za kwenda mashambani linaratibiwa vizuri na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) pamoja na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS).
Kuhusu suala la kukosa mlango wa malimbichi bandarini, Waziri Mkuu Majaliwa amesema analipokea suala hilo na kuahidi kuwa atalifuatilia.
Mapema, Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde alisema Serikali imeshasaini mkataba na kampuni ya Afac Engineering ambayo itajen
“Wana-Mufindi ni watu wanaolima sana. Mbunge wenu amesimamia ahadi ya Mheshimiwa Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan ya kujenga kiwanda cha kusindika maparachichi. Mkataba ulisainiwa na kabla ya Ijumaa ijayo, tutamkabidhi eneo mkandarasi ili aanze kazi,” alisema.
Akielezea kuhusu kusuasua kwa zao la chai, Naibu Waziri huyo alisema kuwa Serikali inatambua changamoto iliyokuwepo ya kiwanda cha DL lakini tayari Serikali imeshafanya maamuzi ya kukinunua kiwanda hicho na kukikabidhi kwa wakulima wadogo wadogo wa chai wa Mufindi ili wakiendeshe kupitia ushirika wao.
Kuhusu soko la mahindi, Naibu Waziri Silinde aliwataka wananchi hao wajiandae kuuza mahindi kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kuanzia Julai 10, mwaka huu na kuahidi kuwa bei itakuwa nzuri. Hata hivyo, hakutaja bei hiyo.
Akifafanua zaidi, alisema: “Kutoka Zambia, tumepokea oda ya tani 650,000 za mahindi. Nchi jirani ya Congo (DRC) nao wametaka tani 500,000 lakini wanataka tuwape tani 200,000 za awali. Kwa hiyo, jiandaeni kuuza mahindi kuanzia tarehe 10 Julai, 2024.”
Naye, Mkurugeni wa kampuni ya Chilongola Agroforestry & Livestock, Andrew Salika alisema kikundi chao kilianza mwaka 2020 kwa kuzalisha miche 9,000 lakini hivi sasa wana miche 250,000 iliyo tayari kwenda sokoni. “Lengo letu ni kuongeza idadi ya miche bora ambapo mahitaji ni miche 730,000 kwa msimu mmoja,” alisema.
Wakati huohuo, Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi alisema mji wa Mafinga ni miongoni mwa miji iliyopo kwenye mradi mkubwa wa maji wa miji 28 nchini lakini mradi umefikia asilimia 18 tu kutokana na kusuasua kwa kasi ya mkandarasi.
Aliiomba Serikali isimamie kwa karibu ujenzi wa barabara ya Mafinga hadi Mgololo kwa kuwa wilaya ya Mufindi inabeba uchumi wa mkoa mzima wa Iringa. “Barabara hii ikiisha, itarahisisha sana usafirishaji wa mazao ya wakulima na kuwa mkombozi wa wananchi wengi,” alisema.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Dkt. Linda Salekwa, alimweleza Waziri Mkuu kwamba wilaya hiyo ina ekari 800,000 ambazo ni miti tupu na kati ya hizo, ekari 500,000 ni za miti ya kupandwa. Alisema wilaya hiyo ina viwanda 40 vya kuchakata mazao ya miti pamoja mazao ya kilimo kama chai na pareto.
Aliishukuru Serikali kwa kuwapelekea umeme ambapo hadi vijiji vyote 312 vya wilaya hiyo vimepata umeme na kuongeza kuwa hivi sasa wamejipanga kukamilisha uwakaji umeme vitongojini. “Tuna vitongoji 612, ambapo vitongoji 412 vimeshapata umeme na kati ya 200 vilivyobakia, 107 vipo kwenye mpango wa kupatiwa umeme mwaka huu,” alisema.
Waziri Mkuu amefuatana pia na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe na Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile.
SIJARIDHISHWA NA UJENZI WA SHULE HII – MAJALIWA
*Ni sekondari ya wasichana ya Lugalo ya Mkoa wa Iringa
*Amsimamisha kazi Mhandisi, aagiza Afisa Elimu apewe onyo
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hajaridhishwa na ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya mkoa wa Iringa na kuagiza Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, Emmanuel Sigachuma asimamishwe kazi mara moja.
Pia ameagiza Afisa Elimu ngazi ya Sekondari ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Nelson Milanzi apewe onyo kwa kushindwa kusimamia matumizi ya fedha za ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Lugalo iliyoko kata ya Mbigili, wilayani Kilolo.
Pia ameagiza Mkurugenzi Mtendaji Mstaafu, Lain Ephraim Kamendu aitwe ili ahojiwe pamoja na wenzakekuhusu matumizi mabaya ya fedha hizo. Yeye alistaafu Aprili, mwaka huu na ujanzi ulianza yangu Agosti, 2023.
Amefikia uamuzi huo leo (Jumatatu, Julai 8, 2024) baada ya kukagua ujenzi wa sekondari hiyo na kukuta kasoro nyingi kwenye madawati, vyumba vya maabara na bwalo la wanafunzi ilhali walishapewa sh. bilioni tatu za kukamilisha majengo yote ya shule hiyo.
Kasoro kubwa zilizobainika ni ukosefu wa nyavu za kuzuia mbu kwenye baadhi ya madirisha wakati mkandarasi ameshalipwa fedha yote, viti na meza za wanafunzi kupasuka wakati havijaanza kutumika. Viti hivyo vilikabidhiwa tangu Desemba, 2023 na muda wa matazamio ulikuwa ni miezi sita lakini mkandarasi keshalipwa fedha zote.
Katika ukaguzi wa bwalo, Waziri Mkuu alielezwa na Mhandisi Sagachuma kwamba bwalo hilo lilitengewa sh. milioni 774 na wamekwishatumia sh. milioni 341 hadi kufikia hatua ya linta ambayo alidai ni sawa na asilimia 40 ya ujenzi wake.
Alipoulizwa fedha zilizobakia ziko wapi, Mhandisi huyo alijibu kwamba hazipo. Afisa Elimu Sekondari naye hakuweza kueleza ziko wapi au kama kuna vifaa vilivyokwishanunuliwa vimewekwa wapi.
"Unasema utajenga kwa chuma hapa juu, hizo nondo ziko wapi? Mabati yako wapi? Majiko yako wapi? Hapa tunatarajia kuwa na watoto 172, je watakula wapi hawa na masomo yameshaanza?" alihoji Waziri Mkuu bila kupatiwa majibu.
“Wewe ni Afisa Elimu na kazi yako ni kusimamia ujenzi wa shule zote, ni kwa nini hukutoa taarifa ya kusuasua kwa ujenzi kwenye Kamati ya Ulinzi ya Wilaya yako? Taarifa nilizonazo ni kwamba Mkurugenzi aliyekuwepo alikuwa anakupangia kazi kwenye vituo vya mbali ili usije hapa, lakini bado ulikuwa na wajibu wa kutoa taarifa juu ya mwenendo huo.”
Kwenye ujenzi wa maabara za shule hiyo, Waziri Mkuu amehoji ni kwa nini mifereji ya kupitisha gesi na maji machafu imezibwa yote. “Mifereji haina vishikio, wamejaza matofali hata mwalimu akitaka kukagua mifumo ya gesi au mifereji ya maji machafu hawezi kuinua hilo tofali. Mifuniko ya mifereji inayopitisha maji, bomba za umeme na gesi kwenye maabara ya shule hiyo itolewe na irekebishwe upya,” ameagiza.
Amemuagiza Mkuu wa Wilaya hiyo, Joachim Nyingo asimamie zoezi la kurudisha madawati yaliyoletwa ambayo ni mabovu kwa gharama za mkandarasi ili yaletwe mengine mapya. Madawati (meza na viti vyake) mengi yalikuwa yamepasuka katikati au pembeni na yalikuwa yamepangwa darasani.
“Nimeagiza fundi aliyejenga madirisha atafutwe, aletwe ili aweke nyavu kwenye jengo la utawala. Aliyetengeneza madawati aitwe akayatengeneze upya madawati hayo kwa viwango vinavyotakiwa na kwa gharama zake.”
Pia amemuagiza Kamanda wa TAKUKURU, Mkoa wa Iringa, awahoji watumishi hao na aanze uchunguzi mara moja.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amekabidhi hati ya kiwanja chenye ukubwa wa ekari 50 kwa uongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) ili waweze kuanza ujenzi wa tawi la chuo hicho katika wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa.
Sasatel, Hydrox kufirisiwa
Na Mwandishi Wetu
WAKALA wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) imetangaza kufilisi kampuni za DOVETEL (T) Limited maarufu kama Sasatel na Hydrox Industrial Serivices Limited baada ya kujiridhisha kuwa kampuni hizo mbili kushindwa kujiendesha na kulipa madeni.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kutolea ufafanuzi kuhusu hatua hiyo, iliyofikiwa ya kufilisi kampuni hizo, Kabidhi Wasii Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Frank Kanyusi alisema inalenga kulinda haki za wanahisa, wabia,wadeni, wafanyakazi na pia kuwezesha kodi na tozo za Serikali kulipwa ipasavyo.
“Ningependa umma wa Watanzania ufahamu kuwa RITA mbali ya kusajili vizazi, vifo, ndoa, talaka na watoto wa kuasili pia katika ufilisi tunaangalia usimamizi wa kampuni na ufilisi wa kampuni, watu binafsi usajili wa bodi za wadhamini, kusimamia mali isiyokuwa na mwenyewe, kuandika na kutunza wosia na kusimamia mirathi,” alisisitiza Kanyusi.
Alisema RITA imepewa idhini na Mahakama, kuzibinafsisha kampuni hizo na kutoa matangazo kwenye vyombo vya habari, kuutangazia umma na hasa wenye maslahi katika kampuni hizo, kujitokeza kabla ya kukamilisha mchakato wa ubinafsishaji.
“Kazi ya ufilisi nchini inaongozwa na sheria kutegemea biashara inayofanywa na kampuni inayofilisiwa. Sheria hizo ni pamoja na ya ufilisi, ya kampuni, ya benki na taasisi za fedha, ya vyama vya ushirika, ya bima, ya mashirika ya umma, ya hati za makubaliano na ya muunganisho wa wadhamini,” alisema.
Kanyusi alisema RITA imejipanga kutekeleza majukumu yake kwa weledi na kufikia matarajio na malengo ya Serikali kupitia falsafa ya R nne (4Rs) yaani Maridhiano, Mabadiliko, Ustahimilivu na Ujenzi Mpya.
Akifafanua Kanyusi alisema ufilisi wa kampuni hizo ni hatua muhimu kwani endapo kampuni hizo zitaachwa bila kufilisiwa, zinaweza kutoweka huku makundi tajwa yakipoteza haki kisheria.
DEVETEL au Sasatel ilianzishwa kufanya biashara ya mawasiliano huku kampuni ya Hydrox Industrial Services Limited ikijihusisha na kuzalisha na kuuza dawa na kemikali za kusafisha maji.