Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

DC KIBAHA- RAIS SAMIA ATOA BILIONI 4 UJENZI WA DARAJA LA KUDUMU MTO MPIJI

$
0
0

NA VICTOR MASANGU, KIBAHA

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Saimon amempongeza Rais kwa kuweza kutoa fedha  kiasi cha shilingi bilioni 4  kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa  daraja jipya la kudumu katika  mto mpiji ambalo litaweza kuwa mkombozi kwa wananchi kuvuka bila shida hasa katika kipindi cha mvua.

Daraja hilo la mto mpiji ambalo kwa sasa limejengwa kwa muda  limekuwa ni kiunganishi na mkombozi mkubwa  kwa wananchi kutoka   Wilaya mbili za Kibaha Mkoa wa Pwani pamoja na Wiyaya ya Ubungo ya Jijini Dar es Salaam

Mkuu huyo wa Wilaya ametoa pongezi hizo wakati wa halfa fupi ya kukabidhiwa daraja la muda kutoka kwa kaimu mkuu wa mafunzo na operesheni wa Jeshi la la nchi kavu Brigadia Jenerali Stanley Mjelwa halfa ambayo imehudhuliwa na viongozi wa serikali,chama,wananchi na Tarura.

Nikson amebainisha  kwamba pia   amemshukuru kwa dhati kwa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe. Silvestry Koka kwa kuwa  mstari wa mbele katika kulipambania kwa hali na mali ujenzi wa  daraja hilo liweze kujengwa ili wananchi waweze kupita kwa urahisi.

Amesema  kwamba Mbunge Koka amepambana na kuwasemea wananchi wa Pangani juu ya adha wanayoipata ndio maana Rais Samia  ameweza kuwa msikivu na kukubali   kutoa fedha hizo  kwa ajili ya ujenzi wa ujenzi wa daraja hilo la kudumu.

  Mkuu huyo  amefafanua kwamba kwa sasa daraja ambalo limejengwa na Jeshi la nchi kavu  litatumika kwa muda na baada ya hapo litajengwa daraja lingine jipya la mto mpji  kwa fedha ambazo zimetolewa na Rais  Samia kiasi cha shilingi bilioni 4

"Kwa kweli nimshukuru sana Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutupatia fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja la kudumu katika mto mpiji licha ya kutoa fedha zingine zaidi ya milioni 250 kwa ajili ya kukarabati daraja la muda nimshukuru sana"

"Pia Mbunge wetu wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kwa kuwa mstari wa mbele katika kuomba fedha na kuchangia michango mbali mbali katika daraja la muda ambalo limekabidhi kwangu leo hii ni juhudi za Mbunge Koka ili wananchi waweze kupata daraja hilo,"alisema Nickson.

Pia amesema kwamba anawashukuru Tarura pamoja kwa juhudi zao pamoja na Jeshi la nchi kavu kwa kuweza kukamilisha ujenzi huo wa daraja la muda katika mto mpiji.

Naye Kaimu wa mkuu wa mafunzo na operesheni wa Jeshi la nchi kavu Brigedia Jenerali Stanley Mjelwa ameitaka Tarura kuhakikisha wanalifanyia ukarabati daraja hilo ili liweze kuharibika mapema.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA) Wilaya ya Kibaha mjini Injinia Samwel Ndoveni amesema kwamba daraja hilo la awali limeweza kufanyiwa marekebisho ili kuweza kuwapa fursa wananchi wa Wilaya ya Kibaha na Wilaya ya Ubungo waweze kupita kwa urahisi zaidi.

Nao baadhi ya wananchi wa kata ya pangani hakusita kuzungumzia jinsi ya Mbunge wa Jimbo lao alivyoweza kuwa na wananchi bega kwa bega katika ujenzi wa daraja hilo la mto mpiji.

Wamesema kwamba Mbunge Koka tangu mwanzoni ameshirikiana na diwani wa kata ya Pangani pamoja na wananchi kwa ajili ya kuweza kuhakikisha daraja hilo la muda  linakamili na kupitika kwa urahisi.


Benki ya CRDB yaadhimisha Siku ya Wajasiriamali Duniani ikitoa Shilingi Bilioni 995 mpaka Mei 2024

$
0
0

 

>Yaahidi kuendelea kuwawezesha kwa mitaji nafuu na safari za kimataifa za kujifunza zaidi

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile (wapili kulia), Mkurugenzi wa Wateja wa Awali na wa Kati wa Benki ya CRDB, Bonaventura Paul (wa pili kushoto), Meneja Mwandamizi wa Bidhaa za Biashara CRDB, Isaac Shao (kushoto) na kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Biashara CRDB, Agnes Kisinini, wakizindua kwa pamoja akaunti ya Biashara (Biashara Account). Hafla hiyo ilifanyika wakati wa kuadhimisha Siku ya Wajasiriamali Duniani (International MSME Day) iliyofanyika Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa Wateja wa Awali na wa Kati wa Benki ya CRDB, Bonaventura Paul, akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wajasiriamali Duniani (International MSME Day) Makao Mkuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile, akizungumza akitoa hotuba yake wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wajasiriamali Duniani (International MSME Day) yaliyofanyika Makao Mkuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam.

 

Dar es Salaam. Tarehe 27 Juni 2024: Benki ya CRDB imeungana na wadau wengine kuadhimisha Siku ya Wajasiriamali Duniani (International MSME Day) kwa kuendesha semina kwa wateja wake na baadhi ya wabia wa kimkakati.

 

Sherehe za maadhimisho hayo zimefanyika makao makuu ya Benki ya CRDB zikifunguliwa na Afisa Mkuu wake wa Uendeshaji, Bruce Mwile aliyesema kuwa kipaumbele chao siku zote ni kumhudumia Mtanzania na kuhakikisha anaboresha maisha yake kwa kumpa huduma zinazoendana na kukidhi mahitaji yake.

 

Ili kukuza ujasiriamali, Mwile amesema Benki ya CRDB inatambua kuwa shughuli zake zikichangia asilimia 27 ya Pato la Taifa na ili itoe mchango wake ipasavyo kunahitajika huduma na mifumo shirikishi itakayowasaidia wajasiriamali kuyafikia malengo waliyojiwekea.


“Kutokana mikakati tuliyojiwekea, Benki yetu imekuwa kinara katika uwezeshaji wajasiriamali kwani hadi Mei 2024 tulikuwa tumetoa zaidi ya shilingi bilioni 995.346 kwa zaidi ya wajasiriamali 21,470 katika sekta mbalimbali ikiwamo sekta ya kilimo, ujenzi na makazi, miundombinu, usafirishaji, afya, elimu, nishati, madini, biashara na viwanda, pamoja na uchumi wa buluu ili kuimarisha shughuli zao,” amesema Mwile.

 

Mwile amesema sekta ya ujasiriamali imekuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi wa mataifa mengi duniani kwa kuchochea ubunifu na uanzishaji biashara mpya ambazo huongeza ajira na kuimarisha kipato cha watu binafsi na jamii kwa ujumla. 

“Kwa kuanzisha biashara ndogo na za kati, wajasiriamali huchangia moja kwa moja kwenye ukuaji wa pato la Taifa na kuongeza mapato ya serikali kupitia kodi. Sekta hii pia ina mchango mkubwa katika kuboresha teknolojia na kuongeza ufanisi katika uzalishaji wa bidhaa na huduma, hivyo kufanya uchumi kuwa na ushindani zaidi kimataifa,” amesema Mwile.

 

Taarifa za Umoja wa Mataifa (UN) zinasema wajasiriamali ni injini muhimu ya kufanikisha utekelezaji wa Maendeleo Endelevu (SDG) kwani kundi hili linachangia asilimia 90 ya biashara zote zilizopo duniani ambazo hutoa kati ya asilimia 60 mpaka 70 ya ajira zenye staha na kuchangia zaidi ya nusu ya pato la dunia. Tanzania kuna zaidi ya biashara ndogo za ujasiriamali milioni 3 zinazowapa uhakika wa kipato wamiliki wake.

 

Ili kumkuza mjasiriamali kuanzia ngazi ya chini kabisa, Mwile amesema Taasisi ya CRDB Bank Foundation ambayo ni kampuni tanzu ya Benki ya CRDB inatekeleza programu ya Imbeju inayotoa  elimu ya ujasiriamali na fedha kwa wanawake na vijana pamoja na kuwapa mitaji wezeshi inayoanzia shilingi 100,000. Hadi sasa tayari programu hiyo imewafikia wajasiriamali zaidi ya 400,000 na kutoa mitaji wezeshi zaidi ya shilingi bilioni 10.

 

Sambamba na maadhimisho hayo, Benki ya CRDB imezindua ‘CRDB Biashara Account’ ambayo ni mahsusi kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo wenye malengo ya kukuza miradi yao ili kuongeza idadi ya wateja wanaowahudumia, kukuza mapato yao ili wakue zaidi na kuanzisha kampuni kubwa zitakazohudumia nchi nzima hata nje ya mipaka pia.

 

Akizungumza kwenye mjadala uliofanyika katika maadhimisho hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Royal Mark, Johnson Kapira amesema, kwa Mtanzania kuwa masikini kunatokana na kutokuwa na ujasiri wa kufanya uamuzi binafsi wa kuzichangamkia fursa zilizopo.


Akieleza jinsi alivyoanza mwanzoni mwa miaka ya 1990 baada ya kuhitimu chuo kikuu, amesema kutokana na changamoto za kupata ajira zilizokuwapo alianzisha kampuni yake na akawa anaomba mikopo ya kufanikisha kazi alizokuwa anazipata na mpaka sasa anakopesheka kiasi kikubwa zaidi.

 

“Nilianza nikiwa mfanyabiashara mdogo sana. Nilianza biashara mwaka 1995 nikiomba zabuni serikalini na kampuni binafsi. Mtaji ulikuwa changamoto lakini Benki ya CRDB imenikuza hasa huduma yake ya Purchase Order Agreement. Leo hii naweza kukopa mpaka shilingi bilioni nne,” amesema Kapira.

 

Naye Josephat Kibwanga ambaye naye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Qualitas amesema: “Mimi ni mteja mkubwa wa Benki ya CRDB. Mikopo yao imeniwezesha kuimarisha huduma katika hospitali yangu na kwa sasa utakuwa muujiza iwapo mgonjwa atakuja hospitalini kwetu na akaambiwa hakuna dawa. Haya yote yamewezekana kutokana na mikopo inayopatikana kwa wakati kutoka Benki ya CRDB.”

Maneno ya wajasiriamali hao yana akisi kile alichokisema Mwile wakati akifungua maadhimisho hayo aliposema: “Leo hii tukiwa tunaadhimisha Siku ya Wajasiriamali Duniani niwahakikishie kuwa Benki yetu ya CRDB itaendelea kuweka mikakati madhubuti ya kuwawezesha wajasiriamali na biashara changa, ndogo na za kati nchini tukiamini kwa kufanya hivyo tunachochea ongezeko la ajira, kuimarisha kipato binafsi na kukuza uchumi wa Taifa letu kwa ujumla wake. Ahadi yetu ni kwamba tupo tayari kuwahudumia na kutembea nanyi katika safari yenu ya mafanikio.”


CCM PWANI YAJIPANGA KUSHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

$
0
0

NA VICTOR MASANGU, PWANI

Chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu kimejiwekea mipango kabambe  ya kuhakikisha  kwamba wanapata wagombea wazuri  na wenye sifa ambao wanakubalika katika jamii  na kuweza kusabisha kuweza kuibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi huo.

Hayo yamebainishwa na Katibu wa (CCM)  Mkoa wa Pwani Bernad Ghathy  wakati wa kikao cha Halmashauri kuu ya (CCM) Mkoa ambapo amesema kuwa lengo kubwa la chama ni kuweka misingi imara ya kuwapata viongozi wazuri ambao watakwenda kuipeperusha vyema bendera ya chama kwa kushinda katika mitaa yote ndani ya Mkoa wa Pwani.

Katibu Ghaty alisema kwamba kikao hicho cha Halmashauri kuu kimeelekeza kwamba katika vikao vyote vya  uteuezi  vitakavyofanyika katika ngazi ya chama  vihakikishe kwamba vinatenda haki bila upendeleo wowote  katika kuwapata viongozi ambao watagombea katika uchaguzi huo wa serikali za mitaa.

"Tumekutana katika kikao cha Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani na hiki kikao ni cha kikatiba kabisa na  tumeweza kuzungumzia mambo mbali mbali ya utekelezaji wa ilani pamoja na kupokea taarifa ya serikali ya Mkoa ikionyesha kazi na miradi mbali mbali ambayo imetekeleza katika sekta tofauti, ikiwa sambamba na kujadili hali ya kisiasa katika Mkoa wa Pwani,"alisema Katibu Ghathy.

Aidha Katibu huyo alifafanua kwamba Halmashauri hiyo imempongeza kwa dhati Mwenyekiti wa (CCM) Taifa ambaye pia ndiye Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuwatumikia wananchi katika nyanja mbali mballi za miradi ya maendeleo ikiwemo elimu, wananchi kuweza kupata huduma ya maji safi na salama, miundombinu ya barabara sambamba na uboreshawaji wa huduma ya afya.

Kadhalika hakusita kutoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge pamoja na wasaidizi wake kwa kuweza kuhakikisha kwamba wanajitahidi kupambana kuboresha miundombinu ya barabara ili iweze kupitika kwa urahisi hata katika kipindi cha mvua zinaponyesha.

Pia amebainisha  kuwa chama cha mapinduzi Mkoa wa Pwani wanajivunia kupata Mwenyekiti wa Taifa ambaye ni msikivu na shupavu kwani ameweza kufanya mambo makubwa mbali mbali ya kukisaidia chama ikiwemo kuchangia katika mradi wa jengo la kitega uchumi ambalo linatarajiwa kuzinduliwa ifikapo Julai 30 mwaka huu na kuanza kutumika.

Katika hatua nyingine amesema kuwa mikakati ambayo wamejiwekea ni kuendeleza sera ya chama ya kuweka mifumo ya kujiimarisha kichumi kuanzia ngazi za chini kwa kushirikiana bega kwa bega na wanachama wote wa chama cha mapinduzi lengo ikiwa ni kuweza kuletaa mabadiliko chanya ya kimaendeleo kupitia vitegaa uchumi vilivyopo.



Vijiji 70 vyanufaika na FORVAC

$
0
0

Na Mwandishi Wetu         

ZAIDI ya vijiji 69 vya mikoa ya Tanga, Mkangara, Dodoma, Lindi na Ruvuma vimenufaika kiuchumi, kijamii na mazingira kupitia Mradi wa Kuongeza Mnyororo wa Thamani kwenye Mazao ya Misitu (FORVAC).

Mradi huo ambao ulianza mwaka 2018 na kufikia mwisho mwaka Julai mwaka 2024 umewezesha vijiji 69 kupata zaidi ya Sh bilioni 9 kwa kipindi cha miaka sita, ambazo zimetumika kutekeleza miradi ya kijamii.           

Hayo yamesemwa na Mtaala wa Misitu kutoka Mradi wa FORVAC, Marcel Mutunda wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ambapo amesema mradi huo umefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 100.
       
Mutunda amesema mradi huo ambao umehusisha hekta 460,000 kati ya 450,000 ambazo zilipangwa awali umeweza kugusa jamii kubwa ya vijijini, huku uhifadhi kuboreka.

"Mradi wa FORVAC umehusisha mikoa mitatu ambayo ni Kongani ya Tanga iliyokuwa na Wilaya ya Handeni, Kilindi, Kiteto mkoani Manyara na Mpwapwa Dodoma, Kongani ya Ruvuma ilihusisha Wilaya ya Nyasa, Mbinga, Songea, Namtumbo na Tunduru na Kongani ya Lindi ni Wilaya ya Nachingwea, Ruangwa na Liwale ambapo vijiji zaidi ya 69 vimegeswa na mradi," amesema.
                              
Mtaalam huyo wa misitu amesema kupitia mradi huo hekta 460,000 zimehifadhiwa kwa mfumo wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu ya Jamii (USMJ) na kuwaingiza wanavijiji zaidi ya Sh bilioni 9 ambazo zimetumika kujenga shule, zahanati, visima vya maji, wananchi kukata bima ya afya na nyingine nyingi.
                    
Amesema wananchi ambao wamenufaika na program hiyo wameweza kuongeza kipato na kuishi maisha bora, huku misitu ikiwa endelevu.              

Mutunda amesema pamoja na mafanikio ambayo wamepata wamekutana na changamoto ya mipaka ya vijiji hasa vile ambavyo havikuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi.                        

"Pia moto holela ilichangia utekelezaji wa mradi kusuasua na mifugo kuingia kwenye msitu ni baadhi ya changamoto tulizokumbana nazo," amesema.
                               
Mratibu wa FORVAC Taifa, Emma Nzunda amesema mradi huo umekuwa na matokeo chanya kwa wanavijiji na serikali kwa ujumla.             

Nzunda amesema mradi umewezesha wizara kutengeneza miongozo, kutafsiri sera na miongozo, kutafutia wanufaika masoko, hivyo wamenufaika kiuchumi
     
Aidha amesema mradi huo umewezesha wanavijiji kupata mashine za kisasa, kifaa cha kukausha mbao, hivyo bidhaa za misitu kwenda sokoni zikiwa na ubora na thamani kubwa.     

"FORVAC imeweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye sekta ya misitu na uhifadhi, tunatarajia kuja na mradi mwingine ambao utaendeleza ilipoishia FORVAC," amesema.                                

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Misitu Wizara ya Maliasili na Utalii, Deusdedit Bwoyo amesema wiraza itahakikisha mazuri yaliyopatikana kupitia mradi huo yanaendelezwa kwani uhifadhi una faida kwa kimazingira, kijamii na kiuchumi
                       
Amesema Tanzania kuna hekta milioni 48.1 ya misitu ambapo hekta milioni 22 zipo kwenye ardhi za vijiji, hivyo kupitia mradi huo wameona umuhimu wa ushirikishwaji wa wananchi katika kuisimamia na kuitunza.     

"Mradi huu umegusa hekta 460,000, ila lengo letu kama wizara ni kufika Tanzania yote, hivyo naomba wadau wengine wa uhifadhi waje tushirikiane," amesema.                                

Amesema mradi huo ambao unaisha Julai mwaka huu unapaswa kuendelezwa na Watanzania wote kwa kuwa una faida kwa nchi.

Naye Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Finland, anayeshughulikia Masuala ya Maliasili, Sanna Liisa Taivalmaa amesema nchi yao itaendelea kusaidia Tanzania kwenye eneo hilo kwani ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.         

Amewataka Watanzania kuthamini na kutambua faida ya misitu kwani ni muhimu kiuchumi, kijamii na mazingira.

Amesema iwapo wananchi watashirikishwa katika uhifadhi wa misitu ni wazi kuwa mafanikio yatakuwa mengi zaidi kuliko hasara.


MISA-TAN yaomba kupunguza ada leseni mitandao ya kijamii

$
0
0

Mwandishi Wetu

TAASISI ya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA-TAN), imeiomba serikali kupunguza viwango vya ada ya kuendesha mitandao ya kijamii (Blogs, Online Tv na YouTube ili kuvutia vijana kumiliki mitandao kisheria na kujiajiri.

Aidha MISA-TAN imeomba serikali kuharakisha kuunda baraza huru la habari na mfuko wa kusaidia wanahabari nchini kujiendeleza kielimu.

Ombi hilo limetolewa na Mjumbe wa Bodi ya MISA-TAN, Mussa Juma  leo June 26, jijini Dar es Salaam, wakati akifunga warsha ya siku moja kwa wanachama zaidi ya 33 wa taasisi hiyo na waandishi waandishi wengine kutoka katika vyombo vya habari.

Warsha hiyo iliandaliwa na MISA-Tan kwa ushirikiano na Shirika la Protection International Afrika na kudhamiwa na  Serikali ya Finland.

Juma amesema, gharama ya sh 500,000 ya leseni ua kumiliki blogs na millioni moja kumiliki luninga za mtandaoni ni kubwa kwa vijana na watu wenye ulemavu.

"Kama ada ya leseni ikiwa ndogo vijana wengi wenye taaluma ya habari na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), watamiliki mitandao ya kijamii kisheria na kutoa habari" amesema.

Amesema kwa sasa kutokana gharama kubwa za leseni karibu robo tatu ya mitandao inaendeshwa  bila leseni .

Amesema muhimu serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kugawa mitandao ya jamii ambayo inamilikiwa kibiashara na ambayo inafanya kazi ya kutoa elimu na kupashanahabari pekee.

Juma  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi katika Vyombo vya Habari (JOWUTA) na Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanahabari ya MAIPAC, pia ameomba serikali kuharakisha kuudwa baraza huru la habari, bodi ya ithibati na mfuko wa kusaidia wanahabari.

Akizungumza kwa niaba ya Msemaji Mkuu wa Serikali, Mkurugenzi Msaidizi wa Maelezo, Patrick Kipangula amesema serikali kupitia TCRA bado inaendelea na utafiti juu ya masuala ya leseni na ada mbalimbali na wakikamilisha watatoa taarifa.

Kipangula hata hivyo aliwataka wanahabari na wadau wa habari kuheshimu sheria na kanuni za masuala ya habari .

Awali wakitoa mada katika warsha hiyo, Mawakili Gedion Mandes , Ofisa Programu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Raymond Kanegene na Deus  Kibamba walitaka wanahabari kusoma kanuni za maudhui ya mitandaoni ili kutovunja sheria.

Wakili Mandes licha ya kushauri kupunguzwa ada za leseni alitaka elimu zaidi kutolewa juu ya kanuni hizo na kuzingatia haki za makundi ya walemavu.

Naye Wakili Kanegene akichambua kanuni hizo amesema zinamapungufu lakini lazima kwa sasa zifuatw.

Alibainisha baadhi ya mapungufu kanuni kukataza kuandika habari za kuchochea biashara ya kamari mitandaoni huku serikali ikipokea kodi.

Kwa upande wake Kibamba amesema lengo la kanuni za maudhui mtandaoni ni kudhibiti usambazaji holela wa habari na taarifa.

"Katika kanuni hii kuna mambo mazuri na mabaya hivyo ni muhimu kuzijua kanuni, ili wakati ukitaka kuzipinga uwe na uelewa," amesema.

Akizungumza katika kongamano hilo Mkurugenzi wa MISA-TAN, Elizabeth Riziki amesema taasisi hiyo itatumia njia ya majadiliano na serikali na wadau katika kudai kanuni nzuri za maudhui ya mitandaoni lakini pia sheria bora.

Amesema anaishukuru serikali ya awamu ya sita walau imeboresha baadhi ya sheria na kanuni na imefungua milango ya majadiliano zaidi ili kuboresha uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza.



SAGCOT kuinua kilimo cha viazi mviringo

$
0
0

Na Mwandishi Wetu, Songea

KITUO cha Kuendeleza Kilimo Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) kimeulezea Mkoa wa Ruvuma kama ni eneo lenye ardhi nzuri inayofaa zaidi kwa uzalishaji wa kilimo cha viazi mviringo na kuinua maisha ya wakazi mkoani humo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Lusitu Agro-Business, Benno Mgaya amesema taasisi yake kwa kushirikiana na SAGCOT walipima udongo maeneo mbalimbali ya Wilaya za Songea, Namtumbo na Halmashauri ya Madaba na kubaini kuwa kuna ardhi nzuri yenye rutuba inayofaa kwa kilimo cha viazi mviringo.


“Kuna maeneo mbalimbali ambayo tumeyaainisha na tayari tumeshaanzisha mashamba darasa kwa mfano shamba letu la kwanza lilikuwa katika Kijiji cha Sirikano, Kata ya Liganga, Wilaya Songea tukianzia mbegu za viazi mviringo tani 100 tu,”amesema Mgaya,

Kwa mujibu wa Mgaya maeneo mengine ambayo mashamba darasa yapo katika Wilaya ya Songeni ni Peramiho, Litapwasi na Namatuhi. Kwa upande Wilaya ya Namtumbo shamba darasa limeanzishwa eneo la Mtyangimbole ambapo kwa Halmashauri ya Madaba lipo Shule ya Tanga Stendi.

“Ubora wa ardhi katika maeneo haya unamwezesha mkulima kupata mazao kati ya tani 20 hadi 25 kwa hekari moja,” amesema na kuengeza kuwa Ruvuma kwa siku za mbeleni utakuwa miongoni mwa mikoa itayoongoza kwa ulishaji wa viazi mviringo.

Amesema zao la viazi linaweza kulimwa katika misimu yote ya mwaka na hivyo kumwezesha mkulima kuwa fedha za kutosha mwaka mzima kwani kilimo cha viazi mviringo kitafanyika wakati wa masika na wa kiangazi kwa kufanya kilimo cha  umwagiliaji.

Akizungumzia kuhusu viazi mviringo, Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT,  Geoffrey Kirenga ambaye ni Bwana shamba mbobezi amesema Ruvuma ipo katika nafasi nzuri ya kuweza kubadilisha maisha ya wananchi endapo watachukulia kilimo cha viazi mviringo kwa uzito wake.

“Kama SAGCOT tupo mstari wa mbele kuhakikisha kuwa zao la viazi mviringo katika Wilaya Songea linakuwa na mafanikio na kuleta mafanio chanya katika kubadilisha maisha ya wakulima,”  amesema Kirenga.

Utafiti uliofanywa na SAGCOT Wilaya ya Songea kuanzia mwaka 2020 hadi 2024 umebaini kuwa viazi mviringo vimetoka matokeo mazuri katika uzalishaji ambapo hekari moja inaweza kuingiza hadi zaidi ya Sh milioni 10.

Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Mjini, Michael Mbano amesema mara ya kwanza aliambiwa kwamba hekari moja ya viazi inawezakulisha gunia 200 za viazi hakuamini mpaka pale alipojioonea mwenyewe.

“Kwa sasa nimeamini pale Mheshimiwa Rais anaposema ajira nyingi zipo shambani ninaungana naye pasipo shaka. Nawashukuru sana SAGCOT na wadau wake kwa kutufungua macho na kutuonyesha fursa iliyojificha,” amesema Meya Mbano.

SAGCOT imekukuwa muhimili mkubwa katika kuchocheo maendeleo ya kilimo biashara kwa kuwaunganisha wakulima wadogo na kati kwa kutoa mafunzo sambamba kuwaunganisha na taasisi za kifedha na masoko ya uhakaki kwa mazao yao.

BILIONI 346 KUTUMIKA KUIMARISHA USALAMA WA MILKI ZA ARDHI - MAJALIWA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma hotuba ya kuahirisha Bunge jijini Dodoma, Juni 28, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

 

 Dodoma, Tanzania

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imesaini mkataba wa sh. bilioni 346 na Benki ya Dunia kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi ambao unalenga kuimarisha usalama wa milki za ardhi na kuwezesha miundombinu ya usimamizi wa ardhi nchini.


Amesema mkataba huo uliosainiwa Februari, 2022 ni wa mradi ambao unatekelezwa kwa miaka mitano (2022/2023 - 2026/2027) katika Halmashauri 67 na Mikoa 26. Mradi huo una vipengele vinne ambavyo ni kuongeza usalama wa milki za ardhi kwa njia ya urasimishaji kwa kutoa Hatimiliki 1,000,000 katika maeneo ya mijini na Hatimiliki za Kimila 500,000; kuimarisha mifumo ya taarifa za ardhi; kujenga miundombinu ya ardhi; na usimamizi wa mradi.
 
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Juni 28, 2024) wakati akitoa hotuba ya kuahirisha mkutano wa 15 wa Bunge jijini Dodoma.  Bunge limeahirishwa hadi Agosti 27, mwaka huu.

Akielezea mradi huo, Waziri Mkuu amesema hadi kufikia Juni 15, mwaka huu, kazi zilizotekelezwa ni pamoja na urasimishaji wa vipande vya ardhi 62,200 katika Halmashauri mbalimbali; usimikaji wa alama za msingi za upimaji 327 katika Halmashauri 26; upimaji, uhakiki mipaka ya vijiji na uandaaji wa Vyeti vya Ardhi ya Vijiji 843 katika Halmashauri 21; uandaaji wa Hatimiliki za Kimila 381,509.

"Mradi umewezesha kununuliwa magari 18 ambayo yanatumika kwenye maeneo mbalimbali nchini na taratibu za ununuzi wa magari mengine 52 zinaendelea na yanatarajiwa kuwasili Septemba, 2024. Hatua hii itapunguza changamoto kubwa ya usafiri iliyopo katika sekta ya ardhi," amesema.

Waziri Mkuu amezitaka Mamlaka za Upangaji Miji chini ya Uratibu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ziendeleze kasi ya utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi kwa ufanisi ili fedha zilizopangwa kutumika kwenye mradi huo ziwe na tija.

Amezitaka pia, zipunguze migogoro kupitia uhakiki na upimaji wa mipaka ya vijiji; Maandalizi ya mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji; kuandaa Mipangokina ya vijiji na kuandaa Hati za Hakimiliki za Kimila; kurasimisha vipande vya ardhi; kubadilisha nyaraka za ardhi kutoka analojia kwenda kidijitali; na kusanifu na kusimika vituo vya kieletroniki vya upimaji. "Nitoe wito kwa wananchi, hususan wa maeneo ya vijijini kuchangamkia fursa ya uwepo wa mradi huo kwa kurasimisha maeneo yao."

Kuhusu malipo ya fidia ya ardhi kwenye maeneo yanayotwaliwa na Serikali kwa ajili ya uwekezaji, Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kutwaa maeneo hayo kwa ajili ya miradi yenye manufaa ya umma ikiwemo ujenzi wa barabara, viwanja vya ndege na uchimbaji wa madini.

"Serikali inatambua kuwa kwa nyakati tofauti kumekuwepo na malalamiko ya wananchi kucheleweshewa malipo ya fidia katika baadhi ya maeneo. Katika kuhakikisha kuwa malalamiko haya yanatatuliwa, nazielekeza taasisi zote zihakikishe kuwa zinatenga fedha katika bajeti zao kwa ajili ya kulipa fidia kabla ya kuanza zoezi la utwaaji kama inavyoelekezwa katika Waraka wa Uthamini na Fidia Na. 1 wa mwaka 2024," amesisitiza.


WAZIRI MKUU: SERIKALI YATENGA SH. BILIONI 787 ZA MIKOPO YA WANAFUNZI

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema katika mwaka 2024/2025, Serikali imetenga kiasi cha sh. bilioni 787 kwa ajili ya kukopesha wanafunzi 250,000 wakiwemo 80,000 wa shahada ya kwanza ambao ni wapya.

"Maandalizi ya awali yameanza ikiwa ni pamoja na kusambaza mwongozo wa upangaji na utoaji mikopo; kufungua dirisha la uombaji mikopo kwa mwaka 2024/2025 kwa muda wa siku 90 kuanzia tarehe 1 Juni hadi 31 Agosti, 2024; kutoa elimu kwa waombaji mkopo na wadau wengine," amesema.

Ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Juni 28, 2024) bungeni jijini Dodoma, wakati akitoa hotuba ya kuahirisha mkutano wa 15 Bunge. Bunge limeahirishwa hadi Agosti 27, mwaka huu.

Amesema katika mwaka wa fedha 2023/2024, Serikali ilitoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu 224,056 na hadi kufikia Juni, 2024 wanafunzi hao walikuwa wamepatiwa mikopo yenye thamani ya sh. bilioni 743.2 sawa na asilimia 94.6 ya fedha zilizotengwa.

Mikopo hiyo ilitengwa kwa ajili ya wanafunzi wa ngazi ya stashahada, shahada ya awali, stashahada ya juu ya mafunzo ya Sheria kwa vitendo, shahada za umahiri na uzamivu, na ufadhili wa Samia (Samia Scholarships) katika masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati.

Kuhusu urejeshaji mikopo hiyo, Waziri Mkuu amesema Bodi ya Mikopo imeendelea kukusanya mikopo iliyoiva kutoka kwa wanufaika wa mikopo. "Kwa mwaka 2023/2024, Serikali ilipanga kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 230 ambapo hadi kufikia Mei 2024, shilingi bilioni 161 zilikusanywa sawa na asilimia 70 ya lengo."

Ili kuimarisha ukusanyaji wa mikopo, Waziri Mkuu amesema Serikali imeweka mikakati kadhaa ikiwemo kuwakumbusha waajiri kuwasilisha majina ya wanufaika ndani ya siku 28 baada ya kuwaajiri; kushirikiana na kuunganisha mifumo na wadau wa kimkakati kama vile NIDA, TRA, taasisi binafsi za ndani na nje ya nchi; kufanya kampeni za kuwafichua wanufaika; kutoa elimu kupitia mitandao ya kijamii; na kufanya kaguzi kila mwezi kwa waajiri wa sekta ya umma na binafsi.

Katika hatua nyingine, akielezea utaratibu wa mikopo inayotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri, Waziri Mkuu amesema Serikali imekamilisha maandalizi ya uratibu wa upelekaji wa fedha za mikopo ya asilimia 10 katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenda kwenye mfuko wa mikopo ya vikundi na kusimamia urejeshwaji wa mikopo iliyotolewa miaka ya nyuma.

"Itakumbukwa kwamba mwezi Aprili 2023, Serikali ilisitisha utoaji wa mikopo wa asilimia 10 kwa ajili ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu wa fedha 2023/2024, Serikali imekamilisha maandalizi ya uratibu wa upelekaji wa fedha za mikopo ya asilimia 10 katika mamlaka za serikali za mitaa kwenda kwenye mfuko wa mikopo ya vikundi na kusimamia urejeshwaji wa mikopo iliyotolewa miaka ya nyuma."

Waziri Mkuu amesema katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali imepanga kutoa mikopo ya sh. bilioni 228 ambapo kati ya hizo, sh. bilioni 63.7 ni fedha za marejesho zilizokuwa zikiendelea kukusanywa kutokana na mikopo iliyotolewa kabla ya kusimamishwa Aprili, mwaka jana; sh. bilioni 63.2 ni fedha zilizokuwa zinatengwa kwa ajili ya mikopo na sh. bilioni 101.1 ni fedha ambazo zimetengwa kutokana na makisio ya makusanyo ya mapato ya ndani ya mwaka 2024/2025.

Akitoa ufafanuzi, Waziri Mkuu amesema Serikali imepanga utaratibu wa kutumia benki kwa Halmashauri 10 za majaribio ambazo ni Majiji ya Dar es Salaam na Dodoma, Manispaa za Kigoma Ujiji na Songea, Miji ya Newala na Mbulu, Wilaya za Siha, Nkasi, Itilima na Bumbuli.

Amesema, halmashauri 174 zilizobaki zitatumia utaratibu ulioboreshwa ikiwemo uanzishwaji wa kitengo cha usimamizi wa mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika Ofisi ya Rais - TAMISEMI, na uanzishwaji wa kamati za usimamizi wa mikopo katika ngazi za Ofisi za Wakuu wa Wilaya, Halmashauri na Kata.



NMB Sabasaba kuhudumia Waoneshaji 3,000, Wananchi 800,000 kwa siku 16

$
0
0

 
Kaimu Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa Benki ya NMB  Ferdinard Mpona (kushoto) akitoa huduma kwa baadhi ya wateja waliofikia kwenye tawi dogo la NMB lililopo kwenye maonyesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea kuanzia leo hadi tarehe 13 Julai. Benki ya NMB imefungua milango yake kuhudumia wateja na kampuni mbali mbali watakahuduria na kushiriki kwenye maonyesho haya ya Saba Saba.

 

NA MWANDISHI WETU

 

BENKI ya NMB imefungua tawi lake katika Viwanja vya Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba, huku ikiahidi utayari wa kuhudumia kwa ufanisi wateja wake, pamoja na waoneshaji zaidi ya 3,000 wanaoshiriki maonesho hayo na wananchi zaidi ya 800,000 wanaokisiwa kuhudhuria.

 

Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi Ijumaa ya Juni 28 na yanatarajia kufungwa Julai 13, ambako tawi hilo na mawakala zaidi ya 35, watatoa huduma kedekede za kifedha, pamoja na Malipo na Tozo za Serikali, Kodi za Mabanda ya Maonesho, Hati za Ardhi, Leseni na TRA kwa siku zote 16.

 

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa tawi hilo, Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Ferdinand Mpona, alisema NMB Sabasaba ni tawi kamili litakalohudumia maelfu ya waoneshaji na wahudhuriaji wa maonesho hayo yanayofanyika chini ya kaulimbiu; Tanzania, Mahali sahihi kwa Biashara na Uwekezaji.

 

   “Tuko tayari kuhudumia waoneshaji wote zaidi ya 3,000 na zaidi ya wananchi watakaohudhuria wanaokisiwa kufikia 800,000, wataalamu wetu watakuwa hapa kutoa masuluhishi mbalimbali ya kifedha ikiwemo ufunguzi wa akaunti na huduma zetu Bima, KilimoBiashara na Malipo ya Kodi na Tozo za Serikali.

 

“Tunawakaribisha kufungua akaunti nafuu ya NMB Pesa kwa Sh. 1,000 tu, NMB Kikundi inayojumuisha wana vikundi, NMB Jiwekee maalum kwa akiba ya baadaye, huku pia tukitoa huduma za Malipo ya Kiserrikali, hasa ukizingatia tunaelekea kufunga Mwaka wa Fedha na kufungua mwaka mpya.  

 

“Tunapoelekea kufunga Mwaka wa Fedha wa 2023/24 na kufungua Mwaka Mpya wa 2024/25, kunakuwa na uhitaji mkubwa wa Huduma za Malipo ya Serikali, NMB Sabasaba tunawakaribisha wote kulipia tozo mbalimbali, Hati za Ardhi, Leseni za Biashara na Kodi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),” alisema Mpona.

 

Aliongeza ya kwamba, hakuna haja ya wateja wao na wananchi kutembea na pesa taslimu mkononi kutokea majumbani, badala yake watapata huduma hizo katika Tawi la NMB Sabasaba na mawakala kibao waliotapakaa katika viwanja hivyo kuthibitisha kwa vitendo kaulimbiu ya NMB Karibu Yako.

 

“Aidha, kuna fursa mbalimbali za uwekezaji, kama ambavyo kaulimbiu ya maonesho haya inavyosema; ‘Tanzania Sehemu Bora kwa Biashara na Uwekezaji, kwa hiyo tutakuwa na wataalamu mbalimbali wanaohusika na elimu ya mikopo ya uwekezaji kwa wafanyabiashara na wawekezaji wengine,” alisisitiza Mpona.

 

Katika Viwanja vya Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara, Tawi la NMB Sabasaba linapatikana kwenye Banda namba 24C, lililopo makutano ya mitaa ya Mabalozi na Carnivore, pembezoni mwa Banda la Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo Tanzania (SIDO).

 

 

RAIS WA APIMONDIA APONGEZA UZURI WA HIFADHI YA NGORONGORO; ASEMA NI UZOEFU USIOSAHAULIKA

$
0
0

Na Mwandishi wa NCAA

Rais wa Shirikisho la wafugaji Nyuki Duniani (Apimondia), Dkt. Jeff Petiz, ametembelea eneo la hifadhi ya Ngorongoro na kutoa pongezi kwa uongozi wa NCAA kwa jitihada za utunzaji wa hifadhi hiyo ya kipekee duniani ambayo imeendelea kuvutia maelfu ya watalii.



Akizungumza kwa furaha na mshangao, Dkt. Petiz amebainisha  kuwa hajawahi kuona sehemu nzuri kama Kreta ya Ngorongoro maishani mwake baada  wa kuona wanyama  wakubwa maarufu kama  Big Five ambao ni faru, tembo, Simba, Chui, Nyati na wengineo ndani ya mda mfupi wakiwa katika eneo moja wakiwa kwenye mazingira yao ya asili.

"Hakika nimepata uzoefu usiosahaulika maishani mwangu, kuona eneo la pekee lililotunzwa na kuwepo wanyama wa kila aina na kushuhudia idadi kubwa ya wageni ni jambo la kupendeza na hakika eneo hilo kila mmoja anapaswa kulitembelea katika uhai wa maisha yake" alisema Dkt. Petiz.

Kwa upande wake Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo aliyembatana na mgeni huyo ameipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuhifadhi eneo hilo mashuhuri duniani katika nyanja za utalii, uhifadhi na utamaduni pamoja na kupambana na mimea vamizi na kutoa rai kwa taasisi nyingine za uhifadhi kujifunza kutoka kwa Ngorongoro ili kubadilishana uzoefu.

Ziara hiyo imefanyika katika Kreta ya Ngorongoro ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mkutano wa kimataifa wa wadau wa nyuki (Apimondia) utakaofanyika mwaka 2027, ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano huo mkubwa unaotarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 6,000 kutoka mataifa mbalimbali.

Katika ziara hiyo Dkt. Petiz ameambatana na Rais wa Kamisheni hiyo kanda ya Afrika , Bw. David Mukomana.



MSOGA MARATHON YAFUNGUA MILANGO KWA WANARIADHA

$
0
0

NA TULLO CHAMBO, RT

MSIMU wa Kwanza wa Mbio za Msoga Half Marathon 2024, umefanyika kwa mafanikio makubwa huku Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete akifungua milango kwa wanariadha wa Tanzania kujifua Msoga, Chalinze mkoani Pwani.

Rais mstaafu Kikwete almaarufu JK, alitanabaisha hayo mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo kwenye Uwanja wa Mpira wa Msoga, mwishoni mwa wiki.


Katika mbio hizo zilizoshirikisha washiriki zaidi ya 2000, JK alishiriki mbio za Km. 5 sambamba mkewe ambaye ni Mbunge wa Mchinga mkoani Lindi, Salma Kikwete, Mbunge wa Chalinze na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Ridhiwani Kikwete, Mbunge wa Rombo na  Waziri wa Elimu, Prof. Adolph Mkenda na viongozi mbalimbali wa kiserikali na kisiasa.



Rais Mstaafu Kikwete, alitoa fursa kwa wanariadha kwenda Msoga kujifua kwa mazoezi na yuko tayari kuwasaidia.


JK alieleza kufurahishwa na mwanzo wa mbio hizo zilizokuwa na lengo la kuchangia afya ya mama na mtoto kwenye hospitali ya Msoga.


Aidha, JK alikoshwa na idadi kubwa ya washiriki na kwamba hakutegemea.


Katika Km. 21 wanawake mshindi aliibuka Sara Ramadhan wa Arusha akitumia saa 1:10:29 na Failuna Matanga 1:12:12 pia wa Arusha huku nafasi ya tatu ikienda kwa Angel John wa Singida saa 1:12:28:73.


Wanaume, mshindi aliibuka Joseph Panga wa JWTZ saa 1:02:06 wa pili Dickson Paulo wa Mwanza saa 1:02:55 wakati Josephat Gisemo wa Polisi Arusha akitumia saa 1:03:30 nafasi ya tatu.
 Km. 10 kwa wanawake, kinara aliibuka Elizabeth Ilanda aliyetumia dakika 37:59 akifuatiwa na  Sarah Hhiitii dakika 38:07 wote kutoka Arusha huku Warda Shaban wa Singida akikamata nafasi ya tatu dakika 39:25.


Wanaume, Jumanne Mnada wa Arusha alishinda akitumia dakika 31:25 akifuatiwa na Inyasi Sulle dakika 31:41:58 na Marco Silvester nafasi ya tatu 31:53:16 wote wa JWTZ.


Kwa upande wake, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, alisema Msoga Half Marathon imeanza kwa mafanikio makubwa katika kutimiza lengo la kusaidia afya ya mama na mtoto na kwamba itakuwa endelevu.


Alisema, Msoga ni kitovu cha Halmashauri ya Chalinze ambako hospitali ya wilaya inajengwa.
"Uwepo wa hospitali hii ndio umechangia kufanyika kwa mbio za Msoga Marathon ambazo zinawakusanya wadau kuchangia huduma ya mama na mtoto hospitalini hapo.


Mratibu wa mbio hizo, Nelson Mrashani kutoka Rhino Sports Talent, alisema muitikio wa washiriki umekuwa mkubwa kwa wakimbiaji msimu huu wa kwanza.


Mrashani, aliwashukuru wadau na wadhamini wote kwa kufanikisha mbio hizo kwa kiwango bora.
Aidha, Mratibu hiyo aliwaomba radhi washiriki kwa changamoto zilizojitokeza na kwamba maoni yote yatafanyiwa kazi kuongeza ufanisi mbio ijayo.


NHIF IKO KITAANI KWAKO MBAGALA WEMEITIKA

$
0
0

Kaimu Meneja wa NHIF Ofisi ya Mkoa wa Temeke, Canon Luvinga akiwahamasisha Wananchi kujiunga na bima ya afya kwenye wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya NHIF Kitaani Mwako katika viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam. NHIF IKO KITAANI  KWAKO MBAGALA WEMEITIKA

Wananchi wakifuatilia.

Meneja wa NHIF Ofisi ya Mkoa wa Kinondoni Dkt. Raphael Mallaba (wapili kulia) akiwa na Meneja wa NHIF Ofisi ya Ilala Dkt. Aifena Mramba wakitoa elimu kwa wakaazi wa mtaa wa zakhem wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya NHIF KITAANI MWAKO iliyozinduliwa jana ktk viwanja vya Zakhem jijini dar es salaam jana. (Na Mpiga Picha Wetu).





Na Mwandishi Wetu

 

Wananchi tambueni  kuwa  kukata bima ya afya SI tu pale unapougua au ndugu anapougua ndiyo tufikirie kuja NHIF.. yamesemwa na kaimu meneja wa mfuko wa bima ya afya Mkoa wa Temeke, Canon Luvinga wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya uhamasishaji Wananchi kujua faida na umuhimu wa kujiunga na bima ya afya katka viwanja wa Mbagala Zakhem jijini Dar es salaam
Huu ni mkakati endelevu  wa  kuwafikia Wananchi kwenye Kila tarafa za wilaya, kwani kuelimika ni jambo la kwanza na kufanya maamuzi ya kujiunga ni hatua nyingine, kwani tumebaini wananchi wengi Wana uelewa mdogo kuhusu bima ya afya. alisema.


Unakuta ndugu anakuja ofisini kuuliza gharama za kuliipia bima ya afya wakati huo huo anakwambia huyu ni mgonjwa na tumejipiga hata hivyo tunaenda kuuza kiwanja Ili tumkatie bima ya afya,hili nalo limetusukuma kutoka ndani ofisini na kuja kumuelimisha mwananchi asiingie kwenye umasikini kwa sababu ya maradhi hili hali bima ya afya ipo..alisema.

 
Ni mafanikio makubwa kwetu kupata idadi kubwa ya Wananchi waliojitokeza kushiriki uzinduzi wa kampeni hii kwani takribani watu 800 walihudhuria,mbali ya elimu pia huduma za upimaji  afya Bure kwenye magonjwa yasiyoambukiza zilitolewa na madaktari kutoka nhif ,ambapo watu 380 waliweza kupima afya zao kati yao 30 walibainika kuwa na dalili za magonjwa ya kisukari na presha hivyo walishauriwa kuhudhuria kwenye vituo vilivyo karibu kwa ufuataliliaji.


Hata hivyo watu 70 waliweza kusajiliwa papo kwa papo.alisema Kaimu Meneja. 


Tumedhamiria kama  ofisi ya Temeke ni kuhakikisha mwananchi anafahamu vyema faida na umuhimu wa kujiunga na bima ya afya kwani tumeona Kuna ombwe kubwa la uelewa kuhusu bima ya afya hivyo Mimi na timu yangu tumejipanga kutokukaa ofisini bali kwenda mtaani mwananchi aone ipo haja ya kujiunga na ukizingatia serikali inakuja na mpango wa bima ya afya kwa wote hii itasaidia kujenga uelewa zaidi.


Nao Wananchi walioshiriki wamekiri kuwa huu ni mpango mzuri kwani tulio wengi tunaona bima ya afya ni gharama kubwa lakini kwa elimu tuliyoipata kwanza tunaweza kubana vipato vyetu kwa kudunduliza na kuweza kulipia bima ya afya kwani tumeambiwa unalipa mara moja unapata huduma mwaka mzima.

SERIKALI KUWANUSURU KIUCHUMI WARAIBU WA DAWA ZA KULEVYA - MAJALIWA

$
0
0

*Azindua Sera ya Taifa ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameziagiza Wizara za Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu zikae pamoja na Wizara ya Fedha na kuandaa mpango wa kitaifa wa kuwawezesha kujikimu vijana wanaoachana na matumizi ya dawa za kulevya nchini.

Amesema kutekelezwa kwa agizo hilo kutawawezesha vijana hao kupata mitaji ambayo itawawezesha kushiriki kwenye shughuli za ujasiriamali ambazo zitawasaidia kukuza kipato chao.

Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Juni 30, 2024) wakati akizungumza na wananchi na wadau mbalimbali walioshiriki kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Nyamagana, jijini Mwanza.

“Wako wengine wanaohitaji kilimo, Wizara ya Kilimo itoe utaratibu; wapo wanaohitaji ufundi, Wizara ya Elimu itoe utaratibu, lengo ni kuhakikisha vijana hawa wakitoka huko wanakuwa na shughuli ya kufanya ili kujikimu.”

“Kamishna Jenerali pamoja na timu yako ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya endeleeni kufanya operesheni dhidi ya dawa za kulevya kwenye mabasi, ndege, bandarini, vituo vya reli, masoko, maeneo yenye watu wengi, kote nchini ili kuhakikisha kuwa tunaendelea kubaki salama.”

“Niwahimize wananchi wote wakiwemo wazazi, walezi, viongozi wa dini na taasisi za afya, tuendelee kupiga vita dawa za kulevya kwa vitendo na kuhakikisha jamii yetu haijihusishi na biashara, haifanyi uzalishaji wala matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo kutokomeza kilimo cha bangi na mirungi,” amesisitiza.

“Sote tunao wajibu wa kuwafundisha watoto wetu namna bora ya kuishi kwa kufuata maadili na kujiepusha na tabia na makundi rika yanayoweza kuwashawishi kuingia kwenye janga la matumizi na biashara ya dawa za kulevya,” amesema.

Pia ametoa pongezi kwa viongozi wa taasisi hiyo kwa jitihada zilizofikiwa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ambapo hadi sasa Serikali imefanikiwa kujenga zaidi ya vituo 16 vinavyohudumia waraibu 16,460 kutoka vituo vitatu vilivyokuwepo mwaka 2017.

“Leo hii ni siku muhimu sana katika historia ya Taifa letu kwani tutashuhudia uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ya Mwaka 2024. Mheshimiwa Waziri amesema pia sera hii mpya inaweka msisitizo kwenye jukumu la kila mmoja wetu kuanzia ngazi ya kaya hadi taasisi za Serikali na asasi za kiraia. Hivyo, napenda kuwahimiza sote tujitolee kikamilifu kutekeleza Sera hii ya Taifa. Tuwe walinzi wa vijana wetu na tukishirikiana, tunaweza kufanikisha lengo la kuwa na jamii salama na yenye afya njema.”

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama amesema Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia imefanya uwekezaji mkubwa ikiwemo ununuzi wa mashine kubwa na ya kisasa yenye kufanya uchunguzi wa haraka wa viashiria vyote vinavyotakiwa kupatiwa sampuli na kuthibitisha uwepo wa matumizi ya dawa za kulevya.

Amesema mashine hiyo iliyopo kwenye maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imepata ithibati ya Umoja wa Mataifa na ina uwezo wa kuchukua zaidi ya sampuli 250 kwa saa 24.

Mapema, Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo amesema katika kipindi cha Juni, 2023 hadi Mei 2024, Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na vyombo vingine imefanikiwa kukamata zaidi ya kilo milioni mbili za dawa ya kulevya kiasi ambacho ni kikubwa kukamatwa katika kipindi miaka 11.

Aidha, Kamishna huyo amesema kuwa juhudi na dhamira ya dhati ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini imeiwezesha Tanzania kuwa moja ya nchi kinara na mfano wa kuigwa duniani katika kukabiliana na matumizi ya dawa za kulevya.

Rais Samia achangia Milioni 50 Ujenzi wa Madarasa

$
0
0


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa mashindano ya kusoma Kurani,Ismail Khalid (kushoto),yaliyofanyika wakati wa Hafla ya Kumbukumbu ya Kusheherekea kuanzishwa kwa Taasisi ya Maawal Islamiy na kumbukumbu ya Muanzilishi, Sheikh Shabaani Mohamed Hariri.Hafla hiyo imefanyika jijini Tanga ambapo Waziri Masauni alialikwa kuwa mgeni rasmi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Na Mwandishi Wetu, Tanga

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Shilingi Milioni Hamsini katika Ujenzi wa Majengo ya Taasisi ya Elimu ya Maawal Islamiya iliyopo jijini Tanga ikiwa ni muendelezo wa Serikali wa Awamu ya Sita kuunga mkono jitihada za wadau katika kutoa elimu.

Kiasi hicho cha fedha kimewasilishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati akihutubia mamia ya waumini wa kiislamu waliokusanyika kusheherekea kuanzishwa kwa taasisi hiyo na kumbukumbu ya Muanzilishi,Sheikh Shabaani Mohamed Hariri ambapo pia alifikisha salamu kwa waumini hao kutoka kwa Rais Samia huku akigusia kuwepo kwa mporomoko wa maadili unaosababisha uhalifu katika sehemu mbalimbali za nchi.

Naomba nitumie fursa hii kuwasilisha salamu za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan wakati nakuja nilimuaga amesema niwasalimie sana na ametoa kiasi cha Shilingi Milioni Hamsini ikiwa ni mchango wake katika ujenzi wenu wa majengo ya madarasa unaoendelea hapa niwaombe pia mumuombee dua ili aweze kuiongoza nchi yetu kwa salama na amani lakini kumekuwepo na mmomonyoko wa maadili niwaombe viongozi wa dini muendelee kutumia  sehemu zenu za ibada kuiasa jamii iachane na mila na tamaduni ambazo zipo kinyume na mafundisho ya dini zetu’ alisema Waziri Masauni

Wakizungumza wakati wa hafla hiyo,Sheikh wa Mkoa wa Dodoma,Mustafa Rajab Shabaani na Sheikh wa Mkoa wa Pwani,Alhaji Khamis Mtupa walisisitiza kulindwa kwa maadili katika jamii ambayo yameendelea kuporomoka katika jamii huku wakiwataka waumini kuendelea kuwa karibu na watoto ili kufahamu changamoto mbalimbali wanazokutana nazo.

‘Jamii imekumbwa na mabalaa mbalimbali watu wamekua na unyama usiomithilika mpaka imefikia sasa hivi wazazi kuambiwa kuwakagua watoto katika maumbile yao kila wanapotoka shuleni sasa tuitake jamii iwe karibu na watoto ili kuweza kubaini changamoto zao mbalimbali wanazokutana nazo kwani kutokua nao karibu upelekea watoto hao kukumbana na mabalaa lakini kutokuwepo ukaribu kati ya mzazi na mtoto upelekea mtoto kukaa kimya wakati tayari ashaathirika.’alisema Sheikh Mtupa.

Taasisi hiyo ya Maawal Islamiy ina miaka 44 tangu ianzishwe na Sheikh Shabaan Hariri ikijikita zaidi katika kutoa elimu,misaada kwa watu mbalimbali wenye uhitaji na huduma za afya.

WAJASIRILIAMALI WAIOMBA SERIKALI KUWAPATIA ELIMU YA UJASIRIAMALI

$
0
0

NA: JOSEPHINE MAJULA, WF, TABORA

 

Wajasiriamali wa Kata ya Tutuo, Wilaya ya Sikonge Mkoa wa Tabora, wameiomba Serikali kuwapatia elimu ya ujasiriamali ili waweze kuzalisha bidhaa zenye ubora, ambazo zitakidhi ushindani wa soko ili kujikwamua kiuchumi.

 

Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Wajasiriamali Kata ya Tutuo, Wilaya ya Sikonge Mkoa wa Tabora, Bi. Doroth Mgombela, alipokutana na Timu ya Wataalamu ya Wizara ya Fedha ambayo ilifika wilayani humo, kutoa elimu ya fedha kwa Wananchi ili waweze kutumia fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya fedha kujikomboa kiuchumi.

 

“Tunaomba tupatiwe elimu ya ujasiriamali ili bidhaa zetu ziwe na mwonekano mzuri, ambao utamvutia mnunuzi lakini pia ziweze kukubalika katika soko la ndani na nje ya nchi ili kipato chetu kiweze kukua,” alisema Bi. Doroth Mgombela.

 

Aliongeza kuwa changamoto wanayokutana nayo katika shughuli ya ujasiriamali ni bidhaa kutokidhi mahitaji ya soko, lakini pia wanatumia njia za kienyeji kutengeneza bidhaa zao ambapo wanatumia muda mwingi kuzalisha bidhaa chache lakini pia kutokuwa na uhakika wa soko kutokana na bidhaa hizo kukosa ubora.

 

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mkoa wa Tabora, Bi. Katoke Kisigiro, aliipongeza Wizara ya Fedha kwa kuwafikia wananchi wa makundi mbalimbali wakiwemo wanavikundi, wajasiriamali, watumishi, wanafunzi na wafugaji, aliahidi kuendelea kuwasimamia na kuhakikisha wanaitumia vizuri elimu ya fedha katika shughuli zao za kiuchumi na kujiongezea kipato kwa kujiwekea akiba, kufanya uwekezaji mbalimbali lakini pia kukopa mahali sahihi.

 

Naye Afisa Mtendaji Kata ya Tutuo Wilaya ya Sikonge, Bw. Alexander Mushongi, aliishukuru Serikali kwa kuweza kuwafikia na kuwapa elimu muhimu ya fedha itakayokuwa mkombozi kwa wananchi na anaamini kupitia elimu waliyoipata wananchi hao watafanya uwekezaji kwenye shughuli ambazo zitawaingizia kipato na kuwainua kiuchumi wao na Taifa kwa ujumla.

 

Kwa upande wake, Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Limi Bulugu, alisema kuwa katika maeneo mbalimbali waliyofika kutoa elimu kwa wananchi, mwitikio ulikuwa mkubwa na wananchi wameonesha utayari wa kubadilika na kuahidi kutumia taasisi rasmi kukopa, kuwekeza na kuanza kujiwekea akiba.

 

“Tunawashukuru na kuwapongeza Wananchi wa Mkoa wa Tabora kwa kujitokeza maeneo mbalimbali kupata elimu ya fedha maana bila wao kufika zoezi letu lisingefanikiwa, kwa upande wa maoni na ushauri tunaahidi kuyazingatia awamu ijayo”, Bi. Limi Bulugu.

 

Alisema hadi sasa mikoa nane imefikiwa na Timu ya Wataalamu ya Wizara ya Fedha na kupatiwa elimu ya fedha ikiwemo mkoa wa Kagera, Manyara, Singida, Kigoma, Rukwa, Simiyu, Shinyanga na Tabora.

 


Rais Dkt. Samia ampokea rasmi Msigwa wa CHADEMA

$
0
0

 

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akipeana mkono na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa ambaye amejiondoa kutoka chama hicho na kujiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Juni 30, 2024, jijini Dar Es Salaam.

Msigwa amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuona Chadema kimepoteza uhalali wa kuwa mkosoaji wa CCM, lakini pia kuunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa anayofanya ya kuiongoza nchi na kuwatumikia Watanzania. Pia baada ya kuchoshwa na siasa za uongo, unafiki na kiulaghai zinazofanywa na Chadema.






WALIOTAFUNA FEDHA ZA MIKOPO YA HALMASHAURI SINGIDA KUSAKWA

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego akizungumza kwenye kikao Maalum cha kujadili hoja za CAG katika Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Singida.

 

Na Mwandishi Wetu

 

Serikali ya mkoa wa Singida imewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Polisi wa Wilaya mkoani humo kuwasaka na kuwakamata watu wote waliochukua mikopo ya asilimia 10 kwenye Halmashauri na kushindwa kuirejesha bila sababu za msingi.


Mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego, ametoa kauli hiyo katika kikao cha Baraza la Halmashauri ya Wilaya ya Iramba cha kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Rc Dendego ametoa mfano kwa Halmashauri ya Iramba pekee zaidi ya Milioni 118 hazijarejeshwa mpaka sasa na kusisitiza kuwa tatizo lazima litafutia ufumbuzi kwa wahusika kukamatwa ili warejeshe mikopo hiyo.
“Nataka Dc na OCD muwasake popote walipo watu waliokopeshwa fedha hizo ili wazirejeshe ili wananchi wengine wakopeshwe,” Amesisitiza Dendego.
Ametaka wote wataokamatwa katika oparesheni hiyo wawekwe kizuizini na wasiachiwe mpaka hapo watakapolipa fedha hizo walizokopeshwa.
Mkuu huyo wa mkoa pia amewaagiza Maafisa Maendeleo ya Jamii mkoani humo washirikiane na Viongozi wengine katika kusaka Vikundi vilivyokopeshwa fedha hizo na kuzirejesha haraka vinginevyo tutazuia mishahara yao mpaka Vikundi hivyo vilipe fedha hizo kwa sababu wao wanavijua vikundi hivyo.
Naye, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Innocent Msengi, ameunga mkono hoja ya wanachama wa vikundi vilivyokopeshwa fedha za Halmashauri kusakwa ili warejeshe fedha hizo.
Msengi amesema fedha hizo zinazodaiwa ni nyingi hivyo lazima nguvu ya ziada itumike ili kuhakikisha waliokopeshwa wanazirejesha ili wananchi wengine waweze kunufaika na mikopo hiyo.
Mwenyekiti huyo pia amemshukuru Rais Samia kwa kuipatia Halmashauri hiyo zaidi ya shilingi Bilioni Tatu kwa ajili ya kutelekeza miradi mbalimbali ya maendeleo hasa katika sekta za afya na elimu.

 

Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba  kikiendelea.

IMEBAKI STORI KWA WANA SIMBA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
 
Clatous Chota Chama amekuwa kwenye rekodi ya wachezaji waliocheza klabu mbili kubwa nchini za Simba na Yanga baada ya uhamisho wake kukamilika rasmi hii leo kuelekea Jangwani.

Chama anaungana na Haruna Niyonzima, Emanuel Okwi, Benard Morrison, Juma Kaseja, Gadiel Michael, Mrisho Ngassa na nyota wengine.

Chama alikuwa anavalia jezi namba 17 ndani ya viunga vya wekundu wa msimbazi na imekuwa tamaduni Duniani kote kuwa mara nyingi mchezaji bora anahama na jezi namba yake.

Chama anaelekea Yanga na huenda tukamshuhudia Farid Mussa akimkabidhi Chama jezi namba 17. Hii si ya kwanza kwani tuliwahi kuwaona wachezaji kadhaa Duniani wakiwaachia wengine namba zao walizozizoea.

Juan Cuadrado alimuachia Ronaldo jezi namba 7 pale Juventus. Martial alimuachia jezi namba 9 Ibrahimovic pale United na Ibrahimovic akamuachia jezi namba 9 Romelu Lukaku pale United.

Tutegemee kumuona Chama kwenye jezi namba 17 huku tukimuona Farid Mussa kwenye namba mpya ya jezi.



UTT AMIS yatoa elimu ya Uwekezaji wa Pamoja kwa Wananchi waliofika katika Maonesho ya Sabasaba

$
0
0

Baadhi ya wananchi wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Mkuu Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTTAMIS, Martha Mashiku kuhusu uwekezaji unaofanywa na taasisi hiyo kupitia mifuko yake ya Uwekezaji wa Pamoja katika banda lao lililopo kwenye Maonesho ya 48 ya Kimataiafa ya Biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. (Na Mpiga Picha Wetu).

Afisa Mkuu Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, Martha Mashiku (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo katika banda lao lililopo kwenye Maonesho ya 48 ya Kimataiafa ya Biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

 

Afisa Masoko wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, Paschazia Charles (kushoto) akimsajili mteja mpya Bw. Nsumbalimi Gilya kwa njia ya mtandao alipofika katiba Banda la UTT AMIS katika Maonesho yua 48 ya Kimataiafa ya Biashara (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.

Afisa Masoko wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, Florence Mwalusito, akitoa maelezo kuhusu uwekezaji unaofanywa na taasisi hiyo kupitia mifuko yake ya Uwekezaji wa Pamoja kwenye viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Afisa Masoko Mwandamizi wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, Oliver Minja (kulia), akitoa elimu kuhusu uwekezaji unaofanywa na taasisi hiyo kupitia mifuko yake ya Uwekezaji wa Pamoja kwenye viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. 

Wananchi wakipata maelezo katika Banda la Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS. Kushoto ni Afisa Masoko na Uhusiano wa kampuni hiyo, Waziri Ramadhan akitoa elimu ya uwezaji wa Pamoja.

Nargis aifagili chai ya Tanzania

$
0
0

            Na Mwandishi Wetu       

 

MISS Tanzania namba tatu mwaka  2003, Nargis Mohamed ametembelea Banda la Chai kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF-2024) na amevutiwa na ladha ya chai inayozalishwa hapa nchini.

Nargis amesema kuwa chai ya Tanzania ina ladha halisi ya chai huku akiwataka wananchi kuiunga mkono kwa kuinunua kwa wingi.

Nargis ambaye pia ni mkulima wa Parachichi wilayani Mafinga amesema jitihada za Rais Samia Suluhu  Hassan ya kuwekeza fedha nyingi katika kilimo, zimerahisisha shughuli za kilimo ambapo kwa upande wake ameona faida za jitihada hizo.


Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>