Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

SEKTA YA MADINI IMEWAFUNGULIA FURSA WATANZANIA, CHANGAMKENI

$
0
0

Na Wizara ya Madini

Kama umekuwa ukifuatilia kwa karibu juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania kuwezesha ushiriki wa Watanzania katika uchumi wa Madini ni vizuri kuona matokeo chanya yanayopatikana kupitia hatua mbalimbali kuanzia Marekebisho ya Sheria ya Madini yaliyofanyika mwaka 2017 ambayo yalijumuisha hitaji la matumizi ya huduma na bidhaa zinazopatikana nchini Tanzania.


Marekebisho haya yalipelekea kutungwa kwa Kanuni za ushiriki wa watanzania katika Sekta ya Madini za Mwaka 2018.

Matokeo ya utekelezwaji wa Kanuni hizo hadi sasa yameonesha dalili nzuri za maendeleo katika eneo hili muhimu la uchumi kwani idadi ya watanzania wanaotoa huduma na kuuza bidhaa kuanzia migodi ya uchimbaji mdogo, Kati hadi uchimbaji mkubwa unazidi kuongezeka.


Dalili hizi zinadhihirishwa na namna ushiriki wa watanzania ulivyoongezeka kupitia takwimu mbalimbali ikiwemo za mwaka 2023 zinazoonesha namna kampuni za kitanzania zilivyouza bidhaa na huduma migodini zenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.48 ambayo ni sawa na asilimia 90 ya mauzo yote yaliyofanyika migodini yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.65. 


 Aidha, mauzo hayo yaliyofanywa na kampuni za kitanzania kwa mwaka 2023 yalikuwa ni zaidi ya mauzo yaliyofanywa Mwaka 2022 ambayo yalikuwa na thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.08 sawa na asilimia 86 ya mauzo yote ya Dola za Marekani bilioni 1.26.

Katika kuendelea kuimarisha huduma hizi kutokana na mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji katika Sekta ya Madini, tayari kampuni tatu (3) za kitanzania zimejenga viwanda vya kutengeneza vifaa vinavyotumika migodini katika eneo la Buzwagi Special Economic Zone.

 

 Kampuni hizo ni East African Conveyors Supplies Limited imejenga kiwanda cha kuzalisha conveyor belts zinazotumika kusafirisha miamba wakati wa uchakataji wa madini kilichopo Manispaa ya Kahama ambapo ujenzi wake umekamilika na tayari  kimeanza usambazaji wa bidhaa hizo katika migodi ya ndani na nje ya nchi. 

 

Pia, Kampuni ya Max Steel Limited iliyopo jijini Dar es Salaam inatarajia kuzalisha vifaa vinavyotumika kushikilia miamba (wire-mesh na rock-bolts) kwenye uchimbaji wa chini ya ardhi ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 90.

Vilevile, Kampuni ya Rock Solutions Limited inajenga kiwanda jijini Mwanza cha kuzalisha core-trays zinazotumika kutunzia sampuli za miamba iliyochorongwa ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 90. Aidha, tayari kuna kampuni 8 zimeonesha nia ya kujenga viwanda vya uzalishaji bidhaa hizi.

Kwa Serikali haya ni mafanikio makubwa na ndiyo sababu Wizara inaendelea kuhamasisha watanzania na wadau wengine kuchangamkia fursa hizo za uwekezaji kupitia eneo la utoaji huduma migodini.  Kwa upande wa Wizara imeendelea kukutana na kujadili kwa pamoja na wadau kupitia majukwaa maalum kwa lengo la kuendelea kuboresha zaidi eneo hilo kwani kupitia uwekezaji huo, taifa litaendelea kupiga hatua kubwa za kiuchumi kupitia Sekta ya Madini.


Hivyo, kupitia makala hii, watanzania na wadau wengine wanahamasishwa kuchangamkia fursa ya kuanzisha viwanda vya kuzalisha vifaa pamoja na bidhaa mbalimbali zinazotumika migodini ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi. Dhamira ya Serikali ni kuona Tanzania inakua kinara duniani kwa kuzalisha bidhaa za migodini zinazokidhi mahitaji na hivyo kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha bidhaa za migodini.

Vilevile, bado  kuna fursa tele katika eneo la utoaji huduma migodini kutokana na migodi mikubwa na ya kati ambayo iko mbioni kuanzishwa katika miaka ya karibuni katika maeneo mbalimbali ya nchi ya Tanzania.

Serikali   kwa upande wake inaendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji nchini na ndiyo sababu inaendelea kuvutia wawekezaji zaidi hivyo, jukumu la kuona fursa hizi na kuzitumia ni la watanzania. Aidha, matokeo haya hayajatokea tu bali kupitia juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano ya kuifanya Tanzania kitovu cha madini duniani.


#VISION 2030: MadininiMaisha&Utajiri


MO DEWJI AMALIZA MAKUNDI MSIMBAZI

$
0
0

Na Walter Izrael 


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Rais wa Heshima wa Simba, Mohammed ‘Mo’ Dewji’ ameendelea na kazi ya kuunganisha timu kupitia vikao viwili vikubwa vilivyolenga kuvunja makundi na kuijenga upya Simba kama alivyoahidi wakati anarejea kuiongoza klabu hiyo.

Bilionea huyo alifanya kwanza kikao cha bodi mpya tangu alipoiunda kwa kuifumua ile ya zamani, kisha kila kitu kilienda sawa. Baada ya kikao hicho, MO alikutana na Baraza la Ushauri lenye watu wazito wakiwemo viongozi wa juu wa zamani kama Azim Dewji, Evans Aveva, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, Kassim Dewji ‘KD’, Hassan Dalali, Swedy Mkwabi na aliyekuwa mgombea nafasi ya mwenyekiti Moses Kaluwa.

Kambi ya Simba Misri itakuwa ya wiki zisizopungua tatu kabla ya kurudi mapema Agosti kuwahi Simba Day ambapo mziki mzima utatambulishwa, kisha itajiandaa na mechi za Ngao ya Jamii zitakazopigwa kati ya Agosti 8-11 na siku chache kuanza vita ya Ligi.



TABORA JITOKEZENI KWA WINGI WAKATI WA UBORESHAJI WA DAFTARI

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa uchaguzi uliofanyika leo Julai 8,2024 mkoani Tabarea.

Washiriki wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo.


Washiriki wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K akiwasilisha mada kuhusu maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya kwanza kwa wadau wa Mkoa wa Tabora. 

Mkurugenzi wa Idara ya Daftari na TEHAMA wa Tume, Stanslaus Mwita akiwasilisha mada ya mfumo. 


Viongozi wa vyama vya siasa mbalimbali kutoka mkoani Tabora wakishiriki katika majadiliano wakati wa mkutano huo. 
Viongozi na watu mbalimbali wakishiriki katika majadiliano wakati wa mkutano huo. 

Viongozi na watu mbalimbali wakishiriki katika majadiliano wakati wa mkutano huo. 
Tume inawatambua wazee wa kimila kama wadau muhimu katika Uchaguzi kwani husikilizwa na kuheshimika sana na jamii wanazoziongoza. Pichani ni wazee hao wa Mkoani Tabora wakiwa katika mkutano huo.  
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K (kulia) akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa wadau wa uchaguzi uliofanyika leo Julai 8, 2024  Mkoani Tabora. Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ilikutana na wadau wake Mkoani Tabora kuwataarifu kuhusiana na zoezi la uboreshaji linalotaraji kuanza Julai 20, 2024 mkoani humo.Kulia ni Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K (kulia) akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa wadau wa uchaguzi uliofanyika leo Julai 8, 2024  Mkoani Tabora. Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ilikutana na wadau wake Mkoani Tabora kuwataarifu kuhusiana na zoezi la uboreshaji linalotaraji kuanza Julai 20, 2024 mkoani humo.Katikati ni Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele na Kushoto ni Mjumbe wa Tume, Mhe. Magdalena Rwebangira. 
*****
Na Mwandishi wetu, Tabora
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetoa wito kwa wananchi na wapiga kura wa mkoa wa Tabora kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaotarajiwa kufanyika kwenye mikoa hiyo kuanzia Julai  20 hadi 26,2024.
 
Akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoani Tabora, leo Julai 8, 2024, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele amesema uboreshaji huu unamhusu kila mwananchi mwenye sifa ya kuandikishwa kuwa Mpiga Kura.
 
“Ni vyema mkatambua kuwa uboreshaji huu unamhusu kila mwananchi mwenye sifa ya kuandikishwa kuwa mpiga kura na anayeboresha taarifa zake. Hivyo, natoa rai kwenu kuwahimiza wananchi kupitia majukwaa yenu ya kisiasa, kijamii, kitamaduni, kiimani na kiuchumi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura,” alisema Jaji Mwambegele.
 
Aidha, Jaji Mwambegele alisema kuwa kila chama cha siasa kimepewa nakala ya orodha ya vituo vyote vya kuandikisha wapiga kura. Dhumuni la kuwapatia nakala hizo ni kuwawezesha kupanga na kuweka mawakala wa uandikishaji katika vituo vya kuandikisha wapiga kura.
 
“Kila chama kitaruhusiwa kuweka wakala mmoja kwenye kituo cha kuandikisha wapiga kura kwa lengo la kushuhudia utekelezaji wa zoezi la uboreshaji kituoni ikiwemo kuwatambua wale wanaokuja kituoni kama wana sifa za kuandikishwa,” amesema Jaji Mwambegele.
 
Jaji Mwambegele alitoa angalizo kwa wadau wa uchaguzi kwa umoja wao kuzingatia sheria za uchaguzi, kanuni za uboreshaji na maelekezo ya Tume kuhusu zoezi la uboreshaji wa Daftari. Huku akisema Tume kwa upande wake itazingatia Katiba, sheria ya uchaguzi na kanuni zilizotungwa chini ya sheria katika zoezi hili la uboreshaji.
 
Akiwasilisha mada wakati wa mkutano huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K,  amesema mkoa wa Tabora Tume inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 259,989.
 
“Hii ikiwa ni ongezeko la asilimia 17.8 ya wapiga kura 1,463,665 waliopo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Hivyo, Tume inatarajia baada ya uandikishaji Mkoa wa Tabora utakuwa na wapiga kura 1,723,654,” alisema.
 
Aidha, Kailima amesema uzinduzi wa zoezi la uboreshaji wa Daftari utafanyika Mkoani Kigoma Julai 20, 2024 ambapo siku ya uzinduzi ndiyo siku ambayo pia uboreshaji utaanza katika Mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi na kufuatiwa na Kagera na Geita.
 
Ameongeza kuwa kwa lengo la kutekeleza jukumu hilo kwa ufanisi, uboreshaji kwa awamu ya kwanza utafanyika kwenye mizunguko 13 itakayobainishwa kwenye ratiba.
 
“Zoezi hili litaendeshwa kwa siku saba kwenye kila kituo cha kuandikisha wapiga kura. Tunatarajia zoezi litakamilika Machi, 2025,” amesema.

UWANJA WA NDEGE WA IRINGA UANZE KAZI AGOSTI MOSI – MAJALIWA

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku 23 kwa Wizara za Ujenzi, Uchukuzi, taasisi zinazosimamia sekta ya anga na uongozi wa mkoa wa Iringa kutatua vikwazo vilivyopo ili uwanja wa ndege wa Iringa uanze kutumika ifikapo Agosti mosi, mwaka huu.


Ametoa agizo hilo leo (Julai 8, 2024) wakati akizungumza na viongozi na wananchi mbalimbali waliokuwepo uwanjani hapo mara baada ya kukagua ujenzi wa uwanja huo. Gharama za ujenzi wa uwanja huo ni sh. bilioni 63.7 na gharama za usimamizi ni sh. bilioni 1.1.

"Nimesema Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Uchukuzi, TAA, ATCL, Mamlaka ya Hali ya Hewa, TANROADS na Kamati ya Ulinzi ya Mkoa wakae, wafanye vikao na kuondoa vikwazo kabla ya tarehe 30 Julai ili ifikapo tarehe 1 Agosti, 2024 uwanja huu uanze kufanya kazi," amesema.

Akiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa, Waziri Mkuu aliwaeleza wananchi waliohudhuria mkutano huo kwamba juhudi za Rais Dkt. Samia za kutangaza utalii kupitia filamu ya Royal Tour zimeanza kuzaa matunda kwa idadi ya watalii wanaokuja nchini inazidi kuongezeka.

"Idadi ya watalii wanaokuja nchini ni kubwa, wengi wanaenda Serengeti. Tunataka waje huku kanda ya Kusini, na kwa kuanzia, barabara ya kutoka Iringa Mjini hadi kwenye geti la Hifadhi ya Ruaha itajengwa na Benki ya Dunia kwa kiwango cha lami."

Amesema ujenzi wa uwanja wa Iringa umefikia asilimia 93 na uwanja huo ni wa viwango vya kimataifa. "Tukikamilisha uwanja wa ndege na barabara ya lami, ni wazi kuwa pato la mkoa wa Iringa litaongezeka."

"Wana-Iringa jipangeni kwa fursa zilizopo, kule mbugani wanahitaji kuwe na mahoteli, wanahitaji vyakula zaidi na magari ya utalii ili yapeleke watalii kwa urahisi zaidi."

Amemwagiza Mkuu wa Mkoa huo, Peter Serukamba aunde timu ya kutangaza vitutio vya mkoa wa Iringa ikiwemo kuipaisha Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.


INEC YASISITIZA USHIRIKIANO KWA WATENDAJI WA UBORESHAJI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

$
0
0

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegeke akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza leo Julai 9 na 10,2024 Mkoani Tabora.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegeke akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza leo Julai 9 na 10,2024 Mkoani Tabora.

Kamishina wa Viapo kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Kundiata Robert akitoa utangulizi kabla ya kuwaapisha watendaji hao wa uboreshaji.
Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri wakila kiapo cga kujitoa uanachama na kile cha kutunza siri mbele ya Kamishina wa Viapo kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Kundiata Robert (hayupo pichani) kabla ya kuanza kwa mafunzo ya siku mbili kwa watendaji wa uandikishaji ngazi ya Halamashauri mkoani Tabora yaliyoanza Julai 9 hadi 10, 2024 katika Ukumbi wa Mkoa wa Tabora. (Picha na INEC).
Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri wakila kiapo cga kujitoa uanachama na kile cha kutunza siri mbele ya Kamishina wa Viapo kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Kundiata Robert (hayupo pichani) kabla ya kuanza kwa mafunzo ya siku mbili kwa watendaji wa uandikishaji ngazi ya Halamashauri mkoani Tabora yaliyoanza Julai 9 hadi 10, 2024 katika Ukumbi wa Mkoa wa Tabora. (Picha na INEC).
Afiza Uhamiaji Wilaya ya Tabora MC, Mkaguzi wa Uhamiaji Muhondo Mashili akitoa mada kuhusu uraia wakati wa mafunzo hayo. 
Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri za mkoa wa Tabora wakiwa katika mafunzo hayo.


Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri za mkoa wa Tabora wakiwa katika mafunzo hayo.
Na Mwandishi wetu, Tabora na Katavi
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewataka watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoani Tabora na Katavi kuwa na ushirikiano kati yao, Serikali, Vyama vya Siasa na wadau wengine wa uchaguzi.
 
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegeke wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza leo Julai 9 na 10,2024 Mkoani Tabora.
 
Mafunzo kama hayo yamefunguliwa pia Mkoani Katavi na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ambaye pia ni Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Asina Omari na yanafanyika ikiwa ni maandalizi ya uboreshaji wa Daftari kwenye mikoa hiyo unaotarajiwa kufanyika tarehe 20 hadi 26, 2024. 
 
“Matokeo bora ya zoezi hili yanategemea uwepo wa ushirikiano mkubwa kati ya watendaji wote wa uboreshaji, Serikali, Vyama vya Siasa na wadau wengine wa uchaguzi,” amesema Jaji Mwambegele.
 
Jaji Mwembegele amewasihi watendaji hao kuwa na ushirikiano mzuri na wa karibu na Tume wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao na ikiwa wanahitaji ufafanuzi au maelekezo yeyote, wasisite  kuwasiliana na Tume.
 
Aidha, Jaji Mwambegele amesema wakati wa uboreshaji wa Daftari mawakala wa Vyama vya Siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura jambo ambalo litasaidia kuleta uwazi katika zoezi hilo.
 
“Mawakala hao watasaidia kutambua waombaji wa eneo husika hivyo kupunguza kutokea kwa vurugu zisizokuwa za lazima. Mawakala hao hawaruhusiwi kuwaingilia watendaji wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao vituoni,”alisema Jaji Mwambegele.
 
Katika hatua nyingine amesema Tume imetoa vibali kwa Asasi za kiraia 157 kwa ajili ya kutoa elimu ya mpiga kura na waangalizi wa zoezi la uboreshaji 33 watakao tazama zoezi la  uboreshaji.
 
Jaji Mwambegele amesema Tume inasisitiza kwa Maafisa Waandikishaji kuwa, wanapofika katika maeneo yao, wapewe ushirikiano kwa kuwa ni wadau muhimu.
 
Mafunzo hayo yanahusisha namna ya ujazaji wa fomu pamoja na kutumia mfumo wa kuandikisha wapiga kura (Voters Registration System - VRS) ili waweze kupata uelewa wa pamoja utakaowapa fursa ya kutumia kwa ufasaha mfumo huo pamoja na vifaa vingine vya kuandikisha wapiga kura.
 
“Mafunzo haya, yanawajengea umahiri wa kuwafundisha Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata kisha nao watatoa mafunzo hayo kwa Waendeshaji wa Vifaa vya Bayometriki na Waandishi Wasaidizi ambao ndio watahusika na uandikishaji wa wapiga kura vituoni,” alisema Jaji Mwambegele.
 
Aidha, Maafisa TEHAMA watapatiwa mafunzo maalum ya jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiufundi (Troubleshooting) endapo zitajitokeza wakati wa zoezi la uandikishaji wa wapiga kura vituoni.
 
Mapema kabla ya kuanza mafunzo hayo, washiriki walikua kiapo cha kujitoa uanachama na kile cha kutunza siri.
 
Tume imetangaza uzinduzi wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utafanyika Julai 20, 2024 mkoani Kigoma ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na kauli mbiu ya uboreshaji ni “Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi Wa Uchaguzi Bora”.

CRDB yakabidhi milioni 24 kwa timu ya Taifa ya Olympic 2024

$
0
0

Katika utekelezaji wa mpango wake wa uwezeshaji kwa vijana kupitia CRDB Bank Marathon, Benki ya CRDB kupitia Taasisi yake ya CRDB Bank Foundation imekabidhi msaada wa fedha kwa timu ya Taifa ya Olympic kushiriki katika Mashindano ya Olympic yatakayofanyika Paris, Ufaransa kuanzia tarehe 26 Julai hadi 11 Agosti 2024, na leo hii tutawakabidhi hundi ya ufadhili.

Akikabidhi mfano wa hundi kwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Riaadha Tanzania, William Kallagjhe, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Group, Abdulmajid Nsekela amesema uwezeshaji wa timu hiyo ya Taifa ya Olympic kwa vijana wanaokwenda kushiriki utailetea Taifa heshima, bali pia itawaweka katika ramani ya kimataifa, ikitoa njia ya mafanikio kwa wao binafsi, familia zao na jamii kwa ujumla.

DKT ABBAS AIPONGEZA SUMA -JKT KWA HATUA NZURI YA UJENZI WA NYUMBA 2500 MSOMERA

$
0
0

Na Mwandishin Wetu, Handeni

Katibu Mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii Dkt Hassan Abbasi amelipongeza Jeshi la Kujenga Taifa kupitia kampuni yake ya SUMA - JKT  kwa kufikia zaidi ya asilimia 90 kukamilisha ujenzi wa nyumba  2,500 zinazojengwa katika Kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga.

Dkt Abbasi ametoa kauli hiyo katika ziara aliyoifanya Kijijini hapo tarehe 8 Julai, 2024 na kusema kazi iliyofanywa na jeshi hilo ni kubwa na ya kizalendo hivyo zoezi lililobaki sasa ni kuendelea kuelimisha, kuhamasisha na kuhamisha wananchi wanaoendelea kujiandikisha kuhama kwa hiyari katika eneo la tarafa ya Ngorongoro.

Amesema kuwa ujenzi wa nyumba hizo unaenda sambamba na ujenzi wa miundombinu mingine ya huduma za kijamii ambapo  wizara za kisekta  zimekuwa zikiendelea kujenga miundo mbinu hiyo ikiwemo  shule,usambazaji wa umeme,maji ,mawasiliano na huduma zote za msingi katika Kijiji hicho.

Katibu mkuu huyo  amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na maono yake kaatika utekelezaji wa mradi huo ambao kukamilika kwake kutatimiza utekelezaji wa malengo ya  serikali ya kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na maisha bora.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Handeni mheshimiwa Albert Msando amemshukuru Dkt Abbasi kwa ziara hiyo na kusema kuwa itaongeza ari kwa wizara nyingine za kisekta kuongeza kasi katika ukamilishaji wa miradi yote muhimu na hivyo kuifanya Msomera kuwa Kijiji cha mfano.

Mheshimiwa Msando amesema kuwa uendelevu wa mradi huo unaondoa propaganda za watu wachache kwamba wananchi wanaohamishwa kutoka Ngorongoro kwenda katika Kijiji hicho wanaondolewa kwa nguvu na kutelekezwa jambo ambalo halina ukweli wowote.

Akizungumzia kuhusu suala la kuhamisha watu kwa hiyari kutoka ndani ya hifadhi ya Ngorongoro Kamishna wa Mamlaka ya Uhifadhi ya Ngorongoro (NCAA)  Dkt.Elirehema Doriye amsema kukamilika kwa nyumba hizo kunaongeza chachu ya mamlaka kuendelea kuhamasisha na kuhamisha wananchi.

Mapema Kamanda wa Operesheni wa Ujenzi wa nyumba hizo kanali Sadiki Mihayo alimweleza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Hassan Abbasi kwamba ujenzi wa nyumba zote 2500 upo hatua za mwisho kukamilika na sasa wanajiandaa kuhamia katika wilaya kijiji cha Kitwai wilaya ya Simanjiro na kijiji cha Saunyi wilaya ya  Kilindi kuendelea na ujenzi wa nyumba zilizobaki kulingana na mpango kazi waliojiwekea.


Mwanafunzi KCMUCo ajinyakulia zawadi ya gari Benki ni SimBanking ya CRDB

$
0
0

NA MWANDISHI WETYU, DAR ES SALAAM

 

MWANAFUNZI wa Chuo cha Kikuu Kishiriki cha Tiba Kilimanjaro (KCMUCo) kilichopo Moshi, Hussein Hamisi Hamadi, ameibuka mshindi wa gari ya pili, kati nne zinazotolewa kwa washindi wa Kampeni ya Benki ni SimBanking inayoendeshwa na Benki ya CRDB.


Benki ni SimBanking kupitia kaulimbiu ya ‘Swahiba – Lako, Langu,’ inalenga kuhamasisha matumizi ya huduma za kibenki kidijitali, ambako washindi wa kila mwezi na kila baada ya miezi mitatu, huzawadiwa zawadi mbalimbali, zikiwemo ‘Tembo Point’ zenye thamani jumla ya Sh. Mil. 200.

 

Kampeni hiyo inatoa zawadi za magari manne aina ya Nissan Dualis (moja kila baada ya miezi mitatu), bajaj 6, bodaboda 12, kompyuta mpakato ‘laptop’ 20, simu janja na ‘Tembo Point’ ambazo mshindi huweza kuzibadili kuwa pesa taslimu na kupewa kiasi cha pointi alizonazo.

 

Droo ya kusaka mshindi wa gari ya pili (wa mwezi Juni), imefanyika jijini Dar es Salaam leo, ambako Hussein amejinyakulia gari hiyo, huku Meneja Mwandamizi wa Huduma za Kibenki Kidijitali wa CRDB, Mangire Kibanda, akisema washindi zaidi wataendelea kuzawadiwa hadi mwisho wa mwaka huu.

 

“Tuko hapa leo kumtafuta na kumtangaza mshindi wa gari la pili la Kampeni ya ‘Benki ni ni SimBanking’, ambako Hussein ameibuka mshindi wetu na amezawadiwa gari aina ya Nissan Dualis, ambayo imekatiwa bima na imejazwa mafuta ‘full tank.’

 

“Lengo la kampeni ni kuchagiza matumizi yasiyo yasiyo ya pesa taslimu ‘cashless,’ badala yake wateja wetu wafanye malipo ya manunuzi kupitia Programu ya SimBanking kama vile kulipia bili za umeme, maji, tiketi za ndege, ada na michango ya shule na kulipia manunuzi ya bidhaa za mtandaoni.

 

“Pia mteja anaweza kushinda zawadi kwa kununua muda wa maongezi, ambako kuna zawadi mbalimbali zikiwemo gari nne, bajaji 6, pikipiki 12, laptop 20 na ‘smartphone,’ na wale watakaoshinda ‘Tembo Point’ wanaweza kuzibadili kuwa pesa taslimu na kuingiziwa kwenye akaunti zao,” alisema.


Aliwataka Watanzania kuchangamkia fursa zinazokuja na Benki ni SimBanking kwa kufungua akaunti kupitia ‘applications’ ya CRDB, au kupitia mawakala wao na kuunganishwa moja kwa moja na Huduma ya SimBanking, kisha kuingia katika droo za kampeni hiyo.

 

“Baada ya leo kumpata mshindi wa pili wa gari, mwisho wa mwezi ujao pia tutakuwa na droo ya kupata washindi wa bodaboda mbili na bajaj moja, na kila baada ya miezi mitatu, (yaani mwezi wa 9 na mwezi wa 12 mwaka huu), tutakuwa tunakabidhi gari moja moja,” alisisitiza Kibanda.

 

Aidha, Kaulimbiu ya ‘Swahiba – Lako, Langu,’ inayopamba kampeni hiyo, inamaanisha kuwa shida za mteja ndio kipaumbele cha CRDB, ambayo ina mazingira sahihi ya kupata suluhishi za changamoto zozote za kifedha anazoweza kupata mteja wa benki hiyo.


Wazazi, walezi watakiwa kuchangamkia Junior Jumbo za CRDB Viwanja vya Sabasaba

$
0
0

MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

BENKI ya CRDB imeyatumia Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Tanzania, yanayoendelea kwenye Viwanja vya Sabasaba, jijini Dar es Salaam, kuwahimiza wazazi na walezi kujitokeza kuwafungulia watoto wao Akaunti za Junior Jumbo, zinazoweza kutumika kulipia bili mbalimbali za mtoto - kielimu na kiafya.

 Junior Jumbo ni akaunti isiyo na makato ya mwezi inayofunguliwa kwa Sh. 20,000 ambayo licha ya kumjengea mtoto utamaduni chanya wa kujiwekea akiba maishani, ina ukomo wa kutoa pesa bila makato ili kuchochea uwekaji akiba, iwapo mzazi ama mlezi atatoa mara nne zinazoruhusiwa kwa mwaka.

Wito huo umetolewa na Afisa wa Benki ya CRDB Tawi la Temeke, Doreen Hermes, alipozungumza na wanahabari katika banda la benki hiyo kwenye viwanja hivyo, akisisitiza Junior Jumbo ni akaunti rafiki kwa ustawi wa maisha ya sasa na baadaye ya mtoto, ambayo anapewa uhuru wa kuitumia anapofikisha miaka 18.

“Banda letu la CRDB lililopo hapa Sabasaba na matawi yetu kote nchini, yanaendelea na utoaji wa huduma mbalimbali na masuluhishi ya kipesa, ikiwemo ufunguzi wa akaunti zote. Wito wetu ni kwa wazazi na walezi kujitokeza hapa kufungua Junior Jumbo Account kwa ajili ya watoto wao.

“Hii ni akaunti maalum kwa ajili ya matumizi yanayomuhusu mtoto kwa sasa na hata maisha yake ya baadaye. Ni akaunti isiyo na makato, ambapo mzazi anapaswa kuja kufungua akiwa na picha mbili za ‘passport size’ za mtoto, cheti cha kuzaliwa cha mtoto, kitambulisho cha mzazi na kianzio cha shilingi 20,000.

“Kupitia akaunti hii, mzazi ama mlezi ataweza kulipia bili za mtoto, ada na michango mbalimbali ya shule, malipo ya huduma za hospitali kwa mtoto na mengineyo mengi, kulingana na kiasi alichomuwekea mtoto husika katika akaunti yake,” alibainisha Doreen.

Aidha, Afisa huyo alisema mwitikio wa wananchi katika banda la lililpo Viwanja vya Sabasaba ni mkubwa sana, huku akiwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi zaidi kutembelea tawi lao katika siku chache zilizosalia kuelekea kufunga kwa maonesho hayo, ili kujipatia huduma mbalimbali tawini hapo.


 

Serikali yajiapiza kwa wadanganyifu wa mitihani vyuo vikuu

$
0
0


NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM


WIKI mbili tangu Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), kutoa taarifa za kukamatwa kwa wanafunzi feki 17 waliokuwa wakijaribu kuwafanyia mitihani wanafunzi wa chuo hicho, Serikali imejiapiza kuwabana na kuwakomesha ili kulinda mfumo wa elimu nchini, na kwamba bado vyuo vikuu nchini viko salama na vinazingatia maadili.

Juni 28 mwaka huu, OUT kupitia Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Elifas Bisanda, kilisema wanafunzi feki 17 walikamatwa katika vituo vya mitihani vya Kinondoni na Ilala, wakijaribu kuwafanyia wanafunzi wa chuo hicho mitihani hiyo iliyoanza Juni 3 hadi 24, ikihusisha vitu 53 vyenye wanafunzi 10,417.

Akizungumza na waandishi wa habari, baada ya mkutano wake na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, alisema Serikali inapambana kukomesha, kwani vyuo vikuu vinazingatia maadili na weledi ili kuhakikisha vinazalisha wahitimu wenye sifa.


“Suala la udanganyifu na majaribio ya udanganyifu kwenye mitihani lipo dunia nzima, suala kubwa ni juhudi gani zinafanyika kudhibiti vitendo hivyo. Kwahiyo pamoja kwamba tunajua kuwa tunaendelea vizuri na udhibiti wa matukio hayo, upo msemo usemao; adhaniaye amesimama, aangalie asianguke.

“Kila tunaposikia ama kushuhudia tuhuma hizi za udanganyifu, tunaumizwa nazo sana. Imekuwa hivyo katika ngazi mbalimbali kuanzia mitihani ya kidato cha nne, cha sita na vyuo vya kati na vyuo vikuu na tumekuwa tukichukua hatua kali ambazo kwa bahati mbaya zinawaumiza hata baadhi ya wawekezaji wa sekta ya elimu.

“Tunasimama imara katika kukomesha vitendo hivi, kwa sababu tunatambua madhara ya udanganyifu kwenye mitihani ni makubwa sana, kwamza linaondoa usawa miongoni mwa wanafunzi, ambao kimsingi wanatakiwa kupimwa kwa haki, asiwepo wa kupita kwa udanganyifu pasipo na juhudi zake,” alisemma Profesa Mkenda.

Akitolea mfano udaktari, Profesa Mkenda alisema ni hatari kubwa kuwatumia madaktari waliofaulu kwa kutumia udanganyifu na kwamba athari zake zinaenda kuumiza wasiohusika na mchakato huo, ambao ni wagonjwa watakaopitia mikononi mwa madaktari hao wasio na sifa kielimu.

“Udanganyifu katika ngazi yoyote ile ya elimu, ni saw ana kulea ama kufumbia macho rushwa klwa wanafunzi wetu, kwamba wewe mwanafunzi njia nzuri na rahisi ya kufanikiwa ni kufanya udanganyifu, mbaya zaidi hatua kali tunazochukua, baadhi ya watu wanatulaumu kwamba tumekuwa wakali sana.

“Tunaomba watuelewe, kwani tunafanya hivyo kwa sababu tunapenda kuulinda mfumo wetu wa elimu, ndio maana Baraza la Mitihani la Taifa limesimama kidete na sasa limekuja na sheria kali ili kuwabana zaidi wadanganyifu na kama mlivyosikia juzi hapa wamehukumiwa, tunazishukuru mamlaka,” alisisitiza Prof. Mkenda.

Kuhusu vyuo vikuu, Prof. Mkenda alisema vyote vina kanuni zake za kusimamia mitihani yao ambazo zinafahamika na TCU inazifahamu, ikiwemo kufukuzwa chuo moja kwa moja kwa wanafunzi wanaokamatwa kwa udanganyifu, ambapo aliviomba vyuo viendelee na adhabu hizo bila kusita.

Aidha, Profesa Mkenda aliviomba vyombo mbalimbali vya habari nchini, kutoa ushirikiano kwa Serikali kupitia Baraza la Mitihani, Tume ya Vyuo Vikuu na vyombo vya dola kwa kutaja viashria na wahusika wa vitendo vya udanganyifu wa mitihani kwa wanafunzi, badala ya kuficha majina na kuandika magazetini kila siku.



 


WAZAZI WAASWA KUWAFUNGULIA WATOTO JUNIOR JUMBO AKAUNTI

$
0
0

Na John Marwa

Benki ya CRDB imewataka wazazi kuwafungulia watoto akaunti ya 'Junior Jumbo' ili kuwawekea akiba kwa ajili ya matumizi yao ya baadae.

Hayo yamebainishwa na Afisa wa Benki ya CRDB Tawi la Temeke, Doreen Hermes wakati akizungumza katika Maonesho ya Sabasaba makala ya 48 yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Temeke, Dar es Salaam.


"Siku ya leo tungependa kuongelea akaunti yetu nzuri ya Junior Jumbo ambapo mzazi atamfungulia mtoto wake kwa ajili ya matumizi mbalimbali hapo mbeleni.

"Akaunti hii ni nzuri ambapo mzazi ataweza kuifungua kwa kuleta tu picha mbili za mtoto, kitambulisho chake, cheti cha kuzaliwa cha mtoto na kianzio ambacho tsh 20,000". Amesema na kuongeza kuw…
SERIKALI YAJIDHATITI UDANGANYIFU WA SHAHADA HEWA VYUO VIKUU

Na John Marwa

Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mamlaka ya Vyuo vikuu Tanzania (TCU) wamejidhatiti kulinda heshima ya mfumo wa eiimu nchini kwa maslahi mapana ya Taifa kwa ujumla.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Elimu Adolf Mkenda wakati akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kuwepo kwa taarifa na tuhuma za udanganyifu wa mitihani katika baadhi ya Vyuo Vikuu nchini.

"Hapa karibuni kumekuwa na tuhuma zinaeleza rushwa kutoka kwa vyombo vya habari kwamba kuna udanganyifu kwenye vyuo vikuu hasa katika masuala ya mitihani na tuhuma hizo zimerudiwa  mara kadhaa na sisi kila tuhuma tukizipata tunazifanyia kazi na tuna omba mtu yoyote ambaye anahisi kuna suala analifahamu alilete TCU moja kwa moja litafanyiwa kazi.

Lakini tuona sasa tuhuma hizi zinavyosemwa zinaweza zikasababisha watu wakadhani kwamba hali ya vyuo vikuu vyetu ni mbaya sana, napenda kuwahakikishia watanzania wote kwamba bado vyuo vikuu vyetu vikuu vinazingatia sana maadili hasa katika masuala ya mitihani na weledi kuhakikisha kwamba tunatoa shahada kwa mujibu wa taratibu zinazokubarika katika taaluma zetu."amesema Mkenda na kuongeza kuwa.

"Suala la udanganyifu majaribio ya udanganyifu yapo Dunia nzima na kwa nchi zote mahali popote Duniani suala kubwa ni juhudi ambazo zinatumika kuzuia udanganyifu na kila tunaposikia tuhuma tunachukulia ni jambo zito sana na ntawakumbusha tu kulikuwa na dalili kama hizo kwa mitihani ya darasa la saba, kidato cha nne, kidato cha sita na mitihani inayosimamwiwa na Baraza la mitihani tulianza kuchukua hatua na tulichukua hatua kali ambazo kwa bahati mbaya zinaumiza hata masilahi ya baadhi ya wawekezaji wa elimu kwaiyo tulizichukua pamoja na mashinikizo ambayo wakati mwingine unayapata na lawama chungu nzima lakini tulisimama imara kwa sababu ya udanganyifu wa mitihani madhara yake ni makubwa sana, kwanza kabisa ni suala ambalo linaondoa usawa, tunataka wanafunzi wanapofanya mitihani wote wapimwe kwa usawa na haki, mmoja asiwe anadanganya anapita na mwingine anatumia juhudi zake anapita.

"Hili ni suala la weledi, unapokuwa umeondoa weledi kwamba mtu mwingine anaweza akapata cheti kwa sababu ya udanganyifu halafu anaweza akapewa majukumu ya kwenda kuhudumia umma, tuseme labda amesomea udaktari lakini akafanya udanganyifu halafu ataenda kutibu mtu madhara yake ni makubwa sana kwa wale ambao wanapata huduma hiyo.

"Na vilevile tukirushusu udanganyifu kwenye elimu ni kama vile kulea ama kuruhusu rushwa kwa wanafunzi wetu kwamba wewe mwanafunzi njia nzuri ya kuendelea ni kuwa mdangaanyifu na ndio maana hatua ambazo tumezichukua baadhi ya watu wanalaumu kwamba tumekuwa wakali sana na naomba tu umma utuelewe kwamba tunafanya hivyo kwa kulinda heshima ya mfumo wetu wa elimu kwaiyo mliona kwenye Baraza la mitihani tumesimama kidete hasa tumeleta mabadiliko ya sheria ili kuwabana zaidi wanaofanya udanganyifu kwenye mitihani." amesema Mkenda na kubainisha kuwa.

"Sasa kuhusu vyuo vikuu, vyuo vikuu vyote vina kanuni za kusimamia mitihani ambazo zinafahamika na TCU na kwa kawaida Chuo Kikuu ukikamatwa umedanganya kwenye mtihani adhabu yake ni kufukuzwa Chuo moja kwa moja, ukishapata uhakika kwamba umedanganya mtihani hukumu yake unafukuzwa chuoni.

"Mimi nina watu chungu nzima ofisini wazazi wao wanaomba kwa waziri, tunaomba mwanetu arudi alifukuzwa, ameonewa, ninachofanya nikurudi kwenye utaratibu wa Chuo kuuliza nini kimetokea, unakuta utaratibu ulifanyika Baraza limemfukuza Chuo amepewa muda wa kukata rufaa hajakata ama amekata lakini mimi kama waziri nimekataa kata kata kuingilia mamlaka ya vyuo vikuu wanapochukua hatua kama hizo kwa sababu tunalinda sana suala la mitihani.

"Sasa tuhuma zingine ni kwamba ambazo tumeziona zimetoka kwenye gazeti moja kwamba kuna utaratibu wa wanafunzi kuhonga ili matokeo yaliyokwisha ingizwa kwenye mfumo wa tehama yabadilishwe, sasa kulitokea tuhuma kama hizo katika chuo kimoja hapa nchini na kikamtaja jina la mwanafunzi na mtu ambaye alihusika kubadilisha yale matokeo, nilimwambia Katibu Mkuu aunde tume huru kwenda kuchunguza, ikiwa ni pamoja na idara ya usalama wa Taifa na wataalamu wa tehama, waliingia wakaangalia mfumo wote wa tehama uzuri ukishaingiza matokeo yote kwenye tehema mabadiliko yeyote yanayofanyika yanaacha kumbukumbu ya mabadiliko, lazima utaona mtu aliingia saa ngapi aliingiza alama ngapi nautaona tarehe ngapi hizo alama zilibadilishwa.

"Kwaiyo tulichunguza tukagundua si kweli na kwenye Chuo hicho nadhani kuna mnyukano tu, kuna mtu au watu kwa sababu wanajua makamu Mkuu wa Chuo anastaafu karibuni basi sijui ni kuchafuana huko kwa sababu kuna dalili kwamba katika kinyang'anyiro cha kutaka kuchukua nafasi watu wanachafuana lakini nasema hivi Katibu Mkuu tumekubalina ataiomba TCRA ichukue Chuo kilekile kama majaribio kwa sababu ya tuhuma tulizozisoma kwenye gazeti kwenda kufanya uchunguzi wa matokeo yote ambayo yameingizwa kwenye  tehama na kuangalia matokeo yanapoingizwa yanapobadilika nani anabadilisha.

Pamoja na hayo Waziri Mkenda amewaomba waandishi wa Habari kutoa ushirikiona pale unapohitajika juu taarifa wanazoziandika ili kuweza kulisaidia Taifa na sekta ya elimu juu udanganyifu unaofanyika katika mitihani na vyuo vinavyohusika.

Vile amesema wataendelea kuchukua hatua kali kwa maslahi mapana ya mfumo mzima wa elimu na wataalamu wanaozalishwa nchini kupitia Vyuo Vikuu nchini.

Wachezaji 124 wakiwemo 52 wa kulipwa na 72 kushiriki mashindano ya Gofu kumuenzi mchezaji wa zamanı wa timu ya taifa ya wanawake ya gofu, marehemu Lina Nkya

$
0
0

 Na Mwandishi Wetu

Baada ya Morogoro mwezi Aprili mwaka huu sasa ni zamu ya Arusha katika viwanja vya Gymkana ambapo mashindano ya Gofu kwa ajili ya kumuenzi mchezaji wa zamanı wa timu ya taifa ya wanawake ya gofu, marehemu Lina Nkya, raundi ya tatu yameanza kurindima leo.

Jumla ya wachezaji 124 wakiwemo 52 wa kulipwa na 72 wa ridhaa wamesajiliwa kushiriki mashindano hayo yatakayofanyika katika viwanja hivyo vya gofu Gymkana mkoani Arusha.

Akizungumza mara baada ya kumaliza kufanya usajili, Mchezaji wa kulipwa Nuru Mollel amesema kuwa amejipanga vizuri kwa ajili ya mashindano hayo na anamatarajio makubwa ya kuhakikisha kuwa anaibuka mshindi.

Amesema anawaomba watanzania kujitokeza kuja kuona kile wanachokifanya na kwamba anawapongeza wale wote waliowezesha mashindano hayo kufanyika kwa weledi na ubora wa hali ya juu.

“Nimejipanga vizuri hasa katika kuhakikisha naibuka mshindi katika mashindano haya, hata hivyo kushiriki kwenye jambo hili kwangu mimi ni fursa haşa ya kukutana na wachezaji wenzangu na kuendelea kubadirishana uzoefu,” amesema Mollel

Naye mchezaji ambaye ni mshindi wa ridhaa kwa raundi mbili za mashindano hayo ambazo ni Morogoro na Moshi, Alli Sanzu amesema mashindano hayo ya Arusha ni ya muhimu kwake kwa sababu ni ya mwisho kuelekea kwenye mashindano makubwa nchini Dubai.

Amesema amewekeza nguvu zake zote katika mashindano hayo kuhakikisha anafanya vizuri na kuibuka mshindi.

Mashindano hayo raundi ya kwanza yalifanyika Mkoani Kilimanjaro ya pili mkaoni Morogoro na Sasa ni Mkoani Arusha ambayo Julai 10,2024
usajili wa wachezaji wa gofu wa mashindano hayo ulifanyika katika viwanja hivyo vya gofu Gymkana Mkoani Arusha.
 
Mashindano hayo yatafanyika kuanzia Julai 11 hadi 14, 2024 ambapo siku ya mwisho ya mashindano hayo shughuli nzima ya kugawa zawadi kwa washindi wote kwa hatua zote zitafanyika na mshindi wa kwanza atajipatia kikombe na pesa taslimu .

Mshindi wa Mashindano ya kwanza kwa msimu huu yaliyofanyika Viwanja vya TPC Moshi mkoani Kilimanjaro alikua Moreli akifuatiwa na Fadhili Nkya , kwa yaliyofanyika Mkoani Morogoro mshindi wa kwanza alikua Hassan Kadio na katika nafasi ya pili ni Abdalah Yusuph.


SERIKALI YAJIDHATITI UDANGANYIFU WA SHAHADA HEWA VYUO VIKUU

$
0
0

Na Mwandishi Wetu

Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mamlaka ya Vyuo vikuu Tanzania (TCU) wamejidhatiti kulinda heshima ya mfumo wa eiimu nchini kwa maslahi mapana ya Taifa kwa ujumla.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Elimu Prof. Adolf Mkenda wakati akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kuwepo kwa taarifa na tuhuma za udanganyifu wa mitihani katika baadhi ya Vyuo Vikuu nchini.

"Hapa karibuni kumekuwa na tuhuma zinaeleza rushwa kutoka kwa vyombo vya habari kwamba kuna udanganyifu kwenye vyuo vikuu hasa katika masuala ya mitihani na tuhuma hizo zimerudiwa  mara kadhaa na sisi kila tuhuma tukizipata tunazifanyia kazi na tuna omba mtu yoyote ambaye anahisi kuna suala analifahamu alilete TCU moja kwa moja litafanyiwa kazi.

Lakini tuona sasa tuhuma hizi zinavyosemwa zinaweza zikasababisha watu wakadhani kwamba hali ya vyuo vikuu vyetu ni mbaya sana, napenda kuwahakikishia watanzania wote kwamba bado vyuo vikuu vyetu vikuu vinazingatia sana maadili hasa katika masuala ya mitihani na weledi kuhakikisha kwamba tunatoa shahada kwa mujibu wa taratibu zinazokubarika katika taaluma zetu."amesema Mkenda na kuongeza kuwa.

"Suala la udanganyifu majaribio ya udanganyifu yapo Dunia nzima na kwa nchi zote mahali popote Duniani suala kubwa ni juhudi ambazo zinatumika kuzuia udanganyifu na kila tunaposikia tuhuma tunachukulia ni jambo zito sana na ntawakumbusha tu kulikuwa na dalili kama hizo kwa mitihani ya darasa la saba, kidato cha nne, kidato cha sita na mitihani inayosimamwiwa na Baraza la mitihani tulianza kuchukua hatua na tulichukua hatua kali ambazo kwa bahati mbaya zinaumiza hata masilahi ya baadhi ya wawekezaji wa elimu kwaiyo tulizichukua pamoja na mashinikizo ambayo wakati mwingine unayapata na lawama chungu nzima lakini tulisimama imara kwa sababu ya udanganyifu wa mitihani madhara yake ni makubwa sana, kwanza kabisa ni suala ambalo linaondoa usawa, tunataka wanafunzi wanapofanya mitihani wote wapimwe kwa usawa na haki, mmoja asiwe anadanganya anapita na mwingine anatumia juhudi zake anapita.

"Hili ni suala la weledi, unapokuwa umeondoa weledi kwamba mtu mwingine anaweza akapata cheti kwa sababu ya udanganyifu halafu anaweza akapewa majukumu ya kwenda kuhudumia umma, tuseme labda amesomea udaktari lakini akafanya udanganyifu halafu ataenda kutibu mtu madhara yake ni makubwa sana kwa wale ambao wanapata huduma hiyo.

"Na vilevile tukirushusu udanganyifu kwenye elimu ni kama vile kulea ama kuruhusu rushwa kwa wanafunzi wetu kwamba wewe mwanafunzi njia nzuri ya kuendelea ni kuwa mdangaanyifu na ndio maana hatua ambazo tumezichukua baadhi ya watu wanalaumu kwamba tumekuwa wakali sana na naomba tu umma utuelewe kwamba tunafanya hivyo kwa kulinda heshima ya mfumo wetu wa elimu kwaiyo mliona kwenye Baraza la mitihani tumesimama kidete hasa tumeleta mabadiliko ya sheria ili kuwabana zaidi wanaofanya udanganyifu kwenye mitihani." amesema Mkenda na kubainisha kuwa.

"Sasa kuhusu vyuo vikuu, vyuo vikuu vyote vina kanuni za kusimamia mitihani ambazo zinafahamika na TCU na kwa kawaida Chuo Kikuu ukikamatwa umedanganya kwenye mtihani adhabu yake ni kufukuzwa Chuo moja kwa moja, ukishapata uhakika kwamba umedanganya mtihani hukumu yake unafukuzwa chuoni.

"Mimi nina watu chungu nzima ofisini wazazi wao wanaomba kwa waziri, tunaomba mwanetu arudi alifukuzwa, ameonewa, ninachofanya nikurudi kwenye utaratibu wa Chuo kuuliza nini kimetokea, unakuta utaratibu ulifanyika Baraza limemfukuza Chuo amepewa muda wa kukata rufaa hajakata ama amekata lakini mimi kama waziri nimekataa kata kata kuingilia mamlaka ya vyuo vikuu wanapochukua hatua kama hizo kwa sababu tunalinda sana suala la mitihani.

"Sasa tuhuma zingine ni kwamba ambazo tumeziona zimetoka kwenye gazeti moja kwamba kuna utaratibu wa wanafunzi kuhonga ili matokeo yaliyokwisha ingizwa kwenye mfumo wa tehama yabadilishwe, sasa kulitokea tuhuma kama hizo katika chuo kimoja hapa nchini na kikamtaja jina la mwanafunzi na mtu ambaye alihusika kubadilisha yale matokeo, nilimwambia Katibu Mkuu aunde tume huru kwenda kuchunguza, ikiwa ni pamoja na idara ya usalama wa Taifa na wataalamu wa tehama, waliingia wakaangalia mfumo wote wa tehama uzuri ukishaingiza matokeo yote kwenye tehema mabadiliko yeyote yanayofanyika yanaacha kumbukumbu ya mabadiliko, lazima utaona mtu aliingia saa ngapi aliingiza alama ngapi nautaona tarehe ngapi hizo alama zilibadilishwa.

"Kwaiyo tulichunguza tukagundua si kweli na kwenye Chuo hicho nadhani kuna mnyukano tu, kuna mtu au watu kwa sababu wanajua makamu Mkuu wa Chuo anastaafu karibuni basi sijui ni kuchafuana huko kwa sababu kuna dalili kwamba katika kinyang'anyiro cha kutaka kuchukua nafasi watu wanachafuana lakini nasema hivi Katibu Mkuu tumekubalina ataiomba TCRA ichukue Chuo kilekile kama majaribio kwa sababu ya tuhuma tulizozisoma kwenye gazeti kwenda kufanya uchunguzi wa matokeo yote ambayo yameingizwa kwenye  tehama na kuangalia matokeo yanapoingizwa yanapobadilika nani anabadilisha.

Pamoja na hayo Waziri Mkenda amewaomba waandishi wa Habari kutoa ushirikiona pale unapohitajika juu taarifa wanazoziandika ili kuweza kulisaidia Taifa na sekta ya elimu juu udanganyifu unaofanyika katika mitihani na vyuo vinavyohusika.

Vile amesema wataendelea kuchukua hatua kali kwa maslahi mapana ya mfumo mzima wa elimu na wataalamu wanaozalishwa nchini kupitia Vyuo Vikuu nchini.

DKT. AYUB RIOBA : VYOMBO VYA HABARI VYA AFRIKA SHIRIKIANENI NA KUBADILISHANA MAUDHUI

$
0
0

Na Magrethy Katengu, Dar es Salaam

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC  Dkt. Ayubu Rioba Chacha amevishauri vyombo vya habari vya Afrika kushirikiana na kubadilishana maudhui badala ya kuchukua kutoka taasisi za Magharibi taarifa ambazo zimekuwa na mitazamo ya nje na mara nyinyi zinabagaza Afrika.

Ushauri huo ameutoa leo Julai 12,2024 Jijini Dar es salaam katika hafla fupi ya kusaini  makubaliano yaliyofanikiwa kati  ya TBC na sauti ya Nigeria (VON)  ambapo amesema Nchi za Afrika zimekuwa zikibagazwa sana hasa na vyombo vya Magharibi kwani ikiangaliwa kwa makini ni  mtazamo uleule uliokuwepo enzi na enzi umeendelezwa sasa ifike wakati Uzalendo uanzishwe kupitia mashirikiano ya kubadilishana maudhui.

"Afrika ikishirikiana kiuchumini itakuwa na mafanikio makubwa sana hivyo naamini tutakaposhirikiana wenyewe kwa wenyewe tutakuwa tunaandaa maudhui na tunarusha taarifa chanya na kuweka katika mitandao ya kijamii maudhui ambayo yatakuwa yanaakisi mitazamo yetu ya kiafrika "amesema Rioba

Hata hivyo Rioba amebainisha kuwa TBC imefanya kielelezo na vyombo vingine havina budi kuiga kwani makubaliano hayo yatasaidia kukuza lugha adhimu ya kiswahili na kupata watangazaji wa lugha hiyo, kuzalisha wataalamu wa kufundisha na kutoa mafunzo ya kiswahili.

"Shirika la utangazaji Tanzania limekuwa na uhusiano mzuri na mashirika na taasisi mbalimbali za habari na utangazaji katika bara la Afrika  kupitia makubaliano haya yataleta tija kubwa ya kukuza ajenda ya Afrika kutokana na umuhimu utakaoonekana kwa kuelezea masuala yanayohusu mazuri ya nchi za Afrika " amesema Dkt Rioba

Hata hivyo Rioba amesema ili kuhakikisha wanakuwa na ushirikiano wa kudumu kati ya Tanzania na Nigeria darasa la lugha ya kiswahil limeanzishwa nchini Nigeria ili wawekezaji wa nchi hiyo waweze kutumia lugha hiyo wanapotembelea Afrika Mashariki na kumekuwa na mazungumzo ya kushirikiana mafunzo ya lugha ya kiswahili na chuo cha Port Harcourt pia chuo kikuu cha  Ghana kutoa Shahada ya lugha ya kiswahili

Pia amesema makubaliano waliyoingia leo yana historia ndefu toka enzi za Rediao Tanzania Dar es salaam (RTD)kupitia idhaa ya kingereza (external services )ilikua na ushirikiano wa karibu na  shirika la utangazaji Nigeria (Nigeria  broadcasting corporation-NBC) kupitia idhaa ya matangazo ya nje ambazo zilishinikiza shughuli za ukombozi barani Afrika .

"Baada ya bara zima kupata uhuru ushirikiano huu ulififia kutokana na mabadiliko yaliyotokea katika mfumo wa kisiasa na kiuchumi duniani  kudhoofisha umoja wa  nchi za Afrika husika kuanza utegemezi katika nyanja mbalimbali kutoka mataifa ya nje hususani Ulaya Marekani"amesema Ndace

Aidha ili kuhakikisha Tanzania mazuri yake yanasemwa huko Duniani TBC inatarajia kuanzisha chaneli ya   mtandaoni itakayotangaza habari kwa lugha ya kingereza kuelezea mazuri yanayotekelezwa na bara la Afrika.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa VON Bw. Jibrin Ndace amesema wanashukuru kwa fursa hiyo ambayo itasaidia kukuza ajenda ya Afrika kutokana na umuhimu ulioonekana kwa waafrika wenyewe kuelezea masuala yanayowahusu kwa mitazamo yao.

IPENI JAMII TAARIFA SAHIHI, UZUSHI USIPATE NAFASI - RAS TANGA

$
0
0

NA MASHAKA MHANDO, Tanga

MAAFISA Habari, Uhusiano na Mawasiliano Serikalini  Mkoani Tanga, wametakiwa kutumia dhamana waliyopewa  kusimamia vitengo vya Mawasiliano kwa kutoa taarifa sahihi kwa jamii juu ya shughuli za maendeleo zinazotekelezwa na Serikali, ili kuondoa taarifa za uzushi.



Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga (RAS) Pili Mnyema alisema hayo wakati akiwapongeza Wakuu wa Vitengo vya Habari na Mawasiliano Serikalini, katika Mkoa wa Tanga vilivyopata tuzo katika utoaji wa taarifa za kazi za Serikali, ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kufuatia tathmini iliyofanywa na Wizara ya Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa kuangalia namna Wizara, Taasisi, Ofisi za Mikoa na Halmashauri zinavyotoa taarifa kwa umma kwa kipindi cha mwaka 2023/2024.

Alisema, jamii ikipata taarifa sahihi, taarifa za uzushi hazitaweza kusambaa na kuipotosha jamii kwavile Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeleta fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali ili kutatua kero za wananchi.

 Alisema ni vizuri jamii ikafahamu kazi kubwa inayofanywa na Serikali yao, na hivyo Maafisa Habari wana wajibu wa kutoa taarifa za utekelezaji wa miradi hiyo.

Akizungumzia umuhimu wa vitendea kazi kwa Vitengo hivyo, Mnyema alisema, kufuatia mabadiliko makubwa katika teknolojia ya habari, ipo haja ya Vitengo kupatiwa vifaa vya kisasa ili watendaji wake waweze kufanya vizuri zaidi.

"Kwa Mkurugenzi hapa (Mkurugenzi wa Jiji la Tanga), sasa ni fursa kwako, kuhakikisha kwamba, tunaimarisha Kitengo chetu cha Mawasiliano kwa kuwapatia vifaa vya kisasa, lakini pia na kuwawezesha masuala ya usafiri kwenda kuzunguka kwenye miradi, najua Halmashauri ya Jiji tuna miradi mingi sana ambayo Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuletea fedha za kutosha, kwa hiyo tuna kazi kubwa ya kuhabarisha umma nini kimefanyika katika kipindi cha awamu ya Sita ya Serikali"  alisema RAS Mnyema.

Vitengo vya Mawasiliano Serikalini vilivyopata tuzo ni kutoka Halmashauri ya Jiji la Tanga, ambayo ilishika nafasi ya tisa (9) kati ya 184, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ya tisa (9) kati ya 26 na Tanga UWASA ya sita (6) kati ya 84.

Tathmini hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya kuimarisha mawasiliano ya Serikali kwa umma, lengo likiwa ni kuwafanya Maafisa Habari kutoa taarifa kwa kina kwa wananchi kuhusu miradi yote ya maendeleo


TCU YAFUNGUA DIRISHA LA UDAHILI KWA MWAKA WA MASOMO 2024/2025

$
0
0

Na Mwandishi Wetu


Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imefungua dirisha la kwanza la udahili kwa mwaka wa masomo ya elimu ya juu 2024/2025 kuanzia leo July 15 hadi August 10 mwaka huu.

Akifungua Dirisha hilo Katibu  Mtendaji Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU, Profesa Charles Kihampa Leo mbele ya vyombo vya habari amesema dirisha la kwanza la udahili kwa litakuwa wazi kuanzia leo July 15 hadi August 10 mwaka huu huku akitoa tafadhali kwa waombaji wote.

"Naomba taarifa hii ifike kwa wadau wetu wa elimu ya juu ndani na nje ya nchi na taarifa hii inahusiana na kufunguliwa rasmi kwa dirisha la udahili kwa waombaji wa shahada ya kwanza kwa mwaka wa 2024/2025 kwa maana ya mwaka wa masomo.

"Kama nilivyosema dirisha hili litakuwa la kwanza, tunafungua dirisha la kwanza kwa mwaka wa masomo 2024/25 na tunategemea kwamba dirisha hili litakuwa wazi kuanzia leo July 15 hadi August 10 mwaka huu.

"Utaratibu wa masomo ama utaratibu wa udahili  kwa mwaka 2024/25 tuna makundi matatu ambayo tunatarajia ya wale ambao wataomba udahili."amesema Kihampa na kuongeza kuwa.

"Kundi la kwanza ni wale wenye sifa stahiki za kidato cha sita na hili ni kundi kubwa, lakini kundi la pili ni wale wenye sifa stahiki za stashahada kwa maana ya diploma ama sifa nyingine linganifu, sifa nyingine linganifu inawezeka kuwa ni mtu ana shahada lakini anataka kwenda kusoma shahada nyingine.

"Lakini kundi la tatu ni wale wenye sifa stahiki za cheti cha awali cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania inayojlikana kama 'Foundation Certificate' hili ndio kundi la tatu." Kihampa amebainisha kuwa.

"Kwa waombaji ili kufahamu sifa stahiki za makundi haya matatu ambayo nimeyataja wanashauriwa kwenda kusoma vitabu vya muongozo na vitabu hivi vya muongozo vinajulikana kama 'Bachelor Degree Admission Guide Box for 2024/2025 Academic Year', vitabu hivi vinapatikana katika tovuti ya Tume ya Vyuo Vikuu, ukiingia tu kwenye tovuti ya Vyuo Vikuu utaona pale vinaonekana vile vitabu, hapo sasa muombaji wa kundi lolote ataweza kujua na tuna vitabu viwili kwa wale wenye sifa stahiki za kidato cha sita na kingine ni kile chenye sifa stahiki kwa stashahada na sifa nyingine linganifu pamoja na cheti cha msingi.

"Utaratibu wa kutuma maombi ni kwamba maombi haya yanatumwa moja kwa moja kwenye Vyuo ambavyo muombaji amevichagua, kile Chuo anachokitaka ataingia kwenye tovuti ya Chuo hicho atakuta maelekezo mahususi ambayo yametolewa na Chuo. Kwaiyo muombaji anashauriwa zaidi ya kusoma ile miongozo kutoka kwenye tovuti ya Vyuo Vikuu aingie kwenye tovuti ya Chuo anachokihitaji atakuta maelekezo mahususi halafu atakuta namna ya kuweza kujisajili au kufungua akaunti yake ili aweze kutuma maombi yake ya kuomba udahili na vingezo na sifa za waombaji wa udahili."amesema.

Katika hatua nyingine amesema "Maswala muhimu ya kuzingatiwa na waombaji na ninaomba hili lieleweke vizuri, tumeweza kuweka kwa ujumla masuala makubwa manne ya kuzingatiwa. Jambo la kwanza ni kusoma kwa makini na kuelewa muongozo wa udahili ambao umetolewa na TCU lakini pia na maelekezo mahususi ambayo yametolewa na Vyuo kabla ya kutuma maombi.

"Lakini pia waombaji wanashauriwa kuingia katika tovuti za vyuo na kuwasiliana na vyuo moja kwa moja ili kujua taratibu za kutuma maombi na kupata taarifa taarifa za kina kuhusu programu za masomo ili kujiridhisha kabla ya kutuma maombi.

"La tatu ni kutuma maombi moja kwa moja vyuoni kupitia mifumo ya kimtandao, kwaiyo hakuna utaratibu wa kusema unampa mtu fulani zile taarifa zako au kuna fomu ambazo utajaza kwa maana ya nakala ngumu lakini muombaji anaingia kwenye Chuo husika atakuta mfumo wa kimtandao atajisajili pale halafu ataendelea kutuma maombi.

"Jambo la nne ni kwa wale waombaji ambao wana vyeti vilivyotolewa na mabaraza ya mtihani ya nje ya nchi hawa wanapaswa kuwasilisha vyeti vyao katika Baraza2 la mitihani la Tanzania kwa wale ambao wana vyeti vya Elimu ya sekondari."

Kihampa hakuishia hapo amesema "Lakini wale ambao wana vyeti vya stashahada hawa wanashauriwa kutuma kwanza vile vyeti vyao katika Baraza la ufundi na mafunzo stadi Nacte, watapeleka kule halafu wataweza kupata ulinganifu lakini pia wataweza kupata namba ambayo itatumika katika wao kutuma maombi yao vyuoni, namba hii inajulikana kama 'Award Verification'.

"Tume inapenda kuwahimiza waombaji wote wa udahili kuendelea kupata taarifa sahihi kupitia tovuti ya TCU, tovuti za Vyuo vilivyoruhusiwa kudahili wanafunzi wa shahada ya kwanza pamoja na taarifa mbalimbali zinazotolewa na TCU kupitia vyombo vya habari kama ambavyo tunazungumza hapa Leo.

Aidha amehitimisha kwa kutoa tahadhali "Nitoe pia tahadhali kunapokuwa na jambo kubwa kama hili kunaweza kukajitokeza watu ambao wanakuwa kama wanakaa katikati, kwaiyo niwaombe kwamba waombaji wote wanaotaka kujiunga na shahada ya kwanza katika Vyuo vya Elimu ya Juu nchini, maombi yanawasilishwa moja kwa moja kwenye Vyuo husika.




Msajili Hazina ateta na Wahariri kuelekea Kikao Kazi cha Rais Samia na ‘Ma-CEO,’ Wakurugenzi wa Bodi Arusha

$
0
0

NA MWANDISHI WETU

KUELEKEA Kikao Kazi cha Ofisi ya Msajili wa Hazina na Maofisa Watendaji Wakuu, Wakurugenzi na Wenyeviti wa Bodi wa Taasisi za Umma, Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu, amebainisha kwamba dhima kuu itakuwa dhana moja muhimu ya kuimarisha utendaji kazi wa Makampuni ya Tanzania nje ya mipaka yetu.

Kikao Kazi hicho siku tatu kinachotarajiwa kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 600, kitafanyika katikati ya mwezi ujao jijijni Arusha, ambako Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi, kuangalia utekelezaji wa maagizo yake aliyoyatoa mwaka jana aliposhiriki kikao kazi cha kwanza kama hicho.

Akizungumza na wahariri na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam, Mchechu alisema dhima ya kuangalia uwekezaji na utoaji huduma wa taasisi za ndani nje ya mipaka, itaanza na taasisi zenye utayari, hususani zile zilizopata mafanikio ndani ya nchi.

“Rais Samia alikubali kuwa mgeni rasmi, kama tulivyomuomba Siku ya Gawio na sasa atashiriki kikao hiki kitachojumuisha Maafisa Watendaji Wakuu, Wakurugenzi na Wenyeviti wa Bodi zaidi ya 600, ambacho kitajielekeza katika kuona makampuni ya Tanzania yanavyoimarisha shughuli zake nje ya mipaka yetu.

“Kwa sababu haya yalikuwa ni maagizo na changamoto kutoka kwa Mheshimiwa Rais Samia mwenyewe aliyokuwa ametupatia katika kikao cha kwanza kama hiki mwaka jana.

“Katika dhima hii ya kutaka kuwa na uwekezaji wa taasisi za umma nje ya nchi, lengo letu ni kuanza na taasisi zenye utayari wa kuvuka mipaka ya nchi, huku lengo la pili likiwa ni kuzifanya taasisi zijue kwamba zinapaswa kubadilika, lakini zifanye hivyo zikiwa na taswira kubwa wanayoiona mbele.

“Kwa hiyo ni wazi lazima watakuwa ni wale wanaofanya vizuri ndani ya nchi, ndio wataweza kwa urahisi kwenda nje ya nchi. Tunaposema kwenda nje ya nchi, haimaanishi tu kwenda kuwekeza mitaji kule, tunalenga pia kufikisha huko huduma zitolewazo ndani ya nchi,” aliongeza.

Akitolea mfano mashirika kama ATCL, alisema ingawa inatambulika kwamba huduma zake zinapatikana nje ya nchi, lakini ofisi yake inadhani kwamba zinapaswa ziende nje na kugusa jamii ya huko kwa ufanisi na ushindani mkubwa.

“Mfano wa pili ni Kampuni kama TRC na Tazara, ni kampuni ambazo ili zifanye vizuri katika huduma zake ni lazima ziguse usafirishaji unaovuka mipaka ya nchi yetu na kwa kufanya hivyo, tutaweza kupata ‘rertuns’ kama nchi, je tunaweza kupata maslahi ya kile tulichokiwekeza huko.

“Kwa hiyo tunapozungumza ‘investment beyonds Tanzania,’ ni kuangalia nini tunaenda kufanya nje. Lakini zipo nyingine zinazoweza kwenda kufanya uwekezaji kabisa nje ya nchi,
tunatamani mabenki yetu makubwa yawe na uwekezaji mkubwa nje ya mipaka yetu, wawe na matawi yao nje ya Tanzania.



“Tuna Benki ya CRDB ambayo wako Burundi na sasa wanaenda DRC, lakini tunamani CRDB au NMB wanakuwa na uwekezaji mwingi zaidi nje ya nchi, kwa sababu tayari washakua wakubwa ndani ya nchi yetu,” alisisitiza Mchechu katika mkutano huo na wahariri na kuongeza:

“Sasa maana yake ni nini? NMB leo hata wakiwa na tawi Zambia, kukiwa na wafanyabiashara wanaoendesha shughuli zao katika kikoa ya Mtwara au Lindi, hawatoumiza kichwa namna ya kufanya miamala ya kibiashara katika nchi za Zambia au Malawi, kwa sababu tayari ana benki ambayo ina matawi ndani ya nchi na nje.”
 

Mchechu alisema ndio maana Wakenya, wananufaika na uwepo wa matawi ya benki zao za KCB na Equity ambazo zipo nchini Tanzania, hivyo ni rahisi sana kwa Mkenya kufanya biashara kwa ufanisi nchini, na kwamba Tanzania nayo inapaswa kuwa mahiri, lakini ianze katika ngazi hizo.

Aliongeza kuwa, pamoja na hayo kikao hicho kina umuhimu mkubwa, ikiwemo kujua maagizo na maelekezo ya Serikali kupitia viongozi wakuu ya wapi wanataka tuelekee na kwa kasi gani, ikiwa ni pamoja na maafisa watendaji wakuu na wenyeviti wa bodi kubadilishana mawazo na mbinu mbalimbali za uendeshaji biashara.

Aidha, Mchezo aliwaleza wanahabari hao kuwa, katika dhima nne (4R’s) alizokuwanazo Rais Samia, Ofisi ya Msajili imechukua R mbili za ‘Reforms na Rebulding’ ambazo wataendelea kuzisimamia hizo na kwamba mabadiliko ya utendaji wa taasisi ni safari ndefu, na sio jambo la siku mmoja, mwaka mmoja wala sio la taasisi moja.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda, alisema agizo la Rais Samia kutaka taasisi, mashirika na makampuni yetu kuvuka mipaka ya nchi katika kuhudumia, liliwahi kutolewa na aliyekuwa Rais wa Kwanza, Hayati Julius Nyerere, akiumizwa na ukubwa wa taasisi zetu kwa ndani tu.



“Mwalimu Nyerere aliwahi kuonesha kuumizwa na uwekezaji wa Benki ya NMB, aliwahi kusema na namnukuu; ‘Tunaposema hizi ni benki kubwa kubwa, hivi ni vibenki viko katika nchi zetu tu Tanzania hapa, hatuzioni zikitoa huduma nje ya nchi huko, zina ukubwa gani..’

“Leo Rais wa Awamu ya Sita Dk. Samia anazungumza kile ambacho Rais wa Awamu ya Kwanza alikizungumza miaka ya 1990 huko na kuweka mikakati ya kuvuka nje. Tumeona NBC wamefanya, tumeona NMB nao wamefanya kubwa.

“Msajili wa Hazina, pamoja na uwekezaji nje, nadhani mnapaswa kufanya kitu kuelimisha Watanzania juu ya kilichofanywa na NMB katika Soko la Hisa la London. Uwekezaji wa nje wa mitaji na kufungua matawi, nimeuliza hapo juu ya nchi zilizoainishwa, nikaambiwa ni nchi za SADC.

“Nadhani kuna haja ya kufikiri na kutafakari kuwekeza mitaji kwa maana ya hisa katika masoko makubwa ya kimataifa ya hisa kwa makampuni na mashirika yetu yanayofanya vizuri, nadhani pengine tutakuwa tumepiga hatua sahihi,” alichangia Kibanda ambaye ni mwenyekiti wa zamani TEF.











TGDC yatoa elimu ya Jotoardhi Sabasaba

$
0
0

Na Mwandani Wetu

KAMPUNI ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) imetoa elimu kwa wananchi kwa siku 16 kuhusu nishati ya Jotoardhi.

Elimu hiyo imetolewa kwa siku 16 na maofisa wa TGDC walioshiriki Maonesho ya 48 ya Biashabara ya Kimataifa Dar es Salaam maarufu Sabasaba yaliyofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam.


Maonesho hayo ambayo yalianza Juni 28 hadi JULAI 13 Julai mwaka huu yameandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ambapo, TGDC iliweza kutoa elimu kwa wananchi na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi waandamizi wa Serikali waliotembelea maonesho haya.

Miongoni mwa viongozi waliofika katika banda la TGDC ni Rais Mstaafu wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete ambaye alionesha kufurahishwa na hatua iliyofikiwa katika utafutaji wa nishati jadidifu ya jotoardhi.

Kikwete alienda mbali zaidi na kusema banda la TGDC limemkumbusha namna alivyoenda nchini Kenya kujionea mradi wa Jotoardhi wa Olkaria wakati wa hatua za mwanzo za utafutaji nishati hiyo.

Pamoja naye, TGDC ilitembelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Felschesmi Mramba ambaye yeye kwa upande wake alishauri kuwa ni vyema kwa kampuni kuongeza juhudi na kutumia njia rahisi zaidi za kuipata nishati ya umeme wa jotoardhi ili uingie kwenye gridi ya taifa pamoja na mambo mengine uchochee na kukuza uwekezaji na uchumi kwa ujumla.

Aidha, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Mhandisi Innocent Luoga alifurahishwa na hatua zilizofikiwa na kushauri kuwa ni vyema kwa kampuni kuongeza juhudi na kutumia maonesho haya kutafuta wawekezaji zaidi ili waje kuwekeza na kuhakikisha umeme wa jotoardhi unapatikana.

Vilevile, Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) DkLucy Mboma aliipongeza TGDC alipotembelea banda lake na kupata elimu juu ya maendeleo ya upatikanaji wa nishati ya jotoardhi ambapo alielezwa kuwa kwa sasa kampuni inaendelea na miradi yake mitano ya kipaumbele hususan mradi wa ngozi (megawati 70) ambao upo katika hatua ya uhakiki ili baadaye ufikie hatua ya uzalishaji unaotarajiwa kuanza na megawati 30.

Wageni waliotembelea banda la TGDC ni pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Halfan Halfan pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo ya PURA Mhandisi Charles Sangweni ambao walionesha shauku yakuwa ipo haja TGDC na PURA kuendeleza mashirikiano katika utendaji kutokana na shughuli zao kuingiliana ambapo kwa kufanya hivyo itaongeza tija kiutendaji na kuleta matokeo kwa haraka.

Wanafunzi na wananchi pia walikuwa ni sehemu ya waliotembelea banda la TGDC ambapo wapo waliosema kuwa TGDC ni mkombozi wa mazingira baada ya kuelezwa jinsi nishati hiyo ilivyo rafiki wa mazingira na ilivyo jadidifu isiyoathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi.

TGDC ni kampuni tanzu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) inayomilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 iliyoanzishwa mwaka 2013 na kuanza shughuli zake rasmi mwaka 2014 ikiwa na jukumu la kuendeleza rasilimali ya jotoradhi nchini ambapo kwa sasa inayo miradi mitano ya kipaumbele yenye lengo la kuzalisha megawati 200 kwa awamu ikiwemo mradi wa Ngozi (MW 70), Kiejo Mbaka (MW60), Songwe (MW5-38), Luhoi (MW5) na Natron (MW60) ambapo kwa sasa TGDC ipo katika hatua ya maandalizi uchorongaji visima vya uhakiki wa rasilimali ya Jotoardhi.

Maonesho haya yalifunguliwa rasmi tarehe 3 Julai na Mheshimiwa Dk Filipe Jacinte Nyusi, Rais wa Jamhuri ya Msumbiji akiwa na mwenyeji wake Mheshimiwa Dk Samia Suluhu Hassan na kufungwa rasmi Julai 13, 2024 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi.

TGDC Tunastahili Nishati Safi


 

Kaya 400,000 kuhitimu TASAF

$
0
0

Na Mwandishi Wetu, Arusha

MFUKO wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), umesema upo katika hatua za mwisho za kuondoa kaya 400,000 ambazo zilikuwa kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini baada ya kuweza kuboreka kimaisha.

Mziray amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao wamefanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na TASAF mkoani Arusha.

Alisema tangu mfuko huo uanzishwe umeweza kusajili zaidi ya kaya milioni 1.3 zenye wanufaika zaidi ya milioni 5.2, hivyo baada ya kufanya tathmini wamebaini kaya laki nne zinapaswa kuhitimu kunufaika na mpango.

"TASAF ipo kwa zaidi ya miaka 24 sasa tumeweza kufikia kaya maskini milioni 1.3 zenye wanufaika milioni 5.2, baada ya kuchakata tumebaini kaya laki nne zimeboreka kimaisha hivyo hazina sifa ya kuendelea na mpango huu," alisema.

Mziray alisema mkakati huo wa kuondoa kaya laki nne haujaungwa mkono na wahusika pamoja na baadhi ya wanasiasa, lakini hakuna namna kwani kutowaondoa kuwakwamisha malengo ya mfuko.

Alizitaka kaya ambazo zitaguswa na uamuzi huo zitambue kuwa mfuko huo unapaswa kuwakomboa Watanzania asilimia 26 wanaoishi katika umaskini.

Mziray alisema hadi sasa mfuko umegusa asilimia 8 ya maskini nchini, hivyo mikakati yake ni kuhakikisha inafikia asilimia 26 iliyopo.

Alisema iwapo uamuzi huo utaungwa mkono na wa wadau wote utasaidia kufanikisha mipango yao.

Mkurugenzi huyo alisema mfuko huo ulianza kwa kutekeleza miradi ya miundombinu ya afya, elimu na maji ambapo halmashauri 42 za Tanzania Bara na Zanzibar ila kwa sasa wapo katika halmshauri zote 186.

“Tanzania kuna umaskini wa mahitaji ya msingi ambapo takwimu zinaonesha ni asilimia 26 ya Watanzania wote na umaskini wa kukosa hata mlo mmoja ni asilimia 8. Hivyo mkakati wetu TASAF ni kuhakikisha hizi asilimia zinaisha kwa kushirikiana na jamii husika,” alisema.

Aidha, Mziray alisema TASAF inatarajia kutumia Sh trilioni 2 kwa ajili ya mpango wa pili ulioanza 2020 hadi 2025 na kuzitaka jamii zitakazo nufaika kutunza na kulinda miradi husika.

“Hapa Arusha tumetekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu kupitia ufadhili wa OPEC, lakini tunashukuru ushiriki wa wananchi ni mkubwa sana,” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miradi TASAF, John Steven alisema mfuko huo umewezesha asilimia 97.6 ya watoto wa kaya za maskini kupata huduma za kliniki na asilimia 98.3 kusoma shule.

Steven alisema pia
TASAF imenufaisha kaya 24,000 zenye watu wenye ulemavu katika kaya milioni 1.3 ambazo wamezitambua na kuzisajili.


Steven alisema TASAF imefikia zaidi ya wananchi milioni 5.2 katika halmashauri za wilaya, miji na majiji 186 ambapo wanawake ni asilimia 55.7 na wanaume asilimia 44.3.


Alisema mfuko huo umeweza kubadilisha maisha ya kaya mbalimbali, hali ambayo inatoa msukumo wa kuendelea na miradi ambayo inatekelezwa.


Mkurugenzi huo alisema takwimu zinaonesha walengwa wamenufaika na huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu, hali ambayo inatoa tafsiri kuwa mradi huo unalipa.

 

“TASAF imeweza kuleta mabadiliko katika sekta mbalimbali, lakini kubwa zaidi ni sekta ya elimu na afya ambapo tumeona asilimia 97.6 ya walengwa wameweza kupata huduma za afya na asilimia 98.3 waneweza kusoma.


Ila kubwa zaidi ni watoto 4,600 kutoka familia maskini wamefanikiwa kujiunga na elimu ya juu katika vyou mbalimbali na kufanikiwa kupata mkopo kwa asilimia 100,” alisema.

 

Alisema kupitia TASAF walengwa wamekuwa wakipata ahueni katika baadhi ya huduma zinazotolewa kwenye huduma za afya na elimu.

 
Mkurugenzi huyo alisema mchakato wa kuwapata wanufaika wa TASAF unahusisha wananchi wenyewe kwa kuchagua nani apate.

 

Steven alisema katika eneo la ukuzaji uchumi wa kaya maskini kwa miaka 24 TASAF imeweza kusajili vikundi 60,327 vyenye walengwa zaidi laki nane wameweza kuweka akiba Sh bilioni 7.9 na kukopeshanya zaidi ya Sh bilioni 3.2.


Pia alisema program hiyo imewezesha wananchi kupata ajira za muda, hali ambayo inakuza uchumi wa wananchi na nchi kwa ujumla.

 

Alisema awamu ya pili ya program hiyo miradi 37, 331 imetekelezwa katika halmashauri 123 na kwamba wanarajia kufikia halmashauri 65 zilizobakia.

Mwenyekiti wa kijiji cha Oldonyowas wilayani Arusha, mkoani humo, Godfrey Ayo alisema TASAF imewezesha kijiji hicho kuwa na shule ya Sekondari Oldonyowas hali ambayo imechochea watoto wengi kusoma.

Diwani wa kata ya Bwawani, Justine Saray ameipongeza Serikali kupitia TASAF kwa kuwajenga hospitali kwenye kijiji cha Temi ya Simba ambayo itapunguza vifo vya mama wajawazito na watoto.


 

MWENYEKITI KIBAHA MJI AFANYA ZIARA MATAWI 14 KUWAHIMIZA WANACHAMA KUJIANDIKISHA

$
0
0

NA VICTOR MASANGU, KIBAHA

Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Wilaya ya Kibaha mjini (UWT) Elina Mgonja  katika kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa amefanya ziara ya kikazi na kufanikiwa  kuyatembelea jumla ya  matawi 14  kwa lengo la kuweza  kujionea hali halisi ya uandikishaji kwa njia ya kieletroniki.


Ziara hiyo ambayo imefanyika katika kata mbili za Tangini na Maili moja pia ilikuwa na lengo la kuwahimiza wanawake kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi katika kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Akizungumza katika ziara hiyo ya kikazi Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini Elina Mgonja amesema kwamba ameamua kufanya ziara hiyo akiwa na wajumbe wa kamati ya utekelezaji ili kujionea mwenendo mzima wa zoezi la uandikishaji wa wanachama wa CCM  kwa njia ya kieletroniki.

Pia Mgonja alibainisha kwamba wamebaini kuwepo kwa mwamko mkubwa kwa wanawake kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo la kujisajili kwa njia ya kisasa kwa ajili ya kuweza kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa ambao unatarajjwa kufanyika mwaka huu.

"Mimi kama Mwenyekiti nimeambatana na wajumbe wa kamati ya UWT na tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutembelea matawi 14 ambayo yapo katika kata ya Tangini pamoja na kata ya maili moja na tumekuta idadi kubwa ya wanawake wamejisajili kwa mfumo wa kieletroniki,"alisema Mgonja.


Mgonja amesema kwamba lengo ni kuhakikisha wanakuwa na wanachama wengi wa CCM ambao wamesajiliwa kwa njia ya kisasa pamoja na kujiandikisha katika daktari la wapiga kura lengo ikiwa ni kufanya vizuri na kushinda kwa kishindo katika uchaguzi wa serikali za mitaa.


Kadhalika Mgonja amewahimiza makundi mbali mbali ya wakinamama,vijana,wazee pamoja na wanachama wote kujiandikisha katika daftari la kupiga kura pamoja na kuboresha taarifa zao ili waweze kupata fursa ya kushiriki katika uchaguzi huo.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo amempongeza kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suhuhu Hassan kwa kuweza kutoa fedha kwa ajiili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo  ikiwemo katika  sekta ya afya.maji,elimu,pamoja na miundombinu ya barabara.


Mgonja amemshukuru kwa dhati Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka pamoja na mke wake Mama Selina Koka  kwa kuweza kushirikiana kwa hali na mali katika kuwasaidia wanawake katika suala zima la kuleta maendeleo chanya katika nyanja mbali mbali.

Kwa upande wake Katibu wa UWT Kibaha mjini Cecilia Ndaru amewahimiza wanachama kuweka misingi mizuri ya kupendana na kuwa na umoja hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguguzi wa serikali za mitaa.

 Katika ziara hiyo ya UWT Mwenyekiti huyo ameambatana na viongozi mbali mbali wa chama cha mapinduzi  wakiwemo baadhi ya madiwani wa kuchaguliwa pamoja na wale madiwani wengine wa viti maalumu sambamba na viongozi wengine wa UWT.


 

Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>