Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

BITEKO AZIASA BENKI KUENDELEA KUDHAMINI MANESHO YA WAFUGAJI KIBIASHARA

$
0
0

 

Naibu Waziri Mkuu Dk. Doto Biteko (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Kilimo, Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Christopher Mwalugenge (wapili kushoto) alipotembelea Banda la benki ya NMB katika sherehe za ufungaji wa maonesho na mnada wa mifugo uliyofanyika katika Kata ya Ubena Zomozi wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Ushauri Kilimo wa Benki ya NMB, Isaac Masusu na wapili kulia na meneja Mwandamizi idara ya Bima wa Benki ya NMB, Catherine Joshua (Na Mpiga Picha Wetu).

 

Na Mwandishi Wetu

 

NAIBU Waziri Mkuu   Dotto  Biteko ametoa wito kwa Wadau wezeshi wa wafugaji nchini kuendelea kutoa elimu na mikopo ili waweze kufuga kibiashara wapate tija katika ufugaji wao.

Amewataka wadau wezeshi hao kutoishia kwa wafugaji wa kibiashara  bali wawafikie  wafugaji wa kienyeji ili na wao waweze kuwa wafugaji wenye tija nchini  kwani hilo ndilo lengo la serikali ya awamu ya sita ambayo inalenga kuwanyanyua wafugaji.


Naibu Waziri Mkuu Biteko amesema hayo leo  Juni 16  wakati akifunga maonesho hayo ya siku tatu  ambayo yamefanyika Ubena Zomozi  ,Halmashauru ya Chalinze  Mkoani Pwani.

Naibu Waziri Mkuu amefunga monesho hayo akimwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amepata udhuru , hivyo natoa  wito huu kwa uongozi  wa Benki zulizo toa  udhamini huu ambazo ni Benki ya Kibiashsra ya Kilimo TADB na NMB  kundelea  kutoa elimu  kwa wafugaji kwani wao wamekuwa wakichangia migogoro na wakulima kutokana na kwenda kulisha mifugo yao kwenye  mashamba.

"Halmashauri za wilaya nchini  zitunze maeneo ambayo yalitengwa kwa ajili ya malisho ya mifugo"

Serikali itaendelea kuunga mkono maonesho  ya Wafugaji wa Kibiashara nchini ili waendeleze haya maonesho ambayo yanatoa elimu na kutoa Uhalisia wa ufugaji wa kibiashara utakaoongeza tija kwa wafugaji na kupata soko katika soko la kimataifa.

"Maonyesho haya muyapeleke katika ngazi za Kanda ambako yatakutana walengwa ambao ni wafugaji wa kienyeji  na wawape elimu wabadilike na kufuga kibiashara".

"Wafugaji wanapitia changamoto nyingi  hivyo hivyo msichoke kuwapa elimu ya ufugaji  wa Kibiashara nina imani watabadilika taratibu na badaye nchi itakuwa na wafugaji wenye mifugo yenye faida.

"Msiwasahau wafugaji wanaofuga kienyeji  na mwakani naomba  baadhi wawepo kwenye maonesho haya kwani watakapokuja watajifunza  na kubadilika"amesema Biteko.

Wakati huohuo  amewaonya wafugaji  kuacha migogoro  na wakulima  na kuacha tabia ya  kupitisha mifugo  yao kwenye mashamba ya wakulima  huku akiwasisitiza elimu itumike pamoja na sheria katika kumaliza migogoro hiyo.

"Hivi sasa dunia  inakwenda kidigitali hivyo hatakwa sisi ambao tulilelewa katika familia za wafugaji nawaasa mbadilike msiwe kama  wafugaji wa zamani ambao walikuwa wakifuga na kulalia ngozi lakini wafugaji wa kisasa wanalalia magodoro hivyo nanyi mbadilike sasa mfuge mifugo itakayowaletea tija acheni kufuga kizamani" amesema Biteko.

Akiwa katika banda la Benki ya Maendeleo ya kilimo nchini TADB akizungumza  kwa niaba ya Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB David Nghambi amesema kuwa  Benki  hiyo kipindi cha miaka mitatu wametoa mikopo ya zaidi ya  Bil.13, wamewawezesha wafugaji kibiashara ili wawe na uhakika wa masoko kimataifa kwa kunenepa mifugo, pia wametoa mikopo ya bilioni 47 kwa wafanyabishara wa maziwa.

Aidha akikagua banda la NMB Mheshimiwa Biteko amezindua huduma ya Bima kwa mifugo ambayo ni 20,000 kwa mwana na  inatoa kinga dhidi ya vifo vya mifugo vitanyotokana na radi,  majeraha ya ndani na nje kwenye eneo la usafiri, moto, dhoruba, kung'atwa na nyoka mafuriko, magonjwa ya asili na yasiyodhibitika kwa mifugo.


RITA yaunda kamati ya kusimamia msikiti Arusha

$
0
0

Na Mwandishi Wetu, Arusha

WAKALA wa Usajili Ufilisi na Udhamini nchini (RITA)umeunda Kamati ya muda itakayochukua majukumu  ya Bodi ya Udhamini iliyomaliza muda wake ya Taasisi ya Arusha Muslim sambamba na kuunda Kamati ya maalumu ya uchunguzi itakayofuatilia malalamiko ya wanachama kuwatuhumu viongozi hao kuhujumu mali za  taasisi hiyo.


Akizitambulisha kamati hizo katika kikao kilichojumuisha uongozi wa RITA, viongozi wa Serikali ya Wilaya ya  Arusha, viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA ), viongozi wa Arusha Muslim pamoja na wanachama wa msikiti huo, Kabidhi Wasii  Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Frank Kanyusi ameziagiza kamati hizo kutekeleza majukumu yao kwa weledi na uadilifu.

 “Nimeiagiza Bodi iliyomaliza muda wake kuwasilisha RITA taarifa ya mapato na matumizi,” alisema Kanyusi na kuiagiza kamati ya mpito kuhakikisha inafanya marekebisho ya katiba na uchaguzi unafanyika ndani ya siku 60 ili kupata viongozi watakaosimamia taasisi kwa mujibu wa katiba.

Aidha, Kanyusi ameaitaka pia Kamati maalumu ya uchunguzi kukamilisha kazi iliyopewa ndani ya  kipindi cha siku 14 na kuwasilisha taarifa ya uchunguzi RITA.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha, Khamana Simba  ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo kwenye kikao hicho aliwataka wanachama wa Arusha Musilim kuwa watulivu na kwamba serikali ipo pamoja nao kuhakikisha mgogoro huo wa muda mrefu unapata ufumbuzi wa kudumu kwa amani, utulivu na haki.

“Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan inafuatilia kila kitu na ninawahakikishia kuwa ufumumbuzi wa tatizo lenu utapatikana,” amesema katibu tawala huyo na kuwataka waendelee kuwa wamoja na watulivu.

Baadhi ya wanachama  Mustapha Mohamedi na Kassim Collins waliipongeza serikali  kwa kufuatilia mgogoro huo huku wakiomba hatua zichukuliwe kwa watakaobainika kuwa wamefanya ubadhirifu.

Naye, Naibu Kabidhi Wasii Mkuu, Irene Kesulie aliwatoa hofu wanachama wanaoidai taasisi hiyo  kwamba wafuate taratibu ikiwemo kuandika barua na kuziwasilisha RITA ili taratimu za kisheria ziweze kufuatwa na wapate haki yao.

“RITA kama ipo hapa kusimamia haki za wanachama kwa wa sheria na katiba. Tunawasihi endeleeni kuwa watulivu na wavumilivu,” amesema Irene.


 

Gawio la TPA lawakosha wadau

$
0
0

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WADAU mbalimbali nchini wamezungumzia gawio la Sh bilioni 153.9 kwa serkali kuu kwa mwaka 2023/24 lilitolewa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) ni matokeo ya maboresho makubwa yanayoendea na uongozi makini wa mamlaka hiyo.

Mbali ya maboresho na umakini wa uongozi wa mamlaka, uamuzi usioyumba wa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan wa kukaribisha makampuni ya kimataifa yenye uwezo na uzoefu wa kusimamia na kuendesha shughuli za bandari duniani kuja kuwekeza kwenye bandari za Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Raphael Maganga amesema uwekezaji wa miundombinu bandarini umechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza ufanisi wa kiutendaji na hatimaye kupaisha mapato yake na hatimaye kutoa gawio kubwa kwa serikali kuu kwa kipindi tajwa.

“Mifumo yake kisasa inasomana vizuri na ile ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) sambamba na ile taasisi zingine. Kwa gawio la Sh bilioni 153.9 si haba ni matokeo  chanya ya uwekezaji na mchango mkubwa wa sekta binafsi,” amesema Maganga na kuipongeza mamlaka hiyo.

Kwa mujibu wa bosi huyo wa sekta binafsi hapa hapa nchini, maono ya Rais Dk Samia na uwezo wa menejimenti ya TPA kutafsiri maono hayo kwa vitendo yamechangia kuongeza ufanisi ikiwemo kuongezeka kwa mzigo unaopita bandarini.

“Idadi ya mzigo inayopita katika Bandari ya Dar es Salaam umeongezeka katika kipindi cha miaka hii mitatu kwanini maboresho makubwa yaliyofanywa yameweza kuvutia mziigo uliokuwa unapita Bandari za Mombasa na Durban sasa unapita hapa,” amesema Maganga.

Wakili Msomi na Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Mbeya, Dk Tasco Luambano amesema TPA imeweza kutoa gawio ambalo hakuna taasisi yeyote ambapo imetoa gawio mwaka 2023/24 imeweza kufika hata nusu yake  na hivyo kufunga kabisa midomo ya wakosoaji.

“Niliwahi kuzungumzia faida zitakapatikana kutokana na serikali kuwakaribisha washindani tofauti kuja kuendesha shughuli za bandari. Gawio la TPA kwa serikali kuu inadhirisha kuongezeka kwa ufanisi ambao unachangia kuongezeka kwa mapato,” amesema Dk Luambano.

Dk Luambano amesisitiza kuwa Bandari kama lango kuu la uchumi ameshauri wadau kutoka sekta binafsi kushirikiana na serikali kuwekeza kwenye miundombinu ya reli na barabara ilikubiliana na uwingi wa mzigo kwenye bandari.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Dk Godwill Wanga mbali ya kuipongeza TPA kwa kuwa kinara kwa kutoa gawio nono kwa serikali amesema hiyo ni ushuhuda kwa kuboreka kwa mazingira ya kufanya biashara na kuvutia uwekezaji hapa nchini.

“Juhudi kubwa zimefanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk Samia kuhakikisha mazingira ya kufanya biashara yanakuwa rafiki na wezeshi kwa makapuni binafsi na mashirika umma kufanya biashara na uwekezaji,” amesema Dk Wanga.

Serikali imepokea gawio la jumla ya shilingi bilioni 637 kutoka taasisi na mashirika 145 ambapo kati ya pesa hizo shilingi 278 zilitolewa na taasisi zinazofanya biashara (Business entities) na shilingi 358 ni kutoka taasisi za udhibiti (Regulatories)

Akipokea gawio hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Dk Samia alisema serikali inataka kupokea gawio la kutosha kutoka kwa taasisi  zote kuanzia mwakani na kuelezea matumaini yake kuwa anategemea TPA itatoa zaidi ya mara mbili kutokana na kushimiri kwa biashara.

Katika kufanya kazi kiushindani na kujiimarisha kibiashara, TPA imeingia mikataba ya kiundeshaji kwenye baadhi ya gati zake katika Bandari ya Dar es Salaam ambapo Kampuni ya DP World kutoka Dubai inaendesha gati namba 4 hadi 7  gati namba 0 hadi 3 zinaendeshwa kwa pamoja kati ya Mamlaka ya Bandari na Kampuni ya DP World.

Mbali ya DP World, kampuni ya Adani International Ports Holding Limited ( AIPH) ya India  inaendesha gati namba 8 hadi 11 zamani zilizokuwa zinaendeshwa na  iliyokuwa kampuni ya kimataifa ya Tanzania International Containers Terminal Services (TICTS) ambayo mkataba wake wake uendeshaji ulimalizika.


Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam wazindua Shindano la Teknolojia (U.S. -Tanzania Tech Challenge) la Dola za Kimarekani 250,000

$
0
0

Dar es Salaam, 18 Juni 2024 – Mshauri wa Diplomasia ya Umma wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania Jeanne Clark leo katika hafla iliyoandaliwa na AidData/REPOA yenye mada kuu isemayo “Wekeza kwa Watu wa Tanzania” ametangaza kuwa Ubalozi wa Marekani kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani wataendesha shindano la wazi kwa sekta binafsi na/au asasi za kiraia watakaowasilisha maandiko ya miradi yatakayosaidia suluhisho za kibunifu za kukuza ushiriki wa raia, kuimarisha jitihada za kukuza uelewa kuhusu dhima, wajibu na utendaji wa vyombo vya habari (media literacy) na utoaji taarifa sahihi na za kuaminika (information integrity) nchini Tanzania. 

 

Tunawakaribisha wataalamu wa teknolojia na waleta mabadiliko kutoka nchini kote Tanzania kuwasilisha mapendekezo yao na suluhisho kwa hadhira mbalimbali ikiwa ni pamoja na serikali, asasi za kiraia na sekta binafsi. Hadi taasisi zipatazo nane zitachaguliwa kuwasilisha teknolojia zao kwa jopo la majaji. Miongoni mwazo, taasisi tatu zitachaguliwa kuwa washindi wa shindano hili na kupokea ruzuku zenye jumla ya Dola za Kimarekani 250,000. Miradi au suluhisho zitakazoshinda zitatekelezwa kwa manufaa ya Tanzania pekee.

 

Washiriki wanaweza kuwasilisha miradi inayotumia teknolojia za kisasa kutoa suluhisho mbalimbali, iwe ni programu za kielimu, majukwaa ya michezo ya kielektroniki (gaming platforms), zana za kuthibitisha ukweli wa taarifa (fact-checking tools), zana za kuthibitisha mtoa maudhui na maudhui yenyewe (content-authentication tools) na mada nyingine mbalimbali. Ni lazima maandiko ya miradi yalenge katika kukuza uwajibikaji wa raia (civic responsibility) na ushiriki kamilifu wa jamii (community engagement); pamoja na kusaidia kupanua uelewa na matumizi ya rasilimali za kidijitali ikiwemo katika maeneo yasiyofikiwa kirahisi na vyombo vya habari.

 

Shindano la Teknolojia litafanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam, tarehe 18 na 19 Septemba. Siku ya kwanza ya shindano itahusisha maonyesho ambapo wataalamu wa teknolojia au taasisi zitakazokuwa zimechaguliwa zitaonyesha kazi zao;  siku ya pili itahusisha majadiliano ya wanajopo watoa mada (panel discussions) na mijadala itakayowahusisha wataalamu wa teknolojia, maafisa wa serikali, asasi za kiraia, taasisi za elimu na vyombo vya habari ili kujadili mafunzo yatakayokuwa yamejitokeza na fursa za kushirikiana katika  kushughulikia changamoto ya kukuza ushiriki wa raia, kuongeza uelewa kuhusu dhima, wajibu na utendaji wa vyombo vya habari na kuimarisha mazingira ya upashaji habari. Kwa wale watakaopenda kutuma maombi ya kushiriki katika Shindano hili la Teknolojia, wanaweza kupata maelezo zaidi katika tovuti https://cvent.me/Z0Am03

 

Kupitia Shindano la Teknolojia, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inalenga kusaidia makampuni ya kiteknolojia na/au taasisi za Kitanzania ili kuendeleza jitihada zao za kubuni na kutengeneza suluhisho za kibunifu zinazolenga kuinua ushiriki na uwajibikaji wa raia kwa kukuza uelewa wao kuhusu dhima, wajibu na utendaji wa vyombo vya habari. Aidha, tunaamini katika majadilino yanayojenga kuhusu ushiriki wa raia, kuboresha uelewa kuhusu dhima, wajibu na utendaji wa vyombo vya habari na mazingira imara ya upashaji habari kati ya makampuni ya teknolojia na Kitanzania, taasisi za elimu, mashirika ya vyombo vya habari na wadau wa serikali.

 

Tafadhali zingatia kuwa mtu mmoja mmoja hataruhusiwa kushiriki katika shindano hili. Zawadi kwa washindi wa Shindano la Teknolojia zitatolewa tu kwa mashirika ya sekta binafsi au asasi za kiraia. Waombaji wa ruzuku watatakiwa kujaza kikamilifu fomu maalumu ya maombi kama ilivyoelezwa katika tovuti.

Serikali yafurahishwa kuanzishwa kwa kampuni ya bima ya ‘CRDB Insurance Company’

$
0
0

 ·       Kamishna sekta ya fedha asema itasaidia kufikia lengo la kuwahudumia walau 50% ya Watanzania wenye umri wa kuanzi amiaka 18 ifikapo mwaka 2030

Kamishna wa Uendelezaji wa Sekta ya Fedha nchini, Dkt. Charles Mwamaja (wapili kulia) akizindua Kampuni Bima ya CRDB ‘CRDB Insurance Company (CIC)’ jijini Dar es Salaam Juni 18, 2024. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.

Kamishna wa Uendelezaji wa Sekta ya Fedha nchini, Dkt. Charles Mwamaja, akitoa hotuba yake kabla ya kuzindua Kampuni Bima ya CRDB ‘CRDB Insurance Company (CIC)’ jijini Dar es Salaam Juni 18, 2024. 

 

Dar es Salaam. Tarehe 18 Juni 2024: Kamishna wa Uendelezaji wa Sekta ya Fedha nchini, Dkt. Charles Mwamaja ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuanzisha kampuni tanzu ya bima ya ‘CRDB Insurance Company (CIC)’ ambapo amesema itasaidia kwa kiasi kikubwa kuchangia ufikiaji wa malengo ya serikali ya kuongeza ujumuishi wa bima kufikia asilimia 50 kwa Watanzania wenye umri wa kuanzia miaka 18 ifikapo mwaka 2030.

 

Dkt. Mwamaja ameyasema hayo alipoizindua kampuni hiyo jijini hapa ukiwa umepita mwaka mmoja tangu ipate leseni ya kutoa huduma za bima zisizo za maisha kwa Watanzania ili kuwalinda dhidi ya majanga yanayoweza kujitokeza. Dkt. Mwamaja ameitaka CIC kutumia uzoefu na wigo mpana wa Benki ya CRDB kuwafikia wananchi hasa kwa kuzingatia kuwa Benki hiyo imeenea katika halmashauri zote nchini.

 

Dkt. Mwamaja ambaye amemwakilisha Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba  amesema sekta ya bima nchini bado ni changa lakini ina fursa kubwa sana za kuwahudumia Watanzania iwapo elimu itatolewa na makampuni ya bima kuwekeza katika ubunifu wa bidhaa zitakazogusa makundi mbalimbali ya wateja, Taifa litafikia lengo lake la kuongeza ujumuishi wa bima ifikapo mwaka 2030.

 

“Niwapongeze kwa ubunifu ambao mmeanza nao kwa kuja na bima ya kilimo kwa kushirikiana na ACRE Africa. Kilimo ni sekta muhimu katika uchumi wetu inayoajiri watu wengi zaidi. Iwapo mtafika mpaka vijijini mtatoa nafuu kwa wakulima wengi kulinda mazao na mifugo yao jambo ambalo litasaidia kuwapa utulivu wa nafsi a wakulima kupitia bima hii. Tunapaswa kujua kuwa huduma bora bima ni msingi wa ustawi wa uchumi na kichocheo cha uwekezaji,” amesema Dkt. Mwamaja.

Kwa upande wake Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dkt. Baghayo Saqware ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuwa taasisi ya kwanza fedha nchini kuanzisha kampuni tanzu ya bima. Dkt. Saqware amesema CIC inakwenda kuitanua sekta ya bima nchini jambo litakaloongeza ushiriki wa Watanzania katika kutumia huduma za bima. 

 

Akieleza ujumuishi wa huduma za bima nchini, Dkt. Saqware amesema hadi mwishoni mwa mwaka 2023 kulikuwa na watumiaji wa bima milioni 12 kutoka watu milioni 6 waliokuwa wanatumia bidhaa hizo mwaka 2022. Dkt. Saqware amesema kupitia jitihada zinazotekelezwa na Serikali ikiwamo kuanzishwa kwa kanuni ya bima za lazima kunatarajiwa kuongeza ujumuishi mara dufu kila mwaka kufikia lengo lililowekwa. 

 

“Serikali pia imeanzisha konsotia ya bima ya mafuta na gesi, pamoja ya ile ya kilimo na mifugo. Ni imani yangu kuwepo kwa makampuni kama CIC kutasaidia kufanikisha malengo kwa kuwekeza mitaji ili sehemu kubwa ya ada za bima ziwe zinabaki nchini,” alisema Kamishna Saqware huku akiitaka kampuni hiyo kuwekeza katika weledi kwa wafanyakazi na kusimamia sera na misingi iliyowekwa kisheria ili kuepukana na udanganyifu.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Omary Mwaimu amemwambia Dkt. Mwamaja kuwa lengo walilonalo ni kuifanya CIC kuwa kampuni ya bima chaguo nambari moja kwa Watanzania wote kupitia huduma bunifu na nafuu ambazo zitatoa fursa kwa makundi mbalimbali ya wananchi kujiunga na hivyo kuchochea ujumuishi wa bima nchini.


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema kuanzishwa kwa CIC ni mwendelezo wa utekelezaji wa azma ya Benki ya CRDB kutanua wigo wake wa kufikisha huduma za fedha ikiwamo bima kwa Watanzania.

Nsekela amebainisha kuwa uamuzi huo umetokana na hali ya ufikiaji mdogo wa huduma za bima nchini huku akieleza kuwa mkazo mkubwa wa kampuni hiyo ya CIC umeelekezwa vijijini ambapo wengi wapo nje ya mfumo rasmi wa bima.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa CIC, Wilson Mnzava amewakaribisha mawakala na madalali wa bima, wateja, pamoja na wadau wengine kuzitumia huduma za CIC akiahidi kuwa watapata utulivu wa maisha, utulivu wa nafsi, utulivu wa biashara, na utulivu wa uchumi wao kipindi majanga yanapojitokeza.

 

CRDB Insurance Company (CIC) inakuwa kampuni tanzu ya nne ya Benki ya CRDB baada ya zile za CRDB Bank Burundi, CRDB Bank DR Congo, na CRDB Bank Foundation. CIC inatoa huduma za bima zisizo za maisha ikiwamo bima ya magari, bima ya nyumba, bima ya vyombo vya moto, bima ya biashara, bima ya usafirishaji, bima ya safari, bima ya ukandarasi, na bima ya mitambo.

DC KISARAWE AUNGANA NA WATAALAM KUJIONEA MWENENDO MRADI WA VISEGESE

$
0
0

NA VICTOR MASANGU, KISARAWE

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mhe. Petro Magoti  amefanya kikao kazi na   wataalam wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyi pamoja na Kamati ya Usalama Wilaya kwa ajili ya kujadili maendeleo ya Mradi wa viwanja vya Uwekezaji wa Viwanda.

Mkuu wa Wilaya hiyo pia katika kikao hicho ameweza kuongozana na  Viongozi mbali mbali  wa Halmashauri ya Kisarawe pamoja na Timu ya Watalaam na kupata fursa ya kutembelea  eneo la Mradi wa upangaji wa Upimaji wa Eneo la Viwanda lililopo Visegese kata ya Kazimzumbwi.

Mhe.Magoti alisema kwamba mradi wa Upangaji wa upimaji  ulibuniwa kwa ajili ya kutenga viwanja kwa ajili ya Viwanda na Maeneo mbali mbali  ya Makazi ya watu.

Magoti alifafanua kuwa utekelezaji wa Mradi huo ulianza kutekelezwa.mnamo  mwaka 2014 na kufanikiwa kuzalisha Viwanja 291 hivyo eneo hilo litakuwa Maalum kwa ajili ya Viwanda vya aina mbali mbali.

"Utekelezaji wa Mradi huu ulifanyika kwa ubia kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe na Wananchi wenye Maeneo katika Eneo lililopendekezwa kwa lengo la uwelezaji huo,"alisema Mhe.Magoti

Mkuu huyo alieleza kuwa muda  si Mrefu Wananchi wote  wenye nia yakutaka kuwekeza nakujenga Viwanda Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa pwani karibuni sana sana.Huduma za Maji zipo na barabara tupo mbioni kuzishughulikia ili kupanua wigo wa usafirishaji.

Pia alifafanua kwamba Mhe. Dkt. Rais Samia Suluhu Hassan  anapenda kuona Wananchi wake wanapata kipato kikubwa na kuinua uchumi wa kimaendeleo yenye kuleta mabadiliko na kuboresha  maisha yao kwa ujumla.



Mbunge Lugangira aongoza maandamano kupinga ukatili

$
0
0

Na Mwandishi Wetu, Kagera

WANAWAKE wa Mkoa wa Kagera wakiongozwa na Mbunge wa Viti Maalum mkoani hapo Neema Lugangira wamefanya maandamano kupinga ukatili dhidi ya watu wenye ualbino, ikiwa ni siku chache baada kifo cha mtoto wenye Ualbino Asimwe Novatus miaka miwili na nusu kuuwawa wilayani Muleba.

Akizungumza baada ya kufika nyumbani kwa kina Asimwe na kumpa pole mama mzazi, Mbunge Lugangira amesema tukio hilo limemuumiza Rais Samia Suluhu Hassan na Watanzania kwa ujumla na kwamba watahakikisha wahusika wanawajibishwa kwa mujibu  wa sheria.

"Tumefanya maandamano haya ya amani kupinga mauji ya kikatili kwa mtoto Asimwe, lakini pia kupinga mauji yoyote ya aina hii, kwani huo sio utaratibu wa maisha yetu, inasikitisha sana, tunawapa pole wafiwa wote hasa mama," amesema.

Amesema Rais Samia ameelekeza vyombo vya ulinzi na usalama vifanye kazi mchana na usiku kuhakikisha wahusika wanakamatwa na hatua stahiki zichukuliwe.

Aidha, Mbunge Lugangira ameahidi waombolezaji kutafuta wadau na kuanzisha kampeni ya kuelimisha jamii kuhusu kulinda wenzetu wenye ualbino, kukataa kutumika na kupinga vikali ukatili wa aina zote kwa albino.

Mbunge huyo aliambatana na Katibu wa Umoja wa Wanawake  (UWT), Mkoa Kagera, Mwenyekiti UWT Wilaya ya Muleba, Katibu UWT Wilaya ya Muleba, Madiwani Viti Maalum kutoka Wilaya ya Muleba na wanachama wa UWT na CCM.




Wakazi Kigoma wahimizwa kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura

$
0
0

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi wa mkoa wa Kigoma uliofanyika leo tarehe 19 Juni, 2024 katika Halmashauri ya Kigoma Ujiji. Tume inataraji kufanya uzinduzi wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura tarehe 01 Julai, 2024. (Picha na INEC). 

Sehemu ya wadau wa uchaguzi kutoka Mkoanbi Kigoma wakishiriki katika kikao cha siku moja baina ya Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) na wadau hao ikiwa ni maandalizi kuelekea uzinduzi wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utakaofanyika Julai 1, 2024 mkoani Kigoma. (Picha na INEC).  

Na Mwandishi Wetu, Kigoma

Wananchi mkoani Kigoma wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao wakati wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linalotarajiwa kuzinduliwa mkoani humo tarehe 01 Julai, 2024.


Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele wakati akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi wa mkoa wa Kigoma uliofanyika leo tarehe 19 Juni, 2024 katika Halmashauri ya Kigoma Ujiji.
 

Jaji Mwambegele amewapongeza wadau wa uchagizi na wananchi kwa ujumla kwenye mkoa wa Kigoma kwa mkoa wao kuteuliwa kuwa sehemu ya uzinduzi wa uboreshaji huo ambao utafanyika kwenye uwanja wa Kawawa uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB).
 

“Uboreshaji wa daftari utazinduliwa hapa mkoani Kigoma tarehe 01 Julai, 2024 na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB). Tayari Tume imeamua kwamba uzinduzi huo ufanyike katika uwanja wa Kawawa uliopo hapa kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji,” amesema Mhe. Mwambegele.


Ameongeza kuwa Tume ilifikia uamuzi wa kufanya uzinduzi huo kwenye mkoa wa Kigoma baada ya kuzingatia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa mwamko mkubwa wa wananchi kujitokeza kwenye uboreshaji wa Daftari uliofanyika mwaka 2019/20.


“Ni matarajio ya Tume kuwa mtakuwa mabalozi wazuri wa kusambaza taarifa na kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao ili kuendeleza sifa hii ya mwamko wa wananchi kujitokeza kwa wingi,” amewaambia wadau hao.

 
Amesema, uzinduzi wa uboreshaji wa Daftari utatanguliwa na shughuli mbalimbali za uhamasishaji ikiwa ni pamoja na matangazo na tamasha la uborshaji wa Daftari ambalo litafanyika siku ya Ijumaa tarehe 28 Juni, 2024 kwenye uwanja wa Kawawa.


Wakati akiwasilisha mada, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K amesema uboreshaji kwa awamu hii ya kwanza utafanyika kwenye mizunguko 13 na kuongeza kwamba baada ya mkoa wa Kigoma uboreshaji utaendelea kwenye mikoa ya Katavi na Tabora.


“Zoezi hili litaendeshwa kwa siku saba kwenye kila kituo cha kuandikisha wapiga kura. Tunatarajia zoezi litakamilika Machi, 2025,” amesema Bw. Kailima.


WANAWAKE UWT KIBAHA MJI YAMPA TANO MBUNGE KOKA NA MKEWE KWA KUWASHIKA MKONO

$
0
0

NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
 
Umoja wa wanawake (UWT) Wilaya ya Kibaha mji umempongeza kwa dhati Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Mhe. Silvestry Koka pamoja na mke wake Mama Selina Koka kwa juhudi na sapoti yao kubwa ya kuwakomboa wanawake kiuchumi kwa kuwawezesha  mradi wa ujenzi wa jengo la kitega uchumi ambalo litakuwa ni mkombozi mkubwa katika kutimiza ndoto zao.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mahojiano maalumu Mwenyekiti wa UWT Kibaha mji Elina Mgonja alisema kwamba   Mbunge Koka amekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia  kwa hali na mali wanawake pamoja na jamii kwa ujumla katika mambo mbali mbali ya uwezeshaji wanawake kiuchumi.

Mgonja alisema kwamba kwa sasa UWT Wilaya ya Kibaha mjini imeweka mikakati kabambe ya kuaznisha miradi mbali mbali mabayo itakuwa ni moja ya mkombozi mkubwa katika kuwasaidia wanawake kuondokana na wimbi la umasikini na hatimaye kuweza kujikwamua kiuchumi.

"Kwa kweli sisi kama wanawake wa UWT Kibaha mji tunasema kwamba tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Mbunge wa Jimbo la Kibaha Silvestry Koka pamoja na mke wake Mama selina Koka kwa moyo wao wa kujitoa kwa hali na mali katika kutusaidia sisi umoja wetu kwani kwa sasa tunamalizika kukamilisha mradi wa ujenzi wa jengo letu la kitega uchumi ambalo kwa sasa lipo tayari isipokuwa tunamalizia kukamilisha  baaadhi ya vitu kadhaa,"alisema Mwenyekiti Mgonja.

Aliongeza kuwa  Mbunge Koka amekuwa akitekeleza Ilani ya chama kwa vitendo na ndio maana ameweza kuwasaidia wanawake hao kuwa na mradi wa jengo lao kwa ajili ya kitega uchumi ambapo wameshirikiana bega kwa bega na mke wake ili kuhakikisha kwamba wanawawezesha wanawake hao kutimiza malengo yao waliyojiwekea.
Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa lengo kubwa la UWT ni kuweka misingi imara ambayo itaweza kumkomboa mwanamke  na mtoto hivyo mradi huo wa kitega uchumi  pindi utakapokamilika wataanzisha miradi  mbali mbali ambayo itaweza kutoa hata fursa za ajili kwa wanawake wa UWT.

"Jambo kubwa amelifanya Mhe. Mbunge kwa ajili yetu sisi kina mama pamoja na mlezi wetu ambaye ni Mama Selina Koka kwa hivyo mimi nasema kwamba sio kwamba tunajipendkeza bali tunaongea ukweli na kwa sasa siasa ni uchumi  na siku hizi tunasema mnyonge anyong'wi na haki yake anapewa maana jengo letu linapendeza,"alisema Mwenyekiti Mgonja.

Kwa upande wake Katibu wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini   Cesilia Ndalu hakusita kumpongeza mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mama Selina Koka ambaye pia ni mlezi wa UWT kwa kuwa bega kwa bega na jumuiya ya umoja wa   wanawake  katika kuwasapoti mambo mbali mbali ya kimaendeleo.

Katika hatua nyingine Katibu huyo alitumia fursa hiyo ya kuwakaribisha wajumbe wote katika mkutano wa baraza la UWT ambalo linatarajiwa kufanyika siku ya kesho Ijumaa katika ukumbi wa jengo la Halmashauri na kuwahimiza kuwahi mapema lengo ikiwa ni kushiriki kikamilifu katika baraza hilo.


Benki ya CRDB, Nala wasaini makubaliano ya kibiashara kuimarisha zaidi huduma za kifedha kwa watanzania waishio nje ya nchi

$
0
0

Mkurugenzi wa Wateja wa Awali na wa Kati wa Benki ya CRDB, Bonaventura Paul (kulia) na Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Nala, Benjamin Fernandes (kushoto) wakisaini mkataba wa makubaliano ya kibiashara yanayolenga kuimarisha zaidi huduma za kifedha kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi ambapo Benki ya CRDB itakuwa ikitoa huduma ya kupokea na kuchakata miamala inayotumwa kutoka nje ya Tanzania kupitia Programu ya Nala kwenda mabenki na taasisi nyingine za fedha pamoja na mitandao ya simu. Hafla hiyomilifanyika Makao Makuu ya CRDB jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Wateja wa Awali na wa Kati wa Benki ya CRDB, Bonaventura Paul (kulia) na Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Nala, Benjamin Fernandes (kushoto) wakionesha mkataba waliosaini.
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Nala, Benjamin Fernandes akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kibiashara baina na Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam.


Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mbelwa Kairuki, akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kibiashara baina ya CRDB na Kampuni ya Nala yanayolenga kuimarisha zaidi huduma za kifedha kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi.

Mkurugenzi wa Wateja wa Awali na wa Kati wa Benki ya CRDB, Bonaventura Paul, akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kibiashara na Kampuni ya Nala yanayolenga kuimarisha zaidi huduma za kifedha kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi.


 

 

MA-RC, MA-DC ANZISHENI OPERESHENI MAALUMU ZA ULINZI – MAJALIWA

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wahakikishe kila halmashauri inaanzisha operesheni maalum za ulinzi kwa watu wenye ualbino.


“Operesheni hizi zihusishe vikosi vya usalama ili kuhakikisha ulinzi wa watu wenye ualbino dhidi ya mashambulizi na vitisho hii ni kwa sababu katika kuzuia unyanyasaji na mauaji ya watu wenye ualbino, Mamlaka za Mikoa na Serikali za Mitaa zinawajibika katika usimamizi, ulinzi na utoaji wa huduma kwa watu wenye ualbino,” amesema.

Ametoa wito huo leo (Alhamisi, Juni 20, 2024) wakati akitoa taarifa kuhusu kupinga ukatili dhidi ya watu wenye ualbino wakati wa kipindi cha maswali ya Papo Kwa Papo kwa Waziri Mkuu, Bungeni, jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amezitaka Mamlaka za Mikoa na Wilaya zihamasishe ushiriki wa jamii katika kuhakikisha ulinzi na haki za watu wenye ualbino kwani vitendo vya mauaji ya albino vinahusisha mtandao wa watu na siyo mtu mmoja mmoja tu.

Amesema Serikali tayari imeshajenga mifumo thabiti ya udhibiti na suala lililobaki ni ushiriki wa makundi yote ya jamii katika kuhakikisha vitendo hivyo viovu vinakomeshwa hapa nchini. “Kwa kutambua jukumu tulilonalo kama Taifa, nitumie nafasi hii kuyataka makundi na taasisi mbalimbali katika jamii kuendelea kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya vitendo hivyo vya ukatili.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewaomba viongozi wa dini waendelee kukemea  kukemea maovu yanayotendeka nchini hususan mauaji kwa watu wenye ualbino kwani kuwepo kwa matukio hayo kunaonesha upotofu wa maadili na kukosa hofu ya Mungu.

“Nitumie nafasi hii kuwaomba viongozi wetu wa dini tuungane pamoja kupambana na mauaji ya watu wasiokuwa na hatia hata kidogo. Ninawasihi watumie majukwaa yao ya ibada kuwahubiria waumini wao waachane na vitendo hivyo vya ukatili ambavyo hata Mwenyezi Mungu anavikataza. Watu wenye ualbino wana haki ya kuishi kama walivyo watu wengine,” amesisitiza.

Waziri Mkuu amesema waganga wa jadi nchini kote wanapaswa kushiriki kikamilifu katika kampeni za kupinga mauaji ya watu wenye ualbino. “Wakati umefika kwenu nyote kushirikiana na Serikali katika kutokomeza imani potofu zinazochangia mauaji haya. Ninawasihi sana elezeni wazi kwamba hakuna tiba wala mafanikio yanayoweza kupatikana kwa kutumia viungo vya watu wenye ualbino.”

Pia amelitaka Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala lifanye usajili wa waganga wa jadi na vituo vyao sambamba na aina ya huduma wanayoitoa kwa wateja wao ili kuweza kudhibiti huduma holela isiyofuata misingi ya utu na haki za binadamu.

Mbali na hao, amewataka viongozi wa kimila kutoka kila kona ya Tanzania washiriki kikamilifu katika kukemea na kupinga mauaji ya watu wenye ualbino. “Ninawaomba viongozi wetu wa kimila wakiwemo machifu washirikiane na Serikali kwa kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama pindi wanapopata fununu za mipango au vitendo vya mauaji ya watu wenye ualbino katika maeneo wanayoishi.”

Ili kuhakikisha matukio ya aina hiyo hayatokei, Waziri Mkuu amelielekeza Jeshi la Polisi lichukue hatua za haraka pindi linapopata fununu ya uwepo wa njama za utekaji na mauaji ya watu wenye ualbino.

Pia ametaka liendelee kufanya operesheni ya kuwakamata wote waliotajwa na watakaotajwa kuhusika kwenye matukio ya aina hii ili kuua mtandao mzima wa wahalifu. “Polisi jamii ishirikishwe kikamilifu ili kupata taarifa zote muhimu katika maeneo husika na watoa taarifa wote walindwe ipasavyo,” amesisitiza.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema lengo la Serikali ni kuwalinda wananchi walioathirika kwa kuwa wanahitaji kuwekwa mahali salama kwa kuwa bado wanakuwa wana hofu kutokana na madhila yaliyowafika.

“Sera yetu ya Serikali ni kuwalinda wote wenye ulemavu wa aina yoyote ili washiriki shughuli za maendeleo huku tukihakikisha wanakuwa salama. Malengo yetu ni kutoa uhakika wa maisha yao wakati wote.

“Bado tunaendelea kutafuta njia mbadala ikiwemo kuwachanganya ili wasijione wametengwa. Tumeanza kuwachanganya katika shule za msingi na sekondari ili nao washiriki pamoja kwenye shughulimbaliza kijamii na michezo bila kujali ulemavu wao.”

Alikuwa akijibu swali la Rashid Shangazi (Mbunge wa Mlalo) ambaye alimtaka Waziri Mkuu aeleze ni kwa nini Serikali inapanga kuwaweka waathirika kwenye kambi ilhali ni kinyume na haki ya kuwa huru kama ilivyoelezwa kwenye ibara ya 15(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wanawake nyenzo ya kuzuia biashara haramu ya viumbe pori

$
0
0

Na Selemani Msuya

IMEELEZWA iwapo wanawake watapewa elimu ya kuzuia biashara haramu ya viumbe pori au wanyamapori, biashara hiyo itakoma na viumbe hao watakuwa endelevu.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Sera Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, Allen Mgaza wakati akijibu swali la mwandishi wa habari kwenye mdahalo  wa asubuhi ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET).

Mdahalo huo ambao umerushwa mbashara kupitia TBC Safaei Chanel, umefadhiliwa Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili ulibeba ajenda ya Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi katika Kutokomeza Biashara Haramu ya Wanyamapori.

Akijibu swali hilo Mgaza amesema vita dhidi ya biashara haramu ya viumbe pori ni jumuishi, hivyo ni lazima wanawake wapewe kipaumbele zaidi katika vita hiyo.

“Mapambano ya biashara haramu ya viumbe pori yanapaswa kuwa jumuishi na kundi la wakina mama ni muhimu sana, nadhani kila mmoja anajua nafasi ya mama nyumbani na kwenye jamii, kwani iwapo baba atashiriki kufanya ujangili na kuleta nyama nyumbani ambaye anaipika ni mama, hivyo mama akielewa hasara zake atakuwa balozi sahihi kuongoza vita hiyo,” amesema.

Mgaza amesema USAID Tuhifadhi Maliasili imehusisha makundi yote katika kutoa elimu ya madhara ya uwindaji haramu wa viumbe pori na wanaanza kuona matokeo chanya.

Mkuu huyo wa kitengo amesema iwapo kila mtetezi wa viumbe pori ataweka mkazo kweenye kutoa elimu hasa kwa wanawake viumbe hao watakuwa salama na endelevu.

“Wanawake ndio chachu ya mabadiliko ya jamii, kwani baba akikamatwa na meno ya tembo, jukumu la kulea watoto litabaki kwa mama, hivyo mama ni mtu muhimu sana katika haya mapambano,” amesisitiza.

Amesema biashara haramu ya viumbepori inafanyika duniani kote ambapo wao kama USAID wanafanya kazi na makundi yote ili kuhakikisha elimu ya kukabiliana na biashara hiyo inafanikiwa.

Mgaza amesema biashara haramu sio mpya, ipo kwa miaka mingi, hivyo kinachohitajika ni kila mwana jamii kuthamini viumbe pori hivyo kwani vinategemeana.

 “Biashara ya viumbe pori ipo na inaruhusiwa kufanyika, lakini ina taratibu zake, lazima iwe halali inayofuata sheria za nchi na za kimataifa na kuwa endelevu, kwa maana kwamba hatutaki biashara ifanyike kwa njia haramu na kumaliza rasilimali zetu zote na vizazi vijavyo vikose,” amesema.

Amesema biashara hiyo inatakiwa kunufaisha wananchi wakiwemo wanawake ambao kwa asilimia kubwa wanakuwa wahanga wa matukio ya biashara haramu ya viumbe pori.

Aidha amesema taarifa zinaonesha kuwa watu wanaofanya biashara haramu ya viumbepori wamekuwa wakitumia fedha hizo kufanya mambo mengi ambayo hayakubaliki kwenye jamii na dunia.

Pia mtaalam huyo amesema biashara haramu kwa ngazi ya dunia inaonesha viumbe pori vya nchi kavu na majini vinahusika katika biashara hiyo, hivyo juhudi zinahitajika katika maeneo hayo ili wanyama hao wawe salama na endelevu.

Mwenyekiti wa Baraza la Wasafirishaji Shehena Tanzania (TSC), Clement Kamendu amesema wanaunga mkono dhana nzima ya ushirikishwaji kwani ndio ngao muhimu ya kukabiliana na janga hilo la dunia.

Amesema baraza lao lina jukumu la kulinda maslahi ya wasafirishaji wa shehena kwenda nje na kuingiza nchini, hivyo watashirikiana na kila mtu kuzuia biashara haramu ya viumbe pori.

Mwenyekiti huyo amesema wanatoa elimu kwa wadau wote ambao wapo kwenye mnyororo huo, ili kuepukana na biashara hiyo.

Kamendu amesema usafirishaji viumbepori kwa njia halali unachangia asilimia tisa ya pato la taifa na fedha za kigeni asilimia 25, hivyo ni wazi sekta hii ina faida iwapo itasimamia vema.

“Kipindi cha 2009 hadi 2018 ripoti ya serikali ilionesha shehena 15 zilikamatwa na watu 1,072 walihusika na kusababisha kesi za jinai 391 kufunguliwa, watu 301 kufungwa, 43 walipigwa faini ya Sh bilioni 1.5 na wahusika kufungwa miaka 3,015,” amesema.

Amesema kuanzia 2009 hadi 2015 zilikamatwa shehena 23 za meno ya tembo ambazo zilipitia Bandari ya Dar es Salaam na Zanzibar na hayo yote yalichangiwa na dhana nzima ya ushirikishwaji.

Amesema takwimu zinaonesha kwa mwaka duniani tani bilioni 12 zinasafirishwa na Afrika ikihusika na asilimia 6 ya bidhaa hizo ambapo katika hizo zipo shehena haramu.

“Asilimia 80 ya bidhaa zinazosafirishwa duniani kibiashara kwa uzito zinatumia njia ya bahari na asilimia 70 kwa thamani pia zinatumia njia hiyo hiyo, hivyo sekta ya usafirishaji ikielewa ukubwa wa tatizo itaweza kusaidia serikali katika mapambano,” amesema.

Kamendu amesema wamekuwa wakitoa elimu kwa wasafirishaji wote wakiwemo wa mabasi, ndege, meli na wengine, jambo ambalo limekuwa na matokeo chanya.

Mkurugenzi Mtendaji wa JET, John Chikomo amesema wameweka kwenye kutoa elimu kwa wahariri na waandishi wa habari ili waweze kuelezea sekta hiyo kwa usahihi.

Amesema biashara hiyo haramu ya viumbe pori au wanyamapori isipopigwa vita miaka michache jamii itakuwa inahadithiwa kuhusu viumbe hivyo na kwamba kalamu za waandishi zinaweza kuifanya Tanzania na dunia kuwa salama zaidi.

“JET kwa kushirikiana na USAID Tuhifadhi Maliasili, imeamua kutoa mafunzo kwa wanachama wake ili wawe na uelewa biashara haramu za viumbe pori na masuala ya uhifadhi tunaamini kupitia kalamu zao hali itakuwa nzuri,” amesema.


Nape awaomba wadau wa habari wamuamini

$
0
0

Na Selemani Msuya

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amewaomba wadau wa sekta ya habari kuwa na imani naye kuhusu vifungu 12 vinavyolalamikiwa katika Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016.

Kauli hiyo ya Waziri Nape ilitokana na maazimio sita ambayo yalisomwa na Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Thobias Makoba, ambapo moja ya azimio lilikuwa ni vifungu 12 vya Sheria ya Huduma ya Habari ambavyo vinalalamikiwa na wadau wa sekta hiyo.

Nape ametoa kauli hiyo wakati akifunga Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari lilifoanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam kwa siku mbili na kushirikisha wadau zaidi 1,200 kutoka sekta umma na binafsi kwenye tasnia ya habari.

Makoba alitaja maazimio mengi kuwa ni wizara na taasisi za serikali kulipa madeni ya vyombo vya habari ifikapo Disemba 24 mwaka 2024 na wamiliki waweze kulipa mishahara, pia azimio lingine serikali kuangalia uwezekano wawekezaji wakigeni kuwa na asilimia 75, vyombo vya habari kuandika habari za kijamii, vyombo vya habari vitoe fursa kwa vyama vyote na vyombo vya habari vya mtandao viongoze ubunifu na kuandaa maudhui yenye tija na kujijengea uaminifu kwa walaji.

Amesema amekuwa akisikitishwa na muendelezo wa kulalamikia vifungu 12 vya sheria hiyo, huku akiwa ameelezea kwanini havikufanyiwa mabadiliko wakati wa mabadiliko yaliyohusisha vifungu tisa pekee vya sheria hiyo.

Waziri Nape amesema kuna vifungu ambavyo vinahitaji mabadiliko ya sera ndio viweze kubadilika na vingine vitaingizwa kwenye kanunu, hivyo anawataka wadau kuacha kulalamika wakihisi kwamba serikali haitaki.

“Hili suala la vifungu 12 vya Sheria ya Huduma ya Habari ambavyo mnavitaja kila mara, nadhani nimefafanua sana kwamba hoja hizi tutazifanyia kazi baada ya sera mpya kutungwa na vingine vitaingia kwenye kanuni, najisikia vibaya kwa sababu tumefanya vikao na kukubaliana.

Nitatoa mfano hoja ya umiliki wa vyombo vya habari, ipo kwenye Sera ya Vyombo vya Habari ya mwaka 2003, mimi sikuwepo, nilikuwa ndio naanza kazi CCM. Jamani naomba tuaminiane, mimi ni mdau wa sekta hii kwa sababu nimeisomea. Sitengenezi kwa ajili yangu au ajili yenu, ni kwa ajili yetu, kwa sababu sijui watoto wangu watafanya kazi gani. Tuaminiane. Tutafika salama,” amesema.

Waziri Nape amesema katika mchakato huo wa kubadilisha sheria aliwashirikisha baadhi ya waandishi na kuwaonesha hali halisi, hivyo anaumia pale ambapo anatiliwa mashaka katika hilo.

Amesema aliwasilisha sheria bungeni na mjadala ukawa mkali kwa wabunge kutaka mabadiliko na alikubali  mabadiliko ambayo wabunge walitaka, jambo  ambalo halijafanywa na waziri yoyote.

“Sikilizeni mimi naipenda sekta hii, kiasi kwamba 2017 nilikuwa tayari kupoteza uwaziri, kulinda uhuru wa vyombo vya habari wa nchi hii, msisahau rekodi hizi, sekta ya habari ipo ndani ya moyo wangu, siku ile wakina Deudatus Balile, Jesse Kwayu na wengine wanaenda kusoma ripoti nilijua nafukuzwa, waliniambia nitafukuzwa nikawaambia nilipofikia siwezi kurudi nyuma, uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu kuliko kazi yangu.

Siwezi kuingi kwenye rikodi ya kuhujumu vyombo vya habari kwa sababu utanifuata maisha yangu yote, kwa sababu ya cheo tu. Si nilitoka leo nimerudi nasonga mbele na heshima yangu ipo, wanahabari msisahu, sekta ya habari ipo mikono salama. Na wao wanajua, wasioitakia mema sekta hii wanajua, ilimradi Nape yupo atasimamia na wanahabari wake,” amesema.

Nape amewahakikishia wadau wa sekta ya habari kuwa serikali chini ya uongozi Rais Samia Suluhu Hassana ina dhamira ya kweli ya kujenga ushirikiano, ili kuhakikisha kila upande unanufaika.


INEC YAWATAKA WATENDAJI WA UBORESHAJI KUTUNZA VIFAA

$
0
0

 Na Mwandishi wetu, Kigoma


Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetaka watendaji wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Mkoani Kigoma kuhakikisha wanatunza vifaa vya uandikishaji ili vikaweze kutumika maeneo mengine nchini.

 

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegeke wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza leo tarehe 20 hadi 21 Juni,2024 Mkoani Kigoma.

“Kwa kusisitiza, ni muhimu kutekeleza majukumu yenu kwa umakini katika kila eneo ikiwemo utunzaji wa vifaa vya uandikishaji hasa ikizingatiwa kuwa, vifaa hivi vimenunuliwa kwa gharama kubwa sana na vinatarajiwa kutumika katika maeneo mengine ya uandikishaji nchini,” alisema Jaji Mwambegele.

Amesema kutokuwa makini katika utunzaji wa vifaa hivi kutapelekea athari kubwa katika ukamilishaji wa zoezi hili muhimu na amewataka kuzingatia maelekezo yote yatakayotolewa na Tume ili muweze kuyafanyia kazi wakati zoezi litakapokuwa limeanza.

Aidha, Jaji Mwambegele amesema matokeo bora ya zoezi hili yanategemea uwepo wa ushirikiano mkubwa kati ya watendaji wote wa uboreshaji, serikali, vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi.

“Ninawasihi muwe na ushirikiano mzuri na wa karibu na Tume wakati wote mtakapokuwa mnatekeleza majukumu yenu na ikiwa mnahitaji ufafanuzi au maelekezo yeyote, msisite kuwasiliana na Tume,” alimema Jaji Mwambegele.

Mapema kabla ya kuanza mafunzo hayo, washiriki walikua kiapo cha kujitoa uanachama na kile cha kutunza siri mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Rose Kangwa.

Mafunzo hayo yanahusisha namna ya ujazaji wa fomu pamoja na kutumia mfumo wa kuandikisha wapiga kura (Voters Registration System - VRS) ili waweze kupata uelewa wa pamoja utakaowapa fursa ya kutumia kwa ufasaha mfumo huo pamoja na vifaa vingine vya kuandikisha wapiga kura.

“Mafunzo haya, yanawajengea umahiri wa kuwafundisha Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata kisha nao watatoa mafunzo hayo kwa Waendeshaji wa Vifaa vya Bayometriki na Waandishi Wasaidizi ambao ndio watahusika na uandikishaji wa wapiga kura vituoni,” alisema Jaji Mwambegele.

Aidha, Maafisa TEHAMA watapatiwa mafunzo maalum ya jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiufundi (Troubleshooting) endapo zitajitokeza wakati wa zoezi la uandikishaji wa wapiga kura vituoni.

Katika hatua nyingine, Jaji Mwambegele amewaambia watendaji hao kuwa  wakati wa uboreshaji wa Daftari mawakala wa vyama vya siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura jambo ambalo litasaidia kuleta uwazi katika zoezi zima lakini pia mawakala hao watasaidia kutambua waombaji wa eneo husika hivyo kupunguza kutokea kwa vurugu zisizokuwa za lazima.

Jaji Mwambegele alitoa angalizo kwa mawakala hao kutoka vyama vya siasa kuwa  hawaruhusiwi kuwaingilia watendaji wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao vituoni.

Tume imetangaza uzinduzi wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura utafanyika tarehe 01 Julai, 2024 mkoani Kigoma ambapo Mgeni rasmi anataraji kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa na kauli mbiu ya uboreshaji ni  “Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura Ni Msingi Wa Uchaguzi Bora”

WAZIRI KAIRUKI AHAMASISHA WATANZANIA KUSHIRIKI SHUGHULI ZA UFUGAJI NYUKI KUJIKWAMUA KIUCHUMI

$
0
0

 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) akiwa ameongozana na Rais wa Apimondia, Dkt. Jeff Pettis (wa pili kutoka kushoto) wakisikiliza maelezo kuhusu shughuli za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) walipotembelea  banda la Wakala hiyo kwenye Maonesho ya kwanza ya Asali (Honey Show 2024mara baada ya hafla ya ufunguzi iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Juni 19,2024.

 

Na Mwandishi Wetu- Dar es Salaam

 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amefungua rasmi Maonesho ya kwanza ya asali kufanyika nchini Tanzania (Honey Show) huku akihamasisha Watanzania kujitokeza kuchangamkia fursa za ufugaji nyuki na uzalishaji wa asali ili kukuza vipato vyao.

 

Ameyasema hayo Juni 19,2024 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

 

Amesema lengo la Maonesho hayo yenye kaulimbiu “Beyond Hives, Beyond Borders” ni kuelimisha umma kuhusu  umuhimu wa ufugaji nyuki, uongezaji thamani na uzalishaji wa asali.

 

Amesema sekta hiyo ndogo ya ufugaji nyuki ina nafasi kubwa  katika uchumi, ajira, utunzaji wa mazingira, uhifadhi, tiba chakula ikizingatiwa kwamba kwa sasa inatoa ajira kwa si chini ya watu milioni mbili na mchango wake katika Uchumi na lishe kuwa mkubwa sana.

 

“Tumewakusanya hapa wafugaji nyuki na wazalishaji wa asali, walio kwenye mnyororo mzima wa utoaji wa huduma wanaotengeneza vifaa na wanaotoa elimu kwa wananchi ili waweze kunufaika na Sekta hii ndogo ya nyuki” amesema Mhe. Kairuki.

 

Amefafanua kuwa Maonesho hayo ni ya kipekee kwa sababu Tanzania inatarajia kuwa Mwenyeji wa Kongamano la 50 la Ufugaji Nyuki Duniani Septemba 2027, ambapo Tanzania itapokea si chini ya wafugaji nyuki takribani elfu kumi ambao  wataambatana na wenza ,watoto, ndugu na marafiki.

 

Amesema  kongamano hilo litasaidia kukuza Sekta ya nyuki sambamba na kuinufaisha sekta ya utalii kwa kuwa italeta watalii wengi zaidi kupitia tukio hilo ambalo pia litaonyesha namna gani Tanzania imepiga hatua katika ufugaji nyuki na asali.

 

“Kongamano hilo pia litawezesha kupata fursa za ufugaji nyuki na asali, kutengeneza soko, kwa wafugaji nyuki na wazalishaji wa asali, kuwepo kwa mafunzo ya namna bora ya kuweza kuzalisha, mizinga ya kisasa,matumizi ya teknolojia na ubunifu katika ufugaji nyuki na uzalishaji wa asali,upatikanaji wa mitaji kupitia taasisi zetu za fedha” amesema.

 

Waziri Kairuki ametumia fursa hiyo kuwakaribisha Watanzania wote kujitokeza kuchangamkia fursa za ufugaji nyuki na uzalishaji wa asali huku akisisitiza kuwa uwekezaji wake ni wa gharama nafuu lakini unazalisha faida kubwa.

 

“Watanzania ufugaji nyuki unalipa, mwezi wa saba Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii inatarajia kusaini mkataba na nchi ya China kuwa mojawapo ya soko la asali na tunaamini soko litakuwa kubwa zaidi” amesema Mhe. Kairuki.

 

Awali katika hotuba yake amesema kuwa Tanzania ni nchi ya pili inayoongoza kwa uzalishaji wa asali Barani Afrika (baada ya Ethiopia) na msambazaji mkubwa wa asali kwa Umoja wa Ulaya kutoka Afrika huku ikikadiriwa kuwa na uwezo wa kuzalisha mazao ya nyuki takriban tani 138,000 za asali na tani 9,200 za nta kwa mwaka. Uzalishaji wa sasa unafikia takriban tani 32,691 za asali na tani 1,907 za nta.

 

“Tanzania inauza nje wastani wa tani 1,695 za asali na tani 467.5 za nta na inazalisha wastani wa mauzo ya dola za Marekani 10,730,294.12 kila mwaka”amesisitiza.

 

Naye, Rais wa Apimondia Dkt. Jeff Pettis amesema kuwa ufugaji nyuki ni njia mojawapo ya kumtoa mtu katika umasikini huku akisisitiza kuwa nyuki ni rafiki wa mazingira na wana nguvu kwa kulinda mazingira asilia.

 

Aidha, amesema ni vyema kushirikiana kufanya kazi kwa pamoja kuuza bidhaa za asali katika masoko ya ndani na pia kufanyia kazi mnyororo mzima wa thamani wa mazao ya nyuki ili kuwapa walaji faraja kwamba wanapata asali halisi.

 

Katika hatua nyingine Dkt. Pettis ameridhishwa na  asali ya Tanzania na kusema kuwa ina sifa nzuri kwenye Soko.

 

Mmoja wa Washiriki wa Maonesho hayo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Asilia African Honey, Reginald Saria amesema kuwa maonesho hayo yamewasaidia kukutana na watu tofauti ndani ya nchi na nje ya nchi hivyo kutangaza bidhaa zao za asali.

 

Maonesho hayo yanayotarajiwa kumalizika Juni 21, 2024 yamehudhuriwa na watu zaidi ya 500 kutoka nchini Tanzania pamoja na nchi za Zimbabwe, Kenya, Uganda, USA, UK, Spain, Lesotho, Botswana, South Africa, Egypt, Mauritius, China, Burundi, Turkey, Zambia na Pakistan.

 


Umoja wa Ulaya, UNCDF yaiunga mkono serikali kufikia malengo ya Nishati Safi ya Kupikia

$
0
0

 

Mkuu wa UNCDF Tanzania, Peter Malika akitoa maelezo kuhusiana na umuhimu wa kongamano hilo la  kujadili mradi wa Nishati Safi ya Kupikia lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa UNCDF Tanzania, Peter Malika (aliyenyoosha kidole kwenye jiko) na Meneja wa Mradi wa mradi wa Cookfund unaosimamiwa na  UNCDF  Imanuel Muro wakionyeshwa moja ya jiko na Mkaa Mbadala kwenye Mabanda ya Ubunifu wa Teknolojia wa Nishati Safi ya Kupikia katika kongamano  lililofanyika jijini Dar es Salaam.

Program Meneja wa Nishati wa  Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) Massimiliano Pedretti akizungumza juu ya Mradi huo na malengo yake kwenye kongamano la Kitaifa la Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mradi wa UN CDF wa Wizara ya Nishati Joyce Msangi akichangia akizungumza katika kongamano la Kitaifa la Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia lililofanyika jijini Dar es Salaam.

 

Na Mwandishi Wetu

Katika kufikia malengo ya mwaka 2034 ya  kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi, wadau wametoa wito wa kutolewa elimu ya kutosha Kwa jamii mijini na vijijini ili kufikia malengo hayo kwa haraka.

Hayo yamesemwa na wadau katika Kongamano la  
wadau wa nishati safi kwa ajili ya utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa miaka 10 liloandaliwa na Shirika la Maendeleo la Mitaji la Umoja wa Mataifa ( UNCDF) kwa siku tatu katika  hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).


Katika kongamano hilo wa wadau wamesema utekelezaji wa ajenda ya nishati Safi utakuwa na mafanikio kwa sababu licha ya  jitihada kubwa za serikali na wadau, una utashi mkubwa ulioyeshwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Meneja wa Mradi wa mradi wa Cookfund unaosimamiwa na  UNCDF  Imanuel Muro amesema kuwa katika kufikia malengo ya mradi huo ni pamoja na kutoa elimu katika ngazi zote juu ya uhamasishaji wa kutumia Nishati Safi ya Kupikia ikiwemo Teknolojia ya Mkaa mbadala na Nishati nyinginezo ambazo hazitokani na ukataji Miti, uchafuzi wa mazingira na hatarishi kwa afya ya binadamu, wakiwemo wanawake na akina mama ambao kwa kiasi kikubwa wanatumia muda mwingi katika mapishi kwa familia.

Muro amesema kuwa katika kufikisha elimu wanatarajia kutoa magari mawili yatakayofanya kazi ya kutoa elimu katika ngazi zote kutoka kwa wataalaam.

Aidha amesema kuwa mwamko umeanza kwa Sekta binafsi kuwa na ubunifu wa teknolojia ya utengenezaji wa majiko ya Kupikia pamoja na Mkaa mbadala ambao ni rafiki, zinaokoa muda na kulinda mazingira.

Mkuu wa UNCDF Tanzania, Peter Malika, amesisitiza juu ya umuhimu wa kongamano hilo lililofanyika kwa siku tatu  linawaleta wadau kwenye majukwaa hayo kujadili na kuona namna gani wanakwenda kutekeleza mradi huo.

Pia amesema kuwa UNCDF inategemea kuwa na majukwaa ya aina hiyo mikoani ili kuwafikia watu wengi zaidi.

Amesema kuwa kuna umhimu kuambatanisha juhudi za kuelekea malengo endelevu ambayo yanasisitiza umuhimu wa Nishati Safi ya Kupikia ambayo itaokoa ukataji miti na kulinda afya ambapo jamii, likiwemo kundi kubwa la wanawake inaathirika na madhara mbalimbali ya moshi wa kuni.

Aidha kongamano hilo  linatoa nafasi kwa ajili ya mazungumzo, ushirikiano na hatua za kuchukua ili kufikia maono sawa ili Tanzania iende sawa na mkakati huu wa kidunia.

Kongamano hilo lenye kauli mbiu ya “Masoko na Teknolojia katika kubadilisha mapishi safi kwa kuzingatia mkakati wa kitaifa wa nishati safi wa 2024-2034’ una  lengo la kuwaleta pamoja wadau muhimu katika mnyororo wa thamani wa nishati safi ya kupikia .

Program Meneja wa Nishati wa  Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) Massimiliano Pedretti  amesema kuwa walipokuwa wanaandika mradi hawakutegemea kupata mwitikio mkubwa lakini wameona mwitikio  huo umeanza na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kama mkuu wa nchi  ameonyesha kwenda kuleta mabadiliko.

Amesema kuwa kazi iliyopo ni kwenda kutoa elimu katika maeneo yote pamoja na kuhakikisha jamii wanakwenda kutumia Nishati Safi ya Kupikia.


Mratibu wa Mradi wa Nishati Safi ya Kupikia wa   Wizara Nishati Joyce Msangi amesema kuwa kazi ya Wizara ni kutengeneza Sera ya kuweza kufikia mipango ikiwemo kuangalia uwezekano wa kodi zinatozwa kupungua ili kila mwananchi awe na uwezo wa kupata Nishati Safi ya Kupikia  kwa kuanzia ngazi ya chini hadi juu.

Amesema kongamano hilo limetoa picha na kufanyia kazi maoni ya wadau katika kuhakikisha huo uelewa unamfikia kila mtu.

Mhandisi wa Maendeleo ya Mradi wa Watu na Umeme Egberth Bashweka amesema katika Ubunifu wao wameona njia rahisi ya nishati Safi ya Kupikia ni pamoja na matumizi ya nishati ya  Umeme jua ambapo umefanya vizuri baadhi ya Taasisi kuwa na majiko ya kutumia umeme wa jua.

Amesema kuwa Umeme wa  jua unapunguza gharama nyingi  na kurahisha shughuli mbalimbali za maendeleo.

ACT-Wazalendo watia neno Bajeti Kuu ya Serikali 2024/25

$
0
0

Waziri Mkuu Kivuli wa Chama cha ACT-Wazalendo, Isihaka Mchinjika, akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uchambuzi wa Bajeti Kuu ya Serikali, iliyowasilishwa bungeni hivi karibu na Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba.

TAASISI ZA UMMA ZITUMIE MIFUMO YA KIDIJITALI – WAZIRI MKUU

$
0
0

*Azindua mifumo minne ya kidijiti Serikalini

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezitaka taasisi za umma ziweke mipango madhubuti ya kutumia mifumo ya kidijitali ambayo italeta mageuzi ya kiutendaji na kuifanya Tanzania kuendana na mapinduzi ya nne ya viwanda yanayotumia TEHAMA.

Amesema kuwa mifumo hiyo pamoja na mambo mengine itasaidia kuwabana watumishi wazembe. “Kunahitajika msukumo kuhakikisha mifumo hii inatumika. Niwaelekeze Watendaji Wakuu na watumishi wa umma kuhakikisha mnaandaa mipango na mikakati ya muda mfupi na mrefu ya jinsi mifumo ya kidigitali itakavyotumika kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa umma.”

Amesema hayo leo (Jumapili, Juni 23, 2024) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika katika viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma. Pia alizindua Mifumo ya Kidijitali ya Uwajibikaji na Usimamizi wa Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma iliyosanifiwa na kujengwa na Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora.

Mifumo iliyozinduliwa ni Mfumo Jumuishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (e-WATUMISHI), Mfumo wa Usimamizi wa Utendaji Kazi (PEPMIS kwa watumishi wa umma na PIPMIS kwa taasisi za umma), Mfumo wa Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma (HR Assessment) na Mfumo wa e-Mrejesho.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaelekeza watendaji wakuu na watumishi wa umma waandae mipango inayopimika. “Mipango hii inapaswa kuwa wazi, yenye malengo yanayopimika na kuzingatia mahitaji ya wananchi na matakwa ya sera za Serikali.”

Katika hatua nyingine, Majaliwa amezitaka taasisi za umma kutoa mafunzo na kuhamasisha matumizi sahihi ya mifumo kwa watumishi wote kwa kuwa ni mipya kwa watumiaji wengi. Ni muhimu kuhamasisha na kuwaelimisha watumishi kuhusu umuhimu wa mifumo hii katika kuboresha huduma kwa umma na kufikia malengo ya Serikali.”

Mapema, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene alisema ubunifu wa mifumo hiyo iliyosanifiwa na kujengwa na Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora umeokoa zaidi ya sh. bilioni 11 ambazo zingetumika kununua mifumo mipya na sh. milioni 616 ambazo zingetumika kila mwka kulipia leseni za mifumo hiyo.

“Mifumo ambayo imekamilika na inasomana, imejengwa na vija25 wa Kitanzania kutoka Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Ofisi ya Rais – Ikulu, Wizara ya Fedha, Wakala wa Serikali Mtandao, Ofisi ya Rais – TAMISEMI na PSRS,” alisema.

Vijana walikabidhiwa vyeti na kutunukiwa tuzo maalumu ili kutambua mchango wao kwa Taifa.



Serikali 'yaipiga Jeki' NHIF kufikisha elimu kwa Umma

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko, akitoa hotuba yake wakati wa kufungua rasmi kituo cha kutoa elimu ya kujiunga na Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya (NHIF) iliyokwenda sambamba na upimaji wa afya bure katika kituo cha mabasi cha kimataifa cha Magufuli jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa NHIF Mkoa wa Kinondoni, Dk. Raphael Mallaba.  (Na Mpiga Picha Wetu).
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Kinondoni, Dk. Raphael Mallaba, akizungumza wakati wa ufunguzi wa kituo cha kutoa elimu ya kujiunga na Mfuko huo iliyokwenda sambamba na upimaji wa afya bure katika kituo cha mabasi cha kimataifa cha Magufuli jijini Dar es Salaam.

 



 
Na Mwandishi Wetu


Serikali imesema upo umuhimu wa kuuongezea nguvu Mfuko wa Afya Bima ya Afya wa NHIF ili uweze kufikisha elimu kwa umma juu ya faida za kuwa na bima ya afya kwa maslahi mapana ya mtanzania mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe; Hassan Bomboko wakati wa ufunguzi wa kituo cha kutoa elimu katika kituo cha mabasi cha kimataifa Mgafuli kilichopo mbezi jijini Dar es Salaam.

"Sisi kama serikali tumeona upo umuhimu wa kuwapa nguvu NHIF kufikisha elimu kwa umma na nitumie hadhara hii kutoa maelekezo kwa watendaji wa kata na mitaa, kwamba kwenye mikutano yote ya hadhara wawape elimu wananchi juu ya umuhimu wa mfuko wa NHIF kwa wananchi wetu, 

"Iwe ajenda, na kaimu afisa tawala uko hapa, magavana wote muifanye hii kazi ya kuhakikisha katika ziara zenu mikutano yenu ya kuwaelewesha wananchi kwamba dunia ya sasa inakuhitaji kuwa na bima ya afya ili uweze kupata huduma kirahisi pasi na kulazimika kutumia pesa ambayo hukuwa umepanga kuitumia .

Japo la pili wananchi tuwe na utamaduni wa kupima afya zetu, leo nimekuta hapa zoezi linaendelea na ni zoezi zuri lialofanywa na wenzetu wa Kairuki nawapongezeni sana, wananchi wetu wamepata huduma hapa na ni huduma ambayo wameipata bila malipo yoyote kwaiyo tunawashukuruni na mfikishe shukrani zetu kwa wakurugenzi na nyie ambao mko hapa kuendesha zoezi hili.

Ilani ya Chama cha Mapinduzi imeelekeza kwamba wananchi wapate elimu juu ya namna ya kujiunga katika bima ya afya, mzifikie na shule zetu za msingi na sekondari muwape elimu wanafunzi na wazazi juu ya faida ya kujiunga na mifuko ya bima ya afya."amesema Bomboko

Niwapongeze sana NHIF kwa kutoa huduma na kuwafikia wananchi wengi. Wananchi wamekuwa wakipatiwa huduma mbalimbali jambo la msingi ambalo limekuekuwa likiendelea ni NHIC kuona ipo haja Serikali kuwa na kituo hapa  katika wilaya yetu ya ubungo. 

Toka kituo hiki kimefunguliwa kimekuwa  na mafanikio makubwa sana nje na utaratibu wa kawaida kimewafikia watu wengi sana na kuwapa elimu na hii elimu ndiyo imewaondoa wasiwasi wananchi  kwamba tunatoa hela lakini yawezekana ni siumwe mimi nikakaa muda mrefu na hela yangu ikaenda bura, lakini leo wamejua umuhimu wa jambo hili.

Amewataka wananchi kutambua kuwa sio lazima hadi uumwe ndio uende hospitali, bali kila mwananchi anaowajibu wa kwenda hospitali kuangalia afya yako na kuweza kujua hali yako kuliko kusubiri kuugua ndio unakwenda hospitali kwani itakusaidia kujua nini ufanye ili afya yako iendeleeee kuwa bora"amesema Bomboko.

"Wananchi wengi walikuwa wanakuja maofisini kwa ajili ya kupima afya zao na changamoto ya wanaokuja maofisini wengi wanakuwa ni wagonjwa. hivyo kama taasisi tumekuwa na mikakati ya kuwafuata huko waliko hapa ni sehemu moja wapo tu lakini tunatembelea kila maeneo ambayo  yana makundi ya wananchi ili tuwape elimu na wananchi wanapojiunga inarahisha kuwafikia kwa kiasi kikubwa zaidi. Hivyo muamko umeendelea kuwepo ndio maana hapa tulipo leo mtashuhudia wananchi wakijaza fomu na kupata bima zao." amesema Meneja wa NHIF Mkoa wa Kinondoni, Dk. Raphael Mallaba.


RAIS MSTAAFU DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE AONGOZA JOPO WAZEE WA JUMUIYA YA SADC NCHINI LESOTHO

$
0
0

Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo tarehe 26 Juni, 2024, yuko katika Ufalme wa Lesotho kwa nafasi yake kama Mwenyekiti wa Jopo la Wazee wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).


Jopo hili la Wazee wa SADC ambalo Makamu Mwenyekiti wake Mheshimiwa Paramasivum Pillay B. Vyapoory, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Mauritius, limekutana na Serikali na wadau mbalimbali ndani ya Ufalme wa Lesotho, kama mwendelezo wa juhudi ya kusaidia upatitanaji wa utulivu wa kisiasa katika Ufalme huo.

Jopo limekutana na Mhe. Ntsokoane Samuel Matekane, Waziri Mkuu wa Ufalme wa Lesotho; Mhe. Nthomeng Justina Majara, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Sheria na Masuala ya Bunge; Mhe. Mamonaheng Mokitimi, Mwenyekiti wa Seneti; Viongozi wa Vyama vya Upinzani; Mhe. Constance Seoposengwe, Balozi wa Afrika Kusini nchini Lesotho; na wadau mbalimbali.
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>