Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

Magazeti ya Tanzania Disemba 14, 2023


Mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa (GDP) wafikia asilimia 9.1 mwaka 2020

$
0
0


Hongera Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuadhimisha miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Umoja na mshikamano ni chachu ya maendeleo ya Taifa letu. Leo, hapa Dodoma, tumeshiriki katika Mkutano wa Kwanza wa Kitaifa wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. 

 

Kupitia Mkutano huu, Mhe. Anthony Mavunde, Waziri wa Madini amechukua fursa ya kutafakari (reflect) utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. 

 

Wizara ya Madini imefanikiwa katika mambo kadhaa nayo ni: 

 

1. Mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa (GDP) umefikia asilimia 9.1 kwa mwaka 2022.

 

2. Ukuaji wa Sekta ya Madini umefikia asilimia 10.9% kwa mwaka 2022. 

 

3. Thamani ya madini yaliyouzwa nje ya nchi kwa mwaka 2022 yalifikia dola za Marekani bilioni 3.4 ambayo ni sawa na asilimia 56 ya mauzo yote ya bidhaa nje ya nchi. 

 

4. Ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali kwa mwaka 2022/23 yalikuwa bilioni 678. 5. Mapato ya kikodi yaliyopatikana kutokana shughuli za madini ni shilingi bilioni 808.9 mwaka 2022/23. 

 

Aidha, tunampongeza Mhe. Prof.Kitila Mkumbo kwa kuteua timu ya wataalamu ya uandaaji na uandishi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050. Timu hii imejaa wabobevu na watu mahiri. Tunawapongeza wateule wote. Vilevile, Wizara ya Madini itashirikiana kwa karibu na timu hii. 

 

Kupitia ushirikishwaji huo tuna imani kuwa Sekta ya Madini itakuwa ni kitovu cha maendeleo ya taifa letu na kutoa mchango mkubwa zaidi kwenye uchumi wetu. Madini ni Maisha na Utajiri. Katika miaka ya karibu tunakusudia yafuatayo: 

 

A. Tanzania kuwa kinara wa madini mkakati barani Afrika.

B. Tanzania kuwa kinara wa madini ya vito barani Afrika.

C. Sekta ya Madini kuzifungamanisha sekta nyingine zote katika uchumi wa taifa letu. Kadhalika, Wizara ya Madini itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo wa ndani na nje ya nchi katika kuendeleza na kukuza uchumi wa Tanzania kupitia sekta ya madini.

KANALI LABAN: MABADILIKO SERA YA ELIMU, MAJIBU YA CHANGAMOTO ZA UCHUMI

$
0
0


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Thomas Laban (wa pili kulia), akikabidhi tuzo kwa Prof. Makenya Maboko (kushoto), mzungumzaji mkuu kwenye kongamano la 33 la Wanadhuoni wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania lililofanyik katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.


Maboresho ya sera mpya ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 yana lengo la kuifanya elimu itakayotolewa nchini kukidhi mahitaji ya soko la ajira na maendeleo ya kiuchumi nchini.


Haya yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mh. Kanali Laban Thomas, alipohudhuria Kongamano la thelathini na tatu la Wanazuoni wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania lilifanyika Disemba 13, 2023 katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ambapo alikuwa mgeni rasmi.


“Maboresho haya yanalenga kujibu maswala yote yahusuyo ajira, yamekuja na suluhisho la namna changamoto za utungaji mitaala na namna sahihi ya uandaaji wanafunzi katika ngazi mbalimbali za elimu ili waweze kutambua nafasi zao na namna ambayo watashiriki katika uzalishaji mali.” Amesema Kanali Laban.


Kwa upande wa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof. Elifas Bisanda, amesema lugha sio kikwazo kwa mitaala mipya kwani kinachotakiwa ni ujuzi na uzoefu wa waalimu ambao watatumia kuutoa kwa wanafunzi.


“Lugha ya kufundishia si tatizo kwa watoto badala yake ni walimu wanaofundisha kwa kutumia Kiswahili badala ya Kiingereza ambayo ndiyo lugha ya kufundishia kuanzia ya elimu ya sekondari. Kimsingi, walimu hao wanatakiwa wawe na uwezo wa kutoa ujuzi kwa lugha husika na wanafunzi wataelewa na kupata ujuzi pale mwalimu anapokuwa mahiri katika lugha ya kufundishia," amesema Prof. Bisanda. 


Aidha, Prof. Makenya Maboko, mhadiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam ambaye alikuwa mzungumzaji mkuu amesema wakati umefika ambao Tanzania inahitaji kubadilisha mitaala yake kupitia sera. Pia kuitekeleza mitaala hiyo kupitia elimu ujuzi kuanzia ngazi za chini ambayo itaamua mustakabali wa wanafunzi baada ya kumaliza kiwango fulani cha elimu.


“Kupitia mtaala mpya wa elimu na mafunzo itatakiwa muundo mpya utakaoimarisha upatikanaji wa maarifa, ujuzi na mitazamo itakayozingatia ajira na kujiajiri. Uanzishwaji wa programu utaendana kwa karibu zaidi na mahitaji ya soko la ajira na fursa za kiuchumi nchini,” amesema Prof. Maboko.


Akizungumza katika kongamano hili muhitimu wa Shahada ya Umahili ya Usimamizi wa Miradi, Dkt. Malneste James, ameipongeza serikali kwa kuleta mabadiliko ya sera ya elimu katika wakati muafaka.


 Hivyo, anategemea maandalizi yanayofanyika kwa ajili ya kuanza kufundisha kupitia sera hii mpya, jamii itashuhudia mabadiliko makubwa.


Kongamano la thelathini na tatu la Wanadhuoni wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania limefanyika Disemba 13, 2023 katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ambapo wanazuoni wamekutana katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kituo cha mkoa wa Ruvuma na kujadili kuhusu  mabadiliko ya sera ya elimu ya mwaka 2014 yanayoanza kutekelezwa hivi karibuni.

MAXIME AIVUTIA KASI SIMBA YA BENCHIKA

$
0
0

 

Na John Marwa


Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema wamefanya maandalizi mazuri na wachezaji wake wako tayari kwa mchezo dhidi ya Simba.



Amesema utakuwa mchezo wa ushindani mkubwa kwa sababu ya wapinzani wao Simba wanacheza ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo wataingia kwa heshima kubwa.


“Hatutaingia kwa kuibeza kwa sababu Simba wanacheza mechi mfululizo wako fiti sana na kuimarika na hatutakiwi kuingia kwa kuwabeza tofauti na sisi tunakaa muda mrefu.


Simba imekutana na timu kama Al Ahly ambayo wanatoka nao sare kwa hiyo sio timu ya kuingia kirahisi rahisi kwa sababu ya ubora wao,” alisema Mecky.


Kuhusu kocha Benchikha amesema katika soka hakuna ugeni kwa sababu mechi wachezaji ndio jukumu lao la uwanjani kocha kazi yake ni kufundisha na mpira hauna ugeni au mwenyeji anayejipanga vizuri.


Nahodha wa Kagera Sugar, Khamis Kiiza alisema mechi itakuwa ya ushindani wamejipanga na wachezaji watajitolea kutafuta matokeo mazuri.

Benchika aipigia hesabu kali Kagera Sugar

$
0
0

Na John Marwa

WAKATI Simba inashuka dimbani leo dhidi ya Kagera Sugar, Uongozi wa timu hiyo umekana kuhusishwa na usajili wa nyota watatu, Lameck Lawi wa Coastal Union na Ladack Chasambi kutoka Mtibwa Sugar pamoja na Eric Mbangossoum kutoka Union Touarga Sportif ya Morocco 

Umesema ni mapema kuzungumzia usajili huo kwa sababu  benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Abdallah Benchikha linafanya tathimini juu ya nani wa kumuingiza katika eneo lipi na nani wa kutoka Simba.



Tayari Simba inahusishwa kumalizana na nyota wawili, mmoja ni mzawa ambaye ni Chasambi na Eric wanaotajwa kuwa miongoni mwa nyota ambao watajiunga na kikosi cha wekundu hao katika usajili ya dirisha dogo lililofunguliwa hapo kesho desemba 16.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally, amesema zoezi lote la usajili liko mikononi mwa kocha Benchikha ambaye amefanya tathimini ya kikosi chake na kuona wapi na nani anaweza kuongeza nguvu.

“Kwa sasa ni mapema sana kuzungumza lolote juu ya usajili na nani anaingia au kutoka, hilo ni jukumu la kocha ambaye amefanya tathimini ya timu yake na tunatarajia kupata mapendekezo juu ya nafasi na wachezaji wataongezwa kikosini.

Muda ukifika kila kitu kitawekwa wazi kwa sasa akili na nguvu zetu kuelekea mechi zilizopo mbele yetu, tunakibarua kigumu cha kutafuta pointi tatu dhidi ya Kagera Sugar baada ya hapo kuna Wydad Casablanca kuwapeleka moto hapa nyumbani na kuacha alama ya Ligi ya Mabingwa Afrika,” Amesema Ahmed.

Kuelekea mchezo wao dhidi Kagera Sugar unaotarajia kucheza leo saa 10:00 alasiri, uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Kocha Benchikha amesema baada ya safari ndefu kutoka Morocco wamerejea na kufanya maandalizi mazuri kwa ajili ya kuvuna alama tatu katika mchezo huo aa ligi kuu.


Amesema amepata fursa ya kuona taarifa za wapinzani wao na ameaandaa kukosi chake kwa ajili ya ushindani mkubwa kulingana na ubora wa mchezo huo.


“Tunahitaji ushundi, tunawaheshimu wapinzani wetu , kwa upande wangu hii mechi ni muhimu sana baada ya hapa nitaifikiria Wydad Casablanca. Hakuna mechi rahisi na kila mchezo umekuwa na maandalizi yake.


Kuwepo kwa mfululizo wa mecho kila baada ya siku mbili au tatu hilo haitakuwa na athari kikubwa ni kuandaa timu kulingana na mpinzani unayekwenda kucheza naye,” alisema Benchikha.


Mwakilishi wa wachezaji kwa upande wa Simba, Ally Salim amesema wamejiandaa vizuri kwenda kuwakabili wapinzani wao Kagera Sugar kuhakikisha wanafanikiwa kuvuna alama tatu muhimu.

Wahitimu 554 watunukia Shahada mbalimbali Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam 2023

$
0
0

Jumla ya wahitimu 554 wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam wametunukiwa shahada mbalimbali na Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein wakati wa Mahafali ya 22 ya chuo hicho. 


Mahafali hayo yalifanyika Disemba 14, 2023 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) ambapo Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Ali Mohamed Shein alisema kuwa kuna haja ya kuendeleza maeneo ya ardhi ya Chuo ambayo yapo jijini Dar es Salaam kwa kuangalia fursa za kiuchumi zilizopo na zenye mwelekeo wa baadae.  


Dkt. Shein amesema Chuo hicho kikiwa na ukumbi mzuri wa aina yake itakuwa ni jambo la maana na fahari kwa chuo na jamii inayowazunguka, na kuongeza kuwa
wanaweza kujenga ukumbi wao unaokidhi haja na mazingira ya kisasa kwa kutumia shughuli zao rasmi na kukodisha watu wengine ili kujiongezea kipato. 

Licha ya hayo ameoumba uongozi wa Chuo kuhakikisha kuwa wanaboresha mazingira ya kusomea katika eneo la Kituo cha Tegeta Ndaki ya Dar es Salaam ambako wanafunzi ngazi ya Shahada ya Kwanza wanasoma pia kutokana na uwingi wao watakuwa mabalozi wazuri wa kukitangaza chuo. 


Dkt. Shein ameeleza kuwa kutokana na kuwa na ndaki tatu sasa wanakamilisha ndaki ya Tanga ambayo itakamilika muda mchache ujao ili kuendelea kutoa elimu kwa maendeleo ya watu kama. Kauli mbiu ya Chuo Kikuu Mzumbe inavyosema. 


Naye Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, William Mwegoha amesema kuwa kwa mwaka wa masomo 2022/2023  kilisajili jumla ya wanafunzi 1,699 Ndaki ya Dar es Salaam. 


Baadhi ya hao, ndiyo watakaohitimu katika mahafali hayo.
Katika mahafali ya 22 ya Chuo Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Dar es Salaam jumla ya wanachuo 554 wamehitimu katika ngazi mbalimbali za kitaaluma na kustahili kutunukiwa shahada mbalimbali. 


Katika ya hao, wahitimu 428 wametunukiwa Shahada za Umahiri na wahitimu 126 wamenukiwa Shahada ya Awali.
Kwa mwaka wa masomo 2022/23, idadi ya wahitimu wa Wanawake ni 311 sawa na asilimia 55.30 na wanaume ni 243 sawa na asilimia 44.70.

“Ni jambo la kujivunia na furaha sana kuona uwiano mzuri kati ya  wahitimu wanawake na wanaume. Sisi kama Chuo Kikuu Mzumbe tutaendelea kupanua fursa na kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia ili kuhakikisha kuwa uwiano huu unadumishwa mwaka hadi mwaka.” Amesema Prof. Mwegoha

Pia amewapongezawaitimu wote kwa kuhitimu masomo yao na amewaomba wakatumikie jamii na taifa kwa ujumla wakatumie vizuri maarifa, elimu na stadi walizopata Chuo hapo

“Elimu na stadi mlizopata kutoka Chuo Kikuu Mzumbe viwe chachu ya kuleta maendeleo chanya katika jamii inayowazunguka, taifa na dunia kwa ujumla. 


Pia amewaomba wakawe mabalozi wazuri wa Chuo Kikuu Mzumbe kwa kuwa waadilifu na wachapakazi bora.

 Baadhi ya wahitimu.
 

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwatunuku Shahada wahitimu katika Mahafali ya 22 ya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam leo Disemba 14, 2023.

 


WANDEWA WAMERUDI, BENCHIKA AANZA KWA TATU BILA

$
0
0

 

Na John Marwa


Wekundu wa Msimbazi Simba wamerejea kwenye michezo ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara NBC PL kwa kuwachapa Kagera Sugar tatu bila, mchezo uliolindima Dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam jioni ya leo.



Mnyama Simba ameshuka dimbani leo kuzisaka alama tatu muhimu ikiwa ni baada ya kutopata matokeo katika michezo miwili ya mwisho ya NBC PL, dhidi ya Yanga na Namungo ambapo walipoteza kwa Yanga kichapo cha mabao 1-5, huku wakienda sare na Namungo ya bao 1-1.


Ushindi huu ni wa kwanza kwa Kocha Bennchika tangu achukue mikoba ya kukinoa kikosi cha Mnyama pia ukiwa ni mchezo wake wa kwanza kuiongoza Simba katika NBC PL.


Mabao matatu ya Simba yamewekwa kimiani na Said Ntibanzonkiza dakika ya 45, Sadio Kanoute dakika ya 75 na John Bocco dakika ya 90.


Simba ushindi huo unawapa morali ya kuelekea mchezo wa marejeano wa Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL hatua ya makundi dhidi ya Wydad Casablanca utakaopigwa Desemba 19 Dimba la Benjamin Mkapa saa kumi jioni.

Kongamano la Kimataifa la Vijana Wanawake Viongozi lafanyika Kibaha

$
0
0




Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Riziki Pembe Juma (kulia) akimkabidhi cheti mmoja wa washiriki wa Vijana  Mtandao wa  Wanawake Barani Afrika.

 

Na Talib Ussi

 

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Riziki Pembe Juma amesema  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua  kuwa Jinsia na Usawa ni vipengele muhimu vya kufanikisha maendeleo endelevu nchini.

 Mhe. Riziki aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akifunga Kongamano la Vijana Wanawake Viongozi  kutoka nchi 16 Baraza Afrika, lililofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere  Kibaha, Mkoa wa Pwani.                                             

Alisema masuala ya jinsia na usawa yameainishwa katika Katiba zote mbili, katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na ya Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar ya mwaka 1984. 

                                                    .                                Alieleza kwamba  lengo la kuainishwa humo ni katika kusimamia haki na usawa na kuhimiza ushiriki wa wanawake katika kufanya maamuzi.                                                                                                  

Pia alisema  katika Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025 imeainisha umuhimu wa Jinsia na Usawa.                                                                                                                    

Alisema katika kufanisha maendeleo hayo Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, na Makundi Maalum (SMT) na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (SMZ) zimeanzishwa kisheria kwa lengo la kuratibu na kusimamia masuala ya Jinsia nchini.

 Aidha alisema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaamini kuwa elimu ni moja ya silaha muhimu hasa kwa wanawake ikiwa watakua na nia ya kufikia maendeleo ya  kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Alieleza kwamba Serikali imeweka makusudi hatua za kukuza elimu ya wasichana na kuwahimiza  waendele kusoma ili wapate elimu ambapo Jamii kwa ujumla inawasaidia wasichana kuendelea na masomo badala ya kuwalazimisha kuingia kwenye ndoa za mapema.

Mhe Riziki alitoa wito kwa washiriki wa kongamano hilo kutumia jukwaa hilo kama fursa ya  kujifunza mbinu bora zaidi ambazo zitafanya kuongeza uwezo wao na ujuzi.                    

Alifahamisha kwamba hatua hiyo itasaidia katika  bara la Afrika kuhimiza vijana wa kike kuthamini elimu itakayowasaidia kupata mapato yao na kupata nafasi katika vyombo vya maamuzi.

Kongamano hilo la siku tatu  limehudhuriwa na watu 100
wanawake vijana ambao ni wanachama wa harakati pamoja na Maafisa wa zamani na wanaharakati wanaoendesha mashirika ya wanawake yenye mafanikio kutoka nchi mbalimbali. 


SAGCOT yapigia chapuo kilimo hifadhi kwa mazingira

$
0
0

Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Abdallah Mitawi (katikati) akizungumza kwenye kikao cha mwaka cha Kikundi kazi cha Kilimo endelevu na jumuishi cha SAGCOT (GRG) kilichofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wapili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Gairo Bw. Jabiri Makame, watatu Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT Bw. Geophrey Kirenga na wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mvumelo Bi. Judith Nguli.

Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Abdallah Mitawi (kushoto) akizungumza kwenye kikao cha mwaka cha Kikundi kazi cha Kilimo endelevu na jumuishi cha SAGCOT (GRG) kilichofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Gairo Bw. Jabiri Makame, na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT Bw. Geophrey Kirenga.
Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Abdallah Mitawi (kushoto) akielezwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Bw. Jabiri Makame, (kulia) namna wilaya yake inavyotekeleza kilimo biashara kinachozingatia uhifadhi wa mazingira wakati wa kikao cha mwaka cha Kikundi kazi cha Kilimo endelevu na jumuishi cha SAGCOT (GRG) kilichofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT Bw. Geophrey Kirenga.


 Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
 

Kikundi cha Kilimo endelevu na Jumuishi cha SAGCOT (GRG)  kimewakutanisha wadau wake kujadili changamoto na kuainisha fursa zitakazo msaidia mkulima kufanya kilimo chenye tija kinachozingatia uhifadhi wa mazingira katika kongani ya Kilombero.

Akizungumza kwenye kikao cha mwaka kilicho wakutanisha wadau kutoka serikalini, Sekta binafsi, asasi za kiraia, taasisi za kifedha na watafiti mbalimbali jijini Dar es Salaam mwishoni mwa, Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Abdallah Mitawi alisema lengo la kikao hiko ni kutathmini na kupitia maazimio ya kikao kilichopita na kuja na maboresho yatakayosaidia sekta hiyo kuleta tija kwa mkulima na kuchangia katika pato la taifa.

“ Wakati Dunia ikikabiliwa na mgogoro wa mabadiliko ya tabia ya nchi na kusabisha uwepo wa mvua wastani hivyo kuna kila sababu ya kuangalia namna bora yaufanyaji kilimo ambacho ni rafiki wa mazingira na tumekutana kukumbushana wajibu wetu tukiwa kama viongozi katika kuhakikisha  kilimo kinakuwa rafiki kwa mazingira,*alisema Bw. Mitawi.

Alisema kilimo kinachangia kati ya asilimia 10  hadi 14 ya hewa ukaa inayosababisha mabadiliko ya tabia nchi, na wanaoathirika zaidi na athari za mabadiliko hayo ni wakulima ambao hutegemea kilimo kwa asilimia 100 hivyo kunakila sababu ya maafisa kilimo kwa kushirikiana na wadau kuhakikisha wakulima wanapata elimu sahihi za kufanya kilimo biashara kinachozingatia uhifadhi wa mazingira nafaida.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Bw. Jabiri Makame alisema katika wilaya yake zaidi ya asilimia 95 ya wananchi wanajiusisha na kilimo hivyo kunakila sababu ya kuhakikisha kilimo kinachofanywa kinatunza na kuhifadhi mazingira sambamba na kuzingatia kanuni za biashara endelevu.

“Katika kusukuma ajenda ya kuendeleza Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa kuzingatia uhifadhi na utunzaji wa mazingira, tumekuwa tukifanya kazi kwa karibu na wadau wakiwemo SAGCOT ambao wamekuwa wakifanya kazi kubwa kutuweka pamoja wadau  kujadiliana changamoto na kuibua fursa zinazochagiza ukuwaji wa pato la taifa sambamba na kuleta mageuzi makubwa kwenye sekta hizo," alisema Bw. Makame.

Naye Meneja wa SAGCOT Kongani ya Kilombero, Bw. John Banga alisema jukwaa hilo linalosimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais linafanya kazi kama chombo cha ushauri kwa SAGCOT katika ngazi za taifa na kongani likingilenga kuratibu na kufuatilia masuala ya kimazingira katika programu zilizoko kwenye Ubia.

"Miongoni mwa vipaumbele vyetu vilivyotokana na kusaini randama ya makubaliano viliangazia ufugaji wa kisasa , kuainisha mazao ya kipaumbele ambayo yatatoa fursa za uchumi kwa wakulima hasa wananchi wa mkoa wa Morogoro sambamba na utunzaji na uhifadhi wa mazingira, *alisema Bw. Banga .

Alisema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipambanua zaidi katika kuhakikisha vijana wanakuwa muhimili wa kukuza uchumi kwa kuzalisha kwa tija.

" Azma  ya Serikali inaonekana wazi kupitia programu za mafunzo atamizi, maarufu kama Building a  Better Tommorow (BBT) kwa upande wa sekta ya Kilimo na BBT- LIFE kwa upande wa sekta ya Mifugo, hivyo kupitia programu hizo zitakenda kuchochea na kuibua ubunifu kwa vijana kushiriki katika kilimo na ufugaji wenye tija pamoja na kuwainua kiuchumi," alisema Bw. Banga.

 

KIKWETE ASEMA MIFUMO MIPYA YA UTENDAJI KAZI SERIKALINI KUWABANA WATUMISHI WASIOFANYA KAZI

$
0
0

 

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete akizungumza  leo na Menejimenti ya Chuo cha Ufundi Arusha ( ATC) ikiwa ni muendelezo wa ziara  yake ya kukagua maendeleo ya mafunzo ya mfumo wa utendaji kazi kwa watumishi wa umma kutika Chuo  Ufundi Arusha ( ATC)  yaliyofanyika katika Chuoni hicho.

Mkurugenzi wa Maadili kutoka Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora  ambaye pia ni Mwezeshaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma, Bi. Leila Mavika akizungumza kabla ya kumkaribisha  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete. 

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwa  na Mkuu wa Chuo cha Arusha( ATC) Dkt.Musa Chacha wakiangalia baadhi ya mashine za kufundishia wanafunzi kwa vitendo katika chuo hicho kilichopo Jijini Arusha.


 

Na Lusungu Helela- Arusha 
 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Ridhiwani Kikwete amesema matumizi ya mfumo wa PIPIMS, PEPMIS na HR Assessment  katika Utumishi wa Umma nchini  itaimarisha Utumishi wa Umma kwa  kuwabana Watumishi wanaopenda kukaa ofisini pasipo kufanya kazi.

Mhe.Kikwete ametoa kauli hiyo leo Jijini Arusha wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na Watumishi wa  Ofisi ya  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha ( AICC) na Chuo cha Ufundi Arusha ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi ya kukagua mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa Kupima Utendaji Kazi wa Watumishi wa Umma na Taasisi (PEPMIS na PIPMIS) na Mfumo Maalum wa Tathmini ya hali ya Rasilimaliwatu Serikalini (HR Assessment).

Amesema Serikali imedhamiria kuimarisha Utumishi wa Umma kwa kuhimiza uwajibikaji  ili kuhakikisha kama Taifa linakuwa na utumishi wa umma unaopimika kwa  kumpima Mtumishi mmoja mmoja pamoja  na Taasisi kwa ujumla.

Ameongeza kuwa mfumo wa PEPMIS umekuja kuwa mbadala wa OPRAS ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anayelenga kuimarisha mifumo ya uwajibikaji inayowezesha viongozi na watumishi wa umma kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi wakati na mahali popote.

Katika hatua nyingine Mhe. Kikwete amewataka Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala kuacha kukaa ofisini badala yake waende maeneo ya kazi ili kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi walio chini yao.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe.John Mongela amesema zama hizi hazihitaji watu wenye misuli kutokana na kukua na teknolojia. Hivyo, teknolojia imerahisisha utendaji kazi na sisi tuko tayari kuisimamia utekelezaji wake.

Amesema ujio wa mafunzo hayo  yamekuja wakati muafaka ambapo  Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala wataanza kubadilika na  kuachana na utaratibu wa kizamani wa utendaji kazi wao.

Hata hivyo ametumia fursa hiyo kuiomba Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora kuwanoa upya  Maafisa Utumishi na Maafisa Utawala  wa mikoa na Halmashauri kwani utendaji wao wa kazi sio wa kuridhisha ikizingatiwa wao ndo wenye jukumu la kuwasimamia watumishi wengine.


Serikali kupima utenda kazi wa maofisa Mkonge

$
0
0

Na Mwandishi Wetu, Tanga


WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe, amesema mfumo wa kupima utendaji kazi wa maofisa kilimo sekta ya mkonge uko kwenye hatua za mwisho ambapo kila ofisa kilimo atapimwa kulingana na kazi alizofanya ikiwamo kuwatembelea wakulima shambani.


Akizungumza katika Mkutano wa Nne wa Wadau wa Sekta ya Mkonge uliofanyika mkoani Tanga hivi karibuni, Waziri Bashe amewataka maofisa kilimo kuacha kufanyakazi kwa mazoea na kuwafuata wakulima walipo.


“Tumewaletea mashine za kupima afya ya udongo na hivi karibuni tumepata fedha tunanunua magari kwa ajili ya maofisa kilimo tunataka wawe na magari bado vinakuja vishkwambi, halafu sasa nisikie mtu anabaki ofisini. 


"...Lazima atapimwa mtu kutokana na kazi. Tunaweka mfumo, sasa ule mfumo unakamilika na lazima watu wajaze ripoti kila siku amemtembelea mkulima gani hata kama umemtembelea hujui tatizo utaweka kwenye mfumo aliyeko wizarani atajua hilo tatizo ni nini,” amesema.


Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba amebainisha ongezeko la wakulima wadogo wa mkonge mkoani humo inatokana hamasa inayoendelea kutolewa lakini pia ushirikiano mzuri wanaopata kutoka Wizara ya Kilimo.


“Hadi sasa Mkoa wetu una wakulima wadogo wapya wa mkonge 11,939 wameongezeka kufikia 2,245,000 mwaka 2021, hii inatokana na hamasa na ushirikiano ambao mmeendelea kutupa kama Wizara ya Kilimo tunawashukuru sana,” amesema.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge (TSB), Saddy Kambona akizungumzia shamba la Kibaranga ambalo linamilikiwa na bodi hiyo, ameiomba Idara ya Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Muheza kuwapatia kanzidata na hati ya shamba hilo.


“Bado kumekuwa na mkanganyiko mkubwa kutoka kwa maafisa ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza kwa sababu wao ndiyo walikuwa na ile kanzi data ya wakulima ambao waligawiwa ardhi miaka ya nyuma ambayo tuliiomba waiwasilishe kwetu ili kuepusha migongano lakini hatukuweza kuipata hadi leo. 



“Hati ilirudishwa wizarani na ikafutwa kwa hiyo lile shamba halina hati ila lilikuwa limekabidhiwa tu halmashauri kwa agizo la aliyekuwa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na sisi tulivyoliomba kwenye huo mchakato bado halijarudishwa kwetu kwa hati lakini kiutawala linaonekana lipo kwetu,” amesema Mkurugenzi Kambona.


Pamoja na mambo mengine, amesema wameanza ukarabati wa korona (mashine ya kuchakata Mkonge) ya Kibaranga kwa sababu baada ya kulichukua lile shamba bodi iliwasilisha maombi ya fedha wizarani kwa ajili ya ukarabati wa korona hiyo ambazo walipatiwa na kuanza kufanya mengine yanayolihusu lile shamba.

BABA HALISI: HIJA HALISI MWAKA HUU SIYO YA KUKOSA, NI YA KUPOKEA BARAKA NA UTAJIRI TELE, MAANDALIZI YAPAMBA MOTO, WAZEE WA DAR NA NJOMBE WAJIWEKA MGUU SAWA KWENDA

$
0
0

Dar es Salaam, Tanzania

 
Wakati maandalizi ya Ibada ya Hija Halisi ya mwaka huu yakizidi kupamba moto kwa wengi kuendelea kujisajili kuungana na maelfu ya waliokwishajisajili kwenda Kigoma kwenye Hija hiyo, Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi, Baba Halisi amesisitiza kuwa Hija hiyo siyo ya kukosa kwa sababu ni ya kwenda kupata Baraka na utajiri tele kutoka kwa CHANZO HALISI na siyo kutalii.

Baba Halisi ametoa msisitizo huo jana Jumapili 12 Thebeti, 1 Majira HalisiI au Disemba 17, 2023 kwa Kalenda ya Gregory, katika Ibada iliyofanyika Makao Makuu ya Kanisa Halisi la MUNGU BABA, Tegeta - Namanga, Jijini Dar es Salaam na kuhudhuria na mamia ya watu wakiwemo Watekeleza Sauti, Uzao na watu wengine mbalimbali.

Kwa mujibu wa Baba Halisi jana lilikuwa lango ambalo Waabuduo Halisi walipatikana, hivyo iliambatana na sherehe ambapo Baba Halisi alitoa makreti kwa makreti ya vinywaji baridi (soda), na kuhakikisha kila yeyote aliyekuwepo kwenye ibada hiyo anakunywa hadi kutosheka.

Baada ya Baba Halisi kuachilia somo la WAABUDUO HALISI TUMEPATIKANA katia Ibada hiyo ndipo, akahitimisha kwa kuzungumzia habari ya Hija Halisi ambayo itafanyika Disemba 31, 2023, ambayo kwa Kalenda inayofuatwa na Kanisa Halisi itakuwa ni Jumapili, 26 Thebeti 1 Majira Halisi.

"Mimi siyo kichaa, ninapoisisitiza kila mtu asiikose Hija hii ninamaanisha. Pale tunaenda kushukuru Utimilifu wa Matahayo 21:43, katika ule Yesu zaidi ya miaka 2000 baada ya Wayahudi kumkataa alisema Ufalme utahama kutoka Mashariki ya Kati kwenda Taifa lingine ambalo kwa wakati ule hakulitaja. Sasa baada ya Sauti kusikika  mara nne Kigoma, tunaenda kushukuru kujua kumbe Taifa lenyewe ni Tanzania. Na siyo tu kushukuru bali pia tunaenda kupokea Utajiri na  Baraka za CHANZO HALISI ", akasisisitiza Baba Halisi.

Ibada kama hiyo ya Hija ambayo hufanyika kila mwaka tangu Kanisa Halisi lilipoasisiwa hapa nchini tariban miaka sita sasa, ilifanyika Kigoma mjini, Januari 29, 2023 sawa na 26 Thebeti 1Majira Halisi, na kuhudhuriwa na maelfu ya mahujaji kutoka ndani na nje ya Tanzania, Mgeni Rasmi akiwa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma-Ujiji Fredinand Filimbi ambaye alimuwakilisha Mkuu wa mkoa wa Kigoma.

Baadhi ya Mahujaji wa Hija hiyo walitoka mikoa yote ya Tanzania Bara, Zanzibar, Marekani, Kenya, Uganda, Zambia, Rwanda, Burundi, Malawi na Msumbiji na kushiriki hatua kwa hatua Ibada hiyo mwanzo hadi mwisho, huku wote wakionyesha kuwa wachangamfu tena wenye furaha.

Ibada ya mwaka huu (kwa Kalenda ya Majira Halisi kabla ya Uharibifu) itakuwa ni ya sita (6), na inatarajiwa kuwa ya 'kukata na shoka' kwa sababu, mbali na mahujaji ambao ni Uzao Halisi lakini pia wanatarajiwa kushiriki Wazee zaidi ya 40 wakiwemo wa kutoka Baraza la Wazee mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mwenyekiti wa baraza hilo Mzee Mohamed Mtulia na  Wazee kutoka mkoa wa Njombe. 

Tazama picha za Ibada ya 'Waabuduo Halisi tumepatikana'.👇

Baba Halisi, Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi la MUNGU BABA akiachilia somo la'Waabuduo Halisi tumepatikana' karika Ibada iliyofanyika Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta Namanga jijini Dar es Salaam, 12 Thebeti, 1 Majira HalisiI (Jumapili Disemba 17, 2023). 

Mwazo

Baba Halisi akiwasili. Kulia ni 'Mtekeleza Sauti' kutoka Star Tv akimkaribisha Baba Halisi wakati akianzisha matangazo Mubashara ya Ibada hiyo iliyoeanda kwa somo la 'Waabuduo Halisi tumepatikana'.
Moja Halisi akiamkaribisha Baba Halisi wakati akiondoka Utajirishoni.
Baba Halisi akiwa tayari utajirishoni huku akionesha kuwa mwenye furaha tele.
'Mtekeleza Sauti' kutoka Star Tv akimualika Baba Halisi kuanza kuongoza Ibada hiyo.
Baba Halisi akianza kuongoza Ibada hiyo kwa kuongoza Shukurani. Kulia ni Mnara Mmoja Halisi na Udhihirisho Halisi wakipokea Shukurani hiyo.
Baadhi ya Watekeleza Sauti na Uzao Halisi wakiwa kwenye Ibada hiyo. Kulia ni Mtekeleza Sauti kutoka Vingunguti Thebeti Halisi.
Baadhi ya Watekeleza Sauti na Uzao Halisi wakiwa kwenye Ibada hiyo.
Baadhi ya Watekeleza Sauti na Uzao Halisi wakiwa kwenye Ibada hiyo.
Baadhi ya Watekeleza Sauti na Uzao Halisi wakiwa kwenye Ibada hiyo.
Baba Halisi akiomba nyimbo mbili zipigwe kabla ya kuendelea kuongoza Ibada hiyo.
Mwimbaji akiongoza kuimba wimbo kama alivyoomba Baba Halisi.
Wacharaza gitaa wakikoleza wimbo huo.
Baba Halisi akifuatilia wakati wimbo aliotaka ukipigwa.
Mwimbaji Uelewa wa Sauti ambaye amejiunga na hivi karibu na Bendi ya Kanisa Halisi akiimba wimbo wa pili wa Hija Halisi Kigoma.
Watekeleza sauti na uzao wakicheza wimbo huo.
Uelewa wa Sauti akikoleza wimbo huo.
Uelewa wa Sauti (Kushoto) kiongoza kucheza wimbo huo.
Uzao wakicheza wimbo huo.
Baba Halisi akiruka kuucheza wimo huo.
Mama Halisi akicheza wimbo huo pamoja na Mnara Mmoja Halisi na Udhihirisho Halisi.
Mama Halisi, Mnana Mmoja Halisi na Udhihirisho Halisi wakifurahia wimbo huo.
Kisha Baba Halisi akabariki Maji kuwa Damu Safi ya Chanzo Halisi kuyaongozea Ibada hiyo.
Mama Halisi, Moja Halisi, Kanisa wa Uzao Halisi na Kanisa wa Fahari Halisi wakiwa na maji wakati Baba Halisi akiyageuza kuwa Damu safi nyeupe ya Chanzo Halisi.
Akiwaonyesha Uzao Damu safi ya Chanzo Halisi baada ya kuyabariki.
Akayanywa.
'Mtekeleza Sauti' kutoka Star Tv naye akanywa aliyokuwanayo.
Baba Halisi akinyunyiza Damu safi nyeupe kuzunguka Utajirisho.
Mama Halisi akigawa Maji kwa uzao baada ya kuelekezwa na Baba Halisi.
Mama Halisi akigawa Maji kwa uzao baada ya kuelekezwa na Baba Halisi.
Moja Halisi akigawa Maji kwa uzao baada ya kuelekezwa na Baba Halisi.
Moja Halisi akisoma Kitabu kufafanua kwa nini Baba Halisi anasema 'Waabuduo Halisi tumepatikana'. walikuwa hawakuweza kupatikana nyakati zilizopita.
Moja Halisi akisoma Kitabu kufafanua kwa nini sasa Baba Halisi anasema 'Waabuduo Halisi tumepatikana'.
Baba Halisi akieleza Waabuduo Halisiwamepatikanaje sasa.
Watekeleza Sauti wakipanga kreti za soda kabla ya kugawa soda Uzao na kila aliyekuwepo apewe kwa ajili ya kunywa kusherehekea 'Waabuduo Halisi tumepatikana'.
Uzao wakijipanga kupokea soda mmoja baada ya mwingine, huku wakitoa matunda.
Baba Halisi akiwa ametulia wakati ugawaji soda ukiendelea.
Fahari Halisi na Kanisa wake wakiwa wametulia wakati ugawaji soda ukiendelea.
Mama Halis, Mnara Mmoja Halisi na Udhihirisho Halisi wakiwa wametulia wakati ugawaji soda ukiendelea.
Uzao wakiendelea kutoa matunda.
Baba Halisi akiongoza shukurani baada ya ugawaji wa soda.
Wakipokea shukurani.
Wakipokea shukurani.
Wakipokea shukurani. Wapili kushoto Dk. Yatosha kutoka Dawati la Polisi la Usalama na Amani katika Jamii.
Baba Halisi akihitimisha Ibada kwa kunyunyiza damu safi nyeupe ya Chanzo Halisi.
Moja Halisi akibarikia Kichanga.
Baba Halisi akikituza noti kichanga hicho.
Faida Halisi na Moja Halisi wakisimamia wakati Uzao wakijiandikisha kwenye dawati la Hija ili kwenda Hija Halisi Kigoma.
Mwimbaji akiimba wimbo wa Hija.
Baba Halisi akieleza umhimu wa Hija, na kuwamihiza Uzao kuhakikisha kila mmoja hakosi kwenda Hija hiyo ya mwaka huu.
Mwimbaji akiongoza wimbo wa Hija.
Mama Halisi, Mnara Mmoja Halisi na Udhihirisho Halisi akifurahia wimbo huo.
Baba Halisi akiendelea na hatua za mwisho za Ibada hiyo.
Baba Halisi akiwatakia heri uzao waliokuwa Ibadani na waliokuwa wakifuatilia Ibada hiyo katika Luninga na mitandao ya Kijamii.
Baba Halisi akiondoka Baada ya kuhitimisha Ibada hiyo.
Mnara Mmoja Halisi akafuatia kuondoka.

Udhihirisho Halisi akafuatia kuondoka.

Picha za ziada👇

Fulana za 'Bila Chanzo Hutoboi' kuimarisha Ibada ni Uzalishaji. Kulia ni Mwimbaji uelewa wa Sauti ambaye ametoa Albamu yenye maneno hayo.
Mtekeleza sauti wa Uzalishaji (kushoto) akizungumza na 'Mtekeleza Sauti kutoka Star Tv.

Uzao Halisi akipendeza ndani ya fulana la 'Bila Chanzo Halisi Hutoboi'.

Burunge WMA, kushirikiana kulinda Shoroba

$
0
0

Mwandishi Wetu, Mugumu 

 

Wajumbe wa Hifadhi ya Jamii ya Burunge WMAs ya Wilaya ya Babati,mkoa wa Manyara  wamekubaliana kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri na serikali   kusimamia masuala ya uhifadhi ikiwemo ulinzi wa Shoroba.

Uamzi huo umefikiwa leo Jumatatu Desemba 18,2023 katika kikao cha pamoja kwenye ukumbi wa Kampango Hotel Mugumu Serengeti,ikiwa ni sehemu ya ziara ya viongozi hao, kutembelea jumuiya ya hifadhi ya jamii ya Ikona, kujifunza  jinsi ya kukabiliana na  migogoro baina   ya wanyamapori na binaadamu.

 

Viongozi wa Burunge WMA wakiwepo Wajumbe wa kamati ya uongozi(AA), wajumbe wa Bodi na viongozi wa halmashauri ya Babati na idara ya wanyamapori mkoa Manyara,wanafanya ziara ya mafunzo Ikona WMA, ziara ambayo inafadhiliwa na taasisi ya chemchem Association, ambayo imewekeza shughuli za uhifadhi  na Utalii katika eneo hilo,

 

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Anna Mbogo amesema,ili kuhakikisha ziara ya viongozi hao wa Burunge WMAinayoundwa na vijiji kumi inazaa matunda wanatakiwa kushirikiana.

 

“Uendelevu wa Hifadhi hii ni kushikamana kwa ajili ya ulinzi wa shoroba na kuwadhibiti wale wavamizi na wanaotaka kutukwamisha lakini pia kuwadhibiti baadhi ya ambao watataka kuwahujumu tena”alisema.

 

Alisema Rais wa Jamuhuri ya Muungano, Dk Samia Suhulu Hassan anafanyakazi kubwa ya kutangaza Utalii ambayo imekuwa na manufaa makubwa hivyo, Burunge WMA ni lazima kuunga mkono jitihada za Rais kuvutia watalii lakini pia kuongeza mapato,kutokana na Utalii.

 

Afisa Wanyamapori mkoa wa Manyara,Felix Mwasenga na Afisa Wanyamapori halmashauri ya wilaya ya Babati, Christopher Laizer walieleza eneo la Burunge WMA ni muhimu sana katika utalii na Uhifadhi nchini ni lazima lilindwe lakini pia kuwa na mikakati na kuongeza mapato.

 

Mwenyekiti  wa Burunge WMA,Erick Lilayoni alisema viongozi wote wa hifadhi hiyo, wamekubaliana kuondoa tofauti zao na tofauti zilizokuwepo na serikali na sasa wanashirikiana na mwekezaji wao chemchem ili kuendeleza uhifadhi na Utalii.

 

“Mkurugenzi wa halmashauri tunaomba radhi kwa yote yaliyotokea nyuma , tulitumika vibaya na kutaka kuyumbisha WMA lakini sasa tupo kitu kimoja na tunataka maendeleo”alisema.

 

Mjumbe wa bodi wa Burunge WMA,Lebrice Makau na Elibariki Lawasara waliomba radhi kwa serikali na halmashauri ya Babati kwani kwa miaka miwili walikuwa katika mgogoro baada ya kupotoshwa na hivyo, kushindwa kupokea ushauri ya wataalam.

 

Lawasara alisema wanamuomba radhi Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Mkuu wa wilaya Lazaro Twange na wataalam wote wa halmashauri na serikali kwa kupuuza ushauri wao kwa miaka miwili kwani walikuwa wamepotoshwa kwa maslahi ya wachache na sasa wamevunja makundi na wamekubaliana kushirikiana na serikali katika uhifadhi na kufata sheria zote.


Dkt. Kikwete akipongeza NIT kuanzisha Kozi ya Urubani

$
0
0
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekipongeza Chuo Cha Taifa ca Usafirishaji (NIT) katika Mpango wao wa kuanza kufundisha Marubani wa  Ndege, akibainisha hatua hiyo itasaidia kuongeza watenda kazi katika sekta  ya anga kwani ina uhaba mkubwa wa rasilimali watu.
 Akizungumza katika Mahafali ya 39 ya NIT, Jakaya amesema kuwa ni ghali  kwa kusomesha marubani nje ya nchi.

"Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imenunua ndege mbili kwa ajili ya mafunzo ya urubani, Injini mbili kwaajili ya mafunzo ya uhandisi wa ndege na Cabin Crew mock ups kwa ajili ya mafunzo ya wahudumu wa ndani ya ndege," alisema Rais Mstaafu.

Ameongezea: "Aidha, Serikali imetoa ardhi katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) lenye ukubwa wa hekta 60, ambalo litatumika katika kutoa Mafunzo ya Taaluma za Usafiri wa Anga. Nimefurahi sana kuona uwekezaji huu mkubwa na muhimu kwa Chuo chetu, hivyo, nitoe wito kwa Chuo, vifaa hivi ambavyo Serikali imenunua kwa gharama kubwa vitunzwe ili Watanzania wengi wanufaike katika kupata mafunzo."
Vilevile, JK aliwapongeza waitimu: 

"Napenda kuwapongeza sana nyote kwa jitihada mlizofanya wakati wote wa masomo yenu hadi kufikia hatua hii ya kutunukiwa vyeti leo hii. Hongereni sana. Ninatambua kuwa tuzo mtakayopata leo ni ya msingi kwenu katika safari ndefu ya kuwa wataalam wazuri na mahiri. Ushauri wangu kwenu msiridhike na ngazi ya taaluma mliyofikia, endeleeni kutafuta maarifa zaidi ili Taifa liwe na wataalam wa kutosha na wenye sifa zote zinazohitajika katika sekta ya Uchukuzi na Usafirishaji. "
Kwa Wanafunzi Mnaoendelea na Masomo, alisema:

"Katika zama hizi ambapo kuna mabadiliko makubwa ya teknolojia hasa dunia inapoingia kwenye Mapinduzi ya Nne ya Viwanda (4th Industrial Revolution), ubunifu ni jambo muhimu  kwa Nchi yetu katika kujenga uchumi imara na stamihilivu. Hivyo, Wanafunzi mnaoendelea na masomo kuweni wabunifu na kusoma kwa bidii ili mtakapohitimu masomo yenu muweze kuwa na maarifa na ujuzi wa kutosha. "

Alisema kuwa amefarijika sana kusikia kwamba Chuo kimeendelea kutanua wigo wa kutoa mafunzo katika sekta hii muhimu ya Uchukuzi, ikiwa ni pamoja na kujiimarisha katika Njia zote za Usafirishaji yaani Usafiri wa Anga, Majini, Reli, Barabara na usafiri kwa njia ya mabomba.

"Nimefarijika kusikia kuwa Chuo kikombioni kuanza kutoa Mafunzo ya Urubani. Mafunzo haya ni muhimu sana kwa Taifa letu kwani yatapunguza mzigo kwa Serikali na Wazazi wa kugharamia mafunzo haya nje ya nchi ambayo hutolewa kwa gharama kubwa, " alisema.

Vilevile, Jakaya alipata wasaa wa kuzindua Kitabu ambacho kimeeleza historia ya Chuo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1975 hadi kilipofika hapa.

"Nimefurahi kuona sasa historia ya Chuo chetu imetunzwa vema kwani inatusaidia kujua tulikotoka, tulipo sasa na wapi tuanataka kufika. Aidha, kitabu hiki kinatunza historia ya Chuo kwa faida yetu, vizavi vijavyo na kwa kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu, " alisema.

Nae, Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile alisema kuwa Katika kutekeleza wajibu wetu wa kusimamia Chuo, Wizara imefanikiwa kusimamia uboreshaji wa miundombinu na mazingira ya kufundishia na kujifunzia; uboreshaji wa mafunzo yanayotolewa na Chuo; pamoja na kuimarisha rasilimali watu ya Chuo.

Usimamizi huu unalenga kukiwezesha Chuo kufikia malengo ya uanzishwaji wake, ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa kama yalivyoainishwa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2025.

"Chuo chetu kinatambua mapinduzi anuai ambayo Serikali ya Awamu ya Sita (6) imeendelea kuyafanya kwa kuanzisha miradi mbalimbali katika sekta ya Uchukuzi ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa Mipango mbalimbali ya nchi ikiwemo Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo, Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025, Sera ya Taifa ya Uchukuzi ya mwaka 2003, pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020," alisema.

Amsisitiza kuwa baadhi ya miradi hiyo ni ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), Ununuzi wa Mabehewa na Injini za treni za kisasa, ujenzi wa Meli, upanuzi wa Bandari, ujenzi na upanuzi wa Viwanja vya Ndege, ununuzi wa Ndege,, ujenzi na upanuzi wa barabara pamoja na ujenzi wa Bomba la Mafuta Gafi kutoka Hoima, Uganda kwenda Tanga, Tanzania.

"Mapinduzi haya yameongeza mahitaji ya Rasilimali Watu yenye weledi wa hali ya juu katika Sekta ya Uchukuzi nchini na ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika," alisema.

Naibu Waziri ametanabaisha "Hii inakifanya Chuo kubuni na kutoa mafunzo yanayoendana na mahitaji ya soko ili kutoa wahitimu bora katika nyanja zote za Usafirishaji (Barabara, Reli, Anga, Maji na Bomba). Hivyo basi, katika Mpango Mkakati wa Nne wa Chuo wa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026), Chuo kitaendelea kuimarisha utoaji wa mafunzo yanayolenga kuzalisha wataalam wenye ujuzi katika sekta ndogo  zote tano za usafirishaji kwa ajili ya ukuaji endelevu wa miradi hii ambayo itachochea kwa kasi ukuaji wa Uchumi wa nchi yetu."

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Chuo Dr Zainabu Mshana amesema kuwa Chuo kimeendelea kuwajengea uwezo wahadhiri na watumishi wake kwa kuwapeleka masomoni ili kuimarisha kiwango cha maarifa na ujuzi wao ambapo katika mwaka wa masomo 2023/2024 jumla ya watumishi 71 wapo masomoni.

Amesema kuwa kati ya hao, watumishi 39 wanasoma ngazi ya shahada ya uzamivu (PhD), 24 wanasoma shahada ya uzamili, mtumishi mmoja (1) anasoma shahada ya kwanza, Watumishi watatu (3) wanasoma Mafunzo ya Urubani  na Watumishi wanne (4) wanasoma Mafunzo ya Leseni ya Matengenezo ya Ndege.

Vilevile, aliongezea kuwa katika kuimarisha na kurahisisha utendaji kazi, Chuo kimefanikiwa kuhuisha muundo wake wa utumishi, ambao uliidhinishwa na Mheshimiwa Rais tarehe 17 Novemba 2022  na umeanza kutekelezwa Mwezi Oktoba 2023.

"Kwa upande wa taaluma, Muundo huu una Vitivo vitano (5), Kurugenzi mbili (2), Idara 14, Vitengo sita (6) na Vituo vinne (4). Kwa upande wa Utawala, Muundo una Kurugenzi (5) na Vitengo vinne (4), "alisema.

Ameongeza kuwa chuo hicho kimefanikiwa kufanya maboresho ya Muundo wake wa Utumishi kwa kuongeza kada za wakufunzi wa usafiri wa anga na wahandisi wa matengenezo ya ndege ili kuendena na matakwa ya sekta ya usafiri wa anga. Muundo huu umeanza kutekelezwa mwezi Oktoba 2023.

Pamoja na hayo, Chuo kimefanikiwa kuidhinishiwa Muundo wa motisha ili kuboresha maslahi ya watumishi na kuongeza ufanisi wa kazi katika shughuli mbalimbali za Chuo. Muundo huu umeanza kutekelezwa mwezi Julai 2023.

"Chuo kina mikakati endelevu ya kutayarisha Rasilimali Watu watakaokidhi mahitaji ya soko la ajira kwenye sekta ya Uchukuzi na Usafirishaji hasa kwa kuzingatia utekelezaji wa mageuzi makubwa ya kiuchumi ambayo Serikali ya Awamu ya sita (6) inayafanya, " alisema.

Alitaja Mikakati hiyo ni Kuanzisha na kuhuisha mitaala ya kozi za mafunzo mbalimbali kuanzia ngazi ya stashahada hadi shahada ya uzamili kuendana na mahitaji ya soko la ndani na la nje ya nchi.

Na vilevile kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia ikiwa ni pamoja na ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya madarasa, karakana, maabara, ofisi  na ununuzi wa vifaa vya mafunzo vinavyoendana na mabadiliko ya teknolojia duniani.

FCS YATOA TATHIMINI YA MWAKA MMOJA UTEKELEZAJI MRADI WA 'URAIA WETU'

$
0
0

Msimamizi wa Mradi wa 'Uraia Wetu' Nicholas Lekule akitoa tathimini juu ya Mradi huo, katika semina ya Wahariri na Waandishi wa Habari iliyofanyika leo Disemba 18,2023 Jijini Dar es Salaam.

Msimamizi wa Mradi wa 'Uraia Wetu' Nicholas Lekule akizungumza kwenye Mahojiano na waandishi wa Habari mara baada ya kumalizika kwa semina hiyo, Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa MTWANGO NET Fidea Ruanda, akitoa wasilisho juu ya tathimini ya Mradi huo katika semina hiyo Jijini Dar es Salaam.

 

DAR ES SALAAM 

Foundation For Civil Society (FCS), kupitia mradi wake wa 'Uraia Wetu' imeendelea kuweka nia ya kuchangia, kuboresha, na kuwezesha mfumo wa sera na mazingira ya ushirikishwaji wa wananchi ili kukuza utawala wa Demokrasia nchini.

Malengo makubwa ya Mradi huo ni kukuza uhuru wa kujieleza, kupata habari, uhuru wa kukusanyika na kubaini fursa na nafasi iliyopo kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika masuala ya kiraia.


Hayo yamebainishwa na Msimamizi wa Mradi wa 'Uraia Wetu' Nicholas Lekule, alipokuwa akitoa tathimini juu ya Mradi huo katika semina ya Wahariri na Waandishi wa Habari iliyofanyika leo Disemba 18,2023 Jijini Dar es Salaam.

"Lengo la mradi huu wa miaka mitatu, ni kuwa asasi za kiraia ambazo zimeratibiwa vizuri kuanzia katika masuala ya kisheria, kisera na utekelezaji, ili kazi zinazofanywa ziwe na ufanisi mzuri"amesema Lekule.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa MTWANGO NET Fidea Ruanda, ameishukuru FCS kwa kutoa ruzuku ya kutekeleza Mradi huo wanaotekeleza kwa miaka mitatu katika mikoa saba ikiwemo Songwe, Ruvuma, Iringa, Njombe, Mbeya, Mtwara, Rukwa, ambapo wanasimamia Kanda ya kusini na kwamba unaolenga kuwajengea uwezo vijana, wanawake, na walemavu.


"Uwelewa mdogo kuhusu sera, sheria na miongozo mbalimbali ikiwemo kulipa ada kwa mashirika machanga bado ni changamoto licha ya kuwa malipo ni shilingi 50,000 kwa mwaka kwani usipolipa hadi kufikia mwezi wa April mwaka unaofuata unapigwa faini asilimia 100 ambapo ni sawa na shilingi 100,000" amesema Fidea.


WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA BANDA LA TANZANIA COMMERCIAL BANK MIAKA 50 CHUO CHA USTAWI WA JAMII DAR

$
0
0



Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Tanzania Commercial Bank, alipotembelea Banda la Taasisi hiyo katika kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Ustawi wa Jamii, yaliyofanyika Disemba 18,2023 Jijini Dar es Salaam.


Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa  (wa pili kulia), akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Tanzania Commercial Bank Tawi la Kariakoo Bw. Faraji Basso, (kushoto) wakati Waziri Mkuu alipotembelea Banda la Taasisi hiyo, kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Ustawi wa Jamii, yaliyofanyika Disemba 18,2023 Jijini Dar es Salaam.

 

DAR ES SALAAM 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kukua kiuchumi kwa kuchangamkia fursa za mikopo zinazotolewa na Taasisi za fedha zikiwemo Benki.


Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo alipotembelea Banda la Tanzania Commercial Bank katika kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Ustawi wa Jamii, na Wiki ya Ustawi wa Jamii, iliyoenda sambamba na uzinduzi wa vipindi vya Malezi, Makuzi na maadili kwa vijana, iliyofanyika Disemba 19,2023 kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha  Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.


Aidha, Mheshimiwa Majaliwa alisema kutokana na changamoto za kiuchumi familia nyingi zinashindwa kupata muda wa kutosha kulea watoto na vijana ambao ni muhimu katika ujenzi wa Taifa la sasa na baadaye, hivyo mada hiyo ni kengele ya amshaamsha kwa kila mtendaji na mwanajamii kutambua kuwa suala la malezi na makuzi ya watoto na vijana ni msingi wa maendeleo ya Taifa letu.


Katika tukio hilo, Tanzania Commercial Bank walishiriki wakiwa ni wadhamini wa maadhimisho hayo.

Hatua hiyo ni katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya kuhakikisha makundi mbalimbali ya kijamii yanaendelea kunufaika kiuchumi, nakwamba Tanzania Commercial Bank imeendelea kuwa mdau mkubwa kwa kuweka mazingira wezeshi yakiwamo huduma za mikopo itakayosaidia kuchochea maendeleo ya wanawake, makundi mbalimbali na watanzania wote nchini.

Magazeti ya Tanzania leo Disemba 20, 2023

WAARABU WAONANA NA ONANA BENJAMIN MKAPA.

$
0
0

 

Na John Marwa


Hatimaye wekundu wa Msimbazi Simba wamerejea kwenye gia ya ushindi kwenye michezo ya Kimataifa baada ya kuichapa Wydad Casablanca ya  Morocco  mabao 2-0.


Ni ushindi wa kibabe kwa Mnyama Simba kwenye Dimba la Benjamin Mkapa jioni ya leo kupitia Willy Essomba Onana ambaye ameweka kambani mabao yote mawili katika kipindi cha kwanza.


Kipindi cha pili Kocha Mkuu wa Simba Abdulhak Benchika aliamua kupaki basi na kuwasubiri Wydad kuwafungua jambo ambalo halijawezekana mpaka filimbi ya mwisho ya mchezo huo.



Kwa ushindi huo Simba wamefikisha pointi tano nyuma ya vinara Asec Mimosas ya Ivory Coast wenye pointi saba huku usiku huu wakiwa nyumbani kuwakabili Jwaneng Galaxy ya Botswana.


Kipigo hicho kwa Wydad kinawafanya kubuluza mkia wakiwa na alama tatu nyuma ya Jwaneng Galaxy nafasi ya tatu na alama zao nne.


Mnyama Simba atarejea dimbani mwakani kuwafuata Asec Mimosas kabla ya kuja kumalizana na  Jwaneng Galaxy Benjamin Mkapa ambapo mwezi wa pili 2024.


Ni ushindi wa kwanza kwa Kocha Bennchika tangu achukue mikoba ya kukinoa kikosi cha wekundu wa Msimbazi Simba katika michuano ya kimataifa huku ukiwa wa kwanza pia kwa Mnyama Simba msimu huu akiwa amecheza mechi nane sare sita, kipigo kimoja na ushindi moja.

BURUNGE WMA wapata tiba kupunguza mgogoro wanyamapori na Binaadamu

$
0
0

Mwandishi Wetu, Maipac

Viongozi wa Hifadhi ya jamii ya wanyamapori  ya Burunge ,pamoja na viongozi wa halmashauri ya Babati,wamejifunza Mbinu ya Kisasa ya kutumia waya wa umeme kuzuia wanyamapori wakali kama Tembo na Simba kuleta madhara kwa binaadamu.

Viongozi wa hao Burunge WMA wakiwepo Wajumbe wa kamati ya uongozi (AA)wajumbe wa Bodi na viongozi wa halmashauri ya Babati na idara ya wanyamapori Mkoa Manyara,wamefanya ziara ya  mafunzo ya siku mbili Ikona WMA kwa ufadhili  wa Taasisi ya Chemchem Association, ambayo imewekeza shughuli za uhifadhi  na Utalii katika eneo hilo n kupata fursa kujifunza.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Babati Anna Mbogo ambaye aliongozana na viongozi hao kwa ajili ya kujifunza namna ya kudhibiti wanyamapori waharibifu amesema, “nimevutiwa na njia hii ya kisasa inayolinda mazingira”amesema na kuongeza,

“Niitakaa pamoja na wataalamu wilayani Babati kutathimini gharama za kuweka uzio huo wa umeme ili kulinda ushoroba katika Hifadhi ya Burunge WMA ambao ni sehemu muhimu ya Ikolojia ya eneo hilo na kuwanusuru wananchi na madhara yanayosababishwa na wanyamapori wakali”amesema.

Katibu wa Ikona WMA Yusuph Manyanda amesema, licha ya  kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo Pilipili,doria ,Elimu na Ulinzi shirikishi kutoka katika makundi ndani ya jamii ili kupambana na wanyama vamizi na kusababisha madhara kwa wananchi lakini matumizi ya fensi ya umeme imekuwa na faida zaidi.

“Uwepo wa uzio huo uliojengwa na Kampuni ya Grumeti Fund umekuwa na matokeo chanya kwa hifadhi na wakazi kwa kuwa umezuia muingiliano, hali iliyopelekea wakazi wa eneo hilo kuanza tena shughuli za kilimo walizokuwa wameziacha kwa muda mrefu kwa hofu ya kuharibiwa mazao yao”amesema.

Emmanuela Galu Mjumbe wa Burunge WMA amesema, “jukumu limebaki kwetu kutoa elimu kwa wafugaji na wakulima waweze kufahamu njia mbalimbali za kudhibiti wanyamapori waharibifu ikiwemo njia ya kuwazuia kisasa bila kutumia nguvu kubwa”amesema.

Felix Mwasenga Afisa Wanyamapori Mkoa wa Manyara amewashukuru Taasisi ya Chem chem iliyowekeza Burunge WMA kwa kuwezesha ziara hiyo ya mafunzo imewasaidia kupata ujuzi utakaosaidia jamii ya Manyara kupunguza migogoro baina yao na wanyamapori.

Meneja wa Chem chem association, Clever Zulu amesema ziara hiyo imekuwa na mafanikio makubwa.

Amesema pamoja na kupata mbinu za kisasa kulinda shoroba wamejifunza pia kutumia uzio wa umeme kudhibiti migogoro ya wanyamapori na Binaadamu.

"Naamini viongozi wetu wa Burunge WMA,Viongozi wa halmashauri Babati na mkoa Manyara watakwenda kuona njia bora ya kumaliza kabisa tatizo la migogoro ya wanyama na wananchi lakini kutunza shoroba"amesema.

Mwenyekiti wa Burunge WMA,Erick Lilayoni alipongeza Chemchem kudhamini mafunzo hayo lakini pia Ikona WMA kuwapa elimu nzuri.

"Tumejifunza mengi tutakwenda kuyatekeleza Burunge WMA ilo wananchi waendelee kunufaika na uhifadhi na Utalii lakini pia kuongeza mapato na kutatua migogoro.


Wafanyakazi NMB watoa Mil. 11.5/- kusaidia gharama za matibabu ya watoto JKCI

$
0
0
Kaimu Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 11.5, Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dk. Delila Kimambo (kulia), msaada huo umetolewa na wafanyakazi wa Idara ya Wateja Wadogo na Biashara ya benki hiyo kwa ajili ya kusaidia gharama za matibabu ya Watoto wenye uhitaji wanaotibiwa katika taasisi hiyo. (Na Mpiga Picha Wetu).

Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dk. Delila Kimambo (kushoto), akitoa maelezo kwa wafanyakazi wa Idara ya Wateja Wadogo na Biashara wa benki ya NMB walipofika kutoa mchango wao wa Sh. 11.5 za kusaidia gharama za matibabu ya Watoto wenye uhitaji wanaotibiwa katika taasisi hiyo. (Na Mpiga Picha Wetu).
Kaimu Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite (kulia), akikabidhi sehemu ya msaada wa vifaa tiba kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Dk. Yona Kabata (kushoto) vilivyotokana na michango ya wafanyakazi wa Idara ya Wateja Wadogo na Biashara ya benki hiyo. Wa pili kushoto ni Muuguzi wa hospitali hiyo, Flora Mchaina, Meneja Mikopo ya Nyumba Benki ya NMB, Miranda Lutege (wa pili kulia) na Meneja Mahusiano Mwandamizi NMB, Pendo Massawe (katikati). (Na Mpiga Picha Wetu).



NA MWANDISHI WETU

 

WAFANYAKAZI wa Idara ya Wateja Wadogo na Biashara ya Benki ya NMB, wameikabidhi Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ya Dar es Salaam, kiasi cha Sh. Mil. 11.5 kusaidia kulipia gharama za matibabu ya watoto wenye uhitaji wanaotibiwa hapo, huku wakitoa vifaa tiba vyenye thamani ya Sh. Mil. 1.7 kwa Wodi ya Watoto ya Hospital ya Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani.

 

Kwa nyakati tofauti Jumanne ya Desemba 19, Kaimu Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa NMB, Bw. Ally Ngingite, alikabidhi kwa niaba ya wafanyakazi hao, hundi ya mfano ya kiasi hicho kwa Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi JKCI, Dk. Robert Aloyce na vifaa tiba hivyo kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Dk. Yonna John Kabata.

 

Akizungumza wakati wa hafla ya jijini Dar es Salaam, Ngingite, alibainisha kuwa kiasi walichotoa kimetokana na michango ya wafanyakazi wa Idara hiyo na nyongeza kutoka benki yake, lengo likiwa ni kugusa maisha ya wenye uhitaji katika jamii, ambapo hufanya hivyo kila mwisho mwaka kupitia idara mbalimbali na Ofisi za Matawi yao kote nchini.

 

"Kwa niaba ya wafanyakazi wenzetu, tuko hapa kutoa kiasi cha shilingi 11,570,000 kilichotokana na michango ya mishahara yetu na nyongeza kutoka taasisi yetu, lengo likiwa ni kugusa maisha ya watoto wenye uhitaji wanaotibiwa hapa. Tunajua matatizo ni mengi na wenye uhitaji ni wengi, lakini tukaona tuje hapa kusaidia wachache kati yao.

 

"Tumaamimi kwa kiasi hiki tunachokabidhi, tutakuwa tumeyagusa na kuokoa maisha ya watoto walio katika 'stage' mbalimbali za matibabu hapa JKCI, ili waweze kufanyiwa upasuaji na baada ya hapo tunawaombea uponaji wa haraka kuwawezesha kuendelea na maisha yao ya kawaida.

 

"Hii yote ni kusapoti uwekezaji mkubwa ulilofanywa na Serikali katika Sekta ya Afya, tumepita idara mbalimbali kujionea hilo na sisi kama wadau tukajiona tunao wajibu na uwezo wa kuunga mkono hilo.

 

"Tumekuwa tukifanya hivi kila mwisho wa mwaka kwa wafanyakazi wa benki yetu kupitia Idara na Ofisi za Matawi kote nchini kujichanga mishahara yao na kuangalia maeneo ya kusaidia iwe kwa mayatima ama wagonjwa kama hivi," alibainisha Bw. Ngingite.

 

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi wa taasisi hiyo, Dk. Delila Kimambo, aliishukuru NMB kwa msaada waliotoa kwa watoto hao wanaotibiwa na taasisi yake na kwamba, kiasi hicho kinaenda kugusa pakubwa mioyo na maisha ya wanufaika miongoni mwa watoto wanaotibiwa hapo.

 

"Mlichofanya hapa ni jambo kubwa, mmewapa watoto hawa na wazazi ama walezi wao, mwisho mzuri wa mwaka, tayari kwa kuingia mwaka mpya na matumaini mapya.

 

"Kwa niaba ya watoto hawa, sisi JKCI tunawashukuru wafanyakazi wote na NMB kwa ujumla kwa kuisapoti Serikali ambayo imefanya uwekezaji mkubwa sana hapa unaopaswa kuungwa mkono na wadau wa afya kama hivi mlivyofanya nyie" alisema Dk. Delila.

 

Kwa niaba ya watoto wengine, Pili Khalfan wa Maneromango mkoani Pwani, ambaye ni mama mzazi wa mmoja wa watoto walionufaika, alisema msaada huo umekuja kwa wakati, kwani alielemewa na gharama za matibabu kiasi cha kukata tamaa, hasa baada ya kutengwa na ndugu pamoja na kukimbiwa na baba wa mtoto wake.

 

"Naishukuru sana NMB kwa kunipa aina hii ya msaada, ambao sikuutarajia na sitousahau maishani mwangu. Nimeteseka sana, sikuwa na msaada wowote, hata ndugu walinitenga, huku baba wa mtoto wangu naye akinikimbia.

 

"Nimekuwa napata wakati mgumu, kulala kwangu shida, kula yangu na mtoto ni shida. Aliwahi kutokea mfadhili wa kusaidia matibabu ya mtoto, lakini bima aliyokatiwa tukaambiwa ni ndogo, hivyo haitoshi kugharamia upasuaji wa moyo.

 

"Leo NMB inaenda kunifuta machozi mimi na mwanangu kusaidia gharama za matibabu yake. Naitakia mafanikio yaliyotukuka benki hii, ili iweze kuendelea kusaidia wenye uhitaji wengi zaidi," alisema Pili wakati akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wazazi na walezi wenzake.

 

Kutoka Kisarawe, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya hiyo, Dk. Yonna John Kabata, hakusita kuipongeza NMB kwa msaada wa vifaa tiba, ambavyo sio tu vitawasaidia watoto hospitalini hapo, bali pia utawapa wepesi katika kuhudumia makundi ya watoto wanaotakiwa kufanyiwa oparesheni (surgery cases) na wale wanaohitaji matibabu ya kawaida (treatment cases).

 

"Kwa niaba ya uongozi wa Hospitali na wagonjwa wote, nitumie nafasi hii kuwashukuru sana NMB kwa msaada huu wa vifaa tiba, ambavyo mnaweza kuona ni mdogo, ila niwahakikishie ni mkubwa na huenda ingetuchukua muda mrefu kuvipata.

 

"Hapa zipo baadhi ya huduma za bure kwa watoto, lakini wahitaji ni wengi, hivyo huongeza changamoto ya kuishiwa vifaa na mwingine kuvikosa. Hii isiwe mara ya mwisho, mtukimbilie kila mtapokuwa na fungu la kusaidia, itaokoa maisha ya wagonjwa wetu," alisema Dk. Kabata, mbele ya Muuguzi Mfawidhi, Sista Barikian Ngona na Muuguzi wa Wodi ya Watoto, Flora Mchaina.

 

Mwisho

Viewing all 19659 articles
Browse latest View live