Miaka 62 ya Uhuru wafungwa 2,244 wapata msamaha wa Rais
HANANG: HONGERENI MMETULETEA HII DAWA NI TIBA INAYOFANYA MAJI KUWA SAFI NA SALAMA-WANANCHI HANANG
Wananchi kutoka katika kata za Gendabi na Katesh Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara wameipongeza Serikali kwa kuweka jitihada za pamoja katika kuhakikisha wanapata maji safi na salama baada ya kuanza kutoa dawa ya kutibu maji bure nyumba kwa nyumba.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti nyumbani kwao mara baada ya kutembelewa na Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kutoa elimu namna ya utumiaji sahihi wa dawa za kutibu maji, baadhi ya wananchi hao akiwemo Innocent Ally wamesema dawa hiyo itawasaidia kutibu maji katika kuondoa vimelea vya magonjwa.
“Tunaishukuru serikali kwa dawa mliotuletea hii dawa ni tiba inayofanya maji kuwa safi na salama naishauri jamii hii ya Gendabi tutumie dawa hii inayotibu maji,namshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alisitisha ziara yake kuja hapa Hanang, Taifa limehamia Hanang Mungu azidi kuwainua katika kazi zenu” amesema Innocent.
Kwa upande wao Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii akiwemo Selestina Salwatt Mratibu wa Afya Ngazi ya Jamii Wilaya ya Hanang wamesema wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na uelewa jinsi ya kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo utumiaji sahihi wa dawa ya kutibu maji.
“Tunatoa elimu kwa jamii namna nzuri ya kutumia dawa ya kutibu maji katika kujikinga na magonjwa ya mlipuko na lita 20 ya maji unaweka vidonge viwili na lita 10 ya maji unaweka kidonge kimoja “ wamesema.
Mbunge Chadema atimiza agizo la Rais Samia

Na Lydia Lugakila, Bukoba
Mbunge wa viti maalum Mkoani Kagera kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Mhe, Conchesta Leonce Rwamlaza ametimiza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan la ugawaji wa mitungi ya gesi kwa Wanawake wa kata za Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba wanaokwenda kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa.
Akizungumza kabla ya zoezi la ugawaji wa mitungi ya gesi yenye matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia ipatayo 75 kwa akina Mama waliofika na kuwakilisha wenzao kutoka baadhi ya kata hizo ikiwemo kata ya Kyaitoke, Kyamulaile Katoma Nyakato na nyinginezo Mbunge Rwamlaza alimpongeza Rais Samia kwa namna alivyowaunga mkono wabunge wa Tanzania kuhusu matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia na kuwafanya wabunge hao kuwa waratibu wa ugawaji wa mitungi hiyo jambo litakalosaidia akina Mama hao kuondokana na madhara yanayoweza kutokana na kupika kwa kutumia kuni na mkaa.
Rwamlaza alisema yeye kama mbunge wa viti maalum kutoka Chadema anamuunga mkono Rais Samia kupitia mabadiliko ya Nchi kuongozwa na Mwanamke na kuwa ukiachana na itikadi za vyama Rais Samia amefanya jambo kubwa na la kihistoria.
"Rais Samia ni Mama mpambanaji nani asiyejua kuwa kawezesha miradi mingi na mikubwa hapa nchini tumeona katika sekta ya Elimu Barabara, afya na nyinginezo hivyo mimi siangalii mambo ya vyama ninachoangalia ni namna anavyowapigania wanyonge kama ambavyo amewainua Wanawake hawa", alisema Mbunge huyo.
Aliongeza kuwa huu ni muda wa akina Mama hao kupika kwa urahisi bila vikwazo kwani awali waliotumia kuni walihusishwa katika imani za kishirikina baada ya macho yao kuonekana mekundu huku akiwahimiza kuitumia mitungi hiyo kwa nia njema na si kuiuza kwani nia ya Rais Samia ni njema kwao.
Mitungi hiyo imegawiwa kidogo kutoka watu wawili wawili kila kata ili wawe mabalozi kwa wengine kutumia na kuchochea matumizi sahihi ya nishati safi na salama ya kupikia.
Naye Mgeni rasmi katika zoezi hilo ambaye ni mratibu wa miradi ya REA Wilaya ya Bukoba Bi Jamila Haroub Juma akitoa darasa na namna ya matumizi sahihi ya mitungi hiyo alisema mitungi hiyo imetolewa mahususi kuhamasisha kutumia nishati safi na salama ya kupikia na imetolewa na Wakala wa nishati Vijijini (REA) kwa kupata ruzuku kutoka Serikali kuu ambapo Rais Samia amewaondolea changamoto za kiafya zitokanazo na moshi kwani wengine ujikuta wanapata madhara kwenye mapafu, kifua kutokana na kuvuta hewa chafu.
Aidha Jamila aliwahimiza akina mama hao kutunza, kutumia na kuendeleza mitungi hiyo wala si kwa matumizi mengine kwani watakuwa wamekwenda tofauti na dhamira ya Serikali.
"Mnatakiwa kurudisha shukrani kwa kutumia nishati hii ili kuepukana na madhara yatokanayo na moshi utokanao na mkaa na kuni tumeona watu wakipata shida kwenye mapafu kutokana na kuvuta hewa chafu hivyo nimpongeze Rais Samia kuwezesha zoezi hilo ambalo litakuwa endelevu kwa Nchi nzima.
Hata hivyo akina Mama hao akiwemo Bi Winifrida Maxmilian wa kata Katoma, Hildagarda Ponsian wa kata Nyakato na Bi Ashura Jafari kutoka Kyaitoke Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba wamemshukuru Rais Samia kupitia mbunge huyo viti maalum Bi Rwamlaza na kuwa mradi huo utawasaidia kutunza Mazingira kwa kutokata miti ovyo kwa ajili ya kupata kuni na mkaa ambapo pia Rais Samia amewaweka katika maisha ya kati huku wakiahidi kutumia vyema mitungi hiyo.
Wanne wafariki katika ajali ya gari Kagera
Na Lydia Lugakila, Bukoba
Watu wanne wamefariki dunia huku wengine 21 wakijeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari lenye usajili namba T 339 DBV aina ya Hiace iliyokuwa ikitokea Izimbya Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba kuelekea Bukoba Mjini mkoani Kagera.
Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Blasius Chatanda,wakati akiongea na waandishi wa habari katika eneo la tukio na kusema kuwa ajali hiyo ilitokea majira saa tano na nusu asubuhi maeneo ya Kyetema katikati mwa Kata mbili za Kemendo na Bujugo Halmashauri ya Bukoba.
Kamanda Chatanda,alisema watu walipoteza maisha ni watu wazima watatu na mtoto moja huku kati ya majeruhi 21 watoto ni 4 watu wazima 17 ambao walikimbizwa katika hospitali ya Bujuna ngoma ambayo ni ya Wilaya hiyo.
Alisema kutokana hali ya majeruhi wengi kuwa mbaya wengine wamehamishiwa katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Kagera Bukoba kwa ajili ya kuendelea na matibabu zaidi.
Alisema chanzo cha ajali hiyo uchunguzi wa awali umebaini ni mwendo kasi dereva alipokuwa akishuka kwenye mteremko mkali aliweka gari free (Newtro )hivyo alishindwa kuirudisha kwenye mfumo wa gia na kugonga nguzo za umeme zilizokuwa kando ya barabara na pikipiki zilizokuwa kwenye maegesho ya barabara.
“Uzembe wa mtu mmoja unaweza kusababisha kesho waliopata ajali kupata elemavu wa kudumu na kuwa tegemezi katika familia au jamii “alisema Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera.
Hata hivyo kamanda wa Polisi Mkoani humo amewataka madereva wazingatie sheria za usalama barabarani wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto na wakiwa na abiria.
Aidha alisema kuwa hadi sasa haijafahamika kama dereva yuko hai au amefariki huku akidai kuwa ikithibitika yuko hai sheria itachukua mkondo wake.
Aliongeza kuwa waliofariki na majeruhi walio wengi bado hawajatambuliwa hivyo amewataka Wananchi kufika katika hospitali hizo kutambua ndugu zao.
Mshindi wa Bingwa kuondoka na gari aina ya Crown
SHINDANO la Bingwa Msimu wa pili linalokutanisha Watu maarufu wa kwenye mitandao ya kijamii, Washiriki wabaki 12 waliofika fainali mshindi wa bingwa kuongoka na zawadi ya gari, aina ya crown.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, Meneja Mradi wa shindano hilo Ombeni Phiri amesema bingwa ni zaidi ya burudani ambapo msimu wa pili mshindi kuondoka na gari aina ya crown pamoja na pesa taslim.
Msimu wa kwanza waliingia washiriki 18 ambao wengi wao ni vijana wenye ushawishi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii na mmoja wao aliibuka mshindi na gari aina ya crown pamoja na pesa taslim.
Hata hivyo ameeleza lengo la kuwepo kwa shindano hilo ni kuwapa fursa vijana Kujifunza vitu mbalimbali ikiwemo fursa zilizopo katika mitandao ya kijamii katika kukuza na kutengeneza majina (brand) yao.
Kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa ameeleza kuwa shindano hilo linasaidia kuwapa vijana ajira na kupata mitaji kupitia vipaji vyao.
Mshindi anakuwa balozi na anapewa taratibu jinsi ya kufanya biashara na kuweza kukuza na kujitamgaza.
Pia amesema Shindano hilo ni daraja la kufunguka kwa fursa nyingi kwani Hata usipofanikiwa kushinda unaweza kupata fursa ya kuwa balozi wa Makampuni.
Pia Malisa amewaambia watazamaji wa bingwa kulipia visimbuzi vyao kwani msimu wa pili una maudhui tofauti tofauti yenye kufunza ambapo hata watazamaji watapata elimu mbalimbali.
Kesi ya shambulio la mwili kunguru kesho
Na Mwandishi Wetu
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam inatarajia kuendelea kusikiliza kesi ya tuhuma za shambulio la mwili kesho inayomkabili mfanyakazi wa benki, Ibrahim Masahi ambae anatuhumiwa kumshambulia kwa nyundo jirani yake Deogratus Minja.
Aidha, inadaiwa kuwa Masahi alimshambulia kwa nyundo jirani yake huyo, baada ya Minja kwenda kumshitaki Serikali za Mitaa kwamba anatililisha maji mchafu katika eneo lake.
Kesi hiyo iliahirishwa mwishoni mwa wiki na Hakimu Mkazi, Amos Rweikiza, baada ya kutoa ahirisho fupi hadi jumatatu kwa sababu muda ulikuwa umeisha, kwa hiyo asingeweza kusikiliza ushahidi wa shahidi wa pili ambae ni askari polisi.
"Hivi sasa ni 10:30 jioni tunaweza kweli kwenda na muda huu, au tupange ahirisho fupi ili tuendelee na usikilizwaji, naahirisha kesi hadi Desemba 12,12, 2023 saa tano asubuhi na siku hiyo upande wa mashitaka uje na mashahidi wawili," amesema Hakimu Rweikiza
Kabla ya ahirisho hilo pande zote mbili zilidai kuwa wapo tayari kuendelea na usikilizwaji, lakini ilishindikana kwa sababu muda wa mahakama ulikuwa umekwisha na hiyo ilitokana na kwamba hakimu huyo alikuwa ana sikiliza ushahidi katika kesi zingine ambazo watuhumia wake wapo gerezani.
Awali, kesi hiyo iliahirishwa kwa sababu shahidi aliyetakiwa kutoa ushahidi wake, alikuwa anasimamia mitihani ya kidato cha nne inayoendelea nchi nzima.
"Kwenye orodha hapa shahidi aliyetakiwa kuwepo leo kwa ajili ya kuendelea kutoa ushahidi ni askari polisi mpelelezi, hajafika kwa sababu yupo anaesimamia mitihani ya kidato cha nne," amedai Jafari.
Masahi anatuhumiwa Januari 11, 2023 akiwa eneo la Mbezi Msakuzi ndani ya Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam alimpiga Deogratus Minja kwa nyundo na kumsababishia kupata madhara makubwa ya mwili mwake.
Katika ushahidi wake, Minja alidai kuwa tarehe hiyo saa mbili na nusu usiku alikuwa akipita nje ya geti la jirani yake Masahi, alimkuta kijana wa jirani huyo, baada ya kumuona alizungumza kwa kilugha kwa sauti kubwa ambae yeye hakuielewa.
"Ghafla kijana alikuja mbele yangu akanizuia nisipite, mara geti likafunguliwa akatoka Masahi akanihoji kwamba mimi ni kama nani na kwenda kumshitaki Serikali za Mitaa, sikumjibu chochote kijana wake akanipiga ngumi,"
"Nilimgeukia jirani yangu ili amuonye kijana wake, lakini na yeye aliinua shati lake akatoa nyundo akanipiga nayo kichwani baada ya kupata maumivu makali nilianza kukimbia huku nikipiga kelele za kuomba msaada,"alidai Minja.
Alidai kuwa, alianguka chini ndipo Masahi akaanza tena kumshambulia na nyundo mgongoni, maumivu yalipomzidi aligeuka, akampiga na nyundo kwenye mkono wa kulia na kwenye bega. Jirani mmoja alifungua geti na kumsaidia kwa sababu alikuwa ana kuja damu nyingi walimpeleka Hospitali ya Bochi kwa matibabu.
TRA PWANI YAMWAGA VIFAA KUBORESHA SEKTA YA AFYA HOSPITALI YA MKURANGA
NA VICTOR MASANGU, MKURANGA
Serikali ya Marekani yaunga Mkono Mradi wa Kutokomeza Ukeketaji
Dar es Salaam, TANZANIA
Ubalozi wa Marekani unafuraha ya kutangaza ushirikiano na WiLDAF katika harakati za kutokomeza ukeketaji. Kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Afrika (ARDF), Ubalozi unafadhili mradi wa miezi 18 wa WiLDAF uitwao ‘Kutokomeza Ukeketaji mkoani Mara-Jamii Imara’ utakaotekelezwa mkoani Mara. Mradi unalenga kuchangia katika kuongeza kasi ya kutokomeza ukeketaji nchini Tanzania kama ilivyoainishwa katika Mkakati wa Kitaifa wa Kupambana na Ukeketaji. Mradi huu wa ‘Jamii Imara’ utatekelezwa katika wilaya tatu za Mara: Tarime, Butiama, na Serengeti.
Lengo la mradi wa ‘Jamii Imara’ ni kukuza maadili ya kijamii na kijinsia katika kutokomeza ukeketaji. Mradi utafanyakazi na vikundi vya wanawake na wasichana ili kuwawezesha kupata uelewa juu ya haki zao na masuala ya kijinsia. Kwa wanawake na wasichana wasio mashuleni, mradi unajumuisha kipengele cha uwezeshaji kiuchumi ili kutoa vyanzo mbadala vya mapato, kujenga uwezo wa kifedha na kupunguza uwezekano wa ukeketaji na aina nyingine za ukatili wa kijinsia. Pia, mradi wa Jamii Imara utafanya kazi na vijana wa kiume, viongozi wa kidini na kimila ili kuwa mashujaa wa mabadiliko na kuongoza mipango ya mabadiliko ya kijamii katika ngazi za chini. Katika ngazi ya kitaasisi, Jamii Imara itasaidia ujenzi wa mitandao imara ya asasi za kiraia na serikali kwaajili ya kujifunza kwa pamoja, kubadilishana uzoefu, kushirikiana na kuimarisha hatua za pamoja za kukomesha ukeketaji wa aina zote, ikiwa ni pamoja na mila zinazovuka mipaka.
Katika maadhimisho ya mwaka huu ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia, mradi wa ‘Jamii Imara’ ni dhamira ya Serikali ya Marekani ya kuendelea kuwekeza na kusaidia asasi za kiraia na Serikali ya Tanzania katika mipango inayolenga kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana.
Magazeti ya Tanzania Disemba 11, 2023
MNYAMA AREJEA AKIIWAZA KAGERA SUGAR
NA JOHN MARWA
KIKOSI cha Wekundu wa Msimbazi Simba kimerejea nchini kikitokea Morocco ambako walicheza mchezo wa tatu wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika CAF CL na kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Waydad Casablanca.
Licha ya kupoteza mchezo huo Simba walicheza vizuri katika dakika zote 90, wakati wakiamini wanaondoka na alama moja katika mchezo mwamuzi alichezesha dakika sita za nyongeza badala ya dakika dakika tatu za nyongeza, Waydad wakapata bao dakika ya 95 ya mchezo.
Kabla ya kuwa kabili Waydad Desemba 19 katika Dimba la Benjamin Mkapa Simba itarudi katika mechi za Ligi Kuu kuwavaa Kagera Sugar Ijumaa Desemba 15 saa 10:00 jioni Uwanja wa Uhuru.
Simba imeshacheza mechi 8 za NBC PL ikivuna pointi 19, inashika nafasi ya tatu nyuma ya vinara Azam FC na Yanga SC huku Kagera Sugar katika mechi 11 imechukua pointi 13 ikiwa nafasi ya 12.
WAZIRI MKUU: MTANZANIA USIKUBALI KUTOA RUSHWA
*Azindua Awamu ya Nne ya Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wasikubali kutoa rushwa mahali popote huku akisisitiza kuwa wananchi ni wadau muhimu sana katika mapambano dhidi ya vita hiyo.
“Ninyi ni wadau wakubwa wa kukomesha rushwa. Nyie ni wadau wakubwa wa kukomesha vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu. Ili nchi yetu isiwe na vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa haki za binadamu, wananchi mnapaswa kufichua vitendo vya ukosefu wa maadili na uvunjifu wa haki za binadamu,” amesema.
“Mtanzania usikubali kutoa rushwa popote, hasa kwenye maeneo unayopaswa kupewa huduma hiyo. Wewe ni Mtanzania unalindwa na sheria za nchi za kupata huduma bure kama vile hospitali bila kutoa rushwa. Inatakiwa kila Mtanzania abebe jukumu hili kwa mikono miwili, alisimamie na alitekeleze,” amesisitiza.
Ametoa wito huo leo (Jumapili, Desemba 10, 2023) wakati akizungumza na washiriki na wadau mbalimbali kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu yaliyofanyika Nyerere Square, jijini Dodoma.
Waziri Mkuu ambaye amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Mheshimiwa Rais amesisitiza umuhimu wa kila mmoja kuendelea kushiriki katika mapambano dhidi ya rushwa na vitendo vingine vya ukiukwaji wa haki za binadamu. Maadhimisho ya mwaka huu yamebebwa na kaulimbiu isemayo:“Zingatia Maadili, Utu, Uhuru na Haki kwa Maendeleo Endelevu.”
Waziri Mkuu amesema kaulimbiu hiyo inachagiza masuala ya msingi yanayohusu maendeleo endelevu kutokana na ukweli kwamba kizazi huru chenye uadilifu, utu na kinazingatia haki ni msingi wa maendeleo ya Taifa lolote.
“Hivyo basi, hatuna budi wananchi wote kuunganisha nguvu katika ujenzi wa kizazi chenye misingi ya maadili. Kaulimbiu hii ni wito kwa sekta ya umma na sekta binafsi kutimiza wajibu wake kuhusu masuala ya maadili, utu, uhuru na haki. Kwa maneno mengine kaulimbiu hii imegusa taasisi zote na inasisitiza uwajibikaji wa kila mmoja wetu.”
Akisisitiza umuhimu wa maadili wa jamii, Waziri Mkuu amesema: “Maadili yanajengwa kuanzia kwenye taasisi ya kwanza ambayo ni familia. Taasisi ya pili ni shule, ambayo inawajibika kuweka mifumo ya kuendeleza kile kilichopatikana nyumbani. Kadhalika nyumba za ibada, tunategemea ziwe chachu ya kujenga maadili mema kwa misingi ya kiroho na hatimaye ushiriki wa jamii nzima kupitia wazee wa ukoo, jadi na maarufu katika makuzi ya mtoto.”
Waziri Mkuu pia alizindua Awamu ya Nne ya Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa na kuugawa nakala kwa wadau na baadhi ya wawakilishi wa makundi yaliyokuwepo.
Mapema, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), George Simbachawene alisema maadhimisho hayo kimataifa huwa yanafanyika Desemba 9, kila mwaka lakini hapa nchini yanafanyika Desemba 10, kwa sababu ya kupisha maadhimisho ya siku ya Uhuru. “Haya ni maadhimisho ya nane kufanyika kitaifa, tangu tuanze mwaka 2016,” alisema.
Alisema katika kuhakikisha haki za raia zinalindwa nchini, Rais Dkt. Samia aliunda Tume ya Haki Jinai ili ipate maoni ya wananchi na wadau mbalimbali yatakayofanyiwa kazi ikiwa ni dhamira yake ya kulinda haki za watu wote.
WAZIRI KAIRUKI AWATUNUKU VYETI WAPANDA MLIMA 228
• Awapongeza kwa kupanda mlima Kilimanjaro kuadhimisha miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akimkabidhi cheti cha kupanda Mlima Kilimanjaro, Kiongozi wa Wapanda Mlima, Kanali Martin Msumari katika hafla ya kuwapokea wapanda mlima Kilimanjaro 228 walioshiriki kampeni ya " Twenzetu Kileleni 2023" kwa ajili ya kuadhimisha miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika Desemba 9,2023, iliyofanyika leo Desemba 10,2023 lango la Marangu, Mkoani Kilimanjaro.
Na Happiness Shayo - Kilimanjaro
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amewatunuku vyeti wapanda mlima Kilimanjaro 228 walioshiriki kampeni ya " Twenzetu Kileleni 2023" kwa ajili ya kuadhimisha miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika Desemba 9,2023.
Hafla ya mapokezi ya wapanda mlima,waliopanda kuadhimisha miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika na kushuka tarehe 10 Desemba 2023 imefanyika katika lango la Marangu, Mkoani Kilimanjaro.
"Niendelee kuwapongeza wapandaji wote kufanikisha zoezi la "Twenzetu Kileleni 2023" na kusimika Bendera ya Taifa katika Kilele cha Mlima Kilimanjaro ili kusherehekea miaka 62 ya uhuru wa Tanganyika" Mhe. Kairuki alisisitiza.
Amefafanua kuwa zoezi la kupanda mlima ili kuadhimisha uhuru wa Tanganyika limeendelea kuvuta hisia za watu wengi ikiwemo Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania kutaka kushiriki kupanda mlima huo.
Amesema lengo ni kujua vivutio vilivyomo na kwenda kuvinadi katika nchi wanazoiwakilisha Tanzania hivyo ujio wao una manufaa makubwa kwa Taifa la Tanzania.
Amewataka Mabalozi hao kuendelea kuvinadi vivutio vya utalii vilivyoko nchini ili dhamira ya Serikali ya kuwa na idadi ya watalii milioni 5 ifikapo 2025 iweze kutimia.
Aidha, ametoa rai kwa Watanzania na wananchi wote kufuata sheria na kutovamia maeneo yaliyohifadhiwa kwani, kwa kufanya hivyo ni kuhujumu rasilimali za nchi.
Hafla hiyo iliyokuwa na kaulimbiu ya " Tunza mazingira ya ukanda wa Pwani okoa barafu ya Mlima Kilimanjaro" imetilia msisitizo Watanzania na dunia kwa ujumla kulinda mazingira ili kuepukana na vitendo vya ukataji miti holela ili kusaidia kurudisha uoto wa asili na hali nzuri ya hewa ambayo ni tunu katika kuendeleza uwepo wa Barafu ya Mlima Kilimanjaro.
Zoezi la kupanda kupanda mlima lilihusisha wawakilishi kutoka Taasisi za Serikali, Taasisi Binafsi, Watu Binafsi pamoja na Wanaha
WANANCHI HANANG WAIPA KONGOLE SERIKALI KWA KUENDELEA KUTOA ELIMU YA KUJIKINGA NA MAGONJWA YA MLIPUKO
Na Elimu ya Afya kwa Umma
Kutokana na Serikali kuweka msukumo wa kutoa elimu ya afya katika kujikinga na magonjwa ya mlipuko wilayani Hanang Mkoani Manyara ikiwemo ugawaji wa vipeperushi vya uelimishaji pamoja elimu ya matumizi sahihi ya dawa ya kutibu maji , baadhi ya wananchi wilayani humo wameipongeza serikali kwa kuweka kipaumbele uelimishaji.
Wakizungumza katika vijiji vinavyozunguka mlima wa Hanang baadhi ya wananchi hao akiwemo mwenyekiti wa Kijiji cha Gendabi wamesema kuwa serikali imefanya jambo jema kutoa elimu ya afya kuhusu kujikinga na magonjwa ya mlipuko pamoja na ugawaji wa vipeperushi kwani itasaidia kuchukua hatua stahiki za kujikinga na magonjwa ya mlipuko hasa katika kipindi hiki cha masika.
“Hili janga na mafuriko na tope kutokana mlimani limepita, ila kutokana na vyanzo vya maji kuchangamana hasa kwa miundombinu na maji ya mafuriko kunaweza kutokea jambo jingine kama vile magonjwa ya kuhara na kutapika,lakini serikali yetu imeona mbali tunashukuru serikali imetujali I kwa kuwatumia hawa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii tunapewa dawa ya kutibu maji pamoja na kupewa vipeperushi bure”amesema mmoja wa wananchi.
PBPA: Ruzuku ya Serikali yapunguza makali ya bei ya Mafuta
Afisa Mwandamizi wa Habari na Mawasiliano kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) Sabato Kosuri, akifafanua jambo wakati akifungua Kikao kazi baina PBPA na Wahariri wa Habari, kilichoratibiwa na OTR na kufanyika Jijini Dar es Salaam Disemba 11, 2023. Kushoto ni Mkaguzi Petroli PBPA, Bruno Tarimo na katikati ni Mkaguzi wa Ndani, Juma Hamidu.
Baadhi ya wahariri wakiwa katika mkutano huo.
Na Mwandishi Wetu
Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (Petroleum Bulk Procurement Agency - PBPA) imesema kuwa katika kipindi cha miezi sita kuanzia Julai 2022 hadi Disemba 2022 Serikali imetoa ruzuku ili kupunguza bei ya mafuta kwa wananchi hatua ambayo ilifanyika baada ya athari ya bei ya mafuta kupanda sana katika soko la dunia kutokana na vita baina ya Urusi na Ukraine.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (Petroleum Bulk Procurement Agency - PBPA) Erasto Simon, kwenye kikao kazi baina ya Wakala na Wahariri wa Habari, kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) jijini Dar es Salaam, leo Disemba 11, 2023.
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za makusudi kupunguza makali ya bei ya mafuta nchini ikiwemo kutoa ruzuku kwenye gharama ya mafuta, bei za nishati hiyo zinapopaa kutokana na changamoto mbalimbali za kidunia.
Simon alizitaja hatua nyingine zilizochukuliwa na Serikali ni pamoja na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika maghala ya kuhifadhia mafuta ili kuhakikisha taratibu za uendeshaji wa maghala hayo zinazingatiwa.
Aidha Simon alisema kuwa pamoja na Serikali ya Awamu
ya Sita kuhakikisha nishati ya mafuta inapatikana kwa wakati, ikiwa bora na bei stahmilivu, alieleza malengo na mafanikio
yaliyofanywa na yanayoendelea kufanywa na PBPA.
Akizungumzia uwezo wa maghala ya kuhifadhi mafuta Mkurugenzi huyo alisema kuwa Tanzania ina maghala 22 yenye uwezo wa kupokea mafuta kutoka kwenye meli katika Bahari ya Hindi ambayo yana uwezo wa kupokea lita bilioni 1.31 kwa aina nne za mafuta ya petroli (dizeli, petroli, mafuta ya ndege & mafuta ya taa.
Magazeti ya Tanzania Disemba 12, 2023
Kilele cha Maadhimisho ya kufunga siku 16 yafanyika Zanzibar
Hati Fungani ya NMB Jamii Yaandika Historia Kwa Kukusanya Tsh Bilioni 400
Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) CPA, Nicodemus Mkama alisema:
“Serikali kupitia Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) ina jukumu la kuweka mazingira ya kisera, kisheria na kiutendaji yanayowezesha upatikanaji wa rasilimali fedha za kugharamia shughuli za maendeleo. Kadiri Taifa letu linavyosonga mbele katika utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26 yaani the Third National Five-Year Development Plan (FYDP III) wenye dhima ya kujenga “Uchumi Shindani kwa Maendeleo ya Watu”, mahitaji ya rasilimali fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo, hususani miradi endelevu na yenye matokeo chanya kwa jamii yanaongezeka.
“Ili kufanikisha azma hii, kunahitajika uwepo wa bidhaa za kutosha, bunifu ambazo zinaleta anuwai katika masoko ya fedha, ikiwa ni pamoja na hatifungani za kampuni kama Hatifungani hii iliyotolewa na Benki ya NMB”.
Aidha, uwepo wa bidhaa nyingi katika masoko ya mitaji unachangia utekelezaji wa Sera za Fedha (Monetary policy) katika Uchumi na Sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi (economic empowerment policy); kuongezeka kwa akiba hapa nchini; kupanuka kwa uwekezaji unaoleta ongezeko la ajira; mapato kwa njia ya kodi kwa Serikali; na kuinua kipato cha watanzania kwa ujumla.
Mkama aliendelea kueleza kuwa:
“Mnamo tarehe 31 Agosti 2023, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) iliidhinisha maombi ya benki ya NMB kuuza toleo la kwanza la hatifungani iitwayo Jamii Bond yenye thamani ya shilingi bilioni 75, ikiwa ni sehemu ya Programu ya Hatifungani ya Miaka Kumi yaani Medium Term Note Programme yenye jumla ya thamani ya shilingi trilioni moja (Tsh 1,000,000,000,000) itakayotolewa katika fedha mbalimbali.
“Hatifungani hii imeweka historia ya kuwa hatifungani kubwa zaidi yenye mlengo maalum (thematic bond) kutolewa nchini Tanzania na katika Ukanda Kusini mwa Jangwa la Sahara na ambayo imewezesha kupata fedha za kutekeleza miradi endelevu na yenye matokeo chanya kwa jamii.
Vilevile CPA, Mkama aliendelea kueleza kuwa, Idhini ilitolewa na CMSA baada ya benki ya NMB kukidhi matakwa ya Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Sura ya 79 ya Sheria za Tanzania; Miongozo ya Masoko ya Mitaji na Dhamana ya utoaji wa Hatifungani kwa umma yaani Capital Markets and Securities (Guidelines for the issuance of Corporate Bonds); uwepo wa Muundo wa Hatifungani yaani Jamii Bond Framework ulioandaliwa na benki ya NMB kwa kushirikiana na Taasisi ya Uendelezaji wa Sekta za Fedha Barani Afrika (FSD Africa) na kukidhi matakwa ya Kanuni za Jumuiya ya Kimataifa ya Masoko ya Mitaji yaani International Capital Markets Association – (ICMA) na kupata ithibati kutoka kwa kampuni ya Sustainalytics ya nchini Uingereza, yenye utaalam kuhusu miradi endelevu kwa maendeleo ya jamii.
“kwa namna ya pekee napenda kutambua mchango wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (European Union) hapa nchini, kwa kujengea uwezo wa kitaalamu wafanyakazi wa Mamlaka na hivyo kuwezesha kuwa na ujuzi na weledi katika masuala ya hatifungani zinazokidhi matakwa endelevu na matokeo chanya kwa jamii”.
“Mauzo ya Hatifungani ya NMB (NMB Jamii Bond) yalifunguliwa tarehe 25 Septemba 2023 na kufungwa tarehe 27 Oktoba 2023, ambapo kiasi cha shilingi bilioni 212.94 kimepatikana, ikilinganishwa na shilingi bilioni 75 zilizotarajiwa kupatikana, sawa na mafanikio ya asilimia 284. Kufuatia kiasi kilichopatikana kufikia shilingi bilioni 212.94, CMSA imeidhinisha Benki ya NMB kutumia kiasi chote kilichopatikana kutokana na uwepo wa mahitaji ya kutosha, kugharamia miradi endelevu na yenye matokeo chanya kwa jamii.
“Mauzo ya hatifungani hii yamekuwa na mwitikio chanya unaoashiria kuongezeka kwa uelewa wa wananchi kuhusu uwekezaji katika masoko ya fedha hapa nchini, ambapo asilimia 98.7 ya wawekezaji walioshiriki ni wawekezaji mmoja mmoja na asilimia 1.3 ya wawekezaji ni kampuni na taasisi”.
Aidha, asilimia 99.9 ya wawekezaji ni wawekezaji wa ndani na asilimia 0.1 ni wawekezaji wa nje. Kwa upande wa kiasi kilichopatikana, asilimia 53.8 inatoka kwa wawekezaji mmoja mmoja na asilimia 46.2 inatoka kwa kampuni na taasisi. Aidha, asilimia 57.4 ya kiasi kilichopatikana inatoka kwa wawekezaji wa ndani na asilimia 42.6 inatoka kwa wawekezaji wa nje ya nchi.
Ushiriki wa wawekezaji mmoja mmoja wa ndani ni hatua muhimu katika kuongeza ukwasi katika soko (liquidity); na utekelezaji wa Mpango wa Huduma Jumuishi za Kifedha yaani National Financial Inclusion Framework wenye lengo la kuongeza ushiriki wa wananchi kwenye sekta rasmi ya fedha. Hivyo, tuna kila sababu ya kuipongeza benki ya NMB na wadau wote walioshiriki katika kuwezesha mafanikio haya. Hongereni Sana!!.
SIMBA SC WAENDELEA NA SHABIKI BINGWA KIBABE
NA JOHN MARWA
Klabu ya Simba imeendelea kuwashukuru mashabiki wake kwa kuunga mkono timu yao wakati huu ambao inaendelea kuimarika, leo hii uongozi wa Simba umekuja na kitu cha zaida kurudi kwa mashabiki wao.
Hayo yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo Imani Kajula ambapo amesema, moja ya wajibu mkubwa wa shabiki wa Simba ni kuisaidia timu yao kwa kununua bidhaa za klabu hiyo.
“Unaponunua bidhaa ya klabu unaisaidia klabu kujijenga kwenye mifumo yake ya kifedha. Ni wazi kwamba uendeshaji wa vilabu ni gharama sana. Ili tuwe na benchi bora, wachezaji wazuri, walipwe mishahara, wakae vizuri, walipwe posho, wasafiri. Ndio maana katika klabu yenu bajeti kwa mwaka ni Tsh. 24 Bilioni.”
“Mwaka huu tulianza na Shabiki Bingwa ambapo mashabiki wanashinda fedha taslimu, safari, tiketi za mechi na wakati hii kuelekea sherehe za mwisho wa mwaka tumekuja na MFALME SHANGWE. Mfalme ni Simba, shangwe ni kuelekea mwisho wa mwaka. Tumekuja na shindano ambalo lina jumla ya zawadi zisizopungua Tsh. 500 milioni na kushinda zawadi ya tiketi za mechi.” Amesema CEO Imani Kajula.
“Simba inaamini kwenye mashabiki wake kuwa na faida, kama atakuwa ni shabiki ambaye anaeleza mambo ambayo anataka lakini hashiriki kuisaidia timu basi ni ushabiki usio na faida. Kwa mashabiki wa faida basi MFALME SHANGWE ni jambo la kushiriki.”
“Eneo moja wapo ambalo litafaidika na mapato ambayo yatapatikana kupitia MFALME SHANGWE ni eneo la timu ya vijana. Mwaka huu tulitafuta vijana bora sana nchini. Mfano tuna vijana 15 katika timu ya vijana ya Zanzibar ambayo ilishinda ubingwa wa CECAFA. MFALME SHANGWE inaunganishwa na maendeleo ya timu kwa ushabiki wenye faida.”
“Tunawakaribisha Wanasimba na mashabiki wa soka Tanzania kushiriki MFALME BINGWA. Tunaamini tutaendelea kujitahidi ili Simba iwe sehemu ya furaha yenu kuelekea mwisho wa mwaka huu.” Imani Kajula
Mwisho
CCM YATOA SALAMU KWA VIONGOZI VIJANA WANAWAKE KUTOKA NCHI 16 ZA AFRIKA
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Anamringi Macha akizungumza wakati wa kutoa salaam za CCM, Jumanne, Desemba 12, 2023, kwa viongozi vijana wanawake kutoka nchi 16 za Afrika wanaohudhuria Mkutano wa Mwaka wa Asasi ya Kiraia ya Young Women of Africa (YWOA), wanaotoka katika vyama tawala katika nchi hizo.
Mkutano huo unaoendelea katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, iliyoko Kibaha, mkoani Pwani, unafanyika sambamba na mafunzo na mijadala ya masuala anuai yanayowahusu wanawake na uongozi katika nyanja mbalimbali kwenye jamii za Afrika na dunia kwa ujumla na kuweka maazimio yatayakochangia mstakabali wa jamii zilizo bora zaidi kwa kila mmoja.
RAIS SAMIA NI MFANO WA KUIGWA BARANI AFRIKA
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kuwa Mwenyekiti wa CCM, ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni mfano wa kuigwa kwa vijana wa Afrika, wakiwemo wa kike wanaotaka kuwa mahiri na kujenga ushawishi mkubwa katika maeneo mbalimbali ya uongozi kadri ya ndoto zao.
Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Anamringi Macha, Dusemba 12, 2023, alipokuwa akitoa salaam za CCM kuwakaribisha viongozi vijana wanawake kutoka nchi 16 barani Afrika, wanaoshiriki Mkutano wa Mwaka wa Taasisi ya Young Women of Africa (YWOA), unaofanyika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, Kibaha, mkoani Pwani.
“Tunapozungumza muda huu kutoka hapa tulipo kuna idadi kubwa ya wanawake katika nyanja mbalimbali za maisha ambao wamefanikiwa kubadilisha mtazamo na mwonekano wa jamii kuhusu wanawake, katika nchi zao, Afrika na dunia kwa ujumla, hasa kutoka kwenye mtazamo dhaifu na kuwa mtazamo wa uimara na umakini.”
“Wamekuwa mfano wa kuigwa kwa namna ambavyo wameweza kudhihirisha pasipo shaka yoyote kuhusu uwezo na nguvu za mwanamke.”
“Kwenye nyanja ya siasa, hapa tunaye Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, ambaye umahiri, uimara na uwezo katika uongozi, unatambuliwa na kukubalika duniani kote sasa. Wiki iliyopita tu, Jarida la Forbes limemtaja kuwa ni mmoja wa wanawake 100 wenye nguvu na ushawishi mkubwa duniani,” amesema Ndugu Macha.
Akiwasisitiza kuhusu umuhimu wa kujiamini kwa kutumia dhana ya uwezo wa mwanamke, kuliko kujikita kwenye udhaifu zaidi, Ndugu Macha pia aliwapatia mfano wa Mgombea Urais wa Chama cha SWAPO cha Namibia kwenye uchaguzi mkuu wa nchi hiyo mwaka kesho, akiwaambia kuwa ni mfano mwingine wa jinsi ambavyo wanawake wanapaswa kubadili mitazamo ya dhana dhalili.
“Tunapozungumza hapa, wenzetu SWAPO wa Namibia, wanajiandaa na uchaguzi na mgombea wao wa Urais ni mwanamke…kwa hiyo nao wanajiandaa kutufuata sisi Tanzania kwa kuwa na Rais mwanamama. Mifano hii tunayo kwenye nyanja zote za maisha sasa, hata zile zinazoendesha dunia, iwe kwenye kisiasa, iwe taaluma, michezo na zingine zote utakazoweza kusema. Kwenye chumba hiki tuna mfano wa Profesa Marcellina Chijoriga. Mnaona jinsi anavyosimamia na kuendesha shule hii kwa viwango na muonekano wa kimataifa,” amesema Ndugu Macha.
Alitoa wito kwa viongozi vijana wanawake kutokuwa wanyonge katika kuhakikisha wanatimiza ndoto za mafanikio makubwa katika nyanja mbalimbali katika maisha yao.