Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

JK ASHIRIKI MISHENI YA SADC KWENYE UCHAGUZI MKUU DRC

$
0
0

 

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa Jopo la Wazee wa SADC (SADC Panel of Elders-POE akitembelea mojawapo ya vituo vya kupigia kura jijini Kinshasha katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambako yuko kushiriki Misheni ya SADC kwenye uchaguzi wa nchi hiyo uliofanyika jana tarehe 20 Desemba 2023.

 

Kufuatia maelekezo ya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (Organ of Troika) ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa Jopo la Wazee wa SADC (SADC Panel of Elders-POE), Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa Jopo hilo yupo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kushiriki Misheni ya SADC kwenye uchaguzi wa nchi hiyo unaofanyika tarehe 20 Desemba 2023.

 

Misheni hiyo ya SADC katika Uchaguzi  Mkuu wa DRC inafanyika kufuatia mapendekezo ya Baraza la Ushauri wa Masuala ya Uchaguzi la SADC (SADC Electoral Advisory Council) kuwa katika uchaguzi huo wa DRC, SADC ipeleke Timu ya Uangalizi Uchaguzi (SADC Election Observation Mission, SEOM) sambamba na Jopo la Wazee (POE).

 

Timu ya Uangalizi wa Uchaguzi ya SADC inaongozwa na Makamu wa Rais Mstaafu wa Zambia Enock P. Kavindele, kwa kuwa Zambia ndiyo Mwenyekiti wa sasa wa Organ hiyo ya Troika. Timu hiyo ya SEOM inafanya majukumu ya kawaida ya uangalizi uchaguzi kama ilivyo utaratibu wa kawaida na SADC.

 

Kwa upande wake, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete anaongoza ujumbe huo wa POE unaojumuisha wajumbe wawili wa Kundi la Wapatanishi (Mediation Reference Group) ambao ni Lucy Mungoma, Katibu Mkuu Mstaafu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Zambia na Balozi na Balozi Joey, Katibu Mkuu Mstaafu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Zimbabwe pamoja na timu ya wataalamu kutoka Sekretarieti ya SADC.

 

Pamoja na mambo mengine, Jopo hilo la Wazee limepewa jukumu la kukukutana na kuzungumza na wadau mbalimbali katika uchaguzi huo wa DRC kwa lengo la kubaini na kutoa ushauri kuhusu maeneo yenye changamoto yanayoweza kupelekea kutokea kwa machafuko kabla, wakati na baada ya uchaguzi.

 

Rais Mstaafu Dkt  Jakaya Kikwete na ujumbe wake walikutana na kufanya mazungumzo na viongozi na wadau kadhaa wa uchaguzi huo wakiwemo Denis Kadima, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Kongo (CENI), Martin Fayulu, Mgombea Urais wa Chama cha Engagement for Citizenship and Development Party (ECIDE), Denis Mukwege, Mgombea Binafsi wa Urais, pamoja na Franck Diongo, Kiongozi wa Chama cha Mouvement Lumumbuste Progressiste aliyemwakilisha Moise Katumbi, Mgombea Urais wa Chama cha Ensemble pour la République. Rais Mstaafu Kikwete pia aliweza kuzungumza kwa simu na Mgombea huyo Mkuu wa Upinzani, Moise Katumbi pamoja na Rais Mstaafu Joseph Kabila.

 

Mbali na viongozi hao wa Kongo, Dkt Kikwete  alikutana na kuzungumza pia na Bintu Keita, Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo ambaye pia ni Mkuu wa Majeshi ya Umoja wa Mataifa nchini humo (MONUSCO).

 

Kiongozi huyo wa POE alitumia fursa ya kuzungumza na wadau hao kuwasihi kushiriki mchakato huo wa uchaguzi kwa amani na kutumia ushawishi wao kuwataka wafuasi wao kutunza amani hususan katika kipindi hiki cha uchaguzi na hata baada ya uchaguzi kumalizika kwa manufaa ya Wanakongo, nchi yao na ukanda mzima.

 

Aidha, kama sehemu ya misheni hiyo, Jopo hilo la POE lilipata fursa ya kutembelea vituo kadhaa vilivyopo katika jiji la Kishasa na kushuhudia zoezi la upigaji kura lilivyofanyika.

 

Rais Mstaafu Kikwete anatarajia kukutana na Kiongozi wa Jopo la Wazee wa Busara la Umoja wa Afrika (AU Panel of the Wise) Domitien Ndayizeye, Rais Mstaafu wa Burundi ambapo pamoja na mambo mengine Viongozi hao wawili waliopo nchini DRC wanatarajiwa kujadili na kubadilishana mawazo kuhusu uchaguzi huo kabla ya kuzishauri mamlaka husika za AU na SADC.

 

 

Ends

 


Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe lawasaka watuhumiwa wa uhalibifu wa mali

$
0
0

Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linawatafuta watuhumiwa wa kosa la kuharibu mali katika kijiji cha Halungu-Mbozi.


Disemba 18, 2013 huko Kata ya Halungu wilaya ya Mbozi mkoani Songwe shamba la mahindi lenye ukubwa wa heka 11 lililolimwa na watu 04 walilokodi kwa Edina Mgala, shamba hilo alilikodisha kwa kuligawa kwa watu hao ambao ni Mailo Msangawale (35) alikodishiwa heka 07, Emi Magwaza (48) alikodishiwa heka 1.5, Salome Nkota (50) alikodishiwa heka 1.5, na Jeremia Ngoya (42) alikodishiwa heka 1 wote ni wakulima na ni wakazi wa Halungu.

Heka hizo zimeharibiwa baada ya kupuliziwa dawa ya kuulia magugu aina  ya Rounup na mtu/watu wasiofahamika.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa ardhi unaohusisha familia mbili kati ya watoto wa mke mkubwa na mke mdogo wa marehemu Focus Makonongo.

Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe kwakushirikiana na maafisa kilimo wilaya ya Mbozi linafanya tathimini ili kuweza kujua thamani halisi ya mali iliyoalibiwa pamoja na kemikali iliyotumika kufanya uharibifu huo.

Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe linatoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za mtu au watu ambao wamehusika katika tukio hilo ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Aidha Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe linatoa rai kwa wananchi kutokujichulia sheria mkononi badala yake kutatua migogoro kwa kukaa vikao na kusuluhisha kwa amani.



Waziri Pembe hazitaka Jamii kudumisha mila na utamaduni wa kizanzibari

$
0
0

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma, akizungumza katika Maonesho ya mavazi ya wiki ya ya Mafunzo ya Amali yanaliofanyika katika viwanja vya Mapinduzi Square Michenzani Mjini Unguja.


WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma ameitaka jamii kuacha tabia ya kuiga tamaduni za kigeni ambazo haziendani na mila, silka na utamaduni wa kizanzibari ikiwemo suala la mavazi na malezi.


Mhe. Pembe ameyasema hayo katika Maonesho ya mavazi ya wiki ya ya Mafunzo ya Amali yanaliofanyika katika viwanja vya Mapinduzi Square Michenzani Mjini Unguja, amesema mavazi ya staha ni moja ya Utamaduni wa wazanzibari hivyo ni vyema kuendelezwa na kuacha kuiga mavazi ambayo hayana staha.

Amefahamisha  kwamba mavazi ya staha na malezi bora ni njia moja wapo ya kuzuia   vitendo vya ukatili na dhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto ambavyo vinajitokeza kila mara ndani ya jamii.

“suala la kuiga tamaduni zisizo za kizanzibari ambazo baadhi yake ndio sababu kubwa ya mporomoko wa maadili ya nchi na kusababisha vitendo vya udhalilishaji kuongezeka kila siku ni vyema kuachana nazo na badala yake kuendeleza mila, silka na Utamaduni wa Zanzibar” Alisema Waziri huyo.

Mhe. Riziki katika hafla hiyo ameomba Mamlaka ya Mafunzo ya Amali pamoja na Vyuo vyengine kuanzisha madawati ya kijinsia katika vyuo vyao ili iwe rahisi kwa wanafunzi wanapopata tatizo au kuona viashiria vya Udhalilishaji waweze kutoa taarifa kwa haraka kuhusu kupinga vitendo vya udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto.

Aidha ametoa wito kwa wazazi na walezi  kuwapeleka watoto wao katika vyuo hivyo vya Mafunzo ya Amali ili kupata taaluma na ujuzi utakaowasaidia vijana kupata ajira na kujiongezea kipata hali ambayo itawasaidia kuinuka kiuchumi.

Mwisho amewaomba Wanafunzi waliomaliza mitihani yao ya Kidato cha nne na hata wale ambao wapo majumbani kujiunga na vituo/vyuo vya mafunzo ya amali kwani ni miongoni mwa fursa za kuweza kujiajiri na kuondokana na umasikini.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt.Bakari Ali Silima amesema maonesho ya mavazi ni moja wapo ya kuonesha kazi zinazofanywa na vyuo hivyo, hivyo ni vyema jamii kuangalia ili kujifunza na kuona ni sehemu sahihi ya kuwapeleka watoto wao kupata ujuzi.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mavazi hayo Fatma Ali amesema vazi la staha  linasaidia kumpa mtu  ujasiri wa kukutana na watu mbali mbali katika  harakati za maisha  kwani mavazi ni mawasiliano katika jamii husika.


CRDB, Visa wakabidhi tiketi kwa mshindi wa kampeni ya ‘Tisha na Tembocard Tukakiwashe AFCON’

$
0
0


 

Mkurugenzi wa Wateja Wadogo Benki ya CRDB, Boniventure Paul (wa pili kushoto) akimkabidhi mfano wa tiketi ya ndege mshindi wa Kampeni ya Benki ya CRDB  ‘Tisha na Tembocard Tukakiwashe AFCON’  Evelyne Rwebugisa, katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo Disemba 22, 2023. Wa pili kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Kadi CRDB, Farid Seif.


 

Na Francis Dande, Dar es Salaam


BENKI ya CRDB kwa kushirikiana na kampuni ya Visa inayoongoza katika mfumo wa malipo ya kidigitali, imekabidhi tiketi kwa mshindi wa kampeni ya  ‘Tisha na Tembocard Tukakiwashe AFCON’.

 

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya tiketi ya ndege kwa mshindi wa Kampeni hiyo, Evelyne Rwebugisa,  jijini Dar es Salaam leo Disemba 22, 2023, Mkuu wa Kitengo cha Kadi Benki ya CRDB, Farid Seif amesema kuwa lengo la kampeni hii ni kuhamasisha matumizi ya kadi zake za TemboCard Visa, ambapo wateja nane watakaofanya miamala mingi zaidi watapelekwa nchini Ivory Coast kushuhudia mashindano ya TotalEnergies CAF Africa Cup of Nations (AFCON) 2024.


Kampeni hiyo ambayo ni sehemu ya juhudi zinazofanywa na Benki ya CRDB kupunguza matumizi ya fedha taslimu na kuhamasisha matumizi ya mifumo ya kidigitali ilizinduliwa Novemba 2, 2023 na itadumu kwa miezi mitatu mpaka Januari mwakani.
 
 
Mshindi wa kampeni hiyo Evelyne Rwebugisa amesema "Nimefurahi sana na sikutegemea kabisa, nachoweza kuwaambia wateja wengine wazidi kutumia kadi, wazidi kuchanja uwezi jua labda kadi yako ndio safari yako"
 
Evelyne ameongeza kuwa ushindi huo umetokana na kufanya malipo kwa kutumia kadi badala ya fedha taslimu katika manunuzi mbalimbali ndani na nje ya nchini.


Washindi wa kampeni hii watalipiwa nauli ya safari yao ya kwenda Abidjan, malazi katika hoteli ya kifahari, tiketi za daraja la juu (VIP) za kushuhudia mchezo wa fainali, kuhudhuria matukio maalum na vingine vingi ambavyo vitawaachia kumbukumbu isiyofutika.

Mbali na kushinda safari hiyo, wateja watakuwa na fursa ya kushinda zawadi nyingine ikiwemo seti ya sofa na vifaa vya kielektroniki mfano runinga na friji. Ili kushinda, amesema wateja wanaweza kutumia kadi zao kulipia bidhaa wanapozinunua dukani au sokoni, kwenye vituo vya mafuta, hotelini, wanaponunua tikiti au kulipia huduma.

Mtandao wapongeza zuio la kuingiza mbegu

$
0
0

Na Mwandishi Wetu

 

MTANDAO na Muungano wa Mashirika ya Kiraia na Vikundi vya Wakulima vinayounda Kikosi Kazi cha Mbegu Tanzania wamepongeza uamuzi wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), kuzuia ingizaji mbegu za mahindi na maharage ya Soya kutoka nchini Malawi.


 

Pongezi hizo zimetolewa mtandao huo, kupitia Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha Mbegu cha Tanzania, Abdallah Mkindi ambapo amesema dhamira yao ni kutetea  haki na ustawi wa wakulima wadogo katika sekta ya mbegu.

Alisema kikosi hicho kinalenga kuendeleza mifumo ya mbegu inayosimamiwa na wakulima, ambayo inategemea kanuni za kilimo ikolojia, bioanuai, na uhuru wa chakula.

“Sisi wanachama wa Kikosi Kazi cha Mbegu cha Tanzania, tunatoa pongezi zetu za dhati kwa juhudi za zilizochukuliwa na Wizara ya Kilimo na TPHPA kwa kuhakikisha maslahi ya wakulima wa Kitanzania na uadilifu wa mfumo wetu wa mbegu na kilimo cha kitaifa,” alisema.

Alisema wanapongeza uamuzi wa kishujaa wa kuzuia uagizaji wa mbegu za mahindi kutoka Malawi, kwani ni hatua muhimu katika kulinda wakulima na watumiaji kutokana na hatari inayoweza kuhusiana na mbegu zilizobadilishwa vinasaba kwa njia ya Uhandisi Jeni  (GMOs).

“Uamuzi wa kuchukua hatua haraka kufuatia ripoti juu ya uwezekano wa kuwepo vinasaba vya GMO unaonyesha dhamira ya kuhakikisha usalama na anuai ya mfumo wetu wa mbegu wa kitaifa,” aliongeza.

Alisema pia wanatambua marufuku ya kuagiza soya na bidhaa zake kutoka Malawi na kwamba uamuzi huo, uliozingatia uchambuzi wa hatari za wadudu, unadhihirisha kwamba walikuwa wanaenda kinyume na azma ya TPHPA ya kuhifadhi anuai ya kilimo na kulinda wakulima wa Kitanzania kutokana na tishio la madhara yanayoweza kusababaishwa na Virusi vya Tobacco Ringspot (TRSV).

Mkindi alisema wakati wakiunga mkono jitihada hizo, wanaiomba Wizara ya Kilimo, inayosimamia majukumu ya wakala wake ikiwa ni pamoja na TPHPA, kuhamasisha marekebisho ya Sheria ya Mbegu (2003) ili kutambua na kulinda mbegu zinazosimamiwa na wakulima.

Aidha alisema wanahimiza TPHPA kusukuma kwa haraka kupitisha Mkataba wa Kimataifa wa Rasilimali za Jenetiki za Mimea kwa Chakula na Kilimo (ITPGRFA) kwa kutoa Sheria ya Kitaifa ya Rasilimali za Jenetiki za Mimea (NPGR) kwa matumizi rasmi na ya mamlaka, kwani itasaidia katika usimamizi na uhifadhi wa rasilimali za jenetiki za mimea.

“Tunahimiza serikali kuimarisha kanuni za tahadhari kwa kudumisha utimilifu wa Sheria za Usalama wa Bioteknolojia. Uangalizi wa kina kwenye mipaka ni muhimu kuzuia kuingia kwa mbegu zisizostahili ambazo zinaweza kuhatarisha mfumo wetu wa kilimo,” alisema.

Mwenyekiti huyo aliyataja mashirika ambayo yapo kwenye kikosi kazi kuwa ni Tanzania Alliance for Biodiversity (TABIO), Iles de Paix (IDP), PELUM Tanzania, Tanzania Organic Agriculture Movement (TOAM), Sustainable Agriculture Tanzania (SAT), ECHO EA, ESAFF, AfroNET, ENVIROCARE na MVIWAARUSHA

Mengine ni MVIWAKI, MVIWAMA, TUSHIRIKI, ACTIONAID Tanzania, SWISSAID Tanzania, HACHAWOTA, SHIWAKUTA na COWEA.

Mwisho

Magazeti ya Tanzania Disemba 27, 2023

MAJALIWA ASHIRIKI SHEREHE ZA KUAPISHWA RAJOELINA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo (Jumamosi, Desemba 16, 2023) ameungana na Marais kutoka nchi sita barani Afrika kwenye sherehe za kumuapisha Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina.

 

Waziri Mkuu ambaye amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, alikuwa miongoni mwa marais kutoka Comoro, Angola, Zimbabwe, Msumbiji, Mauritius, Guinea-Bissau na wawakilishi kutoka nchi zaidi ya 10 ambao wameshiriki sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo zilizofanyika kwenye uwanja wa Barea, eneo la Mahamasina, jijini Antananarivo.

 

Viongozi walioziwakilisha nchi zao wanatoka China (CPPCC), Rwanda, Seychelles, Senegal,Côte d'Ivoire,India na mabalozi mbalimbali. Mbali na Marais wa AU na SADC, viongozi wengine walitoka Kamisheni ya Bahari ya Hindi (Indian Ocean Commission), COMESA na Benki ya Maendeleo ya Afrika.

 

Mapema, akilihutubia Taifa hilo mara baada ya kuapishwa, Rais Andry Rajoelina alisema ana mapenzi ya dhati kwa nchi hiyo na wananchi wake na akawahakikishia kuwa atafanya kila awezalo ili kuendeleza umoja na mshikamano wa Taifa hilo.

 

Rais huyo ambaye anachukua kiti hicho kwa mara ya tatu alisema: “Hatutaki kuwa nchi ambayo haina utulivu. Tutasonga mbele kuhakikisha kila wilaya inapata maendeleo ya kiuchumi kwani tunayo maono (vision) na malengo tunayotaka kuyafikia.”

 

Katika hotuba yake iliyochukua dakika 20, Rais Rajoelina aliongea kwa Kimalagasi, ambayo ni lugha ya Taifa ya nchi hiyo. Alipomaliza, akatumia dakika saba kuhutubia kwa Kifaransa kwa ajili ya viongozi wa Kimataifa ambao waliohudhuria sherehe hiyo.

 

Pia Rais Rajoelina alisisitiza kwamba atakuwa Rais wa watu ambaye anataka kuona ushirikishwaji wa kila mmoja katika kuleta maendeleo ya nchi hiyo.

 

Kabla ya kuondoka uwanjani, Rais Rajoelina alishuhudia bahati nasibu ikichezeshwa na kisha akakabidhi funguo za nyumba ya kisasa iliyowekewa samani zote iliyoko Lake Village eneo la Ivato, kwa mshindi wa bahati nasibu hiyo. Ujenzi wa makazi bora ni moja ya malengo ya 13 ambayo Rais huyo amejiwekea.

 

 

Malengo mengine ni Amani na Ulinzi; Nishati na Maji; Mapambano dhidi ya Rushwa na kuleta Usawa; Elimu na Utamaduni; Afya kwa Wote; Ajira bora kwa wote; Uwekezaji na Viwanda; Mustakabali wa Vijana na Wanawake na Uzalishaji wa Chakula cha Kutosha. Mengine ni Menejimenti Endelevu ya Maliasili; Ujenzi wa Makazi bora na Ukuzaji wa Miji; Uwezeshaji na Uwajibikaji na Michezo kwa Wote.

 

Rais Rajoelina ambaye alishika madaraka ya nchi hiyo mwaka 2009-2014 na 2019-2023 ni kiongozi wa Chama cha Young Malagasies Determined (TGV) ambacho itikadi yake ni mageuzi (reformism), uwazi wa Serikali (government transparency) na demokrasia ya kijamii (social democracy).

 

TAWOMA "yamwangukia" Silanga

$
0
0

 MWANDISHI WETU, SIMIYU


Chama cha Wachimbaji Wanawake Mkoa wa Simiyu, (TAWOMA) kimemuomba radhi  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Simiyu Emmanuel Silanga ambae ni mshauri wa maridhiano pamoja na Muwekezaji wa Mgodi namba 10, Dutwa, Daudi Emmanuel, kwa madai ya kumchafua kutokana na kudanganywa na wanasiasa na kuandamana,  kufanya fujo, huku wakitambua hawana leseni ya umiliki wa mgodi huo.



Hata hivyo, taarifa kutoka katika Ofisi za Madini Mkoa wa Simiyu zinaeleza kuwa Wachimbaji hao Wanawake hawana leseni ya kumiliki wa mgodi huo na kwamba hawakuwa na sifa za kuwepo katika kwa sababu hawakuomba leseni licha ya wao kulalamika kuwa wapo kihalali.


Muwekezaji huyo akizungumza na Waandishi wa Habari alisema hakuna mgogoro wowote uliyokuwepo kati ya wachimbaji hao na yeye, bali ni changamoto chache zilizotokea ambapo wachimbaji  hao hawakukaa nae pamoja na kukubaliaana baadhi ya mambo na kuwaomba  kwamba waache kutumiwa na wanasiasa wasioitakia mema nchi, kwani wao walitambua wazi kwamba hawakuwa na leseni ya eneo hilo la mgodi.


Alisisitiza kwamba  kilichopo ni wachimbaji hao kutumiwa na wanasiasa wasiokitakia mema Chama cha Mapinduzi na kuwa chanzo cha Migogoro isiyokuwa na tija na kuwataka kuacha tabia hiyo ambayo haina afya kwa maendeleo ya taifa.


Kufuatia hatua hiyo ya wachimbaji hao kumuomba radhi mwekezaji huyo, wachimbaji hao wameruhusiwa na mwekezaji huyo kusimamia na kuendelea na uchimbaji katika mgodi huo na kwamba yeye atakuwa akipokea taarifa za uendeshaji wa mgodi kutoka kwao na Meneja Wake.


“Naomba ifahamike kuwa hakuna mgogoro uliyokuwepo kati yangu na Wachimbaji hawa, Mimi nawapenda sana Wachimbaji Wanawake wa Mkoa wa Simiyu. Nimewapa ruhusa ya kusimamia mgodi, nitakuwa nikipokea taarifa za uendeshaji kutoka kwao,”alisema Emmanuel na kuongeza:


“Nawaomba sana Wachimbaji wasikubali kutumiwa na wanasiasa wasio kitakia mema chama.Kama kuna mambo ya msingi ni vema tukaketi pamoja tukazungumza ili kuondoa migogoro isiokuwa na tija na pia endapo mtashindwa kuelewana ama mkipigana tena kwa  sababu ya usimamizi  sina budi kuwaondoa katika usimamizi ili mbaki kuwa wachimbaji tu.”


 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Emmanuel Silanga alisema kuwa kutatuliwa kwa mgogoro huo ni juhudi za kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu katika kuwawezesha akina mama ili waweze kujiinua kiuchumi kwa maendeleo ya taifa la leo na kesho.


“Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia haipendi kuona akinamama wakiwa wanahangaika kwa sababu wao ndio uti wa mgongo wa familia ndio maana tunatamani kuona wakiwa vizuri kiuchumi kwa manufaa ya taifa la sasa na kesho kwa sababu wao ndio walezi wakuu wa familia, serikali inawajali ndio maana imeamua kusimamia hili ili kuhakikisha hakuna mgogoro tena”.Alisema Silanga


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk Yahaya Ismail Nawanda akizungumzia suala hilo, alisema wameketi pamoja kati ya muwekezaji huyo na wachimbaji hao wanawake na kwamba muwekezaji ambaye ndie mwenye leseni amekubali kuwaruhusu kusimamia mgodi huo.


“Tumeketi pamoja kati ya mwekezaji na wachimbaji Wanawake, tumemaliza changamoto zilizotokea na sasa wameruhusiwa kusimamia mgodi huo. Na kuanzia Jumatatu kazi za uchimbaji itanzaa rasmi mgodini,”alisema Dk Nawanda.


Mara baada ya kuruhusiwa kusimamia mgodi huyo na kuendelea na kazi zao za uchimbaji wa dhababu, Mwenyekiti wa Wachimbaji (TAWOMA), Mary Chacha amemshukuru Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya  Chama cha Mapinduzi  Emmanuel Silanga  kwa kuwasaidia  kurejea katika majukumu yao ya usimamizi wa mgodi  na kwamba wamempongeza kwa kuwajali wachimbaji wanawake wa Mkoa wa Simiyu.


“Kwa niaba ya wanawake wachimbaji napenda kumshukuru mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Silanga kwa kutusaidia katika kumaliza huu mgogoro kwa njia nzuri ya maridhiano ya pande zote mbili  na sisi kurejea katika majukumu yetu tunamshukuru sana yeye pamoja na Mkuu wa Mkoa kutusaidia katika hili” alisema Chacha.


Wazazi waaswa kuwachunguza watoto wao

$
0
0

 


Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto bi Abeida Rashid Abdallah (Kushoto) akimkabidhi  cheti cha shukran Mratibu wa mafunzo ya kuwajengea uwezo kikundi cha Banaty Bi Raya Hamad Mchele, Mafunzo hayo yamefanyika Jana, katika ukumbi wa Michenzani Mall Unguja. 

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto bi Abeida Rashid Abdallah (Kati) akiwa katika picha ya pamoja na wanakikundi cha Banaty baada ya kuwakabidhi cheti cha Shukran katika mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyofanyika Jana, Michenzani Mall Unguja. 


Na Talib Ussi


Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto bi Abeida Rashid Abdallah amewataka Wazazi na Walezi Wanawake kuwachunguza watoto wao sehemu za siri katika miili yao ili kuhakikishwa kwamba wako salama na hawajafanyiwa vitendo vya udhalilishaji vya aina ya ngono.


Kauli hiyo ameitowa katika mafunzo ya kuwajengea uweza kikundi cha Banaty yaliyofanyika Michenzani Mall Unguja mara baada ya mtaalam wa Afya Dkt Ummulkulthum Omar kuwasilishaji mada ya afya ya mfumo wa uzazi pamoja na kueleza kwamba katika utekelezaji wa majukumu yake anakutana na kesi za watoto wachanga  wa miezi minane wameingiliwa kinyume na maumbile na kuharibiwa.


Bi Abeida amesema kwa vile Wazazi na Walezi Wanawake hawana vibakio ni vyema kuwa karibu na watoto hasa watoto wa kiume waliyofikia umri wa balegh kwa kuwauliza masuali bila ya kuona haya pamoja na kuwaangalia sehemu zao za siri kama ziko salama na hazijafanyiwa udhalilishaji wa aina ya ngono.


“Tuwe karibu nao hasa watoto wa kiume sisi wanawake hatuna vibakio kwahiyo lazima tuwe karibu na watoto wetu tuwahoji Je hakuna mtu aliyeguza sehemu za siri? Na tusiishie kuwauliza tu. Pia kuwaangalia hasa huko sehemu ya siri  tujue kama kuko salama, tusisuniria azoeshe mchezo mchafu ”. Alisema Abeida.


Alieleza kwamba ripoti ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeonesha matukio ya udhalilishaji 199 yameripotiwa kwa mwezi wa Oktoba, 2023 kati ya idadi hiyo asilimia 78.9 ni watoto na wanawake ni asimia 16.2 hivyo ni vyema Wazazi na Walezi Wanawake kila mara wawe karibu na watoto wao.


Aidha katibu Mkuu huyo alitoa wito kwa  washiriki wa mafunzo hayo  na wanawake wote waliyopata mafunzo ya ujasiriamali  kutumia ipasavyo  elimu hiyo kwani Serikali ya Mapinduzi inatoa fursa ya mikopo kwaajili ya kuwawezesha  kiuchumi  ili waweze kujiongezea kipato na kujikwamua na umasikinini. Alisema kwani umasikini pia unachangia matendo ya udhalilishaji kutokea kwa watoto.


Naye Mtaalum wa Afya bi Dkt Ummulkulthum Omar kutoka Hospital ya Rufaa ya Mnazimmoja Zanzibar katika mada ya mfumo wa uzazi aliyowasilisha alieleza matatizo  mbali mbali yanayowatokea wanawake katika mfumo wa uzazi ikiwemo kutoshika mimba, kutokwa na uchafu usiokuwa wa kawaida katika sehemu za siri, n.k. hivyo amewataka wanawake kukimbilia hospitali endapo wataona dalili yeyote ambayo sio ya kawaida kutokana na elimu aliyofundisha ili kuwahia kutimbiwa.


Aidha katika uwasilishaji wa mada hiyo aliezea kwamba anakutana na kesi ya watoto wa umri tofauti ambao wameingiliwa kinyume na maumbile ikiwemo watoto wa miezi minane, hali ambayo inasikitisha hasa ukiangalia matendo hayo yanafanywa na mtu wa karibu.


Mapema Mratibu wa mafunzo hayo ambaye ni Mkurugeni wa Raha online TV bi Raya Hamadi Mchele amesema lengo la kunadaa mafunzo hayo ni kuwapa elimu kundi la Banaty ikiwemo elimu ya afya, kujitambua na elimu ya ujasiriamali ili waweze kujikwamua kimaisha.


Kikundi cha Banaty kimeanzishwa kwa lengo la kusaidiana katika shughuli mbali mbali za kijamii ikiwemo harusi na msiba. Hivyo kikundi hicho kinamuda wa miaka minane na mfuko wao wafedha una pesa zaidi ya shilingi za Tanzania milioni ishirini.

NAIBU WAZIRI PINDA AASA WANANCHI KUHUSU MATUMIZI BORA YA ARDHI

$
0
0


Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akizungumza wakati hafla malumm ya chakula alichowaandalia wananchi na viongozi wa jimbo lake kusheherekea Siku Kuu ya Chrismas tarehe 26 Desemba 2023 nyumbani kwake Kibaoni mkoani Katavi.

 

Na Munir Shemweta, MLELE

 

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amewaasa watanzania kuhakikisha wanakuwa na mipango bora ya matumizi ya ardhi kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo kwa kuwa ardhi iliyopo haiongezeki na idadi ya watu inazidi kuongezeka.

 

Mhe. Pinda amesema hayo tarehe 26 Desemba 2023 nyumbani kwake Kibaoni, Halmashauri ya Mpimbwe mkoani Katavi katika hafla maalum ya chakula aliyowaandalia wananchi na viongozi wa jimbo lake kusheherekea Siku Kuu ya Chrismas.

 

Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, Naibu Waziri huyo wa Ardhi alisema, wakati serikali ikiandaa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, watanzania wanatakiwa kuwa na mpango wa matumizi ya ardhi huku wakielewa changamoto kubwa iliyo mbele yao ni kuwa ardhi haiongezeki.

 

‘’Miaka 25 inayokuja lazima tufikirie hizi hekta na ekari tulizopopewa na Mungu ikaitwa Tanzania inatushoje itakapofika miaka hamsini ijayo, kwa hiyo ni sisi ndiyo tutakaopanga tutumiaje maeneo yetu’’ alisema Mhe. Pinda.

 

‘’Kila mtu akikaa ajue ardhi ni yake na ndugu zake kwa hiyo tuishi kwa amani na tusigombane, hakuna namna tutakachokifanya katika eneo hili ni lazima tukubaliane namna ya kuitumia ardhi ndogo katika ongezeko kubwa la watu’’. Alisema Pinda.

 

Akigeukia shughuli za maendeleo kwenye jimbo lake la Kavuu, Mhe Pinda amewaambia wananchi wake kuwa, jimbo hilo kwa sasa limepiga hatua kubwa ukilinganisha na miaka ya nyumba kwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amewezesha utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo hata ile ambayo haikutajwa kwenye ilani ya CCM na kutolea mfano ujenzi wa zahanati, shule na miundombinu.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpimbwe Shamimu Mwariko aliwapa ushauri wananchi wa Mpimbwe kuwa, kama wanataka halmashauri yao ifanane kimaendeleo na halmashauri zilizopiga hatua kubwa kimaendeleo basi wahakikishe wanawashika viongozi wanaofanya maamuzi ya kimkakati.

 

‘’Kama kweli mna lengo la kusema sasa sisi Mpimbwe iwe inafanana na eneo fulani shikeni viongozi wanaofanya mamuzi kimkakati, utekelezaji wao, mipango yao ni kuhakikisha wanafungua njia watu waweze kupita njia hizo ndiyo kazi ya kiongozi yoyote duniani’’, alisema Shamim.

 

Naye Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda amemtaka Mbunge wa Jimbo la Kavuu ambaye ni mdogo wake kuwa karibu na wananchi  wakati wote wa juhudi mbalimbali za kuliletea maendeleo jimbo lake.

 

‘’Hoja kubwa ya wananchi unaowaoongoza ni mahusiano, mnaishije? Kila aliyesimama amekupa sifa ni jambo zuri kazi yako sasa ni kutoharibu sifa, kaza uzi na jishushe kadri inavyowezekana na watu wote ni wa kwako hata wale mliopingana’’ alizsema Mizengo Pinda.

 

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda yuko jimboni kwake katika Halmashauri ya Mbimbwe mkoa wa Katavi kujumuika wananchi wa jimbo la Kavuu pamoja na mambo mengine kusheherekea Siku Kuu ya Chrismas na wananchi wa jimbo lake.

NMB yanogesha sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar yatoa zaidi ya Sh. Mil. 200

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Fatma Hamad Rajab, akipokea Masaada wa Traki Suti kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Zanzibar, Naima Shaame ikiwa ni sehemu ya udhamini wa benki hiyo katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar pamoja na sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Hafla hiyo fupi ilifanyika ofisi ya wizara ya michezo Zanzibar.



 

Na Mwandishi Wetu


BENKI ya NMB imetoa zaidi ya shilingi milioni 200 kwa ajili ya zawadi za mashindano ya kombe la mapinduzi Zanzibar na Traki suti  150 kwaajili ya kuvaa kwenye matembezi siku ya Mapinduzi.



Fedha hizo kwa ajili ya bingwa  ambaye atazoa shilingi milioni 100 mshindi wa pili milioni 70, pamoja na medali za mabingwa na mshindi wa pili.

Akizungumza wakati wa halfa ya kukabidhi nguo za mazoezi kwa ajili ya siku ya mazoezi kitaifa yatakayofanyika Januari 1, ambazo zilimetolewa na benki hiyo Meneja Biashara Zanzibar  benki ya NMB Naima Said Shaame .


Alisema udhamini huo  unalenga azma ya benki ya NMB na pia juhudi za Serikali katika kusherehekea miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Alisema benki ni miongoni wa wadau wakubwa inayochangia ukuaji wa wa sekta mbalimbali za  maendeleo Zanzibar, hivyo waliona ni wajibu wao kuwa sehemu ya maadhimisho ambayo kilele chake ni Januari 12.

 
 ‘’Kama Benki tunasema huu sio mwisho wa udhamini wetu. Tunaamini kwamba michezo sio tu inachangia ustawi wetu, lakini pia inatuleta pamoja kama taifa’’aliongeza.

 

Alisema NMB imeamua kutoa Traki suti  hizo za mazoezi 150  kwa jili ya kuunga mkono siku ya mazoezi ikitaifa jambo ambalo hulifanya kila mwaka, kuonyesha kuwa mazoezi ni muhimu kwa wananchi ambao ni wateja wao.

 

‘’Tunapenda kuwa na wateja wenye afya na tunajua kuwa mazoezi ni afya, hivyo tumeamua kuunga mkono jambo hilo ili kuhakikisha wateja wetu wanakuwa na afya njema’’alisema.

 

Akizungumza baada ya kupokea Traki suti hizo Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab, aliishukuru benki ya NMB kwa misaada mbali mbali inayotoa.

 

Alisema benki hiyo ni kiongozi wa kutoa misaada kwa serikali katika nyanja zote za michezo na jamii, hivyo msaada huo umekuja wakati muafaka kwani siku ya mzoezi  ya kitafa ni siku kubwa.

 

Katibu Fatma alisema amepokea misaada hiyo kwa furaha, ambapo ameitaka benki hiyo kuendelea kusaidia kwani bado kuna mahitaji mengi yanatakiwa kuendeleza michezo Zanzibar.

Morogoro, Tanga wapewa kipaumbele kulima karafuu

$
0
0

 

Na Mwandishi Wetu

 

MIKOA ya Morogoro na Tanga imepewa kipaumbele cha kulima zao la karafuu katika mpango wa pamoja wa serikali na wadau wa kilimo kutoka sekta binafasi na taasisi zisizo za kiserikali.

 


Ongezeko la Mkoa wa Tanga katika ulimaji wa karafuu kitaifa limetangazwa katika Mkutano wa Wadau wa Kilimo na Mazingira waliokutana jijini Dar es Salaam.

 

Wadau hao wamesema zao la karafuu limeonesha kustawi katika mikoa hiyo miwili, hivyo waamini ikipewa kipaumbele itaongeza uzalishaji.  

 

"Morogoro ndiyo iliyotangulia na mwaka jana tu ilizalisha tani 2,000 sawa na nusu ya uzalishaji wa Zanzibar wa jumla ya tani 4,000, hivyo ongezeko la Tanga ni wazi Tanzania itakuwa mzalishaji mkubwa wa karafuu," walisema wadau.

 

Ulimaji wa karafuu Tanzania Bara umetokana utafiti na ushauri wa  Kituo cha Kuendeleza Kilimo Nyanda za Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), taasisi inayowashirikisha wadau katika sekta binafsi katika kulima mazao na kuendeleza minyororo ya thamani ya mazao hayo.

 

Akitangaza uamuzi wa kuiongeza Tanga kwenye mpango huo wa zao la karafuu, Ofisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga, amewambia wajumbe wa jukwaa la Wadau wa Kilimo na Mazingira kwamba utafiti umeonyesha kuwa mkoa huo unaweza kulima kwa mafanikio zao la karafuu.

 

Kirenga ameeleza kuwa zao la karafuu ni zao la thamani kubwa na ni sehemu ya mazao muhimu ya viungo na pia ni muhimu katika  mazao ya   mboga, matunda, mizizi na maua (hortculture) ambayo yana masoko yanayaotabirika duniani. 

 

Alisema endapo Watanzania watachangamkia fursa zilizomo katika ulimaji wa zao la karafuu,  basi uchumi wa mkulima mmoja mmoja na  wa Taifa  utaimarika na kukifanya kilimo kiwe na tija.

 

“Mazao ya viungo hususani karafuu yamekuwa na  soko imara na la uhakika. Sasa bei elekezi ya kilo moja ya karafuu ni kati ya shilingi 14,000 hadi  18,000. Bei hizi zinaonyesha ni jinsi gani zao hili  likipewa kipaumbele litakavyokuwa na maana kwa mkulima mdogo  na pia likawa ni zao letu lenye tija kubwa katika soko la kimataifa”, Kirenga alilieleza jukwaa hilo.

 

Aliongeza kuwa  karafuu ni zao la msingi Zanzibar na  wao ndiyo wazalishaji wakuu wa zao hilo, wana masoko makubwa na ya uhakika. 

 

“Hivi karibuni Tanzania Bara imeanza kuzalisha zao hili katika baadhi ya mikoa miwili. Uzalishaji umekuwa na mwelekeo mzuri kwani mikoa hii sasa inazalisha kwa wingi zaidi karafuu ikilinganishwa na  Zanzibar ambao ndio waanzilishi. Mikoa hiyo  kwa sasa ni Morogoro na Tanga”, alisema Kirenga. 

 

Sasa hivi serikali inawashirikisha wadau wengine kuinua pato la Mtanzania kufikia dola za Marekani 3,000 kabla ya mwaka 2025.  

 

Tanzania sasa inahesabiwa kuwa nchi yenye uchumi wa kati wa chini baada ya pato la Mtanzania kuvuka dola za Marekani 1,096, kigezo kinachotumiwa na Benki ya Dunia katika kupima umaskini wa watu katika taifa lao.

 

Ili kulifanya zao la karafuu likubalike kwa wakulima Mkoa wa Morogoro na SAGCOT wameshirikiana serikali ya mkoa kuwapeleka Zanzibar wakulima 20 wa Morogoro kujifunza ulimaji wa zao hilo. 

 

Tayari ulimaji wa zao hilo  umeimarika katika Wilaya za Morogoro Vijijini, Kilombero; katika Halimshauri ya Wilaya ya Mlimba na sasa imeongezeka Wilaya ya Mvomero. 

 

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero,  Judith Nguli, ameeleza uingizaji wa kilimo cha karufuu katika mkakati wa kuinua pato la mkulima una maana kubwa kwa wilaya yao.  

 

Alisema ulimaji wa zao hilo unawaletea wakulima fursa tele na kwani  wadau wamejizatiti kuunga mkono ulimaji wa zao katika wilaya yao.

 

“Wilaya yetu imekuwa ikiathiriwa na kilimo kisichokuwa na tija.  Uwepo wa mazao kama haya ya kimkakati utapelekea kuinua maisha ya mwananchi mmoja mmoja.  

Tumethibitishiwa kuwa ardhi yetu itasitawisha zao la karafuu kama tutazingatia maelekezo ya wataalamu,’’ alisema Nguli.

 

Meneja wa SAGCOT, Mkoa wa Morogoro,  John Banga alieleza kuwa Mkoa wa Morogoro ni miongoni mwa mikoa iliyopewa kipaumbele cha  kuzalisha kilimo cha mazao ya viungo, na hasa  karafuu, huku akianisha sababu zake ni kwamba mkoa una hali  ya hewa inayofaa  na afya ya udongo  ni himilivu kwa zao la karafuu.

 

“Ndani ya miezi miwili wakulima wamegawiwa zaidi ya miche 150,000 ili waweze kuendeleza kilimo cha karafuu. Jambo kubwa na zuri wapo wadau ambao wamekuja kuunga mkono juhudi hizi za kulima karafuu katika milima ya Morogoro. Kilimo cha karafuu kwa njia hii kitasaidia katika kutunza afya ya mazingira ya misitu.  Tutajiepusha na uchomaji wa maeneo na ukataji wa miti kwa ajili ya mkaa,’’ alisema Banga.

Mwisho

SMZ yazidi kuimarisha huduma za Afya vijijini

$
0
0

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  inaendelea kuimarisha huduma za Afya mijini na vijijini  ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025 na azma ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964 yenye lengo la kuwapatia huduma bora  za kijamii wananchi wake bila ya ubaguzi wa aina yoyote ikiwemo huduma ya Afya.

Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla ameyasema hayo wakati akifungua Kituo cha Afya cha Uzi na Ng'ambwa ikiwa ni muendelezo wa shamra shamra za kutimia miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

 

Amesema kuwa ili nchi iwe na uchumi Imara na maendeleo endelevu ni lazima wananchi wake wawe na Afya bora itakayowapa nguvu za kufanya shuhuli zao ambazo zinawapatia kipato pamoja na kukuza uchumi wa nchi.

 

Mhe.Hemed  amesema kituo cha  afya cha Uzi na Ng'ambwa kilichojengwa na fedha za Mradi Tasaf  kwa kushirikiana na Serikeli ya Mpinduzi ya Zanzibar kimekamilika kwa kiwango kilicho bora na asilimia ndogo iliyobakia Serikali itatoa fedha kwa ajili ya umaliziaji ili wananchi wapatiwe huduma bora na kwa wakati stahiki.

 

Makamu wa pili wa Rais amemuagiza Waziri wa Afya kuhakikisha madaktari watakaotoa huduma katika kituo cha Afya Uzi na Ng’ambwa  lazima waishi maeneo ya karibu na kituo hicho ili kuweza kuwahudumia  wagonjwa kwa masaa  ishirini na nne (24).

 

Aidha ameitaka Wizara ya Afya  kuandaa utaratibu wa kutafuta Vijana wenye Taaluma ya Afya wa maeneo ya Uzi na Ng’ambwa  ama kuwasaidia kuwasomesha  kada mbali mbali za Afya ili kuwaandaa kufanya kazi katika kituo hicho mara baada ya kumaliza masomo yao jambo ambalo litaondoa usumbufu na uhaba wa madaktari katika vituo vya afya.

 

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewataka wananchi wa Uzi na Ng’ambwa  kutoa ushirikiano kwa serikali pamoja na madaktari wanaotoa huduma katika kituo hicho na vituo vyengine ili kuweza kutoa huduma zilizobora na kufikia malengo ya serikali ya kuwapatia huduma bora wananchi wake bila ya kujali tofauti za aina yoyote.

                                     

Nae Waziri wa Afya Mhe Nassor Ahmed Mazurui amesema Jengo limekamilika na limekidhi viwango vyote vya kuitwa kituo cha Afya  ambacho kitatoa huduma za matibabu ya aina mbali mbali zikiwemo  za mama na mtoto.

 

Amesema Wizara itahakikisha inalitunza jengo hilo ili liweze kutoa huduma zilizo bora pamoja na kufikia azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kutoa huduma bora kwa wananchi wote bila ya kujali itikadi zao sambamba na kuwajengea nyumba za makaazi  Madaktari watakaofanya kazi katika kituo hicho ili kuwarahisishia ufanyaji wa kazi zao.

 

Akitoa taarifa za kitaalamu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili, Sera, Uratib na Baraza la Wawakilishi Dkt. Islam Seif Salum amesema Ujenzi wa Kituo cha  Afya cha Uzi na Ng'ambwa kimejengwa na Mradi Tasaf kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Zanzibar na Wananchi wa Uzi na Ng’ambwa ambacho kimegarimu zaidi ya Milioni mia tatu na sitini (360) hadi kukamilika ambacho kitatoa huduma za Afya kwa wananchi wa Uzi na Ng'ambwa.

 

Amesema kuwa kituo hicho kitotoa huduma  mbali mbali za matibabu ikiwemo ya Uzazi, matibabu ya meno, mama na mtoto na huduma za maabara ambazo zitatolewa kwa masaa 24 kwa wananchi wote.

 

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud amesema wananchi wa Uzi na Ng'ambwa wanaishukuru Serikali ya Awamu ya Nane (8) inayoongozwa na Rais wa Dkt Hussein Mwinyi  kwa kuwajengea kituo cha Afya ambacho kitawaondolea usumbufu wa kufuata huduma za Afya masafa ya mbali.

 

Amesema kuwa dhamira ya Dkt Mwinyi ni kukuza Uchumi kwa kujenga Misingi  Imara ya Kiuchumi ambayo itaendelea kuifungua Zanzibar kiuchumi hivyo ni lazima kuhakikisha anawawekea mazingira maziri wananchi wake ikiwemo upatikanaji wa huduma za afya kwa wakati na kwananchi wote bila ya kujali itikadi za aina yoyote.

 

Magazeti ya Tanzania Disemba 28, 2023

Mbunge Kyombo apongeza juhudi za wana Bwanjai ahaidi ushirikiano

$
0
0

Mbunge wa Jimbo la Nkenge Wilayani Misenyi Mkoani Kagera na Makamu Mwenyekiti wa kamati  ya kudumu ya Bunge ya utawala, Katiba na sheria Florent Kyombo amepongeza juhudi za wana Bwanjai zinazoonyesha maendeleo ya haraka na ya muda mfupi katika kata ya Bwanjai Wilayani humo.


Kyombo alitoa pongeza hizo baada ya kuona hatua kubwa ya maendeleo na mafanikio yaliyopatikana  kutokana na umoja huo wa Jumuiya ya Bwanjai (BWANJAI COMMUNITY ASSOCIATION) - BCA wakati akiwa Mgeni rasmi katika siku ya Bwanjai maarufu BWANJAI DAY ambayo hufanyika Desemba 27 ya kila mwaka.


Mbunge huyo amesema tangu kuanzishwa kwa Bwanjai Day 2015 wamepiga hatua za maendeleo ikiwa ni pamoja na kuboresha baadhi ya Barabara za vitongoji kwa kuweka vifusi, kuwepo mfuko wa Elimu uliosaidia kuwalipia Wanafunzi wasiokuwa na uwezo na kusomeshwa, ununuzi wa matenki mawili ya maji lita 5, 000 sawa na lita 7,000 katika shule ya Sekondari Bwanjai, utengenezaji wa madawati 162 viti 81 kupitia Bwanjai Day.


"Niwapongeze Wanabwanjai waishio ndani ya kata na nje ya kata ambao mmeonyesha ushirikiano na umoja hadi kufanikiwa haya niwaombe muendelee kushirikiana ili Bwanjai iwe ya mfano alisema Mbunge Kyombo".


Aidha aliahidi kuhakikisha anatoa ushirikiano wa kutosha na kukamilisha baadhi ya ahadi na kuwaomba Wanabwanjai kujikita katika vipaumbele ambavyo wamejipangia huku akisema fedha zinazotakiwa kutoka mfuko wa Jimbo ambazo ni shilingi Bilioni 7 zitawafikia ili kujenga Zahanati na nyingine kuongezwa kwenye umaliziaji wa Bweni la wasichana huku akiongeza kuwa atakaa Madiwani wa kata ya Bwanjai Phocus Rwegasira kama Baraza la Madiwani ili wahakikishe wanaingiza suala hilo kwenye bajeti na mwaka ujao wapate meza na viti.


Aidha akisoma Risala mbele ya Mgeni rasmi katibu wa BWANJAI COMMUNITY ASSOCIATION Mwl. Placidius  France alisema kuwa Viongozi na Wananchi waishio ndani na nje ya kata hiyo kwa ujumla walikaa kwa pamoja, kwa kushirikiana na kamati  ya maendeleo ya kata ambapo walibaini changamoto zilizopo katika maeneo yao na kuanzisha umoja huo ili kuzipatia ufumbuzi.


France amesema baada ya kuanzisha umoja huo waliweka vipaumbele vya kata ambavyo ni ujenzi wa Bweni la  wasichana shule ya Sekondari Bwanjai, ujenzi wa Ofisi ya kata, kuboresha vyanzo vya utalii vilivyopo, kujenga jengo la utawala Bwanjai Sekondari.


Katibu huyo alimuomba mbunge wa Jimbo la Nkenge Florent Kyombo kuwezesha mradi wa Bweni la wasichana shule ya Sekondari Bwanjai kukamilika haraka baada ya mradi huo kusuasua kwa michango ambayo inatolewa na kusababisha ujenzi wa mradi huo kutumia muda mrefu bila kukamilika.


Hata hivyo naye Diwani wa kata ya Bwanjai Phocus Rwegasira amesema kuwa kata hiyo imepiga hatua kubwa kutokana na ushirikiano wa Wanabwanjai na kuwa awali walikuwa hawana Katiba wala uongozi Ila sasa wamesajiliwa huku lengo lao kubwa likiwa ni kutoisubiri Serikali katika shughuli za maendeleo.


KIKUKWE DAY 2023 YANG'ARA

$
0
0

Na Lydia Lugakila,

Misenyi


KATIBU Tawala Wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera Mwanaidi Mohamed Mang'uro amepongeza sherehe za maadhimisho ya maendeleo ya kata ya Kanyigo kwa mwaka 2023 zilizofanyika katika kijiji cha Kikukwe maarufu -KIKUKWE DAY wilayani Misenyi Mkoani Kagera Desemba 27,2023 katika Uwanja wa shule ya Sekondari Kikukwe.



Mwanaidi amesema  kijiji hicho kumempa faraja kubwa  baada ya kuunda umoja wa maendeleo  unaofahamika kwa jina la moja wa maendeleo Kikukwe -UMKI ambao unaoonekana kuleta maendeleo makubwa katika kijijini hapo huku akiviomba vijiji vingine kuiga mfano kupitia kijiji hicho.


Katibu tawala huyo amewapongeza Wanakijiji hicho kwa kufanya maendeleo makubwa ikiwemo kushiriki ujenzi wa zahanati ya kata, kuleta walimu wa ziada katika shule nne za kijiji hicho na kuleta maji katika shule ya sekondari Kikukwe ambapo aliahidi kushiriki kikamilifu katika mipango yote ya maendeleo kwa mwaka 2024.


Naye Katibu wa umoja huo Bi Magreth Domisian alitaja kazi mbalimbali zilizofanywa na umoja huo ambazo  zilimfurahisha Katibu tawala, kuwa mwaka 2023 umoja huo ulichangia katika shughuli za ujenzi wa kituo cha afya cha kata Kanyigo, kuweka maji, kujenga Bweni la Wasichana na kutoa mashine za kudurufu nakala za mitihani katika shule ya sekondari ya Kikukwe, na kuleta Walimu wa ziada katika shule nne kijijijni hapo.


Aidha kijiji hicho kimeanzisha kilimo cha Parachichi, Vanilla pamoja na ndizi ambapo wameendaa Darasa la kilimo  ili Wanakijiji wapate Elimu ya kutosha kuhusu kilimo hicho.


Bi Magreth Ameongeza kwa mwaka 2024 wana mipango mingi ya ikiwemo kujenga maktaba, kumbi mbalimbali na ujenzi wa maduka ya jumla na mradi wa ujenzi tayari umenza lakini pia watawezesha michezo kwa wanafunzi pamoja kuendelea kuchangia katika kuwawezesha Wanafunzi katika Elimu kwa kutoa vitendea kazi kama vitabu na Walimu katika shule za kijiji hicho.


Aidha Mwenyekiti mhandisi Godfrey Mugini wa umoja wa huo amejivunia kuwa mmoja wa wanakijiji hicho kwani matarajio yao ni kijiji kuwa cha mfano wa kuigwa kwa vijiji vingine  huku akiiomba Serikali kutatua baadhi ya changamoto walizonazo ikiwemo miundo mbinu mibovu kama Barabara ya kutoka Gera kwenda mpakani mwa Uganda pamoja na uhitaji wa fedha ili kutimiza malengo ya umoja huo.


Nae Diwani wa kata ya Kanyigo amewapongeza wanakijiji hao kwani wamekuwa mfano mzuri kwa vijiji vingine kwenye kata hiyo huku akiahidi kupambana ili changamoto zinazojitokea zitatuliwe ili wanakijiji hao wafikie malengo yao.

MILIND SOMAN AWAITA WATANZANIA JUMAMOSI

$
0
0

Mkimbiaji mashuhuri kutoka India, Milind Soman (kulia), Balozi wa India anayemaliza muda wake  Binaya Srikanta Pradan (katikati), na Makamu wa Rais Riadha Tanzania (RT), William Kallaghe, wakionyesha fulana zitakazotumika The India-Tanzania Friendship Run.

 

NA TULLO CHAMBO, RT

 

'SUPER STAR' wa kimataifa kutoka India, Milind Soman, amewahimiza Watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio za urafiki kati ya India na Tanzania 'India-Tanzania Friendship Run' zinazotarajiwa kurindima Jumamosi Desemba 30.


Akizungumza na Waandishi wa habari kwenye Ubalozi wa India jijini Dar es Salaam leo Desemba 27, Soman, aliwasihi Watanzania kutumia michezo hususan kukimbia kama sehemu ya kuburudika huku wakijenga afya ya miili yao.


"Ujumbe wangu kwenu, naomba tujenge utamaduni wa kushirikisha ndugu, familia, jamii kufurahia, kusherehekea huku tukijenga afya," alisema Milind ambaye ana ushawishi mkubwa nchini India na kuwaomba Watanzania walianze hilo Jumamosi na Jumapili kwa kujiandisha kushiriki mbio hizo zitakazoanzia viwanja vya Farasi 'Green Park Grounds' Oysterbay jijini Dar es Salaam.


Mbio hizo zitakuwa na Kilomita 5, Kilomita 10 na zile ndefu maarufu kama 'Ultra Marathon' Kilomita 120 kutoka Dar es Salaam hadi Bagamoyo mkoani Pwani na kurejea Dar es Salaam, ambazo ndizo Soman atashiriki.


Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT/AT), William Kallaghe, alisema wamefarijika kushirikishwa na Serikali zote mbili, Tanzania na India, katika tukio hilo la kihistoria.

Kallaghe, alisema RT inashiriki katika upande wa kiufundi na kwamba tukio hilo ni la kwanza kufanyika nchini chini ya usimamizi wa shirikisho.


"Kwa ujio wa tukio hili tuna promote Ultra Marathon nchini, tunazipongeza Serikali zote mbili kwa kufanikisha tukio hili ambalo linaimarisha ushirikiano wa Tanzania na India na kuhamasisha mchezo wetu wa Riadha," alisema Kallaghe na kuongeza.


Haya ni matokeo ya ziara ya Rais Samia Saluhu Hassan nchini India Oktoba mwaka huu na ana matumaini dirisha zaidi la ushirikiano kwa tukio hilo kuwa endelevu na nafasi ya wanariadha kwenda India na India kuja Tanzania, pia ni sehemu ya kutangaza vivutio vya utalii nchini.


Naye aliwasisitiza washiriki kujitokeza kwa wingi kujisajili kushiriki mbio hizo, ambapo usajili ni bure kabisa.


Alibainisha kuwa, ratiba inaanza saa 11 alfajiri Jumamosi kwa mbio za Kilomita 5 na 10, kisha Milind Soman akiungana na wanariadha wengine wa Tanzania wataanza ile mbio ndefu Dar- Bagamoyo Kilomita 60 ambako watapumzika na kesho yake Jumapili watarejea tena viwanja vya Farasi jijini Dar es Salaam Kilomita 60, kutakapokuwa na sherehe kubwa ikipambwa na Msanii Darasa.


Milindi Soman, katika maisha yake ameshiriki marathon zaidi ya 100, amewahi kuwa mshindi wa mashindano ya kuogelea kwa miaka minne nchini India, ni mwanamitindo, mtu wa mazoezi ya viungo na mcheza filamu.


Mbali na kufanikiwa kuishawishi familia yake, mke, watoto wake na mama yake mzazi kushiriki mbio, ana ushawishi mkubwa nchini kwa jamii kuishi kwa utamaduni wa kufanya mazoezi ili kujenga utimamu wa mwili.

Waziri Silaa awapiga Marufuku Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Vijiji kujihusisha Uuzaji Viwanja

$
0
0

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa ameagiza Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Vijiji kote nchini kutojihusisha na mauzo ya viwanja na vipande vya ardhi.

Aidha ameweka wazi kuwa watakaohusika ni maofisa ardhi kwa kushirikiana na kampuni za upangaji na upimaji wa ardhi kwenye maeneo na miji husika huku akipiga marufuku wananchi kutonunua maeneo ya ardhi ambayo hayajapimwa au kupangwa na Serikali.

Waziri Silaa ameyasema hayo alipokuwa akitoa  tathmini ya siku 100 za utekelezaji tangu alipoteuliwa kushika wadhifa wa Waziri mwenye dhamana na masuala ya ardhi kupitia mkutano wa Jukwaa la Wahariri (TEF) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

"Kwa wale wanaokwenda kununua viwanja vijijini hakikisha umeitishwa mkutano wa kijiji kwa ajili ya kujadiliwa na kutolewa uamuzi wa kupewa ardhi na ikiwezekana tumia simu kurekodi kwa kukubaliwa kupewa hilo eneo," amesema Silaa.

Waziri Silaa amewasisitiza Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa Mikoa kuwa wana kazi ya kusimamia watumishi walio chini yao kwa kujipanga vizuri na wana uwezo kubadilisha jinsi sekta ya ardhi inavyoendeshwa nchini kote.

 

Waziri Silaa ameongeza kuwa Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wanachapa kazi vizuri katika mikoa yote, utendaji kazi wao utafanya taswira ya Wizara iende mbele kutekeleza maelekezo ya viongozi wa kifaifa na kuleta tija kwa watanzania.

 

Aidha, Waziri Silaa amesema wizara yake itaendelea kushirikiana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na wataendelea kupokea na kuheshimu ushauri wanaoutoa kuhusu shughuli za sekta ya ardhi nchini.

 

Awali akimkaribisha Waziri kwenye kikao hicho, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Anthony Sanga amesema kuwa Menejimenti ya Wizara na taasisi zilizochini ya Wizara kwa kushirikiana na Makamishna Wasaidiza wa mikoa wapo tayari kupokea maelekezo ya Mhe. Waziri kwa kuwa ndiye mwongoza njia ili kufikia malengo ya Serikali ya kuwahudumia wananchi katika sekta ya Ardhi.

 

Waziri Silaa ametimiza siku 100 katika nafasi hiyo ambayo Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Agosti 30, 2023 na kuapishwa Septemba 01, 2023.



M/KITI KAWAIDA: MATEMBEZI YA MIAKA 60 YA MAPINDUZI YAMEIBUA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA PEMBA

$
0
0

NA IS-HAKA OMAR, PEMBA

 

MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) Taifa Mohamed Ali Kawaida,amesema Umoja huo unaimarisha mazingira bora ya makaazi ya watendaji wake yaendane na hadhi ya taasisi hiyo.

 

Hayo ameyasema wakati akizungumza na maelfu ya vijana wa UVCCM wanaofanya Matembezi ya kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar  mara baada ya kushiriki ujenzi wa Taifa katika mradi wa ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UVCCM Mkoa wa Kusini Pemba.

 

Alisema mradi huo unaendana na dhamira ya UVCCM kwa kuhakikisha kila mtendaji anafanya kazi zake akiwa katika makaazi bora.

 

"Tukio hili la ushiriki wa ujenzi wa Taifa limeshirikisha Vijana kutoka Mikoa yote ya Tanzania, ambapo imeacha alama kwa kuanzisha mradi wenye manufaa makubwa katika maisha ya kila siku ya Watendaji wetu",alisema Kawaida.

 

Katika maelezo yake Kawaida, alisema UVCCM inaendelea kubuni na kuibua fursa za kimaendeleo ili vijana wote wanufaike.

 

Alieleza kuwa miaka 60 ya Mapinduzi ni chachu ya kuendeleza mambo mema yaliyotekelezwa na waasisi wa Mapinduzi hayo yaweze kutekelezwa kwa kufuata mahitaji ya Vijana wa sasa katika nyanja za kiuchumi,kisiasa na kimaendeleo.

 

Pamoja na hayo aliwapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi kwa utekelezaji kwa ufanisi Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 Mijini na Vijijinj.

 

Matembezi hayo yanayowashirikisha Vijana 1000 kutoka Mikoa yote ya Tanzania yamezinduliwa Disemba 28,mwaka 2023 katika Mkoa wa Kusini na leo Disemba 29,mwaka huu yanaendelea Mkoa wa Kaskazini Pemba.

 

CAPTIONS

Picha no.001-MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mohamed Ali Kawaida,akishiriki ujenzi wa Taifa katika mradi wa Ujenzi wa Nyumba ya Katibu wa UVCCM Mkoa wa Kusini Pemba,katika Matembezi ya kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi.

Picha no.003-Vijana wa kikundi Maalum cha kubeba picha za Waasisi wa Mapinduzi na Viongozi wa sasa waliopo madarakani ambao ni aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Abeid Aman Karume,aliyekuwa Rais wa kwanza wa Tanzania Mwl.Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi.

Picha no.005-BAADHI ya Vijana wa UVCCM wakishiriki kazi mballimbali za ujenzi wa Taifa katika mradi wa Nyumba ya Katibu wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Kusini Unguja.

Picha no.006,007-BAADHI ya Vijana wakitembea kwa ukakamavu katika matembezi hayo kutoka Mkoa wa Kusini Pemba kuelekea Kaskazini Pemba.

Picha no.004-VIONGOZI wa Matembezi hayo wakitembea kwa ukakamavu kutoka Mkoa wa Kusini Pemba kwenda Kaskazini Pemba.

 

MEXIME ATUA KWA WANA MOOGO MAJI IHEFU FC

$
0
0

 

Na John Marwa


UONGOZI wa Klabu ya   Ihefu umemtambulisha rasmi kocho,  Mecky Maxime kukinoa kikosi cha timu hiyo kuanzia mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.




Mecky ametambulishwa rasmi kupokea mikoba ya aliyekuwa kocha wa Ihefu FC,  Mganda Mosses Basena aliyefungishiwa virango vyake baada ya uongozi kutoridhishwa na matokeo ya timu yao.


Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Zagalu Chalamila amesema Mecky ni Kocha mkubwa ndani ya Tanzania na mzoefu kisoka kwa ngazi ya klabu na timu ya Taifa.



“Kuanzia sasa kikosi cha timu yetu katika mashindano yote yaliyopo mbele yetu, hatukufanya vizuri mzunguko wa kwanza lakini tunaimani duru la pili tutaenda kufanya vizuri katika michezo iliyopo mbele yetu,” amesema Chalamila 


Aliongeza kuwa wanafahamu ubora wa kocha huyo na suala la usajili wa dirisha dogo wamelikabidhi kwake kwa sababu ameiona timu hiyo na kuona mapungufu ya kikosi chake.


Chalamila amesema wamejipanga vizuri katika masuala ya usajili na wako kwenye mchakato wa kuimarisha timu yao kwa kushirikiana na kocha wao Mecky.

Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>