Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

RAIS MSTAAFU DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE AONGOZA BODI YA WAKURUGENZI WA GPE KUTEMBELEA SKULI VISIWANI ZANZIBAR LEO

$
0
0

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Makamu Mwenyekiti wake Susan Liautaud na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bibi Laura Frigenti, wakilakiwa kwa  burudani waliopowasili skuli ya Maandalizi ya Awali  ya Kikaangoni Wilaya ya Magharibi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Makamu Mwenyekiti wake Bi Susan Liautaud (mwenye barakoa) na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali  Mhe Lela Mohamed Mussa (kushoto kwa Dkt Kikwete)  wakiangalia wanafunzi  katika  darasa la skuli ya Maandalizi ya Awali  ya Kikaangoni Wilaya ya Magharibi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na  na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bibi Laura Frigenti, wakifurahia mchoro wa mwanafunzi katika skuli ya Maandalizi ya Awali ya Kikaangoni Wilaya ya Maagharibi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Makamu Mwenyekiti wake Bi Susan Liautaud (mwenye barakoa) wakiwa na mototo wa mmoja wa wazazi wa watoto wanaosoma skuli ya Maandalizi ya Awali  ya Kikaangoni Wilaya ya Maagharibi.

 

 

Na Mwandishi Maalumu

 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Makamu Mwenyekiti wake Susan Liautaud na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bibi Laura Frigenti, leo wametembelea na kukagua skuli zinazopata ufadhili na shirika hilo.

 

Katika ziara ya leo ujumbe huo mzito wa GPE ulitembelea na kukagua skuli ya Maandalizi ya ya Kikaangoni  pamoja na Skuli ya msingi ya Kisiwandui, ukiwa umeongozana na wenyeji wao Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe Lela Mohamed Mussa,  na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi,  Mhe Suzan Peter Kunambi.

 

Huo ni mwendelezo wa ziara ya viongozi na wajumbe wa bodi ya GPE kutembelea miradi mbalimbali yya bara na visiwani kabla Dkt. Kikwete, akiwa mwenyekiti wa Bodi hio ataongoza vikao vya Shirika hilo hapa Zanzibar kuanzia leo  4 hadi 6 Disemba, hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kwa Shirika hilo la kimataifa kufanya vikao vyake vya bodi barani Afrika na nje ya Marekani na Ulaya.

 

GPE iliyoanzishwa mwaka wa 2002, ni Shirika lililoundwa na mataifa Tajiri duniani ya G& na linasimamiwa na Benki ya Dunia, kufadhili maendeleo ya  elimu katika nchi zinazoendelea.

 

Majukumu ya GPE ni pamoja na  kusaidia serikali za nchi zinazoendelea kufanya mabadiliko ya kimfumo na kuoanisha rasilimali na ufadhili ili kutoa elimu bora kwa watoto Wote, kuinua viwango vya kujifunza na kukabiliana na changamoto mpya nchini.

 

 Kwa mujibu wa Dkt. Kikwete, ambaye ni Mwafrika wa kwanza kuongoza GPE, shirika hilo hadi sasa limeishaipatia Tanzania jumla ya  Dola za Kimarekani Milioni 332 (takriban shilingi 834,980,332,000.00) ili kusaidia sekta ya elimu bara na visiwani.

 

Majuzi GPE imetiliana saini na Serikali ya makubaliano ya kutoa dola za Kimarekani milioni 85 (takriban shilingi 213, 775, 085, 000.0)    kwa ajili ya kusaidia mafunzo ya  walimu nchini.



Rais Samia ashiriki Mkutano wa Kilimo UAE

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye Mkutano wa Afya unaohusu magonjwa yasiopewa kipaumbele, Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) tarehe 03 Desemba, 2023.

Mawaziri na Wakuu wa Taasisi mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano wa Kilimo unaojadili fursa za Uwekezaji na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi pembezoni mwa Mkutano wa (COP28) unaofanyika Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) tarehe 03 Desemba, 2023.

Baadhi ya Viongozi na Wakuu wa Taasisi mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano wa Kilimo unaojadili fursa za Uwekezaji na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi pembezoni mwa Mkutano wa (COP28) unaofanyika Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) tarehe 03 Desemba, 2023.

TUNAFUATILIA UADILIFU KATIKA UTOAJI HUDUMA ZA ARDHI- MHE PINDA

$
0
0

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda akizungumza katika Kongamano la masuala ya Ardhi Tanzania tarehe 4 Desemba 2023 mkoani Morogoro.

 

Na Munir Shemweta, WANMM MOROGORO

 

 

Serikali inaendelea kusimamia ufuatiliaji wa tathmini katika utekelezaji wa majukumu ya Sekta ya Ardhi na uadilifu katika utoaji wa huduma za Ardhi nchini. 

 

 

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda tarehe Desemba 2023 mkoani Morogoro wakati akifungua kongamano la masuala ya Ardhi nchini.

 

 

Amesema, hatua muhimu za kinidhamu na ufuatiliaji zilizochukuliwa na wizara yake ni pamoja na kuboresha mifumo ya TEHAMA ili kuongeza ufanisi tija na uwazi katika utoaji wa huduma.

 

 

Kwa mujibu wa Mhe Pinda, hatua nyingine ni kusimamia uadilifu kupitia vikao vya Kamati za Kudhibiti Uadilifu ili kujadili na kuishauri Wizara kuhusu masuala ya uadilifu katika utendaji kazi, kwa kupitia kamati za nidhamu.

 

‘’Kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali imewachukulia hatua za kinidhamu watumishi wanaokiuka maadaili ya kazi ambapo 12 wamefukuzwa kazi, watumishi nane (8) wameshushwa ngazi ya mishahara, watumishi wawili (2) wamepewa onyo na watumishi watano (5) wameshushwa vyeo lengo la hatua hizo ni kuongeza ufanisi katika kazi na kulinda haki za wananchi’’. Alisema Mhe. Pinda.

 

 

Hata hivyo, Naibu Waziri Pinda aliwaambia washiriki wa kongamano hilo la siku mbili lililobeba ujembe wa Usalama wa Milki za Ardhi kwa Uhakika wa Chakula kuwa, serikali itahakikisha wananchi wanapata haki zao za msingi za umiliki wa ardhi na makazi.


‘’Tunafahamu Watanzania walio wengi na ambao ni maskini wanaishi vijijini na Wizara ina dhamana ya kusimamia eneo hili, kama Wizara tutajitahidi kwa kadri na uwezo wetu na kuendelea kushirikiana na wadau wetu na Wananchi wote kuhakikisha nyaraka rasmi za umiliki ardhi na makazi zinatolewa na kuendelea kukabiliana na changamoto zilizopo nchini kuhusu migogoro ya ardhi’’. Alisema Pinda.

 


Amewaomba wananchi kuendelea kutii Sheria na taratibu zilizowekwa za umiliki wa ardhi na makazi na kuahidi kuwa taarifa itakayotokana na majadiliano ya kongamano hilo wataifanyia kazi.

 

 

Awali Mratibu wa Kogamano hilo lililoandaliwa na Jukwaa la Ardhi Tanzania (TALA) Benard Baha amesema Jukwaa la Ardhi Tanzania ni jukwaa linaundwa na wanachama wanaowakilisha makundi mbalimbali ya kijamii kama vile wakulima, vijana pamoja na wafugaji wanaotegemea zaidi ardhi katika kuendesha maisha yao.


Amewataja baadhi ya wanachama hao kuwa ni pamoja na HAKIARDHI, Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania, Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania, Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu.

 

 

‘’Jukwaa pia ni mwenyeji wa mashirika wanachama wa Jukwaa la Ardhi la Kimataifa linalojumuisha taasisi za ndani na za kimataifa zinazofanya kazi zake nchini  ambapo TALA imepewa jukumu la kuratibu utendaji kazi wa taasissi hizo kwa namna inavyoshirikisha jamii’’. Alisema Baha.

 

 

Mratibu huyo wa Jukwaa la Ardhi Tanzania amefafanua kuwa, kumekuwa na utatamaduni wa kukutanisha wadau kujadili na kutafakari masuala mbalimbali kuhusu milki na utawala wa ardhi pamoja na tathmini katika masuala ya sekta ya ardhi utamaduni alioueleza kuwa, unatoa mwanya wa kusikiliza taarifa za kitafiti, maelezo na ushuhuda kutoka kwa wananchi suala lilalotoa fursa kwa jukwaa hilo kutoa mapendekezo kwa serikali juu ya maeneo yanayohitaji maboresho.

 

WAZIRI MKUU AWASILI KATESH, ATOA POLE AENDA KUKAGUA ENEO LA TUKIO

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasili wilaya ya Hanang mkoani Manyara na kukutana viongozi wa mkoa huo na wa Serikali na kupokea taarifa ya hali halisi ya tukio la maafa lililotokea jana na kusababisha vifo na majeruhi.

 

Waziri Mkuu alitoa pole kwa viongozi na wananchi wa Hanang kwenye kikao kilichofanyika leo (Jumatatu, Desemba 4, 2023) kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, vyombo vua ulinzi na usalama na Watendaji wa taasisi za Serikali.

 

Waziri Mkuu amesema tukio la jana linafanana na tukio jingine lililowahi kutokea mwaka 1990 katika eneo la Ndanda ambako mlima uliporomoka na kusomba nyumba na barabara, hali ambayo ilisababisha vifo na majeruhi.

 

Amezishukuru Kamati za Maafa za Wilaya na Mkoa ambazo zilianza kuchukua hatua za uokoaji tangu jana, lakini pia mawaziri na watendaji wao ambao walikuja kutoa msaada kwa kuungana na viongozi wa mkoa wa Manyara.

 

Amesema matibabu yanaendelea kutolewa kwa majeruhi ambapo timu ya madaktari bingwa kutoka Dodoma, Singida na Arusha imeungana na kuanza kutoa huduma za upasuaji kwa wagonjwa watatu waliovunjika mifupa.

 

Amesema majeneza yameagizwa kutoka Babati na Singida ili ndugu waliotambuliwa waweze kuhifadhiwa kwenye nyumba zao za milele.

 

Hivi sasa, Waziri Mkuu na baadhi ya mawaziri wamekwenda kukagua eneo la Mlima Hanang kwa kutumia helikopta. Eneo hilo ndiko maporomoko ya udongo yalianzia. Baadaye atashiriki kuaga miili ya marehemu na ndipo taarifa rasmi itatolewa.

 

Tume ya Tehama yapeleka wabunifu 7 kongamano la Afrika

$
0
0
Na Mwandishi Wetu

 

KATIKA kuhakikisha inakuza ubunifu kwa kampuni changa za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) nchini, Tume ya Tehama (ICTC) imefanikisha safari ya wabunifu saba kwenda Algiers, Algeria kushiriki katika kongamano la kimataifa la Tehama barani Afrika litakaloshirikisha zaidi ya mataifa 50 kuanzia leo.

Kwa kushiriki katika kongamano hilo la siku tatu, wabunifu hao wa Kitanzania watapata fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutangaza kazi zao, kukutana na wataalamu wengine wa Tehama kutoka sehemu mbalimbali duniani ambako wanatarajiwa kujifunza kuelekea katika ukuaji wao kisekta.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama, Dkt. Nkundwe Mwasaga, akizungumza jana jijini Dar es Salaam, alisema kwa Tume na taifa kwa ujumla, kongamano na maonesho hayo ni faida kubwa kwa nchi kwani vitasaidia kukuza na kuvutia uwekezaji wa Tehama nchini.

“Hiyo ni hatua kubwa kwetu kama Tume ya Tehama lakini pia kwa nchi. Haya ni matunda ya uratibu wa programu ya kukuza kampuni changa za TEHAMA (ICT Startups) ili kuwezesha bidhaa za TEHAMA kuingia katika soko na kuchangia katika kukuza uchumi na kutengeneza ajira kwa vijana. Tume imewezesha kampuni changa kadhaa kuanza kutoa huduma,” alisema.

Kwa mujibu wa Dkt. Mwasaga, ushiriki katika kongamano hilo kubwa Afrika umewezeshwa na ICTC. Ameishukuru Serikali chini ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipa nguvu sekta ya tehama katika mpango wa kujenga uchumi wa kidigitali, kwani umechangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha safari ya wabunifu hao.

Katika kongamano hilo linalotarajiwa kuhudhuriwa na wabunifu 500, watazamaji zaidi ya 10,000, wawekezaji 200, wabobezi katika sekta ya tehama wapatao 100, kampuni za Tanzania zinazotarajiwa kushiriki ni Ngasmake (Lipa kwa Ngasmake (Lipa kwa Uhakika), Niajiri, Neuro-Sarufi AI, Simplitech, Mipango App, Scancode na Settlo. Benki ya CRDB iliyoingia makubaliano na Tume ya Tehama kuendeleza Wabunifu wa Kampuni ndogondogo za TEHAMA kupitia programu ya Imbeju, pia ni sehemu ya washiriki.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa Tume ya Tehama ambaye yuko Algeria na wabunifu hao, Jasson Ndanguzi aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu, akizungumzia manufaa ya ICTC kushiriki katika kongamano na maonesho hayo, alisema ni pamoja na kusaidia kuvutia na kuongeza fursa za uwekezaji mitaji katika kampuni bunifu za TEHAMA nchini.

“Pia kuna fursa ya kuongeza ujuzi wa programu za uanzishwaji wa vituo vya bunifu za TEHAMA nchini kwa kujifunza kutoka nchi zingine zinazoshiriki kongamano hilo, kupata washirika wa kuendesha programu za ubunifu wa kidijitali na kukuza soko la bidhaa za TEHAMA zinazotokana na bunifu za TEHAMA ili kukuza pato la taifa lakini pia kutangaza nafasi ya Tanzania katika uwanda wa masuala ya bunifu za kidijitali.

“Na zaidi ya yote, ni fursa ya kuzitangaza kampuni changa zenye bunifu za TEHAMA ili ziweze kupata mitaji au/na washirika wa biashara nje ya mipaka ya Tanzania kama moja ya mkakati ya kukuza matumizi ya bunifu za TEHAMA nje ya nchi na hatimaye kuongeza pato la fedha za kigeni,” alisema Ndanguzi.

Ukuzaji na kuvutia uwekezaji ni moja ya majukumu ya Tume ya Tehama inayotekeleza Sera ya Taifa ya Tehama pamoja na sera nyingine zinazohusiana na kuendeleza matumizi ya tehama, lengo likiwa kutengeneza ajira na kuchangia katika shughuli za kiuchumi na kijamii, huku ikiimarisha uratibu wa shughuli za Tehama ili kuongeza mchango wa sekta husika katika uchumi wa taifa.

Tume, kwa sasa inaelekeza nguvu katika kuanzisha vituo vya ubunifu wa Tehama kote nchini, ikianza na mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Dodoma, Tanga, Mbeya, Lindi na Zanzibar, lengo likiwa kusogeza huduma karibu na wananchi, hasa ikizingatiwa kumekuwa na ongezeko la uhitaji wa matumizi ya Teknolojia kwenye uchumi wa Tanzania.

 

Ends

 

TTCL YANOGESHA 'TWENZETU KILELENI2023'

$
0
0


Na Andrew Chale, Kilimanjaro

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limetoa huduma ya bure ya intaneti kwa washiriki watakaopanda mlima Kilimanjaro katika kipindi cha kampeni ya twenzetu Kileleni2023 ambao ni msimu wa tatu.



Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari Mjini Moshi, Kilimanjaro, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, John Yahaya Amesema TTCL wanaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha umoja na mshikamano ndani ya nchi yetu, katika kukuza sekta ya utalii sambamba na kuimarisha mawasiliano nchini.

Amesema:
"Washiriki wote watakaopanda mlima Kilimanjaro, katika kipindi hiki cha kampeni ya twenzetu kileleni, watapata fursa hiyo ya intaneti bure wafikapo kila kituo katika mlima huo, ili kutambua umuhimu wa maadhimisho haya ya miaka 62 ya uhuru wa nchi yetu,

Amesema uwepo wa huduma hiyo ya intaneti, itakuwa ni fursa ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika hifadhi ya mlima wetu, ndani na nje ya nchi yetu, lakini itahamasisha Watanzania kujenga mazoea ya kutembelea vivutio vya mlima Kilimanjaro na maeneo mengine ya utalii.

Ambapo washiriki zaidi ya 200 watakaopanda mlima huo kwa ushirikiano wa TANAPA na Kampuni ya ZARA tours ambao wanapanda Desemba 5, asubuhi.

Aidha, Amesema kuwa, Shirika hilo limeendelea kutekeleza mkakati wake wa kuimarisha mawasiliano kwa kuhakikisha kunakuwepo na miundombinu ya kisasa na yenye uwezo mkubwa katika kutoa huduma ndani na nje.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Shirika ka Hifadhi za Taifa (TANAPA), Jenerali Mstaafu, George Waitara amewataka Watanzania kujivunia mlima huo kwa kutumia fursa mbalimbali zilizopo  hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanganyika.

Ambapo Amebainisha kuwa, kusherekea uhuru zilianza mwaka 2008 na sasa ni miaka 15 imepita, huku kila mwaka kukiwa na mwitikio mkubwa.

Aidha,Waitara amesema Wasiachie wageni wa nje kuja kuutangaza mlima hivyo kuwataka Watanzania wenyewe kuutangaza mlima huo.


Kwa upande wake Ibrahim Jama aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Makampuni ya utalii ya Zara tours, amesema zaidi ya watu 200 wanapanda mlima huo kupitia ZARA kutoka katika mashirika na taasisi mbalimbali.

"Tutakuwa na Mabalozi 17,
Lakini pia Mashirika mengine mbalimbali yamehamasika na wanashiriki msimu huu wa tatu wa Twenzetu Kileleni2023."Amesema Ibrahim .


NMB yang’ara Tuzo za Mwajiri Bora mwaka 2023

$
0
0

Na Mwandishi Wetu

Benki ya NMB imenyakua tuzo nne kwenye shindano la mwaka huu la Mwajiri Bora wa Mwaka (EYA 2023), ukiwemo ushindi wa pili kwenye mshindi jumla wa tuzo hizo zilizoandaliwa jana jijini Dar es Salaam na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).

Tuzo nyingine ilizoshinda benki hiyo ni za mshindi wa pili wa Sekta Binafsi, wa kwanza katika Ubora, Tija na Ubunifu, na wa kwanza pia kwenye Masuala ya Usawa wa Kinjinsia.

Hii ni mara ya pili mfululizo kwa benki hiyo kung’ara kwenye tuzo hizo za kila mwaka baada yakutangazwa kuwa Mwajiri Bora wa Mwaka 2022 na kushinda tuzo nyingine mbili kutokana na ubora wake wa kibiashara na katika usimamizi wa rasilimali watu.

Tangu mwaka 2005, ATE imezitumia tuzo hizi kuyahamasisha na kuyatunuku mashirika yanayozingatia maslahi na maendeleo ya watumishi katika shughuli zake. Waajiri wamekuwa pia wakitambuliwa kwa kuwa na sera zinazozingatia ushindani wa kitaasisi, ubora wa kitija pamoja na uwepo wa amani na utulivu sehemu za kazi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mkuu wa Rasilimali Watu wa NMB, Bw Emmanuel Akonaay, alisema tuzo za ATE walizoshinda ni miongoni mwa tuzo nyingi za ufanisi na ubora za kitaifa na kimataifa ambazo imezinyakua NMB mpaka sasa mwaka huu.

Kiongozi huyo aliongeza kuwa tuzo hizo pamoja na ufanisi wa utendaji kifedha uliopatikana mwaka huu hususani faida kubwa iliyopatikana umeufanya mwaka 2023 kuwa mwaka mwingine wa mafanikio makubwa kwa benki hiyo kubwa kuliko taasisi zote za fedha nchini.

“Tuzo hizi pia ni ishara kuwa imani kubwa kwa Benki yetu sio tu kwa wateja wetu lakini zaidi kwa wafanyakazi waliopambana mpaka kufikia hatua hii kubwa ya mafanikio. Wafanyakazi wetu wana imani kubwa na sisi, wanaupendo na Benki yetu na ndio maana wanafanya kazi kwa juhudi kubwa mpaka kunatunukiwa tuzo hizi,” Bw Akonaay alibainisha.

Aidha, alisema hivi karibuni benki hiyo pia ilitunukiwa tuzo ya mlipa kodi mkubwa nchini na ile ya taasisi inayoongoza kwa kuzingatia misingi na kanuni bora za ulipaji kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

“Hii inathibitisha namna ambavyo Benki ya NMB inashirikiana vyema na Serikali pamoja na mashirika yake,” Bw Akonaay aliwaambia waliohudhuria shughuli hiyo akiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu), Prof Joyce Ndarichako, aliyemwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Pia Bw Akonaay alisema NMB imenufaika sana na tuzo hizo za ATE hasa katika kuihamasisha kuwekeza zaidi katika kuwaendeleza wafanyakazi wake na kuweka mazingira rafiki ya kazi kama inavyoelekeza Serikali.

Aliongeza kuwa NMB si tu ina wafanyakazi wengi bali pia inazingatia usawa wa kijinsia kazini ambapo kwa sasa wanawake ni asilimia 48 ya wafanyakazi wake wote huku wanaume wakiwa ni asilimia 52.

NMB Yapokea Tuzo Nne za Mwajiri Bora Tanzania 🏆

$
0
0

Mafanikio makubwa tunayoendelea kuyapata yanatokana na bidii pamoja na ueledi wa wafanyakazi wetu na tunafuraha kutambulika kama Mwajiri Bora nchini Tanzania katika Tuzo zilizotolewa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) - 2023 jana jijini Dar es Salaam.



Tuzo hizo ni:

✅ Mwajiri Bora anaezingatia Ubora, Uzalishaji na Ubunifu Pahala pa Kazi 2023

✅ Mwajiri Bora anaezingatia Usawa wa Kijinsia na Usawa katika Uwakilishi Pahala pa Kazi 2023

✅ Mwajiri Bora wa Jumla (Mshindi wa Pili) kwa Sekta Binafsi kwa Mwaka 2023

✅ Mwajiri Bora wa Jumla (Mshindi wa pili) kwa mwaka 2023.

Tuzo hizo kwa ujumla wake zinatambua weledi wa benki yetu katika kufata misingi bora ya utumishi huku tukiwajengea wafanyakazi wetu mazingira wezeshi ya kiutendaji.

Tuzo hizi zimetolea na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) - Prof. Joyce Ndalichako aliyemuwakilisha Waziri Mkuu - Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na zimepokelewa na Afisa Mkuu wetu wa Rasilimali Watu - Emmanuel Akonaay pamoja na Mkuu wetu wa Idara ya Rasilimali Watu - Joanitha Rwegasira Mrengo, walioambatana na wafanyakazi wengine.

Tunawashukuru wafanyakazi wetu kwa kuendelea kuwa msingi wa mafanikio yetu.


MCB yaleta Kapu la MwalimuSanta sokoni

$
0
0

  Meneja Masoko wa Mwalimu Commercial Bank (MCB), Anna Mbajo akizungumza jijini Dar es Salaam leo, kuhusu Kapu la MwalimuSanta katika msimu huu wa Sikukuu. Kushoto ni Elilumba Kinyau kutoka Idara ya Huduma za Kibenki za Kigitali. 

Elilumba Kinyau kutoka Idara ya Huduma za Kibenki za Kigitali Mwalimu Commercial Bank, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza promosheni ya Kapu la MwalimuSanta inaypoendeshwa na benki hiyo.


Na Francis Dande

BENKI ya Mwalimu (MCB), imezindua kampeni ya Kapu la MwalimuSanta ili kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka na kugawa zawadi mbalimbali kwa wateja wake.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kapu la MwalimuSanta, Meneja Masoko wa MCB, Hannah Mbajo amesema uongozi wa  benki hiyo umedhamiria kurudisha shukrani kwa wateja wake.

Mbajo alisema Kapu la MwalimuSanta limebeba bidhaa muhimu kwa wastaafu watarajiwa na waliostaafu tayari ambao watawekeza fedha zao kwa faida ya asilimia 12 kwa mwaka na kupata bila malipo bima ya nyumba na samani za ndani.

"Wastaafu wengi wanakwama kwenye biashara sababu hawana uzoefu, sisi MCB tumekuja na suluhu ya mafao yao ya kustaafu. Watuamini tuwawekee fedha hizo wakiwa na uhakika wa kupata faida kila mwisho wa mwezi au mwisho wa mwaka.

"...Kapu la MwalimuSanta halikuishia hapo likaendelea kwa kuwalipia wastaafu bima ya nyumba kama anayo ama samani zote za ndani.

"Sote tunaona hivi sasa majanga mbalimbali yameongezeka kuna moto, mafuriko kama kule Manyara na hii ni kwasababu ya mabadiliko ya tabianchi hivyo tunamkinga mstaafu wetu na majanga ya aina yoyote," alisema Mbajo.

Akifafanua zaidi Mbajo alisema MCB ni sehemu salama kabisa kuwekeza kwa wastaafu ambao wanaweza kuchukua fedha zao wakati wowote huku wakijihakikishia usalama wa mali zao kwa kupatiwa bima.

Alisema Kapu la MwalimuSanta linamruhusu mstaafu aliyewekeza fedha zake MCB kukopa asilimia 80 ya fedha alizowekeza kupitia mkopo wa 'Mlinde Mstaafu'.

Akizungumzia bidhaa nyingine iliyopo kwenye Kapu la MwalimuSanta, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kidigitali cha MCB, Elilumba Kinyau alisema kapu hilo pia linagawa zawadi hadi sh. 50,000 kwa wateja wake watakaofanya muamala wa kiwango chochote bila kadi kupitia kwa wakala.

"Hii ni zawadi kwa wateja wetu watano kila wiki kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka mteja akitoa hela bila kadi kwa wakala wa MCB popote alipo atajipatia fedha taslim hadi sh 50,000 hapohapo," alisema Kinyau.

Alisema MCB ina mawakala zaidi ya 500 nchi nzima na huduma za benki kiganjani.


MADINI NI UTAJIRI....KAZI IENDELEEE

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali (aliyechuchumaa) akipokea maelekezo kutoka kwa Waziri wa Madini, Anthony Mavunde. Kazi Iendelee.

WEKEZENI KATIKA MIRADI YA UZALISHAJI KUKUZA AJIRA; MHANDISI. CYPRIAN LUHEMEJA

$
0
0

 

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

 

KATIBU Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja, ameelekeza Menejimenti ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kuendelea kuwekeza kwenye miradi ya uzalishaji ili kuchochea uchumi na fursa za ajira nchini.

 

Mhandisi Luhemeja amesema hayo, alipofanya ziara ya kiutendaji katika Ofisi ndogo za Makao Makuu ya PSSSF, jijini Dar es Salaam, ambapo, pamoja na kujionea shughuli za utoaji huduma, pia alipata fursa ya kuzungumza na Menejimengti ya Mfuko huo ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, CPA. Hosea Kashimba.

 

“Kuna kundi la vijana, kundi ambalo halina matumaini, zamani wahitimu wa chuo kikuu walikutana na ajira, lakini sasa hivi hali hiyo ni tofauti kidogo.” Alifafanua.

 

Alisema, PSSSF ni Mfuko mkubwa, hivyo una jukumu la kuwasaidia wastaafu, lakini pia kujenga mazingira ya kuwawezesha wastaafu wengi siku za usoni.

 

“Fungueni viwanda vingi, vitasaidia kutengeneza ajira kwa vijana,  unaposaidia watu wengi na wewe unajisaidia.” Alifafanua.

 

Pia ameelekeza Menejimenti ya PSSSF, kuendelea kutoa elimu kwa umma, ili wananchi waweze kufahamu kazi kubwa ambayo imefanyika toka kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii ya PSPF, PPF, GEPF na LAPF na kuanzishwa PSSSF.

 

"Kazi kubwa na nzuri imefanyika kwa kipindi cha miaka mitano toka kuunganishwa kwa Mifuko, utendaji umeboreshwa kwa kiasi kikubwa, ni muhimu watanzania waweze kuelewa kazi ambayo Serikali inafanya kwa niaba yao" alisema Mhandisi Luhemeja.

 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba, amesema, yeye na Menejimenti yake kwa ujumla wameyapokea maelekezo hayo na ameahidi kuyafanyia kazi.

 

“Tayari tumewekeza kwenye maeneo ya uzalishaji ya viwanda, tumewekeza kwenye Machinjio ya kisasa, Nguru, kule Mvomero, Mkoani Morogoro, kiwanda cha Kuchakata Tangawizi, Mamba Miamba kilichoko Wilayani  Same, Mkoani Kilimanjaro, kiwanda cha Kimataifa cha Bidhaa za Ngozi, Kilimanjaro (KLIC), kilichoko mjini Moshi na Kiwanda cha Chai Mponde, kilichoko Wilayani Lushoto Mkoani Tanga, na kama aivyoelekeza Katibu Mkuu, wetu, tufanye utafiti wa kina, ili kuendelea kuwekeza katika maeneo mengi zaidi na hivyo tutakuwa tumetimiza azma ya serikali ya kuzalisha ajira nyingi zaidi kwa watanzania.”Alisema CPA, Kashimba.

 

Aidha CPA. Kashimba amebainisha kuwa tokea kuunganishwa kwa Mifuko, uhai wa PSSSF sasa unaonekana, kwani Mfuko umeweza kulipa madeni yote iliyorithi toka Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya awali.

 

“Ukuaji wa Mfuko umefikia kiasi cha trillioni 8, lakini pia gharama ya uendeshaji imepungua kwa asilimia 50 na hivyo tumeokoa kiasi kikubwa cha fedha na kwakweli, jambo ambalo limeboresha utendaji kiasi kikubwa" alisema, CPA Hosea Kashimba.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) akizungumza na Menejimenti ya PSSSF, ikiongozwa na Mkurugenzi wake Mkuu, CPA. Hosea Kashimba (kulia)
Mhandisi Luhemeja, akizungumza na Menejimenti ya PSSSF

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja (katika), akiwa na Mkurugenzi Mkuu, PSSSF, CPA. Hosea Kashimba (kushoto) na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bw. Paul Kijazi.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja, akipoewa maelezo ya kiutendaji ya huduma kwa wateja, kutoka kwa msimamizi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, PSSSF, Ilala, Bi. Mathilda Nyallu. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA Hosea Kashimba.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja,  akipokea mkoba wenye taarifa mbalimbali za kiutendaji za Mfuko, kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA Hosea Kashimba.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian (katikati waliokaa), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Hifadhi ya Jamii, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Frank Kilimba (wakwanza kushoto waliokaa), Mkurugenzi Mkuu PSSSF, CPA. Hosea Kashimba 9wakwanza kulia waliokaa), wakiwa katika picha ya  pamoja na Menejiment ya PSSSF.

GAMONDI AISUKA UPYA SAFU YA ULINZI

$
0
0

NA MWANDISHI WETU


Mkuu wa Benchi la Ufundi wa Yanga SC Miguel Gamondi, ameweka wazi kuwa watafanyia kazi makosa katika mechi za kimataifa upande wa ulinzi ili kutoruhusu mabao mengi ya kufungwa.

Hayo yanajiri mara baada ya kuruhusu mabao manne katika mechi mbili ambazo wameshuka dimbani mpaka sasa katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAF CL

Katika mabao hayo manne Yanga imeruhusu ugenini dhidi ya CR Beloizdad mabao 3-0 huku wakiruhusu bao moja kwenye sare ya bao 1-1 dhidi ya Al Ahly.


Gamondi amesema kuwa makosa waliyofanya kwenye mechi za kimataifa ni sehemu ya mchezo jambo ambalo linafanyiwa kazi katika uwanja wa mazoezi.


“Utaona kwamba mabao ambayo tulifungwa ilitokana na namna ya kuzuia makosa ambayo tulifanya. Hapo ni muhimu kwetu kuangalia namna ya kurejea katika ubora na sehemu ya mazoezi tunafanyia kazi hayo.


Kikubwa ni kuona kwamba hatufanya makosa mengi kwenye eneo letu la hatari kwani wapinzani nao wanatafuta matokeo, hivyo hilo tunalifanyia kazi kwa ajili ya kuwa imara kwa mechi zijazo.”


Safu ya ulinzi ya Yanga inayotarajiwa kuvaana na Medeama ya Ghana Desemba 8 inaongozwa na Dickson Job, Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Bacca.
Mwisho

BENCHIKA APEPEA TUZO ZA CAF

$
0
0


NA MAWANDISHI WETU


Kocha wa Simba, Abdelhak Benchikha ameingia katika orodha ya makocha watatu bora wanaowania tuzo za CAF 2023 ambazo zitafanyika Jumatatu Desemba 11.



Benchikha anachuana na Walid Regraui wa Morocco na Aliou Cisse wa Senegal ambao katika nyakati tofauti walikuwa na mafanikio katika timu zao.



Walid Regraui wa timu ya Taifa ya Morocco alifanikiwa kuifikisha Morocco katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia lililofanyika Desemba mwaka jana nchini Qatar ambapo ni mara ya kwanza timu kutoka Afrika kufika hatua hiyo.

 
Wakati Aliou Cisse alifanikiwa kuipatia timu ya taifa ya Senegal ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika Afcon 2022.



Huku Abdelhak Benchikha alifanikiwa kuipatia USM Alger Kombe la Shirikisho CAF CC akiifunga Yanga SC, lakini pia amechukua kombe la Super Cup akiifunfa Al Ahly kwa bao 1-0

MAYELE, TAU, SHALULILE JINO KWA JINO MVP CAF

$
0
0

NA MWANDISHI WETU


Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Fiston Mayele ambaye kwasasa anakipiga Pyramids ya Misri ameingia tatu bora katika tuzo ya mchezaji wa mashindano ya Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF akiburuzana na staa wa Al Ahly, Percy Tau na Petter Shalulile anayekiwasha Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini. Tuzo hizo zitatolewa Desemba 11 nchini Morocco.



Kama Mayele atafanikiwa kutwa tuzo hiyo itakuwa Tuzo ya pili kuchukuliwa na mchezaji kutoka klabu ya Tanzania kwa maana ya mafanikio ambayo aliyapata alikuwa akiitumikia Yanga SC.
 

Pape Osmane Sakho aliwahi kutwa tuzo ya Bao  bora la msimu akiwa na jezi ya Mnyama Simba ambapo alifanikiwa kuifikisha Simba hataua ya Robo Fainali ya Kombela Shirikisho CAF CC katika msimu huo.

Bao hilo alilifunga katika mchezo wa hatua ya makaundi dhidi ya Asec Mimosas. Wakati Mayele msimu uiopita aliifikisha Yanga Faianli ya CAF CC akiibuka kinara wa mabao saba.

CEO NMB ASHIRIKI MKUTANO WA BENKI YA DUNIA ZANZIBAR

$
0
0


 Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna akizungumza na Rais wa Benki ya Dunia, Ajaypal Singh Banga.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna ameshiriki uzinduzi wa Mkutano Mkuu wa Benki ya Dunia (IDA20 Mid Term Review) unaofanyika kwa siku tatu Zanzibar.


Huu ni Mkutano wa 20, lengo likiwa ni kufanya tathmini ya Muda wa Kati kupitia Taasisi ya Kimataifa ya Maendeleo ya Benki ya Dunia.

Mkutano huo umefunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi - Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi na kuhudhuriwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar - Hemed Suleiman Abdalla, Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Mhe. Mwigulu Nchemba, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania - Emmanuel Tutuba na viongozi wengine.


Akiwa katika mkutano huo, Bi. Ruth alipata nafasi pia ya kukutana na Rais wa Benki ya Dunia - Ajaypal Singh Banga.

Benki ya NMB inajivunia kuwa sehemu ya kufanikisha mkutano huu mkubwa Tanzania unao wakutanisha wajumbe zaidi ya 3,000 kutoka mataifa takribani 100 duniani.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Hemed Suleiman Abdulla (kulia), akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (kushoto) wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa  20 wa Benki ya Dunia (IDA20 Mid Term Review), unaofanyika Zanzibar. (Na Mpiga Picha Wetu).
 

Njaa yakumba milioni 300

$
0
0

Na Selemani Msuya

 

WATU milioni 333 barani Afrika wanakabiliwa na njaa na utapiamlo, hivyo imeelezwa kilimo kinachozingatia Sayansi na Teknolojia ndivyo pekee vinaweza kuwaokoa na kadhia hiyo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia ya Kilimo Afrika (AATF), Dk Canisius Kanangire kwenye utoaji tuzo za Waandishi Bora wa Sayansi na Teknolojia Afrika (OMAS 2023).

 

Nchini tuzo hizo zimeandaliwa na Jukwaa la Bioteknolojia ya Kilimo Afrika (OFAB), AATF na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

 

Tuzo za mwaka huu, zilitolewa Dar es Salaam na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, huku mshindi kwa Tanzania akiibuka mwandishi Lucy Ngowi wa Gazeti la Habari Leo, na mshindi wa Afrika akiwa Tinsae Habte Sibane wa Ethiopia.

 

Dk Kanangire alisema kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), zaidi ya Waafrika milioni 333 wamekumbwa na njaa na utapiamlo, hivyo njia ya kuwakwamua na janga hilo ni kujikita kwenye kilimo kinachozingatia Sayansi na Teknolojia.

 

Mkurugenzi huyo alisema kuna kasi ya mabadiliko ya tabianchi duniani, hivyo AATF kwa kushirikiana na wadau imeanzisha tuzo za uandishi wa habari za sayansi na kilimo teknolojia kama njia kuhamasisha kilimo kitakacho kabiliana na njaa na utapiamlo.

 

Alisema utafiti unaonesha njia zingine zinazotumika katika kilimo zimeshindwa kusaidia wakulima, hivyo ni vema nguvu zikaelekezwa kwenye kilimo teknolojia kwani kimeonesha kumudu kukabiliana na changamoto za mkulima.

 

“AATF ilianza mwaka 2014 kutoa tuzo kwa waandishi wa habari za sayansi na kilimo, ambapo mwaka huu ni za tisa, lengo ni kuona kundi hili linahamasisha viongozi  na wakulima kujikita katika kilimo cha kutumia Sayansi na Teknolojia, kwani kwa hali ilivyo sasa ya mabadiliko ya tabianchi, ni ngumu mkulima kufanikiwa kwa mbinu za kizamani,” alisema.

 

Dk Kanangire alisema iwapo wakulima watajikita kwenye Sayansi na Teknolojia kwenye kilimo, ni wazi changamoto ya njaa na utapiamlo itaisha Afrika.

 

Alisema tuzo hizo zilianzishwa na OFAB kwa kushirikiana na AATF zikihusisha nchi 11 za Afrika za Malawi, Rwanda, Msumbiji, Kenya, Uganda, Tanzania, Burkina Faso, Nigeria, Ghana, Ethiopia na Afrika Kusini.

 

Meneja Mradi wa OFAB, Vitumbiko Chinoko alisema tangu kuanzishwa tuzo hizo, zaidi ya waandishi 250 wameshiriki katika ngazi ya nchi wanachama na zaidi 150 wakishiriki ngazi ya Bara la Afrika.

 

Alisema jitihada zao ni kuona idadi ya waandishi wa habari wenye kuandika habari za kupigania sekta ya kilimo ikiongezeka, huku akisisitiza utafiti kufanyika ili kuendeleza sekta ya kilimo.

 

“Sisi tunajisikia faraja, kwani mradi huu umekuwa ukipanuka siku hadi siku na imani yetu ni siku moja kuona nchi za Afrika zinajikita kwenye Sayansi na Teknolojia, ili kumkomboa mkulima,” alisema.

 

Akizungumza katika hafla hiyo, Profesa Mkenda alisema Serikali inatambua mchango wa wanahabari, katika kutangaza teknolojia zinazochangia mabadiliko endelevu ya kilimo Afrika.

 

Alisema tuzo za OMAS kwa waandishi na vyombo vya habari ni msingi mzuri wa kufanya kundi hilo kuelimisha umma faida za kilimo cha teknolojia.

 

“Kupitia mawasiliano yenye ufanisi na uandishi unaowajibika, bioteknolojia ina uwezo wa kuleta mapinduzi kwenye kilimo, kuimarisha usalama wa chakula na kuboresha maisha ya jamii zetu,” alisema.

 

Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dk Amos Nungu alisema tuzo hizo zinalenga kuhamasisha uandishi wa habari za kisayansi upande wa kilimo, ili kuisaidia jamii kupata tafsiri kirahisi na kufahamu maudhui yanayokusudiwa ili kuongeza uzalishaji wenye tija.

TANZANIA YATAMBULIKA KIMATAIFA KWA MIFUMO BORA YA USIMAMIZI WA MASUALA YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI

$
0
0
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa kazi (OSHA) Khadija Mwenda, alipokuwa akitoa Taarifa ya Utendaji na mafanikio OSHA ndani ya miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, wakati wa Kikao kazi baina yake (Khadija) na Wahariri wa Habari, kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) na kufanyika Jijini Dar es Salaam Disemba 7, 2023. 
Afisa Mwandaamizi wa Habari na Mawasiliano kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) Sabato Kosuri akifungua Kikao kazi baina OSHA na Wahariri wa Habari, kilichoratibiwa na OTR na kufanyika Jijini Dar es Salaam Disemba 7, 2023.
Baadhi ya Wahariri na Waandishi wa habari wakiwa kwenye Kikao kazi hicho.

 

Na Mwandishi Wetu

 
Katika kipindi hiki cha Rais wa Serikali ya Awamu ya Sita Dk. Samia Suluhu Hassan, Tanzania imeweza kupaa hadi kutambuliwa na Mashirika ya Kimataifa na nchi mbalimbali duniani kama nchi yenye mifumo bora ya usimamizi wa masuala ya Usalama na Afya mahali pa kazi.

Ubora huo wa mifumo umetazamwa katika maeneo muhimu mamtatu ambayo ni Uwepo wa chombo mahsusi cha kusimamia masuala ya Usalama na Afya mahali pa kazi ambacho ni Taasisi ya OSHA, Uwepo Sera, Sheria na Kanuni zinazosimamia masuala ya Usalama na Afya mahali pa kazi na Uwepo wa mifumo ya usimamizi wa masuala ya Usalama na Afya katika ngazi ya maeneo ya kazi (at enterprise level).

Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa kazi (OSHA) Khadija Mwenda, alipokuwa akitoa Taarifa ya Utendaji na mafanikio ya OSHA ndani ya miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Dk. Samia, wakati wa Kikao kazi baina yake (Khadija) na Wahariri wa Habari, kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) na kufanyika Jijini Dar es Salaam Disemba 7, 2023.

Alifafanua kuwa uwepo wa nyenzo (maeneo hayo matatu yaliyotajwa unaendana na matakwa ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) jambo ambalo limewezesha nchi mbalimbali Barani Afrika kama Kenye, Zimbabwe na Lesotho kuja kujifunza juu ya mifumo iliyopo Tanzania.

Khadija alisema, kutokana na Tanzania kuaminika, Msimamizi wa Dawati la Usalama na Afya kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) ni mtumishi kutoka OSHA, hiyo ikiwa ni kutokana na uongozi bora wa Serikali ya Awamu ya Sita, ambayo imeona umuhimu waTaasisi hiyo na kuipandisha hadhi kwa kuiwezesha kusimamia masuala ya Usalama na Afya kwa kuipatia wataalam, vitendea kazi na rasilimali nyinginezo muhimu katika kufanikisha utekelezaji wa malengo yaTaasisi hiyo.

Alisema, katika kipindi hiki cha miaka hiyo mitatu ya Rais Dk. Samia, Taasisiya OSHA imepata mafanikio makubwa ambayo yametokana na kuendana na utekelezajiwa Ilani ya Chama Tawala (Chama Cha Mapinduzi-CCM), Ibara ya 130 (f) ambapo Chama kimewaahidi Watanzania kwamba kitajenga uwezo wa waajiri na wafanyakazi kuhusu afya na usalama mahali pa kazi.

Akieleza mafanikio Mtendaji Mkuu huyo alisema, kwa kipindi cha miaka hiyo mitatu ya uongozi wa Rais Dk. Samia OSHA wamepata mafanikio makubwa ikiwemo kuongeza maoneo ya kazi yaliyosajiliwa hadi kufikia 30,309 na pia kwa miaka hiyo mitatu wameweza kuimarisha shughuli za usimamizi wa usalama na afya mahali pa kazi nchini.

“Katika kipindi tajwa, wakala umefanikiwa kuongeza idadi ya maeneo ya kazi yaliyosajiliwa kutoka 4,336 hadi 30,309, ongezeko hili ni sawa na asimilia 599. Aidha idadi ya kaguzi zilizofanyika zimeongezeka kutoka kaguzi 104,203 hadi kufikia kaguzi 776,968 sawa na asilimia 646,”alisema.

Alisema kaguzi hizo zinahusisha, ukaguzi wa jumla, ukaguzi maalum kama vile ukaguzi wa usalama wa umeme, Vyombo vya Kanieneo, ukaguzi wa vifaa vya kunyanyulia vitu vizito, ukaguzi wa kiegonomia pamoja na tathmini ya vihatarishi vya kimazingira.

Alitamba zaidi kwamba kumekuwa na ongezeko la asilimia 44.1 ya wafanyakazi waliopata mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi kutoka wafanyakazi 32,670 hadi kufikia 47,090 akifafanua kuwa mafunzo hayo yanajumuisha ya usimamizi wa masuala ya usalama na afya mahali pa kazi na uundwaji wa Kamati za Usalama na Afya, mafunzo ya kufanya kazi katika maeneo ya juu, Huduma ya Kwanza, Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali katika maeneo ya kazi, Usalama na Afya katika sekta za Mafuta na Gesi na sekta ya Ujenzi na Majenzi na Uendeshaji Salama wa Mitambo.

Mtendaji Mkuu Hadija, akasema pia kwamba kumekuwa na ongezeko la upimaji afya za wafanyakazi kwa asilimia 163 kutoka wafanyakazi 363,820 hadi wafanyakazi 955,959 waliopimwa katika kipindi tajwa na kufafanua kuwa ongezeko hilo limetokana na kukukua kwa uelewa miongoni mwa wadau, matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika kutoa huduma za usalama na afya ambayo imerahisisha upatikanaji wa huduma pamoja na kuimarika kwa uwezo wa taasisi wa kutoa huduma bora kwa wananchi.

MNYAMA MAWINDO TENA MOROCCO

$
0
0

Na John Marwa


Wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL Simba SC leo wanashuka dimbani kumenyana na wababe wa Soka la Morocco katika mchezo wa tatu wa hatua ya makundi, kundi B, katika Dimba la Marrakech.

Mnyama Simba anaingia kwenye mchezo huo akiwa anahitaji ushindi wa kwanza msimu huu katika mechi za kimataifa mara baada ya kucheza michezo sita mtawalia bila kuibuka na ushindi wakipata sare mechi zote.


Wakati wenyeji wao Waydad AC wao wanasaka alama ya kwanza mara baada ya kupoteza michezo yao miwili ya kwanza dhidi ya Jwaneng Galaxy na Asec Mimosas ambazo Mnyama Simba aliabulia sare dhidi yao.


Simba wanahitaji kushinda mechi ya leo ili kujijengea mazingira ya kutinga hatua ya robo fainal msimu huu


huku wakijua wana kazi ya kufanya katika michezo hii miwili dhidi ya Waydad AC kabla ya kuwafuata Asec Mimosas na kisha kumaliza na Jwaneng Galaxy katika Dimba la Benjamin Mkapa.


Mara ya mwisho Simba kwenda Morocco walipoteza kwa mikwaju ya penati dhidi ya hao hao Waydad katika mchezo wa Robo Fainali ya CAF CL.


ZAIDI YA BILIONI 13 ZALETA MIRADI MBALIMBALI WILAYA YA NKASI

$
0
0

NA DENIS MLOWE, NKASI 

 

HALMASHAURI ya Wilaya Nkasi Mkoani Rukwa Katika kipindi cha mwaka 2022/2023 imepokea zaidi ya shilingi bilioni 13.02  kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya hiyo ikiwemo ya elimu, afya iliyotolewa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza na wanahabari, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Peter Lijualikali alisema kuwa fedha hizo zimetolewa na Mama Samia Suluhu Hassan ikiwa ni kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya hiyo ambayo yote iko katika kiwango cha asilimia 96 na mingine kukamilka wananchi kuona matunda yake.

 

Alisema kuwa fedha hizo zimetumika kwenye miradi mbalimbali ikiwemo  ya elimu afya, kilimo na mifugo na miradi mingine ya maendeleo ambayo imejengwa katika maeneo ambayo awali yalikuwa hayana kabisa ikiwemo shule za msingi pembezoni mwa wilaya ya Nkasi na nchi jirani.

 

Lijualikali alisema kuwa Shilingi bilioni 1,535,600,000 zimepokelewa na kufanya kazi ya ujenzi wa shule mpya tatu za msingi za Isaba, Mtakuja na Ntalamila ambapo ujenzi umehusisha vyumba 8 vya madarasa, jengo la utawala, vyumba 2 vya madarasa kwa ajili ya wanafunzi wa awali pamoja na ujenzi wa vyoo vya walimu na wanafunzi na kuongeza kuwa fedha hizo zimetumika kujenga vyumba 15 vya madarasa katika shule za msingi za Mtapenda.

 

Aliongeza kuwa kati Shilingi milioni 200,000,000 zilitumika kwa ajili ya ukamilishaji wa nyumba 8 za walimu katika shule za msingi za Sentamapufi, Mjimwema, Nkata, Lyantwiya, Itanga, Mkiringa, Lwesusi na Lusembwa.Shilingi 180,000,000 zilipokelewa kwa kufanya kazi ya ukarabati wa vyumba 9 vya madarasa katika shule za msingi za Mkwamba, Itete, Kate, Kala, Utinta na Chalantai,Tundu,Mkombe, Kirando na Lupata.

 

Aidha alisema kuwa fedha nyingine zaidi ya sh.milioni 180 zilitumika katika ujenzi wa ukamirishaji wa  maabara sita katika shule sita za Korongwe Beach, Mashete, Sintali, Ninde, Wampembe na Kirando Itete na Shilingi 40,000,000 kwa ajili ya ukamilishaji wa mabweni 2 katika shule mbili za sekondari za Nkasi na Kate ,Shilingi 50,000,000 zimepokelewa na kufanya kazi ya ukamilishaji wa bwalo moja katika shule ya sekondari Nkasi

 

“Sekta ya elimu tushukuru kwamba Mama samia kaitendea haki katika wilaya yetu ya Nkasi na kuwataka wazazi wawapeleke Watoto wao shule kwani hatapenda kusikia kuna michango ya ada wala madawati kwani kila kitu kipo sawa kwenye shule zetu na zimejengwa shule za kisasa kutokana  na fedha za mama samia zilizoletwa kwenye kipindi hiki” alisema

 

Akizungumzia sekta ya afya alisema kuwa miradi mingi imetekelezwa na serikali chini ya Mama Samia Suluhu Hassan ambapo fedha mbalimbali zimepokelewa na katika wilaya hiyo ikiwemo kiasi cha Shilingi 800,000,000 zimepokelewa na kutumika kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba katika hospitali ya Wilaya ,Shilingi 200,000,000 zimepokelewa na kufanya kazi ya ukamilishaji wa zahanati katika vijiji vinne.

 

Aliongeza kuwa Shilingi 659,093,063 fedha za Mfuko wa pamoja wa Afya (HSBF) zimepokelewa Na kufanya kazi ya ufuatiliaji, ununuzi wa dawa, mafunzo pamoja na ukarabati Mdogo wa vituo vya kutolea huduma za afya, shilingi 456,140,548 zimepokelewa na kufanya kazi ya ujenzi wa vyoo bora katika Zahanati za 9 za Utinta, Miombo, Kizumbi, Musilihofu, Mlambo, Mpasa, Kate, Swaila na Lyele na Shilingl 300,132,000 zimepokelewa kwa ajili ya Mitihani kwa wanafunzi wa kidato cha pili na nne.

 

“Kwa kweli tunamshukuru sana Mh. Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutimiza ahadi mbalimbali kwa wananchi wa Nkasi katika sekta ya afya wananchi wanajivunia sana kuwa kiongozi anayewajali kwani sekta ya afya imepokea fedha nyingi zaidi na wanahabari nitawaomba mje kutembelea kujionea wenyewe mambo yaliyofanyika katika wilaya hii.” Alisema LijualikaliS

 

Lijualikali alisema kuwa kwa kipindi hichi Shilingl 315,523,910 fedha ambazo zlipokelewa za ujenzi wa miundombinu katika vituo vya kutolewa huduma za afya ambavyo ni Kasu, Kate, Nkundi (Kantawa) Londokazi, Korongwe, Mwai, Nkomolo, Kabwe, Mashete na Hospitali ya Wilaya.

 

“{Kuna fedha nyingi zimeendelea kutolewa na serikali ya Mama Samia kwa ajili ya wananchi wa wilaya hii hivyo napenda kutoa shukrani za dhati kwa Serikali ya awamu ya sita ikiongozwa na Mhe. Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya Maendeleo. Aidha fedha hizi zimesaidia uboreshaji wa utoaji wa huduma za elimu na afya katika vituo vya kutolea huduma pamoja na huduma zingine.Tunaomba Mungu azidi kumlinda siku zote za Maisha yake “ alisema

 

Waziri Chana azindua mpango wa usajili wa watoto chini ya miaka 5 Dar

$
0
0


Waziri wa Sheria na Katiba,Balozi Dkt. Pindi Chana akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mpango wa kuanza zoezi la usajili wa watoto chini ya miaka mitano kwa mkoa wa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Watoto zaidi laki mbili wanatarajiwa kusajiliwa mpaka zoezi litakapohitimishwa mapema mwakani.


 

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

 

 

Waziri wa Sheria na Katiba,Balozi Dk.Pindi Chana amezindua mpango wa kusajili watoto chini ya miaka mitano Jiji la Dar es Salaam na kuwataka wakazi kujitokeza kwa wingi na kuleta watoto kusajiliwa na kupata vyeti bure.

 

Akizungumza  kwenye sherehe za uzinduzi huo kwenye Viwanja vya Zakhem Mbagala wilayani Temeke mwishoni mwa wiki,Dkt. Chana amesema hiyo ni fursa kwa  wakazi wa Dar es Salaam na vitongoji  vyake kujiokeza na kuchangamkia zoezi hilo linaloratibiwa na Wakala wa Usajili na Udhamini (RITA).

 

‘’Vyeti  vya kuzaliwa vinaumuhimu sana kwa watoto wetu kwakuwa watakapo fika elimu ya juu itawasaidia kuwatambua na kuwaingiza kwenye mifumo mbalimbali na mpango huu umeonekana kuwa na faida kubwa kwa watanzania kwani wameitikia wito huu, na ni wasihi wakazi wa Dar es Salam wajitokeze kwa wingi kwani hili ni agizo kutoka kwa Rais wetu Dkt. Samia suluhu Hassan," Alisema Waziri Chana 

Naye,Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Bw. Frank Kanyusi, amesema kuwa chini ya mpango huo RITA inategemea watoto zaidi 200,000 wasajiliwe wakati wa zoezi hili linalolenga kuhakikisha watoto wote wenye miaka chini mitano wanasajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa bure.

 

‘’Azma yetu ni kuhakikisha kuwa hadi kufikia mwakani asiwepo mtoto yeyote mwenye kukosa cheti kwani zoezi hili ni mahususi kwa watanzania wote na hakuna gharama yoyote katika zoezi hili pia huduma zetu zitatolewa katika vituo vyote vya afya vilivyo katika ngazi ya mkoa, wilaya hadi kata’’ alisema Bw. Kanyusi.

 

Aidha,Bw. Kanyusi aliongeza kuwa hadi sasa mkoa wa Dar es Salaam umefikia asilimia 60 ya utoaji vyeti kwa watoto na sasa wanakamilisha kwa kuwafikia watoto waliobakia ambapo kwa mujibu wa sensa ya makazi na watu ya mwaka 2022 mkoa wa Dar es Salaam unajumla ya watoto 624,755 ambao kati yao asilimia 60 ndio waliopata vyeti na watoto 248,298 ndio waliopo kwenye mpango huu wa kupewa vyeti bure.

 

Kwa upande wake,Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa  la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Bi. Elke wisch, amesisitiza umuhimu wa watoto kuwa na kusajiliwa na kupata vyeti vya kuzawali kwani inaisaidia serikali kuweka mipango yake vizuri kuhusiana na suala la watoto.

 

"Tunatambua umuhimu wa watoto kuwa na vyeti ndiyo maana tumejitokeza kuwaunga mkono RITA kwani cheti kitamtambulisha mtoto mahari popote aendapo na hii itarahisisha sana katika kujua taarifa zake muhimu’’ alisema  Bi.  wisch.

 

Naye Mwakilishi kutoka kampuni ya simu za mkono ya TIGO, Rukia Mtingwa mbali ya kuipongeza RITA kwa mafanikio makubwa katika zoezi la usajili watoto amesema kupitia  kampuni yake ambayo huduma zake zipo nchi nzima naimesaidia kufanya zoezi kuwa rahisi.

 

"Sisi kama tigo tumetambua umuhimu wa hili jambo hivo tumekuja kuwaunga mkono RITA kwa kuhakikisha TEHAMA inasaidia kurahisisha utekelezaji wa mpango huu, hivo tumehakikisha kuwa mtu yeyote anafikiwa na huduma hii kwa simu ya mkononi mahali popote alipo’’ alisema Bi. Mtingwa.

 

Tangu mpango huo uzinduliwe umeshatekelezwa katika mikoa 25 na watoto zaidi ya milioni nane wameshasajiliwa na kupata vyeti bure ambapo mpango utahitimishwa katika Mkoa wa Dar es Salaam na watoto zaidi ya laki mbili wanarajiwa kusajiliwa.


 

Viewing all 19659 articles
Browse latest View live