Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

Mbunge Byabato afanya makubwa Kagera

$
0
0

Na Lydia Lugakila, Kagera

Mhe. Stephen Byabato Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ametatua baadhi ya kero zilizodumu kwa muda mrefu kwa wananchi wanyonge zilizowasilisha kwake wakati wa kupokea kero kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Rwamishenye, baada ya kuhitimisha ziara yake kutembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo.

Mhe. Byabato  aliyeambatana na Kaimu Mkurugenzi pamoja na wataalamu kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, alionekana kuibua hisia za walio wengi huku wengine furaha ikawapelekea kutoa machozi kwa namna alivyoweza kushughulikia kero zao zilizodumu kwa muda mrefu na kuzipatia ufumbuzi yeye na wataaalam alioambatana nao.

Kero alizofanyia kazi ni pamoja na namna alivyoweza kulipa madeni Mawili ya Akina Mama wa kata ya Rwamishenye moja ya deni hilo ni lililohusu madai ya Askari wa Jeshi la Polisi Kituo cha Kati Bukoba, (Jina limehifadhiwa) aliyechukua Nguo zenye thamani ya Shilingi 162,000/= Dukani kwa Mama Mfanyabiashara Sharifa Leonard  na Kuahidi angemlipa lakini limekuwa deni la Muda mrefu licha ya mama huyo kuripoti Kero hiyo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa Kagera Bravius Chatanda.

Kufuatia hali hiyo Mhe. Byabato ameamua kulipa Deni na kwamba yeye atafuatilia madai hayo kwa ngazi husika Ili arejeshewe Pesa yake.

Deni jingine lililolipwa na Mhe. Byabato ni la Bi. Mwatatu Katakweba ambalo alikuwa akidai Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba kutokana na Kushindwa kulipia Ankara ya Maji yaliyochotwa kwake kipindi cha Ujenzi wa Ofisi ya Mtendaji Kata Rwamishenye Miaka Minne iliyopita  ambalo ni jumla ya Shilingi 187,300/= ambazo nazo amesema atakwenda kuzidai kwa wahusika wazimrejeshee.

Katika hatua Nyingine Mhe Babyato ameshiriki kuchangia mchango wa Ofisi ya Mama Mlemavu anayejulikana kwa Jina la Vaileth Augustin Kiasi cha Shilingi Laki Moja ambaye yeye amewasilisha Ombi lake la Kupatiwa mtaji wa shilingi laki mbili na nusu kuendeleza ofisi yake, ambapo kiasi kingine kimechangwa na Wadau wengine kama kumpongeza Mama huyo kwa kujifungua Mtoto wa kike.

Aidha katika hatua nyingine Mhe. Byabato amekabidhi mkopo wa Shilingi laki moja kwa Kikundi cha akina Mama Rwamishenye walioamua kujiunga katika Shughuli ya Ufugaji Samaki ambao kwa kuanzia mahitaji yao yalikuwa ya vifaranga vya Samaki venye thamani ya shilingi laki nane, naye bila ajizi ametoa milioni moja kama Mkopo ikiwa ni Muendelezo wa Kutoa Mikopo ya KOPA KWA MBUNGE LIPA KWA MWENZAKO ambapo akina Mama hao watarejesha Ili wengine wakope bila riba.

Mbunge huyo ametoa shilingi laki tano kwa Wajasiliamali wanaofanya Shughuli zao jirani na Machinjio ya Rwamishenye, Ili kuboresha mazingira ya Biashara yao ya kuuza Utumbo na Viungo vingine vya Ndani ya Ng'ombe... Na Pesa hiyo haitarejeshwa kwani kaitoa Kuwaunga Mkono.

Hata hivyo amewapatia vijana wa UVCCM Kata Rwamishenye Mkopo Kutoka Mfuko wa KOPA KWA MBUNGE LIPA KWA MWENZAKO, ambapo Kiasi cha Shilingi Milioni moja kimekabidhiwa kwao Ili kuendeleza Mradi wao wa Ufugaji Samaki.


CRDB yatoa msaada wa viti na meza katika Shule Mpya ya Sekondari Kisarawe II

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Halima Bulembo (katikati) akipokea sehemu ya msaada wa viti na meza kutoka kwa Kaimu Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Dar es Salaam, Muhumiliza Buberwa (wa nne kushoto) vilivyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya shule mpya ya Sekondari ya Kisarawe II iliyopo wilayani humo. Wengine ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Pwani, Badru Idd (wa pili kushoto), Meneja wa CRDB Tawi la Kibada, (Isaya Lyimo), Meneja Mwandamizi Idara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Benki ya CRDB, Suzan Shuma (wa tatu kushoto). Kulia ni Kaimu Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Kigamboni, Emmanuel Mwakalinga, Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kisarawe II, Ashura Bihongo na Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Kigamboni, Adellah Ntenjera, hafla hiyo ilifanyika Novemba 29, 2023 katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya. (Na Mpiga Picha Wetu).










UTT AMIS yajivunia Mafanikio mwaka 2022/23, ukubwa wa Mfuko wafikia Sh Trilioni 1.535

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS imesema kwa kipindi cha Mwaka mmoja, ukubwa wa mifuko umeongezeka kutoka Sh. Bilioni 996.5 Juni 30, 2022 hadi kufikia Sh trilioni 1.535 Juni 30, 2023.

Hayo yamesemwa jijini humo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya UTT AMIS Simon Migangala akizungumza na wanahabari kuhusu Mikutano ya Mwaka ya Mifuko ya Umoja, Wekeza Maisha, Watoto, Kujikimu, Ukwasi na Hatifungani inayofanyika kuanzia leo Novemba 18 hadi 20 jijini Dar es Salaam.


“Ongezeko hili la kiasi cha shilingi bilioni 538.9 ni sawa na asilimia 54.0 ikilinganishwa na ongezeko la shilingi bilioni 383.7. Ongezeko hili la ukubwa wa Mifuko linatokana na imani ya wawekezaji kwetu, elimu itolewayo juu ya akiba na uwekezaji pamoja na akiba shindani kwenye Mifuko,” amesema Migangala.


Migangala ameeleza kuwa Utendaji wa Mifuko kwa kipindi hicho umeendelea kuwa mzuri kwamba faida kwa wawekezaji ilikuwa kubwa ikilinganishwa na vigezo linganifu.


Amebainisha kuwa faida kwa mwaka kwa upande wa Mifuko inayowekeza kwenye hisa na maeneo yenye Mapato ya kudumu kuwa ni pamoja na Mfuko wa Umoja asilimia 11.2, Mfuko wa Wekeza Maisha asilimia 12.5, Mfuko wa Watoto asilimia 12.4.


Mifuko mingine ni Mfuko wa Jikimu asilimia 14.0 ikilinganishwa na asilimia 7.6 ya kigezo linganifu huku akibainisha kuwa kwa Mifuko iliyosalia yenye uwekezaji kwenye maeneo yenye Mapato ya kudumu faida kwa Mfuko wa Ukwasi ni asilimia 12.5 na Mfuko wa Hatifungani ni asilimia 12.3 ikilinganishwa na asilimia 9.7 ya kigezo linganifu.


Kuhusu maendeleo ya Soko la Hisa, amesema Utendaji wa Kampuni za ndani ya Nchi unapimwa kwa kuangalia mabadiliko ya Fahirisi (Tanzania Share Index).


Hivyo Migangala, ameeleza kuwa katika mwaka wa Fedha ulioishia Juni 30, 2023, Fahirisi imeonesha kuwa na ongezeko la asilimia 4.1 kutoka 3,928.5 kwa Juni 30, 2022 hadi 4,091.8 kwa Juni 30, 2023.


Amesema hiyo inamanisha kuwa katika kipindi cha Mwaka ulioishia Juni 2023, bei za Hisa kwa Kampuni za ndani ya Nchi ziliongezeka sawa na asilimia 4.1.


Amezitaja sababu zilizosababisha kupanda kwa bei za Hisa kuwa ni pamoja na Utendaji mzuri wa Kampuni za ndani kwenye soko la Hisa la Dar es Salaam, kuongezeka kwa imani ya wawekezaji wa Ndani na nje na uboreshwaji wa mazingira ya uwekezaji hapa nchini.


Katika mpango mkakati wa miaka mitano utakaoishia mwezi Juni 2024, amesema Kampuni imeazimia kujikita kwenye matumizi ya Teknolojia katika kutoa huduma KWA wawekezaji.

Kwa upande wake, Mwenyeki wa Bodi ya UTT AMIS, Casmir Kyuki amewaalika wawekezaji wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS kuhudhuria Mikutano hiyo inayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.


Amesema Mikutano hiyo hufanyika ili kukidhi matakwa ya Kanuni ya Mifuko ya uwekezaji wa pamoja ya Mwaka 1997.


RC Chalamila awataka wakazi Dar kujitokeza kusajili watoto

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Albert Chalamila, amewataka wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi kusajili watoto walio chini ya miaka mitano mara zoezi la kuwasajili watoto hao litalapoanza rasmi jijini mapema mwezi ujao. 

Akizungumza jana kwenye semina ya mafunzo kwa waganga na viongozi kutoka wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam iliyoandaliwa na Wakala wa Usajili na Udhamini (RITA) kama sehemu ya maandalizi kabla uzinduzi wa rasmi wa  zoezi hilo litakalohitimishwa kitaifa katika Mkoa wa Dar es Salaam. Bw. Chalamila aliiambia semina hiyo kuwa vyeti hivyo vinatolewa bure na kwamba Serikali tayari imebeba gharama zote.

"Nisisikie mwananchi ametozwa pesa ili kupata cheti cha mtoto wake; vyombo vya ulinzi na usalama vipo macho na vinafuatilia kwa karibu sana. Sote tuwe makini na kila mmoja wetu atekeleze wajibu wake". alisema Bw.Chalamila.

Amewataka wasajili wasaidizi kuhakikisha wanazingatia uadilifu, kujituma na uzalendo na kusema hayo ni mambo ya msingi katika utekelezaji wa mpango huo.

Ametaka viongozi wa dini na wazee maarufu washirikishwe katika utekelezaji wa zoezi hilo.. 

Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Bw. Frank Kanyusi, alisema kuwa chini ya mpongo huo RITA inategemea watoto 248,298 wasajiliwe mkoani humo, kwani watoto waliosajiliwa ni 624,755 au asilimia 60.3 ya watoto wanaostahili kusajiliwa.

 Alisema mpango huo umetekelezwa kwa mafanikio makubwa katika miaka 25 na kwamba Dar es Salaam ndiyo wa mwisho.

Mikoa 25 ya Tanzania Bara imeshapata huduma isipokuwa Mkoa wa Dar es Salaam pekee. Hadi sasa zaidi ya watoto 8,886,778 wamesajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa ambavyo watavitumia kupata huduma nyingine za kijamii ikiwa ni pamoja na kupata huduma ya matibabu kupitia mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, elimu sambamba na ajira, alisema Bw. Kanyusi

Alisema yamefanyika maboresho na mageuzi makubwa kupitia mpango huo ambapo hivi sasa wamegatua majukumu ya usajili kwenda serikali za mitaa ambapo watoto wanasajiliwa karibu na maeneo yao ya makazi; yaani katika vituo vya tiba vinavyotoa huduma ya afya ya mama na mtoto na katika ofisi za watendaji kata,alisema Bw. Kanyusi

Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa  la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Bw Hosea Mitala, ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuupa uzito mpango huu, kupitia RITA. Amewataka wakazi wa Dar es Salaam kuchangamkia hiyo fursa hiyo.

Tangu mpango huo uzinduliwe na kutekelezwa katika mikoa 25 wazazi wamewasajili watoto wao kwa bidii na kupata vyeti vya kuzaliwa bure na kuifanya Tanzania isifike kimataifa katika suala hili.


MAFANIKIO YA MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI KWA MIAKA MIWILI YA MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA AWAMU YA SITA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

$
0
0


Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko, akizungumza na Wahariri na Waandishi wa Habari wakati wa Kikao Kazi kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kuhusu Mafanikio ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika kipindi cha miaka miwili ya Rais Samia Suluhu Hassan.

 Afisa Habari na Mawasiliano kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) Sabato Kosuri, akizungumza wakati wa mkutano huo.

 

UTANGULIZI

 

Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ilianzishwa mwaka 1895.

Lengo kuu la kuanzishwa kwake ilikuwa ni kufanya utafiti wa magonjwa ya Ukanda wa Joto (Tropical diseases).

Baada ya Uhuru, Maabara ilikuwa Idara ya Mkemia Mkuu wa Serikali chini ya Wizara ya Afya  ikihusika na masuala mbalimbali yaliyohitaji uchunguzi wa kimaabara.

Mwaka 1999 ilibadilishwa na kuwa mojawapo ya Wakala za Serikali.

Mwaka 2017, Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kupitia Gazeti la Serikali 248 la tarehe 21/07/2017, ilitangazwa kuwa Mamlaka chini ya Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ya mwaka 2016.

 

 

Majukumu ya Mamlaka

Utoaji wa Ushahidi wa kitaalam unaohusu uchunguzi wa kimaabara Mahakamani

Mashauri ya jamii

Dawa za kulevya , mauaji, uabakaji, ulawiti na ujangili wa wanyama pori.

Mashauri ya madai

Uhalali wa wazazi kwa mtoto, utatuzi wa migogoro inayohusiana na mirathi.

 

MAFANIKIO

Mitambo na vifaa vya Kisasa vya Uchunguzi wa Kimabaara

 

Mamalaka imenunua Mitambo mikubwa Minane (8) na midogo 134 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 9.3 ilinunuliwa katika kipindi cha mwaka wa Fedha 2021/2022 na 2022/2023.

 

 

Mwaka wa Fedha 2021/2022:

watalaam 28 walihudhuria mafunzo ya muda mrefu.

Watumishi 147 walihudhuria ya mafunzo ya muda mfupi ndani na nje ya nchi;

Watumishi 56 waliwezeshwa kuhudhuria mikutano ya kitaaluma; na

Watumishi 23 waliwezeshwa kupata mafunzo ya awali ya Utumishi ya Umma (Induction course).

 

Huduma za Uchunguzi wa Kimaabara

Mwaka wa Fedha 2021/2022 wastani wa sampuli/vielelezo 155,817, sawa na asilimia 139.94 ya lengo la wastani wa kuchunguza sampuli/vielelezo 111,349 ulifanyika.

Mwaka wa Fedha 2022/2023, sampuli 212,306 sawa na asilimia 133.9 ya lengo la kuchunguza sampuli 158,600 zilifanyiwa uchunguzi wa kimabaara.

 

Utoaji wa Matokeo ya Uchunguzi kwa Wakati (Mkataba wa Huduma kwa Mteja)

Wastani wa siku 11 za kazi unatumika kubainisha uwepo wa sumu kwenye sampuli.

Wastani wa siku 6.5 za kazi kukamilisha uchunguzi wa kimaabara kwa sampuli za dawa za kulevya, mioto, na milipuko.

Wastani wa siku 27 za kazi kukamilisha uchunguzi wa kimaabara kwa sampuli za vinasaba vya binadamu (kutegemea aina ya sampuli).

Wastani wa siku 11 za kazi unatumika kubainisha uwepo wa sumu kwenye sampuli.

Wastani wa siku 6.5 za kazi kukamilisha uchunguzi wa kimaabara kwa sampuli za dawa za kulevya, mioto, na milipuko.

Wastani wa siku 27 za kazi kukamilisha uchunguzi wa kimaabara kwa sampuli za vinasaba vya binadamu (kutegemea aina ya sampuli).

 

Umuhimu wa Huduma za Uchunguzi wa Kimaabara

 

Kuleta haki, amani na utulivu wa nchi kwa kutoa ushahidi Mahakamani kwenye mashauri yanayotokana na uchunguzi wake.

Kutatua migogoro kwenye jamii (uhalali wa wazazi kwa mtoto, mirathi).

Kuwezesha kupandikiza figo kwa wagonjwa kwa ushirikiano na Madaktari Bingwa.

Kutambua Ubora na Usalama wa bidhaa za Viwandani na Kilimo kwa ajili ya kulinda afya ya Jamii.


Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali Nchini

 

Usajili wa Wadau

Wadau wanaojishughulisha na biashara ya kemikali wameongezeka kutoka 2125 (2020/2021) hadi 3371  (2022/2023).

 

Huduma za Mamlaka kupitia Matumizi ya TEHAMA

 

Mfumo wa Usajili na Utoaji Vibali kwa Wadau wa Kemikali (Customer Chemicals Management Portal - CCMP).

Mfumo wa Mahudhurio ya Watumishi (Biometric Attendance System).

 

 

Huduma za Mamlaka kupitia Matumizi ya TEHAMA

 

Mfumo wa Usajili na Utoaji Vibali kwa Wadau wa Kemikali (Customer Chemicals Management Portal - CCMP); (Kutoka siku saba hadi ndani ya  saa moja)

Mfumo wa Mahudhurio ya Watumishi (Biometric Attendance System). (Kuongeza uwajibikaji mahala pa kazi)

 

 

Huduma za Kimaabara kwa Viwango vya Ubora wa Kimataifa

 

Ithibati ya Mifumo ya Ubora (ISO 9001:2015) iliyohuishwa kwa mara tatu mfululizo – Mifumo ya Ubora ya uendeshaji wa Mamlaka umekubalika Kimataifa.

Ithibati katika Umahiri wa uchunguzi wa kimaabara (ISO 17025:2027).

 

Utoaji Elimu kwa Umma

Mamlaka katika Mwaka wa Fedha 2021/2022 na 2022/2023:

Ilitoa elimu kwa wadau 24,020 kuhusu  majukumu ya yake kupitia maonesho mbalimbali na mafunzo.

Imeingia mkataba na baadhi ya vyombo vya habari kwa ajili ya kuendelea  kutoa elimu kwa umma kuhusiana na huduma zinazotolewa na Mamlaka.

 

Mipango ya baadaye

 

Ujenzi wa miundombinu wezeshi ya utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka kwa kukamilisha yafuatayo:

 

Kuendelea kusogeza huduma za Mamlaka   kwa wananchi katika kanda/mikoa kulingana na uhitaji na uwezo.

Kuendelea kununua   mitambo na  vifaa vya Maabara kwa ajili ya Maabara za Makao Makuu ya Mamlaka Dodoma pamoja na Ofisi za Kanda.

 

Kuendelea kujenga na kutumia mifumo ya kielektroniki (TEHAMA) ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za Mamlaka.

Kuimarisha huduma za uchunguzi wa kimaabara kwa kuendelea kununua mitambo ya kisasa inayoendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia za uchunguzi wa Maabara.

 

Ujenzi wa miundombinu wezeshi ya utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka kwa kukamilisha yafuatayo:

 

Kuendelea kusogeza huduma za Mamlaka   kwa wananchi katika kanda/mikoa kulingana na uhitaji na uwezo.

Kuendelea kununua   mitambo na  vifaa vya Maabara kwa ajili ya Maabara za Makao Makuu ya Mamlaka Dodoma pamoja na Ofisi za Kanda.

Kuendelea kujenga na kutumia mifumo ya kielektroniki (TEHAMA) ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za Mamlaka. 

Kuimarisha huduma za uchunguzi wa kimaabara kwa kuendelea kununua mitambo ya kisasa inayoendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia za uchunguzi wa Maabara.

 

TBA yaanza kuwaondoa kwenye Nyumba zake Wadaiwa Sugu, zoezi kuendelea nchi nzima

$
0
0
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kushirikiana na Kampuni ya Udalali ya Mahakama imeanza zoezi la kuwaondoka kwenye nyumba zake wapangaji wadaiwa sugu ambao ni Watumishi wa umma na viongozi wa Serikali.

Akizungumza na wanahabari jijini humo Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Dar es Salaam Arch. Bernard Mayemba amesema wameanza kuondoa wapangaji wa Nyumba za XNMC zilizopo Mbezi Beach.


Ameeleza kuwa zoezi hilo lilipaswa kuanza rasmi Nchi mzima Desemba 1, 2023, lakini kwa Mkoa wa Dar es Salaam wameamua kuanza leo kwamba hakuna cha kusubiri kwani notisi imeshaisha muda wake.


“Mkoa wa Dar es Salaam una jumla ya Nyumba 1200 za Watumishi wa umma waliopangisha, na kiasi kinachodaiwa kutoka kwa wapangaji ni shilingi bilioni 1.1,” amesema Arch. Mayemba.

Amesema kuwa zoezi hilo litafanyika kwa takribani wiki tatu na kuwa hawataangalia sura ya mtu na kwamba Fedha watakazopata kupitia madeni hayo yatawasaidia kukarabati Nyumba na miundombinu mingine ili kuhakikisha kunakuwa na Mazingira mazuri kwa wapangaji.

“Lakini pia zitasaidia kuboresha makazi mbalimbali na kuwapatia Watumishi wa umma makazi bora. TBA imekuwa ikitoa Makazi bora kwa Watumishi wa Umma.


Hata hiivyo ameeleza kuwa, pamoja na notisi kupita muda wake ni kwamba wapangaji watakaolipa madeni yao kabla ya kufikiwa na zoezi hilo hawataondolewa.


Amesema wakimaliza kuondoa wadaiwa sugu katika eneo hilo la XNMC Mbezi Beach watahamia Masaki, Mikocheni Oyesterbay, hivyo ameeleza kuwa wadaiwa wote wataguswa.

 

Naibu Katibu Mkuu Dkt. Rwezimula afunga Mkutano wa Kimataifa wa TENMET kuhusu Ubora wa Elimu

$
0
0
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula amefunga Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa Ubora wa Elimu ulioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) na kuwakutanisha Wadau wa Elimu kutoka Nchi 10 za Afrika.
Akizungumza wakati wa kufunga Kongamano hilo Jijini Dar es Salaam Dkt. Rwezimula amesema Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi, wadau na Taasisi mbalimbali zinazojihusisha na maswala ya Elimu katika kuboresha mazingira ya Elimu nchini ili iweze kumkomboa Mtoto wa Kitanzania.

Dkt. Rwezimula amesema kuwa Serikali hajajikita tu katika kutoa ahadi mbalimbali juu ya Elimu bali imeendelea kuboresha mazingira ya Elimu kwa kujenga madarasa na nyumba za walimu, kupitia mitaala, kiboresha sera, Kuboresha uwezo wa walimu kwa kuwapa mafunzo ya mara kwa mara ili kuhakikisha wanakuwa na uwezo wa kuwafundisha wa watoto kulinganana na kasi ya mabadiliko ya Dunia inavyokwenda.

"Serikali itaendelea kuhakikisha elimu nchini inakuwa bora na inayoweza kumkomboa mtoto wa Kitanzania, na ili kufanikisha hilo tutashirikiana na wadau mbalimbali kama TENMET na tunawapongeza kwa kongamano hili ambalo linatoa chachu ya kufanya madiliko mbalimbali katika sekta ya elimu," amesema Dkt. Rwezimula.

Ameeleza kuwa katika majadiliano yao wameweza kubainisha kuwa kunahitajika kuongeza kasi ya utoaji wa mafunzo mbalimbali ya mara kwa mara kwa walimu ili kuhakikisha elimu wanayowapa wanafunzi inakidhi matakwa ya elimu bora ikiwa ni pamoja na kuwa na mitaala yenye kukidhi matakwa ya Dunia ya sasa na kutoa mawanda mapana ya mtoto kujifunza kidigital na kupewa nafasi ya kuonesha ujuzi na kipawa chake nje ya elimu ya darasani.

Kwa upande wake Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania TENMET Ochola Wayoga amesema katika siku tatu za kongamano hilo wameweza kujadili kwa kina maswala ya Elimu ikiwemo kujadili kuhusu maeneo ya kujifunzia,nyenzo za kufundishia,kujifunza kwa njia za digital, changamoto za mimba za utotoni,mitaala na sera ya elimu.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya TENMET Faraja Nyalandu ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ushirikiano inaoutoa kwa kwao pia amewashukuru wadau wote wa elimu na Taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi zilizotoa muda wao kushiriki katika kongamano hilo la Kimataifa la Ubora wa Elimu.

Faraja ameongeza kuwa Tenmet kipaumbele chake kikubwa ni kuhakikisha Tanzania na Afrika kwa ujumla inakuwa na Elimu bora kulingana na Kasi ya mapinduzi ya nne ya viwanda Dunia.


FAO LA HUDUMA YA UTENGEMAO KUONGEZA FARAJA: PROFESA NDALICHAKO

$
0
0
SERIKALI kupitia Mfuko wa Fidia kwa Wafanmyakazi (WCF) imetangaza Fao jipya la Huduma ya Utengemao wa Kijamii (Social Rehabilitation) kwa wafanyakazi wanaopata ulemavu na magonjwa yatokanayo na kazi na hivyo litawaongezea faraja, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, amesema.

Akizungumza jijini Dar es Salaam,  Novemba 29, 2023, alipokutana na wanufaika wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani inayotarajiwa kufanyika kitaifa jijini Dodoma, Desemba 2, 2023. 

Profesa Ndalichako mesema, “Ndugu zangu hivi karibuni tutaanza kutoa Fao la Huduma ya Utengamao wa Kijamii na kutoa mafunzo ya kujenga ujuzi kwa wafanyakazi wanaopata ulemavu wakiwa kazini na aina ya ujuzi tutakaotoa utategemea uhitaji.” Alisema

Alisema lengo la Serikali ni kumpatia mfanyakazi ujuzi ambao utaendana na hali ya ulemavu wake, mfano alikuwa dereva na akapata ajali iliyopelekea ulemavu wa miguu, huyu anaweza kubadilisha ujuzi na kusomea kazi nyingine. 

Sambamba na kuwajengea ujuzi, fao hilo pia litatoa fursa ya kumjengea miundombinu inayoendana na hali yake, na hivyo kumuwezesha kumudu maisha katika mazingira anayoishi.” Alifafanua Profesa Ndalichako.

Kwa upande wao, wanufaika wa WCF wameishukuru Serikali kwa huduma wanazopokea kutoka katika Mfuko huo licha ya kupata ulemavu na wengine kuondokewa na wapendwa wao.

“Naomba kuhamasisha waajiri kuweza kuwachangia wafanyakazi wao, kwani viwango vya uchangiaji ni vidogo, tunaishukuru Serikali imepunguza viwango vya uchangiaji hadi kufikia asilimia 0.5” Alisema Norbert Tesha, ambaye amepata ulemavu wa kudumu baada ya kupata ajali akiwa kazini mwaka 2016.

“Hatuwezi kujua kesho yetu, lakini kama kuna misingi mizuri iliyowekwa leo, basi kesho yetu itakuwa njema, kila mtu ni mlemavu mtarajiwa.” Alisema, Bw. Tesha.

Mnufaika mwingine Bi. Emmaculet Nhigula, ambaye alimpoteza mumewe kwa ajali ya gari, amesema, “Mimi na watoto wangu wanne, tunanufaika sana na Mfuko huu, rafiki yetu kwa sasa ni WCF, huwa nikipita kwenye barabra hii na kuliona jengo lenu, ninasema hawa ni rafiki zangu wanaotembea na mimi nyakazi ngumu." Alisema

Alisema yale mafao ya kila mwezi yamekuwa na msaada mkubwa sana, yamesaidia kusomesha watoto wangu na sikuweza kuwahamisha kutoka shule walizokuwa wanasoma kabla ya kufariki baba yao.” Alisema Bi. Emaculate. 

Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu Wenye Ulemavu, yanalenga kuwahamasisha viongozi wa taasisi za kibiashara Duniani kutambua mchango maridhawa wa watu wenye ulemavu.

Kwamujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kwasasa inakadiriwa kuwa watu bilioni 1.3 duniani wanaishi na changamoto ya ulemavu, hii ni sawa na asilimia 16% ya Watu wote duniani.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “ Tuungane katika hatua za Kuokoa na kufikia Malengo ya SDGs kwa Watu wenye Ulemavu”.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako (wapili kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma (wakwanza kushoto), wakati akizungumza na wanufaika wa Fidia inayotolewa na WCF, kwenye Ofisi za Mfuko huo, jijini Dar es Salaam. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako akizunguzma kwenye mkutano na waandishi w ahabari jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, akizungumza kwenye mkutano na waandishi w ahabari jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma.
 Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma, akizungumza mwanzoni mwa mkutano huo.
Bw. Norbert Tesha (kushoto), Mnufaika wa WCF, akitoa ushuhuda mbele ya waandishi wa habari jinsi anavyonufaika baada ya kupata ulemavu wa kudumu kufuatia kuumia katika ajali iliyotokana na kazi
Bw. Kelvin Cameroon,  mnufaika wa WCF, akitoa ushuhuda mbele ya waandishi wa habari jinsi anavyonufaika baada ya kupata ulemavu wa kudumu kufuatia kuumia katika ajali iliyotokana na kazi
Bi. Emmaculat Nzigula, Mtegemezi anayenufaika na mafao yanayotolewa na WCF baada ya kumpoteza mumewe aliyefariki katika ajali ya gari wakati akitekeleza majukumu ya mwajiri wake.
Profesa Ndalichako, akisalimiana na mmoja wa wategemezi wanaonufaika na mafao ya Fidia. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF.
Profesa Ndalichako, akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za WCF jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma na Bw. Rasheed Maftah, Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa  Wenye Ulemavu, Ofisi ya Waziri Mkuu.

Picha ya pamoja.


NAIBU KATIBU MKUU, TAMISEMI AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UBORA WA ELIMU

$
0
0

 

 

Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt. Charles Msonde akihutubia washiriki wa Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu (3rd International Quality Education Conference – IQEC), linalofanyika katika Ukumbi wa Marquee, Serena Hotel jijini Dar es Salaam, kabla ya kufungua rasmi mkutano huo wa kimataifa unaoshirikisha wadau anuai wa elimu kutoka ndani na nje ya nchi.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Global Partnership for Education akizungumza na washiriki wa Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu (IQEC), linalofanyika katika Ukumbi wa Marquee, Serena Hotel jijini Dar es Salaam, na kushirikisha wadau anuai wa elimu kutoka ndani na nje ya nchi.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Global Partnership for Education akizungumza na washiriki wa Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu (IQEC), linalofanyika katika Ukumbi wa Marquee, Serena Hotel jijini Dar es Salaam, na kushirikisha wadau anuai wa elimu kutoka ndani na nje ya nchi.

Mwenyekiti wa Bodi ya wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT), Bi. Faraja Nyalandu akizungumza kwenye Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu (IQEC), linalofanyika katika Ukumbi wa Marquee, Serena Hotel jijini Dar es Salaam, na kushirikisha wadau anuai wa elimu kutoka ndani na nje ya nchi.
Mratibu Taifa wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga akizungumza kuwakaribisha wajumbe washiriki wa Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu (3rd International Quality Education Conference – IQEC), linalofanyika katika Ukumbi wa Marquee, Serena Hotel jijini Dar es Salaam, kabla ya kufungua rasmi mkutano huo wa kimataifa unaoshirikisha wadau anuai wa elimu kutoka ndani na nje ya nchi.

Mwenyekiti wa Bodi ya wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT), Bi. Faraja Nyalandu akizungumza kwenye Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu (IQEC), linalofanyika katika Ukumbi wa Marquee, Serena Hotel jijini Dar es Salaam, na kushirikisha wadau anuai wa elimu kutoka ndani na nje ya nchi.

Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu (IQEC), linalofanyika kwenye Ukumbi wa Marquee, Serena Hotel jijini Dar es Salaam, na kushirikisha wadau anuai wa elimu kutoka ndani na nje ya nchi wakifuatilia hotuba mbalimbali.

Baadhi ya wanafunzi wanaoshiriki Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu (IQEC), wakiwa kwenye Ukumbi wa Marquee, Serena Hotel jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu (IQEC), linalofanyika kwenye Ukumbi wa Marquee, Serena Hotel jijini Dar es Salaam, na kushirikisha wadau anuai wa elimu kutoka ndani na nje ya nchi wakifuatilia hotuba mbalimbali.

Sehemu ya washiriki wa Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu (IQEC), linalofanyika kwenye Ukumbi wa Marquee, Serena Hotel jijini Dar es Salaam, na kushirikisha wadau anuai wa elimu kutoka ndani na nje ya nchi wakifuatilia hotuba mbalimbali.

Sehemu ya washiriki wa Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu (IQEC), linalofanyika kwenye Ukumbi wa Marquee, Serena Hotel jijini Dar es Salaam, na kushirikisha wadau anuai wa elimu kutoka ndani na nje ya nchi wakifuatilia hotuba mbalimbali.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Global Partnership for Education na mgeni wa heshima katika Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu (IQEC), akipata maelezo kutoka Banda la HakiElimu kabla ya kufunguliwa kwa Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu (IQEC), linalofanyika katika Ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (kulia) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Global Partnership for Education akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti ya TEN/MET kwenye banda lao alipokagua mabanda kwenye Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu (IQEC), linalofanyika katika Ukumbi wa Marquee, Serena Hotel jijini Dar es Salaam, na kushirikisha wadau anuai wa elimu kutoka ndani na nje ya nchi.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (kulia) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Global Partnership for Education akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti ya TEN/MET kwenye banda lao alipokagua mabanda kwenye Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu (IQEC), linalofanyika katika Ukumbi wa Marquee, Serena Hotel jijini Dar es Salaam, na kushirikisha wadau anuai wa elimu kutoka ndani na nje ya nchi.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Global Partnership for Education na mgeni wa heshima katika Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu (IQEC), akitembelea mabanda mbalimbali ya wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) kabla ya kufunguliwa kwa Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu (IQEC), linalofanyika katika Ukumbi wa Marquee, Serena Hotel jijini Dar es Salaam.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Global Partnership for Education na mgeni wa heshima katika Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu (IQEC), akitembelea Banda la UWEZO Tanzania kabla ya kufunguliwa kwa Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu (IQEC), linalofanyika katika Ukumbi wa Marquee, Serena Hotel jijini Dar es Salaam.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Global Partnership for Education na mgeni wa heshima katika Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu (IQEC), akishauri jambo kwa Dkt. Charles Msonde Naibu Katibu Mkuu, TAMISEMI pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT), Bi. Faraja Nyalandu
alipokagua manda kabla ya uzinduzi wa Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu (IQEC), linalofanyika katika Ukumbi wa Marquee, Serena Hotel jijini Dar es Salaam.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Global Partnership for Education na mgeni wa heshima katika Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu (IQEC), akitembelea mabanda mbalimbali ya wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) kabla ya kufunguliwa kwa Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu (IQEC), linalofanyika katika Ukumbi wa Marquee, Serena Hotel jijini Dar es Salaam.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (kushoto) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Global Partnership for Education na mgeni wa heshima katika Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu (IQEC), akitembelea mabanda mbalimbali ya wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) kabla ya kufunguliwa kwa Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu (IQEC), linalofanyika katika Ukumbi wa Marquee, Serena Hotel jijini Dar es Salaam. Aliyeambatana naye ni mgeni rasmi katika mkutano huo Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt. Charles Msonde.

ASKARI TANAPA WAFANIKIWA KUWAONDOA TEMBO WALIOKUWA WAMEVAMIA VIJIJI 5

$
0
0

Na Lydia Lugakila Kyerwa.

ASKARI wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) wamefanikiwa kuyaondoa makundi ya wanyamapori aina ya Tembo walikuwa wamevamia maeneo ya vijiji vitano vilivyoko kwenye kata ya businde iliyoko wilayani kyerwa Mkoani Kagera kwa zaidi ya miaka 10 na kusababisa kaya zaidi ya 50 kuhama katika vijiji hivyo kwa hofu ya wanyama hao walioanza  kuwashambulia na kuwaua pamoja na kuharibu mazao yao ya kilimo mashambani.

Kamishina wa Uhifadhi Dkt. Fredrick Mofulu ambaye ni Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ibanda-Kyerwa iliyoko wilayani kyerwa mkoani humo aliyeongoza operesheni hiyo alisema ilichukua siku tano hadi kufanikiwa.

Alisema  vijiji vilivyokuwa vimevamiwa na tembo hao viko kwenye kata ya Bisinde ambavyo ni Nyakashenyi, Businde, Kibare, Bugara na Kijumbura , alieleza kuwa tembo hao wamedhibitiwa na kuswagwa hadi kwenye umbali wa kilomita zaidi 45 kutoka katika maeneo ya vijiji hivyo yaliyokuwa yamevamiwa.

Kamishina huyo alisema tembo hao wameishadhibitiwa na anayo matumaini ya kuwa  hawatarudi katika vijiji hivyo kwa njia za kuingia alizosema kuwa ni tatu zimeishabainika na zitawekewa ulinzi wa kutosha utakaowazuia kupenya.

Alisema katika kuimarisha ulinzi wa kuwadhibiti tembo wasirudi katika vijiji hivyo umeanzishwa mpango wa kutoa mafunzo kwa vijana wa vijiji hivyo ya namna ya kuwadhibiti tembo hao yatayotolewa na chuo cha wanyamapori cha Pasiasi kilichoko mkoani Mwanza.

Aliendelea kusema kuwa mafunzo hayo yatawajengea uwezo mkubwa vijana hao wa kupata mbinu za kitaalam za kuwadhibiti tembo wasirudi tena katika maeneo ya vijiji, na kila kijiji kitatoa vijana 2 ambao watapata mafunzo hayo.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Kyerwa Bi. Zaitun Msofe alishukuru kazi kubwa iliyofanywa na askari wa TANAPA ya kuwaondoa tembo hao ambao walishakuwa kero kubwa kwa Wananchi ya aVijiji hivyo.

“Wengi wamejaribu wameshindwa lakini nyie mmeweza, nawashukuru sana Wananchi wangu wataishi kwa amani na utulivu, walikuwa wamekata tamaa, sasa nawataka mfanye kazi mpunguze maumivu mliyokuwa mnayapata baada ya kuvamia na tembo" alisema Bi Msofe.

Aliahidi kuwa serikali ya awamu ya sita itaendelea kutatua kero zao zikiwemo za ukarabati wa barabara na kuchimba visima vya maji na pia itaendelea pia kutatua kero zinazosababishwa na Wanyama waharibifu wakiwemo Viboko wanaosumbua na kushambulia watu katika eneo la Kakanja lililoko wilayani Kyerwa.

Nao baadhi ya Wananchi waliolazimika kuhama vijiji vyao kwa hofu ya kushambuliwa na tembo wakizungumza kwa nyakati tofauti waliishukuru serikali kwa kumaliza tatizo hilo na wameahidi kurudi kwenye maeneo yao kuendelea na shughuli zao baada ya kuhakikishiwa usalama wa maisha yao na mali zao.

SERIKALI KUJENGA KAMPASI 14 MIKOA YA PEMBEZONI

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali iko kwenye maandalizi ya awali ya ujenzi wa kampasi 14 mpya za vyuo vikuu kwenye mikoa ya pembezoni isiyokuwa na vyuo vikuu. 

 

Ameitaja mikoa hiyo kuwa ni Kigoma, Ruvuma, Singida, Mwanza, Kagera, Tanga, Njombe, Tabora, Manyara, Simiyu, Shinyanga, Lindi, Rukwa, na Katavi.

 

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Novemba 30, 2023) wakati akizungumza na wahadhiri na wahitimu kwenye mahafali ya 26 ya Chuo Kikuu cha Iringa yaliyofanyika chuoni hapo amako pia alimwakilisha Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan.

 

“Hatua hiyo ni moja ya jitihada za makusudi za Serikali za kuharakisha ukuaji wa uchumi kwenye maeneo ya pembezoni, kuongeza nafasi za elimu ya ufundi, ujuzi na stadi za maisha katika maeneo hayo ili kuongeza wigo wa upatikanaji wa fursa za elimu na ajira.”

 

Akielezea uboreshaji wa miundombinu ya vyuo vikuu, Waziri Mkuu amesema Serikali ya awamu ya sita inaendelea na ujenzi wa miundombinu muhimu ambayo ni vyumba vya mihadhara, maabara, nyumba za walimu na maktaba.

 

“Kupitia mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), Serikali inaendelea na ujenzi wa mabweni 34; vyumba vya mihadhara na madarasa 130; kumbi za mikutano ya kisayansi 23; maabara/karakana za kufundishia 108; miundombinu ya shambani na vituo atamizi 10.

 

Amesema kukamilika kwa ujenzi huo kunatarajiwa kuongeza idadi ya wanafunzi wanaosoma programu za kipaumbele (STEM) kutoka wanafunzi 40,000 kwa mwaka 2020 hadi kufikia 106,000 mwaka 2026.

 

Kuhusu ombi la kujengewa bweni la wasichana litakaloitwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu amesema amelichukua na ltaenda kufanyiwa kazi Serikalini.

 

Awali, Mkuu wa Chuo hicho, Jenerali Mstaafu Venance Mabeyo aliwatunuku wahitimu 1,994 wakiwemo 108 wa shahada za uzamili wa elimu (Ualimu), Utawala na Usimamizi wa Biashara, Sanaa ya Maendeleo ya Jami na Usimamizi wa Miradi, Sayansi katika Saikolojia Nasihi, Misheni na Maendeleo ya Jamii, Sheria za Habari na Mawasiliano ya TEHAMA, na mfumo wa sheria za Jinai za Kimataifa na Haki za Binadamu.

 

Mapema, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, CPA. Lilian Badi Manara alisema wanamuomba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan awasaidie kujenga bweni la wanachuo wa kike kwani wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa kifedha.

 

“Kutokana na changamoto ya upungufu wa kifedha, tuna upungufu wa mabeni na hasa wa kike. Na matokeo yake baadhi wanalazimika kuishi mitaani ambako wanakutana na ukatili wa kijinsia na baadhi wanalazimika kuingia kwenye ndoa za muda mfupi,” alisema.

                                                                                                    

(mwisho)

 

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

ALHAMISI, NOVEMBA 30, 2023.

--

NMB, Oryx Tanzania wazindua 'Moto Mkali Bei Poa,' kukopesha gesi ya kupikia

$
0
0

 

Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi na Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Gas Tanzania, Benoit Araman wakibadiliashana mikataba baada ya utiaji saini hati ya makubaliano  ya ushirikiano. Kushoto ni Meneja mauzo wa Oryx Gas, Shaban Mohamed, wapili kutoka kulia ni Mkuu wa Idara ya Kadi wa Benki ya NMB, Philbert Casmir na kulia ni kaimu Meneja wa Benki ya NMB kanda ya Dar es salaam.


Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi na Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Gas Tanzania, Benoit Araman wakitiliana saini hati ya makubaliano  ya ushirikiano. Kushoto ni Meneja mauzo wa Oryx Gas, Shaban Mohamed, wapili kutoka kulia ni Mkuu wa Idara ya Kadi wa Benki ya NMB, Philbert Casmir na kulia ni kaimu Meneja wa Benki ya NMB kanda ya Dar es Salaam.






NA MWANDISHI WETU

 

BENKI ya imeingia Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) na Kampuni ya Uuzaji na Usambazaji Gesi ya Oryx Gas Tanzania, yaliyopewa jina la 'Moto Mkali Bei Poa', ambao ni mpango mkakati unaolenga kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala ya kupikia, ili kuunga mkono juhudi za utunzaji mazingira kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

 

Makubaliano hayo yamesainiwa jijini Dar es Salaam Novemba 26, ambako NMB iliwakilishwa na Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Filbert Mponzi, huku Oryx Tanzania ikiwakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Benoit Araman, mbele ya Mkuu wa Idara ya Rasirimali Watu Oryx Energies, Kanda ya Afrika Mashariki, Loveness Hoyange..  

 

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mponzi alisema utunzaji mazingira ni agizo lililopewa msisitizo na Benki hiyo kinara kwa suluhishi mbalimbali za kifedha na kijamii, wanajisikia fahari kusaini makubaliano hayo, yanayoenda kuwapa urahisi wa upataji gesi  kwa mikopo ya riba nafuu na punguzo la bei.

 

“Makubaliano haya yanaakisi dhamira ya dhati tuliyonayo NMB katika utunzaji wa mazingira, eneo ambalo wiki jana tulizindua kampeni ya kitaifa ya ugawaji mizinga ya nyuki kwa vikundi vya wafugaji nchini, ikifuata nyayo za ile kampeni ya mapema mwaka huu ya upandaji miti milioni moja kote nchini, ambayo tunatarajia kukamilisha kama tulivyopanga.

 

“NMB tunatambua, kujali na kuthamini utunzaji wa mazingira kwa ustawi wa kizazi cha sasa na cha baadaye, ndio maana tukaja na Kampeni hii ya Moto Mkali, Bei Poa, lengo likiwa ni kuhamaisha wateja wetu kuungana na Serikali katika kumaliza changamoto ya uharibifu wa mazingira.

 

“Kupitia kampeni hii, tunaenda sio tu kukopesha wateja wetu mikopo ya ununuzi wa gesi na kunufaika na punguzo la bei wataponunua kwa njia za malipo ya kadi na yale ya kidijitali kwa maana ya Lipa Mkononi, bali tumeangalia mnyororo mzima wa thamani unaowajumusiha wauzaji, ambao nao watakopeshwa fedha za kuongeza bidhaa katika vituo vyao vya mauzo,” alisema Mponzi.

 

Kwa upande wake, Araman, alitambia mashirikiano hayo baina yao ambao ni vinara wa huduma za nishati mbadala na NMB wanaoongoza sekta ya fedha nchini, na kwamba ukongwe wao katika masuluhisho ya kifedha, unawapa uhakika wa mafanikio katika vita waliyoshiriki kwa miaka mingi ya mabadiliko ya tabianchi.

 

“Sisi ni wakongwe katika utunzaji wa mazingira kwa kusambaza na kuuza nishati mbadala mbadala, lengo likiwa kuunga mkono juhudi za Serikali yar AIS Samia Suluhu Hassan, ambaye alitoa agizo la kuhakikisha hadi mwaka 2030, tunatokomeza uharibifu wa mazingira na kila Mtanzania awe anatumia gesi ya kupikia na sio mkaa au kuni, ambazo ni hatari pia kwa afya.

 

“Tumekuwa watoa huduma wa muda mrefu zaidi barani Afrika na Tanzania ikiwa sehemu ya wanufaika wa huduma zetu na tunaamini katika ushirikiano huu na NMB, utaenda kuwa chachu ya ufanisi wa mpango mkakati wetu wa kuhakikisha tunawapa wateja wetu suluhisho la kupata nishati bora ya kupikia kwa ukaribu, uharaka na unafuu mkubwa.

 

Awali, Mkuu wa Biashara ya Kadi wa NMB, Philbert Casmir, alisema Moto Mkali, Bei Poa ni kampeni inayodhihirisha dhamira yao katika kuhakikisha wanagusa maisha ya wateja wa benki yake, na kuwa hiyo ndio siri ya makubaliano hayo, ambayo yatatoa mchango mkubwa katika utunzaji mazingira na kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi.

 

“Kupitia malipo ya kidijitali kwa maana ya Lipa Mkononi, QR Code na Vituo vya Mauzo (PoS), wateja wa NMB wanaenda kunufaika sio tu na manunuzi ya gesi kwa njia ya kadi na kuachana na matumizi ya pesa taslimu, bali wataingia moja kwa moja droo zetu za Kampeni inayoendelea ya MastaBata Halipoi, inayotoa zawadi hazi za Shilingi Milioni 350,” alibainisha.

 

Naye Meneja Mauzo wa Oryx Tanzania, Shaban Mohamed, alisema Moto Mkali, Bei Poa utajikita katika maeneo ununuzi wa haraka wa Oryx Gas utakaoambatana na unafuu wa bei, Uwezeshaji wa Wasambazaji, Wauzaji wa Maduka ya Oryx pekee (Oryx Exclusive Shops), Punguzo la Bei kwa Wanunuzi wateja wa NMB na mikopo yenye riba nafuu kwa wateja wote.

TRA PWANI YAMWAGA VIFAA ZAHANATI YA MISUGUSUGU KUSAIDIA UJENZI JENGO LA MAMA NA MTOTO

$
0
0

NA VICTOR MASANGU, KIBAHA 


Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani katika kuanza wiki ya shukrani kwa mlipa kodi imeamua kurudisha fadhila kwa jamii kwa kutoa msaada wa vifaa mbali mbali vya ujenzi kwa ajili ya kuendeleza  mradi wa jengo la mama na mtoto lililopo katika zahanati ya Misugusugu halmashauri ya mji Kibaha.

Akizungumza katika halfa ya kukabidhi msaaada wa vifaa hivyo Meneja wa TRA Mkoa wa Pwani Masawa Masatu alisema kwamba wameamua kusapoti sekta ya afya kwa lengo la kuweza kuwakomboa wakinamama kupata huduma bora hasa wakati wa kujifungua.

Meneja huyo alibainisha kwamba TRA katika zahanati ya misugusugu kuna changamoto ya miundombinu ya jengo la mama na mtoto hivyo wakaona kuna umuhimu wakusaidia vifaa hivyo ambavyo vitasaidia katika ujenzi huo.

"Tupo katika wiki ya shukrani kwa mlipa kodi na sisi kama TRA Mkoa wa Pwani tumeona ni vuzuri tukaungana na wananchi katika ujenzi huu ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa changamoto ya wakinama kupoteza maisha yao hasa wakati wa kujifungua,"alisema Masatu.
Meneja alisema kuwa ana imani msaada huo utaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa wanawake wa kata ya misugusugu na maeneo mengine kuweza kupata fursa ya kuweza kuondokana na usumbufu waliokuwa wanaupata katika kipindi cha nyuma.
Kwa upande wake  Afisa Maendeleo ya jamii wa kata hiyo, Kezia Olambo aliwashukuru kwa dhati TRA kwa msaada huo wa kuisaidia jamii katika suala zima la kuboresha sekta ya afya.

Alisema wananchi wa kata hiyo wamekuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu kwenda kutafuta huduma za mama kujifungua katika eneo la Mlandizi na hospitali ya  rufaa ya mkoa wa Pwani ya Tumbi jambo ambalo limekuwa likichangia kuongea Vifo vya mama na mtoto.

"TRA tunawashukuru Kwa kutupatia msaada  wa vifaa hivi vya ujenzi maana ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika zahanati hii itaokoa maisha ya wanawake wanahitaji huduma ya kujifungua maana wengi wamekuwa wakitoka hapa kwenda kufuata huduma mlandizi au hosptali ya rufaa ya mkoa wa Pwani"alisema


Naye Afisa mtendi wa kata hiyo, Elizabeth Mwakalikwa, alisema ujenzi wa jengo Hilo utagaharimu zaidi ya shilingi milioni 60, na kwamba bado jitihada za makusudi zinahitajika ili kumalizia ujenzi huo na kuwaomba wadau wengine kujitokeza ili kukamilisha mradi huo.
"TRA wametupatia msaada na tunamshukuru na kupitia msaada huu tutaendelea kuhamasisha wananchi kulipa Kodi Kwa ajili ya maendeleo yetu wenye...ujenzi huu bado haijakamilika tunaomba wadau wengine wajitokeze kutoa misaada ambayo itusaidia"alisema

Swaiba Kaisi mkazi wa kata ya misugusu, alisema kukamilika Kwa ujenzi wa jengo Hilo litakuwa mkombo Kwa wanawake kuondokana na adhamba ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma umbali mrefu ambapo utapunguza vifo vya wanawake wajawazito.

Katika hatua nyingine mamlaka hiyo imetoa msaada wa vyakuka na vinywaji katika kituo Cha watoto yatima cha Fadhillah Ophanage Center ambayo ni, sabuni, unga, Mchele, mafuta, sukari na mahitaji mengi ya msingi.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya  mwaka huu ya mamlaka ya mapato  (TRA)  Mkoa wa Pwani katika wiki ya shukrani kwa mlipa kodi inasema kodi yetu  maendeleo yetu tuwajibike.

KUMEKUCHA MAREKEBISHO YA KATIBA RIADHA TANZANIA

$
0
0

NA TULLO CHAMBO, RT

BAADA ya kuzinduliwa na kutambuliwa rasmi, Kamati Maalumu ya Marekebisho ya Katiba ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), imeweka hadharani namna ya kupokea maoni ya wadau ili kufanikisha zoezi hilo muhimu kwa mustakabali wa mchezo huo.



Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari, iliyotolewa na Katibu wa Kamati hiyo, Wilhelm Gidabuday, imewahimiza wadau kujitokeza kushiriki zoezi hilo, kwani maoni na mapendekezo yatafanywa na wao na kazi ya Kamati itakuwa kuyaweka katika mfumo wa rasimu, kabla ya kuwasilishwa Kamati Tendaji RT na kisha Mkutano Mkuu kwa ajili ya kupitishwa.


Kamati hiyo, imeweka wazi utaratibu huo kama ifuatavyo:

TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI.

01.12. 2023.

Arusha.

1.     Kamati ya Marekebisho ya katiba iliyoundwa na Shirikisho la Riadha Tanzania na kuanza kutekeleza majukumu ya kazi hiyo tarehe 16.10.2023, imeendelea na mchakato wa shughuli zake kwa kupitia nyaraka mbalimbali ili kuisadia kutimiza wajibu huo kikamilifu.

2.     Kamati inapenda kuwatangazia kuwa mchakato wa marekebisho ya katiba utafanywa na wadau na wakereketwa wa mchezo wa riadha wenyewe na kazi ya kamati ni kuyaratibu maoni hayo na kuyaunganisha kwa kuyatafsri katika muundo wa rasimu ya Katiba itakayowasilishwa kwa kamati ya utendaji ya shirikisho la riadha Tanzania (RT) na baadaye mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa shirikisho kwa ajili ya maamuzi.

3.     Kwa mazingatio hayo, kamati inawatangazia rasmi kuwa maoni hayo yatawasilishwa na kukusanywa mbele ya kamati kwa kupitia mfumo/utaratibu wa njia kuu mbili (2).

3.1.         Kujaza dodoso maalum ambalo litapatikana kwa kila katibu mkuu wa chama cha riadha cha mkoa mwanachama wa shirikisho. Ukisha jaza dodoso hiyo utairejesha kwa katibu wa mkoa wako husika au waweza kuiwasilisha kwa mjumbe wa kamati aliye karibu na mahali ulipo au kuituma mwenyewe kwenye akaunti ya kamati rekebishakatiba@gmail.com moja kwa moja.

3.2.         Kujaza dodoso la kimtandao (google docs) kupitia rink maalum ya maswali https://forms.gle/fgcwhQhPvLkX38xo7 ukishajaza itakweleza kuwasilisha (submit).

4.     Kamati inapenda kusisitiza kwamba, maoni hayo yakishakusanywa na kuratibiwa ndiyo yatakayotengeneza rasimu mpya ya katiba ya shirikisho, hivyo kila mdau na mkereketwa wa mchezo huu anao wajibu wa kutumia fursa hii muhimu kupitia mfumo na utaratibu uliowekwa.

5.     Kamati inawatangazia wadau wote kwamba dirisha la kukusanya maoni litakuwa la siku 35 (thelathini na tano) kuanzia siku na tarehe ya tangazo hili.

Karibuni – kwa maendeleo ya riadha nchini na ustawi wa kiuchumi wa Taifa letu.

Kamati inawatakiwa sikukuu njema ya Christimas 2023 na heri ya mwaka mpya 2024.

 

Imetolewa na katibu wa kamati.

Wilhem F. Giddabuday

SHIRIKISHO LA RIADHA TANZANIA

‘Kamati ya ukusanyaji maoni na mchakato wa marekebisho ya katiba ya Shirikisho’

rekebishakatiba@gmail.com

 

TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI.

 

01.12. 2023.

Dar es salaam.

 

MAKUNDI MAALUM YANAYOKUSUDIWA.

 

 

S/NA

KUNDI

IDADI

MRATIBU

1

Kamati ya Utendaji iliyopo madarakani

15

 

2

Wenyeviti wa Mikoa – Mkoa Mwanachama

30

 

3

Makatibu wa Mikoa

30

 

4

Baraza la Michezo la Taifa

10

 

5

Viongozi wa kisiasa

15

 

6

Viongozi wastaafu -  RT

10

 

7

Kamisheni ya wachezaji

25

 

8

Wanariadha wakongwe

15

 

9

Wanariadha wa kimataifa wanaocheza sasa

15

 

10

Wanariadha wa kitaifa

30

 

11

Wakereketwa wa riadha nchini

15

 

12

Wana taaluma wa taaluma ya michezo

·       Vyuo vya kati

·       Vyuo vikuu

 

20

 

13

Kundi mchanganyiko

40

 

14

Uwakilishi wajumbe wa kamati tendaji za mikoa

60

 

15

Wana Habari wakereketwa na mchezo wa riadha

20

 

 

Jumla

350

 

 

RETIRED PRESIDENT DR. KIKWETE BESTOWED LIFETIME ACHIEVEMENT AWARD BY THE TANZANIA CEO ROUNDTABLE

$
0
0


The Tanzania CEO Roundtable has bestowed the esteemed Lifetime Achievement Award upon retired President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete during its annual gala dinner at the Kilimanjaro Hyatt hotel in Dar es Salaam on Saturday night.


 This prestigious recognition is a heartfelt tribute to Dr. Kikwete's exceptional and visionary leadership, unwavering dedication, and transformative impact on the nation throughout his illustrious career, according to Mr. David Tarimo, Chairman of the Tanzania CEO Roundtable.


Mr Tarimo also expressed that the award serves as a testament to Dr. Kikwete's outstanding public service, highlighting his extraordinary contributions to the nation's betterment.

Pictured is Dr. Kikwete receiving the Award from Mr Tarimo and when he delivered  his acceptance speech.



CHUO KIKUU DODOMA YATWAA TUZO YA NBAA 2022

$
0
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Ikulu, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Jamal Kassim Ali (kushoto), akimkabidhi Tuzo Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Chuo Kikuu Dodoma, CPA David Mwakapala tuzo ya mshindi wa pili katika kundi la Taasisi za Elimu ya Juu ya Uandaaji wa hesabu kwa kutumia viwango vya kimataifa kwa taasisi za Umma. Kulia ni Mkaguzi wa Ndani Chuo Kikuu cha Dodoma, CPA Fredy na wa pili kulia ni Mhasibu Mkuu wa Kitengo cha Malipo huo Kikuu cha Dodoma CPA, Dickson Hango. Hafla ya kukabidhiwa tuzo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Mkurugenzi wa Fedha Chuo Kikuu Dodoma (UDOM), CPA Mwanjaa Lyezia, akiwa ameshika tuzo ya mshindi wa pili katika kundi la Taasisi za Elimu ya Juu ya Uandaaji wa hesabu kwa kutumia viwango vya kimataifa kwa taasisi za Umma. Hafla ya kukabidhiwa tuzo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 

ULIPAJI FIDIA MRADI MADINI TEMBO KIGAMBONI WAFIKIA ASILIMIA 92 Bilioni 18 Zatumika kuwalipa Waliopisha Mradi Mradi wa Madini Tembo Pangani Waombewa Leseni ya Uchimbaji Mkubwa

$
0
0

Kigamboni na Pangani

 

Imeelezwa kuwa, zoezi la kuwalipa fidia wananchi waliopisha mradi wa Uchimbaji Madini Tembo (heavy mineral sands) utakaotekelezwa eneo la Fungoni Kigamboni Mkoani  Dar es Salaam limefikia asilimia 92 huku kiasi cha  shilingi bilioni 18  kikiwa tayari  kimekwishakulipwa.

 

Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali alipotembelea eneo hilo mwishoni mwa wiki kwa lengo la kuangalia hatua za uendeleaji wa mradi huo ikiwemo kujua changamoto zinazokabili utekelezaji wake ambapo alihimiza zoezi la ulipaji fidia kukamilishwa haraka ili mradi uanze kama ulivyokusudiwa.

 

Mradi huo unamilikiwa na kampuni ya Nyati Mineral Sand Limited ambayo ni kampuni ya ubia kati ya Serikali inayomiliki asilimia 16 ya hisa na kampuni ya Strandline Resources Limited inayomiliki asilimia 84 ya hisa unatarajia kuanza shughuli za uchimbaji madini hayo mara zoezi la kulipa fidia wananchi wanaotakiwa kupisha mradi huo utakapokamilika.

 

Katika taarifa iliyotolewa wakati wa ziara ya Katibu Mkuu, ilielezwa kuwa kulingana na utafiti uliofanywa, mradi wa uchimbaji madini tembo una kiasi cha tani milioni 12 za mbale na uhai wa mradi ni miaka 6 kwa kuchakata tani milioni 2 za mbale kwa mwaka na kuelezwa kuwa, uchorongaji zaidi utafanyika katika maeneo hayo ili kuongeza kiasi cha mashapo na hivyo kuongeza uhai wa mgodi.

 

Katika hatua nyingine, Desemba 2, 2023, Katibu Mkuu Mahimbali alitembelea katika   mradi mwingine wa uchimbaji madini tembo unaomilikiwa na kampuni hiyo katika eneo linalojulikana kama Tajiri Wilayani Pangani Mkoa wa Tanga ili kuangalia maendeleo ya mradi pamoja na kufahamu changamoto zilizopo katika utekelezaji wa mradi husika.

 

Kadhalika, mradi huo, Serikali inamiliki asilimia 16 ya hisa na Kampuni ya Stradline Resources Limited inamiliki hisa asilimia 84. 

 

Katika ziara hiyo ilielezwa kuwa, kulingana na utafiti uliofanywa katika eneo hilo, kiasi cha mashapo yenye kiasi cha tani milioni 268 katika ubora wa asilimia 3.3 kimegunduliwa na uhai wa mradi huo unatarajia kuwa miaka takribani 23. 

 

Aidha, kulingana na taarifa za Wizara ya Madini, kampuni ya Nyati Mineral Sand Limited imeomba leseni kubwa ya uchimbaji madini (Special Mining Licence) na mchakato wa kutolewa leseni hiyo unaendelea. Vilevile, imeelezwa kuwa, utaratibu wa kulipa fidia wananchi watakaoathirika na mradi katika eneo hilo la pangani utafanyika mara leseni ya uchimbaji madini itakapotolewa na mara baada ya zoezi la kulipa fidia kukamilika shughuli za uchimbaji madini tembo kwenye mradi huo zitaanza.

 

Kampuni ya Strandline ni miongoni mwa kampuni 4 za uchimbaji wa  madini ambazo  mnamo  Desemba 13, 2021 Serikali  na kampuni husika zilitia saini makubaliano ya mikataba ikiwa ni matokeo ya marekebisho ya Sheria ya Madini  ambayo ilipelekea kuipa nguvu Serikali kumiliki rasilimali hizo kwa niaba ya wananchi kwa lengo la kuleta manufaa zaidi kwa watanzania.

 

Kampuni nyingine zilizoweka saini mikataba ya makubaliano kipindi husika ni pamoja Black Rock Mining Limited itakayochimba madini ya kinywe wilayani Mahenge mkoani Morogoro, Nyanzaga Mining Limited itakayochimba madini ya dhahabu wilayani Sengerema mkoani Mwanza na kampuni ya Petra Diamond Ltd inayochimba madini ya Almasi Mkoani Shinyanga ambapo katika makubaliano hayo Serikali iliongeza umiliki wa hisa katika mgodi huo kutoka asilimia 25 kufikia asilimia 37.

 

Hafla ya utiaji saini mikataba hiyo ilishuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu ambaye katika hotuba yake alisisitiza kuhusu shughuli za uongezaji thamani madini hayo kufanyika nchini ili kuleta manufaa zaidi kwa taifa.

 

Miradi ya madini tembo inatarajia kuinufaisha nchi kiuchumi ikiwa  ikiwa ni pamoja na Serikali kupata mapato yatokanayo na kodi, mrabaha, ada ya ukaguzi, ushuru wa huduma na malipo mengine yanayotakiwa kulipwa kwa  mujibu wa sheria za nchi, ikiwemo fursa za ajira kwa watanzania wakiwemo wanaozunguka eneo la mradi pamoja na ajira kupitia shughuli za utoaji huduma mbalimbali katika migodi hiyo.

 

Madini tembo yatakayochimbwa katika miradi hiyo ni pamoja na rutile, ilmenite, zircon na monazite. Madini hayo yana matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutengeneza vioo, rangi mbalimbali hususan za magari, kutengeneza ceramics (kauri) na pia hutumika katika kinu cha nyuklia.

ADAM MIHAYO ATINGA RASMI TCB KUANZA MAJUKUMU YA KIKAZI

$
0
0

  

Afisa Mtendaji Mkuu mpya wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Adam Mihayo (kushoto), akipata maelezo kutoka Kwa Mkurugenzi wa Mipango ya Benki hiyo Bw. Muondakweli Kaniki alipofika kuripoti rasmi nafasi ya kuongoza Benki hiyo baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB mwengine pichani ni Mkurugenzi Rasilimali Watu Wa Benki hiyo Bi. Diana Myonga. Hafla hiyo imefanyiaka hivi karibuni makao makuu ya TCB jijini Dar es Salaam

Afisa Mtendaji Mkuu mpya wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Adam Mihayo (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi wa Mipango ya Benki hiyo Bw. Muondakweli Kaniki alipofika kuripoti rasmi nafasi ya kuongoza Benki hiyo baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB wengine pichani ni Mkurugenzi Rasilimali Watu Wa Benki hiyo Bi. Diana Myonga, Mkurugenzi Wa Uendeshaji Karoli Shayo, Mkurugenzi Wa Sheria huyo ni Bi. Mystica Ngongi. Hafla hiyo imefanyiaka hivi karibuni makao makuu ya TCB jijini Dar es Salaam.

Afisa Mtendaji Mkuu mpya wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Adam Mihayo (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Benki hiyo Bi.Diana Myonga wakati alipokwenda kuripoti kushika nafasi ya kuongoza Benki hiyo wengine pichani ni maafisa wa TCB.
Afisa Mtendaji Mkuu mpya wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Adam Mihayo akipokea maua ikiwa ni ishara ya upendo kutoka kwa maafisa wa benki hiyo alipofika kuripoti rasmi nafasi ya kuongoza Benki hiyo baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB.

Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB awataka vijana kunoa ujuzi wao wa Karne ya 21

$
0
0

 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (kushoto) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya Kidato cha Nne ya shule za Feza Girls na Feza Boys akipokea zawadi kutoka kwa Joshua Zaipuna baada ya kutoa hotuba yake wakati wa Mahafali ya Kidato cha Nne yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaama.  (Na Mpiga Picha Wetu).

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (kushoto) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya Kidato cha Nne ya shule za Feza Girls na Feza Boys akimpongeza mwanafunzi aliyesoma risala Iqra Jamal, wakati wa Mahafali ya Kidato cha Nne yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaama. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Shule za Feza Tanzania, Ali Nungu na kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Feza Girls, Ibrahim Zanga. (Na Mpiga Picha Wetu).

  

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (kulia) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya Kidato cha Nne ya shule za Feza Girls na Feza Boys akimkabidhi cheti Loi Kitundu, wakati wa Mahafali ya Kidato cha Nne yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaama. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Shule za Feza Tanzania, Ali Nungu. (Na Mpiga Picha Wetu).

 

 

Na Mwandishi Wetu 

 

 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, amewashauri vijana nchini Tanzania kunoa ujuzi wao wa Karne ya 21 ili kufanikiwa katika soko la kisasa la kiushindani la ajira.

 

Akizungumza katika mahafali ya wanafunzi wa kidato cha nne wa Shule za Sekondari za Feza yaliyofanyika jijini Dar es Salam mwishoni mwa wiki, Zaipuna alisema ujuzi wa Karne ya 21 ni pamoja na kufikiri kwa kina, ubunifu, ushirikiano, mawasiliano, tekinolojia ya habari, uongozi, na stadi za maisha.

 

“Mkiwa na ujuzi huu, nina hakika kabisa kwamba mtafaulu katika shughuli zenu za maisha iwe mnataka kuajiriwa au kujiajiri. Mtawavutia waajiri na wawekezaji na kwa moyo wa kuendelea kujifunza, mtaimarika siku hadi siku na kujiongezea thamani,” Zaipuna alisema.

 

Aliongeza, “Kwa miaka mingi, nimekuwa sehemu ya Shule za Feza na ninathamini sana msisitizo ambao shule inaweka katika elimu ya maisha na maendeleo, ushirikiano na jamii na ukuzaji wa stadi za uongozi, sifa ambazo naamini zitakuwa na athiri chanya kwa watoto wetu kwa miaka mingi ijayo,” alisema.

 

Zaipuna alibainisha kuwa maisha ni safari na kuwataka vijana hao kufanya kazi kwa bidii na kuongeza kuwa wanaweza kufikia chochote wanachokusudia endapo wataendelea kuwa na nidhamu.

 

“Nilianza safari yangu takriban miongo mitano iliyopita. Miaka 32 iliyopita, nilihitimu kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Kilakala, Morogoro. Siku hii imenifanya kutafakari maisha yangu yote tangu nilipohitimu mwaka 1991,” alisema.

 

Aliwataka wanafunzi hao kujiamini, kufuata nafsi zao na kamwe wasipoteze maadili na kanuni walizopandikizwa wakiwa shuleni.

 

Alibainisha kuwa baadhi ya vitu ambavyo vimesaidia kupanda daraja la mafanikio ni pamoja na nidhamu, bidii, uadilifu, ubora katika kila kazi iwe kubwa au ndogo na kuendelea kujifunza mambo mbalimbali.

 

 “Licha ya vikwazo ambavyo mmekumbana navyo mkiwa hapa, mmeibuka kuwa nyota zinazongaa. Katika miaka yenu yote katika Shule za Feza, mmeonyesha dhamira isiyoyumba kwa kuendela kufanya vyema. Mafanikio haya ni uthibitisho wa bidii zenu" alisema.

 

Aliwashauri wahitimu hao kuchangamkia fursa zinazowajia huku akiongeza kuwa mafanikio hayapimwi kwa alama au sifa tu, bali pia kwa matokeo yanayopatikana katika maisha ya wengine.

 

Awali, Naibu Mkurugenzi wa Shule za Feza Ali Nungu aliwataka wahitimu kuendeleza miiko ya shule hiyo ilikuleta mabadiliko katika njia watakayochagua.

 

Aliwapongeza walimu wa shule hiyo, wafanyakazi wengine na wazazi ambao walichukua jukumu kubwa katika safari ya wahatimu hao na kuwataka wahitimu kuamini katika uwezo wao.

 

Alionyesha imani kwamba kwa tabia zao nzuri, uwezo bora wa kitaaluma na ustahimilivu, watakuwa wakakamavu na wenye shauku katika kutimiza ndoto zao.


ACT Wazalendo: Tumeshtushwa na Maafa ya Hanang

$
0
0

Chama cha ACT Wazalendo tumepokea kwa mshtuko, majonzi na simanzi kubwa taarifa za vifo vya watu 47 na majeruhi 85 vilivyotokea wilayani Hanang mkoani Manyara kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali nchini. 

 

Taarifa rasmi zinasema vifo hivyo na majeruhi vimesababishwa na mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia Jumapili Desemba 3, 2023 baada ya sehemu ya Mlima Hanang kumomonyoka na kusababisha tope kutiririka katika makazi ya watu wa maeneo ya Katesh na Gendabi wilayani humo.

 

Chama chetu kinatoa pole na salaam za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa maafa haya makubwa yaliyotokea huku tukiwaombea kwa Mwenyezi Mungu majeruhi waweze kupona haraka na kuendelea na maisha yao ya kila siku. 

 

 Aidha kutokana na maafa haya mazito, tunatoa wito kwa Serikali kuhakikisha majeruhi wanapata huduma zote stahiki zinazohitajika, huduma za kibinadamu kwa wakazi wote wa maeneo yaliyoathirika na maafa hayo sambamba na kukarabati miundombinu mbalimbali iliyoharibika kwa haraka zaidi.

Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>