Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

NMB yazindua Programu ya Kitaifa ya Ugawaji Mizinga ya Nyuki-Gairo

$
0
0


Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbas (wa pili kulia), akipokea sehemu ya mizinga 200 ya kufugia nyuki kwa ajili ya vikundi vya ufugaji vya wilaya za Gairo na Kilombero, kutoka kwa Afisa Mkuu wa Biashara za Serikali wa Benki ya NMB, Alfred Shao, wakati wa uzinduzi wa kitaifa wa Programu ya ugawaji mizinga hiyo kwa wafugaji wa mikoa ya Morogoro, Tabora na Njombe. Uzinduzi huo ulifanyika katika msitu wa Msingisi uliopo eneo la Kijiji cha Msingisi, wilayani Gairo. Wa pili kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Janeth Shango na kulia Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Jabir Makame. Na Mpiga Picha Wetu.  

 

 Na Mwandishi Wetu, Morogoro

 

Serikali imesema Tanzania ina mazingira mazuri ya uzalishaji wa mazao ya nyuki yenye kiwango cha juu cha ubora kutokana na uwepo wa misitu yenye mimea inayotoa chakula kwa nyuki huku sekta hiyo ikichangia ajira zaidi ya ajira ya watu milioni mbili na kukadiliwa kuwa na uwezo wa uzalishaji wa asali tani 138,000 kwa mwaka.


Akizungumza katika uzinduzi wa kitaifa wa ugawaji wa mizinga 500 iliyotolewa na benki ya NMB wilayani Gairo mkoani hapa, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk Hassan Abbas amesema uzalishaji watani 138,000 za asali ya nyuki kwa mwaka ni kiwango kidogo ikilinganishwa na fursa zilizopo na tathmini iliyofanywa na wizara hiyo inaonesha kuwa asilimia 90 ya wafugaji nyuki nchini wanatumia mizinga ya jadi.


Dk Abbas amesema mizinga hiyo ya jadi inachangia uharibifu wa misitu kwani utengenezaji wake unahusisha ukataji wa miti hivyo wadau na serikali wanajukumu la kuendeleza sekta hiyo kwa kuandaa mazingira mazuri ya upatikanaji wa mizinga ya kisasa ambayo italeta tija na kulinda misitu.


“Mizinga ya jadi inazalisha kiwango kidogo cha asali lakini asali ya Tanzania inakubalika kwenye masoko mbalimbali nje ya nchi sekta za misitu na ufugaji nyuki zinachangia wastani wa asilimia 3.5 ya pato ghafi la taifa ukilinganisha na fursa za rasilimali za misitu na nyuki zilizopo na niwaombe wenzetu wa NMB kuongeza mizinga ya kisasa ifikie 600 wakati serikali ikiandaa na kutekeleza mikakati ya ujenzi wa viwanda ambavyo kwa sasa vipo sana vya kuchakata na kufungasha mazao ya nyuki.”amesema Dk Abbas.


Juhudi hizi pia ni sehemu ya maandalizi yetu kuelekea Mkutano Mkuu wa Wafugaji Nyuki Duniani utakaofanyika Tanzania mwaka 2027, ambao utawahusisha waataalum wakimataifa  zaidi ya 4000.


Kwakweli Benki ya NMB mnastahili pongezi kubwa sana kwa kuzindua Programu Endelevu ya Ugawaji Mizinga ya Nyuki 500 kwa vikundi 17 vyenye wafugaji zaidi ya 300, katika mikoa ya Morogoro, Tabora na Njombe, mkishirikiana na Mamlaka ya Uhifadhi wa Misitu Tanzania (TFS).


Afisa mkuu wa wateja wakubwa na serikali benki ya NMB, Alfred Shao amesema benki hiyo imewezesha kutengeneza mizinga 500 ya kisasa kwa ajili ya kuwagawia wafugaji nyuki katika mikoa ya Morogoro, Tabora na Njombe.


Shao amesema licha ya kutoa mizinga hiyo, benki hiyo imetenga sh41milioni kwa ajili ya kuwezesha mafunzo kwa wanufaika wa mizinga hiyo katika mradi wa kusapoti ufugaji wa nyuki.


“Nyuki ili wazaliane ni lazima misitu ilindwe na moja ya sababu ya NMB kutoa mizinga hii 500 ni juhudi za kulinda misitu yetu ikienda sambamba na upandaji miti ambapo mpaka sasa miti 750,000 tayari imepandwa nchini kwa kushirikiana na TFS na wananchi wanapata mazao ya misitu kwa kutunza mazingira.”amesema Shao.


Shao amesema benki ya NMB kupitia NMB Foundation imetoa mizinga 500 ya kisasa kwa mikoa mitatu ambapo mkoa wa Morogoro umepata mizinga 200, Tabora 200 na Njombe 100 kwa vikundi 17 vya ufugaji nyuki na vikundi hivyo vitapatiwa elimu ya ufugaji nyuki wa kisasa, elimu ya kifedha na elimu ya uvunaji wa asali ili asali itayovunwa iwe ya ubora wa kiwango cha juu na kuuzwa nje ya nchi.


Serikali ya Rais Samia imeweka mkazo mkubwa katika sekta ya asali na nyuki, ambako tayari kuna Watanzania takribani milioni mbili wamejiari huko, na tunatambua hii ni sekta ya kimkakati ambayo ikitiliwa mkazo, itawakwamua wengi, vijana tuipe mkazo sekta hiyo ambayo ni itakuwa ya kijanja zaidi huko tuendako, yenye ‘maokoto’ ya kutosha,aliongeza Dk. Abbas.


“Usisubiri NMB waje, anza leo wakukute pazuri. Sekta hii inachangia Pato la Taifa kwa asilimia 3.5, pia mazao ya misitu na asali yanachangia asilimia 5.9 ya fedha za kigeni, huasusani Dola za Kimarekani, sio sekta yenye eneo dogo, bali ina mawanda mapana, vijana wasidharau sekta zenye kuingiza pesa kama hii, ambayo Serikali hatulali kwa kuchakata mipango mikubwa juu yake.


“Tumeanza ujenzi wa viwanda saba vya kuchakata na kufungasha asali, ili kukuza uchumi ambako Serikali imewekeza zaidi ya Sh. Bilioni 2 katika mikoa ya Tabora, Katavi, Geita, na Kigoma, NMB mtapoenda huko mtawakuta wafugaji. Mradi mwingine ni wa Sh. Bilioni 27 wa kujenga madarasa na mabweni ya Chuo cha Ufugaji Nyuki Tabora, NMB tunawaomba mje kuona uwekezaji wetu,” alibainisha.


Dk. Abbas aliongeza ya kwamba, Rais Samia hivi karibuni amefanya uamuzi mgumu wa kimkakati, kwa kuiingiza sekta ya asali na nyuki katika Programu ya Kujenga Kesho Iliyo Bora kwa Vijana na Wanawake nchini (BBT), hivyo akaziomba Sekta za Fedha na Sekta Binafsi, zifuate nyayo za NMB kwa kuisapoti Serikali katika kuipa thamani zaidi Kampeni ya Achia Shoka, Kamata Mzinga.


“Tutawaalika wadau tutapokamilisha kampeni hiyo waone jinsi ya kusaidiana na Serikali, ili kutanua sekta hii kuelekea Mkutano Mkuu wa Wafugaji Nyuki Duniani hapo mwaka 2027, utakaowaleta nchini zaidi ya washiriki 4,000 kutoka mataifa mbalimbali duniani. Mkutano huo ni uthibitisho wa Jumuiya ya Kimataifa kuridhishwa na hatua iliyopigwa na Serikali ya Rais Samia,” alisisitiza.


Naye Mkuu wa wilaya ya Gairo, Jabir Makame amesema programu ya boresha mazingira na uchumi kupitia ugawaji wa mizinga kitaifa kufanyika wilaya ya Gairo na wataendelea kuwapa hamasa jamii ya wilaya hiyo kuendelea kuhifadhi na kutunza mazingira.


Kamishna wa Uhifadi Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) TFS, Profesa Dos Santos Silayo amesema benki ya NMB imekuwa na ushirikiano nao katika utunzaji mazingira na upandaji miti tangu mwaka 2022 na sekta ya ufugaji nyuki inaonekana kama ni kazi ya wazee na kuwekeza nguvu utawafanya riba nyingine kuona tija katika sekta hiyo.


UCSAF: Bilioni 326 kuwezesha upatikanaji wa mawasiliano ya uhakika maeneo ya vijijini

$
0
0

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashiba, akiwasilisha Ripoti ya Utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo kwenye kikao kazi kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kilichofanyika jijini Dar es Salaam.



Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Deodatus Balile akizungumza wakati wa Kikao Kazi kilichoandaliwa na Ofisi ya Hazina jijini Dar es Salaam.



Na Mwandishi Wetu

 
Serikali kupitia mfuko wake wa mawasiliano kwa wote (UCSAF), imesema wananchi zaidi ya milioni 23 watapata huduma ya mawasiliano ya Simu kwa uhakika, baada ya kukamilika kwa mradi wa Ujenzi wa Minara 2,149 kwenye maeneo ya Vijijini, ambapo kiasi cha Shilingi Bilioni 326 zitatumika.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashiba, ametoa kauli hiyo leo Novemba 21, 2023 Jijini Dar es Salaam wakati akiwasilisha Ripoti ya Utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo kwenye kikao kazi kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.

"UCSAF kama taasisi ya Serikali  imeingia makubaliano ya Kimkata na watoa huduma ya Mawasiliano ili kufikisha huduma hiyo kwenye kata 1,974 zenye Vijiji 5,111, ambapo mpaka sasa Jumla ya Kata 1,197 zenye Vijiji 3,613 huduma hiyo ya mawasiliano imekwisha fika kwenye maeneo hayo" amesema  Bi Justina.

Kuhusu mradi wa Tiba mtandao Afisa Mtendaji Mkuu huyo amesema UCSAF inatekeleza kwa Kushirikiana na Taasisi ya DIT, Hospitali ya Muhimbili, Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Milango ya Fahamu (MOI) pamoja na Hospitali zingine kubwa hapa nchini.

"Hospitali zilizounganishwa mpaka sasa ni Hospitali ya mkoa wa Morogoro, wakati hospitali ambazo zipo kwenye hatua ya kukamilishwa ni pamoja na Hospitali ya mkoa wa Ruvuma, Tanga pamoja na Katavi" ameeleza Bi Justina Mashiba.

Benki ya CRDB yaipiga 'jeki' Shule ya Sekondari Bunju 'A'

$
0
0


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule (wa tatu kushoto), akipokea sehemu ya msaada wa viti na meza 5o kutoka kwa Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd (wa tatu kulia) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Wengine katika picha ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge, Mkuu wa Shule ya Sekondari Mbunju 'A' Bupe Mkondola (wa pili kushoto), Meneja wa Tawi la CRDB Kinondoni, Beatrice Bangesi (kulia), Meneja Mwandamizi Idara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Benki ya CRDB, Suzan Shuma (wa pili kulia).

Tawi la NMB Dumila lazinduliwa rasmi!

$
0
0

Wananchi wa Mji wa Dumila wilaya ya Kilosa wameondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kati ya kilometa 35 hadi 70 kufuata huduma za kibenki, baada ya benki ya NMB kufungua tawi la NMB Dumila.

 

Akizungumza katika uzinduzi wa tawi hilo, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi amesema wananchi wa Dumila na vijiji vinavyoizunguka walikuwa wakilazimika kusafiri umbali wa kilometa 35 kwenda Mvomero kufuata huduma za kibenki wakati kwenda Gairo kilometa 50, Kilosa kilometa 69 na Turiani kilometa 70.

 

Ameongeza kuwa, kufunguliwa kwa tawi hili inafanya NMB kuwa na matawi 231 nchi mzima na kuendelea kuongoza kwa kuwa na matawi mengi kuliko benki yoyote hapa  nchini na kuishi maana halisi ya kauli mbiu yao ya NMB Karibu yako.

 

Mgeni rasmi katika ufunguzi huo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima amesema, benki hiyo inawafikia wananchi wengi na kuwaomba wananchi kutumia benki hiyo, kwa sababu Dumila ina shughuli nyingi za kiuchumi ikiwemo kilimo na ufugaji.

 

Mhe. Malima amesema, uwepo wa tawi hilo katika Mji wa Dumila utaongeza tija kwa wakulima kupata mikopo ya kilimo lakini na wafugaji kupata mikopo ya kunenepesha mifugo, ili jamii inayoizunguma benki hiyo kunufaika kihuduma na kubadilika kiuchumi kwa mitaji yao kukua kwa sababu, Dumila sasa ni Mji wenye shughuli nyingi za kiuchumi kwa kukuza biashara zao.

 

Mhe.Malima alisisitiza kuwa Dumila ni miongoni mwa miji ya kibiashara unaokua kwa kasi na kwamba ukubwa wa mtandao wa NMB, uimara wake kimapato na huduma rafiki kwa wateja, vinaenda kuneemesha na kuwastawisha kiuchumi wafanyabiashara, wajasiriamali, wakulima na wafugaji wa kada zote watakaotumia fursa hiyo.

 

Alimaliza kwa kuipongeza NMB kwa lengo lake la kukopesha kiasi cha Sh. Bilioni 1 kwa wajasiriamali, wafanyabiashara, wakulima na wafugaji kwa mwaka wa kwanza, huku akiwataka wana Dumila, Kilosa na Morogoro kwa ujumla, kuchangamkia fursa za ujio wa tawi hilo alilolitabiria kuwa kinara kimafanikio kuliko matawi yote ya mkoa huo.

 

Wakati huohuo, Benki ya NMB kupitia sera yake ya uwajibikazi kwa jamii, imetumia fursa hiyo kutoa meza 30 na viti 30 kwa ajili ya walimu wa Shule ya Sekondari ya Sokoine na madawati 53 kwa shule ya Msingi Kwadoli vyote vikiwa na thamani ya Sh. Milioni 11.

 

 

 

UTT AMIS ilivyoshiriki Wiki ya Huduma ya Fedha Kitaifa jijini Arusha 2023

$
0
0
WAZIRI MKUU AFUNGUA WIKI YA HUDUMA YA FEDHA KITAIFA





 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Fedha iimarishe mifumo ya kuwalinda watumiaji wa huduma za fedha ili baadhi ya watoa huduma wasio waadilifu wasitumie changamoto ya uelewa mdogo wa masuala ya fedha kwa baadhi ya wananchi na kuwadhulumu.

Pia, Mheshimiwa Majaliwa amesema Wizara ya Fedha iendelee kushirikiana na na watoa huduma za fedha kutoa elimu kwa wananchi katika maeneo muhimu yakiwemo ya usimamizi wa fedha binafsi, kuweka akiba, mikopo, uwekezaji kupitia hatifungani na hisa, bima, mpango wa kujiandaa na maisha ya uzeeni pamoja na kodi.

“Wizara ya Fedha iandae mpango maalumu wa kutoa hamasa kwa Watanzania ili wajenge utamaduni wa kutumia huduma rasmi za kifedha, pia elimu iendelee kutolewa kuhusu wajibu wa kila mmoja kudai na kutoa risiti kwa malipo yanayofanyika. “

Ametoa maagizo hayo leo (Jumatano, Novemba 22, 2023) alipofungua Wiki ya Huduma ya Fedha Kitaifa, jijini Arusha, ambapo ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa watoa huduma za kifedha wapunguze gharama za upatikanaji wa huduma za fedha zikiwemo riba na ada ili wananchi wengi watumie huduma za fedha zilizo rasmi.

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameisisitiza Wizara ya Fedha iendelee kusimamia na kuratibu utekelezaji wa Programu ya kutoa elimu ya fedha kwa umma na kuhakikisha kuwa elimu hiyo inawafikia wananchi wengi zaidi mijini na vijijini.

Waziri Mkuu amesema Wizara ya Fedha inatakiwa iandae mpango maalumu wa kutoa hamasa kwa Watanzania ili wajenge utamaduni wa kutumia huduma rasmi za kifedha pamoja na kuratibu gharama za huduma za fedha. “Pia, elimu iendelee kutolewa kuhusu wajibu wa kila mmoja kudai na kutoa risiti kwa malipo yanayofanyika.“

Waziri Mkuu amesema watoa huduma za kifedha hawana budi kujenga uelewa wa kutosha kwa wananchi kabla ya kufunga nao mikataba, pamoja na kuwafafanulia taratibu na masharti yao kabla hawajatoa kwao huduma hizo za fedha. Pia amewataka watoa huduma hao waweke mkakati mahususi wa kuongeza matumizi huduma kwa njia ya kidijitali pamoja na kuzisogeza hadi maeneo ya pembezoni na vijijini ili wananchi walio wengi wanufaike.

“Watoa huduma za fedha ongezeni ubunifu katika utoaji wa huduma. Toeni huduma zinazoendana na wakati, mahitaji ya soko na kuzingatia uhitaji wa makundi mbalimbali katika jamii. Suala hili liende sambamba na kuwaunganisha wajasiriamali na fursa mbalimbali zinazotolewa na sekta ya fedha katika kukuza na kuimarisha biashara zao. “

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amewataka wasimamizi wa Sekta ya Fedha na wadau wengine wazingatien sheria na kanuni za kuwalinda watumiaji wa huduma za fedha ikiwemo kutatua malalamiko na migogoro na kulipa fidia na mafao kwa wakati.

Amesema lengo la maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa na Maonesho ya Huduma za Fedha yamejikita katika kujenga uelewa kwa wananchi kuhusu matumizi sahihi ya huduma za fedha zinazotolewa, kusimamia vizuri rasilimali fedha ikiwa ni pamoja na kuimarisha utamaduni wa kujiwekea akiba, kukopa kutoka vyanzo salama na njia sahihi za kulipa madeni ili kujenga uchumi na kuondoa umaskini.

Naye, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali inaendelea kukuza uelewa kwa Watanzania kuhusu masuala ya kifedha huku akitoa wito kwa Watanzania kuweka utaratibu wa kusoma vigezo na masharti ya huduma za kifedha wanazopata kutoka katika taasisi mbalimbali za kifedha ili kuepuka changamoto zinazoweza kujitokeza baadae.

"Ni vyema tukaweka utaratibu wa kusoma na kuelewa vigezo na masharti tunapokuwa tunapatiwa huduma za kifedha hasa mikopo ili tujiepushe kuingia kwenye mikopo yenye masharti magumu ambayo wakati mwingine tunaweza kushindwa kuyatekeleza."

Kwa Upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Bi. Natu El-maamry amesema maadhimisho hayo ya tatu ni muendelezo wa jitihada za Serikali katika kuongeza uelewa wa masuala fedha kwa Watanzania ili waweze kuwa na uelewa kuhusu matumizi sahihi ya huduma za kifedha.

Amesema taasisi mbalimbali za kifedha na wadau wa kisekta wanatumia kipindi hiki kutoa elimu na huduma kwa wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.

MIKTA kusherehekea muongo mmoja wa ushirikiano, yaahidi kuongeza mashirikiano na Tanzania

$
0
0

Balozi za Indonesia, Korea na Uturuki (MIKTA) zilizopo nchini Tanzania zimeahidi kuongeza mashirikiano na Taasisi ya Mafunzo ya Maendeleo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

 


Balozi hizo zilisema hayo katika warsha waliyoandaliwa kwa kulikutanisha Jopo la wanazuoni iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Kampasi ya Mlimani kwenye majadiliano ya maendeleo ambapo Mada Kuu ilikuwa “Jifunze kutoka MIKTA: njia ya Tanzania kuelekea ukuaji na mabadiliko katika ulimwengu wa kidijitali”.

 

Akizungumza katika warsha hiyo, Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mehmet Güllüoğlu amesema kuwa uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Uturuki unaendelea kuwa imara kutokana na viongozi waliopo madarakani.

 

Naye Balozi wa Indonesia, Triyogo Jatmiko amesema kuwa mwezi Februari Mwaka 2024, Indonesia mafunzo yakilenga usindikaji wa muhogo baada ya kuvuna.

 

Kwa upande wake Balozi wa Korea, Kim Sun Pyosaid, aliipongeza MIKTA kwa kuandaa mkutano nchini Tanzania ambapo amesema kuwa mkutano uo umefungua muhusiano na mashirikiano mema ya kimaendeleo  kati ya MIKTA, Tanzania na washirika wengine.

 

Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Dk. William Anangisye alifungua mjadala huo kwa kukumbusha kazi kubwa ya Hayati Rais Julius Nyerere katika kukuza ushirikiano na mashirikiano kati ya Tanzania na nchi nyingine za Ulimwengu wa Kusini kupitia Jumuiya zisizofungamana na upande wowote.

 

Ambapo amesema kuwa inapaswa kukuzwa na kuimarishwa kwa ahadi za pamoja kati ya Tanzania na nchi hizo.

 

Jukwaa la MIKTA lilianzishwa mwaka 2013 kwenye Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la 68 la Umoja wa Mataifa, likiwa ni jukwaa la mashauriano kati ya nchi za kidemokrasia zenye uchumi huria.

 

Hivyo, mwaka huu MIKTA inasherehekea mkutano wake muhimu wa viongozi wa maadhimisho ya miaka 10 kwenye Mkutano wa Bali G20, Novemba 15, 2022.

 

MIKTA kikiongozwa na maadili ya kidemokrasia ya pamoja kama maadili ya pamoja ya demokrasia ina jukumu muhimu katika kushughulikia masuala ya kimataifa kama vile mabadiliko ya hali ya hewa, maendeleo endelevu, na uwezeshaji wa wanawake.

 

Katika kukabiliwa na changamoto za kimataifa, kikundi cha MIKTA kinasimama kwa umoja katika kutatua migogoro na kuchangia amani ya kimataifa, utulivu na ustawi.

 

Wakati ulimwengu unapambana na hatari inayoendelea ya magonjwa ya milipuko, kuongezeka kwa mivutano ya kijiografia, na kuongezeka kwa migawanyiko kati ya mataifa, MIKTA inaendelea kujitolea kukuza umoja na usawa.

 

Mkutano mkuu wa MIKTA, unajumuisha mikutano miwili ya mawaziri wa Mambo ya Nje ambapo kunakuwa na majadiliano ya wazi kuhusu masuala ya kimataifa.

 

Vile vile, mkutano mkuu wa MIKTA unajumuisha viongozi kutoka serikalini, mabunge, wasomi, mizinga ya kufikiri, na vyuo vya kidiplomasia.

 

MIKTA kama wanachama wa G20 wanaochangia zaidi ya asilimia 10 kwa biashara za kimataifa, wanasisitiza kukuza demokrasia, uchumi na kuimarisha ushirikiano kwa nchi na mashirika mbali mbali ya kimaendeleo.

 

 

 

Mkutano huo utahusisha wazungumzaji ambao ni wataalam kutoka nchi zote wanachama wa MIKTA, kukuza ushirikiano na kubadilishana maarifa na nchi nyingine za Pembezoni (Global South) ikiwa ni pamoja na Tanzania.

 

Chini ya uenyekiti wake ambaye ni Indonesia kuanzia Machi 2023 hadi Machi 2024, MIKTA imeimarisha dhamira yake ya kuimarisha ushirikiano, maendeleo kupitia njia za kidijitali.

 

MIKTA iliundwa na nchi za (Mexico, Indonesia, Korea, Uturuki na Australia)  

TBA kuwachukulia hatua za kisheria Wadaiwa Sugu, yawadai Wapangaji Sh Bilioni 7.8

$
0
0
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA,) umesema kuwa hadi sasa jumla ya fedha kiasi cha Sh bilioni 7.8 zinadaiwa kwa wapangaji wake zikiwemo taasisi za umma zinazotumia nyumba na majengo yake.

Akizungumza na wanahabari jijini humo Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Daud Kondoro amesema kuwa wapangaji wote zikiwemo taasisi za umma zinatakiwa kuhakikisha zinalipa madeni yao kwa wakati kabla hatua kali hazijachukuliwa dhidi yao.

 

"Kwa sasa TBA imeazimia kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wapangaji wote tunaowadai, moja ya hatua zitakazochukuliwa ni kuwaondoa wadaiwa sugu kwa nguvu kwa kutumia dalali wa Mahakama ambaye amepewa zabuni hiyo kufanya kazi kwa niaba ya TBA. Mpaka sasa tayari dalali wa mahakama ambaye ni Twins Auction Mart amekabidhiwa orodha ya wadaiwa wote kwa hatua zinazofuata na zoezi hili litafanyika kuanzia Desemba 1, 2023 katika Mikoa yote nchini." ameeleza Kondoro.

 

Aidha amesema, hatua hiyo itakwenda sambamba na kuwafungulia mashtaka wadai wote watakaondolewa katika nyumba na majengo hayo ili kuhakikisha kuwa fedha yote inayodaiwa inakusanywa.

 

Vile vile ameeleza juu ya maboresho yaliyofanyika kwenye mfumo wa kielekroniki. “Kuanzia tarehe 1 Desemba, 2023, tutaanza kutumia mfumo mpya wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Miliki za Serikali (GRMS) toleo la 2.Mfumo huu mpya utakuwa unatoza riba ya 20% kwa mpangaji atakae kaa zaidi ya miezi 3 bila kulipa kodi ya pango. Riba hiyo itaendelea kutozwa kila mwezi kwa kiwango mfuto (automatically) cha 20% mpaka deni lote litakapokamilika kulipwa” amesema Arch. Kondoro.

 

"Hadi kufikia Oktoba 31 mwaka huu TBA inadai zaidi ya Bilioni 7.8 za kodi ya pango kutoka kwa wapangaji wa nyumba na majengo yanayomilikiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) nchi nzima ambapo zaidi ya Bilioni 3.5 ni madeni ya Taasisi mbalimbali za Serikali." Amesema.

 

Kuhusiana na hatua ya kuwaondoa wadaiwa sugu kwa kutumia dalali wa Mahakama ambaye amepewa zabuni hiyo kwa niaba ya TBA; Arch Kondoro amesema kampuni ya udalali wa Mahakama ya Twins Auction Mart imeshakabidhiwa orodha ya wadaiwa wote kwa ajili ya utekelezaji wa zoezi la kuwaondoa kuanzia Desemba Mosi mwaka huu na hatua itakayofuata mara baada kuondolewa katika nyumba hizo kuwafungulia kesi za madai mahakamani wadaiwa hao ili kuhakikisha wanalipa madeni hayo.


"Madeni haya ni ya mwaka wa Fedha uliopita...Na Mikoa kinara ni taasisi za Umma katika mikoa ya Dodoma, Arusha, Mwanza na Mbeya ambayo deni limefikia shilingi Bilioni 1.4......Nitoe rai kwa wapangaji wote zikiwemo taasisi za Umma kuhakikisha wanalipa madeni yao kwa wakati mara baada ya kupokea namba za kumbukumbu za malipo yaani control number ambazo hutumwa kwa kila mpangaji Kila mwezi kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS.)" Amefafanua.
 

Aidha, Arch. Kondoro ameeleza kuwa; Kuanzia Desemba 1, 2023, Wakala hiyo itaanza kutumia mfumo mpya wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Miliki za Serikali (GRMS) toleo la 2.
 

"Mfumo huu mpya utakuwa unatoza riba ya 20% kwa mpangaji atakae kaa zaidi ya miezi 3 bila kulipa kodi ya pango. Riba hiyo itaendelea kutozwa kila mwezi kwa kiwango mfuato (automatically) cha 20% mpaka deni lote litakapokamilika kulipwa. Utekelezaji huu ni kwa mujibu wa kifungu Na. 5.2 cha mkataba wetu wa upangishaji." Amesema.
 

Takribani nyumba 1716 zinazomilikiwa na TBA zimepangishwa kwa watumishi na viongozi wa Umma nchi nzima huku utekelezaji wa miradi hiyo ukiendelea nchi nzima na katika jitihada za kuepukana na ulimbikizwaji wa madeni ya pango TBA imekuja na ubunifu kwa miradi inayotekelezwa sasa kutumia vitasa janja (smartlock) kwenye majengo mapya ili kudhibiti malimbikizo ya kodi ya pango huku mpango huo wa kufunga vitasa janja ukidhamiriwa kutekelezwa katika nyumba za zamani.

Mradi kuimarisha mtandao wa mifumo ya Mbegu wazinduliwa

$
0
0

Na Selemani Msuya


WAKULIMA wa Afrika wameshauriwa kutumia mbegu asili katika kilimo kwa kuwa nichangia salama kwa afya, uhuru wa chakula, kukuza uchumi na uhakika wa soko.


Ushauri huo umetolewa leo na Mratibu wa Mtandao wa Bioanuai Afrika (ABN), Dk Fassil Gebeyehu wakati akizindua  Mradi wa Kuimarisha Mtandao wa Mifumo ya Mbegu (FMSS) inayosimamiwa na wakulima kwa uhuru wa chakula kwa upande wa Tanzania.


Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam katika makoa makuu ya Shirika la Envirocare, ambapo mratibu huyo amesema dunia inatakiwa kusisitiza kilimo cha kutumia mbegu asili kwani ndio salama kwa maisha ya watu.


Dk Gebeyehu amesema mradi huo unatekelezwa katika nchini tatu ambazo ni Kenya, Uganda na Tanzania na utamalizika Oktoba 2024, ambapo lengo kuu ni kuhakikisha mbegu asili zinapewa kipaumbele kwenye kilimo.


"Leo tumezindua Mradi wa Kuimarisha Mtandao wa Mifumo ya Mbegu inayosimamiwa na wakulima kwa uhuru wa chakula kwa upande wa Tanzania utatekelezwa na Mtandao wa Bionuai Tanzania (TABIO) na Shirika la Envirocare, tunaamini ndani ya mwaka tutapata mwelekeo kuhusu eneo hili, muhimu kwa maisha yetu, kwani mimi naamini usalama wa mbegu ni usalama wa maisha yetu," amesema.


Amesema ABN imekuwa ikitumia mbinu ya kukutana na jamii na kuielezea faida za matumizi ya mbegu asili, hivyo ni imani yake kuwa mradi huo utajikita katika kutoa elimu kwa makundi yote ili yaelewe umuhimu wake.


"Lengo kuu la jitihada hii ni kuimarisha mifumo ya mbegu inayosimamiwa na wakulima, kukuza uhuru wa chakula Kenya, Uganda, na Tanzania kwa kuwawezesha wakulima wa ndani, mradi unalenga kuongeza tofauti (anuai) ya mbegu, kuimarisha ushiriki wa jamii, na kuchangia kwenye uhakika na usalama wa chakula Afrika ya Mashariki, tukijikita kwenye elimu tutaweza kupata suluhisho,"ameongeza.


Amesema tafiti zilizofanyika zimeonesha wazi kuwa mbegu asili zinachangia uzalishaji mwingi, usalama wa chakula na soko la uhakika, hivyo ni vema nguvu ikaelekezwa huko.


Kwa upande wake Mratibu Mawasiliano, Ushauri wa ABN, Venter Mwongera amesema mradi huo unafadhiliwa na Bread for the World (Brot) na unatarajia kufukia makundi mbalimbali 2,000 ya wakulima, watunga sera 50 na wadau wa sekta hiyo 5,000 katika nchi husika.


Amesema ABN inatamani kuona mkulima mdogo ananufaika na kilimo na hilo litawezekana iwapo mbegu zao zitapewa kipaumbele kwenye Serikali na wadau wengine.


"Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), 2, 13 na 15 yanazungumzia uhakika wa chakula na mazingira, hivyo ili watu wasiwe na njaa ni vema tuungane pamoja kusisitiza kilimo cha mbegu asili kwani kina uhakika zaidi," amesema.


Venter amesema ili kampeni hiyo iweze kupenya kwa urahisi ni muhimu vyombo vya habari vinatumika, kwani ni nyenzo muhimu katika kufikisha ujumbe kwa jamii na wafanya maamuzi.


Aidha, mratibu huyo ameshauri wadau wa mbegu asili kuweka mkazo kwenye matumizi ya mitandao ya kijamii ambapo kuna wafuatiliaji, hali ambayo itaongeza msukumo wa kampeni hiyo muhimu kwa maisha ya wanadamu.


Mratibu wa TABIO, Abdallah Mkindi amesema mradi huo umezinduliwa nchini, hivyo wataweka mkazo mkubwa wa kuhakikisha wanafikia makundi yote ambayo yanaweza kufanikisha mchakato mzima wa kuzifanya mbegu asili ziweze kutambulika na kuthaminiwa.


Mkindi amesema mbegu asili zimethibitika kuwa ni salama kwa afya ya binadamu, hivyo ujio wa ABN na  miradi huo unafungua ukurasa mpya wa mapambano ambayo yatawezesha wakulima nchini kunufaika na mbegu hizo.


"Sisi TABIO na Envirocare tutashirikiana na wadau wote ambao kwa njia moja au nyingine wanashiriki kuhamasisha matumizi ya mbegu asili, ili serikali iweze kuweka mazingira mazuri yatakayofanywa mbegu hizi zitambulike kisheria na kisera," amesema.


Amesema mbegu za mkulima zinapitia changamoto kubwa ya teknolojia ambayo ndio imechukua nafasi, hivyo ni vema kila mpenda usalama wa chakula kuungana nao.


Naye Ofisa Program wa ABN, kutoka Envirocare Euphrasia Shayo amesema watakutana wadau kutoka serikali yaani watunga sera, mashirika yanayojihusisha na kilimo na wakulima ili dhamira ya kukuza sekta hiyo kupitia mbegu asili iweze kufikiwa.


"Sisi na TABIO tutahakikisha mbegu asili zinapewa msukumo kwa kutoa elimu kwa makundi yote," amesema.


Ofisa Uraghibishi na Uchechemuzi wa Kituo cha Bioanuai Afrika, Sabrina Masinjila amesema uwepo wa sera na sheria kuhusu mbegu za wakulima ambazo bado hazijapewa kipaumbele.


Pia Masinjila amesema uwepo wa sheria na sera utafanikiwa kwa haraka kwa elimu kutolewa zaidi hasa kwa makundi ya wakulima ambao wengi wapo vijijini.


Kwa upande wake Mtafiti kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, William Ernest amesema chuo hicho kimejikita kwenye utafiti wa mbegu asili kwa kuwa wanaona ni eneo muhimu kwa hatima ya mkulima na walaji.


Ernest amesema kukosekana kwa uhuru wa mbegu matokeo yake ni kukosekana kwa uhuru wa chakula, hivyo wameamua kutafiti eneo hilo ili uhuru wa chakula uwepo.


"Mbegu asili ni endelevu, salama na zinatoa uhuru wa chakula, lazima tupambane kwa pamoja kufanikisha kampeni hii," amesema.


Nao wakulima wa mbegu asili Yusuph Ndama kutoka kijiji cha Italagwe wilayani Gairo mkoani Morogoro na Deodatus Bajuta kutoka Karatu mkoani Arusha wamesema mbegu hizo ndio uhakika wa afya bora na endelevu.


Wakulima hao wamesema mazao yanayozalishwa kwa mbegu asili ni tiba ya magonjwa mengi na kuomba Serikali iweke mkazo kwenye eneo hilo.


DUKE ABUYA ANG'AA MWEZI OKTOBA SFG FC

$
0
0

Na John Marwa


Kiungo Mshambuliaji wa Singida Fountain Gate FC Duke Abuya amenyakua tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Oktoba inayotolewa na Jet & Sons Campany Limited ambao ndio wadhamini wa tuzo inayotolewa kila mwezi klabuni hapo.



Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Singida Fountain Gate FC kupitia mitandao ya kijamii imemtangaza Duke Abuya kutwaa tuzo hiyo mwezi Oktoba.



"Leo tumepokea Tuzo yazaji Bora wa Mwezi Oktoba, Duke Abuya, kutoka kwa Mdhamini wetu Jet & Sons Company Limited.


"Abuya ametunukiwa tuzo hii baada ya kikidhi vigezo vilivyotumika kumchagua katika mechi zote alizocheza Mwezi Oktoba, 2023." Imeeleza taarifa hiyo na kuongeza kuwa.


"Miongoni mwa vigezo vilivyotumika ni pamoja na; Nidhamu, msaada wake kwa timu kwenye nafasi anayocheza, Mwendelezo mzuri na kucheza 85% ya mechi zote za Oktoba.


"Ndani ya mwezi Oktoba, timu yetu ilicheza mechi tano zifuatazo:


"1. Future FC vs Singida FG (CAFCC)

2. Mtibwa Sugar FC vs Singida FG (NBCPL)

3. Singida FG vs Simba SC (NBCPL)

4. Namungo FC vs Singida FG (NBCPL)

5. Yanga SC vs Singida FG (NBCPL).


Tuzo iliyoambatana na zawadi ya kitita cha shilingi milioni moja (1,000,000/=) ilikabidhiwa na Mkurugenzi wa Jet & Sons Company Ltd, Ndg Edgar Tarimo na kupokelewa na Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Singida Fountain Gate, Hussein Massanza, kwa niaba ya mchezaji ambaye anatarajia kurejea Tanzania leo akitokea kwenye majukumu ya Timu ya Taifa nchini Kenya." Imebainisha kuwa.


"Makabidhiano ya zawadi na Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi yamefanyika katika ofisi za Jet & Sons Jijini Dodoma." Imehitimisha taarifa hiyo.

Waziri Prof. Mkenda kufungua Kongamano la Wathibiti Ubora wa Elimu ya Juu Barani Afrika (AfriQAN)

$
0
0

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kwa kushirikiana na Mtandao wa Wathibiti Ubora wa Elimu ya Juu Barani Afrika (African Quality Assurance Network -  AfriQAN), imeaandaa Kongamano la Mtandao wa Wathibiti Ubora wa Elimu ya Juu Barani Afrika litakalofanyika tarehe 28 - 30 Novemba 2023 katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

Kongamano hili lenye lengo la kujadili mchango wa uthibiti ubora katika kuongeza umahiri wa elimu ya juu Barani Afrika linatarajiwa kuhudhuriwa na washiriki wapatao 100, wakijimuisha: Taasisi za Uthibiti Ubora wa elimu ya juu; Makamu Wakuu wa Vyuo Vikuu na Wakuu wa Taasisi za Elimu ya Juu; Jumuiya na Asasi za Kimataifa na Kikanda zinazojihusisha na Elimu ya Juu; Wanataaluma; Mabaraza na Bodi za Usajili wa Wataalamu; na Wadau wa Elimu ya Juu kutoka ndani na nje ya nchi.

Mgeni Rasmi tarehe 28 Novemba 2023 katika ufunguzi wa kongamano hili ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Profesa Adolf Mkenda.

Kampuni ya T-PESA yatoa elimu kwa wateja wao

$
0
0

 

Bw. Thomas Lemunge Afisa Mauzo Shirika la Mawasiliano Tanzania akitoa elimu kuhusu huduma za T- PESA kwa kwa wakazi wa Arusha walipotembelea Banda la T-PESA wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu 'Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi yanayoendelea katika Viwanja vya Shekhe Amri Abeid jijini Arusha.


Bw. Thomas Lemunge Afisa Mauzo Shirika la Mawasiliano Tanzania akitoa elimu kuhusu huduma za T- PESA kwa kwa wakazi wa Arusha walipotembelea Banda la T-PESA wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu 'Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi yanayoendelea katika Viwanja vya Shekhe Amri Abeid jijini Arusha.

Bi. Catherine Simba wa Shirika la Mawasiliano Tanzania akitoa elimu kuhusu huduma za T- PESA kwa mkazi wa Arusha alipotembelea Banda la T-PESA wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu 'Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi yanayoendelea katika Viwanja vya Shekhe Amri Abeid jijini Arusha.

Bw. Thomas Lemunge Afisa Mauzo Shirika la Mawasiliano Tanzania akitoa elimu kuhusu huduma za T- PESA kwa kwa wakazi wa Arusha walipotembelea Banda la T-PESA wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu 'Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi yanayoendelea katika Viwanja vya Shekhe Amri Abeid jijini Arusha.


KAMPUNI Tanzu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania, T-PESA imesema kuwa uwepo wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa umeleta chachu katika utoaji wa elimu kwa Wateja wake na Wananchi kwa ujumla kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni hiyo.

 

Hayo yameelezwa na Afisa Uhusiano wa TTCL, Bi. Adeline Berchimance akizungumza katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha yanayofanyika Viwanja vya Shekhe Amri Abeid jijini Arusha.

 

Amesema Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na kuzishirikisha Taasisi ndogo za fedha, Mabenki, Mifuko ya Hifadhi za Jamii pamoja na wajasiriamali yameisaidia Kampuni ya T-PESA kukutana na Wananchi na kuwajengea uelewa kuhusu matumizi sahihi ya fedha mtandao na fursa mbalimbali zinazopatikana katika Kampuni hiyo zinazoweza kuwasaidia kujikwamua kiuchumi.

 

Amesema katika kuunga juhudi za Serikali za kutatua changamoto ya ajira kwa vijana T-PESA imetoa fursa mbalimbali kwa vijana zinazoweza kuwasaidia kujitengenezea kipato na hivyo kujikwamua kiuchumi.

 

"T-PESA inazo fursa mbalimbali hasa kwa vijana ikiwa ni pamoja na uwakala ambapo wanaweza kufanya biashara hii ya kuwa Wakala na kujipatia kipato cha kusaidia familia zao kwani T-PESA tunatoa kamisheni kubwa zaidi ukilinganisha na mitandao mingine," amesema Bi. Adeline.

 

Aidha amesema Maadhimisho hayo pamoja na mambo mengine yametoa fursa kwa Kampuni hiyo kukutana na Wateja na Wananchi kwa ukubwa zaidi na kujibu hoja, maswali na kero zao na hivyo maadhimisho hayo yamekuwa muhimu katika kupata mrejesho sahihi kuhusu huduma na bidhaa zinazotolewa na T-PESA.

 

Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanafanyika kwa mara ya tatu sasa huku kwa mwaka huu yakibeba kaulimbiu ya, ‘Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi na kuzinduliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali.

WATENDAJI KATA, MAAFISA TARAFA WATAKIWA KUFANYA KAZI KAMA TIMU SINGIDA

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Muragili ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa Peter Serukamba, akifungua  mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo Watendaji wa Kata na Maafisa Tarafa wa Mkoa wa Singida yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mtaa (TAMISEMI) yaliyoanza leo Novemba 23, 2023.

 

...............................................


Na Dotto Mwaibale,Singida

 

 WATENDAJI wa Kata na Maafisa Tarafa wa Mkoa wa Singida wametakiwa kufanya kazi kama timu ili kuondoa misuguano isiyo ya lazima wakati wa utendaji wa kazi za kuwahudumia wananchi kwenye maeneo yao.

 

Ombi hilo limetolewa na Mhadhiri kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo ki;ichopo Dodoma, Paul Faty wakati akitoa mada kwenye mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo maafisa hao yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mtaa (TAMISEMI) yaliyoanza leo Novemba 23, 2023.

 

Faty alisema mara nyingi kumekuwa kukitokea muingiliano katika utendaji wa kazi kwa maafisa hao na kusababisha kushindwa kufanya kazi ipasavyo za kuwahudumia wananchi kutokana na sababu mbalimbali.

 

“Kufanya kazi kama timu na kushirikishana kutawafanya muweze kuwahudumia wananchi vizuri katika maeneo yenu kwa kusimamia utekelezaji wa sera, sheria kanuni na miongozo ya Serikali ,” alisema Faty.

 

Aidha, Fati alisema kuwa moja ya majukumu wanayopaswa kuyafanya ni kuwasikiliza wananchi na kutatua kero zao kwani wao ndio waliopewa dhamana ya kuonana nao moja ka moja na ni kiunganishi kati yao na Serikali.

 

Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Muragili ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa Peter Serukamba kufungua mafunzo hayo alisema  lengo la mafunzo hayo ni kuwaongezea ujuzi na maarifa  wakati wa kutekeleza majukumu yao ili kupunguza kama siyo kuziondoa kabisa changamoto wanapo wahudumia wananchi na kuimarisha mahusiano baina yao na Serikali.

 

Mragili aliwakumbusha baadhi ya majukumu yao maafisa Tarafa na watendaji hao wa kata kuwa ni pamoja na kumwakilisha na kumsaidia mkuu wa wilaya katika utekelezaji wa shughuli za Serikali kuu na Taifa, kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo kwenye Tarafa zao na kuwa kiungo cha wananchi na kata husika.

 

Mambo mengine aliyowakumbusha ni kushughulikia malalamiko ya wananchi katika Tarafa, kufuatilia na kuhimiza utekelezaji wa Sera za Serikali katika maeneo yao na kuhakikisha zinatekelezwa ipasavyo, kushiriki katika kupanga miradi ya maendeleo katika kata na kuwa mtendaji mkuu wa kata ni kiungo wa idara zote katika kata.

 

Alitaja mambo mengine aliyowakumbusha maafisa hao kuwa ni kuandaa mpango kazi wa maendeleo katika kata na kuhuwasilisha kwa mkurugenzi na Afisa Tarafa, kutafsiri na kusimamia utekelezaji wa sera, sheria kanuni na miongozo ya Serikali katika kata, mratibu wa upangaji wa mipango shirikishi ya maendeleo katika kata na kupokea na kutatua malalamiko na matatizo ya wananchi katika kata.

 

Naye Naibu Mkuu wa chuo hicho Dkt. Michael Msendekwa akizungumza kwa niaba ya mkuu wa chuo hicho, alisema chuo hicho kilianzishwa kwa sheria namba 26 sura 396 lengo kubwa likiwa ni kuziwezesha mamlaka za Serikali za Mitaa ziweze kutekeleza majukumu yake.

 

Alisema chuo hicho kimekuwa kikitoa mafunzo ya muda mfupi na mrefu yenye programu sita kuanzia ngazi ya cheti na sasa wanatoa shahada ya kwanza na kueleza kuwa kimejipanga kuiwezesha Serikali za Mitaa.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Idara ya TAMISEMI, Hamisi Mkanga alisema mafunzo hayo yalianzishwa kwa ajili ya kuwajengea uwezo maafisa Tarafa na watendaji kuanzia ngazi ya chini kabisa ndipo walipo omba chuo hicho kiwatafutie mada ambazo zitaendana na maafisa hao kwa kukumbushana mambo mbalimbali.

 

Alisema mafunzo hayo ya siku mbili yatawashirikisha walengwa hao katika mada mbalimbali ambazo wataweza kuzifanyia kazi.

 

Alisema mada ambazo watafundishwa ni takribani 13 na kuwa mafunzo hayo kwa awamu ya kwanza yalifanyika mikoa ya Katavi, Rukwa, Njombe pamoja na Songwe na kwa awamu hii ya pili kuna mikoa ya Singida, Shinyanga, Tabora, Pwani, Dar es Salaam, Lindi pamoja na Mtwara na kuwa wataendelea kutoa mafunzo hayo kwenye mikoa mingine kulingana na jinsi watakavyokuwa wanapata fedha.

 

Mkanga alitumia nafasi hiyo kuwasihi washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia mada wanazofundishwa kwani ni za muhimu sana.

 

Baadhi ya mada zilizofundishwa kwa siku ya kwanza ni Uongozi na Utawala, Sera na Sheria zinazosimamia Tawala za Mikoa na MSM, Maadili ya Utumishi wa Umma, Majukumu ya Watendaji wa Kata na Maafisa Tarafa, Muundo, mfumo wa uwajibikaji na mawasiliano Serikalini na mafunzo ya awali ya MUKI.

NMB Mlipa Kodi Mkubwa na Bora Zaidi Tanzania 2023 🇹🇿

$
0
0

 

Jana Tarehe 24 November  2023 kwenye siku ya Mlipa Kodi 2023, Benki ya NMB iliibuka Mshindi wa Jumla Kitaifa, kama Mlipa Kodi Mkubwa Zaidi Tanzania na kama Mlipa Kodi Bora Zaidi anayelipa Kodi kwa hiari (Most Compliant Tax Payer).

Huu ni mwaka wa pili mfululizo kwa Benki ya NMB kupata tuzo hizi.

Jumla ya Tuzo ilizopata Benki ya NMB ni:

1️⃣ Mshindi wa Jumla Kitaifa: Taasisi inayolipa Kodi kubwa zaidi nchini Tanzania (Sekta zote).

2️⃣ Mshindi wa Jumla Kitaifa: Taasisi Bora inayolipa Kodi kwa hiari kwa  kuzingatia misingi na kanuni bora za ulipaji kodi (Most Compliant Tax Payer).

3️⃣ Mshindi wa Kwanza: Mlipa Kodi mkubwa zaidi katika kundi la Taasisi za Fedha nchini Tanzania (mara ya tatu mfululizo).

Akiongea mara baada ya kupokea tuzo hizo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna alisema tuzo hizo ni matokeo chanya ya misingi imara ya utawala bora na uadilifu, kuzingatia kanuni za ulipaji kodi, ufanisi katika kuendesha biashara na ubunifu wa suluhishi bora za kifedha kwa wateja.

Bi. Ruth Zaipuna alisema:  
“Nawashukuru wateja wetu na Watanzania wote kwa kuendelea  kuiamini Benki ya NMB kama mshirika wao kwenye biashara na shughuli zao, naishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya kufanya Biashara nchini na kipekee nawashukuru wafanyakazi wenzangu wote wa Benki ya NMB kwa kuendelea kufanya kazi kwa ari, bidii na kwa uzalendo mkubwa kwa maslahi mapana ya Benki na nchi yetu kwa ujumla.”

Tuzo hizo za Mamlaka ya Mapato Tanzania zimetolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Dotto Biteko katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Kama mdau wa maendeleo, Benki ya NMB tutaendelea kuendesha biashara yetu kwa kuzingatia sheria na kanuni za nchi ili kuendelea kuchangia kikamilifu ujenzi wa uchumi wa Taifa letu.

#NMBKaribuYako



NEC: MWITIKIO NI MKUBWA UBORESHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA KATA ZA NG'AMBO NA IKOMA

$
0
0

 

Mkurugenzi wa Daftari na Tehama , Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Bw. Geofrey Mpangala akishuhudia wakati msimamizi wa kituo cha Masempele katika Kata ya Ng'ambo , Bi. Mwatano  Juma Gervas, akimkabidhi kadi ya mpiga kura Wilson Shango mwananchi  wa Kata ya Ng'ambo Halmashauri ya Tabora mara baada ya kujiandikisha  katika kituo cha Masempele.
Mkurugenzi wa Daftari na Tehama , Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Bw. Geofrey Mpangala akipata maelezo kutoka kwa msimamizi wa kituo cha Masempele katika Kata ya Ng'ambo , Bi. Mwatano  Juma Gervas wakati akichukua taarifa za Wilson Shango mpiga kura wa Kata ya Ng'ambo Halmashauri ya Tabora alipokuwa akijiandikisha  katika kituo cha hicho.
Afisa Tehama Mkuu Tume ya Uchaguzi NEC Bw. Lazaro Madembwe akishuhudia wakati Mwandishi Msaidizi Tume ya Uchaguzi Bw. Mwandishi Msaidizi NEC Bw. Emmanuel Madaha alipokuwa akichukua taarifa na mmoja wa wananchi waliofika kwenye kituo cha Masempele ili kujiandikisha kwenye daftari la Kudumu la Mpiga kura katika Halmashauri ya Tabora.
Gasper Kiswaga Msimamizi wa kituo cha Kizigo akiendelea kuchukua taarifa za mpiga kura Zuhura Masoud aliyefika kujiandikisha katika kituo cha Kizigo Halmashauri ya Tabora mkoani humo.
Akimu Gervas Kinyaga Mwandishi Msaidizi Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC akimuandikisha Bw. Simon Nicholas Mlimanazi katika kituo cha kujiandikisha  cha Kizigo Halmashauri ya Tabora. 
************
Na Mwandishi Wetu, Tabora.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesema zoezi la uboreshaji wa majaribio wa daftari la kudumu la mpiga kura katika Kata za  Ikoma iliyoko wilayani Rorya mkoani Mara na Kata ya Ng'ambo iliyoko  Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Mkoa wa Tabora linaendelea vizuri, huku kukiwa na mwitikio mkubwa wa watu.

Akizungumzia zoezi la uboreshaji wa majaribio ya daftari la kudumu la wapiga kura katika kituo cha Masempele, Kata ya Ng'ambo Mkurugenzi wa Daftari na Tehama , Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Bw. Geofrey Mpangala, amesema , kuwa zoezi linaendelea vizuri na hadi kufikia Novemba 24, 2023 mwitikio wa wananchi ni mkubwa.

Amesema Kata ya Ikoma kuna vituo sita na kata ya Ng'ambo vituo kumi ambapo kwa kata ya Ikoma  jumla ya wapiga kura 310 walijiandikisha na walioboresha taarifa zao walikuwa 71. Hata hivyo hakuna aliyeondolewa kwenye daftari la mpiga kura.

Ameongeza kuwa kwa Kata ya Ng'ambo jumla ya wapiga kura wapya 484 walijiandikisha, huku walioboresha taarifa zao wakiwa 309 na aliyeondolewa kwenye daftari  la mpiga kura alikuwa mtu 1 tu.

Takwimu za Jumla mpaka jana kwa kata zote mbili wapiga kura wapya waliojiandikisha walikuwa 704 na walioboresha taarifa zao walikuwa 380 huku aliyeondolewa kwenye daftari alikuwa mmoja.

"Tunao mfumo wa kuboresha taarifa za wapiga kura kwa njia ya mtandao (OVRS ) Lakini mpaka sasa hakuna aliyeboresha taarifa hizo kwa njia ya mtandao. Hivyo, kuna kila sababu ya kuelimisha zaidi wananchi ili wauelewe zaidi mfumo huo wa kuboresha taarifa zao kwa njia ya mtandao na waweze kuutumia", Amesema Mpangala.

Naye msimamizi wa kituo cha Masempele katika Kata ya Ng'ambo , Bi. Mwatano  Juma Gervas, amesema kuwa zoezi linaendelea vizuri kwani wapiga kura wote wanaofika katika Kituo hicho wanafuata taratibu zote za uandikishaji kwa kutoa taarifa zao  muhimu kwa ajili ya kuandikishwa au kuboresha taarifa zao.

Aidha, mpiga kura aliyefika katika Kituo  cha Kizigo kwa ajili ya kujiandisha Bw. Simon Mlimanazi, amesema kuwa zoezi linaendelea vizuri kwani katika kituo hicho amepata huduma kwa wakati na amekamilisha taratibu zote hatimaye amekabidhiwa kadi yake ya mpiga kura.

Ametoa wito kwa wakazi wa eneo hilo kujitokeza  kwa wingi kujiandikisha kabla muda haujaisha na kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la mpiga kura kwakuwa  hili ni jambo muhimu kwa maendeleo ya Taifa.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) hivi karibuni ilitangaza kuanzia tarehe 24 hadi 30 Novemba, 2023 kuanza zoezi la uboreshaji wa majaribio wa daftari la kudumu la wapiga kura katika Kata ya Ng’ambo iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Mkoa wa Tabora na Kata ya Ikoma iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Mkoa wa Mara .

NEC YARIDHISHWA NA UBORESHAJI WA MAJARIBIO RORYA, 1,613 WAJITOKEZA

$
0
0

Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji wa Rufaa Mwanaisha Kwariko (wapili kushoto), akifuatiwa na Mhe. Jaji Asina Omar na Mhe. Magdalena Rwebangira wakiangalia namna Mpiga Kura anavyo boreshewa taarifa zake wakati Wajumbe hao wa Tume walipotembelea vituo vya uboreshaji katika Kata ya Ikoma iliyopo Halmashauri ya Rorya mkoani Mara leo Novemba 27,2023.
Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiwa katika kituo cha Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Ikoma, wakati walipotembelea Vituo vya uboreshaji katika Kata ya Ikoma iliyopo Halmashauri ya Rorya mkoani Mara leo Novemba 27,2023.
Mjumbe wa Tume, Mhe. Magdalena Rwebangira (kushoto) akizungumza jambo na 
Mwandishi Msaidizi katika Kituo cha Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Ikoma. 
Mjumbe wa Tume, Mhe. Jaji Asina Omar akishuhudia BVR Operator, Felician Meena akiingiza taarifa za Mpiga Kura Mariam Wankyo aliyefika katika Kituo cha Kuandikisha Wapiga Kura cha Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji Ikoma kujiandikisha kuwa Mpiga Kura. 
Mjumbe wa Tume, Mhe. Jaji Asina Omar akishuhudia BVR Operator, Felician Meena akimchukua alama za vidole Mariam Wankyo aliyefika katika Kituo cha Kuandikisha Wapiga Kura cha Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji Ikoma kujiandikisha kuwa Mpiga Kura. 
Mpiga Kura Mariam Wankyo akionesha Kadi yake ya Mpiga Kura mara baada ya kukamilisha taratibu za Uandikishwaji. 
Mpiga Kura akijaziwa taarifa zake.
Wajumbe wa Tume wakiwa katika ziara ya kutembelea vituo. 

BVR Opareta akichukua picha ya Mpiga Kura aliyefika kuandikishwa. 
Mjumbe wa Tume, Mhe. Jaji wa Rufaa Mwanaisha Kwariko akizungumza jambo na Mpiga Kura aliyefika kituoni kuboresha taarifa zake.  
Mjumbe wa Tume, Magdalena Rwebangira akiangalia Mwandishi Msaidizi akimwandikisha Mpiga Kura. 
 
 
Na Mwandishi wetu, Mara
 
 
Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wameonesha kuridhishwa na zoezi la Uboreshaji wa majaribio wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaoendelea katika Kata ya Ikoma iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rorya Mkoani Mara ambapo hadi kufikia jana Wapiga Kura 1,613 wamejitokeza.
 
Wajumbe hao wa Tume, Mhe. Jaji Asina Omar, Mhe. Jaji wa Rufaa Mwanaisha Kwariko na Mhe. Magdalena Rwebangira wametembelea vituo vya uboreshaji katika Kata ya Ikoma na kushuhudia ufanisi wa zoezi hilo.
 
Wakizungumza wakati wa ziara hiyo, Jaji Asina Omar amesema mwitikio wa wananchi kujitokeza kujiandikisha na kuboresha taarifa zao ni mkubwa na mawakala wanashiriki kikamilifu katika zoezi hilo ikiwa ni pamoja na kuwabaini wananchi wasio na sifa za kuandikishwa kuwa Wapiga Kura.
 
“Zoezi linakwenda vizuri, tumeshuhudia katika vituo tulivyotembelea hakuna changamoto na zilizopo zimetatuliwa na wataalam kwa kushirikiana na makawala wa vyama waliopo vituoni jambo ambalo linaonesha lengo la zoezi hili kutimia kama ilivyo kusudiwa,” alisema Mhe. Jaji Asina.
 
Jaji Asina amesema, muda unaotumika kuandikisha au kuboresha taarifa za Mpiga Kura unazidi kuwa mfupi na kuimarika kwa huduma vituoni hivyo kuleta ufanisi zaidi siku hadi siku na kuonesha uwezo wa vifaa vinavyotumika.
 
Kwa upande wake Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Magdalena Rwebangira amesema ameridhishwa namna zoezi linavyofanyika hivyo lengo la zoezi hilo la kufanyia majaribio vifaa vya uboreshaji pamoja na mifumo ya uboreshaji wa Daftari linatimia kwani changamoto zinabainika na kutatuliwa mapema.
 
Akitoa taarifa ya siku nne za uboreshaji huo wa majaribio katika Kata ya Ikoma, Mkurugenzi wa Idaya ya Usimamizi wa Uchaguzi, Ndg. Grayson Orcado kwa niaba ya Mkurugenzi wa Uchaguzi alisema, zoezi hilo linakwenbda vizuri na kwa ufanisi mkubwa kwani hadi sasa wananchi 1,613 wamejitokeza vituoni ambapo kati ya hao 1,356 wamejiandikisha kuwa wapiga kura na wapiga kura 257 wameboresha taarifa zao huku hakuna walioondolewa katika Daftari.
 
Orcado amesema, mawakala wa vyama wanaonesha ushirikiano wa hali ya juu hasa katika changamoto za utambuzi wa wakazi wa maeneo yao kwa kuzingatia kuwa Kata ya Ikoma inamwingiliano wa raia wanchi jirani.
 
Kwa mujibu wa mawakala wa vyama waliokuwepo katika kituo cha kujiandikisha wapiga kura cha Shule ya Msingi Nyamasanda, walieleza kuwabaini raia 8 wakigeni kutoka nchi jirani ambao walikiri kuwa si watanzania na hivyo Mwandishi Msaidizi hakuweza kuwaandikisha kuwa wapiga kura.
 
Wakala wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Silvanus Owan’ge aliyepo katika Kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata ya Ikoma amesema, wanarisdhishwa namna zoezi hilo lilivyo la uwazi na kupongeza Tume kwa namna inavyofanya kazi kwa kushirikiana nao.
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaendesha zoezi la uboreshaji wa majaribio wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Kata ya Ikoma iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Mkoa wa Mara na Kata ya Ng’ambo iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Mkoa wa Tabora kuanzia tarehe 24 hadi 30 Novemba, 2023.

NI VITA YA HISTORIA NGAO YA JAMIII WANAWAKE

$
0
0

NA JOHN MARWA


KWA mara ya kwanza historia inaenda kuandikwa katika vitabu vya kumbukumbu kushuhudiwa Ngao ya Jamii ya kwanza tangu soka la Wanawake lianze kushika kasi Tanzania.

Ni jambo lililo subiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa Soka la Wanawake nchini kuona siku moja Ligi Kuu Soka la Wanawake linakuwa na michezo ya ufunguzi wa msimu na hatimaye wakati umefika.


Timu nne za Wanawake zitashiriki michuano ya ngao ya jamii na baadhi ya wachezaji wamefunguka mikakati yao kwenye kipute hicho kinachoanza Disemba 9 hadi 12, Uwanja wa Azam Complex.  

.

Yanga wanaanza na Simba huku Fountain ikipangwa na bingwa wa Ligi Kuu, JKT Queens. 


Kiungo mshambuliaji wa Simba Queens, Vivian Corazone alisema wamefurahi kupangwa na Yanga na utakuwa mwanzo mzuri kwao kujua wanaianza vipi Ligi Kuu. 

.

“Ni mashindano tunayocheza kwa mara ya kwanza, najua kila timu imejipanga vizuri kwa mashindano na sisi tunaendelea kujifua kuweka historia nyingine,” alisema Vivian. 


Kiungo mkabaji wa JKT Queens, Donisia Minja alisema kama wachezaji wamepokea vizuri kuanza na Fountain Gate Princess lakini maandalizi yao mazuri ndio yatawavusha kwenda fainali. 


Kwa upande wa beki wa Yanga, Lucy Pajero alisema; 

“Nataka kufanya makubwa kwenye mashindano hayo na kubeba ubingwa.”

Waandishi wa habari wapigwa msasa mikataba ya kimataifa

$
0
0

 Na Selemani Msuya, Dodoma

WAANDISHI wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini wamepatiwa mafunzo kuhusu Mikataba ya Kimataifa ya Uwekezaji ambayo imekuwa ikitekelezwa kwenye sekta tofauti.

Mafunzo hayo yametolewa jijini Dodoma na Mtandao wa Muungano wa Asasi za Kiraia zinazofanya Uchambuzi wa Sera za Uwekezaji na Biashara Tanzania (TATIC).

Akizungumza na waandishi hao Mkurugenzi  Mtendaji wa TATIC, Olivia Costa Balilo wakati akifungua mafunzo hayo ya siku mbili, ambapo ameweka bayana kuwa kuna ombwe  katika uandishi wa habari za mikataba ya uwekezaji baina ya nchi na nchi, hivyo kupitia mafunzo hayo anaamini kutakuwa na mabadiliko chanya.

Alisema Tanzania ni moja ya nchi ambayo imeingia mikataba ya uwekezaji na nchi nyingine, hivyo TATIC imeamua kutoa mafunzo ili kuwezesha jamii kupata taarifa za uhakika kuhusu eneo hilo.

"Tumeamua kutoa mafunzo haya kwa waandishi wa habari tukiamini ni kundi muhimu katika kutoa taarifa za uwekezaji wa kimataifa mfano Mikataba ya uwekezaji kati ya nchi mbili MIUMBI ambayo sisi Tanzania tumeingia au tunatarajia kuingia na nchi nyingine, iwapo nyie mtakuwa na uelewa ni wazi jamii kwa ujumla itapata elimu ya kutosha,"alisema.

Balilo alisema washiriki wa mafunzo watajifunza kuhusu mikataba ya uwekezaji wa kimataifa na uchumi wa kisiasa, mikataba ya uwekezaji na makubaliano,  masuala ya sheria na uchumi na mengine.

Mkurugenzi huyo alisema pia mafunzo hayo wametoa kwa watendaji wa serikali hasa wizara zinahusiana na mikataba hiyo kama mambo ya nje, viwanda na biashara, sheria na katiba na taasisi zingine mtambuka.

Alisema iwapo wadau hao na waandishi watakuwa na taarifa kuhusu mikataba ya uwekezaji ni wazi kuwa kila pande itanufaika na kuondokana na dhana ya pande moja kunyonywa.

Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya TATIC, Wakili Steven Msechu alisema hadi sasa Tanzania imesaini mikataba 18 BITs(MIUMBI) na nchi mbalimbali ambayo inatekelezwa kwa hatua tofauti.

Wakili Msechu alisema MIUMBI kama ilivyo mikataba mingine ina faida na hasara zake, hivyo ametoa raia kwa nchi kuangalia wapi wanaweza kurekebisha ili nchi zote ziweze kunufaika.

"Sisi Tanzania tumeingia BIT na baadhi ya nchi kama Canada, Finland, Italia, Mauritius, China, Denmark, Switzerland, Uingereza, Sweeden, Ujerumani na Uturuki. Lakini pia zipo nchi kama Kuwait, Oman, Jordan, Afrika Kusaini, Zimbabwe, Korea na Misri," alisema.

Naye mtoa mada Dk Clement Mashamba alisema changamoto anayoiona katika BIT ni wahusika kushindwa kutafuta taarifa kwa kina, hali ambayo inapelekea madhara kwa nchi.

Dk Mashamba alisema iwapo kila anayepata nafasi kushiriki kwenye michakato ataweka uzalendo mbele na wazi kuwa manufaa yatapatikana.



Waziri PROF. Mkenda avitaka Vyuo Vikuu vya Afrika kushirikiana Uthibiti wa Ubora wa Elimu

$
0
0


 

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Vyuo vya Elimu ya Juu Barani Afrika ni vyema vikashirikiana katika kutoa mafunzo yenye ubora ili kuzalisha Wahitimu wenye sifa zinazokidhi viwango vya kimataifa.

Profesa Mkenda ameyasema hayo wakati akifungua kongamano la kimataifa la wadhibiti ubora ya Elimu barani Afrika lililozileata pamoja nchi zaidi ya 22 kujadili mambo muhimu kuhusu Elimu ya juu, lililofunguliwa rasmi leo Novemba 28,2023 Jijini Dar es Salaam.

Amesema idadi ya Vyuo Vikuu na wanafunzi wanaosoma Elimu ya juu inazidi kuongezeka, hivyo ni vyema suala la ubora wa Elimu likazingatiwa ili kuwa na Wahitimu wenye sifa.

""Washiriki watumie nafasi hii kujadili namna ya kuhakikisha ubora wa vyuo vikuu unakuwa vilevile. Changamoto tulizonazo ni kuongeza wanafunzi wa vyuo vikuu pamoja na ubora sababu wakiwa wengi watashindwa kufanya utafiti,"alisema Prof. Mkenda.

Amesema kuwa Ili elimu ya juu iwe bira kunatakiwa kuwa na wakufunzi wenye sifa zinwzokidhi viwango vya kimataifa na kwamba Wanafunzi wanatakiwa kupata ufaulu mzuri ili waweze kumudu ushindani katika soko la ajira.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini –TCU , Prof Charles Kihampa amesema kongamano hilo litasaidia kuweka mikakati ya pamoja ya kuendelea kutoa Elimu Bora Kwa wanafunzi wa Elimu ya juu.

"Kongamano hili lina manufaa kwa kuwa elimu ya juu sio ya nchini kwako tu, Kuna umuhimu sa kushirikiana katika ubora ili mhitimu aweze kuajirika ndani na nje ya nchi," alisema Prof. Kihampa.

MSAJILI WA HAZINA AZUNGUMZIA MABADILIKO SHERIA YA UWEKEZAJI 2023

$
0
0

Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, Akizungumza leo Novemba 28, 2023 kwenye Kikao kazi na wahariri wa vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam.

 

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile akizungumza katika kikao kazi cha Msajili wa Hazina na Wahariri wa Habari kilichofanyika leo Novemba 28,2023 Jijini Dar es Salaam.

Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu, (kulia), akiagana na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile (kushoto), mara baada ya kumalizika kwa Kikao kazi hicho Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF, Anitha Mendoza akishiriki kwenye Kikao kazi hicho.

 

 Na Mwandishi Wetu

 

Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina inatarajia kufanya maboresho ya sheria ambazo zitasaidia sekta za umma kufanya kazi kwa ufanisi na kuleta tija katika utendaji.

 

Akizungumza kwenye Kikao kazi na wahariri wa vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam, Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amesema kuwa wakati umefika kwa wakurugenzi wa mashirika ya umma kufanya kazi kwa weledi katika kuhakikisha wanapata mafanikio katika utendaji wao.

 

"Ili mashirika ya umma yapige hatua yanapaswa kutoingiliwa katika utekelezaji wa majukumu yake, kuwekeza rasilimali fedha katika kufanikisha mipango mbalimbali ya maendeleo, pamoja na kuwekeana malengo na wasimamizi katika kufikia viwango vya mafanikio ndani ya muda fulani" amesema Mchechu.

Amesema miongoni mwa sheria hizo, ni kuanzisha Mamlaka ya Uwekezaji wa Umma (PIA) kwa kubadilisha jina la ofisi ya Msajili kuwa Mamlaka ya Uwekezaji wa Umma (Public Investment Authority- PIA) ili kuakisi majukumu na mwenendo wa ukuaji wa uchumi wa Duniani.

 

Amesema kuwa kuanzishwa kwamfuko wa Serikali kwa kufanya uwekezaji wa kimkakati itasaidia kuongeza ufanisi wa uendeshaji, kuokoa mashirika ambayo bila mfuko huo yanaweza kuanguka, pamoja na kuwezesha mashirika ya umma kustahimili ushindani.

 

"Kuainisha vyanzo vya fedha za mfuko wa uwekezaji wa umma ambapo vyanzo vya fedha za mfuko vitakuwa ni pamoja na sehemu ya maduhuli yatakayokusanya na mamlaka ambayo kiwango chake kitabainishwa kwenye kanuni" amesema Mchechu.

 

"Lengo ni kuhakikisha mashirika ya umma yanafanya kazi kwa ufanisi na kuleta faida kwa serikali katika kuhakikisha yanasonga mbele" amesema Mchechu.

Amesema kuwa kwa utaratibu wa kuishirikisha Mamlaka kwenye mchakato wa kuwapata wenyeviti, wajumbe wa Bodi na watendaji wakuu wa taasisi itasaidia katika ufanisi wa kazi.

 

Mchechu ameeleza kuwa taasisi za umma zinapaswa kuwekewa mifumo rafiki ambayo itasaidia kutengeneza mapato na kuleta tija kwa Taifa.

 

Katika hatua nyengine amesema kuwa Serikali imefanya uwekezaji wa shilingi trillioni 73 katika Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala wa Serikali 298 ambazo zinafanya shughuli mbalimbali, huku asilimia 86 za taasisi hizo zikitoa huduma za kijamii.

 

Amesema kuwa kutokana na uwekezaji huo kwa mwaka wa fedha 2022/23 mashirika 108 yameweza kupata mapato ya shilingi bilioni 777.

 

Mchechu amesema kuwa kwa mwaka 2021/2022 mashirika 136 yameweza kupata mapato ya shilingi Bilioni 645 na mwaka 2020/2021 mashirika 200 yamepata Bilioni 477, huku mwaka 2019/2020 mashirika 236 yameingiza mapato ya Bilioni 696.

MAMA KOKA AMUENZI BIBI TITI KWA KUWAKOSHA KWA DOTI 80 ZA VITENGE UWT KIBAHA MJI

$
0
0

 

VICTOR MASANGU, KIBAHA 

Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Selina Koka ametoa doti za vitenge 80 kwa ajili ya  wanawake wa UWT Kibaha mji mkoani Pwani kwa lengo kushona sare kwa ajili ya kumuenzi Bibi Titi Mohamed.

Selina Koka ambaye pia mlezi wa umoja UWT Kibaha mjini amesema kwamba lengo lake kubwa ni kushitiki  kikamilifu katika killed  cha kumuenzi Bibi Titi kwa yale mambo mbali mbali  mazuri ambayo ameyafanya katika Taifa la Tanzania.

Aidha Mama Koka alisema ameamua kutoa sapoti ya vitenge  hivyo kwa wanawake wa UWT ili waweze kuungana kwa pamoja na wanawake wengine wa Mkoa wa Pwani na maeneo mengine  katika sare ya pamoja ili waweze kukutana na kukumbuka yale mazuri ambayo ameyafanya katika nyanza mbali mbali.


"Tunatambua mchango mkubwa ambao ameufanya Bibi Titi Mohamed kwani alikuwa ni mwanamke wa kwanza kujiunga na harakati mbali mbali katika suala zima la kupigania uhuru wa Tanganyika kwa hivyo na sisi ni vema na sisi kama wanawake tumuenzi,"alisema Selina.

Kadhalika Selina aliwahimiza wanawake wengine wa UWT wKibaha mji kujitokeza kwa wingi katika kushiriki kikamilifu katika sherehe za  kumuenzi Bibi Titi katika kilele ambacho kitafanyika Wilayani Rufiji mkoani Pwani.
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Kibaha mji Elina Mgonja amempongeza kwa dhati mke wa Mbunge kwa kujitoa kwake kwa hali na mali katika kuwasapoti kwa vitenge hivyo ambavyo vitawasaidia wawe katika sare ya pamoja.

Bibi Titi Mohamed ambaye alizaliwa mnamo mwaka 1926 katika jiji la Dar es Salaam na kufariki dunia novemba 5 mwaka 2000  ambapo alishawahi kushika nafasi mbali mbali za chama pamoja na masuala mbali mbali ya harakati hasa kwa upande wa wanawake.
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>