Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

ACT WAZALENDO YAJIPANGA KUITEKA DAR ES SALAAM

$
0
0

Chama cha ACT Wazalendo kimesema kimejipanga kuuteka kisiasa Mkoa wa Dar es salaam kwa kujiimarisha katika Mitaa yote 365, Kata zote 102 na Majimbo yote 10 ya Mkoa huo.


Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ndugu Ado Shaibu Ado kwenye ziara yake katika Jimbo la Segerea leo tarehe 14 Novemba 2023.


Kwenye ziara yake, Katibu Mkuu amekutana na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jimbo hilo ambao ni viongozi wa Kata zote 13 za Jimbo hilo.


Kwenye hotuba yake Ndugu Ado amesema kuwa ACT Wazalendo, kwa mwaka mzima kimejikita katika kufanya kazi za chini katika Mkoa wa Dar es salaam na mikoa mingine Nchini na kwamba mafanikio yaliyofikiwa katika Jimbo la Segerea katika uchaguzi wa ndani ni ishara za matunda ya kazi hiyo.


"Ninawapongeza sana viongozi wa Segerea kwa kukamilisha uchaguzi kwenye Kata zote 13 na Mitaa yote 62 ya Jimbo la Segerea. Nia yetu ni kuuteka kisiasa Mkoa wa Dar es salaam. Segerea mmeonesha mfano mzuri katika kufanikisha hilo" alisema Ndugu Ado.


Katika hatua nyingine, Ndugu Ado amesema kuwa viongozi wa Chama hicho kwa kushirikiana na vyama vingine vya siasa na wadau wa demokrasia kwa ujumla wake wanapambana kuhakikisha kuwa chaguzi zijazo Nchini zinakuwa za haki, huru na za kuaminika. 


ICTC kujenga vituo 8 vya Tehama nchini

$
0
0

Na Mwandishi Wetu,

Lindi


SERIKALI inakusudia kujenga vituo nane (one-stop centres) nchini vya ubunifu wa teknolojia vitakayowezesha vijana na wananchi kwa ujumla kuvitumia kuboresha kazi zao za kibunifu.


Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama (ICTC), Dkt. Nkundwe Mwasaga, ameyasema hayo Novemba 14, 2023 mjini Lindi wakati wa Mkutano wa 7 wa Jukwaa la Wahariri nchini.


Amesema vituo hivyo vinatarajiwa kujengwa katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Lindi, Tanga, Mwanza, Mbeya na Zanzibar.


“Huu ni mpango wa awali, lakini mkakati uliopo ni kujenga vituo katika mikoa yote na wilaya zote, ili wananchi waweze kuvitumia na kujifunza suala zima la teknolojia,” alisema.


Aidha, alisema, vituo hivyo vitajengwa katika maeneo karibu na vyuo na shule ambavyo vitasaidia vijana nchini kubuni na kuanzisha kampuni changa za ubunifu wa vitu mbalimbali vinavyuohusiana na teknolojia pamoja na kuendeleza, ambapo vitakuwa na uwezo wa kuingiza watu 200 kwa wakati mmoja.


Amewaomba wadau mbalimbali kushirikiana katika kuanzisha vituo hivyo, lengo likiwa ni kukuza vipaji tofauti.


Dkt. Mwasaga alisema, watu wengi wamekuwa na hofu na akili bandia au akili mnemba (Artificial Intelligence – AI) kwamba inaweza kuwakosesha kazi, jambo ambalo alisema siyo kweli, kwani AI inaleta tija na kwamba watu wakipewa ujuzi mpya kuhusu teknolojia hiyo itasaidia.


Alisema watajenga kituo cha Artificial Intelligence kwa ajili ya kuendeleza wataalam wa Tehama pamoja na kuwezesha mafunzo maalum ya wataalam wa Tehama 500 ili kukuza na kuendeleza ujuzi wa Tehama nchini.


Inaelezwa kwamba, ujenzi wa vituo hivyo ni sehemu ya vipaumbele 13 vya ICTC ambavyo vina lengo la kuleta mapinduzi ya teknolojia na ubunifu nchini.

“Tunatarajia kuanzisha kituo cha kutengeneza na kuboresha vifaa vya Tehama (ICT Refurbishment and Assembly Centre) na vituo vya majaribio vya ubunifu Tehama (District ICT Startups Innovation Hubs) katika wilaya 10,” alisema Dkt. Mwasaga.


Aidha, alisema watafanya tafiti za maendeleo ya Tehama nchini na kufanya tathmini ya kitaifa ya hatua za utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya Tehama.


Aliongeza kwamba, wataratibu na kuandaa matukio ya kuvutia uwekezaji na kutangaza masoko ya bidhaa za Tehama ndani na nje ya nchi.


“Tutashirikiana na washirika wa maendeleo na kampuni za kimataifa katika kuendeleza bunifu za Tehama ikiwemo kuwezesha utengenezaji wa bidhaa za Tehama hapa nchini,” alisema.


Alisema, majukumu mengine watakayoyafanya ni pamoja na kukuza soko la bidhaa na huduma za kampuni ndogo ndogo “startup” kwa kushiriki maonesho na makongamano yanayohusu fursa za startups duniani.


ICTC pia inakusudia kuratibu na kutengeneza mfumo wa usimamizi wa utekelezaji wa Sera ya Tehama na kufanya tafiti za kuweza kufanya maboresho ya sera kulingana na mabadiliko ya teknolojia.


Mikakati mingine ni pamoja na kujenga Metaverse Studio kwa ajili ya kutengeneza maudhui ya metaverse na pia kuboresha maudhui ya mitandao ikiwa ni pamoja na kufanya tafiti za maendeleo ya Tehama kwa kila wilaya na kuanzisha Kituo cha Resilience Academy hapa nchini.

Rais Samia awafungulia njia TIC, wawekezaji wamiminika

$
0
0

           


Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) John Mathew Mnali akizungumza kwenye Mkutano wa Waandishi wa Habari kuhusu Mafanikio ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyofanya nchini Morocco na Saudi Arabia. Mkutano huo umefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Novemba, 2023.


Na Selemani Msuya.             


KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kimesema ziara anazofanya Rais Samia Suluhu Hassan katika nchi mbalimbali duniani zimeongeza wawekezaji kwa kiwango kikubwa.  


Kauli hiyo ya neema ya ziara za Rais Samia inatolewa na TIC, huku kukiwa na baadhi ya watanzania wanalalamikia ziara hizo kwa kile wanachodai kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za umma.           


Akizungumza na waandishi wa habari leo, Ikulu jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Uhamasishaji Uwekezaji, John Mnali amesema miaka miwili ya Rais Samia madaraka imefungua sekta ya uwekezaji jambo ambalo linatoa picha nzuri kuelekea 2025 ambapo wanatarajia wawekezaji wachangie shilingi trilioni 30 kwa mwaka.  


Alisema uwekezaji katika ulimwengu wa sasa umetawaliwa na ushindani wa nchi zinazoendelea kuwekeza katika nchi zilizoendelea, hivyo ili nchi za dunia ya tatu kufanya vizuri ni lazima kujitangaza kama anavyofanya Rais Samia. 

 

"Inawezekana ikatafsirika inavyotafsirika ila ili uweze kuvutia wawekezaji ni lazima utangaze fursa ulizo nazo kwa nchi zilizoendelea, kwani tafiti zinaonesha kuwa nchi hizo zinawekeza kwa nchi zilizoendelea pia, kusema kweli Rais Samia anatupaisha na kutufungulia njia sisi TIC tukienda kuwatafuta wawekezaji kazi inakuwa rahisi," alisema.              


Mnali alisema kutokana na Rais Samia kuzunguka dunia kutangaza fursa zilizopo Tanzania katika kipindi cha Juni  hadi Septemba 2023 TIC imesajili miradi 137 mpya ambayo itawezesha kupatikana ajira 86,900.       


Mkurugenzi huyo alisema katika kipindi kama hicho mwaka 2022 walisajili miradi 86 ambayo iliwezesha kupatikana ajira 12,000, ila kwa ziara za hivi karibuni ongezeko limekuwa kubwa. Alisema uwekezaji ni sekta ambayo ina ushindani mkubwa, hivyo hakuna njia mbadala ya kufikia huko bila kuchangamana na watu, kama anavyofanya Rais Samia.                


Mkurugenzi huyo alisema pamoja na ziara za Rais Samia kutangaza fursa zilizopo nchini, pia marekebisho ya sheria ya uwekezaji yamechangia ongezeko la wawekezaji hasa wazawa. 


Alisema kwa sasa asilimia 49 ya wawekezaji nchini ni wazawa, hali ambayo imechangia na sheria nzuri iliyopo, hasa kwenye kipengele cha mtaji.            


Pia tumeweka vivutio vingi na wawekezaji wameonesha kuridhishwa na imani yetu lengo la Rais Samia kuona mchango wa sekta hiyo kwa mwaka unafikia shilingi trilioni 30, ifikapo 2025 linaenda kutimia,"alisema.

Kongamano la kutangaza fursa za Uchumi kufanyika jijini Tanga

$
0
0

 Na Mashaka Mhando, Tanga


Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa,  Alhamisi Novemba 16  anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi kwenye kongamano la uwekezaji lililolenga kutangaza fursa za uchumi .



Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba ametoa kauli hiyo wakati Akizungumza na waandishi wa habari dhidi ya mpango huo  ofisini kwake. 


Kindamba amesema kongamano Hilo ambalo litakutanisha wawekezaji mbalimbali kutakuwa ni sehemu pekee ya kutoa picha halisi ya fursa ambazo zipo mkoa wa Tanga ambazo zinahitaji watu kuwekeza na hivyo kuchangia Kasi ya uchumi wa mkoa wa Tanga na na wa mtu Moja moja. 


"Tukio hili ni kubwa na la kihistoria katika Mkoa Tanga kwasababu tukio laa aina hii liliwhi kufanyika miaka 10 iliyopita serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Haassan inaupiga mwingi kwa kumimina bilioni 429.1 na kuifanya bandari ya Tanga kuwa kati ya bandari kubwa lakini pia kuwa bandari yenye ubora, "alisisitiza Waziri Kindamba. 


Katika mkutano huo na Wanahabari Kindamba akaeleza uwekezaji wa mabilioni ya shilingi ambayo tayari yameshawekezwa na serikali katika mkoa Tanga katika sekta mbalimbali. 


Kongamano Hilo linalenga kuleta mabadiliko chanya ya kiuchumi kwenye mkoa wa Tanga yatakayosaidia kuwepo kwa ajira kwa wananchi wa Tanga na nje ya mkoa.

EDUKWANZA WANADI FURSA VYUO VIKUU VYA CANADA & USA KWA WANAFUNZI WA TANZANIA

$
0
0

Na Andrew Chale, Dar es Salaam


EDUKWANZA Consultants Limited ambao ni Mawakala wa Vyuo  vya nje ya Nchi kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya ushauri huduma za Wanafunzi ya ILLUME imeendesha zoezi kwa Wanafunzi wa Tanzania kupata fursa za masomo katika Vyuo vya nchi za Canada na Marekani (USA) tukio lililofanyika Jijini Dar es Salaam mapema leo Novemba 15,2023.



Akizungumza katika tukio hilo lililowakutanisha wanafunzi mbalimbali waliofika kupata muongozo sahihi wa Vyuo vya nje, Mkurugenzi wa Edukwanza, Bw. Sarfraz Kassam amesema taasisi yao hiyo ina ushirikiano na Vyuo zaidi ya 500 Duniani ikiwemo Vyuo hivyo vya Canada na Marekani.


"Edukwanza Consultants Limited leo Novemba 15,2023 tumefanya maonesho ya kuvinadi Vyuo vya Canada na Marekani katika mpango wa ‘Study in Canada & USA Fair 2023 ambao unasaidia kutoa fursa kwa in wanafunzi kusoma nje.


Wanafunzi mbalimbali wa Tanzania wamefika na kupata ushauri kutoka kwa Wawakilishi wa vyuo hivyo vya nje, wakipata ushauri wa kujiunga na vyuo hivyo, namna ya kupata visa za masomo, ama namna ya masomo ya kuchagua na muongozo mwingine kwa ajili ya taaluma yao." Amesema Sarfraz Kassam

 


Aidha, amesema kuwa, Vyuo hivyo vya Canada na Marekani ni miongoni mwa vyuo bora na wanafunzi wamepata namna bora ya kupata ushauri wa jinsi ya kuomba  kusoma kwenye vyuo hivyo.


Lakini pia amewataka wanafunzi hao kuweza kupitia mitandao ya kijamii ya Edukwanza kupata muongozo sahihi kwa ajili ya hatma yao ya kuchagua Vyuo bora nje ya Nchi.


Edukwanza ni miongoni mwa Mawakala wa Vyuo vya nje ya Nchi iliyosajiliwa na Tume ya vyuo vikuu nchini (TCU) imekuwa kinara katika kunadi na kuongoza kushauri wanafunzi kwenda kusoma nje.

NYOTA AZAM FC ATIMKIA MAREKANI

$
0
0

Na John Marwa


Kinda wa matajiri wa Jiji la Dar es Salaam Cyprian Kachwele amejiunga na Vancouver Whitecaps inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani  (MLS)



Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu ya Azam FC kupitia mitandao yao ya kijamii imethibitisha kuuzwa kwa kinda huyo mshambuliaji ambaye amekuwa na kiwango bora katika mashindano ya Ligi ya Vijana chini  ya miaka 20.


“Tunamtakia kila la kheri mshambuliaji wetu chipukizi, Cyprian Kachwele, aliyejiunga na timu yake mpya ya Vancouver Whitecaps inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani (MLS).


“Kachwele, amelelewa kwenye kituo chetu cha Azam FC Academy kabla ya kupandishwa timu kubwa mwishoni mwa msimu uliopita na kucheza baadhi ya mechi, akifunga mabao matatu katika mechi za mashindano. ‘All the best champion boy!’ imeeleza taarifa hiyo.


MNYAMA APANIA UBAYA KWA ASEC MIMOSAS

$
0
0

Na John Marwa

Zikiwa zimesalia siku kadhaa kuelekea michezo ya mzunguko wa kwanza hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika CAF CL Uongozi wa klabu ya Simba umeweka wazi mipango yao kuelekea mchezo huo ambao watawaalika Asec Mimosas ya Ivory Coast Novemba 25 katika Dimba la Benjamini Mkapa.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo Meneja wa Habari na Mawasiliano Ahmed Ally ameweka wazi viingilio na namna ambavyo uongozi umejipanga kuendea mchezo huo.

 

“Leo tunazungumzia maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas. Utachezwa siku ya Novemba 25, 2023 saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Mkapa. Wageni watawasili Novemba 23, 2023 wakiwa na msafara wa watu 31. Waamuzi wa mchezo watatoka nchini Misri.”


“Viingilio vya mchezo huu ni;

Mzunguko - Tsh. 5,000.

VIP C - Tsh. 10,000.

VIP B - Tsh. 20,000.

VIP A - Tsh. 30,000

Platinum - Tsh. 150,000.”


“Kikosi kipo mazoezini kuanzia siku ya Jumatatu. Mazoezi yanawahusu wachezaji wote ambao hawana majukumu ya timu za taifa. Ambao wapo kwenye timu za taifa watajiunga na wenzao wakitoka huko. Kikosi bado kipo chini ya Kocha Seleman Matola na Dani Cadena. Uongozi unaendelea na jitihada za kutafuta kocha mpya, mchakato utakamilika muda si mrefu.” Amesema na kuongeza kuwa.


“Tupo katikati ya mashindano lazima tutafute kocha ambaye yupo active, atakuwa tayari kuanza majukumu ili akifika kazi ianze.”


“Kuhusu majeruhi Kibu tayari amerudi, Kanoute anaendelea vizuri, Isra Mwenda tayari amerudi mazoezini na Kramo bado anaendelea kuuguza jeraha. Akipona atarudi kutumikia klabu.”


“Wageni rasmi wa mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas watakuwa ni mashabiki wa Simba. Kwanza wametoka kushinda tuzo ya mashabiki bora hivyo kila Mwanasimba akija siku hiyo ajue yeye ni mgeni rasmi.”

Ahmed ametaka mashabiki na wanachama kusahau yaliyopita na kuganga yajayo ili kuweza kufanya vizuri katika michezo iliyombele yao.


“Tusahau yaliyopita na tuangalie mbele. Huu ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa tukipoteza na tukiwa nyumbani hatutakuwa kwenye sehemu nzuri ya kwenda hatua ya mbele. Twendeni tukawape moyo wachezaji wetu kwamba tunaanguka pamoja na kusimama pamoja.”.


“Siku hiyo tukawaonyeshe sisi ni mashabiki bora kwa kuja wengi uwanjani. Lakini pia tuna wajibu wa kwenda kuipigani Simba yetu. Pamoja na yote uliyonayo moyoni lakini wewe ni shabiki wa Simba, ukisusa maana yake unainunia Simba yako.”


Amebainisha kuwa “Wachezaji sisi tuna imani nao, tarehe 25 wakaendeleze makubwa. Waamke sasa wakaipiganie Simba. Wanayo kazi kubwa ya kutufutia hizi kejeli kwa wao kufanya vizuri. Tukipata matokeo mazuri watapunguza machungu makubwa tunayopita hivi sasa.”


“Ni muhimu wajue pale hawachezi tu kwa ajili yao bali kwa ajili ya Simba. Sisi tutaenda kutimiza wajibu wa kushangilia, na wao watupe furaha ili turejeshe hali yetu ya kutamba. Tunawambia hivyo kwa niaba ya mgeni rasmi, mashabiki wa Simba.”


“Tutakuwa na hamasa kama kawaida, na tutaanza mapema kuanzia Jumatatu tukiwa na matukio mbalimbali ya kuwahamasisha mashabiki kuja uwanjani. Ratiba tutatoa Jumapili ya mtaa kwa mtaa. Tunataka kuujaza Uwanja wa Mkapa, tuwaonyeshe kwamba hii ni Simba.”


Kuhusu jezi za Ligi ya Mabingwa amesema “Tutakuwa na jezi maalumu ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kama mnavyojua mdhamini rasmi huwa hatumiki kwenye jezi ya mashindano hayo na kwa miaka ya nyuma tulikuwa tunatumia Visit Tanzania. Kuanzia Jumatatu tutatoa taarifa itakavyokuwa msimu huu.”



“Nimepewa baraka na viongozi wa klabu kutembelea matawi ya Simba nikianza na jana katika Tawi la Simba Soko la Samaki Msasani. Tunafanya hivi kwa ajili ya kukutana na kuzungumza na Wanasimba. Kupokea maoni yao na kuwaalika kuja uwanjani.” Amesema, Ahmed Ally. 

DC KIBAHA AAHIDI NEEMA KWA WAFANYABIASHA WADOGO PWANI

$
0
0

  NA VICTOR MASANGU,KIBAHA



Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Saimon amezindua rasmi mfumo kwa wafanyabiashara ndogo ndogo(Wamachinga) ambao uwapa fursa ya kuweza kujisajili kwa njia ya simu zao lengo ikiwa ni kutambulika kwa urahisi pamoja na kufahamu aina ya bidhaa wanazoziuza.

Mkuu huyo amezindua mfumo huo wakati wa mkutano maalumu ambao uliandaliwa kwa lengo la kuweza kujadili mambo mbali mbali ikiwemo suala muhimu la wafanyabiashara hao wahame kutoka mfumo wa zamani na kujisajili kwa njia ya kisasa zaidi ili watambulike.


"Kitu kikubwa wafanyabiashara ndogo ndogo natambua mpo wengi lakini suala la kuhakikisha sisi kama serikali tunawatambua ni vema mkajisajili kwa kutumia simu zenu na lengo lake kubwa ni kutambulika mnafanya nini katika shughuli zenu hii itatusaidia kupata na takwimu halisi,"alisema Saimon.


Kadhalika Mkuu huyo aliongeza kwamba ni lazima kujiwekea mipango madhubuti ambayo itaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa wafanyabiashara kuendesha shughuli zao katika mazingira mazuri na  ambayo yametengwa rasmi kwa shughuli zao.


Pia aliongeza serikali ya Wilaya itaendelea kushirikiana bega kwa bega na wafanyabiashara wote wadogo wadogo na kuwawezesha kiuchumi ili wawze kufikia malengo ambayo yamejiwekea ikiwemo kuweza kutambulika na serikali kupata takwimu za idadi yao.



Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho la umoja wa machinga Mkoa wa Pwani (SHIUMA) Filemon Malinga alibainisha kwamba lengo lao ni kuwahimiza wafanyabiashara wote kujisajili kwa njia ya kisasa zaidi.


Mwenyekiti huyo alisema kuwa endapo wafanyabiashara hao wakiingizwa katika mfumo mpya na kusajiliwa kwa njia ya simu zao itasaidia kupata idadi ya takwimu halisi ikiwemo na aina ya biashara ambazo wanazifanya katika maeneo yao mbali mbali.


"Tumejitahidi kupata wataalamu wa Tehama kutoka taasisi ya TIVA ambapo imeweza kupata fursa ya kuelimisha jinsi ya umuhimu wa wafanyabiashara hao kujisajili kwa mfumo wa kanzi data ambayo hii tutaondoka na ile hali ya kujisajili katika makaratasi,"aliongeza Mwenyekiyi.


Aidha Mwinyekiti huyo hapo awali waliwasajili wanachama wao kwa kutumia makaratasi lakini kutokana na teknolojia ilivyokuwa watajisajili kwa kutumia simu zao za kiganjani ili kuondokana na usumbufu wa hapo awali katika suala zima la ukusanyaji wa taarifa.



Kwa upende wake Mwenyekiti wa soko la Mnalani(Loliondo) Mohamed  Mnembwe amesema kwamba utaratibu huo wa wafanyabiashara kuweza kuingia katika mfumo wa kujisajili utasasaidia kujua idadi halisi pamoja na bidhaa wanazouza.


"Leo tumekutana katika huu mkutano ambao umewajumuisha wafanyabiashara ndogo ndogo wa Mkoa wa Pwani na haya maelekezo tuliyopewa na mtaakanu wa Tehama yataweza kutusaidia sisi kama wafanyabiashara "alisema Mnembwe.


Mnembwe alisema kwamba ana imani endapo wafanyabiashara wote wakielimishwa umuhimu wa kujisajili kwq simu kutaweza kuleta mabadiliko ya kimaendeleo kutoka na kufanya kazi kwa mfumo wa kidigitali na itasaidia kutambulika.
      

Tozo kero 231 kati 380 zafutwa

$
0
0

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


SERIKALI kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara (MKUMBI) imefuta na kupunguza jumla ya tozo, ada na faini zisizopungua 232 kati ya 380 zilizobainishwa katika utekelezaji wake sawa na asilimia 61.


Akizungumza Kikao Maalum cha Kikundi Kazi cha Mazingira ya Biashara jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu wa Bunge, Dkt Jim James Yonazi alisema ufutwaji wa tozo, ada na faini hizo ambazo zilikuwa kero kubwa kwa ustawi, ukuaji na maendeleo ya biashara na uwekezaji hapa nchini.


“Maamuzi haya yanaonyesha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuifungua Tanzania na kuwa kivutio cha kufanya biashara na uwekezaji,” alisema Dkt. Yonazi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kikundi kazi hicho cha Baraza la Taifa la Biashara(TNBC).


Akielezea zaidi mafanikio yaliyopatikana tangu MKUMBI uanze kutekelezwa, Dkt. Yonazi alisema jumla ya Sheria, Kanuni na Taratibu zipatazo 40 kati ya 88 sawa na asilimia 45.5 zimeshapitiwa na kufanyiwa marekebisho.


“Maboresho haya yote ya Sheria,Kanuni na Taratibu yamesaidia kuchochea ukuaji wa sekta za uchumi hapa nchini zikiwemo sekta za uwekezaji, viwanda na biashara, kilimo, mifugo, afya, maliasili na utalii,” alisema.


Dkt. Yonazi alisema Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa TNBC ameelekeza kuendelea kusimamia utekelezaji stahiki wa MKUMBI sambamba na uhamasishaji wa matumizi ya mifumo yaTeknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa lengo la kuongeza ufanisi kwa wafanyabiashara na wawekezaji hapa nchini.


“Nina agiza Wakurugenzi na Idara za Uratibu, Ufuatiliaji na Tathmini pamoja na Maendeleo ya Sekta Binafsi katika Ofisi ya Waziri Mkuu,wafuatilie utekelezaji wa Maazimio ya TNBC na kuwaandikia barua Makatibu Wakuu wote ambao bado hawajawakilisha taarifa za utekelezaji wa maazimio hayo,” alisisitiza Dkt. Yonazi.


Dkt. Yonazi alimpokeza Katibu Mtendaji wa TNBC Dkt. Godwill Wanga na watendaji  pamoja na wafanyakazi wote wa baraza  kwa kazi nzuri na kuwakumbusha wajumbe wote kwenye Kikundi Kazi cha Mazingira ya Biashara kuendelea kufanyia kazi maono na matarajio ya Rais Hassan.


Kwa upande wake, Dkt. Wanga alisema Kikosi Kazi cha Mazingira ya Biashara kina jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa mazingira ya kufanya biashara yanaendelea kuwa rafiki kwa biashara, uwekezaji na uchumi kwa ujumla na kuvutia uwekezaji kujenga uchumi wan chi.


“Kikundi kazi hiki kina jukumu kubwa la kuondoa na kupunguza  gharama za kufanya biashara na uwekezaji. Hivi hatuna budi kufanya kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha tunaandaa na kuwakilisha mapendcekezo yenye tija kwa Baraza,” alisema Dkt. Wanga.


Alisema TNBC hufanya kazi kupitia mikutano na vikao katika ngazi mbalimbali kama vile ya Baraza,Kamati Tendaji za Baraza, Mashauriano ya Kiwizara kati ya Sekta Binafsi na Umma(MPPD), Kikosi Kazi cha Kiufundi cha Kiwizara(MTWG), Mikutano ya Baraza la Biashara ngazi ya Mkoa (RBC) na Wilaya (DBC).

SANGU AIPA KONGELE SUMAJKT KWA MIRADI

$
0
0

Na Mwandishi Wetu 


MWENYEKITI wa Kamati ya  Kudumu ya Bunge na Uwekezaji wa Mitaji ya Umma na Mbunge wa Kwela, Deus Sangu  amepongeza kamati hiyo kwa kufanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali inayoendeshwa na Kampuni ya SUMAJKT ya uzalishaji mali.

Amesema kipekee wamepata fursa ya kutembelea sehemu kuu mbili kwanza wametembelea Kampuni tanzu ya uzalishaji jwa maana ya uzalishaji nguo pia kampuni tanzu nyingine ya uzalishaji maji na kikubwa nikuendelea kuipongeza Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwanamna ambavyo ameiwezesha SUMAJKT katika uwekezaji .


Sangu ameyasema hayo Novemba 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam,  ambapo ambapo kamati hiyo  imejionea kiwanda cha nguo ambacho kimewekeza fedha takribani  milioni 361...


Mbunge huyo amesema kampuni hizo zimefanya  kazi kubwa na Serikali inastahili pongezi, huku akizitaka kuendelea na uzalishaji kwa kasi.


"Uwekezaji huu umeweza kuongeza uzalishaji, mwanzo kiwanda kilikuwa na uwezo wa kuzalisha nguo 350 lakini  umeongezeka na sasa wanazalisha pisi 500 na bado wanahitaji kupewa nguvu zaidi na sapoti ili waweze kuzalisha pisi 1,000 kwa siku na kwakweli tunaona namna walivyojipanga na idadi ya wateja imeongezeka hadi nje ya nchi," amesema Mbunge Sangu 


Amesema SUMAJKT wametoa fursa ya ajira kwa vijana wakitanzania takribani 350 wakiwa ni askari na raia wa kawaida ambao ni asilimia 70.


Kwa upande mwingine amepongeza uamuzi wa SUMAJKT kuwekeza takribani Shilingi bilioni 1 832 kwenye uzalishaji wa chapa za maji kutoka chupa 3,200 hadi 10,000 na kwamba wataendelea kushauri serikali iongeze mtaji zaidi.


Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali, Rajabu Mabele amesema wanampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanya mahusiano ya kidiplomasia ambayo yameweza kuwasadia kupata soko la bidhaa zao hadi nje ya nchi.


Alisema mikakati yao ni kuhakikisha miradi wanayosimamia inachangia ukuaji wa uchumi wa nchi


"Kulikuwa na laini mbili za uzalishaji lakini sasa hivi tunalaini sita na uzalishaji wa kuzalisha nguo 300 kwa siku, hivi sasa tunazalisha nguo 700 na lengo letu nikuelekea katika kuzalisha nguo 1,000 kwa siku kwa hiyo bado tunaendelea kuzalisha na masoko kiukweli tunamshukuru sana Rais Samia kwa kuendelea kutanua wigo katika diplomasia ya uchumi kwani mahusiano na nchi nyingi ni mazuri," alisema.

SERIKALI YARIDHISHWA NA UWEKEZAJI WAKE KATIKA KIWANDA CHA SUKARI CHA TPC

$
0
0

“Sisi wawekezaji tumefurahi na kuridhishwa na ufanisi katika uendeshaji wa kiwanda hiki cha sukari cha TPC Limited, ufanisi huu unatoka na faida iliyopatikana katika kipindi cha mwaka 2022/23 ambapo kiwanda kimeweza kuzalisha faida baada ya kodi ya shilingi 72.7. bilioni kutoka katika mauzo ya shilingi bilion 235 huku gawio kwa wanahisa ikiwa ni shilingi bilioni 69.9” hayo yamesemwa na Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu baada ya kikao cha wanahisa kilichofanyika jana mkoani Kilimanjaro.

Mchechu anasema tangu mwaka 2000 kiwanda hiki kimekuwa kikiongeza uzalishaji mwaka hadi mwaka ambapo kwa sasa uzalishaji wa sukari umeongezeka kutoka Tani 36,000 za mwaka 2000 hadi kufikia Tani 116,700 kwa mwaka huu.

Mchechu anaeleza ongezeko hilo la uzalishaji wa sukari limetokana na ongezeko la mavuno ya miwa ambapo kwa mwaka huu kiwanda kimevuna miwa zaidi ya Tani 1,150,000.

“Katika uzalishaji wa sukari kwa mwaka huu, TPC Limited imezalisha zaidi ya tani 116,700 katika kipindi cha juni 2022 hadi machi 2023, hiki ni kiwango kikubwa sana cha sukari  ambacho hakijawahi kuzalishwa katika miaka yote tangu TPC Limited kuanza uzalishaji wake mwaka 1936”.
Anasema wakati wanafanya ubinafsishaji wa kiwanda hicho, serikali ilikuwa imeweka malengo shamba la TPC baada ya kuwa imeongezewa  eneo la shamba la Kahe, itaweza kuzalisha tani 750,000 kwa mwaka, lakini kwa sasa wanazalisha Tani 1,150,000 ambayo ni juu ya malengo waliyokuwa wamewekwa na serikali wakati wa ubinafsishaji.

“Eneo lile lile lakini uzalishaji unazidi kuwa mkubwa kutokana na tija katika uzalishaji kwani kwa mwaka huu  TPC tumeweza kutoa tija ya wastani wa tani 148 (tani mia moja na arobaini na nane)  kwa hekta kiwango ambacho ni cha juu barani Afrika, na ni moja kati ya viwango bora vitatu duniani” anasisitiza Mchechu.


Akizungumzia sababu ya ufanisi na mafanikio hayo, Mchechu anasema Serikali ya awamu ya sita imeweka nguvu na jitihada kubwa za kuhamasisha kilimo na kuvutia uwekezaji katika kilimo hususani katika sekta ya sukari na hilo limeweza kufungua fursa nyingi kwenye sekta ya sukari nchini.

Anasema mambo ambayo yamefanyika katika kipindi cha serikali ya awamu ya sita ni pamoja na kuendelea kulinda soko la ndani dhidi ya sukari zinazoingizwa zenye kiwango cha chini na kuja kushindana na sukari inayozalishwa nchini yenye kiwango bora.

Anaeleza kuwa kitendo hicho kimefanya sukari kuendelea kuuzwa katika bei nzuri na hivyo kuhamasisha wazalishaji wa sukari kuendelea kuwekeza zaidi katika soko la sukari.
“Tumeshuhudia serikali imekuwa na mfumo unaoeleweka na endelevu wa uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi na hii ni kutokana na maboresho yaliyofanyika katika sheria ya sukari pamoja na kanuni zake ambapo uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi, umewekewa utaratibu mzuri zaidi”.

Anasema eneo lingine ambalo serikali imefanya ni kuhamasisha na kuhakikishia wawekezaji mazingira mazuri ya uwekezaji hali ambayo imechangia kupanda kwa idadi ya wekezaji kutoka ndani na nje ya nchi wanaowekeza katika sekta ya sukari.

“Vipo viwanda mbavyo vimeanza kufanya kazi lakini pia kuna viwanda vingine vinakuja kuweza kuongeza uzalishaji wa sukari nchini, hivyo katika mazingira haya tumeona serikali ya awamu ya sita, imesukuma mbele jitihada za kukuza kilimo hususani cha miwa, ili kuongeza uzalishaji wa sukari hapa nchini”.

Anasema katika kuunga mkono jitihada hizo za serikali, TPC kwa mwaka huu wanatazamia kuwekeza fedha Dola 45 milioni hadi 50 milioni kwa kujenga kiwanda kipya cha kuchakata Molasses ambayo imekuwa ikibaki baada ya uzalishaji wa sukari.
 
“Bodi yetu leo itaidhinisha matumizi ya fedha zaidi ya Dola 45 milioni ama Dola 50 milioni kwa ajili kuweka kiwanda kingine cha uchakataji Molasses na kuweza kuzalisha bidhaa nyingine ambayo itakuwa ni spirit kwa ajili ya matumizi ya viwanda na watumiaji wengine".
Anasema kiwanda hicho kitajengwa TPC na ujenzi wake unatarajiwa kuanza mapema 2024, na kwamba hicho ni kiwango kikubwa cha fedha kitakachowekezwa ambapo ni pamoja na kukuza zao la miwa na bidhaa zinazotokana na zao la miwa.

Anaeleza kuwa uwekezaji huo kwa TPC utakuza ajira pamoja na kuongeza mapato ya ndani ya kiwanda na kuwezesha kulipa kodi nyingi zaidi na manufaa mengine yatakayopatikana kutokana na uwekezaji huo.

Anasema kubwa zaidi kutakuwa na ongezeko la uzalishaji wa nishati ya umeme ambapo katika kiwanda hicho wanatarajia kufunga mashine nyingine ya kuzalisha umeme na hivyo kutakuwa na ziada ya megawati Nne hadi saba ambazo zitaingizwa katika gridi ya Taifa.
Akizungumzia mchango wa Kiwanda cha Sukari cha TPC kwa jamii, Jafarry Ally ambae ni Mkuu wa Utawala katika kiwanda hicho anasema TPC imeweza kulipa kodi, ushuru pamoja na gawio kwa serikali zaidi ya Sh. 99 bilioni, kiwango ambacho ni kikubwa ukilinganisha na kiwango cha Sh. 2 bilioni kilichokuwa kikitolewa wakati kampuni hiyo imebinafsishwa mwaka 2000 na sababu kubwa ya kuongezeka kwa kiwango hicho ni uzalishaji,mauzo mazuri na ulipaji sahihi wa kodi kwa mujibu wa sheria na miongozo ya ulipaji kodi.

“Mwaka 2010 ndipo kiwanda kilianza kulipa gawio serikali na hadi mwaka 2022/2023 tumekuwa tukilipa gawio na kiwango kimekuwa kikiongezeka mwaka hadi mwaka na kuifanya TPC kuongoza kwa miaka mitatu mfululizo kwa kutoa gawio zuri na kubwa serikalini kuliko mashirika mengine yote ambayo serikali ina hisa kidogo”.

Akizungumzia mchango wa kiwanda hicho kwa jamii  Ally anasema kwa kupitia shirika lao lisilo la kiserikali la FTK, wamekuwa wakitumia  Sh1.2bilioni kwa mwaka kwa ajili ya kuhudumia jamii ya vijiji vinavyowazunguka ambapo fedha hiyo inaelekezwa kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za elimu, afya, miundombinu na miradi endelevu ya vijiji kama miradi ya umwagiliaji.

“Kwa upande wa utoaji wa huduma katika vijiji vinavyotuzunguka tumeendelea kuboresha huduma na kwa upande wa elimu, hivi karibuni tumejenga shule ya sekondari ya Chekereni/Weruweru(CHEWE) ambayo ni ya serikali, na serikali ilituletea fedha za uviko ikaja kuongezea majengo ambayo imefanya shule hiyo kuwa na vitu vingi vilivyokamilika.”

“Ni shule inayoanza lakini ina vitu vyote muhimu ikiwemo madarasa, vyoo, jiko, madawati, maabara zote pamoja na jengo la utawala na shule hii itazinduliwa hivi karibuni baada ya serikali kukamilisha uwekaji wa samani”

“Lakini pia tumeweza kutoa huduma za afya na kujenga mundombinu ya barabara kutokana na uwezo tunaokuwa nao ikiwa ni pamojana kuchimba visima na kujenga mabwawa ya kuoshea mifugo katika vijiji vinavyotuzunguka”.

DICOCO yatoa elimu kuhusu ugonjwa wa kisukari

$
0
0

 Na Mwandishi Wetu

TASISI  inayojihusisha na utoaji elimu ya ugonjwa wa kisukari kwa jamii (DICOCO) imetoa elimu kwa wananchi wa Wilaya za Bagamoyo na Kisarawe mkoani Pwani kuhusu ugonjwa wa kisukari sambamba na kujiepusha na dalili za ugonjwa huo.

Mbali ya kutoa elimu kuhusu ugonjwa wa kisukari, taasisi hiyo imetoa huduma ya kupima kisukari, shinikizo la damu,  urefu na uzito kwa wananchi hao pamoja na kuwakumbusha umuhimu wa kupima afya zao mara kwa mara.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwanzilishi wa Taasisi ya DICOCO ambaye pia anaishi na ugonjwa wa kisukari Lucy Johnbosco akieleza sababu za kutoa elimu ya ugonjwa huo na kutoa huduma ya kupima magonjwa bure amesema mwezi wa 11 kila mwaka ni mwezi wa kutoa elimu.

Pia ni mwezi wa kusambaza uelewa , kueneza na kutoa hamasa kwa jamii ili waweze kujua ugonjwa wa kisukari lakini maadhimisho ya ugonjwa huo hufanyika kila Novemba 14, hivyo kama taasisi ya kutoa elimu ya ugonjwa wa kisukari kwa jamii  wametumia nafasi hiyo kutoa elimu hiyo ya ugonjwa wa kisukari.

Pia wametoa huduma kupima kisukari na maradhi yote yanayoambatana na ugonjwa huo huku akieleza kuwa walianzia katika Hospitali ya Wilaya Bagamoyo lengo likiwa kuwafikia wananchi wengi wanaotoka katika hospitali mbalimbali.

"Tumewaelimisha na kuwahudumia  mama wajawazito,  wenye watoto, watu wenye shida ya akili,  Waraibu wa Dawa za kulevya pamoja na makundi mengine ya rika mbalimbali.Tukawaelimisha tukawapima sukari, uzito , urefu, tukaangalia  uwiano na uzito na urefu wao...

" Tukawaelimisha  namna gani ya kuepuka ugonjwa wa kisukari,  tukawaelimisha namna gani wanaweza wakala chakula killichokuwa bora na chakula ambacho kinaafya zaidi pamoja na umuhimu wa makundi yote ya vyakula, "amesema.

Ameongeza kuwa baada ya kutoka Hospitali ya Wilaya Bagamoyo, walienda Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe ambako nako walitoa huduma mbalimbali kwa wananchi wa makundi yote.

"Novemba 14 tulienda Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe  ambako tulikusanya kliniki zote tukawaweka pamoja  lakini hata watu wa nje walikuja  na wanajamii, wamehamasika.Watu Kisarawe na Bagamoyo wanaomba  twende tena, " amesema.

Aidha amesema pamoja na kuendelea kuihudumia jamii ya Watanzania, taasisi ya DICOCO ingependa kupata ufadhili zaidi na  watu kuamini kuwa taasisi hiyo  inaweza kuleta matokeo chanya."Kwahiyo wasiogope kutupa msaada na kutuwezesha ili tuendelee kufanya hii kazi ya kijamii.

"Lakini kauli mbiu ya mwaka huu ya mwezi huu wa kisukari inasema Jua hatari za ugonjwa wa kisukari ili uweze kujua namna gani ya kuziepuka.Wakati tunatoa elimu kwa wananchi tulikuwa tunakazia katika dalili za ugonjwa wa kisukari pamoja na madhara yanayotokana na ugonjwa wa kisukari  ili watu wajue namna gani wanaweza kuziepuka, " amesema.


NEC YAKUTANA NA VYAMA VYA SIASA KUHUSU UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele akizungumza na wawakilishi kutoka Vyama vya Siasa kuhusu majaribio ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yanayotarajiwa kufanyika katika Kata za Ng’ambo iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Mkoa wa Tabora na Ikoma iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Mkoa wa Mara kuanzia tarehe 24 hadi 30 Novemba, 2023.
Vyama vya siasa vimehimizwa kushiriki kwenye majaribio ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yanayotarajiwa kufanyika katika Kata za Ng’ambo iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Mkoa wa Tabora na Ikoma iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Mkoa wa Mara kuanzia tarehe 24 hadi 30 Novemba, 2023.
 
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele ametoa wito huo leo tarehe 16 Novemba, 2023 wakati akifungua mkutano wa Tume na vyama vya siasa jijini Dar es Salaam.
 
“Vyama vya siasa kwenye zoezi hili vitashiriki kwa kuweka wakala mmoja katika kila kituo cha kuandikisha wapiga kura, lengo ni kushuhudia na kujiridhisha juu ya taratibu zitakazotumika wakati wa majaribio ya uboreshaji wa Daftari,” amesema Jaji Mwambegele.
 
Amenongeza kuwa majaribio ya uboreshaji yanafanyika kwa lengo la kupima uwezo wa vifaa na mifumo itakayotumika wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaotarajiwa kufanyika nchi nzima kwa tarehe zitakazopangwa na kutangazwa na Tume.
 
Majaribio ya uboreshaji yatahusisha kuandikisha raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 au zaidi na atakayetimiza umri wa miaka 18 kabla au ifikapo tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
 
Kundi lingine litakalohusika kwenye zoezi hili ni; wapiga kura wanaoboresha taarifa zao ambao wamehama kutoka eneo moja la uchaguzi kwenda eneo lingine, waliopoteza au kadi zilizoharibika, wanaorekebisha taarifa zao na kuondoa wapiga kura waliopoteza sifa za kuwemo katika Daftari.
 
Majaribio ya uboreshaji yatafanyika katika vituo 16 vya kuandikisha wapiga kura. Kati ya hivyo, vituo 10 ni vya Kata ya Ng’ambo na vituo sita (6) ni kutoka Kata ya Ikoma. Vituo vya uandikishaji vitafunguliwa saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
 
“Tume inatoa wito kwa wakazi wa Kata ya Ng’ambo iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora na Kata ya Ikoma iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, kujitokeza kwa wingi kushiriki katika majaribio ya uboreshaji wa Daftari na kutoa ushirikiano kwa Tume wakati wote wa utekelezaji wa jukumu hili muhimu kwa mustakabali wa Taifa,” amesema Jaji Mwambegele.
Sehemu ya viongozi wa vyama vya siasa vikishiriki katika mkutano huo wa Tume na Vyama vya siasa.

Sehemu ya viongozi wa vyama vya siasa vikishiriki katika mkutano huo wa Tume na Vyama vya siasa.
Viongozi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) nao wakiwa katika mkutano hao.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Ramadhani Kailima akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uboreshaji wa majaribio wa Daftari La Kudumu la Wapiga Kura. 
BVR Kits zenye vifaa mbalimbali vinavyowasiliana ili kuchukua na kutunza taarifa za wapiga kura BVR Kits za sasa ambazo zinatumia programu ya android tofauti na BVR Kits za awali ambazo zilikuwa zinatumia programu ya Microsoft Windows.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele akifafanua jambo wakati wa majadiliano. 
Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa wakichangia mada wakati wqa mkutano huo wa Tume na Vyama vya siasa katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo Novemba 16,2023. 
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Ramadhani Kailima akifafanua jambo wakati wa mjadala na wawakilishi wa vyama vya siasa. 

RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE AKUTANA NA BALOZI WA CANADA NCHINI MHE KYLE NUNAS JIJIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0

Na Issa Michuzi


Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  akisalimiana na baadaye kuongea na Balozi wa Canada nchini Mhe. Kyle Nunas pembezoni mwa  Mkutano wa Pili wa Kisayanzi ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto katika Ukumbi wa Kimataifa  wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.

Mkutano huo wa siku tatu umeandaliwa na Wizara ya Afy na Ofisi ya Rais TAMISEMI  kwa kushirikiana na washirika kadhaa ikiwa ni pamoja na taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF), kwa lengo la kuleta wadau muhimu pamoja ili kusambaza, kuthibitisha, na kujifunza mafundisho yanayopatikana kwa vitendo bora na hatua za msingi zinazotokana na ushahidi wa kisayansi ili kuhakikisha utekelezaji bora.

 

Mkutano huo hutumika kama jukwaa kubwa kwa wataalamu wa afya, watunga sera na wadau kukutana ili  kushirikiana maarifa, kutathmini athari za mikakati iliyopo, kushughulikia masuala magumu, kufikiria suluhisho za ubunifu, na hatimaye kuleta mabadiliko chanya.

 

Moja ya mada kuu ya mkutano huu ilikuwa ni mikakati ya Tanzania kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030 (SDG) na malengo ya Mwaka 2025 yanayohusiana na ubora wa huduma za RMNCAH+N.

 

Tayari Tanzania imeandaa mfululizo wa mipango ya kitaifa muhimu kuboresha ubora wa huduma, ikiwa ni pamoja na Mpango wa Miaka Mitano wa Maendeleo (2021-2025), Mpango wa Sekta ya Afya wa Mkakati (HSSP V, 2021), na Mpango Mmoja wa III (2021-2026).

 

Mipango hii inalenga kuboresha mfumo wa afya, kuongeza upatikanaji wa huduma za RMNCAH, na kupunguza viwango vya vifo vya  mama wajawazito na watoto wachanga. Kufikia malengo haya  kunahitaji kuweka kipaumbele katika mikakati ya kuongeza athari na kuanzisha mifumo bora ya kuhakikisha ubora.

 

Huduma za RMNCAH+N  zinaunganishwa katika ngazi mbalimbali za utunzaji, kutoka kwa wafanyakazi wa afya wa jamii hadi watoa huduma za afya katika hospitali za rufaa za kitaifa na hospitali maalum. Ushirikiano wa ufanisi kati ya ngazi hizi, sasisho la miongozo kwa kawaida, na motisha na fidia za kutosha kwa wafanyakazi husababisha kuongezeka

 

Ushirikiano wa ufanisi kati ya ngazi hizi, sahisisho la miongozo, motisha na fidia za kutosha kwa wafanyakazi husababisha kuongezeka kwa utoaji wa huduma na matokeo bora kwa ujumla. Hata hivyo, kuna masuala kadhaa na uchunguzi unaokwamisha ushirikiano huu.

 

Ubora wa huduma za RMNCAH+N unatumika kama kipimo cha mfumo wa afya wa Kitaifa. Ushirikiano kati ya wadau mbalimbali, kutoka kwa watoa huduma za afya hadi taasisi za serikali na wafadhili, ni muhimu kuhakikisha ustawi wa akina mama na mtoto. Kutekeleza changamoto na mapendekezo yaliyoainishwa ni muhimu kwa mustakabali bora kwa akina mama na watoto ulimwenguni.

 

Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF) inalenga kubadilisha maisha ya jamii kupitia masuluhisho ya kibunifu na endelevu, wakati leongo lake katika RMNCAH+N  ni kufanya kazi kama mwendeshaji  ili kuhakikisha hakuna vifo visivyo vya lazima vya akina mama. Misingi yake mikuu ni kubadilisha Maisha watu, kukuza ushirikiano, na kuweka kipaumbele katika matokeo ya pamoja kupitia ushirikiano.

 

 

 

Marekani na Taasisi ya Jane Goodall Tanzania Yazindua Mradi mpya wa Maendeleo Endelevu wenye thamani ya dola milioni 30 unaofadhiliwa na USAID

$
0
0

Leo, Marekani na Taasisi ya Jane Goodall (JGI) Tanzania wamezindua rasmi mradi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) Tumaini Kupitia Vitendo (Hope through Action).

 

Ukifadhiliwa na watu wa Marekani kupita USAID, mradi huo utasimamiwa na kuongozwa na wazawa kupitia shirika la Jane Goodall tawi la Tanzania. Mradi huo ni matokeo ya uhusiano wa miaka 20 kati ya USAID na Taasisi ya Jane Goodall nchini Tanzania. Katika kipindi cha miaka mitano, mradi wa USAID Tumiani Kupitia Vitendo utapanua kazi ya maendeleo endelevu ya JGI-Tanzania na kurejesha makazi na ulinzi wa hifadhi zilizopo Magharibi mwa Tanzania.

 

“Ushirikiano huu na Taasisi ya Jane Goodall - Tanzania ni kielelezo kikuu cha dhamira ya USAID ya kuwaweka watandaji wazawa mbele na kukuza maendeleo yanayoongozwa na wazawa,” alisema Mkurugenzi wa USAID wa Ofisi ya Manunuzi Bi. Leslie-Ann Nwokora. “Hongera JGI -Tanzania; hii ni hatua muhimu na USAID inawaunga mkono.”

 

Mradi wa USAID Tumaini Kupitia Vitendo unaangazia maendeleo ya muda mrefu ili kuboresha maisha ya watu, uzalishaji wa kilimo chenye tija, na usimamizi wa misitu. Unasaidia uwekezaji kwa ajili ya uhifadhi wa kudumu wa misitu, manufaa kwa jamii na mapato dhabiti kwa kuimarisha haki za ardhi., kuboresha usimamizi wa misitu, kukuza kilimo endelevu, kuanzisha malipo ya huduma za mfumo ikolojia, kushughulikia ukatili wa kijinsia, na kusaidia uongozi wa vijana nchi nzima.

 

Kwa kuzingatia kukabiliana na ustahimilivu wa jamii kwa mabadiliko ya tabia nchi na ulinzi wa viumbe hai, athari za mradi zitawasilishwa kwa takwimu za sasa. teknolojia bunifu ya kijiografia na sayansi, mbinu bora za usimamizi wa maarifa, mawasiliano, na usimulizi za hadithi. Msisitizo zaidi utawekwa kwenye usawa wa kijinsia na ushirikishwaji wa kijamii kupitia ufadhili wa mfuko wa USAID wa Usawa wa Kijinsia na Vitendo vya Usawa.

 

Magharibi mwa Tanzania ni nyumbani mwa sokwe wengi takribani 2,200 nchini na ni sehemu kubwa ya urithi wa asili wa Tanzania. Changamoto za kiuchumi, kiafya na kielimu zinazowakabili watu wake zimesababisha kuongezeka kwa vitisho vya mabadiliko ya tabia nchi na viumbe hai, hasa mabadiliko yasiyo endelevu ya misitu kwa ajili ya kilimo. Kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, mradi wa USAID Tumiani Kupitia Vitendo (Hope Through Action) unalenga kutatua changamoto hizo.



Kampuni ya Huawei kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kuchangia ukuaji wa kidijitali endelevu Barani Afrika

$
0
0

 Na Mwandishi Wetu, Cape Town

 

Kampuni ya Huawei imejizatiti kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kuchangia ukuaji endelevu wa kidijitali Barani Afrika kwa mujibu wa Leo Chen, Rais wa kampuni ya Huawei, Kusini mwa Jangwa la Sahara.

 


Chen aliyasema hayo katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa AfricaCom 2023, mkutano mkubwa zaidi wa kiteknolojia barani Afrika, unaoendelea hivi sasa mjini Cape Town.

 

Afrika, alisema, inaweza kupata wimbi jipya la muunganiko wa kidijitali”, ambayo inaashiria awamu mpya katika enzi ya uchumi wa kidijitali.

 

Ili kufikia malengo haya, Chen anaamini kwamba "kipaumbele cha kwanza cha Afrika lazima kiwe kuharakisha maendeleo ya miundombinu ya uunganisho. Hiyo ni kwa sababu, katika siku zijazo, watu zaidi, vitu, na programu zitaunganishwa.

 

"Utaratibu huu utatoa data nyingi zaidi kuliko ilivyo leo. Kwa hivyo, tunahitaji mtandao ulio salama zaidi, unaotegemeka na ulioendelezwa ili kufanya kazi kama msingi wa kidijitali.

 

Miundombinu hii, alidokeza, inapaswa kuwa ya juu zaidi, na uthubitisho zaidi wa siku zijazo, na kujumuisha zaidi na kupatikana.

 

"Kufikia hatua za awali kunamaanisha lazima tuhakikishe kuwa nchi za Kiafrika zinapata teknolojia ya uunganishaji inayoongoza kama ulimwengu wote, kama vile huduma ya 4G ya Huawei, huduma za 5G na hata suluhu za 5G," alisisitiza.

 

Chen alibainisha kuwa miundombinu inapaswa kuunga mkono hali za matumizi ya siku zijazo, kama vile suluhu mahiri katika tasnia ya nyumba janja (smarth homes) na kuongeza kuwa muunganisho wa pamoja unasalia kuwa changamoto kubwa katika Bara.

 

Kulingana na Chen, kukumbatia uwezo kamili wa wingu (cloud) ni kipengele kingine muhimu cha uwekaji digitali.

 

"Ni muhimu kwamba nchi za Afrika zianzishe vituo vya kitaifa vya data vya wingu ili kutoa rasilimali za kompyuta kwa serikali, umma na wafanyabiashara wadogo (SMEs)" alisema.

 

"Hii itaendesha mfumo wa ikolojia wa uvumbuzi. Kwa kuanzisha 'e-Government Clouds'", aliongeza, "Serikali zinaweza kuboresha ufanisi wa utendaji kazi, na kuwapa wananchi huduma moja na ya kibunifu."

 

Aliongeza kuwa kutumia huduma ya wingu pia ni njia rahisi na ya kiuchumi kwa nchi za Kiafrika kupata uwezo wa AI

 

Chen pia aliangazia ukweli kwamba ni 'watu' wanaofanya uvumbuzi huu wote. "Hii ndiyo sababu Huawei daima imekuwa ikiweka ukuzaji wa talanta katikati ya mfumo wake wa ikolojia wa dijiti," alisema.

 

 

"Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Huawei imetoa mafunzo kwa vijana wenye vipaji zaidi ya 100,000 katika Bara la Afrika . Kati ya mwaka 2022 na 2025, tutafundisha vijana wengine 100, 000,” Alisema.

 

Alisema Huawei inaamini katika uvumbuzi wa pamoja wa ndani, na inajivunia kuunga mkono uvumbuzi maarufu duniani wa M-Pesa pamoja ma masuhulisho mengine ya kutuma fedha kupitia simu Barani Afrika.

 

"Kuharakisha Afrika ya kidijitali ni kuunda Afrika yenye mafanikio na endelevu," Chen alihitimisha. "Kwa maana hii, tuko tayari kufanya kazi na pande zote ili kufikia dhamira hii kubwa."

 

TANZANIA, ROMANIA KUSAIDIANA KWENYE KILIMO, MAJANGA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mgeni wake Rais wa Romania Mhe.  Klaus Iohannis mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Novemba 2023.


 Na Selemani Msuya


KATIKA kuendeleza ushirikiano wa Tanzania na Romania nchi hizo zimetia saini za makubaliano katika sekta ya kilimo, mazingira na majanga.


Hayo yamesemwa leo, Ikulu jijini Dar es Salaam na Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Romania Klaus Iohannis wakati wakizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza mazungumzo ya ndani. 


Akizungumzia ushirikiano huo, Rais Samia alisema Tanzania na Romania zimekuwa na ushirikiano mzuri, hivyo ujio wa Rais huyo nchini imeendelea kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili huku akieleza katika mazungumzo yao wamekubaliana kushirkiana katika masuala mbalimbali yakiwemo ya dawa na usindikaji kwa mazao ya kilimo.


Rais Dk.Samia amesema kwa niaba ya wananchi wa Tanzania wanayofuraha kubwa ya kumpokea Rais na ujumbe wake na kwamba wataendelea kudumisha ushirikiano, ili uweze kulete tija kwa wananchi wa nchi zao.


Dk Samia amesema uhusiano wa Tanzania na Romania ulainza Mei mwaka 1964 ikiwa ni mwezi mmoja tu baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Hivyo Romania ni mbia wa maendeleo kwa muda mrefu na kwamba atahakikisha mashirikiano hayo yanakuwa endelevu.


“Tumekubaliana kuendelea kuimarisha sekta mbalimbali kama sekta ya dawa, usindikaji wa mazao ya  kilimo, madini, biashara, ulinzi, majanga na nyingine," amesema.


Pia Rais Samia amesema katika mazungumzo yao wamekubaliana ufadhili wa masomo katika udaktari na famasia, eneo ambalo bado lina uhitaji mkubwa," ameongeza.


Amesema katika mazungumzo hayo, Romania imekubali kutoa nafasi 10 za Watanzania kwenda kusoma kwa masomo ambayo watachagua, huku Tanzania ikitoa nafasi tano za ufadhilii kwa wanafunzi wa tano wa Romania  kuja kusoma nchini.


“Tumezungumzia kuhusu kuimarisha sekta ya biashara hasa kukuza zaidi biashara kwa kuangalia maeneo ambayo tunaweza kufanya pamoja, kualika wafanyabiashara wa Romania kuja Tanzania na Watanzania kwenda Romania kubadilisha uzoefu.


Amesema wamekubaliana mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zao kuendelea kuzungumza mara kwa mara, ili kuhakikisha fursa zilizopo baina yao zinatumika ipasavyo kwa maslahi ya pande zote.


Aidha, Rais Dk.Samia ameipongeza  Romania kukubali kuendelea kushirikiana na nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania.


Pia amesema wameomba Romania isaidie kuwapa nguvu katika kuhakikisha Tanzania inafanikiwa katika eneo la nishati safi ambayo inahitaji kwa matumizi mbalimbali kwa sasa.


Kwa upande mwingine Rais Samia amesema wakati umefika kwa kuanza utekelezaji wa makubaliano waliyosaini mwaka 2018, kuhusu kufanya mikutano ya mazungumzo ya kisiasa.


Amesisitiza ni matumaini yote ambayo wameyazungumza yatatekelezwa kwa maslahi ya nchi zote mbili.


Naye Rais Iohannis amesema mwakani Romania na Tanzania zinatumiza miaka 60 ya ushirikiano wa kidiplomasia, hivyo kupitia ziara hiyo ya kwanza kufanywa na kiongozi wa kitaifa wamejadiliana namna ya kuboresha na kuendeleza mazuri ambayo yamefanyika.


Rais Iohannis amesema Tanzania ni moja ya nchi ambayo wamekuwa wakishirikiana kwa mafanikio makubwa na kwamba watahakikisha unaendelea.


Amesema mikakati yao ya kurejesha ushirikiano na nchi za Afrika utahakikisha Tanzania inanufaika zaidi.


Rais Iohannis amesema sekta ya kilimo na majanga itapewa msukumo mkubwa kwani zina mchango kwenye maendeleo.


"Tunatamani sekta ambazo tumekubaliana zinafanikiwa kwa kasi ili kuhakikisha maendeleo yanapatikana. Mfano sekta ya ulinzi, teknolojia na usalama wa mitandaoni,"amesema.


Tamasha la FFC Krismasi ni kubwa hustahili kulikosa

$
0
0

Kufanyika JNICC, nyimbo za Classical kutawala

 


DESEMBA 25 kila mwaka, Wakristo ulimwenguni kote usheherekea maadhimisho ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita.

 

Sherehe hizo maarufu kwa jina la Krismasi uwaleta pamoja wazazi, ndugu, jamaa na watoto kukaa pamoja kwa kula na kunywa huku wakipeana zawadi mbalimbali.

 

Katika kuadhimisha sikukuu hiyo kwa mwaka huu, Kwaya Flying Family inayojumuisha waimbaji kutoka madhehebu mbalimbali ya kikristo wenye vipaji vya uimbaji wameamua kumtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji wa nyimbo zenye ufundi wa hali ya juu.

 

Kwa namna ya pekee tamasha la mwaka huu litaambatana na maadhimisho ya kusherehekea miaka mitano tangu kwaya hiyo ianzishe mwaka 2018.

 

Kwaya inajivunia kujenga umoja na upendo kwa wakristu kwa kutumia muziki na kuweza kuimba pamoja bila kujali tofauti zao za kimadhehebu kwa kipindi cha miaka mitano na kufanikiwa kuandaa matamasha makubwa sita yaliyowakusanya waumini na viongozi mbalimbali chini ya mchungaji mmoja Yesu Kristo.

 

Kwaya hiyo itafanya tamasha na wanakwaya wake kuimba ‘Classical music’ ambao ni maarufu duniani kote na umejizolea umaarufu tangu miaka ya zamani.

 

Innocent Fundisha ni Kiongozi wa kwaya hiyo anasema wapenzi wa muziki mtakatifu wakifika katika tamasha hilo ambalo linatarajiwa kufanyika Desemba 10, mwaka huu katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC), jiini Dar es salaam watapata kusikia kazi za watunzi nguli kama George Handel, Wolfgang Mozart, Johan Bach, Joseph Haydn, Felix Mendelson, Anthonio Vivald na wengine wengi.

 

Anasema tiketi za tamasha hilo zinapatikana Kanisa Katoliki la St Peter Osterbay, Kanisa la Kiinjili na Kilutheri (KKKT) Msasani, Ofisi za Paones Posta Samora tower, KKKT Kijitonyama, Kanisa Katoliki Mwenge na Kanisa la Anglican Ilala.

 

Hata hivyo anasema pia wanatumia kazi za watunzi wazawa kama John Mgandu, Egidius Mushumbusi na Mathias Msafiri bila kusahau tenzi za rohoni.

 

Fundisha anasema si kazi rahisi kwa wanakwaya kujifunza nyimbo hizo lakini kwa msaada wa Mungu wanafanikiwa kushika na kujifunza kwa usahihi.

 

“Kwaya hii ilianzishwa Aprili, 2018 jijini Dar es Salaam ikiwa na wanakwaya wasiozidi 15 ila kwa sasa ina wanachama hai 40, tumeamua kumsifu Mungu na kutangaza sifa zake hapa duniani kwa njia ya uimbaji,” anasema Fundisha.

 

Anasema anatambua kuwa sikukuu ya Krisimasi uwaleta pamoja na ndugu, jamaa na marafiki hiyo anaamini kupitia tamasha hilo watu wataburudika, watafurahi na kudumisha utamaduni wa kusheherekea Krismasi kwa njia ya muziki wa classical.

“Tunatarajia kuwa na Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo Kuu la Dar es Salaam, Thaddaeus Ruwa,ichi, Askofu wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dk. Alex Malasusa, Askofu Jackson Sosthenes wa Kanisa la Anglican Dayosisi ya Dar es salaam.

 

“Pia tutakuwa na maaskofu wasaidizi Stephano Musomba na Henry Mchamungu wa Kanisa Katoliki jimbo kuu la Dar es Salaam, mapadre na wachungaji. pamoja nao tutakuwa na ushiriki wa viongozi wa serikali pamoja na viongozi wastaafu, wanadisplomasia wanaowakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na washiriki kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania,” anasema

 

 Lengo la kwaya hiyo

 

Fundisha anasema lengo la kuanzishwa kwa kwaya hiyo ni kuleta umoja na mahusuano mazuri katika madhehebu ya kikristu kwa njia ya kushirikishana vipaji vya kimuziki.

 

“Tunashirikishana vipaji hivyo vilivyopo kwa kuandaa kwaya ya pamoja, matamasha mbalimbali, huduma kwa wahitaji pamoja na kushiriki matukio ya kijamii yanayolenga kudumisha umoja wa wakristu na taifa kwa ujumla,” anasema Fundisha.

 

Anasema kwaya hiyo yenye viongozi wa tano akiwa yeye ndiyo mwenyekiti imeanzisha bodi ya wadhamini yenye wajumbe tisa ambayo itazinduliwa Disemba 11, 2022 siku ya tamasha lao la Krismasi ikijumuisha viongozi maarufu kwa ajili ya kusimamia kwaya pamoja na kuweka mikakati bora ya kwenda mbele zaidi.

 

 Utendaji kazi wa kikundi

 

Anasema kwaya inafanya mazoezi mara moja kwa wiki siku ya jumapili kuanzia saa tisa alasiri hadi saa kumi na mbili jioni.

 

Aidha anasema sehemu kubwa ya mazoezi yanafanyika kwa njia ya mtandao wa Whatsup ambapo kila sauti ina kundi lake na walimu wa kuwasimamia siku zote za wiki na jumapili inakuwa ni siku ya kuunganisha tu.

 

“Mwalimu anajirekodi na kuwatumia, kisha kila mwanakwaya anasikiliza na kujifunza na kisha kujirekodi na kutuma tena kwenye group kwa ajili ya mwalimu kusikiliza na kurekebisha. Kwa sasa tumeenda mbali zaidi ambapo nyimbo nyingi wanakwaya wanasikiliza wao wenyewe kupitia mtandao wa Youtube.

 

“Kisha mwalimu wa kila sauti ukutana na kundi lake kwa ajili ya masahihisho kabla ya kwaya nzima kukutana na kuunganisha siku ya jumapili. Kwaya ina walimu kumi na moja wenye uwezo mkubwa wa kusoma muziki, kupiga kinanda na piano, utunzi wa kiwango cha juu kabisa pamoja kufundisha somo la muziki kwa wanakwaya na wasio wanakwaya,” anasema Fundisha

 

Anasema yote hayo yanafanyika chini ya kikosi imara cha wataalamu kikiongozwa na Mwalimu Wakili Nereus Mutongore, CPA Innocent Fundisha, Egidius Mushumbusi, Jerry Newman, Deogratias ngereza, Mathias Msafiri, Ainamringi Foya, Pauline Tumaini, Lucy Mutongore, Gloria Mugisha na Elizabeth Malenga.

 

 Matarajio ya kikundi

 

Fundisha anasema matarajio ya kwaya hiyo ni kutambulika na kuheshimika kimataifa kupitia kiwango cha juu kabisa cha ubora wa muziki na matamasha yake na kwamba hayo yote yatatokana na mipango sahihi ya kujutuma na nidhamu ya hali yajuu katika kuishi malengo ya kwaya.

 

Wito kwa watu wengine

 

Anasema wanawashauri vijana kujituma muda na vipaji vyao kumtukuza Mungu kwani ndiye aliyewapa vyote walivyo navyo.

 

Fundisha anasema kupitia vikundi vya uimbaji wanamtukuza Mungu na kupata wasaa wa kuepuka kushiriki vitendo viovu huko mitaani hivyo upata baraka na neema kwa kufanya yampendezayo Mungu.

 

“Tunatoa wito kwa wakristu wote kutambua kuwa sisi sote ni kondoo na mchungaji wetu ni mmoja Bwana wetu Yesu Kristo, hivyo yatupasa kuishi kwa umoja na mshikamano na inawezekana kushirikiana bila kujali tofauti zetu za kimadhehebu.

 

“Lakini pia tunatoa wito kwa wenye vipaji vya kuimba au kupiga vyombo vya muziki wajiunge nasi kwa kufuata taratibu watakazopewa ili kudumisha umoja huu na kuueneza kwa wengi zaidi,” anasema

 

Hata hivyo anasema wanawashukuru wadau mbalimbali hasa walezi wao ambao ni maaskofu, wachungaji, mapadre pamoja na waamini kwa kuwapa moyo, kuwaongoza na kuwashauri, kuwawezesha kwa hali na mali bila kuwasahau Paones General trading ambao wanawafadhili kwenye matamasha yao.

NMB yabainisha sababu za kuipa kipaumbele miradi rafiki kimazingira

$
0
0

Na Mwandishi Wetu
 
BENKI ya NMB imesema imeanza kuzingatia kwa karibu masuala ya uhifadhi wa mazingira katika uendeshaji wake na kufadhili miradi mbalimabli kutokana na umuhimu wake katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.
 

Akizungumza jijini Dar es Salaam Alhamisi wiki hii, Afisa Mwandamizi wa Benki hiyo, Bi Hellen Dalali, alisema kutokana na hilo NMB sasa inaipa kipaumbele miradi rafiki kimazingira na wakopaji wanaolitambua hilo.
 
Bi. Dalali aliuambia mkutano kuhusu masuluhisho asilia (NBS) dhidi ya janga la mabadiliko ya tabianchi kuwa ufadhili unaofanywa na benki hiyo umejikita zaidi kupunguza athari za hewa ukaa na kuongezeka kwa joto duniani.
 
Alisema NMB imeweka msimamo huo kutokana na umuhimu wa miradi ya kijani na ile yenye tija kijamii kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo endelevu.
 
Aidha, Meneja Miradi Mwandamizi huyo alibainisha kuwa athari za mabadiliko ya tabianchi si tu ni hali halisi iliyopo bali pia ni hatari kubwa ambayo madhara yake tayari yanaziyumbisha biashara na chumi nyingi duniani.
 
Akizungumzia athari za janga hilo wakati wa jopo la utangulizi la mkutano huo, alisema sekta ya fedha nayo tayari imeahirika hivyo kuongeza umuhimu wake kushiriki na kuwekeza vilivyo katika hatua za kupambana na changamoto hizo.
 
“Hakuna hata mmoja wetu ambaye hajaathirika kwa hiyo wote tunawajibika kushiriki kikamilifu kupambana na athari hizi,” Bi Dalali aliwaambia washiriki wa Mkutano wa NBS Tanzania 2023, ambao ulilenga hasa maendeleo ya biashara ya hewa ya ukaa nchini.
 
Alisema hatari za mabadiliko ya tabianchi zimeilazimu NMB na benki nyingine kubuni mbinu mpya za kibenki na uendeshaji ili kupunguza kaboni hewani na kukidhi matarajio ya kuhifadhi mazingira.
 
"Mabadiliko ya tabianchi yameathiri biashara nyingi duniani na kupekea chumi nyingi na sekta ya fedha kuathirika vile vile kutokana na biashara hizi kufadhiliwa na benki,” alibainisha.
 
Kwa mujibu wa Bi. Dalali, benki hazijikiti tu kupunguza shughuli zake kuathiri mazingira bali pia zinaongeza umakini katika tathmini za athari za kitabianchi na kijamii kwenye michakato ya mikopo.
 
Hilo linafanyika kuunga mkono juhudi za kitaasisi kukabiliana na janga la mabadiliko ya tabianchi na kuhakikisha miradi na biashara zinazofadhiliwa zinakuwa na madhara madogo au haziathiri kabisa mazingira, alifafanua.
 
Aliongeza kuwa athari za mabadiliko ya tabianchi kwa benki zipo za aina mbili, moja ikiwa ni zile zinatokana na uharibifu wa mali na rasilimali kutokana na majanga kama mafuriko  au mvua kubwa.
 
Kundi la pili ni lile la athari za kimpito ambazo hasa zinatokana na madiliko ya kikanuni, kisera, kiteknolojia na kimasoko yanayolenga kuchagiza shughuli za kiuchumi zinazozalisha hewa kidogo ya ukaa na kupambana na changamoto nyingine za mabadiliko ya tabianchi.
 
Bi Dalali aliuambia mkutano huo wa siku moja kuwa pamoja na athari zake nyingi, mabadiliko ya tabianchi pia yana fursa lukuki za kibiashara, ambazo mgeni rasmi kwenye shughuli hiyo, Waziri Angela Kairuki, alisema ni pamoja na biashara ya hewa ukaa ambayo inazidi kuimarika nchini.
 
Akitolea mifano ya hatifungani ya NMB Jamii Bondi na kampeni ya kupanda miti iliyozinduliwa na benki hiyo mwanzoni mwa mwaka huu, mtaalamu huyo wa masuala ya uendelevu alisema benki zinaweza kuongoza kuzifungua fursa hizo kupitia ufadhili endelevu na ule wa kijani.
 
"Athari za mabadiliko ya tabianchi zinatoa fursa na mazingira muafaka ya biashara kwa sekta binafsi na benki kushiriki. Hii ni kupitia uhamasishaji stahiki wa fedha na mitaji ili kuweza kufadhili miradi ya kukabiliana na changamoto hizo,” alibainisha na kusisitiza umuhimu wa uwezeshwaji kimaarifa ili kuwa na kada yenye ufahamu mzuri wa ufadhili wa aina hiyo.
 
Suala jingine, ambalo alisema ni nyeti katika kuishirikisha sekta binafsi katika masuala ya tabianchi, mijadala ya biashara ya hewa ukaa na mipango ya masuluhisho asilia, ni lile la ushirikiano kama ambavyo NMB imefanya na Wakala wa Misitu Tanzania kwenye mradi wa kupanda miti milioni moja nchi nzima mwaka huu.



NMB yakabidhi mabati ya Mil. 28/- kwa shule 5 Kisarawe

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Fatma Nyangassa (wa tatu kushoto), akipokea sehemu ya msaada wa mabati 600 yenye thamani ya Sh. Milioni 28.2 kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper (wa tatu kulia), wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo kwa shule tano za msingi wilayani humo. Kulia ni Diwani ya Kata ya Kisarawe, Abel Mudo na wa pili kulia ni Meneja wa NMB Tawi la Kisarawe, Bertha Mungure. (Na Mpiga Picha Wetu).

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Fatma Nyangassa (kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada wa mabati 600 yenye thamani ya Sh. Milioni 28.2 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Beatrice Dominic, yaliyotolewa na Benki ya NMB kwa ajili ya shule tano za msingi wilayani humo. Katikati anayeshuhudia ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper.

Baadhi ya wanafuzi wa Shule ya Msingi Kibasila wakiwa katika picha ya kumbukumbu baada ya kupokea msaada wa mabati 600 kutoka Benki ya NMB kwa ajili ya shule tano za msingi wilayani Kisarawe.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Fatma Nyangassa, akizungumza wakati wa hafla ya kupokea msaada wa mabati 600 yenye thamani ya Sh. Milioni 28.2 kutoka Benki ya NMB kwa ajili ya shule tano za msingi wilayani humo. Kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper na wa tatu kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Zuberi Kizwezwe.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Fatma Nyangassa (katikati) akiagana na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper (kushoto) baada ya kupokea msaada wa mabati 600 yenye thamani ya Sh. Milioni 28.2 kutoka Benki ya NMB kwa ajili ya shule tano za msingi wilayani Kisarawe. Kulia ni Meneja wa NMB Tawi la Kisarawe, Bertha Mungure. (Na Mpiga Picha Wetu).

 
 

NA MWANDISHI WETU, KISARAWE

 

KATIKA kuendeleza utamaduni wa Programu ya Uwekezaji kwa Jamii (CSI), Benki ya NMB imekabidhi msaada wa mabati 600 yenye thamani ya Shilingi Milioni 28.2 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Fatma Almasi Nyangassa kwa ajili ya shule tano za msingi za Halmashauri hiyo.

 

Makabidhiano hayo ymefanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Kisarawe, ambako Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper, alimkabidhi DC Nyangasa mabati hayo, naye kuyakabidhi kwa Walimu Wakuu wa shule hizo, mbele ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Beatrice Dominic.

 

Shule zilizonufaika na msaada huo, ambao thamani yake ni sehemu ya asilimia moja ya faida baada ya kodi ya Benki ya NMB kwa mwaka jana, ni Kibasila (bati 200), Titu (bati 100), Panga la Mwingereza (bati 100), Mtunani (bati 100) na Vilabwa (bati 100).

 

Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper, alisema thamani ya mabati hayo ya Sh. Mil. 28.2 ni sehemu tu ya kiasi cha Sh. Bil. 6.2 zilizotengwa na benki hiyo kusapoti jitihada za Serikali katika sekta za Elimu, Afya, Majanga na Mazingira kwa mwaka 2023.

 

“Tuko hapa kukabidhi mabati 200 yenye thamani ya Sh. Mil. 9.4 kwa Shule ya Msingi Kibasila, huku shule za Panga la Mwingereza, Mtutani, Titu na Vilabwa - kila moja tukiikabidhiwa mabati 100 yenye thamani ya Sh. Mil. 4.7, hivyo kufanya jumla kuu kuwa Mil. 28.2.

 

“Kiasi hiki ni sehemu ya Programu ya Uwekezaji kwa Jamii ambayo NMB tumekuwa tukiifanya kwa zaidi ya miaka saba sasa, ambako kwa mwaka huu peke yake tumetenga Sh. Bil. 6.2 kusaidia utatuzi wa changamoto zinazokwaza sekta za elimu, afya, majanga na mazingira.

 

“Mheshimiwa mgeni rasmi, elimu ni miongoni mwa sekta za kipaumbele kwa benki yetu na hii ni kutokana na ukweli kwamba ndio ufunguo wa maendeleo ya taifa lolote duniani, na wanafunzi wanaopata elimu mashuleni wanatokana na jamii iliyotufikisha NMB hapa tulipo,” alisema.

 

Alibainisha kuwa, usaidizi wao katika utatuzi wa changamoto za elimu, unalenga kuunga mkono juhudi za Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, ambayo inapambana kuhakikisha kunakuwepo na upatikanaji wa elimu bora mijini na vijijini na wao kama wadau, hilo ni jukumu lao.

 

DC Nyangassa kwa upande wake aliishukuru NMB kwa kujitoa kwao katika kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi, na kwamba ingawa kutoa kupitia CSI ni utaratibu wa kawaida kwa taasisi hiyo, lakini kwa Serikali ni jambo kubwa linalopaswa kuungwa mkono na wadau wa elimu.

 

“Mnalofanya hapa NMB ni jambo kubwa sana kwetu, mnaunga mkono juhudi za Serikali ya Rais Samia, ambayo kwa mwaka huu wa fedha,  imetupa kiasi cha Sh. Mil. 443.42 kwa ajili ya maboresho mbalimbali ya miundombinu ya elimu Wilaya ya Kisarawe tu.

 

“Hii sio mara ya kwanza kwenu, mmefanya hivi kwa kutoa madawati mashuleni, vifaa tiba mahospitalini na zaidi ya yote mlikuwa nasi kuwezesha na kushiriki ‘Programu ya Kisarawesha’, inayolenga kuboresha mazingira ya kiuchumi kwa wanawake wa Kisarawe,” alisema DC Nyangassa.

 

Alisema yote hayo ni uthibitisho wa moyo wa kujali na kuthamini jamii walionao NMB, huku akiwapongeza Walimu wa shule zilizonufaika na msaada huo, kwa kufanya kazi kwa bidii licha ya ugumu wa mazingira ya kufundishia yanayozikabili shule zao.

 

Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>