Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

Wafanyabishara Mkuranga, Kibiti wampongeza Samia uhuru wa kibiashara

$
0
0

Na Mwandishi Wetu, Mkuranga


WAFANYABISHARA wilayani Mkuranga na Kibiti, wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuliza dhorobu ya hali ya biashara nchini.


Wamesema kwenye wilaya hizo biashara zinafanyika kwa amani na utulivu bila usumbufu tofauti na miaka ya nyuma.


Wametoa pongezi hizo kwa nyakati tofauti kwenye mkutano kati ya wafanyabishara wa wilaya hizo na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara (JWT) inayoendelea mkoani Pwani yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wafanyabishara.



Mfanyabiashara Hassan Mbwana Kambangwa, amesema wafanyabiashara kwa asilimia kubwa wilayani humo wananufaidika sana tangu kuingia kwa utawala wa Rais Samia.


Amesema "Kimsingi namshuruku Rais Samia kwa kutuletea ugeni uliotupa fursa ya kuzungumza changamoto zinazotukabili, lakini sisi tangu kuingia kwa utawala huu wa Mama Samia tunafaidika nao kwa asilimia kubwa."


Mfanyabiasha huyo ametolea mfano wa mambo wanayofaidika nayo kuwa ni  mikopo, uhusiano mazuri na halmashauri lakini pia taasisi mbalimbali za kifedha ziko huru kuwasaidia wafanyabiashara.


Amesema serikali imezingatia suala la amani na utulivu na kwa mikoa mingi ilikua inapata changamoto nyingi lakini hapa wilaya ya Mkuranga wafanyabiashara wako huru na wanafanyabiashara bila bugudha.


"Tunamshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan tunafanyabiashara kwa amani lakini pia tunashukuru ujio huu wa leo umefanya tuweza kufunguka yale ambayo yako ndani ya moyo na tunaamini mtayafikisha," Kambangwa.


Naye mfanyabishara Wilaya ya Kibiti, Salim Juma, amempongeza Rais Samia kwa kuona sekta ya wafanyabishara ni sehemu ya uchumi wa Taifa na kuamua kuungana kwa pamoja kutatua kero zao.


"Ili kuwa na ustawi tumefanikiwa kumpa Rais Samia, ambaye ameona umuhimu wetu na kutambua mchango wetu ndio maana leo viongozi mpo hapa," amesema Juma.


KIPIGO CHAENDELEA KUITESA SIMBA

$
0
0
Na Mtandao 

Baada ya kipigo cha magoli 5-1 cha Simba kinaleta presha kubwa ukizingatia ni derby nje ya kufukuzwa kwa Kocha Mkuu Robertinho na Mtaalam wake wa viungo Hategikima ila kuna stori ambazo zimeanza kusambaa na kuwalenga baadhi ya wachezaji na wafanyakazi wa Simba kwa madai ya kuhujumu timu.

Hizi tuhuma za fulani kahujumu hazijaanza leo toka nacheza lakini sijawahi kuwa na imani nazo kwa sababu leo unatuhumiwa kuwa umeuza mechi kwa Simba au Yanga lakini baadae timu hizo hizo zinapigana vikumbo kukusajili , mimi naamini kama leo uko Simba na umeuza mechi sijui Yanga sidhani kama Yanga kesho watataka kukusajili sababu hata wao wangekuwa na mashaka na wewe ila kwakuwa hakuna ndio maana wakati wa usajili unaona mchezaji aliyetuhumiwa kuuza kasajiliwa na hiyo timu.

Hivyo nafikiri hizi stori za kutuhumiana huwa zinalenga vitu viwili naamini moja kisaikolojia kwa maana mashabiki wakisikia hivi wanaamini na kufarijika kuwa viongozi wao wanafanya kazi lakini pia lina athari sababu hata Mchezaji au Kiongozi ambaye leo hajatuhumiwa ataona kweli hapa sio mahali salama pia kwangu.


Hii pia ina madhara maana ikitokea na mechi ijayo mkafungwa maana mtatafu watu wengine wakuwatoa kafara ila kiukweli kwangu mimi kwa namna mpinzani Yanga alivyocheza sidhani kama kuna viashiria vya usaliti zaidi ya kuona Yanga tu walikuwa bora zaidi ya Simba SC.

Watu Wenye Ulemavu Wapewa Visaidizi

$
0
0

 


Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji na Utumishi, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (WMJJWW) Dkt. Salum Khamis (Kulia) akimkabidhi mwakilishi wa Zanzibar Maisha Bora Foundation Mohamed Nyahega visaidizi vya Watu wenye Ulemavu, kwa niaba ya katibu Mkuu wa Wizara hiyo Abeida Rashid Abdallah

Hafla ya makabidhiano imefanyika leo, Novemba 07, 2023, katika ukumbi wa Makao ya Wazee Sebleni, Unguja.


Na Talib Ussi


Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Abeida Rashid Abdallah amesema Wizara hiyo itaendelea kusimamia maendeleo ya jamii ikiwemo kundi la watu wenye ulemavu ili kuona wanaishi katika mazingira mazuri na salama.

Akizungumza kwa niaba ya katibu mkuu huyo  Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji na Utumishi Dkt. Salum Khamis Rashid wakati akikabidhi visaidizi vya watu wenye Ulemavu kwa Taasisi ya Maisha Bora Fondation, katika ukumbi wa Wazee Sebleni.

Dkt Salum alivitaja visaidizi hivyo ikiwemo na lotion 72 kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi ALBINO, fimbo nyeupe 20 kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa uoni, pamoja na viti vya magurudumu mawili 30 (Wheel chair) kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa miguu.

Alisema Wizara itaendelea kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi kadiri hali itakavyoruhusu ili kuhakikisha hakuna kundi ambalo limeachwa nyuma. 



Alileza kwamba  moja kati ya jukumu la Wizara hiyo ni kujenga ustawi mzuri kwa jamii hivyo Wizara hiyo itaendelea kutatua changamoto za watu wenye ulemavu na makundi mengine ili waondokane na changamoto hizo.

“Wizara inaelewa changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu na makundi mengine katika jamii lakini hali itakavyokuwa inaruhusu, Wizara itaendelea kutatua changamoto hizo” Alisema Dkt Salum

Naye mwakilishi kutoka Maisha Bora Foundation Mohammed Nyahega amesema watu wenye ulemavu bado wanahitaji vitu vingi ili waweze kuishi vizuri. Hivyo msaada uliyotolewa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto utasaidia kutatua baadhi ya changamoto zao.

Aidha ameishukuru Wizara hiyo pamoja na kuahidi kwamba visaidizi alivyokabidhiwa  atavifikisha kama alivyopewa bila ya kwenda kinyume  na hatimae vitawafikia walengwa kama Wizara ilivyokusudia kuendeleza kujenga Ustawi wa Jamii.

Visaidizi hivyo vimetolewa na Ubalozi wa Kuwait kwa ajili ya kuendeleza mashirikiano mazuri na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.



SERIKALI YATOA UFAFANUZI WA MIFUGO ILIYOKAMATWA SERENGETI

$
0
0

 Na Happiness Shayo- Dodoma


Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amesema kuwa suala linalohusisha ng'ombe 806, kondoo 420 na  mbuzi 100 waliokamatwa Serengeti na kupigwa mnada  baada ya Mahakama ya Musoma kutoa hukumu, limeshahitimishwa kimahakama baada ya taratibu zote kukamilika.


Waziri Kairuki ameyasema hayo leo Novemba 9,2023 Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu hoja ya Mbunge wa Ngorongoro, Mhe. Emmanuel Ole Shangai aliyeilalamikia Serikali kuhusu mifugo hiyo iliyokamatwa na Askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) katika eneo la Mugumu Serengeti na kupelekwa mahakamani kisha kupigwa mnada.


“Ni suala ambalo limehitimishwa mahakamani kupitia kesi ya jinai namba  10 ya mwaka 2023 kwa kuingiza mifugo hifadhini isivyo halali na tayari hukumu ilitolewa, na tarehe 1 Novemba 2023 ilielekezwa dalali wa mahakama ateuliwe kwa ajili ya kupiga mnada wa hadhara kwa kufuata taratibu kama ambavyo sheria yetu ya wanyamapori ya mwaka 2009 lakini vilevile sheria yetu zinazosimamia Hifadhi za Taifa zinavyoelekeza ” Mhe. Kairuki amesisitiza.


Amesema, kufuatia mnada huo kutokana na hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu ya Musoma zilipatikana fedha kiasi cha shilingi milioni 169,264.


Aidha, ameongeza kuwa  lengo la Serikali kwa mujibu wa Ibara ya 27 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria  ambazo zimewekwa ni kuendelea kulinda hifadhi za Taifa pamoja, maliasili na uoto wa asili uliomo ikiwa ni pamoja na wanyama na viumbe vingine vilivyoko katika maeneo yaliyohifadhiwa 


Kufuatia ufafanuzi huo, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson ameipa Serikali muda wa kuliangalia upya suala hilo.

Masheha Zanzibar watakiwa kushirikiana na Waratibu kupinga vitendo vya udhalilishaji

$
0
0

Masheha Zanzibar wametakiwa kushirikiana vyema na waratibu wa kupinga vitendo vya udhalilishaji ambao wanafanyakazi katika Shehia mbali mbali za Unguja  na Pemba ili changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa Majukumu yao ziweze kutatuliwa kwa wepesi/urahisi.


Akizungumza mmoja kati Maafisa  kutoka Divisheni ya Maendeleo ya Jamii ndugu Omar Haji Omar wakati walipofika kutambulisha kazi za Idara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto katika shehia, kwa Mashesha na Waratibu wa shehia kwa Wilaya ya kati Unguja, amesema mashirikiano yao yatawezesha kutatua changamoto kwa haraka.


Amefahamisha kwamba shughuli zote za  maendeleo au changamoto ya jamii katika shehia zao zinapaswa kuripotiwa katika Wizara husika lakini mashirikiano yao yatawezesha Wizara ya maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto kufanya kazi kwa ufanisi.


Amesema utaratibu huu umekuja baada ya kuundwa kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ikiwa miongoni mwa shughuli zake ni kutambua na kusimami shughuli zote za maendeleo ya jamii katika shehia zao zinatambuliwa na Wizara hiyo.


Amesmea ni lazima kuhakikisha kuwa shughuli zote zinazofanyika katika shehia zao wanaziwasilisha kupitia katika Wilaya ili nao waweze kuziwasilisha katika Wizara husika.


Amesema wanatambua kuwa masheha wanafanya kazi kubwa katika jamii, hivyo katika kuendeleza maendeleo mbalimbali katika shehia zao, ni lazima kuondoa changamoto baina ya masheha na waratibu ili  wafanye kazi zao vizuri kwa kwa kuleta ustawi mzuri kwa jamii.


Amesema lengo ni kuona maendeleo yote yanayotaka kufanyika na yaliyofanyika yanatambuliwa na kuona kila penye uhitaji wa huduma zinafikiwa kupitia shehia zao ili kupunguza matatizo madogo madogo yanayojitokeza.


Kwa upande wao Masheha wameonesha kufurahishwa kuwepo kwa utaratibu huo kwani awali haukuwepo na kusema kuwa wamepata usaidizi mzuri juu ya utendaji wao wa kazi.


Wamesema suala la kuripotiwa masuala ya Maendeleo ya Jamii katika shehia zao haufanyiki kwani hata wao baadhi ya shughuli hawashirikishwi, hivyo utaratibu huo utawasaidia wao katika kupata taarifa  sahihi za kumsaidia Rais katika kuelezea masuala mbalimbali ya Maendeleo yanayofanyika katika nchi kwa ujumla.


Nao waratibu wamewaomba Maafisa hao kuwafikishia utaratibu huo viongozi wao wa siasa wakiwemo Wabunge na Wawakilishi kuhusu miradi yao wanayoitoa katika shehia zao kuwashirikisha na Masheha pamoja na waratibu kwani wao ndio wahusika wakuu wa shehia.

MAJALIWA ATAKA WATHAMINI WAWE WAADILIFU

$
0
0

*Asisitiza kazi ya uthamini si ya wababaishaji au vishoka

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wathamini wote wawe waadilifu, wenye weledi na wazingatie miiko ya taaluma katika kazi zao za kila siku.

 

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa wathamini ni watu muhimu katika kufanikisha mipango ya maendeleo ya Taifa. “Mnapaswa kuwa waadilifu na kuzingatia thamani halisi ya ardhi, jengo au chochote kinachofanyiwa uthamini,” amesema.

 

Amesema hayo leo (Alhamisi, Novemba 9, 2023) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nne wa Mwaka wa Wathamini unaofanyika kwa siku mbili katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.

 

“Kazi ya uthamini si ya wababaishaji au vishoka, hivyo basi kila mthamini hana budi kuthamini na kuheshimu taaluma yake.”

 

Mheshimiwa Majaliwa amesisitiza kuwa: “Wapo baadhi ya wathamini ambao si waadilifu kwa kushirikiana na watendaji wengine hutoa makadirio ambayo hayawiani na thamani halisi. Vitendo hivyo husababisha kupoteza mapato ya Serikali lakini pia kuwanyima haki wale wanaostahili kupata haki.”

 

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewataka watendaji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi hususani wathamini washirikiane na sekta binafsi kufanya kazi za uthamini. “Tumieni fursa ya uwepo wa wathamini binafsi ili kutoa huduma bora na ya haraka hapa nchini, kufanya hivyo mtakuwa mnatekeleza maagizo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya ushirikishaji wa sekta binafsi kwa maendeleo ya Taifa.”

 

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amewataka wathamini hao watumie mkutano huo kufanya majadiliano ya kina kuhusu masuala ya taratibu za utwaaji ardhi na sheria zake, ukokotozi wa fidia katika maeneo ya madini, viwango vya thamani ya ardhi na mazao, changamoto za kisera za utwaaji ardhi pamoja na kupata suluhu ya malalamiko ya wananchi.

 

Naye, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geoffrey Pinda amesema kuwa uthamini wa fidia ni ufunguo wa maendeleo na mabadiliko chanya ya kiuchumi kwa kuwa unawezesha wawekezaji kupata ardhi na kuwekeza mitaji yao.

 

Amesema kuwa Wizara kwa kushirikiana na Bodi ya Usajili wa Wathamini nchini imejipanga kuhakikisha shughuli zote za uthamini zinaboreshwa. “Wizara itasimamia upatikanaji wa huduma hii kwa wananchi kwa wakati, kutatua kero mbalimbali za wananchi katika eneo hili la fidia na kuwezesha Bodi kuwachukulia hatua kali wale wote wanaohujumu shughuli za uthamini nchini.”

 

Amesema kuwa uthamini hufanyika na kuwezesha upatikanaji wa ardhi itakayotumika kwa ajili ya matumizi ya umma, kuweka miundombinu ya msingi, huduma za jamii, viwanda na kupanga makazi.

 

DC Mpogolo azindua Duka kubwa la Hisense Dar

$
0
0
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Serikali ya Awamu ya Sita imesema itaendelea kudumisha amani na usalama wa Taifa pomoja kutengeneza mazingira rafiki ya biashara jambo ambalo litasaidia kuongeza kasi ya wadau wa maendeleo kuja nchini Tanzania kufanya uwekezaji katika sekta mbalimbali.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi wa duka la vifaa vya umeme la Hisense Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameifungua nchi na kuifanya kuwa sehemu salama ya kufanya uwekezaji.


 Amebainisha  kuwa duka la Hisense litakuwa linauza vifaa vinavyoendana na Teknolojia ya kisasa jambo ambalo litasaidia kuwa na bidhaa Bora Tanzania

“Hisense wamekuwa wakiuza bidhaa zenye ubora na gharama nafuu, wakati umefika kwa Tanzania kuchangia fursa ya kupata bidhaa zenye ubora” amesema Mpogolo.

Amesisitiza kuwa Hisense wanatambua Tanzania ni sehemu salama ya kufanya biashara kutokana mazingira mazuri tafauti na nchi nyengine

Mpogolo ameongeza kuwa watanzania wanapaswa kuja katika duka la Hisense kwa ajili ya kujifunza namna ya kutengeneza mazingira mazuri ambayo yanaweza kushawishi wateja.

“Hisense ni wafanyabiashara wazuri ambao wamekuwa wakitekeleza jukumu lao la kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa” amesema Mhe. Mpogolo.

Kwa upande wake, Mfanyabiashara Sabaha Said, amesema kuwa kuwa bidhaa za Hisense inaongoza kwa ubora na teknolojia rafiki kwa matumizi mbalimbali.

TUME YA MADINI YAAINISHA MIKAKATI YAKE*

$
0
0

 _Kuelekea kwenye utekelezaji wa Dira 2030: Madini ni Maisha na Utajiri……._ 


 _Wachimbaji wadogo wa madini  zaidi ya milioni 1.5 kuendelea kunufaika_ 



 _Kipaumbele kwa watanzania kwenye huduma na ajira kwenye migodi ya madini kutolewa_ 


 *DODOMA* 



Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Mhandisi Yahya Samamba amesema kuwa katika utekelezaji wa Dira ya 2030 yenye kueleza kuwa, “Madini ni Maisha na Utajiri, Tume imejipanga kuboresha usimamizi wa Sekta ya Madini ikiwa ni pamoja na kuendelea kutenga maeneo yaliyofanyiwa utafiti wa kijiolojia kwa wachimbaji wadogo ili uchimbaji wao uweze kuwa na tija pamoja na kuhakikisha kipaumbele kinatolewa kwa watanzania kwenye utoaji wa huduma kwenye migodi ya madini nchini.


Mhandisi Samamba ameyasema hayo leo Novemba 10, 2023 kwenye kipindi cha Goodmorning kilichorushwa mubashara na kituo cha Televisheni cha Wasafi chenye lengo la kuelezea mikakati ya Taasisi za Wizara ya Madini kwenye utekelezaji wa Dira ya 2030 yenye lengo la kuimarisha Sekta ya Madini.



Amesema kuwa utekelezaji wa Dira hii katika Sekta ya Madini inawalenga zaidi wachimbaji wadogo wa madini ambao wamekuwa wakiwekeza lakini manufaa yamekuwa si ya kuridhisha kutokana na kutokuwa na taarifa za kutosha za utafiti za madini na teknolojia duni kwenye uchimbaji wa madini.



Amefafanua kuwa Tume itaendelea kuimarisha usimamizi katika shughuli za madini kwa kutenga maeneo yenye taarifa za kijiolojia yaliyofanyiwa tafiti ili kuweza kunufaika na rasilimali hizo sambamba na kuandaa Mpango Kazi utakaolenga kusimamia maeneo ya elimu za ugani; kuboresha mfumo wa utoaji wa leseni; ukaguzi migodi na mazingira; usimamizi wa masuala ya afya na usalama mahala pa kazi pamoja na kuimarisha mifumo ya makusanyo ya maduhuli.



Akielezea mikakati iliyowekwa na Tume ya Madini kwenye utekelezaji wa Dira ya 2030, hususan kwenye ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta  ya Madini  Mhandisi Samamba amefafanua kuwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wamiliki wote wa migodi kuhusu kutoa kipaumbele kwa huduma na bidhaa zote zinazotolewa na watanzania pamoja na kuandaa namna bora ya kuingia ubia kati ya kampuni za watanzania na kampuni za nje na uwepo  wa utekelezaji wa Sheria ya Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini  pamoja na Urejeshaji wa Huduma kwa Jamii.



Ameendelea kufafanua mikakati mingine  kuwa ni pamoja na uwepo wa mfumo wa usimamizi wa ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini na kutoa elimu kwa wakandarasi wote ili kuwaandaa kushiriki katika mikataba yenye thamani kubwa kwa lengo la kuchangia ajira na kuongeza uzalishaji wa bidhaa nchini.



Hata hivyo ameeleza mikakati mingine kuwa ni pamoja na kuhakikisha kampuni za madini zinaboresha huduma za jamii kwenye vijiji vinavyozunguka migodi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu kama vile barabara, maji, vituo vya afya na shule.



Tume ya Madini ni Taasisi iliyo chini ya Wizara ya Madini ambayo iliundwa kutokana na Sheria ya Madini Sura ya 123 na ilianza utekelezaji wa majukumu yake Mwezi Aprili, 2018 kwa kutekeleza majukumu 22, ambapo jukumu kubwa ni kusimamia na kudhibiti Sekta ya Madini nchini.


TAARIFA SAHIHI ZA KIJIOLOJIA NDIYO UTAJIRI WA WATANZANIA – WAZIRI MAVUNDE

$
0
0

#Asema kupitia taarifa hizo Sekta ya Madini itafungamanisha sekta nyingine


#Asisitiza itamaliza migogoro ya Wachimbaji Wakubwa na Wadogo*


Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde amesema kuwa uwepo wa taarifa sahihi za kijiolojia za miamba ndiyo zimebeba dhana ya utajiri na maisha bora kwa Watanzania. 

Amesema hayo leo Novemba 10, 2023, jijini Dodoma, wakati akizungumza katika kipindi cha runinga na radio cha Good Morning kinachorushwa na Wasafi Media. 


Amesema kuwa dhana ya Vision 2030, Madini ni Maisha na Utajiri ni kuhakikisha Watanzania wananufaika na rasilimali madini kwa kutengeneza matajiri wengi kupitia Sekta ya Madini sambamba na kuboresha maisha ya Watanzania na kwamba hayo ni maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuona madini yanaleta maisha bora kwa Watanzania. 


Waziri Mavunde amesema ili kutimiza malengo hayo, Serikali imekuja na mkakati wa kuiongezea uwezo Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ili ifanye utafiti wa kina wa miamba yote yenye madini iliyopo hapa nchini kwa lengo la kutengeneza kanzidata ya taarifa sahihi za kijiolojia.


“Malengo yetu ni kufanya tafiti za kina kwa angalau asilimia 50 kufikia asilimia 2030, ukilinganisha na sasa ambako ni asilimia 16 pekee ndiyo imefanyiwa utafiti wa kina kwa kutumia teknolojia ya kisasa, unaweza kuona mchango mkubwa iliyonao sekta ya madini pamoja udogo wa sehemu iliyofanyiwa utafiti wa kina wa miamba, sasa tukifanya mara tatu ya hapo tutakuwa na mchango mkubwa zaidi katika uchumi sambamba Pato la Taifa kwa ujumla” amesema Mhe. Mavunde


Aidha, amesema kuwa taarifa hizo zitaenda kufungamanisha Sekta ya Madini na sekta zingine zikiwemo za Kilimo, Maji,  Afya sambamba na uchumi kwa ujumla.


“Tukizungumzia maisha, tafiti hizi zitatuonesha sehemu maji yalipo, maji safi na salama ni muhimu kwa maisha ya watu wetu, lakini pia Wizara ya Kilimo ina mkakati wa kujenga mabwawa 100 kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji na kuacha kutegemea mvua zisizotabirika pia madini ya jasi yanasaidia kuondoa tindikali kwenye ardhi kwa ajili ya kilimo, mpaka hapo unaweza kuona jinsi sekta ya madini inavyogusa maisha wa Watanzania kupitia kilimo na maji.” amesema Mhe. Mavunde. 


Amesema taarifa za tafiti hizo pia zitafungamanisha Sekta ya Afya kwa kuwa zitasaidia kujua miamba yenye gesi ya Hellium ambayo inatumika katika teknolojia ya upigaji picha za kina za anatomia (MRI), vipimo vinavyotumika hospitalini, na hivyo kuonesha jinsi sekta ya madini inavyoenda kugusa sekta ya afya.


Sambamba na hilo, Waziri Mavunde amesema kuwa uwepo wa taarifa hizo zitasaidia kuondoa  migogoro baina ya wachimbaji wakubwa na wadogo kwasababu chanzo cha migogoro hiyo ni wachimbaji wadogo kuamini madini yapo kwenye maeneo ya wachimbaji wakubwa kwa kuwa yamefanyiwa utafiti wa kina, hivyo migogoro hiyo itaisha baada ya kupata maeneo mengine yaliyofanyiwa tafiti .


“Tunataka Wachimbaji wadogo waache kuchimba kwa kubahatisha, madini sio ushirikina wala bahati ni sayansi, wachimbe kwa kuwa na uhakika kutokana na taarifa sahihi za kijiolojia, kwa kufanya hivi tutaokoa mitaji yao kwa kuwa watachimba kwa uhakika na kuuza madini wanayopata, watalipa mikopo waliyonayo, lakini pia watapata mikopo kwa kuwasilisha taarifa hizi kama dhamana katika taasisi za kifedha tofauti na sasa ambako wanalazimika kuweka dhamana nyumba, viwanja na mali zao zingine.” ameongeza Mhe. Mavunde. 


Waziri Mavunde amehitimisha wiki ya Vision 2030, Madini ni Maisha na Utajiri ambapo Wizaya ya Madini na Taasisi zake zilipata fursa ya kuelezea mikakati na utekelezaji wa dira hiyo kufikia mwaka 2030.


*VISION 2030: MADINI NI MAISHA NA UTAJIRI*

MTANZANIA ATUA RADA ZA BAYERN MUNICH

$
0
0

Na Mawndishi Wetu


Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Adelaide United ya nchini Australia Nestory Irankunda aliyezaliwa mkoani Kigoma nchini Tanzania anatajwa kujiunga na kikosi cha Bayern Munich kwa kiasi cha Euro Million 3, mazungumzo tayari yamefanyika na makubaliano yamefikiwa.



Nestory Irankunda ana umri wa miaka 17 na anavaa jezi namba 66 kwenye klabu ya Adelaide United, amejiunga na kikosi hicho tangu mwaka 2021 akitokea Adelaide United alipotumika tangu 2018-2020.


2021 aliitumikia klabu ya Adelaide United NPL akacheza michezo 30 akafanikiwa kufunga magoli sita (6), 2022 aliichezea Adelaide United michezo 38 akifunga magoli tisa (9).


Nestory tayari ameitumikia timu ya Taifa ya Australia chini ya miaka 17, amecheza michezo 7 na amefunga magoli 11.

NEC KUFANYA UBORESHAJI WA MAJARIBIO DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

$
0
0

 


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Ramadhani Kailima akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uboreshaji wa majaribio wa Daftari La Kudumu la Wapiga Kura.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa yua Uchaguzi, Ramadhan Kailima (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura na Tehama, Geofrey Mpangala (kulia) wakionesha BVR Kits zenye vifaa mbalimbali vinavyowasiliana ili kuchukua na kutunza taarifa za wapiga kura.

Na Mwandishi wetu, Dodoma.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kufanya zoezi la uboreshajia wa majaribio wa daftari la kudumu la wapiga kura katika Kata ya Ng’ambo iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Mkoa wa Tabora na Kata ya Ikoma iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Mkoa wa Mara kuanzia tarehe 24 hadi 30 Novemba, 2023.

Akitangaza uboreshaji huo leo Novemba 10,2023 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Ramadhani Kailima amesema zoezi hilo litafanyika katika vituo 16 vya kuandikisha wapiga kura kati ya hivyo vituo 10 ni katika kata ya Ng'ambo na 6 vipo kata ya Ikoma.

“Uboreshaji wa majaribio utahusisha kuandikisha raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 au zaidi na atakayetimiza umri wa miaka 18 kabla au ifikapo tarehe ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 , wapiga kura wanaoboresha taarifa zao ambao wamehama kutoka eneo moja la uchaguzi kwenda eneo jingine, wapiga kura waliopoteza sifa za kuwemo daftarini,”amesema Bw. Kailima.

Kailima amesema lengo la kufanya majaribio hayo ni kupima uwezo wa vifaa na mifumo ya uandikishaji itakayotumika wakati wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura unaotarajiwa kufanyika nchi nzima kwa tarehe na ratiba itakayopangwa na tume.

“Katika zoezi hili tume itatumia BVR Kits zenye vifaa mbalimbali vinavyowasiliana ili kuchukua na kutunza taarifa za wapiga kura, BVR Kits hizo zimeboreshwa na ni tofauti na zile zilizotumika katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura mwaka 2015 na 2019,”amesema Kailima.

Aidha, Kailima amesema Tume imesanifu na kuboresha mfumo wa uandikishaji wa Wapiga Kura (Voters Registration System-VRS) ili kukidhi muundo na BVR Kits za sasa ambazo zinatumia programu ya android tofauti na BVR Kits za awali ambazo zilikuwa zinatumia programu ya Microsoft Windows.

“Mfumo wa uandikishaji ulioboreshwa utawawezesha wapiga kura ambao wameshaandikishwa na wapo kwenye daftari la wapiga kura, kuanzisha mchakato wa kuboresha taarifa zao ama kwa kubadilisha kituo cha kupigia kura iwapo amehama Mkoa au Wilaya nyingine au kurekebisha taarifa zao kwa njia ya mtandao kwa kutumia simu zao za mkononi au kompyuta,”amesema Kailima.

Amesema kuanzisha mchakato mtandaoni, mpiga kura ataingia kwenye tovuti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi www.nec.go.tz kwa kutumia kompyuta au simu janja kisha atabonyeza kiunganishi (link) kilichoandikwa “Boresha Taarifa za Mpiga Kura” au atatumia anuani ya ovrs.nec.go.tz itakayompeleka moja kwa moja kuanzisha mchakato. Baada ya kufuata utaratibu huo, mfumo utamletea ukurasa wenye vipengele vitakavyomruhusu kuweka taarifa zake kulingana na mahitaji.

“Baada ya kukamilisha taratibu zote na kuwasilisha taarifa kwenye mfumo, mpiga kura atapokea ujumbe mfupi wenye kumbukumbu namba kupitia namba yake ya simu aliyoitumia wakati wa kuboresha taarifa zake kwenye mtandao. Kumbukumbu namba hiyo atakwenda nayo kwenye kituo cha kuandikisha wapiga kura kwa ajili ya kumalizia hatua zilizobaki na kupatiwa kadi,”amesema Kailima.

Katika hatua nyingine Bw.Kailima amesema kuwa uboreshaji huo utahusisha vyama vya siasa kwa kuweka wakala mmoja katika kila kituo cha kuandikisha wapiga kura lengo likiwa ni kushuhudia na kujiridhisha kuhusu taratibu zitakazotumika wakati wa uboreshaji wa majaribio wa daftari.

Amesema utaratibu huo wa uboreshaji wa taarifa kwa njia ya mtandao hautawahusisha wapiga kura wapya wanaotaka kuandikishwa kwa mara ya kwanza na waliopoteza kadi zao au kuharibika.

“Hawa wanashauriwa wafike kwenye kituo cha kuandikisha wapiga kura na kufuata taratibu watakazo elekezwa na maafisa wa Tume watakaokuwepo kwenye kituo,”amesema.

Pia, Kailima amesema Tume inatoa wito kwa wananchi wenye sifa zilizotajwa wa Kata ya Ng’ambo iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora na Kata ya Ikoma iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uboreshaji wa majaribio wa Daftari na kutoa ushirikiano kwa Tume wakati wote wa utekelezaji wa jukumu hili muhimu kwa mustakabali wa Taifa.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa yua Uchaguzi, Ramadhan Kailima wakionesha BVR itakayotumika katika uboreshaji huo wa Majaribio.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa yua Uchaguzi, Ramadhan Kailima (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura na Tehama, Geofrey Mpangala (wapili kushoto) wakionesha BVR Kits zenye vifaa mbalimbali vinavyowasiliana ili kuchukua na kutunza taarifa za wapiga kura.
Muonekano wa Mfumo wa uboreshaji wa Taarifa Mtandaoni utakao kuwa katika Tovututi na kutumika kuanzisha mchakato mtandaoni, ambapo mpiga kura ataingia kwenye tovuti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi www.nec.go.tz kwa kutumia kompyuta au simu janja kisha atabonyeza kiunganishi (link) kilichoandikwa “Boresha Taarifa za Mpiga Kura” au atatumia anuani ya ovrs.nec.go.tz itakayompeleka moja kwa moja kuanzisha mchakato. Baada ya kufuata utaratibu huo, mfumo utamletea ukurasa wenye vipengele vitakavyomruhusu kuweka taarifa zake kulingana na mahitaji.


Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari wakifuatilia taarifa ya Mkurugenzi wa Uchaguzi.

Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Bi. Giveness Aswile akizungumza jambo.

Baadhhi ya Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi wa Idara mbalimbali za Tume wakiwa katika Mkutano huo na Wanaandishi wa Habari.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Ramadhani Kailima akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uboreshaji wa majaribio wa Daftari La Kudumu la Wapiga Kura.
Baadhhi ya Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi wa Idara mbalimbali za Tume wakiwa katika Mkutano huo na Wanaandishi wa Habari.



Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari wakifuatilia taarifa ya Mkurugenzi wa Uchaguzi.

DC MSOFE AKEMEA VIONGOZI WANAOINGILIANA KI MAJUKUMU

$
0
0

Na Lydia Lugakila

Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Zaitun Msofe amekemea vikali tabia ya baadhi ya viongozi wanaoingilia majukumu ya watendaji kuanzia ngazi ya kijiji na kusababisha kushindwa kutimiza majukumu yao kwa ufanisi na kwa wakati.

Msofe ametoa kauli wakati akitoa maelekezo ya serikali katika kikao cha Baraza la Madiwani kwa robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 katika Halmshauri ya wilaya ya Kyerwa likichofanyika Novemba 10, 2023 katika ukumbi wa Rweru Plaza ulioko katika Wilaya humo.

 Mkuu wa Wilaya hiyo amesema kila mmoja anapaswa kubaki katika misingi ya kazi yake na sio kuingilia majukumu ya mtu yoyote ili kuepusha migogoro katika utendaji kazi.

Msofe amesema kuwa ni jukumu la watendaji wote kuanzia ngazi ngazi ya kijiji kufanya kazi kwa kuzingatia sheria kanuni taratibu na miongozo iliyopo.

"Tusifanye kazi kwa kufuata utashi wetu, wala utashi wa mtu mwingine wala Viongozi tuache kuingilia majukumu ya watendaji ambayo yako kisheria,"alisema Msofe.

Pia Mkuu huyo wa Wilaya amemuagiza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kyerwa pamoja na madiwani kuhakikisha wanatumia wakaguzi wa ndani ili kupata dondoo mapema na kuzifanyia marekebisho haraka kabla ya ukaguzi wa nje kukuta hoja za kujibu.


DKT. BITEKO AZINDUA KITUO CHA KISASA CHA KUJAZIA GESI ASILIA KWENYE MAGARI (CNG)

$
0
0

                 Serikali kuwapa ushirikiano wawekezaji

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha kwanza cha kisasa cha kujazia gesi asilia kwenye magari na karakana ya kuweka mfumo wa gesi asilia ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa mipango ya Serikali kuchochea matumizi ya gesi asilia kama nishati safi na salama kwa mazingira jijini Dar es Salaam.

 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo amezindua kituo cha kwanza cha kisasa cha kujazia gesi asilia kwenye magari na karakana ya kuweka mfumo wa gesi asilia ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa mipango ya Serikali kuchochea matumizi ya gesi asilia kama nishati safi na salama kwa mazingira.

Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam tarehe 11 Novemba, 2023 na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, Balozi Sherif Ismail wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Balozi Isaac Njenga wa Jamhuri ya Kenya, Balozi Fred Mwesigye wa Jamhuri ya Uganda, Mha. Felchesmi Mramba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya TAQA, Pakin Kafafy.

Dkt. Biteko amesema kuwa, kujengwa kwa kituo hicho na TAQA Arabia na washirika wao JCG Oil & Gas niutekelezaji wa maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa na maono ya kuleta wawekezaji nchini wakiwemo wanaowekeza kwenye Sekta ya Nishati, hivyo ameahidi kuwa Wizara itafanyia maelekezo yake ili kutekeleza maono yake.

Dkt. Biteko amesema kuwa, Serikali inaweka msukumo mkubwa kwenye matumizi ya gesi ya asilia yakiwemo magari, mitambo ya viwandani, hivyo kuzinduliwa kwa kituo hicho ni kuonesha azma ya Serikali ya kuhakikisha kuwa Gesi inayopatikana Tanzania inatumika ndani ya nchi kwanza.

Amesema kituo hicho kitajaza gesi kwenye magari 800 kwa siku na kina pampu sita zitakazojaza gesi kwenye magari sita kwa maramoja ambapo ujazaji wa gari moja utakuwa ni wa dakika tatu hivyo hicho ni kituo kikubwa kitakachosaidia kubadilisha magari na kufanya yatumie gesi badala ya mafuta pekee.

Amesema Kampuni hiyo inatarajia kujenga vituo 12 vya CNG jijini Dar es Salaam ili kuwa na vituo vingi zaidi vya kujazia gesi kwenye magari.

Ameongeza kuwa, kampuni hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wapo kwenye majadiliano ili kujenga vituo vidogo vya Gesi ya Kusindika (LNG) ili kuweza kutoa Gesi jijini Dar es Salaam na kupeleka kwenye mikoa mbalimbali ili nayo iweze kujaza gesi hiyo kwenye magari..

Amesema kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono katika uwekezaji wao ili kuchochea ukuaji wa nishati nchini.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Edward Mpogolo ameishukuru Wizara ya Nishati kwa kutekeleza maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya usambazaji nishati katika maeneo yote ikiwemo gesi asilia.

Amesema kuwa Wilaya ya Ilala, inaona faraja kufunguliwa kwa kituo wilayani humo kutokana na kuwa kitovu cha Mkoa wa Dar es Salaam kwani Wilaya hiyo ina wananchi wasiopungua milioni 1.6 ukilinganisha na idadi yote ya wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao jumla yao ni milioni 5.3.

Mbinu za kuondoa tatizo la watu kujiua Karagwe kuanza kutumika

$
0
0

 Na Lydia Lugakila, KARAGWE


Baraza la madiwani Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera limesema kutokana na wimbi kubwa la watu kujiua Wilayani humu unapaswa kuandaliwa utaratibu na mbinu kutoka kwa wataalamu kuanza kutoa ushauri nasaha kwa jamii ili kuondoa changamoto hiyo kwani inapunguza nguvu kazi ya Taifa.


Kauli hiyo imekuja baada ya Madiwani hao kutoa taarifa za kata na kata nyingi kuonesha wimbi kubwa la wananchi kujinyonga na kunywa sumu.


Akieleza hayo Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Wallesi Mashanda amesema inabidi kamati ya Ulinzi na usalama pamoja na idara ya ustawi wa jamii zifanye utafiti kujua nini chanzo cha Wananchi kujiua na utakapobaini ianze kutoa elimu kwa wananchi ili kuondoa changamoto hiyo.


Kupitia kikao hicho Mashanda amesema inabidi wananchi wajue umuhimu wao kuishi na kushiriki katika shughuli za maendeleo katika Taifa lao na sio kujikatisha uhai wa kuishi.

Namanga Jogging Club yawakutanisha wadau wa michezo

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Micky Commercial Company (LTD) Michael Juma, akizungumza katika Bonanza la Namanga Jogging, lililofanyika katika Uwanja wa Namanga jijini Dar es Salaam leo Novemba 12, 2023 na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa michezo.
Meneja wa Miradi Charles Juma, akizungumza katika Bonanza la Namanga Jogging, lililofanyika katika Uwanja wa Namanga jijini Dar es Salaam leo.


ACT WAZALENDO KUICHAMBUA MISWADA YA UCHAGUZI

$
0
0

Chama cha ACT Wazalendo kimeielekeza Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho kuichambua Miswada ya Sheria kuhusu Uchaguzi, Tume ya Uchaguzi na Vyama vya Siasa iliyosomwa kwa mara ya kwanza Bungeni tarehe 10 Novemba 2023.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo kwenye Mkutano Mkuu wa Jimbo la Ilala uliofanyika leo tarehe 12 Novemba 2023 katika Ukumbi wa Simple Motel, Ilala, Dar es salaam.

"Ni jambo la faraja kuwa hatimaye miswada hii imewasilishwa Bungeni. Yapo masuala yaliyotufurahisha kama vile kuondosha suala la kupita bila kupingwa. Lakini, yapo masuala yanayohitaji maboresho ili kuhakikisha chaguzi zijazo zinakuwa huru, za haki na kuaminika. Chama chetu kitafanya uchambuzi wa kina wa miswada yote mitatu. Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Chama imeagizwa kufanya uchambuzi huo ambao utawasilishwa kwenye vikao vya Chama kabla ya kuwasilishwa Bungeni" alisema Ado Shaibu.

"Tunapenda pia kurudia rai yetu kuwa itakuwa ni jambo la ajabu kwamba Tume ya Uchaguzi itayoundwa isisimamie Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. ACT Wazalendo hatuungi mkono uchaguzi wa Serikali za Mitaa kusimamiwa na TAMISEMI" alisisitiza Ndugu Ado.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa ACT Wazalendo inaongozwa na Wakili Omar Said Shaaban ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar akisaidiwa na jopo la Mawakili wa Chama.

Mbali na hayo, Katibu Mkuu Ndugu Ado Shaibu amesema kuwa Chama cha ACT Wazalendo kinaendelea na chaguzi katika ngazi ya majimbo akiweka bayana kuwa Ilala inakuwa Jimbo la 80 kukamilisha Uchaguzi.

"Mwezi Machi 2024, ni mwaka wa kukamilisha uchaguzi wa Chama ngazi ya Taifa. Hadi kufikia mwisho wa mwezi Desemba 2023, majimbo yote 264 yatakuwa yamekamilisha chaguzi zake. Baada ya hapo tutafanya chaguzi za Mikoa na mwishowe chaguzi za Taifa Mwezi Machi mwishoni" alihitimisha Ndugu Ado.

Imetolewa na Janeth Joel Rithe, Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, ACT Wazalendo.

12 Novemba 2023.


NMB yaazimia kushirikiana kimkakati na wanasheria

$
0
0
Waziri wa Sheria na Katiba, Balozi Dk. Pindi Chana (kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (katikati) Waziri wa Viwanda na Biashara wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Omary Said Shabaan (kulia), wakijadiliana jambo wakati wa hafla maalum iliyoandaliwa na Benki ya NMB iliyoikutanisha benki hiyo na Taasisi za Sheria Mkoa wa Dar es Salaam, ikiwa ni muendelezo wa ushirikiano baina ya pande hizo mbili. (Na Mpiga Picha Wetu).

Waziri wa Sheria na Katiba, Balozi Dk. Pindi Chana (katikati), akiwa ameshikana mikono na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Omary Said Shabaan (wa pili kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (wa pili kushoto), wakati wa hafla maalum iliyoandaliwa na Benki ya NMB iliyoikutanisha benki hiyo na Taasisi za Sheria Mkoa wa Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara Benki ya NMB, Filbert Mponzi na kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper. (Na Mpiga Picha Wetu).

 

Na Mwandishi Wetu

 

Benki ya NMB imeazimia kuwa na ushirikiano wa kimkakati na taasisi za kisheria nchini kutokana na umuhimu wa tasnia ya sheria katika maisha ya binadamu na maendeleo kwa ujumla.

 

Azma hiyo ilibainishwa rasmi mwishoni mwa wiki jana jijini Dar es Salaam kwenye mkutano maalumu wa kwanza kati ya benki hiyo na wanasheria binafsi.

 

Akizungumza katika hafla hiyo iliyoaandaliwa kwa ajili ya wanasheria wa Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi Ruth Zaipuna, alisema mikutano kama hiyo ya kujengana na kubadilishana uzoefu itafanyika nchi nzima na itakuwa endelevu.

 

“Lengo la mikutano hii ni kujenga na kudumisha mahusiano mazuri kati ya Benki ya NMB na wadau wa sheria na wanasheria binafsi nchini,” kiongozi huyo alisema na kusisitiza kuwa Taaluma ya Sheria ni miongoni mwa taalumu muhimu katika ujenzi wa taifa.

 

“Sheria ina mchango mkubwa sana kwenye maisha ya kila siku ya mwanadamu, na hivyo basi ni taaluma ambayo kwa pamoja inatupasa kuilinda, na kuikuza,” aliongeza.

 

Aidha, Bi Zaipuna aliwaambia waliohudhuria hadhara hiyo kuwa sekta ya sheria pia ina mchango mkubwa katika ukuaji wa biashara na uchumi wa taifa kwa ujumla.

 

Hiyo ni kupitia sheria, sera na kanuni bora za uwekezaji, umiliki wa vyanzo vya uzalishaji na utendaji wa kibiashiara vitu ambavyo ni moja ya misingi imara ya uchumi wa kiushindani na unaojitegemea.

 

Katika muktadha huo, Bi Zaipuna aliishukuru Serikali kwa mageuzi chanya inayoendelea kuyafanya kuweka mazingira wezeshi ya kibiashara nchini ambayo yameifanya Tanzania kuorodheshwa kama nchi bora zaidi kwa vigezo vya uwekezaji katika ukanda wa Afrika Mashariki.

 

Mazingira hayo pamoja na mchango wa tasnia ya sheria yameiimarisha sekta ya kibenki nchini na kuifanya NMB kuwa na ufanisi mkubwa kihuduma na kiutendaji.

 

“Tasnia ya sheria imeendelea kuwa na mchango mkubwa na muhimu sana katika sekta ya kibenki. NMB, tukiwa miongoni mwa taasisi kubwa zaidi za kifedha nchini Tanzania, tumekuwa bega kwa bega na taasisi za kisheria tukishirikiana kwenye masuala mbalimbali ya kibiashara.”

 

Bi Zaipuna alibainisha kuwa ushirikiano huo pamoja na mabadiliko makubwa ya kuitendaji iliyopitia NMB na uwekezaji katika mifumo, rasilimali watu na utawala bora, vimeiwezesha taasisi hiyo kuwa benki kubwa, imara na bora nchini.

 

Kwa sasa, NMB inayoongoza kwa faida nchini, inalihudumia taifa kupitia matawi zaidi ya 230, mawakala 24,000 na masuluhisho ya kidigitali kama NMB Mkononi.

 

Mgeni rasmi wa shughuli hiyo, Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Pindi Chana, aliipongeza benki hiyo kwa mtandao huo mpana ambao alisema umesaidia sana kupatikana kwa huduma za kifedha hata katika maeneo ya pembezoni mwa nchi.

 

Waziri huyo alisema wazo la kukutana na kushirikiana kwa karibu na wanasheria ni ubunifu mkubwa unaostahili kuingwa na taasisi nyingine.

 

“Ushirikiano huu ni muhimu sana kwa maslahi mapana ya taifa hususani katika kuwahudumia wawekezaji ambao wanazidi kuongezeka kutokana na juhudi zinazofanywa na Serikali chini ya uongozi imara wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan,” Dkt Chana alisisitiza.

 

Mkutano huo ulihudhuliwa pia na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Zanzibar, Bw Omar Said Shaaban, aliyesema mikutano ya aina hiyo pamoja na mada zilizotolewa na wataalamu kutoka TRA, Brela, Tume ya Madini na Kituo cha Uwekezaji Tanzania zitasaidia kuwajenga wanasheria kiutendaji.

 



 

WAWEZESHAJI WA KITAIFA WA MAFUNZO YA MTAALA MPYA WAPASWA KUZINGATIA MAFUNZO KWA UMAKINI.

$
0
0

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Tecknolojia, Dkt. Franklin Rwezimula amewataka wawezeshaji  kitaifa  wa mtaala wa Elimu ya Awali nchini kuzingatia mafunzo kwa umakini ili kuwawezesha walimu kutekeleza mtaala huo  kwa weledi, kwani mtaala unaotarajia kuanza mwaka 2024  kwa ngazi ya elimu ya awali na msingi.

Ameyasema hayo leo tarehe 13/11/2023 alipofungua mafunzo  kwa wawezeshaji  hao ambao watakwenda kutoa mafunzo kwa walimu  wengine nchini katika kutekeleza mtaala mpya.

“ Ili mitaala itekelezwe kwa ufanisi ni lazima kuwe na walimu wenye  weledi katika ufundishaji, naomba sana wawezeshaji mzingatie haya mafunzo mnayopatiwa hapa  ili muweze kuifanya kazi yenu ya uwezeshaji vyema” amesema, Dkt. Rwezimula.

Ameongeza kwa kusema kuwa Wizara inaendelea  na  mikakati mbalimbali ya kuboresha mafunzo  endelevu kazini ili kuhakikisha walimu wanakuwa bora katika maeneo yao ya kazi. ikiwemo uboreshaji wa mazingira ya kazi kwa kuboresha miundombinu na vifaa vya kujifunzia na kufundishia vikiwemo vifaa vya TEHAMA.

Katika hatua nyingine, Dkt. Rwezimula ameipongeza TET kwa usimamizi mzuri wa mitaala huku akioongeza kuwa  mabadiliko ya mtaala yaliyofanyika  yataanzia katika ngazi ya Darasa Awali, darasa la kwanza na darasa la tatu; kwa kuanzia na kusema serikali imejipanga katika kuhakikisha mtaala huo unatekelezwa  vyema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba amesema kuwa Mitaala imefanyiwa maboresho   ambayo  ni  makubwa  na  ya sita tangu nchi yetu ipate uhuru.
 

"Tumeboresha muundo wa elimu na sasa elimu ya awali itatolewa kwa muda wa mwaka mmoja kwa watoto wenye umri wa miaka mitano  ambapo elimu ya awali itatanguliwa na elimu ya malezi na makuzi itakayotolewa kwa miaka miwili kwa watoto wenye umri wa miaka mitatu mpaka minne, elimu hii itasimamiwa na wizara inayosimamia ustawi wa watoto ambayo kwa sasa ni wizara ya maendeleo ya jamii jinsia ,wanawake na makundi maalumu “amesema Dkt. Komba.

Ameongeza kwa kusema kuwa  yapo maboresho yaliyofanywa kwenye maeneo ya ujifunzaji ambapo kwa sasa mtaala una maeneo makuu matano ambayo ni 1. Utamaduni, elimu ya imani, sanaa na michezo.  2. Lugha na mawasiliano 3. Stadi za awali za maisha. 4 Afya na mazingira 5.Stadi za awali za kihisabati, kisayansi na TEHAMA.

Mafunzo hayo yatafanyika katika maeneo mbalimbali , ambapo awamu ya kwanza yameanza kufanyika Mkoani Iringa  na baadae kufanyika katika mikoa ya Mwanza na Dar es salaam, ambapo yanaratibiwa na TET kupitia mradi wa GPE LANES II ambao utahusisha waratibu wawezeshaji wa kitaifa ambao watapeleka ujuzi wao kwa walimu wengine nchi nzima.



FUKUTO LA JOTO MSIMBAZI LAMUIBUA AMBAGILE

$
0
0

Na John Marwa

Wakati Fukuto likiwe limetanda mitaa ya Msimbazi Mchambuzi wa Michezo nchini kutoka Wasafi FM George Ambagile amesema kufanya kazi Simba ama Yanga lazima kuwe na presha, hivyo ni wa kuwapima ukomavu viongozi wa Simba.


Kinachoendelea Unyamani ni baada ya kupokea kipondo kutoka kwa mtani wake Yanga SC cha mabao (1-5) mchezo ulipigwa Novemba 5 katika Dimba la Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

"Binafsi yangu sidhani kama inawezekana kufanya kazi Simba au Yanga bila presha ya mashabiki. Yani kama hutaki kupata presha kwa mashabiki basi kafanye kazi kwenye klabu tofauti na hizi klabu mbili."


"Na sio kwa Tanzania tu, kwa nchi yeyote ukienda kisha ukaambiwa hii ni klabu kubwa hapa nchini basi tegemea presha kubwa kutoka kwa mashabiki, yani ikishakuwa klabu kubwa basi ni klabu yenye mashabiki, mashabiki wenye mitazamo tofauti. Kama hautaki presha kubwa basi tafuta klabu ndogo, huko utafanya kazi miguu ikiwa juu."


"Na hiki ndicho kipindi hawa viongozi tunajua kwa kiasi gani wana utimamu wa akili, kuendana na presha ya mashabiki kipindi hiki ndicho kipindi cha kujua ubora na utimamu wa kiongozi.

Kiukweli sio kipindi rahisi na sitamani hata kuvivaa viatu vya viongozi wa Simba sababu ni kipindi kigumu mno." Amesema mchambuzi wa soka George Ambangile.


Kamati ya Bunge yaridhishwa na mradi wa uboreshaji usalama wa milki ardhi vijijini

$
0
0

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeridhishwa na utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi katika vijiji vya Mwadila, Zabazaba na Igongwa katika halmashauri ya wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.


Akieleza mbele ya wakazi wa vijiji hivyo Mwenyekiti wa Kamati ya ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe. Timotheo Mzava wakati wa Ziara ya kamati hiyo wilayani humo amesema ni jambo la kuipongeza Wizara ya Ardhi katika kuwezesha mradi huo kuweka mazigira mazuri ya matumizi bora ya ardhi.


Amesema kuwa kazi ya kamati hiyo ambayo wamekuja kuifanya ni kufuatilia na kujiridhisha fedha zilizotolewa na Rais Dkt Samia Suluhu baada ya kupitishwa na bunge ili kutekeleza mradi huo zilizotengwa kwa wilaya ya Maswa zimefika na zimefanya kazi iliyokusudiwa.



Amesema kuwa kulingana na maelezo waliyoyapata kutoka kwa watekelezaji wa mradi huo pamoja na wananchi wa vijiji hivyo sambamba na kuonyesha ramani zilizotengwa kwa ajili ya kuonyesha matumizi bora ya ardhi kwa pamoja wamejiridhisha kuwa kazi imefanyika vizuri.


Amesema kwa kuwa mradi huo  unatekelezwa na serikali kwa kupitia wizara ya ardhi na wananchi wameshirikishwa ni mradi mzuri ambao unafaida nyingi zikiwemo kuondoa tatizo la migogoro ya mipaka katika ya Kijiji na Kijiji, mipaka ya mashamba sambamba na kuongeza thamani ya Ardhi.


Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi mhe. Geophrey Pinda amesema  kuwa wilaya hiyo inakwenda kupima vijiji vyote 120 kwa mchanganuo kuwa vijiji 106 vitapimwa, Vijiji 5 vitaingizwa katika mji wa Maswa na vijiji 9 vitapewa hadhi ya kuwa miji midogo na wananchi watapatiwa Hati Milki za Ardhi.


Amesema kuwa mradi huo utakuwa endelevu na moja ya  umuhimu wa kupima miji ni kuweka matumizi bora ya ardhi na kuondoa changamoto zilizokuwa zinajitokeza za migogoro ya ardhi ya mara kwa mara.


Amesema Wizara yake imeweza kutenga Hekta 77,000 kwa ajili ya kilimo cha Umwagiliaji, Hekta 481 kwa ajili ya taasisi za serikali na Hekta 713 kwa ajili ya kuweka Viwanda na Uwekezaji.

Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>