Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

KUMEKUCHA LADIES FIRST DAR

$
0
0

 


Katibu Mtendaji BMT, Neema Msitha, akizungumza kuelekea mashindano ya Ladies First. Wengine kutoka kushoto ni Katibu wa ZAAA Muhidin Masunzu, Mwakilishi Mkuu JICA Tanzania Naofumi Yamamura na Mwasisi wa mashindano hayo, Kanali mstaafu Juma Ikangaa.



NA TULLO CHAMBO


WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dr. Dorothy Gwajima, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Mashindano Maalum ya Riadha ya Wanawake maarufu kama 'Ladies First' yanayotarajiwa kurindima kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa January 21 na 22 jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha, alisema mashindano hayo yamendaliwa na BMT, Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), na kuwezeshwa na Shirika la Maendeleo la Japan ( JICA), na huu ni msimu wake wa nne,  yakiwa na lengo la kuwahamasisha wanawake kushiriki katika mchezo wa Riadha.


"Lengo la mashindano haya ni kuwahasisha  watoto wa kike kushiriki katika michezo hususan Riadha, kutoa fursa ya wanariadha wa like kuonyesha vipaji vyao na kuendeleza vipaji vya wanariadha ambao watawakilisha nchi katika mashindano ya kitaifa na kimataifa siku zijazo," alisema Msitha.


Alisema mashindano ya mwaka huu, yatashirikisha wanariadha 186 kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani yakishirikisha mbio za Mira 100, 200, 400, 800, 1500, 5000, 10000, Kupokezana Vijiti 4x400 na Kurusha Mkuki na kushuhudiwa na watazamaji mbalimbali wakiwemo wanafunzi 1000 kutoka shule za Msingi na Sekondari za Manispaa ya Temeke.


"BMT inaishukuru Sana JICA na kampuni za Kijapan zinazofanya shughuli zake hapa nchini kwa kufadhili mashindano haya kwa mara ya  nne, pia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kutoa uwanja ambao utatumika kwa mshindano na ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke ambayo imetoa ruhusa kwa wanafunzi kushiriki na kujifunza katika mashindano haya," alisema Msitha na kuongeza.


Baraza linaendelea kusisitiza Kamati za Michezo za Mikoa, kuhakikisha zunawezesha ushiriki wa wanaridha wa mikoa yao katika mashindano haya na kuwaomba wananchi wote wa Jiji la Dar es Salaam  kujitokeza kwa wingi siku ya Jumamosi na Jumapili kushuhudia mashindano hayo ambapo hakuna kiingilio.


Kwa upande wake, Mwakilishi Mkuu wa JICA Tanzania, Naofumi Yamura, alisema wanajivunia kuanza kutoa ushirikiano kwa Tanzania toka mwaka 1962 na mashindano ya mwaka huu watayatumia kama maadhimisho ya miaka 60 ya ushirikiano wao na Tanzania.


Yamura, alisema mashindano ya mwaka huu yatahudhuriwa na watu mbalimbali maarufu akiwemo Balozi wa Japan Tanzania, viongozi kutoka Sudan ya Kusini, Mwanariadha nguli Kanali mstaafu Juma Ikangaa na mwanariadha anayewika hivi sasa Alphonce Simbu.


Naye Katibu wa Chama cha Riadha Zanzibar (ZAAA), Muhidin Masunzu akimwakilisha Kaimu Katibu Mkuu wa RT, Wakili Jackson Ndaweka, alisema wamejiandaa vema kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa ufanisi.


Wazo la kuanzishwa mashindano hayo liliasisiwa na Kanali Ikangaa, ambaye pia no Balozi wa Hiari wa JICA, likitokana na kuenzi historia ambapo medali ya kwanza Tanzania kimataifa ililetwa na Mwanamama Thereza Dismas, aliyekuwa akirusha Mkuki. 


Mabadiliko sheria za habari Zanzibar wadau watakiwa kuongeza juhudi kupigania mabadiliko

$
0
0


Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt. Mzuri Issa akizungumza na waadishi wa habari vyombo tofauti kutoka Unguja na Pemba wakati wa uwasilishaji wa ripoti maalumu iliogusia changamoto katika utekelezaji wa tasnia ya habari.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifanya mazoezi ya viungo kabla ya kuendelea na mkutano huo.


Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA-ZNZ) kimesema licha ya juhudi kubwa zinazochukuliwa  na wadau wa habari katika kupigania  mabadiliko ya sheria mbalimbali bado kunaonekana kugumu.


Kauli hiyo imetolewa huko Tunguu Zanzibar nje kidogo ya mji wa Unguja na Maneja uchechemuzi Tamwa Zanzibar ambaye pia ni afisa mdhamini baraza la habari la Tanzania upande wa Zanzibar Shiffa Said Hassan wakati akizungumza na waandishi katika mkutano wa kuwasilisha ripoti ya sheria za habari Zanzibar zilizofanyiwa mapitio na TAMWA ZNZ kwa kushirikiana na Shirika la INTERNEWS Tanzania ambazo zinakinza uhuru wa habari pamoja na uhuru wa kujieleza


“Sisi kama wadau tumeshatoa mapendekezo yetu ya kuhitaji mabadiliko ya sheria mbalimbali za habari ikiwemo Sheria ya tume ya utangazaji ya Zanzibar namba 7 ya mwaka 1997 na tunaendelea kufanya ushawishi ili tuweze kupata sharia bora zitakazotoa nafasi kwa wandishi na vyombo vya habari kutekeleza majukumu yake kwa uhuru,” ’Shifaa Said Hassan,.


Mkurugenzi wa Chama hicho Zanzibar, Dkt. Mzuri Issa akifungua mkutano huo alisema kuna haja ya taasisi husika za mabadiliko ya sheria kuweka kipaumbele kufanyiwa marekebisho yanayoendana na matakwa ya wadau katika sheria za habari Zanzibar ili zitoe mazingira ya uwepo wa uhuru wa vyombo vya habari katika kutekeleza majukumu yao.

 


Alisema uhuru wa habari ni nguzo muhimu inayoweza kusaidia kwa kiasi kikubwa ukuzaji wa maendeleo kwenye taifa loloote Ulimwenguni hivyo inapotokea sheria ya tasnia hiyo kubanwa ni sawa na kuchelewesha maendeleo ambayo yanahitajika na kila mtu.

 

“Bila ya uhuru wa habari na kujieleza itakuwa ngumu nchi yoyote kupata maendeleo, hivyo wakati wa kuzifanyia mabadiliko Sheria za habari umefika ili na sisi  nchi yetu ipege hatua” alieleza Dr Mzuri

 

Akitolea mfano changamoto za sheria hiyo alisema ni pamoja na Sheria namba nane, (27) (i) ya Wakala wa Habari Magazeti na Vitabu ambacho kinaeleza afisa yoyote wa Jeshi la Polisi anaweza kuzuia au kukamata gazeti lolote lile lisichapishwe iwapo atashuku linakwenda kinyume jambo ambalo linakwenda kinyume na mikataba ya kimataifa kuhusu uhuru wa kujieleza.


 “Tuna kila sababu ya kuona kwamba Sheria zetu, Sera na matendo yaendane na mikataba ya kimataifa kuhusu uhuru wa habari ili iweze kuleta maslahi kwa makundi yote,” alieleza Dkt. Mzuri Issa.

 

Aliongeza “tumepitia sheria kumi za habari na katika kufanya mapitio hayo tunasukumwa zaidi na mambo matatu. kama Zanzibar na Tanzania tunapaswa kwendana na mikataba ya kimataifa.”

 

 Wakichangia katika mkutano huo baadhi ya wanahabari walisema kuwa ni muda sasa ya wanahabari kujifunga kibwebwe hadi sheria ambazo haziendani na wakati ziondolewe.

“Lazima tupambane ili sheria zifanyikiwe kwani bila sheria hizo kubadilishwa hakuna heshima kwa waandishi wa habari hapa nchini” alisema Mwandishi Msomi Jabir Idirsa.

NATALIA, SULLE KUSHIRIKI CROSS COUNTRY KENYA

$
0
0

WANARIADHA wawili wa Tanzania, Natalia Elisante na Herman Sulle, wanatarajia kushiriki Mashindano ya Taifa ya Mbio za Nyika Kenya 'Kenya National Cross Country' kwa upande wa Senior.


Mashindano hayo, yanatarajiwa kufanyika jijini Nairobi Januari 21, kwenye viwanja vya Chuo cha Magereza Ruiru.


Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Wakili Jackson Ndaweka, wanariadha hao, wamepata hiyo baada ya RT kupokea mwaliko kutoka kwa wenzao wa Kenya (AK).


Katika mashindano hayo, mshindi wa kwanza atajipatia Dola 1000 za Marekani zaidi ya Sh. Milioni 2 za Tanzania.


Mshindi wa pili Dola 800 huku wa tatu akiondoka na dola 700 ambapo hadi mshindi wa 12 atapata zawadi ya fedha.


Nchi mbalimbali ikiwamo Tanzania, hivi sasa zinajiandaa na mashindano ya Nyika ya Dunia yanayotarajiwa kufanyika nchini Australia February 18 mwaka huu.


Timu ya Tanzania, inatarajiwa kuingia kambini Februari Mosi jijini Arusha.

TFS MANYONI WATAKIWA KUHAMASISHA WANANCHI KUJIUNGA NA MIRADI YA UFUGAJI NYUKI

$
0
0



Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Manyoni imetakiwa kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kujiunga na miradi ya ufugaji nyuki ili kuendeleza uhifadhi wa mazingira na kujiongezea kipato kutokana na mazao yatokanayo na ufugaji nyuki kama asali.



Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) wakati wa kikao na watumishi wa TFS kilichofanyika Januari 20, 2023 wilayani Manyoni mkoani Singida.


‘Wajibu wenu ni kutoa elimu kuhusu umuhimu wa uhifadhi ili jamii ielewe na muwe na programu zinazooneshwa kwenye luninga kuelimisha jamii. Pia muhakikishe asilimia kubwa ya wawekezaji kwenye miradi ya ufugaji nyuki wawe ni wananchi wa kawaida ili kuwafanya wasikate miti” amesisitiza Mhe. Masanja.


Aidha, amewataka wahifadhi kuendelea kutoa elimu kuhusu umuhimu wa Uhifadhi kuanzia ngazi ya uongozi wa Wilaya na Mkoa hasa wakati wa ufunguzi wa mashamba ili kuwepo na uhifadhi endelevu.


Naye, Mhifadhi Mkuu Shamba la Nyuki Manyoni, Hashimu Gau amesema madhumuni ya kuanzisha hifadhi hiyo ni kulinda ikolojia ya Itigi ambayo ni maarufu kwa kuzalisha mazalia ya nyuki, eneo hilo pia hutumiwa na jamii kwa kutundika mizinga yao hivyo kujipatia kipato na ajira za muda mfupi za usafishaji mipaka ulinzi na usafi wa mizinga.


Amesema Hifadhi ya Nyuki ya Taifa ya Aghondi ina jumla la Manzuki 7 ambazo  kati ya hizo 5 ni za TFS na mbili za wadau zikiwa na jumla ya mizinga 581 ambapo  kati ya hiyo mizinga 331 ni ya TFS na 252 ya wadau.


Ziara hiyo ni utekelezaji wa majukumu yake ya kusimamia maeneo ya hifadhi na kuhamasisha miradi ya ufugaji nyuki.

Mshindi NMB MastaBata Kote-Kote akabidhiwa Pikipiki

$
0
0

  Meneja Masoko wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Trifon Malkiory (wa pili kulia) akimkabidhi ufunguo wa Pikipiki mshindi wa Kampeni ya NMB MastaBata Kote-Kote, Emmanuel Marumbo kutoka mkoani Tabora, katika hafla ya kukabidhi zawadi hiyo iliofanyika katika Tawi la Mihayo Mjini Tabora. Kulia ni Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mihayo, Prudence Rwegasira na kushoto ni Afisa Mwandamizi wa Biashara ya Kadi, Said Kiwanga. (Na Mpiga Picha Wetu).

 

Meneja Masoko NMB Kanda ya Magharibi Trifon Malkiory (wa pili kulia) akimkabidhi kadi ya Pikipiki Mshindi wa kampeni ya NMB MastaBata Kote-Kote, Emmanuel Marumbo kutoka mkoani Tabora. Hafla hiyo iliofanyika katika tawi la Mihayo Mjini Tabora. Kulia Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mihayo, Prudence Rwegasira na kushoto ni Afisa Mwandamizi wa biashara ya kadi wa benki hiyo, Said Kiwanga.

 

 

Na Mwandishi Wetu

 

Mshindi wa shindano la NMB MastaBata KoteKote linaloendeshwa na Benki ya NMB Emmanuel Marumbo kutoka mkoani Tabora amekabidhiwa rasmi Pikipiki yake aina ya Boxer.

Mshindi huyo wa jumla aliyepatikana katika droo ya nane ya shindano hilo iliyofanyika wiki iliyopita Mkoani Tanga, amekabidhiwa zawadi yake na Meneja Masoko NMB Kanda ya Magharibi Trifon Malkiory.

Hafla ya kumkabidhi zawadi hiyo imefanyika kwenye Tawi la NMB Mihayo mjini Tabora, ambapo kabla ya kumkabidhi zawadi mshindi Meneja huyo aliendesha droo ya tisa ya shindano hilo kwa wiki hii.

Meneja Masoko Trifon amesema kuwa NMB imekuwa ikiendesha shindano hilo ukiwa ni mwaka wa nne tangu limeanza, ambapo linalenga kuhamasisha wateja wake kutumia kadi na Lipa Mkononi (QR).

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya Pikipiki mshindi wa droo ya wiki iliyopita, Emmanuel Marumbo amesema mwanzoni hakuamini kama kweli ameshinda zawadi hiyo licha ya kuwashirikisha wenzake na kuongezea kuwa yeye ni mtu wa kutumia kadi yake ya NMB kwa ajili ya manunuzi ya vitu mbalimbali, huku akibainisha kuwa huwa hatembei na pesa taslimu bali ufanya manunuzi kwa kutumia kadi yake.

Zimesalia siku 10 tu kuelekea grand finale ambapo tutashuhudia wateja 8 wakijishindia safari ya kwenda Dubai kwa siku 4 huku benki ya NMB ikiwalipia kila kitu.

Usiache kadi yako ya NMB mastercard nyumbani kufanya malipo ya matumizi yako au  kwa kuscan QR kujiweka katika nafasi ya kuweza kuwa mmoja wa washindi wa #MastaBataKoteKote

 Luteni Kanali Mshana afanya ziara , aahidi ushirikiano

$
0
0

Mkuu was kikosi Cha 06 akimkabidhi  Mkuu wa Mkoa wa BERIBERATI Mambele kadei fulana yenye nembo ya Mali ya asili kama moja ya kutanga za utaliinwa Tanzania (kushoto).



Mkuu wa Kikosi cha sita cha Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania (TANBAT 6), Luteni Kanali Amani Stephene Mshana ametoa shukurani zake Kwa Mkuu wa Mkoa wa Beriberati  Mambele Kadei akieleza kuwa amefarijika kumtembelea huku akiahidi ushirikiano wa karibu katika jukumu la kulinda amani ya wananchi wa Afrika ya Kati.


Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Ofisa habari wa kikosi hicho, Kapteni Mwijage Inyoma alisema Luteni Kanali Mshana ameahidi kushirikiana na mkoa huo katika jukumu la kulinda amani ya wananchin wa Afrika ya kati pamoja na kuwapa taarifa pale ambapo kutahitajika msaada wa kusimamia amani Kwa wananchi wa Mambele.


Naye Mkuu wa Mkoa huo baada ya ziara hiyo alisema Kuwa,"Tanzania na wanajeshi wake wana upendo sana kwetu, sisi ni kama dada au kaka au mama na hata baba hivyo kuja kwako Mkuu wa Kikosi kunitembelea kama ziara yako kwangu  ni ishara tosha kwa undugu wetu namimi ninahaidi ushirikiano huu kudumisha kama ilivyokuwa kwa vikundi vilivyopita kutoka Tanzania,"


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo alisema tangu kikundi hicho kimefika, kimeonyesha kasi kubwa katika ushirikiano wa karibu na wananchi wake anaowaongoza hapo Mambele kadei.


"Tumeshudia mkitoa matibabu, dawa hata elimu za ujasiliamali kwa akina mama na vijana Ili wajipatie kipato na kuepuka kuingia katika vikundi vyenye nia mbaya na serikali, hii ni ishara tosha kwetu kuwa walinda amani kutoka Tanzania chini ya Umoja wa Mataifa wanafanyakazi kuwa yenye tija kwetu tangu waanze  jukumu la ulinzi wa amani"


Benki ya NMB yaingia makubaliano na Serikali ya Zanzibar uhifadhi bustani ya Forodhani

$
0
0

 



Benki ya NMB imeingia makubaliano na Mamlaka ya Hifadhi Mji Mkongwe, chini ya usimamizi wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuboresha bustani ya Forodhani.



Chini ya makubaliano hayo, Benki ya NMB itasimamia vipengele vifuatavyo:


✅ Kuhakikisha uwepo wa huduma na suluhishi za kifedha, elimu za kifedha na mikopo kwa wafanyabiashara wa Forodhani.



✅ Kuweka maeneo maalum ya polisi, kubadilishia nguo wapiga mbizi na NMB Wakala.


✅ Kuboresha maeneo ya kupiga mbizi Forodhani, na kutoa maboya kwa wapigambizi kwa ajili ya usalama wao.


✅ Kuboresha taa zilizopo eneo la Forodhani


Makubaliano haya yametiwa saini na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi Mji Mkongwe, Eng. Ali Said na Afisa Mkuu wetu wa Wateja Binafsi na Biashara - Filbert Mponzi huku wakishuhudiwa na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Mhe. Simai Mohamed Said na viongozi wengine.

Dully Sykes kufungua Pazia Tamasha la Bongo Fleva Honors

$
0
0


Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

MSANII wa mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Abdul Sykes 'Dully Sykes' atafungua pazila la Tamasha litakalofanyika kwenye Kituo Cha Utamaduni Cha Ufaransa 'Alliance Francaise' Upanga Dar es Salaam Januari 27 mwaka huu.

Dhumuni la tamasha hilo ambalo limepewa jina la Bongo Fleva Honors ni mahusus kwa wasanii wakongwe kuwakumbusha na kuwapa burudani wadau na mashabiki wa muziki huo waliyoikosa kwa kipindi kirefu.

Katika shoo hiyo ambayo itafanyika kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi, msanii mkongwe atakayepanda jukwaani atafanya show  live kwa kupigiwa vyombo na vyombo na Swahili Blues. 

Pia katika kila onesho msanii atakayekuwa siku hiyo historia yake itasimuliwa tangu kuanza kwake muziki hadi alipo sasa na nini anafanya kwa kipindi hiki na mipango yake endelevu kupitia sanaa hiyo na mambo mengine.

"Madhumuni makubwa ya Jukwaa hili la Bongo Fleva Honor zaidi litatumika kutambua na kuheshimisha muziki wa wakongwe wa Bongo Fleva na kuwapa fursa mashabiki wa enzi hizo kujikumbusha na kupata burudani ambayo wameikosa kwa muda mrefu huku wakiwa bado na kiu ya kusikiliza ngoma hizo," amesema Joseph Mbilinyi 'Sugu' wakati akimtambulisha Dully Sykes.

Baada ya kutambulishwa mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Dully Sykes ambaye alitambulika kwa mashabiki wa muziki huo kupitia ngoma ikiwamo 'Nyambizi',Shikide''Hunifahamu', 'Inde', 'Ladies Free', 'Baby Candy', 'Dhahabu Funga''Domo Lako', 'Hi', 'Kabinti Special', 'Salome', 'Nampenda Yeye', 'Action'  na nyinginezo amesema ni furaha kwake kupata heshima ya kuwa wakwanza kufanya onesho hilo litakalofanyika kila mwezi.

"Namshukuru Sugu kwa kunichagua kua wa kwanza kufanya onesho katika mfululizo wa matamasha yajayo yatakayohusisha wasanii wengine wakongwe, kwangu ni historia na heshima kubwa naahidi kufanya makubwa siku hiyo kikubwa Mungu aniamshe salama na ninawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi," amesema mkongwe huyo ambaye yupo kwenye 'game' kwa zaidi ya miaka 20.

Katika mfululizo wa matamasha hayo ambayo yameandaliwa na Msanii nguli, 'Sugu' kupitia timu yake ya Deiwaka World kwa kushirikiana na Kituo Cha Utamaduni Cha Ufaransa na Kampuni ya Paisha inayojishughulisha na Huduma ya Tax Mtandaoni na Usafirishaji wa Chakula na Vifurushi kwa wateja wao, zitasaidia kuondoa 'gap' kati ya wasanii wa zamani na sasa na mashabiki wa zama mpya watapata fursa ya kuona wakongwe mbalimbali na kufuatilia historia ya muziki huo kupitia ratiba ya kila mwezi.

Pia Kiongozi wa  Bendi ya Swahili Blues, Leo Kanyia kwa upande wake amesesma kuwa wana uzoefu wa kutosha wa kufanya live show kwani wameshafanya na wasanii wengi wa ndani na nje hivyo wameahidi kufanya show ya hali ya juu na ya kimataifa.

Naye Mkurugenzi wa Kituo cha Utamduni cha Ufaransa nchini Tanzania, Flora amesema kuwa kiingilio cha maonesho hayo yatakayofanyika kila mwezi kitakuwa Sh 20,000 kwa kila onesho.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Paisha inayojishughulisha na Huduma  ya Tax Mtandaoni  Usafirishaji ,Abraham Lesulie, amesema kuwa wameona kua sehemu ya historia kwao kushirikiana na mkongwe wa muziki huo Sugu kufanikisha maonesho hayo na zaidi kutokana na kuvutiwa na wazo hilo.


GWAJIMA ANOGESHA UFUNGUZI LADIES FIRST DIMBA LA BENJAMIN MKAPA, DAR

$
0
0


Waziri Dk. Dorothy Gwajima, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Riadha ya Ladies First.

 Kaimu Katibu Mkuu RT, Wakili Jackson Ndaweka, akitoa salamu za shirikisho. 

 Viongozi wa RT, Makamu wa Rais William Kallaghe, Kaimu Katibu Mkuu Wakili Jackson Ndaweka na Mwanariadha Simbu, waliosimama nyuma wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu, wakati wa ufunguzi Ladies First.

Waziri Dr. Gwajima, wa pili kutoka Julia akishiriki mazoezi ya viungo wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Ladies First. Wa kwanza kutoka kulia ni Mwenyekiti BMT, Leodegar Tenga, Balozi wa Japan Tanzania kushoto kwa Waziri na Katibu Mtendaji BMT, Neema Msitha.

 

NA TULLO CHAMBO

MSIMU wa Nne wa Mashindano ya Riadha ya Wanawake maarufu kama 'Ladies First' umefunguliwa kwa kishindo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Januari 21 na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dr. Dorothy  Gwajima.

Mashindano hayo  ya siku mbili yameandaliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), kwa kushirikiana na  Shirikisho la Riadha Tanzania (RT).
 
Ufunguzi huo, ulipambwa na vikundi mbalimbali vya Joging, burudani mbalimbali akiwamo Msanii maarufu wa Singeli, Dullah Makabila, aliyepagawisha vilivyo na wanariadha wa kike

Akizungumza katika uzinduzi huo, Dr. Gwajima, alisema wataend…
[10:45 PM, 1/21/2023] Tullo Vd: Mashindano hayo, RT, vyama vya Riadha vya Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa kwa kuwezesha wachezaji wao kufika Dar Ed Salaam kwa ajili ya mashindano hayo, Ofisi ya Mkurugenzi Manispaa ya Temeke kwa kuruhusu zaidi ya wanafunzi 1,000 kuhudhuria mashindano hayo na kujifunza, na Mwanariadha mahiri wa zamani, Kanali Mstaafu Juma Ikangaa, ambaye pia ni Balozi wa Hiari wa JICA, kwa kuasisi wazo la kuanzishwa mashindano hayo.

Balozi mwingine wa hiari wa JICA, Mwanariadha mshindi wa medali ya Fedha Jumuiya ya Madola, Alpohonce  Simbu, aliwataka wanariadha wa kike hao watumie fursa hiyo kujituma na kurejesha enzi za Mwanamama Theresia Dismas, ambaye ni mchezaji wa kwanza kuipa Tanzania medali ya kimataifa katika michuano ya All African Games 1965.

Simbu, alisema kuwa ushiriki huo utakuwa chachu ya kujifikiria namna ya  Theresia Dismas alieweza kupata medali.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu RT, Wakili Jackson Ndaweka, aliishukuru Serikali kwa kuwezesha kupata muungano na JICA kwa kudhamini Riadha hususani kwa wanawake.

Àlisema kuwa wanawake wanatakiwa kutumia fursa ya kujiendeleza  ,kwani mahitaji kuleta ushindani .

Mashindank hayo yatakayofikia tamati Januari 22, yanashirikisha wanariadha zaidi ya 186 kutoka mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani.

Uzinduzi huo, pia ulihudhuriwa na Balozi wa Japan nchini Tanzania, viongozi kutoka Wizara ya Michezo Sudan Kusini, Naibu Meya Jiji la Nagai Japan, Mwenyekiti wa BMT Leodegar Chilla Tenga na Makamu wa Rais RT, William Kallaghe.

Sanlam General Insurance yazindua Kampeni, yatoa zawadi ya Gari na Pikipiki kwa Mawakala

$
0
0

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Kampuni ya Bima ya Sanlam General Insurance imezindua kampeni kabambe kwa mawakala wake ambapo washindi watajinyakulia zawadi mbalimbali ikiwemo Gari, Bodaboda na zingine nyingi kupitia Program ya Vuna Point.

 

Akizungumza jijini Dar es salaam katika hafla ya uzinduzi huo Meneja Masoko na Maendeleo ya Biashara, Matawi na Mawakala wa kampuni hiyo,  Charles Magori amesema lengo la kuanzishwa kwa tuzo hizo ni kutoa hamasa kwa mawakala wa kampuni hiyo pamoja na kuongeza ufanisi katika utendaji wao.

"Lengo kubwa la kuanzishwa kwa Tuzo hiI ni kutambua mchango wa mawakala wetu sambamba na zitawasaidia kuongeza ufanisi na ubunifu zaidi katika kutoaji wa huduma zao hivyo kupelekea kukua kwa mtandao wa biashara zao" Alisema Bw. Magori.

Amebainisha kuwa kampuni hiyo ambayo ina mtandao mkubwa wa mawakala ambao wanapatikana katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Mwanza, Mbeya, Arusha, Dodoma, na Mbagala, Zanzibar na pia wanataraji kufungua mkoani Morogoro.

Katika hatua nyingine, Magori ametoa wito kwa wale wote wanaotaka kujiunga kuwa wakala wa kampuni hiyo kujitokeza kwa wingi ambapo ameeleza kuwa wanachotakiwa kufanya ni kupiga simu kupitia namba 0800750236 na kusajiliwa kuwa wakala.

Kampuni ya Bima ya Sanlam General Insurance ina  uzoefu wa zaidi ya miaka 40 ya utoaji wa huduma za bima na soko la bima nchini imekuwa ikitoa huduma za Bima za Watu na Bima za  biashara.

KASKAZINI UNGUJA, ARUSHA WANG'ARA LADIES FIRST 2023

$
0
0


Makamu wa Rais, Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), William Kallaghe, akimvisha medali ya shaba mshindi wa tatu katika mbio za Mita 10000, Maycelina Mbua wa Arusha.
Mabingwa Unguja Kaskazini mara baada ya kukabidhiwa kombe lao.




 

NA TULLO CHAMBO

MKOA wa Kaskazini Unguja, Zanzibar umeibuka mabingwa katika Mashindano ya  Riadha ya Wanawake maarufu kama Ladies First, yaliyofikia tamati Januari 22 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar Ed Salaam.

Katika mashindano hayo ya siku mbili yaliyoshirikisha mikoa 30 Kati ya 31 ya Tanzania Bara na Visiwani, Kaskazini Unguja, ilipata ushindani wa karibu kutoka mikoa ya Arusha na Pwani.

Kaskazini Unguja, iliibuka mabingwa baada ya kujikusanyia jumla ya medali sita, tano za dhahabu na moja ya fedha, huku Arusha ikifuatia kwa medali nane, nne za dhahabu na nne fedha.

Nafasi ya tatu ilikwenda kwa Pwani iliyopata jumla ya medali nne, tatu fedha na  moja ya shaba.

Wanariadha walioubeba Mkoa wa Kaskazini Unguja walikuwa ni Winfrida Makenji, aliyenyakua dhahabu mbili mita 100 na 200, Jane Maige dhahabu moja mita 400, Mwanaamina Hassan Kurusha Mkuki huku pia wakinyakua dhahabu Mbio za Kupokezana Vijiti 4x100.

Kwa upande wa Arusha, Magdalena Shauri alitwaa dhahabu tatu, mita 800, 1500 na 5000 huku Jack line Sakilu akishinda dhahabu mita 10000.

Nafasi ya nne ilinyakuwa na Kusini Unguja medali nne, fedha mbili na shaba mbili huku nafasi ya tano ikienda kwa Mara medali mbili zote za fedha,Tanga nafasi ya saba medali moja ya fedha, Kilimanjaro ya saba medali moja ya shaba wakati nafasi ya nane ikinyakuliwa na Mjini Magharibi medali moja ya shaba.

Mikoa yote iliyosalia, ilitoka kapa bila medali wakati Songwe ilishindwa kuleta timu katika mashindano ya mwaka huu.

Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), na Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), yakiwa na lengo la kuhamasisha watoto wa kike kushiriki katika michezo hususan Riadha.

Rais Dk. Mwinyi atoa maagizo kwa watendaji taasisi za Umma

$
0
0

 

NA MWASHAMBA JUMA, IKULU

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewaagiza watendaji wa taasisi za Umma kutekeleza kwa wakati maagizo yote yanayotolewa na Serikali ili kujenga ufanisi wa majukumu yao.

Dkt. Mwinyi alitoa maagizo hayo wakati akifungua Mkutano wa tano wa Baraza la Taifa la Biashara Ikulu, Zanzibar.

Alisema ameunda taasisi ya Ofisi ya Rais ya Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini, (PDB) ili ifuatilie mambo yote yanayoamuliwa na Serikali kwa nia ya kuyapatia suluhisho kwa wakati uliokubaliwa.

“Nimeunda taasisi hii lengo ni kufuatilia utekelezaji wa mambo yote tunayoyaamua serikalini” Alisisitiza Rais Mwinyi.

Alisema Uchumi wa Zanzibar unakabiliwa na changamoto mbalimbali licha ya kuendelea kuboreka na kueleza kuwa baadhi ya changamoto hizo ziko ndani ya uwezo wa Serikali kwaajili ya kuzitatua na baadhi yao ziko nje ya uwezo kutokana na sababu za kiulimwengu.

Rais Dk. Mwinyi alisema, athari za ugonjwa wa COVID 19 ziliathiri sana uchumi wa dunia na mataifa mengi kutetereka kiuchumi haswa uchumi wa nchi za visiwa ikiwemo Zanzibar.

Alisema licha ya ugonjwa huo kupungua na kumalizika kwa baadhi ya mataifa lakini bado umendelea kuyaandama mataifa mengine ikiwemo China ambae ni Mshirika mkubwa wa Maendeleo kwa Uchumi wa Zanzibar.

Aliongeza sekta ya usafirishaji bidhaa ni moja ya changamoto inayohujumu uchumi wa dunia kutokana na sababu mbali mbali za kidunia na kueleza kuwa Zanzibar kwa kiasi kikubwa imeathiriwa na changamoto hiyo mbali na ufinyu wa bandari ya Malindi, unaodhorotesha huduma kwenye eneo hilo.

Akitoa ufafanuzi juu ya ujenzi wa bandari ya Mpigaduri, Dk. Mwinyi alieleza, Serikali ya awamu ya nane baada ya kuingia madarakani ilikuta tayari hatua za ujenzi wa bandari hiyo zilikamilika kwa ajili ya ujenzi wa bandari ya makontena pekee nakueleza kuwa Serikali ya awamu ya nane iliona haja ya mahitaji yaliyopo kwenye bandari ya Malindi hayakidhi haja, ndio maana ilikuja na wazo la ujenzi wa bandari ya Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja ambao utakwenda kuondosha changamoto zote.

“Wakati serikali ya awamu ya nane inaingia madarakani, ilikuta tayari mpango wa ujenzi wa bandari ya Mpigaduri ulikuwepo kwaajili ya kuanzisha bandari ya makontena pekee, hatua ya ujenzi huo ilifikia pazuri, lakini sisi tukaona tuzungumzie ujenzi wa bandari kubwa wenye kukidhi haja zote” alifafanua Dk. Mwinyi.

Alisema Zanzibar kwasasa inahitaji bandari yenye kukidhi haja zote ikiwemo bandari ya Makontena, bandari ya mafuta, bandari ya Samaki na bandari itakayotoa huduma za kubeba mizigo ya nafaka ikiwemo mchele na mambo mengine yenye uhitaji mkubwa, na kueleza kwamba Mpigaduri pekee isingetosha.

Alisema Serikali imefanya uamuzi wa ujenzi ya bandari ya Mangwapwani kutokana na kukidhi kwa eneo kwaajili ya mahitaji yote pia alieleza kina kirefu cha bahari kwa eneo hilo kinakidhi haja ya ujenzi na kuongeza kuwa Mpigaduri kutasaidia mahitaji ya bandari ya Malindi ambayo kwasasa imezidiwa kutokana na ufinyu wa nafasi na msongamano mkubwa wa huduma zinazotolewa.

Dk. Mwinyi alifafanua ujenzi wa bandari ya Mangapwani utashirikisha sekta binafsi na kueleza kwamba hautojengwa kwa fedha za mikopo.

Wakati huo huo Rais Dk. Mwinyi alizitaka Mamlaka za ulinzi ikiwemo Wizara yenye dhamana na Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Kusimamia utendaji wa Polisi Utalii kwa kuwafunza juu ya kuwachunguza watembeza watalii na kuhakikisha kuwa wanavibali halali vya kutembezea wageni kwaaajili ya usalama wa watalii, mali na maisha yao pamoja na kuwaondoshea bugudha wageni.

Akiwasilisha taarifa ya Kamati za Baraza la Taifa la Biashara, Katibu wa Baraza hilo ambae pia ni Katibu Kiongozi wa Baraza la Mapinduzi, Mhandisi Zena A Said alieleza baraza lina kamati nne ambazo ni Kamati ya Uchumi na Biashara, Uwekezaji na Kulipa kodi, Kamati ya Kilimo Ufugaji, Uvuvi na Mazingira, Kamati ya Utalii na Kamati ya masuala ya Ardhi.

Mhandis Zena alieleza Baraza lilifanikiwa kuzifanyia kazi kwa kuzipatia ufumbuzi hoja mbalimbali zilizowasilisjwa na kamati hizo miongoni mwao alieleza ni Maslahi ya wanaopoteza ajira kwenye taasisi binafsi, Udhibiti wa wanaotembeza watalii wasiorasmi, Udhibiti wa nyumba za kulala wageni, Maegesho ya magari yanayotumia VAT, Athari za michezo ya baharini na Madai ya wakulima wa mbogamboga kwa uchelewashwaji wa madeni yao kwa taasisi za Serikali.

Aidha, Mhandisi Zena alieleza bahadhi ya mafaniko yaliyotokana baada ya kufanyiwa kazi kwa hoja za kamati hizo alisema Kuanzshiwa kwa Fao la ukosefu wa ajira kupitia marekebisho ya Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii, (ZSSF) nambari 5 ya mwaka 2005, Kutungwa kwa Sheria ya Mfuko wa huduma za Afya, Kuanzishwa kikosi cha Polisi Utalii na Diplomasia, Kuanzishwa kanuni za kusimamia nyumba za kulala wageni, Kuanzishwa mfumo wa ofisi Mtandao, Kuandaliwa mwongozo wa mahusiano baina ya wakulima na wamiliki wa mahoteli Pamoja na kuundwa kwa bodi ya ushauri ya masuala ya ajira na mishahara

Mkutano wa tano wa Baraza la Taifa la Biashara uliofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo Mawaziri wa Serikali, Makatibu Wakuu, Wakurugenzi wa taasisi za Serikali na Sekta binafsi.

Aidha, mada mbalimbali ziliwasilishwa kwenye mkutano huo ikiwemo Muhtasari wa Sheria ya Baraza la Taifa la Biashara la Zanzibar, Nafasi ya sekta binafsi katika kuchochoea ukuaji wa uchumi wa Zanzibar na nyengine ambazo zilichangiwa na wajumbe waliohudhuria mkutano huo.

Magazeti ya Tanzania Januari 23, 2023

Takukuru yatakiwa kuchunguza tuhuma za rushwa kwa Majaji na Mahakimu

$
0
0

Kufuatia tuhuma za rushwa kwa baadhi ya majaji na mahakimu, zilizotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mkoani humo, Dk. Rashid Chuachua, Jaji kiongozi wa Mahakama Kuu Mustapher Mohamed Siyani ametaka tuhuma hizo zichunguzwe na Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

 Jana Januari 22 wakati wa sherehe za uzinduzi wa wiki ya sheria mkoani humo, Dk. Chuachua alinukuliwa akisema kuna baadhi ya majaji na mahakimu wanajihusisha na vitendo ya ukiukaji wa maadili kwa kupokea rushwa kwa njia ya miamala ya simu.

Baada ya tuhuma hizo, Jaji kiongozi Siyani amemuagiza Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Rose Ebrahim kuwasilisha hoja hiyo kwa uongozi wa Takukuru wa mkoa huo ili kufanya uchunguzi wa tuhuma hizo na kubaini ukweli.

Taarifa iliyotolewa leo Januari 23 na mkuu wa kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano, Artemony Vicent imesema;

“Ikithibitika pasipo na shaka kwamba tuhuma hizo zina ushahidi wa kutosha bila ya kuathiri hatua nyingine zitakazochukuliwa na vyombo husika, hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa watumishi watakaothibitika kutenda kosa hilo.

"Ni matumaini ya uongozi wa mahakama kwamba waliotoa tuhuma watakuwa tayari kuthibitisha ili sheria ichukuae mkondo wake bila kumuonea yeyote au kuchafua taswira ya muhimili wa mahakama na watumishi wake," imeeleza taarifa hiyo.

TANBAT 6 wawashauri wananchi Afrika ya Kati kuilinda amani, kukomesha migogoro

$
0
0


Mkuu wa wilaya ya Mambere kadei akimkaribisha mmoja wa wawakikosi kutoka TANBAT6 baada ya kufika kwa ajili ya kuungana na wananchi ili kutatua mgogoro wa wakulima na wafugaji.



Na Janeth Jovin

KIKOSI cha sita cha Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania (TANBAT 6), kimewashauri wananchi kijiji cha Sapuoa kilichopo kilometa 37 kutoka Mjini Beriberati nchini Afrika ya Kati,  kuilinda amani waliyonayo na kukomesha migogoro ya mara kwa mara.


Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Ofisa habari wa kikosi hicho, Kapteni Mwijage Inyoma alisema kijiji hicho hapo awali kilikuwa na migogoro baina ya wakulima na wafugaji haki iliyotishia amani lakini tangu kilipokuja kikosi cha TANBAT 6 kimefanikiwa kukomesha tatizo hilo.


Alisema walinda amani kutoka Tanzania wanaendelea kuwashauri wananchi wa kijiji hicho kushirikiana kwa umoja na kupendana ili kuleta maendeleo na kuendeleza amani ambayo inazidi kujengeka nchini mwao.


"Kijiji cha Sapuoa kilikuwa katika mgogoro wa muda kati ya wakulima na wafugaji kwa kuibiana mifugo na wakulima kuhalibiwa mazao, hali liyosababisha wadau wa walinda amani kusaidia kuondoa mgogoro huo kwa kuwakutanisha na kufanya mazungumzo yaliyoleta muafaka wa mgogoro huo," alisema Kapteni Inyoma katika taarifa yake


Aidha alisema walinda amani wa UN kutoka Tanzania katika utekelezaji wa jukumu la kuimalisha mahusiano na upendo kati ya wananchi wa Afrika ya kati wanaendelea na mikakati wa kuunga mkono wadau wa Umoja wa Màtaifa MINUSCA kwenye kuhamasisha amani katika vijiji mbalimbali mkoani Beriberati, Mambele kadei.


Kwa upande wake kiongozi wa Kijiji hicho cha Sapuoa, And Darius alisema anawashukuru walinda amani wa Tanzania kwa kazi wanazofanya hasa za kuhakikisha amani inapatikana wakati wote eneo hilo.


Alisema walinda amani hao  wamesaidia kuwakutanisha na kuondokana na mgogoro ambayo ulikuwa na sura mbaya kwenye jamii yao.


"Hakika Walinda amani kutoka Tanzania chini ya Umoja wa Màtaifa (UN) wanatujali sana na lazima tuendelee kuwaunga mkono katika kazi zao za ulinzi wa amani hapa nchini kwetu Afrika ya Kati," alisema


LADIES FIRST 2023 YAZIDI KUFUNGUA NEEMA RIADHA TANZANIA

$
0
0


*Sudan Kusini yaipa shavu RT, Simbu Balozi mpya JICA
 
Balozi wa Japan nchini Tanzania (kushoto mbele), akiwa na Muasisi wa Ladies First, Kanali mstaafu Juma Ikangaa, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washindi Ladies First 2023.

Baadhi ya washiriki wakichuana Ladies First 2023.
Balozi wa Hiari mpya JICA, Alphonce Simbu, akizungumza wakati wa ufunguzi Ladies First 2023.


NA TULLO CHAMBO, RT

MASHINDANO Maalum ya Riadha ya Wanawake nchini Tanzania maarufu kama Ladies First, yamezidi kufungua ushirikiano wa mchezo huo kimataifa.

Ladies First ikiwa ni wazo la Nguli wa Riadha nchini Tanzania, Kanali mstaafu Juma Ikangaa, imefanyika mwaka huu ukiwa ni msimu wa nne na kushirikisha mikoa 30 Kati ya 31 Tanzania Bara na Visiwani.

Mwaka huu, mashindano hayo yalifanyika January 21 na 22 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam na kushirikisha zaidi ya wanariadha 186.

Kanali Mstaafu Ikangaa, ambaye enzi zake aliiwakilisha vema Tanzania kimataifa katika mbio za marathoni, ikiwemo nchini Japan, nchi hiyo imekuwa ikimuenzi na kumpa heshima kubwa ambapo hivi sasa ni Balozi wa Hiari wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA).

Katika kumuenzi Kanali Ikangaa, Japan ilimtaka kusema kitu ambacho nchi hiyo iifanyie Tanzania, ndipo kwa kushirikiana na wadau wake mbalimbali, akaja na wazo la kuwaenzi na kuhamasisha wanawake kushiriki katika mchezo wa Riadha, hasa ikizingatiwa medali ya kwanza ya kimataifa Tanzania ililetwa na Mwanamke Theresia Dismas mwaka 1964, katika michezo ya All Africa nchini Congo Brazzaville, kupitia mchezo wa Kurusha Mkuki 'Javelin'.

Wazo hilo lilianza kutekelezeka mwaka 2017 kwa mashindano yaliyofanyika Uwanja wa Taifa, sasa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, ambapo baadhi ya washindi wamekuwa wakipata nafasi ya kwenda kushiriki mbio za Nagai City nchini Japan.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Tanzania (BMT), Bi. Neema Msitha, aliipongeza JICA na kampuni mbalimbali za Kijapan zinazofanya kazi nchini, Kanali Ikangaa,serikali ya Tanzania na Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), kwa kufanikisha mashindano hayo kwa msimu wa nne sasa.

Bi. Msitha, anasema mashindano hayo yalianza mwaka 2017 na kufanyika kwa mafanikio makubwa miaka mitatu mfululizo hadi 2019 kabla kusitishwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo janga la UVIKO 19 'Covid 19'.

"Lengo la mashindano haya ni kuhamasisha ushiriki wa watoto wa kike katika michezo hususan Riadha, kutoa fursa kwa wanariadha wa kike kuonyesha vipaji vyao na kuendeleza vipaji vya wanariadha ambao wataiwakilisha nchi katika mashindano ya kitaifa na kimataifa," anasema Bi. Msitha.

Tangu kuanza kwa mashindano hayo mwaka 2017, Wanariadha wa Tanzania na viongozi wao, wamekuwa wakipata nafasi ya kwenda kushiriki Nagai Marathon, ambapo wanariadha akiwemo Angel John Joseph Yumba, Fabian Nelson Sulle, Fabian Joseph, Alphonce Felix Simbu na wengineo wameweza kung'ara.

Mbali na hilo, Ladies First iliweza kuishirikisha nchi ya Sudan Kusini na kushiriki mashindano ya mwaka 2019 jijini Dar es Salaam.

Mwaka huu 2023, Ladies First imezidi kufungua milango katika mchezo wa Riadha Tanzania, ambapo Sudan Kusini iliwakilishwa na viongozi wake mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo nchini humo, Peter Baptist, Balozi wa nchi hiyo nchini Tanzania, Deng Abel na wengineo.Baptist katika salamu zake, mbali na kushukuru na kupongeza Tanzania kwa mashindano hayo, anasema na kwao wana mashindano kama hayo yajulikanayo kama 'Umoja na Amani', yakilenga kutumia michezo kuhamasisha amani na umoja katika Taifa hilo ambalo liliandamwa na vita miongoni mwao kwa miaka kadhaa.

Mwakilishi huyo, anasema katika kuendeleza ushirikiano na Tanzania, wanatoa mwaliko kwa wanariadha wanne waliofanya vizuri katika Ladies First 2023 wa mbio tofauti ukiondoa mita 5000 kwenda Sudan Kusini kushiriki mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika miezi miwili ijayo.

Mbali na fursa hizo zilizojitokeza Ladies First 2023, nyingine ni kwa Mwanariadha anayefanya vema hivi sasa, Mshindi wa Medali ya Fedha Common Wealth Games 2022, Alphonce Simbu, naye kuteuliwa kuwa Balozi wa Hiari JICA, akiungana na Kanali mstaafu Ikangaa.

Haya ni kati ya mafanikio ya Ladies First 2023, na hakika uwajibikaji ukizidi kuongezeka, bila shaka milango zaidi itazidi kufunguka katika medani ya riadha Tanzania.

IBENGE AFUATA 'UBANI' WA KLABU BINGWA TANZANIA

$
0
0

Kocha wa Al Hilal ya Sudan, Frolent Ibenge, ameamua kuweka kambi nchini Tanzania ambapo watacheza mechi 3 za kirafiki wakijiandaa kwa hatua ya makundi ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika. Mechi hizo watacheza dhidi ya Namungo FC, Azam FC na Simba SC.



Ibenge na vijana wake watakuwa Tanzania kuanzia Januari 25 mpaka Februari 6 ambapo watahitimisha kambi yao hiyo. Al Hilal waliiondosha Yanga katika hatua ya mtoano CAFCL na kufanikiwa kutua hatua ya makundi.


Mhe.Gekul aiagiza Bodi ya Filamu kupitia Upya Katiba ya Shirikisho la Filamu

$
0
0

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul leo Januari 23, 2023  Ofisini kwake Mtumba Dodoma  amekutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa Shirikisho la Filamu Nchini.

Katika kikao hicho Naibu Waziri Gekul, amepokea changamoto na mapendekezo kuhusu namna bora ya kuboresha uendeshaji na utendaji wa Shirikisho na Vyama vinavyounda Shirikisho hilo.

Mhe. Gekul, ameelekeza Bodi ya Filamu na Baraza la Sanaa la Taifa kupitia upya Katiba ya Shirikisho hilo pamoja na Vyama vyote ili kuangalia mapungufu na kuyafanyia kazi.

Aidha ameagiza Bodi ya Filamu pamoja na BASATA kukutana na viongozi wa Shirikisho na Vyama hivyo  kwa lengo la kuimarisha utendaji na ufanisi wa Shirikisho na Vyama vyake.


TANZANIA COMMERCIAL BANK YAIPIGA JEKI SEKTA YA ELIMU YATOA MSAADA WA MIFUKO 150 YA CEMENT KUBORESHA MADARASA

$
0
0

Meneja wa Benki ya Tanzania Commercial Bank (TCB) Tawi la Mbagala Edward Mwoleka, (watatukulia), akikabidhi sehemu ya msaada wa mifuko 150 ya Cement,  kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kilamba iliyopo mbagala Charambe iliyotolewa na TCB kwaajili yakufanya maboresho ya madarasa ya shule hiyo Hafla yakukabidhi msaada huo imefanyika hivi karibuni. kutoka kulia ni Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Gloria Mutta, Diwani wa Kata ya Charambe Twahil Shabani,  pamoja na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Temeke Betha Minga.

Meneja wa Benki ya Tanzania Commercial Bank (TCB) Tawi la Mbagala Edward Mwoleka, (watatukulia), akikabidhi sehemu ya msaada wa mifuko 150 ya Cement, kwa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Temeke Betha Minga, iliyotolewa na TCB kwaajili yakufanyia maboresho ya madarasa ya shule ya msingi Kilamba iliyopo Charambe.  Hafla yakukabidhi msaada huo imefanyika hivi karibuni kutoka kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Leah  Masaba,  Diwani wa Kata ya Charambe Twahil Shabani,  pamoja na mjumbe wa shule.Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Gloria Mutta, (watatukulia), akikabidhi sehemu ya msaada wa mifuko 150 ya Cement,  kwa Mtendaji kata ya Charambe Theodora Malata iliyotolewa na TCB kwaajili yakufanyia maboresho ya madarasa ya shule ya msingi Kilamba iliyopo Charambe.  Hafla yakukabidhi msaada huo imefanyika hivi karibuni wengine pichani Meneja wa Benki ya Tanzania Commercial Bank (TCB) Tawi la Mbagala Edward Mwoleka,  pamoja na uongozi kutoka kamati ya shule.

Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kilamba Leah Masaba, akizungumza wakati wa hafla yakupokea msaada wa mifuko 150 ya Cement iliyotolewa na TCB kwaajili yakufanyia maboresho ya madarasa ya shule hiyo Mtendaji kaya ya Charambe Theodora Malata, akitoa shukrani kwa niaba ya shule ya Msingi Kilamba kwa uongozi wa TCB baada ya kupokea  msaada wa mifuko 150 ya Cement iliyotolewa na TCB kwaajili yakufanyia maboresho ya madarasa ya shule hiyo iliyopo Charambe jijini Dar es Salaam.

 

 

 

 

NMB yaendelea kufadhili upatikaji wa huduma bora za afya

$
0
0


Naibu Waziri wa Afya Dk. Godwin Mollel (kulia) akipokea sehemu ya msaada wa vifaa tiba kutoka kwa Afisa Mkuu wa Huduma Shirikishi wa Benki ya NMB, Nenyuata Menjooli kwa ajili ya vituo vya afya vya Mkonoo na Levolosi katika hafla iliyofanyika jijini Arusha, mwishoni mwa wiki. Vifaa vilivyokabidhi ni vitanda 10 vya kujifungulia akinamama wajawazito, vitanda 10 vya kulazwa wagonjwa huku mabenchi 20 yakitolewa kwa Kituo cha Afya cha Levolosi. Kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini, Dismas Prosper. (Na Mpiga Picha Wetu).

 

Na Mwandishi Wetu

 

Sekta ya afya ni sekta muhimu kwa maendeleo ya jamii zetu na kwa kulitambua hilio, Benki ya NMB imeshirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Afya kusaidia kuboresha huduma za Afya kwa Wilaya ya Arusha kwa kutoa msaada wa vifaa tiba vyenye jumla ya thamani ya zaidi ya sh. 26,000,000 katika kituo vya Afya - Mkonoo ambavyo ni;


✅ Vitanda 10 vya kujifungulia kwa kina mama
✅ Vitanda 10 vya kulazia wagonjwa wa kawaida

Huku, kwa Kituo cha Afya Levolosi waliwakabidhi mabenchi 20 ya kusubiri huduma na kukalia kwa wasindikizaji.

Kabla ya kukabidhi vifaa hivyo, Afisa Mkuu wa Huduma Shirikishi wa NMB, Nenyuata Mejooli alisema kuwa vifaa hivyo ni moja ya ushiriki wetu katika maendeleo ya jamii na wao kama benki inayoongoza Tanzania, wanao wajibu wa kuhakikisha jamii inayowazunguka inafaidika kutokana na faida wanayoipata.

Lakini pia, aliongezea kuwa Benki ya NMB imekuwa ikipokea maombi mengi sana ya kuchangia katika miradi ya jamii, lakini benki imejikita zaidi katika maeneo ya elimu, afya, na misaada ya hali na mali katika nyakati ngumu kama za majanga na tumekuwa mstari wa mbele kuchangia huduma za kijamii kwa lengo la kurejesha sehemu ya faida yetu kwa jamii.

kwa zaidi ya miaka kumi mfululizo, Benki ya NMB  imekuwa ikitenga asilimia 1℅  ya faida yake kama sehemu ya uwajibikaji kwa jamii inayoizunguka.

Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>