Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

WAZIRI MASAUNI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MABALOZI WA UINGEREZA, INDIA, PALESTINA NA UNHCR NCHINI, JIJINI DAR ES SALAAM LEO JANUARI 24, 2023

$
0
0


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akizungumza na Balozi wa Uingereza Nchini, David Concar kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Uingereza katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam, leo Januari 24, 2023. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 

 Na Mwandishi Wetu, MoHA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amekutana na kufanya mazungumzo na mabalozi wa nchi za Uingereza, India, Palestina pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) kwa nyakati tofauti kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizo na Tanzania kwenye maeneo mbalimbali ya ulinzi na usalama.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo Januari 24, 2023 katika ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es Salaam huku yakihudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Wizara na walioongozana na mabalozi hao.

Katika mazungumzo yake na Mabalozi hao nchini, wamejadili maeneo ya ushirikiano ambayo yakiwemo kutoa mafunzo mbalimbali kwa Askari,  masuala ya Wakimbizi pamoja na ushirikiano katika masuala ya ulinzi na usalama.

Akizungunza katika Kikao hicho Waziri Masauni amewashukuru mabalozi hao kwa nyakati tofauti kwa ushirikiano wao wa kuisaidia Tanzania kupitia misaada mbalinbali wanayoitoa na pia amewakaribisha wawekezaji wa kutoka katika nchi zao kuja kuwekeza nchini kwa kuwa Tanzania ipo salama na itaendelea kuwa salama hivyo inamazingira mazuri kwa ajili ya uwekezaji.

Kwa uoande wake Balozi wa Uingereza nchini, David Concar amesema Serikali ya Uingereza ipo tayari kutoa msaada kwa Serikali ya Tanzania kwenye masuala ya mbalimbali Wakimbizi nchini hasa kuhusiana na Wakimbizi wa Burundi kurejeshwa nchini kwao.

Naye Balozi wa India nchini, Binaya Pradhan amesema SAerika ya India imetoa misaada mbalimbali kwa Serikali ya Tanzania, ikwemo katika sekta ya maji, msaada wa mafunzo ya elimu ya muda mrefu pamoja na kutoa mafunzo ya kupambana na uhalifu wa mtandao kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi.

Kwa upande wake Balozi Palestina, Hamdi Mansour AbuAli amesema Serikali yake ipo tayari kushirikiana na Srerikali ya Tanzania katika mapambano ya uhalifu na ugaidi.

Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wakimbizi (UNHCR), Mahoua Parums ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano katika masuala ya Wakimbizi na hivi karibuni shirika hilo linatarajia kufanya zoezi la uhakiki wa wakimbizi walipo nchini katika kambi zote za wakimbizi nchini na pia amesema hivi karibuni Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini wanatarajia kufanya ziara katika Kambi za Wakimbizi nchini Tanzania.


Serikali yaipongeza Benki ya NMB

$
0
0

Benki ya NMB imepata nafasi ya kutembelewa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalum - Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima katika ofisi zao za Makao Makuu jijini Dar es Salaam.

Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB - Ruth Zaipuna aliembatana na Afisa Mkuu wa Fedha NMB - Juma Kimori, amempokea Mhe. Gwajima na kumuelezea kuhusu masuluhisho yanayogusa moja kwa moja makundi mbalimbali katika jamii.

Lakini pia, aliahidi kushirikiana na serikali  kuhakikisha masuluhisho yao yanakuwa chachu ya maendeleo kwa makundi yote katika jamii kwa kuendelea kuwekeza kwenye teknolojia na ubunifu.

Katika salamu zake, Mhe. Gwajima alimpongeza Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB pamoja na uongozi mzima wa benki hiyo kwa mafanikio waliyoyapata, na kuahidi kuna balozi mzuri kufikisha fursa zinazotolewa na benki hiyo kwa wananchi ili waweze kujijenga kiuchumi.



UTAFITI STADI ZA MAISHA NA MAADILI KWA VIJANA KUZINDULIWA KESHO

$
0
0

Mratibu wa Mradi wa ALIVE – Tanzania kutoka Shirika la Milele Zanzibar Foundation, Bw. Samson Sitta (katikati) akizungumza na wanahabari leo kuzungumzia uzinduzi wa tathmini ya utafiti wa ALiVE uliofanyika katika wilaya 34 ndani ya mikoa 18 ya Tanzania Bara, uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika Januari 26, 2023 jijini Dar es Salaam Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Kulia ni Mtafiti Kutoka UDSM, Daniel Marandu pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Uwezo Tanzania, Bw. Benjamin Masebo (kushoto) wakifuatilia.

Kaimu Mkurugenzi wa Uwezo Tanzania, Bw. Benjamin Masebo (katikati) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kuzungumzia uzinduzi wa tathmini ya utafiti wa ALiVE uliofanyika katika wilaya 34 ndani ya mikoa 18 ya Tanzania Bara, unaotarajiwa kufanyika Januari 26, 2023 jijini Dar es Salaam Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Kulia ni Mratibu wa Mradi wa ALIVE – Tanzania kutoka Shirika la Milele Zanzibar Foundation, Bw. Samson Sitta pamoja na Mwalimu na Mdau wa Elimu, Richard Mabala. 

Mwalimu na Mdau wa Elimu, Richard Mabala (katikati) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kuzungumzia uzinduzi wa tathmini ya utafiti wa ALiVE unaotarajiwa kufanyika Januari 26, 2023 jijini Dar es Salaam Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uwezo Tanzania, Bw. Benjamin Masebo pamoja naye Afisa Mawasiliano wa Uwezo Tanzania, Bw. Greyson Mgoi (kushoto). 

Mratibu wa Mradi wa ALIVE – Tanzania kutoka Shirika la Milele Zanzibar Foundation, Bw. Samson Sitta (katikati) akizungumza na wanahabari leo (hawapo pichani) kuzungumzia uzinduzi wa tathmini ya utafiti wa ALiVE uliofanyika katika wilaya 34 ndani ya mikoa 18 ya Tanzania Bara, uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika Januari 26, 2023 jijini Dar es Salaam Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Kulia ni Mtafiti Kutoka UDSM, Daniel Marandu pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Uwezo Tanzania, Bw. Benjamin Masebo (kushoto) wakifuatilia.

Na Mwandishi Wetu 

UTAFITI uliofanywa na Mradi wa ALiVE-Tanzania kupima stadi za maisha na maadili kwa vijana nchini Tanzania umebaini kuwa vijana wengi wenye umri kati ya miaka 13 – 17, wana kiwango cha chini cha stadi za maisha (LifeSkills). Imebainika kuwa kundi hilo la vijana linauwezo mdogo wa utambuzi wa matatizo na hata kutumia namna bora ya kulitatua kwa jamii.

Matokeo ya kina ya utafiti huo uliofanywa ndani ya Wilaya 34 kutoka katika mikoa 18 ya Tanzania yanatarajiwa kuzinduliwa Januari 26, 2023 jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Mradi wa ALIVE – Tanzania kutoka Shirika la Milele Zanzibar Foundation, Bw. Samson Sitta anasema tathmini ya utafiti wa ALiVE imefanyika katika wilaya 34 ndani ya mikoa 18 ya Tanzania Bara, kati ya mwezi Juni hadi Septemba 2022, huku akishirikisha jumla ya vijana 14,645 wenye umri wa miaka 13-17 walifanyiwa tathmini/upimaji kutoka katika kaya 11,802. 

Akifafanua zaidi juu ya utafiti huo alisema umebaini ni asilimia 8 tu ya vijana wana uwezo wa utatuzi wa matatizo, yaani, wanaweza kutambua kuwepo kwa tatizo kutoka kwa mitazamo tofauti tofauti, wakielewa kuwa kunaweza kuwa na njia nyingi na kuchagua iliyobora. 

"Kwa kutilia mkazo, stadi za maisha na tunu zinatambuliwa kuwa ni sehemu ya msingi ya elimu kwani huongeza uwezo wa kujifunza kwa wanafunzi. Pia kwa upande wa ajira, waajiri nao wanazingatia zaidi umahiri wa stadi za maisha na maadili kama vile utatuzi wa matatizo, ubunifu, mawasiliano, fikra tunduizi, ushirikiano, kujitambua na stadi nyinginezo ili kuongeza ufanisi katika kazi," alisema Bw. Sitta.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Uwezo Tanzania, Bw. Benjamin Masebo aliongeza kuwa licha ya ukweli kwamba watu wengi wanakubaliana kwamba stadi za maisha ni muhimu, hakuna ushahidi wa kutosha unaotoa taswira ya kiwango cha umahiri wa watoto katika stadi za maisha na maadili, zaidi ya matokeo ya kitaaluma. 

"Sasa tumeweza kufanya kwa mara ya kwanza tathmini ya kitaifa ya stadi za maisha na maadili kwa vijana na kupata matokeo. Hivyo basi baada ya uzinduzi wa ripoti hiyo, ni wakati maridhawa kujikita katika mijadala chanya kuhusu nini tutaweza kufanya ili kuwajenga watoto wa Tanzania katika stadi hizi kupitia mfumo wa elimu na malezi nyumbani. 

“Tunatarajia ripoti hii ya kipee kabisa kuwahi kutolewa Tanzania, na Afrika Mashariki, itachochea mijadala chanya kuhusu umuhimu wa stadi za maisha na nini kifanyike kuhusu ujifunzaji wa watoto wetu ili kuwasaidia kujenga stadi hizi.” alifafanua Kaimu Mkurugenzi wa Uwezo Tanzania, Bw. Masebo.

ALiVE ipo chini ya Mtandao wa Kikanda wa Elimu na Ujifunzaji (Regional Education Learning Initiatives-RELI), kupitia kongani ya maadili na stadi za maisha (VALi) hii inaratibiwa na Zizi Afrique Foundation NGO iliyoko nchini Kenya, Luigi Giussani Taasisi ya Elimu ya Juu nchini Uganda na Milele Zanzibar Foundation kwa Tanzania. 

Tathmini ya ALiVE kwa Tanzania bara ilifanywa kwa Ushirikiano wa mashirika mawili; Milele Zanzibar Foundation na Uwezo Tanzania.

Serikali yashauriwa kutoa elimu ya usimamizi maliasili

$
0
0

 Na Janeth Jovin

SERIKALI imeombwa kutoa elimu na kuweka usimamizi mzuri wa rasilimali za maliasili ili kuepusha migogoro mbalimbali kwa jamii inayozungukwa na raslimali hizo.


Hayo yalibainishwa hivi karibuni wilayani Bagamoyo mkoani Pwani na Meneja Ufuatiliaji na Tathmini, katika Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, John Noronha wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu uhifadhi wa maliasili yaliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET).




Noronha amesema ili kukomesha tatizo hilo la migogoro baina ya wananchi na wanyama hasa katika shoroba mbalimbali nchini ni muhimu wananchi wakaelezwa na kupatiwa elimu jinsi rasilimali hizo zitakavyowasaidia kukuza kipato chao.


Amesema wananchi hao wanapaswa kuelimishwa kwa undani umuhimu wa  uhifadhi wa maliasili na jinsi zitakavyo wanufaisha na endapo wakiziharibu wataathirika vipi.


"Ili kuhakikisha sasa rasilimali hizo za maliasili nchini zinaendelea kuimarika na kuleta manufaa kwa Watanzania kupitia shoroba  zilizopo, Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAIDS) kwa kushirikiana na JET tumekuja  na mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili ambao ni wa miaka mitano  na umeanza June 2021, umegharimu  dola za Marekani milioni 30.5.


"Mradi huo unalenga kutatua na kupunguza changamoto zote zinazozikabili hifadhi nchini na kuangalia mapitio ya wanyama  na jinsi ya kuifadhi maliasili endelevu," amesema Noronha.


Noronha amesema utekelezaji wa mradi huo umejikita katika maeneo matatu yakiwa kuzijengea uwezo taasisi  za serikali na binafsi kuhusu uhifadhi wa wanyamapori na kuwapa vifaa mbalimbali vya utendaji.


"Kwa sasa utekelezaji wa mradi huu umeziangalia shoroba saba za hifadhi kati ya 61 zilizopo nchini  ili kuhakikisha zinaleta mafanikio  kwa Watanzania endapo zikisimamiwa vizuri kwa kuepusha migogoro mbalimbali inayosababishwa na shughuli za kibinadamu," amesema


Naye Meneja wa Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi wa Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, Dk. Elikana Kalumanga amesema kuwa katika mapitio ya wanyama kuna fursa nyingi zilizopo zikiwemo za kiuchumi, kijamii na kikolojia kutokana na aina mbalimbali za ufugaji zinazoendelea.


Dk. Kalumanga amesema mbali na uwepo wa fursa hizo lakini shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo ni moja ya vitu vinavyoathiri shoroba mbalimbali zilizopo hapa nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa JET, John  Chikomo amesema wamekuwa wakitoa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya utunzaji wa mazingira hasa katika masuala ya uhifadhi wa maliasili.


“Mafunzo tuliyoyatoa yamejikita katika utunzaji wa shoroba za wanyamapori kwa lengo la kuisaidia jamii kujua namna ya kutunza na kuhifadhi kwani nyingi zimetoweka kutokana na shughuli za kibinadamu hasa kilimo,”ameeleza.


Naye Mwenyekiti wa JET, Dk. Ellen Otaru amewataka waandishi wa habari kuwa mstari wa mbele kuibua na kuelimisha jamii juu ya athari zitokanazo na shughuli za kibinadamu kama kilimo na nyinginezo ndani ya shoroba pamoja na faida za kiuchumi zinazopatikana.


Dirisha la udahili lafunguliwa NACTVET

$
0
0

 Na Mwandishi Wetu


BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limefungua dirisha la udahili wa mkupuo wa mwezi Machi kwa mwaka wa masomo wa 2023/24 kuanzia Januari 16 mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mtendaji wa Baraza hilo imesema kwamba vyuo vyote vinaruhusiwa kudahili wanafunzi katika mkupuo huu, isipokuwa vyuo vinavyotoa mafunzo ya Afya na Sayansi Shirikishi kwa Tanzania Bara.         

Taarifa hiyo imesema vyuo vya Afya na Sayansi shirikishi vilivyopo Tanzania Visiwani vyenye uwezo wa kudahili katika mkupuo huo vinaruhusiwa ikiwa vitakidhi vigezo.

Katika taarifa yake hiyo, NACTVET limevielekeza vyuo vinavyohitaji kudahili wanafunzi kwa mkupuo huu kutuma maombi yao kabla ya Januari 27, 2023 kwa kujaza fomu inayoonesha uwezo wa chuo kuendesha mafunzo na kuiwasilisha katika ofisi za Kanda za Baraza ambapo chuo husika kipo.

“Uwezo huo ni pamoja na kuwa na miundombinu na walimu wa kutosha kutoa mafunzo katika mikupuo miwili kwa mwaka (Machi na Septemba)” imesema sehemu ya taarifa hiyo. 

Baraza hilo limesema kwamba fomu ya maombi inapatikana katika tovuti ya Baraza hilo www.nacte.go.tz kwa kubofya fomu ya maombi ya udahili March Intake 2023/24.              


Zaidi ya watanzania 142 Wanufaika na ajira

$
0
0


Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Meridianbet Tanzania, Matina Nkurlu (kulia) pamoja na Meneja Maudhui ya mtandao wa kampuni hiyo, Twaha Ibrahim wakizindua duka la kampuni hiyo lililopo temeke eneo la Tandika Majaribio. Katikati ni Mhasibu wa duka hilo, Joyce Songalele. Kampuni hiyo imezindua jumla ya maduka 58 nchi nzima na kutengeneza ajira zaidi ya 142 kupitia maduka hayo.

Baadhi ya wateja wa kampuni ya Meridianbet wakishirikiana na Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu kukata keki ikiwa ni ishara ya Uzinduzi wa duka hilo  lililopo temeke eneo la Tandika Majaribio,Kampuni hiyo imefikisha maduka 58 na kutengeneza ajira zaidi ya 142 kupitia maduka hayo.
 


 NA MWANDISHI WETU

 

Zaidi ya watanzania 142 wamenufaika na ajira kupitia Meridianbet Tanzania, ikiwa ni moja ya ndoto ya kampuni hiyo inayotoa huduma za michezo ya kubashiri mtandaoni.

Akizungumza katika uzinduzi wa duka la Meridianbet lililopo Mtaa wa Tandika Majaribio, Temeke, Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Meridianbet Tanzania, Matina Nkurlu, alisema kuwa kama kampuni, wana malengo madhubuti ya kimkakati ya kutengeneza ajira za moja kwa moja kwa watanzania wengi wenye uhitaji mkubwa kwa sasa na kwa baadaye.

 

“Hatimaye leo tumezindua duka la Meridianbet hapa Mtaa wa Tandika Majaribio, Wilaya ya Temeke, baada ya uzinduzi wa duka hili, tunatumaini litatoa ajira zaidi kwa ndugu zetu ambao watafanya kazi hapa na maduka yetu mengine zaidi ya 18 yaliyopo maeneo tofauti hapa Tanzania.

 

“Mpaka sasa Kampuni ya Meridianbet inayotoa huduma za michezo ya kubashiri mtandaoni, imesaidia kutoa ajira kwa zaidi ya watanzania 142 ambao wanafanya kazi kwenye maduka yetu yaliyosambaa nchi nzima, ikiwemo hili la Max 25 hapa Tandika Majaribio,” alisema Nkurlu.

 

Alisema kuwa lengo kubwa la Meridianbet ni kuhakikisha wanatoa huduma bora na za uhakika kwa wateja wao, bila kujali jinsia, kabila, rangi wala rika ilimradi tu mteja awe ametimiza miaka 18 na kuendelea ambapo anaruhusiwa kujiunga na kampuni yao ambayo alisisitiza ni mabingwa nambari moja wa michezo ya kubashiri kwa sasa Tanzania.

 

Aliwashukuru wateja wao kwa kuwawezesha kufika hatua walipo sasa tangu wameanza kutoa huduma za kubashiri michezo mbalimbali kama soka na kasino.

 

Alizitaja huduma zinazotolewa na kampuni yao kuwa ni Odds bomba na kubwa zaidi kwa kila mechi na ligi zote, machaguo ya kila aina zaidi ya 1000 yanayopatikana kwa kutembelea tovuti yao ya www.meridianbet.co.tz.

“Kuna huduma moja inapendwa sana ya KUTURBO mkeka wako unapoona unaelekea kuchanika, hii pia ipo Meridianbet. Sio jambo dogo hili, bali ni hatua kubwa tunayopiga pamoja na wateja wetu,” alisisitiza Nkurlu.

 

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mmoja wa wateja wa kampuni hiyo, Jackson Kuchumu , alisema kuwa duka hilo litampunguzia gharama za kwenda umbali mrefu kubashiri.

“Duka hili litapunguza usumbufu wa kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya kubet. Hiyo nauli niliyokuwa natumia, sasa nitaongezea na kuweka dau kubwa zaidi ili nishinde pesa nyingi,” alisema.

Mteja mwingine, Hassan Juma, alisema: “Napenda huduma nyingi za Meridianbet, ikiwemo ile ya kuturbo kwani inanifanya niokoe dau langu endapo kuna timu inaelekea kuchana mkeka wangu, lakini pia machaguo mengi yananipa uhuru wa kuchagua kipi niweke na kipi niache.”

Nkurlu aliongeza: “Tangu mwaka 2019 tulianza kuzindua maduka taratibu ambayo yanamilikiwa na Meridianbet, tukianza na maduka ya Kariakoo, Manzese, Gongolamboto na maeneo mengine ya Jiji la Dar es Salaam, na mpaka leo Januari 26, 2023 ambapo ni miaka minne inatimia kwa kuzindua duka hili linalofikisha idadi ya maduka ya Meridianbet kutimia 58.

 

“Lakini pia hilo pekee halitoshi, Kampuni hii inayojitahidi sana kila siku kufungua fursa kwa kila mtu mwenye lengo la kufanya biashara na sisi, anapata nafasi hiyo, Meridianbet tumeamua kutoa uwakala wa maduka yetu jumla 39 yanayomilikiwa na mawakala wetu ambao nao kwa kushirikiana nasi wamekuwa wakitoa huduma nzuri kwa wateja wetu waliosambaa nchi nzima, na hii inatoa ishara ya namna ambavyo Meridianbet imepiga hatua kubwa kwa ukuaji na kudhihirisha ukongwe wetu.”

 

Aidha, alisisitiza kuwa lengo kuu la Meridianbet ni kuendelea kuzindua maduka mbalimbali na kutanua wigo mkubwa wa masoko kwa kuwafikia wateja wao kwa urahisi na kutengeneza wepesi wa kutoa huduma bora kwa kila mt una kuwatengenezea wananchi ajira.


Mico Halal, Wafanyabiashara wakutana kujadiliana Idhibati za Bidhaa Kongamano la Biashara Halal

$
0
0

 Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Taasisi ya Kimataifa ya Ithibati (Viwango) Mico imefanya Kongamano la Kwanza lililowakutanisha wafanyabiashara jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadiliana na kutoa elimu na kuweka wazi masoko ya bidhaa mbalimbali ya Biashara Halal


Akizungumza katika kongamano hilo jijini Dar es Salaam Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania Skeikh Hamid Jongo ameipongeza taasisi ya Halal kwa kuandaa kongamano hilo.

Amesema kuwa uwepo wa taasisi hiyo nchini ni jambo jema kwani imekuwa ni kiu ya muda mrefu kwa wafanyabiashara na Serikali.

Skeikh Jongo amebainisha kuwa uwepo wa taasisi hii nchini itasaidia kutoa uthibati kwa bidhaa mbalimbali hivyo kusaidia kupenya katika masoko ya ndani na nje na kuchangia pato la Taifa.

“Tumekuwa tukikosa soko la kuuza bidhaa, hivyo wafanyabiashara bidhaa zao zitathibitishwa kupitia Halal na hivyo kuongeza mapato kwa kwa Serikali,” amesema Sheikh Jongo.

Ameongeza kuwa taasisi hiyo itasaidia kupatikana kwa bidhaa bora kama vile za chakula, nguo na kadhalika kwa ajili ya afya njema za wateja.

Amesisitiza kuwa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) linaunga mkono na kupongeza  jambo hilo kwani litasaidia Mtanzania kula chakula safi, mavazi safi na hivyo kuwa na maisha mazuri.

Pia amesema kuwa wafanyabiashara wa Tanzania wamekuwa wakienda nchi zingine kwa ajili ya kufata ithibati ya bidhaa zao hivyo Halal itawarahisishia kupata ithibati ndani ya nchi.

“Kwa kupatikana kwa Taasisi ya Halal itasaidia na kuwezesha kuwa rahisi kwa wafanyabiashara kupata ithibati na kufanya biashara ndani na nje,” ameongeza Sheikh Jongo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TanTrade, Latifa Khamis amesema soko la Halal limekwenda kimataifa hivyo kupitia Halal wafanyabiashara watasaidiwa kujua bidhaa halali na zisizo halali ili kuweza kuhimili soko la ndani na nje.

“Kupitia taasisi hii wafanyabiashara hili waweze kufanya vizuri wanatakiwa kijua Halal ni nini, naomba waitumie sana Halal kwani itawapatia ithibati ya bidhaa zao,” amesema Latifa.

Mapema akiongea katika kongamano hilo Naibu Mkurugenzi wa Mico Halal, Muhamed Juma amesema kongamano hilo ambalo linafanyika kwa mara ya kwanza lengo lake ni kujadiliana, kubainisha, kuelimisha na kuweka wazi masoko.

Amefafanua kuwa kongamano hilo limewaleta pamoja wafanyabiashara na wasio wafanyabiashara kwa lengo la kujifunza na kupata ufahamu kuhusu Halal.

Kadhi Mkuu wa Dar es Salaam atoa ufafanuzi Majukumu ya Ofisi yake

$
0
0
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Kadhi Mkuu wa Dar es Salaam Sheikh Ramadhani Kitogo amewataka Waislam nchini kutambua Majukumu ya Ofisi za Makadhi  na kufuata miongozo wanayopewa katika uendeshaji wa mashauri yao.


Ameyasema hayo wakati akiongea na wanahabari ofisini kwake jijini Dar es Salaam na kuwataka Waumini na Waislamu kutambua Majukumu ya ofisi hizo yanaendeshwa kwa kufuata utaratibu.

Amebainisha kuwa suala hilo la uendeshaji limegawanyika katika mafungu matano ya kiuendeshaji ikiwemo Mirathi ya ndoa, Nyumba za wakfu Kutoa maelekezo ya kisheria yahusuyo uislamu sanjari na migogoro ya misikiti.

"Waislam wanahaja ya kubadili mitazamo ya kifikra kutambua ofisi hizi hazishughulikii utoaji wa talaka pekee bila kufuata utaratibu na miongozo iliyowekwa ikiwemo usuluhishi na utoaji wa maamuzi ya mashauri yao"

Amesema kwamba hatua hizo zikifuatwa hakutakuwa na malalamiko Wala manung'uniko Kwani kila Moja ataona haki imetendeka Kwa kujua Baraza linania nzuri ikiwemo vikao kuanzia ngazi ya Kata nyumbani hadi kufikia katika Ofisi hizo.

"Utakuta watu wanashindwa kufuata utaratibu wanatoa lawama za wazi Kwa mihemuko bila kujua Ofisi hizi zinaendeshwa Kwa mujibu wa sheria za dini tujenge hofu ya Mungu twende na utaratibu kuanzia ngazi zilizopo Ili kuwa rahisi Kutoa maamuzi yenye tija Kwa mashauri yao" Amesema Kadhi Kitogo.

Amesisitiza kuwa sio kila shauri linaloletwa ofisini kwake litolewe maamuzi hapo hapo bila kufuata utaratibu kwani huko ni kuwanyima haki stahiki ya kuwasikiliza wengine na kufanya maamuzi ya upande mmoja.

Ameongeza kuwa tuhumu za kwamba ofisi hiyo imekuwa haiwatendei haki wakinamama wanaoleta mashauri sio za kweli kwa mujibu wa uislamu tumekuwa tunaanzia ngazi ya malezi hadi makuzi na uislamu upo wazi kwa miongozo na utoaji haki.

"Haki katika uislamu zimebainishwa wazi katika Quran na Sunah ya Mtume Muhammad S.W.A  kwa mafundisho ya wazi katika sheria za kiislamu hivyo hakuna jipya ila utaratibu wao wa uendeshaji mashauri ni muhimu kufuatwa na wengi watambue utaratibu huo na kuuheshimu"



Watuhumiwa wa ujambazi waliouawa na Polisi kuzikwa na Halmashauri

$
0
0

Na Lydia Lugakila, Ngara

Halmashauri ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera kupitia idara ya Afya wamefanya mazishi ya watu wawili waliouawa na Jeshi la Polisi usiku wa kuamkia Januari 22, 2023 kwa madai ya kuhusika kwenye  tukio la ujambazi katika Kata ya Kasulo.

Afisa Afya wa wilaya hiyo Salum Kimbau amesema utaratibu wa kufanya mazishi ya watu hao umekamilika baada ya kukosa ndugu wa kutambua miili hiyo ya watu waliofariki kwa kupigwa risasi wakati wakijiandaa kufanya uhalifu.

Kimbau amesema Idara  ya Afya imesubiri  ndugu kujitokeza  bila mafanikio na kwamba miili hiyo imeharibika

Ameongeza kuwa kwa mujibu  wa sheria mtu akifariki na kukosa mtu kumtambua Halmashauri inaingia gharama za kufanya mazishi.

Hata hivyo kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani humo mapema Jumatatu wiki hii alibainisha kuwa watu hao wawili mara baada ya kuuawa walipekuliwa na kukutwa na Bunduki moja aina ya AK47 risasi 25 na mabomu mawili ya kurushwa kwa mkono

TWIJUKE AWAWAKIA WANAOBEZA SAFARI ZA RAIS DOKTA SAMIA

$
0
0


Naibu Katibu Msaidizi Siasa Habari na Mawasiliano Chama Cha Mapinduzi Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera

 

Na Lydia Lugakila Kyerwa

Naibu Katibu Msaidizi Siasa Habari na Mawasiliano Chama Cha Mapinduzi Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera Tulakila Twijuke amewakemea baadhi ya watu wanaosema juu ya  Safari za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan pamoja na kukopa.

Twijuke ametoa kauli hiyo katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) kilicholenga kujadili Rasmu ya Makadilio ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa fedha 2023/2024 kilichofanyika katika ukumbi wa Wilaya hiyo.

Amesema hadi Sasa hakuna Mtanzania ambaye hajaona au kunufaika na Safari za Rais Dokta Samia kwani zimesaidia  kuweiweka Nchi katika ushirikiano mzuri   na Mataifa ya nje.

"Nakerwa na wanaosema Mama anasafiri sana na anakopa na tajiri huwa anakopa, na Maskini wakubwa hawakopi kwa sababu hawana maono tupunguze maneno tuangalie matendo ya Kiongozi wetu" alisema Twijuke.

Amesema Tajiri mwenye maono lazima akope na asafiri hivyo wakumbuke Rais wetu halali kwa ajili ya Watanzania wote na matokeo yanaonekana.

Aidha amempongeza Rais Dokta Samia kwa namna alivyoiwezesha Wilaya hiyo kuwa na miradi mikubwa huku akiwahimiza wasimamizi wa miradi hiyo kuitunza kwani Serikali inatumia Gharama kubwa katika Miradi hiyo.

MIKOA YATAKIWA KUHAKIKISHA MASHINDANO YA RIADHA VIJANA YANAANZIA NGAZI YA WILAYA.

$
0
0

 

Kaimu Katibu Mkuu RT, Wakili Jackson Ndaweka.


NA TULLO CHAMBO, RT

SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), limeitaka mikoa yote nchini kuhakikisha inaendesha mashindani ya Vijana chini miaka 20 na 18 'U-20 U-18' kuanzia ngazi ya Wilaya.

Maelekezo hayo yametolewa na Kaimu Katibu Mkuu RT, Wakili Msomi Jackson Ndaweka, katika barua yake ya Januari 25 kwenda kwa viongozi wa vyama vya mikoa Tanzania Bara.

Amewaelekeza viongozi hao, kukumbuka kwamba kuna jukumu kubwa mbele yao, kwani mwaka huu una mashindano mengi ya vijana wa umri huo.

 Wakili Ndaweka, aliyataja mashindano hayo kuwa ni Afrika Mashariki U-18 na 20, Tanzania ikiwa mwenyeji, ambapo awali yalikuwa yamepangwa kufanyika Kigali, Rwanda.

Alisema, mashindano hayo yatafuatiwa na ya Afrika kwa umri huo Lusaka, Zambia Aprili 27 hadi Mei 3, 2023.

"Ili kuhakikisha nchi inashiriki kwa mafanikio mashindano hayo, lazima mashindano yaanzie ngazi ya Wilaya, kisha Mkoa na mwisho mashindano ya Taifa ya Wazi kwa vijana wa umri huo ambayo yanatarajiwa kufanyika Februari 25," alisema na kuongeza.

 Mashindano ya Wilaya yafanyike kati ya Februari 9-11 na Mikoa Februari 13-19.
 
"Utaratibu huu, unakusudia kuhakikisha wanapatikana wachezaji wenye uwezo mkubwa, ili kuleta tija katika ushiriki wa nchi kwenye mashindano ya kimataifa," alisema Wakili Ndaweka.

Sambamba na hilo, RT inakusudia na imejipanga kuhakikisha kuwa kalenda yake inafuatwa na matukio yote yanafanyika kama yalivyopangwa.

BUWEA KAGERA WAIOMBA SERIKALI KUWASHIKA MKONO

$
0
0


Mwenyekiti wa Bukoba Women's Empowerment Association Bi Regina Majaliwa akizungumzia Kikundi hicho.


Na Lydia Lugakila  Bukoba


Kikundi Cha Bukoba Women's  Empowerment  Association (BUWEA) Wameiommba Serikali kuwasaidia katika uwezeshaji ili wawafikie akina Mama Wengi na kuwakwamua kiuchumi na kuondokana na utegemezi katika  Familia zao.


Wakiongea na mtandao huu Januari 27, 2023 akina Mama hao wanajihusisha na shughuli mbali mbali za kiuchumi ikiwemo mradi wa usindikaji wa Vyakula akiwemo Bi Consolatha Emanuel, Recho Ndyamukama na Theodozia Rugangira wamesema kuwa tangu kikundi chao kianzishwe Mwaka 1996 yamekuwepo  manufaa makubwa kwa akina Mama hao ikiwa ni pomoja na kuisaidia jamii kupata lishe inayotokana na Soya upande wa Maziwa na Unga huku wakitaja  kuwa na changamoto ya kukosa watu wa kuwashika mkono hivyo kuiomba Serikali kuwaunga mkono ili wawe na akina Mama Wengi waliobobea katika Masuala ya uwekezaji na kujiinua kiuchumi.


Wameshukuru ubalozi wa Marekani hapa Nchini ambapo awali walitoa vyerehani na Baiskeli kwa ajili ya Wana Kikundi hao.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kikundi hicho Cha BUWEA Bi Regina Majaliwa amesema hadi sasa wanajivunia mafanikio yaliyopatokana kwani yamewakwamua baadhi ya akina Mama ambapo wamewezesha watoto wao kwenda Shule, wameboresha Makazi yao pamoja na kufanya Biashara   mbali mbali.


" Ili tufikie malengo tunaomba Serikali ituwezeshe maana tumeona Rais Dokta Samia amekuwa akituwezesha Watanzania upande wa  Miradi ikiwemo ya Maji sasa na Sisi Vikundi tunaomba atuangalie hasa akina Mama wa Hali ya chini kwani tayari tumeishaonesha Mwanga Kiuchumi" alisema Bi Majaliwa.


Ameongeza kuwa Kikundi hicho chenye wanachama zaidi ya 1,000 wamejipanga ki vingine katika kutoa Elimu kwa jamii kutumia Vyakula vitokanavyo na zao la Soya yenye kiini cha Protini.


Naye Godfrey Gaudioza anayefanya Shughuli za usindikaji mazao ya Soya yanayotokana na Mbegu ya Soya ameiomba Serikali kuwaboreshea uzalishaji huo ikiwemo kuwatembelea mara kwa mara.


Ameongeza kuwa ni vyema pia Serikali itoe Elimu ya umuhimu wa zao la Soya kwani lina lishe nzuri.


Hata hivyo Kikundi hicho kinapatikana mtaa wa Kafuti Kata Bakoba Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera na tayari kimehudumia wanachama katika baadhi ya Kata za Wilaya ya Bukoba ikiwemo Bujugo na  Kemondo na Kata nyinginezo za Wilaya hiyo.

NMB yatenga Bilioni 6.2 kwa ajili ya Uwekezaji katika Miradi ya Kijamii

$
0
0

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (kushoto), akipongezana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. Edwin Mhede (katikati), baada ya kuwasilisha muhtasari wa taarifa ya fedha ya Benki ya NMB kwa mwaka 2022 jijini Dar es Salaam. Katika hafla hiyo, Benki ya NMB ilitangaza faida ya bilioni 429 baada ya kodi. Kulia ni Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Juma Kimori. (Na Mpiga Picha Wetu).

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. Edwin Mhede.

 

Na Mwandishi Wetu
 

BENKI ya NMB imeendelea kuboresha rekodi yake ya kutengeneza faida baada ya mwaka jana kuongeza kwa kiasi kikubwa pato hilo na kuweza kutenga TZS bilioni 6.2 kwa ajili ya uwekezaji katika miradi yenye tija kijamii.


Kiasi hicho ni kikubwa kuwahi kutumika na taasisi yoyote humu nchini kusaidia kufadhili uwajibikaji kwa jamii (CSR) ni matokeo ya NMB kupata tena faida ya kihistoria ya TZS bilioni 429 baada ya makato ya kodi.


Akitangaza matokeo ya fedha ya NMB kwa mwaka 2022 jana jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu, Bi Ruth Zaipuna, alisema faida hiyo ilitokana na ufanisi wa mapato jumla yaliyovuka TZS trilioni 1 na kufikia TZS trilioni 1.2.


“Kutokana na mafanikio haya, sanjari na nafasi ya benki katika uchumi na jamii ya Kitanzania, Benki ya NMB inaendelea kuwa benki kiongozi katika maswala muhimu yanayoigusa jamii,” Bi Zaipuna alibainisha.


“Kwa muktadha huu, Benki ya NMB imetenga jumla ya kiasi cha TZS  bilioni 6.2 ili kusaidia miradi mbalimbali ya kijamii.  Kiasi hiki cha kihistoria ni ongezeko la zaidi ya asilimia 114 ukilinganisha na kiasi cha TZS bilioni 2.9 kilichotengwa na kutumika kwa mwaka 2022,” aliongeza.


Aidha, alisema fedha hizo ni kwa ajili ya kuleta matokeo makubwa na chanya kwenye maeneo ya afya, elimu, mazingira na mabadiliko ya tabia nchi kwa kushirikiana na wadau muhimu pamoja na serikali kupitia wizara husika.


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Dkt Edwin Nhede, alisema mara hii bajeti ya CSR imeongezewa ziada ya TZS bilioni 2 kwa ajili ya mazigira na maswala ya tabia nchi kwani maeneo hayo ni nyeti sana kwa NMB.


Tofauti na mwaka huu, sera ya NMB ni kutenga asilimia moja ya faida baada ya kodi kwa ajili ya kuwekeza kwenye shughuli za kijamii na kurudisha fadhila kwa wanannch wanaochangia mafanikio yake.


“Utendaji huu muhimu kifedha na kujitolea kwa kiasi kikubwa sana kuendeleza ustawi wa jamii, kunadhihirisha jinsi Benki ya NMB inavyozingatia kwa makini ajenda ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Tanzania, pamoja na kuimarisha nafasi yake ya uongozi sokoni,” ilibainisha taarifa kwa vyombo vya habari.


Bi Zaipuna alisema moja ya sababu za mafanikio kiutendaji mwaka 2022 ni mazingira rafiki ya kibiashara yaliyotokana na sera wezeshi za serikali. Alibainisha kuwa mafanikio hayo ni ushahidi wa kasi ya ufanisi mkubwa wa NMB katika kipindi cha miaka minne na umuhimu wa huduma zake bora kimaisha na kiuzalishaji.


Alisema faida ya TZS bilioni 429 baada ya kodi ilikuwa ni ongezeko la asilimia 47 ukilinganisha na ile ya TZS 290 bilioni ya mwaka 2021. Hili lilikuwa ongezeko la zaidi ya TZS bilioni 130 ndani ya mwaka moja na ukuaji mkubwa sana ukilinganisha na faida ya TZS bilioni 98 mwaka 2018.


Faida kabla ya kodi nayo iliongezeka kwa asilimia 47 kutoka TZS bilioni 414 hadi TZS bilioni 617.
NMB ilianza kupata faida za kihistoria mwaka 2020 baada ya pato hilo lililokatwa kodi kuvuka TZS bilioni 200 huku mwaka uliofuata rekodi hiyo iliboreshwa kwa asilimia 41.


Sambamba na juhudi za kuongeza ukopeshaji, mali jumla za benki hiyo nazo pia zilivuka kiasi cha TZS trilioni 10 na kuwa TZS trilioni 10.25, huu ukiwa ni ukuaji wa kasi wa mizania wa asilimia 18 kwa mwaka mzima.


Mafanikio mengine makubwa yaliyopatikana mwaka jana ni kufanikiwa kuboresha mali za benki kupitia usimamizi mzuri wa ukopeshaji. Tengo kwa ajili ya mikopo chechefu lilipunguzwa kwa asilimia 33 hadi TZS bilioni 76 huku uwiano wa mikopo hiyo wa asilimia 3.3 ukibaki ndani ya kiwango cha kikanuni cha asilimia tano.


Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa Fedha, Bw Juma Kimori, alisema NMB imekuwa ikifanya vizuri kiutendaji tangu mwaka 2018 na hilo linaonekana vizuri kwenye ukuaji wa mizania yake.
Mtaalamu huyo alisema thamani ya mali za benki hiyp ambayo sasa imefikia zaidi ya TZS trilioni 10 ilikuwa ni TZS trilion 5.5 miaka minne iliyopita. Nazo amana za wateja, aliongeza, sasa hivi ni TZS trilioni 7.5 kutoka TZS trilioni 4.2 miaka mitatu iliyopita.


Mikopo iliyotolewa mwaka jana hasa kwa ajili ya makampuni, watu binafsi na uwekezaji katika sekta za kimkakati ikiwemo kilimo pamoja na biashara ndogondogo na za kati ilifikia TZS trilioni 6 ukilinganisha na TZS trilioni 3.2 mwaka 2018.


“Mizania yetu iko imara na mtaji kutoka kwa wana hisa amboa sasa ni TZS trilioni 1.6 una maana kubwa sana kwetu katika kuendeleza ufanisi ambao tumekuwa tunaupata miaka ya hivi karibuni, kuongeza ukopeshaji na kendelea kutengeza faida,” Bw Kimori alisisitiza.

TAASISI YA JAKAYA MRISHO KIKWETE FOUNDATION KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUBORESHA UTOAJI WA ELIMU NCHINI

$
0
0


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JKMF) Rais Msaafu Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika Kikao kilicholenga kuboresha utoaji wa elimu nchini, Leo tarehe 27 Januari 2023 jijini Dodoma. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na  Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JKMF) Rais Mstaafu, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na  Kaimu Mkurugenzi wa ElimuMsingi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bi. Suzan Nusu (kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi Jakaya Mrisho Kikwete Foundation, Vanessa Anyoti (wa tatu kulia), Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Bi Albina Chuwa (wa pili kulia). Leo tarehe 27 Januari 2023 jijini Dodoma. 



Na Eliud Rwechungura - OR TAMISEMI


Ofisi ya Rais - TAMISEMI inatarajia kuanzisha ushirikiano na Taasisi Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JKMF) unaolenga kuanzisha mpango maalum wa kutoa ajira ya muda mfupi kwa walimu wa kujitolea watakaofundisha Shule za  msingi za Serikali kwa kipindi kisichopungua miaka miwili.


Lengo hilo la ushirikiano limejadiliwa leo katika kikao cha pamoja kati ya Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya JMKF, Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI kilichofanyika Dodoma leo tarehe 27 Januari 2023.


Katika kikao hicho, pamoja na mambo mengine , Mhe. Dkt. Kikwete ameishauri Ofisi ya Rais TAMISEMI katengeneza kanzidata ya Walimu wote wanaojitolea nchini na kuandaa muongozo wa utakaosimamia mchakato wa kuwapata walimu wa kujitolea na kuratibu maslahi yao. 


Mhe. Dkt. Kikwete ameelezea utayari wa Taasisi ya JMKF kushirikiana kwa karibu na Serikali kutekeleza mpango huo ambao tayari Taasisi hiyo imejipanga kuanza kuutekeleza kwa kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) na wadau wengine.


Kupitia kikao hicho, Mhe Dkt Kikwete aliomba Serikali iweke utaratibu mzuri wa kuwaajiri walimu wa kujitolea watakaomaliza muda wao wa kujitolea ili kufanya mpango huo uwe endelevu.


Waziri Mhe. Angellah Kairuki alimweleza pia Mhe. Dkt. Kikwete kuwa Ofisi ya Rais TAMISEMI imejipanga kuboresha sekta ya elimu kwa kuanzisha utoaji elimu kidijitali kwa kuanzisha maabara za TEHAMA katika shule zote za Serikali hapa nchini, ambapo kwa kuanzia shule mpya zote zinazojengwa zitaunganishwa na mfumo wa intaneti ili kufikia lengo hilo. 



Aidha, Waziri Angellah Kairuki alipongeza Taasisi ya JMKF kwa kuanzisha programu ya kutoa elimu kidijitali na kuwa tayari kushirikiana na Serikali katika eneo hilo.


Waziri Kairuki alihitimisha kwa kuishukuru Taasisi ya JMKF kwa jitihada zake za kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita katika kuendeleza na kuboresha sekta ya elimu nchini na ameahidi  kuwa Ofisi ya Rais TAMISEMI itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Taasisi hiyo na wadau wengine wa sekta binafsi na washirika wa maendeleo wanaoiunga mkono Serikali katika kuimarisha sekta ya elimu.

NMB kupeleka washindi 8 Dubai kupitia Droo ya ‘Grand Finale’

$
0
0


Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Wami, Harold Lambileki (kushoto) akimkabidhi kadi ya pikipiki mshindi wa Pikipiki katika droo ya NMB MastaBata Kote-Kote, Aidan Stephen Lukindo (katikati) kutokea Morogoro. Kulia ni Meneja Kituo cha Biashara NMB Tawi la Morogoro, Hamis Rashid. Benki ya NMB imeshatoa Pikipiki kumi na 14 mpaka sasa zikiwa ni zawadi kwa wateja wa NMB wanaofanya malipo kupita NMB mastercard au Lipa Mkononi (QR) katika msimu huu wa MastaBata.

Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Wami, Harold Lambileki (katikati), akibonyeza kitufe cha kompyuta wakati wa kuchezesha droo ya  Kampeni ya NMB MastaBata Kote-Kote iliyofanyika mkoani Morogoro. Kushoto ni Mkaguzi wa Michezo ya Kubahatisha, Joram Mtafya na kulia ni Meneja Kituo cha Biashara Tawi la Wami, Hamis Issa.

 

Na Mwandishi Wetu

 

Ikiwa zimesalia siku 3 tu kuelekea ‘Grand finale' ambapo tutashuhudia wateja 8 wakijishindia safari ya kwenda Dubai kwa siku 4 huku benki ya NMB ikiwalipia kila kitu, benki hiyo iliendesha droo ya wiki ya mwisho ya kampeni ya NMB #MastaBataKoteKote katika Manispaa ya Morogoro kwenye tawi la NMB - Wami

Kwenye droo za kila wiki, washindi 75 wamekuwa wakinyakua TZS 100,000 kila mmoja na wa 76 akishinda pikipiki aina ya Boxer. Hii imepelekea jumla yao katika droo zote 10 za kila wiki kuwa 760.

Thamani ya zawadi walizoshinda ni pamoja na TZS milioni 75 pesa taslimu kwa washindi 750 na TZS milioni 30 za Boxer 10. Jumla ni TZS milioni 105 na thamani ya zawadi zote za shindano hili la kuchagiza malipo kidijitali ni zaidi ya TZS milioni 300.

Kabla ya zoezi la kuwapata washindi wa mwisho 76 wa kila wiki, Meneja wa Tawi la NMB Wami, Bw Harold Lambileki, alisema droo ya kuwapata washindi wa kwenda Dubai itafanyika makao makuu ya benki hiyo wiki ijayo jijini Dar es Salaam.

Meneja huyo alisema kila mteja wa NMB anayefanya miamala yake kwa kutumia NMB Mastercard na Lipa Mkononi (QR) anayo nafasi ya kushinda zawadi ya safari ya Dubai huku wanaochanja sana na kulipa zaidi kidijitali wakiwa na nafasi kubwa ya kuibuka kidedea.

Hata wewe unaweza kuibuka mshindi kwenye droo ya ‘Grand Finale’ wiki ijayo hivyo, usiache kadi yako ya NMB mastercard nyumbani kufanya malipo ya matumizi yako au kwa kuscan QR kujiweka katika nafasi ya kuweza kuwa mmoja wa washindi wa #MastaBataKoteKote

 

 



TANZANIA COMMERCIAL BANK YATOA MSAADA WA MIFUKO 100 YA SARUJI KUKAMILISHA UJENZI WA ZAHANATI YA KATA YA GOWEKO

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhusiano wa Tanzania Commercial Bank TCB, Bi Chichi Banda (kulia), akikabidhi sehemu ya msaada wa mifuko 100 ya saruji kwa Diwani wa kata ya Goweko Mhe. Shaban Katalambula iliyotolewa na TCB kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa kituo cha afya katika kata hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhusiano wa Tanzania Commercial Bank TCB, Bi Chichi Banda akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mifuko 100 ya saruji iliyotolewa na Benki hiyo kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa kituo cha afya katika kata hiyo.

TCB imeunga mkono jitihada zilizoanzishwa na wanakijiji wa kata hiyo kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Uyui mkoani Tabora. Kwa muda mrefu wananchi wa kata ya Goweko wamekuwa wakitembea umbali mrefu kwa ajili ya kupata huduma za afya, hivyo kwa msaada toka benki ya TCB itawezesha kutatua changamoto hizo kwa wananchi hao.

Katika kuhakikisha kuwa Tanzania Commercial bank TCB inaendelea kuwakaribu zaidi na watanzania ambao ndio wateja wake wakubwa, Iimeunga mkono juhudi za Wananchi wa kata ya Goweko kwakukabidhi msaada wa mifuko 100 ya Saruji.

Akikabidhi msaada huo, Mkuu wa kitengo cha Mahusiano na Uhusiano wa Benk ya TCB, Bi Chichi Banda alisema kuwa Tanzania Commercial Bank kama ilivyokawaida yake imeguswa na imefanya maana inaamini hawa wananchi ndio wateja wa benki.

leo tunakabidhi msaada wa mifuko 100 hapa kwaajili yakukamilisha ujenzi wa kituo cha afya lakini pia hatukuishia hapa tumekabidhi mifuko 100 mingine kwa Diwani wa Kata ya kiburugwa Mbagala Dar es salaam kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo cha polisi cha kata hiyo".

Pia tukatambua umuhimu wa sekta ya elimu nako tumeweza kutoa mifuko 150 ya saruji katika Shule ya Msingi Ikamba iliyoko wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam kwaajili yakufanya maboresho ya madarasa.

tunawapongeza sana wakazi wa hapa kwakuona kuwa swala la afya sio la serikali pekeyake hivyo sisi kama TCB tumeguswa sana tumeona tuje hapa kusaidiana na wananchi kwa hali na mali kwani nyinyi ni sehemu yetu na sisi ni sehemu yenu,"

Tanzania Commercial Bank ni benki pekee nchini yenye mtandao mpana wamatawi na mawakala nchi nzima hivyo niwasihi ndugu wananchi muitumie Benki ya TCB kwani inabidhaa bora na rafiki.

UTT AMIS YADHAMINI BONANZA LA WABUNGE

$
0
0

 




 


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson wameipongeza Kampuni ya UTT AMIS kwa kudhamini Bunge Bonanza 2023 lililowashirikisha Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar pamoja na watumishi wa Bunge.

Walitoa pongezi hizo wakati wa hafla ya kukabidhi medali na vikombe kwa washindi wa michezo mbalimbali katika Bonanza hilo lililofana na kufanyika kwenye viwanja vya Shule ya John Merlin, Miyuji Jijini Dodoma Januari 28, 2023 ambapo ushindi wa jumla walipata wabunge.

JOWUTA yapata viongozi wapya, Serikali yaahidi ushirikiano

$
0
0



Mwandishi Wetu, Dodoma



CHAMA cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA) kimepata viongozi wapya ambao wataongoza chama hicho kwa miaka mitatu katika mkutano Mkuu uliofanyika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Viongozi wapya wa chama hicho, wamechaguliwa juzi katika mkutano  Mkuu wa JOWUTA  ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Technolojia ya habari, Mhandisi Kundo Methew.



Viongozi wengine waliohudhuria ni Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi nchini, Pendo Perege, Maofisa Kazi Wandamizi kutoka Ofisi ya Kamishna Kazi Makao Makuu Dodoma, Honesta Ngolly na Musa Msami, Naibu Mkurugenzi Idara ya Habari ya Maelezo, Rodney Thadeus na Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini (UTPC) Kenneth Simbaya.



Mkutano Mkuu wa huo wa pili wa JOWUTA , ulidhaminiwa na Mamlaka ya Bandari nchini(TPA), Mamlaka ya Mwasiliano (TCRA) Mfuko wa Hifadhi kwa Watumishi wa Umma ( PSSSF ), Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Taasisi ya Wanahabari ya (MAIPAC).

Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi huo, Honesta Ngolly kutoka Ofisi ya Kamishna wa Kazi Makao Makuu, alimtangaza  mwandishi mwandamizi wa magazeti ya Mwanachi Communication Ltd, Mussa Juma kushinda  nafasi ya Mwenyekiti wa JOWUTA baada ya kupata kura 58 kati ya 61 mbili zikiharibika na moja ya hapana na alikuwa   mgombea pekee.

Ngolly alimtangaza  Saphia Ngalapi kushinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti baada ya kupata kura 42 dhidi ya Bahati Nyakiraria aliyepata kura 18, wakati Selemani Msuya alichaguliwa tena kuwa Katibu Mkuu baada ya kupata kura 42 dhidi ya Mike Mande aliyepata kura 19.

Katika Uchaguzi huo, Lucy Ngowi alishinda nafasi ya Mwekahazina kwa kupata kura 49 dhidi ya Christina  Mwakangale aliyepata kura 12.

Ngolly alimtangaza Said Mmanga kushinda nafasi ya Naibu Katibu Mkuu baada ya nafasi huyo wagombea kuingia katika duru ya pili, Mmanga alipata kura 33 dhidi ya kura 26 za Robinson Wangaso ambapo awali Sangito Msafiri alipatakura tisa.



Katika uchaguzi huo pia walichaguliwa wajumbe watatu wa bodi ya udhamini ambao ni Rutta Robert alipata kura 51,Tausi Mbowe aliyepata kura 43 na Claud Gwandu kura 27.

Akizungumza baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti Juma, ambaye pia ni Mkurugenzi MAIPAC, aliahidi kushirikiana na viongozi wengine na Serikali kudai maslahi bora kwa wanahabari.

Juma alisema kwa kuzingatia sheria JOWUTA itaungana na Serikali na wadau wengine kuhakikisha waandishi  wanaofanyakazi kuwa na mikataba ya kazi, kuwa na bima na kuwataka waandishi nchini kujiunga na JOWUTA.

"Lakini pia kama ambavyo alishauri Msajili wa vyama tutahakikisha ndani ya muda mfupi tunakuwa na mkakati wa kazi (Strategy plan) Ili JOWUTA iweze kuwa na sehemu ya kuanzia kufanya kazi na kuwa na vyanzo vya uhakika vya mapato.

Katika mkutano huo, kila mkoa ulichagua mjumbe mmoja wa baraza la wafanyakazi na mjumbe mmoja kila Kanda kuungana na katika utendaji wa kazi.

Seif Mangwangi alichaguliwa kuwa mjumbe wa kamati Utendaji kutoka Kanda ya Kaskazini, Latifa Ganzel Kanda ya Mashariki na Grace Mwakalinga Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Wengine ni Robinson Wangaso Kanda ya Ziwa, Mwajabu Hoza Kanda ya Magharibi, Editha Majura (Kanda ya Kati).

Waliochaguliwa kuwakilisha mikoa ni Nasra Abdalah (Dar es Salaam) Emmanuel Ibrahim(Geita) Witney Joseph (Mara) Veronica Ignatus (Arusha) Rehema Cleopas (Tabora) na Msafiri Sangito (Pwani), Ashura Kazinja (Morogoro), Bahati Nyakiraria (Kilimanjaro) na Asha Mwakyonde (Dodoma).

Wengine waliochaguliwa kuwa wajumbe wa baraza ni pamoja na Elizabeth Nyivambe (Mbeya) Beatha Yosam (Njombe) na Adela Madyane (Kigoma).


Akifungua Mkutano huo kwa niaba ya mgeni rasmi, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo, Rodney Thadeus alisema Serikali itashirikiana na JOWUTA na akataka waandishi wa habari nchini kujiunga na JOWUTA Ili iwe rahisi kutatua changamoto zao.

Kwa upande wake Msajili wa vyama vya wafanyakazi Pendo Perege alipongeza JOWUTA kufanya mkutano Mkuu kwa kuzingatia sheria na taratibu na kuahidi kushirikiana na chama hicho Ili kuwasaidia wanachama wake.

Mkurugenzi wa UTPC Kenneth Simbaya aliahidi UTPC kushirikiana na JOWUTA na kueleza tayari wameingiza JOWUTA katika mpango kazi wake kwa kuzingatia bila maslahi bora kwa waandishi hata uhuru wa habari haitakuwa na faida kubwa.

Magazeti ya Tanzania Januari 30, 2023

Maeneo zaidi ya 30 ikiwemo Hospitali ya Taifa Muhimbili kukosa maji kwa saa 36

$
0
0

 
Na Janeth Jovin



MAENEO zaidi ya 30 yaliyopo jijini Dar es Slaam na Pwani ikiwemo Hospitali ya Taifa Muhimbili yanatarajiwa kukosa maji kwa saa 36 kutokana na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu chini uliyopo Bagamoyo kuzimwa leo Jumatatu Januari 30, 2023.


Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Kitengo wa Mawasiliano cha Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) imeeleza kuwa mtambo huo utazimwa lengo ni kuruhusu kazi ya kusafisha mifumo yote ya mtambo ikiwemo machujio, matanki na mabomba makuu yote ya kusafirisha maji kutoka katika mtambo huo.


"Kutokana na kazi hiyo maeneo yanayohudumiwa na mtambo huo yatakosa huduma za maji kuanzia Jumatatu (leo) Januari 30,2023 hadi Jumanne jioni," ilieleza taarifa hiyo


Taarifa hiyo imetaja maeneo yatakayoatjiriwa mbali na Hospitali ya Taifa Muhimbili mengine ni Mwananyamala, Kinondoni,  Buguruni,  Vungunguti, Ilala, Katikati ya mji,Msasani, Masaki, Osterbay, Mikocheni, Kijitonyama, Lugalo, Kawe, Makongo, Keko, Kurasini, Magomeni, Kigogo


Maeneo mengini ni Mji wa Bagamoyo,  MapingaZinga, Kerege, Mabwepande, Bunju, Kunduchi, Chang'ombe, Teresa, Mbezi Beach, Mbweni, Boko, Salasala, Goba, Kunduchi, Mivumoni, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Uwanja wa Ndege, Mwenge, Lugalo pamoja na Kiwalani.


Aidha taarifa hiyo ilieleza kuwa Dawasa inawaomba wananchi kukumbuka kuhifadhi maji ya kutosha ili kuweza kuyatumia katika kipindi chote cha matengenezo.


Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>