Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

SMZ, SMT wakaa meza moja kujadili sekta ya ujenzi

$
0
0

 

Mashirikiano ya Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya  Makaazi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) yanatarajiwa kuibua kasi ya kiutendaji  katika sekta ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu ili wananchi waweze kudhimudu.

Akizungumza Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi (SMZ) Dkt. Mngereza Mzee Miraji katika kikao cha mashirikiano ya kiutendaji kilichofanyika mwisho wa wiki iliyopita  katika ukumbi wa Wizara hiyo  Maisara Unguja, alisema kupitia vikao  vya mashirikiano baina sekta mbili hizo vitasaidia katika kuibua kasi ya utendaji hasa katika sekta ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu zenye kukidhi mahitaji ya wananchi wenye kipato tofauti.

Alisema kwamba kunamafanikio yameanza kuonekana kupitia vikao hivyo ikwemo kukamilika rasimu mbili ya makubaliano (MOU) zimekamilika kiutendaji ambapo zitarajiwa kusainiwa katika kikao kijao cha ngazi ya mawaziri wa pande zote mbili wa wizara ya Ardhi ya SMZ na SMT.

Dkt Mngereza alifafanua kwamba ‘MOU’ zilizokamilika ikiwemo ya Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC) na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na ‘MOU’ inahusu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi (SMT) ambapo kuna mambo mengi ya ushirikiano wamekubaliana ikiwemo ngazi ya kitalaamu, kubadilishana uzoefu pamoja na mafunzo kwa watendaji wa taasisi mbili hizo.

Pia alisema wizara ya Ardhi ya SMT imepiga hatua zaidi kiutendaji ambapo wanamfumo unayojulikana kwa jina la Intergreted Land Information System unasaidia kutatua changamoto ya urasimu pamoja na kuboresha huduma hivyo wizara yake kupitia Idara ya Kamisheni ya ardhi  imeanza maandalizi ya kuwa na mfumo huyo na wamefika katika hatua nzuri.

Sambamba na hayo Dkt Mngereza alisema wamekubaliana wawe na mashirikiano ya tafiti katika sekta ya ardhi na makaazi ya bei nafuu lakini katika kuanzia hilo watakuwa na kamati ya pamoja (Joint committee) ambayo imeshaingizwa katika mazungumzo ya yanayoendelea baina ya  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na taasisi ya Shelterafrique.

Alifahamisha kwamba taasisi ya Shelterafrique   inautaratibu wa kutoa mikopo ya bei nafuu kwa nchi wanachama zaidi ya nchi 30 na mwaka huu wanatarajia kutakua na mkutano  pamoja na maonesho ya teknolojia ya ujenzi wa maakazi ya bei nafuu.

Aidha Dkt Mngereza alisema wizara yake inakabiliwa na changamoto ya wataalamu wa upimaji ardhi ndani ya maji (Hydrographic Survey) hivyo wamekubaliana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi SMZ watakuwa na mpango mkakati wa kuwajengea uwezo  watendaji wao ambapo kila wizara italazimika kuingiza katika bajeti yake.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi (SMT) Dkt. Allan H. Kijazi alisema watahakikisha wanaweka misingi imara kwa watanzania wote kumiliki nyumba za bei nafuu na kuendeleza matumizi ya ardhi bila ya kuangalia tofauti yoyote.

Alieleza kwamba matarajio ya kikao hicho ni kuwa na mifumo ya pamoja ya uboreshwaji wa utoaji huduma kwa viwango vinavyofanana baina ya Taasisi mbili hizo kwa lengo la kukidhi mahitaji ya Taifa.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu Shirika la Nyumba Zanzibar(ZHC)Mwanaisha Ali Saidi  kupitia kikao hicho aliwaahidi wananchi wategemee mabadiliko katika sekta ya maakaazi nakusemba kwamba  Shirika lake limejipanga kimkakati katika kuhakikisha linatoa huduma ya nyumba bora na salama kwa bei nafuu.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemiah Kyando Mchechu alisema Shirika hilo kwa sasa limejikita zaidi kwenye miradi  ya ujenzi ambapo ndio kipamumbele chake kujenga nyumba katika jiji la Dar es salaam, Dodoma na maeneo ya miji na nyumba hizo ni za ghoroma na   bei nafuu.

Kwa upande wa watendaji waliyoshiriki kikao hicho wamezipongeza Serikali zote mbili(SMZ na SMT)  kwa kuagiza kuweko na mashirikiano ya kiutendaji katika Taasisi ambazo zinalingana kimajukumu na hazimo katika orodha ya sekta ziliyomo katika Muungano.


RAIS WAPONGEZA VIJANA WA KITANZANIA KWA KUPATA MEDALI YA FEDHA

$
0
0


 *Ni baada ya kuibuka washindi wa pili katika mashindano ya ubunifu duniani


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipewa maelezo na moja ya kijana Mtanzania aliyeshiriki mashindano ya ‘global robotic challange’ Maria Mtega, kuhusu roboti iliyoundwa na vijana wa Kitanzania ya kukamata hewa ukaa (Carbon dioxide), kwenye Ukumbi wa Ofisi Ndogo za Waziri Mkuu Magogoni Jijini Dar es Salaam Januari 15, 2023. Mashindano hayo yalifanyika nchini Geneva Uswisi na kujumuisha zaidi ya Mataifa 190. Katikati ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

 

 

MHESHIMIWA Rais Dkt. Samia Suluhu Hssan amewapongeza vijana wa Kitanzania walioibuka washindi wa pili na kupata medali ya fedha katika mashindano ya kwanza ya Global Robotics Challenge yaliyofanyika Geneva Uswisi na kushirikisha mataifa zaidi ya 190. 

Amefarijika kusikia kuwa roboti iliyoundwa na vijana kutoka Tanzania chini ya maudhui ya kukamata hewa ukaa (Carbon dioxide) inaweza kusaidia kusafisha kaboni hewani na kusaidia kupunguza ongezeko la joto kwenye angahewa ya Dunia.

Kauli hiyo imetolewa leo (Jumapili, Januari 15, 2023) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia katika hafla ya kuwapongeza vijana hao iliyofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.

Amesema hayo ni mafanikio makubwa na Watanzania wote wanapaswa kujivunia kwa kuiwakilisha nchi yetu vizuri. “Nitumie nafasi hii kuwaahidi kuwa Serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari itaendelea kufuatilia maendeleo yenu na kuona namna ya kuendeleza vipaji vyenu. ”

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuielekeza Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari iandae mpango wa kuwa na vituo vya ubunifu nchini katika ngazi za Mikoa na Wilaya mbalimbali ili kusaidia kuinua vipaji vya vijana.

Amesema Wizara iimarishe utaratibu wa kuwatambua na kuwaendeleza wabunifu mbalimbali ili kuwamotisha na kukuza ajira nchini na ishirikiane na mamlaka husika kuandaa utaratibu wa kuwasaidia wabunifu mbalimbali na kuwaunganisha na taasisi pamoja na makampuni kwa ajili ya kuendeleza bunifu za kazi zao kulingana na mahitaji.

Vilevile Waziri Mkuu ameielekeza Wizara hiyo na mamlaka husika zijipange kuwekeza katika kulinda usalama wa taarifa za watumiaji wa mifumo mbalimbali ya TEHAMA sambamba na  kutoa elimu kuhusu usalama sahihi wa vifaa na matumizi salama ya mifumo ya kompyuta.

Amesema Wizara hiyo kupitia Tume ya TEHAMA ifanyie kazi vikwazo mbalimbali vya kisera na kikodi vinavyoleta changamoto kwa wabunifu katika masuala ya TEHAMA na matokeo ya bunifu mbalimbali yawekewe utaratibu wa  kubidhaishwa/kupata soko badala ya kuwekwa maktaba.

Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ameipongeza Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo kwa kuamua kutumia sehemu ya mapato yao kwa kuwasaidia vijana wa kike nchini katika kuendeleza bunifu nchini kupitia APPS and Girls.

Waziri huyo mesema kuwa takwimu mbalimbali zinaonesha kuwa ushiriki wa mabinti na wanawake katika matumizi ya TEHAMA si mzuri sana, Barani Afrika asilimia 24 tu ya wanawake wanashiriki kwenye TEHAMA huku wanaume ni asilimia 35.

Tanzania ukienda mashuleni watu wanaosoma Computer Science na mambo yanayohusiana na TEHAMA wanawake ni asilimia 10 tu, ni muhimu kuendelea kuongeza nguvu katika kupunguza pengo hilo. ”

Naye, Afisa Mkuu wa Udhibiti Kampuni ya MIC Tanzania PLC (TIGO), Innocent Rwetabula amesema kampuni yao inafanya kazi kwa kuzingatia vipaumbele vya Serikali kwa sekta ya mawasiliano na kuongoza safari ya kidigitali hadi kufikia Tanzania ya kidigitali.

Amesema uwezeshaji wa wasichana ni mojawapo ya programu zao kuu za uwajibikaji kwa jamii kwa lengo la kuwawezesha wasichana walio katika shule za sekondari na wale walioacha shule kwa sababu mbalimbali wenye umri wa kuanzia miaka 12 hadi 24 kupata ujuzi wa kidigitali na stadi za ujasiriamali.

Amesema lengo la ufadhili huo ni kuziba pengo kati ya wavulana na wasichana katika sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM), kutoa ujuzi na stadi za ujasiriamali kupitia utoaji wa mafunzo ya TEHAMA, ushauri na uanzishaji wa biashara mpya za kiteknolojia ambapo mwaka jana wasichana 1,590 walinufaika na mpango huo.

Akizungumzia kuhusu shindano la kwanza ya Global Robotics Challenge amesema hufanyika kila mwaka kwa mtindo wa Olimpiki na kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa ni cabon capture, ambayo ni mchakato wa kukamata hewa ukaa iliyopo na kuzuia isiingie angani. Kundi la wanafunzi watano kati ya 11 waliiwakilisha nchi na kupata nafasi ya pili.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Maria Mtega ambaye anasoma kitado cha pili shule ya sekondari ya St.Theresa amesema anashukuru kwa mafunzo waliyoyapa ambayo yamewezesha kupata nafasi ya pili na pia wataendeleza vipaji vyao na hatimaye waweze kuwa wabunifu wakubwa nchini.

 NAIBU WAZIRI MASANJA AONGOZA KIKAO CHA KUPITIA TAARIFA YA UTENDAJI KAZI WA NGORONGORO

$
0
0

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja, ameongoza kikao kazi cha watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia taarifa ya utendaji kazi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kipindi cha mwezi Januari 2021 hadi 2022 leo Januari 16,2023 jijini Dodoma.


Abdallah Hussein Bingwa Pool, miaka 59 ya Mapinduzi

$
0
0

 

Abdallah Hussein akifurahia kitita cha pesa taslimu shilingi 250,000/= mara baada ya kuibuka Bingwa wa mashindano ya Pool ya Maadhimisho ya miaka 59 ya  ya Mapinduzi yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Klabu ya Snipers Mwenge Mpakani jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi wa Snipers Klabu, Willfred Makamba mara baada ya kumkabidhi mshindi huyo.

Bingwa wa mashindano ya Pool ya Maadhimisho ya miaka 59  ya Mapinduzi, Abdallah Hussein akifurahia Medali ya Dhahabu, Pesa taslimu shilingi 250,000/=  pamoja na tuzo maalumu ya mashindano hayo yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Klabu ya Snipers Mwenge jijini Dar es Salaam.

 

Dar es Salaam, Tanzania

 

MCHEZAJI wa Pooltable kutoka Klabu ya Snipers yenye makazi yake Mwenge Mpakani jijini Dar es Salaaam, Abdallah Hussein ameibuka Bingwa kwenye Mashindano ya mchezo wa Pool katika kuadhimisha miaka 59 ya Mapinduzi na hivyo kuzawadiwa  Medali ya Dhahabu, Pesa taslimu Shilingi 250,000/= pamoja na tuzo maalumu ya mashindano hayo yaliyomalizika mwishoni mwa wiki Snipers Klabu Mwenge jijini Dar es Salaam.

 

Abdallah Husein ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Pooltable alipata ubingwa huo kwa kumfunga Jackson Steven 9 – 6 katika fainali ilifanyika katika Klabu ya Snipers Mwenge Mpakani iyojumuisha wachezaji 32 wa Jijiji la Dar es Salaam kuadhimisha miaka 59 ya Mapinduzi.

 

Jackson Steven alikamata nafasi ya pili ambapo alizawadiwa Medali ya Dhahabu pamoja na Pesa taslimu Shilingi 100,000/=

 

Mshindi wa tatu katika Mashindano hayo ni Patrick Nyangusi ambaye alipata nafasi hiyo kwa kumfunga Charles Venance kwa penati ya 7 – 6 na hivyo kuzawadiwa Medali ya Dhahabu na Pesa taslimu Shilingi 40,000/=

 

Patrick Nyangusi pamoja na kukamata nafasi ya tatu pia alishinda nafasi ya uchezaji bora wa mashindano na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu shilingi 50,000/=

 

Katika mashindano hayo pia kulikuwa na nafasi ya mchezaji aliyeonyesha nizamu bora katika mashindano ya maadhimsho ya miaka 59  ya Mapinduzi ambayo ilikwenda kwa Khalid Kondo ambaye alizawadiwa pesa taslimu shilingi 50,000/=

 

Akizungumza mara baada ya zoezi la zawadi, Mkurugenzi wa Snipers Klubu aliwapongeza Wachezaji na Wadau wote waliojitokeza katika Mashindano hayo ya Maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi na kuwaomba Wadau wote tuendelee kushikamana ili mchezo wetu ufike tunapopahitaji kwa pamoja.

 

Maakamba pia aliwapongeza wote waliofanikiwa kushinda na kuzawadiwa zawadi kwani safari ya ushindi wao haikuwa nyepesi ni dhahili walipambana sana.

 

Nae Mwenyekiti wa Chama cha Pool Taifa, Isach Togocho aliwapongeza Snipers Klabu kupitia Mkurugenzi wa Klabu hiyo, Willfred Makamba, kwa kuandaa na kufadhili mashindano hayo ya maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi kwani jambo hilo ni heshima kubwa kwa Chama  cha Pool laakini pia kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanyika kwa Mashindano hayo.

 

Pili aliwapongeza wachezaji wote waliojitokeza kushiriki mashindano hayo pamoja na mashabiki pia waliojitokeza kushuhudia lakini Zaidi aliwapongeza wote waliofanikiwa kushinda na kupata zawadi na kuwaomba zawadi hizo zikawe chachu ya kuwafanya wajiandae vyema na mashindano mengine yajayo.

 

Aidha pia Togocho alitoa taarifa kuwa mwaka huu kutakuwa na uchaguzi ndani ya chama cha pool ambao utagusa ngazi ya Taifa tu hivyo wadau wote tujiandae na uchagguzi huo.

 

Togocho alimaliza kwatoa taarifa pia mwezi Octoba kutakuwa na Mashindano ya Pool ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika Nchini Afrika Kusini.Hivyo wachezaji na Wadau tujiandae kisaikolojia wakati wowote timu ya Taifa itaitwa na kuingia Kambini kwani lazima tushiriki.

 


  MAJALIWA: TULINDE MBOLEA YA RUZUKU ILIYOTOLEWA NA RAIS DKT. SAMIA

$
0
0

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wananchi kuwa walinzi wa mbolea ya ruzuku iliyotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuhakikisha inatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ya kuongeza uzalishaji wa mazao katika msimu wa 2022/2023 litimie.


 

Amesema kuwa kumekuwa na watanzania wachache wasiokuwa na nia njema wanaotorosha mbolea kwenda nchi jirani na kuwaacha watanzania bila kuwa na mbolea ya kutosha ”jambo hili lazima tulikemee na tulisimamie sote ili kuhakikisha mbolea iliyopo nchini ni kwa ajili ya watanzania, kila mmoja awe mlinzi kwa mwenzake”

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Januari 16, 2023) wakati akisalimia na wananchi kwenye eneo la Mbalizi jijini Mbeya akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali. Amesema utoaji wa ruzuku hiyo ya mbolea unalenga kuongeza uzalishaji wa chakula nchini na ni marufuku kuiuza nje.

Ameongeza kuwa awali mbolea iliuzwa kwa zaidi ya shilingi 100,000 lakini Mheshimiwa Rais Dkt. Samia akaridhia kutoa ruzuku shilingi bilioni 150 ili ikashushe bei ya mbolea na sasa inauzwa kwa shilingi 70,000. ”Tusikubali fedha hiyo kutumika nje la malengo, tulinde mbolea yetu isiuzwe kwa wasiohusika.”

”Nimefurahi sana kwa hatua zilizochukuliwa mkoani Songwe, tani 2199 zimekamatwa zikipelekwa nchi jirani hii haikubaliki, watanzania tuwe walinzi hii ni pesa yetu inatoroshwa na wachache, malengo yetu ni kuwahudumia ninyi kwa usimamizi wa Rais Dkt. Samia”

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuelekeza hatua zilizofikiwa katika maendeleo ya uboreshwaji wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe kuwa tayari njia ya kurukia ndege imekamilika kwa asilimia 100, jengo la abiria ujenzi umefikia asilimia 96 na sasa zoezi la ufungaji taa linaendelea na litakapokamilika uwanja huo utatumika wakati wote.

”Tunafanya hivi ili kuvuta masoko kutoka nchi jirani ikiwemo Kongo, Zambia na malawi walete ndege zako, haya yote yanafanywa na Rais wetu Dkt. Samia kwasababu ana maono ya mbali na dhamira yake ya dhati ya kuwaletea watanzania maendeleo.”

 

Kwa upande wake, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ameidhinisha kiasi cha shilingi bilioni 3.3 kwa ajili ujenzi wa mradi wa maji wa Shongo - Igale ambao umekamilika na watu wanapata huduma ya maji.

 

Ameongeza kuwa, pamoja na mahitaji ya maji katika eneo la mbalizi kuwa lita milioni 8, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia alitoa shilingi bilioni. 4.8 kwa ajili ya kujenga mradi wa maji wa Inunga ili kuongeza uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 8 hadi 12.

 

Naye, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, David Silinde amesema Serikali imetenga kiasi cha shilingi milioni 580 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 29 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ambapo yote yamekamilika kwa asilimia 100 na yanatumika.

 

Awali, baadhi ya wananchi walimuomba Mheshimiwa Majaliwa awasaidie katika kutatua changamoto ya fidia iliyotokana na kupisha ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe tangu mwaka 2002, ambapo Meneja wa uwanja huo, Mhandisi Danstan Komba alisema wanachodai wananchi hao ni mapunjo ya fidia.

Alisema baada ya eneo lao kutwaliwa walilipwa fidia ambapo baadae yalitokea malalamiko ya mapunjo ya fidia ambapo timu ya uchunguzi ya suala hilo iliundwa na ilishafika katika eneo hilo, hivyo aliwaomba wananchi watulie wakati suala lao linaendelea kufanyiwa kazi.

DKT MWINYI AKUTANA NA VIONGOZI WA UWT TAIFA, WAMPONGEZA

$
0
0




Mwenyekiti wa UWT Taifa, Ndg Mary Chatanda akikabidhi Tuzo ya Pongezi kwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar na Kutekeleza Ilani ya CCM ya Uchaguzi 2020-2025. #UWTImara #JeshiLaMama #KaziIendelee

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na ujumbe waViongozi wa Umoja  wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa Ikulu Zanzibar mapema leo.

Ndg Riziki Kingwande, Naibu Katibu Mkuu UWT - Bara


Mbunge Neema Lugangira: Mbunge Neema Lugangira akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi leo Jumatatu. 

 Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Zainab Shomari mara baada ya kuteta na Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa Ikulu Zanzibar mapema leoujumbe ambao uliongozwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Mary Chatanda.

 

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar


Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi leo Jumatatu Januari 16, 2023 amekutana na Viongozi wa Umoja  wa Wanawake Tanzania (UWT) Ikulu Zanzibar.

 

Uongozi wa Jumuiya hiyo uliongozwa  na Mwenyekiti wa  UWT Taifa Ndugu, Mary Chatanda, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa aliyeambatana na  Makamu Mwenyekiti UWT Zanzibar Ndugu Zainab Shomari, viongozi mbalimbali wa  kitaifa wa Jumuiya hiyo kwa nia ya kujitambulisha baada ya kuchaguliwa.

 

 Pia wamempongeza Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kuchaguliwa  kuwa Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar na Kutekeleza Ilani ya CCM ya Utekelezaji 2020-2025.

 KAMATI YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YAPOKEA TAARIFA YA UTENDAJI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

$
0
0

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imepokea taarifa ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa kipindi cha nusu mwaka (Julai-Desemba, 2022) katika kikao kilichofanyika leo jijini Dodoma.



Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Ally Juma Makoa (Mb) ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuendelea kutekeleza majukumu yake ipasavyo pia kwa kuendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza.

“Wizara mnafanya kazi nzuri tunaziona, changamoto zinazoendelea kujitokeza naomba muendelee kuzitatua kwa wakati” Mhe. Makoa amesisitiza.

Aidha, ameitaka Wizara hiyo kufanyia kazi maoni yaliyotolewa na wajumbe wa Kamati hiyo hususani katika eneo la kukabiliana na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu pamoja na migogoro kati ya wananchi na maeneo yaliyohifadhiwa.

“Katika kutatua na kumaliza migogoro inayotuhusu nashauri tuendelee kutumia busara ili wananchi waweze kuishi kwa amani na kuendelea kushiriki kikamilifu katika shughuli za uhifadhi” Amesisitiza Mhe. Makoa.

Naye, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Masanja  ameishukuru Kamati hiyo na kuahidi kufanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolewa ili kuikuza Sekta ya Maliasili na Utalii na hatimaye kuongeza pato la Taifa.



Miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa ni utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwamo Mradi wa Usimamizi wa Maliasili na Kuendeleza Utalii Kanda ya Kusini (REGROW), Mradi wa Kukabiliana na Ujangili na Biashara Haramu ya Wanyamapori, Mradi wa Panda Miti Kibiashara, Mradi wa Kuwezesha Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Nyuki(BEVAC), Mradi wa Kuongeza Thamani kwa mazao ya Misitu (FORV AC) na ukamilishaji wa baadhi ya shughuli za Mpango wa Ustawi kwa Maendeleo ya Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO-19.v



WANANCHI MBARALI WAMPONGEZA RAIS SAMIA KUMALIZA MGOGORO WA ARDHI

$
0
0

 *Wasema sasa wapo huru kuendelea na shughuli zao za ufugaji na kilimo kwa amani

 

WANANCHI wa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 15 na hivyo kuwawezesha kuendelea kufanya shughuli zao za ufugaji na kilimo kwa uhuru na amani.

Wamesema kumalizika kwa mgogoro huo ambao ulihusisha wakazi wa wilaya hiyo wanaoendesha shughuli za ufugaji na kilimo katika eneo la Bonde la Usangu dhidi ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Pongezi hizo zimetolewa leo (Jumanne, Januari 17, 2023) baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwatangazia wananchi hao kuwa Serikali imefanya maboresho makubwa kwenye Tangazo la Serikali namba 28 na kuliacha nje ya mpaka wa hifadhi eneo lenye ukubwa wa zaidi ya hekta 74,000 kwa ajili ya kuwawezesha wananchi hao kufanya shughuli za kilimo na ufugaji. Mkutano huo umefanyika kijijini Kapunga.

Tunamshukuru mama yetu, Mheshimiwa Rais Samia kwa uamuzi mkubwa alioufanya wa kuboresha GN 28, sasa tutalima kwa uhuru na tutaongeza uzalishaji kwa sababu awali tulikuwa tunalima kwa wasiwasi,” Amesema Elibauti Mwinuka mkulima katika kata ya Itamboleo wilayani Mbarali.

Kwa upande wake, Anle Kifute ambaye ni mkulima katika kijiji cha Kapunga amesema amefurahishwa na kauli ya Serikali ambayo inakwenda kuwaondolea migogoro katika maeneo yao na hivyo wataweza kuendesha shughuli zao bila ya usumbufu wa aina yoyote.

Naye, Mwenekiti wa Wafugaji katika ranchi ya Matebele-Madunguru, Lokordu Siloma amesema amefarijika kwa uamuzi huo wa Serikali pamoja na elimu ya ufugaji wa kisasa na wenye tija waliyopatiwa ambayo inakwenda kuongeza mnyororo wa thamani.

Kadhalika amemshukuru Mheshimiwa Rais Samia kwa kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi na sasa wanakwenda kufuga kwa uhuru na kwa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa. Awali watu wenye uwezo walikuwa wanavamia maeneo ya ranchi na kuendesha shughuli za kilimo lakini kwa kauli hii wafugaji tutaachiwa ranchi zetu tulishe mifugo yetu. Tunaishukuru sana Serikali.”

Kwa upande wake, Mheshimiwa Majaliwa baada ya kutangaza maamuzi hayo ya Serikali, amewataka Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Zuberi Homera na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune wahakikishe wanasimamia vizuri sheria pamoja na kuendelea kutoa elimu kuhusu umuhimu wa uhifadhi na utunzaji wa vyanzo vya maji.

Pia, Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki pamoja na viongozi wa Ranchi ya Usangu waende kwenye eneo hilo na kuwapanga upya wafugaji ili manufaa ya ufugaji yaonekane ikiwemo uanzishwaji wa viwanda vya kuchakata mazao ya mifugo.

Amesema Serikali imefanya maboresho hayo kwa lengo la kuwawezesha wakulima na wafugaji wilayani humo kuendesha shughuli kitaalamu na kuwaongezea tija. “Marekebisho ya tangazo hilo yatawezesha baadhi ya vitongoji vilivyokuwa vimetangazwa awali kuwa ndani ya hifadhi kuachwa nje ya mipaka na kutumiwa na wananchi kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji.”

Naye, Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema awali walishindwa kutekeleza mradi wa maji katika kijiji cha Kapunga wenye thamani ya shilingi bilioni 3.5 ambao kwa sababu walikuwa hawajui hatma ya wananchi hao kama wataendelea kubaki au wataondoka, hivyo baada ya kauli ya Serikali iliyotolewa leo amemuagiza Mhandisi wa Maji wa wilaya hiyo kuanza utekelezaji wa mradi huo.


Rais Samia ahudhuria Ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum), Davos, nchini Uswizi

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum) uliofanyika katika Ukumbi wa Congress, Davos nchini Uswizi tarehe 17 Januari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dkt. Abdallah Possi mara baada ya kuhudhuria ufunguzi wa Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum) uliofanyika katika Ukumbi wa Congress, Davos nchini Uswizi tarehe 17 Januari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na kuzungumza na Washiriki  pamoja na viongozi mbalimbali wanaohudhuria Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum) uliofanyika katika Ukumbi wa Congress, Davos nchini Uswizi tarehe 17 Januari, 2023.


 


Singida Big Stars yapata CEO mpya

$
0
0

Bodi ya Wakurugenzi ya Singida Big Stars imefanya mabadiliko katika ofisi ya Mtendaji Mkuu kwa kumteua John Kadutu kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu akichukua nafasi ya Dismas Ten.


Kadutu aliyewahi kuwa Mbunge wa Tabora (Buzwagi) ametangzwa rasmi katika nafasi hiyo baada ya kuibuka kwa sintofahamu ya nafasi ya Ten ndani ya kikosi hicho.


Pia Bodi hiyo imemuongezea majukumu kocha wa timu ya vijana Muhibu Kanu ambaye ameteuliwa kuwa msaidizi katika Ofisi ya Mtendaji Mkuu.

RT YATANGAZA TIMU YA TAIFA YA NYIKA MASHINDANO YA DUNIA AUSTRALIA

$
0
0


Kuanzia Kushoto ni, Rais Mstaafu wa RT, Kocha Francis John, Mjumbe wa Kamati ya Riadha Mkoa wa Arusha, Kocha Thomas John , Makamu wa rais RT, William Kallaghe, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Mbio za Nyika, Kocha Dennis Malle na Katibu Mkuu Mstaafu Wilhelm Gidabuday wakizungumza na Vyombo vya Habari Mbalimbali katika Hoteli ya Premier Palace, Jijini Arusha, Tanzania , Leo 18-01-2023.


Na Mwandishi Wetu


SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), limetoa Kalenda yake ya matukio ya mwaka 2023 na tayari mikoa wanachama wamekwishatumiwa.


Mikoa inatakiwa izingatie na inatarajiwa kufuatwa na kutekelezwa kikamilifu.


RT inapenda kutoa pongezi za dhati kwa Chama cha Riadha Mkoa wa Arusha (ARAA), kwa utekelezaji wake wa matukio ya Riadha kikamilifu na linaitaka mikoa mingine kuiga mfano wa Arusha.


Mikoa yote, inatakiwa kuhakikisha inafanya vikao na mashindano ya ndani ya mikoa yao na inapaswa kuwasilisha matokeo angalau mwezi mmoja kabla ya tarehe ya mashindano ya Taifa kama ilivyoainishwa kwenye kalenda na hayataahirishwa mwaka huu.


Mkoa ambao hautatekeleza hilo, hawatapewa nafasi kwenye mashindano ya Taifa. 


Shirikisho, halitaki viongozi wa mikoa wanaookota wachezaji ambao hawajawaandaa, wala kuwapima mkoani kwao. 


RT inawakaribisha wadau na wadhamini mbalimbali, kushiriki katika matukio mbalimbali ya riadha, na shirikisho linawakikishia ushirikiano mkubwa na watapata mrejesho kulingana na walichokiwekeza.


VIKAO MBALIMBALI


Katika kupunguza gharama za uendeshaji, Shirikisho kuanzia sasa limejipanga kuendesha baadhi ya vikao vyake vya Kamati Tendaji na Kamati mbalimbali kwa njia ya mtandao 'Virtual meetings'.


WAANDAAJI WA MBIO (RACE ORGANISERS)


RT, inawapongeza waandaaji wote wanaofuata kanuni zilizopo bila usumbufu, wakiongozwa na Kilimanjaro International Marathon, CRDB, NMB, NBC, Mbeya Tulia Marathon na wengineo.


Wale ambao mwaka 2022, wanajijua kuvunja au kutofuata kanuni, Shirikisho halitawafumbia macho na mwaka huu hawatawekwa kwenye kalenda, hadi watoe maelezo na sababu zitakazojitosheleza. 


RT, haiwezi kuwa na matukio yasiyofuata taratibu. Shirikisho limekasimiwa mamlaka ya kusimamia mchezo wa riadha kwa niaba ya serikali, hivyo lina wivu na mamlaka hayo, halitakubali mtu au taasisi yoyote kuliingilia labla iwe kwa maelekezo ya serikali kupitia Wizara au Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

MIRADI 630 YA UWEKEZAJI YENYE THAMANI YA SH. BIL. 3.68 YASAJIWA NA TIC-MAJALIWA

$
0
0


*Imesajiliwa katika mwaka wa fedha 2021/2022 na inatekelezwa na makampuni kutoka India

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema katika mwaka wa fedha 2021/2022 miradi mipya ya uwekezaji 630 yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 3.68 inayotekelezwa na makampuni ya India imesajiliwa kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Amesema hatua hiyo inatokana na jitihada mbalimbali za kuboresha mazingira ya uwekezaji zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Hivyo, ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji wengine kutoka nchini India waje wawekeze Tanzania.

Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Alhamisi 19 Januari 2023) wakati alipokutana na ujumbe wa Bunge la India (Lock Sabha) ulioongozwa na Spika wa Bunge hilo, Mheshimiwa OM Birla. Waziri Mkuu kutana na viongozi hao  kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ambaye yupo nje ya nchi kikazi.

Mheshimiwa Majaliwa amesema Nchi ya India na Tanzania zimekuwa na ushirikiano Mkubwa wa kiuchumi na biashara huku India ikishika nafasi ya tatu kwa kuwa na ushirikiano wa biashara unaofikia Dola za Marekani bilioni 4.58 kwa mwaka 2021 – 2022.

Waziri Mkuu amemuhakikishia Spika huyo kuwa Tanzania itaendeleza ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati yake na India. “Rais anamatumaini makubwa na ushirikiano uliopo baina ya nchi ya Tanzania na India na kwamba ushirikiano huo umekuwa na manufaa makubwa kati ya nchi zetu.”

Amesema Tanzania na India zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu katika sekta mbalimbali zikiwemo za uchumi, nishati, maji, elimu, afya, biashara na teknolojia na hivyo kuleta manufaa makubwa.“Mheshimiwa Rais amefurahia ujio wako Nchini Tanzania, ni matarajio yake kuwa ujio huu utakuwa na manafuu makubwa baina ya Nchi zetu.”

 “Mwezi juni 2022 tumeshuhudia makampuni sita kutoka nchini India yakitia saini mikataba ya miradi ya maji kwa miji 28 yenye thamani ya zaidi ya dola za Marekani milioni 500 ambayo ikikamilika itawawezesha watanzania zaidi ya milioni sita kupata maji ya uhakika.”

Nitoe wito kwa Nchi ya India ambayo kwa sasa ni mwenyekiti wa Nchi za G 20, kuwa mtetezi wa Nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania katika suala zima la mabadiliko ya hali ya hewa, Usalama wa chakula, uwezeshaji wa wanawake na vijana pamoja na kupambana na athari za uviko 19”

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amesema ujio wa Spika huyo na ujumbe alioongozana nao utaboresha uhusiano baina ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Bunge la India kwa wabunge na viongozi wa mabunge hayo kubadilishana uzoefu.Nitoe wito kwa mabunge yetu haya kuweka utaratibu wa kutembeleana na kubadirishana uzoefu, ili kukuza ushirikiano.”

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameishukuru Serikali ya India kwa ushirikiano na namna ambavyo imeendela kutoa fursa za masomo kwa wataalam wa Tanzania katika sekta mbalimbali nakuiomba nchi hiyo iendelee kutoa ufadhili huo wa masomo katika nyanja nyingine za teknolojia ya mawasiliano, afya, uhandisi, kilimo, maji, madini na gesi.

Kwa Upande wake, Spika wa Bunge la India Mheshimiwa Birla amesema, Bunge la India litakuwa msemaji mzuri wa ushirikiano na maendeleo baina ya Tanzania na India ili nchi hizo ziendelee kunufaika na ushirikiano uliopo.

Kwa niaba ya Serikali na Bunge la India, tunawasilisha pongezi zetu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi wake wa mfano, sasa tunaona uchumi wa Tanzania unakuwa kwa kasi na tunaona miradi mikubwa ikitekelezwa, tafadhali fikisha pongezi zetu kwake.”

Mheshimiwa Birla na ujumbe wake yuko katika ziara ya kikazi ya siku tatu Nchini Tanzania ambapo pamoja na mambo mengine atatembelea vituo mbalimbali vya utalii ikiwemo mbuga za wanyama.

SINGIDA WAANZA MSAKO WA WANAFUNZI AMBAO HAWAJA RIPOTI MASHULENI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akizungumza na Maafisa elimu na wakuu wa Wilaya ili kujadili hali ya usaili wa wanafunzi  mashuleni katika kikao kilichofanyika Januari 18, 2023. Kulia ni Afisa Elimu Mkoa wa Singida, Maria Lyimo.

Na Mwandishi Wetu, Singida

MAAFISA elimu na Wakuu wa Wilaya Mkoani Singida  wametakiwa kutumia muda wa Siku tatu kuanzia leo  kuhakikisha hakuna mtoto atakayebaki nyumbani wakati wengine wakiwa shuleni.

Kauli hiyo imetolewa leo na  Mkuu wa Mkoa huo Peter Serukamba alipokutana na Maafisa elimu na wakuu wa Wilaya ili kujadili hali ya usaili wa wanafunzi  mashuleni.

Amesema idadi ya wanafunzi wa Sekondari walioripoti mashuleni ni ndogo ikilinganishwa na uwingi wa madarasa yalijengwa na Serikali hivi karibuni hivyo ni jukumu la Maafisa elimu hao kuhakisha wanasakwa popote walipo na wapelekwe shuleni.

RC Serukamba ameendelea kueleza kwamba ifikapo Siku ya jumatatu tarehe 23 January 2023 anataka taarifa ya kutoka kila kata  kuhusu wanafunzi wangapi wamesajiliwa na wangapi bado na Sababu za kutosajiliwa.

Aidha, ametoa wito kwa wazazi na walezi Mkoani Singida kuhakikisha hakuna Mtoto aliyechaguliwa kujiunga na kidato Cha kwanza atakayebaki nyumbani.

"Nimejiridhisha kwamba hali ya usaiili wa wanafunzi wa kidato Cha kwanza inasuasua Sana, Serikali imejenga madarasa ya kutosha,imefuta Ada mashuleni lakini bado wapo wazazi hawawapeleki watoto wao shuleni hili halitakubalika" Serukamba.

Kwa upande wake DC wa Iramba Suleimani Mwenda amesema bado Katika Wilaya yake bado hali ya kujiunga na kidato Cha kwanza unaenda kwa kusuansua Jambo ambalo waliamua kuchukua hatua kwa kuwaita wazazi na wanafunzi ofsini kwake ili kuwasikiliza.

DC Mwenda anasema amebaini kwamba wapo wazazi wanaozuia watoto kwenda shule ili waweze kujiunga na Shughuli za kiuchumi za kulima kuchunga mifugo na bàadhi Kutafuta ajira binafsi.

Mwenda amesema wanapenda kutumia mbinu zote zikiwemo kuwashawishi kutumia Dola kuwapeleka shule na kuwachukulia hatua wazazi Watakao bainika kuwazuia watoto kwenda shule.



Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Afisa Elimu Msingi wa Wilaya ya Ikungi, Margaret Kapolesya akichangia jambo kwenye kikao hicho.




Kusini waongoza kwa uvamizi wa Ardhi- SMZ

$
0
0

Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Rahma Kassim Ali (Kati), Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Mzee Ali Haji ( kusho) na Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Rajab Mkasaba wakizungumza masheha wa Wilaya hiyo kuhusu uvamizi wa ardhi ya akiba.


 

Na Mwandishi Wetu

 

Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar imesema kumekua na uvamizi pamoja na uuzaji holela wa maeneo ya ardhi ya akiba kitendo ambacho kinachangia ongezeko la migogoro ya ardhi Zanzibar.

 

Kauli hiyo imetolewa jana na waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar Rahma Kassim Ali alipokutana na Masheha wa Wilaya ya Kusini Unguja, kikao maalum kilichofanyika ofisi za Mkuu wa Wilaya hiyo alisema   kumekua na uvamizi na uuzaji holela wa maeneo ya ardhi ya akiba yaliyotengwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

 

Waziri Rahma alisema Wizara yake itahakikisha inaweka mikakati imara ya udhibiti wa uuzaji ardhi kiholela hasa katika maeneo ya ardhi ya akiba yaliyotengwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

 

Aidha alieleza kwamba Wilaya ya Kusini Unguja inaongoza kwa uvamizi na uuzaji wa  ardhi kiholela hasa katika maeneo ya fukwe za bahari yiliyopo wazi  hivyo kutokana uwezo wa wizara yake kupewa dhamana ya usimamizi wa ardhi kwa mujibu wa tangazo la kisheria Nam 137 ya Mwaka 2020 itahakikisha inayadhibiti maeneo hayo.

 

“ Wilaya ya kusini Unguja  inaongoza kwa uvamizi na uuzaji wa maeneo kiholela hasa maeneo ya fukwe na yaliyo wazi  hivyo kwa vile Wizara yangu ndio iliyopewa dhamana ya usimamizi wa ardhi kwa mujibu wa sheria nitahakikisha ninayadhibiti maeneo hayo na atakaebainikia kwenda kinyume hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake” Alisema waziri huyo.

 

Hivyo  Waziri huyo amewataka masheha hao kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika usimamizi wa masuala ya ardhi pamoja na kufanya kazi zao ipasavyo kwa kutojihusiha na vitendo vya uuzaji wa ardhi bila kufuata sheria zilizowekwa.

 

Naye Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Mzee Ali Haji alitoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya ardhi kwa wageni ambapo alisema kwa mujibu wa Sheria ya ardhi Nam.12 ya mwaka 1992 imekataza kuuziwa ardhi mgeni yeyote bali atatakiwa kukodishwa kwa ajili ya uwekezaji na sio vyenginevyo.

 

Kwa upande Mkurugenzi Mipango Miji na Vijiji Kutoka Kamisheni ya Ardhi Muchi Juma Ameir alisema tayari Kamisheni ya Ardhi  imeyaainisha  maeneo yote yenye ardhi ya akiba yaliyoko katika Mkoa wa Kusini Unguja yakiwemo Paje, Muungoni,na Muyuni kwa lengo la kuyapanga na kuyapima kwa kuyawekea alama na  kuyadhibiti ili yasiweze kuvamiwa kwa uuzaji wa viwanja kiholea.

 

Kwa upande wa mashe Shehia ya paje Mohammed Rajabu Makame alisema kuwa  kwa kiasi kikubwa wanasheria ndio wanaohusika na masuala ya ukiukwaji wa sheria kwa kufanya vitendo hivyo na hata wao kuwakosesha ufanisi mzuri wa kiutendaji hasa katika kazi zao za usheha.

 

Mapema Mkuu wa Wilaya ya Kusini Rajab Mkasaba alimkaribisha waziri huyo na kuwataka masheha kuwa mabalozi wazuri katika kutoa elimu kwa jamii juu ya umiliki wa ardhi katika shehiya zao.

 

Kikao hicho kimefanyika kwa lengo la kujadili na kuweka mipango mikakati  ya usimamizi madhubutu ambao utasaidia kuondoa changamoto ya uuzaji wa ardhi kiholela  pamoja na kupunguza migogoro ya ardhi nchini.


MWEKEZAJI WILAYANI MKALAMA ADAIWA KUKITAPELI KIJIJI, ARDHI ALIYOPEWA KUWEKEZA SHULE AIKODISHA KWA KILIMO

$
0
0

 Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba akizungumza Januari 18, 2023 wakati wa kikao cha kusikiliza kero za Wananchi wa Wilaya ya Mkalama katika ziara zake za kutembelea kila wilaya kwa ajili ya kusikiliza kero na kuzipatia ufumbuzi.
 

Na Dotto Mwaibale, Mkalama

 

MWEKEZAJI aliyetaka kujenga shule ya sekondari katika moja ya kijiji  wilayani Mkalama mkoani Singida anadaiwa kufanya utapeli baada ya ardhi aliyopewa na kijiji kwa ajili ya kujenga shule  kuigeuza matumizi na kuanza kukodisha watu kuendesha shughuli za kilimo kwa zaidi ya miaka 14.

 

Suala hilo limeibuliwa na wananchi wa Wilaya ya Mkalama kwenye kikao na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba ambaye anaendelea na ziara yake ya kutembelea kila wilaya kwa ajili ya kusikiliza kero na kuzipatia ufumbuzi.

 

Katika ziara hiyo wilayani humo Serukamba alipokea kero 49 huku kero 43 zikihusu migogoro ya ardhi kama mashamba, viwanja na nyumba.

 

Akizungumza baada ya kusikiliza kero hiyo Serukamba aliagiza ardhi hiyo irudishwe kwa halmashauri ya kijiji hicho kama sheria inavyoelekeza kuwa kama ardhi haijaendelezwa kwa muda mrefu inapaswa kurejeshwa kwa walengwa.

 

Kero nyingine iliyoleta msisimko kwenye kikao hicho ni ya serikali ya Kijiji cha Iglansoni kudaiwa kuipora familia ya mama Melisiana mashamba zaidi ya ekari 60 na kisha kuanza kuyakodisha kwa wananchi kwa ajili ya kuendesha shughuli za kilimo huku fedha zinazopatikana zikinufaisha viongozi wa kijiji hicho.

 

Serukamba alimuagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mkalama, Mkurugenzi na Afisa Ardhi wa Wilaya hiyo kwenda katika kijiji hicho na kufanya utaratibu wa kumrudishia mashamba mama huyo.

 

Katika hatua nyingine Maafisa ardhi, Watendaji waVijiji na Kata wilayani humo wametakiwa kuacha vitendo vinavyo sababisha migogoro ya ardhi ambayo imetajwa kama chanzo cha umaskini kwa wananchi na kuacha kushiriki vitendo vya uuzaji wa ardhi ambazo tayari zinaumiliki wa watu wengine na badala yake wajikite kuwashauri wananchi kuhusiana na mambo ya ardhi.

 

"Maafisa ardhi, watendaji wa kata na vijiji msiwe chanzo cha umaskini wa wananchi, watu wanataka kulima, kufanya maendeleo lakini mnawakwamisha mnaposhindwa kuwatatulia shida zao" alisema Serukamba.

 

Aidha Serukamba amewataka watumishi wilayani humo kutekeleza wajibu wao kikamilifu na kuwa kwa kufanya hivyo kutapunguza kero za wananchi.


Utaratibu huu ulioanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa kusikiliza kero za wananchi kila wilaya umepewa kongole na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mkalama James Mgwega ambaye alisema utasaidia kupata majawabu ya kero za muda mrefu za wananchi ambazo zilikaliwa na viongozi wa maeneo husika.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba akisisitiza jambo kwenye kikao hicho.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba akiteta jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, James Mkwega wakati wakitoka kwenye kikao cha kusikiliza kero za wananchi.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Amoni Sanga akizungumza kwenyekikao hicho.

Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Elizabeth Rwegasira akizungumza kwenye kikao hicho.Mkuu wa Polisi wa wilaya hiyo akichangia jambo kwenye kikao hicho.

Afisa Ardhi Wilaya ya Mkalama, Imikigwe Kagubila Mwanitu, akijibu maswali kufuatia kero mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wananchi.
Viongozi wa Taasisi mbalimbali za Serikali na wakuu wa idara wakiwa kwenyekikao hicho.
Kero zilizokuwa zikitolewa zikiandikwa.




Kikao kikiendelea.

Baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa kwenye kikao hicho. 

 VIONGOZI WA SHIRIKA LA UNTOLD FOUNDATION WATEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA

$
0
0

Na Mwandishi Wetu

Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Kimepokea wageni zaidi ya 300 ambao ni viongozi wa Shirika lisilo la kiserikali la Untold Foundation kutoka nchi mbalimbali Afrika Mashariki na nje ya Afrika Mashariki. Imekuwa ni utaratibu wao wa kutembelea nchi mbalimbali ambazo Shirika hilo lina matawi yake na awamu hii ilikuwa Tanzania.

Vingozi wao waliweza kuandaa Safari ikiwa ni kutembelea vituo vya utalii vinavyopatikana Dar Es Salaam na moja ya kituo walichotembelea ilikuwa ni Makumbusho ya Taifa la Tanzania, kwenye kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni.

Naye Mratibu wa safari hiyo ndugu Donald Mbeke alisema " tuliona Makumbusho ya Taifa ni sehemu sahihi kuwaleta wageni wetu ili waweze kujifunza juu ya Masuala ya uongozi, historia ya nchi yetu na utamaduni wetu". Aliendelea kwa kusema ni muda sana sijafika hapa Makumbusho ya Taifa nimekuta mambo yamebadilika sana. Alimalizia kwa kutoa shukrani kwa uongozi wa Makumbusho ya Taifa kwa ujumla namna walivyo waliwapokea na kuwapatia huduma rafiki kwa kila mmoja na kuahidi kurudi kwa awamu ya pili.

Afisa Elimu Mwandamizi wa Makumbusho ya Taifa Anamery Bagenyi alimshukuru Mratibu wa safari hiyo kwa kuona Makumbusho ya Taifa ni sehemu sahihi ya kutembelea na kujifunza, na kutoa wito kwa Mashirika mengine ya kiserikali na yasio ya Kiserikali pia kuiga mfano wa Shirika hili la Untold Foundation.


Makumbusho ni sehem sahihi sana kwa kujifunza historia ya nchi lakini zipo kumbi ambao wanaweza kufanyia Mikutano yao mbalimbali.

ANZANIA COMMERCIAL BANK YASHIRIKI UZINDUZI UJENZI WA RELI YA KISASA KUTOKA TABORA HADI ISAKA

$
0
0
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Phillip Mpango akisikiliza maelezo ya ushiriki wa benki ya Tanzania Commercial Bank TCB katika ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) kutoka kwa Mkurugenzi wa wateja Wakubwa wa Tanzania Commercial Bank (TCB),  Adolphina William wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa ujenzi wa reli ya SGR LOT 4 kati ya Tabora na Isaka, uliofanyika leo mjini Isaka, mkoani Shinyanga
Mkurugenzi wa wateja Wakubwa wa Tanzania Commercial Bank (TCB),  Adolphina William wakati (kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa ujenzi wa reli ya SGR LOT 4 kati ya Tabora na Isaka, uliofanyika leo mjini Isaka, mkoani Shinyanga ambapo katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Phillip Mpango.


Tanzania Commercial Bank (TCB) Imeendelea kushiriki zoezi endelevu la ujenzi wa kipande cha nne cha ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Tabora hadi Isaka chenye urefu wa kilomita 165.

TCB imeshirikia kikamilifu katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha kutoka Tabora hadi Isaka chenye urefu wa kilomita 165..

TCB imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo katika sekta mbalimbali na kuhakikisha kuwa inatoa huduma stahiki kila kona ya Tanzania na kuhakikisha inaunga mkono kwa asilimia zote maendeleo ya nchi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa wateja wakubwa wa  Tanzania Commercial Bank Adolphina William  wakati wa uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa reli ya Kisasa (SGR) awamu ya nne leo Mkoani Shinyanga

Adolphina amesema, Tanzania Commercial Bank  ni Benki ya Wananchi na  wamejitoa na wameshiriki kwa hatua kubwa katika kuhakikisha shirika la Reli Tanzania (TRC) linafanikisha mradi wa SGR   kwa mafanikio makubwa.

“Tanzania commercial Bank ni wadau wakubwa wa maendeleo hapa nchini na kuchangia ujenzi wa Taifa, TRC wanafanya kazi nzuri sana kuhakikisha wanaunganisha wananchi kwa njia ya usafiri wa reli hivyo mradi huu wa SGR utaleta mafanikio makubwa hapa nchini.

Adolphina ameeleza kuwa kwa Sasa Tanzania Commercial Bank ina matawi kila pembe ya Tanzania hivyo imejipanga vyema kutoa huduma kwa watanzania pamoja na wageni kutoka nje hivyo amewasihi watanzania ambao bado hawajafungua akaunti na benki ya TCB wakafungue akaunti ili kunufaika na huduma zinazopatikana katika Benki hiyo.

 


Rais Samia azungumza katika Mkutano wa Nishati

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wakati akizungumza katika mkutano wa masuala ya Nishati (Powering the World) uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Congress Davos nchini Uswizi tarehe 19 Januari, 2023.

 

 

  TAIFA GAS yatoa Msaada wa Mitungi ya Gesi 150

$
0
0
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Kampuni ya Usambazaji wa Gesi Majumbani ya Taifa Gas imetoa msaada wa mitungi ya gesi 150 kwa Baba na Mama Lishe wa Kisutu jijini Dar es Salaam.
 
Akizungumza jijini humo wakati wa hafla ya kukabidhi kwa mitungi hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ngw’ilabuzu Ludigija amempongeza Mbunge wa Jimbo la Ilala ambaye pia ni Naibu Spika Mussa Zungu kwa kushitikiana na Taifa GAS kutoa msaada huo.

“Hongereni kwa kazi nzuri ya kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kuhimiza matumizi ya nishati mbadala, hivyo mama lishe na baba lishe haya ni matunda ya maelekezo ya Rais,” amesema Ludigija na kuongeza,

“Hivyo nyie ndiyo wakwanza kula matunda haya ya kuwekwa pamoja mahali rasmi pa kufanyia shughuli zenu,”.

Hivyo Ludigija amewataka baba na mama lishe hao kuwa mabalozi kwa wemgine kuwaeleza kiacha kipikia barabarani kwani kufanya hivyo kuna haribu miundombinu ya barabara.

Ametumia fursa hiyo kuwataka wana Ilala kuhakikisha wanaitikia witu wakufanya shughuli zao katika maeneo rasmi.

Akizungumzia gesi hiyo, amesema kwamba ni salama na itawasaidia kiwaondolea matatizo mbalimbali yakiwemo ya kiafya na mazingira.

Ameelza kwamba Taifa GAS kwa sasa imesambaa nchi nzima, hivyo ameipongeza kampuni hiyo kwa kuunga mkono juhudi za Rais Samia za kuhimiza matumizi ya nishati mbadala ambayo inasaidia kuepusha Taifa kuingia katika hali ya jangwa.

Kwani jambo hilo litasaidia kuokoa misitu kukatwa kwa matumizi ya kuni na mkaa.

Kwa upande wake, Naibu Spika Zungu, amesema kwamba wamesaidia mitungi hiyo kwa sababu baba na mama lishe wamekuwa wakihangaika na moshi kutokana na kutumia mkaa na kuni.

Aidha amesema kwamba baada ya kukaa nao hivi karibuni waliona ni bora kuwasaidia ili waweze kutumia nishati mbadala badala ya mkaa na kuni. 

Naibu Spika Zungu amesema kwamba kutokana na matumizi ya nishati ya kuni na mkaa, takribani viwanja milioni moja vya mpira vyenye misitu vimekuwa vikiharibiwa hali inayosababisha nchi kuingia katika jangwa.

“Tumekaa na Taifa GAS kuwaomba, hivyo mitungi hii 150 inatolewa bure, lakini sharti yake gesi ikiisha utanunua kwa yule aliyekupatia, ukinunua kwingine sio uungwana,” amesema Zungu.

Zungu amewataka kutokuendelea kutumia mkaa na kuni kwani kutumia nishati hizo ni kuliumiza Taifa kwa kuliingiza kwenye ukame.

Nae, Meneja wa Mahusiano Mema kutoka Taifa GAS, Angel Mwita, amesema wametoa msaada wa mitungi hiyo kwa kushirikiana na Mbunge wa Ilala ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais Samia za kuhimiza matumizi ya nishati mbadala.

Amesema gesi hiyo ni salama kwa matumizi kwani inasaidia katika utunzaji wa mazingira na kwamba wana gesi ya kutosha kwa matumizi ya nchi nzima

 Aga Khan Tanzania na Elekta Wasaini Mkataba wa Manunuzi na Uwekaji Vifaa Tiba vya Mionzi 

$
0
0

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Kwa kuzingatia maono ya Mtukufu Aga Khan, ya kuwezesha huduma bora za afya kupatikana kirahisi, Taasisi ya Utoaji Huduma za Afya ya Aga Khan, Tanzania (AKHST) kupitia Mradi Mtambuka wa Saratani Tanzania (TCCP) imenunua moja ya kifaa cha kisasa cha tiba ya mionzi na vifaa vingine vinavyohusisha matibabu hayo vitakavyofungwa katika Kituo cha Huduma za Saratani cha Aga Khan kilichopo Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam (AKHD).

 

Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam itakuwa hospitali ya kwanza nchini Tanzania, na ya pili Afrika Mashariki na Kati kuwa na vifaa vya teknolojia hiyo.

Kwamba hii ineonesha kuwepo kwa maono na uvumbuzi unaolenga kusaidia wagonjwa ambapo leo imeshuhudiwa utoaji huduma bora za afya nchini na pengine katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, ukipata teknolojia bora zaidi ya matibabu ya saratani, na kuifanya kuwa kituo mahususi cha matibabu ya saratani Afrika Mashariki na Kati.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba wa manunuzi wa vifaa hivyo jijini Dar es Salaam Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam na Meneja wa Mradi Mtambuka wa Saratani Tanzania (TCC) Dkt. Harrison Chuwa amesema kifaa kitakachofungwa ni modeli mbili za linear accelerator kuongeza kasi ya matibabu ya saratani kwa njia ya mionzi.

Dkt. Chuwa ameongeza kuwa “Kusainiwa kwa mkataba huu manunuzi na uwekaji wa mashine ya mionzi unakifanya kituo cha matubabu ya saratani kuwa na mashine za kisasa, ya kwanza na ya aina yake nchini na Kanda ya Afrika Mashariki, ikiwezeshwa na CT simulator: Discovery TM RT kutoka kampuni ya GE Healthcare na Wide-bore, teknolojia ya MaxFOV inayoruhusu mwonekano kamili na sahihi, kingo-kwa-kingo, picha ya CT na teknolojia ya MicroVoxel ambayo hutoa na kutupatia miundo midogo, kuwezesha njia sahihi na kutoa DRR zenye mwonekano bora na usahihi wa picha,”.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tiba na Afya, Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN), Dkt. Gijs Walvaren, amesema “ Lengo letu linabakia katika kukuza ubora wa utoaji wa huduma za afya na usalama wa wagonjwa na kuongezeka kwa upatikanaji kutoka huduma ya msingi hadi ngazi ya tatu/ juu kupitia uwekezaji katika maeneo mbalimbali ikijumuisha vifaa, teknolojia, wafanyakazi waliofunzwa vyema na wenye uwezo pamoja na ithibati ya JCI ikifuatiwa na uidhinishaji ujao wa OECI, hizi zifuatazo kituo cha huduma ya saratani cha Aga Khan (AK-CC) kuwa moja ya vituo vya juu vya saratani barani Afrika na ulimwenguni,”.

Ameongeza “Pili, kituo hicho kitasaidia juhudi za Serikali katika kupanua huduma za matibabu ya saratani kwa Watanzania na kuongeza utalii wa kimatibabu katika ukanza mzima,”.

Nae, Makamu wa Rais, Huduma za Kimabara kutoka Elekta Feres Al Hasan amesema Kampuni ya Elekta ina kusudi moja ambalo linawapatia motisha kama kampuni na mtu binafsi.

“Matumaini kwa kila mtu anayehusika au kuguswa na Saratani. Hili linatuongoza kuelekea maono yetu ya kuwa ulimwengu ambapo kila mtu anaweza kupata huduma bora ya matibabu ya saratani. Na tunapanga kufika huko kupitia dhamira yetu ya kuboresha maisha ya wagonjwa kwa kufanya kazi pamoja na wateja na washirika wetu,” amesema Al Hasan.

Kwamba kama mvumbuzi mkuu wa tiba ya mionzi, kampuni ya Elekta imejitolea kuhakikisha kwamba kila mgonjwa anapata huduma bora zaidi ya saratani kadri iwezekanavyo.
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live