Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

TANZANIA COMMERCIAL BANK YAPIGA JEKI WAKULIMA WA ZAO LA MWANI UNGUJA

$
0
0


Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi  (kushoto), akikabidhi   msaada wa kisima cha maji kwa Mbunge wa Jimbo la Paje Unguja  Mh Sudi Hassan kwa niaba ya wamama wa Jimbo hilo wanaojishughulisha na Kilimo cha mwani kwaajili ya kustawisha Kilimo cha zao hilo  hafla ya makabidhiano hayo yefanyika unguja mwishoni mwa wiki wengine pichani ni baadhi ya wamama waliopatiwa msaada huo.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali pamoja na wakulima wa zao la mwani kutoka jimbo la paje Unguja.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi  akifurahi pamoja na viongozi mbalimbali na wamama wakulima wa zao la mwani  Unguja mara baada yakukabidhi msaada wa kisima kwaajili ya kustawisha Kilimo cha zao hilo  hafla ya makabidhiano hayo yefanyika unguja.


Madereva wa Serikali watakiwa kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani

$
0
0


Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabani, Wlbroad Mutafungwa.

 

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Jeshi la Polisi Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini limewataka madareva Wanaofanya kazi Serikalini kuzingatia sheria za barabarani nakuacha tabia ya kudhani kuwa wapo juu ya sheria kwani wamekuwa wakisababisha ajali.

Hayo yamesemwa jijini humo na Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini, Wilbroad Mutafungwa wakati wa Mafunzo ya siku moja Kwa Madereva wa Serikali yenye lengo la kuwakumbusha kutekeleza majukumu yao Kwa kuzingatia sheria za Barabarani Ili kupunguza ajali zinazojitokeza nakusababisha vifo na ulemevu wa kudumu.

"Ninyi Madereva mnafanya kazi bila kuzingatia sheria japokuwa mmepata  Mafunzo kutoka katika vyuo vya usafirishaji vinavyotambulika kisheria,mmetahiniwa na kukabidhiwa chombo cha moto Kwa mujibu wa sheria,lakini mmekuwa ni sehemu ya kusababisha ajari kutokana na kuzalau sheria za Barabarani nakujiona nyinyi mpo juu ya sheria" amesema Mutafungwa 

Amebainisha  kuwa asilimia 90 ya ajali zinazojitokeza zimekuwa zikisababishwa na tabia za madereva hao kitokuzingatia sheria za barabarani huku asilimia zingine za ajali zikisababishwa na masuala ya miundombinu ya barabara na sababu zingine.

Mutafungwa amesisitiza katika kipindi cha mwezi January 2022 hadi Agosti 2022 ajali zilikuwa 1,177 katika hizo ajali zilizotokana magari ya serikali 135 sawa na asilimia 11.5 huku jumla ya vifo vyote 11038 na 90 vilitokana na magari ya serikali sawa na asilimia 8 .7

Sambamba na hayo amesema Majeruhi wote wa ajali walikuwa 1,556 walitokana na magari ya serikali 211 sawa na asilimia 13 .6 hivyo ajali ya magari ya serikali umekuwa siyo jambo la kustua imekuwa kawaida kwani asilimia kubwa hujisababishia wenyewe kutokana na viongozi kuwafanya Madereva wao wawe juu ya sheria hawaonywi.

VITENDO VYA UKATILI HAVIVUMILIKI-WAZIRI GWAJIMA

$
0
0

 Na WAJJWM, Dar es salaam 


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema Serikali haitavumilia vitendo vya ukatili vinavyoendelea kutokea kwenye jamii.


Waziri Gwajima ameyasema hayo tarehe 07 Oktoba, akiwa katika ziara yake Jijini Dar es salaam, kata ya Kivule alipomtembelea Mtoto Daudi Mabwega mwenye umri wa miaka minne aliyefanyiwa ukatili na baba yake mzazi wa kuchomwa ya maji ya moto mkononi kwa kosa la kula mboga bila idhini ya mzazi huyo.

Amesema Jamii inatakiwa kuwatunza watoto kwani ni hazina kwa Taifa hivyo wanapaswa kulindwa kwa hali yoyote na akiwa ni Waziri mwenye dhamana ya watoto atahakikisha haki zao zinalindwa.

"Mzazi ni mtu wa kwanza anayetakiwa kuwa Faraja kwa Mtoto wake aliyemzaa, hatuwezi kuendelea kuvumilia kuona Wazazi ambao badala ya kuwa viongozi wanawakatili hawa watoto, Serikali itamfikia kila mzazi, mlezi na mwanajamii aliyefanya ukatili kwa mwanajamii mwingine hususani watoto" amesema Mhe. Gwajima.

Kwa upande wake Afisa Utawi wa Jamii, hospitali ya Wilaya ya Kivule Irene Shembelu aliyeibua  ukatili huo amesema Mtoto huyo alifanyiwa ukatili na baba yake baada ya migogoro ya kifamilia iliyosababisha mama wa mtoto kuondoka na kuwaacha watoto na baba yao pekee.

"Tuliipokea kesi ya Mtoto huyu kuwa amekatiliwa na baba yake mzazi kwa kosa la kula maharage waliyotegemea kula  baada ya baba kurudi, kwani watoto hawa wanajilea wenyewe, baba akitoa asubuhi anarudi usiku" Alisema Irene Shembelu.

Kwa upande wake Inspekta Mdasi Lukato akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Dawati la Jinsia Kanda Maalum ya Polisi Dar es salaam amesema hatua kali zitachukuliwa kwa kitendo kilichofanyika na baba huyo.

Naye mlezi aliyeaminiwa kumlea Mtoto Daudi na ndugu zake Bi. Zahra Omary (fit person) amesema alimpokea Mtoto huyo mwezi Agosti mwaka huu kutoka kwa Afisa Ustawi wa Jamii akiwa na Hali mbaya.

Baadhi ya wananchi wakizungumza katika mkutano wa hadhara wamemshukuru Mhe. Gwajima kwa kuwatembelea na kujua changamoto zao kwani vitendo vya ukatili katika kata hiyo ni vingi lakini wanajamii wanakabiliana navyo kwa jitihada mbalimbali.


Tanzania, India kuongeza Ushirikiano kuboresha Sekta ya Filamu

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Ushirikiano baina ya Tanzania na India Jijini Dar es Salaam.

Balozi wa India nchini, Binaya Pradhan akiwasilisha hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Ushirikiano baina ya Tanzania na India Jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja


Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Serikali ya Tanzania pamoja na Serikali ya India zimekubaliana kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano ikiwemo sekta ya filamu. 

Akifungua Mkutano wa Kimataifa wa Ushirikiano baina ya Tanzania na India leo Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula, amesema ushirikiano wa Tanzania na India ni wa kihistoria na umekuwa imara nyakati zote, na kwa sasa mataifa hayo yamekusudia kuongeza maeneo ya ushirikiano hususan katika sekta ya filamu.

Balozi Mulamula ameongeza kuwa, maeneno mengine ambayo Tanzania na India zimekusudia kuongeza ushirikiano ni katika sekta ya filamu hasa katika kuwaendeleza wasanii wa Tanzania katika kujifunza zaidi masuala ya uzalishaji wa filamu bora kama wanavyofanya wenzetu wa India.

“Tumekubaliana na Balozi kuwa tufufue ushirikiano katika eneo hili muhimu ili kuwawezesha wasanii wetu hapa nchini kuwa na uwezo wa kutengeneza filamu zenye viwango kama wenzetu wa India,” amesema Balozi Mulamula

Awali Balozi Mulamula amesema ushirikiano wa Tanzania na India umekuwa imara wakati wote kutokana na misingi ya kihistoria iliyowekwa na waasisi wa mataifa hayo mawili, Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julias Nyerere wa Tanzania na Baba wa Taifa la India, Mahatma Gandhi. 

Waziri Mulamula amesisitiza kuwa misingi hiyo imesaidia kukuza ushirikiano wa Tanzania na India katika sekta za elimu, afya, maji, ulinzi, utalii, tehama, kilimo, mabadiliko ya tabia nchi, nishati na uchumi wa buluu pamoja na biashara na uwekezaji. Alama ya ushirikiano katika nyanja hizo iliachwa na waasisi wa mataifa haya mawili (Mwl. Nyerere na Mahatma Gandhi) imekuwa chachu ya kuimarisha uhusiano wa Tanzania na India nyakati zote kwa maslahi ya pande zote mbili.

Amefafanua kuwa ushirikiano baina ya nchi hizo mbili umesaidia watanzania 4,500 kufaidika na fursa ya ufadhili wa masomo ya elimu ya juu inayotolewa na Serikali ya India.

Kwa upande wake, Balozi wa India nchini, Binaya Srikanta Pradhan ameongeza kuwa India imekuwa na uhusiano mzuri na Tanzania, ambapo uhusiano huo umesaidia kuimarisha maendeleo baina ya mataifa hayo katika nyanja za elimu, afya, biashara na uwekezaji, kilimo na utamaduni.

“Ushirikiano uliopo baina ya India na Tanzania umekuwa chachu ya maendeleo kwa mataifa yetu na tumeshuhudia mabadiliko makubwa katika sekta za biashara na uwekezaji ambayo yamekuwa chachu ya maendeleo ya uchumi wetu,” amesema Balozi Pradhan. 

Nae, Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, Achiles Bufure amesema mkutano huo utasaidia kuamsha ari ya vijana kujua ushirikiano kati ya Tanzania na India ulipotoka na unapokwenda. 

Mwezi Agosti, 2022, Tanzania na India ziliahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano ikiwemo kuhakikisha sekta za afya na nyingine zinaimarika ikiwemo kilimo.

Aidha, India kupitia Hospitali ya Apollo zilisaini mkataba wa makubaliano (MoU) na Kampuni ya Eclipse Group Afrika ya Jijini Dar es Salaam wa kujenga Kituo cha Kisasa cha Kutoa Huduma za Uchunguzi za Magonjwa ya Saratani kinachotarajiwa kuanza kujengwa nchini kuanzia mwezi Novemba 2022.

TANGA TAJIRI MATUNDA

$
0
0


 

Adeladius Makwega-MAKOLE

 

Siku moja nilikuwa nasafiri kutokea Dodoma kuelekea Tanga, kwa kuwa siku hiyo usafiri ulikuwa unasumbua sana iliniladhimu kuunganisha magari tangu Dodoma hadi Chalinze kwanza, niliposhuka Chalinze jua lilikuwa limezama huku mji huu ukiwa umechangamka mno.

 

Hata nilipofika hapa usafiri pia ulikuwa mgumu mno, nilisubiri kwa saa kadhaa na baadaye ilikuja gari moja ndogo ya ndugu mmoja ambaye alitufanyia hisani kutuchukua abiria kadhaa lakini hisani yake hiyo haikuweza kupunguza abiria waliopo stendi.

 

Gari nililopanda nilibaini lilikuwa la kiafisaliafisali, ndani yake walikuwapo watu wengine wawili, dereva akawa watatu mie na mwezangu tukawa jumla watu watano. Wakati tunajipanga namna ya kukaa vizuri, kwanza tuliiweka mizigo yetu ya mikononi yakiwa mabegi kadhaa na mie mwanakwetu nilikuwa boksi moja dogo.

 

Ndugu mmoja niliyemkuta ndani ya gari akaniuliza hilo boksi lako umebeba nini? Nilijibu, Nimebeba zabibu, akaniambia weka hapo katikati ya kiti cha dereva, kweli nikafanya hivyo. Akaniuliza umetoka nazo Dodoma? Nilimjibu naam, nawapelekea wanangu huko Tanga, kwa maana Tanga tajiri wa matunda lakini fukara wa zabibu.

 

Ndugu huyu akasema yeye ni mfanyabiashara wa zabibu na kwa mwaka 2022 zabibu zimezaa sana kwa kuwa ni mwaka wa mvua chache. “Hivi tunavyoongea nimetoka kuupokea mzigo wangu wa zabibu kutoka Dodoma ulipelekwa Dar es Salaam. Hapa nakwenda Arusha kuupokea mzigo wangu mwingine umepakiwa Dodoma na umeanza safari kwetu Arusha zabibu zina pesa sana.”

 

Nikampongezi ndugu yetu huyu kwa kufanya biashara hii akisema kuwa mwaka huu watapata pesa nyingi, nilimpa heko kwa kuchagua biashara hii ya msimu akisema msimu ukiiisha huwa anafanya biashara zingine.

 

Ndugu huyu akasema kuwa hata kama unawapelekea wanao jitahidi sana kuwapa zabibu kiasi kidogo usiwape nyingi kwa wakati mmoja, zinalewesha sana hizi. Nikauliza kweli? Ndugu huyu akasema ni kweli kabisa hakuna utani katika hili.

 

“Wakati ninaanza biashara hii nilijifunza jambo moja kubwa sana, wakati wa mavuno ukifika nilikuwa nasimamia kuvuna, kwa kuwa nilikuwa mgeni nilikuwa navuna huku nakula zabibi kidogo kidogo, baada ya muda kidogo naenda kulala nikiwaacha vijana wa kuvuna wakiendelea. Nikija kuzinduka nilibaini kuwa mzigo wangu ulikuwa pungufu mno.”

 

Nilijiuliza maswali shida nini hata gari likija kupakia lilikuwa nusu ya mzigo haupo nikawa napata hasara mno. Jambo hilo lilimsumbua hadi alipokuja kuambiwa kuwa wakati wa kuvuna zabibu mwiko mkubwa hautakiwi kula na kama unahitaji kula zabibu ziliwe wakati zoezi la kuvuna limekamilika.

 

Nikamuuliza ni zabibu zote sharti ni hilo hilo? Ndugu huyu akasema ndiyo tena zile zabibu nyeupe zenyewe ni kali zaidi, kubwa ni kutokuzila kabisa wakati wa kuvuna maana ukifanya hivyo mwanakwertu utakula wa chuya.

 

Vijana wa kigogo ni wajanja sana watakwambia mzee chukua zabibu hii ni tamu zaidi ya ile utapewa kitita cha kwanza utakila utakimaliza utapewa cha pili utakimaliza ukipewa cha tatu mwanakwetu ukikimaliza hali itabadilika.

 

“Sasa hivi nimewambia wadogo zangu ambao wananisimamia kuvuna, kula kula zaibibu wakati wa kuvuna huo ndiyo mwiko wake, kula baada ya kumaliza zoezi.” Alisema ndugu huyu.

 

Dereva wa gari hili akasema siyo katika kuvuna zabibu tu hata hata katika mambo ya uongozi jamii, taasaisi , shirika hata serikalini walio chini wanakutazama mkubwa wewe ukoje kama unapenda kuonja onja iwe pesa au tamaa yoyote. Wakitambua kuwa wewe ni mwanachama wa tamaa watakuwa wanakuletea letea kidogo kidogo, tambua kuwa na wao wanaiba ukishazoea utalewa na mwisho wa siku hamuwezi kuvuna chochote.

 

“Hamuwezi kufikia malengo yenu, mtakwama tu maana mtakuwa ni nyumba ya hasara kila uchao.”

 

Mwanakwetu nilifika Tanga salama salimini na mzigo wangu wa zabibu mkononi na kuwapa wanangu kidogo kiogo kuogopa ule ulevi wa zabibu kama walivyoniambia ndugu zangu hawa na simulizi ya uwoga wa kuvuna hasara na Tanga tajiri matunda.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

TANESCO TABORA INATHAMINI MCHANGO WA TAASISI NA WATU BINAFSI

$
0
0
Mkurungezi wa Tanesco kanda ya Magharibi Mhandisi Richard Swai akimkabidhi  ngao ya shindi kwa kwanza kwa walipaji wa kubwa wa bili za umeme mkoani Tabora mwakilishi wa mkurungezi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira TUWASA Namyaki Molel na aliyevaa hijab ni Meneja wa shirika hilo mkoa wa Tabora mhandisi Khadija Mbarouk.

 

Na Lucas Raphael,Tabora


Shirika la umeme mkoa waTabora Tanesco limetoa zawadi ya ngao kwa  Taasisi na watu binafsi walifanya vizuri  kwa kulipa bila za umeme baada ya kupata huduma hiyo kwa mwaka huu kwa lengo la kutambua mchango wao kwa shirika   .

Akizngumza katika hafla fupi ya kuwapongeza wateja hao meneja wa shirika hilo mkoa wa Tabora mhandisi Khadija Mbarouk iliyofanyika katika ofisi za shirika hilo jana

Alisema kwamba shirika limechukua hatua hiyo ya kuwatambua wateja hao wa kubwa ,baada ya kuonyesha jitiada za kuchangia pato la shirika na serikali kwa ujumla .

Alisema kwamba licha ya shirika kutoa huduma pia linafanya biashara ya usambaza uememe kwa wateja wake hivyo wanawajibu wa kulipa bili zao kila mwezi na kila mwaka kwa wakati.

Mhandisi Khadija alisema kwamba katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja tumeona kutambua wateja wachache waliweza kutumia huduma ya Tanesco na kulipa zaidi ya shilingi milioani 200  kwa mwaka

Meneja huyo wa Tanesco mkoa wa Tabora aliwataja wateja huo kuwa ni  Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoa wa Tabora (TUWASA) iliyotumia huduma ya umeme na kulipia kiasi cha shilling milioni 764,831,278 kwa mwaka huu .

Alisema kwamba licha ya Tuwasa pia Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira wilaya ya Nzega( NZUWASA) ambayo ilitumia huduma ya  hiyo na kulipia kiasi cha shilingi milionbi 164,898,690 kwa mwaka huu.

Wengine ni Kampuni ya simu za mikono ya TTCL ambayo imelipa kiasi cha shilingi milioni 51,083,142 kwa mwaka  na Kampuni ya uchenjuaji wa Dhahabu wilayani Igunga mkoani hapa ya Taur Tanzania ilifanikiwa kulipa kiasi cha shilingi milini 217,976,835 kwa mwaka huu.

Alimtaja mteja mwingine ni  mmiliki wa Hotel ya JM, Jimmy Marco aliyelipa kiasi cha shilingi milioni 25,705,592 mwaka  huu  .

Akizungumza kwa niaba ya wateja wengine mwakilishi wa mkurungezi wa Mamlaaka ya maji safi na usafi wa mazingira mkoani Tabora Tuwasa Namyaki Moleli alisema kwamba wanalishukuru shirika la Tanesco kwa kufanya kitu kama hiki amchao kinachochea ujirani mwema licha ya kupita bilia kwa wakati

Alisema ni wajibu kwa kila Taasisis na watu binafsi wanatumiahuduma ya  umeme au huduma yoyote nyingine ikiwemo maji kukumbuka kulipa bila kwa wakati .

“ umeshapata huduma na umetumia huduma ndivyo hivyo hivyo inakupasa kukumbuka kulipa bili kila mwezi ulipotumia huduma hiyo .alisem Namyaki  



Na Haika Mamuya na Eva Ngowi, WFM, Dodoma

$
0
0

Kamishna wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Elijah Mwandumbya, akisisitiza wadau wa ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kuongeza jitihada zaidi, wakati wa  Semina ya taratibu za ukusanyaji wa mapato hayo, jijini Dodoma.

 

Na Mwandishi Wetu

 
Serikali imezitaka wizara, idara zinazojitegemea na taasisi za Serikali zinazokusanya Mapato yasiyo ya kodi, kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato ili kufikia malengo ambayo Serikali imejiwekea kwaa mwaka wa fedha 2022/2023.

Rai hiyo imetolewa jijini Dodoma na Kamishna wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Elijah Mwandumbya, wakati wa Semina ya taratibu za ukusanyaji wa Mapato yasiyo ya kodi iliyowakutanisha maafisa mipango, TEHAMA, wahasibu na wakaguzi wa ndani.

Bw. Mwandumbya alisema tathmini za hivi karibuni zinaonesha mwenendo usioridhisha wa mapato yasiyo ya kodi kwa Wizara, Idara zinazojitegemea na Taasisi za Serikali zinazokusanya mapato hayo ukilinganisha na  mapato ya kodi.

“Katika Bajeti ya mwaka huu Serikali imejipanga kutumia shilingi trilioni 41 hivyo ni lazima tuikusanye ili kuweza kutekeleza Bajeti iliyopitishwa na Bunge, Mapato hayo ni ya kodi yanakusanywa kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na mapato yasiyo ya kodi yanayokusanywa na Wizara, Idara zinazojitegemea na taasisi za Serikali”, alieleza Bw. Mwandumbya.

Alisema kuwa licha ya mapato yanayokusanywa na TRA, wizara na idara zinazojitegemea, kiasi kinachobaki katika utekelezaji wa bajeti Serikali hukopa mikopo yenye gharama nafuu au mikopo ya kibiashara ambayo ni takribani asilimia 40 ya bajeti yote.

Alisema Serikali hufanya maamuzi ya kukopa ili kutekeleza mipango iliyojiwekea ikiwemo ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ambayo ikikamilika inafungua fursa nyingine za kiuchumi kwa Sekta binafsi kukua na hatimaye kuzalisha mapato zaidi.

Bw. Mwandumbya alibainisha kuwa inapotokea kuna eneo ambalo halijafanikiwa  katika ukusanyaji wa mapato hata kama lilipangiwa kiwango kidogo cha mapato, huathiri utekelezaji wa bajeti Serikali.

Hivyo aliwataka wataalamu walioshiriki semina hiyo kuwa chachu kwa wengine katika maeneo yao kwa kuwajengea uwezo ili kuleta ufanisi na kuhakikisha kuwa taratibu stahiki zinazingatiwa katika ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya Serikali.

Kwa upande wake mshiriki wa semina hiyo, Bi. Rose Werema, kutoka Mahakama ya Tanzania alisema wanaishukuru Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuandaa mafunzo hayo kwa kuwa yatawasaidia kuweka mikakati ambayo itawezesha kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato kulingana na vyanzo vilivyoainishwa.

“Tumeweza kupitishwa katika malengo ambayo Serikali imeweka kwa ajili ya kuweza kuendesha huduma zake mbalimbali na katika hayo tuna sehemu ya kuweza kuchangia ili kufanikisha lengo la Serikali.” alisema Bi. Werema

Wizara ya Fedha na Mipango imeandaa semina hiyo ikiwa ni moja ya jukumu lake katika kusimamia mapato ya kodi na yasiyo ya kodi na pia kutoa fursa ya wadau kubadilishana mawazo na uzoefu katika ukusanyaji wa mapato hususani yasiyo ya kodi.

POSTA SINGIDA YAFANYA MABORESHO MAKUBWA YA KITEKNOLOJIA KWENYE UTOAJI HUDUMA

$
0
0

Wafanyakazi wa shirika la Posta Mkoa wa Singida wakishiriki zoezi la kufanya usafi ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja yaliyofanyika jana mkoani hapa. Wa pili kulia ni  Meneja wa Posta mkoani hapa, Michael Mwanachuo.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Ufanyaji usafi ukiendelea.
Wafanyakazi hao wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa zoezi hilo la kufanya usafi.
 

Na Godwin Myovela, Singida

KAULI Mbiu inayovuma kwa kasi ya Shirika la Posta nchini (TPC) isemayo ‘Posta Twenzetu Kidijitali-Haijawahi Tokea! imezidi kujidhihirisha kupitia ofisi za shirika hilo mkoani hapa, ambapo kupitia wiki ya huduma kwa wateja, mamia ya wananchi wameonyeshwa kufurahishwa na maboresho ya kihuduma yanayoendelea kutolewa kwa sasa.

 Akizungumza muda mfupi baada ya wafanyakazi wa shirika hilo kushiriki zoezi la kufanya usafi wa mazingira na kutoa faraja kwa wagonjwa ndani ya hospitali ya mkoa wa Singida-kama azma yake kwenye ushiriki wa majukumu ya kijamii, Meneja wa Posta mkoani hapa, Michael Mwanachuo, pamoja na mambo mengine alisema mwaka huu shirika hilo limekuja kivingine.

Alisema wakiwa kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja, inayokwenda sambamba na shamrashamra za shirika hilo kuelekea kilele cha siku ya Posta Duniani ambayo huadhimishwa ifikapo Oktoba 9 kila mwaka shirika kwa kuzingatia mifumo ya kasi ya TEHAMA linaendelea kusafirisha barua kwa njia ya haraka (EMS) ndani na nje ya nchi na usafirishaji mizigo mikubwa.

Pia kwa kutumia TEHAMA ya Posta Kiganjani ambayo humwezesha mteja yeyote kupata huduma za posta popote, Mwanachuo alisema mpaka sasa fursa mbalimbali kwa matokeo bora na ya uhakika zinaendelea kutolewa kwa kuzingatia kasi na ufanisi, ikilinganishwa na siku za nyuma.

“Posta kwa sasa tupo kidijitali zaidi nitoe wito kwa umma kuzidi kutembelea ofisi za shirika letu na kutuunga mkono kwa kujipatia huduma zetu mbalimbali za kidijitali zilizoboreshwa.” Alisema Mwanachuo.

Shirika hilo kwa sasa pamoja na mambo mengine linatoa huduma za kidijitali za Uwakala wa Fedha, Masanduku ya Barua, Duka Mtandao, Intaneti Café, na mfumo madhubuti wa kufuatilia barua au kifurushi kilichotumwa kupitia mtandao kujua kimefikia wapi au kimepokelewa na nani.

Huduma nyingine ni pamoja ‘Posta Cash’, Uwakala wa Bima, Huduma za uuzaji wa hisa za makampuni mbalimbali na huduma za Bodi ya Mikopo na Baraza la Mitihani sanjari na huduma kwa wananchi wanaohitaji vyeti vya kuzaliwa ambapo kazi ya kujaza fomu na nyaraka zote ni sehemu ya majukumu ya shirika hilo ambapo mwananchi akikamilisha taratibu zote anakwenda kwa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa hatua ya mwisho ya kuchukua cheti.

Shamrashamra hizo zilipambwa na shughuli mbalimbali kwa shirika hilo mkoani hapa kufanya usafi wa mazingira, utoaji wa huduma za kidijitali sanjari na kujumuika kukata na kula keki na wateja wake ‘wakiwemo wachezaji wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Singida Big Stars’ kama sehemu ya kurudisha shukrani.


LANDESA:UWEKEZAJI WAJIBIFU WA ARDHI YA JAMII UTAPUNGUZA MIGOGORO

$
0
0

Mkurugenzi wa Landesa Tanzania, Godfrey Massay akipekua baadhi ya taarifa za ardhi wakati wa mafunzo ya wanahabari na wadau wa ardhi yaliyofanyika mjini Morogoro.

KARIBU ALI MAYAI

$
0
0


 

Adeladius Makwega–MAKOLE

 

Oktoba 5, 2022 nikiwa Mji wa Serikali Jijini Dodoma, nilipata bahati ya kumuona Ali Mayai Tembele akipita katika ofisi moja ya watumishi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo alimsabai mwanakwetu. 

 

Katika msafara wake ndugu Tembele ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo nchini aliambatana na Ado Komba ambaye mimi natambua cheo chake cha awali ni Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo nchini kabla ya kuondolewa mwalimu Yusuf Singo.

 

Mwalimu Ado Komba ni kiongozi ninayeheshimiana naye sana na kumfahamu muda mrefu tangu akiwa TAMISEMI, siku hiyo alimuongoza ndugu Tembele nilipo na kusema neno hili,

 

“Huyu jamaa unayemuona anaitwa Kazimbaya Makwega, hatari sana, kuwa naye makini.” Aliyasema maneno haya kwa utani huku na mwanakwetu akicheka, akilini mwangu nikatafakari sana kwa kuwa Ado Komba ni mwalimu wa michezo wa muda mrefu na utani katika michezo una nafasi kubwa katika kupeleka ujumbe. 

 

Nilijiuliza kwanini Mwalimu Komba anitanie mbele ya kiongozi mgeni? Kwani asinitanie hivyo tukiwa wenyewe ? Mbona hajawai kunitania hivyo? Nikatafakari hilo nikasema hapa na mimi niseme jambo kwa kiongozi huyu mpya wa michezo nchini Tanzania ambaye ndiyo kwanza ameingia ofisini. Ofisi nilipokuwapo kwa juu kulikuwa na picha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ikishuhudia Tembele na Komba nikizungumza nao.

 

“Tembele wasaidie hawa jamaa, kwa sasa ni sawa na ile simulizi ya nitampiga mchungaji wa kondoo na kundi lake litatawanyika, waweke pamoja, fanya nao kazi kwa karibu hili tupate maendeleo ya michezo nchini Tnazania.”

 

Ali Mayai akacheka, wakaondoka zao kuelekea ofisi zingine za wizara hiii.

 

Kwa bahati nzuri Mkurugenzi wa Michezo aliyeondoka ndugu Yusuf Singo binafsi ninamfahamu na nimewahi kuingia nae katika vikao kadhaa vya kamati za Bunge akiwa na viongozi kadhaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na baadaye Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Ninaweza kusema haya dhidi yake,

 

“Yusufu Singo alikuwa ni Mkurugenzi mwenye umahiri mkubwa katika propaganda ya michezo na hata anapolielezea suala la michezo kwa mtu anayefahamu elimu hii na hata yule ambaye hafahamu elimu hiyo ilikuwa ni rahisi mno kumuelewa, kwa hakika alikuwa anafahamu michezo ya darasani vizuri sana. Lakini Singo hakuwa mchezaji wa moja kwa moja kitu ambacho Ali Mayai Tembele anacho japokuwa Tembele nayeye kuwa mahiri katika propanganda ya michezo yote anakosa, lakini mchezo wa soka propaganda yake anaifahamu.”

 

Tembele kuwa mchezaji wa mchezo mmoja shida yake bado anahitaji mno elimu ya kuwekeza kujifunza uongozi katika michezo mingine kama vile riadha, ngumu, netibali na kadhalika na kuifahamu hiyo ndiyo kurugenzi ya michezo, ili afuzu katika hilo ndugu huyu anawajibu wa kuwakusanya kondoo waliotayawanyika baada ya kupigwa mchungaji wao.

 

Ninaamini Ili kuboresha michezo nchini nafasi kama hizi wakati mwingine kama itatupendeza tuchukue maafisa michezo waliopo katika katika vyombo vya ulinzi ili waje kujenga ari ya michezo kitaifa na mwisho mafanikio ya michezo.

 

Swali ambalo linabaki kwa kila mmoja wetu kama Yusuf Singo alishindwa je alishindwa yeye mwenyewe peke yake? Sie tulio chini au wale walio juu hawakumkwamisha? Je adhabu inapaswa kuendelea kwa walio chini na walio juu yake? Je Tembele hayawezi kumkuta yalimkuta Yusuf Singo?

 

“Katika michezo tukishinda tunashinda sote; tukifungwa tunafungwa sote.” Hii tafakari sana msomaji wangu.

 

Mwanakwetu ninaomba niishie hapo kwa leo,  kwaheri Yusuf Singo Karibu Ali Mayai.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

 

 

 

DUWASA YAITUNUKU CHETI UDOM

$
0
0


Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) inaungana na taasisi, mamlaka na kampuni mbalimbali kuadhimisha ‘Wiki ya Huduma kwa Mteja’ kwa kuwafikia wateja wake wakubwa na wadogo katika maeneo tofauti tofauti.

Mkurugenzi wa Manunuzi DUWASA, Bw. Alex Maheri akiongoza ujumbe wa Mamlaka hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Mhandisi Aron Joseph amekabidhi cheti cha kumtambua mteja wetu mkubwa ambaye ni Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).


Cheti hicho, kimepokelewa na Naibu Makamu Mkuu wa UDOM, Profesa Wineaster Saria.

Baadhi ya viongozi wengine wa DUWASA walioambatana na Maheri ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja, Bw. Philipo Funga, Meneja Huduma kwa Wateja, Bi. Pendo Mkali.

Wengine ni, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, Bw. Edwin Mwijage na Meneja wa DUWASA Kanda ya Kongwa, Bw. Amran Gama ambapo walitoa elimu, kupokea na kusikiliza malalamiko na ushauri kutoka kwa wateja katika Kanda ya Kongwa eneo la Morisheni, Machinjioni na Ngonga.

YANGA YAJITEGA KWA IBENGE

$
0
0

 



Na Mwandishi Wetu

Halijawaka wala Haijanyesha lakini ngoma sare sare mauwa, mechi dume ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL)

Dakika 90 za kwanza zimetamatika kwa Yanga kulazimishwa sare ya bao (1-1) matokeo ambayo sio mazuri licha ya kuwa na dakika 90 za kujiuliza mjini Khatoum nchini Sudan wiki ijayo.

 Si matokeo mazuri kwa Yanga kwa sababu walihitaji tofauti kubwa ya mabao katika uwanja wao wa nyumbani, kwa matokeo haya maana yake ni lazima akafunge bao ugenini, sare ya 0-0 amepita Al Hilal, hapa pia inatategemea wao wanakwenda vipi kuzuia kule Omdurman, mechi imekuwa ngumu zaidi kwao kuliko Al Hilal kutokana na nature ya mashindano ya CAF, mtu anashinda kwake.

Florent Ibenge alikuja na game approach ambayo ilifanikiwa katika matendo ya mwendo, Al Hilal ilikuja na mpango kazi wa kucheza dhidi ya namna ya uanzishwaji wa mashambulizi ya Yanga, waliwatia presha Yanga wakiwa na mpira wachezaji watano wanakuwepo katika nusu  ya Yanga ili waanze kukabia juu.

Kuna nyakati ambazo Yanga walifanikiwa lakini katika nyakati ambazo Yanga ilifika kwenye eneo la mwisho bado ilimkosa mtu ambae anaweza kuutuliza mchezo, timu ikakosa utulivu.

Mapema kipindi Cha pili bao la Fiston Mayele likawamusha Al Hilal waliamua kukabia katikati mwa uwanja Ili kuziba mianya ambayo Yanga walichotaka kuzitumia na kushambulia kwa mashambulizi ya kushitukiza bao likapatikana.

Mkoba wa mbinu za  Mohammedi Nabi ni kama alijifunga,  mosi kukosa kiungo wa kunusa hatari na mwenye sifa za ukabaji Ili aweze kuziba mianya kati ya viungo washambuliaji na mabeki wa pembeni.

Al Hilal waliendelea kutumia udhaifu huo bahati nzuri kwa Yanga ni ubora na bahati kwa ya mlinda mlango wao Digui Diarra akiokoa zaidi ya nafasi tatu za wazi.

Ni kibarua kizito kwa Yanga mosi kukubali presha ya wasudan lakini pia kukabiliana na Ufundi wa vijana wa Florent Ibenge.

WANASIIIMBA, RUKENI NA MBAWA ZENU

$
0
0



Na John Richard Marwa


'Kila Ndege huruka na mbawa zake' ndio, kama Popo na mbawa zake huruka kivyake, Mwewe na mbawa zake hunyakua mwenyewe, ni kama kasi ya binadamu Iko miguuni mwake.


Leo ni siku adhimu kwenu wanasimba, siku inayowakumbusha mapito yenu yaliyojenga jina lenu na limekaa kwenye mioyo ya Waafrika na wapenda soka.


Ni kipindi cha kwanza cha dakika 90 za ugenini dhidi ya De Agosto fanyeni kama mlivyowafanya Mbabane Swallows, Nkana Red Devils na Red Arrows hapo jana.


Njia ni ileile ya kusini mwa Afrika, kwenda kuwatesa kaskazini mwa Afrika mliyoifanya kuwa mbuga yenu. Sio Serengeti wala Ngorongoro bali mapori yote ya Afrika mnayatawala.


Kumbukeni 'Maji ukiyavulia nguo huna budi kiyakoga' kawaonyeshe hao wa Angola namna ya kukoga na kunawa, namna ya kutafuna kisha njooni nao muwafunze kumeza.


Vipi Ndugu yenu kawaangusha?? ama mlimuachia mzinga asijue cha kufanya? Nyuki wamemwachia nundu, sumu Iko kwenye utamu wake. Si mnajua mzinga wenu na nyuki wake, basi 'Mfuata nyuki hakosi asali', asali' yenu ni De Agosto, mumunyeni ama lambeni lunyasi.


Mnatambua kuna ugumu, lakini msisahau.. 'Mchumia juani hulia kivulini' kubalini kuteseka leo, kivuli cha makundi mtashibia hapo si mnajua zigo limetuna?!


Kama kuna ugumu utajitokeza kumbukeni Mkoba wenu... 'Mbinu hufuata mwendo' ishini humo maana mwendo wenu mnaujua, basi rejesheni mbinu zenu kwenye uwanja wa vita.


Vipi nafsi zenu zimepooza baada ya mtani kushindwa kutamba ama Azam kulishwa 'ice cream zake mwenyewe'?! Kumbukeni kuwa 'Mchimba kisima huingia mwenyewe' ndio hiki ni kisima chenu wenyewe mlichokichimba ingieni kunyweni maji yenu kwa utulivu, ndugu zenu wataendelea kujifunza wawe kama nyinyi.


Kila la heri Simba SC, kumbukeni mna Chama, Okrah, Phiri, Sakho, Bocce, Zimbwejr, Kanoute, Mkude, Mzamiru, Inonga, Onyango, Manula na vijana wenu, Afrika inawaamini ndo fahari ya  hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL.


NMB yaongeza kiwango cha mkupuo mmoja wa mkopo hadi 250bn/-

$
0
0

 

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng’wilabuzu Ludigija (wa pili kushoto) akipeana mkono na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa katika hafla ya kukutana na wateja wakubwa wa Benki ya NMB katika hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mstahiki Meya wa jiji la Ilala, Omar Kumbilamoto na kulia ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard.

 

Na Mwandishi Wetu

 

Ufanisi mkubwa wa kiutendaji ambao Benki ya NMB imeupata miaka ya hivi karibuni umeiwezesha taasisi hiyo kinara wa huduma za kifedha nchini kuimarika kiufadhili.

 

Viongozi wake waandamizi wamebainaisha mwishoni mwa juma lililopita kuwa miongoni mwa matokeo ya kufanikiwa huko kifedha ni kuiwezesha benki hiyo kuongeza kiasi cha mkupuo mmoja wa mkopo kwenye miaka ya hivi karibuni.

 

Akizungumza Ijumaa jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya Mtandao wa Wateja Wakubwa na Wanaochipukia (BEN) wa NMB Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa benki hiyo, Bw Benedicto Baragomwa, alisema kiwango kikubwa cha mkupuo mmoja wa mkopo sasa kimefikia TZS bilioni 250.

 

Kiasi hicho ni kikomo cha kikanuni ambacho benki hiyo inaweza kumkopesha mteja mmoja kwa mkupuo.

 

Hilo limewavutia sana wateja wa NMB na viongozi wa jiji na mkoa wa Dar es Salaam walioudhuria mkutano huo walioipongeza kwa hatua hiyo kubwa kiufadhili na kusema ni matokea ya uwezo wake kiubunifu na uwekezaji wa kizalendo inaoufanya nchini.

 

“Sisi ndio mkopeshaji mkubwa mwenye viwango vya faida ambavyo havina mpizani sokoni na haina tofauti tofauti za huduma za mikopo kama ile ya dharura inayopatikana papo kwa papo kidijitali kwa kutumia simu za mkononi,” Bw Baragomwa aliwaambia washiriki 100 wa mkutano wa BEN wa Mkoa wa Dar es Salaam.

 

Akizungumza katika hafla ya namna hii iliyofanyika pia katuika jiji la Mbeya, mkuu wa idara ya mikopo wa benki ya NMB, Demetus Kamguna alisema sasa hivi NMB inajivunia kuwa na mizania mipana yenye rasilimali zenye thamani ya takribani TZS trilioni 9 pamoja na amana zipatazo TZS trilioni 6.6.

 

Aidha, alisema kukua kwa mali zake zote kumesaidia kupanua kiasi cha mtaji wake hadi zaidi ya TZS trilioni 1 na kupelekea kuzidisha ukomo wa mkupuo mmoja kwa kila mkopaji mwenye sifa.

 

“Pia NMB tunatoa mikopo kadri ya uwezo wa mfanyabiashara, tukiwa na uwezo wa kutoa hado TZS bilioni 250 kwa mkopaji mmoja,” kiongozi huyo mwandamizi alisema kwenye mchapalo huo wa kujadili masuala muhimu na wateja wake wakubwa wa Mkoani Mbeya uliofunguliwa rasmi ya Mkuu wa Mkoa ya Mbeya, Bw Juma Homera.

 

Akielezea kiwango kipya cha mkupuo wa juu wa mkopo kwa kila mteja, Mkuu wa Idara ya Biashara wa NMB, Bw Alex Mgeni, alimwambia mwandishi wa habari hii kuwa maendeleo ya ukopeshaji yaliyopatikana pia ni matokea chanya ya faida kubwa ambazo NMB imekuwa ikipata miaka ya hivi karibuni.

 

Pamoja na mambo mengine mengi, faida za NMB zimekuwa pia zikitumika kuimarisha utendaji na uendeshaji wa benki hiyo na pia kudhatiti mtaji wake. Matokeo ya uwekezaji huo, Bw Mgeni alifafanua, ni pamoja na kuongeza kiwango cha NMB kuwakopesha wateja wake.

 

“Kimsingi, mtaji wetu sasa ni TZS trilioni 1.2 ambazo zinapelekea mkupuo mmoja wa mikopo yetu kufikia hadi TZS bilioni 300 kwa kuzingatia kanuni ya Benki Kuu ya benki kukopesha asilimia 25 ya mtaji wake,” Bw Mgeni alisema.

 

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mkjuu wa mkoa wa Mbeya aliwasihi Benki ya NMB kuendelea kuwaunga mmono wakulima kwani ni sekta inayokuwa kwa kasi sasna kwa hivi Karibuni huku akisisiktiza juu ya kuendelea kuwek nguvu kubwa katika ufadhili wa kilimo cha maparachichi, mchele na pareto.

 

Aidha, katika hafla ya jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bw Ludigija, aliimwagia sifa NMB kwa kuja na wazo la BEN akisema si muhimu tu kwa ajili ya kupata mrejesho kutoka kwa wateja lakini pia kusaidia kuchangia mawazo ya sera za kitaifa.

 

NMB ilianzisha mtandao wa BEN mwaka 2014 ikilenga kuitumia mikutano yake kama jukwaa la kukutana na wateja wake wenye mzunguko wa fedha kuanzia TZS bilioni 5 kwa mwaka kwa ajili ya kubadirishana wazo na uzoefu wa kibiashara.

 

Mpango huo ulilenga mikoa mikubwa na inayoongoza kiuzalishaji na mpaka sasa, mtandao huu upo kwenye mikoa saba tu ambako ina washirika zaidi ya 1,000. Mikoa hiyo ni Dar es Salaam, Dodoma, Morogoro, Kilimanjaro, Mwanza, Arusha na Mbeya.

 

Kwa upande wake, Meya wa Ilala, Bw Omary Kumbilamoto, alisema NMB sasa ni mshirika wa kimkati wa maendeleo ya kibiashara wa kitaifa ambaye anaisaidia Serikali ya Awamu ya Sita kuboresha upatikanaji wa huduma za kijamii.

SIKU 558 ZA SAMIA MADARAKANI MISINGI YA FALSAFA ZA UCHUMI KUONGOZA UCHUMI ZAFANIKIWA- MWENEZI SHAKA

$
0
0

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, AKIKAGUA Baadhi ya Mabanda ya Maonesho 
alipotembelea Maonesho ya Tatu ya Uwekezaji na Biashara Mkoa wa Pwani leo Oktoba 9, 2022, Kibaha mkoani Pwani (Picha na Fahadi Siraji CCM).
 
 
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amesema ndani ya siku 558 tangu Rais Samia Suluhu Hassan aapishwe kuwa Rais wa Tanzania, amefanikiwa kutekeleza Misingi ya falsafa za uchumi kuongoza uchumi waTanzania

Shaka ameyasema hayo leo Oktoba 9, 2022, Kibaha mkoani Pwani alipotembelea Maonesho ya Tatu ya Uwekezaji na Biashara Mkoa wa Pwani amesema misingi hiyo ni pamoja na kuvutia wawekezaji, ushirikishaji sekta binafsi na kutumia diplomasia badala ya mabavu katika kufungua uchumi.

"Leo ni takribani siku 558 tangu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aapishwe kuwa Rais wa nchi yetu, ambapo baada ya kiapo alitoa mwelekeo wa serikali atakayoiunda na kuiongoza kuwa, nia yake ni kuifungua nchi kiuchumi.

"Sote ni mashuhuda tumeanza kushuhudia akiruhusu misingi ya falsafa za uchumi kuongoza uchumi badala ya nguvu za kiutawala. Tumeshuhudia Rais Samia akitumia taaluma yake ya uchumi na uzoefu wake wa kiuongozi na masuala ya kidiplomasia akibadili kabisa mazingira na kasi ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo," amesema.

Shaka amesema ndani ya kipindi hicho kupitia diplomasia ya uchumi Rais Samia amefanikiwa kutafuta na kuvutia wawekezaji, kuimarisha mazingira ya biashara na kuongeza shughuli za uzalishaji zitakazoongeza ajira na mapato ya serikali.

Aidha, amesema ameimarisha mazingira ya bishara na uwekezaji kwa kuondoa urasimu, ukusanyaji kodi wa mabavu, kufanya maboresho ya sheria na mifumo mbalimbali kwa lengo la kuondoa kero kwa wafanyabiashara na wawekezaji ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ibara 22, 46 na 49.

Akiwa katika maonyesho hayo, Shaka ambaye aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Sara Msafiri ametembelea mabanda mbalimbali yanayoshiriki maonesho hayo yakiwamo ya taasisi za umma, binafsi na wajasiriamali.


Akitoa shukran, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas alisema ziara na maonyesho hayo yamempa funzo kubwa katika kwamba akirudi mkoani kwake atakwenda kulifanyia kazi.

Akiwa katika maonyesho hayo, Shaka alitembelea mabanda mbalimbali yakiwemo ya taasisi za umma, binafsi na wajasiriamali ambao wameyatumia kuonyesha bidhaa na huduma mbalimbali wanazozitoa.

DE AGOSTO WAKUBALI YAISHE KWA MNYAMA

$
0
0


Na Mwandishi Wetu


Fantastic, yes it was fantastic for Simba SC, wanachokifanya Simba kimataifa hata kama hujui kiingereza utafurahi tu.

Mechi ngumu huchezwa kigumu na akili kubwa, unaweza sema wanakutana na wapinzani wepesi lakini itazame Simba wanavyocheza wakiwa Ligi ya Mabingwa Afrika utaelewa wamekomaa kila eneo japo mapungufu yapo lakini ni ngumu kuzima roho zao ngumu huku.

Ulikuwa mchezo wenye ushindani kwa pande zote mbili lakini hesabu za Juma Mgunda ni kuicheza mechi kimkakati, pata bao mapema kisha miliki mpira wape mpira. Ndicho lilionekana dakika 45 za kwanza.

Chama ni kama mishipa ya damu kwenye Moyo ndani Simba, huamua mapigo yaende kasi ama taratibu, utulivu wake ni zaidi ya kasi ya Hussein Bolt, alifunga kabla ya kufunga alivyowahadaa walinzi wa De Agosto.

De Agosto walijaribu kupeleka presha kwenye lango la Simba kupitia pembeni lakini zao lao la mwisho lilikuwa linaishia kwa Onyanga na Inonga ama Mzamiru na Kanoute.

Simba walikuwa bora sana jinsi walivyokuwa wanafanya shinikizo katika kuutafuta mpira, hapa ndio ubora wa wachezaji wote ulikuwa mtaji wa Simba kuwazima De Agosto.

Kipindi cha pili De Agosto ni kama walitiwa ndimu na kulazimisha mashambulizi huku viungo wao wa ulinzi wakiacha nafasi kubwa na walinzi wao na mawinga wakawa hawawasaidii walinzi wa pembeni wanapopotez mipira.

Chama na Phiri walizama kwenye hayo mashimo kulia na kushoto mabao mawili yakapatikana kupitia kwa Mwenda na Phiri.

Jenerali Moses Phiri anachojia ni kufunga na kufunga kuko damuni mwake anatumia vema pasi ya Chama na kuipatia Simba bao la tatu na la ushindi.

De Agosto walikuwa hawana namna kwa sababu walitaka kutumia mipira ya juu lakini shinikizo la Simba lilikuwa linaua mipango yao na kukosa makali.

Licha ya ubora wa mchezaji mmoja mmoja kushindwa kuwapa walichohitaji iliwallpa kwa kupata mkwaju wa penati na kuweza kupata  bao la kufutia machozi.

Mzamiru Yassin ni ngumu kumpenda kama hupendi mpira ila mapafu yake ndio silaha ya Simba katika kujilinda na kushambulia.

De Agosto wanahitaji kushinda mabao 4-0 mchezo wa marejeano katika Dimba la Benjamin Mkapa wiki ijayo, swali ni je wataweza kuupanda mlima huo ni jambo la kusubiri na kuona.

Kocha Juma Mgunda ni swali gani hajajibu ndani ya mechi Saba ameruhusu bao moja kwa mkwaju wa penati.

Ni dakika 90 za ugenini zilizolibeba jina la Simba kwenye bendera ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL.

Nape awataka watoa huduma wote nchini kutumia mfumo wa anuani za makazi

$
0
0

Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Macrise Mbodo akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Posta duniani katika ukumbi wa Julius Nyerere Internationa Convention Centre, jijini Dar es Salaam Oktoba 09, 2022.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Posta duniani katika ukumbi wa Julius Nyerere Internationa Convention Centre, jijini Dar es Salaam Oktoba 09, 2022.


Na Mwandishi wetu


Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye

amewataka watoa huduma wote nchini kutumia mfumo wa anuani za makazi ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi nchini.


Nape ameyasema hayo leo wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Umoja wa Posta Duniani (UPU) yaliyofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam (JNICC).


Amesema ni muhimu kwa watoa huduma wote nchini kutumia mfumo huo wa anuani za makazi ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.


"Na hapa niwashukuru sana Shirika la Posta Tanzania (TPC), kama kuna taasisi ambayo imeshiriki vizuri sana kuhakikisha mfumo wa anuani za makazi unakaa mahali pake ni shirika hili la Posta, tunapaswa kuwapongeza,"  amesema Nape


Aidha amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan  imejipanga kuwawezesha watoa huduma za posta ili waweze kuwafikia wananchi kwa urahisi bila kulazimika kufika kwenye ofisi za posta.


"Hilo litawezekana kwa kuwa serikali inakamilisha utekelezaji wa mfumo wa anuani za makazi ambao ni miundombinu muhimu katika utekelezaji wa huduma za posta hasa katika kumfikishia mteja barua au mzigo katika eneo lake la makazi," amesema


Aidha amesema takwimu za Tanzania zinaonesha kuwa simu ambazo zipo mtaani kwa sasa ni Milioni 58 lakini kati ya hizo, milioni 37 wanatumia simu kama njia yao ya kufanya manunuzi.


"Kwa takwimu hizo ni wazi kuwa watanzania wengi wanatumia simu na Posta wanasema wapo kiganjani hivyo wakiweza kiwatumia watu hapo Milioni 37 ni mtaji wao mkubwa sana," amesema


Kwa upande wake Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Macrise Mbodo amesema Posta ya sasa ni ya kila mtanzania kwani katika eneo la usalama wamekuwa wakishirikiana kwa ukaribu na vyombo vya ulinzi na usalama katika kudhibiti usafirishaji haramu wa silaha za kivita.


"Tunashirikiana na vyombo vya usalama katika kudhibiti mtandao wa usafirishaji wa dawa za kulevya, na ikitokea watu wanajaribu kufanya uhalifu huo kwa namna ambavyo tumejipanga, wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria," amesema


Hata hivyo amesema pia Posta wamekuwa wakishirikiana kwa ukaribu na Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia duka mtandao kwa kutoa fursa kwa watanzania ambao ni wafanyabiashara kuuza na kuunua bidhaa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kupitia duka hilo.


"Katika eneo la elimu, tunashirikiana kwa ukaribu na Baraza la Mitihani (NECTA) na Bodi ya Mikopo katika kuwasaidia wanafunzi wanapofanya usajili wa kufanya mambo yao kisha kuyasafirisha kwa njia ya Posta," Mbodo na kuongeza


"Pia tunashirikiana na Wizara ya Afya katika kusafirisha sampuli za maabara zote nchini kutoka kwenye vituo vya afya ngazi ya kwanza kwenda vituo vya afya ngazi ya pili na kisha kwenda kwenye maabara za uchunguzi na baadae kùrejesha majibu, kupitia mfumo huo tumeajiri zaidi ya vijana 500 wa bodaboda," amesema a

Wafanyakazi wa Benki ya NMB waanza safari kupanda Mlima Kilimanjaro

$
0
0

 

Msafara wa wafanyakazi wa NMB wanaopanda Mlima Kilimanjaro wakiwa katika picha ya pamoja na wenzao wa Matawi ya Moshi, waliofika kuwatakia kila la kheri kabla ya safari yao ya siku 7.

  Ofisa Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) - Charles Ng'endo, akiwakabidhi rasmi bendera wafanyakazi wa Benki ya NMB watakayoipeperusha katika kilele cha Mlima Kilimanjaro. Akishuhudia ni Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini-Dismas Prosper (Mwenye  tisheti ya bluu).

Msafara wa wafanyakazi wa NMB wanaopanda Mlima Kilimanjaro wakiwa wameanza safari yao ya siku 7.

 

Na Mwandishi Wetu

 

Ikiwa ni mwendelezo wa kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja, wafanyakazi 6 wa Benki ya NMB jana wameanza safari ya siku 7 ya kupanda Mlima Kilimanjaro kupitia geti la Machame ambapo wataipeperusha bendera ya benki hiyo katika kilele cha mlima huo.

 

Akizungumza katika hafla ya kuwaaga na kuwakabidhi rasmi bendera wafanyakazi hao, Ofisa Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro(KINAPA), Charles Ng'endo alisema kama Hifadhi ya KINAPA wamefarijika sana na utaratibu iliofanywa na NMB katika kuadhimisha mwezi huu muhimu wa huduma kwa wateja kwa kupanda Mlima Kilimanjaro, aidha wao kama hifadhi  watahakikishia kuwa wamewawekea mazingira mazuri na utaratibu mzuri wa kuwahudumia mpaka wanafika kileleni.

 

Aliongeza kuwa “kufanya hivi kunatusaidia kutangaza utalii wa ndani na tunafahamu hifadhi ya Taifa TANAPA na NMB tumekuwa na mahusiano ya karibu ya kibiashara na kiutoaji wa huduma kwa wananchi. Hivyo, kupanda Mlima Kilimanjaro na kufika kileleni kutaimarisha mahusiano kati yetu sote na kupeleka ujumbe kwa wateja wetu kuweza kutangaza utalii wa ndani,"

 

Nae Meneja wa benki hiyo Kanda ya Kaskazini-Dismas Prosper alisema kuwa, NMB kwa kutambua umuhimu wa sekta ya Utalii hapa nchini, waliona ni jambo la kifahari kusherekea mwezi wa huduma kwa wateja pamoja na wateja wao ambao wapo katika hii kwa kupandamlima Kilimanjaro ili kuutangaza mlima huo. Timu hiyo imepandishwa Mlima na kampuni ya Zara tours yenye uzoefu wa miaka mingi.

 

Akimalizia kuzungumza, kiongozi wa msafara huo wa wafanyakazi wa NMB ambaye pia ni Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa wa NMB – Alfred Shao alisema kuwa, NMB imefanya mambo mengi makubwa hapa nchini ikiwamo kuwa Benki bora na yenye masuluhisho mengi ya kifedha kwa wateja wao na kwamba wanataka kuwadhihirishia umma na wateja wao kuwa wanao uwezo wa kuwahudumia mpaka kilele cha Mlima Kilimanjaro na wajue wanamaanisha wanaposema ‘NMB Karibu Yako’.

 

Wengine waliopanda Mlima ni Nishad Jinah, Stella Motto, Reginald Baynit, Agnes Mlolele na Christopher Mwalugenge

 

 

 

 

KANISA LA CAG KUFANYA MAOMBI KWA VIONGOZI WAKUU WA NCHI LEO

$
0
0


Dunstun Maboya, Askofu Mkuu wa Kanisa la CAG, Ubungo jijini Dar es Salaam.

 

Na Mwandishi Wetu

MAOMBI maalum ya  kuwaombea viongozi wakuu wa nchi, pamoja na Tanzania kwa ujumla yanatarajia kuanza leo (jumatatu) jijini Dar es Salaam.

Maombi hayo ya wiki moja yatakayoambatana na semina ya neno la Mungu yameandaliwa na kanisa la Calvary Tanzania Assemblies of God (CAG) 'Chuo cha Manabii', lililopo eneo la Bandari Kavu, Ubungo Maziwa.

Akizungumza kanisani hapo jana,Katibu wa Kanisa hilo Lucas John alisema maombi hayo ni sehemu ya kutimiza maandiko katika biblia.

"Maandiko katika waraka wa kwanza kwa Timotheo 2:1-2,Mungu ameliagiza kanisa kufanya maombi kwa ajili ya viongozi na wenye mamlaka ili Taifa lidumishe upendo,amani na utulivu,"alisema

"Kufanya hivi ni katika kutii agizo hilo pamoja na kutekeleza moja ya majukumu ya msingi ya kanisa letu,"aliongeza

Katibu huyo alisema maombi hayo yataongozwa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo,Imelda Maboya akishirikiana na viongozi wengine,yatafikia tamati jumapili ijayo Octoba 16,2022

"Tunawakaribisha watu kutoka sehemu mbalimbali jijini kuhudhuria maombi haya yatakayokuwa yakianzaa saa 11 jioni kanisani hapa,"aliongeza.

CAG ina makanisa zaidi ya 1500 Tanzania Bara na Zanzibar.
 

TEMBO WORRIES YAITWANGA ITALIA TANZANIA IKISHIKA NAFASI YA SABA DUNIANI

$
0
0


Na Mwandishi Wetu

Timu ya Taifa ya Tanzania Soka la Watu wenye ulemavu 'Tembo Warriors', baada ya kufika robo fainali ya Fainali za Kombe la Dunia la Soka kwa Walemavu, imemaliza mechi za kuwekwa katika viwango vya ubora duniani kwa kuitandika Timu ya Taifa ya Italia kwa mabao 2-0 katika mechi kali iliyochezwa mjini Istanbul, Uturuki.

Tembo Warriors inarejea nyumbani leo mchana inatarajiwa kupokewa na maelfu ya mashabiki wa michezo.

Timu tatu za Afrika; Angola, Morocco na Tanzania ndio pekee zimeingia 10 Bora ya Orodha ya Viwango vya Shirikisho la Soka kwa Walemavu Duniani (Waff). Hongera Tembo Warriors, Hongera Tanzania.

Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>