Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

FEISAL ATWAA TUZO YA MWEZI NBC PREMIER LEAGUE

$
0
0


Na Mwandishi Wetu
 
KIUNGO wa timu ya Young Africans, Feisal Salum, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Septemba wa Ligi Kuu ya NBC, huku Kocha Mkuu wa timu ya Namungo FC, Honour Janza akiibuka Kocha Bora wa mwezi huo.  
 
Kikao cha Kamati ya Tuzo za TFF kilichokutana Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita kilimchagua Feisal, baada ya kuonesha kiwango kizuri kwa mwezi Septemba na kutoa mchango mkubwa kwa klabu ya Yanga ikiwa ni pamoja na kufunga mabao mawili.
 
Feisal aliwashinda Mosses Phiri wa Simba SC na Reliants Lusajo wa Namungo FC. Kwa upande wa Honour Janza aliwashinda Charles Mkwasa wa Ruvu Shooting na Thiery Hitimana wa KMC FC ambapo kwa mwezi huo Namungo iliifunga Ruvu Shooting bao 1-0, pia ikaifunga Coastal Union bao 1-0.
 
Pia Kamati ya Tuzo imemchagua Meneja wa uwanja wa Majaliwa, Lindi, Simon Mwambe kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Septemba kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.


KMC FC TAYARI KUWATOZA KODI MTIBWA SUGAR

$
0
0


Na Mwandishi Wetu

Kikosi cha KMC FC leo kimeanza  maandalizi kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa siku ya Jumamosi Oktoba 15 katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.

Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni inayonolewa na Kocha Mkuu Thierry Hitimana imeingia kambini jana jioni baada ya mapumziko ya siku mbili tangu ilipocheza mechi ya mzunguko wa sita dhidi ya Ruvu Shooting nakutoka sare ya kutokufungana.

KMC inajiandaa katika mchezo huo ikihitaji ushindi baada ya kutoa sare katika michezo miwili ambayo ni dhidi ya Namungo iliyocheza katika uwanja wa Majaliwa Ruangwa mkoani Lindi sambamba na dhidi ya Ruvu Shooting uliopigwa katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salam.

Katika mchezo huo , KMC FC inafanya mazoezi yanayolenga benchi la ufundi  kusahihisha makosa mbalimbali yaliyojitokeza  katika maeneo ambayo yalionekana kwenye mchezo huo uliopita na hivyo kupelekea Timu kukosa alama tatu muhimu.

"Tunajiandaa na mchezo ambao kimsingi utakuwa mgumu kutokana na kila Timu kuhitaji matokeo, tunawafahamu Mtibwa ni Timu nzuri na hata ukiangalia kwenye mchezo wao uliopita ambao wametoka sare walicheza vizuri na hivyo kama Timu tunajiandaa Ili kupata matokeo mazuri.

" Ukiangalia kwenye mchezo ambao tulitoka sare na Ruvu Shooting wachezaji walicheza vizuri lakini bahati mbaya hatukupata matokeo mazuri lakini tunaamini ubora wa wachezaji wetu, umakini walionao utaleta matokeo chanya  kwenye mchezo unaokuja kwasababu KMC tuna kikosi kizuri.

Hata hivyo hadi sasa KMC FC kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ipo kwenye nafasi ya tisa ikiwa na jumla ya alama saba huku ikiwa imeshacheza jumla ya michezo sita na kwamba kati ya hiyo imeshinda mchezo mmoja na kutoka sare michezo minne huko ikipoteza mmoja.

SMZ kutatua changamoto ya upatikanaji wa chakula

$
0
0

Serikali iko makini katika kupanga na kutekeleza mipango yake kwa kutilia maanani suala la ongezeko la idadi ya watu kwa kutatua changamoto ya upatikanaji na kujitosheleza kwa  chakula nchini.

Hayo yamesemwa na  Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. HUSSEIN ALI MWINYI katika hutuba  aliyoisoma kwa niaba yake na Makamo wa pili wa  Rais wa Zanzibar  Mhe. HEMED SULEIMAN ABDULLA katika ufunguzi wa Maonesho ya siku ya Chakula Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Chamanangwe mkoa wa kaskazini Pemba.

Amesema katika kutekeleza mipango hiyo serikali imeanzisha Taasisi za utafiti wa kilimo na mifugo pamoja na wakala wa Matrekta na zana nyengine za kilimo kwa lengo la kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo  na kubuni  njia bora za uzalishaji kulingana na mazingira pamoja na kurahisisha shughuli za kilimo kwa kutumia zana mbali mbali.

Dkt. Mwinyi amewataka wananchi na wakulima kuchukua tahadhari katika uzalishaji wa mazao ya chakula kwani taarifa za hali ya hewa zinaonesha kuwepo kwa upungufu wa mvua za vuli ambazo zinatarajiwa kunyesha kwa mtawanyiko usioridhisha.

Rais wa Zanzibar amesema kuwa mara nyingi nchi hupatwa  na hali kama hii hivyo amewataka wakulima kupanda mazao yanayoweza kuhimili hali ya hewa hiyo na kutumia mbegu za mazao yanayoweza kukomaa kama muhugo, viazi vitamu.mtama na jamii ya kunde.

Aidha Dkt. MWINYI amewaasa wafugaji kufuga mifugo ambayo wanaweza kuihudumia kwa malisho sambamba na kuhifadhi sehemu zote za malisho kwa maslahi ya wanyama hao.

 

Katika hatua nyengine Rais wa Zanzibar  amewataka wananchi na wadau wengine kuacha kuvamia maeneo ya kilimo na misitu pamoja na ujenzi wa kiholela kwa visingizio vya uwekezaji na badala yake kufuata utaratibu wa ujenzi wa makaazi kwa maslahi ya nchi.

" maeneo yote ya kilimo na mifugo pamoja na misitu  ni mali hivyo ni vyema kuyatunza na kuyatumia vyema kwa kuongeza tija na juhudi katika uzalishaji wa chakula ili kuweza kujikinga na balaa la njaa” amesema

Sambamba na hayo Rais Dkt. MWINYI amesema kuwa serikali kupitia wizara ya kilimo umwagiliaji maliasili na mifugo itahakikisha inasimamia vyema sekta ya kilimo ili kuongeza uzalishaji wa chakula pamoja na kuwa karibu na wakulima na wafugaji kwa kuwapa huduma, nyenzo na utaalamu ili kuhakikisha nchi inazalisha chakula kingi na chenye kutosheleza pamoja na kuiweka nchi katika hali ya kuwa na uhakika wa chakula.

Pia Dkt. Hussein amesisitiza umuhimu wa kuweka kipaombele katika ulaji wa chakula bora chenye lishe na kuwataka wananchi kujenga utamaduni wa kula vyakula bora, ikiwemo unywaji wa maziwa hususan watoto walio chini ya miaaka mitano (5) ili kupata watu wenye afya, akili na utaalamu unaohitajika.

Amesema serikali imekuwa ikichukua hatua mbali mbali za kuhakikisha upo ukakika wa upatikanaji chakula na lishe bora na kuunda mabaraza na kamati zenye kuhakikisha kuwa nchi inabakia salama na chakula cha kutosha.

Vile vile Rais Dkt. MWINYI amesema kwa sasa serikali inakamilisha ujenzi wa Maghala mawili (2) ya kuhifadhia chakula yenye uwezo wa kuhifadhi tani 2500 unguja na pemba.

Pia Rais MWINYIamesema kuwa serikali tayari imeshakabidhi mashine maalum za uchunguzi wa mazao na vyakula kwa taasisi ya utafiti wa kilimo (ZARI) na ZFDA ili kuhakikisha chakula kinahifadhiwa sehemu salama na wananchi wanakula chakula bora na chenye afya.

Nae  waziri wa kilimo, umwagiliaji maliasili na mifugo  mhe SHAMATA SHAAME KHAMIS amesema kuwa wizara imejipanga kuhakikisha inaongeza ufanisi mzuri katika upatikanaji wa chakula na lishe bora kwa wananchi wote.

Mhe SHAMATA amesema kuwa wizara kupitia maonesho haya itatoa elimu kwa wananchi wote kujifunza kulima kilimo cha kisasa na chenye tija kwa maslahi ya taifa.

Kwa upande wake katibu mkuu wa wizara ya kilimo,umwagiliaji maliasili na Mifugo Nd. SEIF SHAABAN MWINYI amesema maonesho haya yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa  kutokana na umoja na ushirikiano uliopo  baina ya serikali na mashirika binafsi wa muda mrefu.

Nd.SEIF amesema kuwa maonesho haya ni tofafauti sana na maonesho yaliyopita kwani wizara imepanga kuweka siku maalum ya kuimarisha afya ya kijiji kwa kuwepo unywaji wa maziwa kwa wananchi wote.

Amesema kuwa jumla ya shilingi milioni 170.9 zinatarajiwa kutumika katika maonesho haya ambazo zitatumika kuboresha huduma muhimu maeneo haya na zaidi ya washiriki mia moja (100) wameeshiriki katika maonesho haya wakiwemo taasisi za serikali na taasisi binafsi.

Wenye Umri wa Miaka 50-59 Wanogesha Riadha SHIMIWI

$
0
0

 

Mshindi wa kwanza katika mbio za mita 100 kwa Baraka Mashauri kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya Uchukuzi) akimaliza mbio hizo ambazo ni sehemu ya mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara za Serikali, Wakala na Mikoa (SHIMIWI) yaliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Tanga Oktoba10, 2022 yaliyofanyika jijini Tanga.


 

Na Mwandishi Wetu, Tanga

 

Mchezo wa riadha watu wazima wenye umri wa miaka 50-59 umekuwa kivutio katika Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara za Serikali, Wakala na Mikoa (SHIMIWI) inayoendelea jijini Tanga.

 

Usemi wa “Yake ni dhahabu” umejidhihirika katika viwanja vya Shule ya sekondari ya Ufundi Tanga kwenye mashindano ya SHIMIWI ambapo watu wazima wenye umri wa miaka 50-59 wamechuana vikali kuonesha makali yao katika mchezo wa riadha mbio za Mita. 100 wanaume na wanawake.

 

Katika mbio hizo kwa wanaume Juma Chikuku kutoka Wizara ya Kilimo ameshika nafasi ya kwanza na kuwaacha Sulemani Juma kutoka Hazina ambaye ameshika nafasi ya pili na nafasi ya tatu kwenda kwa Charles Kulila kutoka RAS Mara na kwa upande wa wanawake nafasi ya kwanza imeenda Melania Kapungu kutoka RAS Arusha, nafasi ya pili imeshikwa na Anitha Kihiyo kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na nafasi ya tatu imekwenda kwa Salome Makubi kutoka Wizara ya Maji.

 

Kwa upande wa awtumishi wengine mchezo huo pia umerindima kwa wanamichezo kuoneshana makali yao katika mbio mbalimbali ikiwemo Mita 100, 200, 400, 1500 pamoja na mbio za Mita 100 kupokezana vijiti michezo yote ikishirikisha wanaume na wanawake,

 

Mshindi wa kwanza katika Mita 100 wanawake ni Anitha Brown kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, nafasi ya pili imekwenda kwa Furaha Kaboneka kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi huku nafasi ya tatu imekwenda kwa Jamila Mkomwa wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya Uchukuzi) wakati kwa upande wa wanaume kwenye mbio hizo nafasi ya kwanza imekwenda kwa Baraka Mashauri kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya Uchukuzi), nafasi ya pili imekwenda kwa Martine Zulumo kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia huku nafasi ya tatu ikienda kwa William Valentino kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

 

Mbio nyingine zilizochezwa ni Mita 400 wanaume na wanawake, kwa upande wa wanawake nafasi imekwenda kwa Mastura Kaiza Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya Uchukuzi), nafasi ya pili imekwenda kwa Emerisiana Mtimbi kutoka RAS Pwani na nafasi ya tatu imekwenda kwa Mary John kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakati kwa upande wa wanaume katika mbio hizo nafasi ya kwanza imekwenda kwa Aidan Adrian kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya Uchukuzi), nafasi ya pili imekwenda kwa Innocent Mbizo kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) wakati nafasi ya tatu ikienda kwa Mussa Himapande kutoka Wizara ya Kilimo.

Mwanariadha Anitha Bown wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ameibuka kidedea katika mbio za mita 200 wanawake akishika nafasi ya kwanza, akifuatiwa na Naomi Dominic wa Wizara ya Maji na watatu ni Neema Manyama wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi); wakati kwa upande wa wanaume Martin Zalumo wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ametwaa media ya dhahabu, akifuatiwa na Baraka Mashauri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), na watatu ni Omar Mwenda wa RAS Shinyanga.

 

Katika mbio za mita 1,500 wanaume mwanariadha wa kimataifa Elibariki Buko wa Wizara ya Maliasili na Utalii ametwaa ubingwa akifuatiwa na Joseph Kachala wa Wizara ya Afya na watatu ni Eliud Kitwila waWizara ya Mifugo na Uvuvi; wakati kwa upande wa wanawake Nyamiza Ndibalema wa Wizara ya Madini ya ameibuka bingwa akifuatiwa na Scolastica Halisi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) na watatu ni Johaness Sarakikya wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

 

Wakati huo huo michuano ya riadha imehusisha pia mbio za Mita 100 kupokezana vijiti wanaume na wanawake ambapo ushindi wa kwanza kwa upande wa wanawake umekwenda kwa Wizara Maji, nafasi ya pili Wizara ya Afya na nafasi ya tatu imekwenda kwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya Uchukuzi) wakati kwa upande wa wanaume nafasi ya kwanza imeenda kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, nafasi ya pili Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya Uchukuzi) na nafasi ya tatu imekwenda kwa Wizara ya Afya.

 

Nao mabingwa watetezi kwenye mchezo wa kuvuta kamba wanaume timu ya Idara ya Mahakama wamevuliwa ubingwa kwa kuvutwa na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) kwa mivuto 2-1, katika mechi ya robo fainali iliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Ufundi ya Tanga.

 

Mchezo huo ulikuwa mkali na wakuvutia ambapo katika mivuto miwili ya kwanza timu hizo zilitoka sare kwa kuvutana mvuto 1-1, na ndipo ukaongezwa mvuto wa tatu na ndipo Sekta ya Uchukuzi wanaibuka washindi na kutinga hatua ya nusu fainali.

 

Timu nyingine zilizoshinda kwa mivuto 2-0 kwa wanaume ni Wizara ya Mambo ya Ndani wamewavuta Wizara ya Maliasili na Utalii; huku Wizara ya Mifugo na Uvuvi waliwachapa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia; na Ofisi ya Rais Ikulu waliwavuta Wizara ya Kilimo.

 

Kwa upande wa wanawake timu zilizoshinda kwa mivuto 2-0 na zote zimeingia hatua ya nusu fainali ni Idara ya Mahakama waliwavuta RAS Iringa; huku Ofisi ya Waziri Mkuu Sera wamewashinda Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI); nao Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) waliwaliza Wizara ya Madini; wakati Wizara ya Maji waliwavuta Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mvut

Benki ya NMB yatwaa tuzo tisa

$
0
0

 

Mkuu wa Idara ya Miamala ya Kibenki wa Benki ya NMB, Linda Teggisa (katikati), akipokea Tuzo za Uwezeshaji Wanawake ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Uendelevu wa EABL, Juanita Mramba (kulia) na Mkuu wa Sera za Umma wa EABL, Zach Munyi wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo hizo iliyofanyika Nairobi nchini Kenya mwishoni mwa wiki. NMB ilitwaa jumla ya tuzo tisa. (NA MPIGA PICHA WETU).

 

 

Benki ya NMB imenyakua tuzo tisa wakati wa Tuzo za Accenture 10th Gender Mainstreaming Awards zilizofanyika jijini Nairobi kutokana mchango wake wa uwezeshaji wa wanawake ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki.

 

Tuzo hizo huzawadiwa mashirika na watu binafsi ambao wako mstari wa mbele katika kuendeleza biashara za tofauti za kijinsia barani Afrika.

 

Tuzo hizo zilitambua Benki ya NMB na Afisa Mtendaji Mkuu wake Ruth Zaipuna kwa kuanzisha mabadiliko yanayochochea maendeleo na ushirikishwaji ndani ya kanda.

 

Wakati wa hafla ya utoaji tuzo, Benki ya NMB ilitangazwa kuwa Bingwa wa Utawala wa Jinsia Afrika Mashariki, Mshindi wa Afrika Mashariki; Uwezeshaji wa Wanawake katika Jumuiya na Mshindi wa kipengele cha Uwezeshaji wa Wanawake katika Jumuiya.

 

Benki hiyo pia iliibuka Mshindi wa Pili, Uwezeshaji Kiuchumi, Mshindi wa Tatu, Uwezeshaji Wanawake Mahali pa Kazi na Mshindi wa Tatu, Uwakilishi Sawa  na Ushiriki.

 

Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB Ruth Zaipuna aliibuka Kiongozi Jumuishi nchini Tanzania, Mshindi, Mfano wa kuigwa nchini Tanzania na Mshindi katika Sekta ya Huduma za Kifedha.

 

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hizo, Mkuu wa Miamala ya Kibenki, wa Banki ya NMB Linda Teggisa alisema tuzo hizo ni matokeo ya jitihada za pamoja za benki hiyo kuweka kipaumbele katika usawa wa kijisia kupitia mfumo wa  ‘NMB Balance.

“Katika Benki ya NMB, tunaamini kuwa usawa wa kijinsia unaweza kupatikana kwa kuchukua hatua. Ndiyo maana tunaendeleza dhamira yetu ya kuunda masuluhisho ya kifedha ambayo yanajumuisha na kushughulikia mahitaji ya makundi yote - ikiwa ni pamoja na wanawake katika jamii zetu," Alisema.

 

Aliongeza kuwa benki yake inakaribia kufikia uwiano wa kijinsia wa 50/50 na kuthibitisha dhamira ya benki yake ya kuendeleza usawa wa kijinsia mahali pa kazi.

 

Teggisa alisema benki mwaka huu benki ya NMB ilitoa hati fungani maarufu kama NMB Jasiri Bond ambayo inalenga biashara zinazoongozwa na wanawake kama sehemu ya dhamira yake ya kuongeza mikopo kwa wanawake.

UCHAGUZI WATINGA 16 BORA YA MICHUANO YA SHIMIWI TANGA

$
0
0

Timu ya Kamba ya wanaume ya Uchaguzi ikivutana na Bungeo jioni ya leo na kufuzu hatua ya 16 bora.
Kikosi cha Tume ya taifa ya Uchaguzi kilichopo jijini Tanga kewa michuano ya SHIMIWI 2022.
 
 
TIMU za Kamba za wanaume na wanawake za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) zimefuzu kucheza hatua ya 16 bora ya michuano ya Wizara na Taasisi za Serikali (SHIMIWI) inayoendelea jijini Tanga.

Uchaguzi wamejikatia tiketi hiyo bada ya kuchezo mechi mbili za mtoano kutafuta kufuzu hatua ya 16 bora kwa kucheza na Bunge na Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa zote za kundi E baada ya awali kufungana kwa pointi sita kila moja.
 
Wakishuka katika dimba la Mkwakwani jijini Tanga jioni ya leo Oktoba 8,2022, Uchaguzi iliwavuta Bunge kwa mara nyingine kwa mivuto miwili na kupata alama mbili kisha kucheza tena na timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na kutoka nao sare ya mvuto mmoja kwa mmoja.
Timu ya kamba ya Bunge wanaume 
 Katika Mchezo mwingine Bunge nao wamejikatia tiketi ya kucheza 16 bora baada ya kuwavuta Wizara ya mambo ya nje kwa mivuto miwili.
 
Matokeo ya jumla ya kundi E ni Uchaguzi alama 9, Bunge alama 8 na Wizara ya Mambo ya Nje alama 7 hivyo timu za Uchaguzi na Bunge wamefuzu kucheza hatua ya pili ya mashindano ya SHIMIWI 2022.
 
Kwa matokeo hayo sasa Uchaguzi wanaume inayoongoza kundi E itakutana na Wizara ya Elimu wakati Uchaguzi wanawake kutoka Kundi F itakutana na Wizara ya Katiba na Sheria.

PSSSF INAINGIZA KARIBU SHILINGI BILIONI 200 KWENYE UCHUMI WA NCHIKILA MWEZI KAMA MALIPO YA PENSHENI NA MAFAO KWA WANACHAMA WAKE

$
0
0

 

 NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, DAR ES SALAAM

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) unaingiza karibu bilioni 200 kila mwezi kwenye uchumi wa nchi kupitia malipo ya Mafao wanayolipa Wanachama wake, Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko huo, Bw. James Mlowe amesema.

Bw. Mlowe ameyasema hayo kwa nyakati tofauti kwenye ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari jijini Dar es Salaam iliyokamilika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akifafanua Bw. Mlowe amesema, PSSSF ina wastaafu 150 ambao hulipwa shilingi bilioni 60 kama malipo ya pensheni ya kila mwezi sambamba na kulipa zaidi ya shilingi bilioni 120 kila mwezi kama malipo ya Mafao mbalimbali kwa wanachama ambao bado hawajafikia umri wa kustaafu.

“Wastaafu na wanachama wetu wamesambaa kila kona ya nchi, wastaafu wengi pensheni yao siyo pesa ya kuwekeza ni ya matumizi ambayo inaenda kwa mama ntilie, na huduma mbalimbali za kijamii kwa hivyo inachachua uchumi, kwa hiyo bilioni 120 ukijumlisha na bilioni 60 ni bilioni 180 na wakati mwinhine hufikia shilingi bilioni 200 ambazo kila mwezi zinaenda kwenye uchumi wa nchi.” Alifafanua Bw. Mlowe.

HUDUMA ZA TEHAMA

Akizungumzia maboresho ya utoaji huduma kwa Wastaafu na Wanachama wa Mfuko huo Bw. Mlowe ambaye alifuatana na Afisa Uhusiano Mkuu Bw. Abdul Njaidi alisema, Mfuko umeimarisha mifumo yake ya TEHAMA ambapo Mwnachama na Mwajiri wanawasiliana na Mfuko kwa urahisi zaidi kwa njia ya kidijitali.

“Tuna huduma za PSSSF Kiganjani na huduma ya PSSSF Popote Ulipo Mtandaoni, lakini pia Wastaafu ambao wanatakiwa kujihakiki kila mwezi sasa wanajihakiki kupitia alama za vidole (Biometric).” Alifafanua.

MALIPO YA MALIMBIKIZO YA PENSHENI YA KILA MWEZI

Bw. Mlowe amemshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuuwezesha Mfuko kulipa Malimbikizo ya Pensheni ambapo ametoa cash bond ya shilingi trilioni 2.17 sawa na asilinmia 50% ya deni na tayari ameanza kuweka pesa hizo.

“Ni uamuzi wa kupongezwa ameufanya Mhe. Rais, kwani tayari tumelipa malimbikizo yanayofikia shilingi trilioni 1 na sasa tunaendelea na kulipa mafao mapya ya hivi sasa.” Alifafanua.

UWEKEZAJI.

Alisema Mfuko unawekeza kwa kufuata Sera ya Uwekezaji ya Mfuko, miongozo/kanuni za Benki Kuu ya Tanzania na Wizara yenye dhamana ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii.

“Tumewekeza kwenye Ardhi na Majengo, Dhamana za Serikali (Government Bonds), Amana za Mabenki, Hisa kwenye soko la Mitaji na Viwanda.”

Akifafanua kwanini Mfuko unawekeza, Bw. Mlowe alisema “Kulinda thamani ya michango ya wanachama, kuboresha mafao kwa wanachama na kuchangia juhudiza serikali kuinua uchumi wan chi.”

Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. James Mlowe (kulia) akiwa na Afisa Uhusiano Mkuu wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi akifafanua jambo wakati alipotembelea chumba cha habari cha magazeti ya Chama Uhuru barabara ya Lumumba jijini Dar es Salaam.











SIMBA WAIPANDISHIA SOKSI DE AGOSTO

$
0
0



Na Mwandishi Wetu


LICHA ya ushindi wa mabao 3-1 walioupata ugenini klabu ya Simba imeingia kambini leo kujiandaa na mchezo wa marejeano wa hatua ya awali kuwania kufuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).


Simba walirejea alfajiri ya jana kutoka nchini Angola wakiwa na ushindi huo unaowafanya waingie kwenye mchezo wa marejeano wakiwa na mtaji mkubwa wa mabao .


Baada ya kutua hapo jana timu ilipata siku moja ya mapumziko na kisha leo imerejea kwenye uwanja wa mazoezi kujiandaa na mtanange huo utakaopigwa Uwanaj wa Benjamin Mkapa Oktoba 16.

Kwa mujibu wa Menaja Habari wa Simba SC Ahmed Ally amesema kikosi kimeingia kambini tayari kujiandaa na mchezo huo ambao wanahitaji kupata matokeo chanya Ili kuweza kufuzu hatua ya makundi licha ya kupata matokeo chanya katika mchezo wa kwanza.


"Kikosi kimerejea uwanaja wa mazoezi asubui ya leo kwenye Uwanja wetu wa Mo Simba Arena tayari kwa maandalizi ya mchezo wetu wa mkondo wa pili Ili tuweze kukamilisha lengo la kwanza kutinga hatua ya makundi."


"Ni kweli tulipata matokeo kwenye mchezo wa kwanza lakini bado haiondoi kuwa mchezo huo utakuwa mgumu kwa sababu wapinzani wetu bado wanaihitaji mechi na hii ni mechi ya Ligi ya Mabingwa, tunafahamu mechi haijaisha ndio maana tunatia uzito na Nguvu kwa ajili ya kupata matokeo." Amesema Ahmed Ally.


Ahmed amesema timu Iko kwenye mikono salama ya Kocha Juma Mgunda hivyo mashabiki waendelee kuisapoti timu Ili kwa pamoja waweze kufikia malengo kama taaisisi.


CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE CHAWAKUTANISHA WANATAALUMA KATIKA KUMUENZI BABA WA TAIFA

$
0
0


 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Dk. Francis Michael, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Kitaaluma la kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius  Nyerere. Kongamano hilo liliandaliwa na Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na kufanyika jijini Dar es Salaam leo. (PICHA NA FRANCIS DANDE).
 
Mkuu wa Chuo cha kumbukumbu Mwalimu Nyerere, Prof Shedrack Mwakalila, akizungumza katika kongamano la kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere.


Baadhi ya washiriki.
Meza Kuu.

 

Na Mwandishi Wetu

Kuelekea maadhimisho ya kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere, Oktoba 14 mwaka huu Wizara ya Elimu imetoa mikakati ya kuboresha sera na mitaala ya Elimu nchini.

Akizungumza katika ufunguzi wa kongamano la kumuenzi Mwalimu Nyerere katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Francis Michael amesema Serikali inaenda kuboreha sera na mitaala ya Elimu ikiwa ni maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan.

"Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na mageuzi kwenye sekta ya Elimu, ukiangalia mageuzi ya Elimu ambayo Rais Samia Suluhu Hassan anayasimamia ni kwamba anaendelea kupita hatua zilezile ambazo Hayati Baba wa Taifa alipitia. Baba wa Taifa alisisitiza kuwa na Elimu ya kujitegemea mahususi kwa mtu yeyote anayemaliza ngazi yoyote ya Elimu awe na uwezo wa kujiajiri"

"Mheshimiwa Rais wetu anaelekeza tuweze kuifanya mabadiliko ya mitaala yetu ya Elimu Ili tuweze kupata hiyo hali ambayo tulikuwa tunaikosa, Elimu ambayo itamuwezeha mtu sio tu kujiriwa tu bali kujiajiri, kwa sababu tunapokuwa tunatoa Elimu ya mtu kuajiriwa tu tunakuwa tunatengeneza bomu kwamba unapotaka watu wote watoke waajiriwe na ajira ni chache na vyuo vinatoa wahitimu kila mwaka tunatengeneza bomu." Amesema na kuongeza kuwa.

"Kwaiyo watu wakitoka na kujiajiri, kuanzisha biashara ni kutengeneza ajira kwani sekta binafsi ndio injini ya maendeleo ya Taifa lolote. Lakini pia wanachangia uchumi wa nchi tofauti na mtu ambaye anakaa kusubiri ajira tu. Kuna kazi kubwa ya kufanya kutokana na kile ambacho Rais wetu anahitaji Wizara ya Elimu anataka tufanye  kubadilika katika mitaala na sera ya Elimu ya nchi hii na kile  ambacho alikuwa anakihubili Baba wa Taifa." amesema Dk. Michael

Naye Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu Mwalimu Nyerere, Prof Shedrack Mwakalila amesema Chuo hicho katika kumuenzi Mwalimu Nyerere wamefanya tafiti za namna gani ya kupambana na adui ujinga.

"Kwanza kabisa nipende kusema kwamba Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere huwa na kawaida ya kuwa na makongamano ya kuenzi waasisi wa Taifa letu ambao Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Karume hawa ndio waasisi wa Elimu na muungano tulionao.

"Kongamano hii ni kwa ajili ya kumuenzi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lakini pia huwa tuna kongamano la kumuenzi Mzee Karume." Ameongeza kuwa.

"Hawa waasisi walifanya makubwa sana lakini Moja wapo ya jambo ambalo tumeona mwaka huu tumeona tuweze kulifanya kongamano maalumu ni maadaui watutu wa maendeleo ambao ni Ujinga, Umasikini na Malazi, hawa maadaui bado hatujaweza kuyashidna kwa asilimia zote."


"Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere kama taaisi ya Elimu ya juu ni wajibu wetu kulisaidia Taifa kwa kutoa mafunzo ya kuendesha seminar, warsha na makongamano ambayo ni sehemu ya kupambana adui yetu ujinga. Lakini kongamano la mwaka huu kwa kutambua kuwa katika jamii kuna changamoto mbalimbali , hizi changamoto zinahitaji majibu na namna ya kuzitatua, Ili uweze kupata majibu sahihi na njia sahihi ya kukabiliana na hizo changamoto lazima ufanye tafiti." Pia amebainisha kuwa.

"Kumekuwa na janga la Covid, sasa hivi kuna Ebola lakini kuna mambo mengine yanayohusu mazingira kwahiyo sasa sisi kama taaisisi ya Elimu ya juu wanataaluma wanafanya tafiti mbalbali kama sehemu ya majukumu ya Chuo kuja na majibu ya changamoto ambazo zinaikabili jamii."

"Katika kongamano hili ambalo ni la siku mbili, tutakuwa na uwasilishwaji wa Mada mbalimbali ambazo zimefanyiwa utafiti na hizi Mada zinatoa majibu kwamba nini kifanyike katika jambo hili ajambo lile, kwaiyo kuna tafiti zaidi ya 30 na Mada zaidi ya 30 zinazotokana na watafiti wa Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere pamoja na watafiti kutoka katika taaisisi nyingine."

"Tunatengemea kuwa mwisho kongamano hili tutakuwa tukeshajua namna gani tumekuwa na mchango wa kupambana na ujinga na nini kiendelee kufanyika Ili kumuenzi Mwalimu Julius Nyerere kwa sababu yeye alipambana kuweka misingi mizuri na namna ya kuapmabana na hao maadui." amesema.


TEN/MET WAPINGA MILA ZINAZOMKANDAMIZA MTOTO WA KIKE

$
0
0


Mratibu wa TenMet  Taifa, Ochola Wayoga.


 Na Mwandishi Wetu


MTANDAO wa Elimu nchini Tanzania (TenMet) imelaani vikali mila potofu ambazo bado zinambagua mtoto wa kike katika kupata elimu, kama ilivyo kwa mtoto wa kiume. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mratibu wa TenMet  Taifa, Bw. Ochola Wayoga ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya mtoto wa kike ulimwenguni inayofanyika kila Oktoba 11.

Bw. Wayoga amesema ni jambo la kusikitisha kuona hadi leo bado kuna jamii nchini Tanzania ambazo zinaendekeza mila potofu zinazokandamiza haki ya mtoto wa kike kupata elimu, licha ya jitihada zinazofanywa na Serikali na wadau wengine katika kumlinda mtoto wa kike.

"... Tunatoa wito kwa jamii zote nchini Tanzania kuipa kipaumbele Elimu kwa mtoto wa kike kama nyenzo muhimu ya maendeleo yao, ukuaji, ushiriki wa kijamii kiuchumi na maendeleo. Tanzania imepiga hatua za kupongezwa katika kutunga sera na sheria zinazolinda haki za mtoto ikiwa ni pamoja na, Sheria ya Haki ya Mtoto ya mwaka 2009 na Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (NPAVAMWC 2017/18 -2021/22), ambayo inalenga kulinda na kudumisha ustawi wa mtoto na kushughulikia ukatili dhidi ya wanawake na watoto," alisema katika taarifa hiyo.

Hata hivyo, wameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kitendo cha kuridhia kurejea shuleni tena kwa wanafunzi wa kike waliopata ujauzito ambao huenda waliacha shule kutokana na ujauzito. Kurejeshwa tena kwa kundi hilo kumekuja hivi karibuni ikiwa ni jitihada za kushughulikia usawa wa kijinsia katika elimu kama inavyotamkwa kupitia (Waraka wa Elimu Na. 2, 2021).

Aliongeza kuwa licha ya maendeleo hayo yanayoonekana bado kuna changamoto katika viwango vya mpito vya wasichana kwenda kidato cha tano na sita sekondari hali inayosababisha tofauti kubwa ya kijinsia katika elimu ya sekondari na elimu ya juu nchini.

"...Takwimu zilizotolewa na Shirika la UNICEF -2020 zinaonesha kuwa asilimia 31 ya wasichana nchini Tanzania wanaolewa wakiwa na umri wa miaka 18, huku asilimia 5 kati yao wakiwa kabla ya umri wa miaka 15. Kimsingi hizi ni takwimu za kutisha ambazo zinathibitisha idadi kubwa ya wasichana ambao bado wameachwa nje ya mfumo wa shule kwa sababu ya ndoa za utotoni na umaskini na pia inatoa wito kwa hatua kali za kukabiliana na changamoto hizi miongoni mwa nyinginezo," alisema katika taarifa hiyo.

Wakati Tanzania inapoelekea kuadhimisha miaka 10 ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike, tuhakikishe dhamira yetu ya kutokomeza mila potofu kwa watoto kwa kuweka mazingira bora ya kupata elimu bora, usawa na kupatikana kwa urahisi. TEN/MET inaitaka serikali kuchukua hatua madhubuti katika nyanja mbili za kushughulikia changamoto nyingi zinazomkabili mtoto wa kike katika kupata haki yake ya kupata elimu nchini.

Marekebisho ya Sheria ya Elimu ya 1978 Kujumuisha kipengele cha sera ya kujiunga tena kwa wanafunzi wote wanaokatisha masomo kutokana na sababu tofauti ikiwemo mimba. Marekebisho haya yatazingatia ajenda ya kuingia tena nchini na uendelevu wake.

Wakati Tanzania inaelekea kuadhimisha miaka 10 ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike, TEN/MET inaiomba Serikali na wadau wengine kushirikiana kuhakikisha inaweka mikakati thabiti ya kutokomeza mila potofu kwa watoto kwa kuweka mazingira bora ya kupata elimu bora, usawa na kupatikana kwa urahisi.

"Serikali ichukue hatua madhubuti katika nyanja mbili za kushughulikia changamoto nyingi zinazomkabili mtoto wa kike katika kupata haki yake ya kupata elimu nchini. Pia tunapendekeza marekebisho ya Sheria ya Elimu ya 1978 Kujumuisha kipengele cha sera ya kujiunga tena kwa wanafunzi wote wanaokatisha masomo kutokana na sababu tofauti ikiwemo mimba.

Aidha alibainisha kuwa mazingira mazuri huwezesha mchakato mzuri wa ufundishaji na ujifunzaji hivyo basi kuboresha matokeo ya ujifunzaji, Hivyo ni wakati muafaka kwa serikali kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa kuwekeza katika miundombinu bora hasa katika ngazi ya shule za msingi.

SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI: TUONDOE VIKWAZO KUHAKIKISHA HAKI NA USTAWI WAKE

$
0
0



Kila ifikapo tarehe 11 ya mwezi Oktoba kila mwaka Dunia huadhimisha siku ya Mtoto wa Kike. Siku hii imewekwa makhususi ikilenga kuleta uelewa kwa jamii na watu wote duniani juu ya umuhimu na thamani ya kulindwa na kuhakikishiwa haki anazostahiki mtoto wa kike popote alipo duniani.

Haki na stahiki hizo ni pamoja na kupatiwa malezi bora, elimu, afya, hifadhi na uwezeshwaji katika kutimiza ndoto na malengo yake.

Siku hii pia ni kielelezo cha kujenga taswira mpya na kupigania mageuzi ya kisera, kisheria na kimkakati ili mtoto wa kike apate mafunzo, haki na stahiki nyinginezo kutoka kwa wazazi, jamii, serikali na wadau wengine. Ni siku inayotumbusha kuungana katika kutetea kupatikana haki na ustawi bora wa mtoto wa kike.

Ni kutokna na msingi huo, Umoja wa Mataifa uliona haja wa kuwepo na siku hii ili kuzitaka serikali za nchi zote duniani, wakiwemo watunga sera, wadau na wahusika wote kuhakikisha wanawekeza vya kutosha katika kupatikana, kulinda, kuhifadhi na kuendeleza haki za Mtoto wa Kike Duniani.

Hatua hiyo itaongeza uwezo na thamani ya mtoto wa kike popote alipo na kumuwezesha kumudu maisha yake na kuondokana na vikwazo mbalimbali katika kupata elimu, makuzi bora, afya stahiki na mahitaji yake muhimu na ya msingi katika makuzi na ustawi wake.

Kwa upande wetu Chama cha ACT  Wazalendo, tukiwa taasisi ya wananchi na umma kwa ujumla tunaungana na watu wote duniani katika maadhimisho ya siku hii muhimu ya Mtoto wa Kike Duniani.

Aidha, kama Chama tunaamini kuwa tuna haki na wajibu wote kuwa mstari wa mbele katika kupigania haki na stahiki zote za mtoto wa kike wa ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu. Ustawi wa mtoto wa kike ni kipaumbele chetu kama Chama cha watu, kinachosimamia na kupigania masuala ya watu.

Chama chetu kiko katika rekodi za kupigania na kutetea haki, maslahi na stahiki za mtoto wa kike.

Kiongozi wa Chama Ndg. Zitto Zuberi Kabwe ni mfano halisi wa mapambano ya haki za mtoto wa kike.

Tarehe 22 Januari, 2020 aliandika barua rasmi Benki ya Dunia  akiitaka taasisi hiyo kubwa ya kifedha duniani kutoifadhili Tanzania katika elimu kwani Serikali ililenga kuutumia ufadhili huo kuendelea ubaguzi wa watoto wa kike na kukiuka haki za watoto wa kike kupata elimu bila vikwazo.

Benki ya Dunia ilikubaliana na hoja za Kiongozi wa Chama na kusitisha ufadhili huo mpaka pale Serikali ilipobadilisha sera na msimamo ili kuondoa ubaguzi na vikwazo kwa watoto wote wa kike kupata elimu pasipo kujali hali zao. Huu ulikuwa ushindi mkubwa kwetu kama Chama na kama nchi katika kutetea na kulinda haki za mtoto wa kike. Mpaka sasa tunafurahi kuwa watoto wote wa kike nchini wanapata fursa na haki ya elimu katika mfumo rasmi pasipo kubaguliwa kwa namna yoyote.

ACT Wazalendo inaungana na kila nchi ambayo inaweka mikakati bora, sera nzuri na mipango thabiti yenye dhamira ya kukuza, kuendeleza na kustawisha haki ya mtoto wa kike duniani zikiwemo elimu, afya, kulindwa dhidi ya ndoa za utotoni na changamoto nyingine zinazowakabili watoto wetu.

Aidha, tunazitaka serikali mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania kuendelea kuchukua hatua imara ikiwemo kuzitathimini sera, mipango na taratibu zote za kusimimamia haki za mtoto wa kike ili kuhakikisha zinakuwa bora na zenye maana kwa maslahi ya mtoto wa kike wa Tanzania na kokote duniani.

Tunazitaka na kuzihimiza taasisi za serikali, Asasi za Kiraia, wadau na wanaharakati wengine kuendelea kupigania kuondoa vikwazo dhidi ya mtoto wa kike ili kuhakikisha uwepo wa mfumo bora wa maisha na ustwi wa maisha yake.


NAIBU WAZIRI MASANJA AWATAKA WAKUU WA WILAYA KUSIMAMIA IPASAVYO MAENEO YA HIFADHI*

$
0
0




Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amewataka Wakuu wa Wilaya nchini kusimamia vyema maeneo ya hifadhi ili kuepusha migogoro baina ya shughuli za kibinadamu na hifadhi.


Ameyasema hayo Oktoba 11, 2022 mkoani Rukwa wakati wa Ziara ya Mawaziri wa Kisekta ya kutatua migogoro ya Ardhi katika vijiji 975 nchini.


“Kila mtu akisimamia eneo lake vizuri hii migogoro itapungua sana ama kuisha lakini tukisubiri Serikali iseme au Kamati ya Mawaziri iseme, maeneo ya hifadhi yatakwisha” Mhe. Masanja amesisitiza.


Amefafanua kuwa changamoto kubwa inayoipata Serikali kwenye uhifadhi ni muingiliano wa shughuli za kibinadamu na utunzaji wa maeneo ya hifadhi ambapo wananchi wanaanzisha vijiji katikati ya hifadhi. 


Mhe. Masanja amewaelekeza Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Watendaji wa Vijiji kuhakiki wahamiaji wanaoingia katika maeneo yao ili kujua sababu inayowafanya waanzishe vijiji katika hifadhi na pia watoe maelekezo ya kutosha kwa wananchi kuhusu umuhimu wa uhifadhi na kuwasimamia ili kuondokana na migogoro ya ardhi.


“Ifike mahala wananchi wafahamu umuhimu wa uhifadhi na shughuli za kibinadamu” ameongeza.


Amesema endapo hifadhi zitaendelea kuvamiwa changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi zitaendelea kujitokeza.


Aidha, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa jinsi ambavyo ameelekeza migogoro hiyo itatuliwe ambapo kwa sasa hifadhi zinaheshimika na wananchi wanaendelea na maisha yao ya kila siku.


Ziara ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta itaendelea katika mkoa wa Katavi tarehe 12 Oktoba kabla ya kuelekea Kigoma Oktoba 13,2022.

TET, wachapa vitabu washiriki tamasha Dar

$
0
0


Na Mwandishi Wetu


TAMASHA la 31 la kimataifa la vitabu Tanzania limeanza leo Oktoba 11 hadi 15,2022 katika viwanja vya Posta Kijitonyama Jijini Dar es Salaam ambapo  Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) imeshiriki pamoja na wachapishaji mbalimbali wa vitabu nchini.


Katika ufunguzi wa tamasha hilo mgeni rasmi Profesa Evaristo  Liwa ambaye alimwakilisha Waziri wa  Elimu ,Sayansi na Teknolojia  ambaye amesema kuwa , maonesho haya ni muhimu kwani vitabu ni nyezo muhimu katika suala la ufudishaji na ujifunzaji na kusema kuwa serikali itaendelea kuhamasisha jitihada za usomaji nchini .


Prof.Liwa amesema usomaji wa vitabu unatoa ufahamu na uelewa wenye kutoa maarifa ambayo yanaishi  ambapo amesisitiza kuwa serikali itaendelea kutambua umuhimu wa  uchapishaji nchini .


‘’Usomaji wa vitabu ni jambo muhimu sana nchini hivyo tamasha hili ninaamini litasaidia katika kuendelea kuhamasisha usomaji wa vitabu kwa lengo la kupata maarifa " amesema Prof. Liwa.


Hata hivyo ameeleza kuwa kwa sasa Wizara iko kwenye mchakato wa maboresho ya Sera ya Elimu na Mitaala ambapo baada ya maboresho hayo itaaandaliwa uandishi wa vitabu ambayo  itafanyika kwa ushirikiano wa serikali na waandishi  binafsi ambavyo vitaweza kutumika katika shule nchini.


 Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TET ,Dkt.Aneth Komba amesema kuwa wataendelea kuungana na sekta binafsi katika kuhakikisha usomaji wa vitabu unakuwa kwa kiasi kikubwa nchini.


‘Tunasisitiza usomaji wa  vitabu vyote  kila mwanafunzi vya kiada na ziada kwani anapojisomea vitabu tunajenga  taifa lenye maarifa katika kujenga nchi yetu tunashirikiana na katika kuamsha ari mpya ya usomaji na tutaendelea kuhimiza ari ya usomaji wa vitabu, tusome vitabu vyote kwa ajili ya kupata maarifa’’ amesema Dkt.Komba


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha  wachapishaji nchini(PATA) Bwana Gabriel Kitua amesema kuwa ,tamasha hili litasaidia katika uhimizaji wa usomaji wa vitabu nchini na kwamba kwa kupitia vitabu masuala muhimu kama maadili yanapatikana na kufanya ufahamu mkubwa katika usomaji wa vitabu.


Tamasha hilo linawakutanisha wachapishaji mbalimbali na wananchi wa kawaida ambao watapata nafasi ya kusoma vitabu mbalimbali vinaoneshwa kwenye maonesho hayo.

SIMBA MZUKA UMEPANDA KWA WA ANGOLA

$
0
0


Na Mwandishi Wetu


Kuelekea mchezo wa mkondo wa pili hatua za awali kuwania kufuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF-CL) Uongozi wa Klabu ya Simba umeweka wazi mikakati ya mchezo huo.


Akizunggumza na vyombo vya Habari mchana wa lep, Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu hiyo Ahmed Ally amesema.



"Kikosi chetu kimerejea rasmi mazoezini baada ya juzi kurejea kutokea Angola. Kilianza mazoezi jana asubuhi kwenye uwanja wetu wa Mo Simba Arena na leo kitaingia kambini."


"Tulishinda lakini bado hatujafuzu, safari hii hatutaki kurudia makosa. Tumeweka nguvu kubwa kuona kwamba mchezo wa jumapili tunapata matokeo mazuri ili tuingie makundi. Tumemiss kushiriki hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika." Ameongeza kuwa.


"Tutaendelea kuwakosa Shomari Kapombe ambaye sasa anaendelea kufanya mazoezi akiwa hospitali, ataukosa mchezo wa jumapili lakini michezo itakayofata atakuwepo. Jimmyson Mwinuke pia tutamkosa, taarifa njema ni Peter Banda amerejea kikosini."


"Wageni wetu Primeiro de Agosto watawasili nchini Oktoba 14 majira ya mchana, kwa wale ambao wangependa kwenda kuwapokea wanakaribishwa uwanja wa ndege. Waamuzi wanatokea Afrika Kusini na watawasili nchini siku hiyo hiyo ya Oktoba 14."


"Upande wa hamasa tunaendelea kupita kwenye vyombo vya habari na kupita mitaani, siku ya ijumaa tutakuwa Temeke, tutazunguka na kispika twende tukaiunge mkono timu yetu. Tukio la kipekee tutakuwa na chakula cha pamoja, biryan la kwenda hatua ya makundi." amesema Ahmed Ally.


Hata hivyo hakuishia hapo amesema utaratibu wa mashabiki kuingia uko tayari na kuwataka kujitokeza kwa wingi.


 "Siku ya mchezo milango itafunguliwa mapema, kutakuwa na burudani kabla ya mchezo. Tutagawa bendera uwanja mzima kwa kila shabiki wa Simba jukumu lake ni kupeperusha. Lengo letu ni kutengeneza hali ya kuvutia uwanjani ili ionekane ni mechi ya Simba."


"Kwa wale ambao wana maflashflash ya kuwakawaka wanaruhusiwa kuja nayo. Muhimu liwe jekundu ili kuendana na rangi yetu." 


Kuhusu tiketi kwa mashabiki watakao hudhuria mtanange huo amesema.


"Tiketi zinaendelea kununuliwa lakini bado kasi ni ndogo, tunajua asili yetu Watanzania ni kununua siku za mwisho, tunategemea manunuzi yatakuwa makubwa kuanzia kesho. Siku ya mchezo tutauza pia tiketi uwanjani. Tunasisitiza watu kununua mapema."


"Kwa anayetaka kununua Platinum muda ni sasa mpaka naingia hapa zilikuwa zimebaki kama 20 hivyo inabidi kuwahi mapema kabla hazijaisha." Hakuishia hapo amebainisha kuwa.


"Tutaingia kwenye mchezo tukijua haujaisha, bado tunajua tunatakiwa kupambana kwa dakika zingine 90. Mechi haijaisha."


"Kocha Mgunda anafanya vizuri na kila mmoja anaona. Simba tuliyokuwa tunaitaka tunaiona kwake. Namna watu wanashambulia, wanavyokaba na mpira unavyotembea. Bodi ya Wakurugenzi itafanya maamuzi lakini ametupa tunachotaka na tunaamini atatupeleka makundi."


Pia ametoa neno kwa mashabiki wote wa Simba watakaojitokeza Uwanjani siku hiyo kuhamasisha wenzao.


"Kila shabiki wa Simba afanye kila anachoweza yeye binafsi kuja uwanjani na muhimu zaidi kuhamasisha wenzake kuja uwanjani. Lengo letu ni kuingia makundi tukiwa watu wasiopungua 60,000."- amesema Ahmed Ally.

ZECO yawaahidi Umeme wakazi wa Kiboje-Unguja

$
0
0



Wanawake wa eneo la Kinooni shehia ya Kiboje waliyohudhuria kusikiliza ahadi ya Naibu waziri wa Maji Nishati na Madini Shaaban Ali Othman.


 Naibu waziri WMNM Shaaban Ali Othman ( wapili kulia) akiwa na maafisa wa ZECO  wakisikiliza malalamiko ya umeme eneo la Kinooni, Shehia ya Kiboje, Unguja.


 

NA TALIB USSI

 

NAIBU Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Shabaan Ali Othman, amewaahidi  wakaazi wa eneo la Kinooni, Shehia ya Kiboje, Unguja kuwa ndani ya wiki moja Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) litafikisha umeme katika eneo hilo ili waondokane na  gharama za kupandisha maji kwa kutumia umeme wa jenereta.

Kauli hiyo ameitoa alipofanya ziara ya  kikazi katika jimbo la Uzini, Unguja  kufuatia malalamiko ya Mwakilishi wa jimbo hilo kwamba waakazi wa eneo hilo hawana huduma ya umeme  wala maji safi na salama.

Shabaani alisema atahakikisha kuanzi tarehe 13 hadi tarehe 19, mwezi huu umeme utafikishwa katika maeneo hayo ili waakaazi wa eneo hilo waandokane na gharama za kutia mafuta kwenye jenereta kwa ajili ya kupandisha maji kutoka kwenye kisima hadi  tangi la maji la juu.

Alisema wizara yake kupitia ZECO inatoa nguzo za umeme bure ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi hivyo atahakikisha Shirika hilo linafikisha umeme haraka eneo hilo.

Aidha aliwaomba wakaanzi wa maeneo mengine ya shehia hiyo kuwa na subra wakati wataalamu wa ZECO wakifanya upembuzi yakinifu, kwani muda sio mrefu huduma ya umeme itafikishwa maeneo yote ya jimbo la Uzini.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo alitembea maeneo mengine ya jimbo hilo la Uzini ikiwemo Kwambani na Kidimni ambapo waakazi wengi wamekabiliwa na changamoto ya maji safi ya salama, wengine wakiyapata kwa mgao huku wengine wakiyakosa kabisa.

Alieleza kwamba wizara yake inatekeleza miradi ya maji kwaajili ya kuwaondolea shida wananchi sio muda mrefu miradi hiyo itakamilika kwani kuna visima vingi vimechimbwa katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba.

Mapema Mkaazi wa Kinooni bi Mastura Mgeni Hamadi alisema wanawake wa eneo hilo wamekuwa wakichangishana shilingi 3,000 kwa ajili ya kutia mafua ya dizeli kwenye jenereta ili wapandishie maji kwenye tangi kutoka katika kisima chake alichokichimba.

“Naiomba Serikali iwafikiria wanawake hii shida ya maji kwani wamekuwa wakiteseka sana, hali duni ya maisha wakati mwengini mtu anakua anakosa pesa elfu tatu,” alisema Mastura.

Kwa upande wake Mwakilishi wa jimbo la Uzini, Haji Shabaani Waziri, alimshukuru  Naibu Waziri kwa kufanya ziara katika jimbo hilo kusikiliza kero za wananchi ambao kwa muda mrefu wamekua wakilalamikia ukosefu wa upatikanaji wa huduma za maji na umeme.


John Lisu, Sinach kutikisa jukwaa la Festival of Praise

$
0
0

John Lisu.

MWIMBAJI mahiri wa nyimbo za Injili nchini Nigeria, Sinach Joseph Egbu anatarajia kuongoza jukwaa la Festival of Praise linalotarajia kufanyika keshokutwa Oktoba 16 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam pamoja na mwimbaji nguli hapa nchini John Lisu.

Akizungumza  jijini Dar es Salaam muandaaji wa tamasha hilo, John Lisu alisema umahiri wa Sinach utafanikisha ujumbe wa neno la Mungu kuwafikia watanzania wote kupitia tungo zake na waimbaji wengine wa hapa nchini.

Lisu alisema Sinach atapanda jukwaani na wimbo wake uliokamata anga la muziki wa Injili duniani wa ‘Way Maker’ uliotazamwa na mashabiki zaidi ya milioni 200.

Lisu alisema waimbaji wa hapa nchini watakaomsindikiza mwimbaji huyo ni pamoja na yeye mwenyewe, Christina Shusho, Ambwene Mwasongwe, Pasta EPA, Kwaya ya Kanisa la Moravian, Ruach Worship Team (Kenya) na Kwaya ya Gospel Winners.

Aidha Lisu alitoa wito kwa waamini wa muziki wa Injili kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo ambalo ni mojawapo ya matukio muhimu ya kusifu na kuabudu yanayofanyika hapa nchini.

Viingilio katika tamasha hilo ni Sh 30,000 kawaida, VIP Sh. 100,000, VVIP Sh 200,000 na watoto watatoa Sh 10,000 ambako aliwaomba waamini wa makanisa mbalimbali hapa nchini kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo.

Sinach

MAHAKAMA KUU YAWAHOJI WABUNGE WALIOVULIWA UANACHAMA CHADEMA

$
0
0


Wabunge wa Viti Maalum, Hawa Mwaifunga (kushoto), Naghenjwa Kaboyoka (katikati) na Cecilia Pareso waliovuliwa uanachama na Chadema, wakijadiliana jambo ndani ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo Oktoba 13, 2022. (PICHA NA FRANCIS DANDE).
Mbunge wa viti maalum aliyevuliwa uanachama Chadema, Grace Tendega (kulia), akizungumza na mawakili wake katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo Oktoba 13, 2022.

 

Grace Tendega akitoka mahakamani leo.

TANZANIA YAMALIZA MUDA WAKE WA KUONGOZA VIKAO VYA IMF KWA MAFANIKIO MAKUBWA

$
0
0


Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati), akiongoza kikao cha Kundi la Kwanza la Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency) katika Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), linalojumuisha Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi 23 za Afrika, kilichofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo, wakati wa mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kmataifa (IMF), inayoendelea Jijini Washington D.C, nchini Marekani.

 

 

Na Benny Mwaipaja, Washington DC
 

TANZANIA imemaliza muda wake wa miaka miwili wa kuwa Mwenyekiti wa Kundi la Kwanza la Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency) katika Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), linalojumuisha Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi 23 za Afrika, ambapo katika muhula wake, mafanikio makubwa yamepatikana, licha ya kukabiliwa na changamoto za UVIKO-19 na vita inayoendelea baina ya Urusi na Ukraine.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amesema hayo Jijini Washington D.C, nchini Marekani, baada ya kuongoza mkutano wake wa mwisho Mawaziri  na Mgavana wa Kundi hilo na kukabidhi rasmi uongozi wa miaka mingine miwili kwa Namibia kama Mwenyekiti na nchi ya Botswana kama Makamu Mwenyekiti.

Katika kipindi cha uongozi wa Tanzania, Kundi hilo limenufaika kwa ongezeko la upatikanaji wa rasilimali fedha kwa nchi wanachama wake na kuwa na sauti zaidi katika shughuli za uendeshaji za Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).  

Nafasi ya Tanzania katika kundi hilo iliwezesha kuimarisha mashirikiano kati yake na IMF ambapo imeshudiwa Shirika hilo likiongeza uwekezaji wake nchini kwa takriban shilingi trilioni 1.3. zilizotolewa kama mkopo usio na riba kwa ajili ya kukabiliana na athari za UVIKO-19 katika sekta za elimu, afya, maji na utalii hivi karibuni.

Aidha, katika kipindi hicho, IMF iliidhinishia Tanzania mkopo nafuu wenye thamani ya jumla ya shilingi trilioni 2.7 za kukabiliana na athari za UVIKO-19 na vita ya Ukraine ambapo tayari kiasi cha shilingi bilioni 347 zimeshatolewa ili kuleta ahueni kwa wanachi kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. 

Alisema kuwa ajenda kubwa ya mkutano huo ambao aliuongoza kwa mara ya mwisho, ilijikita katika kutafuta namna IMF inavyoweza kuzisaidia nchi wanachama kukabiliana na uhaba wa chakula  na mfumuko wa bei uliosababishwa na athari za UVIKO-19, vita vya Urusi na Ukraine na mabadiliko ya tabia nchi.

Dkt. Nchemba alilita Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kuendelea kushirikiana na uongozi mpya wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu kutoka Kundi la Kwanza la nchi za Afrka, kwa kutoa mikopo na misaada itakayosaidia kufufua uchumi na kukabiliana na uhaba wa chakula katika nchi hizo.

Aidha, Dkt. Nchemba, alitoa wito kwa nchi wanachama wa Kundi hilo kuwa na sauti moja ya kupigania maslahi ya nchi zao katika Shirika hilo kubwa la Fedha la Kimataifa na kuhakikisha wanatunga sera rafiki zitakazoimarisha sekta za uzalishaji, hususan kwenye kilimo. 


UJUMBE WA KAMATI YA KUDUMU YA SHERIA NDOGO BARAZALA WAWAKILISHI WATEMBELEA WCF KUJIFUNZA

$
0
0

 NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

UJUMBE wa Kamati ya Kudumu ya Sheria Ndogo ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, ukiongozwa na mwenyekiti wake, Mhe. Mihayo Juma Nunga umetembelea ofisi za Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) jijini Dar es Salaam kwa nia ya kubainisha masuala muhimu ya Fidia.

Akizungumza baada ya kukutana na Watendaji wa WCF wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Dkt. John Mduma, Mwenyekiti huyo amesema ziara hiyo imewawezesha kupata uelewa mpana wa namna Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi inavyotekelezwa na faida ambayo Watanzania wamepata kutokana na uwepo wa chombo hicho.

“Kwetu jambo hili ni geni bado halijatengenezewa utaratibu bora zaidi wa kuwalipa fidia wafanyakazi waliopata changamoto kwenye maeneo ya kazi, Zanzibar tuko katika maandalizi ya kutengeneza utaratibu wa jinsi gani Mfanyakazi atapata fidia pindi anapoumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi, kwahivyo tukaona tutembelee Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ambao wana uzoefu mkubwa katika masuala haya nasi tuweze kuishauri serikali ili tuwe na chombo walau chenye uwiano na WCF.” Alifafanua Mhe. Nunga.

Alisema wameona jinsi watu wengi walivyonufaika na uwepo wa WCF kwa hivyo ni wakati muafaka kwa Zanzibar kuwa na Mfuko utakaotoa huduma bora kama ambavyo wameshuhudia hapo WCF.

Naye Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), Bw.Ali Nassor Shaaban, alisema Mfuko huo uko katika maandalizi ya kuanzisha huduma kama hiyo ya kufidia wafanyakazi wanaoumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi.

“Tumeona kabla ya kuanzisha chombo hicho ni vema kujifunza kwa wenzetu WCF ambao kwa kweli wamefanikiwa sana ili kujua sheria na kanuni zake zilivyo hatimaye tuwe katika nafasi nzuri ya kuanzisha chombo chetu kitakachotoa huduma kulingana na mazingira ya Zanzibar.” Alifafanua.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dtk. John Mduma ameema , WCF ina uzoefu wa miaka saba (7) katika masuala ya utoaji fidia kwa wafanyakazi na imekuwa ni wakati mzuri wa kubadilishana mawazo ya namna bora ya kuendesha vyombo hivi vya Fidia kwa Wafanyakazi.

“Tumewaeleza namna tunavyotenda katika miaka hii saba (7) na mafanikio tuliyopata, tumejifunza mambo mengi ambayo wamekuwa wakituuliza na tunaamini wamejifunza mengi.” Alifafanua.

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Sheria Ndogo ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Mihayo Juma Nunga (kushoto), akibadilishana mawazo na Mkurtugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dtk. John Mduma (kulia) na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Bw. Ali Nassor Shaaban wakati wa ziara ya Kamati hiyo na watendaji wa ZSSF kwenye Ofisi za Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ili kujifunza jinsi unavyoendesha shughuli zake hususan ulipaji fidia kwa wafanyakzi.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dtk. John Mduma (kushoto), akizungmza mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Sheria Ndogo ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Mihayo Juma Nunga wakati wa ziara ya ujumbe wa kamati hiyo na watendaji wa ZSSF kwenye ofisi za WCF jijini Dar es Salaam Oktoba 12, 2022
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), Bw.Ali Nassor Shaaban, akifurahia jambo wakati wa mazungumzo na watendaji wa WCF.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati wakifuatilia elimu iliyokuwa ikitolewa na wataalamu wa WCF kuhusu masuala ya fidia kwa wafanyakazi
Baadhi ya wajumbe wa Kamati wakifuatilia elimu iliyokuwa ikitolewa na wataalamu wa WCF kuhusu masuala ya fidia kwa wafanyakazi
Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar, akifafanua kuhusu namna Mfuko unavyofanya tathmini ya madhara aliyopata Mfanyakazi kutokana na ulemavu uliosababishwa na ajali iliyotokana na kazi.
Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter akifafanua kuhusu majukumu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
Mkuu wa Huduma za Sheria WCF, Bw. Abraham Siyovelwa, akizungumzia Sheria iliyoanzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
Japhet akizungumzia masuala mbaimbali yanayohusu utendaji wa Mfuko
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Sheria Ndogo ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Mihayo Juma Nunga (wakwanza kushoto) na ujumbe wake wakisikiliza kwa makini.














Pwani 'Kuchere' kujenga vituo 36 kuwasaidia watoto kupata elimu ya awali

$
0
0
 
Afisa Elimu wa Mkoa wa Pwani, Sara Mlaki, akizungumza na washiriki wa warsha hiyo hawapo pichani iliyofanyika Wilayani Kibaha.
 
 
Na Victor Masangu, Pwani


Serikali mkoani Pwani katika kuunga juhudi za Rais wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan kuboresha sekta ya elimu kuanzia ngazi za chini imejenga vituo vya utayari vipatavyo 36 katika halmashauri zote lengo ikiwa ni kuwapatia elimu watoto waliosahaulika kupata fursa ya elimu ngazi ya awali.


Hayo yamebainishwa na Afisa elimu wa Mkoa wa Pwani wakati wa kufungua warsha ya mpango maalumu kwa ajili ya kuwandaa watoto hao waweze kuandaliwa vizuri katika  elimu ya awali kabla awajajiunga na darasa la kwanza.

Aidha afisa elimu huyo alibainisha kwamba nia yao kubwa katika mpango huo wa utayari ni kuwajengea uwezo na mahalifa ya katika suala zima la kuweza kujua kusoma,Kuhesabu na kuandika kabla ya kuingia darasa la kwanza.


Pia aliongeza kuwa wameamua kuwakutanisha wadau mbali mbali wa elimu wakiwemo madiwani,watendaji kata,waratibu elimu,wakuu wa shule ili tuweze kuweka mpango wa kuboresha sekta ya elimu kwa watoto hao ambao walishindwa kupata fursa ya kupata elimu ya awali.


"Lengo letu ni kuanzisha vituo vya utayari katika halmashauri zetu tisa kwa ajili ya watoto wetu wa kuanzia miaka 5 hadi 9  ili waweze kupata elimu ya awali kabla ya kuanza kujiunga na darasa la kwanza na halmashauri zetu zinatupa ushirikiano katika kufanikisha Jambo hili"alibainisha Sara.

 Kadhalika alisema kuwa mpango huo ambao umeanzishwa na serikali utawasaidia watoto ambao wamekosa fursa ya kupata elimu kuweza kujifunza zaidi katika kusoma,kuhesabu na kuandika.

 
Kwa upande wake afisa elimu ya watu wazima katika halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Hamisi Chikaula amebainisha mpango huo wa utayari wa kuanzia vituo utaweza kuwa mkombozi mkubwa wa kuwasaidia watoto kupata elimu iliyo bora kuanzia ngazi za chini.


Chikaula ambaye pia alikuwa ni mmoja wa wawezeshaji katika Warsha hiyo aliongeza kuwa katika mpango huo kila halmashauri inajenga vituo vinne ambavyo vitakuwa ni mkombozi mkubwa kwa watoto kupata elimu ya awali.


Kwa upande wake diwani wa kata ya mkuza Focus Bundala ambaye ameshiriki katika Warsha hiyo ameahidi kuyafanyia kazi mafunzo yote ambayo wameyapata katika suala zima la kuwahimiza wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao katika vituo hivyo.

Diwani wa kata ya Visiga Kambi Legeza aliipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuanzisha mpango huo wa kujenga vituo ambavyo vitatumika katika kuwasaidia watoto ambao walikosa nafasi katika elimu ya awali.
 
Caption- 1 Afisa elimu wa Mkoa wa Pwani Sara Mlaki akizungumza na washiriki wa warsha hiyo hawapo pichani iliyofanyika Wilayani Kibaha.

Caption-2 Baadhi ya washiriki waliohudhulia katika warsha hiyo.
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>