Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

NMB yaihakikishia JWTZ udhamini zaidi CDF Trophy

$
0
0

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania , Jenerali Jacob Mkunda akimkabidhi Kikombe mshindi kutoka timu ya NMB, Bw. Abdallah Gunda kwenye mashindano ya NMB CDF TROPHY 2022, yaliyofanyika katika viwanja vya Golf Lugalo, Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Mkuu wa Biashara na wateja Binafsi, Bw. Filbert Mponzi na kushoto ni Mkuu wa Majeshi wa Malawi, Generali Vincent Nundwe.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob Mkunda akimkabidhi Kikombe mshindi kutoka timu ya NMB, Bw. Sigfrid Ophishas kwenye mashindano ya NMB CDF TROPHY 2022, yaliyofanyika katika viwanja vya Golf Lugalo, Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Mkuu wa Biashara na Wateja Binafsi, Filbert Mponzi na kushoto ni Mkuu wa Majeshi wa Malawi, Generali Vincent Nundwe.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob Mkunda akimkabidhi Kikombe na zawadi mshindi wa Jumla wa mashindano ya NMB CDF TROPHY 2022, Cpl ,Malius Kajuna, yaliyofanyika katika viwanja vya Golf Lugalo, Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Mkuu wa Biashara na Wateja Binafsi, Bw. Filbert Mponzi na kushoto ni Mkuu wa Majeshi wa Malawi, Generali Vincent Nundwe.

Picha ya pamoja.


NA MWANDISHI WETU

 

BENKI ya NMB imemhakikishia Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob Nkunda, udhamini endelevu wa Mashindano ya Gofu ya Mkuu wa Majeshi (NMB CDF Trophy), ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya kuzaliwa kwa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

 

Ahadi hiyo imetolewa na Afisa Mkuu wa Biashara na Wateja Binafsi wa NMB, Filbert Mponzi, wakati wa hafla ya utoaji zawadi kwa washindi wa NMB CDF Trophy 2022, iliyofanyika katikaVviwanja vya Gofu Lugalo jijini Dar es Salaam, ambako kwa siku mbili wakali wa mchezo huo wapatao 243 walichuana.

 

Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Mkuu wa Majeshi Mstaafu Tanzania Jenerali George Waitara na Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu Lugalo, Brigedia Jenerali Michael Luwongo (Mstaafu), pamoja na Mkuu wa Majeshi wa Malawi, Jenerali Vicent Nundwe, aliyeambatana na nyota wa timu za Jeshi la Malawi.

 

Awali akiwasilisha salamu za Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna na Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Edwin Mhede, Mponzi alimpongeza Jenerali Nkunda kwa kuaminiwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kuteuliwa, na kuahidi kumuunga mkono ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

 

“Kwa kutambua umuhimu wa mchezo wa gofu, lakini pia mahusiano ya NMB na JWTZ, tumeona umuhimu wa kuendelea kudhamini mashindano haya ya Mkuu wa Majeshi na tumefanya hivyo kwa miaka sita sasa. Mwaka huu katika CDF Trophy, NMB imetoa shilingi milioni. 60 za kugharamia zawadi na vifaa mbalimbali. 

 

“Nikuahidi CDF Nkunda, NMB tukiwa benki ya kizalendo, benki ambayo Serikali ina hisa za kutosha na ukweli kuwa sisi ni wadau wakubwa wa Serikali na kwa kutambua umuhimu wa JWTZ, tutaendelea kudhamini CDF Trophy kwa miaka mingi ijayo.

 

Aliongeza “Kwa hiyo, mnapaswa kutambua kwamba mtakuwa na sisi kwa miaka mingi ijayo katika mashindano haya, ambayo tumeyasapoti majeshi yetu katika mashindano mengi inayoshirikisha timu za majeshi yetu kitaifa na kimataifa,” alisisitiza Mponzi.

 

Aidha, Mponzi pia aliahidi kugharamia ununuaji wa viatu na jezi kwa ajili ya watoto walioshiriki mashindano hayo, baada ya kupokea ombi kutoka kwa kocha wa vijana hao.

 

“Jioni wakati tunakabidhi zawadi za watoto (juniors),kocha alilalamika vijana wake kukosa viatu, nasi NMB tukalichukua hilo, baada ya kuambiwa Sh. Milioni 5 zinatosha kuwezesha vijana wale kupata viatu na jezi ili kuwachagiza kushiriki kwa ufanisi mchezo huu na kupata mafanikio,” alisema.

 

Mponzi alitumia nafasi hiyo kumueleza Generali Nkunda kuwa NMB inayo Matawi Maalum kadhaa nchini kwa ajili ya maofisa ‘private banking’ na kwamba kwa Dar es Salaam, wana matawi ya Oyster Plaza na Makao Makuu, hivyo kuwakaribisha majenerali wa jeshi na maofisa wengine kufika kuhudumiwa.

 

Kwa upande wake, Jenerali Nkunda alianza kwa kuipongeza na kuishukuru NMB kwa kudhamini uliofanikisha mashindano hayo kwa kiwango cha kimataifa,  huku akisisitiza kuwa matumaini yake ni benki hiyo kuendelea kuisapoti JWTZ na kuiunga mkono Serikali.

 

“Nimefurahishwa na udhamini wa NMB kwa mwaka wa sita mfululizo sasa, hii inaonesha na kuthibitisha ni kwa namna gani NMB ilivyo karibu na JWTZ, lakini pia inatumia fursa hiyo kurudisha fadhila kwa jamii.

 

“Nitoe wito kwa taasisi za Serikali na mashirika mengine kuiga mfano wa NMB na wadhamini wengine katika kushirikiana na jeshi kwa kudhamini mashindano haya na pia kusaidia ushiriki wa timu za majeshi katika Mashindano ya Majeshi ndani nan je ya nchi,” alisisitiza. 

 

Generali Nkunda aliongeza kuwa NMB CDF Trophy ni shindano lenye historia ndefu na umuhimu wa kipekee katika historia ya JWTZ, na kufichua kuwa baada ya uteuzi wake, alikabidhiwa ulezi wa timu na mtangulizi wake Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Venance Mabeyo, huku akiahidi kuyaboresha ili kuyaongezea mvuto.

 

“CDF Trophy ni shindano la kuadhimisha kuzaliwa kwa JWTZ, ambayo huwa ni Septemba 1 kila mwaka, lakini mwaka huu kutokana na sababu mbalimbali likasogezwa mbele. Tunamshukuru Mwanzilishi Jenerali Waitara na walioliendeleza, kwani JWTZ ni kisima cha kuendeleza michezo,” alibainisha.

 

Jenerali Nkunda alimpongeza CDF wa Malawi, Vicent Nundwe kwa kuacha majukumu yake na kuja kushiriki CDF Trophy 2022 yeye na timu za maofisa wa Jeshi la Malawi, ushiriki ambao umeliongezea shindano hilo hadhi kimataifa.

 

Katika mashindano hayo yaliyoanza Oktoba 1, Koplo Marius Kajuna aliibuka mshindi wa jumla wa CDF Trophy, yaliyohusisha kategori za ‘Combat Competition,’ ‘Professional,’ ‘Main Event CDF Trophy,’ ‘Juniors’ na ‘Sponsors Competition,’ ambako Abdallah Gunda wa NMB aliwagaragaza wadhamini wengine.


BAADA YA FISTULA, WAZIRI MKUU AITAKA NMB KUGEUKIA MAGONJWA MENGINE

$
0
0

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna (kulia) wakimkabidhi Afisa Mtendaji Mkuu wa hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Mil. 600 wakati wa mbio za hisani za NMB Marathon 2022 ‘Mwendo wa Upendo’ kwa ajili ya kusaidia matibabu ya akinamama wenye Fistula wanaotibiwa katika hospitali ya CCBRT. Mbio ziliandaliwa na Benki ya NMB zilianzia na kuishia kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya NMB, Dk. Edwin Mhede. (NA MPIGA PICHA WETU).


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (katikati) akiongoza mbio hisani za NMB Marathon 2022 ‘Mwendo wa Upendo’ zilizoanzia na kuishia kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es Salaam. Mbio hizo zilizoandaliwa na Benki ya NMB, zililenga kukusanya kiasi cha Sh. Mil. 600 za kusaidia matibabu ya akinamama wenye Fistula wanaotibiwa katika hospitali ya CCBRT. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya NMB, Dk. Edwin Mhede. 

Mwenyekiti wa Bodi ya NMB, Dk. Edwin Mhede (kulia), akimvisha medali Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa mbio za hisani za NMB Marathon 2022 ‘Mwendo wa Upendo’ zilizoanzia na kuishia kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Mbio hizo ziliandaliwa na Benki ya NMB kwa ajili ya kusaidia matibabu ya akinamama wenye Fistula wanaotibiwa katika hospitali ya CCBRT. Katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna.

 

 Na Mwandishi Wetu


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, ameiomba Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya NMB chini ya Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Edwin Mhede na Menejimenti ya benki hiyo chini ya Afisa Mtendaji Mkuu Ruth Zaipuna, kuendeleza Mbio za Hisani za NMB Marathon licha ya kuvuka lengo la kukusanya Sh. Bil. 1 katika kipindi cha miaka miwili.

NMB Marathon zilianzishwa mwaka jana 2021, lengo likiwa kukusanya Sh. Bil. 1 katika kipindi cha miaka minne (sawa na Sh. Mil. 250 kila mwaka), lakini mwitikio chanya ukawezesha kukusanya Sh. Mil. 400 mwaka jana na kisha Mil. 600 mwaka huu na kufikia lengo ndani ya miaka miwili.

Akizungumza wakati wa kutoa shukrani kwa waandaaji, wadhamini na washiriki, mwishoni mwa mbio hizo katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam Jumamosi Oktoba Mosi, Waziri Mkuu Majaliwa alisema baada ya kuvuka lengo hilo, ni wakati sahihi sasa makusanyo yatokanayo na mbio yakaelekezwa kwingine.

“Niipongeze Bodi ya Wakurugenzi NMB chini ya Mwenyekiti, Dk. Edwin Mhede na Menejimenti ya benki hii chini ya Afisa Mtendaji Mkuu, Ruth Zaipuna kwa uratibu wa jambo hili zuri.

“Wito wangu kwa NMB, malengo yalikuwa kukusanya fedha za fistula kiasi cha Sh. Bil. 1 katika kipindi cha miaka minne, bahati nzuri tumefikia lengo ndani ya miaka miwili, niwasihi endeleeni kutafuta maeneo mengine ya kusaidia kama vile magonjwa ya saratani.

“Mwakani mbio hizi ziwepo na miaka ijayo ziwepo pia, makusanyo yakasaidie changamoto zingine. Pia kuwe na mbio endelevu, kwa ajili ya sio tu kukusanya fedha za kusaidia matibabu, bali pia liwe jukwaa la mazoezi ambayo ni mhimili wa afya  ya kila Mtanzania katika ujezni wa taifa,” alibainisha.

Waziri Mkuu Majaliwa, alikiri kuvutiwa na ubunifu wa NMB uliozaa Mbio za Hisani za NMB Marathon, huku akizipongeza Kampuni za Bima za Sanlam na UAP, kwa udhamini mnono uliowezesha kuvuka lengo la makusanyo ya kusaidia matibabu ya kinamama wenye Fistula nchini.

“Shukrani pia kwa wadhamini walioamua kuiunga mkono NMB wakiongozwa na Kampuni ya Sanlam na UAP, ambao wameota kiasi kikubwa zaidi, Sanlam Sh. Mil. 150 na UAP Sh. Mil. 100. Kwa kweli Sanlam, UAP na wadhamini wengineo tunawashukuru, kama tunavyowashuku wakimbiaji wote.

“Niwasihi wakimbiaji, wadhamini, waandaaji NMB na CCBRT, tuendeleze ‘Mwendo wa Upendo,’ tusichoke kuchangia, kwani wahenga walisema kutoa ni moyo. Pamoja na jitihada kubwa za Serikali katika kuboresha mazingira na miundombinu ya afya, bado inahitaji uungwaji mkono na Watazania na wote,” alisema.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, alisema ukubwa wa tatizo la Fistula nchini, ambako kuna wagonjwa takribani 10,000, ambao wanaongezeka kwa mwaka wagonjwa 3,000, huku wanaotibiwa wakiwa ni 1,300 pekee, uliwasukuma kujitoa kusiadia eneo hilo la jamii.

Alimshukuru Waziri Mkuu Majaliwa kwa kukubali kuwa sehemu ya walioshiriki tukio hilo, lililofanyika chini ya kaulimbiu ya Mwendo wa Upendo, uliolenga kurejesha tabasamu usoni mwa kinamama wasio na uwezo wa kumudu gharama za matibabu ya Fistula yanayofikia takribani Sh. Mil. 4.

“Kiasi cha Sh. Bil. 1 tulichokusanya katika miaka miwili hii badala ya minne, kinaenda kugharamia matibabu ya fistula kwa zaidi ya wanawake 250 kwenye Hospitali ya CCBRT.

“Wanawake 10,000 wana Fistula kote nchini na kuna ongezeko la watu 3,000 kila mwaka, wakati wanaotibiwa ni takribani kinamama 1,300 tu. Kwahiyo tukaona umuhimu wa kuongeza nguvu ya makusanyo ili kusaisdia zaidi, kwani Mil. 4, ni kiasi kikubwa mno kwa Mtanzania wa kawaida kumudu kugharamia matibabu.

“Hii ndio siri iliyotusukuma kuona umuhimu wa kuharakisha zaidi, kwani wagonjwa wapo wengi na wana uhitaji, ambao haupaswi kusubiri miaka minne. Leo tumekamilisha lengo kwa miaka miwili, tunawashukuru Watanzania waliojitoa kusaidia kulikomboa kundi la kinamama wasiojiweza pale CCBRT,” alisisitiza.

Kwa nyakati tofauti, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Sanlam, Julius Magabe na Mkurugenzi Mtendaji wa UAP, Donard Muthem aliyewakilishwa na Aulerio Kimario, walifichua kwamba afya ya jamii ni miongoni mwa vipaumbele vyao kama taasisi kongwe za Bima na kwamba ndio siri ya udhamini wao mnono.


 

Waziri Mkuu azitaka Asasi za kiraia kufungua akaunti katika benki za nchini

$
0
0

 


Meneja Mwandamizi Mahusiano Benki ya NMB, Bi. Dorah Monyo (kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu, Mhe. Kassim majaliwa (kulia) alipotembelea banda hilo kwenye maonesho ya Jukwaa la mwaka la Mashirika yasiyo ya Kiserikali – Dodoma. 


Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) akijadiliana jambo na wafanyakazi wa Benki ya NMB alipotembelea banda hilo kwenye maonesho ya Jukwaa la mwaka la Mashirika yasiyo ya Kiserikali lilolofanyika Jijini Dodoma. Benki ya NMB ni mmoja wa wadau wa jukwaa hilo. 


Na Mwandishi Wetu


Mashirika yasiyo ya kiserikali nchini yameagizwa kufungua akaunti zao katika benki za nchini na kitendo hicho kimetajwa kama ni sehemu ya uzalendo.


Wito huo ulitolewa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wananchi na watumishi wa Benki ya NMB alipotembelea banda la benki hiyo katika kilele cha Jukwaa la Mwaka la mashirika yasiyo ya kiserikali.


Waziri Mkuu alitembelea NMB kuanza mazungumzo na mashirika yasiyo ya kiserikali kote nchini ili kuwafungulia akaunti ndani ya benki hiyo ambayo ina matawi 228 nchi nzima na kusema mpango huo mbali na kuonyesha uzalendo, lakini itasaidia kuongeza mzunguko wa fedha ndani ya nchi, jambo litakalotafsiriwa kama kitendo cha kizalendo.


Meneja Mwandamizi wa Mahusiano wa benki ya NMB, Bi. Dorah Monyo alisema utaratibu wa kuweka fedha kwa benki za ndani utakuwa na faida kubwa kwa wananchi kwani mzunguko wa fedha unabaki ndani na kumuahidi kuwa NMB itakuwa benki ya kwanza kusaidia mashirika hayo kuwa na akaunti ndani ya benki na zenye uendeshaji wa gharama nafuu.


Mwenyekiti wa Mtandao wa Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali, Dk Lilian Badi alisema ni wakati kwa taasisi binafsi kuwekeza fedha zao kwa mabenki ya nyumbani ili kuchangia ukuaji wa uchumi.Lakini pia, aliiomba Serikali kuzipa nafasi taasisi zisizo za kiserikali ikiwemo kuwapa uhuru wa kufanya majukumu yao kwan kwa sasa wamebanwa hasa kipengere cha usajili wa miaka 10 kwani kinawakosesha nafasi ya kujadiliana na wadau kuhusu miradi mikubwa.

ZAWA WASAKENI MAFUNDI WA MAJI MITAANI - KADUARA

$
0
0

 



Na Salma Lusangi


Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar Shaibu Hassan Kaduara ameagiza Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kuwatafuta na kuwachukulia hatua mafundi wa maji wa mitaani ambao wanaunga maji kwa wananchi kinyume na Sheria zilizoekwa na Wizara yake.


Akizungumza katika kikao na uongozi pamoja na wafanyakazi wa ZAWA huko Gombani, Pemba mwishoni mwa wiki aliwataka watendaji hao kuwatambua  wateja wao pamoja na kuwasaka mafundi wa maji wa mitaani ambao wanaunga maji kwa watu kinyume na Sheria.Alisema Wizara ya Maji, Nishati na Madini kupitia taasisi yake ZAWA imeshatoa muongozo kwamba watu wanaohitaji kuungiwa maji wafike katika ofisi hiyo kwaajili ya kujisajili.“ ZAWA hamuwajui wateja wenu, hamuwatambui mafundi wa mitaani! Mapato ya maji yanapotea kwasababu hamjawajibika ipasavyo. 


ZAWA watambueni wateja wenu, mafundi wa mitaani wanaowaungia watu maji kinyume na sheria ”. Alisema kaduaraPia alisisitiza umuhimu wa ZAWA kujipanga katika kukusanya mapato ya maji. Alisema endapo taasisi hiyo itajipanga vizuri katika ukusanyaji wa mapato basi wataweza kujilipa mishara mizuri sana na fedha zingine zitabakia.


 “Mkisimamia mapato vizuri basi mnaweza kujilipa mishara na pesa ya chenji zitabaki, simamieni mapato vizuri, kwani siku za nyuma makusanyo yalikua yanaenda vizuri, Mji wa Wete tu, mkisimamia vizuri basi mapato yataongezeka” Alielezea Kaduara.Aidha Waziri huyo alikemea tatizo la uwepo wa makundi ndani ya ofisi, ununuzi wa vifaa ambavyo sio sahihi kwa maana ya kutokua na vigezo vinavyotakiwa.


 Pamoja na kuwataka watendaji hao kusameheana endapo mtu amekwanzana na mtumishi mwenzake. Alisema kwani bila ya kusameheana watendaji hao hawataweza kufanya kazi kwa pamoja na kufikia malengo yaliyokusudiwa. 


Naye Katibu Mkuu wa wizara hiyo Joseph Kilangi aliwakumbusha watendaji hao nidhamu ya kazi, lugha nzuri kwa wateja  wao, umuhimu wa kusimamia matumizi sahihi ya fedha kwa kufuata mfumo uliyowekwa na Serikali, pamoja  na kuwahimiza kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) haraka.Pia aliwataka watendaji hao kuwa wabunifu wa kubuni miradi ya maendeleo ambayo italeta tija kwa Serikali na wananchi. Alielezea kwamba kuna baadhi ya Idara/Taasisi hazina miradi.


Aidha Katibu Mkuu huyo aliwataka mafundi wa ZAWA wasifunge mota za maji bila ya kushirikiana na wataalamu wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) kwa sababu mota zinaungua, hivyo Serikali inapata hasara zaidi ya milioni mia tano.“Wizara yetu inamgusa kila mtu tujitahidi kuzuia malalamiko na kuzuia malalamiko hayo  ni kuwajibika, nidhamu, sisi tuliyopo ofisini tunatakiwa tutowe ripoti ya miaka miwili ya uongozi wa Rais Zanzibar Dkt Hussein kwa kuangalia ilani, hivyo timu iliyopo chini ya Afisa Mdhamini Pemba itekeleze wajibu wao” Alisema Kilangi.

TEMBO WORRIES YAONDOSHWA NA HAITI KWA MBINDE

$
0
0



Na Mwandishi Wetu

TIMU ya Taifa Soka la Watu wenye ulemavu Tembo Worries imeshindwa kufua dafu mbele ya wababe Timu ya Taifa y Haiti mchezo wa Robo Fainali Kwa mabao (4-1).

Haiti waliingia kwenye mchezo huo kwa kasi na kuandika mabao ya haraka haraka kiasi cha Tembo kushindwa kuhimili hiyo presha.

Hadi kipindi cha kwanza kinahitimika Haiti (3-1) Tembo Worries. Kipindi cha pili Haiti walipigilia msumari wa mwisho na hadi kipyenga cha mwisho Haiti (4-1) Tembo Worries.

Kwa matokeo hayo Tembo Worries wameondoshwa kwenye mbio za kusaka Bingwa wa Fainali hizo zinazoendelea nchini Uturuki.

Licha ya kushindwa kutinga Nusu Fainali Tembo Worries bado wataendelea kusalia nchini Uturuki kutafuta ubora wa viwango vya Dunia kuanzia namba moja hadi nane.

Kwa mujibu wa kanuni timu zote zilizotinga hatua ya Robo Fainali ama nane Bora zinaendelea kuwa kwenye kituo cha mashindano kutafuta viwango vya ubora.


Ikumbukwe kuwa Tembo Worries katika hatua ya Robo 16 Bora  baada ya kuwachakaza Japan (3-1). Mchezo WA hatua ya 16 Bora ulipigwa jioni ya leo huko nchini Uturuki.

Ulikuwa ushindi wa pili mtawalia kwa Tembo Worries kushinda katika fainali hizo ikiwa ni baada ya kuwachakaza Uzbekistan katika mchezo wa mwisho hatua ya makundi.

Haya ni mafanikio makubwa zaidi kwa timu za Taifa hasa kwa Tanzania kuwa na uwakilishi Bora ikiwa ni mara ya kwanza kama Taifa limepata nafasi ya kushiriki mashindano hayo makubwa Ulimwengu kwa watu wenye ulemavu.

Awali Tembo Warriors, ilitinga  16 Bora ya Fainali za Dunia za Soka la Walemavu baada ya kumaliza ikiwa na pointi nne katika  kundi lake ikiwa ya tatu nyuma ya Poland na Uzbekistan.

Tembo Warriors imekata tiketi hiyo baada ya kuwa moja ya timu nne zilizoshika nafasi ya tatu zikiwa na uwiano mzuri (best looser) baada ya kuifunga Uzbekistan, kutoka sare na Hispania na kufungwa na Poland.

Kila la heri Tembo Worries katika michuano hiyo mikubwa Watanzania wako nanyi katika kupeperusha bendera ya Jamhuri ya Wapambananji.

Shirika la Posta Tanzania kuzindua stempu yenye lengo la kutangaza utalii, vivutio vya nchi

$
0
0


Kuelekea kilele cha maadhimisho ya wiki ya posta duniani yanayotarajiwa kufanyika Oktoba 9 mwaka huu, Shirika la Posta Tanzania limeazimia kuzindua rasmi huduma mpya za kidigitali ikiwepo huduma ya posta kiganjani inayomuwezesha mteja kupata huduma mbalimbali za shirika hilo kwa njia ya simu janja yake.


Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Msemaji wa Shirika la Posta Tanzania, Elia Madulesi amesema kuwa wiki ya posta inaenda sambamba na wiki ya huduma kwa wateja hivyo shirika hilo limejipanga kikamilifu kuongeza uwajibikaji na ufanisi katika utoaji wa huduma zake.


Hata hivyo amesema katika maadhimisho hayo  yatahusisha uzinduzi wa stempu maalumu iliyotengenezwa kwa ushirikiano wa serikali za Tanzania na Oman yenye lengo la kutangaza utalii wa vivutio mbalimbali vya nchi kimatafa ili kuendelea kukuza sekta hiyo.


Amesema pia kabla ya kilele cha maadhimisho hayo yatatanguliwa na kongamano la biashara mtandao na anwani za makazi lenye lengo la kuonesha maendeleo kwenye sekta na namna ukuajiwa teknolojia unavyoweza kutumika kurahisisha maisha ya wananchi.


Amesema kongamano hilo litafanyika Oktoba 8, mwaka huu katika ukumbi wa JNICC huku wadau wakitaraj8wa kujadili mafanikio na changamoto wanazozipitia watoa huduma ya biashara mtandao.


"Miongoni mwa mada zitakazojadiliwa katika kongamano hilo ni pamoja na fursa kwa wanawake vijana katika biashara mtandao,  ubunifu katika ushindani kwenye biashara mtandao, wakulima na biashara mtandao, duka mtandao la Posta na wajasiriamali pamoja na anwani za makazi zinavyowezesha biashara mtandao," amesema


Mbali na hayo, Madulesi alisema Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya Umoja wa Posta Duniani (UPU) yatakayofanyika Oktoba 9, mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).


Amesema katika kilele hicho kutakuwa na utoaji zawadi kwa washindi walioshinda katika mashindano mbalimbali yaliyoandaliwa kwa ajili ya maadhimisho hayo.


"Makundi yanayotarajiwa kupewa zawadi na mgeni huy rasmi ni uandishi wa barua kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wenye umri usiozidi miaka 18, uandishi wa insha wanamichezo na jamii, uandishi wa makala kwa wanahabari pamoja na wabunifu wa mifumo Tehama katika mawasiliano ya posta.


"Washindi watatangazwa mbele ya Waziri Nape na watapewa zawadi zao siku hiyo ya kilele cha maadhimisho haya ya UPU pale JNICC, pia tutashuhudia matokeo ya ushirikiano wa kibiashara nakihuduma kati ya Shirika la Posta la Tanzani na Omani ambao hivi karibuni walitiliana saini ya makubaliano hayo," amesema Madulesi


Kwa upande wake Meneja Biashara, Barua na Usafirishaji kutoka Shirika hilo la Posta, Jasson kalile amebainisha kuwa shirika la posta litaendela kujikita katika kutatua changamoto mbalimbali za kimawasiliano ndani ya jamii huku akitaja baadhi ya maeneo ya kitakii yanayotarajiwa kutangazwa kupitia stempu zao mpya kuwa ni pamoja na house of wonders(jengo la maajabu), mali kale, wanyama pori pamoja na mlima kilimanjaro.

Dawasa yadhamiria kuleta mapinduzi kwa wawekezaji kwa huduma ya maji

$
0
0

 


             

Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Dk. Jakaya Kikwete, akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Injinia Cyprian Luhemeja , alipotembelea banda la Dawasa wakati wa maonesho ya Uwekezaji na Biashara Mkoa wa Pwani.
 

Na Victor Masangu,Pwani 


Mamlaka ya maji Safi na usafi wa mazingira (DAWASA) imeahidi kuendelea kuboresha na kufikisha huduma ya maji kwa wawekezaji mbali mbali wa viwanda vidogo na vikubwa lengo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda.

Hayo yamebainishwa leo na mtendaji mkuu wa Dawasa Injinia Cyprian Luhemeja wakati akitoa taarifa kwa Rais mstaafu wa awamu  ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete alipotembelea Banda la Dawasa wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho ya tatu ya uwekezaji na biashara Mkoa wa Pwani.

Alisema kwamba lengo lao kubwa ni kuweza kuboresha zaidi huduma ya maji kwa wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Pwani ikiwemo wawekezaji wa viwanda vyote kuwapatia huduma ya maji.

"Tumeshiriki katika maonesho haya kwa lengo la wananchi waweze kufahamu utekelezaji wa majukumu yetu mbali  mbali ambayo tumekuwa tukiyafanya katika mikoa ya yetu ya Dar es Salaam pamoja na Pwani na tunawahidi kuwaboreshea huhuma ya maji kuanzia ngazi za vitongoji,"alisema Luhemeja.

Aidha Luhemeja amesema kuwa hakuna tatizo la maji kutokana na mitambo yote ya ruvu chini pamoja na ule wa ruvu juu yote inafanya kazi vizuri na kwamba wameshakukua tahadhari endapo kama kukitokea na ukame.

Kadhalika alisema miradi mbali mbali kwa ajili ya usambazaji wa maeneo tofauti bado kazi inaendelea ikiwemo Sambamba na kuchimba mabwawa ambayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha ukame wa mvua.

Kwa upande wake Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete aliupongeza Mkoa wa Pwani kwa kuandaa maonesho hayo ambayo yataweza kutoa fursa ya wafanyabiashara kuonesha bidhaa wanazozizalisha.

Kadhali alimpongeza mtendaji mkuu wa Dawasa kwa kuweza kuendelea kuwahudumia wananchi katika kuwasambazia maji safi na salama ili wananchi waweze kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa maji.


SULUHISHO LA UCHELEWESHAJI WA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO LAPATIKANA

$
0
0

 


Kamishina wa Idara ya Mipango ya Kitaifa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Mursali A.Milanzi akizungumza na Washiriki wa Mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa Kitaifa wa Kusimamia Miradi ya Maendeleo - National Project Management Information System (NPMIS) yanayofanyika Jijini Arusha.

 

 

 

Na Ramadhani Kissimba,WFM - Arusha

 

Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imekuja na suluhisho la tatizo lililokuwa linasababisha baadhi ya Miradi ya Maendeleo kuchelewa kutekelezwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mlolongo mrefu uliokuwepo katika hatua za awali za utekelezaji wa miradi hiyo.

 

Hayo yamesemwa na Kamishina wa Idara ya Mipango ya Kitaifa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt Mursali Milanzi wakati akifungua mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa Kitaifa wa Kusimamia Miradi ya Maendeleo - National Project Management Information System (NPMIS) yanayofanyika Jijini Arusha.

 

Dkt. Milanzi amesema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na wadau wengine kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali wakati wa uratibu au utekelezaji wa miradi na programu za maendeleo changamoto ambazo zimekuwa zikipelekea kupunguza kasi ya utekelezaji na ufuatiliaji wa miradi mbalimbali nchini.  

 

‘’Napenda kuchukua nafasi hii kuelezea kwa ufupi baadhi ya changamoto ambazo Wizara ya Fedha na Mipango na wadau wengine wanaoratibu au kutekeleza miradi na programu za maendeleo wamekuwa wakikabiliana nazo kwa muda mrefu ikiwemo, barua za miradi mipya na inayoendelea kupokelewa bila kuwa na viambatisho muhimu vya nyaraka za miradi, baadhi ya viambatisho kuwa vikubwa na kushindwa kuingizwa kwenye majalada na upatikanaji usioridhisha na usio wa haraka wa taarifa za miradi pindi zinapohitajika’’. Alisema Dkt. Milanzi.

 

Dkt. Milanzi aliongeza kuwa katika kutatua changomoto hizo, Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikisha wadau mbalimbali imeona ije na suluhisho kwa kuanzisha Mfumo utakaohusika moja kwa moja na Utekelezaji wa Miradi na Programu za Maendeleo nchini, Mfumo ambao umezingatia mahitaji ya wadau wote na utendaji kazi wa majukumu ya kila mdau nchini katika uratibu na utekelezaji wa miradi na programu za maendeleo.

 

Aidha, Dkt. Milanzi alisema kuwa kuna umuhimu wa Mfumo huu kuanza kutumika ipasavyo na ndio maana Wizara ya Fedha na Mipango ikaandaa Waraka wa Hazina Na.5 wa mwaka 2020/21 kuhusu matumizi ya Mfumo wa Kitaifa wa Kusimamia Miradi ya Maendeleo na Waraka wa Hazina Na. 1 Kuhusu Utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2022/23 unaosisitiza uzingatiaji na utekelezaji wa Mfumo huu.

 

 

Awali akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mifumo ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. John Sausi amesema lengo la uanzishwaji wa Mfumo huo ni kutaka Serikali kuwa na orodha ya Miradi yote inayoitekeleza na kuwa na taarifa sahihi ya miradi hiyo.

 

Dkt. Sausi aliongeza kuwa Serikali itaendelea kuuboresha mfumo huu kulingana na mahitaji ya wadau na kuwaomba washiriki na wadau wote wanaotumia Mfumo huo kuendelea kutoa maoni yatakayosaidia kurahisha utendaji kazi wa Mfumo huo.

 

 

Pia kwa kumalizia Kamishina wa Idara ya Mipango ya Kitaifa, Dkt. Milanzi alisema kuwa utumiaji wa Mfumo wa Kitaifa wa Kusimamia Miradi ya Maendeleo – National Project Management Information System (NPMIS) utasaidia kuongeza ufanisi kwenye uibuaji, upangaji, uwasilishaji, uchambuzi, utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya Miradi ya Maendeleo, pamoja na kurahisisha utunzaji wa kumbukumbu za Miradi ya Maendeleo iliyopo katika hatua mbalimbali za mzunguko wa utekelezaji wa miradi (Project cycle).

 

Mafunzo hayo ya matumizi ya Mfumo wa Kitaifa wa Kusimamia Miradi ya Maendeleo yanahudhuriwa na washiriki 58 ambapo washiriki 26 wanatoka katika Ofisi za Tawala za Mikoa na  Serikali za Mitaa na Watumishi 32 kutoka katika Wizara, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Ofisi ya Msajili wa Hazina.

 

WAZIRI DKT MABULA ATAKA UFANYIKE UPEMBUZI MASHAURI YA ARDHI YALIYOKAA MUDA MREFU

$
0
0


 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (wa pili Kulia) pamoja na Katibu Mkuu Dkt Allan Kijazi (wa pili kushoto) pamoja na viongozi wengine wa Wizara wakiwasili kwenye kikao kazi baina ya Kitengo cha Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya na Chama cha Wnasheria Tanganyika (TLS) kilichofanyika jijini Dodoma Oktoba 6, 2022.

 

Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA

 

Wzairi wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameagiza ufanyike upembuzi kawa mashauri yote ya ardhi yaliyokaa muda mrefu kutokana na sababu zisizo na mashiko.

Amemtaka Msajili wa Mabara ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya Stella Tullo kusimamia agizo hilo kwa kumpatia taarifa mapema mwezi Novemba 2022.

Aidha, alimtaka Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuangalia kwa jicho la tatu Mabaraza yote ya Ardhi ya mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwa kumekuwa na malalamiko mengi ya mlundikanao wa kesi za muda mrefu.

Dkt Mabula alitoa agizo hilo Oktoba 6, 2022 wakati wa Kikao kazi cha Kitengo cha Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kilichofanyika jijini Dodoma.

Dkt Mabula alisema, serikali inatambua umuhimu na michango ya mawakili katika kuvisaidia vyombo vya utoaji haki na kuwakumbusha mawakili suala la maadili ya kiutendaj hasa kwa baadhi ya wajumbe kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, uzoefu unaonesha mashauri mengi yanayowakilishwa na mawakili ndiyo yenye kuchukua muda mrefu kumalizika.

‘’Mshauri mengi ya ardhi katika mabaraza hayapewi kipaumbele na Wakili anaweza kupanga tarehe ya kesi ambayo kwa siku hiyo ana mashauri katika vyombo vingine vya kutoa haki ‘’

Waziri wa Ardhi aliongeza kwa kusema kuwa, uchunguzi wa awali unaonesha pia baadhi ya mapingamizi yana dhamira ya kupoteza muda hususan yale mashauri yanayohusu taasisi za fedha.

‘’Mashauri mengi yanayofunguliwa na wananchi walioshindwa kurejesha mikopo  kwa wakati au kukiuka mikataba ya mikopo, wananchi wanakimbilia kwenye mabaraza kwa kushauriwa na mawakili’’. Alisema Dkt Mabula

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, ucheleweshaji mashauri kwa sababu zozote zile ni kuchelewesha kupata haki kwa wakati na kutoa rai kwa mawakili kuona umuhimu wa kuunga mkono juhudi za serikali kwa kutumia nafasi zao kama maafisa wa mahakama kwa nia ya kuhakikisha mashauri ya ardhi yanamalizika kwa wakati na kwa haki kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Allan Kijazi alisema, wizara yake imeitisha kikao cha pamoja na mawakili wa kujitegemea kwa lengo la kuhakikisha mashauri ya ardhi katika mabaraza yanasikilizwa na kumalizwa kwa wakati.

‘’Mawakili wa kujitegemea mnapotekeleza kwa uadilifu uaminifu na weledi jukumu lenu la kuwakilisha wananchi katika mashauri mnawarahisishia wenyeviti wa mabaraza ya ardhi kazi ya kusikiliza na kutoa maamuzi kwa wakati kwani uwakilishi wenu kwa namna moja ama nyingine unatoa dira mapema ya kufahamu mwananchi yupi ana haki na yupi hana haki katika shauri husika’’ alisema Dkt Kijazi.

Kikao Kazi cha Kitengo cha Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kina lengo la kupata uelewa wa pamoja, kupokea changamoto wanazokutana nazo katika mabarza ya ardhi pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya Wizara na TLS katika kutatua kero za wananchi nwenye mashauri ya ardhi.

Waziri Nape ashiriki wiki ya huduma Airtel, awashukuru kwa kuunga mkono uchumi wa kidigitali

$
0
0

 

 Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akishiriki kumhudumia mteja wakati alipotembelea kituo cha kutolea huduma kwa wateja cha Airtel ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya huduma ya wateja.

 

Dar es Salaam Alhamisi 6 Oktoba 2022, Waziri wa  Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Haabri Nape Nnaye leo ameshiriki kwenye maonyesho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja yaondaliwa na kampuni ya Airtel Tanzania jijini Dar es Salaam.

Maonyesho hayo ambayo yalianza tangu mwishoni mwa wiki ni kwa ajili ya kuleta wateja wa Airtel kwa ukaribu, kujua changamoto zao na kuweza kuzitatua ili kuendelea kutoa huduma za mawasiliano yaliyo bora.

Akizungumza baada ya kumalizika kutembelea maonyesho hayo, Waziri Nnauye alitoa pongezi kwa Airtel kwa kuweza kuendelea kuboresha huduma zake. ‘Naomba nichukue fursa kuwafahamisha Watanzania kuwa Airtel ni kampuni inayomilikiwa na serikali ya Tanzania kwa asilimia 49 kwa hivyo ni muhimu kutambua kuwa wanapotumia huduma za Airtel wanatumia kilicho chao’, alisema Nnauye.

‘Nimefurahi kuona jinsi Airtel imejipanga kuwahudumia Watanzania huku ikiendelea kuboresha huduma zake. ‘Serikali imekuwa ikiwahimiza watoa huduma kuangalia namna ya kusaidiaWatanzania kuendana na ulimwengu wa kidigitali kwa kuongeza upatikanaji wa simu njanja. Kwa kuona na kutambua umuhimu huo, Airtel imekuja na njia ya kutoa simu njanja kwa mkopo, ambapo mteja analipia elfu 70 na kisha kumalizia kwa kulipa kidogo kidogo’, alisema Nnauye.

‘Natoa shukrani kwa niaba ya serikali kwa watoa huduma za mawasiliano akiwemo Airtel kwa kazi nzuri mnayo endelea kufanya na mpaka kutambulika na Shirikisho la Mawasiliano Duniani na hatimaye kuweza kuchanguliwa kuingia kwenye Baraza hilo kwa kupata kiti katika ya 48. Hii ni kazi nzuri ambayo watoa huduma za mawasiliano wamekeza na nawapongeza sana.

Waziri Nnauye pia alitembelea kituo cha kutoa huduma kwa wateja na kushiriki kwenye kusikiliza na kutatua baadhi ya changamoto kutoka kwa Wateja wa Airtel.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji Airtel Tanzania Dinesh Balsingh alimpongeza Waziri Nnauye kwa kushiriki wiki ya huduma kwa wateja, na kusema imeleta hamasa kubwa kwa wafanya kazi wa Airtel kuendelea kutoa huduma za hali ya kimataifa.

‘Wiki ya Huduma kwa wateja inatoa fursa nyingine kwa Airtel kujiweka karibu na wateja wake ambao ni watu muhimu sana kwenye biashara yetu. ‘Huku kauli mbiu ya Wiki ya Huduma kwa wateja ikiwa ni furahia huduma, Airtel inajivunia kwa Watanzania kuwa wateja wetu na tunahidi kuendelea kutoa huduma bora na za kisasa, alisema Balsingh.

 ‘Moja kati ya hatua ambazo Airtel tuweza kuzipiga vizuri na tunazojivunia ni teknolojia. Tunayo furaha kubwa kuwa kwa sasa wateja wetu wanaweza kutumia teknolojia na kujihudumia papo hapo. Wateja wa Airtel kwa wanaweza kupata LUKU TOKEN kwa kujihudumia mwenyewe, kurudisha muamala uliokosewa, kurudisha laini ya simu iliyopotea bila kuongea na mtoa huduma wa Airtel. Huduma zote hizi mteja anaweza kuzipata kwa urahisi na hii ni moja ya faraja yetu tunayojivunia kwenye teknolojia kama watoa huduma, aliongeza Balsingh.

KITUO CHA AFYA MOSHI-ARUSHA CHAKABIDHIWA MANISPAA YA MOSHI

$
0
0


Naibu katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo, akimkabidhi Meya wa Manispaa ya Moshi Mjini, Mhe. Mhandisi Zuberi Kidumo, nyaraka za umiliki wa kituo cha afya Moshi-Arusha katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. Katikati ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Jairy Khanga.



Na Saidina Msangi, WFM, Kilimanjaro

 

Serikali imekabidhi kituo cha Afya Moshi-Arusha pamoja na mali mbalimbali ikiwemo kiwanja na majengo vyenye thamani ya Shilingi bilioni 4.3 kwa Manispaa ya Moshi ili iweze kukiendeleza kwa kutoa huduma za afya kwa wananchi wa manispaa hiyo na maeneo ya jirani. 

 

Makabidhiano ya kituo hicho yamefanyika katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro kati ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo na Meya wa Manispaa ya Moshi, Mhe. Mhandisi Zuberi Kidumo.

 

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi kituo hicho, Bi. Omolo alisema kuwa Serikali inakabidhi kituo hicho pamoja na mali zake zote kwa manispaa hiyo ili iweze kutoa huduma kwa wananchi.

 

‘’Pamoja na majengo tunakabidhi mali nyingine ikiwemo samani352, mitambo 70 na gari moja vyenye thamani ya Sh.milioni 94.21, mali chakavu zenye thamani ya Sh. 280,000, bunduki, bakaa za benki zilizoishia Julai 2022, madai ya kodi ya pango yenye thamani ya shilingi milioni 1.2 namadai kwa taasisi za bima za afya yenye thamani ya Sh. milioni 32.4,’’alisema Bi. Omolo.

 

 

Pia ilikabidhi madeni yenye nyaraka yenye thamani ya Sh. milioni 610.3na yasiyo na nyaraka zinazojitosheleza yenye thamani ya sh.milioni 71.9 na ufuatiliaji wa mauzo ya magari mawili yenye thamani ya Sh.milioni 2.3.

 

 

Aidha, Bi. Omolo alimtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi kuhakikisha kuwa kituo hicho kinafanyiwa maboresho ili kirejeshewe hadhi yake ya Hospitali na kuendelea kutoa huduma kwa wananchi wa manispaa hiyo na maeneo ya Jirani.

 

 

Alimtaka Mkurugenzi huyo kufuatilia taratibu za kuhamisha umiliki kwa kumshirikisha Kamishna wa Aridhi na kufuatilia nyaraka zilizokosekana za madai ya watumishi pamoja na kuchukua hatua stahiki kwa watumishi waliyojimilikisha mali za kituo hicho kinyume na sheria.

 

 

Aidha alisisitiza kuwa jukumu la kulinda mali za Serikali ni la wote, na kuelekeza kuwa baada ya makabidhiano mali zote ziingie kwenye daftari la mali za Serikali ambalo limeboreshwa na kuliweka katika mfumo wa kielektroniki wa usimamizi wa mali za Serikali ujulikanao kama GAMIS.

 

 

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Chotto Sendo, alisema kuwa uhakiki wa mali na madeni ya kituo hicho umekamilika na Serikali kwa kutambua umuhimu wa kituo hicho imeamua kikikabidhi kwa Manispaa ya Moshi ili iweze kukiendesha kuhudumia wananchi.  

 

‘’Lengo ni kutoa huduma kwa wananchi kwa hiyo Serikali imeamua kurejesha kituo hicho Serikalini kwa Manispaa ya Moshi ili wananchi waendelee kupata huduma za kiafa katika kituo hiki’’ alisema Bw. Sendo.

 

Naye Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Ubinafsishaji, Ufuatiliaji na Tathmnini kuitoka Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Abissay Ndaki, alisema kuwa hospitali hiyo imerejeshwa Serikalini kwa jina la Msajili wa Hazina wakati taratibu nyingine zikiendelea kufanyika na kuishukuru Serikali kwa kuridhia kurejesha kituo hicho kwa Manispaa ya Moshi ili kiweze kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.

 

Naye Mbunge wa Moshi Mjini Mhe. Priscus Tarimo, ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha manispaa hiyo kupatiwa kituo hicho ili kuweza kutoa huduma kwa wananchi wake na kuboresha upatikanaji wa huduma za kiafya.

 

Kituo cha afya Moshi/Arusha kilianzishwa mwaka 1973 kama utekelezaji wa agizo la Serikali kwa mashirika ya Umma Na.2/46/050 la tarehe 17 Novemba, lililotaka mashirika ya Umma yanayohusika na viwanda kutoa huduma za tiba na kinga pamoja na huduma za kuzuia na kutibu madhara yanayotokana na mazingira ili kuboresha afya za wafanyakazi.

 

 

Majengo ya Kituo hicho yalijengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Uholanzi na kituo kikikiwa na hadhi ya Hospitali huku kikitegemea michango ya wenye viwanda vilivyopo Moshi na Arusha wakati huo ili kukiendesha.

 

 

Hata hivyo miaka ya 1990 baada ya viwanda hivyo kushindwa kujiendesha kulisababisha Wizara ya Afya kuishusha Hospitali hiyo kuwa Kituo cha Afya.

DK. NCHEMBA AWAFUNDA WAKAGUZI WA NDANI WA SERIKALI

$
0
0

 


 
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza na Wakaguzi wa ndani 140 kutoka halmashauri 69 nchini( hawapo pichani), wanaoshiriki mafunzo ya siku tatu ya namna ya kukagua kwa ufanisi taarifa za fedha, yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali katika Kituo cha Mikutano cha NBAA, Bunju, Dar es Salaam.
 
 
Na Josephine Majula na Scola Malinga WFM - DSM

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amewataka Wakaguzi wa Ndani kufanya kazi zao bila kupepesa macho kwa kufichua upotevu wote wa fedha za umma kwa kuwa Serikali ipo na itawalinda ili kuhakikisha fedha za umma vinatumiwa vizuri kama ilivyopangwa

Dkt. Nchemba ametoa maelekezo hayo wakati akifungua mafunzo ya Siku tatu ya Wakaguzi wa Ndani wapatao 140 kutoka Halmashauri 69 nchini, kuhusu ukaguzi wa taarifa za fedha kutoka katika Taasisi za Umma yanayofanyika katika Kituo cha NBAA, Bunju, Jijini Dar es Salaam.

“Wekeni wazi upotevu wote wa fedha za umma katika miradi inayotekelezwa ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa wale wote watakaokuwa wametumia vibaya fedha ya umma”, alisisitiza Dkt. Nchemba

Aidha, Dkt. Nchemba aliahidi kuzipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ufinyu wa bajeti, vitendea kazi na wataalamu mbalimbali wakiwemo wahandasi watakaoshiriki katika ukaguzi wa mali za umma Pamoja na kukamilisha muundo mpya wa tasnia ya ukaguzi wa ndani ili kuleta tija.

“Serikali itazifanyia kazi haraka changamoto hizo ili zisiwe kikwazo katika kutekeleza majukumu yenu ya msingi”, alisisitiza Dkt. Nchemba.

Alisisitiza umuhimu wa wataalam hao kuyatumia mafunzo watakayoyapata kuboresha mifumo ya ukaguzi wa ndani kwa sababu kada hiyo ni muhimu kuchangia udhibiti wa matumizi ya serikali kuoitia ukaguzi wanaoufanya.

Kwa Upande wa Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Bw. Athumani Mbuttuka, alitoa wito kwa maafisa masuuli kutenga fedha kwa ajili ya ukaguzi katika miradi yote inayoibuliwa ili kupata thamani halisi ya utekelezaji wa miradi hiyo.

“Kada ya Wakaguzi wa ndani inakabiliwa na changamoto za kibajeti hivyo ninakuomba mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mioango, kuwaelekeza maafisa Masuuli, wakati wanaanda miradi, waweke fungu la ukaguzi katika miradi hiyo, hatua hii itasaidia kupunguza ama kuondoa kabisa malalamiko ya wananchi kuhusu utekelezaji wa miradi yao” alisema Bw. Mbuttuka

Aidha, Bw. Mbuttuka alielezea umuhimu wa wakaguzi wa ndani kujengewa uwezo na ujuzi wa kufanya ukaguzi kwenye mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ambayo inatumika kwa kiasi kikubwa ili kudhibiti upotevu wa fedha za umma na kuongeza mapato ya Serikali.

“Tumeanza kutoa mafunzo kwa wakaguzi wetu wa ndani ili kuwajengea uwezo wa kufanya ukaguzi kupitia mifumo ambapo hadi kufikia mwaka 2026, tunatarajia kuwa na wataalam zaidi ya 320 watakaopatiwa mafunzo hayo ili kukabiliana na ushindani na mataifa mengine Jirani waliowekeza kwa kiwango kikubwa katika taaluma hiyo” Alisema Bw. Mbuttuka


Kwa upande wao, Mkaguzi Msaidizi wa Ndani Mkuu wa Serikali Bw. Emmanuel Subi na mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo ambaye ni Kaimu Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, CPA Wamilika Mlangi, waliishukuru Serikali kwa kuendesha mafunzo hayo yatakayo waongezea ujuzi wa kufanya kaguzi mbalimbali kwa ufanisi Zaidi na hivyo kuleta tija katika matumizi ya fedha za Serikali.

Washiriki wa mafunzo hayo wamekubaliana kwenda na kauli mbiu isemayo: Tutakwenda, Tutakagua na Tutatoa taarifa kama ilivyo, baada ya kupewa changamoto hiyo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Wakaguzi wa Ndani wapatao 520 kutoka nchi nzima wanatarajiwa kupatiwa mafunzo hayo ya ukaguzi wa taarifa za fedha ili kujiridhisha kuhusu usahihi wake kabla ya kuwasilishwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).


SERIKALI KUTENGA SH.BILIONI 4.6 KUNUNUA ZANA ZA KILIMO SINGIDA

$
0
0

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akiongoza kikao cha kupanga mkakati wa kuongeza uzalishaji wa zao la alizeti kilicho washirikisha mkuu wa mkoa wa Singida, wakuu wa wilaya, wenyeviti na wakurugenzi wa halmashauri pamoja na maafisa kilimo ambacho kiliketi leo Oktoba 5, 2022 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba.akizungumza katika kikao hicho.
 

Na Dotto Mwaibale,Singida

 

SERIKALI katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2023/2024 inatarajia kutenga Sh.Bilioni 4.6 kwa ajili ya kununua zana za kilimo Mkoa wa Singida. 

 

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameyasema hayo kwenye kikao cha kupanga mkakati wa kuongeza uzalishaji wa zao la alizeti kilicho washirikisha mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya, wenyeviti na wakurugenzi wa halmashauri pamoja na maafisa kilimo ambacho kiliketi leo Oktoba 5, 2022 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. 

 

Alisema Serikali baada ya kununua zana hizo halmashauri zitatakiwa zitenge maeneo maalumu ambapo zana hizo zitawekwa na kutakuwepo mtu maalum wa kuzisimamia na  wakulima watakuwa wakienda kukodisha. 

 

Alisema fedha zitakazopatikana baada ya wakulima kukodi zana hizo zitarudishwa Serikalini na kwenda kununua zana hizo katika mikoa mingine. 

 

Awali akitoa mchanganua wa bajeti ya ununuzi wa zana hizo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya mkakati ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo Justice Kijazi alisema Halmashauri za Wilaya za Ikungi,Mkalama, Iramba na Itigi kila moja zitahitaji zana zenye thamani ya Sh.706 Milioni. 

 

Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni itahitaji Sh.791Milioni huku Singida DC ikiwa ni Sh.309 Milioni. 

 

Akizungumzia kuhusu mpango mkakati wa zana hizo Kijazi alisema ni kuimarisha upatikanaji wa zana bora za kilimo, mkoa unaboresha mazingira ya uwekezaji ili kuvutia wawekezaji wa zana za kilimo, kuanzisha vituo vya umahiri wa zana (Agricultural mechanization hub) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo. 

 

Alitaja mkakati mwingine kuwa ni kuwaelimisha wakulima kuhusu mikopo ya kibenki yenye lengo la upatikanaji wa zana bora za kilimo kwa masharti nafuu na Mfuko wa Pembejeo (AGITF) uwezeshe wakulima upatikanaji wa mikopo nafuu ya zana za kilimo mkoani hapa. 

 

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba alisema mkoa umejipanga kusimamia kilimo ili kiwe sababu ya kuondoa umasikini kwa wananchi. 

 

“Mheshimiwa Waziri napenda kukuhakikishia kuwa hapa Singida kazi kubwa ni kilimo tutakifanya usiku na mchana ili tuweze kuwasaidia wananchi wetu na maelekezo yako yote tutayafanyia kazi” alisema Serukamba. 

 

Serukamba alisema awali watu walidhani kuwa kilimo ni jambo la kawaida na la mtu binafsi lakini sasa ni biashara na mkombozi kwa wananchi na kuwa wanazipongeza jitihada zote zinazofanywa na Serikali za kuinua kilimo na wao kama mkoa wanaziunga mkono na kutekeleza maagizo yote waliyopewa.

NABI ATAMBA KUNASA 'FILE' LA IBENGE

$
0
0


Na John Marwa

KOCHA Mkuu wa klabu ya Yanga SC Nasriddine Nabi ametamba kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL dhidi ya Al Hilal ya Sudan.



Nabi ataiongoza Yanga kesho katika mchezo wa hatua za awali kuwania kufuzu hatua ya makundi msimu huu wa 2022/2023.

Mchezo huo utapigwa katika Dimba la Benjamin Mkapa majira ya saa 16:00 kwa saa za Afrika Mashariki.

Akizungumza na wandishi wa Habari kuelekea mchezo huo Nabi amesema kikosi chake kiko tayari kuwakabili Al Hilal huku akijinadi kunasa njia za kuwaangamiza wapinzani wao.

"Ni mechi ambayo inahitaji ushindi wa jumla Ili kuweza kufuzu. Kwa upande wetu tumejiandaa kwa utulivu mkubwa sana, mashabiki wanahitaji kusikia nini tunaenda kufanya lakini tumetulia sana kwa ajili ya hii mechi"

"Tunaenda kukutana na timu nzuri, yenye rekodi nzuri kwenye michuano hii, miaka nane iliyopita niliifundisha na kuipeleka makundi,  wamekuwa bora mtawalia sasa wamekuwa wakifuzu hatua ya makundi. Al Hilal wanaifahamu Yanga na wanaiheshimu ndio maana wamecheza mechi ya kirafiki dhidi ya TP Mazembe." Amesema nankuongeza kuwa.

"Kitu ambacho ninawaambia wachezaji wangu ni kutambua kuwa tunaenda kucheza na timu nzuri na yenye uzoefu Mkubwa, hatuwezi kuwadharau kwa matokeo waliyopata katika mechi ya kirafiki kwa sababu huu ni mchezo mwingine kabisa"

"Wachezaji wako tayari kupambana kwenye mchezo wa kesho, wakijiamini kwa sababu wanamheshimu mpinzani wetu, mechi hii haitaishia kwa Mkapa bali itaenda kuishi Khatoum Sudan, ni mechi ngumu kwa sababu mshindi anaingia hatua ya makundi." Nabi ameongeza kuwa.

"Hali ambayo wachezaji waliyokuwa nayo juzi na jana inaonyesha wako tayari kupambana na Al Hilal hapo kesho, ni jambo linalonipa faraja kuwa tunaweza kupambana.

"Hii mechi ni mechi ambayo Al Hilal wamejiandaa kisawasawa, wametufatilia na sisi tumewafuatilia kujua wachezaji wao wana ubora wapi na madhaifu yao." Amesema Nabi

Licha ya mechi zao kutotaka zionyeshwe Lakini Nabi amesema amefanikiwa kutuma watu wa kuwatazama.

"Naamini namna watakavyocheza na sisi ni tofauti na walivyocheza na TP Mazembe na St George." Amesema Kocha Nabi.

Yanga watashuka kwenye mchezo huo wakihitaji matokeo zaidi ili kuvunja rekodi ya kutoshiriki hatua ya makundi kwa miaka 24.

TFF YAZIFUNGIA KUSAJILI TANZANIA PRISONS NA SINGIDA BIG STARS

$
0
0


 

Na Mwandishi Wetu

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imezifungia kusajili klabu za Ligi Kuu ya NBC za Tanzania Prisons na Singida Big Stars kwa kosa la kusajili wachezaji wenyewe mikataba na klabu nyingine.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na TFF imeeleza kuwa klabu hizo hazitaruhusiwa kusajili kwa dirisha Moja la usajili.

"Uamuzi wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji umefanywa kwa kuzingatia kanuni ya 47(21)  ya Ligi Kuu baada ya kuzikuta na kosa hilo. Adhabu hiyo ni kwa dirisha moja la usajili."

"Tanzania Prisons ilimsajili kipa Musa Mbise wa Coastal Union wakati ikifahamu kuwa bado ana mkataba klabu hiyo. Nayo Singida Big Stars ilimsainisha mkataba Kipa Metacha Mnata huku akiwa bado ana mkataba na Polisi Tanzania." Imeeleza taarifa hiyo na kuongeza kuwa.

"Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji inazikumbusha klabu zote nchini kuwa usajili wa wachezaji unafanywa kwa kuzingatia kanuni, na ambazo zitakiuka kanuni zitachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni." Imeeleza taarifa hiyo.


WANANCHI KILA MLANGO NA UFUNGUWO WAKE

$
0
0

 


Na John Marwa


'Kila mlango na ufunguwo wake' ni kiswahili tu na nahau zake, kiswahili tu na ubantu wake. Ndio hakuna fundi wa kutengeneza milango kwa funguwo moja bali kila mmoja unawake, kama mwili wa biandamu na moyo wake.


Kama amabavyo siku moja ina masaa 24, kwa nini wiki moja isiwe na siku 24 ama mwaka mmoja uwe na miezi 24 kwa sababu kila mlango nafunguwo yake. Ni kama mbio na umbali wake ndio huleta madaraja.


Leo Wananchi jogoo kawika kawakumbusha kuwa kumekucha na siku ndio hii ya kwenda kufungua mlango uliojifunga kwa miaka 24, yaani mwaka mmoja kabla ya Taifa kumpoteza Mtanzania namba moja na mwasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.


1998 Mwaka huu alizawa mdogo wangu kipenzi Paschalia, leo ana miaka 24 na yuko pale KCMC anamalizia shahada yake ya Udaktari. Funguwo hamjaipata tu!


Bahati mbaya ni Mwananchi mwenzenu lakini tangu azaliwe hadi leo hajawahi kusikia mko makundi Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), Na shaka yangu asije anza kujitibia yeye badala ya kuwatibia ninyi  Moyo wake.


Labda Kipendacho Moyo ni dawa, lakini siamini hii hali mnaipenda, na kama mnaipenda haijawatibu maradhi yenu japo dawa yake mwaijua imejificha kwenye miaka 24. (Tuseme Mwananchi Dozi24)


Sitaki kuwasemea kwa ndugu yenu wa damu japo mnampopoa lakini yeye fungo yake kaifanya iwe 'Kawaida ni kama Sheria' ndio acha tuendelee na Mwananchi Dozi24 hii ndio tiba yenu hii ndio funguwo yenu kufika makundi Ligi ya Mabingwa Afrika Msimu huu.


Mwananchi Dozi24 mnawakumbuka Asec Mimosa, Manning Rangers na Raja Casablanca? hawa ndio chanzo Cha Mwananchi Dozi24, hawa ndio walishindwa kuwaambia kwa nini siku ina masaa 24 na wiki ina siku saba.


Asec Mimosa alikuwa bingwa kutoka kwenye kundi lenu ambalo mlishika mkia, tulizeni akili zenu hapa ndipo mlipo usahau ufunguwo wa Mwananchi Dozi24.


Yaani kumbukeni vizuri mlicheza na bingwa wa msimu wenu lakini hamkurudi tena hadi leo! Mwananchi Dozi24 amka kumekucha Lupaso panakuita funguwo Iko mikononi mwenu.


Kaujazeni Uwanja, kaionyesheni Afrika mmeipata funguo, msiwaonyeshe Nasreddine Nabi, msiwaonyeshe Fiston Mayele waonyeshe Mwananchi Dozi24 yenye funguo za kutinga makundi na sio kuwa na Azizi Ki.


Kuna Methali ya waswali inasema 'Ikiwa hujui kufa tazama kaburi' Mwananchi ikiwa mmesahu machungu ya kutocheza CAF CL hatua ya makundi basi kumbukeni kifo chenu cha mara ya mwisho katika hatua hiyo.


Mlishika mkia kundi akiongoza Asec Mimosas. Jeneza lenu liligongwa mabao 19 ya kufungwa na mkifunga mabao 5 yaani mlihusika kuzalisha mabao 24, kati ya mabao 155 ya msimu huo. (Mwananchi Dozi24)


Mwananchi kumbuka dawa ya moto ni moto, amkeni kauwasheni moto, amkeni kawapeni morali wanajeshi wenu, amkeni maana chanjo ya gonjwa lenu la Mwananchi Dozi24 mnayo wenyewe.


Mna Mayele, Morrison, Aziz Ki, Feisal Salum, Gael Bigirimana, Khalid Aucho,  Yanick Bangala na Djuma Shabani amini hao hawatoshi ila ninyi Wananchi mnatosha kuifanya Lupaso iwe Benjamin Mkapa jina la heshima bali machinjio ya Swahiba wenu Ibenge na vijana wake.


Wananchi msiseme maneno matupu 'IWE JUA IWE MVUA ' kumbukeni Kuambizana kuko kusikilizana hapana.


Kila la heri Wananchi kila la heri Young Africans.


Hii ni kalamu ya maskini yenye wino wa DAMU 

John Richard Marwa

@johmasterplan

0717982635

SIMBA WAIFUATA DE AGOSTO NA DOZI KAMILI

$
0
0

 


Na Mwandishi Wetu


Kikosi cha wawakilishi bora wa Michuano ya Afrika, ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Simba SC kimeondoka alfajiri ya leo kuwafuata De Agosto ya Angola tayari kwa mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua za awali Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL kuwania kufuzu hatua ya makundi.


Simba wameondoka na na Ndege ya kukodi ambayo itawapeleka na kuwatudisha baada ya kucheza hapo kesho kurejea kujiandaa na mchezo wa mkondo wa pili.


Wana Robo Fainali hao wa Kombe la Shirikisho msimu uliopita wameondoka na kikosi cha wachezaji 24 huku wale walioko majeruhi wakisalia kuendelea na matibabu.


Simba wanatarajiwa kushuka dimbani kesho majira ya saa 12 jioni majira ya saa za Afrika Mashariki kuwakabili wenyeji wao De Agosto.


Akizungumza kabla ya kudondoka Kocha Mkuu Juma Mgunda amesema wamejiandaa vema na maandalizi yamekamilika kulingana na aina ya mpinzani wanaenda kucheza nae.


"Maandalizi yamekamilika na tuko tayari kwa ajili ya mapambano, tunatambua nakuheshimu ubora wa wapinzani wetu, tuko tayari kuukabili.


"Katika hatua hizi hakuna mchezo rahisi kama benchi la ufundi na wachezaji tunatambua kuwa jukumu lililoko mbele yetu ni kubwa lakini tunapaswa kufanya vizuri na tuko tayari kwa hilo.


"Kikosi kiko imara ukiachilia vijana wetu watatu, Peter Banda, Jimson Mwanuke ambao walipata kadhi hiyo tulipokuwa Zanzibar na kijana wangu Shomary Kapombe. Wengine wote wako timamu na imara tunaamini wataifanya kazi vyema ya kuiwakilisha Simba na Taifa kwa ujumla." Amesema Mgunda.


Kwa uapnde wa Nahodha John Bocco amesema maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa na wao kama wachezaji wanafahamu umuhimu wa mchezo ulioko mbele yao.


"Maandalizi yamekamilika kwa ajili ya mchezo ulioko mbele yetu, tunafahamu umuhimu na ugumu wa mechi hii na tumejiandaa kwa hilo.


"Ni hatua kubwa na ngumu lakini kama Simba tunatambua tunapaswa kufanya vizuri Ili kuweza kufuzu hatua ya makundi na kufikia malengo kama Klabu na kuiwakilisha nchi vizuri" amesema Bocco. 

BIGIRIMANA; WANANCHI NJOONI TUWAPIGE KAMA NGOMA AL HILAL

$
0
0

 


Na Mwandishi Wetu




Na Mwandishi Wetu


NYOTA wa Klabu ya Yanga SC Gael Bigirimana amewaomba mashabiki wa Klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wao wa kesho dhidi ya Al Hilal ya Sudan.


Yanga watashuka kwenye Dimba la Benjamin Mkapa kuwkaribisha Al Hilal katika mchezo wa kwanza hatua za awali Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL kuwania kufuzu hatua ya makundi kabla ya kurejeana nao mjini Khatoum wiki moja ijayo.


Akizungumza na wandishi wa Habari mchana wa leo Bigirimana amesema kama wachezaji wanafahamu umuhimu wa mchezo huo na wako tayari kupambana na Al Hilal hapo kesho.


"Kama Wachezaji tunafahamu umuhimu wa mchezo huu, tunafahamu una maana gani kwa klabu na mashabiki. Jambo kubwa na la muhimu kwentu ni kuhakikisha kuwa tunaenda kushinda huu mchezo"


"Kutokana na uzoefu wa baadhi yetu ndani ya kikosi tunahimizana jinsi ya kuiwezesha timu iweze kufikia malengo,  tumewatazama wapinzani wetu na tumejua uimara wao na madhaifu yao hivyo tupo tayari." Amesema na kuongeza kuwa.


"Kwa kutambua umuhimu wa mashabiki wetu nawaomba sana wajitokeze kwa wingi waujaze uwanja na kushangilia muda wote wa mchezo na kazi ya matokeo watuachie sisi tutawapatia"


"Natambua tuna mashabiki bora hivyo waje waonyeshe ubora wao katika mchezo mkubwa ambao wao ni muhimu kuwepo" amesema Bigirimana.


Mwisho wa mchezo na kazi ya matokeo watuachie sisi tutawapatia"


"Natambua tuna mashabiki bora hivyo waje waonyeshe ubora wao katika mchezo mkubwa ambao wao ni muhimu kuwepo" amesema Bigir 21imana.

JK AONESHA PICHA ZA WAZAZI WAKE

$
0
0

 

 

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akionesha picha ya Baba yake Mzazi  Mzee Kikwete Mrisho Kikwete a.k.a Khalfani Mrisho Kikwete.


 
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akionesha picha ya Babu yake Mzaa baba  Chifu Mrisho Kikwete.


 

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akionesha picha ya mama yake mzazi.


 

Na Issa Michuzi

 

Akiwa katika mahojiano katika kipindi maalumu cha kuadhimisha miaka 72 ya kuzaliwa cha  JK72 na watangazaji wa Clouds FM na Clouds TV, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mkewe Mbunge wa Mchinga Mhe. Mama Salma Kikwete alitumia wasaa huo kuonesha picha za wazazi wake, ikiwa ni pamoja na za Babu yake mzaa baba, Baba Mzazi na Mama Mzazi.

 

Katika mahojiano hayo yaliyofanyika kijijini Msoga IJUMAA OKTOBA 7, 2022 Dkt. Kikwete alisimulia kwamba Babu yake Mzee Mrisho Kikwete alikuwa Chifu wa Wakwere na kwamba baba yake mzazi Mzee Kikwete Mrisho Kikwete au kwa jina lingine Khalfani Mrisho Kikwete alikuwa Mkuu wa Wilaya PanganiSame na Tanga katika vipindi tofauti tofauti. Alisimulia kwamba  wakati mama yake alipokuwa mja mzito naye, babu alitamka kuwa ikiwa mtoto atakuwa wa kiume atampatia urithi wa cheo chake, cha Uchifu.

 

Historia fupi ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni kwamba alizaliwa tarehe 7 Oktoba mwaka 1950 katika kijiji cha Msoga, mkoa wa Pwani, akiwa mtoto wa sita katika familia ya watoto tisa. Alimuoa mama Salma Kikwete mwaka 1989 na wamebarikiwa watoto nane.


Alipata elimu ya msingi na ya kati katika shule za Msoga na St. John Bosco Lugoba kati ya mwaka 1958 na 1965. Aidha, alipata elimu ya sekondari katika shule za sekondari za Kibaha (1966 – 1969) na Tanga (1970 – 1971). Alihitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1975 na kupata Shahada ya Uchumi, 

Mwaka 1976 alijiunga na Chuo Kikuu cha Maofisa wa Jeshi Monduli na kutunukiwa Cheo cha Luteni Kanali na baadaye kuwa Mkufunzi Mkuu na Kamisaa wa Siasa katika chuo hicho. Mheshimiwa Kikwete amefanya kazi katika Chama cha Mapinduzi kwa nyadhifa mbalimbali kwenye mikoa ya Singida na Tabora na  wilaya za Nachingwea na Masasi.

 

Mwaka 1988 aliteuliwa kuwa Mbunge na Naibu Waziri wa Nishati na Madini. Mwaka 1990 alichaguliwa kuwa mbunge wa  Jimbo la Bagamoyo na akateuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini. Nyadhifa nyingine alizoshika ni Waziri wa Fedha mwaka 1994 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuanzia mwaka 1995 hadi 2005.

 

Alishika rasmi wadhifa wa urais mwaka  2005 na kuchaguliwa tena 2010 kwa muhula mwingine wa  miaka mitano.

 

Mengine, kama wanavyosema, ni historia. 

 

Katika kumalizia mahojiano hayo Dkt. Kikwete alibainisha kwamba yuko katika hatua za mwisho mwisho kukamilisha kuandika kitabu cha maisha yake ambacho amesema kitakuwa na kila kitu kinachomhusu.



TANZANIA COMMERCIAL BANK YAJIVUNIA KUSHEREHEKEA HUDUMA BORA

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi akimlisha keki Mteja wa Benki hiyo Bi Janemary Rutahoile ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea katika Tawi la Tanzania Commecial Bank lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu na utawala wa benki ya TCB Diana Myonga, Mkurugenzi wa Teknohama na Uendeshaji wa benki hiyo Jema Msuya na kushoto ni Meneja wa TCB Tawi la Mlimani City Happy Ernest.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi akimlisha keki Mteja wa Benki hiyo Bi Anna Philemoni ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea katika Tawi la Tanzania Commecial Bank lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu na utawala wa benki ya TCB Diana Myonga. Kushoto ni Meneja wa Tanzania Commercial Bank Tawi la Mlimani City Happy Ernest.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi akimlisha keki Mteja wa Benki hiyo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea katika Tawi la Tanzania Commecial Bank lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu na utawala wa benki ya TCB Diana Myonga pamoja na wateja wa wa benki hiyoAfisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi akimlisha keki Mteja wa Benki Deodarus Nkeyera ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea katika Tawi la Tanzania Commecial Bank lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu na utawala wa benki ya TCB Diana Myonga na Kushoto ni Meneja wa Tanzania Commercial Bank Tawi la Mlimani City Happy Ernest.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi akimlisha keki Mteja wa Benki hiyo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea katika Tawi la Tanzania Commecial Bank lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu na utawala wa benki ya TCB Diana Myonga.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa benki hiyo.

Tanzania Commercial Bank (TCB)  imewahakikishia wateja wake kuwa inabuni mipango madhubuti ya kuzindua bidhaa mpya zinazoendana na mahitaji ya watumiaji wa huduma za kibenki kote nchini.

Akizungumza na wateja wake waalikwa wakati wa wiki ya Huduma kwa Wateja inayoendelea katika Tawi la Tanzania Commercial Bank lililopo Mlimani city jijini Dar es Salaam leo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi,  alisema  wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanatoa huduma bora na yenye kumdhamini mteja.

"Thamani yetu kuu iko katika uhakika kwamba tunamjali  na kuvutiwa na mteja, tunataka kuwahakikishia wateja wetu wapendwa kuwa tumejitolea kufanya uzoefu wako wa kibenki kuwa wa kufurahisha zaidi," alisema.

 

Anna Philemon, mteja wa Tanzania Commercial Bank alisema Benki ya TCB imeweka huduma zake na bidhaa ziko mikononi mwa mteja, na hivyo kuwasaidia wateja kufanya miamala kwa njia rahisi zaidi.

 

Anna alitoa wito kwa Watanzania kutoka nyanja mbalimbali kujiunga na Tanzania Commercial Bank na kufurahia baadhi ya huduma bora na bidhaa za kipekee zinazotolewa na benki hiyo.


Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>