Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

TET YAKABIDHI NAKALA 4400 ZA VITABU KWA TAASISI YA MWANAMKE INITIATIVE NA NAKALA 31,100 KWA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI

$
0
0




Na Mwandishi Wetu

SERIKALI kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) leo tarehe 1/10/2022 imekabidhi jumla ya nakala 4,400 za vitabu vya kidato cha Kwanza hadi cha Nne kwa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Mwanamke Intiative Foundation (MIF) na nakala 31, 100 za vitabu vya kidato cha Tano na Sita kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.

Katika halfa hiyo ya makibidhiano iliyofanyika katika Skuli ya Dkt. Hasnuu Makame iliyopo Mkoa wa Kusini Unguja, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Leila Mohamed Mussa  amewaasa Walimu na Wanafunzi wavitumie vyema vitabu hivyo katika kupata Elimu bora.

"Hakuna Elimu ya kuhadidhiwa, Elimu inapatikana kwa katika vitabu hivyo mkavitumie na kuvitunza  vitabu hivi ili mpate elimu bora kwa Taifa" Amesema Mhe.Leila.

Pia amewataka wazazi na wanafunzi kutumia simu zao kuingia katika aktaba mtandao ya TET kuweza kujipatia machapisho mbalimbali kwani maktaba hiyo ni bure.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa TET Dkt.Aneth Komba amesema TET imetoa jumla ya nakala 4400  za vitabu zenye thamani ya shilingi Ml.51 laki 3.5  kwa MIF kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha kwanza hadi cha nne  na nakala 31,100 za vitabu vya kidato cha 5 na 6 zenye thamani ya shilingi Ml 329 kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.

Dkt.Komba ameishukuru MIF kwa kuja na wazo la kutokomeza zero Unguja na kusema kuwa ni wazi wazo hili linapaswa kuwa Tanzania nzima kwani bado shule nyingi hazifanyi vizuri.

Aidha amesema ,licha na kukabidhi nakala ngumu, wanafunzi na walimu bado wana fursa ya kusoma machapisho mbalimbali katika Maktaba mtandao ya TET.

Aidha amesema, TET ipo tayari kutoa mafunzo kwa walimu wa Mkoa wa Unguja  ili waweze kupata ujuzi wa kumuandaa mhitimu aweze kujiajiri au kuajiriwa.

Naye Mwenyekiti wa MIF Mhe.Wanu Hafidhi Amiri ameishukuru TET kwa kukabidhi vitabu ambavyo vitasambazwa katika skuli 33 za Mkoa wa Unguja kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

Mhe.Wanu amesema MIF ilifanya tafiti mbalimbali ili kubaini changamoto zinazosababisha wanafunzi wa Mkoa wa Kusini Unguja kufeli, moja ya changamoto ni uhaba wa vitabu vya kujifunzia kwa wanafunzi hivyo MIF ilichukua jukumu la kuomba TET kuwapatia vitabu vya kiada kwa shule za sekondari ambavyo vitasaidia kupunguza sifuri (zero) kwa wanafunzi hao.

Ameeleza  kuwa malengo ya MIF ni  kusaidia wanafunzi wa Zanzibar  kufaulu kidato cha Nne na kuiindoa Zanzibar katika shule 10 za mwisho Kitaifa katika matokeo ya kidato cha Nne.


TEMBO WORRIES KAZI INAENDELEA UTURUKI

$
0
0



Na John Marwa


Timu ya Taifa ya Soka kwa watu wenye ulemavu Tembo Worries leo itashuka tena dimbani katika mchezo wa pili hatua ya makundi Fainali za Kombe la Dunia zinazofanyika nchini Uturuki.

Ni mchezo wa pili kwa Tembo Worries leo dhidi ya Poland baada ya jana kutoka suluhu dhidi ya Hispania.

Tembo Worries wanahitaji kupata ushindi leo ili kuiweka hai nafasi ya kusonga mbele kabla ya mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi hapo kesho.

Kama Tembo leo wataibuka na ushindi watafikisha alama nne huku wakisaliwa na mchezo mmoja mkononi hapo kesho dhidi ya Uzbekistan.

Ikumbukwe kuwa hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuwashiriki Fainali hizo za Kombe la Dunia kwa watu wenye ulemavu.


NGOMA IMELIA, MVINYO UMENYWEKA LUPASO

$
0
0

 


Na John Marwa

HATIMAYE ngoma imelia na mvinyo umenywekwa ndani ya Dimba la Benjamin Mkapa kwa Dodoma Jiji kukubali kipigo cha mabao (3-0) kutoka kwa Simba SC.

Ulikuwa mchezo mgumu kwa walima zabibu wa Dodoma Jiji mapena tu kupitia kwa mlinzi wake Abdallah Shaibu Ninja kujifunga baada ya krosi iliyomiminwa na Clatous Chama.

Bao hilo ni kama lilizima mpango wa Simba SC waliokuja nao katika mtanange wa leo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara NPL wa kusaka ushindi na kuendeleza mdundo wa kutopoteza mchezo .

Kipindi cha pili kilikuwa kigumu zaidi kwa vijana wa Masoud Djuma kwani kila gia waliojaribu kuingiza ni kama swichi kwa wanajeshi wa Juma Mgunda kuendeleza maangamizi.

Dodoma Jiji walikuwa bora katika kujilinda nankaunzisha mashambulizi katika mfumo wa 3:5:2 lakini ubora wa Simba eneo la katikati lilikuwa katika kuziba nafasi na kufungua nafasi ulikuwa unawafanya Dodoma Jiji kuacha mianya pale walipokuwa wanapoteza mpira.

The General Moses Phiri aliendeleza wimbi lake la kufumania nyavu kwa kaundika Bao la nne msimu huu katika michezo mitano aliyoshuka Dimbani.

Super Sub Habib Kyombo aliandikia Simba bao la tatu na la ushindi akimalizia krosi mujarabu kutoka kwa Mohamed Hussein.

Ushindi huo unaifanya Simba kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi kwa kufikisha point 13 na mabao 11 ya kufunga, clean sheets 4 huku wakiwa wameruhusu mabao 2 kwenye mchezo mmoja dhidi ya KMC FC.

Ligi hiyo itaendelea kesho kwa Mabingwa watetezi kushuka dimbani kuwakabili Ruvu Shooting. Azam FC wao watawakalibisha Singida Big Stars.

TCU yaongeza muda wa udahili wa Shahada ya Kwanza katika Taasisi za Elimu ya Juu nchini kwa program ambazo bado zina nafasi kwa mwaka wa masomo 2022/2023

$
0
0


TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imeongeza muda wa udahili wa shahada ya kwanza katika taasisi za elimu ya juu nchini kwa programu ambazo zina nafasi kwa mwaka wa masomo 2022/2023.


Akizungumza na waaandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa Uratibu na Udahili wa tume hiyo, Dk. Kokuberwa Katunzi-Mollel amesema kuwa katika awamu zote tatu kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza katika Taasisi za Elimu ya Juu nchini kwa mwaka wa masomo 2022/2023 umekamilika kwa mujibu wa ratiba ya udahili. 


Majina ya waliodahiliwa katika Awamu ya Tatu yanatangazwa na vyuo husika. 2.0 WAOMBAJI WALIODAHILIWA KATIKA CHUO ZAIDI YA KIMOJA Waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja katika Awamu ya Tatu na wale ambao hawakuweza kuthibitisha udahili katika awamu zilizopita wanahimizwa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimojawapo kuanzia leo tarehe 03 hadi 24 Oktoba, 2022 kwa kutumia namba maalum ya siri iliyotumwa kwa ujumbe mfupi kupitia namba zao za simu au barua pepe walizotumia wakati wa kuomba udahili. Wale ambao hawatapata kwa wakati ujumbe huo, wanashauriwa kuingia kwenye mifumo ya udahili ya vyuo walivyodahiliwa na kuomba kutumiwa ujumbe mfupi wenye namba maalum ya siri ili kuweza kujithibitisha katika chuo husika. Uthibitisho wa udahili unafanyika kupitia akaunti ambayo muombaji alitumia wakati wa kuomba udahili. 


Orodha ya majina ya waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja imewekwa kwenye tovuti ya TCU (www.tcu.go.tz). 3.0 KUFUNGULIWA KWA AWAMU YA NNE YA UDAHILI Baada ya kukamilika kwa awamu zote tatu za udahili, Tume imepokea maombi ya kuomba kuongezwa muda wa kutuma maombi ya udahili kutoka kwa baadhi ya waombaji ambao hawakufanikiwa kupata udahili katika awamu zilizopita na pia vyuo ambavyo bado vina nafasi vimeomba vipewe muda kuendelea kudahili. Hivyo, Tume imeongeza muda wa udahili kwa kufungua Awamu ya Nne na ya mwisho ya udahili inayoanza leo tarehe 03 hadi 07 Oktoba, 2022. Tume inasisitiza kuwa waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi ya udahili au hawakufanikiwa kudahiliwa katika 2 Jengo la Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, S.L.P 6562, 7 Mtaa wa Magogoni, 11479 Dar es Salaam, Simu: +255 22 2113694, 2113691, Nukushi: +255 2113692, Barua Pepe: es@tcu.go.tz, Tovuti: www.tcu.go.tz awamu zilizopita kutokana na sababu mbalimbali, watumie fursa hii vizuri kwa kutuma kwa usahihi maombi yao ya udahili kwenye vyuo wanavyovipenda. Tume inaelekeza Taasisi zote za Elimu ya Juu nchini zinazofanya udahili wa Shahada ya Kwanza kuendelea kutangaza programu ambazo bado zina nafasi. 


Aidha TCU imetoa utaratibu wa udahili katika awamu ya Nne ambapo waombaji wa udahili na vyuo wanahimizwa kuzingatia utaratibu wa udahili kwa Awamu ya Nne kama ilivyoainishwa katika Jedwali namba moja, Utaratibu wa udahili katika Awamu ya Nne kwa mwaka wa masomo 2022/2023, ambapo Oktoba 3 hadi 07, 2022 Kutuma maombi ya udahili katika Awamu ya Nne, Oktoba 11-12, 2022 Vyuo kuwasilisha Tume majina ya waliodahiliwa katika Awamu ya Nne na Oktoba 15, 2022 Vyuo kutangaza majina ya waliodahiliwa katika Awamu ya Nne. Oktoba 15 hadi 24, 2022 Kuthibitisha udahili kwa waliodahiliwa zaidi ya chuo kimoja katika Awamu ya Nne na wale walioshindwa kuthibitisha udahili wao katika awamu za udahili zilizopita.


Tume hiyo imetoa wito kwa waombaji wa udahili udahili wa Shahada ya Kwanza kuwa masuala yote yanayohusu udahili au kujithibitisha katika chuo kimoja yawasilishwe moja kwa moja kwenye vyuo husika. Kwa wale ambao watapata changamoto katika kujithibitisha, vyuo vyote vimeelekezwa kupokea taarifa zao na kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo na taratibu.

TCU inawaasa wananchi kuepuka kupotoshwa na watu wanaojiita mawakala au washauri wanaodai wanatoa huduma ya jinsi ya kujiunga na vyuo vya Elimu ya Juu hapa nchin


CRDB yazindua rasmi Wiki ya Huduma kwa Wateja Dar, wateja wafurahia huduma zake

$
0
0

Mkuu wa Wilya ya Kinondoni (wa pili kulia) akikabidhi zawadi  mmoja wa wateja wa benki ya CRDB, Dk. Redempta Mbatia (kushoto) wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi wa wiki ya huduma kwa wateja yenye kauli mbiu 'Sherehe Huduma'  iliyofanyika leo katika Tawi la Ostabey Masaki jijini Dar es Salaam (wa pili kushoto ni Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo na kulia ni Mkuu wa Kitengo Cha Huduma kwa Wateja wa benki ya CRDB, Yolanda Uriyo.

 
Benki ya CRDB imenza wiki hiyo kwa kuwashukru wateja wake kwa maoni na ushauri ambao umeiwezesha benki hiyo kutoa huduma Bora na zenye viwango vya kimataifa kwa jamii
 

Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo, akizungumza na wateja wa benki hiyo katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika Tawi la Oyster bay Masaki jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo Cha Huduma kwa Wateja wa benki ya CRDB, Yolanda Uriyo, na wateja wa Benki ya CRDB wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja.



 

Mamlaka ya Masoko Ya Mitaji na Dhamana (CMSA), imezindua wiki ya uwekezaji duniani.

$
0
0

 


NA MWANDISHI WETU

Mamlaka ya Masoko Ya Mitaji na Dhamana (CMSA), imezindua wiki ya uwekezaji duniani.

CMSA kwa kushirikia na Taasisi ya Kimataifa inayohusika na Usimamizi na watoaji wa viwango vya Kimataifa vya masoko ya mitaji ulimwenguni  (IOSCO) inashiriki katika kuadhimisha wiki ya wawekezaji ulimwenguni iliyoanza Oktoba 3 mpaka Oktoba 7, 2022.

Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, CPA, Nicodemus Mkama, katika taarifa yake amesema lengo la kushiriki Wiki ya Wawekezaji Duniani ni kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa elimu kwa umma na ulinzi wa maslahi ya wawekezaji kwa kuangazia jitihada mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka za usimamizi wa masoko ya mitaji katika maeneo haya muhimu.

"Wiki ya Wawekezaji Ulimwenguni inahusisha Mamlaka za usimamizi wa masoko ya mitaji ambazo ziko chini ya IOSCO pamoja na wanachama wengine wa IOSCO katika mabara sita ambazo hufanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa njia za mawasiliano na huduma zinazomlenga mteja, kukuza ushindani wenye tija unaolenga kuongeza wigo wa mikakati mbalimbali ya utoaji wa elimu ya wawekezaji,"amesema.

Pia wataandaa warsha na makongamano, pamoja na kutumia Mamlaka zao kuendesha kampeni za kitaifa. 

Mkama amesema Wiki ya wawekezaji inatoa nafasi ya upendeleo maalumu kwa wanachama wa IOSCO kufanya kazi kwa kushirikiana na wadau wote wanaotoa elimu ya uwekezaji kwa umma kwa ngazi ya kitaifa, kikanda na kimataifa.

 Kauli mbiu ya mwaka huu ni uhimilivu wa wawekezaji na Mitaji Endelevu.

Mkama amesema Wiki ya Wawekezaji Ulimwenguni inatarajiwa kuongeza uelewa wa fursa na faida za kutumia masoko ya mitaji nchini ambao unalenga “ Kutambua Ushindani na Maendeleo ya Viwanda kwa Maendeleo ya Watu”. 

Pia inalenga kuongeza ushiriki wa wawekezaji katika masoko ya mitaji hivyo kuwezesha utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha na Mpango Mkuu wa Taifa wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha.
Aidha amesema wiki ya Wawekezaji Ulimwenguni imeambatana na maono ya Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi uliotukuka wa Rais Samia Suluhu Hassan, ambao unalenga kuweka mazingira wezeshi kwa maendeleo ya sekta ya fedha kwa kuchochea maendeleo na ukuaji wa uchumi Nchini.

Katika kuadhimisha wiki hii, CMSA itafanya shughuli mbalimbali zinazolenga kuongeza uelewa, upatikanaji, ushiriki na kulinda maslahi ya mwekezaji katika masoko ya mitaji kuanzia tarehe 3 mpaka 7 Oktoba 2022. 

Programu hii inalenga kuimarisha uelewa kuhusu masoko ya mitaji hivyo kuchangia kwenye ajenda ya Taifa ya kuboresha Huduma Jumuishi za kifedha na maendeleo ya uchumi.
Mwisho

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KUFUNGUA MKUTANO WA 65 WA UNWTO

$
0
0

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Mkutano wa 65 wa Shirika la Utalii Duniani Kamisheni ya Afrika (65th UNWTO-CAF Meeting) utakaoanza tarehe 5 Oktoba 2022 katika ukumbi wa Hoteli ya Gran Melia jijini Arusha. Kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John Mongela.

Baadhi ya watumishi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na wadau wa utalii wakifuatilia taarifa wakati wa mkutano wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb)  (hayupo pichani) na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Arusha.

Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Wizara ya Maliasili na Utalii, Lucy Saleko, Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Maurus Msuha na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Prisca Lwangili wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb)(hayupo pichani) wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Arusha.

 

Na Mwandishi Wetu

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa 65 wa Shirika la Utalii Duniani Kamisheni ya Afrika (65th UNWTO-CAF Meeting) utakaoanza tarehe 5 Oktoba 2022 katika ukumbi wa Hoteli ya Gran Melia jijini Arusha.

 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Arusha.

 

Amefafanua kuwa lengo la mkutano huo ni kujadili kuhusu mustakabali wa ustawi wa maendeleo ya sekta ya utalii barani Afrika hasa baada ya athari za mlipuko wa janga la UVIKO-19 iliyokuwa imeathiri utalii wa kimataifa kwa wastani wa kati ya asilimia 50 hadi 85 katika nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania.

 

Aidha, amesema mkutano huo ni muhimu kwa kuwa ni mojawapo ya jitihada za Serikali katika kuongeza idadi ya watalii na kutanua wigo wa mazao ya utalii nchini kupitia uendelezaji wa mazao ya utalii ya kimkakati hususan Utalii wa Mikutano na Matukio.

 

Vilevile, ameweka bayana kuwa mkutano huo utawezesha kujengea uwezo wataalam na wadau wa utalii katika kutangaza utalii, kuendeleza na kufungamanisha mazao ya utalii katika kanda mbalimbali za utalii nchini kulingana na shabaha ya kuongeza idadi ya watalii kufikia watalii milioni 5 na mapato ya Dola za Marekani Bilioni 6 ifikapo mwaka 2025.

 

“Mkutano huo ni nyenzo mojawapo ya kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais katika kutangaza utalii ndani na nje ya nchi kupitia programu ya Tanzania - The Royal Tour” Mhe. Balozi Chana amesema.

 

Mkutano huo wenye Kauli Mbiu ya “Kuujenga upya Utalii Stahimilivu wa Afrika kwa Maendeleo Jumuishi ya Kiuchumi na Kijamii” utahudhuriwa na Katibu Mkuu wa Shirika hilo Bw. Zurab Pololikashvili na kukutanisha mawaziri wenye dhamana ya masuala ya utalii na maliasili kutoka nchi wanachama wa UNWTO wa Kanda ya Afrika zaidi ya 50 na wadau wengine wakiwemo wataalam wa utalii na ukarimu katika ngazi ya kimataifa na kikanda, watoa huduma mbalimbali katika mnyororo wa utalii, wawekezaji, pamoja na watu mashuhuri zaidi ya 150.

 

NEC YAWABURUZA BUNGE MICHEZO YA SHIMIWI

$
0
0

 

Timu ya Kamba wanaume ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kiwavuta Timu ya Kamba ya Bunge (hawapo pichani) wakati wa Michuano Shirikisho la Michezo ya Wiraza na Idara za Serikali na Mikoa (SHIMIWI) inayoendelea jijini Tanga. Timu ya Uchaguzi ilishinda mchezo huo kwa mivuto yote miliwi. (Picha na Mroki Mroki).


MICHUANO Shirikisho la Michezo ya Wiraza na Idara za Serikali na Mikoa (SHIMIWI) imezidia kurindima katika viunga vya jiji la Tanga ambapo Timu za Kamba za Tume ya Taifa ya Uchaguzi zimeendeleza ubabe wao kwa timu za kundi E wanaume na kundi F Wanawake.

 

Katika michezo ya leo Oktoba 4,2022 timy ta Kamba ya Uchaguzi wanaume wamewahenyesha na kuchukua lama tatu kutoka kwa Mhimili wa Bunge.

 

Mchezo huo ambao awali ulikua unaonekana kuwa mgumu kwa pande zote mbili kutokana na aina ya wachezaji waliopo lakini ulikuwa mwepesi kwa miamba ya Uchaguzi.

 

Katika mchezo mwingi Timu ya wanawake wa Uchaguzi ilipata alama tatu za mezani kufuatia wapinzani wao RAS Ruvuma kuingia mitini katika mchezo wa kundi F.

 

Baada ya matokeo hayo sasa Timu ya Wanawake wa Uchaguzi imebakiza mchezo dhidi ya Wizara ya Madini ambapo wanaume wanasubiri kukutana na RAS Shinyanga.

 

Kundi la Kamba wanaume lina timu za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika Mashariki, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, RAS Shinganga na RAS Manyara.

 

Upande wa Kundi F timu ya Kamba wanawake kuna timu za Tume ya Taifa ya Uchaguzi, RAS Dodoma, RAS Ruvuma na Wizara ya Madini.


Sinach kuongoza jukwaa Festival of Praise

$
0
0

 



Na Mwandishi Wetu

 

MWIMBAJI mahiri wa nyimbo za Injili nchini Nigeria, Sinach Joseph Egbu anatarajia kuongoza jukwaa la Festival of Praise linalotarajia kufanyika Oktoba 16 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza jijini Dar es Salaam muandaaji wa tamasha hilo, mwimbaji maarufu hapa nchini, John Lissu alisema umahiri wa Sinach utafanikisha ujumbe wa neno la Mungu kuwafikia watanzania wote kupitia tungo zake na waimbaji wengine wa hapa nchini.

 

Lissu alisema Sinach atapanda jukwaani na wimbo wake uliokamata anga la muziki wa Injili duniani wa ‘Way Maker’ uliotazamwa na mashabiki zaidi ya milioni 200.

 

Lissu alisema waimbaji wa hapa nchini watakaomsindikiza mwimbaji huyo ni pamoja Nay Eye, Christina Shusho, Ambwene Mwasongwe, Pasta EPA, Kwaya ya Kanisa la Moravian, Ruach Worship Team (Kenya) na Kwaya ya Gospel Winners.

 

Aidha Lissu alitoa wito kwa waamini wa muziki wa Injili kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo ambalo ni mojawapo ya matukio muhimu ya kusifu na kuabudu yanayofanyika hapa nchini.

Marafiki Festival siku nne Dar, Bagamoyo

$
0
0


 


SIMU wa tatu wa Tamasha kubwa la Marafiki Music Festival umewadia ambapo kivumbi kizito cha burudani kinatazamiwa kuanza kutimka Alhamisi hii ndani ya Kijiji cha Makumbusho, Dar es Salaam kwa mtonyo mdogo wa buku 15 tu.

Bosi wa Kampuni ya Asedeva ambao ndio waandaaji, Isack Abeneko, amesema bendi 20 pamoja na zaidi ya wasanii 128 kutoka mataifa mbalimbali Afrika, wakiwamo Man Fongo na Balaa MC kwa hapa nchini, wanatarajiwa kupamba shughuli hiyo.


"Tamasha la mwaka huu litakuwa ni la siku nne ambapo kuanzia Oktoba 6 hadi 8, litarindima hapa Dar es Salaam kabla ya Oktoba 9 kufunga dimba kwenye ukumbi wa Firefly, Bagamoyo, Pwani," amesema Abeneko na kuongeza:

"Viingilio kwenye shughuli hiyo vitakuwa ni sh 15,000 kwa watu wazima na 5,000 kwa wanafunzi watakaokuwa na vitambulisho vya shule, lakini pia tiketi za awali tayari zimeshaanza kuuzwa kwa bei ya sh 20,000 kwa shoo zote nne na 10,000 kwa tukio moja."

NMB Mlimani City washerehekia Wiki ya Huduma kwa Wateja

$
0
0

Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Rehema Madenge, akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika Tawi la Benki ya NMB Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Rehema Madenge, akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika Tawi la Benki ya NMB Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Meneja wa NMB Tawi la Mlimani City, Deogratius Kawonga, akizungumza na wateja wa benki hiyo wakati wa hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika Tawi la Benki ya NMB Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, akizunguza na wateja wa benki hiyo hiyo wakati wa hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika Tawi la Benki ya NMB Mlimani City jijini Dar es Salaam. 

Mkuu waHuduma kwa Wateja Benki ya NMB, Abela Tarimo, akizungumza wakati hiyo wakati wa hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika Tawi la Benki ya NMB Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Rehema Madenge (katikati) akikata keki wakati wa hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika Tawi la Benki ya NMB Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard na kulia ni Mkuu waHuduma kwa Wateja Benki ya NMB, Abela Tarimo.

Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Rehema Madenge (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa benki ya NMB.


RIPOTI: DAR ES SALAAM INAWEZA KUPUNGUZA UZALISHAJI WA HEWA CHAFU KUTOKA KATIKA SEKTA YA TAKA KWA ASILIMIA 65 KUPITIA MIKAKATI YA TAKA SIFURI

$
0
0

.Sekta ya uzimamizi wa taka sifuri inaweza kutengeneza ajira zaidi ya kazi 18,000 jijini

.Ulimwenguni, usimamizi bora wa taka unaweza kupunguza uzalishaji wa jumla kwa asilimia 84 (tani bilioni 1.4) na kupunguza kwa kiasi kikubwa uzalishaji katika sekta zingine.

.Eyes on Africa kama mwenyeji wa COP27 Misri inapanga kuzindua Mpango wa 50 kwa 2050. 

 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nipe Fagio, Ana le Rocha, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu kuanzishwa kwa mfumo wa Taka Sifuri katika miji yote ulimwenguni ikiwa ni njia za haraka na nafuu zaidi za kupunguza joto duniani.

 

NA MWANDISHI WETU

 

Kuanzishwa kwa mfumo wa Taka Sifuri katika miji yote ulimwenguni utakuwa mojawapo ya njia za haraka na nafuu zaidi za kupunguza joto duniani na kufikia chini ya nyuzi 1.5° ya ongezeko la joto, kulingana na ripoti mpya iliyotolewa na Global Alliance for Incinerator Alternatives (GAIA).
Ripoti iligundua kuwa kupitia mikakati taka sifuri, ifikapo mwaka 2030 Dar es Salaam, Tanzania inaweza kufikia upunguzaji wa gesi chafuzi kwa asilimia 65 kutoka katika sekta ya taka.


Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lenye makao yake makuu nchini Tanzania, Nipe Fagio, Ana le Rocha alisema, "Taka sifuri jijini Dar es Salaam inatoa fursa ya kukabiliana na tofauti za kihistoria za kijamii, zilizowazi kwamba jamii nyingi za kipato cha chini katika jiji hilo hazina huduma za usimamizi wa taka. mapambano na athari za kiafya na kiuchumi za uchafuzi utokanao na taka. 

 

Kupitia njia ya taka sifuri, makundi yaliyo katika mazingira hatarishi- kama vile wanawake, vijana, wakusanya taka wasio rasmi na wenyeji i- yanajumuishwa katika utatuzi wa changamoto ya usimamizi wa taka, na kuleta mabadiliko chanya ya kimfumo katika sekta ya taka ambayo yatajenga msingi wa jiji linastohimili hali ya hewa na lenye usawa."


Haya yanajiri wakati Misri ikijiandaa kuwa mwenyeji wa Kongamano la Umoja wa Mataifa la Mabadiliko ya Tabianchi (COP 27) la 2022 mwezi Novemba, ambapo taka itakuwa mojawapo ya ajenda kuu za hali ya hewa kwa bara la Afrika–Misri inapanga kuweka mbele Mpango wa 50 kwa 2050, unaolenga kutibu na kuchakata asilimia 50 ya taka zinazozalishwa barani Afrika ifikapo 2050, juhudi ambazo hazijawahi kufanywa na zenye matarajio makubwa.


“Katika ngazi ya kimfumo, Afŕika ina uwezo mkubwa wa kupiga hatua kuelekea ulimwengu usio na taka kutokana na asilimia kubwa ya viumbe hai, sheŕia inayoendelea juu ya plastiki na kuwepo kwa waokota taka katika miji barani kote. 

 

Kwa sababu zinazowezesha, kama vile uchambuzi wa taka kwenye vyanzo, usimamizi tofauti wa taka hozo, ujumuishaji wa waokota taka na utekelezaji bora wa sheria zilizopo za plastiki, Afrika inaweza kuwa eneo ambalo linaonyesha utekelezaji mzuri wa mifumo ya Taka Sifur," alisema Niven Reddy. Mratibu wa Kanda ya Afrika wa GAIA.


Ripoti ya GAIA ilitoa mfano wa upunguzaji wa hewa chafu kutoka kwa miji minane kote ulimwenguni. Waligundua kuwa kwa wastani, miji hii inaweza kupunguza uzalishaji wa hewa chafu katika sekta ya taka kwa asilimia 84 kwa kuanzisha sera bora za usimamizi wa taka kama vile kutenganisha taka, kuchakata tena,na kutengeneza mboji, kupunguza uzalishaji wa jumla kutoka kwa sekta ya taka kwa zaidi ya tani bilioni 1.4, sawa na uzalishaji wa kila mwaka wa magari milioni 300.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nipe Fagio, Ana le Rocha, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu kuanzishwa kwa mfumo wa Taka Sifuri katika miji yote ulimwenguni ikiwa ni njia za haraka na nafuu zaidi za kupunguza joto duniani. Kulia ni Ofisa Mawasiliano Nipe Fagio, Olary Tomito. (NA MPIGA PICHA WETU).

Miradi ya Maji Zanzbar kukabidhiwa Disemba

$
0
0

Na Salma Lusangi

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Nishati na Madini Mwanajuma Majid Abdullah amesema Wizara yake inatarajia kukabidhiwa miradi ya maji ifikapo Disemba mwaka huu, hivyo amewaomba wananchi wawe na subra kwani miradi hiyo imefikia asilimia 80 ya utekelezaji wake ikiwemo wa uchimbaji wa visima, ulazaji wa mabomba na ujenzi wa Matangi ya maji.

Akizungumza mara baada ya kushiriki ziara ya pamoja na kamati ya Ardhi, Mawasiliano na Nishati ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika maeneo mbali mbali ya miradi hiyo. Alisema anafahumu kwamba tatizo la maji halistahamiliki lakini amewaomba wananchi kuendelea kupokea huduma ya maji kwa mgao kwani sio muda mrefu tatizo la maji litamalizika Zanzibar.

Alisema tatizo la maji Zanzibar limetokana na uwepo wa visima vichache ambavyo vinatumika pamoja na uchakavu wa miondombinu ya maji lakini kupitia jitihada za Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Mwinyi za kuwaondolea shida ya maji wananchi wake. Wizara ya Maji inaendelea kusimamia ipasavyo miradi hiyo ambapo ifikapo Januari, 2023 maji yatapatikana katika maeneo mengi ya Unguja na Pemba.

“Tumepiga hatua, tunamshukuru Mhe. Rais wa Zanzibar Dkt Mwinyi, miradi ya maji inayotekelezwa kwa fedha za Uviko 19, na fedha za Exim Bank ya India itakabidhiwa kwa Serikali Desemba, nimejionea mwenyewe ZAWA imefanya kazi kubwa, hivyo tatizo la uhaba wa maji litatatuka muda sio mrefu, naomba wananchi wamuunge mkono Mhe Rais  kwa kustahamili kidogo tu” Alisema. Mwanajuma”

Naye Mkurugenzi Idara ya Huduma za Maji Mudrik Fadhil Abas alisema kukamilika kwa miradi hiyo kusaidia maeneo mbali mbali ya wananchi kupata maji  kwasababu matangi ya maji yaliyojengwa hayapungui 300 kwa Unguja na Pemba hivyo asilimia kubwa ya wananchi watapata maji. Pia alisema na kila tangi limeshapangiwa maeneo ya kupeleka maji.

Alifahamisha kwamba mabomba ya maji yaliyolazawa kutoka kwenye kila tangi  yanaupana wa nchi 12 hali ambayo itasaidia kufikisha maji kwa haraka katika maeneo yaliyokusudiwa ili wananchi waweze kuendelea na shughuli zao za kiuchumi na kijamii na kusahau kabisa tatizo la maji Zanzibar.

Kwa upande wake Kaimu wa kamati ya Ardhi, Mawasiliano na Nishati ya Baraza la wawakilishi Zanzibar Kombo Mwinyi alisema ameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maji, lakini amesisitiza kwamba miradi hiyo imalizwe kwa wakati unaotakiwa. Pia aliiagiza Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kuhakikisha kwamba wanawataalam wa wakutosha kwaajili ya kuendeleza usimamizi wa miradi hiyo.

Aidha alihoji changamoto ambazo zinaikabili (ZAWA) katika utekelezaji wa miradi hiyo kwa sababu hawapendi kusikia ifikikapo Mwezi Desemba miradi hiyo kuwa haijakamilika, kwani wananchi wamekabiliwa na tatizo la maji katika maeneo mengi ya Zanzibar.

Kwa Upande wake Mkurugunzi Mkuu ZAWA Mhandisi Dkt Salha Mohammed Kasim alisema changamoto ambazo zinamkabili ni uchelewaji wa vifaa kuingia nchini lakini changamoto kubwa inayomsumbua sana ni  ukosefu wa wataalamu hivyo ameiomba Serikali kuzingatia na kulifanyia kwani hata miradi ikikabidhiwa bado ZAWA inahitaji wataalamu kwasabau miradi inahitaji usimamizi wa hali ya juu.

Mwisho Mhandisi Dkt Salha aliihakikishie kamati hiyo kwamba ifikikao Desemba mwaka huu miradi ya maji itakabidhiwa, kutokana na hatua iliyofikiwa na juhudi zinazochukuliwa na taasisi yake.

Miradi ya Maji Zanzibar ikiwemo ujenzi wa matangi, ulazaji wa mabomba ,uchimbaji wa visima inatekelezwa kwa fedha za ahuweni Uviko 19 na  fedha za Exim Bank ya India na itawanufaisha wananchi wote wa Zanzibar.

 

KITUO CHA UTAFITI CHA NCHINI UJERUMANI (CRC) CHATUA MZUMBE

$
0
0

Mtafiti Kiongozi wa mradi wa "Future Rular Afrika"Prof. Detlef Müller-Mahn akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi Kuu Morogoro.

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William J. Mwegoha akiwakaribisha Watafiti hao waliotembelea Chuo Kikuu Mzumbe.

Watafiti wakimsikiliza Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, katika kikao cha utambulisho

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William J. Mwegoha (Kushoto) akimkabidhi zawadi Mtafiti Kiongozi wa mradi wa "Future Rular Afrika"

Watafiti wa Mradi wa "Future Rular Afrika" wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya  viongozi na watumishi wa Chuo Kikuu Mzumbe wanaotekeleza mradi huo.

Watafiti wa mradi wa "Future Rular Afrika" wa Kituo shirikishi cha Utafiti cha nchini Ujerumani (CRC) wakiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Chuo Kikuu Mzumbe na Wabia wanaotekeleza mradi huo Tanzania na Kenya.


Na Mwandishi Wetu


Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William J. Mwegoha, amepokea ujumbe kutoka kituo Shirikishi cha Utafiti (CRC) cha nchini Ujerumani,  wafadhili wa mradi wa ‘Future Rural Africa’ unaotekelezwa na Chuo Kikuu Mzumbe, kikiwa ni chuo pekee nchini kinachotekeleza mradi huo.

Akizungumza katika kikao maalumu cha utambulisho kilichofanyika leo , ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo, Kampasi Kuu Morogoro, Mtafiti Kiongozi wa mradi huo  Prof. Detlef Müller-Mahn,  amesema wanafurahia kufanya kazi na Chuo Kikuu Mzumbe, chini ya uratibu wa Dkt. Frank Theobald, ambapo mradi huo umefanikiwa kumaliza awamu ya kwanza, na kuanza utekelezaji wa  awamu pili ya miaka minne (2022 -  2026).

Akielezeka mradi huo, Prof. Detlef amesema, mradi huo umelenga kufanya utafiti wa “maendeleo vijijini na mabadiliko ya kiekolojia”, ambapo matokeo ya utafiti huo yatasaidia mabadiliko ya Sera, kuimarisha na kuboresha maisha ya jamii zinazoishi vijijini.  

Akiwakaribisha chuoni hapo, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Prof. William Mwegoha, amesema Chuo Kikuu Mzumbe kinatambua mchango mkubwa wa  mradi huo katika maendeleo ya Taifa na kwamba kipo tayari kuendelea kushirikiana na kituo hicho katika maeneo mengine ya utafiti hasa wakati huu ambao chuo kinajiimarisha zaidi na  kujenga uhusiano na Taasisi za kimataifa zinazojishughulisha na tafiti na masuala ya elimu ya juu.

Akitoa dira ya utekekelezaji,  wa mradi huo, Mratibu wa Mradi huo  Dkt. Frank Theobald, amesema awamu ya pili ya Mradi itahusisha utafiti katika mikoa ya Morogoro, Dar es Salaam, Njombe, Pwani, Iringa, Songwe, Dodoma na Mbeya na kwamba kwasasa timu ya watafiti iliyowasili inatembelea maeneo ya utafiti ili kazi hiyo kuanza.

Amesema zipo faida nyingi za mradi huo kwa Taifa, ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wanafunzi wa Shahada za Uzamivu na Umahiri watakahusika moja kwa moja na utafiti huo pamoja na kuwapatia wanataaluma fursa mbalimbali za kujiendeleza katika masuala ya Utafiti.

Mbali na Tanzania, nchi nyingine zinazotekeleza mradi huo barani Afika kwa ufadhili wa Kituo Shirikishi cha Utafiti (CRC) cha nchini Ujerumani ni  Kenya na Namibia.

TEMBO WORRIES KIBABE SANA HUKO UTURUKI

$
0
0



Na Mwandishi Wetu

TIMU ya Taifa Soka la Watu wenye ulemavu Tembo Worries imefuzu hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia, ni baada ya kuwachakaza Uzbekistan mabao (2-0).



Tembo Warriors, imefuzu kuingia 16 Bora ya Fainali za Dunia za Soka la Walemavu baada ya kumaliza ikiwa na pointi nne katika  kundi lake ikiwa ya tatu nyuma ya Poland na Uzbekistan.

Tembo Warriors imekata tiketi hiyo baada ya kuwa moja ya timu nne zilizoshika nafasi ya tatu zikiwa na uwiano mzuri (best looser) baada ya kuifunga Uzbekistan, kutoka sare na Hispania na kufungwa na Poland.

Sasa Tembo Warriors watacheza na Japan katika hatua hiyo mchezo utakao chezwa kesho Jumatano Oktoba 5, 2022, kusaka tiketi ya robo fainali.

Akizungumza katika chakula cha jioni kilichoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania hapa Istanbul, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohammed Mchengerwa amewataka vijana hao kuendelea kulishamirisha Taifa huku akizindua kampeni ya kuzifunga kila timu zinazokuja mbele yao iitwayo #LeteniMzungu.


KMC FC YAANZA MAANDALIZI MCHEZO DHIDI YA RUVU SHOOTING

$
0
0



Na Mwandishi Wetu

Kikosi cha Timu ya KMC FC kimerejea Jijini Dar es Salaam jana na leo kimeanza mazoezi kwa ajili ya mchezo unaofuata dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa siku ya Ijuma OKtoba 07 katika uwanja wa Uhuru hapa Jijini Dar es Salaam.

Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni chini ya kocha Mkuu , Thierry Hitimana ilirejea jana mapema alfajiri na hivyo kupumzika kabla ya leo kuanza maandalizi ya mchezo mwingine dhidi ya Ruvu Shooti ambapo KMC FC itakuwa nyumbani.

KMC FC inajiandaa na mchezo huo ambao ni wapili kuchezwa ikiwa nyumbani kati ya michezo mitano ambayo imeshacheza hadi sasa na kwamba jitihada kubwa na mikakati ni kuhakikisha kuwa licha ya Ligi kuwa naushindani mkubwa lakini kama Timu inajiandaa kuwapa burudani  itakayoambatana na matokeo mazuri kwenye mchezo huo.

Aidha kwa upande wa Afya za wachezaji wamerejea wakiwa na hari, morali nzuri isipokuwa Ibrahimu Ame pamoja na Hance Masoud ambao waliumia kwenye mchezo  dhidi ya Namungo uliopigwa siku ya Jumamosi ya Oktoba moja katika uwanja wa Majaliwa Ruangwa Mkoani Lindi.

“ Tumerejea jana alfajiri kutoka Ruangwa, ambapo tulikuwa kwenye mchezo dhidi ya Namungo, tumerudi salama, na tulipumzika na leo tumeanza maandalizi kwa ajili ya mchezo unaokuja dhidi ya Ruvu, tunafahamu ushindani wa mchezo huo namna ulivyo, lakini tutafanya maandalizi yetu vizuri kwakuwa malengo ni kupata alama tatu.

“Kwenye ligi hivi sasa unapo kwenda kukutana na mpinzani wako, kila mmoja anakuwa amejipanga vizuri, na hii nikutokana na ushindani uliopo, hivyo na sisi kama Timu ya KMC tunajiandaa vema, mchezo upondani ya uwezo wetu na siku zote Timu bora haiwezi kukosa alama tatu muhimu mara mbili, tumekosa dhidi ya Namungo na sasa tunajipanga dhidi ya Ruvu Shooting.

KMC FC hadi sasa ipo kwenye nafasi ya tisa ikiwa imecheza michezo mitano na kujikusanyia jumla ya alama sita na magoli sita ambapo michezo ambayo tayari imeshacheza ni dhidi ya Coast Union ya mkoani Tanga, Polisi Tanzania ya mkoani Kilimanjaro, Simba ya Jijini Dar es Salaam, Ihefu ya Mbarali mkoani Mbeya pamoja na Namungo ya Ruangwa mkoani Lindi.

YANGA, AZAM ZACHEKA KUELEKEA CAF

$
0
0

Kikosi cha Yanga.


Na John Marwa

Klabu za Yanga SC na Azam FC zimeangua vicheko kuelekea michezo yao ya hatua za awali Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL na Kombe la Shirikisho CAFCC.

Yanga wamecheka kwa kuwabugiza mabao (2-1) dhidi ya Ruvu Shooting mtanange uliopigwa Dimba la Benjamin Mkapa.

Licha ya ubora wa kikosi cha Charles Boniface Mkwasa 'Master' na upinzani walioutoa kwa Wananchi bado haukufua dafu na kukubali kichapo hicho kutoka kwa vichwa vya Feisal Salum na Bakari Mwamnyeto huku bao la kufutia machozi la  Ruvu Shooting likiwekwa kimiani na Lorand Msonjo.

Ushindi huo umeifanya Yanga kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa NBC Primier League nyuma ya  watani wao kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa wakiwa wamelingana pointi 13 kwa kila timu baada ya kucheza michezo mitano kila mmoja.

Ushidi huo wa Yanga unawapa kujiamini kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL dhidi ya Al Hilal ya Sudan jumamosi ya wiki hii.

Wakati Yanga wakitakata Azam nao wamezikamua  alzeti za Singida Big Stars kwa bao (1-0).

Bao la Azam limewekwa kimiani na Sospeter Bajana akifunga bao kali na kuwapatia wanalambalamba ushindi na point tatu muhimu.

Kimekuwa kipigo cha kwanza kwa Singida Big Stars msimu huu tangu wapande Ligi Kuu wakiwa wamecheza michezo mitano, wameshinda miwili sare miwili na kupoteza mmoja.

ZAKA ZAKAZI AFUATA NYAYO ZA MANARA

$
0
0


WAKATI Bado sakata la aliyekuwa Ofisa mhamasishaji wa Klabu ya Yanga Haji Manara likiwa bado linafukuta tangu alipopigwa nyundo wa miaka miwili ya kutojihusisha soka na faini ya million 20 kabla ya kupunguzwa.

Ofisa Habari wa Azam FC Thabiti Zakaria amekutana na rugu la Bodi ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara TPLB kwa kufungiwa miezi mitatu na faini juu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi inaeleza kuwa.

KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Oktoba 4, 2022 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi yafuatayo;
 

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Azam FC, Thabiti Zakaria amefungiwa kwa kipindi cha miezi mitatu (3) na kutozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kushutumu waamuzi wa mchezo tajwa hapo juu kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari.

Thabiti alitenda kosa hilo huku akifahamu kuwa klabu yake ilikuwa imeshatumia njia sahihi ya kikanuni kwa kuiandikia barua Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kuhusu malalamiko yao kwa Waamuzi.
 
Kanuni ya 39:(8 & 10) ya Ligi Kuu kuhusu Waamuzi na Kanuni ya
46:(3 & 10) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Viongozi zinasisitiza
Klabu kutumia njia sahihi kuwasilisha malalamiko yao kwa TPLB/TFF na kuwataka viongozi kuepuka kulalamika ama kushutumu waamuzi kupitia vyombo vya habari na mahali pengine popote.

Adhabu hii ni kwa uzingativu wa Kanuni ya 46:10 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Viongozi.
 
Hata hivyo mwamuzi wa kati wa mchezo tajwa hapo juu, Hans Mabena kutoka mkoani Tanga amepelekwa Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kosa la kushindwa kutafsiri vema sheria 17 za mpira wa miguu jambo lililosababisha ashindwe kumudu mchezo huo kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Septemba 30, 2022.

Katika hatua nyingine Klabu ya Namungo imetozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la mashabiki kuingia eneo la kiufundi la mchezo mara baada ya mchezo tajwa hapo juu kumalizika.

Tukio hilo lilifanyika wakati watangazaji wa Azam TV (mdhamini mwenye haki za matangazo ya Televisheni) wakiendelea kufanya mahojiano na makocha.

Adhabu hii ni kwa uzingativu wa Kanuni ya 47:1 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Klabu.
 
Kwingineko Mechi Namba 43: Simba SC 3-0 Dodoma Jiji FC  
Timu ya Dodoma Jiji imetozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kuchelewa kutoka kwenye chumba cha kuvalia jambo lililosababisha mchezo tajwa hapo juu kuchelewa kuanza kwa dakika moja (1) na sekunde 30.

Adhabu hii ni kwa uzingativu wa Kanuni ya 17:(33 & 60) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
 

Ndumbaro atoa ujumbe mzito asasi za kiraia

$
0
0
Mwenyekiti wa ICGLR, Joseph Butiku akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Mkutano Mkuu wa Tano wa RCSF unaofanyika jijini Dar es Salaam.


Na Mwandishi Wetu


JUKWAA la Asasi za Kiraia (RCSF) za Ukanda wa Nchi za Maziwa Makuu Afrika (ICGLR) limetakiwa kusimamia mambo nane ambayo yatagusa jamii ya wananchi wa nchi 12 za jukwaa hilo.

Hayo yamesemwa na  Waziri wa Sheria na Katiba Dk Damas Ndumbaro wakati akifungua mkutano mkuu wa tatu wa ICGRL unaofanyika jijini Dar es Salaam kwa siku mbili kuanzia leo.

Mkutano huo mkuu wa ICGLR unatarajia kuchagua viongozi wapya ambapo kwa sasa Mwenyekiti wake ni Joseph Butiku.

Waziri Ndumbaro amesema jambo la kwanza kwa RCSF katika Ukanda wa Maziwa Makuu ni kusimamia amani na usalama ili kuhakikisha jamii zilizopo zinafanya shughuli za maendeleo bila usumbufu.

"Amani na usalama ni nguzo ya muhimu kwa jamii yoyote, sisi Tanzania tunajivunia amani kuwepo na tutaendelea kusaidia nchi wanachama wa ICGLR ziendelee kuwa na amani,"amesema.

Amesema jambo la pili ambalo anazitaka asasi za kiraia kusimamia ni utawala bora, sheria na demokrasia.

Dk Ndumbaro amesema utawala bora, sheria na demokrasia sio vitu ambavyo vinashuka kutoka angani, bali vinatengenezwa na jamii husika ambapo asasi za kiraia ni moja wadau muhimu.

"Tatizo la nchi za Kiafrika ni kufikiria kuwa utawala bora, sheria na demokrasia vinapatikana kwa wazungu, hii sio kweli, lazima tutengeneze mifumo yetu na sio kukopi, kwa mfano Chancellor wa Ujerumani anaongoza hata miaka 17, ila sisi wananchi wakisema 10 huo ndio utaratibu wetu, hivyo asasi zina wajibu wa kusimamia hilo," amesema.

Waziri Ndumbaro amesema asasi za kiraia zinapaswa kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi na kwamba mifumo ya kufikia huko haiwezi kuwa sawa kwa nchi zote na kusisitiza kila nchi kutumia mifumo yake.

Waziri huyo wa Katiba na Sheria amesema jambo la nne ni asasi hizo kupigania utengemano wa kikanda kama Jumuiya ya Afrika Mashari (EAC), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na nyingine ambazo ni muhimu katika kuchochea maendeleo.

"Jambo la tano naomba mjadili uwepo wa vita na mambo yote yanayoweza kusababisha vita na sita mjadili masuala ya kijamii katika nchi wanachama wa ICGLR na zingine," amesema.

Dk Ngumbaro amesema jambo la saba asasi zinapaswa kujadili mazingira ambapo amesema Tanzania imefanikiwa katika eneo hilo kwa kuwa thelusi moja ya nchi imetunzwa.

Amesema jambo la nane ambalo anatamani kuona asasi za kiraia zinasimamia ni masuala mtambuka ambayo yatahusisha makundi yote kama wanawake, vijana, watoto na wazee ambao wanashiriki katika yote ambayo ameyataja awali.

Waziri Ndumbaro amesema Tanzania chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan itatoa ushirikiano chanya kuhakikisha hoja za asasi za kiraia zinafanyiwa kazi.

Amesema pamoja na Serikali kushiriki kufanikisha hilo pia vyombo vya habari vinapaswa kupewa kipaumbele kwa kila hatua.

Mwenyekiti wa RCSF katika ICGLR Joseph Butiku amesema kwa miaka takribani 18 wamekuwa wakijadili mambo ya amani, usalama, demokrasia, utawala bora, maendeleo ya uchumi, mshikamano wa nchi wanachama, vurugu zilizozalisha wakimbizi, mazingira na jinsia kwa ufanisi mkubwa.

Butiku amesema wanazipongeza nchi wanachama wa ICGLR zimekuwa zikitoa ushirikiano kwao jambo ambalo limerahisisha utekelezaji wa ajenda zao.

Mwenyekiti huyo amesema wamekuwa wakisimamia Serikali za nchi wanachama kuhakikisha zinatekeleza majukumu yao kwa kufuata utawala wa sheria.

"Leo asasi za kiraia za nchi wanachama ICGLR tumekutana hapa Dar es Salaam kujadili mambo mbalimbali ambapo pia tunarajia kesho kufanya uchaguzi kupata viongozi wapya," amesema.

Butiku amesema ICGLR inahusisha nchi za Afrika ya Kati, DR Congo, Tanzania, Kenya, Uganda, Sudan, Zambia, Sudan Kusini, Burundi, Rwanda na Congo Brazzaville ambapo kwa kiasi fulani wameweza kujenga mshikamano.

Amesema jitihada zao ni kuhakikisha mfumo wa sheria unachukua nafasi katika kuendesha nchi zote wanachama.

Naibu Katibu Mkuu wa wa ICGLR Balozi Mohamed Yassir amesema mikakati yao ni kuendeleza mazuri yote ambayo wamekubaliana, ili kuhakikisha nchi wanachama zinapata maendeleo kwa kasi.

"Sisi tumekuwa tukisimamia mipango yetu, pamoja na changamoto ambazo zinatokea, tunaamini tutafanikiwa iwapo mshikamano wa Wadau wote utapewa kipaumbele," amesema.

Balozi Yassir amesema katika kipindi cha janga la Uviko-19 walipitia wakati mgumu, ila wanaendelea kuimarika siku hadi siku.

Naye Hodan Addou kutoka UN Women akiwamwakilisha Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, katika Ukanda wa Maziwa Makuu amesema wataendelea kushirikiana na ICGLR ili kuhakikisha amani na usalama unaongezeka katika ukanda huo.

Amesema UN Women itashirikiana na ICGLR kuhakikisha kundi la wanawake linapewa msukumo ili liweze kushiri kikamilifu katika kupigania amani na usalama.

Kwa upande wake Dk Majaliwa Marwa kutoka UNFPA amesema watatoa ushirikiano kwa asasi za kiraia ambazo zitakuwa zinapigania haki za raia wake kwa kufuata misingi ya kisheria na utawala bora.

Dk Marwa amesema UNFPA inaamini katika majadiliano ili kuweza kujenga jamii yenye maelewano na maendeleo, hivyo wanazitaka asasi za kiraia kusimamia eneo hilo kama inavyofanya RCSF kupitia ICGLR.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Asasi za Kiraia nchini Kenya Peter Ole amesema asasi za kiraia ndio zimefanya Kenya kuwa nchi ya mfano kwa nchi nyingine hasa mfumo wake wa uchaguzi.

Naye Makamu Mwenyekiti wa CSO Sudan Kusini Akuoch Ajang amesema nchi yao imepitia wakati mgumu ila kupitia ujio wa asasi za kiraia jamii inaanza kubadilika na kutambua haki zao za msingi.

MDAKA MISHALE PODO IMEJAA SUMU

$
0
0


 

Na Mwandishi Wetu


NI nyakati chache sana katika maisha ya mchezo wa mpira wa miguu mlindo mlango anakuwa gumzo ama kuchukua nafasi kwenye vichwa vya habari hasa katika zama hizi za Soka la Maabara.

Yawezekana ikawa sababu ya ubora ama udhaifu lakini Soka la kisasa linahitaji walinda mlango ambao ni 'sweper' kwa maana mwenye uwezo wa kuanzisha mashambulizi kwa uwezo wake wa kupiga pasi.

Ni wazi kuna walinda mlango wengi kwenye Ligi Kuu Soka Tanzania Bara wenye huo ubora lakini katika kupiga pasi basi NBC PREMIER LEAGUE imeshihudia mlinda lango wenye uwezo Mkubwa wa kupiga pasi kushinda wachezaji wengi sana.

Hapa ndipo jina la Djigui Diarra ambaye ni moja ya makipa bora wanaofanya vizuri sana tokea ameingia hapa nchini.

Diarra ni aina ya makipa wa kisasa ambao moja ya silaha yake kubwa ni upigaji wake wa pasi. Makocha wengi duniani kwa sasa wanapendelea sana aina ya makipa ambao wanaweza kuanzisha mipira kwenye eneo la nyuma na kuhusika kwenye utengenezaji wa nafasi.

Diarra amethinitisha hilo juzi kwenye mchezo  Ruvu Shooting dhidi ya Yanga SC, Diarra aliweka rekodi kadhaa

Diarra ndiye kipa aliepiga pasi nyingi bila kupoteza (45). Diarra alivunja rekodi ya hapo awali ambayo ilishikiliwa na Aboutwalib Mshery ambapo msimu uliopita alifanya hivyo kwenye mchezo wa Yanga  dhidi Polisi Tanzania katika uwanja wa Benjamini Mkapa, katika mchezo huo Aboutwalib Mshery alipiga pasi 45 lakini akapoteza pasi moja tu.

Kabla ya hapo Beno Kakolanya nae aliweka rekodi ya kupiga pasi nyingi, ambapo alipiga pasi 40 zilizokamilika Yanga  dhidi ya KMC. Diarra ameweka rekodi pia ya kucheza muda mwingi zaidi nje ya eneo lake ambapo alitumia dakika 70 nje ya eneo lake huku akitumia dakika 20 kwenye eneo lake.

Kwa mujibu wa Kocha Abely takwimu hizi za Diarra ni rekodi mpya kwenye ligi yetu kwa miaka ya hivi karibuni hususani kipindi cha mapinduzi ya kidigital kwenye matangazo ya ligi kuu kwa njia ya runinga.

Viewing all 19659 articles
Browse latest View live
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>