Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

DKT. NCHIMBI AMKABIDHI RASMI OFISI MKUU MPYA WA MKOA WA SINGIDA

$
0
0

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi (kulia)  akimkabidhi kabrasha  Mkuu wa Mkoa huo Mpya Dkt. Bilinith Mahenge katika hafla iliyofanyika ofisi ya mkuu wa mkoa mjinini hapa.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi (kulia), akizungumza katika hafla hiyo.

Hafla ikiendelea.


Wakuu wa Wilaya  Mkoa wa  Singida wakijitambulisha kwa mkuu wa mkoa mpya.
Wakurugenzi wa Halmashauri wakijitambulisha kwa mkuu wa mkoa mpya.


Na Dotto Mwaibale, Singida


ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi ambae amestaafu utumishi wa umma amekabidhi ofisi kwa mkuu mpya wa mkoa huo Dkt.Binilith Mahenge ambapo amewashukuru watumishi wote wa mkoa huo kwa ushirikiano mkubwa waliompatia na kupelekea kustaafu kwa heshima.

Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano ya ofisi hiyo Dkt. Nchimbi limuomba Dkt. Mahenge kutumia uzoefu alionao kutoka makao makuu ya nchi kuisaidia na kuivuta Singida ili kuongeza kasi ya kuwaletea maendeleo wananchi wake kwa kuwa ni jirani na makao makuu ya nchi hasa kwa kuyaendeleza mazao ya Parachichi na Korosho.

Dkt. Mahenge akizungumza baada ya kukabidhiwa ofisi hiyo amewaomba ushirikiano watumishi wa ofisi hiyo kama walivyokuwa wakimpatia mtangulizi wake ili kuwatumikia wananchi wa mkoa kwa kuwaletea maendeleo.

"Jamani ninawaomba sana ushirikiano wenu kama mlivyoona hapa  mimi Mahenge nimeingia mimi kama mimi  sijaja na wale niliokuwa nafanya nao kazi,nyinyi ndio wenzangu hapa sasa." alisema Mahenge.

Aliwaomba watumie fursa hiyo kutafakari pale ambapo hawakufanya vizuri wakati wa Nchimbi kama ambavyo na yeye atatumia hiyo fursa kuongeza ufanisi wa utendaji wake wa kazi kama hakufanya vizuri wakati alipokuwa Dodoma.

Aidha aliwaahidi viongozi na wananchi wa mkoa huo kuyasimamia na kuyaendeleza yote yaliyoanzishwa na Dkt. Nchimbi hususani katika sekta ya kilimo ambapo amehamasisha kilimo cha Korosho na Parachichi,huku akitumia fursa hiyo kumshukuru Mh.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini ili amsaidie katika mkoa huu.

Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Ahmed Kaburu alimwambi mkuu wa mkoa mpya kuwa Chama kitampa ushirikiano na kuwa kitaendelea kushirikiana na Serikali.

Makabidhiano hayo ya ofisi yamefanyika leo mbele ya viongozi wa mkoa huo akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Mstaki Meya, Viongozi wa Ulinzi na Usalama, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakuu wa Idara.



Meja Jenerali Charles Mbuge awasili mkoani Kagera

$
0
0

 Meja Jenerali Charles Mbuge akipokelewa baada ya kuwasili mkoani Kagera.
 

Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akimpokea mkuu mpya wa mkoa huo Meja Jenerali Charles Mbuge katika Ofisi za mkoa huo.

 

 Lydia Lugakila, Bukoba

Mkuu mpya wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge amewasili mkoani Kagera tayari kwa makabidhiano ya ofisi mpya baada ya mtangulizi wake Brigedia Jenerali  Marco Gaguti kuhamishiwa katika mkoa wa Mtwara.
 

Meja Jenerali Charles Mbuge amewasili mkoani Kagera Mei 24, 2021 kwa ajili ya makabidhiano rasmi ya Ofisi chini ya mtangulizi wake Brigedia jenerali Marco Elisha Gaguti.

Akizungumza baada ya mapokezi ya mkuu huyo mpya wa mkoa Brigedia Gaguti amesema kuwa makabidhiano hayo ya kiofisi yatafanyika leo Mei 25 mwaka huu ambapo baadhi ya viongozi wa mkoa huo, wawakilishi kutoka Manispaa ya Bukoba na wananchi watashiriki katika shughuli hiyo ambapo baada ya hapo Brigedia jenerali Marco Elisha Gaguti atakuwa tayari kwenda mkoani Mtwara katika kituo chake kipya cha kazi.

NMB yaendesha semina ya walimu kuwapa elimu ya fedha

$
0
0

Washiriki wa Semina ya walimu wakuu wa Shule za msingi na wakuu wa Shule za Sekondari zilizopo Mkoa wa Arusha, wakisikiliza hotuba ya mgeni rasimi kwenye uzinduzi wa semina ya  mafunzo ya bidhaa za NMB. Semina hiyo yenye lengo la kutoa elimu ya fedha na bidhaa mbalimbali za NMB ilifanyika leo jijini Arusha na kuhudhuriwa na walimu zaidi ya 300.

  Mkuu wa kitengo cha biashara ya kadi Benki ya NMB, Bw. Philbert Casmir akihutubia katika shughuli hiyo.


  Meneja wa  wateja binafsi Benki ya NMB, Bi.Nyamisinda Manyonyi akitoa elimu ya Mikopo kwa walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari Mkoa wa Arusha.

   


Na Mwandishi Wetu

 

Walimu wametakiwa kujiendeleza kwa kukopa mikopo nafuu, yenye tija na kuwawezesha kutatua  changamoto zinazowakabili ili kuweza kunufaika na kufurahia kazi wanayoifanya.

 

Akizungumza wakati wa mafunzo ya walimu wa mkoani Arusha yaliyoandaliwa na Benki ya NMB, Afisa elimu sekondari wa mkoa huo, Khalifani Omary alisema mafunzo hayo yatawajenga walimu katika kujiwekea kipato na kufahamu fursa mbalimbali zilizoko benki ili kuweza kujiendeleza kimaisha.

 

"Mafunzo haya yatawasaidia katika kuwaongezea ufahamu namna wanavyoweza kunufaika na benki ya NMB ikiwa jitihada hizi zitaleta matokeo chanya nakuleta faraja kwa jamii,"alisema Omary.

 

Afisa elimu alisema jitihada hizo ni nzuri na  zinaunga mkono juhudi za serikali katika kuhakikisha watanzania walio wengi wanajumuhishwa katika mfumo rasmi wa kifedha ili kuinua  vipato vyao hivyo ametoa rai kwa taasisi nyingine za kifedha nchini kufanya jitihada hizo kama NMB.

 

Alisema anashukuru huduma za kibenki zimeboreshwa na kusogezwa karibu na wateja wake kwani hapo awali walimu walipata taabu kutembea umbali mrefu hivyo benki ya NMB imekuwa chachu ya maendeleo katika jamii kwa kuwanufaisha wateja wake.

 

Kwa upande wake Mkuu wa biashara ya Kadi wa benki ya NMB, Philbert Casmir  alisema  wameandaa mafunzo yanayoitwa siku ya walimu ambapo wameanza mkoani Arusha kwa kutambua mchango wa mwalimu katika jamii na kutoa suluhisho ya changamoto zao katika kujikwamua kimaisha ikiwemo mikopo nafuu na bima mbalimbali.

 

"Tunatambua mwalimu ni mwezeshaji katika jamii hivyo NMB tumekuja na suluhisho mahususi kwa walimu ikiwemo mikopo nafuu ya kujenga au kununua nyumba,"alisema Mkuu huyo.

 

Casmir alisema pia kuna bima za walimu na watanzania kwa ujumla zinazoweza kuwasaidia kupata nafuu wakati wa majanga mbali mbali.

 

Baadhi ya walimu hao walisema wanashukuru benki ya NMB kwa kuwapa mafunzo hayo ambayo yatawasaidia katika kuwekeza fedha nakutumia katika matumizi sahihi ya kujiendeleza kiuchumi na kuwaletea maendeleo.

Mwalimu  mkuu wa shule ya msingi Daraja mbili, Zukra Kalunde alisema mafunzo hayo yatawasaidia katika kufahamu umuhimu wa kadi pamoja na kujifunza namna ya kupata mikopo nafuu ya benki hiyo itakayowasadia kujiendeleza kiuchumi kama ujenzi wa nyumba zao za kuishi na biashara.

 

 


WAZIRI AWESO ATOA ONYO KALI JUMUIYA ZA MAJI, AJA NA SULUHISHO LA KUMALIZA CHANGAMOTO

$
0
0


WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso,ameagiza kuvunjwa kwa Jumuiya ya Maji katika kijiji cha Berege wilayani Mpwapwa huku akitoa onyo kali la ubadhilifu wa fedha za Jumuiya ya watumia maji katika mradi wa maji kijijini hapo.

Kauli hiyo ametoa Mhe.Aweso wakati wa  ziara yake ya kukagua utekelezaji na uendeshaji wa miradi ya maji pamoja na kuzungumza na wananchi katika kijiji cha Berege kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.

Waziri Aweso alipokea malalamiko ya wananchi kuhusiana na jumuiya ya watumiaji maji katika Kijiji cha Berege  kuwa fedha zinakusanywa bila ya kupelekwa benki na hivyo kulazimika kuivunja jumuiya hiyo.

Waziri Aweso amesema kuwa Jumuiya za Watumia Maji nchini zimekuwa na changamoto kubwa kwenye usimamizi wa miradi na matumizi sahihi ya makusanyo ya fedha;
amesisitiza na kutoa wito nchi nzima ikiwa ni suluhisho la kudumu la changamoto hii kuwa kuanzia sasa Jumuiya zote za watumia maji nchini ziwe na mafundi sanifu wanaotokana na Chuo cha Maji na kuwa na Watu wenye sifa ya Uhasibu na tayari Wizara imeingia makubaliano na Chuo hiki.

Pia  amemuagiza Meneja wa RUWASA Mpwapwa, Mhandisi Syprian Warioba kurejesha fedha zilizochukuliwa katika Jumuiya ya Watumia Maji Berege kuwalipa wataalam kwa ajili ya usimamizi wa miradi kwa kuwa serikali imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya kazi hiyo.

Hata hivyo amemuagiza Meneja wa Wakala wa Uchimbaji Visima (DDCA) Peter Mdalangwila kuhakikisha wanafika Mpwapwa Jumamosi Mei 29, 2021 kuchimba visima vitatu katika Wilaya hiyo na kati ya visima hivyo kimoja kichimbwe katika Shule ya Sekondari Berege ili kupunguza adha ya maji inayowakabili wanafunzi shuleni hapo.

Wizara ya Afya yaanza utekelezaji wa maboresho ya huduma za matibabu kwa Wazee

$
0
0

Na WAMJW-Dodoma

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeanza kufanya ufuatiliaji  wa maelekezo yake  katika kuboresha huduma za matibabu kwa wazee kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Dkt. Dorothy Gwajima alipotembelea hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma na kujionea jinsi walivyoweza kutekeleza maagizo ya utoaji wa huduma za afya kwa wazee wanaofika kupata matibabu hospitalini hapo.

Dkt. Gwajima amesema mahitaji ya maboresho ni mengi  hivyo wizara yake imeona ianze na vitu  vile vya msingi  ambavyo wazee wamekuwa wakiyalalamikia   kila siku wanapofika kwenye vituo vya kutoalea huduma za afya.

Ametaja malalamiko yanayokuwa yakilalamikiwa na wazee  wanapofika kwenye vituo vya afya ni pamoja na mapokezi yasiyoeleweka na kutokupata huduma iliyokusudiwa na kuongeza kuwa   wazee nguvu zimekwisha hivyo wanahitaji kuongozwa kwahiyo wizara yake wamefanya maboresho kwa kuwa na watu maalumu wa kuwapokea wazee hao pale wanapoifika hadi kuondoka na kuwatambulisha kwa kuvaa sare maalumu.

“Kila kituo lazima kiwe na nesi mmoja, afisa ustawi wa jamii pamoja na daktari aliyepangwa zamu na lazima wavae sare ambayo itamtambulisha na imeandikwa ‘Mzee ni Tunu, Tunakupenda, Tunakuheshimu’  pamoja na kuweka mabango yanayomuelekeza au kumuongoza mzee wapi atapata huduma anazozihitaji na ambayo yameandikwa "Mpishe Mzee apate huduma kwanza".

Dkt. Gwajima amesema maelekezo hayo wameyatoa katika hospitali na vituo vya afya vyote na kwa hatua hiyo sasa wizara inaenda kutengeneza muongozo ambao utakua wa uwiano kwa hospitali zote.  Hata hivyo ameipongeza hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma kwa kuanza utekelezaji huo na kuwa itakuwa ya mfano wengine kujifunza utaratibu unaotumika na kuboresha kulingana na mazingira yao.

Aidha, Dkt. Gwajima amewataka hospitali zingine kutokusubiri miongozo katika kutekeleza  maelekezo yanayolewa na kusiwe na visingizio vingi kwamba haiwezekani kwani maagizo yanayotolewa yanawezekana na utekelezaji wake ni wa mara moja hususan katika hospitali za kuanzia halmashauri hadi ngazi ya Taifa.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya Dkt. Vivian Wonanji  amesema idara yake imeandaa mkakati wa huduma wa wazee wa  miaka kumi na ifikapo mwezi Juni mwaka huu wataanza kuandaa mpango wa utekelezaji wake.

Dkt. Wonanji amesema mpango mkakati huo utakuwa na mambo makuu yakiwemo kuzalisha wataalam wa kutoa huduma za wazee,"kama tunavyofahamu wazee wanahitaji mambo mengi ikiwemo masuala ya lishe na utengamao hivyo mkakati huo utakua na maono muhimu ambayo yatasaidia kuboresha huduma za wazee nchini”.

Wakati huo huo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma Dkt. Ernest Ibenzi amesema hospitali yake imejipanga kuwahudumia wazee wa rika tofauti wakiwemo wenye uoni hafifu na hivyo waratibu wa wazee huwafuata wazee mara wafikapo hospitalini  hivyo wanashukuru mapokeo ya wazee pamoja na wagonjwa wanaofika kupata huduma.

Mnamo tarehe 7 Mei, mwaka huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akiongea na wazee wa Mkoa wa Dar es salaam aliahidi kuboresha tiba kwa wazee  kwani tiba ni haki yao ya msingi  katika daraja lolote lile watakalokua wanaugua kuanzia vituo vya afya, zahanati hata hospitali za Taifa.
-Mwisho-

ADO SHAIBU AKABIDHI SARUJI MSIKITI WA MSINJI-TUNDURU

$
0
0


Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu ambaye pia alikuwa Mgombea wa Ubunge katika Jimbo la Tunduru Kaskazini Kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, leo amekabidhi Mifuko thelathini (30) ya Saruji kwa Uongozi wa Msikiti wa Kijiji cha Msinji Kata ya Ligoma Wilaya ya Tunduru.

Makabidhiano hayo yaliyohudhuriwa pia na Katibu wa ACT Wazalendo wa Mkoa wa Kichama wa Selou Ndugu Mtutura Abdallah Mtutura ni utekelezaji wa ahadi yake kwa viongozi hao aliposwali Sala ya Idd El Fitr Msikitini hapo.
 

Ado Shaibu aliwapongeza viongozi na waumini kwa jitihada wanazozifanya kujenga msikiti mpya utaoendana na mahitaji ya sasa Kijijini hapo. Aliwaahidi kuwa yeye  Mwenyewe na kwa kushirikiana na marafiki atawasaidia kuhakikisha kuwa msikiti huo unakamilishwa.

Akiwasilisha Saruji hiyo, Ndugu Ado amesema kuwa atawashirikisha marafiki zake zaidi ili kuhakikisha mahitaji mengine kama vile kokoto, nondo, mbao, bati n.k yanapatiwa ufumbuzi ili Waislamu wa Msinji waweze kuswali kwenye msikiti bora.

KALEMANI ATOA MAAGIZO MAZITO KWA REA

$
0
0


 NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA


WAZIRI wa Nishati Medard Kalemani amewaagiza wakandarasi wa mradi  wa wakala wa umeme vijijini (REA) awamu ya tatu mzunguko wa pili kuhakikisha hadi kufikia 2022 vijiji vyote nchini vinapata umeme.

Aidha katika Mpango huo pia amesema hatomfumbia macho mkandarasi ambae ataleta kikwazo Cha miundo mbinu,na kubagua baadhi ya nyumba za nyasi, tembe na zile za tope.

Waziri Kalemani ameyasema hayo leo jijini hapa kwenye kikao kazi kilichowajumuisha wakandarasi mbalimbali ambapo pamoja na mambo mengine amewataka  wakawe wabunifu katika utekelezaji wa  majukumu yao.

"Kumekuwa na tabia ya mkandarasi kuruka nyumba hizi za tope ,nyasi na nyumba za tembe hivyo basi natoa maelekezo vijiji vyote vilivyo baki muende mkavipelekee Nishati hii ya umeme ndani ya miezi hiyo 18 mliosaini katika mikataba yenu na Serikali," .

Na kuongeza kusema " Tumekuwa tukipata malalamiko mengi kwamba kuna baadhi ya maeneo yamerukwa, hivyo muende mkaone ni namna gani mnaweza kufanya  Ili vijiji vyote vilivyopitwa vipate umeme kwa wakati," amesema Kalemani.

Hata hivyo amewataka wakandarasi hao waliosaini mkataba kwenda kuwasili eneo la Kazi na waende kutoa taarifa kwa Viongozi  wa eneo wanalotaka kufanyiwa Kazi.

" Hili ni muhimu sana kwani mtaondoa taharuki kwa wenyeji wenu hivyo muende mkajitambulishe kwa Mkuu wa Wilaya ,Mbunge, na hata Viongozi wa vijiji  kwani hawa ndio wawakilishi wa wananchi mnaokwenda kuwahudumia na mkawasikilize  au wawakilishi wao na mkifanya hivi hakika kazi yenu itakuwa nyepesi ," amesema Kalemani.

Amesema huo ni Mpango wa Mwisho miezi 18 ni michache hivyo amewashauri wakati wanatekeleza magenge au vituo viwe vingi angalau kila mkandarasi awe na vituo 5 ambapo ameeleza vituo hivyo vitawasaidia kukuwa kikazi.

Pia amewataka wakandarasi hao kupunguza kero kwa kuhakikisha wanatoa ajira kwa Vijana wazawa na kuachana na habari za kuja na vibarua wao ,kwa kufanya hivyo Kazi zao zitakuwa shirikishi kwa  wananchi.

Sambamba na hayo Waziri Kalemani ametoa maagizo mengine mahususi kwa wakandarasi hao na kuwaelekeza vibarua wao kuacha kuwauzia wananchi nguzo za umeme, kuwepo na stoo,kusiwepo na visingizio vya kutofikika kwa maeneo na kuondoa kero ya uunganishwaji wa umeme (wiring).

Naye Naibu Waziri wa Nishati Steven Byabato amesema ameyapokea maelekezo na sasa ni muda wa kwenda kuyafanyia Kazi ambapo amesema mikakati ya Serikali ni kwamba hadi kufikia 2022 kila mtanzania kijiji chake kiwe kimefikiwa na Nishati ya umeme.

Hata hivyo amewataka wakandarasi hao kuhakikisha wanawasili haraka iwezekanavyo katika maeneo yao ya Kazi na kuanza Kazi haraka kama walivyosaini katika mikataba yao.

Tutamuenzi hayati JPM kwa kutimiza ahadi zake Veta

$
0
0

 

Mkurugenzi Mkuu wa Veta, Dk. Bujulu akitoa maelekezo kwa Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako na Balozi wa China hapa Tanzania, Ke kuhusu  vifaa vilivyotolewa na serikali ya China kwaajili ya mafunzo ya uvuvi na uchakataji wa mazao ya samaki kwa Chuo cha Veta wilayani Chato Mkoa wa Geita.


Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako na Balozi wa China hapa nchini, Ke wakibadilishana mikataba waliyosaidi kuhusu upokeaji wa vifaa vya mafunzo ya Uvuvi na uchakataji wa mazao ya samaki, utiaji saini wa mkataba huo ulifanyika kwenye Makao Makuu ya Veta jijini Dar es Salaam leo Mei 25.2021.

 

Na Irene Mark

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema watatekeleza ahadi zote walizozitoa kwenye Vyuo vya Ufundistadi VETA ikiwa ni sehemu ya kumuenzi Hayati Rais John Magufuli.

Profesa Ndalichako amesema hayo Dar es Salaam leo Mei 25.2021 wakati akipokea msaada wa vifaa vya mafunzo ya uvuvi na uchakataji wa mazao ya samaki vilivyotolewa serikali ya China kwaajili ya Chuo cha Veta, Wilaya ya Chato mkoani Geita.

Akizungumza muda mfupi baada ya kuvikagua na kuvipokea, Profesa Ndalichako, amesema vifaa vilivyotolewa ni majokofu, mashine za kusindika samaki, kutengeneza soseji za samaki na boti ya uvuvi ambavyo thamani yake ni Sh. milioni 350.

“Tunaishukuru sana Serikali ya China kwa msaada huu ambao ni mwendelezo wa urafiki na undugu wetu wa siku nyingi, naomba uongozi wa VETA ukavitunze vifaa hivi ili vidumu”, alisema Profesa Ndalichako.

Kuhusu kuwepo kwa somo jipya la uvuvi na uchakataji wa mazao ya uvuvi, amesema kutawawezesha wananchi wa Chato, Kagera na mikoa ambayo wananchi wake wanategemea uvuvi kuinua kipato chao.

“Hili somo nataka sasa Veta mkalifundishe kwenye mikoa yenye maziwa kama kule kwetu Kigoma kuna Ziwa Tanganyika... hii itaboresha uchumi wa wananchi wa maeneo hayo.

Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke amewapongeza watanzania kwa kuwa na rasilimali nyingi huku akiahidi kuendelea kushirikiana na VETA katika kusukuma mbele gurudumu la ujuzi kwa vijana.

“Niwatakie heri ya siku ya Afrika... Serikali ya China inafurahishwa naa juhudi zenu za kuwekeza kwenye ujuzi. Tutaendelea kushirikiana ili kuleta maendeleo ya Tanzania na Afrika,” amesema Balozi Ke.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Veta, Dk. Pancras Bujulu amesema mchakato wa upatikanaji wa vifaa hivyo ulianza Januari 6.2021 baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China alipotemebelea Tanzania na kuzindua rasmi Chuo cha Veta wilayani Chato.


VIONGOZI SIMAMIENI HAKI, MAENDELEO KATIKA UKUSANYAJI MAPATO-MKUU WA MKOA WA KAGERA

$
0
0

Na Lydia Lugakila, Bukoba

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia  Jenerali Marco Gaguti amekabidhi rasmi ofisi za mkoa tayari kuelekea Mtwara kituo chake kipya cha kazi, Brigedia Gaguti amekabidhi ofisi hiyo kwa Meja Jenerali Charles Mbuge.

Hafla ya makabidhiano rasmi ya ofisi kati ya aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti na Meja Jenerali Charles Mbuge yamefanyika katika ukumbi wa mkoa huo na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali wa mkoa huo zikiwemo taasisi za dini.

Akikabidhi rasmi nyaraka za kiofisi Brigedia Jenerali Gaguti amewashukuru wananchi na viongozi mbalimbali wa mkoa huo kwa ushirikiano katika shughuli za maendeleo zilizopelekea mkoa huo unakuwa wa kiwango cha tofauti.

"Nimefanya kazi Kagera miaka 2 nawashukuru wana Kagera wapatao takribani milioni 3.1 kwa kipindi ambacho nimekuwepo Kagera nimeshiriki mambo mengi na makubwa ya kimaendeleo, wapo wengi walionisaidia katika majukumu yangu nimeuacha mkoa salama  muendelee kuniombea ninapoelekea mkoani Mtwara kituo changu kipya cha kazi wana Kagera niwaombe mkampatie ushirikiano wa kutosha kwa asilimia 200 Ila nitabaki kuwa mwana Kagera licha ya kuwa mwana Mtwara" alisema Brigedia Gaguti.

Gaguti ameongeza kuwa hakujutia kuwepo katika mkoa huo kwani amejifunza mambo mengi ikiwemo kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali za wananchi na kumuomba mkuu mpya wa mkoa huo meja jenerali Charles Mbuge kumalizia changamoto kubwa kwa wananchi hao ikiwemo ujenzi wa soko, stendi ya magari ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam tawi la Kagera na kuahidi ushirikiano kwa Meja Jenerali Mbuge.

Aidha baada ya makabidhiano hayo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge ameahidi ushirikiano kwa viongozi mbalimbali wa mkoa huo ikiwemo kusimamia haki, kusimamia maendeleo katika ukusanyaji wa mapato kwa halmashauri zote, huku akiwataka watendaji wake kutoa huduma nzuri kwa kutambua kuwa ofisi za serikali si za nyumbani kwao kwamba zifungwe watu wasiingie.

" Ili kiongozi ufanye kazi vizuri unatakiwa kuondoa ubinafsi mimi huwa najishusha nikiwa kazini ili mambo yasonge mbele kumbukeni taifa letu hatuna mjomba wala wala babu ni sisi wenyewe kikubwa tuwe wawazi na maendeleo yanaletwa na sisi hivyo hatuhitaji kusukumwa" alisema meja jenerali Charles Mbuge.

Jenerali Mbuge ameahidi  kushirikiana  na uongozi wa CCM ili kuendelea kutekeleza ilani ya chama ambayo inalenga kuwaletea maendeleo wananchi wa mkoa huo.

Hata hivyo kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo amempongeza mkuu wa mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti kwa uongozi wake mzuri kwa wanakagera na kuwataka watumishi wa mkoa huo kuendelea kuwatumikia wananchi ili wilaya hizo ziweze kuwa na maendeleo huku akimkaribisha mkuu mpya wa mkoa huo.

Naye mwakilishi wa wazee mkoani humo Suleiman Kabyemela mwenye umri wa miaka 94 amesema " Brigedia  Gaguti sisi wazee wa Kagera na wanakagera kwa ujumla ingewezekana tungesema subiri tunashukuru kwa yote  uliyotutendea kwa wakati wote uliokuwa hapa unakokwenda tunamuachia mwenyezi Mungu, Mbuge tunakukaribusha sana waswahili husema karibu mgeni mwenyeji apone"alisema mzee Kabyemela.

Ikumbukwe kuwa mnamo Mei 15 mwaka huu Rais Samia Suruhu Hassan alifanya mabadiliko na uteuzi kwa baadhi ya wakuu wa mikoa hapa nchini ambapo aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti alihamishiwa mkoani Mtwara na Kagera kukabidhiwa kwa Meja Jenerali Charles Mbuge.
Meja Jenerali Charles mbuge akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya ofisi na mtangulizi wake Brigedia Jenerali Marco Gaguti.
Meja Jenerali Charles Mbuge akionyesha kitabu cha makabidhiano ya kiofisi.
 

RC MAKALLA AONYA MAJAMBAZI DAR AAGIZA POLISI KUYAKAMATA

$
0
0


 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa huo, Amos Makalla, akizungumza kuhusiana na watu wanaojihusisha na ujambazi na kuliagiza Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kuwashughulikia kikamilifu majambazi na vibaka jijini humo.  

 

Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa huo , Amos Makalla amewaonya watu wanaojihusisha na ujambazi na kuliagiza Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kuwashughulikia kikamilifu majambazi na vibaka jijini humo. 

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kutokea matukio ya ujambazi katika eneo la Mbezi ambapo majambazi walisababisha kifo cha mtu mmoja aliyekuwa akitoka benki kuchukua fedha na kwamba tukio la pili lilitokea Mabibo na kwamba majambazi walimjeruhi mfanyabiashara katika harakati za kutaka kumpora fedha zake.

Aidha, amewataka watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kuzisalimisha polisi mara moja na kwamba watakaokaidi watachukuliwa hatua kali za kisheria.

RC  huyo ameliagiza jeshi hilo kuanza kwa operesheni ya kufagia watu wote wanaofanya uhalifu mkoani humo ambapo amewaomba wazazi kufuatilia mienendo ya watoto kwa kuwakanya endapo wanashiriki waache kushiriki.

Amesema kwakuwa uzoefu unaonyesha wahalifu  hutumia silaha kujeruhi na kusababisha vifo,  hivyo  ni vyema jeshi hilo likawachukulia hatua kikamilifu kabla hawajazitumia katika uporaji na mauaji wakati wakiwa kwenye matukio ya ujambazi.

Amewahikikishia wananchi usalama na kuwataka kuendelea kufanya shughuli zao kama kawaida kwani vyombo vya ulinzi na usalama viko macho kuwashughulikia wale wote wenye nia ya kuhatarisha usalama wa wakazi na mali zao.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Camilius Wambura amesema Katika msako ulioanza Mei 21 hadi Mei 25 wamefanikiwa kuwakamata Majambazi na vitu mbalimbali ikiwemo magari manne, pikipiki moja, bunduki moja, laptop na vifaa vinginevyo.

Aidha Kamanda Wambura amesema kuwa maagizo yaliyotolewa wameyapokea kwa mikono miwili na watayafanyia kazi kwa ufanisi mkubwa.


Kamanda huyo amewaonya wahalifu wanaoshindana na vyombo vya ulinzi na usalama kuacha kujidanganya kwani mkono wa sheria ni mrefu.

RC Makalla akutana na Wazee wa CCM Dar, awaahidi ushirikiano

$
0
0

 

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam , Amos Makalla  ameanza rasrmi majukumu yake kwa kukutana na Baraza la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi wa mkoa huo na kuahidi kushirikaina nao bega kwa bega ili kuendelea kuchochea maendeleo.
Aidha, amesema ataweka utaratibu wa kukutana na wazee wa chama hicho kila baada ya miezi mitatu kujadili masuala mbalimbali yawahusuyo na kupokea ushauri kutoka kwa wazee hao.


Amesema ameamaua kukutana nao kwani anatambua thamani na Mchango wa Wazee Katika jamii hivyo ameona ni vyema kuanza majukumu yake kwa kukutana nao ili kuchota busara na Baraka zao kwani anatambua Wazee ni hazina muhimu.

 Amebainisha kuwa  kutatua kero na changamoto za Wananchi atawaeka utaratibu kukutana na wanananchi wa kata zote za Dar es Salaam ili kusikiliza changamoto zinazowakabili na kuzipatia majibu.

 Amesisitiza kuwa mkoa huo ni mkubwa na wenye taswira  ya nchi nzima katika nyanja mbalimbali, hivyo amejipanga kuhakikisha Jiji linakuwa shwari na watu wanafanya shughuli zao pasipo usumbufu wowote Kama maono na mategemeo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa baraza Wazee wa chama hicho, Hemed Mkali amesema wanaahidi kumpatia ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake na   kumpongeza RC kwa namna anavyowaheshimu na kuwathamini.


Naye Mjumbe wa baraza la wazee hao kutoka Wilaya ya Kinondoni Janeth Kahama amesema wanamtakia kila la kheri katika shughuli zake na kwamba wataendelea kumuunga mkono ili afikikie malengo aliyojiwekea katika mkoa huo.

Balozi Mstaafu Chrispoher Liundi amesema watajitahidi kufanya kazi na RC huyo bega kwa bega na kumuomba kuweka mahusiano mazuri na kundi hilo na kuwasisitiza wazee hao endap0 kuna dosari wasisite kueleza ila kwa kufuata taratibu, kanuni na sheria.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Ramadhan Madabida amesema wapo tayari kumuunga mkono na kwamba wanafahamu uwezo wa RC Makalla tangu alipoanza kuitumikia CCM hivyo amemuomba afikishe salamu kwa Rais Samia ya kuunga mkono jitihada zake za kiuongozi.

Mikopo ya NMB Masta Boda sasa yatua rasmi Kanda ya Kaskazini

$
0
0

 

 

Kutoka Kushoto: Mwendesha bodaboda wa Jijini Arusha Stella Nguma, Mkuu wa kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB Alex Mgeni, Mwenyekiti wa chama cha pikipiki za miguu mitatu Twaha Mpera, Mwenyekiti wa chama cha pikipiki za miguu miwili Okero Costantine, Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Allan Rushokana, Kaimu Mkaguzi Mkuu wa ndani Benki ya NMB Benedicto Baragomwa na Meneja Mwandimiz wa Bidhaa, Clara Mwichumu, wakizindua kampeni ya Miliki Chombo jijini Arusha inayowawezesha waendesha bodaboda na bajaji kupata mikopo nafuu. Hafla ya Uzinduzi huo ilifanyika leo jijini Arusha katika Ukumbi wa  Lush Garden.

Baadhi ya waendesha boda boda na bajaji wa jijini Arusha wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Allan Rushokana na wafanyakazi wa Benki ya NMB baada ya kufanyika uzinduzi wa Mikopo ya NMB Masta Boda  leo.

 

Na Mwandishi Wetu 

Kutokana na changamoto ya madereva boda boda na pikipiki aina ya miguu mitatu kutomiliki vyombo vyao vya kazi, Benki ya NMB imekuja na njia ya kuwakomboa na hali ya utegemezi kwa kuwapatia mikopo nafuu ya umiliki wa vyombo hivyo.

 

Hakimu Saimon ni katibu wa bodaboda mkoa wa Arusha alisema anaishukuru taasisi hiyo kwani wamekuwa wanaendesha pikipiki za wengine kwa muda mrefu hali inayopelekea kuwa tegemezi katika umiliki wa vyombo hivyo kwa kuwarejeshea wamiliki wao fedha waliopangiwa.

 

"Kwa kufanya hivyo wamekuwa wakiingia mikataba ya kurejesha sh.10,000 kila siku ndani ya miezi 13 ilikuwa ni mateso lakini kupitia benki ha NMB kila mmoja wetu atanufaika na mkopo huu na kuweza kumiliki chombo chake na kujikwamua kiuchumi katika kujiletea maendeleo,"alisema Katibu huyo.

 

Alisema ni jambo la furaha kwao kutumia fursa ya mkopo huo katika kumiliki vyombo vyao kwani wao watatoa asilimia 20 na 80 wataongeza Benki ya NMB hivyo watafanya juhudi katika marejesho hawatakuwa na mchezo katika kutumia fursa hiyo.

 

Kaimu Afisa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Benki ya NMB, Benedicto   Baragomwa alisema baada ya uzinduzi huo waendesha bodaboda na bajaji watapata fursa ya kupata pikipiki za miguu mitatu na miwili ikiwa zoezi hilo lilianzia Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma na sasa Arusha ikiwa mkoa unaofuata ni Mbeya.

 

Baragomwa alisema benki hiyo imetenga Sh. bilioni 5 kwa kuanzia kwa mwaka huu ambapo zitawanufaisha waendesha bodaboda zaidi ya milioni mbili nchini.

 

"Kwa kuwa bodaboda wengi ni vijana na hawana dhamana, NMB imekuja na njia ya kuwakopesha kwa mikopo nafuu. Ni vyema wakatumia fursa hii ili kila mmoja amiliki chombo chake,"alisema.

 

Awali akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Arusha, Kenani Kihongosi katika uzinduzi huo, Afisa Afya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Allan Rushokana alisema swala la kuwakopesha mikopo hiyo madereva hao itawasaidia kuwaletea maendeleo yao na kujikwamua kiuchumi.

 

"Lengo kubwa la taasisi ya fedha ya NMB ni kuwasaidia kujikwamua kiuchumi kwani suala la ajira nchini limekuwa changamoto lakini kujiajiri kuna nyanja pana hivyo wazingatie utaratibu wa kupata mikopo ili kila mmoja aweze kumiliki chombo chake na mpango huu ukatoe matokeo mazuri katika kuleta maendeleo  na kujikwamua kiuchumi,"alisema Mwakilishi huyo.

Maelekezo ya Rais Samia, IMF yaanza kutekelezwa

$
0
0


Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia)akimsikiliza Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Fedha Kimataifa (IMF) nchini, Bw. Jens Reinke (kushoto) katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma.

 

 

 NA FARIDA RAMADHAN, WFM – DODOMA 

 

Serikali imeanza utekelezaji wa maelekezo ya kikao cha Rais Samia Suluhu Hassan na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Kimataifa (IMF), Kristalina Georgieva kilichofanyika kwa njia ya mtandao mwanzoni mwa mwezi huu ambapo pamoja na mambo mengine walijadili kuhusu athari za kiuchumu na kijamii zilizotokana na changamoto za janga Corona (COVID- 19).

Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba alipokutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa IMF nchini, Jens Reinke katika ofisi za Wizara hiyo.

Mwigulu alisema wamekutana ili kutafsiri maelekezo hayo katika utekelezaji ili kuiwezesha IMF kushirikiana na Tanzania katika kujenga uchumi ambao umekumbana na misukosuko inayoendelea duniani inayotokana na changamoto za janga la Corona.

Tumekutana na IMF pamoja na Wataalam wa Wizara na baadhi ya taasisi zake kujadili namna ya kuandaa taarifa ya maeneo yaliyoathirika zaidi na misukosuko hiyo pamoja na kuangalia kiwango cha athari katika maeneo husika”, alisema.

Alisema athari za misukosuko hiyo ya uchumi zinatofautiana kisekta kwa kuwa kuna sekta ambazo zimeathirika moja kwa moja kama biashara, utalii na makusanyo, na kuna zile ambazo haziathiriki moja kwa moja.

Waziri huyo alisema, wataangalia athari za misukusuko hiyo katika huduma za jamii kwa upana wake kama huduma za Afya hususani kuboresha miundombinu, dawa na upatikanaji wa vifaa tiba pamoja na suala la upatikanaji wa maji.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa IMF nchini, Jens Reinke alisema shirika hilo lipo tayari kushirikiana na Tanzania ili kuhakikisha uchumi wa nchi unakuwa kwa kasi kama ilivyopangwa.

Katika hatua nyingine, Mwigulu  amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika anayeshughulikia Maendeleo na Biashara Afrika Mashariki, Nnenna Nwabufo kuhusu namna bora ya kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na benki hiyo.

Alisema Serikali itaufanyia kazi ushauri na mapendekezo yaliyotolewa na benki hiyo ili kuhakikisha kuwa miradi yote inayofadhiliwa inatekelezwa kwa haraka kama ilivyopangwa.

“Benki ya Maendeleo ya Afrika ni miongoni mwa benki ambazo zinatoa fedha nyingi katika kuhudumia miradi nchini hususan miradi ya miundombinu, na kesho Mwakilishi wa Benki na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha watasaini mkataba kule Dar es Salaam kwa ajili ya miradi”, alibainisha.

Alisema kwasasa benki hiyo inafadhili miradi ya miundombinu takribani 22 ikiwemo mradi wa ujenzi wa barabara za mzunguko mkoani Dodoma na mradi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato jijini Dodoma.

Afafanua kuwa Serikali inangojea utekelezaji wa benki hiyo kuwezesha Tanzania kunufaika zaidi na madirisha ya mikopo inayotolewa ili kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa miradi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika anayeshughulikia Maendeleo na Biashara Afrika Mashariki, Nwabufo alisema benki hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali.

Alisema benki hiyo iko tayari kuyafanyia kazi mambo yote muhimu waliyojadili ikiwa ni pamoja na kuwezesha Tanzania kunufaika zaidi na madirisha ya mikopo inayotolewa.

Nwabufo alimpongenz Rais, Samia  kwa kupata nafasi hiyo na kutoa salam za pole kutokana na msiba mzito ulioikumba nchi kwa kuondokewa na Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dk. John Magufuli.


WANANCHI TUNDURU WATAKIWA KUTUMIA VYEMA UJUZI WA KUKABILIANA NA TEMBO

$
0
0

Afisa Wanyamapori Wilaya ya Meatu, Revocatus Menei akitoa maelekezo ya namna ya kutumia tochi maalum kufukuza tembo kwa baadhi ya wanakijiji cha Jakika Wilaya ya Tunduru katika mafunzo kwa vitendo yaliyofanyika jana kijijini hapo.

Mratibu wa Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori (WWF) Kanda ya Kusini, Richard Katombo akionesha namna ya kutumia mizinga ya nyuki kufukuza tembo aliyevamia makazi ya watu, onyesho lililofanyika katika kijiji cha Jakika Wilayani Tunduru jana.

Mtafiti wa Wanyamapori kutoka Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori (TAWIRI), Dkt. Emmanuel Masenga akionesha namna ya kuchanganya pilipili na oili chafu itakayotumika kumfukuza tembo aliyevamia makazi ya watu,onesho lililofanyika kijiji cha Jakika Wilayani Tunduru.

Mtafiti wa Wanyamapori kutoka Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori (TAWIRI), Dkt. Emmanuel Masenga akionesha namna ya kutumia fataki kumfukuza tembo aliyevamia makazi ya watu,onesho lililofanyika kijiji cha Jakika Wilayani Tunduru. Wanaoshuhudia ni ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori (TAWIRI), Dkt. Janemary Ntalwila (kushoto) na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii, Silvanus Okudo (wa pili kutoka kushoto).

Wahitimu wa mafunzo ya kupunguza migogoro baina ya binadamu na wanyama waharibifu kama tembo wakionyesha wanavijiji kwa vitendo namna ya kutumia honi kuwafukuza tembo katika kijiji cha Jakika Wilayani Tunduru jana. Wa kwanza kulia ni Afisa Wanyamapori Wilaya ya Meatu, Revocatus Menei.

Baadhi ya wanakijiji cha Jakika Wilaya ya Tunduru wakionyesha kwa vitendo namna ya kutengeneza bomu la pilipili linalotumika kumfukuza tembo mara baada ya kupewa mafunzo hayo na Watendaji kutoka Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori (TAWIRI), jana kijijini hapo.

Wananchi waliopewa mafunzo ya kukabiliana na tembo wakionyesha kwa vitendo namna ya kutumia wigo wa pilipili na oili chafu ili kumfukuza tembo aliyevamia makazi ya watu onesho lililofanyika katika kijiji cha Jakika Wilayani Tunduru jana.

************************


Na Happiness Shayo -TUNDURU

 

Wananchi 20 kutoka vijiji vya Wilaya ya Namtumbo na Tunduru waliopewa mafunzo ya ulinzi wa wanyamapori na namna ya kukabiliana na wanyama wakali na waharibifu kama tembo wametakiwa kuhakikisha wanautumia vizuri ujuzi huo ili kuilinda jamii inayokabiliwa na tatizo la kuvamiwa na tembo.

 

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mhe. Julius Mtatiro wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kupunguza migogoro baina ya binadamu na wanyama waharibifu kama tembo yaliyofanyika katika ukumbi wa Klasta Wilayani Tunduru.

 

“ Ndugu zangu ambao mmekuja kwenye haya mafunzo msiende kuyaweka kabatini, muende mkayafanyie kazi na mkatoe elimu kwa wananchi na mtumie mafunzo haya kuwadhibiti wanyama waharibifu ” Mhe. Mtatiro amefafanua.

 

Aidha, amewaasa wakufunzi hao kuwa wepesi kutoa taarifa za uvamizi wa wanyamapori waharibifu katika makazi ya watu pindi inapotokea.

 

“Nimewakamata wenyeviti kadhaa wanaochukua rushwa na kuruhusu ng’ombe kuingia hifadhini, lakini hii haitasaidia isipokuwa tu pale ambapo mtaamua kutoa taarifa kwa watendaji wa vijiji na ofisi ya mkuu wa wilaya mnapoona makundi ya ng’ombe hifadhini” Mhe. Mtatiro amesema.

 

Mhe. Mtatiro amewaagiza wakufunzi hao kuhakikisha wanawaelimisha wananchi wengine juu ya mbinu mbalimbali walizojifunza za namna ya kukabiliana na wanyama wakali na waharibifu na pia kuzalisha watu wengi kwenye maeneo yao ambao wana weledi wa udhibiti wa wanyamapori wakali na waharibifu ili jamii ibaki salama.

 

Akizungumza kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori (TAWIRI), Dkt. Janemary Ntalwila amesema kuwa mafunzo hayo yamejikita katika kuelezea njia rafiki za kukabiliana na uvamizi wa tembo.

 

“ Njia zitakazotumika ni njia rafiki na za gharama nafuu kwa mfano matumizi ya mabomu ya pilipili , tochi maalum za kufukuzia tembo, fataki, honi, mizinga ya nyuki, uzio wa vitambaa vilivyolowekwa kwenye mchanganyiko wa oili chafu na pilipili ” Dkt. Ntalwila ameongeza.

 

Dkt. Ntalwila amesisitiza kuwa, njia hizo zikitumika ipasavyo zitasaidia kuboresha maisha ya wananchi kwa kusaidia kuongeza kipato akitolea mfano matumizi ya njia ya mizinga ya nyuki ambayo ina uwezo wa kufukuza tembo na pia kutoa asali, nta na gundi ya nyuki.

 

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Wanyamapori kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii Silvanus Okudo amesema mafunzo hayo yatasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la uvamizi wa tembo.

 

”Nia ya Serikali ni kuisaidia jamii kupunguza au kuondokana kabisa na tatizo hili la kuvamiwa na wanyama wakali na waharibifu na tunaamini kuwa wakufunzi hawa watajitahidi kuzuia changamoto hiyo kabla haijajitokeza” amesema Bw. Okudo.

 

Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Amiri Abeid ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Libangu Wilaya ya Namtumbo amesema kuwa mafunzo hayo yatawawezesha wanavijiji kuwadhibiti wanyama wakali na waharibifu pindi wanapovamia makazi yao.

 

“Lengo la mafunzo haya ni kutuwezesha namna ya kuishi na kukabiliana wanyama wakali na waharibifu kama tembo lakini pia kuchukua ujuzi na kwenda kuwafundisha wanavijiji wengine” amesema Bw. Abeid.

 

Mafunzo ya kudhibiti wanyama wakali na waharibifu yamehudhuriwa na wakufunzi ishirini kutoka vijiji vya Wilaya ya Namtumbo na Tunduru na yameandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).

Vyuo Vikuu vyahimizwa kufanya tafiti zenye tija kijamii na kiuchumi

$
0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo (kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Mhadhiri Mwandamizi Idara ya Sayansi na Teknolojia, Dk. Lilian Kaale alipotembelea banda la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kabla ya kufunga Maadhimisho ya Sita ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu yaliyoandaliwa na chuo hicho.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo (katikati), akipata maelezo alipotembelea banda la NMB kabla ya kufunga Maadhimisho ya Sita ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo, akifunga Maadhimisho ya Sita ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo (kulia), akimkabidhi tuzo ya
ya Mtafiti Bora aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Rwekaza Mukandala wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Sita ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu yaliyoandaliwa na chuo hicho.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo (kulia), akimkabidhi tuzo ya Mtafiti Bora wa Mwaka Dk. Samwel Mchele Limbu, wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Sita ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

 

Mshindi wa Kwanza wa Mradi Bora wa Utafiti Dk. Mwita Mangora, akipokea mfano wa hundi ya Sh. Mil. 20 kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo, wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Sita ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).


Hussein Ndubikile, Dar es Salaam 


Vyuo Vikuu nchini vimehimizwa kujikita katika tafiti na bunifu endelevu zitakazosaidia kutatua changamoto mbalimbali za jamii pamoja na kuchochea maendeleo ya uchumi wa nchi.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Profesa Joyce Ndalichako wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Sita ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Amesema kuwa vyuo hivyo vinatakiwa kufanya tafiti zitakazoweza kujitofautisha na taasisi zingine za elimu na kwamba zilenge katika kuisaidia jamii kupunguza changamoto na kuleta maendeleo.

" Vyuo Vikuu lazima vifanye tafiti za kuilenga jamii visipofanya vitakuwa havina utofauti na shule za kawaida tafiti ziibue majibu kusaidia nchi kimaendeleo," amesema Dkt. Akwilapo.

Amebainisha kuwa tafiti zinazofanywa na vyuo vikuu huvisaidia kujiweka karibu na jamii pamoja na kujitangaza kimataifa kwani matokeo ya tafiti husambazwa sehemu mbalimbali.

Amekipongeza chuo hicho kwa kuandaa maadhimisho hayo kwa kutenga fedha zake za ndani huku kwani kinaonyesha dhahiri kilivyojipanga kutatua kero za jamii na kuchochea maendeleo ya viwanda.

Ameongeza kuwa wizara hiyo iko pamoja na UDSM kimahusiano na kwamba ni mojawapo ya chuo kinachotambulika kwa ufanyaji tafiti zenye tija kwa nchi.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa William Anangisye amesema maadhimisho ya kilele cha wiki hiyo yamelenga kuonyesha jinsi gani UDSM haijajitenga na jamii kupitia tafiti na bunifu zilizowasilishwa.

Amesisitiza kuwa wiki hiyo ni kiungo muhimu kati ya chuo na umma huku akiwapongeza washindi na walioshinndwa kuendelea kutafuta kuendelea kutafuta mawazo mengine ya utafiti na ubunifu.

Amefafanua kuwa chuo hicho kitatekeleza agizo la Waziri Mkuu Kassim Maajaliwa linaloelekeza kuhakikisha tafiti wanazofanya zinakuwa na mwelekeo wa kiuchumi.

Naye Naibu Makamu Mkuu wa Utafiti wa chuo hicho Profesa Bernadeta Killian amesema maadhimisho hayo yalianza mwaka 2015 yakijulikana kama wiki ya utafiti na baadaye yalifanyiwa maboresho ya jina lake.

Profesa Bernadeta amesema jumla ya kazi 218 za vitengo ziliwasilishwa zikiwemo za wafanyakazi na wanafunzi ambapo washiriki 1,000 wamehudhuria wiki hiyo.

Aidha, amesema maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kauli mbiu isemayo Utafiti na Ubunifu kwa Maendeleo ya Viwanda na Jamii Tanzania na kwamba kulikuwa na mawasilisho ya makampuni, wanafunzi na viongozi wa serikali
 
Katika kilele hicho tuzo na hundi za fedha taslimu zilizotolewa ikiwemo ya Jarida bora la mwaka 2021, Tuzo ya Idara iliyoleta fedha nyingi za utafiti chuoni hapo ilikwenda kwa Shule ya Biashara iliyoleta Sh Bil 2.5, Mtafiti hodari wa mwaka 2021 imechuliwa na Dkt.Samwel Lyimo amepata Sh mil 5.

Tuzo nyingine ni ya Mbunifu hodari aliyepata ni Dkt.Budeba kutoka Chuo cha Kishiriki cha Elimu cha Dar es Salaam (DUCE) amepata tuzo ya ngao na hundi ya Sh mil 5 huku Tuzo ya Miradi Bora ya Makundi ikienda kwa  Mshindi wa kwanza Dkt.. Mwita Mangira aliyepata hundi ya Sh mil 20.

Mwakinyo kumpa asante Rais Samia kwa kumchapa Mayala

$
0
0

Bondia Hassan Mwakinyo ameahidi kumpa kipigo kikali mpinzani wake  Antonio Mayala kutoka Angola ikiwa asante kwa Rais wa kwanza mwanamke wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan.

Mwakinyo ambaye atawania mkanda wa Afrika (ABU) wa uzito wa Super welter atapanda ulingoni  kesho kwenye ukumbi wa Next Door Arena, Masaki katika pambano lililoandaliwa na kampuni ya Jackson Group Sports.

Alisema kuwa amejiandaa vyema na kwa vile atakuwa anapigana kwa mara ya kwanza chini ya uongozi wa Rais Samia, hatofanya makosa zaidi ya kushinda katika raundi  za mwanzoni tu katika pambano hilo lililodhaminiwa na KCB Bank, Plus TV, Multichoice Tanzania, Tanzania Tourism Board, Onomo Hotel, Precision Air, Prestine Logistics, Urban Soul na washirika wa kimataifa Global Boxing Stars na Epic Sports Entertainment.

“Nitakuwa napigana kwa mara ya kwanza chini ya Rais Mama Samia Suluhu Hassan. Sitamwangusha Rais na watanzania kwa ujumla, nawaomba mashabiki kufika kwa wingi ili kunipa sapoti,” alisema Mwakinyo.

Wakati Mwakinyo anasema haya, mpinzani wake Mayala amesema kuwa pamoja na kupata taarifa za muda mfupi, amejiandaa vyema ili kuonyesha kuwa yeye ni bondia wa ngumi za kulipwa.

“Nimekuja kwa ajili ya kushinda na si kupoteza, nilikuwa nafanya mazoezi kwa sababu ngumi ni kazi yangu na siwezi kuruhusu  Mwakinyo kushinda  na kuchukua mkanda wa Afrika,” alisema Mayala.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Jackson Group Sports, Kelvin Twissa amesema kuwa mbali ya pambano hilo, pia bondia Daniel Matefu atazichapa na bondoa kutoka Bulgaria Pencho Tsvetkov huku bondia wa kike Leila Yazidu atazichapa na bondia wa Bulgarian Joana Nwamerue.

Pia bondia Hamisi Palasungulu atazichapa na bondia wa Congo Brazzaville Ardi Ndembo  huku Imani Daudi Kawaya akionyeshana kazi na bondia kutoka Afrika Kusini  Chris Thompson.

Pambano lingine la ABU litakuwa kati ya bondia Shabani Jongo  chini ya Mnigeria Olanrewaju Durodora ambao watawania uzito wa juu na nyota mwingine  Ibrahim Class atazipiga na bondia wa Afrika Kusini, Sibusiso Zingange.

Mabondia wa kigeni na  makocha mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja tayari kwa kupambana na wapinzani wao wa Tanzania katika pambano la Rumble in Dar 2 lililoandaliwa na kampuni ya Jackson Group Sports.

MKUU WA MKOA WA PWANI AKUTANA NA WADAU WA ZAO LA KOROSHO WILAYANI RUFIJI KUJADILI NJIA ZA KUFANIKIWA

$
0
0

 

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Aboubakar Kunenge akizungmza katika kikao cha wadau wa zao la Ufuta kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha ufundi stadi  cah (FDC) ambacho kilihudhuliwa na viongozi mbali mbali wa seriklai kwa lengo la kuweza kujadili mikakati ya kukza zao hilo.


Baadhi ya wadau wa zao la Korosho waliohudhulia katika kikao hicho ambacho kilikuwa na lengo la kujadili mambo mbali mbali juu ya suala hilo.

 

 

NA VICTOR MASANGU, RUFIJI

 

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Aboubakar Kunenge amekerwa na madhaifu mbali mbali yaliyopo kwa baadhi ya watendaji kutokuwa na tabia ya ucheleweshwaji wa Pembejeo za kilimo hali ambayo inawakwamisha wakulima kutoweza kufanya shuguli zao za kilimo kwa ufanisi ambao unatakiwa.

Kungenge ametoa kauli hiyo wakati akiendesha  kikao cha wadau mbali mbali wa zao la Ufuta kilichofanyika katika ukumbi wa cho cha ufundi stadi (FDC) Wilayani Rufiji amabpo kilihudhuliwa na wadau  mbali mbali wa maendeleo pamoja na viongozi wengine wa serikali wa ngazi za Wilaya na Mkoa.

 

Pia Mkuu   aliongeza kuwa anasikitishwa sana na kuona baadhi ya watendaji na viongozi wengine kuwa na urasimu na kuwataka wabadilike na kuhakikisha kwamba wanaweka mikakati madhubuti ambayo itawasaidi wakulima hao waweze kulima kilimo chao amabcho kina tija katika Mkoa wa Pwani.

“Kwa kweli  kwa upande wangu nina kerwa sana na madhaifu ambayo ambayo yanafanywa na baadhi ya watendaji wety, jambo hilo sio sawa kabisa hata kidogo na wengine bado wana tabia ya kufanya ursarimu lakini lengo letu sisi ni kuona wakuli wa zao la ufuta kwa kushirikiana na serikali wanalima killomo chenye tija.”alisema Kunenge.

 

Kadhalika aliwataka viongozi kuweka mpango kabambe ambao utaweza kuondokana na changamoto ya uhaba wa vifungashio vya ufuta na kwamba ataendelea kuwapa ushirikiano wa kutosha ili waweze kutimiza malengo yao waliyojiwekea.

Pia Kunenge aliongeza kuwa  katika kuwasaidia wakulima wa zao la ufuta kunaitajika ushirikiano madhubuti kutoka kwa wadau mbali mbali wa zao hilo ili kuweza kusimamia zoezi zima la uendeshaji wa  mnada wa kwanza  bila ya kuwa na ucheleweshwaji wowote.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa  aliwataaka wakulima  wote  kulima kilimo chenye Tija, na kuahidi kuwa serikali ya awamu ya sita ipo tayari  kuwasaidia ili waweze kuzalisha kwa kiwango kinachotakiwa na chenye kuleta mafanikio kwa Mkoa.

 

Kungene katika kikao hicho aliwaagiza Wataalamu mbali mbali wa kilimo pamoja na Ofisi yake  kufanya Tathmini ya zao hilo na kuja na Mkakati  endelevu ambao utaleta matokeo chanya katika sualazima la kukuza kilimo cha zao la ufuta katika Mkoa wa Pwani.

ALICIOS AJA NA KIMYAAAA, KIZITOOO

$
0
0


Mwanamuziki Mashughuli kutoka Congo na Afrika Mashariki - ALICIOS baada ya kutoa albamu yake 2020 na kufanya vizuri katika Mitandao maarufu ya kusikiliza muziki ndani na nje ya afrika .

Mwezi huu wa Tano (May) amekuja na Wimbo mpya “KIMYA” ambao unazungumzia mapenzi kwa namna ya kuridhia na kuyafurahia kiasi cha kuongeza kadri siku zinapozidi kwenda.

Licha ya Mji anaotoka Congo - GOMA kukumbwa na mlipuko wa Volcano tena siku ambayo alitoa wimbo huu, habari njema ni kuwa yuko mbioni kufanya changizo kusaidia wahanga wa volcano. Kwa kirefu zaidi tembelea kwenye account zake za mitandao ya kijamii @alicioscongo

“Kimya imetengenezwa na Mtayarishaji wa muziki kutoka Congo anayeitwa MASTOLA MUSIC, na imeandikwa na Alicios mwenyewe.

Unaweza kuusikiliza kupitia platform zote za kusikiliza muziki duniani na kwakubonyeza link hii

WILAYA YA MANYONI YAZINDUA TASAF AWAMU YA TATU SEHEMU YA PILI

$
0
0

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa  Mfuko wa Maendeleo wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) kutoka Makao Makuu,, Peter Lwanda akisoma taarifa ya TASAF Awamu ya Tatu Sehemu ya  Pili wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika jwilayani humo mkoani Singida jana.

Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Rahabu Mwagisa, akizungumza katika uzinduzi huo.

Mwenyekiti wa Halmashauri wa Wilaya ya Manyoni, Jumanne Mgalaza, akitoa mkazo kkwa Madiwani kwenda  kuhakikisha walengwa ndio wanaonufaika na mpango huo.


Wawezeshaji  wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya hiyo na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa TASAF na Viongozi wa Halmashauri.ya Manyoni.



 Alinikisya Humbo na Dotto Mwaibale, Manyoni

MKUU wa Wilaya ya Manyoni,  Rahabu Mwagisa amezindua kikao kazi cha kujenga uelewa kuhusu kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya TASAF.

Akizungumza na wawezeshaji waliofika ili kupata mafunzo hayo Mwagisa alisema kuwa madhumuni ya mpango wa kipindi cha pili ni kuwezesha Kaya za walengwa kutumia fursa za kuongeza kipato, kuboresha huduma za jamii na kiuchumi, na kuwezesha katika maendeleo ya Watoto ambao ni raslmali watu.

Mwagisa ameishukuru Serikali ya awamu ya sita na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasan kwa kuendelea kuuborehsa mpango huu wa TASAF na kuona tija ya kuzisaidia kaya hizo maskini ili ziweze kunufaika. 

Aidha amewataka wawezeshaji kuzingatia mafunzo watakayopatiwa na wataalamu  na kwamba wazingatie na kuhakikisha mpango unawafikia walengwa pindi watakapokuwa uko vijijini na wafuate miongozo iliyowekwa na kuwa makini.

“Nitoe rai kwenu wote kuzingatia mafunzo haya na kuhakikisha mnatekeleza mpango kazi huu mtakapokuwa huko vijijini basi mkazingazitie miongozo mliyopewa na kuhakikisha walengwa wote wananufaika na mpango huu”alisema  Mwagisa.

Akisoma hotuba mbele ya Washiriki wa Mafunzo hayo Afisa  Mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA ) wa TASAF,  Peter Lwanda amesema kuwa  kipindi cha awamu ya tatu ya mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAFIII) kinatekelezwa katika 
Halmashauri zote 184 za Tanzania Bara na Wilaya zote za Zanzibar..

Aidha ameongeza kuwa kipindi cha pili cha awamu ya tatu TASAF kitafika kaya milioni moja laki nne na nusu zenye jumla ya watu zaidi ya million saba nchi nzima.

“Mkazo mkubwa katika kipindi hiki cha pili umewekwa katika kuwezesha kaya zitakazoandikishwa kwenye mpango kufanya kazi ili kuongeza kipato”alisema Lwanda.

Lwanda alisema kuwa kipindi hiki cha pili kitahakikisha kwamba huduma za jamii zinaongezwa na kuboreshwa ili kutoa huduma na kuendeleza rasilmali Watoto hususani katika upatikanaji wa Elimu na Afya.

Akitaja walengwa wa awamu hii ya pili Lwanda amesema kuwa ni kaya zinazoishi katika hali duni kwenye Vijiji,Mitaa na, Shehia na kwamba wanufaika ndani ya kaya ni Watoto wenye umri chini ya miaka mitano wanaohudhuria kliniki,wanafunzi wa  shule za awali,shule za msingi na shule za sekondari,mama wajawazito na mwanakaya mwenye ulemavu.

“Niseme tu kwamba mpango huu unatoa ruzuku za aina mbili,ruzuku ya msingi na ruzuku ya masharti kwa wale ambao wanatakiwa kwenda shuleni na Watoto wanaohudhuria kliniki”alisema Lwanda.

Hata hivyo Lwanda alisema kuwa kuna ajira mpya ambazo pia zitaweza kuwanufaisha mwanakaya mmoja ambaye ataonekana kuwa na uwezo wa kufanya kazi. 

Lwanda  amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji Charls Fuss kwa kutoa wawewzeshaji wengi na hasa ngazi ya kata ili kuja kushiriki mpango kazi huo.

Naye Mratibu wa TASAF Wilaya ya Manyoni Kenenan Kidanka ameshukuru wataalamu hao kwa kuweza kuiweka Wilaya ya Manyoni katika mpango huu kwa awamu nyingine tena na kuwaweka watu wenye ulemavu katika mpango huo.

Kidanka alisema  kuwa watahakikisha wanaweka usimamizi na mkazo zaidi ili kuhakikisha mpango unawafikia walengwa katika vijiji vyote na kaya zote.

“Nitoe shukrani kwa wataalamu kuweza  kuiweka Manyoni katika mpango na awamu hii na hasa niwashukuru pia kwa kuwakumbuka na watu wenye ulemavu nao kuingia kwenye mpango huu tunashukuru sana”alisema Kidanka.
 

JAMII YA WAFUGAJI MBARALI KUNUFAIKA NA MAFUNZO YA MKURABITA KUBORESHA MAISHA YAO

$
0
0


Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), Anthony Temu  (wa pili kulia) akiwaelekeza maafisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, jinsi ya kujaza dodoso kwa kutumia mfumo wa ukusanyaji taarifa kwenye simu janja alipofanya nao kikao cha maandalizi ya kwenda kutoa mafunzo  ya kuijengea uwezo jamii ya wafugaji katika Kitongoji cha Mogelo wilayani humo. Kutoka kushoto ni Afisa Mifugo, Abbas Mubanga, Afisa Kilimo, Issa Mwambela na Afisa Ushirika, Grace Samwel.
 
Na Mwandishi Wetu
 
 JAMII ya wafugaji ambao wengi wao ni wamasai kupatiwa mafunzo na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara wa Wanyonge Tanzania (MKURABITA) ya kuwajengea uwezo kiuchumi  jinsi ya kuboresha mifugo yao na kilimo kwa kutumia hati miliki za kimila kama dhamana kukopea fedha benki na taasisi zingine za kifedha.

Akizungumza wakati wa kikao cha maandalizi ya mafunzo hayo, kilichohudhuriwa na maafisa wa Halmashauri ya Wilaya Mbarali, mkoani Mbeya, Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mkurabita, Anthony Temu amesema mafunzo hayo yanafanyika katika Kitongoji cha jamii ya wafugaji cha Mogelo kesho Mei 27,2021.

Ametaja mafunzo watakayopatiwa kuwa ni; kuboresha mifugo yao, Kanuni za kilimo bora, kuthaminisha mali zao, jinsi ya kutunza kumbukumbu za mahesabu, faida za ushirika, kuchangamkia fursa mbalimbali ikiwemo mikopo kwa kutumia hati miliki za kimila kama dhamana, faida za kujiunga na mabenki kwa ajili ya mikopo na ufugaji bora wa nyuki wa asali.

Kabla ya kikao na maofisa hao, Temu alikutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Kivuma Msangi ambapo alijitambulisha na kumueleza jinsi mafunzo hayo yatakavyoendeshwa na kuinufaisha jamii hiyo ya wafugaji.

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza clip hii ya video ujue kilichozungumzwa kuhusu maandalizi ya mafunzo hayo yatakayohudhuriwa na zaidi ya kaya 60 za jamii ya wafugaji......

Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>