Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

NMB Bonge la Mpango - Mkazi wa Chamwino anyakua gari aina ya TATA Ac

$
0
0

Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Benki ya NMB-Benedicto Baragomwa akimkabidhi kadi ya gari aina ya Tata Lifan alimaarufu Kirikuu ,Jacqline Kihongozi, aliyepokea kwa niaba ya mshindi wa kampeni ya bonge la Mpango inayoendeshwa na NMB, Hadija Idd Mkazi wa Chamwino mkoani Dodoma ambaye ndiye mshindi wa kwanza kujishindia zawadi ya gari aina ya Tata Ace kwenye kampeni hii. Akishuhudia ni Meneja wa NMB Kanda ya Kati- Nsolo Mlozi.

Kwa niaba ya mshindi wa kwanza wa gari aina ya Tata Ace kwenye kampeni ya Bonge la Mpango - Hadija Idd Mkazi wa Chamwino mkoani Dodoma,  ambaye ndiye mshindi wa kwanza kujishindia zawadi ya gari aina ya Tata Ace kwenye kampeni hii - Jacqline Kihongozi akifungua gari hilo(Lifan) baada ya kukabidhiwa  na Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Benki ya NMB-Benedicto Baragomwa katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika Tawi la NMB Chamwino. Akishuhudia ni Meneja wa NMB Kanda ya Kati- Nsolo Mlozi.
 
 
Na Mwandishi Wetu
 

Hadija Iddi mkazi wa Chamwino mkoani Dodoma amekuwa mshindi wa kwanza kuzawadiwa gari aina ya TATA Ace maarufu kama Kirikuu yenye thamani ya sh. Millioni 25, baada ya kushinda katika kampeni ya Bonge la Mpango inayoendeshwa na Benki ya NMB.

 

Akimkabidhi gari hiyo Bi. Hadija, Kaimu Afisa Mkuu Ukaguzi wa Ndani wa NMB, Benedicto Baragomwa alisema, Bonge la Mpango inaendelea nchini kote na zawadi mbakimbali zinaendelea kutolewa, hivyo wateja wanaendelee kufungua akaunti na kuweka hela kuanzia sh. 100,000 kwenye akaunti zao za NMB ili waweze kuingia katika kinyanganyiro cha Zawadi mbalimbali zinazotolewa katika kampeni hii ikiwemo, gari ya kifahari aina ya Toyota Fortuner mpya yenye thamani ya Sh.169 milioni, gari ya miguu mitatu(Lifan) na pesa taslimu.

 

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa gari hilo, Hadija aliishukuru benki ya NMB na kusema kuwa gari hilo litamsaidia katika shughuli zake za kujiongezea kipato lakini pia akawashauri watanzania kuwekeza katika benki hiyo kwani ndiyo benki bora Tanzania na pia inawajali wateja wake kwani amekuwa shahidi.

 

"Nimeamini kuwa yanayozungumzwa ni kweli,nimekabidhiwa gari mpya,nimepewa ufunguo na Kadi ya gari vikiwa kamili kabisa, kweli NMB ndiyo mpango mzima,"alisema Hadija.

 

Wakati huo huo, Meneja wa NMB Kanda ya Kati - Nsolo Mlozi na mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania walichezesha droo nyingine kwa ajili ya kuwapata washindi wa wiki, ambapo watu mbalimbali walipata fedha taslimu wakati na Henry Semwanza kutoka Chamwino and Faustine Nyawigrika wa Biharamulo wakijishindia  gari ya mataili matatu (Lifan) mpya kila mmoja.

 

Hadi sasa, NMB imetoa zawadi zenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 145 zikiwemo; fedha taslimu, pikipiki za miguu mitatu aina ya LIFAN na Tata Ace kwa washindi wa Bonge la Mpango.


Katibu Mkuu CCM Chongolo atoa maelekezo katika Wizara tatu

$
0
0

 

Na Hamida Ramadhani, Dodoma


KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Daniel Chongolo amekutana na waandishi wa habari huku akitoa maelekezo ya kuondoa vikwazo kwa wananchi katika Wizara tatu ambazo ni Wizara ya Ardhi Nyumaba na Maendeleo ya Makazi ,Kilimo na Wizara ya Nishati

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma Katibu Mkuu huyo  amesema hadi kufikia 2025 Chama Cha Mapinduzi iliahidi kutunza rasilimali za aridhi ikiwemo kutatua migogoro yote ya ardhi kwani migogoro hiyo ya ardhi imekuwa ikiwapotezea muda wananchi.

Aidha amesema Chama Cha Mapinduzi CCM kupitia ilani yake imeielekeza Serikali kuhakikisha wanatoa hati miliki Katia umiliki wa ardhi na kwakufanya hivyo utawasaidia wananchi kuwa na Usalama wa maeneo yao.

" Tumefanya tathimini na tumegundua kwamba mpaka sasa ni wananchi wachache wanaomiliki ardhi wengi umiliki wa ardhi hawana ," amesema Chongoro.

Pia amesema kwa Upande wa uthaminishaji na fidia Wizara utengeneze  mfuko wa fidia  utakao leta haki kwa wananchi ambapo amewataka Viongozi wote wa ngazi zote kuhakikisha wanatatua migogoro ya ardhi katika maeneo yote yalionekana kuwa na migogoro.

KWA UPANDE WA MABARAZA YA ARDHI

Amesema Mabaraza ya ardhi yapewe fursa ya kusikiliza nakutatua changamoto mbalimbali na kuachana na mfumo wa kutoa hukumu na badala yake wahahikishe wanatoa Suluhu ya migogoro hiyo.

Amesema katika suala Zima la upimaji wa ardhi wahahikishe wanapima maeneo Ili kuyapanga na kuondoa ukuaji holela wa miji usiopanga.

" Pia Wizara ya Aridhi Nyumba  na Maendeleo ya makazi  kuhakisha wanaandaa mfumo wa utambuzi  kwa maeneo yanayoonekana kukua kwa kasi ili kuepuka kuwa na miji usiopanga," amesema Chongoro.

WIZARA YA  KILIMO 
 
Amesema Kilimo ndio Wizara mama ambayo inabaeba Watu wengi asilimia 70 hadi 80 wapo wananchi wamejikita kwenye Kilimo.

" Sisi kama Chama tawala tumeiona tuishauri Serikali kwenye bajeti ya Mwaka 2021/2022 kuweka mkazo Kilimo cha umwagiliaji kwani kwasasa ndio kimbilio la wengi wakulima kutokana na mvua zisizo  eleweka," amesema 

Amesema ili kukuza maeneo ya uzalishaji hekta Milioni 1.2 zitengwe na kila mwaka watenge maeneo ya umwagiliaji na sikimu za zilizoazishwa kujenga zikamilike na kwakufanya hivyo wigo wa uzalishaji wa Kilimo utaonekana.
 
MBEGU

Amesema changamoto kubwa kwa wakulima ni upatikanaji wa Mbegu bora hivyo Sisi kama Chama tawala tunaishauri Serikali kuweka bajeti ya Utafiti wa Mbegu bora Ili kuwapa uhakika wa mazao yao wakulima .

Amezitaka Taasisi zote zinazoshughulika na masuala ya tafiti zijiekekeze na ziwezeshwe Ili ziweze kutoka Mbegu bora.

" Ili kuwakuza wakulima wetu tunaishauri Serikali kupitia bajeti hii ya kilimo inayotalijiwa kusomwa hivi karibuni Wizara ya kilimo ijikite katika kutoa mikopo yenyemanufaa kwa wakulima ikiwemo pembejeo," amesema.

WIZARA YA NISHATI

Amesema kupitia bajeti ya mwaka 2021/2022  Chama Cha Mapinduzi CCM kinaelekeza yafuatayo kuweka kipaumbele katika upatikanaji wa umeme sehemu zote.

Pia amesema Chama kimesokitishwa na wale wote waliokuwa na nia mbaya au ovu na kusababisha kwa siku ya tati mfurulizo Watu kukuosa huduma ya umeme kuanzia tarehe 17 mwezi wa 5 hadi tarehe 20 mwaka huu.

" Chama CCM kinaonya vikali kwa wale wote watendaji waliokuwa  na nia mbaya kwa wananchi,kwani wananchi Wamepata hasara kwa kitendo hicho cha kukuza umeme kwa muda wa siku tati," amesema .

Sambamba na hayo amesema Ili kuwa na Nishati ya kutosha Chama Cha Mapinduzi kinaelekeza miradi yote ya usafirishaji, usambazaji unatekeleza kwa haraka.

Pia amesema vijiji na vitongoji vote vilivyoachwa katika usambazaji  vipate umeme na umeme uwe wa gharama za chini.

MAFUTA NA GESI ASILIA

Amempongeza  Rais wa Awamu ya Sita Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake katika kuhakikisha Ujenzi wa bomba kubwa la Mafuta inafanyikia kutaka Hoima nchini Uganda mpaka Tanga nchini Tanzanaia.


TMDA Kanda ya Kati yatoa mafunzo kwa wahudumu wa afya

$
0
0

 NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA


MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) mkoani Dodoma imetoa mafunzo kwa watoa huduma wa afya kwa lengo la kupunguza matumizi mabaya ya dawa na vifaa tiba huku ikikumbushwa kuendelea kutoa elimu  kwa jamii juu ya matumizi mabaya ya dawa na vifaa tiba.

Akizungumza  katika mafunzo maalum juu ya matumizi ya dawa,  Kaimu katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma  Aziza Rajabu Mumba  amesema lengo kubwa la kutoa mafunzo kama hayo  ni kuhakikisha   kupuguza madhara makubwa juu ya athari za dawa kwa watumiaji.

Amesema wamewapa elimu wataalamu hao ambao wako kwenye vituo vya Afya ili waweze kudhibiti madhara ya dawa na Vifaa Tiba yasitokee kwa watumiaji.

Aidha Kaimu katibu tawala huyo wa mkoa  ametoa wito kwa mamlaka ya dawa na vifaa tiba[TMDA]kuendelea kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya dawa na vifaa tiba.

Katika hatua nyingine  amesema  kwa sasa hali sio mbaya  hasa kwenye eneo la madhara ambapo , mambo yamekuwa mazuri, kutokana na elimu kuendelea   kutolewa kila wakati kwa jamii kuhusiana na utumiaji wa dawa na vifaa tiba katika afya ya mwanadamu.

Kwa upande wake kaimu meneja wa mamlaka ya dawa na vifaa tiba[TMDA]   kanda  ya kati  Sonia Henry amesema mafunzo hayo dhima yake kubwa ni kuwakumbusha watoa huduma katika majukumu yao ili kuwa makini katika kutoa huduma inayostahili na kulinda afya ya jamii .

" Tumewapa mafunzo watumishi 30 wa sekta hii ya Afya kutoka Halmashauri zote za Dodoma  lengo likiwa ni kuwajengea uwezo Ili waweze kutoa taarifa zitakazosaidia kupunguza madhara kwa wananchi pindi watumuapo dawa na Vifaa Tiba," amesema 

Mamlaka ya dawa na vifaa tiba ni Taasisi ya serikali iliyopo chini ya wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto yenye jukumu la kudhibiti ubora,usalama na ufanisi wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi ili klinda Afya ya jamii.

WATOTO WANUSURIKA KATIKA AJALI BUKOBA

$
0
0

 


Kaimu Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Kagera, Thomas Majuto, akizungumza katika eneo la tukio.

 Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo.
 

 

Na Lydia Lugakila, Bukoba

Watoto wawili wakazi wa Bukoba mkoa Kagera  akiwemo dereva wa gari  aina Scania lenye namba za usajili T351BXG wamenusulika kifo baada ya kufunikwa na mzigo wa cement uliokuwa umebebwa na gari hilo mali ya kampuni ya Magu lililokuwa likitokea  Dodoma kuja Bukoba  kuferi break na kuacha njia kupinduka kisha kuingia kwenye korongo.

Akiwa katika eneo la tukio kaimu Kamanda wa  zimamoto mkoa wa Kagera Thomas Majuto amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa 2:50 baada ya gari hilo kuferi break na kupinduka huku dreva wa gari hilo aliyetambulika kwa jina Rwegasira Devid mwenye umri wa miaka 41 kubanwa  ndani ya gari hilo, huku watoto wawili waliotambuliwa kwa jina la Avitus Renald miaka (7 )na Switbert Nassoro mwenye umri wa miaka 4 wote wakazi wa Bukoba kunusurika kifo.

Majuto amesema kuwa baada ya juhudi za jeshi la polisi na zimamoto kufika eneo la tukio na kumuokoa dreva huyo pamoja na majeruhi wengine wamefanikiwa kuwapeleka katika hispitali ya rufaa ya Mkoa huo kwa ajili ya matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.

Adha kamanda huyo ameongeza kuwa eneo hilo si sahihi kwa matumizi ya barabara na kuwa sio mara ya kwanza na kuwa kamati husika ya usalama itahakikisha inaweka alama zenye kuonyesha alama za mteremko.

Hata hivyo kwa upande wa wao baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo akiwemo Abdalla Muaga na Bashir  wameomba serikali kukarabati maeneo korofi     likiwemo eneo la round about ambalo limekuwa likisababisha ajali mara kwa mara.

Mwigulu aipongeza Benki ya CRDB kuendelea kuwa kinara katika soko

$
0
0

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati alipowasili katika Semina ya Elimu ya Fedha na Uwekezaji iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wanahisa na Watanzania katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC). Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay na Makamu  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Prof. Neema Mori. Semina hiyo ilihudhuriwa na zaidi ya watu 2,000 ambao wengi walihudhuria kupitia mtandao.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba akihutubia katika Semina ya Elimu ya Fedha na Uwekezaji iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wanahisa na Watanzania katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC). Semina hiyo ilihudhuriwa na zaidi ya watu 2,000 ambao wengi walihudhuria kupitia mtandao. 
Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye, akiongoza semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB, jijini Arusha leo Mei, 21, 2021.
Mshauri wa Masuala ya Fedha, Emilian Kusara, akitoa mada juu ya Elimu ya Fedha na Uwekezaji katika semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB  jijini Arusha.
 
 


Na Mwandishi Wetu

 

 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuendelea kuwa kinara wa ubunifu wa huduma na bidhaa katika soko na kutengeneza faida kubwa inayoiwezesha benki hiyo kutoa gawio kwa wanahisa wake.

Dkt. Mwigulu ametoa pongezi hizo wakati wa Semina ya Elimu ya Fedha na Uwekezaji iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wanahisa wake na Watanzania kuelekea Mkutano Mkuu wa Wanahisa unaotarajiwa kufanyika hapo kesho 22 Mei 2021 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).

Akielezea namna ambavyo Serikali inajivunia utendaji wa Benki hiyo, Dkt. Mwigulu alisema Benki ya CRDB imekuwa ikishiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi kwa kusaidia miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali, pamoja na kuwekeza katika kupanua wigo wa ufikishaji huduma na kuongeza ujumuishi wa kifedha kwa wananchi.

“Serikali inaichukulia Benki hii kama Benki kiongozi, na namna ambavyo mmekuwa mkifanya vizuri inadhihirisha hilo. Nimesikia hapa mwaka jana mmetengeneza faida kubwa pamoja na changamoto ya COVID-19, hii inaonyesha uimara wa benki hii na uimara wa sekta ya fedha nchini kwetu, hongereni sana na asanteni kwa kutupa heshima,”alisema Dkt. Mwigulu huku akiwahamasisha Watanzania kuwekeza katika hisa za Benki ya CRDB ili kupata faida.

Dkt. Mwigulu alisema ili sekta ya fedha iweze kufanya vizuri zaidi na uchumi wa Tanzania uendelee kukua kunahitajika elimu ya kutosha juu ya masuala ya fedha na uwekezaji kwa wananchi. Alisema kwakutambua hilo mwaka 2011 Serikali ilianzisha Mpango wa Taifa wa Elimu ya Fedha ikiwa na lengo la kujengajamii yenye uelewa mpana wa masuala ya fedha, kuongeza ujumuishi wa kifedha na kuchochea ukuaji wa uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na taifa.

“Niwapongeze Benki ya CRDB kwa kuwa bega kwa bega na Serikali katika kutoa elimu hii kwa wananchi, hii inaonyesha ni jinsi gani mnaishi maono ya Serikali, asateni sana,”aliongezea Dkt. Mwigulu ambapo pia alibainisha amekuwa akifuatilia semina hizo zinazoendeshwa na Benki ya CRDB ikiwamo ile ya uwezeshaji iliyofanyika mwezi Apri 2021 katika Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Dkt. Mwigulu pia alielezea mikakati mbalimbali inayowekwa na Serikali katika kuboresha sekta ya fedha nchini ambapo alisema Wizara yake inampango wa kuandaa kikao kazi cha mabenki na wadau wengine wa sekta ya fedha ili kujadili changamoto zilizopo na maeneo ya uboreshwaji ili kuweza kufikia lengo. “Naiomba Benki ya CRDB kama Benki kiongozi kuongoza katika hili, naamini mtatusaidia kuyaongoza mabenki na taasisi nyengine za fedha katika hili,”aliongezea Dkt. Mwigulu.

Akitaja baadhi ya mambo ambayo Serikali imapanga kuyajadili, Dkt. Mwigulu alisema ni pamoja na uboreshaji wa sera za usimamizi wa sekta ya fedha, kuboresha upatikanaji wa mikopo kwa wafanyabiashara hususan wajasiriamali wadogo kwa kuhakikisha benki zinatoa mikopo yenye riba rafiki, kuongeza ajira kwa wananchi, kupanua wigo wa biashara katika nchi jirani na kuwajengea wafanyabiashara uwezo wa kushiriki katika biashara katika masoko ya kimataifa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay alimshukuru Dkt. Mwigulu kwa kuikaribisha benki hiyo kushirikiana na Serikali katika kutekeleza mikakati ya kuimarisha sekta ya fedha nchini. Vilevile alimhakikishia kuwa benki hiyo itakwenda kuandaa sera ambayo itakwenda kuelekeza na kusimamia uwezeshaji katika sekta mbalimbali za maendeleo nchini. “Mheshimiwa Waziri nikuahidi kuwa tutakwenda kufanyia maelekezo yako kazi kwa kuweka mikakati itakayoongeza ushiriki wa benki yetu katika kukuza uchumi,” alisisitiza Dkt. Laay.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema malengo ya Semina hiyo ni kuwajengea uwezo Wanahisa wao pamoja na Watanzania wengine ili kuwajengea uwajibikaji wa kifedha na kuongeza  ushiriki katika fursa za uwekezaji hapa nchini pamoja na kupata uelewa wa huduma za benki hiyo zitakazowasidia kuboresha maisha yao.

“Kwa kutoa elimu hii Wanahisa wetu pia wanapata kufahamu zaidi faida za kuwekeza katika Benki yao ya CRDB, hivyo basi kuongeza uwekezaji na kupata faida nono zaidi, lakini pia kuwahamasisha na Watanzania wengine pia kuwekeza katika hisa za Benki ya CRDB na kuanza kupata gawio,” aliongezea Nsekela.

Aidha, Nsekela alisema kuwa mwaka huu Bodi ya Wakurugenzi imependekeza gawio la shilingi 22 kwa hisa kufuatia ikiwa ni ongezeko la asilimia 29.4 kulinganisha na gawio la shilingi 17 kwa hisa lililotolewa mwaka jana ikitokana na kuongezeka kwa faida ya benki hiyo mwaka 2020 kufikia shilingi bilioni 175. “Niwakaribishe Watanzania wengine waje kuwekeza ndani ya Benki yetu ili nawao waanze kunufaika na fursa hii,” alisisitiza Nsekela.

Mada mbalimbali ziliwasilishwa katika Semina hiyo ikiwamo; Elimu ya Fedha na Uwekezaji, Biashara ya Hisa Kidijitali, Huduma za Bima na CRDB Wakala. Washiriki wa Semina hiyo waliipongeza Benki ya CRDB kwa kuandaa semina hiyo huku wakisema imesaidia sana kuongeza uelewa juu ya masuala ya fedha na uwekezaji. Baadhi ya washiriki walipendekeza semina hiyo kufanyika mara kwa mara kwani bado uelewa wa masuala ya fedha na uwekezaji katika jamii bado ni mdogo.

Mwigulu aipongeza Benki ya CRDB kuendelea kuwa kinara katika soko

$
0
0

 

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati alipowasili katika Semina ya Elimu ya Fedha na Uwekezaji iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wanahisa na Watanzania katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC). Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay na Makamu  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Prof. Neema Mori. Semina hiyo ilihudhuriwa na zaidi ya watu 2,000 ambao wengi walihudhuria kupitia mtandao.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba akihutubia katika Semina ya Elimu ya Fedha na Uwekezaji iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wanahisa na Watanzania katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC). Semina hiyo ilihudhuriwa na zaidi ya watu 2,000 ambao wengi walihudhuria kupitia mtandao. 
Mwenyekiti wa Semina ambaye pia ni Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye, akiongoza semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB, jijini Arusha leo Mei, 21, 2021.
Mshauri wa Masuala ya Fedha, Emilian Kusara, akitoa mada juu ya Elimu ya Fedha na Uwekezaji katika semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB inayofanyika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.
 
 


Na Mwandishi Wetu

 

 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuendelea kuwa kinara wa ubunifu wa huduma na bidhaa katika soko na kutengeneza faida kubwa inayoiwezesha benki hiyo kutoa gawio kwa wanahisa wake.

Dkt. Mwigulu ametoa pongezi hizo wakati wa Semina ya Elimu ya Fedha na Uwekezaji iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wanahisa wake na Watanzania kuelekea Mkutano Mkuu wa Wanahisa unaotarajiwa kufanyika hapo kesho 22 Mei 2021 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).

Akielezea namna ambavyo Serikali inajivunia utendaji wa Benki hiyo, Dkt. Mwigulu alisema Benki ya CRDB imekuwa ikishiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi kwa kusaidia miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali, pamoja na kuwekeza katika kupanua wigo wa ufikishaji huduma na kuongeza ujumuishi wa kifedha kwa wananchi.

“Serikali inaichukulia Benki hii kama Benki kiongozi, na namna ambavyo mmekuwa mkifanya vizuri inadhihirisha hilo. Nimesikia hapa mwaka jana mmetengeneza faida kubwa pamoja na changamoto ya COVID-19, hii inaonyesha uimara wa benki hii na uimara wa sekta ya fedha nchini kwetu, hongereni sana na asanteni kwa kutupa heshima,”alisema Dkt. Mwigulu huku akiwahamasisha Watanzania kuwekeza katika hisa za Benki ya CRDB ili kupata faida.

Dkt. Mwigulu alisema ili sekta ya fedha iweze kufanya vizuri zaidi na uchumi wa Tanzania uendelee kukua kunahitajika elimu ya kutosha juu ya masuala ya fedha na uwekezaji kwa wananchi. Alisema kwakutambua hilo mwaka 2011 Serikali ilianzisha Mpango wa Taifa wa Elimu ya Fedha ikiwa na lengo la kujengajamii yenye uelewa mpana wa masuala ya fedha, kuongeza ujumuishi wa kifedha na kuchochea ukuaji wa uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na taifa.

“Niwapongeze Benki ya CRDB kwa kuwa bega kwa bega na Serikali katika kutoa elimu hii kwa wananchi, hii inaonyesha ni jinsi gani mnaishi maono ya Serikali, asateni sana,”aliongezea Dkt. Mwigulu ambapo pia alibainisha amekuwa akifuatilia semina hizo zinazoendeshwa na Benki ya CRDB ikiwamo ile ya uwezeshaji iliyofanyika mwezi Apri 2021 katika Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Dkt. Mwigulu pia alielezea mikakati mbalimbali inayowekwa na Serikali katika kuboresha sekta ya fedha nchini ambapo alisema Wizara yake inampango wa kuandaa kikao kazi cha mabenki na wadau wengine wa sekta ya fedha ili kujadili changamoto zilizopo na maeneo ya uboreshwaji ili kuweza kufikia lengo. “Naiomba Benki ya CRDB kama Benki kiongozi kuongoza katika hili, naamini mtatusaidia kuyaongoza mabenki na taasisi nyengine za fedha katika hili,”aliongezea Dkt. Mwigulu.

Akitaja baadhi ya mambo ambayo Serikali imapanga kuyajadili, Dkt. Mwigulu alisema ni pamoja na uboreshaji wa sera za usimamizi wa sekta ya fedha, kuboresha upatikanaji wa mikopo kwa wafanyabiashara hususan wajasiriamali wadogo kwa kuhakikisha benki zinatoa mikopo yenye riba rafiki, kuongeza ajira kwa wananchi, kupanua wigo wa biashara katika nchi jirani na kuwajengea wafanyabiashara uwezo wa kushiriki katika biashara katika masoko ya kimataifa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay alimshukuru Dkt. Mwigulu kwa kuikaribisha benki hiyo kushirikiana na Serikali katika kutekeleza mikakati ya kuimarisha sekta ya fedha nchini. Vilevile alimhakikishia kuwa benki hiyo itakwenda kuandaa sera ambayo itakwenda kuelekeza na kusimamia uwezeshaji katika sekta mbalimbali za maendeleo nchini. “Mheshimiwa Waziri nikuahidi kuwa tutakwenda kufanyia maelekezo yako kazi kwa kuweka mikakati itakayoongeza ushiriki wa benki yetu katika kukuza uchumi,” alisisitiza Dkt. Laay.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema malengo ya Semina hiyo ni kuwajengea uwezo Wanahisa wao pamoja na Watanzania wengine ili kuwajengea uwajibikaji wa kifedha na kuongeza  ushiriki katika fursa za uwekezaji hapa nchini pamoja na kupata uelewa wa huduma za benki hiyo zitakazowasidia kuboresha maisha yao.

“Kwa kutoa elimu hii Wanahisa wetu pia wanapata kufahamu zaidi faida za kuwekeza katika Benki yao ya CRDB, hivyo basi kuongeza uwekezaji na kupata faida nono zaidi, lakini pia kuwahamasisha na Watanzania wengine pia kuwekeza katika hisa za Benki ya CRDB na kuanza kupata gawio,” aliongezea Nsekela.

Aidha, Nsekela alisema kuwa mwaka huu Bodi ya Wakurugenzi imependekeza gawio la shilingi 22 kwa hisa kufuatia ikiwa ni ongezeko la asilimia 29.4 kulinganisha na gawio la shilingi 17 kwa hisa lililotolewa mwaka jana ikitokana na kuongezeka kwa faida ya benki hiyo mwaka 2020 kufikia shilingi bilioni 175. “Niwakaribishe Watanzania wengine waje kuwekeza ndani ya Benki yetu ili nawao waanze kunufaika na fursa hii,” alisisitiza Nsekela.

Mada mbalimbali ziliwasilishwa katika Semina hiyo ikiwamo; Elimu ya Fedha na Uwekezaji, Biashara ya Hisa Kidijitali, Huduma za Bima na CRDB Wakala. Washiriki wa Semina hiyo waliipongeza Benki ya CRDB kwa kuandaa semina hiyo huku wakisema imesaidia sana kuongeza uelewa juu ya masuala ya fedha na uwekezaji. Baadhi ya washiriki walipendekeza semina hiyo kufanyika mara kwa mara kwani bado uelewa wa masuala ya fedha na uwekezaji katika jamii bado ni mdogo.

KINDOYA : TANZANIA FOOTBALL PLAYER HIS PROFILE MARKET

$
0
0

First Name: Kindoya

Full Name: Abbas Hassan

Nationality: Tanzania

Date of Birth :23.5.2003

Position : Straika Lw,RW

Weight :165Lbs(75)

Height :6'0(183 cm)

Passport No 162030

Favourite foot : right



PLAYER HISTORY

2020:Present - ambassador Super Gym and Sports Club Limited

2019-2020- Gwambina FC

2015-2018-Wakala Msomi Academy

    

  For more informations

Contact Player agent advisor

  James Kitia

Super Gym and Sports Academy Limited

Phone: + 17734744225

Global Ministers Classroom

$
0
0

 

 

 

https://bit.ly/37qQOza.            link hiyo Tafadhali naomba ujisajili na washirikishe Watumishi  wa Mungu  wengine wengi wajisajili


Simba Jamii yasaidia yatima kituo cha UMRA

$
0
0

 >Watoto waiombe ushindi Simba kesho


Watoto Yatima wa Kituo cha Umra kilichopo Magomeni wilayani Kinondoni wakiomba dua pamoja na baadhi ya wawakilishi wa Taasisi ya Simba Jamii Tanzania Enterprise (SJTE), ili kusaidia Klabu ya Simba kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa marudiano na timu ya Kaizer Chief.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Simba Jamii Tanzania Enterprise (SJTE), Patrick Mwanakatwe akikabidhi mashuka 30 kwa Muasisi wa Kituo cha Umra  Rahma Kishumba (katikati) na Mlezi wa Kituo hicho Thuwaybaty Ahmada Nassoro (kushoto) wengine ni watoto.



 
Muasisi wa Kituo cha Umra kilichopo Magomeni wilayani Kinondoni jijini Dar, Ramha Kishumba alielezea furaha waliopata kupatiwa msaada waashuka 30 kutoka Simba Jamii Tanzania Enterprise (SJTE), kutosho ni Mwenyekiti wa SJTE, Patrick Mwanakatwe.
 
 
Na Mwandishi Wetu

TAASISI ya Simba Jamii Tanzania Enterprise (SJTE), imetoa msaada wa mashuka 30 kwa Kituo cha Kulea Watoto Yatima cha Umra kilichopo Magomeni Wilayani Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Msaada huo umekabidhiwa na Mwenyekiti wa SJTE, Patrick Mwanakatwe ambaye aliambata na Mjumbe wa Utendaji Mussa Mongi, Mlezi wa Hassan Mbilili na Mjumbe wa Kamati ya Habari na Matangazo Suleiman Msuya.

Akizungumza baada ya kutoa msaada huo Mwenyekiti wa SJTE, Mwanakatwe amesema dhamira ya taasisi hiyo pamoja na kuishabikia Klabu ya Simba ila wanahakikisha wanatatua changamoto za jamii kwa kujichangisha kidogo walichonacho.

Amesema kwa leo wametoa mashuka 30 kwenye kituo cha Umra ambacho kilikuwa kinahitaji hilo.

Mwanakatwe amesema wamekuwa wakitoa misaada kwa watoto yatima, watu wenye ulemavu kwa kuwapatia viti lengo likiwa ni kuwapunguzia adha mbalimbali.

"Simba Jamii Tanzania Enterprise ni taasisi ambayo inahusika na kuishabikia Klabu ya Simba na huduma za jamii kama kusaidia watoto yatima na wenye ulemavu wa viungo hivyo leo ni zamu ya Umra tunaendelea kujipanga kuendelea kusaidia makundi hayo kila kona ya nchi.

Mashuka 30 tuliyotoa hapa ni sehemu ya msaada wetu na tunaendelea kuchangishana tuweze kuwapatia mahitaji mengine kama magodoro ambayo bado wanahitaji," amesema.

Mwenyekiti amesema SJTE ina wanachama kutoka pande zote dunia ikiwemo Japani, Afrika Kusini, Marekani, Uingereza, Tanzania na kwingineko.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Utendaji SJTE, Mongi amewaomba wana Simba popote walipo duniani kujiunga na taasisi hiyo ili kuweza kusaidia jamii.

Mongi alisema kwa sasa wapo kwenye mikakati mbalimbali ya kuhakisha SJTE inatangazwa zaidi ili kufikia wana Simba wengi.

Mlezi wa Simba Jamii, Mbilili alisisitiza kuwa kupitia taasisi hiyo wameweza kusaidia watu wengi hivyo ni imani yao wataweza kufikia kundi kubwa.

Muasisi wa Kituo cha Umra, Rahma Kishumba amesema wanashukuru kupata msaada wa mashuka 30 kutoka Simba Jamii na kuwataka waendelee kusaidia makundi maalum.

Amesema Kituo cha Umra kina watoto yatima 117 ambao wamewapata katika maeneo mbalimbali hivyo kuwataka wadau wengine kuunga mkono juhudi zao za kulea watoto hao.

"Tunawapongeza SJTE kwa kuweza kutatua changamoto hii ya mashuka kwani ilikuwa inatuumiza vichwa ni imani yetu wengine watakuja kutupatia magodoro," amesema.

Aidha, amesema watoto hao yatima waliopo kwenye vituo vyao vinne ambavyo ni Magomeni, Buza, Mbezi na Vikawe wanahitaji bima ya afya hivyo kuomba wadau kuwasaidia kwenye eneo hilo.

Kishumba amesema watoto hao yatima wanasoka katika shule mbalimbali jambo ambalo linasaidia kutimiza ndoto zao.

Muasisi huyo alitumia nafasi hiyo kuiombea ushindi timu ya Simba dhidi ya Kaizer Chief wanaotarajiwa kuchezwa kesho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini hapa.
 
Kwa upande wao watoto Yasira Dauda na Abdul Hakimu Nassor wameishukuru SJTE kuwapatia zawadi hizo na kuahidi kuzitunza.

Aidha, watoto hao wameombea dua timu ya Simba iweze kuibuka na ushindi katika mchezo wa marudiano wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Timu ya Kaizer Chief.

KAMPUNI YA SD BIOSENSOR YA KOREA YAKABIDHI VIFAA VYA MAABARA VYA UCHUGUZI WA CODIV 19 KWA WIZARA YA AFYA,USTAWI WA JAMII,WAZEE,JINSIA NA WATOTO ZANZIBAR

$
0
0

 

 

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vital Supplies Limited Bw. Jimmy C. Apson na CEO wa kampuni hiyo Bw. Sunjay.Patadia wakiwa na Viongozi wa Wizara ya Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee,Jinsia na Watoto Zanzibar,alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar wakati wa hafla ya kukabidhiwa Vifaa vya Maabara vya Vipimo vya Uchunguzi wa Covid 19, vilivyotolewana Kampuni ya SD.Biosensor ya Korea.


CEO wa Kampuni ya Vital Supplies Limited Tanzania Bw.Sanjay Patadia akizungumza katika hafla ya kukabidhi Vifaa vya Maabara vya Uchunguzi wa Covid 19 kwa Wizara ya Afya Zanzibar, vilivyotolewa na Kampuni ya SD Biosensor kutoka Korea, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.


BAADHI ya Madaktari na Maofisa wa Wizara ya Afya Zanzibar wakifutilia hafla ya kukabidhi Vifaa vya Maabara vya uchunguzi wa Covid -19, vilivyotolewa na Kampuni ya SD Biosensor ya Korea, hafla hiyo imefanyika katika ukumbiu wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.

  KATIBU Mkuu Wizara ya Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar Dkt. Omar Dadi Shajak akizungumza na kutowa maelezo ya makabidhiano ya Vifaa vya Maabara vya uchunguzi wa Covid 19, vilivyotolena Kampuni ya SD Biosensor ya Korea, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.


CEO wa Kampuni ya Vital Supplies Limited Bw.Sanjay Patadia akimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman, akizungumza na kutowa shukrani kwa Kampuni ya SD.Biosensor ya Korea kwa kutowa msaada huo wa Vifaa vya Maabara vya uchunguzi Covid 19,kwa Wizara ya Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee,Jinsia na Watoto Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.

WAZIRI wa Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee,Jinsia na Watoto Zanzibar. Mhe Nassor Ahmed Mazrui, akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa Vifaa vya Maabara vya uchunguzi wa Covid 19, vilivyotolewa na Kampuni ya SD Biosensor ya Korea kwa Wizara ya Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee,Jinsia na Watoto  Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.


 

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa Vifaa vya Maabara kwa ajili ya Wizara ya Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee,Jinsia na Watoto Zanzibar, vilivyotolewa na Kampuni ya SD Biosensor ya Korea, kwa ajili ya uchunguzi wa Covid 19, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.


 MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman akikabidhiwa Vifaa vya Maabara vya uchunguzi wa Covid 19, vilivotolewa na Kampuni ya SD Biosensor ya Korea akikabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vital Supplies Limited ya Tanzania Bw. Jimmy C Apson. hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar, na (kushoto kwa Makamu) Waziri wa Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee,Jinsia na Watoto Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui na (kulia kwa Mkurugenzi) CEO wa Vital Supplies Limited Bw.Sanjay Patadia wakipika makofi wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano. 

WADAU WA ELIMU WATOA MAONI JUU YA ELIMU WAITAKAYO

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Shule Direct, Faraja Nyalandu (kushoto) akiendesha mjadala kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Elimu Bora ulioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET). Wadau mbalimbali wa ikiwepo serikali, wanachama wa mtandao, Washirika wa Maendeleo pamoja na wadau wengine wanashiriki katika mkutano huo.
Baadhi ya wadau mbalimbali na wanachama wa mtandao wa Elimu, Washirika wa Maendeleo pamoja na wadau wengine wakishiriki katika mkutano huo.
Wadau mbalimbali wakishiriki katika mkutano huo wa Elimu Bora ulioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET).
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi (kushoto) akiendesha mjadala kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Elimu Bora ulioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET). Wadau mbalimbali wa ikiwepo serikali, wanachama wa mtandao, Washirika wa Maendeleo pamoja na wadau wengine wanashiriki katika mkutano huo.
Mmoja wa wadau wa elimu akiwasilisha mada kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Elimu Bora ulioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET). 

BAADHI ya wadau wa elimu walioshiriki mkutano wa kimataifa wa elimu Bora ulioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), wametoa maoni yao kuhusiana na elimu nchini huku wakipendekeza kuwa elimu inayotolewa sasa haina budi iendane na karne 21 na kutatua changamoto anuai zilizopo katika mfumo wa elimu.

Akizungumza katika mjadala kwenye mkutano wa kimataifa wa elimu Bora, Mkurugenzi Mtendaji Uwezo Tanzania, Zaida Mgalla alisema kumekuwepo na mjadala mkubwa juu ya elimu inayotakiwa, hivyo kushauri ipo haja ya elimu ya sasa iendane na karne ya 21. "...Tunataka elimu itakayo waandaa watoto wafahamu mambo ya sayansi, wafahamu mambo ya teknolojia, lakini pia wapate zile stadi za maisha. Zipo stadi za kufikiri kwa makini, kuwa wabunifu, kuweza kufanya maamuzi ya busara, kuweza kufanya mawasiliano na wenzao na hata mahusiano yenye tija na si potofu, kutambua jambo hili ni nzuri au baya," alipendekeza Mkurugenzi huyi ambaye pia ni mwanachama wa TEN/MET.

Alisema Tanzania kwa sasa inaitaji elimu inayoweza kuwatanua vijana ki-fikra, waweze kutenda mambo mbalimbali wamalizapo masomo yao na si kuwaandaa vijana kutegemea kuajiriwa tu. "...Tujaribu kuipitia mitaala yetu kwa makini na kuangalia tuongeze nini, pia tunachotaka kiongezwe kwenye mitaala tukifanyie utafiti, tuhusishea wadau mbalimbali ili kuweza kuibuka na mabadiliko muhimu na sahihi kwenye mitaala hiyo," alisisitiza Bi. Mgalla.

"...Wadau kama wazazi wanaweza kuulizwa wanataka watoto wao wakimaliza shule waweze kufanya nini, wadau kama mashirika na asasi nazo ziseme zinashauri kitu gani. Mfano sisi tuliosoma zamani tulifundishwa kitu kinaitwa maarifa ya nyumbani, tulijifunza kupika vitu mbalimbali, tulijifunza kushona, tulijifunza kutengeneza bustani, tulijifunza malezi ya watoto na vitu anuai...mambo kama haya tunaweza kuangalia ni yepi tuyarejeshe katika mitaala yetu na kwa namna gani yanaweza kuwasaidia vijana."

Naye Meneja wa Programu, Nicodemus Shauri kutoka Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) alisema kwa sasa nchi yetu inaitaji elimu inayotufaa kuweza kutatua changamoto zinazotukabili, alisema elimu wanayopokea vijana wetu kwa sasa inatakiwa kumjenga na kumuwezesha na hata kumuendeleza kwa karama aliyonayo kijana yoyote ili imsaidie hata kumkwamua kiuchumi.

Aliongeza kuwa kwa namna nyingine watoto wetu wanaweza kupewa elimu huku wakiendelezwa vipawa mbalimbali walivyojaliwa na Mungu ili vije kuwasaidia hapo baadaye. Mfano kama mtu amejaliwa kipaji cha sanaa apate elimu huku akiendelezwa kipaji chake ili baadaye kumuwezeshe kiuchumi, kama amejaliwa historia aendelezwe ili baadaye aje kuwa mwalimu mzuri wa historia, kama amejaliwa kipaji cha muziki aendelezwe ili akitoka shule aje kufanya muziki vizuri utakao msaidia katika maisha yake na kama mtu amejaliwa kipaji cha michezo (mfano riadha au uigizaji) basi aendelezwe ili baadaye imsaidie kwenye maisha yake," alisema Bw. Shauri.

Alisema vijana wakipewa elimu huku wakiendelezwa kwenye vipaji vyao hawawezi kumaliza shule na kusubiri au kutegemea ajira ambazo kwa sasa ni changamoto ya ki-ulimwengu jambo ambalo litaipunguzia taifa mzigo na kujikuta limewawezesha vijana kiuchumi mmoja mmoja na hata taifa ki ujumla. Alisema kwa sasa tunazungumzia elimu bora lakini pamoja na mambo mengine tuangalie elimu inayotufaa na kujikuta inatukwamua katika changamoto zilizopo.

Kwa upande wake mdau mwingine wa elimu, Bw. Doglas Mwisaka ambaye kitaaluma ni mwalimu alisema licha ya kuzungumzia elimu bora hatuna budi kuwakumbuka walimu ambao ndio wanaokwenda kutoa elimu hiyo, kwamba wanaandaliwa vya kutosha kwa kuzingatia vigezo vyote ili waweze kuifanya kazi hiyo kiufasaha.

"...Tunazungumzia mabadiliko ya elimu kutaka elimu bora, lakini tusisahau kuanza na walimu kwani ndio wadau muhimu wa mabadiliko hayo...siku zote tunafanya maboresho huku mwalimu akibaki nyuma sasa tutapataje elimu bora huku tukiwasahau walimu wenyewe," alihoji Mwalimu Mwisaka akizungumza na mwandishi wa  habari hizi.



KAMPUNI YA UTALII YAMTUNUKU TUZO YA HESHIMA KATIBU MKUU WA TAMUFO

$
0
0

Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania  (TAMUFO) Stella Joel.akizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha baada ya kutunukiwa Tuzo ya Heshima na Kampuni ya Phide Intertermet and Tours yenye makao yake makuu jijini Arusha inayojishughulisha na masuala ya utalii hapa nchini.

Hii ni moja kati ya Tuzo nane alizowahi kutunukiwa.


Dotto Mwaibale


KAMPUNI ya Phide Intertermet and Tours yenye makao yake makuu jijini Arusha inayojishughulisha na masuala ya utalii hapa nchini imemtunuku Tuzo ya Heshima Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania  (TAMUFO) Stella Joel kutokana na mchango wake mbalimbali katika jamii.

Akizungumza kwa furaha baada ya kukabidhiwa Tuzo hiyo Joel aliishukuru kampuni hiyo kwa kutambua mchango wake anaoutoa kwa jamii.

" Naishukuru kampuni hii kwa kunitunuku Tuzo hii ya heshima kutokana na mchango wangu katika jamii kupitia TAMUFO na vyama vingine ambavyo ni mwanzilishi ambavyo niliviongoza." alisema Joel.

Alisema Tuzo hiyo kati ya nane ambazo amewahi kutunukiwa 
imempa nguvu na ari ya kuendelea kutumikia jamii katika nyanja mbalimbali pindi atakapokuwa anapata nafasi ya kufanya hivyo.

Joel alisema licha ya kutunukiwa Tuzo hiyo siyo yake peke yake bali ni ya wote alioshirikiana nao kwa njia moja au nyingine katika kazi hizo alizozifanya na kuonekana katika jamii na hatimaye kutunukiwa tuzo hiyo ya heshima.

" Tuzo hii ni yetu sote maana bila ya ushirikiano wenu nisingeweza kuipata kwani imenipa hamasa na kunitia moyo sana." alisema Joel.

Katibu Mkuu huyo wa TAMUFO alitumia nafasi hiyo kuishukuru Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo,  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Afisa Utamaduni wa Jiji la Arusha, Kampuni ya Phide Intertermet and Tours Wanahabari kupitia vyombo vyao mbalimbali pamoja na wadau wote wa maendeleo kwa ushirikiano wao wa mara kwa mara wanaompa wakati akitekeleza majukumu yake.

Mlezi wa TAMUFO, Frank Richard alimpongeza Joel kwa kutunukiwa Tuzo hiyo akamtaka kutolewa sifa badala yake aendeleze moto wa kufanya kazi na kuwa mbunifu zaidi jambo litakalo panua wigo mkubwa wa kuwatumikia wanamuziki na jamii kwa ujumla.

TCRA yakutanisha wadau wa Sekta Ndogo ya utangazaji kujadili uboreshaji wa sekta hiyo

$
0
0


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Jabir Bakari akitoa maeleylzo kuhusiana na Sekta ya utangazaji katika kikao cha Majadiriano ya Jinsi ya Kuboresha Sekta ya Utangazaji ,kilichofanyika jijni Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Leseni wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka akitoa maelezo katika kikao cha Majadiriano ya Jinsi ya Kuboresha Huduma za Utangazaji, kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia Habari Dkt.Jimmy Yonazi akisikiliza maoni ya wadau katika kikao cha majadiriano ya jinsi kuboresha Sekta ya Utangazaji kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

 

 Na Mwandishi Wetu 


Serikali imeahidi kufanyia kazi maoni ya uboreshaji wa huduma za Utangazaji   yaliyotolewa na wadau katika kikao cha mashauriano ya jinsi ya kuboresha huduma za Utangazaji nchini.


Akizungumza katika ufunguzi wa kikao hicho kilichofanyika leo jijini Dar es salaam, ambacho kiliunganisha wadau kutoka maeneo mbalimbali  ya Tanzania,  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jimmy Yonazi amesema Serikali  iko tayari kujifunza kutoka kwa wadau hivyo washiriki wawe huru katika kuchangia.


Kikao hicho ambacho kimeratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kimekusanya maoni katika maeneo matano ambayo ni pamoja na tozo za leseni za Redio, Televisheni, Maudhui mtandaoni na Masafa ya Utangazaji.

Maeneo mengine yaliyojadiliwa ni pamoja na mfumo wa biashara kwenye urushaji wa matangazo ya televisheni yanayorushwa bila kulipia na mfumo wa biashara kwenye matangazo ya televisheni ya kulipia.

Aidha, matumizi ya kisimbusi kimoja ili kupata maudhui kutoka kwa watoa huduma tofauti; mikataba ya kibiashara kati ya vituo vya utangazaji na wasambazaji wa matangazo; na wajibu wa vituo hivyo katika leseni pia vimejadilidiwa.

Hii ni mara ya sita kwa mwaka huu 2021 ambapo TCRA imekuwa ikiandaa mikutano ili kubadilishana mawazo na uzoefu kwa lengo la kuboresha huduma za Mawasiliano.

BENKI YA CRDB YAJIVUNIA MAFANIKIO ILIYOYAPATA

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Dk. Ally Laay, akiwasilisha ripoti ya mwaka na taarifa ya fedha ya Benki ya CRDB wakati wa Mkutano Mkuu wa Wanahisa uliofanyika jijini Arusha ambapo kwa mwaka wa fedha ulioishia Disemba 31, 2020 benki hiyo imeweza kupata matokeo bora ya kifedha licha ya changamoto zilizojitokeza.
Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Benki ya CRDB ambaye pia ni Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, akiongoza mkutano huo unaofanyika jijini Arusha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akitoa taarifa ya benki hiyo katika Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Benki ya CRDB uliofanyika jijini Arusha Mei 22, 2020.

Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia), akipitia taarifa za benki hiyo katika Mkutano Mkuu wa 26 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB jijini Arusha.


Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 26 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 26 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB.
 Ofisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo akitoa taarifa za fedha 2020 katika Mkutano Mkuu wa Wanahisa ya Benki ya CRDB unaofanyika jijini Arusha.

Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambwa, akizungumza katika mkutano wa Wanahisa wa Benki ya CRDB.

UJENZI WA MAHAKAMA KYERWA KUANZA MWEZI JUNI

$
0
0

 


 Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, Rashid Mwaimu akizunguza katika maadhimisho hayo.

 

Na Lydia Lugakila, Kyerwa

Kutokana na changamoto ya wananchi wilayani Kyerwa mkoani Kagera kutembea umbali mrefu wa takribani kilometa 80 kufuata huduma ya kimahakama katika Wilaya ya Karagwe mahakama hiyo inatarajia kuanza ujenzi wa mahakama ya wilaya mnamo mwezi juni mwaka huu ili kuwaondolea adha wananchi hao.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera Rashid Mwaimu katika maadhimisho ya utoaji wa msaada wa kisheria kwa wanawake na wasichana uliolenga kuwawezesha upatikanaji wa haki kupitia ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kagera  kwa kushirikiana na mtandao wa watoa huduma za msaada wa kisheria TANLAP chini ya ufadhili wa shirika la umoja wa mataifa linalohusika na wanawake (UNWOMEN) yaliyofanyika katika uwanja wa parokia ya mabira jimbo Catholic la kayanga.
 

Mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa wananchi katika wilaya ya Kyerwa kwa muda mrefu wamekuwa wakifuata huduma hiyo kutoka wilayani humo hadi wilaya ya Karagwe kwa umbali wa takribani kilometa 80 jambo ambalo huwalazimu wananchi hao kukata tamaa wakati wakifuatilia masuala ya kisheria.

"Hongereni idara ya mahakama kufikiria mpango wa kujenga mahakama ya wilaya hii itasaidia kuwapunguzia adha wananchi katika kupata huduma ya kisheria ya mahakama ndani ya wilaya yetu"alisema mkuu wa wilaya hiyo.

Akieleza changamoto ya ukosaji wa huduma hiyo muhimu hakimu wa mahakama ya wilaya Anajoyce Chrisostom amesema ujenzi wa mahakama hiyo utawasaidia pakubwa wananchi hao kwani changamoto kubwa ni pale inapotokea wakapokea kesi ya jinai yule mlalamikaji hulazimika  kulipa nauli ya mtu anayemlalamikia kwa ajili ya kumpeleka mahabusu ambapo kama amekosa mdhamini, tarehe ya kesi ikifika mlalamikaji hulipa tena nauli ya kumrudisha kutoka mahakama ya wilaya ya karagwe ikiwa ni pamoja na kumlipia nauli askari mgambo aliyemsindikiza jambo linalosababisha wananchi hao kupoteza fedha, pamoja na muda na kusababisha kukata tamaa ya kupata huduma hivyo kisheria.

Aidha kwa upande wake msajili msaidizi wa watoa huduma za msaada wa kisheria Mkoani Kagera Issa Mrimi ameitaka jamii mkoani Kagera  kujenga mazoea ya kujitokeza na kupeleka kero zao katika vyombo vya kisheria ili kupatiwa ufumbuzi.

Hata hivyo kilele cha maadhimisho ya huduma ya utoaji msaada wa kisheria kwa wananchi wa wilaya ya Kyerwa imeanza mei 21 mwaka huu katika kata ya Mabira na  kilele chake ni mei 22, katika kata ya Nkwenda huku kauli mbiu  ikiwa ni "mwanamke inuka omba msaada wa kisheria kwa ustawi wa maendeleo yako"


SHERIA BORA NI CHACHU YA MAENDELEO-TAMWA-ZNZ

$
0
0

 


 

Talib Ussi Zanzibar 


Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa habari Wanawake TAMWA-ZNZ Dkt, Mzuri Issa amesema kuna umhimu mkubwa wa madiliko ya sheria ya habari Zanzibar kwani uwepo wa sheria bora ni chachu ya maendeleo na kivutio kikubwa kwenye sekta ya uwekezaji.


Aliyasema hayo leo katika mkutano maalumu uliowashirikisha wadau mbali mbali wa habari wenye lengo la kujadili rasimu ya sheria ya hio visiwani hapa uliofanyika ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe mjini Unguja.


Alisema  kwa miaka mingi Zanzibar imekua na sheria ya habari isiolingana na wakati uliopo sasa na kupelekea changamoto mbali mbali ambazo ili ziweze kuondoka ni lazima iwepo sheria mpya na yenye kukidhi maakwa ya wadau wa sheria hio kwa kuwa ndio wenye kufahamu kwa kina nini kinachohitajika na kisichopaswa kuwepo kwa wakati uliopo sasa.


Akifafanua zaidi alisema kwa sasa sheria nyingi za habari zilizopo zimepitwa na wakati na hakuna budi lazima mamlaka kubadilisa sheria hizo kwa manufaa ya pande zote.


Mkurugenzi huyo alieleza kuwa kutokuwepo kwa mazingira bora ya sheria ya habari kupelekea tasnia hio kuonekana kutokua bora wakati tasnia ya habari ni muhimu sana popote pale duniani.


Akifafanua zaidi alisema kuwepo kwa mazingira magumu ya sheria ndio maana baadhi ya vyombo vya habari vimekua vikifungiwa ovyo bila ya kuelezwa sabau za msingi za kufunggiwa kwake jambo ambalo anaamini kutwepo kwa sheria mpya kutaondokana na kadhia za ina hio.


Katika hatua nyengine alisema wadau wa sekta ya habari Zanzibar wanawajibu wa kutafakari kwa kina na kuhakikisha wanachangia kwa kiasi kikubwa  upatikanaji wa sheria mpya itakayokidhi vigenzo vyote.


Kwa upande wake mwandishi wa habari na mkufunzi wa taaluma hio Rashid Omar amesema upatikanaji wa sheria mpya ya habari ni matakwa ya wadau wengi Zanzibar na wakati umefika kuzingatiwa kwa matakwa hayo.


Nae Shifaa Sadi Hassan mwakilishi wa Baraza la Habari Tanzania MCT ofisi ya Zanzibar alisema hadi leo hii Zanzibar haina sheria mahsusi ya habari yenye kukidhi vigenzo na hadi sasa imekua ikitumika sheria ya mwaka 1988 inayogusia kwa uchache sana kuhusu sekta ya habari.


Alisema kwa kuwa suala la  kukuza na kueneza habari ni jambo  muhimu linalopaswa kuungwa mkono na kila mtu kwani ni haki ya kikatiba ambayo inapaswa kuzingatia ikiwemo kupata sheria bora.

SERIKALI YAPONGEZWA KWA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA SEKTA YA ELIMU

$
0
0
 

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chuo Kikuu Mzumbe, Bi. Rose Joseph (mwenye raba nyeupe) akiwapokea Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari mara walipowasili chuoni hapo.



Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe (Mwenye tai ya Bluu) Prof. Lughano Kusiluka, akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania Bw. Deodatus Balile wakati wakizunguka kukagua jengo la mabweni lililomalizika ujenzi. Wanaoonekana nyuma yao ni Wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari nchini.


Baadhi ya wahariri wakisikiliza kwa makini maelezo kuhusu ujenzi wa miundombinu iliyokamilika.Wahariri hao walikuwa wanashiriki  kikao cha Jukwaa la Wahariri kilichofanyika mkoani Morogoro.


   Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka akijibu baadhi ya hoja za wahariri wakati  walipofanya ziara chuoni hapo.

 Wahariri wakikagua mazingira ya eneo la ujenzi Chuo hapo.

Wahariri wakiwa katika picha ya kumbukumbu na uongozi wa Chuo wa Kikuu Mzumbe, baada ya kuhitimisha ziara yao chuoni hapo. 
 
 
Na Mwandishi Wetu


Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Lughano Kusiluka, ameeleza mafanikio makubwa ambayo chuo hicho kimeyapata katika Awamu ya Tano na Sita ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Profesa Kusiluka amebainisha mafanikio hayo mbele ya Wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali nchini kupitia Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), waliotembelea Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi Kuu ya Morogoro na kupata fusra ya kutembelea maendeleo ya ujenzi wa miundombinu iliyokamilika.

.

Profesa Kusiluka amefafanua kuwa Chuo Kikuu cha Mzumbe kimewekeza zaidi ya Bil 13 kutokana na fedha zilizotolewa na Serikali, katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na mabweni ya wanafunzi wa chuo hicho.

 

Amefahamisha kuwa ujenzi huo unalenga kukabiliana na changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa ya kufundishia na mabweni ya kulala wanafunzi, ambao baadhi yao wanalazimika kutafuta makazi nje ya kampasi.

 

Vyumba vya kufundishia vilivyo katika miradi mipya ya miundombinu iliyokamilika ina uwezo wa kuhudumia wanafunzi 1,000 huku mabweni yakiwa na uwezo wa kutoa malazi kwa wanafunzi 1,024.

 

Aidha, amewashukuru Wahariri wa vyombo vya habari kwa kutenga muda wao kutembelea Chuo Kikuu cha Mzumbe, chuo ambacho kinajivunia mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuzalisha viongozi wengi ndani Serikali akiwemo Rais wa Awamu ya Sita Mhe. Samia Suluhu Hassan.

 

Aidha Profesa Kusiluka amebanisha kuwa Vyombo vya Habari,  Wahariri na Waandishi wa habari wana umuhimu mkubwa wa kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha jamii ikiwa ni pamoja na kuchochea maendeleo.

 

Wakizungumza baada ya kutembelea majengo yaliyokamilika (Vyumba vya madarasa na mabweni ya wanafunzi), wahariri hao wamepongeza mafaniko makubwa yaliyotokana na dhamira ya Serikali ya kuwekeza kwenye Sekta ya elimu ili kutoa fursa kwa Watanzania wengi zaidi kunufaika na Elimu nchini.

Jafo aipa kongole Manispaa Moshi uhifadhi wa taka ngumu

$
0
0


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo akiwa na viongozi wa Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro wakati akiangalia dampo la kisasa lililojengwa manispaa hapo.

Muonekano wa dampo la kisasa lililojengwa Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

 

NA SULEIMAN MSUYA


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Selemani Jafo amewapongeza viongozi na watendaji wa Manispaa ya Moshi Wakiongozwa Mstahiki Meya Wa Manispaa hiyo Juma Raibu kwa namna wanavyohifadhi taka ngumu zinazozalishwa kila siku katika manispaa hiyo. 

Jafo aliyasema hayo alipokuwa katika ziara ya Kikazi katika Manispaa ya Moshi leo Mei 22, 2021. 

Katika ziara hiyo waziri huyo alitembelea dampo la kisasa la manispaa hiyo ambapo aliridhishwa na namna wataalamu wanavyosimamia vyema utupaji wa taka hizo sambamba na ubadilishaji wa baadhi ya taka hizo kuwa mboji.

Jafo amezitaka halmashauri nyingine kuiga mfano wa manispaa hiyo ya Moshi katika uhifadhi bora wa taka ngumu.

Aidha, Waziri Jafo pamoja na ukaguzi wa dampo hilo alitembelea kiwanda cha China Paper Industry ambapo aliwataka wamiliki wa kiwanda hicho kutafuta njia ya kutumia nishati mbadala kwani kwa sasa wanatumia magogo mengi kwa ajili ya nishati na hivyo kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira. 

Amewapa mwaka mmoja wamiliki wa kiwanda hicho kuja na njia nyingine ya nishati mbadala wa magogo yanayotumika sasa. 

Pia waziri huyo amewataka wamiliki wa kiwanda cha kutengeneza nondo cha Five Star Steel kinachotumia chuma chakavu kuepuka kununua vyuma vinavyotoka katika miundombinu ya umma ikwemo madaraja, alama za barabarani na kutoka kwa watu binafsi ili kutoleta hasara kwa jamii. 

Hata hivyo, Jafo amekipongeza kiwanda hicho kwa kudhibiti kusambaa kwa moshi kutoka katika kiwanda hicho ambapo kwa siku za nyuma ulikuwa unakera raia wanaoishi jirani ya kiwanda hicho.


Wanawake wa kilsamu watakiwa kusambaza elimu ya dini yao

$
0
0

 


NA HAMIDA RAMADAHANI, DODOMA


JAMII ya Wanawake wa Kiislamu wameaswa kusoma elimu ya dini ya kiislamu na kumjua  Allah pamoja na kumcha Allah ili kutengeneza kizazi chenye maadili.

Rai hiyo imetolewa jijini Dodoma na mbunge viti Maalumu mkoa wa Tanga Bi Mwantum Zodo wakati wa uzinduzi wa jengo la kituo cha elimu ya watoto na madarasa ya kinamama lilojengwa na umoja wawanawake wa jumuiya ya bi Khadija Dodoma.

Amesema Ili kutimiza Malengo makubwa ya kuishi hapa duniani wanawake wa kiislamu hawana budi kuwa mfano Bora katika jamii kwani Wanawake ndio walezi wa familia.

 "Umuhimu wa wanawake kuwa na elimu itawasaidia kulea familia zao katika madili mazuri ya kumjua Allah na kutenda matendo mema katika maisha yao," amesema Zodo.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima cha Al-haafidhu Islamic ophance center kondoa ukht Aisha Khalfan amewaomba wakinamama wakiislam ambao wamejaaliwa kusoma elimu ya dini ya kiislamu kwenda kuisambaza .

" Niwaombe wakinamama wate wa kislamu waliobahatika kupata elimu muende kuisambaza kwa kufundisha watu wengine ili nao waweze kuelimika na kumcha Mwenyezi Mungu," amesema .

Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi mwalimu wa madarasa ya Mhijirina Rahma Iddi amebainisha changamoto zinazoikabili taasisi hiyo ya jumuiya ya Bi Khadija Dodoma .

Ametaja changamoto hiyo nipamoja na kukosa vyanzo malumu vya kuiingizia tasisi hiyo mapato na taasisi hiyo kujiendesha kwa kutegemea misaada kutoka kwa watu mbalimbali wanaoiunga jumuiya hiyo mkono.

UVCCM yaendelea kulia na gharama za vifurushi

$
0
0

 NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA

KATIKA kuwepo kwa malalamiko ya wananchi kuhusu kupanda kwa gharama za vifurushi  Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umeishauri Serikali kuona haja ya kuangalia upya suala la huduma za vifurushi.


Hayo yamesemwa leo jijini hapa na katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Raymond Mwangwala  wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa kikao cha baraza kuu la umoja wa vijana CCM.

aidha ameishauri Serikali kuona haja ya kuangalia upya suala la huduma za vifurushi  kwa kulichukulia kwa umakini ili kuokoa ajira kwa vijana waliojiajiri katika uchumi wa kidigitali.
 
 
"sisi kama vijana wa CCM  tunaishauri  serikali ,vijana wetu wanaelekea kukosa ajira kutokana na gharama kubwa za bando,tunaiomba Serikali yetu tukufu kuona namna ya kuboresha changamoto ya huduma za vifurushi kupitia mitandao ya simu;
 
Kwani uwepo wa gharama za juu katika manunuzi hukwamisha vijana kukua kiuchumi kutokana  na wengi kufanya shughuli zao kupitia mitandao ya kijamii,"amesema
 
 pia baraza kuu limemvua uongozi Hussen Salehe aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM wa wilaya ya moshi vijijini kwa kutokuwa na maadili pamoja na nidhamu baada ya kupokea mapendekezo yaliyowasilishwa katika kikao cha halmashauri kuu ya ccm ya mkoa wa Kilimanjaro.

"Baraza kuu lilijiridhisha,Kamati ilijiridhisha na kuona kwamba kwa tuhuma zile na mapendekezo yaliyotolewa katika kikao halmashauri kuu ya mkoa hivo limemvua uongozi,

“Hivyo naagiza mkoa wa Kilimanjaro kutangaza nafasi  ya mwenyeki wa uvccm, katika wilaya ya moshi vijijini”amesema.

 Sambamba na hayo UVCCM pia imeazimia kumuenzi hayati Dkt. John Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya tano kwa kuyaendeleza yale yote mazuri aliyoyafanya katika kipindi cha uongozi wake.

Lakini pia wamempongeza Rais wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuteuliwa kwa ushindi mnono huku akiwawataka vijana kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Samia pamoja na serikali yake.

Tutamlinda ,tutamtetea Rais wa chama chetu iwe mvua au jua,pia kwa kuongeza juhudi katika kufanya kazi na uzalendo katika nchi yetu

Pia wamempongeza Daniel Chongolo pamoja na wajumbe wote walio chaguliwa kuunda sekretarieti mpya ya chama chetu,tunaimani kubwa nao,tupo tayari kushirikiana nao kwa maslahi ya chama chetu kwa kazi nzuri pia tunakiopongeza chama chetu kwa kazi nzuri ya kusimamia cham,a chetu.

“Sisi kupitia wawakilishi wetu wa ngazi mbalimabli za maamuzi tunaendelea kusimamia serikali na hususani kupitia vijana wakiwa bungeni,kusimamia serikali kuhakikisha inatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kwa maslahi ya vijana na taifa kwa ujumla.
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live