Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

MTANDAO WA ELIMU TANZANIA KUADHIMISHA JUMA LA ELIMU WILAYANI RORYA

$
0
0


Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Ochola Wayoga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na Maadhimisho ya Juma la Elimu (Global Action Week for Education-GAWE) kwa mwaka 2021 yatakayofanyika Wilaya ya Rorya, mkoani Mara. Kushoto ni Afisa Uratibu wa TEN/MET, Alistidia Kamugisha akifuatilia.



MTANDAO wa Elimu Tanzania (TEN/MET) umetangaza kufanya maadhimisho ya Juma la Elimu (Global Action Week for Education-GAWE) kwa mwaka 2021 katika Wilaya ya Rorya, mkoani Mara, huku ukiwataka wananchi na wadau wa elimu kujitokeza ili kuweza kushiriki kwenye maadhimisho hayo. 

 

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na vyombo vya habari, Mratibu wa Taifa TEN/MET, Bw. Ochola Wayoga amesema shughuli za maadhimisho ya mwaka huu zitaanza rasmi Mai 31, 2021 hadi Juni 4, 2021 zikiambatana na mijadala ya wananchi kuhamasisha upatikanaji wa elimu bora kwa watoto.

 

Bw. Wayoga alisema TEN/MET imeambua kupeleka maadhimisho ya Juma la Elimu wilayani Rorya kutokana na changamoto za elimu zinazojionesha kwa kiasi kikubwa eneo hilo, hasa kwenye matokeo ya mitihani kwa elimu ya msingi na sekondari kidato cha nne.

 

"...Wadau wa TEN/MET kwa kushirikiana na serikali na Halmashauri ya Rorya tunakwenda kuhamasisha wanafunzi, wazazi, waalimu na watumishi katika sekta ya Elimu kusimamia ufahulu na uwekezaji katika mifumo ya elimu kwa maendeleo endelevu. Ni matarajio yetu kuwa wana Rorya watakuwa tayari kuungana nasi katika jitihada hizi," alisema Wayoga.

 

Alisema lengo kuu la maadhimisho hayo mwaka huu ni kuhamasisha juu ya lengo endelevu namba 4 (SDG4) kwa ujumla wake kwa kuhakikisha elimu bora inatolewa kama sehemu ya haki, huku malengo mengine yakiwa ni kuongeza uelewa kwa umma juu ya madai ya haki ya elimu iliyo bora na kuhamasisha elimu kwa makundi maalumu kama vile watoto wenye ulemavu.

 

Aidha akitaja shughuli zitakazofanyika katika maadhimisho hayo, alisema baada ya ufunguzi wa maadhimisho hayo Mai 31 kutakuwa na mikutano itakayofanyika vijiji mbalimbali na wananchi Juni Mosi na Pili kuwahamasisha wanajamii kushirikiana na Serikali katika kuboresha elimu iliyo jumuishi.

 

"Tarehe 3 Juni kutakuwa na Kongamano la Elimu kimkoa litakalofanyika wilayani Rorya na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu. Kwa wiki nzima kutakuwa na maonesho mbalimbali yakiendelea ndani ya uwanja wa Mji wa Shirati na Juni 4 itakuwa kilele cha maadhimisho hayo." Alisema Mratibu huyo wa TEN/MET Taifa.

 

Hata hivyo alisema lengo lingine la maadhimisho hayo itakuwa ni kuhamasisha jamii, Serikali na mashirika yasiyo na kiserikali umuhimu wa uwajibikaji wa pamoja katika masuala ya elimu na utekelezaji wa lengo la maendeleo endelevu la nne na hasa kuimarisha mifumo ikiwemo ya kuwekeza katika TEHAMA.


ZAWADI MISS KAGERA 2021 HII HAPA

$
0
0


 Mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo akizunguza baada ya kuzindua zawadi ya gari kwa ajili ya mshindi wa taji la miss Kagera 2021.

Mkuu wa wilaya ya katika majaribio ya gari hilo jipya.
Mwekezaji na muandaaji kutoka Zachwa Investment Muganyizi Zachwa akizungumza katika uzinduzi huo.

 

Mratibu wa shindano hilo  Regina Samweli Zachwa akitoa ufafanuzi wa shindano hilo.

 

Zawadi ya gari kwa ajili ya mshindi wa kwanza wa shindano la miss Kagera 2021.

 

 

Lydia Lugakila, Bukoba

Zawadi ya gari mpya yenye thamani ya shilingi milioni 18 yatambulishwa rasmi kuelekea shindano la Miss Kagera itakayotwaliwa na mshindi wa kwanza wa shindano hilo.

Akitambulisha zawadi hiyo ya gari mpya aina ya Rectus yenye thamani ya shilingi milioni 18 mratibu wa shindano la miss Kagera 2021 Regina zachwa kutoka Zachwa Investment kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wakiwemo Serengeti Breweries Ltd wametaja kukamilika kwa mchakato mzima wa shindano hilo.

Regina amewashukuru wabunge wa mkoa huo pamoja na serikali kuunga mkono suala hilo huku akieleza  maadalizi hayo kuiva na kuwa wanategemea ushindi mkubwa kwani mpango wao ni kuifia miss Tanzania 2021.

Amesema mwanzoni walianza na kamati ya miss Tanzania ambayo kwa kushirikiana na wizara ya michezo tamaduni na sanaa ambapo walikubakiana kurudisha heshima ya miss Kagera.

" Miss Kagera ya mwaka huu itakuwa ya tofauti Sana kwani tayari maandalizi yamekamilika    tunategemea mshindi atakayepatikana atauwakilisha mkoa wa Kagera" alisema Regina

Akizindua rasmi zawadi hiyo ya gari mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo amewapongeza waandaaji wa shindano hilo na kuwa tayari serikali inathamini mashindano hayo kwani yanaiweka Tanzania katika ramani nzuri kwa kutambulika dunia nzima .

Kinawilo amesema serikali imeruhusu mashindano hayo kuendelea na kuomba mshindi atakayepatikana kuhakikisha anatangaza vivutio na rasilimali zikizopo mkoani Kagera huku akiwataka wazazi kulipa kipaumbele suala hilo na kuondoa fikra mbaya iliyojengeka katika jamii kuwa Umiss ni Uhuni.

Aidha kwa upande wake muandaaji na mwekezaji ambaye pia ni mmiliki wa kituo cha redio cha Kasibante Muganyizi Zachwa amesema shindano hilo kwa mwaka huu litakuwa la tofauti na yaliyowahi kufanyika hivyo wasichana wajitokeze kwani licha ya zawadi ya gari Kuna zawadi nyingine kabambe.

Naye Meneja vipindi wa Kasibante FM Redio ambaye ni moja kati ya waandaaji amewaomba wazazi kutoweka vikwazo kwa mabinti zao walio tayari kujitokeza katika kinyanga'nyiro cha taji hilo kwani kwa kufanya hivyo ni kubinya ndoto za vipaji vyao.

Hata hivyo kamati hiyo ya shindano la Miss Kagera limeweka wazi ratiba ya shindano hilo kwa wilaya za mkoa huo ambapo Mei 28 na 29 mwaka huu shindano hilo litaanzia wilaya ya Biharamulo na Ngara na mwezi julai itakuwa Karagwe na Kyerwa huku kilele cha shindano hilo kikiwa ni Agosti 08, 2021 na kufanyika katika Manispaa ya Bukoba mkoani humo.

KUNENGE ATUA BAGAMOYO KWA KISHINDO AANZA KUWAPA SOMO WATAALAMU WAZEMBE KATIKA KUWAJIBIKA

$
0
0


Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Aboubakar Kungenge akiwa amenyanyua zawadi maalumu aliyopatiwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Bagamoyo kwa ajili ya kukaribishwa rasmi, kulia kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dk. Delphine Magera.

 

 

NA VICTOR  MASANGU, BAGAMOYO 

 

MKUU wa Mkoa wa Pwani    Mh. Aboubakar Kunenge  amewataka na kuwaagiza wataalamu na watumishi  wote wa halmashauriya Bagamoyo kuhakikisha kwamba wanafanya kazi kwa weledi na kutumia vema ipasavyo ujuzi walionao katika kukabiliana na changamoto mbali mbali zinazowakabili katika maeno yao ya kazi na kutumia fursa zilizopo katika kuleta maendeleo kwa wananchi.

Kunenge ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika halmashauri ya Bagamoyo kwa lengo la kuweza kujitambulisha pamoja na kuzungumza na baadhi ya watumishi wakuu wa idara pamoja na wataalamu kwa lengo la kuweza kupeana maelekezo katika suala zima zima uwajibikaji.

Aidha kunenge katika kikao hicho amewakumbusha wataalamu kuhakikisha kwamba wanaweka mikakati madhubuti katika suala zima la ukusanyaji wa mapato kwa lengo la kuwez kuwaletea wananchi maendeleo.

“Napenda kuchukua fursa hii kumshukuru sana Rais wa awamu ya sita Mama Samia Samia Suluhu kwa kuweza kuniamini tena naa kunipanafasi ya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani lakini lengo langu kubwa nimekuja kuwasalimia ili tuweze kuweka miapango madhubuti ambayo itasaidia katika kuleta chachu ya maendeleo katika maeneo yetu.”alisema Kunenge.

Aidha Kunenga aliwataka wataalamu mabali mbali kujenga tabia ya kufanya utafiti ambao utawasaidia katika kubaini fursa mbali mbali zilizopo katika maeneo yao kwa lengo la kuweza kuzitumia kikamilifu ili ziweze kuleta matokeo chanya na mafanikio katika maeneo ambayo wanayafanyia kazi.

 

Pia alibainisha kwmaba watumishi na waattalamu wanatakiwa kushirikiana bega kwa bega katika Nyanja mbali mbali na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zilizopo ilengo ikiwa ni kuweka mipango madhubuti ambyo itaweza kuzaa matunda katika siku za usoni na kwamba lengo la serikali ni kuwaletea wananchi maendeleo.

Kadhalika Kunenge alisema kwamba lengo la serikali iliyopo madarakani ni serikali ya Chama cha mapinduzi (CCM) hivyo ni lazima itatekeleza Ilani ya Chama katika ni kuhakikisha inatumikia wananchi wananchi na kuzisikiliza kero na changamoto zao mbali mbali zinazowakabili.

 

“Kitu kikubwa ambacho nina kiomba kwa watumishi wote wa umma ni lazima kuweka mikakati ya kutekeleza ilani ya cahama cha mapinduzi kwa vitendo kwa serikali hii ndio inasimamiwa na CCM na kwamba ni lazima watumishi wote kw akipindi hiki inapaswa kchapa kazi kweli kweli kwa bidii  ili  tuweze kutumiza yale yote amabyo yameelekezwa katika Ilani ya Chama.

 

Katika hatua nyingine Kunenge aliongeza kwamba atahakikisha kwamba anashirikiana na viongozi mbali mbali wakiwemo wakuuu wa wilaya wakurugenzi ili kuweza kufikia lengo ambalo limekusudiwa na serikali katika kuwatumikia wananchi pamoja na kuwaletea mabadiliko chanya ya kimaendeleo.

 

Awali kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bgamoyo Zainabu Kawawa akisoma taarifa ya Wilaya hiyo alisema kwa sasa bado kuna changamoto mbali mbali amabzo zinatakiwa zifanyiwe kazi ikiwemo kukithiri kwa  uwepo wa bandari bubu 19 amabzo zimekuwa zikitmika katika kufanyia biashra za magendo.

Aidha Kawawa aliongeza kwa sasa katika kukabiliana na changamoto hiyo wameshaanza kufanya misako na doria mbali mbali katika bahari ya hindi kwa lengo la kuwabaini wale wote ambao wanahusika na matukio mbali mbali ya kuharifu kupitiabandari hizo bubu.

 

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dr. Delphine Magere aliwahimiza watumihshi na wataalamu mbali mballi kufanya kazi kwa bidii katika kuwatumikia wananchi naa kuahidi kuyafanyia kazi maagizo yote ambayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa maslahi ya wananchi.

MHE.CHAMUHIRO ATEMBELEA BANDA LA BRELA KATIKA MAONESHO YA WADAU WA SEKTA YA UJENZI

$
0
0

Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Mhandisi Leonard Chamuhiro, akipatiwa maelezo na maafisa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), alipotembelea banda hilo mapema leo, baada ya ufunguzi wa maonesho ya Wadau wa Sekta ya Ujenzi, yanayofanyika leo na kesho katika viwanja vya Diamond Jubilee, Dar es Salaam. Maafisa wa BRELA kutoka kushoto ni Afisa Usajili Bw. Englibert Barnabas, Msaidizi wa Usajili Bi. Yvonne Massele na Afisa Leseni Bi. Saada Kilabula.

Maafisa wa BRELA wakitoa elimu na huduma kwa watembeleaji wa Maonesho ya Wadau wa Sekta ya Ujenzi yanayofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Afisa Leseni wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bi. Saada Kilabula ( aliyesimama kushoto) akitoa maelekezo ya huduma zitolewazo na BRELA kwa Msanifu majengo Bw. E.Nnunduma, katika maonesho ya Wadau wa Sekta ya Ujenzi, yanayofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, tarehe 27 -28 Mei, 2021.

Afisa Usajili kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Englibert Barnabas (kulia), akitoa ufafanuzi wa huduma zitolewazo na BRELA kwa mteja kutoka Kampuni ya Agrovision Limited Bw. Arfaan Ahmed Alwani, alipotembelea banda la BRELA, katika maonesho ya wadau wa Sekta ya Ujenzi, yanayofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Rais Samia Suluhu Hassan akutana na kufanya mazungumzo na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN)

$
0
0

 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake UN Women Dkt. Phumzile Mlambo Ngcuka mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 28 Mei, 2021.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake UN Women Dkt. Phumzile Mlambo Ngcuka mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 28 Mei, 2021.

MAJALIWA: NACTE VISAIDIENI VYUO KUTOA ELIMU YENYE KUKIDHI MAHITAJI

$
0
0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameliagiza Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) liimarishe usimamizi na kuvisaidia vyuo kutoa elimu inayozingatia viwango vya ubora na vyenye kukidhi mahitaji ya soko ya ajira la sasa na lijalo. 

 

Amesema kuwa ni wajibu wa vyuo hivyo kuhakikisha vinatoa elimu bora ili kuwafanya wahitimu wake wawe mahiri na kukidhi mahitaji ya nchi na pia kuwawezesha kujiajiri wao wenyewe.

 

Ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Mei 28, 2021) wakati akifungua Maonesho ya Pili ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

 

Amesema kuwa vyuo vya elimu na mafunzo ya ufundi vinapaswa kutumia fursa ya maonesho hayo kujitathmini na kujipima ili kuona ni kwa namna gani vinaweza kutoa Elimu na Mafunzo ya Ufundi bora yanayokidhi mahitaji ya sasa ya soko la ajira na kutoa fursa kwa vijana kujiajiri.

 

“Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025 imeweka wazi kuwa elimu ni kipaumbele cha juu kwani ndiyo kitovu cha kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwenye jamii”.

 

Aidha, Waziri Mkuu amesema kuwa ulimwenguni kote elimu na mafunzo ya ufundi na ufundi stadi hujulikana kwa mchango wake mkubwa katika ukuaji wa maendeleo ya viwanda, uchumi na ustawi wa jamii. “Vyuo na taasisi zinazotoa elimu hii ni lazima vihakikishe vinatoa elimu bora inayokidhi viwango na mahitaji ya soko la sasa la ajira”

 

Kadhalika, Waziri Mkuu aliongeza kuwa Serikali kwa upande wake itaendelea kuweka sera ambazo zinatoa fursa kwa wadau mbalimbali kuwekeza katika sekta ya elimu na hivyo, kuunga mkono juhudi za kuliletea Taifa maendeleo. 

 

“Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na taasisi za umma na binafsi ambazo zinatoa Elimu na Mafunzo ya Ufundi hapa nchini. Hivyo, natoa wito kwa wadau wote kuungana na Serikali kuwekeza katika utoaji wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika fani mbalimbali”

 

Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa Wizara itaendelea kuhakikisha inatoa elimu ya mafunzo ya ufundi kwa kuzigatia mahitaji ya soko ya kipindi husika na kuwaandaa vijana kwa siku zijazo.

 

Naye, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uongozi NACTE Prof. John Kondoro amesema kuwa watashirikiana na vyuo, taasisi za elimu ya mafunzo ya ufundi na wadau wengine kusimamia utoaji wa mafunzo na kuhakikisha elimu ya ufundi na mafunzo inatolewa kwa ubora ili kukidhi mahitaji ya soko la ajira la ndani na nje.

 

Serikali kuweka sera nzuri kwa Vyuo vya Ufundi na Sekta Binafsi

$
0
0

 Na Jasmine Shamwepu, Dodoma

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuweka sera nzuri zinazotoa fursa kwa Vyuo vya ufundi na  sekta binafsi  ili kuhakikisha mafanikio yanapatikana.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Mei 28, 2021  wakati akifungua maonyesho ya pili ya elimu ya ufundi yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte) kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kuweka sera nzuri zinazotoa fursa kwa Vyuo vya ufundi na  sekta binafsi  ili kuhakikisha mafanikio yanapatikana huku akiitaka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuimarisha ushirikiano kati ya sekta binafsi ili kukuza ujuzi huo.

Vilevile, ameitaka  sekta binafsi nchini inapokutana na changamoto yoyote kufika Serikali ili waweze kufanya kazi kama timu na  kukabiliana changamoto hiyo ya ajira.

Waziri Mkuu ,ametoa wito  kwa wadau wote kuendelea kushikamana, kuzungumza lugha moja kwa kuhakikisha mwelekeo huo unaeleweka kwa Watanzania.

Aidha, Majaliwa amesema Serikali imeendelea kuimarisha mazingira ya kuwekeza katika sekta ya elimu nchini na kwamba hadi kufikia mwaka 2021 idadi ya vyuo vilivyosajiliwa nchini na Nacte 430.

Amesema  pia idadi ya wanafunzi waliojiunga na vyuo hivyo imeongezeka kutoka 117,478 mwaka 2015 hadi 172,312 mwaka 2020.

Amesema  wanafunzi hao ni wa ngazi za astashahada na stashahada na kwamba ongezeko hilo limepanua wigo kwa wahitimu wa kidato cha nne kujiunga na masomo katika ngazi hizo.

“Ongezeko hili limetoa nafasi kwa vijana waliomaliza darasa la saba kujiunga na vyuo vya Veta na wale ambao hawakupata elimu kabisa kujiunga katika taasisi ambazo zinatoa elimu ya ufundi na ujuzi ili waweze kujiajiri na kuajiri wengine,”amesema.

Katika hatua nyingine,Majiliwa ametaja mbinu zinazofanywa na Serikali katika kukabaliana na tatizo la ajira  ni pamoja na kuweka msisitizo katika ujenzi wa viwanda nchini.

Waziri Mkuu Majaliwa ametaja mbinu nyingine ni kutoa fursa kwa wajasiriamali kubuni vifaa mbalimbali na kuimarisha eneo la elimu hasa ya ufundi.

Amesema  bado kuna changamoto kubwa  na kwamba ukubwa huo ni wakufikia soko la ajira la kufikia idadi ya raslimali watu wenye ujuzi zaidi ya milioni 15.

Waziri Mkuu amesema suala la changamoto ya ajira si kwa Tanzania tu bali ni duniani kote lakini kila nchi inatafuta mbinu za kukabiliana na changamoto hiyo ambapo amedai  moja kati ya mbinu muhimu ni kutoa fursa kwa wajasiriamali wabunifu kubuni vifaa mbalimbali na kwenda  kuvionyesha kwa lengo la kutafutia masoko.

“Pia, kuweka msisitizio katika ujenzi wa uchumi wa nchi kupitia viwanda kwa kukaribisha wawekezaji nchini wa kujenga viwanda vyenye ukubwa tofauti.Serikali inaendelea kukaribisha wawekezaji wa viwanda nchini na kwamba Tanzania inafursa nzuri ya kuendesha viwanda pamoja na malighafi nyingi,”amesema.

Majaliwa amesema  licha fursa ya viwanda, Tanzania ina uwepo wa ardhi nzuri unatoa fursa ya kupeleka vijana na watanzania  kwenye maeneo hayo kwa ajili ya kuajiriwa na pia kupata mbinu mpya za kujiajiri.

Amesema  wanaimarisha katika eneo la elimu  hasa kwenye vyuo vya ufundi ambapo nako pia kutatoa waajiriwa wengi sana

Kwa upande wake,Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema  kupitia maonyesho hayo wadau wataweza  kubadilishana mawazo ya nini kifanyike katika kuboresha utoaji wa elimu ya ufundi hapa nchini.

“Tutaweza  kukuza mashirikiano katika kuhakikisha vijana wanapata sehemu za kwenda kufanya mafunzo kwa vitendo.Serikali inatambua umuhimu wa elimu inayozingatia ujuzi na umahiri kwa vijana wetu katika kufanikisha mageuzi ya uchumi hapa nchini,”amesema.

Awali, Mwenyekiti wa  Uongozi wa Nacte, Profesa John Kandoro  amesema  Nacte itaendelea kwa juhudi kubwa kusimamia utoaji wa mafunzo na kuhakikisha elimu ya ufundi inatolewa kwa ubora unaotakiwa ili iweze kukidhi mahitaji ya soko la ajira la ndani.

Amesema mitaala ya umahiri inayotolewa na vyuo vya elimu ya mafunzo ya ufundi inawawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo zaidi na sio nadharia.

“Tatizo kubwa linalovikabili vyuo vyetu ni ukosefu wa nafasi za mafunzo kwa vitendo.Ukosefu huo unasababishwa na ushiriki mdogo wa wadau katika utoaji wa mafunzo na kwamba inatoka na wadau kutotilia maanani ushiriki wao katika utoaji wa mafunzo,”amesema.

Amesema changamoto hiyo inatokana na baadhi ya wanafunzi kushindwa kumudu gharama za mafunzo hayo.

Marie Stopes, Lavy Pads washerehekea hedhi salama

$
0
0

Na Irene Mark

Siku ya hedhi duniani huadhimishwa kila mwaka, siku ya tarehe 28 Mei. Siku hii ina lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali kwa dhumuni la kuongeza uelewa kuhusu maswala ya hedhi  na kuhamasisha upatikanaji maji safi na taulo (visodo)  kwa wasichana/wanawake hasa wale walio katika mazingira  magumu  ili wanapoingia katika siku zao za hedhi  waweze kujisitiri na kuendelea na shuguli zao kama kuhudhuria masomo na shughui nyingine.
 
Hedhi ni nini ?
Ni kipindi maalumu katika mzunguko wa mwanamke mwenye umri wa kuzaa. Wakati huo, ambao kwa kawaida unarudi kila baada ya mwezi mmoja hivi, yeye hutokwa na damu kwenye uke. Sababu ya damu kutoka ni kwamba, kijiyai kilichokomaa na kutoka nje ya kifuko cha vijiyai kisipopata mbegu ya mwanamume baada ya siku moja kinaharibika harakaharaka; hapo ngozi nyembamba ya tumbo la uzazi, iliyotanuka kwa damu ili kupokea na kulisha mimba, inajiengua  na kutoa damu.
Kumbe mbegu ikikifikia kijiyai, mimba inapatikana na kujishikiza kwenye kuta za tumbo la uzazi ili iendelee kukua; hapo damu haitoki na mama anaweza kujihisi mja mzito.Mizunguko mingi ya hedhi huwa na siku kadhaa za mwanzo ambapo mimba haiwezi kupatikana (muda wa kutoshika mimba kabla ya kudondosha kijiyai), halafu siku ambazo mimba inaweza kutungika, na kisha siku kadhaa tu kabla ya hedhi ambazo mimba haiwezi kutungika (muda wa kutoshika mimba baada ya kijiyai kudondoshwa).
Hedhi salama nini ?


Hedhi salama ni ile ambayo inahusisha mtoto wa kike/mwanamke kupata mahitaji yake yote muhimu akiwa kwenye siku zake za hedhi. Mahitaji hayo huhusisha taulo za kike ama pedi kama ijulikanavyo na wengi, maji safi na salama na sehemu ya kubadilishia. Wataalamu wa afya wanasema kuwa mtoto wa kike akipata hedhi salama basi ataweza kuondokana na matatizo mengi ya kiafya kama vile miwasho, fangasi pamoja na magonjwa mengine na hivyo huwa hedhi yenye amani na furaha.


Suala la hedhi halipaswi kuwa kero kwa mtoto wa kike. Hata hivyo, imekuwa tofauti kwa watoto wengi wa kike ambao wamekuwa wakipata wasiwasi na kukosa raha pindi wanapokaribia mzunguko wao. Hii inatokana na changamoto ambazo watoto hawa wa kike wanazopitia katika kupata hedhi salama.
Jambo la kusikitisha ni kwamba mara nyingi tumekuwa tukigusia tu masuala ya kiafya pindi tunapozungumzia hedhi salama na kusahau kuwa kukosekana kwa jambo hili kunaweza kuleta athari katika nyanja mbalimbali za maisha ya mwanamke huyu.  Baadhi ya mazingira yanayoweza kumkwamisha mtoto wa kike ni pamoja na:

Kutojihusisha katika shughuli mbalimbali za jamii kutokana na kukosekana kwa nyenzo ambazo zitamsaidia mtoto wa kike katika kipindi aonapo hedhi basi mara nyingi watoto hawa hujitenga katika shughuli mbalimbali kama vile shule, kazi, michezo, mikutano mbalimbali kwani huona aibu na hofu ya kuonekana kwa watu akiwa  na hali ile. Kutojihusisha na shughuli hizi huweza kuleta madhara makubwa sana kwa mtoto huyu wa kike na yanaweza kuwa ya papo kwa papo au ya muda mrefu.

Kukosa fursa kama mwanamke atakuwa wa kukaa tu nyumbani kipindi akiwa kwenye siku zake sababu tu amekosa vitu vya kumsaidia kupata hedhi salama basi ni wazi kuwa atakuwa anakosa fursa nyingi sana zinazoweza kujitokeza katika jamii yake kipindi yeye akiwa katika siku zake za hedhi
 
 
Ni kwa jinsi gani hedhi salama inahusiana na haki za binadamu?

Ni wazi kuwa kila mtu ana stahili haki za kimsingi bila kuangalia cheo wala taifa wala tabaka, wala jinsia, wala dini; anapaswa kufaidi haki zake za msingi kwa sababu tu yeye amezaliwa binadamu. Kuna baadhi ya haki za binadamu ambazo  mtoto wa kike atazikosa ikiwa tu hedhi salama itakosekana.

Haki kuthaminiwa utu wake, ikiwa mwanamke atakosa nyenzo ambazo zinzaweza kumsaidia kupata hedhi salama basi ni wazi utu wake kwa watu wengine wanaomtazama utashuka hasa kwa wale wasiolewa suala lake pindi watapomtazama. Embu fikiria maoni ya watu katika jamii yako yatakavyokuwa pindi watakapomuona msichana akitembea nguo yake ikiwa imechafuka na damu ya hedhi. Ni wazi katika jamii yetu ya hapa Tanzania wengi watamtazama kwa kumdharau na kumkebehi na ile aibu atakayoipata basi itaponza utu wake.

Haki ya kuwa kupata matibabu stahiki na kuwa na afya bora, wanawake wanaweza kukumbwa na matatizo mbalimbali ya kiafya pindi watakoshindwa kupata nyenzo muhimu za kuwasaidia wakati wakiwa katika siku zao za hedhi. Wanaweza pata fangasi, miwasho, maumivu sehemu zao za siri pamoja na madhara ya kisaikolojia yanayotokana na hali ya unyonge na aibu ya kujua madhara hayo yametokana na wao kukosa vifaa muhimu vya kujisitiri vinaweza kumfanya aone aibu kwenda kwenye kituo cha afya ili kupata matibabu.

Haki ya kupata elimu, mtoto wa kike anaweza shindwa kupata haki yake ya kupata elimu pindi awapo katika siku zake za hedhi kwa kuwa tu amekosa vitu vya kumsitiri kipindi hicho. Kipindi hicho kwake huwa kigumu kwani hushindwa kuhudhuria shule hali inayoweza pelekea matokeo mabaya na muda mwingine hata adhabu kwa walimu wasioelewa mazingira anayopitia binti huyu.

Haki ya kufanya kazi, kukosekana kwa vitu muhimu vya kujisitiri kwa mtoto wa kike kunaweza mpelekea akashindwa kufanya kazi au kupoteza fursa mbalimbali za kazi. Mwanamke huyu atalazimika kubaki nyumbani kwa muda wote atakaokuwa katika siku zake za hedhi na matokeo yake yanaweza kuwa ni kupoteza nafasi ya kazi au malipo aliyopaswa kupata kutokana na kazi hiyo. Embu fikiria wale watu wanaofanya kazi za malipo ya kila siku, ni wazi kuwa suala hili litaathiri kazi na kisha kipato chake.

Haki ya kutokubaguliwa na mtu au chombo chochote katika kutekeleza majukumu yake, Mwanamke anaweza kubaguliwa na watu wanaomzunguka pindi atakapokosa nyenzo muhimu za kujistiri akiwa katika siku zake. Jaribu kufikiria wale watu ambao bado wana imani potofu kuhusu damu ya hedhi ya mwanamke kuwa ni sumu na inaweza kusababisha mimea kukauka, chakula kuchacha, pombe kuwa chungu nk, anaposhuhudia damu ya hedhi ya mwanamke imesambaa kwenye nguo zake, ni wazi kuwa atamtenga na kumbagua. Na ubaguzi huo unaweza jitokeza katika mashule, na hata shughuli mbalimbali za jamii.

 
Kwanini wavulana kushiriki kwenye masuala ya hedhi ?
Ni muhimu wavulana kushiriki kupata Elimu ya musuala ya hedhi  kama washiriki wenza na kiini cha mabadiliko .
 
Maadhimisho ya siku ya hedhi


Katika kuadhimisha siku ya hedhi duniani , shirika la Marie stoipes Tanzania kushirikiana na Lavy Limited Company watatembelea baadhi ya shule na kutoa Elimu ya masuala ya hedhi kwa wasichana lakini  ushirika huu utaweza kuwashika mkono wasichana kwa kutoa  Zawadi mbalimbali ikiwemo taulo za kike.
 
Wito
Kwa mashirika ya afya ,  mashirika ya maendeleo na taasisi mbalimbali kuzisaidia jamii kwa namna mbalimbali  kuhakikisha wasichana hasa walio mashuleni wanakuwa na mazingira rafiki ili wanapoingia kwenye siku zao za hedhi wasikose mahitaji yao muhimu yatakayowasababisha kushindwa kushiriki kwenye masomo na masuala mengine ya jamii kutokana na hedhi.


Kuliangalia suala la upunguzaji wa garama za taulo za kike, upatikanaji wa maji safi na salama katika shule , kusaidia maeneo yenye uhitaji ili wasichana waweze kupata taulo za kujisitiri kwa muda wa mwaka mzima ili wasiweze kukosa mahudhurio shuleni.
 
Ushauri
Kwa wasichana wanaokutana na changamoto za hedhi ikiwemo maumivu yasiyo ya kawaida basi watembelee vituo vya afya vilivyo karibu nao kwa msaada zaidi. Lakini pia wanaweza kutupigia Marie stopes bure 0800 753 333 kwa ajili ya ushauri wa masuala ya hedhi na wanaweza pia kutembelea vituo vyetu vilivyopo Dar es salaam, Zanzibar, Mwanza, Musoma, Kahama, Arusha , Iringa , Mbeya na Kimara .


MAJALIWA: MARA WEKENI MKAKATI WA KUITANGAZA MBUGA YA SERENGETI

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mara kwenye ukumbi wa Bishop Rudin uliopo kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya Mwembeni mjini Musoma, Mei 18, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).



 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mara kwenye ukumbi wa Bishop Rudin uliopo kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya Mwembeni mjini Musoma, Mei 18, 2021.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhandisi Robert Gabriel na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mara, Samweli Kiboye. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa Mkoa wa Mara na Watendaji katika Sekta ya Utalii wabadilike na waweke mkakati wa kuitangaza mbuga ya Serengeti ili kuweza kuvutia zaidi watalii na kuitambulisha mbuga hiyo kuwa iko mkoa humo.
 
Amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan inaboresha mazingira ya uwekezaji na biashara ili kuvutia uwekezaji utakaoinua uchumi wa nchi na watu na mwongozo huo ni sehemu ya utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuvutia uwekezaji na kuimarisha biashara.
 
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Mei 28, 2021) wakati akizindua Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Mara katika Ukumbi wa Bishop Rudin uliopo katika viwanja vya Mwembeni mjini Musoma. Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaagiza viongozi wa mkoa huo wahakikishe watendaji, wataalamu na wananchi wanakuwa nyenzo ya kurahisisha kazi ya kuvutia uwekezaji.
 
“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa hakikisha watendaji wote wa mkoa wanausoma na kuuelewa ipasavyo mwongozo huu. Hakikisha watendaji wako wanatekeleza majukumu yao kwa weledi, uadilifu na uaminifu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa”.
 
Waziri Mkuu amesema mkoa huo una fursa nyingi za uwekezaji ambazo endapo zitatumika vema, zinaweza kuipaisha nchi kimaendeleo. “…Nitoe wito kwa uongozi mzima wa mkoa uhakikishe unaratibu vilivyo shughuli za uzalishaji hasa wa malighafi, bidhaa na huduma mbalimbali kwa ajili ya wananchi na mahitaji ya viwanda vya ndani.
 
Amesema miongoni mwa maeneo ambayo mkoa wa Mara unaweza kunufaika zaidi kwenye uwekezaji kutokana na fursa zilizopo ni kilimo, mifugo na uvuvi. Serikali ilitoa maelekezo yenye lengo la kuboresha sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ili kuzalisha malighafi za kutosha zitakazotumika kwenye viwanda.
 
Wakati huo huo, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Uwekezaji ishirikiane na mkoa ili kuwezesha Kituo cha Uwekezaji cha Kanda (TIC) kilichopo mkoani Mwanza kuanzisha Kituo cha Kutolea Huduma kwa Pamoja (One Stop Centre) ambacho kinapaswa kuwa na rasilimali za kutosha, vifaa na wataalam wote muhimu.
 
“Watu wote muhimu wanaopaswa kutoa huduma katika kituo wawepo, wakiwemo wataalamu wa Ardhi, Biashara, Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO), Wakala wa Vipimo, NEMC, Bodi ya Nyama, Bodi ya Maziwa”.
 
Pia Waziri Mkuu ameziagiza idara zote za kisekta katika ngazi ya mikoa na wilaya, zishirikiane katika kubuni njia rahisi zitakazosaidia kuondoa urasimu na kurahisisha uwekezaji katika maeneo yao ili kuongeza ajira na vyanzo vya mapato ya Serikali.
 
“…Viongozi na watendaji wa sekta ya umma, fanyeni vikao na sekta binafsi kupitia Mabaraza ya Biashara ili kujadili na kutatua kero za kibiashara na uwekezaji zinazowakabili kwa wakati”.
 
Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amezitaka mamlaka husika zihakikishe zinaweka mipango ya urasimishaji sekta isiyo rasmi, kurasimisha namba msimbo, kuwapatia wafanyabiashara ndogo ndogo maeneo ya kufanyia biashara na kuongeza kasi ya upimaji ardhi na kasi ya utekelezaji wa anuani za makazi na postikodi kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuchochea fursa za kibiashara.
 

WAJASILIAMALI WAASWA KUZALISHA BIDHAA ZENYE BORA

$
0
0
 

********

Wajasiriamali kote nchini wameaswa kuzalisha bidhaa zenye ubora ili kuweza kuhimili ushindani katika soko la ndani na kimataifa.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya SIDO kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Kwaraa Babati mkoani Manyara.

Naye Meneja wa Uthibiti Ubora wa TBS Bw.Gervas Mwanjabalaakizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho hayo, alisema maonesho hayo yamekuwa fursa muhimu ya TBS kutoa elimu ya masuala ya viwango kwa wajasiriamali waliokusanyika kutoka sehemu mbalimbali nchini na vilevile n fursa ya kusikiliza maoni na changamoto za wajasiriamali na wananchi kwa ujumla na kutafutia ufumbuzi changamoto hizo.

.“Ushiriki katika haya maonesho umetufanya tuweze kukutana na wadau wenye viwanda,wananchi, wajasiriamali na kuweza kuwaelimisha kuhusu masuala ya viwango pamoja na kusikiliza changamoto zao”. Amesema Bw. Mwanjabala.

Aidha Meneja wa kanda ya kaskazini wa TBS, Bi. Happy Brown aliwataka wajasiriamali wote katika kanda hiyo kutosita kutoa taarifa zozote ili waweze kusaidiwa na hata kupatiwa ushauri wa kitaalam ili waweze kuzalisha bidhaaa bora.

Kwa upande wake Afisa Masoko wa TBS Bi. Deborah Haule amesema muitikio wa watu katika maonesho haya umekuwa mkubwa na wajasiriamali wengi wamejitokeza kutaka kufahamu zaidi kuhusiana na taratibu za kufuata ili kuthibitisha ubora wa bidhaa zao.

Amesema wajasiriamali wadogo nchini hawaingii gharama zozote bali wanatakiwa kupitia SIDO ili watambulike na wakipata alama ya ubora wanaweza kufikia masoko mbalimbali hasa ya Afrika Mashariki na zitaweza kuvuka mipaka ya nchi hizo bila vikwazo vyovyote.

Pamoja na hayo Bi. Deborah amesema TBS inawahimiza wahakikishe wanazalisha bidhaa zilizo na ubora hatua itakayosaidia kulinda mitaji yao na kuhimili ushindani kwenye soko la kitaifa na kimataifa.

KIVUMBI CHA MASHINDANO YA UMITASHUMTA MKOA WA PWANI CHAZINDULIWA RASMI

$
0
0

 


Baadhi ya wanafunzi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga wakiwa katika maandamano huku wakipiga saluti kwa mgeni rasmi hayupo picha wakati wa ufunguzi wa michuano ya umoja wa michezo na taaluma kwa shule za msingii (UMITASHUMTA) ngazi ya Mkoa wa Pwani yamefunguliwa rasmi katika viwanja vya shirika la elimu Kibaha.


 
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Edrward Mwakipesile ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika ufunguzi huo wa mashindano akizungumza na wanafunzi, walimu, maaafisa michezo pamoja na maafisa utamaduni.

 

 

NA VICTOR MASANGU, PWANI 

 

MASHINDANO ya umoja wa michezo na taaluma kwa shule za msingi i (UMITASHUMTA) ngazi ya Mkoa wa Pwani yamefunguliwa leo rasmi katika viwanja vya shirika la elimu Kibaha kwa kuwashirikisha wanamichezo wapatoa 637 kutoka halmashauri zote tisa na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja , viongozi wa vyama vya michezo pamoja na walimu.

Akifungua mashindano hayo Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Edrward Mwakipesile ambaye alikuwa ni mgeni rasmi amewataka wanamichezo hao ambao ni wanafunzi wa shule za msingi kutoka halmashauri mbali mbali kuhakikisha kwamba wanakuwa na nidhamu katika kipindi chote cha michuano hiyo.

Aidha aliwahimiza kucheza kwa juhudi zote na kuonyesha vipaji vyao ambavyo vitaweza kuwafanya kuweza kuchaguliwa katika suala zima la kuunda  kikosi cha timu ya Mkoa mabcho kinatarajiwa kwenda kushiriki katika michuano ya ngazi ya Taifa mwezi wa sita Mkoani Mtwara.

 

“Kitu kikubwa kinachotakiwa ni kuhakikisha kwamba pamoja na kuwa nyinyi  ni wanafunzi lakini ni wana mchezo hivyo katika kipindi hiki chote cha mashindano haya ambayo yameandaliwa maalumu kwa ajili ya kuweza kuchagua timu ya Mkoa wa Pwani ili kiweze kushiriki katika michuano ya Kitaifa mimi ninawaomba wachezaji wote ambao watachaguliwa kucheza kwa bidii pamoja na kujituma wakati wote,”alisema Mwakipesile.

Pia  aliwataka  wanafunzi hao kuhakikisha kuwa wanatumia fursa za michezo mbali mbali katika kutimiza ndoto zao ikiwemo kujipatia ajira kupitia nyaja ya michezo katika siku za usoni na kuwaomba kuzingatia taratibu na sheria zote ambazo zinatumika katika michezo hiyo.

 

Mwakipesile pia hakusita kuwaomba walimu pamoja na maafisa michezo kuwa na ushirikiano wa pamoja katika kuhakikisha wanafanya uteuzi wa kuchagua kikosi bora amabcho kitaweza kuuuletea heshima Mkoa wa Pwani katika  michuano hiyo ngazi ya Taifa kwani anatambua kutakuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na Mikoa mbali mbali kujiandaa vya kutosha.

Katika hatua nyingine Mwakipesile aliwataka waamuzi mbali mbali amabo wanachezesha katika michezo tofauti kuzingatia miongozo yote  n ataratibu ikiwemo sambamba na kuhakikisha wanatenda haki bila ya kuwa na upendeleo wowote lengo ikiwa ni kupata wawakilishi ambao wana uwezo katika kutimiza wajibu wao,

Aidha alisema kwamba serikali ya Mkoa wa Pwani itaendelea kushirikiana bega kwa began a walimu wa michezo, maafisa michezo pamoja na maafisa utamaduni katika kuleta mabadilio chanya ya kukuza vipaji kwa wanafunzi mashuleni na kuwahimiza waweke mikakati ya kwenda kujiendeleza zaidi katika vyuo ambavyo vimetengwa kwa ajili ya kufundisha micheoz.

 

Kwa Upande wake Kaimu Afisa Elimu wa Mkoa wa Pwani Hildegard Makundi alisema kwamba katika mashindano hayo yameweza kuwajumisha wanafunzi wapatao 637 kutoka katika halmashauri zote tisa za Mkoa wa Pwani.

Alifafanua kwamba katika mashindano hayo michezo mbali mbali itachezwa ikiwemo mchezo wa soka, Riadha, netiboli, kurusha tufe pamoja na mingineyo na kwamba baada ya hapo watachaguliwa wachezaji 86 ambao wataunda kikosi cha Mkoa wa Pwani kwa ajili yakwenda kushiriki katika hatua ya ngazi ya Taifa Mkoani Mtwara.

“Leo ndio tumefungua rasmi mashindano yetu haya kwa shule  mmbali mbali za msingi na kwamba kwa sasa tuna jumla ya wanamichezo wapatao 637 lakini baada ya kumalizika kwa mchujo ambao utafanywa na walimu tutabakisha wachezaji wapatao 86 tu ambao ndio sasa wanauwakailisha Mkoa wetu wa Pwani katika mashindano ya Taifa,”alisema Kaimu huyo.

 

Naye Afisa michezo wa Mkoa wa Pwani Grace Buleta alibainisha kwamba lengo lao kubwa ni kuhakikisha kwamba katika msimu huu wa mwaka wa 2021 wanafanya vizuri katika michuano hiyo ngazi ya Taifa na kuwaomba wadau wa michezo mbali mbali kutoa sapoti na ushirikiano wakati wa kipindi chote timu itakapokuwa katika Mkoani Mtwara kwa lengo la kurudi na ubingwa.

WAITARA ATAKA TATHMINI MV MBEYA II

$
0
0

 

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, akishuka katika chelezo kilichopo bandari ya Kiwira, mara baada ya kukagua chelezo hicho wilayani Kyela, Mkoani Mbeya.

 

 

 

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mwita Waitara, amezitaka taasisi za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Shirika la Wakala wa Meli (TASAC), Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kufanya tathmini ya kina kabla ya kuanza matengenezo ya meli ya MV Mbeya II.

 

Ametoa kauli hiyo wilayani Kyela baada ya kukagua miundombinu katika bandari za Kiwira na Itungi na kubaini ucheleweshaji wa matengenezo ya Meli hiyo iliyosimama kutoa huduma katika Ziwa Nyasa mapema mwezi Aprili kutokana na hitilafu za kifundi.

 

“Meli hii imesimama zaidi ya wiki tatu sasa na ninajua meli hii bado iko kwenye muda wa uangalizi hivyo ninawaagiza TPA, TASAC, DMI na Kampuni ya Songoro kukaa na kuwasilisha ripoti haraka iwezekaavyo ili matengenezo yaanze” ameagiza Naibu Waziri Waitara.

 

Naibu Waziri Waitara amesema fedha za Serikali zilizowekezwa kwenye ujenzi wa meli zilirahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo kwa wananchi wanaozunguka Ziwa Nyasa kwa nchi za jirani na kuitaka TPA kurejesha huduma mapema iwezekanavyo.

 

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Waitara imeitaka Kampuni ya Songoro Marine kufanya tathmini ya Chelezo ambayo imekuwa bandarini Kiwira kwa zaidi ya mwaka bila kufanyiwa matengenezo  ili kujiridhisha na ufanisi wake kabla ya kupandisha meli zinazohitaji matengenezo.

 

Akiwasilisha taarifa yake kwa Naibu Waziri Waitara Kaimu Meneja wa Bandari katika Ziwa Nyasa Abdallah Mohammed amesema  kuwa tangu kuanza kutumika kwa meli ya MV. MBEYA II kumekuwa na changamoto mbalimbali za kiufundi ambazo Mamlaka imekuwa ikielekeza Kampuni ya Songoro kuzirekebisha.

 

“Mamlaka ya Bandari ilileta wataalamu kukagua Meli hii na walibaini kuwepo kwa hitilafu kwenye baadhi ya mifumo na imekuwa ikirekebishwa mara kwa mara”. Amesema Mohamed.

 

Meli ya MV Mbeya II ni moja ya meli tatu ambazo zimejengwa na TPA kwa fedha za ndani lengo likiwa ni kuboresha usafirishaji wa abiria na mizigo Ziwa Nyasa, meli nyingine ni pamoja na MV. RUVUMA na MV. NJOMBE.

 

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.


NMB yazindua jukwaa la kuwawezesha vijana

$
0
0

 

 

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu, Patrobas Katambi  (wapili kulia), Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe (wa tatu kulia) na Afisa Mkuu wa wateja binafsi na Biashara Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa tatu kushoto), wakizindua kwa pamoja Jukwaa la Vijana ‘Go na NMB’ lenye lengo la kutoa elimu ya kifedha pamoja na fursa za mikopo kwa vijana. Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. (Na Mpiga Picha Wetu).


Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu, Patrobas Katambi  (watatu kulia), Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe (wapili kulia) na Afisa Mkuu wa wateja binafsi na Biashara Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa tatu kushoto), wakifurahia baada ya uzinduzi wa Jukwaa la Vijana ‘Go na NMB’.


 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu, Patrobas Katambi  (watatu kulia), akipeana mkono na Afisa Mkuu wa wateja binafsi na Biashara Benki ya NMB, Filbert Mponzi, mara baada uzinduzi wa Jukwaa la Vijana ‘Go na NMB’.


Na Mwandishi Wetu
 
Benki ya NMB imeanzisha utaratibu wa kipekee wa kuwasaidia vijana nchini kupitia jukwaa la huduma suluhishi za kibenki utakaowawezesha kifedha na kuwakwamua kiuchumi.
 
Serikali imeukubali na kuunga mkono mpango huo wa huduma maalumu za kibenki kwa ajili ya vijana ambao kibiashara unaitwa ‘Go na NMB’ kwa sababu unaendana na sera zake za kuwashirikisha katika ujenzi na maendeleo ya taifa.
 
Katika hotuba yake ya kulizindua rasmi jukwaa hilo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi, alisema kuanzishwa kwake kumekuja wakati muafaka na ni uwekezaji stahiki.
 
Hii ni kutokana na umuhimu na unyeti wa kada ya vijana kwenye shughuli za uzalishaji mali kwani wao ni raslimali watu ya msingi kiuchumi na katika maendeleo ya nchi kwa ujumla. Kwa mantiki hiyo, naibu waziri huyo alifafanua, lazima vijana wawe na ufahamu mkubwa wa maswala ya pesa, wahusishwe kifedha, wasaidiwe kibiashara na kuwezeshwa kiuchumi.
 
“Jukwa la ‘Go na NMB’ ambalo ninalizindua rasmi leo linayazingatia hayo yote na ndiyo maana serikali inaliunga mkono kwani mikakati bunifu kama hii inatusaidia sana kuzikabili changamoto mbalimbali za vijana,” Katambi alisema.
 
Pia kiongozi huyo alisema kuwa sifa moja kubwa ya jukwaa hilo ni kutobagua vijana watakaonufaika nalo kwani lipo kwa ajili ya vijana wote wa Kitanzania. Wawe ni wakulima, walioajiriwa ua kujiajiri na hata wanafunzi wa vyuo vikuu na vya kawaida, wote watasaidiwa na kuhudumiwa, alisisitiza.
 
Benki ya NMB imesema jukwaa la ‘Go na NMB' ni maalumu kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya kibenki ya vijana lililoongezwa thamani kuwavutia ambalo litakuwa msingi wa kuwajenga na kuwapa uwezo wa kujitegemea kwa kuwapatia suluhishi za kifedha huku likitanguliza mbele maslahi yao pamoja na ndoto walizonazo.
 
Moja ya malengo ya NMB katika hili ni kuwahudumia vijana kisasa zaidi na ni mpango mkakati wake kupanua wigo wa wateja kwa kujenga mazingira bora ya huduma za kibenki kwa vijana ili wao na benki hiyo waweze kuchangia kikamilifu ukuaji wa uchumi wa taifa.
 
Jukwaa la ‘Go na NMB’ ambalo ni kwa ajili ya nchi nzima ni soko la rejareja kwa vijana litakalokuwa nembo maalumu ya huduma za kidijitali za NMB. Mkazo wa jukwa hilo la kwanza sokoni utaelekezwa kwa vijana wanaojishughulisha kwenye shughuli rasmi na zisizo rasmi hususani wanaojishughulisha na  kilimo, biashara ndogo ndogo na za kati pamonja na wanafunzi wa ngazi zote mpaka wa vyuo vikuu.
 
Akizungumza kwenye tamasha la uzinduzi wa ‘Go na NMB’ jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Bw Filbert Mponzi, alisema kila kijana ana haki ya kupata huduma salama inayofikika kwa urahisi na yenye tija.
 
Ni kwa kuzingaitia hilo, na wajibu wake wa kuwasaidia ili wakue kama Watanzania wenye mchango kwenye uchumi na maendeleo ya nchi yao, ndiyo maana ‘GO na NMB’ imeanzishwa.
 
“Dhamira yetu ni kutanua wigo wa huduma zetu ili tuwafikie vijana wote. Hii itawawezesha vijana wengi zaidi kufikiwa na huduma za kifedha huku ikiwasaidia kujenga utamaduni wa kuwa na nidhamu ya fedha wanapoandaa maisha yao ya baadae hatua ambayo pia itakachangamsha uchumi wa nchi,” Mponzi alisema.
 
“Tunafanya haya yote tukiwa sambamba na malengo ya maendeleo ya Serikali yakiwemo ya utoaji wa huduma salama na bora za kifedha kwa jamii nzima,” alisisitiza na kuongeza:
 
“Takwimu mbalimbali zinaonyesha kuwa Tanzania ina vijana takribani asilimia 64 hivyo kufanya kundi hili kuwa sehemu muhimu ya ukuaji wa uchumi. Benki ya NMB imejipanga kuwafikia wote, kuanzia wanafunzi mpaka vijana wenye shughuli za uzalishaji kwenye sekta zote za uchumi.”
 
Awali, meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, alisema faida na huduma wezeshi za kifedha za jukwaa la ‘Go na NMB’ ni nyingi na zenye tija kimaendeleo binafsi na taifa kwa ujumla.
 
Huduma hizo ni pamoja na kujiunga kidijitali, kupata nafasi ya kushiriki promosheni na kujishindia zawadi zitakazokuwa zinatolewa kupitia vituo vya mauzo vya NMB pamoja na kupata mikopo nafuu ya bodaboda na Pikipiki za miguu mitatu.
 
Nyingine ni bima ya bure ya simu za mkononi, mafunzo ya uelewa wa masuala ya kifedha na kupata fursa za kuhudhuria matukio mbalimbali kama makongamano ya wanafunzi vyuoni, fursa za mafunzo kwa wanafunzi na kupata huduma ya mtandao ya bure kwenye baadhi ya vyuo vikuu

Taaasisi ya MOI ina uhitaji wa damu

$
0
0

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dkt. Respicious Boniface.

 

NA ASHA MWAKYONDE. DAR ES SALAAM

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dkt. Respicious Boniface amesema taasisi hiyo inauhitaji mkubwa wa damu kutokana na asilimia 65 ya wagonjwa wanaopokelewa wanahitaji kufanyiwa upasuaji.

Haya aliyasema jijini Dar es Salaam juzi wakati wa maadhimisho ya siku ya Wauguzi yaliyofanywa na waungzi wa taasisi hiyo, alisema MOI ni taasisi ya ubongo na mifupa na ni ya ajali matibabu mengi yanahitaji upasuaji.

Mkurugenzi huyo alisema asilimia 65 ya wagonjwa wanaofika MOI wataingia katika chumba cha upasuaji  ambao ni mrefu na kwamba sio wa muda mfupi.

Alitolea mfano upasuaji wa kutoa  uvimbe kwenye ubongo upasuaji wake ni mrefu na unahitaji damu  na kwamba watu waliopata ajali wanatoka damu hivyo uhitaji ni mkubwa katika taasisi hiyo.

" Damu haitengenezwi hakuna kiwanda cha damu hivyo tunawaomba Watanzania kuja kuchangia damu. Na nyie waandishi kupitia taaluma yenu tunaomba muhamaisishe jamii kuchangia damu, " alisema Dkt.Boniface.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA)  Tawi la MOI, Mosee Moses alisema damu imekuwa ni changamoto kubwa kwao kwa kuwa wanaishi na wagonjwa  na kwambwa waliliona kuna sababu ya kuihamasisha jamii kuchangia damu kwa muda wa siku tatu.

Alisema kuwa katika chupa walizozipata 133 kiwango kikubwa kimetoka kwa wauguzi ikiwa ni ujmbe kwa jamii ili iweze kuelewa changamoto waliyonayo

" Ukiwa na lishe njema unakuwa na kiwango kizuri cha damu unasaidia mwenzako  na unakuwa uneokoa maisha yake kwani damu hutibiwa kwa damu,' alisema Moses.

Kwa upande wake Miss Tanzana 2020/ 2021, Rose Manfere alisema kikubwa zaidi katika maadhimisho hayo wameweza kuchangia damu na kuokoa maisha ya watu wengine.

" Leo nimejumuika na Wauguzi wa MOI kwenye maadhimisho haya ya siku ya Wauguzi duniani ikiwa tumeanza tangu Mei 26 hadi 28 ambapo tunaendelea kuadhimisha "alisema.

ACT yahimiza mshikamano

$
0
0

 Mjumbe  wa  Kamati Kuu ya  Chama  cha  ACT  Wazalendo ambae  pia  ni  Makamo  wa Kwanza  wa  Rais Zanzibar    Othman  Masoud  Othman  amewataka  wanachama wa chama  hicho  kushikamana  kwa pamoja  ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa.

 

Kauli hiyo  alitoa huko  shangani Mkokotoni Wilaya ya Kaskazini A Unguja wakati kikao cha kutambulishwa kwake kwa viongozi na wafuasi wa chama hicho.

 

 Alisema umoja na  mshikamano  uliomo  ndani  ya  chama hicho  ndio  uliokipa  nguvu  na  heshima  ndani  ya  Zanzibar  na Tanzania  kwa  ujumla.

“Wazee  wetu  walisema  umoja  ni  nguvu  na  utengano  ni  udhaifu na  ambapo mshikamano huo   ndio uliopelekea uimara wa chama  ”

 

Alieleza  kuwa  mshikamno uliopo  ndani  ya  Act Wazalendo  imepelekea  kuzuia  migogoro  na malumbano  ndani  ya  chama hicho.

 

“Kwa sababu  ya  mshikamano  wetu  tumekuwa  hatuyumbi  katika  kudai haki pamoja na  mamlaka  ya Zanzibar  ndani  ya  Tanzania  na  nje  ya Tanzania ”  alisema Othman.

 

Alifahamisha  kua  wanzanzibar  na  watanzania  wengi  wanaingia  katika chama  cha  Act  wazalendo  kwa  kile  alichokitaja  kuvutiwa  na mashirikiano, Juhudi  na  dhamira njema.

 

Aliwataka  wafuasi wa chama  hicho  kutoichezea dhana  waliyonayo kwani ndio   njia  pekee yakufikia  kule  waliko kusudia  kuongoza Zanzibar  na Tanzania kwa ujumla.

 

Aidha alisema ili  kuyaenzi  aliyoyaacha kiongozi  wetu marehemu  maalim  Seif  Sharif  Hamad ni  kuendeleza umoja na mshikamano alioupigania kwa miaka   mingi uhai wake na historia ya  nchi  ya  Zanzibar.

 

Mjumbe  huyo  wa  kamati  kuu alisema  kuwa  mshikamano  umewajenga  ari  wanachama na  kuweza  kushindana  na  watu  waliokuwa  na  nguvu  ya  dola na  kueleza  kuwa  chama  hicho  kinajivunia  rasilimali  watu.

 

Sambamba  na  hayo  alisema  chama  cha  Act  wazalendo  kimeingia  katika serikali ya  umoja  wa kitaifa  GNU kwa ya kuleta  umoja  na  mshikamano  bila  ya  kujali  madhila waliyopitia  kutokana na  nguvu  kubwa  walizotumia  watawala.

“Tunalopigania  tuendeshe  nchi  yetu  kistarabu pasina mtu  yoyote  kupata  madhara  wakati  wa uchaguzi  na baada  ya  uchaguzi kwani tuna haki ya  kuishi  kwa  amani  katika  nchi  yetu.”alisema.

Mapema makamo mwenye  kiti  wa chama  hicho  Juma  Duni  Haji  akimtambulisha kiongozi huyo  alimtaka kuyasimamia  yote aliyoyaacha maalim Seif ambayo  yana  maslahi  Zanzibar pamoja  na  chama  kwa  ujumla.

“leo  nakutambulisha  kwa viongozi  wa  mikoa  ninachokuomba sasa usikae  nyuma  tuanze  kazi  ya  kujenga  chama  na kupigania  haki za wazanzibar” alisema Babu Juma.

Alisema kuwa Mjumbe huyo awali alikuwa msaidizi Mkubwa wa maalim Seif sharif wakati wa Uhai wake hasa kwa upande wa sheria.

Kwa upande  wake  katibu  wa  habar  na  uenezi  wa chama  hicho  Salum Abdalla Bimani alisema nchi  hii inataka  demokrasia  ya  kweli  yenye  maelewane  ili  nchi  iweze  kuneemeka  kutokana mashirikiano anamini  Zanzibar  itarudi  kwenye  hadhi yake.

“Mshikamano  na  umoja  wetu  ndani  ya  Zanzibar  utapelekea  kupata viongozi ambao watachaguliwa na wananchi kwa maana kwamba Yule aliyeshinda  katika  uchaguzi  apewe haki  yake”alisema Bimani.

 Akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa Mkoa wa Kaskazini A Kichama  Ali Angali Ali kwa niaba ya wafuasi wa chama hicho alisema wakotayari kumpatia mashirikiano yale ambayo yatampatia nguvu katika kutekeleza majukumu yake kichama na kiserikali.


SHAMBA LENYE EKARI 100 LINAUZWA,LIMEPIMWA

$
0
0

Shamba lenye Ekari 100  ambalo tayari limeishapimwa linauzwa .

Mahali: Shungumbweni, Mkuranga karibu na Kiwanda cha Chumvi Neel Salt

Bei: Mil.150,000,000 (mazungumzo yapo) .

Umbali: Kilomita 5 kutoka baharini, Kilomita 26 kutoka barabara kuu ya Dar-Lindi, (Unaweza Ingilia kwa njia ya Kibada-Mwasonga pia).

Shamba lina miti ya mikorosho na mianzi,kisima cha maji safi mita 72, kinatoa lita 20,000 kwa saa.


KWA MAWASILIANO ZAIDI 0763000053

VIONGOZI TUMIENI WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2021 KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WATUMISHI WALIOPO PEMBEZONI

$
0
0
Na James Mwanamyoto-Karema


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro amewataka viongozi katika Taasisi za Umma kutumia Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka huu kutembelea maeneo ya pembezoni ili kusikiliza na kutatua kero na changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma, ikiwa ni pamoja na kupokea maoni na mapendekezo ya namna bora ya kuboresha Utumishi wa Umma nchini. 

 

Dkt. Ndumbaro amesema hayo katika Tarafa ya Karema akiwa ameambatana na Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome pamoja na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu ambao kwa pamoja wamehimiza uwajibikaji na ufanisi kiutendaji katika taasisi zinazosimamia utoaji wa haki kwa wananchi.

 

Aidha Dkt. Ndumbaro amewata viongozi katika Taasisi za Umma kuhakikisha wanajenga utamaduni wa watumishi kufanya kazi kwa bidii, na kuongeza kuwa utamaduni huo utajengwa kwa kutambua na kuwapongeza wanaofanya kazi kwa juhudi na maarifa na kwa wanaolegalega warekebishwe ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi.

 

Amefafanua kuwa, watumishi wanaochapa kazi wakipongezwa kwa kuandikiwa barua au kupewa cheti kutokana na mchango wao ndio njia pekee itakayowawezesha waajiri kujenga utamaduni wa watumishi kufanya kazi kwa bidii na weledi. tofauti na kuchukua hatua hiyo morali ya watumishi wanaowajibika ipasavyo itashuka kwa kiwango kikubwa.

 

Akizungumzia kuhusu mtazamo hasi wa baadhi ya watumishi wa Tarafa ya Karema kuamini kuwa wanafanya kazi katika mazingira magumu sana, Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amewataka kubadili fikra zao kwani Serikali imewaajiri kwa lengo la kuwahudumia wananchi wa eneo hilo na si kuwapa adhabu kama baadhi yao wanavyodhani.

 

Dkt. Jingu amewaambia watumishi hao kuwa, Utumishi wa Umma ni popote hivyo amewataka kutumia fursa zilizopo katika Tarafa ya Karema kuongeza kipato na kuboresha maisha yao.

 

Naye, Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome amesema katika sheria na masuala ya katiba ndio taifa linapata mfumo wa utoaji haki ambapo haki zipo za aina nyingi kama vile haki madai, haki jinai pamoja na haki utawala inayosimamiwa na Katibu Mkuu - UTUMISHI kuhakikisha inakwenda sawasawa ili wananchi wapate huduma bora katika Taasisi za Umma.

 

Sanjali na hilo, Prof. Mchome amesema, migogoro ya ardhi iliyopo Karema ni changamoto kama ilivyo kwenye maeneo mengine, hivyo amewataka watumishi kushirikiana na wananchi hususani wazee wenye busara katika kutatua migogoro hiyo kwa njia ya usuluhishi badala ya kukimbilia Mahakamani kwani Mahakama kwa mujibu wa Katiba ni chombo cha mwisho cha utoaji haki.

 

Ziara ya Makatibu Wakuu hao mkoani Katavi ililenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi mkoani humo.

WAZALISHAJI WA MAZIWA TANGA WAJIUNGA NA NHIF KWA KUWEZESHWA NA BENKI YA CRDB

$
0
0
Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB Dkt. Joseph Witts kushoto akiwa Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa NHIF, Christopher Mapunda kulia wakisaini  makubaliano na Wazalishaji wa Maziwa kupitia chama cha TDCU linaashiria utekelezaji wa makubaliano ambayo Benki ya CRDB na NHIF  wataweza kunufaika na mpango wa Ushirika Afya unaoratibiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kuwezeshwa kujiunga na Benki ya CRDB kupitia Chama cha Ushirika cha Wazalishaji wa Maziwa Tanga mjini (Tanga Diary Cooperative Union(TDCU) kulia ni Meneja wa CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa halfa ilifanyika Jijini Tanga.
Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB Dkt. Joseph Witts kulia wakibadilishana hati za makubaliano na Mwenyekiti wa  TDCU Shamte Saudi mara baada ya kuingia makubaliano hayo wanaoshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima na Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tanga Jackline Senzighe.

 

WAZALISHAJI wa Maziwa Tanga mjini wataanza kunufaika na mpango wa Ushirika Afya unaoratibiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kuwezeshwa kujiunga na Benki ya CRDB kupitia Chama cha Ushirika cha Wazalishaji wa Maziwa Tanga mjini (Tanga Diary Cooperative Union(TDCU).

Hatua hiyo inatokana na kuingia makubaliano na Wazalishaji wa Maziwa kupitia chama cha TDCU linaashiria utekelezaji wa makubaliano ambayo Benki ya CRDB na NHIF waliingia siku chache zilizopita za kuwawezesha wana ushirika kujiunga na bima ya afya kwa utaratibu wa Ushirika Afya. 

Katika makubaliano hayo, Benki ya CRDB itamlipia mwana ushirika michango ya bima ya afya kwa wakati na mwana ushirika huyu atairejesha bila riba wakati wa msimu wa mauzo. 

Akizungumza katika uzinduzi wa mpango huo, Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa NHIF,Christopher Mapunda amesema kuwa ushirikiano huo na Benki ya CRDB ulianza tangu Mei 5, 2021 kwa pande zote mbili kusaini Makubaliano ambayo yatawawezesha wanachama walio kwenye Vyama vya Ushirika kunufaika na huduma za matibabu kupitia bima ya afya bila kuwa na changamoto ya kifedha.

 

“Mfuko umeazimia kuwafikia watanzania wote na huduma za Bima ya afya ili waweze kupata huduma za matibabu kwa urahisi ndio maana tumekubaliana na Benki ya CRDB ambao ni wadau wakubwa wa wana ushirika nchini kuwawezesha wana ushirika kujiunga na bima ya afya bila changamoto ya kifedha”alisema Mapunda.

 

Akizungumzia huduma, Mapunda alisema kuwa mwana ushirika na familia yake atapata huduma zote za matibabu katika mtandao mpana wa vituo zaidi ya 8,000 Tanzania Bara na Zanzibar kuanzia ngazi ya Zahanati hadi Hospitali ya Taifa.

 

Akizingumza katika tukio hilo, Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB Dkt. Joseph Witts amesema Benki ya CRDB iko mstari wa mbele katika kuhudumia wana ushirika kwa namna mbalimbali na sasa inamwezesha mwana ushirika kujiunga na bima ya afya kwa kulipia michango yake kwa mwaka ili wakati wa mauzo ndipo airejeshe bila riba yoyote juu yake.

 

“Tunaungana na Serikali yetu katika kuhakikisha wana ushirika nchini wanafanikiwa kwa kuwa na uhakika wa matibabu na katika hili Benki ya CRDB tutamchangia mwana ushirika mchango wa bima ya afya wa mwaka wa Shilingi 76,800 na mwenza wake kiwango hicho hicho na kwa kila mtoto Shilingi 50,400 kwa mwaka.

 

Alisema nia yao ni kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha Watanzania wote wanakuwa na bima ya afya kama ambavyo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza na tumeanza na kundi la wana ushirika kwa sababu ndio sekta inayoajiri watu wengi zaidi nchini” alisema Dkt. Witts.

 

Akizungumzia huduma za Benki ya CRDB alisema Wana ushirika hawata pata shida ya huduma za kibenki kwa kuwa ina mtandao mpana wa matawi 246, wakala zaidi ya 19,000 na ATM 550 nchi nzima hivyo ni rahisi kwao na wananchi wengine kupata huduma kwa karibu zaidi.

 

Mpango huu unazinduliwa kwa Wazalishaji wa Maziwa Tanga mjini ukiwa ni mwendelezo wa kuwafikia wana ushirika wote nchini hivyo wanachama kupitia Vyama vyao vya Ushirika wanahimizwa kujiunga kwa kuwa ni wa manufaa, hauna riba yeyote kwa mkulima na wanarejesha michango ya bima ya afya baada ya mauzo ya bidhaa husika.

 

Tangu kuanza kwa ushirikiano huu baina ya NHIF na Benki ya CRDB Mei 5, 2021, vyama vya Chunya Tobacco-growers Cooperative Union (CHUTCU), Maziwa Cooperative Union (MCU), Muungano wa Wauza Maziwa wa Rungwe (MWAMARU) na Tanga Diary Cooperative Union (TDCU) vimeshaanza kunufaika na tunategemea vyama vingi zaidi kujiunga na kunufaika na mpango huu.

 

Awali akizungumza wakati tukio la kutiliana saina kwa ajili ya kutekeleza makubaliano Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima alisema hilo ni jambo nzuri na lenye tija kubwa kwa kwa manufaa zaidi ya wazalishaji wa maziwa mkoani humo

 

DC Mwilapwa Benki ya CRDB na NHIF kwa jinsi walivyokuja na mpamgo huo utasaidia kuleta  manufaa makubwa kwa wananchi kutokana na kwamba dira ya Taifa ya maendeleo 2020/2025 inaeleza kwamba itakapofika 2025 watanzania wote wawe wameingia kwenye mpango utakaowahakikishia wanaweza kupata huduma ya afya wakati wowote bila kujali vipato vyao.

 

“Wakati huo utakapofika kwenye lengo hilo namna peke yake kuhakikisha watanzania wanapata tiba bila kupitia vipato vyao ni kupitia huduma ya afya hivyo ni wazo jema kutekeleza azma ya serikali lakini kutekeleza mambo makubwa lazima uwe na uwez,i rasiliamali fedha”Alisema

 

Mkuu huyo wa wilaya aliwapongeza kwa mpango huo ambao alisema unaitoa kimasomaso Serikali watanzania ni jambo jema watokee watu ambao wanakubaliana nalo nao ni Benki ya CRDB ambao wamesaidia kuwezesha kwenye uwezeshaji wa kifedha.

 

 “Mmewezsha mkopo usio na riba mnapofanya hilo hamtekelezi lile la 2020/2025 ambalo ni la Tanzania lakini mnatekeleza malengo ya maendeleo endelevu ambavyo yanafikia mwaka 2030 wenzetu umoja wa mataifa wanafikiria dunia watu wote wawe wameingia kwenye mpango wa bima ya afya lakini sisi tunasema kabla ya wengine wote duniani hawajafikia tutakuwa tumefika 2025”Alisema DC Mwilapwa.

 

Alisisitiza kwamba Mfuko wa Bima ya Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wamefanya kazi yao kutekeleza agizo la serikali na CRDB wanafanya kazi kusaidia jitihada za mfuko huo lakini jambo jingine mliloliangalia ili unufaike lazima uwe mwana ushiriki hivyo watakwenda kuona maendeleo makubwa kwenye ushiriki kwa kupatiwa bima ya afya,

 

Naye kwa upande wake Mrajis wa vyama vya Ushiriki mkoa wa Tanga Jacquiline Senzighe  alitoa shukruani kwa mwelekeo uliopo mbele yao wa kuwa na bima ya afya kwa wafugaji lakini mpango huo unategemewa kwenye ushiriki wote na hizo ni habari njema zenye manufaa makubwa kwao.

 

Alisema kwa sababu wanaushirika lazima watoke ili waweze kutoka wanapaswa kuwa na afya njema huku akieleza kwa sasa mkoa wa Tanga inafanyika kwa kuanzia vyama vya ushirika vya wafugaji ambao vikifanya vizuri zaidi vitasaidia vyama vyengine kufikika kwa urahisi zaidi.

 

“Lakini nitoe wito kwa vyama vya ushirika na viongozi mliopata mkopo lakini lazima mtambue kwamba marejesho yake ni kupitia zile shughuli ambazo wanaushirika wanazifanya kila siku ”Alisisitiza .

 

Mrajisi huyo alisema iwapo mkopo huo ukiendelea vizuri na wakiendelea kufanya ushirikiano mzuri wataendelea kufungua wigo mpana kwa vyama vyengine vya ushirika vya mchepuo mwengine kuweza kunufaika nao.

 

Hata hivyo kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Chama cha Ushirika cha Wazalishaji wa Maziwa Tanga mjini (Tanga Diary Cooperative Union (TDCU) Athumani Mahadhi alisema chama hicho kilianzishwa mwaka 1993 wakiwa na lengo la kutafuta soko la wafugaji wa Ng’ombe wa maziwa mkoa wa Tanga.

 

Alisema kwea sasa wana vyama wanachama 28 na wafugaji mmoja mmoja wamefikia kwa mkoa mzima wamefikia 6285 huku akieleza katika mpango huo wa bima ya afya wao kama TDCU na vyama vya  wanaona kama itakuwa itachochea baadhi ya watu ambao sio wanachma  kuona ipo haja ya kujiunga kwenye vyama vya ushirika kutokana na kwamba huduma ya afya pia inapatikana huko.

 

Mabalozi Wahimizwa Kulitumia Bakita

$
0
0

 


Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

 

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul ametoa wito kwa mabalozi wa nchi mbalimbali zilizopo hapa nchini kulitumia Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kujifunza lugha ya Kiswahili pamoja na kupata tafsiri sahihi ya nyaraka mbalimbali.

 

Gekul ametoa wito huo  alipokutana na Mabalozi kutoka nchi za Indonesia, Uturuki, Oman,Comoro Viet Nam na Cuba wakati wa Tamasha la Utamaduni wa Indonesia lililofanyika tarehe 29 Mei, 2021jijini Dar es Salaam.

 

"Serikali ilianzisha Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kwa lengo la kuendeleza lugha adhimu ta Kiswahili, hiki ndicho chombo chenye uwezo wa kutoa mafunzo sahihi ya lugha ya Kiswahili kwa wageni" Gekul.

 

"Natoa wito kwa Balozi wa Indonesia hapa nchini Mhe. Prof. Dkt. Ratlan Pardede pamoja na Mabalozi wengine wote mlioko hapa na Maafisa wa balozi kuitumuia taasisi hii ya BAKITA kwa ajili ta mafunzo ya lugha ya Kiswahili, ukalimani pamoja na tafsiri za nyaraka mbalimbali" Gekul.

 

Aidha Balozi wa Indonesia alimuhakikishia Gekul kuwa Serikali ya Indonesia itaendeleza ushirikiano uliopo wa Kiuchumi na Kiutamaduni hususani katika eneo la Utalii wa Kiutamaduni.

 

JAFO ATOA MIEZI MIWILI KWA UONGOZI WA KIWANDA CHA QUAIM STEEL MILLS KUHAKIKISHA WANADHIBITI MOSHI

$
0
0
 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa viongozi wa kiwanda cha Quaim Steel Mills limited mara baada ya kutembelea kiwanda hicho katika ziara yake ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika viwanda vinavyozalisha nondo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara yake ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika viwanda vinavyozalisha nondo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akisikiliza maelekezo kutoka kwa baadhi ya viongozi wa kiwanda cha Kamel Steel Industry kinachozalisha nondo katika ziara yake ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika viwanda vinavyozalisha nondo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akikagua baadhi ya nyaya zilizotengenezwa na madini ya kopa kwenye kiwanda cha OK Plast Limited katika ziara yake ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika viwanda vinavyozalisha nondo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akisikiliza maelekezo kutoka kwa mmoja wa viongozi wa kiwanda cha OK Plast limited kinachotengeneza nyaya za umeme kwa kutumia madini ya kopa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika viwanda vinavyozalisha nondo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akizungumza na uongozi wa kiwanda cha OK Plast limited kinachotengeneza nyaya za umeme kwa kutumia madini ya kopa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika viwanda vinavyozalisha nondo Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

**************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo amekiagiza kiwanda cha Quaim Steel Mills limited kuhakikisha kufikia miezi miwili kiwe kimejitengenezea mkakati wa kuhakikisha moshi wa kiwanda hicho hautoki na kusambaa kusababisha uchafuzi wa mazingira.

Ameyasema hayo leo Mhe.Jafo mara baada ya kutembelea kiwanda hicho katika ziara yake ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika viwanda vinavyozalisha nondo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika ziara hiyo Waziri Jafo amewaagiza wenye kiwanda hicho kuhakikisha wanakifanyia marekebisho kiwanda hicho kwaajili ya kulinda afya za wananchi hususani ajenda ya utiririshaji wa moshi hivyo amewataka NEMC baada ya miezi miwili kufika katika kiwanda hicho na kukagua kama kimeshafanyiwa marekebisho.

"Kiwanda cha Quaim Steel Mills limited nimewapa miezi miwili waweze kufanya marekebisho makubwa katika kiwanda chao kwa lengo la kukidhi sheria ya mazingira no.20ya mwaka 2004". Amesema Waziri Jafo.

Aidha Waziri Jafo mewataka wenye viwanda nchini kuhakikisha wanazingatia afya za wananchi kwa kuhakikisha viwanda hivyo havitirirshi moshi ama maji taka ambayo yataenda kuathiri watanzania.

Hata hivyo Waziri Jafo amesema atakaa na kuzungumza na Wizara ya Viwanda na Biashara kuhakikisha wanavisaidia viwanda vya ndani viweze kufanya kazi vizuri na kuhakikisha mazingira yanatunzwa na vijana wa kiktanzania kupata ajira kupitia viwanda hivyo.

Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>