Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

FANYENI TATHMINI UTENDAJI WA MASHIRIKA YA UMMA - DK. MWIGULU

$
0
0


 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt Khatibu Kazungu akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Mwigulu Nchemba wakati wa uzinduzi wa Mafunzo ya Mikataba ya Utendaji Kazi kati ya Ofisi ya Msajili wa Hazina na Bodi za Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za Serikali jana kwenye Ukumbi wa AICC, jijini Arusha. Kulia ni Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka na katikati ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu katika Ofisi ya Msajili wa Hazina, Pili Mazowea.


Maofisa kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina wakifuatilia ufunguzi wa Mafunzo ya Mikataba ya Utendaji Kazi kati ya Ofisi ya Msajili wa Hazina na Bodi za Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za Serikali uliofanywa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt Khatibu Kazungu kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Mwigulu Nchemba jana kwenye Ukumbi wa AICC, Arusha. (Picha na Ofisi ya Msajili wa Hazina).

 

Na Mwandishi Maalumu, Arusha

 

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba amemuelekeza Msajili wa Hazina kufanya tathmini ya utendaji na ufanisi wa Taasisi na Mashirika ya Umma ili aje na ushauri mzuri kwa Serikali ikiwemo kupendekeza kufutwa na kuunganishwa kwa baadhi ya taasisi au kuanzishwa kwa taasisi mpya kama kutakuwa na ulazima huo.

“Hii itasaidia serikali kubaki na taasisi na mashirika yenye kuleta tija badala ya kuwa mzigo kwa serikali,” ameeleza.

Aidha, amesema hatakubali kuona taasisi, mashirika ya umma na wakala za serikali zinashindwa kuwasilisha hesabu zake kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mwaka huu, huku akianisha maeneo 10 ambayo wanatakiwa kuyawekea msisitizo na kuimarisha mifumo ya utendaji na uwajibikaji wa taasisi ili zitoe huduma sahihi na endelevu.

Dk Mwigulu aliyasema hayo jana jijini hapa wakati akifungua mafunzo ya mikataba ya utendaji kazi ya Ofisi ya Msajili wa Hazina na bodi za taasisi, mashirika ya umma na wakala za serikali yanayofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC).

Katika hotuba yake iliyosomwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Khatibu Kazungu, Dk Mwigulu alisema serikali imefanya uwekezaji wa takriban Sh trilioni 65 kwenye taasisi na mashirika yapatayo 237 kwa lengo la kutoa huduma mbalimbali za kijamii, kiuchumi na kusaidia katika kuchangia Pato la Taifa.

“Ni vyema mkafahamu kwamba taasisi na mashirika haya yanatumia kiasi kikubwa cha fedha za umma kwa njia ya mitaji, mishahara na matumizi mengineyo. Kwa misingi hiyo ni matarajio ya Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni kwamba, taasisi na mashirika haya yatasimamiwa ipasavyo ili yaweze kutoa huduma sahihi na endelevu,” alisema Dk Mwigulu.

Aliongeza kuwa pamoja na jitihada zinachokuliwa na serikali, bado kuna maeneo 10 ambayo ni muhimu kuweka msisitizo wa kuimarisha mifumo ya utendaji kazi na uwajibikaji wa taasisi hizo.

Aliyataja kuwa ni baadhi ya taasisi bado zinachelewa kuwasilisha hesabu za taasisi kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa ajili ya ukaguzi. “Katika mwaka huu wa fedha na miaka ijayo sitapenda kusikia tena taasisi yoyote ya umma kwamba imeshindwa au kuchelewa kuwasilisha hesabu kwa wakati,” alieleza.

 

“Aidha, taarifa hizo (za utekelezaji za robo mwaka na mwaka) zinazowasilishwa kwa Msajili wa Hazina ni lazima zipitiwe na kumilikiwa na uongozi wa taasisi,” alibainisha na kumuagiza Msajili wa Hazina kuchukua hatua stahiki kwa watakaoshindwa kutekeleza hilo.

Jingine ni kuagiza taasisi na mashirika yote kuhakikisha matumizi yao yanazingatia Mwongozo wa Bajeti wa Mwaka 2021/22 na kanuni zake zinafuatwa ipasavyo katika utekelezaji wa bajeti.

“Na kwa taasisi na mashirika ambayo hazikuzingatia mwongozo wa bajeti hususan kwa fedha za maendeleo, nakuagiza Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango mzichambue upya na kusitisha miradi yote itakayoshindwa kukidhi matakwa ya mwongozo wa Bajeti kwa mwaka 2021/22,” aliagiza.

Aidha, alisema maombi ya fedha au idhini ya mikopo kwa taasisi na mashirika ya umma yote yapitishwe kwa Msajili wa Hazina kufanyiwa uchambuzi wa maandiko husika kabla ya kuwasilishwa Hazina ili kukidhi matakwa ya Sheria ya Misaada, dhamana na mikopo ya mwaka 1974 kama ilivyorekebishwa 2017.

Dk Mwigulu alisema hatua hii inalenga kuiwezesha kuwa na kumbukumbu sahihi na udhibiti wa mikopo na matumizi ya fedha kwenye miradi ya maendeleo kwa taasisi na mashirika ya umma.

“Taasisi ziwasilishe michango kwa wakati na kiasi kinachohitajika kwa mujibu wa Sheria ya Msajili wa Hazina na Fedha. Ili kuhakikisha maduhuli na michango inakusanywa ipasavyo na kwa wakati, nakuagize Msajili wa Hazina kuhakikisha makusanyo ya maduhuli ya taasisi zote pamoja na michango yote ya asilimia 15 inakusanywa kwa njia ya kielektroniki,” alibainisha eneo jingine Dk Mwigulu linalopaswa kusimamiwa.

Alisisitiza taasisi kutumia Mfumo wa Mipango na Bajeti (PLANREP), Mfumo wa Kihasibu wa Serikali (MUSE) na Mfumo wa Taarifa za Kimenejimenti na Bodi wa Msajili wa Hazina (OTRMIS) pamoja na mingine yote kama itakavyoelekezwa ili kuimarisha udhibiti wa matumizi ya fedha na utekelezaji wa mipango ya taasisi.

Alisema matumizi ya bodi za wakurugenzi za taasisi yafuate miongozo iliyotolewa na serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina. Aliagiza vitengo vya ukaguzi vya taasisi vidhibiti matumizi ambayo ni kinyume cha miongozo hiyo.

Pia kwa taasisi za umma ambazo sehemu ya mapato zinakusanya zenyewe, alisema zinapaswa kupunguza utegemezi toka serikali.

“Bado kuna taasisi nyingi hata matumizi ya kawaida bado zinategemea zilitewe na serikali. Nawakumbusha tena katika hili, zitumieni fursa mlizonazo kuongeza na kukusanya mapato. Kuweni wabunifu kwa kutumia fursa mlizonazo ili kujiongezea mapato. Badilikeni na kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea,” alisema Dk Mwigulu na kuongeza kuwa anatarajia eneo hilo lichangie angalau asilimia 10 ya bajeti za taasisi.

Aidha, aliagiza taasisi ziwe na mipango madhubuti ya kujenga uwezo wa watumishi wa vitengo vya Ukaguzi wa Ndani ili wawe na uelewa mzuri kuhusu majukumu yote ya taasisi pamoja na mifumo mbalimbali inayotumika katika utendaji kazi ili kuviwezesha kuleta tija katika kutekeleza majukumu yake ya ushauri na udhibiti mahala pao pa kazi.

“Mwisho kabisa nikuagize Msajili wa Hazina, nenda kafanye tathmini ya utendaji na ufanisi wa taasisi na mashirika ya umma ili uje na ushauri mzuri kwa serikali ikiwemo kupendekeza kufutwa na kuunganishwa kwa baadhi ya taasisi kama au kuanzishwa kwa taasisi mpya kama kutakuwa na ulazima huo. Hii itasaidia serikali kubaki na taasisi na mashirika yenye kuleta tija badala ya kuwa mzigo kwa serikali,” alieleza Dk Mwigulu.

Alisema ni matarajio yake kuwa masuala hayao yatafanyiwa kazi na taasisi zote na kuhakikisha mapungufu hayo hayajirudii katika taasisi, huku akiagiza kuwa kuanzia mwaka 2022/23 matokeo ya tathmini ya mikataba ni vizuri yawekwe wazi ikionesha taasisi itayofanya vizuri zaidi hadi ile itakayofanya vibaya. 

Awali, Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka alisema mafunzo hayo yanahusisha washiriki 711 kutoka taasisi, mashirika ya umma na wakala za serikali 237 yaliyoko chini ya Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Mbuttuka alisema katika mwaka huu wa fedha (2020/21), ofisi yake imesaini Mikataba ya Utendaji Kazi na taasisi na mashirika ya umma 230 kati ya taasisi na mashirika ya umma 237 sawa na asilimia 97 ya taasisi zote 237 ambazo zimekeleza matakwa ya kisheria ukilinganisha na mikataba 13 iliyosainiwa mwaka 2014/15.


RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AFUNGUA KIWANDA CHA USHONAJI CHA JESHI LA POLISI TANZANIA -KURASINI

$
0
0

 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akivuta utepe kufungua Kiwanda cha Ushonaji cha Jeshi la Polisi Tanzania kilichopo Kurasini mkoani Dar es Salaam leo tarehe 18 Mei, 2021. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Khamis Hamza Khamis pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro. 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipiga makofi na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Khamis Hamza Khamis pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro mara baada ya kukata utepe kuashiria ufunguzi wa Kiwanda cha Ushonaji cha Jeshi la Polisi Tanzania kilichopo Kurasini mkoani Dar es Salaam leo tarehe 18 Mei, 2021.

  

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikagua kazi mbalimbali zinazofanywa katika kiwanda hicho cha ushonaji cha Jeshi la Polisi Tanzania kilichopo Kurasini mkoani Dar es Salaam mara baada ya kukifungua leo tarehe 18 Mei, 2021. 

  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikagua kazi za upimaji na ukataji wa vitambaa vinavyotumika katika kushona sare za Jeshi la Polisi katika Kiwanda cha Ushonaji Nguo cha Jeshi la Polisi Tanzania kilichopo Kurasini mkoani Dar es Salaam.

  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Polisi Kurasini mkoani Dar es Salaam mara baada ya kufungua Kiwanda hicho cha Ushonaji.

  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Askari pamoja na Maafisa mbalimbali wa Jeshi la Polisi pamoja na Wageni wengine Kurasini mkoani Dar es Salaam mara baada ya kufungua Kiwanda cha Ushonaji cha Jeshi la Polisi Tanzania. PICHA NA IKULU.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 18 Mei, 2021 amefungua kiwanda cha ushonaji bohari kuu ya Jeshi la Polisi kilichopo Kurasini Mkoani Dar es Salaam.

Kiwanda hicho kimejengwa kwa utaratibu wa nguvu kazi (force account) kwa gharama ya shilingi Milioni 666.4 badala ya shilingi Bilioni 1.4 kama kingejengwa kwa utaratibu wa zabuni.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IJP Simon Sirro amesema ujenzi wa kiwanda hicho umepanua uwezo wa kiwanda kutoka vyerehani 70 hadi 130 vyenye uwezo wa kushona sare 125,000 za Askari kwa mwaka.

IJP Sirro amemshukuru Mhe. Rais Samia kwa kufungua kiwanda hicho na amesema Jeshi la Polisi linapanga kuanzisha shirika la uzalishaji litakaloendesha miradi mbalimbali kikiwemo kiwanda cha ushonaji, kiwanda cha kuzalisha maji na usindikizaji wa fedha.

Pia, IJP Sirro amemshukuru Mhe. Rais Samia kwa Serikali kutoa shilingi Bilioni 6 kwa ajili ya kuwalipa wastaafu wa Jeshi la Polisi ambao wameanza kulipwa.

Akizungumza na Maafisa wa Polisi, Askari na viongozi mbalimbali katika uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini, Mhe. Rais Samia amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kujenga kiwanda hicho kwa kutumia mapato yake ya ndani na kwa kutumia nguvukazi iliyotumia kiasi kidogo cha fedha ikilinganishwa na endapo lingetumia wazabuni.

Mhe. Rais Samia ameelezea kufarijika kwake kukifungua kiwanda hicho ambacho kiliwekwa jiwe la Msingi na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli na amesema kukamilika kwa kiwanda hicho ni uthibitisho wa kumuenzi Hayati Dkt. Magufuli.

Ameelekeza Majeshi mengine kushona sare zao katika kiwanda hicho na pia kujielekeza kushona sare nyingine kama vile viatu badala ya kila Jeshi kushona aina ileile ya sare zinazoshonwa na Jeshi lingine ili kudhibiti uagizaji wa sare za Askari kutoka nje ya nchi.

Aidha, Mhe. Rais Samia amelitaka Jeshi la Polisi kujielekeza kudhibiti matukio ya uhalifu na uvunjaji wa sheria ikiwemo makosa ya usalama barabarani badala ya kujikita katika kutoa adhabu ama kuwa kitega uchumi.

Amelitaka jeshi hilo kuongeza juhudi katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu ambavyo vimeanza kujitokeza na ameonya kuwa katika upandishaji wa vyeo, uteuzi na kutengua uteuzi wa Maafisa wakiwemo Makamanda wa Polisi wa Mikoa kipimo cha juhudi za udhibiti wa matukio ya uhalifu hasa ujambazi kitatumika.

Mhe. Rais Samia amelitaka Jeshi la Polisi kuweka mfumo utakaowezesha kutambuliwa kwa wavunja sheria za usalama barabarani popote walipo hapa nchini ili ikitokea dereva kafanya makosa katika mkoa mmoja aonekane katika mkoa mwingine na achukuliwe adhabu stahiki ikiwemo kufutiwa leseni.

Amelitaka Jeshi la Polisi kuendelea kupunguza msongamano wa Mahabusu waliokamatwa kutokana na makosa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwaachia wenye kesi za kubambikizwa kama ambavyo imefanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambayo imefuta kesi 147 za rushwa za kubambikizwa.

Mhe. Rais Samia ameagiza sheria inayolazimu majeruhi kuwa na fomu ya PF3 ndipo wapatiwe matibabu katika vituo vya tiba irekebishwe ili majeruhi wasikoseshwe matibabu pale wanapokuwa hawana fomu hiyo.

Mhe. Rais Samia ameahidi kufanyia kazi changamoto mbalimbali za Jeshi la Polisi kadiri Serikali itakavyokuwa na uwezo wa kifedha.

CRDB YAKUTANA NA WADAU KUJADILI UCHUMI KIDIGITALI

$
0
0


Afisa Mwendeshaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile, akizungumza katika mdaharo wa pamoja  kati Vodacom na benki  hiyo ukiangazia  namna ambavyo uchumi kidigitali utaboreshwa ili kuwanufaisha wananchi, iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. 


Mkuu wa Kitengo cha Mabadiliko Endelevu ya Biashara  Benki ya CRDB, Winniefrida Wanyacha, akizungumza katika mdaharo wa pamoja  kati Vodacom na benki hiyo ukiangazia  namna ambavyo uchumi kidigitali utaboreshwa ili kuwanufaisha wananchi, iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.

 



NMB #Miliki Chombo yatinga Kanda ya Ziwa!

$
0
0

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB – Ruth Zaipuna, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza – Salum Kalli, Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa Baraka Ladislaus (Kulia Mwisho), Afisa Mkuu wa Rasilimali watu wa Benki ya NMB – Emmanuel Akoonay (wa pili kutoka kulia) Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB – Filbert Mponzi (kushoto Mwisho) na Mkuu wa Idara ya Kadi wa NMB – Philbert Casmir (Mwenye fulana nyeupe) wakifurahia muda mfupi baada ya uzinduzi rasmi wa mikopo ya boda boda na piki piki za miguu mitatu inayoitwa ‘Mastaboda Loan’ leo jijini Mwanza.

Mameneja wa NMB matawi ya Mwanza mjini wakitambulishwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mastaboda Loan.

Zoezi la kufungua akaunti likiendelea mara baada ya uzinduzi wa Mastaboda Loan.


Sehemu ya waalikwa katika uzinduzi wa Mastaboda Loan.

 

Na Mwandishi Wetu

 

Benki ya NMB imezindua huduma ya Mikopo ya pikipiki za miguu miwili na miguu mitatu kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa na kuahidi kutumia zaidi ya shilingi Bilioni 5 kutoa mikopo kwa vijana zaidi ya elfu 75 nchini.

 

Akizungumza katika uzinduzi wa mikopo hiyo kwa vijana waendesha bodaboda na pikipiki za miguu mitatu jijini Mwanza, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna aliwataka wanufaika kujitokeza na kuchagamkia fursa hiyo.

 

Alisema ikiwa vijana na watu wengine waliojiunga katika umoja wa waendesha bodaboda na pikipiki za miguu wajitokeze na kuchangamkia fursa hiyo, NMB inaweza kuongeza kiwango cha utoaji mikopo kwa baadae.

 

Ruth alisema kwa mara ya kwanza walizindua huduma hiyo jijini Dar es Salaam mwezi uliopita na sasa ni zamu ya jiji la mwanza huku akisisitiza kuwa wote wamepata elimu ya fedha, ikiwemoo nidhamu ya fedha.

 

"Hatutaki mikopo hii iwe mizigo kwenu bali baraka kwenu na NMB imedhamiria kufika katika mikoa mingine  hapa nchini kwa ajili ya utoaji wa mikopo hii," alisema Ruth

 

Nae, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara Benki ya NMB - Filbert Mponzialisema uzinduzi wa mpango huo ni pamoja na NMB kuandaa mfumo wa malipo ya Master Boda QR utakaomuwezesha mteja kumlipa bodaboda nauli kiurahisi.

 

Ili kupata mkopo huu, lazima kila mwanachama wa umoja wa waendesha bodaboda na pikipiki ya miguu mitatu afungue akaunti ya NMB na kuanza kuingiza fedha anayolipwa na wateja kama nauli walau kuanzia miezi mitatu.

 

Mponzi aliwaomba watanzania kukatia vyombo vyao vya moto Bima kupitia benki ya NMB. Akizindua mpango mikopo huo, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli aliwahakikishia usalama waendesha bodaboda na pikipiki za miguu mitatu muda wote watapokuwa kazini.

 

Aidha, aliwataka kuheshimu mikopo watakayopatiwa ili iweze kuwasaidia na kusaaidia makundi mengine ya kijamii katika jiji la Mwanza na maeneo mengine.

   

  

 

 

 


ALLY KAYOMBO AIBUKA MSHINDI WA SHINDANO LA GOFU KWA WATOTO

$
0
0

Mwenyekiti wa klabu Brig Jen Michael Luwongo Mstaafu akimvisha medali Nahodha wa timu ya watoto kwa wasichana Jonada Omuteku mara baada ya kumalizika zoezi la kugawa zawadi kwa waliofanya vizuri katika shindano la (Junior’s golf Tournament) lililofanyika Mei 16,2021 Lugalo.


Mchezaji Ally Kayombo aliyeibuka mshindi wa jumla wa shindano la  (Junior’s golf Tournament) akipiga mpira katika moja ya kiwanja cha gofu Lugalo.

 Katibu wa Mashindano TGU Injinia Enock Magile akimuangalia mchezaji  Ibrahim Juma anavyopiga mpira katika viwanja vya gofu Lugalo wakati wa shindano la  (Junior’s golf Tournament) lililofanyika Mei 16, 2021.

Wachezaji watoto wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Brig. Jen Michael Luwongo Mstaafu viongozi na walezi na viongozi mara baada ya kumalizika zoezi la kugawa zawadi kwa waliofanya vizuri katika shindano la (Junior’s golf Tournament) lililofanyika Mei 16,2021 Lugalo.

WAKALA WA VIPIMO (WMA) WATEMBELEA VITUO VYA AFYA NA KUHAKIKI MIZA

$
0
0

 

Muuguzi wa kituo cha afya mama na mtoto Chanika akimpima uzito mtoto pembeni wakiwa maafisa wa Wakala wa Vipimo (WMA) wakihakiki mizani hiyo kama ipo sahihi katika vipimo mara baada ya kutembelea katika kituo hicho kama kushiriki maadhimisho Siku ya Vipimo Duniani.

Maafisa wa Wakala wa Vipimo (WMA) wakihakiki mizani ya mtoto mdogo mara baada ya kutembelea katika kituo cha afya mama na mtoto Chanika kama kushiriki maadhimisho Siku ya Vipimo Duniani.

Maafisa wa Wakala wa Vipimo (WMA) wakihakiki mizani ya uzito mara baada ya kutembelea katika kituo cha afya mama na mtoto Chanika kama kushiriki maadhimisho Siku ya Vipimo Duniani.

Mama mjamzito akipimwa uzito.

Meneja wa Uhusiano kwa Umma wa Wakala wa Vipimo (WMA) Bi.Irene John akitoa elimu kwa wazazi kuhusu umuhimu wa mizani katika vituo vya afya mara baada ya kutembelea katika kituo cha afya mama na mtoto Chanika kama kushiriki maadhimisho Siku ya Vipimo Duniani.

Maafisa wa Wakala wa Vipimo (WMA) wakihakiki mizani inayopima uzito na urefu kwa wakati mmoja mara baada ya kutembelea katika kituo cha afya mama na mtoto Chanika kama kushiriki maadhimisho Siku ya Vipimo Duniani.

Mgonjwa akipima uzito

Maafisa wa Wakala wa Vipimo (WMA) wakihakiki mizani ya mtoto mchanga mara baada ya kutembelea katika kituo cha afya Buguruni kama kushiriki maadhimisho Siku ya Vipimo Duniani.

PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO

***************************

NA EMMANUEL MBATILO

Kuelekea siku ya Vipimo Duniani, Wakala wa Vipimo (WMA) wamezindua maadhimisho hayo kwa kutembelea vituo vya afya na hospitali katika eneo la Chanika na Buguruni kuhakiki mizani ambazo hutumika kwaajili ya vipimo.

Akizungumza mara baada ya kutembelea katika hospitali hizo, Meneja Wakala wa Vipimo Mkoa wa Ilala Bw.Saad Haruna amesema katika uhakiki walioufanya wamegundua mizani mingi bado inausahihi unaokubarika kwa matumizi.

Aidha Bw.Haruna amesema kuwa umhumu wa vipimo katika sekta ya afya ni pamoja na matumizi ya dawa kwani ili mgonjwa apate dawa sahihi anatakiwa kupimwa uzito ili apewe dozi kulingana na uzito wake.

"Vipimo kwa maana ya mizani ni muhimu katika sekta ya afya na sisi kwa kuliona hilo na kushirikiana na uongozi wa hospitali tumekuwa tukishirikiana nao katika uhakiki wa mizani kwenye hospitali za Ilala.Lakini hii si Ilala peke yake kwasababu Wakala wa Vipimo ina ofisi nchi nzima hivyo maadhimisho haya yamefanyika nchi zima katika mikoa na wilaya zote nchini". Amesema Bw.Haruna.

Kwa upande wake Muuguzi wa Kituo cha afya mama na mtoto Chanika Bi.Barry Fundi amewashukuru Wakala wa Vipimo kufika na kuhakiki mizani katika kituo hicho kwani kupitia hivyo kuna wapa mwangaza kuwa huduma wanazozitoa ni sahihi hata kwa vipimo vya dawa wanavyovitua kwa watoto kulingana na uzito kwa maana watoto wengi wanapewa matibabukulingana na uzito wao.

Nae fundi sanifu vifaa tiba katika kituo cha afya Buguruni Bw.Gidion Maganga amesema uhakiki wa mizani kwenye vipimo kwa maana inaongeza kitu katika matibabu yake ambapo itamsaidia kufahamu ni matumizi gani ya dawa anaweza kutumia na zisimletee madhara.

"Kuna wale ambao wanadharau mizani hizi ni hatari kwao kwasababu utakuja kupata dawa ambazo hazijaendana na uzito wao kitu ambacho kitaweza kukuletea madhara katika afya zao kwani hautakua unafahamu ni dozi gani unatakiwa kutumia". Amesema Bw.Maganga.

Maadhimisho haya hufanyika Mei 20 kila mwaka ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni "VIPIMO KATIKA SEKTA YA AFYA".

TANZANIA KUENDELEA KUONGZA KWA UZALISHAJI WA MPUNGA

$
0
0

.Mhandisi wa kilimo kutoka Wizara ya Kilimo Idara ya Mafunzo,Huduma za ugani na Utafiti Mhandisi Maregesi Geofrey akifungua Mkutano huo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Prof. SIza Tumbo.

Bi. Ridda Dally afisa miradi ya Kilimo kutoka Shirika la maendeleo la Japan (JICA) akitoa salamu za wadau wa zao la mpunga wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.


Na Calvin Gwabara, Dar es Salaam


SERIKALI kwa kushirikiana na wadau wa zao la Mpunga nchini wameazimia kuimarisha utoshelevu wa chakula katika ukanda wa Afrika mashariki, Jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa jangwa la sahara (SADIC) na kuwa kinara wa soko la mchele katika jumuiya za kikanda kupitia mkakati wa taifa wa pili wa maendeleo ya Mpunga.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa wizara ya kilimo Prof. Siza Tumbo kwa niaba yake na Mhandisi wa Kilimo wizara ya Kilimo katika Idara ya Mafunzo huduma za ugani na Utafiti Mhandisi Maregesi Geofrey wakati akifungua Mkutano wa Kikanda  kuhusu mnyororo wa thamani wa zao hilo unaofanyika jijini Dar es salaam.

“Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na wadau wa zao la mpunga nchini tumejipanga kuhakikisha tunaongeza eneo la uzalishaji wa mpunga kutoka hekta milioni 1.1 za mwaka 2018 hadi hekta milioni 2.2 ifikapo mwaka 2030 na hivyo kuongeza uzalishaji kutoka tani 2.2 kwa hekta za sasa hadi kufikia tani 4.4 ifikapo mwaka 2030”Alisisitiza Mhandisi Maregesi.

Ameongeza kuwa mambo mengine ambayo yatatekelezwa ni kuimarisha mifumo ya masoko na biashara,kuongeza upatikanaji wa mbolea na usambazaji,kuimarisha kilimo cha umwagiliaji na kuhamasisha teknolojia zake sambamba na kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno kutoka asilimia 30 hadi 10 ifikapo 2030.

Aidha ameeleza kuwa zao la mpunga ni mojawapo wa zao muhimu la chakula linalozalishwa takribani mikoa yote nchini katika wilaya zaidi ya 26 ambazo kwa utafiti wa mwaka 2018 inazalisha tani milioni 2,219,628.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufuangua Mkutano huo, Mtafiti kiongozi na mkuu wa mradi huo kwa upande wa Tanzania Prof. Aida Isinika amewataka wadau wote kwenye mnyororo wa thamani wa zao la mpunga nchini  kujipanga ili kuhakikisha Tanzania inajitosheleza kwa zao hilo na kuendelea kuwa kinara wa uzalishaji wa Mpunga kwa nchi za Afrika mashariki.

 “Sote Tunajua kuwa Tanzania tunaongoza kwenye uzalishaji wa zao la Mpunga kwenye ukanda huu wa Afrika ya mashariki lakini lazima tutambue kuwa kuna nchi mbalimbali sasa zinakuja kwa kasi katika kuongeza tija hivyo ni lazima wadau wote tujipange ili nchi yetu izidi kuwa kinara na kushika soko la dunia” Alisisitiza Prof. Isinika.

Prof. Isinika amesema wazalishaji wakubwa wa Mpunga duniani uwezo wao kwenye tija umefikia mwisho na sasa wanaangalia bara la afrika kwakuwa bado lina fursa kubwa za uzalishaji na tija hivyo Tanzania lazima ijipange zaidi katika kutumia fursa nyingi zilizopo kuzalisha na kuuza nje ya nchi badala ya kutegemea kuingiza kutoka nje ya nchi.

Mkuu huyo wa mradi amewashukuru wadau wote kwenye mnyororo wa thamni waliokubali kushiriki mkutano huo muhimu ambao utaangalia maeneo yote muhimu hasa na kuja na maazimio ya njia bora ambazo zitasaidia kufikia malengo hayo ya taifa kwa pamoja .

Akitoa salamu kwa niaba ya wadau wengine wa mkutano huo kwenye mnyororo wa thamani afisa miradi ya kilimo  wa shirika la maendeleo la Japan (JICA) Bi. Ridda Dally amesema kwa miaka mingi wamekuwa wakishirikiana na wadau wengine na serikali katika kusaidia ukuzaji wa zao la mpunga nchini na wataendelea kushiriki ili kufikia malengo.

Amesema zao la mpunga ni moja ya mazao yanayochangia katika maendeleo ya wananchi na taifa ndio maana JICA waliamua kufadhili kikosi kazi kilichokuwa kikiandaa mpango mkakati wa kwanza na wa pili ambao lengo lake lilikuwa ni kuongeza uzalishaji wa zao hilo hivyo mkutano huo utasaidia kuja na mikakati bora itakayowezesha kufikia mpango huo wa serikali.

Mkutano huo wa siku tatu unahusisha wadau kwenye mnyororo mzima wa thamani wa zao hilo hapa nchini ambapo kwa siku ya kwanza wanajadili mipango ya Tanzania na siku ya pili nay a tatu mkutano utajumuisha wadau kutoka nchi zote duniani ambapo zaidi ya wadau 500 watashiriki kwa njia ya mtandao.

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AFUNGUA RASMI MKUTANO WA KIMATAIFA WA ELIMU BORA

$
0
0

 

Rais mstaafu wa Awamu ya Nne nchini Tanzamia, Dk. Jakaya Kikwete akihutubia kabla ya kufungus Mkutano wa kimataifa wa elimu Bora ulioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), ambao unashirikisha wadau mbalimbali wa elimu kutoka serikalini, asasi na taasisi za kimataifa za ndani na nje ya nchi. Mkutano huo ulioanza leo unafanyika kwa siku tatu Ukumbi wa Kisenga Jengo la LAPF jijini Dar es Salaam, yaani tarehe 18 hadi 20 Mei 2021.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. John Kalage akizungumza leo wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa elimu Bora ulioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), ambao unashirikisha wadau mbalimbali wa elimu kutoka serikalini, asasi na taasisi za kimataifa za ndani na nje ya nchi. Mkutano huo ulioanza leo unafanyika kwa siku tatu Ukumbi wa Kisenga Jengo la LAPF jijini Dar es Salaam, yaani tarehe 18 hadi 20 Mei 2021.
Mratibu wa Taifa TEN/MET, Bw. Ochola Wayoga akizungumza leo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa elimu Bora ulioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), ambao unashirikisha wadau mbalimbali wa elimu kutoka serikalini, asasi na taasisi za kimataifa za ndani na nje ya nchi. Mkutano huo ulioanza leo unafanyika kwa siku tatu Ukumbi wa Kisenga Jengo la LAPF jijini Dar es Salaam, yaani tarehe 18 hadi 20 Mei 2021.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu, Gerald Mweli akizungumza kwenye mkutano huo.
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne nchini Tanzamia, Dk. Jakaya Kikwete akitembelea Banda la Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Kwenye hafla ya uzinduzi wa Mkutano huo ulioanza leo unafanyika kwa siku tatu Ukumbi wa Kisenga Jengo la LAPF jijini Dar es Salaam, yaani tarehe 18 hadi 20 Mei 2021.
Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mh. Anders Sjöberg akizungumza leo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa elimu Bora ulioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), ambao unashirikisha wadau mbalimbali wa elimu kutoka serikalini, asasi na taasisi za kimataifa za ndani na nje ya nchi. 

Rais mstaafu wa Awamu ya Nne nchini Tanzamia, Dk. Jakaya Kikwete (kushoto) akipata maelezo ndani ya Banda la Uwezo kabla ya kufungua Mkutano wa kimataifa wa elimu Bora ulioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), ambao unashirikisha wadau mbalimbali wa elimu kutoka serikalini, asasi na taasisi za kimataifa za ndani na nje ya nchi. 

Rais mstaafu wa Awamu ya Nne nchini Tanzamia, Dk. Jakaya Kikwete akitembelea banda la Hakielimu kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa kimataifa wa elimu Bora ulioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), ambao unashirikisha wadau mbalimbali wa elimu kutoka serikalini, asasi na taasisi za kimataifa za ndani na nje ya nchi.
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne nchini Tanzamia, Dk. Jakaya Kikwete akitembelea mabanda mbalimbali ya wanachama wa TEN/MET.
Sehemu ya wajumbe washiriki wakiwa katika mkutano huo.
Mratibu wa Taifa TEN/MET, Bw. Ochola Wayoga (katikati) akiendesha mjadala katika mkutano wa kimataifa wa elimu Bora ulioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), ambao unashirikisha wadau mbalimbali wa elimu kutoka serikalini, asasi na taasisi za kimataifa za ndani na nje ya nchi.
Sehemu ya washiriki katika Mkutano wa kimataifa wa elimu Bora ulioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), ambao unashirikisha wadau mbalimbali wa elimu kutoka serikalini, asasi na taasisi za kimataifa za ndani na nje ya nchi.
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne nchini Tanzamia, Dk. Jakaya Kikwete pamoja na meza kuu, akipata picha ya kumbukumbu na wawasilisha mada katika Mkutano wa kimataifa wa elimu Bora ulioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), ambao unashirikisha wadau mbalimbali wa elimu kutoka serikalini, asasi na taasisi za kimataifa za ndani na nje ya nchi.

Rais mstaafu wa Awamu ya Nne nchini Tanzamia, Dk. Jakaya Kikwete akisisitiza jambo alipokuwa akijibu maswali ya wajumbe wa Mkutano wa kimataifa wa elimu Bora ulioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), ambao unashirikisha wadau mbalimbali wa elimu kutoka serikalini, asasi na taasisi za kimataifa za ndani na nje ya nchi.

WANAFUNZI ARUSHA WAPATIWA ELIMU YA MAKUMBUSHO YA TAIFA YA VIUMBE

$
0
0

Mkurugenzi wa Makumbusho ya Viumbe Hai Iliyopo jijini  Arusha Dkt. Christine Ngereza (kulia) akizungumza na wanafunzi waliotembelea makumbusho hiyo katika  kilele cha maadhimisho ya siku hiyo  yaliyoadhimishwa duniani kote leo. 
Wanafunzi wakiwa mbele ya Makumbusho ya Viumbe Hai iliyopo jijini  Arusha baada ya kuitembelea katika kilele cha  Maadhimisho.ya  Siku ya Makumbusho yaliyoadhimishwa duniani kote leo.



Na Dotto Mwaibale  


WANAFUNZI jijini Arusha wamejengewa uwezo wa kujua Makumbusho ya Taifa katika kilele cha maadhimisho  yaliyoadhimishwa duniani kote leo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho hayo jijini Mkurugenzi wa Makumbusho ya Viumbe Hai iliyopo jijini  Arusha Dkt. Christine Ngereza alisema moja ya shughuli walioifanya  ni kuwajengea uwezo wanafunzi wa shule mbalimbali waliofika katika maadhimisho hayo.

" Tumekuwa na wanafunzi kutoka shule mbalimbali ambao tumewapa elimu kuhusu masuala ya makumbusho ambayo wameyafurahia" alisema Ngereza.

Alisema kumekuwa na changamoto kwa wanannchi kutojua masuala ya makumbusho kama ilivyo kwa nchi zingine duniani.

Alisema ni vizuri sasa kukawa na makongamano, semina na midahalo maeneo mbalimbali ya kufundishana masuala ya makumbusho ambayo ni muhimu kwa nchi yoyote duniani.

"Katika maadhimisho haya kitu kikubwa kilicho nifurahisha ni jinsi wanafunzi walivyo kuwa na kiu ya kuuliza maswali mengi kutaka kujua makumbusho" alisema Ngereza.

Ngereza alisema  mwaka huu Tanzania imeungana na nchi zaidi ya 158 duniani kuadhimisha siku hiyo chini ya kauli mbiu isemayo The Future of Museums Recover and Re imagine.

Akizungumzia kuhusu  Makumbusho hayo alisema kazi kubwa walioifanya ni kutoa elimu ya kuwajengea uelewa wananchi juu ya kutembelea makumbusho  kama sehemu ya kupata elimu na burudani kuhusu urithi wa nchi wa kale na wa Sasa wa Asili Mazingira Utamaduni Sayansi,Teknolojia na Historia.

Dkt. Tungereza alisema tangu asubuhi makumbusho ya jijini Arusha ilikuwa wazi ambapo wananchi wakiwepo wanafunzi walipata fursa ya kuitembelea. 

CHUO KIKUU MZUMBE DAR KAMPASI -TEGETA YATOA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WANAFUNZI

$
0
0

 
Mlezi wa wanafuzi Chuo Kikuu Mzumbe ndaki ya Dar es salaam -Tegeta, Zitta Mnyanyi, akizungumza na wanafunzi wa mwaka wa kwanza wakati wa mafunzo ya kujiandaa na na soko la ajira. Mafunzo hayo yamefanyika tawi la Tegeta.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam Prof. Honest Ngowi akifungua mafunzo ya kuwaandaa wanafunzi wa mwaka wa kwanza namna ya kuingia katika soko la ajira.
 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe ndaki ya Dar es  Salaam- Tegeta wakiwa katika mafunzo hayo.

 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam Prof. Honest Ngowi akifungua mafunzo ya kuwaandaa wanafunzi wa mwaka wa mwaka wa kwanza namna ya kuingia katika soko la ajira.
 Baadhi ya wanafunzi wakisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa.

Afisa Rasilimaliwatu wa Kampuni ya CVPeople Tanzania, Noemi Mseven, akitoa mafunzo ya namna ya kuandika CV kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam-Tegeta.
Rais wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Festo Karoli, akizungumza na wanafunzi wa chuo hicho wakati wa mafunzo hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CV People, Naike Moshi, akitoa mada wakati wa mafunzo ya kuwaandaa wanafunzi wa mwaka wa kwanza namna ya kuingia katika soko la ajira.

Tilioni 4 zatengwa miradi ya ujenzi

$
0
0


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Malongo, akizungumza na wahandisi walioshiriki mafunzo ya usimamizi wa miradi wakati alipokuwa akifungua mafunzo hayo, jijini Dodoma.
 
 
 
NA HAMID RAMADHANI, DODOMA


KATIKA mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali imetenga jumla ya shilingi Tilioni 4 kwa ajili ya miradi ya Ujenzi ambayo umepangwa kutekelezwa hapa nchini.

Kutokana na hayo serikali  imewataka Wahandisi kuhakikisha  wanakamilisha miradi yote mikubwa ya kimkakati iliyoanzishwa na serikali ya awamu tano kwa lengo la kukuza uchumi na kujenga Tanzania ya viwanda.

Hayo yalibainishwa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi(ujenzi)  Mhandisi Joseph Malongo wakati akifungua warsha ya siku tatu kwa wahandisi nakuitaja miradi hiyo kuwa ni Daraja la Salenda,Daraja la Busisi, Miradi wa kufua umeme na Reli ya kisasa

Amesema Serikali iliyopitia iliandaa miradi mikubwa ya kimkakati na serikali ya awamu ya sita imeahidi kutekeleza, waandisi mnajukumu kubwa la kuhakikisha miradi hii inakamilika kwa wakati kwasababu kukamilika kwake itakuwa ni chachu ya maendeleo kwa Taifa,

"Katika nchi hizi ambazo bado zinaendelea sekta ya ujenzi ni muhimu sana kwasababu inachangia asilimia kubwa ya maendeleo ya viwanda na biashara hivyo kuongeza ukuaji wa uchumi," alisema

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wahandisi Prof Ninatubu Lema amesema wamejipanga kuhakikisha wanashirikiana na serikali kukamilisha miradi yote mikubwa ambayo tayari ilishaanzishwa.

Amesema serikali imewapa jukumu hilo la utekelezaji wa miradi hiyo ya
maendeleo hivyo nao watajitahidi kuhakikisha wanakwenda kufanya kazi
hizo kwa weledi mkubwa hasa ukizingatia taifa linakwenda kasi ili
kukuza uchumi wa nchi.

“Tunaishkuru sana serikali kwa kutuamini wahandisi,ndio maana
tumeandaa warsha hii ili kujadili mambo mazuri ya uendeshaji miradi
nasi tutaishauri serikali nini kifanyike ili tukamilishe miradi kwa
wakati,".

"Pia sisi wahandisi zaidi ya 30,000 tunaahidi kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hasan na kushirikiana nae katika shughuli mbalimbali za ujenzi na kutekeleza miradi ambayo itakuwa na manufaa kwa taifa," amesema Prof Lema

Prof Lema amewataka wahandishi. kujiongeza
kielimu wao wenyewe ili waweze kuendana na wahandisi waliko katika
sehemu nyingine ambazo wanauwezo wa kufanya kila aina ya kazi na kuwahasa kutobweteke katika kazi ya aina moja

Naye Msajili  wa Wahandisi Mhandisi Patrick Barozi alisema mafunzo hayo yataenda sambamba na kutafakali chanzo cha wahandisi wengi wa miradi ya maji kushindwa kutekeleza miradi hiyo kwa wakati na kufanya wahandisi wote nchini kuongelewa vibaya na jamii.

Amesema ukiachana na miradi mikubwa ambayo inatekelezwa hapa nchi ipo miradi ya maji ambayo ilitekelezwa na wahandisi lakini hadi Leo haifanyi kazi katika warsha hii watajua tatizo lilikuwa wapii

" Kwa upande wa miradi ya maji malalamiko yamekuwa mengi hasa yakienda kwa wahandisi, sasa kwenye warsha hii tutajua kwanini malalamiko yanakuwa mengi na tatizo liko wapi na nini kifanyike ilikuondoa malalamiko hayo,"ameeleza


KAMPUNI YA KIWANDA CHA SUKARI CHA KILOMBERO YATANGAZA UPANUZI WA KIWANDA CHA KILOMBERO

$
0
0
"Wakulima wa Miwa wa Kilombero watakuwa wanufaika wakuu kwani ongezeko kubwa la usambazaji wa miwa utahitajika kuendesha kiwanda baada ya upanuzi"

 

Kampuni ya Kiwanda cha Sukari cha Kilombero ambayo inamilikiwa na Kampuni ya Illovo Sugar Africa  kwa Asilimia 75 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Msajili wa Hazina kwa asilimia 25, imetangaza kuidhinishwa kwa Mradi wa Upanuzi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero.

 

Mradi wa upanuzi wa kiwanda hicho utagharimu kiasi cha Shilingi bilioni 571.6. Ili kuendana na Sera na Mipango ya Nchi Mradi huu utaongeza uzalishaji wa sukari kwa tani 144,000 kutoka viwango vya sasa vya tani 127,000 kwa mwaka, hadi kufikia tani 271,000 ifikapo mwaka 2023.

 

Sababu za kuidhinishwa kwa mradi wa upanuzi wa kiwanda hicho ni pamoja na matarajio ya ongezeko la usambazaji wa miwa kutoka kwa wakulima wadogo wa Bonde la Mto Kilombero kutoka tani 600,000 cha hivi sasa mpaka kufikia tani 1,700,000. Hivyo, Mradi wa upanuzi wa kiwanda umezingatia ongezeko la miwa kwa sasa nautawezesha miwa yote iliyopo kuchakatwa kila mwaka ifikapo mwishoni mwa Desemba, lengo likiwa ni kupunguza usumbufu na upotevu unaosababishwa mara kwa mara hasa kipindi cha mvua.

 

Mradi wa Upanuzi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero umekuwa kwenye mipango ya muda mrefu, pamoja na malengo ya kuongeza uzalishaji wa sukari na kukidhi mahitaji ya watumiaji,. Mradi pia utahusisha ujenzi wa vifaa vya ziada vya kuhifadhia wa sukari na vifungashio ili kupunguza gharama na kuongeza uwezo wa kampuni kuchapa vifungashio vyake.

 

Aidha, mradi utazalisha umeme kwa ajili ya matumizi ya kiwanda na hata kuelekeza umeme mwingine kwenye gridi ya taifa kuiuzia TANESCO. Vilevile, mradi utaboresha ufanisi katika uzalishaji kwa kupunguza gharama kubwa kwa kiasi kikubwa, kwani vifaa na vipuri chakavu vitabadilishwa na hivyo kuimarisha uwezo wa usindikaji.

 

Ongezeko la kilolita 4,000 katika uzalishaji wa ethanoli kwenye kiwanda cha ethanoli, italeta kiwango cha uzalishaji wa kilolita 16,000 kwa mwaka ili kukidhi mahitaji ya ndani na yale ya Afrika Mashariki.

 

Mradi huo umeidhinishwa na wanahisa wote wakati wa Mkutano Maalumu wa Wanahisa uliofanyika Mei 14, jijini Dar es Salaam, Tanzania. Katika mkutano huo, Illovo Sugar Africa iliwakilishwa na Bwana Gavin Dalgleish na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliwakilishwa na Msajili wa Hazina, Bwana Athumani S. Mbuttuka.

 

Kuidhinishwa kwa Mradi huo inaonesha kuunga mkono kwa Kampuni ya British Foods, inayomiliki Kampuni ya Illovo Sugar Africa, na imani kubwa iliyonayo kwa Kampuni ya Illovo Sugar Africa inayokuwa hasa kwenye soko la Sukari barani africa.

 

Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Sukari ya Kilombero, Balozi Ami Mpungwe anasema: "Dhamira kubwa ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kujenga mazingira mazuri ya uwekezaji kwa sekta binafsi hususan sera na hatua za makusudi za Serikali katika kulinda viwanda vya ndani vya sukari, kimekuwa kichocheo kikubwa kwa  wanahisa kuunga mkono na kuidhinisha mradi huu hapa nchini.”

 

Faida za kiuchumi katika kipindi baada ya utekelezaji wa mradi huo zinatarajiwa kuwa: 

 

·      Ongezeko maradufu la kiwango cha miwa kutoka kwa wakulima wa nje na kuongeza mara tatu ya kipato cha wakulima hao kufikia Shilingi bilioni 270 ifikapo mwaka 2028;

 

·      Idadi ya wakulima wadogo wadogo wanaosambaza miwa kwa kiwanda kipya itaongezeka kutoka 7,500 hadi 14,000 - 16,000, na hivyo kugusa moja kwa moja zaidi ya wananchi 50,000 wa maeneo yanaozunguka bonde la Kilombero na kujishughulisha na uzalishaji wa sukari;

 

·      Kutakuwa na ongezeko la ajira ya moja kwa moja ya zaidi ya  watu 2,000 Kutokana na upanuzi wa kiwanda na uzalishaji wa miwa;

 

·      Jumla ya kodi ya shilingi bilioni 66.8 zinazolipwa sasa na Kampuni ya Sukari ya Kilombero inakadiriwa kuongezeka mara tatu kutokana na upanuzi na ufanisi wa biashara mpaka kufikia mwaka 2028; na

 

·      Aidha, inakatazamiwa kuwa mchango wa Kampuni ya Sukari ya Kilombero kwa uchumi wa nchi utaongezeka maradufu kutoka kiasi cha sasa cha shilingi bilioni 340 kwa mwaka hadi kufikia wastani wa shilingi bilioni 750 kiwanda kipya kitakavyoanza uzalishaji.

 

Akizungumza kwa niaba ya mbia wa Kilombero, Illovo Sugar Africa, Gavin Dalgleish alisema uwekezaji wa Illovo katika mradi huo wa upanuzi wa kiwanda ndio uwekezaji mkubwa zaidi uliowahi kufanywa nao katika bara zima la Afrika.

 

"Tunajivunia sana kushirikiana na watu wa Tanzania katika uwekezaji huu wa kihistoria unaolenga kupunguza kiwango cha pengo la sukari ambayo inapaswa kuingizwa nchini kila mwaka na kukidhi mahitaji ya matumizi. Kwa kupunguza uagizaji wa sukari kwa tani 144,000, makadirio yetu ni kwamba Tanzania itaokoa dola milioni 71 kila mwaka, ”alisema Dalgleish.

 

Ujenzi wa mradi inatarajiwa kuchukua miezi 25 na unatarajiwa kukamilika Julai 2023.

 

Bodi ya Kampuni ya Sukari ya Kilombero na Menejimenti inapenda kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (mwekezaji mwenza katika mradi huo kupitia hisa zake asilimia 25), Illovo Sugar Africa na wakulima wa Kilombero kwa ushirikiano na kuunga mkono mradi huu tangu kuanzishwa kwake. Aidha, Kampuni inawashuru wafanyakazi wake na wadau wengine wengi, washirika, wateja na watoa huduma ambao wamekuwa wakihimiza na kusaidia kufanikisha mipango ya upanuzi wa kiwanda.

 

Kiwanda cha Sukari cha Kilombero kinamilikiwa na Kampuni ya Illovo Sugar kwa asilimia 75 huku Serikali ya Tanzania ikimiliki asilimia 25.

TANZIA-MHE. KHATIB

MCHENGERWA AWATAKA MAAFISA WA TAKUKURU KUTUNZA SIRI ZA WANAOTOA TAARIFA ZA VITENDO VYA RUSHWA

$
0
0


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akiagana na Viongozi Wakuu wa TAKUKURU mara baada ya kikao kazi cha Waziri huyo na Viongozi hao wa TAKUKURU Jijini Dar es Salaam chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji. 

  

Na James Mwanamyoto, Dar es Salaam


 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU) kutotoa siri za wananchi wanaowasilisha taarifa za uwepo wa vitendo vya rushwa kwenye taasisi hiyo ili ziweze kufanyiwa kazi.

Akizungumza wakati wa kikao kazi chake na Viongozi wa TAKUKURU jijini Dar es Salaam, Mhe. Mchengerwa amemuelekeza Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna wa Polisi (CP) Salum Hamduni kuhakikisha vyanzo vya taarifa za rushwa vinalindwa ili kuhamashisha wananchi kuendelea kutoa taarifa zitakazoiwezesha Serikali kulinda rasilimali za taifa.

Mhe. Mchengerwa amehimiza uadilifu kwa Watumishi wa TAKUKURU hususan kwenye eneo la utunzaji siri za watoa taarifa ili kuwajengea wananchi imani ya kuendelea kushirikiana na TAKUKURU katika mapambano dhidi ya rushwa.

“Utoaji wa siri za wanaowasilisha taarifa za vitendo vya rushwa, unahatarisha usalama wao, hivyo Mkurugenzi Mkuu uanze na suala hili ili tubaini watumishi wote wanaotoa siri za watoa taarifa na kuwachukulia hatua za kinidhamu.” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.

Mhe. Mchengerwa amewaasa watumishi hao kutenda haki wanaposhughulikia vitendo vya rushwa ili kutoitia dosari Ofisi hiyo inayoaminiwa na wananchi.

Kuhusu utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais juu ya taasisi hiyo kujikita moja kwa moja katika majukumu yake, Mhe. Mchengerwa amewakumbusha Viongozi hao kutekeleza maelekezo hayo ipasavyo kwa kushughulikia masuala yanayohusiana na rushwa, ubadhirifu wa mali za umma na uhujumu uchumi na si vinginevyo.

Aidha, Mhe. Mchengerwa amesema, Serikali ina imani na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP Salum Hamduni na Naibu wake Bi. Neema Mwakalyelye na ndio maana Mhe. Rais amewapa dhamana ya kuiongoza taasisi hiyo nyeti.

 

Akizungumza na viongozi wa TAKUKURU kabla ya kumkaribisha Mhe. Mchengerwa, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewahimiza watendaji wa TAKUKURU kutofanya kazi zisizoihusu TAKUKURU kama ambavyo Mhe. Rais na Waziri Mchengerwa wamekuwa wasisitiza.

Mhe. Ndejembi ameitaka TAKUKURU kuhakikisha inayakamilisha kwa wakati mashauri ya msingi yanayoihusu taasisi hiyo na kwa yale yasiyokuwa na msingi yafutwe ili kutoa fursa kwa taasisi hiyo kuendelea kutekeleza majukumu yenye tija kwa taifa.

Kwa upande wake. Mkurugenzi wa TAKUKURU, CP Salum Hamduni amekiri kupokea maelekezo ya Mhe. Waziri na kuahidi kuyafanyia kazi ndani ya muda aliolekeza.

Ili kutekeleza maelekezo ya Mhe. Mchengerwa kwa wakati, CP Hamduni amewataka watumishi wake kujitoa kikamilifu katika utekelezaji wa majukumu ya TAKUKURU ili kufikia malengo ya taasisi hiyo.

Mhe. Mchengerwa amefanya kikao kazi na Viongozi wa TAKUKURU mara baada ya Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo na Naibu wake kuapishwa na Mhe. Rais-Ikulu Jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kuhimiza uwajibikaji na utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais ya kuongeza ufanisi wa utendaji kazi katika taasisi hiyo.

Tigo host Innovation Week Panel Discussion on how technological advancement can enhance business efficienc

$
0
0


          Emmanuel Mallya - Chief Technical Officer at Tigo Tanzania addressing how our technical innovation has transformed our customers' businesses during the panel discussion on how Technological Advancement can enhance business efficiency. #Innovationtz #DigitalInnovation 


DIGITAL LIFESTYLE: "Technology has changed our lives, adoption of mobile money is very huge in TZ" Josina Njambi-Head of Innovation & Development @NMBTanzania during the panel discussion on how technological advancement can enhance business efficiency #IWTz2021 @innovationweektz



"Tigo are enablers for commerce/economy grow" Sameer Hirji - CEO @SelcomTanzania  during the panel discussion on how technological advancement can enhance business efficiency.#IWTz2021 @innovationweektz



LIVING DIGITAL LIFE: "We are happy to work with Tigo ensuring that our community who have small saving & lending groups are able to access an app to enable them to operate in a better way" Marianna Balampama - Country Director PACT #BusinessEnhance#IWTz2021 @innovationweektz



"We have very strong, innovative and remarkable products and service" @SimonAKarikari Managing Director

#UbunifuNdioJadiYetu#MaishaKidigitaliNaTigo #TigoPesa#TigoBusiness#IWTz2021 @innovationweektz




RUZUKU YA BILIONI 7 YATOLEWA KWA VIJANA KUJIKIMU NA KUANZISHA BIASHARA

$
0
0

  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mwitikio wa Kitaifa kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS)  Audrey Njelekela, akizungumza katika kikao kazi wakati wa kuutambulisha Mradi wa Awamu ya Pili wa Timiza Malengo (AGYW) mjini hapa jana.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Victorina Ludovick, akizungumza kwenye kikao hicho.


Na Dotto Mwaibale, Singida


JUMLA ya Sh. 7,442,100,000 zimetumika kwa Wasichana Balehe na wanawake Vijana walio ndani ya shule wapatao 16,011 na jumla ya walengwa 9,971 walio kuwa nje ya shule kwenye mradi wa Timiza Malengo (AGYW)  kwa Awamu ya Kwanza walipatiwa ruzuku ya  kujikimu na kuanzisha biashara. 

Hayo yamebainishwa na mratibu wa mradi huo kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) , Edgar Mapunda wakati akizungumzia mafanikio ya mradi huo Awamu ya Kwanza ulioanza kwa majaribio Mwaka 2018 hadi Desemba 2020  na kuutambulisha mradi wa Awamu ya Pili katika kikao kazi kilichofanyika mjini hapa jana.

Mapunda alisema Sh. 3,888,430,333.00 zilitumika kwa Wasichana Balehe 9971 walio kuwa nje ya shule kwa ajili ya mitaji ya kuanzisha biashara.

" Mafanikio mengine yaliyopatikana ni kuongeza hamasa na kuimarisha mikakati ya kuwafikia Wasichana Balehe na Wanawake Vijana  walio ndani ya shule 16,011 katika Halmashauri na Mikoa iliyoanishwa Kitaifa." alisema Mapunda.

Alisema Vijana 47,705 walifikiwa na kampeni ya kipepeo na  inakadiriwa kuwafikia vijana zaidi ya 8,630,161 kupitia redio.

Aidha Mapunda alisema Wazazi wapatao 10,470 walipatiwa mafunzo ya malezi na makuzi, viongozi 1,114 waliemishwa kuhusiana na mila na desturi zinazoweza kusababisha maambukizi ya VVU na kupunguza unyanyapaa na ubaguzi.

" Inakadiriwa takribani Wasichana Balehe na Wanawake Vijana 200,000 walipata habari kupitia radio za kijamii kupitia vipindi 15 vilivyoandaliwa" alisema.

Akitaja mafanikio zaidi Mapunda alisema jumla ya kondomu ‘dispenser’ zipatazo 5,000 zilinunuliwa na kusimikwa kwenye maeneo hatarishi na maeneo ya kazi na Vijana balehe 165,497 walipatiwa elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya  VVU na UKIMWI huku Wasichana Balehe na Wanawake Vijana 148,002 walifikiwa na huduma za upimaji wa VVU ambapo kati yao 3,191 waligundulika kuwa na maambukizi na jumla ya 2,873 walianzishiwa huduma za tiba.

Alitaja baadhi ya changamoto kwenye Awamu ya Kwanza kuwa ni upungufu wa elimu ya VVU na UKIMWI, Afya ya Uzazi na stadi za maisha mashuleni, Upungufu wa mifumo,Madhubuti wa ufuatiliaji kwa ngazi ya mlengwa pamoja na upungufu wa huduma Rafiki kwa vijana katika vituo vya afya na mafunzo kwa wafanyakazi Mikakati Madhubuti ya kushughulikia masuala ya Ukatili wa kijinsia Wanaume wengi kutojitokeza kupata huduma. 

Alitaja changamoto nyingine kuwa ni ucheleweshwaji wa uhaulishaji fedha kwa walengwa wakati wa kipindi cha mpito kwenye mradi wa TASAF kutoka TASAF I kwenda TASAF II.

Awamu ya Pili ya mradi huo utatekelezwa katika maeneo ya Morogoro (Mlimba DC, Ifakara TC, Morogoro MC, Ulanga DC na Malinyi DC) na Dodoma (Kongwa DC, Mpwapwa DC, Chamwino DC, Kondoa TC , Dodoma MC, na Bahi DC) Singida ni (Iramba DC, Singida MC na Singida DC), Geita (Geita DC and Chato DC)Tanga (Tanga MC).

Mradi huo unatekelezwa kwa ufadhili wa Global Fund  kwa kushirikiana na  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,  Jinsia Wazee na Watoto, TAMISEMI, Amref Health Africa pamoja na Taasisi ya Vijana Tanzania  (TAYOA)

TASAC Yawajengea Uwezo Wahariri na Wanahabari Dar

$
0
0
Na Hussein Ndungulile,  Dar es Salaam
 
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imeendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wahariri na waandishi wa habari juu ya  shughuli zake na sheria zinazosimamia sekta ya majini.

Akiwasilisha mada katika semina hiyo Afisa Uhusiano wa TASAC, bw.Nicholaus Kinyariri  alisema  lengo la semina hii ni kuwajengea uelewa na uwezo wa jinsi ya kuripoti maswala yanayohusu sekta hiyo.

Amebainisha kuwa TASAC ipo chini ya wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na kwamba imeanzishwa chini ya kifungu namba 4 cha sheria 14 ya mwaka 2017 ambayo rasmi ilianza kutumika mwaka 2018.

"TASAC imeamua kutoa semina hii kutokana na kuwepo uelewa mdogo kwa jamii kuhusiana na shughuli zake na sheria mbalimbali zinazosimamia sekta ya majini, " Alisema bw. Nicholaus.

Alisema TASAC ina majukumu mbalimbali inayotekeleza yakiwemo ya usimamizi na udhibiti huduma za Bandari na usafiri wa Meli, Biashara ya Meli katika maeneo husika pamoja na kusimamia maslahi mapana ya bidhaa za kipekee wanzaopaswa kuzisimamia.

"TASAC pia imepewa jukumu la kusajili vyombo vya majini kuanzia mita nne,  vyombo vya Uvuvi na Starehe." Alisema.

Aliongeza kuwa tangu TASAC kuanzishwa kwake imeweza kupata mafanikio mbalimbali ikiwemo kuchangia gawio kwa serikali la Sh Bilioni 40, utoaji wa leseni 804 za Uwakala wa meli, kachangia mapato ya serikali pamoja na kuboresha huduma za usafiri wa majini.

Pia alibainisha kuwa shirika katika kutimiza majukumu yake wanashirikiana na wadau wengine wakiwemo mamlaka ya Mapato Tanzania {TRA), Jeshi la Polisi-kikosi cha Majini, Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini ( TMA).

Kwa upande wake Meneja Udhibiti wa huduma za Bandari bw. Julius Mitinje Alisema shirika hilo linafanya udhibiti katika maeneo ya mwambao wa bandari za Dar es salaam, Tanga na Mtwara pia kwa upande wa maziwa ni Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa.

Alisema wamekuwa wakifanya uhakiki wa uzito wa mizigo ndani  ya makasha, Bandari kavu na watoa huduma mchanganyiko bandarini.

KATIBU MKUU AKUTANA NA WATAALAM KUTOKA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA (AfDB)

$
0
0

 

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akizungumza na ugeni wa wataalam kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (African Development Bank (AfDB) kuhusu maandalizi ya utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Farkwa.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akiwa katika picha ya pamoja na ugeni wa wataalam kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (African Development Bank (AfDB) na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Maji.

 

 Na Mwandishi Wetu


Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga amekutana na wataalam kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (African Development Bank (AfDB) na kufanya nao mazungumzo kuhusiana na ujenzi wa bwawa la Farkwa.

 

Mhandisi Sanga amefanya kikao na wataalam hao katika ofisi za Wizara katika mji wa serikali Jijini Dodoma.

 

Wataalam hao wapo katika ziara ya maandalizi ya awali ya utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Farkwa ambapo Mhandisi Sanga amesema serikali imejiandaa kwa mradi huo ikiwamo kulipa fidia kwa wananchi wa maeneo ambayo wanatakiwa kuhama na kupisha ujenzi.

 

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeonesha nia ya ya kushiriki katika kazi ya ujenzi wa Bwawa la Farkwa.

 

Akizungumza kwa niaba ya (AfDB) Bwana Benson Nkhoma amesema awali katika kufanya maaandalizi ya utekelezaji wa mradi huu walifanya vikao viwili mapema mwaka huu kwa njia ya kieletroniki.

 

Amesema katika vikao hivyo walikubaliana kuwe na ziara ya maandalizi ya utekelezaji wa program ili kukusanya taarifa na takwimu za msingi.

 

Watalaam hao kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika wamepata fursa pia ya kufanya kikao na Maafisa wa  Wizara ya Fedha na Maafisa wa Ofisi ya Makamu wa Rais kujadili kwa upana utekelezaji wa mradi wa bwawa la Farkwa linalotarajiwa kuongeza huduma ya maji katika Jiji la Dodoma.

Jeshi la Polisi lapokea vitabu vya mwongozo wa kuzuia na kufichua uhalifu

$
0
0

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro (katikati) akipokea baadhi ya nakala za vitabu vya mwongozo wa kuzuia na kufichua uhalifu katika Kata/Shehia kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Jamii wa Kampuni ya vinywaji ya Coca Cola, Salum Nassoro, ambapo jumla ya nakala 2000 zilichapishwa na kukabidhiwa kwa Jeshi hilo kupitia ufadhili wa kampuni hiyo ya vinywaji, kushoto anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI Robert Boaz, hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es salaam. Picha na Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro (katikati) akionesha baadhi ya nakala za vitabu vya mwongozo wa kuzuia na kufichua uhalifu katika Kata/Shehia kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Jamii wa Kampuni ya vinywaji ya Coca Cola, Salum Nassoro, ambapo jumla ya nakala 2000 zilichapishwa na kukabidhiwa kwa Jeshi hilo kupitia ufadhili wa kampuni hiyo ya vinywaji, kushoto ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI Robert Boaz, hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.

DAWASA YABADILI "GIA ANGANI" NI KUHUSU MITA ZAKE

$
0
0

Baadhi ya Watumishi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wakitoa elimu ya mabadiliko ya usomaji mita na upokeaji wa bili za maji uliofanyika hivi karibuni.
 
 
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 
 

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeendelea na zoezi la kutoa elimu kwa wateja wake wa Jiji la Dar es Salaam na miji ya  Pwani juu ya mabadiliko ya usomaji wa mita za maji na upokeaji wa bili za maji uliofanywa hivi karibuni.

 

Hatua hiyo inatokana na mabadiliko ya usomaji wa mita yaliyofanywa na Mamlaka kutoka tarehe 1 hadi 15 kwenda tarehe 20 hadi 30 ya kila mwezi.

 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti juu ya mabadiliko hayo, wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na baadhi ya mikoa ya Pwani wamepongeza mabadiliko hayo na kusema yamefanyika wakati muafaka na yataleta tija kwa Mamlaka na Wananchi kwa ujumla.

“Tunaishukuru DAWASA kwa mabadiliko haya ya usomaji mita kwa tarehe za mwisho wa mwezi, sisi wananchi tulishasema sana kuhusu kuletewa bili tarehe tofauti tofauti wakati vipato vyetu vinatofautiana” alisema ndugu Ramadhan Abdul mkazi wa Kinondoni Shamba.
 

Zakia Mrisho mkazi wa kitongoji cha Sanze, wikaya ya Kisarawe anasema mabadiliko hayo yamewasaidia sana wananchi wanaotegemea vipato vyao mwisho wa mwezi.

 

“mfano sisi watumishi wa umma kipato chetu kikuu ni mshahara unalipwa mwisho wa mwezi, vile DAWASA walikuwa wanatusomea bili na kutuma message muda wowote halikuwa jambo zuri, tuliishia kugombana nao na wakati mwingine kuleteana vitisho mbalimbali. Lakini kwa mabadiliko haya tunajua wamesikia kilio chetu na wakaamua kujirekebisha” alisema bi Zakia.

 

Kwa upande wake *Mkurugenzi wa Biashara na huduma kwa wateja  DAWASA, Bi Rithamary Lwabulinda* amesema mabadiliko  hayo yaliyofanywa na Mamlaka yalifanyiwa utafiti wa kina na shirikishi yaliyolenga  kuboresha huduma za majisafi na usafi wa mazingira.

 

"Mara kwa mara huwa tunatenga muda wa kuongea na wateja wetu,hivyo mabadiliko haya ni miongoni mwa sauti za wateja wetu walizotushauri juu ya uboreshaji wa huduma zetu ili kuweza kuwafikia wengi zaidi" alisema Bibi Lwabulinda.

Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>