RAIS WA ZANZIBAR ALHAJ DK.HUSSEIN ALI MWINYI ALIHUTUBIA BARA LA EID EL FITRY KATIKA UKUMBI WA SHEIKH IDRISA ABDULWAKIL KIKWAJUNI ZANZIBAR
Jafo atoa Siku kumi kwa Mkurugenzi wa Kigoma
NA LULU MUSSA, KIGOMA
RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AHUTUBIA KATIKA BARAZA LA EID ELFITR LILILOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA KARIMJEE JIJINI DAR ES SALAAM
MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AHUTUBIA MKUTANO WA KAMPENI ZA CCM MUHAMBWE KIGOMA
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Muhambwe Wilayani Kibondo MKoani Kigoma Dkt. Florence Samizi kwenye Mkutano wa Kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mdogo unaotarajiwa kufanyika tarehe 16 Mei 22021, kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Hayati Atashasta J Nditiye leo Mei 14,2021.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akiinadi Ilani ya Utekelezaji ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM alipokua akihutubia Mkutano wa Kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM Jimbo la Muhambwe Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma kwa ajili ya Uchaguzi Mdogo unaotarajiwa kufanyika tarehe 16 Mei 22021, kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Hayati Atashasta J Nditiye leo Mei 14,2021. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
MKE WA RAIS WA ZANZIBAR MAMA MARIAM MWINYI AMETOA MKONO WA EID EL FITRY
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwasalimia Watoto wa Kijiji cha SOS Mombasa Zanzibar alipofika kuwasalimia na kuwapa mkono wa Eid El Fitry Kijijini Kwao Mombasa Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Maria Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watoto wa Kijiji cha SOS alipofika kuwasalimia na kuwapa mkono wa Eid El Fitry, alipofika katika makazi yao Mombasa Wilaya ya Magharibiu B Unguja.(Picha na Ikulu),
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwa na Mtoto wake Tariq Hussein Mwinyi wakitowa mkono wa Eid El Fitry kwa Watoto wa Kijiji cha SOS, alipofika kuwasalimia na kutowa mkono wa Eid.(Picha na Ikulu).
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Watoto wa SOS (kulia kwake) Wahida Abdalla na (kushoto kwake) Yusseuf Abdalla, baada ya kumalizika kwa hafla ya kutowa mkono wa Eid El Fitry kwa Watoto wa Kijiji cha SOS Mombasa Zanzibar.(Picha na Ikulu).
WATOTO wa Nyumba ya Watoto Mazizini Jijini Zanzibar wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (hayupo pichani) alipofika kjatika makazi yao kwa kuwasalimia na kutoa mkono wa Eid El Fitryt.(Picha na Ikulu).
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwasalimia na kutowa nasaha zake kwa Watoto wa Nyumba ya Watoto ya Serikali Mazizini Jijini Zanzibar Wilaya ya Magharibi B Unguja.(Picha na Ikulu).
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwa na Mtoto anayelelewa katika Nyumba ya Watoto Mazizini Hawa Abdalla, alipofika kuwatambelea na kutoa mkono wa Eid El Fitrey.(Picha na Ikulu).
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Wazee Jinsia na Watoto Bi.Abeida Rashid Abdalla (kushoto kwake) na Watoto wake Jamila Hussein Mwinyi na Siti Hussein Mwinyi, wakiwa wamepakata watoto wanaolelewa katika Nyumba ya Watoto Mazizini Jijini Zanzibar Wilaya ya Magharibi B Unguja.(Picha na Ikulu).
SIMBA MATUMAINI KIBAO IKIVAANA NA KAIZER CHIEFS
Wachezaji wa Simba wakiwa katika mazoezi ya mwisho kujiandaa na mchezi wao wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (Muda wa mazoezi ya kujiandaa na robo fainali ya (TotalCAFCL).
"Hii ni Ligi ya Mabingwa, tunatarajia mchezo mgumu kesho hasa sababu tupo ugenini lakini hatutaki kuzuiliwa. Kaizer Chiefs ni timu kubwa hatuwezi kuidharau lakini tupo tayari kupambana."- Kocha Didier Gomes kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Kaizer Chiefs.
MSUDANI ALIYEKIMBIA KUFUNGWA KWA UJANGILI AREJEA NCHINI
RAIA wa Sudan, Amir Mohamedi aliyetoroka nchini baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani kwa makosa ya ujangili na kufanya biashara haramu ya pembe za ndovu amerejea nchini.
Taarifa za kurejea nchini kwa Amir Mohammed zimetolewa na aliyekuwa mshirika wake wa karibu katika biashara haramu ya pembe za ndovu (jina limehifadhiwa) na kuthibitishwa na yeye mwenyewe katika mahojiano yake na blog hii.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, Amir Mohamedi alikamatwa katika nyumba aliyokuwa akiishi eneo la Kijitonyama, Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam akiwa na idadi kubwa ya pembe za ndovu alizokuwa amezificha darini na kufikishwa Kituo cha Polisi cha Mabatini na baadaye alifunguliwa mashtaka Mahakama ya Kisutu.
"Alikuwa nje kwa dhamana wakati kesi yake na wenzake inaendelea. Siku moja kabla ya hukumu alidokezwa na watu wake kuwa anahukumiwa kufungwa, akatoroka akakimbilia kwao Sudan. Na alifanikiwa kujua kinachoendelea mahakamani na kutoroka kwa sababu ya pesa.
"Siku ya hukumu hakuwepo mahakamani hivyo alihukumiwa akiwa hayupo alikuwa ameishatoroka. Alihukumiwa kufungwa jela miaka kumi.
"Tangu alipotoroka ni zaidi ya miaka kumi sasa ndiyo amerudi na anafanya biashara ya madini na mimi alinidhulumu mpaka leo namdai lakini hataki kunilipa. Niseme ana migodi ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini. Kuna kijana mmoja mweupe anafanya kazi ubalozi wa Sudan huyu anajua sana hilo kasheshe lao mkimpata huyo atawapa historia hiyo vizuri sana," alisema.
Alipotafutwa Amir Mohamedi kupitia simu yake ya mkononi anayoitumia baada ya kurejea nchini na kuhojiwa alikiri kwamba ni kweli hilo ni jina lake, ni raia wa Sudan na kwamba aliwahi kushtakiwa katika Mahakama ya Kisutu lakini hakuwa tayari kueleza alishtakiwa kwa makosa gani na kesi yake iliishaje.
Amir pia alikiri kuondoka nchini na kwenda kuishi Sudan na Kenya kwa muda mrefu kabla ya kurejea nchini na kuanza kujishughulisha na uchimbaji wa madini.
Taarifa zaidi zimeonyesha kuwa Amir Mohamedi kwa sasa ana makazi yake eneo la Mikocheni mkoani Dar es Salaam lakini muda mwingi anakuwa mikoani ambako ana migodi ya madini.
Uchunguzi wa sakata hili unaendelea.
UTEUZI
MZEE PINDA, RC MAHENGE WAONGOZA KAMPENI YA UPANDAJI MITI ZUZU, DODOMA
MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO APIGA KURA KUCHAGUA MBUNGE BUHIGWE
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akisubiria kukabidhiwa karatasi ya kupiga kura kutoka kwa Msimamizi wa Kituo cha kupiga kura Polling Station Wilayani Buhigwe MKoani Kigoma Anania Emily leo Mei 16,2021 kwa ajili ya Uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Buhigwe (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akipiga Kura ya katika Kituo cha kupiga kura Polling Station Wilayani Buhigwe MKoani Kigoma leo Mei 16,2021 kwa ajili ya Uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Buhigwe.
Mkurugenzi Mtendaji LHRC awafunda vijana Dar na Pwani
MKURUGENZI Mtendaji Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Bi. Anna Henga amewataka vijana kuwa na malengo katika maisha yao na kuhakikisha wanafanya jitihada za kuyasimamia ili yaweze kutimia. Mkurugenzi huyo ameyasema hayo jana alipokuwa akifungua kongamano la vijana toka vyuo vikuu, vyuo vya kati na sekondari jijini Dar es Salaam lililoandaliwa na Club inayohamasisha elimu na maadili kwa vijana (EEMC).
Alisema kijana mwenye malengo hana budi kuweka jitihada katika kuyakamilisha na kutokubali kukata tamaa hata kama anakumbana na vikwazo fulani kwenye maisha yake. "Kijana mwenye malengo hana budi kung'ang'ania malengo yake katika kuyakamilisha, usikate tamaa wala kukubali kushindwa kirahisi," alisema Bi. Henga akiwasilisha mada yake kwa vijana hao.
Aliwataka vijana kutumia changamoto wanazokutana nazo kama fursa za mafanikio kuelekea katika malengo yao. Ameongeza kuwa hata yeye katika mafanikio yake amekuwa akitumia vikwazo kama fursa kukamilisha malengo jambo ambalo linawezekana kwa vijana endapo watafanya maandalizi na jitihada kukamilisha malengo yao.
"..Jambo la msingi ni kufanya maandalizi kuelekea kukamilisha malengo yako, tujiandae na tufanye kazi kwa bidii na sisi ambao tunasoma tusome kwa bidii sana hakuja jambo zuri linalokuja kirahisi bila kufanya jitihada wewe binafsi..pia tusikubali kupoteza muda 'keep time'...," alisisitiza Mkurugenzi huyo Mtendaji wa LHRC.
Alisema kijana mwenye malengo anatakiwa kujenga mahusiano mazuri na watu mbalimbali (networking) jambo ambalo linaweza kumsaidia mbeleni kuelekea kukamilisha malengo yake, hivyo kuwataka vijana kuto puuza mahusiano mazuri na watu.
Pamoja na hayo aliwataka vijana kuwa waadilifu na wacha Mungu katika kila jambo wanalolifanya kwani ni moja ya daraja la mafanikio kuelekea kutimiza ndoto zao. Unapokuwa mwadilifu na kumshirikisha Mungu mbele kwa kila jambo lako huwezi kushindwa kamwe, siku zote utafanikiwa katika jambo lako," alisisitiza kiongozi huyo.
Kwa upande wao mmoja wa waratibu wa mkutano huo, David Sospita alisema kongamano hilo kubwa la vijana toka vyuo vikuu, vyuo vya kati na sekondari lililoandaliwa na taasisi ya EEMC toka Dar es Salaam na Pwani na kupewa kauli mbiu ya 'kijana na malengo' limelenga kukutanisha vijana kuwaelimisha na kuchagiza malengo yao.
Alisema limeandaliwa ili kuchochea hamasa ya elimu, elimu dhidi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi, elimu ya kujitegemea kwa vijana na pamoja na uongozi na maadili kwa vijana. Aliongeza katika kongamano hilo linalofanyika Chuo Kikuu cha Muhimbili Dar es Salaam vijana watanolewa namna ya kujiajiri na kutimiza ndoto za malengo yao.
RAIS MSTAAFU KIKWETE KUFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA ELIMU BORA, DAR
RAIS mstaafu wa Awamu ya Nne nchini Tanzamia, Dk. Jakaya Kikwete anatarajiwa kufungua mkutano wa kimataifa wa elimu Bora ulioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) ambao utashirikisha wadau mbalimbali wa elimu kutoka serikalini, asasi na taasisi za kimataifa za ndani na nje ya nchi.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na vyombo vya habari, Mratibu wa Taifa TEN/MET, Bw. Ochola Wayoga amesema mkutano huo wa kimataifa juu ya elimu bora unatarajiwa kufunguliwa na Rais mstaafu Awamu ya Nne, Kikwete siku ya Jumanee ya tarehe 18 Ukumbi wa Kisenga Jengo la LAPF na utafanyika hadi tarehe 20 Mei 2021.
Bw. Wayoga alisema Mkutano huo wa Ubora wa Elimu utajadili Uwajibikaji wa pamoja katika kugharamia elimu bora nchini, ambapo utatoa fursa kwa wadau wa elimu ikiwepo serikali, wanachama wa mtandao, Washirika wa Maendeleo (Development Partners) pamoja na wadau mbalimbali wa elimu nchini kujadili hali ya ubora wa elimu kwa nia ya kuboresha zaidi.
Aidha aliwataja baadhi ya washiriki wa Mkutano huo ni pamoja na wajumbe kutoka Wizara ya Elimu, SayansinaTekinolojia, TAMISEMI,Mashirika yasiyo ya kiserikali, Wadau wa maendeleo, waheshimiwa Wabunge, Taasisi za elimu ya juu, tasisi za utafiti, Vyuo na shule za ufundi, Walimu, Wazazi na Wanafunzi.
"...mkutano huu utahudhuriwa pia na mabalozi wanao ziwakilisha nchi zao, wageni wengine mbalimbali kutoka nchi za ng’ambo, makampuni na taasisi za watu binafsi. Wajumbe takriban 200 wamethibitisha kushiriki katika mkutano huu; baadhi watakuwa wakishiriki kwa njia ya Mtandao," aliongeza Mratibu wa Taifa TEN/MET, Bw. Wayoga.
Alibainisha kuwa pamoja na mambo mengine Mkutano huo unatarajiwa kutoka na maazimio ambayo ni mapendekezo ya namna ya kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu hapa nchini kwa kutumia matokeo ya taarifa za tafiti na uzoefu kutoka nchi nyingine.
"...Maandalizi yote yamekamilika hivyo naomba kuwashukuru wadau mbalimbali ambao wamewezesha kufanyika kwa Mkutano, ubalozi wa Swedeni , Global Partnership for education kupitia mradi wa Education Out Loud, Norad kupitia Action Aid Tanzania, Pestalozzi na HDIF Tanzania." Alisema kiongozi huyo.
KAIMU SHEIKH WA MKOA WA SINGIDA KUPELEKA AJENDA BAKWATA YA KUJENGA HOSPITALI YA WAISLAMU
Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro, akitoa salamu za Eid katika Baraza la Eid lililofanyika Msikiti wa Kata ya Mandewa mkoani hapa juzi. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bakwata Mkoa wa Singida, Jumanne Nkii, Katibu wa Bakwata Mkoa wa Singida, Burhan Mlau na Sheikh wa Msikiti wa Kata ya Mandewa, Salumu Chima
Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro amesema anatarajia kuwasilisha katika Mkutano Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) ajenda ya nia ya Waislamu wa Mkoa wa Singida kutaka kujenga hospitali yao.
Sheikh Nassoro ameyasema hayo wakati akitoa salamu za Eid katika Baraza la Eid lililofanyika Msikiti wa Kata ya Mandewa mkoani hapa jana.
" Taasisi zote zilizopo Tanzania hakuna taasisi yenye rasilimali watu kama Taasisi ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania Bakwata ambayo ina majority ya watu tatizo ni watu hao wanatumiwaje nasema Waislamu Mkoa wa Singida tunaweza kuanza kujenga Hospitali yetu ili dada zetu na mama zetu waweze kupata staha." alisema Nassoro.
Nassoro alisema jambo hilo analitanguliza na anatarajia kuliwasilisha kwenye mkutano huo na kuwa hiyo ni ajenda ya waislamu wa mkoa huo na mara moja kamati zitaundwa ili kuanza taratibu za kazi hiyo.
Alisema ana uhakika kazi hiyo itakapo anza watu wa chini, watu wanyonge na taasisi kubwa na matajiri watawaungwa mkono na hospitali hiyo itasimama kama uyoga na watu watashangaa.
Sheik Nassoro alisema walipotoka ni mbali na wanapokwenda ni karibu na kuwa kwa sasa majukumu pia yameongezeka na ni mengi na makubwa hivyo ni wakati wa kujifunga mkanda na muda wa kufanya majungu, fitina na kuwa fulani hafai sasa basi
kwani ni muda wa kusikiliza rai kutoka kwa mtu anayetaka waislamu wa Mkoa wa Singida kupata maendeleo na kuwa ofisi ya Bakwata mkoa ipo wazi wakati wote na kama mtu atakuwa na rai waambiwe viongozi au Katibu ambaye ataiwasilisha.
Alisema kukamilika kwa hospitali hiyo kutatoa ajira kwa mabinti na vijana wa kiislamu ambao ni wauguzi na madaktari ambapo aliwataka waanze mbio za kuyatekeleza hayo kwani wamechelewa mno.
Aidha Nassoro alihimiza kufanyike mara moja hatua za usajili wa Chuo cha Nnujumu ili kipate usajili kama anavyokiangalia kwa umuhimu wake Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubery.
Katika hatua nyingine Nassoro alisema muda huu anaokaimu nafasi hiyo kwa udogo wa mambo amejifunza kuwa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) linauchache wa wataalamu licha ya kuwepo wataalamu wengi lakini hawapo ndani ya baraza hilo hivyo alitumia nafasi hiyo kuwaomba wataalamu wa sekta zote waingie ndani ya Bakwata ili uislamu upate faida ya taaluma zao.
Nassoro alisema ndani ya Bakwata kuna changamoto ya mambo ya utawala 'Admistration' na kuwa anauhakika ndani ya uislamu kuna wataalamu wa jambo hilo hivyo wasikae nyuma tu kwa sababu wao sio wajumbe wa Bakwata ambapo aliwataka waende ili baraza hilo liwe na sura ya hali waliyonayo na hali ya dunia inavyokwenda.
Nassoro pia alizungumzia changamoto ya ofisi ya Katibu wa Bakwata Mkoa kuwa inapaswa kuboreshwa na kuwa na vitendea kazi kama kopyuta ili viweze kumrahisishia kazi badala ya kwenda kuchapa barua za ofisi kwenye maeneo nje na hivyo kutokuwa na siri ya mambo yao.
" Ni vema kila ofisi zetu kuanzia ngazi ya kata wilaya hadi mkoa zikawa na mfumo wa kompyuta na kuwa na wataalamu wakutengeneza hizo barua ambao ni mabinti zetu wasio na ajira na watakuwa wasiri kwa mambo yatakayokuwa yameandikwa ndani ya barua hizo." alisema Nassoro.
Mwenyekiti wa Bakwata Mkoa wa Singida, Jumanne Nkii alisema uongozi wa Mufti umenyooka lakini changamoto kubwa ipo kwa viongozi wa chini ambao wanaendesha dini yao kwa mazoea hawafuati miongozo ya qulaan, suna na katiba ya baraza kwani baadhi yao wamekuwa wakikurupuka na kujikuta wakiharibu kwa sababu ya tamaa zao.
"Sisi viongozi na waislamu wote kwa ujumla ni vizuri tuendeshe masuala yetu kwa kufuata kauli mbiu ya Mufti wetu isemayo Jitambue, Badilika Acha Mazoea." alisema Nkii.
Katibu wa Bakwata Mkoa wa Singida, Burhan Mlau aliipongeza Kata ya Mandewa kwa kuandaa baraza la Eid kwani kwa mkoa mzima hakuna walioandaa ila ni kata hiyo tu ambapo alimuomba Mwenyezi Mungu awajaalie.
MFUMO WA ANWANI NA POSTIKODI WATAMBULISHWA
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akimkabidhi Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Tina Sekambo wakati Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ikitambulisha programu tumizi ya simu za mkononi (Mobile Application) ya Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi kwa Wakurugenzi wa halmashauri na Makatibu Tawala wa mikoa katika Mkutano wa 11 wa TOA uliofanyika jijini, Dodoma.
Mkurugenzi Idara ya Mawasiliano wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Clarence Ichwekeleza akiwasilisha utekelezaji wa Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi wakati Wizara hiyo ikitambulisha programu tumizi ya simu za mkononi (Mobile Application) ya Mfumo huo kwa Wakurugenzi wa halmashauri na Makatibu Tawala wa mikoa katika Mkutano wa 11 wa TOA uliofanyika jijini, Dodoma.
Na Faraja Mpina, WMTH, Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula na timu yake ya wataalamu wametoa wasilisho la programu tumizi ya simu za mkononi (Mobile App) ya Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi pamoja na hatua iliyofikiwa ya usimikaji wa Mfumo huo nchini kwa Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Mikoa katika Mkutano wa 11 wa Maboresho ya Utendaji Kazi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa (TOA).
Akizungumza katika mkutano huo jijini Dodoma, Dkt. Chaula amesema kuwa Wizara hiyo inatekeleza ujenzi na usimikaji wa Mfumo huo kupitia Halmashauri zote nchini ambapo kwa mwaka wa fedha 2020/21 halmashauri 13 ziliingizwa kwenye mpango wa kusimikwa mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi.
Ameongeza kuwa mpango wa Wizara hiyo ni nyumba zote nchini ziwe na Anwani za Makazi ifikapo June 2022 na kuzipongeza halmashauri za mji wa Bukoba na Jiji la Mwanza kwa kuwa vinara wa utekelezaji wa Mfumo huo
“Ili kuongeza ufanisi wa matumizi ya Mfumo huu Wizara imetengeneza programu tumizi ya simu ya mkononi (mobile application) ambayo itawezesha kutambua na kuonesha nyumba ilipo au popote mwananchi anapotaka kwenda na pia utarahisisha shughuli za biashara”, alizungumza Dkt. Chaula
Akizungumzia mwongozo wa utekelezaji wa Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi, Dkt. Chaula amesema kuwa mwongozo huo umefanyiwa maboresho na utagawanywa kwa wadau kwa sababu utekelezaji wake unahusisha Wizara zaidi ya moja ikiwemo TAMISEMI na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,ambapo Ofisi ya Waziri Mkuu inaratibu kama Serikali na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ikiwa kama sekretarieti.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano wa Wizara hiyo ameizungumzia programu tumizi ya Mfumo huo kuwa na manufaa mengi kiuchumi na kijamii hasa katika dhana nzima ya uchumi wa kidijitali ambapo mfumo huo utarahisisha shughuli za kiuchumi kuweza kufanyika kidijitali.
Ameongeza kuwa chimbuko la mfumo huo ni Sera ya Taifa ya Posta inayoelekeza kuwa na Anwani ya Makazi ili kuweza kufikishiwa huduma mahali mwananchi alipo na kuongeza manufaa ya kijamii, kiuchumi na pia kimataifa ambapo nchi ya Tanzania ni mwanachama wa Umoja wa Posta Afrika.
Naye Mhandisi Jampyon Mbugi wa Wizara hiyo amezungumza na wajumbe wa Mkutano huo na kuwaomba kila mmoja kutimiza wajibu wake na kufanya kazi kwa ushirikiano ili kurahisisha zoezi zima la usimikaji wa majina ya barabara, mitaa na namba za nyumba pamoja na ukusanyaji wa taarifa za makazi.
Aidha, wataalamu wa programu tumizi ya mfumo huo waliitambulisha program hiyo kwa wajumbe wa kikao hicho na kuonesha namna ya kuingia katika program hiyo na jinsi ya kuitumia ambapo inaonesha njia na barabara ya kupita mpaka kufika mahali ambapo mtumiaji anataka kufika.
TAMUFO KUSHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA MAKUMBUSHO DUNIANI
UMOJA wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) unaratajia kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Makumbusho Duniani. Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa juzi Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stella Joel alisema tayari wanamuziki kadhaa wameonesha nia ya kuadhimisha siku hiyo. " Baadhi ya wanamuziki wameonesha nia ya kuhudhuria maadhimisho hayo ya makumbusho ya Taifa yatakayofanyika Mei 18, 2021." alisema Joel. Mlezi wa TAMUFO, Frank Richard alisema muziki ni sehemu katika Kuadhimisha Siku ya Makumbusho Duniani. " Muziki ni wa muhimu sana hasa katika kipindi hiki ambacho tunahamasisha uanzishwaji wa makumbusho mbalimbali hapa nchini zikiwemo za Wanamuziki kama mataifa mengine yaliyoendelea yanavyofanya. Richard alisema nchi nyingi duniani zina makumbusho mbalimbali zikiwemo za wanamuziki hivyo umefika wakati kwa wanamuziki wa Tanzania kupata elimu kuhusu makumbusho ili waweze kuzianzisha chini ya taratibu na sheria za nchi. |
Rais Samia Suluhu Hassan awasili Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Marubani pamoja na Wahudumu wa Ndege ya Shirika la Ndege la ATCL muda mfupi kabla ya kuondoka Zanzibar na kurejea Jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Mei, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Aboubakar Kunenge mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati akiwasili kutokea Zanzibar leo tarehe 17 Mei, 2021. PICHA NA IKULU.
Benki ya NMB kufungua fursa kwa wateja kupitia wiki ya ubunifu
Mkuu wa Kitengo cha Ubunifu wa Benki ya NMB, Josina Njambi akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi rasmi wa tamasha la Wiki ya Ubunifu (Innovation Week) iliyoanzishwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH) na wadau mbalimbali. Benki ya NMB ni mdhamini wa wiki hiyo ya ubunifu.
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya NMB imeazimia kufungua fursa zaidi kwa wateja wake kupitia huduma mbalimbali zinazoendana na mabadiliko ya kiteknolojia ili kurahisisha upatikanaji huduma.
Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya wiki ya ubunifu ambapo NMB ni sehemu ya wadhamini jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Ubunifu kutoka benki hiyo, Bi. Josina Njambi alisema lengo la kuwa sehemu ya tukio hilo ni kutaka kujivuta karibu zaidi na wadau wanaojihusisha na ubunifu.
Alisema, Benki ya NMB ni miongoni mwa benki kubwa nchini iliyokuwa ya mwanzoni kutumia ubunifu kuwapa wateja huduma wanazostahiki ikiwemo huduma ya NMB Mkononi.
“Tulipunguza mlolongo wa wateja kupanga foleni kwenye matawi yetu kwa kutoa huduma ya benki kwa simu za mkononi, tulipunguza mlolongo kwenye mashine za kutolea fedha (ATM) kwa kuanzisha NMB Wakala nchi nzima, huu ni ubunifu wa kipekee tuliopata kuufanya,” alisema Bi. Njambi.
Aidha, aliweka wazi kuwa kila siku wanafikiria namna ya kumthamini mteja wao kwa kuwa wabunifu zaidi, ambapo alieleza kuwa ubunifu unasaida vilevile kuongeza ajira kwa vijana na watanzania wote kwa ujumla kupitia utoaji huduma.
“Ndiyo maana tulitangaza shindano la kupata vijana watakaokuja na ubunifu wa kipekee kwenye huduma ya NMB Mkononi, ambapo tayari tumeshapata vijana 15 watakaoanza kuchuana kwa siku nne kuanzia kesho Jumanne hadi Ijumaa wiki hii. Mshindi atapata Shilingi Milioni 1. Tunachotaka ni kuona kikundi gani kitakuja na utaalamu wa kipekee kwenye ubunifu wa kupata app na huduma zingine za NMB zilizo kidijitaliii zaidi kwa manufaa ya wateja wetu ili wapate urahisi zaidi katika kufanya miamala popote walipo na wakati wowote,” alieleza Bi. Njambi.
Awali, katika tamasha la Wiki ya Ubunifu (Innovation Week) iliyoanzishwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (Tanzania Commission for Science and Technology - Costech) washiriki walieleza mambo mbalimbali juu ya safari yao katika ubunifu hasa vijana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Costech, Dk. Amos Nungu alisema awali wazo lilikuwa ndani ya tume hiyo lakini baadae wadau wakaamua liwe wazo la nchi nzima kwa kuwa kila kijana wa Kitanzania anahitaji kunufaika na ubuifu.
“”Tunafahamu kuwa kazi ya serikali ni kuweka mazingira wezeshi, sisi taasisi nyingine tunatakiwa kuzitumia fursa zinazoletwa na serikali kunufaika na kufanya mambo ya kiubunifu hasa katika zama hizi za Sayansi na Teknolojia,” alisema Dk. Nungu.
Aidha, mmoja wa watoa mada Dk. Flora Ismail Tibarazwa ambaye ni Mkurugenzi wa Programu ya Kusaidia Ubunifu kwa nchi za Ukanda wa Kusini: Southern African Innovation Support Programme (SAIS) alisema ubunifu ni miongoni mwa vyombo vinavyotoa suluhu ya tatizo la ajira duniani na hasa bara la Afrika.
“Uchumi unakua kupitia ubunifu, lakini pia unatoa suluhu ya tatizo la ajira na kujiajiri kwa vijana, wawekezaji pia wanapata uwanja mpana wa kusaidia jamii katika maeneo wanayotaka kuanzisha biashara zao,” alisema Dk. Tibarazwa.
Kwa mwaka huu tamasha hilo lenye kaulimbiu ‘Innovation for a Resilient and Inclusive Digital Economy’ ambapo kwa Kiswahili linasomeka: “Ubunifu kwa Uchumi wa Kidijitali Stahimilivu na Jumuishi” limetimiza miaka saba tangu liwe la kitaifa lakini pia limesaidia kufungua fursa nyingi kwa vijana.
RAIS SAMIA APOKEA RIPOTI YA TATHMINI YA UGONJWA WA CORONA
TBS YAWATAKA WATUMIAJI WA VIPIMO VYA AFYA KUVIHAKIKI UBORA

Afisa vipimo Mwandamizi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bw.Ramadhan Mfaume(Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuelekea Siku ya Vipimo Duniani yenye kauli mbiu "VIPIMO KATIKA SEKTA YA AFYA". Mkuu wa Maabara ya Vipimo (TBS), Bw.Joseph Mahila (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuelekea Siku ya Vipimo Duniani yenye kauli mbiu "VIPIMO KATIKA SEKTA YA AFYA".
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
******************************
NA EMMANUEL MBATILO
Kuelekea Siku ya Vipimo Duniani Mei 20,Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limewataka watumiaji wa Vipimo katika sekta ya afya nchini kuhakikisha vipimo hivyo vimepitishwa na Shirika hilo kabla havijatumika.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Afisa Vipimo Mwandamizi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bw.Ramadhan Mkumba amesema wamekuwa wakikutana na Changamoto kubwa ya watumiaji wa Vipimo kutokuwa na uwelewa wa kufanya uhakiki wa vifaa vyao ili kuboresha huduma wanazozitoa kwenye sekta za afya.
"Vipimo vinavyotumika katika sekta ya afya ni muhimu vikahakikiwa na kujulikana ubora wao kwa kufanya hivi itakuwa inalinda afya ya wagonjwa kwasababu daktari anaweza kufanya maamuzi kupitia vipimo vinavyotoka maabara vikiwa vipimo sio sahihi vinaweza kupelekea kumpatia madhara mgonjwa". Amesema Bw.Mfaume.
Aidha Bw.Mfaume amesema kuwa dhumuni la kauli mbiu ya mwaka huu ni kuleta uelewa katika jamii jinsi gani vipimo kwenye sekta ya afya vina umuhimu kama tunavyotambua vipimo katika sekta ya afya vinatumika kugundua, kutambua na kutibu magonjwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Maabara ya vipimo (TBS), Bw.Joseph Mahila amesema katika maadhimisho ya Siku ya Vipimo kwa mwaka huu watajikita zaidi katika sekta ya afya hasa kutokana na kauli mbiu ya mwaka huu "VIPIMO KATIKA SEKTA YA AFYA".
SERIKALI MBIONI KUTUNGA SHERIA YA KULINDA TAARIFA BINAFSI
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza wakati Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwasilisha taarifa kuhusu huduma za mawasiliano na intaneti kwa Wabunge Bungeni Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Seleman Kakoso.
Na Prisca Ulomi, WMTH
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt Faustine Ndugulile amesema kuwa Wizara yake iko mbioni kupeleka Bungeni muswada utakaowezesha kutungwa kwa Sheria ya Kulinda Taarifa Binafsi iili kulinda faragha na taarifa za mwananchi
Dkt. Ndugulile ameyasema hayo kwenye ukumbi wa Bunge, Dodoma wakati akijibu mijadala mbalimbali iliyotolewa na Wabunge kwenye semina iliyotolewa kwao kuhusu huduma za mawasiliano na intaneti ili waweze kufahamu namna Wizara inavyotekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na taasisi zilizochini yake
Ameongeza kuwa Wizara inaandaa sheria hiyo ili kulinda faragha na taarifa binafsi za wananchi katika hatua ya ukusanyaji wa taarifa, usafirishaji, matumizi na utunzaji wa taarifa hizo kwa kuwa taasisi mbalimbali zinatumia taarifa husika hivyo amewataka Wabunge kuwa tayari pindi pendekezo la muswada litakapowasilishwa Bungeni ili sheria hiyo iweze kutungwa kwa maslahi mapana ya taifa
“Hivi sasa ujambazi umehama kutoka silaha za mkononi na kuhamia mtandaoni, Serikali itaendelea kuelimisha wananchi, kuboresha mifumo na teknolojia ili nchi iwe mbele zaidi katika kudhibiti uhalifu mtandaoni,” amesisitiza Dkt. Ndugulile
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Seleman Kakosoameishauri Serikali iongezee fedha za kuuwezesha Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kutoa ruzuku ya kutosha kwa kampuni za simu ili mawasiliano yafike kwa wananchi wote ikiwemo kuongeza usikivu wa redio kwenye maeneo ya mipakani
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Akson aliipongeza Wizara kwa kuleta semina hiyo kwa Wabunge na anatamani katika kipindi kifupi Wabunge wasizungumzie changamoto ya mawasiliano katika maeneo yao kwa kuwa mawasiliano ni huduma ya msingi kama ilivyo maji, barabara
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA), Dkt. Jabir Kuwe amesema kuwa nchi inaelekea kutumia huduma ya 5G na majaribio yatafanyika ili kuhakikisha kasi ya teknolojia inayotakiwa inapatikana ili kuongeza huduma ya mawasiliano ya data nchini