Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano (UTT AMIS), Daudi Mbaga akitoa mafunzo kwa wafanyakazi wapya wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS juu ya Uwekezaji wa Pamoja mkoani Morogoro.
UTT AMIS YATOA MAFUNZO KWA WAFANYAKAZI WA TANROADS
Milioni 500 kukusanywa mbio za 'CRDB Bank Marathon 2021'
kusaidia upasuaji wa moyo kwa watoto na ujenzi wa kituo cha mawasiliano Taasisi ya Saratani Ocean Road
Dar es Salaam, Tanzania
Benki ya CRDB imetangaza kusajiliwa kimataifa kwa mbio zake za hisani za “CRDB Bank Marathon” ambazo zilizinduliwa mwaka jana kwa kauli mbiu ya “Kasi Isambazayo Tabasamu,” zikilenga kuhamasisha kuchangia maendeleo na kusaidia wenye uhitaji katika jamii.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa msimu mpya wa CRDB Bank Marathon 2021, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa amesema mapema mwaka huu mbio hizo zilipewa usajili wa kimataifa na Chama cha Usajili na Upimaji wa Mbio za Kimataifa (AMIS) kwa kushirikiana na Shirikisho la Kimataifa la Mchezo wa Riadha (World Athletics)
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa, akizungumza wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa CRDB Bank Marathon 2021.
“Ninafuraha kuwajulisha kuwa mafanikio ambayo tuliyapata mwaka jana yamefungua milango kwa CRDB Bank Marathon kutambuliwa na kupata usajili wa kimataifa. Usajili huu wa kimataifa sio tu unakwenda kupanua wigo wa kusambaza tabasamu, lakini pia unafungua fursa za kibiashara kwa Watanzania kwani tunarajia wakimbiaji wengi wa kimataifa kujumuika nasi,” aliongezea Tully huku akibainisha kuwa usajili huo wa kimataifa pia utasaidia kuitangaza Tanzania kimataifa.
Akielezea kuhusiana na msimu wa CRDB Bank Marathon 2021, Tully alisema lengo la mwaka huu ni kukusanya shilingi milioni 500 kusaidia gharama za upasuaji kwa watoto wenye matatizo ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI). Alisema pamoja na kuendelea kusaidia eneo hilo, sehemu ya fedha itakayo kusanywa itapelekwa kusaidia ujenzi wa Kituo cha Huduma kwa Wateja “Call Centre” kwa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.
Kaimu Katibu Mkuu Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Ombeni Zavalla, akizungumza katika uzinduzi huo.
“Kama mnavyofahamu magonjwa ya saratani ni moja ya changamoto ambazo zinakiabili jamii yetu. Ili kupambana nayo na kupunguza tatizo tunahitaji kutoa elimu ya kutosha na kurahisisha utaratibu wa kukutana na madaktari na kupata huduma. Kituo hiki kitakwenda kurahisisha yote haya,” alisisitiza Tully.
Akizungumzia namna ya kushiriki mbio hizo ambazo zinatarajiwa kufanyika tarehe 15 Agosti 2021, Tully alisema dirisha la usajili kwa wakimbiaji litafunguliwa siku ya jumamosi ya tarehe 15 Mei 2021 ambapo watu binafsi au vikundi wataweza kusijajili kushiriki kupitia tovuti maalum ya mbio hizo ya www.crdbbankmarathon.co.tz .
Makamu wa Rais wa Chama cha Baiskeli Tanzania, Hussein Ali, akizungumzia namna watakavyoshitiki katika mbio hizo.
“Kujisali na kuchangia mbio hizi kwa binafsi ni shilingi 30,000 au kupitia vikundi ni 25,000. Malipo yanaweza kufanyika kupitia matawi ya Benki ya CRDB, CRDB Wakala, SimBanking App, mitandao ya simu na kupitia kadi ambazo zinawawezesha hadi watu wa nje ya nchi kufanya malipo,” alisema Tully huku akisisitiza kuwa fedha hizi zote zitaelekezwa katika kusaidia gharama za upasuaji wa watoto wenye magonjwa ya moyo na ujenzi wa Kituo cha Huduma kwa Wateja kwa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.
Aidha mkurugenzi huyo aliwahamasisha Watanzania wote kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio hizo huku akibainisha kuwa safari hii mbio hizo zinajumuisha km 42.2, km 21.1, km 10, km 5 na mbio za baiskeli za km 65.
GOODWILL YAWAKARIBISHA WATANZANIA KUTUMIA BIDHAA ZAKE
Kiwanda cha kuzalisha vigae cha Goodwill Tanzania Ceramic Company Limited kimewakaribisha watanzania kutumia bidhaa zake kwa ajili ya ujenzi wa nyumba kwa kuwa bidhaa zake ni bora.
Akizungumza katika ziara ya waandaaji wa kipindi maalum kinachoangazia mchango wa madini ujenzi na madini ya viwanda kwenye Sekta ya Madini kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wakiongozwa na Meneja Habari na Mawasiliano wa Tume ya Madini, Greyson Mwase, leo tarehe 10 Mei, 2021 Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani, Meneja Rasilimaliwatu wa kiwanda hicho Jerry Marandu amesema kuwa kiwanda kimekuwa kikizalisha bidhaa zenye ubora wa hali ya juu kwa ujenzi wa nyumba.
Amesema kuwa kiwanda hicho kimeweka mikakati ya kutoa ajira kwa watanzania zaidi ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wa kuzalisha bidhaa bora kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
Akielezea manufaa ya kiwanda hicho, Marandu amesema kuwa ni pamoja na kununua malighafi kutoka katika mikoa ya Lindi, Morogoro, Pwani, na Dodoma kwa asilimia 96 huku asilimia 4 ya malighafi ikitokea China.
Amesema kuwa manufaa mengine ni pamoja na kutoa ajira kwa watanzania wengi huku wakiendelea kulipa kodi mbalimbali Serikalini.
Ametaja manufaa mengine kuwa ni pamoja na uboreshaji wa huduma za jamii ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Mkiu, Kituo cha Huduma cha Mkuranga ambapo wamejenga wodi ya wazazi na ujenzi wa kituo cha polisi Mkuranga.
Naye Meneja Masoko wa kiwanda hicho, Salum Zuberi akielezea mwenendo wa soko la vigae vinavyozalishwa na kiwanda hicho amesema kuwa wamekuwa wakiuza bidhaa nchini Tanzania na katika nchi nyingine jirani za Afrika Mashariki na Afrika ya Kati.
Naye Mkaguzi wa Madini katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, Muhsin Mustapha akielezea namna Serikali inavyokusanya mapato kutokana na uwepo wa kiwanda hicho amesema kuwa wamekuwa wakisimamia kwa karibu kwa kuangalia mwenendo mzima wa malighafi zinazoingizwa katika kiwanda hicho na kuhakikisha kunakuwepo na nyaraka zote zinazohitajika kisheria.
SERIKALI YAJA NA ELIMU MBADALA KWA WANAFUNZI WANAOPATA MIMBA SHULENI

Waziri wa Serikali ya Uingereza anayeshugulika na mambo ya Afrika, James Duddridge (katikati), akipata maelezo wakati alipofanya ziara katika Shule ya Sekondari Kibasila jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2021. Kulia ni Balozi wa Uingereza nchini, David Concar na wapili kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako.
Waziri wa Serikali ya Uingereza anayeshugulika na mambo ya Afrika, James Duddridge akizungumza na wanafunzi wa kidato cha tano Shule ya Sekondari Kibasila jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2021.
Waziri wa Serikali ya Uingereza anayeshugulika na mambo ya Afrika, James Duddridge, akipata maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa kidato cha tatu Shule ya Sekondari Kibasila, Asha Shabani, alipotembelea maabara ya shule hiyo jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2021. Katikati ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako.
Balozi wa Uingereza nchini, David Concar (kushoto), akifafanua jambo wakati wa ziara ya kutembelea Shule ya Sekondari Kibasila Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuja na mpango wa Elimu mbadala kwa wanafunzi wa kike wanaopata mimba wakiwa shuleni kupata fursa ya kurudi na kuendelea na Masomo.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako wakati wa ziara ya Waziri wa Serikali ya Uingereza anayeshugulika na Mambo ya Afrika James Duddridge, katika Shule ya Sekondari Kibasila jijini Dar es Salaam.
Waziri Ndalichako alisema Serikali imejipanga kuhakikisha wanafunzi wanaokatisha masomo yao kwa kupata mimba wakati wa masomo kurejea na kuendelea na masomo kwa mfumo wa Elimu mbadala.
"Tumeweka utaratibu kwa watoto ambao wanapata ujauzito kuendelea na masomo yao kupitia njia ya Elimu mbadala ambapo katika mfumo huo, inategemea ameacha Shule akiwa kidato gani ama darasa gani kwa mfano ameacha akiwa kidato cha kwanza anaweza akasomo kupitia mfumo wa Elimu mbadala akifika kidato cha pili akafanya mtihani akafaulu anaweza kurudi katika mfumo wa kawaida.
"Vilevila yule ambae labda anakuwa ameacha akiwa kidato cha tatu akifanya mtihani wake kupitia mfumo usio rasmi akafaulu mtihani wa kidato cha nne anapata nafasi fursa sawa kama yule ambaye amekuwa shuleni kupangiwa shule yoyote kulingana na ufaulu wake." Alisema Waziri na kuongeza kuwa.
"Kwa hiyo tutaendelea kuhakikisha tunasimamia Elimu kwa watoto wa kike na kuondoa vikwanzo ambavyo vinasababisha watoto wa kike wasifanye vizuri katika masomo yao sambamba na kuboresha Elimu kwa ujumla kwa watoto wa kike na wakiume ili wapate Elimu bora.
Akizungumzia ziara ya Waziri wa Serikali ya Uingereza anayeshugulika na Mambo ya Afrika Prof. Ndalichako alisema Waziri huyo amekuja nchini kuangalia mambo mbalimbali huku akibainisha kuwa amemleta mwaliko wa kuhudhuria mkutano unaohusiana na Ushirikiano katika Elimu.
"Katika mkutano huo mambo yatakayo zungumziwa ni pamoja na namna ambavyo nchi zinahakikisha zinatekeleza jukumu lake la msingi la kutoa elimu iliyo bora kwa wananchi wake lakini pia na kuangalia zaidi elimu kwa mtoto wa kike.
"Na amekuwa anapenda kufahamu jinsi ambavyo kama nchi timepiga hatua au ni hatua gani ambazo tunachukua kuhakikisha kwamba mtoto wa kike anapata elimu iliyo bora. Kwa hiyo niseme kwanza Uingereza ni nchi ambayo tumekuwa tunashirikiana nayo vizuri kwenye sekta ya Elimu.
Kwa upande wa Waziri wa Serikali ya Uingereza anayeshugulika na Mambo ya Afrika James Duddridge aliipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada zake za kuboresha mazingira ya Elimu kwa watoto wa kike.
"Niko hapa kuangalia malemgo na mikakati ya Elimu jinsi gani inaboreka ama tunaiboreha na kufikia viwango vya juu, tukiwa tunatambua hapa Tanzania kuna mfumo wa Elimu bure.
"Asubuhi ya leo (jana) nimeonana na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na kujadili jinsi gani mpango wa Elimu unaenda kuboreka pamoja na kuajiri walimu wapya, lakini pia nimemualika Waziri wa Elimu katika Mkutano ambao utajadili masuala mbalimbali katika mashirikiano kwenye sekta ya Elimu ili kusaidia kuondoa changamoto zinazoikumba sekta ya hiyo."alisema Duddridge.
Waziri huyo anaendelea na ziara yake ya siku mbili ambapo ataimalizia Zanzibar ambako atakutana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi kuzungumzia masuala mabalimbali ya kimaendeleo na mashirikiano.
INTERNET IWE CHANZO CHA MAENDELEO
TBS YATOA ELIMU YA VIWANGO KWA WANAFUNZI , WANANCHI WILAYANI KILOSA NA MKINGA




Maafisa wa TBS wakitoa elimu kwa wanafunzi wa shule za Sekondari na MsingiWanafunzi hao waliahidi kuwa mabalozi na kufurahishwa na hatua ya TBS kuona umuhimu wa kuwafikia kwani vita ya bidhaa hafifu ni ya wananchi wote na si TBS pekee.
Mkaguzi wa TBS Bw.Venance Colman akitoa elimu katika stendi ya Horohoro na soko la Duga lililopo wilayani Mkinga Mkoa wa Tanga.Wananchi hao walifurahishwa na kuishukuru TBS kwa kuwafikia na kutoa elimu itakayowasaidia kuokoa fedha na kuepuka madhara yatokanayo na bidhaa hafifu kwa kununua bidhaa zilizokidhi matakwa ya viwango.
************************************
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
WANAFUNZI wa shule za Msingi na Sekondari na wananchi wanaoendesha shughuli zao kwenye maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu, kama stendi, kwenye masoko, minada,magulio katika maeneo mbalimbali ya Wilaya za Kilosa, mkoani Morogoro na Mkinga, mkoani Tanga wamepewa elimu kuhusiana na umuhimu wa kutumia bidhaa zilizothibitishwa ubora na kusajiliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) .
Kampeni hiyo ya elimu kwa umma ilianza kutolewa maeneo mbalimbali ya Wilaya za Kilosa na Mkinga na maofisa wa TBS kuanzia Mei 4 hadi 10, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Afisa Uhusiano wa TBS, Neema Mtemvu, alisema kitu kikubwa ambacho wamekifanya ni kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari juu ya umuhimu wa kutumia bidhaa zilizothibitishwa na kusajiliwa na TBS, ikiwa ni pamoja na kuwapa namba ya mawasiliano kwa ajili ya kupiga bure kuwasiliana na shirika hilo pindi ikitokea wakapata matatizo au changamoto kwenye bidhaa.
Alisema wamefikisha elimu hiyo kwa wanafunzi kwa kutambua kwamba wataenda kuwa mabalozi wazuri kwa wazazi na walezi kuhusiana na umuhimu wa kutumia bidhaa zilizothibitishwa na TBS.
Kwa upande wa maeneo yenye mikusanyiko ya watu, Mtemvu alisema elimu hiyo imetolewa Mkinga katika Stendi ya Hororo na gulio la Duga, huku kwa upande wa Kilosa elimu hiyo ikitolewa Uhindini, Sabasaba na Kimamba.
Kuhusu mwitikio wa wananchi katika maeneo hayo yenye mikusanyiko ya watu, Mtemvu alisema wengi wamefurahishwa na elimu hiyo na wameomba iwe endelevu .
"Wananchi wameshukuru shirika kwa kuona umuhimu wa kuwapatia taarifa hizo kuhusu viwango kwa sababu wamekuwa wakipata changamoto kubwa, lakini walikuwa hawajui wafanyeje.
Lakini kwa sasa na wenyewe wameahidi kuingia kwenye vita ya bidhaa hafifu kwa sababu wana uwezo wa kuwasiliana na TBS, kwani wanajua tupo," alifafanua Mtemvu.
Alisema miongoni mwa mambo walioelimishwa wananchi hao kupitia kampeni hiyo ni pamoja na majukumu ya TBS, umuhimu ya kuangalia tarehe ya mwisho ya matumizi ya bidhaa wanazotaka kununua, ambapo taarifa hizo zinapatikana kwenye vifungashio.
Eneo lingine ambalo wananchi hao walielimishwa ni umuhimu wa wao kununua bidhaa zilizothibitishwa na kusajiliwa na TBS. Mtemvu alitaja baadhi ya faida za kununua bidhaa zilizothibitishwa na shirika hilo kuwa ni pamoja na kulinda afya zao na thamani za fedha zao.
Alisema mtu anaponunua bidhaa ambazo zimethibitishwa na TBS anakuwa na uhakika na bidhaa anazozitumia. Kwa sasa maofisa hao wanaendelea kutoa elimu hiyo wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.
NTD IMEJIPANGA KUTOKOMEZA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE IFIKAPO 2030
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi wa Halmashauri,Waganga Wakuu wa Wilaya na Waratibu wa NTD na wa Afya Idara ya elimu wakiwa Kwenye kikao kazi hicho.
Afisa Mradi wa NTD, Isaac Njau, akionesha Kingatiba ya kichocho 'Praziquantel' ambazo zoezi la umezaji unatarajia kuanza mwishoni mwa mwezi huu mkoani Kigoma.
Na Jasmine Shamwepu, Kigoma
Mpango wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele (NTD) una lengo la kuhakikisha jamii yote ya watanzania wameondokana na athari za magonjwa hayo ifikapo mwaka 2030 ambapo Tanzania kampeni ya kudhibiti magonjwa hayo yalianza mwaka 2009.
Hayo yamebainishwa leo na Mratibu wa taifa wa Mpango huo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. George Kabona wakati wa kikao kazi cha uraghibishaji na uhamasishaji kwa viongozi wa mkoa, wilaya na halmashauri za mkoa wa kigoma.
Dkt. Kabona amesema kuwa kati ya magonjwa 13 ambayo Mpango huo wanapambana nayo,magonjwa matano ya Usubi, Takoma, Matende na Mabusha, Kichocho na Minyoo ya Tumbo yamepewa kipaumbele katika utekelezaji wa shughuli za kuyadhibiti na kwa maana hiyo yanatakiwa kudhibitiwa mapema kwa njia ya kugawa kingatiba ngazi ya jamii pamoja na watoto mashuleni.
“Kwa kupitia takwimu zilizopom Shirika la Afya duniani(WHO) liligundua kwamba magonjwa Yaliyokuwa hayapewi kipaumbele yameathiri sana jamii kwa kiasi kikubwa na takribani watu wapatao bilioni 2 walikuwa kwenye hatari ya kupata madhara ya magonjwa haya na hatimaye kuishi maisha ambayo watashindwa kuzalisha mali na kuwa mzigo kwa jamii hivyo ikaja na mpango mkakati wa kupambana na kudhibiti magonjwa hayo”.
Dkt. Kabona alitaja mafanikio yaliyopatikana kupitia mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa hayo kuwa ni pamoja na ugawaji wa kingatiba kwa magonjwa yote matano kufanyika katika maeneo yote nchini kwa asilimia 100. “Kwa upande wa Matende naMabusha kati ya halmashauri 119 zilizokuwa zimeathirika hadi kufikia mwaka huu ni halmshauri 7 tu ndio bado zimebaki na tatizo hilo na kama Wizara wanaimarisha mkakati wa kumaliza kabisa tatizo hilo”.
Kwa upande wa ugonjwa wa Trakoma (Vikope) amesema kulikuwa na halmashauri 71 zilizoathirika na kwa sasa zimebaki halmshauri sita tu ambazo kati ya hizo halmashauri mbili za Kongwa na Chamwino ugonjwa umerudi baada ya kufaulu kupunguza maambukizi miaka miwili iliyopita na kufuatia kurudi huko kwa ugonjwa hivyo wanaendelea kufuatilia sababu zake kwa kufanya tafiti za kiutendaji na taarifa itatolewa hivi karibuni.
Hata hivyo Dkt. kabona aliwataka wananchi kujenga tabia ya kufanya usafi wa uso ,matumizi wa vyoo pamoja na usafi wa mazingira kwa dhumuni la kuzuia mazalia ya inzi ili kuweza kujikinga na ugonjwa wa trakoma
Amesema pia Ugonjwa wa Kichocho na minyoo ya tumbo umeathiri halmashauri zote 184 kwa kiwango tofauti tofauti. Dr Kabona ameongeza kwa kusema kuwa zipo athari za magonjwa hayo ambazo husababisha utegemezi kwa jamii na kusababisha ndugu wa karibu kushindwa kuzalisha mali kwa sababu ya kutumia muda mwingi na rasilimali kuwahudumia wagonjwa wao.
Amesema pia kuwa toka mwaka 2008 Mpango umeweza kutoa huduma ya upasuaji wa Mabusha kwa wagonjwa zaidi ya 6000 na huduma hiyo bado inahitajika kwa kiwango kikubwa hasa mikoa na halmashauri za ukanda wa Pwani
kwa ajili ya kuzuia mazalia ya Inzi na hatimaye kutokomeza kabisa magonjwa hayo .
Awali akifungua kikao kazi hicho Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ambaye ni Katibu Tawala wa mkoa huo Bw. Rashid Mchatta amesema kila halmashauri zinatakiwa kufikia malengo ya asilimia 80 ya umezeshaji kingatiba hizo na kuwataka viongozi wa mkoa, wilaya na halmashauri kushirikiana kwa kubadilishana mawazo jinsi ya kutatua changamoto ili kila mmoja aweze kuwafikia watoto wote waliolengwa kwa kutoa elimu kwa jamii na kuhamasisha wazazi na walezi.
TCRA: Kila mtu aweke ‘password’ simu yake
NA HAMIDA RAMADHANI, MOROGORO
MAMALAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema, ujio wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), umeleta mabadiliko makubwa katika tasnia ya habari bila kusahau haki za msingi za binadamu.
Pia, TCRA imewataka wananchi wote, kuhakikisha wanaweka nywila ‘password’ kwenye simu zao na kutokubali kumwonyesha mwenzaa wake kwani ni hatari.
Hayo yamebainishwa leo Jumanne, tarehe 11 Mei 2021 na Dk. Philip Filikunjombe, Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi na Utekelezaji wa Sheria wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Alikuwa akiwasilisha mada katika semina ya kuwajengea uwezo waandishi na wahariri wa habari wa mtandaoni, mkoani Morogoro, iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC).
Dk. Filikunjombe amesema, Tehama imeleta mabadiliko katika dunia ya sasa ambapo, dunia imekuwa kijiji kwa kuongeza kwa watumishi wa mtandao huku kasi ya mtandao kuwa ya kasi kubwa.
"Ni ukweli usiopingika, tumetoka kwenye matumizi ya kizamani na sasa tupo katika mitandao ya kijamii ambapo huko tunapata habari zetu kwa rahisi na haraka zaidi," amesema Dk. Filikunjombe.
Aidha ametoa rai kwa watumishi wa mawasiliano kwanjia ya mtandao kuweka nywila (Password) ikiwemo kwenye simu zao, ili taarifa zao ziwe na usiri ili kuepuka wadukuzi.
Amesema, suala la kuweka nywila, haijalishi kama uko kwenye mahusiano ikiwemo ndao kwani Kanuni za Maudhui ya Mtandaoni za mwaka 2020, zinataka kila mmoja awe na nywila yake mwenyewe pasina mtu mwingine kuijua.
Dk. Filikunjombe amesema, kutokana na mjadala wa uwepo wa wadau mbalimbali kutaka maboresho ya kanuni hizo hivyo, TCRA imeanza kupokea maoni ya wadau ili ziweze kuboreshwa.
Amesmea, kila mmoja, ajitokeze kutoa maoni yake kwa kuangalia ni eneo gani linahitaji maboresho zaidi yatakayozifanya kanuni hizo kuwa rafiki kwa watumiaji wote.
Wafanyabiashara, Wajasiriamali na Mamalaka za Mitaa wahamasishwa kushiriki Maonesho ya SabaSaba
Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo.
Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Wandishi wanakumbwa na vitisho na manyanyaso kazini
Jaji mstaafu Justice Makaramba.
NA HAMIDA RAMADHANI
JAJI Mstaafu Justice Makaramba amesema, wanahabari wengi wamekuwa wakikumbwa na vitisho na manyanyaso pindi wanapokuwa katika majukumu ya kila siku kazini.
Pia, amesema kumekuwa na kasumba nyingine ya waandishi wa habari kesi zao kutofatiliwa mahakamani kwa dhana ya kuwashitaki watu wasio julikana.
Amebainisha hayo leo Jumatano, tarehe 12 Mei 2021 na Jaji Makaramba wakati akiwasilisha mada ya mifumo ya kikanda na kimataifa ya kuhakikisha usalama wa wanahabari katika mafunzo yalioandaliwa na Mtandao wa Utetezi wa haki za binadamu Tanzania THRDC Mkoani Morogoro.
Aidha ameyataja matukio mabaya yanayowakumba waandishi kuwa ni pamoja na kuuawa, kutekwanyara, kupotea, kuwekea kizuizini huku akisisitiza matukio hayo huwakumba waandishi wanaoandika habari hususan za uchunguzi au kuigusa hasa serikali.
Hata hivyo, amesema kwa Mujibu wa Takwimu ilizotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), zinasema kuanzia mwaka 2018 mpaka 2019 kulikuwa na matukio 156 ya kuuawa kwa waandishi duniani.
"Hii inamaanisha kila ndani ya siku nne, mauaji ya mwandishi yanatokea na mauaji mengi yamekuwa yakitokea kwenye nchi ambazo hazina vita, nchi ambazo zimejaa na amani na utulivu wa kutosha," amesema Jaji Mstaafu Makaramba.
Jaji huyo amesema, kazi ya mwandishi ni pamoja na kuihabarisha jamii kuhusu masuala mbalimbali.
SABABU 3 ZA KWANINI WAANDISHI KUWA SALAMA.
Jiji Mkaramba amezitaja kuwa
1: Ili aweze kufanya kazi yake kwa weledi,
2: Tasnia ya habari isiwe hatarini, waandishi wa habari wakiuawa na Watu wasiadhibiwe kila mtu atogopa kuwa mwanahabari
3: Wasijulikane, kwani kunaweza kuwaweka katika hatari.
Hata hivyo, amesema ili kuzuia majanga hatari yanayowakumba waandishi, ni pamoja na kuwepo kwa mifumo ya kudai haki za binadamu kuanzia ngazi ya Kimataifa na Kikanda ili haki za waandishi wa habari ziweze kupatikana.
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AIPONGEZA PSSSF KUFANIKISHA MAONESHO YA MAKISATU
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya Pamoja na wadau waliofanikisha maonesho hayo.
China yaipatia Tanzania msaada wa Bil 35/-
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Emmanuel Tutuba (kulia) na Balozi wa China, Wan Ke (kushoto), wakisaini Mkataba wa msaada wa kiasi cha Sh. Bilioni 35.37 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini, Jijini Dar es Salaam.
NA BENNY MWAIPAJA, DAR ES SALAAM
Machinjio Tabora yamkera Waziri Jafo
Rais Samia Suluhu Hassan ahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni nchini Uganda
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Kololo, kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni zilizofanyika katika uwanja huo uliopo Kampala nchini Uganda leo tarehe 12 Mei, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati Wimbo ya Taifa la Uganda ukipigwa mara baada ya Uapisho wa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni uliofanyika katika Uwanja wa Kololo, Kampala nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Marais wengine wa Nchi za Kiafrika pamoja na Wageni wengine waliohudhuria sherehe za Uapisho wa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni zilizofanyika katika Uwanja wa Kololo, Kampala nchini Uganda.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika uwanja wa Kololo Kampala nchini Uganda katika sherehe za Uapisho wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
MBUNGE WA KIBAHA MJINI ATEMBELEA NYUMBA MBILI ZILIZOUNGUA NA MOTO ACHANGIA FEDHA KWA WAHANGA
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka, akimfariji mmoja wa mtoto aliyebebwa na mama yake baada ya kunususirika kupoteza maisha baada ya nyumba yao waliyokuwa wakiishi kuungua kwa moto na kuteketeza mali zote.
Mmoja wa wahanga wa tukio la janga la moto akikabidhiwa msaada wa fedha kutoka kwa Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka ambaye alifunga safari kwa ajilli ya kwenda kuzitembelea familia zilizopatwa janga hilo.
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
KAYA zipatazo sita zimenusurika kupoteza maisha katika eneo la mitaa miwili ya Muharakani na Mkuza Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani baada ya nyumba zao walizokuwa wakiishi kupata janga la kuunguliwa na moto na kusababisha uharibifu mkubwa ambao umepelekea kuteketea kwa mali zao zote huku wakiwa katika hali ya sintofahamu kutokana na kukosa makazi ya kuishi.
Kufuatia tukio hilo Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Silvestry Koka, ametembelea katika eneo la tukio akiwa ameambatana na baadhi ya vongozi wa serikali pamoja na viongozi wa Chama na kujionea uharibufu ambao umejitokeza ambapo amewafariji wahanga waliounguliwa na nyumba zao kwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni 1.2 ambazo zitaweza kuwasaidia kujikimu katika kipindi hiki kigumu walichonacho.
Koka alibainishwa kwamba amesikitishwa sana na tukio hilo la moto ambalo limeweza kuwafanya baadhi ya wananchi ambao walikuwa wanaishi katika nyumba hizo kuishi katika mazingira ambayo sio rafiki ndio maana akaamua kuacha mambo mengine kwa ajili ya kwenda kuwafariji wahanga hao ambao kwa kweli mali zao zote zimetekea kwa moto na mimi nitaendelea kuwapa sapoti kadiri ya uwezo wangu.
“Mimi kama Mbunge wenu wa Jimbo la Kibaha mjini tukio hilo la wananchi wangu kupatwa na janga la moto limenishitua sana na kwamba nilipatiwa taarifa hizi wakati nipo katika vikao mbali mbali vya Bunge lakini kutokan na hali jinsi ilivyo na wananchi wamepoteza mali zo na kuunguliwa na vitu mbali mbali imelazimu sasa niache shughuli zingine ili nije nije kuangalia hali halisi ya tukioa na nimeweza kuona hivyo nimechangia kiasi cha shilingi milioni 1.2 na huu ni mwanzo tuu,’alisema Koka.
Aidha Mbunge huyo alisema kwamba licha ya kwamba familia hizo zipo katika wakati mgumu wa kupata janga la kuunguliwa na nyumba zao ataendelea kushirikian nao bega kwa bega katika kipindi chote cha tatizo hili kwani pamoja na kutoa fedha hizo lakini bado kuna michango mingine ambayo inahitajika ili wananchi hao waweze kurejea katika hali yao ya kawaida.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wa Mtaa wa Muharakani alibainisha kwamba majirani waliweza kufanya jihihada zote kwa ajili ya kuuzima moto huo ili kuokoa mali zilizokuwa ndali lakini walishindwa kufanikiwa na kusababisha mali zote kuteketea na moto huku akibainisha hakuna mtu yoyote aliyepoteza maisha kwani waliwahi kutoka nje.
“Mheshimiwa Mbunge kwanza sisi kama wananchi wako tumefarijika sana kwa ujio wako maana kwa kweli hizi kaya kwa sasa zipo katika mazingira magumu lakini msaada wako huu utaweza kusaidia kununua mahitaji mbali mbali amabyo ni muhimu maana siku ya tukio tulijitahidi kupambana kuokoa mali lakini tulishindwa kabisa na gari la zima moto pindi lilipofika tayari vitu vyote vilikuwa vimeteketea,”alibainisha Mwenyekiti.
Nao baadhi ya wahanga wa janga hilo la moto hawakusita kumpongeza Mbunge huyo wa Jimbo la Kibaha mjini kwa kuamua kuacha vikao vinavyoendelea Bungeni na kwenda kuwafariji pamoja na kuwapatia msaada wa fedha ambazo zitaweza kuwasaidia katika baadhi y mahitaji muhimu na kuiomba serikali na wadau wengine kuwasaidia msaada wa hali na mali ili waweze kijikimu kimaisha.
“Kwanza kabisa tunapenda kutoa shukrani zetu za kipekee kwa baba yetu ambaye ni Mbunge wetu wa Jimbo la Kibaha mjini Koka kwani ni viongozi wachache sana ambao wana moyo kama wake kwani ameweza kuacha shughuli zake mbali mbali ikiwmeo vikao vya Bunge ili kuweza kuja kutufariji na kutupa msaada huu hivyo tunamshukuru sana Mbunge wetu”alisema wahanga hao.
Pia aliongeza kuwa pamoja na kupatiwa msaada huo lakini kutokana na ukubwa wa tukio hilo wamesema kwamba bado wahahitaji msaasa wa vitu mbali mbali ikiwemo nguo, vyakula, pamoja na mahitaji mengine na kuimba serikali kuiliangalia zaidi jambo hili kwa jicho la tatu kwa lengo la kuwasaidia katika jambo hilo ambalo limewafanya waweze kurudi nyuma katika kutimiza malengo yao.
Tukio hilo la janga la moto limetokea hivi karibuni katika mtaa wa Muhazakani pamoja na mtaa wa mkuza Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani na kusababisha nyumba mbili kuungua na kaya sita kukosa makazi ya kuishi kutokana na mali zote zilizokuwemo ndani kuteketea kwa moto na kwamba inadaiwa chanzo cha moto huo ni itirafu ya umeme.
Jafo: Nunueni tumbaku iliyokaushwa kupitia mabani ya kisasa
SABAYA AWEKWA KANDO KUPISHA UCHUNGUZI
TANZANIA KINARA KWA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI NCHI ZA KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Amos Maganga (kushoto kwa Mwenyekiti), wakicheza pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Nishati na REA, kufurahia uzinduzi wa Mradi wa Usambazaji Umeme katika kila Kitongoji nchini, uliofanyika katika Kitongoji na Kijiji cha Ufuruma, wilayani Uyui, Mkoa wa Tabora.
Transfoma ikiwa imesimikwa katika kijiji cha Ufuruma, wilayani Uyui ikiwa ni utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini unaofanywa na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini nchini kote.
Na Dotto Mwaibale
TANZANIA ni kinara kwa usambazaji umeme vijijini katika nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Amos Maganga wakati akizungumza katika kipindi maalumu cha Mizani kinachorushwa na Runinga ya Taifa (TBC).
Akizungumzia dhima, alisema taasisi hiyo ya Serikali ilianzishwa kwa sheria namba 8 ya mwaka 2005 ambayo ilitoa madhumuni ya kuanzishwa wakala huo ili kuwezesha upatikanaji wa nishati hiyo vijijini, ikiwa ni pamoja na kutunza mazingira kutokana na nishati ya kuni iliyokuwa inatumika kutokuwa rafiki kwa mazingira.
"Lengo kuu la utunzaji mazingira hayo kwa kutumia nishati hiyo ya umeme ilikuwa ni kuyatunza vizuri ili dunia iwe mahali pazuri pa kuishi," alisema Mhandisi Maganga.
Alisema utekelezaji rasmi wa sheria hiyo ulianza Mwaka 2008 licha ya kuwa miradi hiyo ilianza Mwaka 2007 ambapo vijiji 518 kwa Tanzania nzima vilianza kupata huduma ya umeme kati ya vijiji 12,268 na kufikia mwaka huu 2021 takribani vijiji 10,400 vimekwisha pata umeme sawa na asilimia 84.
"Juhudi kubwa zilifanyika toka Mwaka 2008 hadi sasa zaidi ya vijiji 10,400 sawa na asilimia 84 kati ya vijiji 12,268 vilivyopo hapa nchini vimepata umeme ambapo vijiji chini ya 2,000 bado havijapata umeme," alisema Mhandisi Maganga.
Alisema kwa sasa REA imeandaa Mradi Mwingine wa Usambazaji Umeme Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili ambao umechukua vijiji vyote vilivyosalia na kuwa tayari wamepata wakandarasi wa mradi huo na ambao ulizinduliwa Machi 15 mwaka huu na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani wilayani Igunga mkoani Tabora na kuwa wanatarajia kati ya Julai na Disemba 2022 vijiji vilivyobakia vitakuwa na umeme.
Mhandisi Maganga alisema siri ya mafanikio hayo makubwa ni kutokana na Serikali kuwekeza fedha Shilingi Trilioni 3.4 kwa REA na kuwa toka mwaka 2015 hadi sasa ni zaidi ya Shilingi trilioni 2.8 zimekwisha tumika.
Alisema kutokana na usimamizi mzuri wa REA pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wametekeleza miradi mikubwa ya REA Awamu ya Pili, REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza na miradi mingine ikiwemo ya kuvipatia umeme vijiji vyote vinavyopitiwa na Mradi wa ujenzi wa njia kubwa ya umeme kutoka Iringa kupitia Dodoma, Singida, Tabora hadi Shinyanga wa kilovoti 400 na kuwa vijiji vyote vinavyopitiwa na njia hiyo vimepata umeme.
Alisema kwa wakati wote utekelezaji wa mradi huo REA wameimarisha usimamizi na kuwa wanafanya kazi hiyo kwa kushirikiana na TANESCO na ambao ndio wasimamizi wakubwa wa miradi hiyo.
Alisema juhudi hizo za kuhakikisha wananchi wanapata umeme zinaenda sanjari na utoaji wa elimu juu ya matumizi bora ya nishati hiyo.
Alisema kuanzishwa kwa Viwanda vya kuzalisha vifaa vya umeme hapa nchini vimechangia kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo na kufufua fursa za ajira ambapo zaidi ya wafanyakazi 4,000 wameajiriwa.
Akichangia mada hiyo, Mhandisi Deogratius Nagu ambaye ni Mhandisi Miradi kutoka REA, alisema miradi hiyo imewanufaisha wananchi kwa kufungua fursa za ajira kwa wakandarasi kuingia mikataba ya ajira na wananchi inakotekelezwa miradi hiyo ikiwa ni moja ya takwa la kisheria.
Mhandisi Nagu alisema mbali na kutoa ajira hizo umeme huo umesaidia kuinua huduma za kiuchumi na kijamii kwa kupeleka umeme huo mashuleni, Zahanati, kuanzishwa kwa viwanda vidogo vidogo na kuongeza thamani ya mazao ya wakulima vijijini ikiwa ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo walisafirisha mahindi lakini kwa sasa wanasafirisha unga.
MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AZURU KABURI LA HAYATI DKT. JOHN M,AGUFULI CHATO
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Geita Engineer Gabriel pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali, wakati alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Chato Mkoani Geita leo Mei 14,2021. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
PROF. MSANJILA AAGIZA KUKAGULIWA KWA LESENI ZA MADINI NJOMBE
Na Asteria Muhozya, Njombe
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila amemwagiza Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Njombe kufanya ukaguzi wa Leseni zote 245 za Uchimbaji Madini mkoani humo ili kujua maendeleo ya uendelezwaji wake.
Agizo hilo linafuatia ombi lililowasilishwa na wachimbaji wadogo wa Madini mkoa wa Njombe ambao wameiomba Wizara kuwapatia maeneo ya kuchimba kutokana na sehemu kubwa kushikiliwa na wawekezaji kwa kipindi kirefu pasipo kuyaendeleza.
" Nakuagiza RMO fanya uchambuzi wa Leseni zote kujua zina hali gani, ikiwa zinalipiwa, ni maendeleo gani yamefanyika ili kuanzia hapo wizara ichukue hatua. Tunapotoa leseni tunataka watu waziendeleze na wachimbe siyo kuzifungia kabatini,’’amesisitiza Prof. Msanjila.
Prof. Msanjila ameongeza kuwa, moja ya vipaumbele vya Serikali na kama alivyoeleza Waziri wa Madini katika Hotuba yake ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2021/22 ni pamoja na kuwaendeleza, kuwarasimisha na kuwapatia maeneo wachimbaji wadogo ili wachimbe, hivyo, wizara itahakikisha inalifanyia kazi kwa karibu suala hilo.
Amefanunua kuwa, endapo mmliki wa leseni ana nia ya kuiuza leseni yake hakatazwi isipokuwa anapaswa kuiendeleza kwanza kabla ya kufanya maamuzi mengine. ‘’ Ukitaka kuuza leseni lazima useme uliifanyia nini kabla ya kuiuza. Huu ndiyo utaratibu wa Sheria,’’ amesema.
Akizungumzia mwenendo wa makusanyo katika mkoa huo amesema bado kiwango kiko chini ikilinganishwa na rasilimali madini zinazopatikana katika mkoa huo ikiwemo chuma na makaa ya mawe na kuongeza kwamba, hadi sasa Mkoa wa Njombe umekusanya kiasi cha shilingi milioni 240 kati ya shilingi bilioni 1 uliyopangiwa kukusanya huku akitaja moja ya sababu ikiwa ni wamiliki kutozifanyia kazi leseni zao.
Pia, ametumia fursa hiyo kuwapongeza wachimbaji wadogo katika mkoa huo kwa kufanya shughuli zao huku wakishirikiana kwa karibu na Ofisi ya Madini pamoja na ofisi ya Mkoa wa Njombe suala ambalo limepelekea kutokuwepo kwa migogoro inayozuia maendeleo ya Sekta.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wachimbaji Wadogo Mkoa wa Njombe Alfred Luvanda, amemhakikishia Prof. Msanjila kuwa, wachimbaji mkoani humo wako tayari kimitaji ikiwemo kulipa kodi za serikali pindi itakapowapatia leseni za kuchimba madini, huku wakiahidi kuendeleza ushirikiano na Ofisi ya Madini.
‘’ Kwanza tunashukuru sana kwa ujio wako, tunaamini kilio chetu kimefika sehemu sahihi. Tunakuahidi tutachimba, tutalipa kodi za serikali na tutaipa serikali heshima,’’ amesema Luvanda.
Naye, Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Njombe Henry Mditi amewaeleza wachimbaji hao kuwa ofisi ya madini mkoani humo haitomuonea mtu yoyote na hivyo akawataka wachimbaji hao kufanya shughuli zao kwa kufuata Sheria.
Prof. Msanjila amekutana na wachimbaji hao Mei 13, 2021, wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo iliyolenga kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili wachimbaji pamoja na watumishi wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.