Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

VIFAA VYA KUZIMIA MOTO

$
0
0

 


VIFAA VYA KUZIMIA MOTO

Kwa wanaohitaji huduma ya Fire Extinguisher za aina zote pamoja na Fire Alarm Systems, Water System Equipment ,Safety Gears na Spare Parts  kutoka kampuni ya Kimataifa ya NAFFCO na kusambazwa Tanzania na kampuni ya Safety Limited pekee naomba tuwasiliane.

Huduma ya vifaa hivyo  ni muhimu majumbani mwetu, maofisini, kwenye shule na maeneo yote ambayo watu hukusanyika.

Tafadhali wasiliana na Afisa Masoko,  Happiness  Katabazi  kwa namba 0716 774494 ili upate huduma hii muhimu.

Kumbuka, 🧯 inaweza kuokoa uhai wa familia yako na mali zako na jamii kwa ujumla.


UTT AMIS YATOA MAFUNZO JUU YA UWEKEZJI WA PAMOJA KWA WAFANYAKAZI WA TANROADS

$
0
0
Mwezeshaji Daudi Mbaga kutoka UTT AMIS akitoa mafunzo kwa wafanyakazi wapya wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS juu ya Uwekezaji wa Pamoja  mkoani Morogoro.
 
Baadhi ya wafanyakazi wa TANROADS wakipata mafunzo juu ya Uwekezaji wa Pamoja kutoka kwa Daudi Mbaga wa UTT AMIS.



Benki ya CRDB yakusanya wadau kujadili uvumbuzi katika sekta ya fedha

$
0
0

 

Mkurugenzi wa FSDT, Sosthenes Kewe akiongoza Kongamano lililoandaliwa kwakushirikiana kati ya Benki ya CRDB na Vodacom Tanzania na kuhudhuriwa na maafisa kutoka Wizara ya Elimu, wanafunzi na wakufunzi kutoka vyuo mbalimbali vya Dodoma. Hii ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za maadhimisho ya wiki ya uvumbuzi “Innovation Week” ambayo yataambatana na Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU).


Meneja Mwandamizi wa Huduma za Ziada za Benki ya CRDB Ndugu Mangire Kibada akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.



     Dodoma, Mei 06, 2021 – Benki ya CRDB imefanya kongamano lililobeba mada ya “Ni kwa namna gani sekta ya fedha inapaswa kuenenda kwa mwaka 2021?” ukizingatia dunia inapita katika changamoto ya janga la COVID-19 liloshika kasi mwaka 2020. Kongamano hilo lilioandliwa kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Vodacom liliongozwa na Mkurugenzi wa FSDT, Sosthenes Kewe na kuhudhuriwa na maafisa kutoka Wizara ya Elimu, wanafunzi na wakufunzi kutoka vyuo mbalimbali vya Dodoma.


Kongamano hilo limefanyika ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za maadhimisho ya wiki ya uvumbuzi “Innovation Week” ambayo yataambatana na Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) yaliasisiwa mwaka 2019 kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT), Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA). 


Akizungumza katika kongamano hilo, Meneja Mwandamizi wa Huduma za Ziada za Benki ya CRDB, Mangire Kibada amaesema kuwa Benki ya CRDB imeamua kudhamini wiki ya uvumbuzi kwa kuwa inaamini katika kutoa huduma na bidhaa bora kwa wateja ambazo zinapatikana kwa njia ya kuwekeza katika uvumbuzi.

“Kwetu Benki ya CRDB tunaamini uvumbuzi ni kitu pekee ambacho kinaweza kututofautisha na wengine katika soko na hivyo kuifanya benki yetu kuendelea kuwa kinara sokoni kwa kuweza kutimiza mahitaji ya wateja wa makundi mbalimbali” alisema Kibanda.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa FSDT, Sosthenes Kewe alisema kuwa lengo la kongamano hilo ni  kuainisha na kupendekeza hatua zinazopaswa kuchukuliwa katika kutengeneza na kutekeleza mipango ya uvumbuzi katika sekta ya fedha. 

MAKAMU WEA RAIS DKT. MPANGO AMTEMBELEA MAMA JANETH MAGUFULI

$
0
0

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akisalimiana Mjane wa Hayati Dkt. John Magufuli Mama Janeth Magufuli wakati alipomtembelea Nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam leo Mei 08,2021. Katikati ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango.

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akizungumza na  Mjane wa Hayati Dkt. John Magufuli Mama Janeth Magufuli wakati alipomtembelea Nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam leo Mei 08,2021. Katikati ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

NDALICHAKO AKIPONGEZA CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA) KWA KUIBUA WABUNIFU

$
0
0
Waziri wa Elimu Sayansi naTeknolojia  Prof. Joyce Ndalichako na Naibu Waziri wake na viongozi wengine wakimuangalia Mbunifu wa FARM CUT kutoka SUA, Mussa Dotto akionyesha matrekta shamba hilo linavyofanyakaz iwakati wa MAKISATU 2021 Dodoma.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Leonard  Akwilapo akitoa maelezo ya mashindano hayo ya MAKISATU 2021 kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua maonesho na mashindano hayo jijini Dodoma.
Wananchi wakimiminika kwenye banda la SUA kuangalia bunifu na teknolojia mbalimbali ambazo wamekuja kuzionyesha kwenye maonesho hayo ya MAKISATU 2021 Jijini Dodoma.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda akiwa kwenye picha ya pamoja na waonyeshaji kutoka SUA Kwenye banda la SUA lililopo kwenye maonesho ya MAKISATU 2021 jijini Dodoma.

Fundi sanifu wa maabara ya Kemia na Fizikia SUA,  Anneth Coster akiwaonyesha Wanafunzi namna Indicator iliyozalishwa na SUA kwa ajili ya somo la kemia kwa wanafunzi wa shule za sekondari.



Na Calvin Gwabara - Dodoma


WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwa jitihada wanazozifanya katika kuibua Wabunifu,Teknolojia na mbinu zingine za kisayansi pamoja na kuwa saidia na kuendeleza wabunifu hao ili waweze kufikia ndoto zao na kusaidia jamii na taifa.

Pongezi hizo ametoa wakati akitembelea kukagua kazi za wabunifu wa SUA na maonesho yao kabla ya kuzindua rasmi mashindano ya kitaifa ya sayansi,teknolojia na ubunifu (MAKISATU 2021) jijini Dodoma yanayokutanisha wabunifu kutoka nchi nzima kwenye makundi saba ya ushindani.

Akizungumza wakati akifungua mashindano hayo amesema kuwa miongoni mwa mafanikio ambayo Serikali imeyapata katika kuendeleza Sayansi na Ubunifu nchini ni pamoja na kuibua na kutambua wabunifu wachanga 1066 kupitia MAKISATU 2019/2020 ambapo kati ya hao wabunifu mahiri 130 wanaendelezwa na Serikali ili bunifu zao zifikie hatua ya kubihasharishwa na hivyo kuongeza fursa za ajira kwa vijana na kuchangia kwenye pato la taifa.

 “Ni matumaini na matarajio yangu kuwa bidhaa zinazozalishwa na wabunifu na wavumbuzi nchini zitaongeza tija katika uzalishaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda na kuongeza thamani ya bidhaa zinazo zalishwa pamoja na kuboresha na kurahisisha utoaji wa huduma katika Nyanja mbalimbali” Alisisitiza Prof. Ndalichako.

Aidha Prof. Ndalichako ameeleza kuwa katika kipindi cha mwaka 2015 hadi mwaka 2020 Serikali imefadhili jumla ya miradi 215 ya sayansi teknolojia na ubunifu kwenye sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo na Mifugo, Afya, Nishati, Maliasili na Viwanda aidha kupitia mfuko wa taifa wa uendelezaji Sayansi naTeknilojia Serikali imewajengea  uwezo watafiti 579 katika masomo ya uzamili na uzamivu ili kuwaongezea weledi kwenye utafiti.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi huyo kufungua maonesho hayo ya MAKISATU 2021Katibu Mkuu wa wizara  hiyo Dkt.Leonard Akwilapo amesema mashindano hayo ya MAKISATU yalianzishwa mwaka 2019 yakiwa ni moja ya mikakati ya Wizara ya kuibu,kutambua na kuendeleza bunifu na vumbuzi zinazofanywa na Watanzania na kukuza hamasa ya ubunifu na kuhamasisha matumizi ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu katika shughuli ya kijamii na  kiuchumi utakaotegemeza maendeleo ya uchumi wa viwanda.

Amefafanua kuwa katika kipindi cha miaka miwili ya MAKISATU jumla ya wabunifu 1066 waliibuliwa na kutambuliwa na Wizara na wabunifu mahiri 130 wanaendelezwa na Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi naTeknolojia (COSTECH) ili ubunifu wao ufikie kubiasharishwa na hivyo kuongeza fursa za ajira kwa vijana.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof.Raphael Chibunda alimwambia Waziri huyo kuwa katika kuhakikisha wabunifu wa SUA wanafikia hatua za kubihasharisha wanatarajia kumpatia kiasi cha shilingi milioni 20 mmoja wa wabunifu wao Mussa Dotto aliyebuni Trekta la kulimia aliloliita FARM CUT ili aweze kuzalisha matrekta hayo matatu yaingie sokoini.

Amesema walipoonaamebuni trekta hilo waliamua kumsaidia kupitia mfuko wa ubunifu wa Chuo lakini lengo lingine ni kutaka kuwaonyesha wanaosema elimu imeshuka waone namna ambavyo vijana  wanawezakufanya mambo makubwa vyuoni na kunufaika pamoja na kunufaisha jamii na taifa.

Chuo Kikuu cha Sokone cha Kilimo SUA kinashiriki maonesho hayo kwa kuonyesha kazi zake mbalimbali za kitafiti na kibunifu lakini pia kimeingiza Wabunifu watatu  kwenyemashindano hayo ya MAKISATU kupitia kundi la vyuo vikuu ambalo lina wabunifu 10.

Kauli mbiu ya mwaka huu inasema Sayansi Teknolojia na Ubunifu kwa Uchumi Endelevu.


OSHA YAWANOA WAFANYAKAZI WA KIWANDA CHA NONDO MIKOCHENI

$
0
0

Mwezeshaji wa mafunzo ya usalama na afya kutoka OSHA, Respicious Kundawa , akitoa mafunzo kwa wafanyakazi wa kiwanda cha PNP Industries Limited.

Mwezeshaji wa mafunzo ya usalama na afya kutoka OSHA, Respicious Kundawa , akizungumza na mmoja ya washiriki wa mafunzo wa kiwanda cha PNP Industries Limited. OSHA imetoa mafunzo hayo kuwawezesha wafanyakazi kujilinda dhidi ya vihatarishi wanapokuwa kazini.

Mwezeshaji wa mafunzo ya usalama na afya kutoka OSHA, Respicious Kundawa , akitoa maelekezo kuhusu kuboresha mazingira ya kazi kwa wasimamizi wa wafanyakazi wa kiwanda cha PNP Industries Limited mara baada ya kutoa mafunzo ya usalama na afya kiwandani hapo.

Wafanyakazi wa kiwanda cha PNP Industries Limited wakifuatilia mafunzo ya usalama na afya yaliyotolewa na OSHA kiwandani hapo. Mafunzo hayo yalilenga kuwawezesha wafanyakazi kujilinda dhidi ya vihatarishi wanapokuwa kazini.

******************************

Na Mwandishi Wetu

Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) umetoa mafunzo maalum ya usalama na afya kwa wafanyakazi wa kiwanda cha kuzalisha nondo cha PNP Industries Limited yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kujilinda dhidi ya ajali na magojwa yanayotokana na mazingira yao ya kazi.

Mwezeshaji wa Mafunzo hayo kutoka OSHA, Respicious Kundawa, amesema mafunzo hayo ni muhimu hususan kwa wafanyakazi wanaohusika moja kwa moja katika mchakato mzima wa uzalishaji wa bidhaa hiyo muhimu.

“Katika mafunzo ya leo tumewalenga wafanyakazi katika viwanda vya kuzalisha nondo ambao tunafahamu wanakabiliwa na vihatarishi mbali mbali katika mlolongo mzima wa uzalishaji wa bidhaa husika kuanzia wanapopokea vyuma chakavu, kuvichambua, kuviyeyusha, kutengeneza nondo zenyewe na hata kuzipakia katika magari tayari kwa kuzisafirisha kwenda kutumika,” alieleza Kundawa.

Aliongeza: “Katika hatua zote hizo mfanyakazi anaweza kuumia hivyo ni muhimu kuwapa wafanyakazi nyenzo za kujilinda.”

Kwa upande wa uongozi wa kiwanda hicho umeeleza kuridhishwa na mafunzo yaliyotolewa na OSHA na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo yaliyotolewa kupitia mafunzo hayo.

“Tunashukuru OSHA kwa mafunzo waliyotupatia kwa siku ya leo ambayo yatatusaidia sana katika kuboresha mazingira yetu ya kazi pamoja na namna ambavyo tunafanya kazi,” alisema Iddy Hamis, Afisa Rasilimali Watu wa Kiwanda cha PNP Industries Limited.

Aidha, wafanyakazi walioshiriki katika mafunzo hayo wamesema akiwemo Juma Kajembe na Solomon Lukas wamesema mafunzo waliyoyapata yatasaidia katika kuboresha namna ambavyo wamekuwa wakitekeleza majukumu yao na hivyo kujiepusha na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.

“Tunashukuru kwa mafunzo tuliyoyapata kwa siku ya leo, tunaimani yatatutoa kutoka hatua moja kwenda nyingine kahusiana na usalama wetu tuwapo kazini. Kwasasa tunaweza kutambua vitu gana ni hatarishi katika maeneo yetu kazini pamoja na matumizi sahihi ya vitendea kazi na vifaa kinga,” alisema Juma Kajembe ambaye ni mfanyakazi wa kiwanda cha PNP.

Mafunzo hayo ambayo yamefanyika katika eneo la kiwanda, Mikocheni jijini Dar es Salaam, yamejumuisha wafanyakazi zaidi ya 90 ambao wanahusika na shughuli mbali mbali katika mlolongo mzima wa uzalishaji nondo pamoja na wasimamizi wao.

Wakati huo huo, OSHA imehitimisha darasa la mafunzo ya usalama na afya katika sekta ya mafuta na gesi yaliyofanyika katika ofisi za OSHA ambayo yalijikita katika kuwaandaa wataalam ambao watatumika kusimamia usalama wa wafanyakazi katika miradi ya mafuta na gesi inayotarajiwa kuanza kutekelezwa hapa nchini.

PAMBANO LA SIMBA NA YANGA, TFF YABADILISHA MUDA WA KUANZA, YANGA WAINGIZA TIMU SA 11

Naibu Waziri Gekul Asisitiza Michezo Kufanyika kuanzia Ngazi ya Vijiji

$
0
0

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa KM 42 Wanawake Bi.Monica Cheluto kutoka Kenya katika mbio za Tulia Marathon zinazodhaminiwa na Mhe. Tulia Ackson Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizofanyika Mei 08, 2021 Jijini Mbeya.

 

Na Shamimu Nyaki-WHUSM, Mbeya

 

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Pauline Gekul amezitaka Halmashauri zote nchini kusimamia michezo kuanzia ngazi za vijiji ili wananchi  waweze kuimarisha afya zao  na kukuza michezo kuanzia ngazi ya chini hadi Taifa.

 

Mhe. Gekul ametoa maagizo hayo Mei 08, 2021 Jijijini Mbeya akiwa Mgeni Rasmi katika Mbio za Tulia Marathon  zinazodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini ambaye pia ni  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson.

 

"Nafahamu kuna asilimia 40 inayotengwa na Halmashauri kwa ajili ya shughuli za maendeleo, natoa rai kwa viongozi wa Halmashauri kutenga fedha kidogo kwenye hiyo asilimia ambazo zitawezesha shughuli za michezo kwenye maeneo yenu kuanzia ngazi za chini kabisa kwenye vitongoji", amesisitiza Mhe. Gekul.

 

Kwa upande wake, Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amesema lengo la mashindano hayo ni kuboresha Miondombinu ya Elimu na Afya kupitia Taasisi ya TuliaTrust Fund kwenye Jimbo hilo ambapo zinatarajiwa kufikia Watanzania wengi hapo baadae.

 

"Tulia Trust Fund ipo kwa ajili ya kusadia na kuwezesha wananchi kiuchumi,tangu mwaka 2018 taasisi hii imesadia wananchi kupitia miradi mbalimbali ikiwemo kuboresha madarasa, mabweni na upatikanaji wa maji na kazi inaendelea" amesema Mhe.Tulia

 

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya  Riadha Nchini Filbert Bay amempongeza Naibu Spika huyo kwa kuanzisha mashindano hayo ya riadha. 

 

Mbio hizo zinajumuisha mbio za ndani na nje ya uwanja ambapo kwa hapa nchini zimefanyika kwa mara ya kwanza.

 

Naye Mshiriki aliyeshika nafasi ya tatu katika  mbio za KM 21 ambaye pia ni miongoni mwa Timu ya Taifa ya Riadha  inayowakilisha nchi katika mashindano ya Riadha yatakayofanyika baadae mwaka huu nchini Japan, Bw. Alphonce Simbu amesema mashindano hayo yamemsadia kufanya mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mashindano yajayo ya Kimataifa  ambapo ameahidi kufanya vizuri na kuitangaza nchi.

 

Mbio hizo hufanyika kila mwaka ambapo kwa mwaka huu zimegawanyika katika makundi ya KM 42 na 21 kwa wanaume na wanawake, Mbio za ndani ya Uwanja kwa Mita 100, 200, 400, 800 na 1500 ambapo pia Viongozi na Waheshimwa Wabunge wameshiriki.

 


KUSUASUA MIRADI YA MAJI MKUU WA WILAYA YA MULEBA ATOA NENO

$
0
0

 


Mkuu wa wilaya ya Muleba mhandisi Richard Luyango.

 

Na Lydia  Lugakila, Muleba

Mkuu wa Wilaya ya Muleba mkoani Kagera Mhandisi Richard Luyango ametoa siku 5 kwa baadhi ya madiwani wilayani humo pamoja na  watendaji wa halmashauri kukutana ili kujua  kwanini  wameshindwa kukamilisha baadhi ya miradi ikiwemo ya maji agizo lililotolewa na naibu waziri wa maji.

Mkuu wa wilaya ya Muleba mhandisi Luyango ametoa agizo hilo katika kikao cha baraza la madiwani kilichojadili masuala mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri hiyo.

Mhandisi Luyango amesikitishwa na baadhi ya madiwani ambao katika kata zao wameshindwa kusimamia miradi ikiwemo ya maji ikiwa ni agizo la naibu waziri wa maji mhandisi Maryprisca Mahundi alilolitoa baada ya kufanya ziara katika baadhi ya kata wilayani humo lililoelekeza mradi wa maji katika kata ya Nshamba kukamilika mapema na kukabidhiwa mnamo Aprili 30 mwaka huu.

" Naibu waziri aliagiza mradi kukamilika mapema leo tupo mwezi Mei, diwani upo watendaji mpo, mamlaka upande wa  maji mpo lakini hamtekelezi ipasavyo, kumbuka  tija  ya mradi ya serikali ni kukamilika na wananchi kuendelea kupata huduma, hivyo basi kupitia kikao hiki ifikapo mei 11, 2021 diwani wa kata ya Nshamba Gozibert Masilingi, diwani  watendaji wa halmashauri tukutane ili kujua kwa nini agizo la naibu waziri halijatekelezwa alisema mkuu huyo wa wilaya".

Ameutaja pia mradi wa maji katika kata ya kamachumu kutokamilika na kuwahimiza viongozi hao akiwemo mwenyekiti wa halmashauri na kamati yake  kwenda kata kwa kata kukagua miradi hiyo na kujenga mazoe ya kupeana taarifa kujua miradi ambayo haijakamilika katika maeneo yao ili kuisaidia serikali.

Aidha ameongeza kuwa miradi ya elimu fedha ilitolewa ambapo ilifanyika harambee kupitia waziri wa elimu katika shule ya msingi na sekondari kaigara na mradi haukukamilika licha ya wananchi na serikali kutoa fedha jambo lililompelekea kutaka majibu ya wapi wamekwama.

Hata hivyo amewahimiza  viongozi hao kukamilisha miradi ya maendeleo katika maeneo yao ikiwemo elimu, maji na barabara pia kusimamia miradi hiyo huku akiwapongeza watendaji hao kwa kuendelea kutekeleza wajibu katika shughuli mbali mbali katika wilaya hiyo ambapo katika makusanyo katika wilaya  hiyo imefikia  asilimia 76 kwa mwaka 2019/2020 huku matarajio yakiwa ni kufikia asilimia 85.

WANAVIJIJI 30 SIMIYU WAPEWA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA TEMBO

$
0
0

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii, Pellage Kauzeni akizungumza na madiwani wa Wilaya ya Meatu kuhusu mikakati ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya kukabiliana na tembo wanaovamia makazi ya watu katika kikao kilichofanyika Wilayani Meatu mwishoni mwa wiki.

Wananchi waliopewa mafunzo ya kukabiliana na tembo wakionyesha kwa vitendo namna ya kutumia honi ili kumfukuza tembo aliyevamia makazi ya watu katika onesho lililofanyika baada kikao cha Wizara ya Maliasili na Utalii na Madiwani wa Wilaya Meatu kilichofanyika mwishoni mwa wiki.

Wananchi waliopewa mafunzo ya kukabiliana na tembo wakionyesha kwa vitendo namna ya kutumia wigo wa pilipili na oili chafu ili kumfukuza tembo aliyevamia makazi ya watu katika onesho lililofanyika baada kikao cha Wizara ya Maliasili na Utalii na Madiwani wa Wilaya Meatu kilichofanyika mwishoni mwa wiki.

*******************************

Na Happiness Shayo- MEATU

Wanavijiji 30 kutoka wilaya zote za mkoa wa Simiyu wamefundishwa namna ya kukabiliana na wanyama waharibifu hasa tembo ikiwa ni mwendelezo wa mikakati ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya kuhakikisha usalama wa wananchi wanaoishi kwenye maeneo yenye changamoto ya kuvamiwa na tembo.

Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Pellage Kauzeni alipofanya kikao na madiwani wa Wilaya ya Meatu mwishoni mwa wiki.

Bw. Kauzeni amefafanua kuwa mafunzo hayo yamefanyika chini ya Mradi wa utafiti wa tembo kwa ukanda wa Serengeti, Maswa na Ngorongoro.

Ametaja mafunzo yaliyotolewa kwa wananchi hao kuwa ni kutumia honi, kutumia mabomu ya pilipili na kutumia mabomu ya kisasa ya kufukuza tembo.

Njia nyingine zilizofundishwa za kupambana na tembo ni kutumia wigo wa pilipili na oili chafu pamoja na kutengeneza tofali au mkate wa pilipili na kinyesi cha wanyama kama ngombe,mbuzi n.k.

Bw. Kauzeni ameweka bayana kuwa njia hizo za kupambana na wanyama waharibifu zimeshawahi kutumika katika maeneo mbalimbali na zimeleta matokeo chanya.

“Njia hizi zimeshawahi kutumika na Jumuiya za Hifadhi kwa Jamii (WMA) za Kaskazini mwa Tanzania kupitia mradi wa Fredkin na pia Kusini mwa Tanzania upande wa Selous Game Reserve na zimeonyesha mafanikio makubwa” amefafanua Bw. Kauzeni.

Akizungumzia mikakati ya Serikali ya kuendelea kupambana na wanyama waharibifu Bw. Kauzeni amesema Serikali kupitia taasisi ya TanzaniaWildlife Research Institute (TAWIRI) inaendelea na tafiti ili kugundua mbinu za gharama nafuu zaidi zitakazotumiwa na wananchi kupambana na tembo na pia Wizara ya Maliasili na Utalii inaendelea kuelimisha wananchi ili kupunguza changamoto ya uvamizi wa wanyama waharibifu katika makazi ya watu.

Naye, Mkazi wa Kijiji cha Mwanzalamba Wilaya ya Meatu, Sololo Malando amesema kuwa amefundishwa mbinu mbalimbali za kujilinda na wanyama waharibifu kama kutumia vilipuzi vya kurusha kwa mkono.

“Mbinu hii ya kutumia vilipuzi ikitumika vizuri itasaidia sana wananchi kuondokana na hili tatizo la tembo kwa kuwa inasaidia kuwakimbiza tembo endapo wamevamia mashamba” amesema Malando.

Mkazi mwingine wa wilaya ya Meatu, Magembe Sita ametaja mafunzo aliyoyapata akitolea mfano wa mafunzo ya kutumia tochi, honi na baruti ya kutumia mchanga na pilipili kufukuza tembo.

Kikao hicho kiliambatana na maonyesho ya mbinu za kukabiliana na tembo yaliyofanywa na wanavijiji kutoka wilaya za Mkoa wa Simiyu na kushuhudiwa na wakuu wa wilaya za Busega, Itilima na Meatu

TAMUFO YAMPONGEZA WAZIRI BASHUNGWA KWA KUSIKIA KILIO CHAO

$
0
0

Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stella Joel.
Mlezi wa TAMUFO, Frank Richard.
 


 Na Dotto Mwaibale


UMOJA wa Wanamuziki Tanzania ( TAMUFO) umempongeza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa kwa kusikia kilio chao kwa kuwatoa hofu Wasanii kuhusu suala la ugawaji wa Mirabaha. 

Hatua hiyo ya Bashungwa imekuja ikiwa ni siku moja tu baada ya TAMUFO kuliomba  Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA)  kuhakikisha linashirikisha wadau wa muziki  kabla ya kutoa maamuzi ya kuwabana wasanii.

Ombi hilo lilitolewa na Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stella Joel  jijini Arusha juzi baada  ya kutokea malalamiko ya wanamuziki kulalamikia kitendo cha Basata kuweka  utaratibu wa kuwataka wanamuziki nyimbo zao zikaguliwe baada ya kurekodi kwa  sababu za kimaadili.

Joel alisema jambo hilo lilikuwa linawaumiza wanamuziki wa Tanzania ambao wanahangaika sana kuwezakumudu gharama za kurekodi kazi zao.

Katibu mkuu huyo wa TAMUFO Stella Joel alisema wanamuziki wengi hawana kipato  cha kutosha na kurudia rudia katika kurekodi kazi zao na bado hawajaweza kufaidika nazo.

Akizungumza jana jijini Dodoma katika kikao chake na  Viongozi wa Vyama na Mashirikisho ya Muziki na Filamu nchini kilicholenga kuzungumzia Kanuni ya 26 ya BASATA inayohusu uhakiki wa kazi za Muziki na Filamu  kabla ya kuingia sokoni au kusambazwa, Bashungwa aliwatoa hofu wasanii kuhusu suala la ugawaji wa Mirabaha kwa kuelezea kuwa Serikali imeandaa mifumo ya kidijitali ambayo itarahisisha  ukusanyaji wa mirabaha hiyo na kuongeza gawio.

“COSOTA imekuwa na changamoto ya ukusanyaji wa mirabaha kutokana na uhaba  wa watumishi hivyo kwa kupitia mfumo mpya wa kidijitali utakao anzishwa hivi karibuni utarahisisha ukusanyaji wa mirabaha hiyo, Serikali inataka kutoa gawio la pesa nyingi kwa wasanii na siyo fedha kidogo hivyo tunawaomba mvumilie kidogo kuanzia mwaka mpya wa fedha mambo yatakuwa mazuri.” alisema Bashungwa.

Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho Bashungwa alitoa maelezo mahususi kwa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) akiwataka kusitisha utekelezaji wa Kanuni ya 26 inayotaka kazi zote za Muziki kukaguliwa nao kabla ya kusambazwa.

Aidha, Bashungwa alisisitiza kuwa maelekezo hayo ya kusikitishwa kwa matumizi ya kanuni hiyo ni kwa upande wa Muziki pekee ila kwa upande wa Filamu itaendelea kutumika kama kawaida. 

Pamoja na hayo Bashungwa alitoa maelekezo ya haraka kwa BASATA kwa kuwataka kuanzisha mchakato wa kurekebisha kanuni hiyo kwa kuwashirikisha wadau  hao wa vyama na mashirikisho ili kuweza kupata Kanuni mpya isiyodumaza tasnia ya Muziki lakini izingatie maadili ya Taifa.

Halikadhalika Waziri huyo ameelekeza BASATA kwa kushirikiana na wadau kuandaa mwongozo utakao kuwa kukitoa dira njema ya uendeshaji na ukuzaji wa tasnia ya Muziki.  

Naye mmoja wa wasanii hao Soggy Doggy alimshukuru Bashungwa kwa maamuzi  aliyoyafanya na kumpongeza na kuahidi kuendelea kushirikiana na wasanii wa Muziki katika  kukuza na kuiendeleza tasnia ya muziki nchini.

Mlezi wa TAMUFO, Frank Richard, akiongea juzi na waandishi wa habari  aliiomba Serikali kuziwezesha taasisi zenye nia ya kusaidia maendeleo ya sanaa hapa nchini Ikiwemo Basata.

Richard aliomba kuwepo na 
 utaratibu wa kuandaa semina kwa ajili ya kutoa elimu ya kuwajengea uelewa wasanii juu ya kazi zinazokubalika kimaadili na katika kulinda heshima ya muziki na utamaduni wa Tanzania.

Aidha Richard ameoimba Serikali kuhakikisha idadi ya studio zote hapa nchini zinajulikana ili kuweza kutoa elimu kupitia vipeperushi vinavyozungumzia maadali na taratibu zinapaswa kufuatwa kabla ya kutoa wimbo.

Alisema hali hiyo itaepusha hasara zinazosabisha msanii kurudia wimbo pia kuepusha malalamiko hayo yanayojitokeza.

Richard alisema taasisi zinazosimamia kazi za sanaa na wasanii kwa Ujumla ni muhimu ziandae vipindi vya Redio na Tv na mitandao ya Kijamii kwa ajilo ya kutoa elimu kwa wasanii na wamiliki wa studio  ili kuwajengea uelewa   juu ya jambo hilo.


FIDIA UWANJA WA NDEGE MSALATO NA BARABARA YA MZUNGUKO KULIPWA HIVI KARIBUNI

$
0
0

 


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi, Dkt. Leonard Chamuriho, akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, mara baada ya kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa barabara ya mzunguko ya jiji la Dodoma kwa njia nne (Km112.3) pamoja na eneo utakapojengwa Uwanja wa Ndege  wa Msalato hivi karibuni, jijini Dodoma.

 

Baadhi ya wananchi wa kata ya Matumbulu, Jijini Dodoma, wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho (hayupo pichani) kuhusu malipo yao ya fidia kwa waliopisha ujenzi wa barabara ya mzunguko ya jiji la Dodoma kwa njia nne (Km112.3), jijini Dodoma.

 

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale, akitoa taarifa kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, kuhusu hatua za ujenzi wa barabara ya mzunguko ya jiji la Dodoma kwa njia nne (Km112.3) unaotarajiwa kuanza hivi karibuni mara baada ya wananchi kulipwa fidia zao, jijini Dodoma.


 

Serikali imesema kuwa itaanza zoezi la ulipaji fidia hivi karibuni kwa  wananchi wote waliochukuliwa maeneo yao ili kupisha miradi ya kimkakati ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato na barabara ya mzunguko ya jiji la Dodoma kwa njia nne (Km 112.3).

Aidha imeelezwa kuwa kiasi cha Shilingi Bilioni 12.7 imeshatolewa na kupelekwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa ajili ya fidia za mradi wa ujenzi wa barabara ya mzunguko ya jiji la Dodoma na kiasi cha shilingi Bilioni 14.5 kwa ajili ya malipo ya fidia kwa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa
Msalato. 

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Msalato na Matumbulu jijini Dodoma, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho, amesema kuwa fidia hiyo italipwa kwa kuzingatia sheria na kusisitiza kuwa kila anayedai fidia hiyo atalipwa fedha yake yote.

“Leo nimekuja hapa kuwaeleza kuwa msiwe na wasiwasi juu ya fidia zenu, fedha zimepatikana na mtalipwa kwa mujibu wa sheria zote za nchi zilizopo, pia malalamiko yatasikilizwa kwa wale ambao hawataridhika”, amesema Waziri Chamuriho.

Dkt. Chamuriho amewaelezea wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuwa barabara hiyo itajengwa kwa sehemu mbili ambapo sehemu ya kwanza itahusisha Nala – Veyula – Mtumba – Ihumwa Dry Port (Km 52.3) na sehemu ya pili itaanzia Ihumwa Dry Port – Matumbulu – Nala (Km 60) na tayari wakandarasi wa ujenzi wa sehemu hizo wameshapatikana.  

Amebainisha kuwa miradi hiyo ikikamilika itasaidia kuvutia fursa za uwekezaji  na hivyo kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa jiji la Dodoma na Taifa kwa ujumla.

Amewataka wananchi wa maeneo yanayopitiwa na miradi hiyo kutoa ushirikiano ili kurahisisha zoezi la ulipaji fidia kufanyika kama lilivyopangwa ili miradi hiyo ya kimkakati kuanza mapema na kukamilika kwa wakati.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Selemani Kakoso, ameitaka Wizara kusimamia wakanadarasi hao kikamilifu katika miradi hiyo na kuhakikisha kuwa inakamilika kwa wakati kwa mujibu wa mikataba iliyowekwa.

Ametoa wito kwa wananchi wanaopitiwa na miradi hiyo kuhakikisha kuwa wanatoa ushirikiano kwa makandarasi na kuacha tabia ya kuhujumu miundombinu ili kupelekea miradi kukamilika kwa wakati.

Awali akitoa taarifa kwa Kamati, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale, ameeleza kuwa mradi wa ujenzi wa barabara ya mzunguko utahusisha pia ujenzi wa miradi mingine inayohusisha jamii moja kwa moja ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya vinne, visima vya maji vinne na magari matano ya kubebea wagonjwa.

Naye Mbunge wa Dodoma Mjini, Mheshimiwa Anthony Mavunde, ameishukuru Serikali kwa kuamua kuanza utekelezaji wa miradi hiyo hivi karibuni kwani kukamilika kwa miradi hiyo kutapelekea kuchangamsha na kuleta maendeleo katika jiji la Dodoma.

Miradi ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya mzunguko ya Dodoma (Km 112.3) kwa njia nne na Uwanja wa Ndege wa Msalato inafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa fedha za mkopo nafuu  kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA VIONGOZI KUAGA MWILI WA MAREHEMU TEDDY HOLLO MAPUNDA KATIKA VIWANJA VYA KARIMJEE JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha maombelezo kabla ya kuaga mwili wa Marehemu Teddy Mapunda katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam leo tarehe 09 Mei, 2021. PICHA NA IKULU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi wengine wakati wa shughuli za kumuaga Marehemu Teddy Mapunda katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam leo tarehe 09 Mei, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akitoa Heshima za mwisho kwenye Jeneza lenye mwili wa Marehemu Teddy Mapunda katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam leo tarehe 09 Mei, 2021.

NDAHANI AWATAKA VIJANA KUWA WAMINIFU KUREJESHA MIKOPO

$
0
0
NDAHANI AWATAKA VIJANA KUWA WAMINIFU KUREJESHA MIKOPO.



Kaimu Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahan (wa tatu walio kaa kutoka kushoto) akiwa na Vijana wa  Kikundi cha Jitume Vijana Ikungi.baada ya kutembelea mradi wa ufyatuaji matofali wilayani humo jana.
Kaimu Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahan (wa pili walio kaa kutoka kushoto) akiwa na Vijana wa  Puma Youth Group.baada ya kutembelea mradi wa ufyatuaji matofa wilayani humo jana.

Vijana wakipakia matofali kuzipeleka eneo la ujenzi wa nyumba tano za watumishi.


Na Dotto Mwaibale, Singida


KAIMU Afisa Vijana Mkoa wa Singida,  Frederick Ndahani amewataka vijana waliokopa asilimia 4 kutoka Halmshauri zote za  Mkoa wa Singida kuwa waaminifu kwa kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.

Ndahani alitoa ombi hilo jana wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya vikundi vya vijana wilayani Ikungi.

Akizingumuza katika kikundi cha Vijana cha Puma  kilichopo wilayani Ikungi alisema
vijana wengi wanajuwa kuwa fedha za halmshauri ni ruzuku au sadaka ,nataka mtambue kuwa fedha hizo ni mkopo ambao kwa upendo wa Serikali umeweka masharti nafuu hivyo ninawataka vijana kurejesha fedha mlizokopa kulingana na mkataba uliowekwa ili zikawasaidie vijana wengine ambao hawajapata.

Aidha Ndahani amewakumbusha wanavikundi kutunza kumbumbuku za biashara zao na kuwa waaminifu wao kwa wao.

Alisema vikundi vingi havitunzi kumbumbuku jambo ambalo linasababisha kushindwa kudhibiti mapato na matumizi ya fedha zao ikiwemo usomaji wa taarifa za vikundi.

Ndahani amewahakikishia vijana wa Mkoa wa Singida kuwa Serikali ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan iko bega Kwa bega kuhakikisha  vijana wanawezeshwa kiuchumi ili kuondokana na umaskini hivyo vijana wanapaswa kuanzisha vikundi na kuvisajili katika maeneo yao.

Aidha Serikali ya sita inaendelea kuhakikisha kila kijiji kinapata umeme ambao utasaidia vijana kuanzisha miradi mbalimbali vikiwemo viwanda vidogo vidogo na vya kati.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Peter Mussa alisema  wanaendelea kuwapatia vikundi vya vijana, wanawake na walemavu elimu ya ujasiriamali sanjari na kuwawezeshaji kiuchumi.

Benki ya NMB yadhamini mashindano ya kitaifa ya sayansi, teknolojia na ubunifu

$
0
0

  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Joyce Ndalichako (kushoto) akipokea mfano wa hundi ya thamani ya sh milioni 15 kutoka kwa Mhazini Mkuu wa Benki ya NMB, Azizi Chacha jana kwa ajili ya udhamini wa mashindano ya Kitaifa ya Sayansi na Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) yaliyoanza jana uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Naibu Waziri Elimu, Omari Kipanga na watatu ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dk Leonard Akwilapo.  BENKI ya NMB imekabidhi kitita cha shilingi milioni 15 kwa ajili ya udhamini ya Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu (Makisatu) yaliyofunguliwa rasmi  jana Jijini Dodoma.

 

Na Mwandishi Wetu

 

BENKI ya NMB imekabidhi kitita cha shilingi milioni 15 kwa ajili ya udhamini ya Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu (Makisatu) yaliyofunguliwa rasmi  jana Jijini Dodoma.

Akizungumza jana Mhazini Mkuu wa Beniki ya NMB,Azizi Chacha alisema benki hiyo imetoa fedha hizo ikiwa ni udhamini wa mashindano hayo yanayoandaliwa na Serikali kupitia wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia.

Chacha alibainisha kuwa lengo la NMB  kutoa fedha hizo ni kuisaidia Serikali katika kufanikisha mashindano hayo ya Kitaifa ambayo yamekuwa na malengo ya kuibua wabunifu wapya kila mwaka.

Alisema NMB  inashiriki katika mashindano hayo kwa kuwa ni wadhamini na wamekuwa wakiwasaidia baadhi ya wabunifu katika kufanikisha ndoto zao za kuendeleza ubunifu huo kwa kuwapa mikopo.

Alibainisha kuwa kuna baadhi ya wabunifu wamekuwa na miradi ambayo inaajiri watu wengine hivyo wakiwezeshwa watatoa ajira zaidi kwa vijana na makundi mengine.

Kadhalika alisema NMB imekuwa ikishirikiana  na Serikali katika mashindano hayo kila mwaka ili kuhakikisha wabunifu wapya wanaibuliwa kila mwaka kwa lengo la kulisaidia taifa.

Aidha alisema NMB inamilikiwa na serikali kwa asilimia 38 hivyo ni jukumu la benki kuiunga mkono serikali katika kuwezesha miradi na mipango mizuri iliyokusudiwa.

Aliongeza kuwa NMB imekuwa ikisaidia Jamii katika maeneo mbalimbali ikiwa ni juhudi za kuunga mkono Serikali katika kuwahudumia wananchi.

Hata hivyo alisema NMB imekuwa ikitoa misaada mbalimbali katika shule za msingi na sekondari kwa kutoa madawati,meza na viti kwa ajili ya wanafunzi kutumia wakati wa masomo .

Kwa upande wake Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Prof. Joyce Ndalichako  aliwashukuru Benki ya NMB na wadau wengine  kwa kuwaunga mkono katika mashindano hayo kwa kutoa kiasi hicho cha fedha.

Prof.Ndalichako  aliwaomba NMB kuendelea kudhamini mashindano hayo ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka kwa washiriki kufanya maonesho kwa wiki moja.

Aliongeza kuwa Serikali itaendelea kutenga bajeti zaidi ili kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa lengo la kuibua wabunifu wapya kila kona ya nchi.

Alisema mashindano hayo yanashirikisha wabunifu kutoka vyuo vya ufundi,shule za msingi, vyuo vikuu na wabunifu binafsi kutoka maeneo mbalimbali.


SIMBA KUONDOKA KESHO KWENDA KUUMANA NA KAIZER CHIEFS

$
0
0

  

Kikosi cha mabingwa wa nchi kitaondoka alfajiri Mei 11, 2021 majira ya saa 9:45 kuelekea Afrika Kusini kupitia Kenya tayari kwa mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CCL) dhidi ya Kaizer Chiefs utakaopigwa siku ya Jumamosi Mei 15, 2021.  (Picha kwa hisani ya Simba).

SERIKALI INAHITAJI SHILINGI TRILIONI NANE KUSAMBAZA UMEME KATIKA VITONGOJI VYOTE

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja akifungua Mkutano wa Kwanza wa Mwaka baina ya REA na Wabia wa Maendeleo wanaofadhili miradi ya nishati uliofanyika tarehe 7,2021 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Juliusi Kalolo,akizungumza wakati wa mkutano wa Kwanza wa Mwaka baina ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Wabia wa Maendeleo wanaofadhili miradi ya nishati uliofanyika Mei 7,2021 jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Jones Olotu, akizungumza wakati wa mkutano wa Kwanza wa Mwaka baina ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Wabia wa Maendeleo wanaofadhili miradi ya nishati uliofanyika Mei 7,2021 jijini Dodoma.

**********************

Na Jaina Msuya - REA

Serikali inahitaji zaidi ya Shilingi Trilioni Nane kwa ajili ya kusambaza miundombinu ya umeme katika vitongoji ambavyo havijafikiwa na nishati hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo alisema hayo katika Mkutano wa Kwanza wa Mwaka kati ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Wabia wa Maendeleo wanaofadhili miradi ya nishati kilichofanyika tarehe 7 Mei 2021.

Wakili Kalolo alisema kuwa kazi ya kusambaza miundombinu ya umeme katika vijiji vilivyobaki inaenda sambamba na kupeleka umeme katika vitongoji kupitia miradi ya ujazilizi.

"Vijiji vilivyobaki ni vichache hivyo kwa wakati huu pia tunaendelea na zoezi la kupunguza idadi ya vitongoji ambavyo havina umeme" alisema.

Akizungumzia lengo la kikao hicho, Wakili Kalolo alisema kuwa ni pamoja na REA kuwasilisha Mpango Kazi wa Mwaka ujao wa Fedha pamoja na Mpango wa Miaka Mitano wa REA kwa ajili ya kujadiliwa na Wabia wa Maendeleo kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa mipango hiyo.

"Moja ya mambo tunayotarajia katika kikao hiki ni ahadi kutoka kwa wafadhili kuhusu utayari wao wa kusaidia katika baadhi ya maeneo. Ni muhimu tujenge hoja zinazokidhi vigezo vyao vya kupata ufadhili," alisema Wakili Kalolo.

Awali, akifungua Mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja alisema kuwa utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini umeongeza fursa za uwekezaji katika maeneo ya vijijini. Alitoa wito kwa wananchi kutumia umeme kwa ajili ya shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kuanzisha biashara ndogo ndogo na za kati pamoja na viwanda.

"Umeme ni nyenzo muhimu kwa ajili ya maendeleo, ukiwa na umeme fursa nyingi za biashara zinafunguka," alisema.

Mhandisi Masanja alitoa wito kwa viongozi wa vijiji na mitaa kuwahamasisha wananchi kutoa maeneo yao kwa ajili ya kupitisha miundombinu ya kusambaza umeme pamoja na kutoa ushirikiano kwa kutunza na kulinda miundombinu hiyo.

"Nchi yetu imepiga hatua kubwa sana katika kusambaza umeme vijijini. Mwaka 2015 ni vijiji takribani 2,000 tu vilikuwa na umeme, lakini leo tunazungumzia vijiji 10,400 vyenye umeme kati ya vijiji 12,268 vya Tanzania Bara," alisema

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini, Mhandisi Jones Olotu aliwataka wananchi kuchangamkia fursa ya kuunganishiwa umeme ili waweze kuanzisha miradi mbalimbali itakayowainua kiuchumi.

Mhandisi Olotu alisema katika baadhi ya maeneo mwitikio wa wananchi kuunganisha umeme bado upo chini na kuwataka kuunganisha umeme kwa bei nafuu ya Shilingi elfu 27.

Kwa wale wasioweza kumudu gharama za kutandaza nyaya katika nyumba zao aliwahamasisha kutumia kifaa maalum kijulikanacho kama Umeme Tayari ambacho ni mbadala wa _wiring_.

Akizungumza katika Mkutano huo, Mwenyekiti wa Wabia hao wa Maendeleo, Børjn Midthun aliipongeza REA kwa kazi nzuri ya kusambaza nishati vijijini na kuongeza kuwa imefungua fursa ya uwekezaji wa miradi ya nishati vijijini.

THRDC yawapiga msasa Waandishi wa habari mtandaoni

$
0
0

 

 

Mratibu wa Mtandao wa Utetezi wa Hakiza binadamu Tanzania (THDRC), Onesmo Ole Ngurumwa.

 


Waandishi wa habari wa Mtandaoni Vyombo tofauti tofauti wakiwa kwenye mafunzo Morogoro. 

 

NA HAMIDA RAMADHANI, MOROGORO



MRATIBU wa Mtandao wa Utetezi wa Haki za Binadamu Tanzanaia (THDRC), Onesmo Ole Ngurumwa amesema, wandishi wa habari wa mtandaoni, wanatakiwa kupewa mafunzo ya mara kwa mara kwani eneo hilo limeonekana likikuwa kwa kasi kubwa.

 

Amesema lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa mtandaoni ni pamoja na maono yanayoonekana kukuwa kwa kasi kubwa kwa vyombo vya habari vya mtandaoni siku hadi siku.

 

Akizungumza katika mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa mtandaoni, leo Jumatatu, tarehe 10 Mei 2021, Mkoani Morogoro, Ole Ngurumwa ambaye kitaaluma ni wakili amesema, vyombo vya habari vya mtandaoni vimepewa sheria ambazo ni kandamizi.

 

“Kutokana na uwepo wa sheria mbalimbali kandamizi kwa eneo la usimamizi wa vyombo vya habari, Sisi kama watetezi wa haki za binadamu Tanzania tumefungua kesi mahakamani ya kuzipinga sheria hizo,” amesema

 

Na kuongeza kusema, “Tunaimani mwisho wa mafunzo hayo ya siku tatu, yatawafanya waandishi wa habari wa mitandoni kuwa na uelewa mpana wa masuala mbalimbali ili waweze kutimiza majukumu yao kwa weledi,’’ amesema Ole Ngurumwa.

 

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji  wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga, akizungumza katika semina hiyo amesema, kumekuwepo na sintofahamu kubwa juu ya kufunguliwa kwa vyombo vya habari vilivyo fungwa.

 

 “Tunamuomba Rais waawamu ya sita wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aziondoe sheria hizi kandamizi kwa vyombo vya habari,“ amesema Mukajanga.

 

Akizungumzia agizo la Rais Samia, alilolitoa hivi karibuni la kuvifungulia vyombo vya habari vilivyofungiwa kutokana na sababu mbalimbali amesema, agizo la Rais Samia sio suluhu ya changamoto ya vyombo vya habari kufungiwa na kuminywa visifanye kazi zake kwa uhuru, bali inatakiwa sheria zibadilishwe ili uhuru wa vyombo vya habari uenziwe na viongozi watakaofuata.

 

"Rais Samia akiapisha makatibu wakuu, aliongelea kidogo suala la uhuru wa habari na aliagiza vyombo vifunguliwe. Hili lina mjadala sababu wengine tulisikia ametamka vyombo vya habari lakini wasaidizi wake wamesema agizo lilihusu vyombo  ya habari vya mtandaoni.”

 

“Kwa sababu ofisi yake haijatoa kauli juu ya tarifa ya wasaidizi wake hao, agizo la kufunguliwa mtandaoni bila shaka hilo ndio sahihi," amesema Mukajanga

 

Katibu mtendaji huyo amesema “tunadhani bila kushughulikia sheria zinazoongoza, zinazosimamia na kudhibiti kazi zetu, tatizo halitaweza kuondoka.”

 

“Kwa nia njema hiyo, anaweza akaamua kama hivyo mfungulieni fulani, lakini kama sheria ipo maana yake kesho anaweza pata tatizo mtu mwingine au yuleyule aliyefunguliwa akapata tatizo kutokana na sheria zile zile," amesema Mukajanga.

 

Amesema, “hii inatupeleka wapi, tunadhani hii inaonesha umuhimu kutazama mazingira yetu kwa umuhimu zaidi."


Naye , Mwenyekiti wa Chama cha Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Deogratius Nsokolo amesema, “hakuna safari isiyokuwa na mwisho, tumekuwa katika maumivu kwa kipindi kirefu na kundi la ‘social media’ lilisaidia sana, katika kuhabarisha umma.”

 

Amesema, wakati kukiwa na mtanziko kwenye vyombo vya habari vingine, mitandao ya kijamii ilifanikiwa kwa sehemu kubwa kuhabarisha kwani wahusika waliokuwa wakihabarisha, haikuwalazimu kuwa sehemu moja.

 

 

“Kuna sheria na kanuni mbalimbali zinatukwaza katika utendaji kazi, wakati tukiendelea kupambana kuhakikisha zinaondoka, tuendelee kufanya kazi tukijua kabisa kuna hizi sheria,” amesema Nsokolo

 

Naye Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, (TEF) Deodatus Balile amesema, mchakato wa mabadiliko ya sheria za mtandaoni umeanza kufanywa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kuwaomba wadau kujitokeza kutoa maoni

 

Amesema, kauli ya Rais Samia haikusema vyombo vya habari vya mtandaoni, “alisema vyombo vya habari vilivyofungiwa, vifunguliwe” na akagusia suala la kanuni ziwe wazi.

 

Balile amesema, mkanganyiko ulikuja kwa watendaji wa Rais Samia wamekuwa waking’ang’ana ni vya mtandaoni pekee jambo ambalo linaendeleza mjadala wa agizo hilo la Rais.

 

Kuhusu mchakato wa mabadiliko ya sheria amesema tayari umeanza na kuvitaka Vyombo vya habari  vya mtandaoni  kushiriki kwani TCRA imeanza, wakatoe  mawazo na maoni yao 

Na kuwataka waandishi wa habari kuonyesha weledi katika kuhabarisha umma.

 

 

Jumanne ya tarehe 6 Aprili 2021, Rais Samia alitoa amri ya kuachia huru vyombo vyote vya habari wakati akihutubia baada ya kuwaapisha makatibu, manaibu katibu wakuu na viongozi wa taasisi za umma, Ikulu ya Dar es Salaam.

 

Rais Samia alisema, wizara ya habari inapaswa kusimamia vyombo vya habari "nasikia kuna vijivyombo vya habari mmevifungia fungia, sijui viji- TV vya mikononi vile, vifungulieni lakini wafuate sheria na miongozo ya serikali."

 

"Vifungulieni tusiwape mdomo wa kusema tunabinya uhuru wa vyombo vya habari, lakini mhakikishe kila mliyempa ruhusu ya kuendesha chombo cha serikali anafuata sheria za serikali na kanuni ziwe wazi, kosa hili adhabu yake ni hii na mnakwenda kwa adhabu mlizoziweka kwenye kanuni," amesema  

 

 

Katika kusisitiza hilo, Rais Samia alisema "tusifungie tu kibabe. Wafungulieni lakini tuhakikishe wanafuata kanuni na miongozo ya serikali."

 

Hata hivyo, baadhi ya vyombo vya habari vilivyofungiwa, futiwa leseni au kunyimwa leseni za uendeshaji ni MwanaHALISI, Mawio, Tanzania Daima, Mseto na televisheni ya mtandaoni ya Kwanza TV.

 

Amesema, mwisho wa mafunzo hayo ya siku tatu, yatawafanya waandishi wa habari wa mitandoni kuwa na uelewa mpana wa masuala mbalimbali ili waweze kutimiza majukumu yao kwa weledi.

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA MABALOZI WA NCHI 5 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula pamoja na Viongozi wengine kwa ajili ya kupokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Ireland hapa nchini Mary O’nell Ikulu Jijini Dar es Salaam.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Namibia hapa nchini Lebbius Taneni Tobias pamoja mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama katika picha ya kumbukumbu na Balozi wa Namibia hapa nchini Lebbius Taneni Tobias pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (kulia) mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu Jijini Dar es Salaam.


Balozi Mteule wa Namibia hapa nchini Lebbius Taneni Tobias akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo tarehe 10 Mei, 2021.

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula pamoja na Viongozi wengine kwa ajili ya kupokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Namibia hapa nchini Lebbius Taneni Tobias Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Mei, 2021.

 Balozi Mteule wa Ireland hapa nchini Mary O’nell akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo tarehe 10 Mei, 2021.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula pamoja na Viongozi wengine kwa ajili ya kupokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Ireland hapa nchini Mary O’nell Ikulu Jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama katika picha ya kumbukumbu na Balozi wa Ireland hapa nchini Mary O’nell pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (kulia) mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu Jijini Dar es Salaam.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula pamoja na Viongozi wengine kwa ajili ya kupokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Uturuki hapa nchini Dkt. Mehmet Gulluoglu mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama katika picha ya kumbukumbu na Balozi wa Uturuki hapa nchini Dkt. Mehmet Gulluoglu pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (kulia) mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu Jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama katika picha ya kumbukumbu na Balozi wa Italia hapa nchini Marco Lombardi pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula Ikulu Jijini Dar es Salaam.

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula pamoja na Viongozi wengine kwa ajili ya kupokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Msumbiji hapa nchini Ricardo Ambrosio Sampio Mtumbuída Ikulu Jijini Dar es Salaam.

   

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama katika picha ya kumbukumbu na Balozi wa Msumbiji hapa nchini Ricardo Ambrosio Sampio Mtumbuída Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula. Picha na IKULU.

Mawaziri wakubaliana kutoivunja Tume ya Kiswahili

$
0
0
NA BENNY MWAIPAJA, ARUSHA

MAWAZIRI wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekutana Jijini Arusha katika mkutano wao wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi ambapo, pamoja na mambo mengine wamekubaliana kutoivunja Tume ya Kiswahili ya Jumuiya hiyo kutokana na umuhimu wa kukuza na kutumia lugha hiyo kwa mustakabali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Uamuzi huo umetokana na msimamo wa Tanzania na nchi za Kenya na Uganda ambazo zimekataa mapendekeo ya mtaalamu mshauri aliyependekeza kuvunjwa kwa tume hiyo na kupendekeza majukumu yake yasimamiwe na Idara ya Habari, Teknolojia, Utamaduni na Michezo iliyopo Sekretarieti ya Jumuiya kwa kushirikina na nchi wanachama ili kupunguza gharama za uendeshaji wa Jumuiya hiyo.

Akichangia hoja kuhusu kuvunjwa kwa Kamisheni ya Kiswahili yenye Makao yake Makuu Zanzibar ili kupunguza gharama za uendeshaji wa Jumuiya, Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba (Mb) alisema kuwa hoja hiyo inalenga kudidimiza malengo na misingi liyopo ya kuiunganisha jumuiya na kwamba ni wakati wa kuienzi Kamisheni hiyo kwa kuifanyia mageuzi badala ya kufikiria kuivunja.

 “Tusiongelee suala la kiswahili kama lugha ya kufundishwa shuleni lakini tukione Kiswahili kama lugha inayotuunganisha kama wanajumuiya ya Afrika Mashariki” Alisisitiza Dk. Nchemba.

Aidha katika kikao hicho, Baraza la Mawaziri wa Sekta ya Fedha na Uchumi wamekubaliana na mapendekezo ya mshauri elekezi kuhusu kupunguza idadi ya wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka 9 kutoka kila nchi wanachama hadi kufikia wabunge 5 ili kupunguza gharama za uendeshaji wa Jumuiya pamoja na kuongeza ufanisi.

Katika Mkutano huo nchi wanachama ziliwasilisha miongozo na kauli mbiu za bajeti za nchi wanachama kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Mkutano huo pamoja na mambo mengine umepokea na kujadili agenda mbambali zilizowasilishwa kama vile taarifa za Kamati zinazoshughulikia masuala ya Fedha ikiwemo ile ya Makamishna Wakuu wa Mamlaka za Mapato za Nchi Wanachama pamoja na kufanya mashauriano ya awali ya Bajeti ya Mawaziri wa Fedha na masuala ya Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kadhalika, Mkutano huo umepokea Taarifa ya Utekelezezaji wa Maazimio mbalimbali yaliyofikiwa wakati wa Mkutano wa 11 wa Baraza hilo la Kisekta pamoja na taarifa ya Utafiti wa kuboresha Mifumo na Miundo ya Uendeshaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kulingana na rasilimali zilizopo.

Awali akifungua mkutano huo, Mwenyekiti ambaye ni Waziri wa Fedha wa Kenya, Ukur Yatani Kanacho alitoa, pole kwa niaba ya Mawaziri walioshiriki Mkutano huo kwa Ujumbe wa Tanzania na Serikali kwa ujumla kwa kuondokewa na Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dk. John Magufuli.

Aidha, alitoa pole kwa Nchi Wanachama kufuatia janga la ugonjwa wa Corona ambalo limeathiri uchumi wa Nchi nyingi na kuwataka wajumbe kuendelea kushirikiana kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Kadhalika kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Dk. Nchemba alipokea salamu za pole zilizotolewa na kusisitiza Nchi Wanachama kuendeleza umoja na mshikamano kama njia mojawapo ya kumuenzi Hayati Dk. Magufuli.

Mkutano wa Mawaziri umepitisha kwa kauli moja kauli mbiu ya mwaka wa fedha 2021/2022 wa Jumuiya ya Afrika Mashariki isemayo “Economic Recovery through Industralization and Inclusive Growth”.

Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano huo umewahusisha pia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uwekezaji Uchumi na Ajira Zanzibar, Mudrick Ramadhan Soraga, Waziri, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Jamal Kassim Ali,  Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Zanzibar, Dk. Juma Malik Akil, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Zanzibar, Mussa Haji Ali, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamis Shaaban na Maafisa Waandamizi kutoka Serikalini.

Mkutano huo ambao umeitishwa na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ulitanguliwa na kikao cha Ngazi ya Wataalam kutoka Sekta za Fedha na Uchumi uliofanyika kuanzia tarehe 3 hadi 5 Mei 2021 na kufuatiwa na kikao cha Makatibu Wakuu kilichofanyika Mei 6, mwaka huu.

Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC zilizoshiriki mkutano huo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na nchi ya  Sudani Kusini haijahudhuria, ambapo nchi zilizoshiriki moja kwa moja kwenye mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo Jijini Arusha ni Tanzania, Uganda na Burundi wakati walioshiriki kwa njia ya mtandao ni Kenya na Rwanda.
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>