Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

WIZARA YA AFYA YATOA MAFUNZO KWA WABUNGE KUHUSU MAGONJWA YA KIFUA KIKUU NA UKOMA

$
0
0


NA WAMJW-DODOMA


Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto leo imetoa mafunzo kwa wabunge wa Bunge la Tanzania kuhusiana na magonjwa ya Kifua Kikuu na Ukoma ili kuwajengea uwezo na uelewa kuhusu magonjwa haya mawili yanayosumbua jamii.

Akiongea wakati ufunguzi wa mafunzo hayo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amesema Wajumbe wengi wa kamati ya bunge ya masuala ya ukimwi, kifua kikuu na madawa ya kulevya waliomba na kupendekeza kuandaliwa kwa mafunzo mahususi kwa ajili ya kuongeza ufahamu wa magonjwa ya Kifua Kikuu na Ukoma.
 
Dkt. Gwajima amesema Mwaka 2006, Serikali iliitangaza rasmi ugonjwa wa TB kuwa Janga la Kitaifa ambapo mwenendo wa utekelezaji katika kudhibiti TB hapa nchini unaonesha kuwa nchi imefanikiwa katika kupunguza vifo na maambukizi mapya yatokanayo na ugonjwa wa Kifua Kikuu.

“Ripoti za Shirika la Afya duniani zinaonesha kwamba nchi yetu inafanya vizuri katika mapambano ya kudhibiti Kifua Kikuu, Pamoja na mafanikio haya bado tuna changamoto ya kumfikia kila mtanzania mwenye tatizo hili”. Amesema Dkt. Gwajima.

Aidha, Waziri Gwajima ameongeza kuwa Matibabu ya TB yanagharimiwa na Serikali katika kituo chochote cha afya bila kujali kama ni cha Umma au binafsi, mgonjwa hapashwi kutozwa malipo yoyote.

Ameendelea kusema kuwa TB inaweza kumpata mtu yoyote bila kujali jinsia, cheo, au umri na kuitaka jamii kufuata kanuni za afya ili iweze kujiepusha na maambukizi mapya.

Hata hivyo Dkt. Gwajima amesisitiza kuwa TB inatibika na kupona kabisa iwapo mgonjwa atawahishwa katika kituo cha kutolea huduma za afya, lakini endapo atacheleweshwa na kuwekwa kwenye utaratibu wa matibabu anaweza kupoteza maisha.

Kwa upande wa ugonjwa wa Ukoma, Waziri Gwajima amesema nchi yetu ilifikia kiwango cha kimataifa cha utokomezaji mnamo mwaka 2006, kwa sasa nchi imejielekeza katika mbinu na mikakati ya kukamilisha utokomezaji katika Halmashauri chache zipatazo 21 ambazo hajizifikia viwango vya utokomezaji ifikapo mwaka 2025.

Mwisho Waziri Gwajima amesema ni matarijio ya Wizara mafunzo hayo kwa wabunge  yataongeza ufahamu juu ya magonjwa haya na hivyo kuongeza chachu ya kuyatokomeza. Pia yatasaidia kuongeza hamasa katika Jamii hususani katika kupambana na ugonjwa wa Kifua Kikuu ambao bado ni tatizo kubwa nchini.


Mtafiti: Zingatia ulaji huu katika mfungo wa Ramadhani

$
0
0

NA ASHA MWAKYONDE, DAR ES SALAAM

AFISA Lishe Mtafiti kutoka  Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Fatma Mwasora amesema kuwa Kama mtu atakula futari, daku ahakikishe chakula hicho kinakuwa ni mlo kamili ambao unatokana na makundi matano ya vyakula.

Futari ni kile chakula au mlo ambao mara nyingi hutayarishwa katika kipindi cha kufunga mwezi Mtukufu wa Ramadhani  na daku ni mlo ambao hupaswa kuliwa wakati wa usiku kabla ya funga inayofuatia.

Akizungumza jijini Dar es Salaam  leo, Mwasora amesema kuwa wanasisitiza ulaji huo kwani kumekuwa na tabia katika kipindi cha mfungo wa Ramadhani watu wengi huwa wanaangalia vyakula kutoka kundi moja ambalo linahusisha vyakula aina ya nafaka na  mizizi.

Afisa huyo Mtafiti amefafanua kuwa kwenye kundi la mizizi ni viazi vitamu, mviringo mihogo  na ndizi mbichi kisayansi hilo ni kundi moja.

" Hata vile virutunishi ambavyo tunavipata vinatokana na kundi moja hivyo kusababisha hukosekana vingine vinavyotokana na makundi mengine ya vyakula," ameongeza.

Imekuwa ni mazoea kwa Waislamu katika mfungo akili yetu futari ni lazima iwe ni chakula kinachotokana na mizizi au nafaka," amesema Mwasora.

Ameongeza kuwa vyakula hivyo  mara nyingi vinapoliwa mwili hupata nishati lishe au wanga kwa ajili ya kuupatia mwili nguvu na joto tu na kukosa virutubishi toka kwenye makundi mengine.

" Vyakula hivi sisi tunaona ndio vyakula vya futari ukiangalia uji unatokana na nafaka, kwenye futari utakuta tambi wakati nayo imetoka katika kundi hilo hilo tunapata virutunishi vya aina moja vya nishati lishe, " amesema Mtafiti huyo.

Amesema kuna athari zake iwapo mtu atakula kundi moja la chakula ambavyo ni vyakula vya vinavyotokana na nafaka na mizizi tu, kwani atakosa vyakula vya aina ya Protini, vitamini na madini ambavyo ni muhimu katika kujenga mwili na kuimarisha kinga mwili.

Aidha amewataka Waislamu kula vyakula vinavyotokana na makundi yote matano ili kukamilisha mlo kamili, ambao ni vyakula vya aina ya nafaka, mizizi na ndizi mbichi, jamii ya mikunde na nyama na vile vinavyotokana na  mboga mboga na matunda na kwa kiasi  vile vinavyotokana na sukari na mafuta.

Benki ya NMB yaendesha droo ya 'Bonge la Mpango'

$
0
0

 

Meneja Mwandamizi wa Bima Benki ya NMB, Catherine Joshua akibofya kitufe kumpigia mmoja wa washindi kwenye shindano la 'Bonge la Mpango' droo ya saba iliyofanyika leo Tawi la NMB Mbezi Louis jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mkaguzi toka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Elibariki Sengasenga na Afisa Huduma kwa wateja Benki ya NMB, Neema Kazaviyo (kulia) wakishuhudia.


Meneja Mwandamizi wa Bima Benki ya NMB, Catherine Joshua akizungumza kwenye shindano la 'Bonge la Mpango' droo ya saba iliyofanyika leo Tawi la NMB Mbezi Louis jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mkaguzi toka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Elibariki Sengasenga na Afisa Huduma kwa wateja Benki ya NMB, Neema Kazaviyo (kulia) wakishuhudia.
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mbezi Louis, Nestory Mwombeki (kushoto) akizungumza kwenye shindano la 'Bonge la Mpango' droo ya saba iliyofanyika leo tawini hapo. Wa pili kushoto ni Ofisa Mkaguzi toka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Elibariki Sengasenga, Meneja Mwandamizi wa Bima Benki ya NMB, Catherine Joshua na Afisa Huduma kwa wateja Benki ya NMB, Neema Kazaviyo wakiwa kwenye hafla hiyo.
 
 
NA MWANDISHI WETU

WASHINDI 12 wa droo ya saba ya Kampeni ya Weka Akiba na Ushinde 'NMB Bonge la Mpango', inayoendeshwa na Benki ya NMB, wamepatikana leo, wakiwemo wawili waliojinyakulia pikipiki za miguu mitatu aina ya Lifan Cargo.

Droo hiyo imefanyika kwenye Tawi la Mbezi Louis jijini Dar es Salaam, ambako idadi hiyo inafanya jumla ya wateja 82 kunufaika na NMB Bonge la Mpango, wakiwemo 70 waliojinyakukia pesa taslimu (hadi wiki saba) na washindi 14 waliotwaa zawadi ya pikipiki ya miguu mitatu.

 Akizungumza kabla ya kufanyika kwa droo hiyo, Meneja Mwandamizi wa Bima wa Benki ya NMB, Catherine Joshua, amesema hadi sasa wametoa zawadi zenye thamani ya zaidi ya  Sh. Mil. 109, tangu kuanzishwa kwa NMB Bonge la Mpango - kampeni itakayotoa zawadi za Sh. Mil. 550 hadi itakapofikia ukomo.

"NMB Bonge la Mpango ni kampeni inayo hamasisha utamaduni chanya wa uwekaji akiba, ambako washindi 10 kila wiki hujishindia pesa taslimu, pamoja na pikipiki ya Lifan Cargo (mbili kila wiki), sambamba na gari dogo ya mizigo (maarufu Kama Kirikuu) katika droo za kila mwezi.

"Pia, imo zawadi kuu ambayo ni ya gari la kifahari aina ya Toyota Fortuner yenye thamani ya Sh. Mil. 169. Wito wetu kwa wateja wetu ni kuendelea kuweka akiba inayoanzia Sh. 100,000 katika akaunti zao na kwa wasio na akaunti, kufungua na kuweka akiba kuanzia kiasi hicho ili kujiwekea nafasi ya kushinda," alisema Catherine.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Elibariki Sengasenga, aliwahakikishia wateja wa NMB kuwa Bonge la Mpango ni kampeni inayoendeshwa kwa mujibu wa sheria, ikizingatia taratibu zote na kuwataka kushiriki bila hofu, kwani inafanyika chini ya usimamizi wao.

"Niko hapa kwa ajili ya kusimamia droo hii, ambako ni jukumu letu kama Bodi yenye dhamana. Niwahakikishie washiriki kuwa kampeni hii inatoa washindi kwa kufuata taratibu zote, wito wetu kwao ni kuendelea kujiwekea akiba - ambacho ni kigezo kikuu cha kupata nafasi ya kushiriki," alisema Sengasenga.

Katika droo hiyo, waliojinyakukia pesa taslimu (kiasi walichoshinda na matawi yao kwenye mabano) ni: Imelda Christopher Laizer na Annastazia George Lukinga (500,000), Marietta Kashindye Ndanshau (129,391.60), Mary  Tungucha  (300,000), Sawiya Rashid Mtawala ( 407,200 ).

Washindi wengine wa pesa taslimu wa droo ya saba ni: Joyce Massawe Edesi (298,200), Linus William Rwinwa (298,200) Jonas John Dasare (202,300) ,Bernadetha Philipo William  (304,200) na Letinga Matangi Lyama ( 104,933)

Katika droo hiyo, washindi wawili walioshinda pikipiki za Lifan Cargo walikuwa ni  EMMANUEL ENOS MWAVIPA Mkazi wa BARIADI na KIJIWE MISHKAKI.

NMB Bonge la Mpango ni kampeni ya miezi mitatu iliyozinduliwa mapema mwezi wa tatu (Machi) mwaka huu, ambako licha ya kuhamasisha utamaduni chanya wa kuweka akiba, inatumiwa pia na Benki ya NMB kurejesha kwa jamii sehemu ya faida yake ya mwaka. 

Tutasimama na wakunga kuhakikisha uzazi unakuwa baraka, furaha Tanzania – Dk. Gwajima

$
0
0

Na Catherine Sungura

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima amewahakikishia wakunga kwamba Serikali itaendelea kusimama nao vema ili waweze kutimiza majukumu yao ipasavyo katika kusimamia akina mama kujifungua salama.

Dk. Gwajima ametoa pongezi hizo mapema leo alipozungumza kupitia kipindi cha Good Morning kinachorushwa na Kituo cha Radio cha Wasafi FM, kilichokuwa na mada kuhusu Siku ya Wakunga Duniani ambayo hufanyika Mei 5, kila mwaka.

Amewapongeza wakunga na wadau wote waliofanikisha maadhimisho ya siku hiyo nchini hususan UNFPA (Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Idadi ya Watu).

“UNFPA wametuunga mkono siku zote kuhakikisha tunakwenda vizuri na agenda hii ambayo wao wanaisimamia vema kuhusu idadi ya watu duniani  na maisha bora ikiwemo masuala ya afya.

“Siku ya leo tutakuwa tunaelekeza nguvu nyingi kuangalia vipaumbele vyote vya Umoja wa Mataifa (UN) na malengo yake 17 (SDGs), lengo namba tatu linahusu watu wa afya na ustawi wa jamii yetu tunavyoihudumia.

Ameongeza “Wakunga wanafahamu siku ya leo kauli mbiu inaeleza tuongozwe na takwimu maana ndiyo eneo muhimu litatufanya tuweze kujipima kama tutafika hayo malengo ya 2030.

“Katika malengo haya ambayo tumejiwekea kwamba vifo vya uzazi vitokomezwe kabisa, isifikie kwamba mama anabeba ujauzito anakwenda kujifungua anapoteza maisha au mtoto anapoteza maisha.

“Mchezo huu unawahitaji wakunga, wao ndiyo Baraka ya kwanza kabisa ya kiumbe hai ambacho mungu amekileta duniani, nini jukumu letu tunatakiwa tuwasaidie, tuwajali, tuwaenzi, wawe na imani.

“Kwa sababu kama wakirudi nyuma kwenye hotuba ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Nchi, Samia Suluhu Hassan, alipokuja bungeni alisema kwamba mradi huu wa masuala ya kuboresha huduma za uzazi wajawazito, wazazi na watoto wasifariki ni mradi wake wa moyoni.

“Kama Rais amesema ni mradi wa moyoni na ameniamini mimi na kunipa dhamana kusimamia sekta hii mimi ndiyo nazama kabisa moyoni mwake kabisa mzima mzima,” amesisitiza.

Dk. Gwajima ameongeza “Kwa hiyo naunga na mheshimiwa Rais. kwamba na mimi mradi huu ni wa moyoni mwangu na nitahakikisha nasimama na wakunga.

“Kuhakikisha kwamba tunawekeza kuwahakikishia wana uwezo wa kitaaluma mahitaji, miundombinu wanayohitaji, dawa zote na wanafanya kazi zao vizuri kuhakikisha wanakuwa Baraka kwa mtoto huyu anayezaliwa mikononi mwao, wao wakiwa wanafungua njia ya maisha bora yenye afya na furaha kwa mtoto huyu ambaye ni Taifa la kesho,” amesema Dk. Gwajima.

JAFO: MAENDELEO YA VIWANDA YAENDE SAMBAMBA NA HIFADHI YA MAZINGIRA

$
0
0

 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akitoa maelekezo Mkurugenzi wa Kiwanda cha Lodhia Steel Industry Ltd.  Bw. Sailesh Pandit mara baada ya kufanya ziara ya kikazi Wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani.


 

Mkurugenzi wa Kiwanda cha Lodhia Steel Industry Ltd.  Bw. Sailesh Pandit akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo kuhusu shughuli za uendeshaji na hifadhi ya mazingira kiwandani hapo, Waziri Jafo hii leo amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Mkuranga kujionea uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira.

 

Na Lulu Mussa, Dar es Salaam

Serikali imesema kamwe haitakuwa kikwazo kwa wawekezaji wanaolenga kuwekeza katika sekta ya viwanda bali maendeleo ya viwanda ni lazima yaende sambamba na hifadhi ya Mazingira.

Rai hii imetolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo katika ziara ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika Kiwanda cha saruji cha Diamond na Kiwanda cha kutengeneza nondo cha Lodhia Steel Industry vilivyopo Mkuranga, Mkoa wa Pwani.

Katika ziara ya kukagua kiwanda cha Saruji Waziri Jafo ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuwachukulia hatua za kisheria wamiliki wa Kiwanda hicho kutokana na malalamiko ya wananchi juu ya uchafuzi wa mazingira kutokana na kukithiri kwa vumbi linalosababishwa na shughuli za uzalishaji wa saruji kiwandani hapo.

“Nimekuja hapa kufuatia malalamiko mengi ya wananchi na wakazi wa maeneo haya wamiliki wa kiwanda hiki wamezima mitambo yote wakijua nakuja, wamekimbia hivyo NEMC chukeni hatua mara moja, watozwe faini na nipate taarifa mapema Ofisini” Jafo alisisitiza.

Hata hivyo, Waziri Jafo ameridhishwa na uzingatiaji na utekelezaji wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 katika Kiwanda cha Lodhia Steels Industry na kuwataka wawekezaji wengine kwenye sekta ya viwanda kuiga mfano wa kiwanda hicho kwa kuhakikisha shughuli za uzalishaji zinafanyika bila kuharibu mazingira na kuhatarisha afya za binadamu na viumbe hai.

“Katika Viwanda vyote vinavyofanya shughuli ya uzalishaji wa nondo hapa nchini, kiwanda hiki ni mfano wa kuigwa katika kuhifadhi na kutunza mazingira, pia kimetoa ajira kwa watanzania wapato 700 na kuzalisha tani 200 za nondo kila siku zenye ukubwa wa milimita 8 - 40 ambazo zinatumika katika miradi ya kimkakati hapa nchini kama ujenzi wa Reli ya Kisasa, Ujenzi wa Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere pia daraja za Tanzanite” Jafo alisisitiza.

Jafo ametoa onyo kwa waharibifu wa miundombinu ya nchi kwa kigezo cha kuuza chuma chakavu na kusisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wabadhirifu wa mali ya umma.

“Serikali inatumia fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu ya reli na barabara, baadhi ya watu wanaokoteza mitaani chuma chakavu, tusipokuwa wakali tutatengeneza miundombinu na kuharibu miundombinu pia, lazima tulinde miundombinu ya Nchi” aliongezea Waziri Jafo.

Mkurugenzi wa Lodhia Steel Bw. Saileth Pandit ameiomba Serikali kufanya mabadiliko ya Sera na mikataba ya kimataifa inayozuia uingizwaji wa malighafi ya chuma chakabu kutoka nje ya nchi ili kuwezesha viwanda kupata malighafi za kutosha kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa za chuma hapa Nchini.

Benki ya CRDB yaingia mkataba wa makubaliano na NHIF kurahisisha upatikanaji wa Bima ya Afya kwa Wakulima

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akizungumza wakati wa kusaini mkataba wa makubaliano na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kurahisisha upatikanaji wa bima ya afya kwa wakulima“Ushirika Afya Premium Loan.”
 

Baadhi ya wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiwa katika uzinduzi huo.

 Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga, akizungumza katika uzinduzi huo.

 Baadhi ya maafisa na wakurugenzi wa NHIF.


Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga, akisaini mkataba wa makubaliano na Benki ya CRDB kurahisisha upatikanaji wa bima ya afya kwa wakulima“Ushirika Afya Premium Loan.”
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akisaini mkataba wa makubaliano na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kurahisisha upatikanaji wa bima ya afya kwa wakulima“Ushirika Afya Premium Loan.”

 Benki ya CRDB imesaini mkataba wa makubaliano na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kurahisisha upatikanaji wa bima ya afya kwa wakulima. 


Akizungumza katika hafla hiyo ya utiaji saini mkataba wa makubaliano, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema ushirikiano huo utawawezesha wakulima kupata bima ya afya za NHIF kwa mkopo. Katika makubaliano hayo Benki ya CRDB kupitia itakuwa ikisaidia kulipa gharama za bima ya afya (premium) na wakulima kulipa mwisho wa msimu baada ya kuuza mazao.


Akielezea taratibu za upatikanaji wa huduma hiyo ambayo imepewa jina la “Ushirika Afya Premium Loan,” Nsekela alisema huduma hiyo itatolewa kwa wakulima ambao wapo katika vyama vya ushirika huku pia ikiwanufaisha wategemezi yao, kwa maaana ya mke/ mume na watoto.


“Mkopo hutolewa kulingana na kiwango cha gharama za malipo ya bima ya afya (premium) ambapo kwa mtu mzima ni shilingi 76,800 na mtoto shilingi 50,400,” aliongezea Nsekela huku akibainisha kuwa mkopo huo wa bima ya afya utatolewa bure bila ya makato wala riba yoyote.


Aidha, kupitia huduma hiyo ya “Ushirika Afya Premium Loan,” Mkulima pia anaweza kuchukua kifurushi cha familia cha malipo ya shilingi 355,200 ambapo atapata bima ya afya kwa watu 6 (watu wazima 2, watoto 4). Nsekela alisema wamefanya hivyo ili kutoa kuhamasisha wakulima kukata bima kwa familia zao.


“Dhumuni letu ni kusaidia jitihada za Serikali kuboresha afya za Watanzania kwa kuhakikisha watanzania wote wanapata bima ya afya kama ambavyo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza,” alisema Nsekela huku akibainisha kuwa wameanza na kundi la wakulima kwasababu ndio sekta inayoajiri watu wengi zaidi nchini.


 “…ukiboresha afya ya mkulima umeboresha afya ya Tanzania. Ni Imani yangu kuwa utaratibu huu wa bima ya afya ni suluhu kubwa ya kila mkulima kuipatia kaya yake uhakika wa matibabu wakati wowote,” alisema.


Akizungumza kwenye uzinduzi wa mpango huu, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga aliweka wazi kuwa, Mfuko umejipanga kuhakikisha unawahudumia kikamilifu wakulima ili wawe na uhakika na shughuli zao za kilimo katika kipindi chote cha mwaka.


“Lengo kubwa la mpango huu ni kuwawezesha wakulima wawe na uhakika wa afya zao kwa maana ya kupata huduma za matibabu wakati wowote wanapozihitaji na kwa upande wa Mfuko tumeboresha zaidi huduma zetu ili mwanachama wetu asipate usumbufu wa aina yoyote,” alisema Konga.


Alisema kuwa endapo wakulima wataitumia fursa hiyo vizuri itawapa ufanisi katika uzalishaji mali kwani wakati wote mkulima anakuwa na amani lakini pia mapato yake yatatumika kwa maendeleo na sio kulipia huduma za matibabu.


TANNA yakabiliwa na uhaba wa Wakunga

$
0
0

 


Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila, Redemptha Matindi akizungumza na wauguzi wakati wa ufunguzi wa kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya waaguzi duniani ambayo kitaifa inatarajiwa kufanyika mkoani Manyara Mei 12 mwaka huu.

 

NA ASHA MWAKYONDE, DAR ES SALAAM

CHAMA cha Wauguzi Tanzania (TANNA), kimesema kuwa idadi ya wauguzi na wakunga bado haijafikia kiwango kinachostahili kutoa huduma stahiki  na ni changamoto inayokikabili chama hicho.

Hayo yalisema jijini Dar es Salaam jana na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila, Redemptha Matindi wakati wa ufunguzi wa kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya waaguzi duniani ambayo kitaifa inatarajiwa kufanyika mkoani Manyara Mei 12 mwaka huu.

Katika maadhimisho hayo  mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Alisema kuwa kuna  idadi  kubwa ya wastaafu ambao ni wauguzi na wakunga hali inayofanya idadi hiyo kuzidi  kupungua na kwamba ni changamoto kwa watoa huduma hao.

Matindi alisema kuna sababu nyingi ambazo zinasababisha kuanzia pale mkunga anayetengenezwa bado haijawa nzuri vyuoni na kuweza kufikia kiwango.

"Pia idadi kubwa ya wagonjwa wanaokwenda hospitali kwa wakati mmoja ikilinganishwa na idadi ndogo ya watoa huduma ya uuguzi na wakunga " alisema Matinda.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TANNA tawi la Mloganzila Wilson Fungameza ambaye ni muuguzi  alisema wameungana na wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-(MHN), ili kuweza kujadili changamoto zao kwa pamoja.

"Tupo hapa kwa ajili ya kuazimisha siku hii muhimu  ya wauguzi duniani sisi tumewahi lengo ni kujadili changamoto zetu na kuwasilisha matukio mbalimbali kabla ya Mei 12 ambapo kilele chake, "alisema.

Aliongeza kuwa mada zilizowasilishwa  zitasaidia katika kukuza taaluma uuguzi  na kwamba itasaidia kuboresha afya za wagonjwa.

Mkataba wa huduma kwa mteja wazinduliwa Dodoma

$
0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojiahiyo Dkt. Leonard Akwilapo, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mkayaba wa huduma kwa mteja uliofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Omary Kipang, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mkayaba wa huduma kwa mteja uliofanyika jijini Dodoma.

HAMIDA RAMADHANI, DODOMA


NAIBU Waziri Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga amezindua  Mkataba wa huduma kwa Mteja ambao una lengo la kuboresha utendaji kazi kwa watumishi wa wizara hiyo .

Pia amesema mkataba huo wa huduma kwa mteja utalenga hasa katika kutoa huduma kwa wateja ambao ndio wadau wakubwa wa wizara hiyo.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa  Mkataba huo leo Jijini hapa Naibu Waziri  huyo  amewaonya watumishi  wa Wizara ya hiyo watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao  kwa kufuata mkataba wa huduma kwa mteja unavyoelekeza  watachukuliwa hatua kali za kisheria.

"Niseme wazi kwa wale ambao watafanya vizuri katika kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia mkataba huo watatambuliwa kwa kupewa tuzo na kwawale wasiozingatia mkataba huo pia hatutasita kuwachuchulia hatua kali za sheria," amesema Kipanga.

Aidha amesema Mkataba huo unalenga kupunguza kama siyo kumaliza kabisa changamoto zinazoikabili wizara hiyo hivyo.

" Hivyo basi watumishi wa Wizara ya Elimu mnapaswa kuutekeleza mkataba huu wa huduma kwa mteja kwa weledi mkubwa katika kuhakikisha huduma katika wizara ya elimu zinaendelea kuboreka  ili kuiwezesha wizara yetu kujua namna ya kutatua changamoto zao," amesema Kipanga.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.Leonard Akwilapo amesema, utekelezaji wa mkataba huo ufungue  ukurasa mpya wa uwajibikaji kwa watumishi wa wizara hiyo katika kuwahudumia wananchi.

"Mkataba huo umeainisha aina za huduma zinazotolewa na wizara, wateja wanao wahudumia na viwango vya ubora kwa lengo la kuimarisha na kuboresha mahusiano yao na wateja," amesema Dkt. Akwilapo.

Awali Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara hiyo Moshi Kabengwe amesema,Mkataba huo ni chombo kinachowezesha mawasiliano mazuri kati ya mtoa huduma na anayepokea huduma.

Pia mesema pamoja na mambo mengine mktaba huo unaeleza ubora na viwango vya huduma zinazotolewa na unatoa mrejesho kutoka kwa wateja ili wizara iweze kufahamu huduma zinazotolewa kwa wateja


TIMU YA TAIFA RIADHA KUPIMA VIWANGO TULIA MARATHONI

$
0
0


Kocha wa timu ya Taifa ya riadha, Thomas John akielezea namna timu yake ilivyojiandaa kuelekea mashindao ya riadha ya Tulia Akson Mbeya City Marathoni yatakatofanyika Jumamosi Mei 8/2021 jijini Mbeya.
Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Riadha Tanzania, John Bayo akizingumzia maandalizi ya timu ya Taifa ya Riadha Tanzania.



Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Riadha wakifanya mazoezi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.


 
NA SULEIMAN MSUYA, ARUSHA

WACHEZAJI tisa wa Timu ya Taifa ya Riadha inatarajiwa kushiriki mashindano ya riadha ya Tulia Akson Mbeya City Maradhoni yanayotarajiwa kufanyika  jijini Mbeya Mei 8,2021.

Wachezaji hao tisa ni kati ya 14 waliopo kwenye kambi inayiendelea kwenye Chuo cha Misitu Olmotonyi wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Riadha Tanzania John Bayo, wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii jijini Arusha ambapo timu hiyo iliweka kambi ya mazoezi.

Bayo amesema wameamua kupeleka wachezaji hao tisa ili waweze kutumia mbio hizo kujipima kabla ya kushiriki mashindao ya riadha ya kimataifa ikiwemo Mashindano ya Olimpiki Japani.

Amesema wachezaji wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanaibuka na medani zitakazotolewa.

"Wachezaji wamejiandaa vizuri kushiriki Tulia Maradhoni imani yetu ni wao waibuke kidedea na kujiandaa na mashindano ya kimataifa," amesema.

Bayo amesema wameamua kuweka kambi ya muda mrefu ili kuandaa wakimbiaji wenye uwezo watakao wakilisha nchi vizuri.

Makamu Mwenyekiti huyo alisema shirikisho hilo linakabiliwa na ukata hivyo ameomba wadau kujitokeza ili kusaidia wachezaji.

Kuhusu faida inayopatikana kwa kuandaa marathoni mara kwa mara amesema kwa upande fulani wamenufaika kwa kupata fedha na maandalizi wachezaji.

Kwa upande wake Mwalimu wa Timu ya Taifa ya Marathoni Thomas John amesema vijana wake wamejindaa vizuri kuhakikisha wanaibuka ushindi.

Amesema wiki iliyopita walifanya jaribio ya mbio za uwanjani kwenye mita 100, 200, 500, 800, 1,500 na 5,000 hivyo ni imani yake wakiwa Mbeya wataonesha uwezo wao kwa kuibuka na ushindi.

"Tulia Akson Mbeya City Marathoni itakuwa kipimo sahihi kwa vijana wetu naomba Watanzania wajitokeze Jumamosi kushuhudia vipaji vya kukimbia," amesema.

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Wanaridhia Tanzania, Endrew Boniface amesema wao kama wachezaji wamejiandaa vizuri kutumia Tulia Akson Mbeya City Marathoni kupima viwango.

"Tumejipanga kushiriki mashindano haya kwa nguvu zote kuhakikisha tunaibuka washindi pamoja na changamoto chache amambazo zinatokea," amesema.

Boniface amesema Serikali inapaswa kusaidia wachezaji waliofikia viwango vya olimpiki ya Japani ili waendelee kujiandaa.

Pia amesema serikali inawajibu wa kuandaa wachezaji wengine ili waweze kufikia viwango vinavyohitaji.

Naye Mdau wa Riadha, Juliana Mwamsuva amesema mashindao ya Tulia Akson Mbeya City Marathoni amewataka wanariadha wanaoshiriki kujituma ili kuitangaza Tanzania kimataifa.

"Mchezo huu unalipa iwapo kila mdau ataunga mkono bila kuleta ubaguzi," amesema


Mwisho

Caption

1.Picha No.5
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Riadha wakifanya mazoezi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

2.Picha no.4 Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Riadha Tanzania, John Bayo akizingumzia maandalizi ya timu ya Taifa ya Riadha Tanzania.

3.Picha No.9

DKT. MWIGULU NCHEMBA AHIMIZA UFUGAJI WA KISASA

$
0
0

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dk. Mwigulu  Nchemba (Mb) akiongoza Mkutano kati yake na Waziri wa Mifugo na Uvuvi,  Mashimba Ndaki (Mb) na  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja (Mb), ambao pia uliwakutanisha Wataalamu kutoka Wizara hizo, jijini Dodoma.

 

NA BENNY MWAIPAJA, DODOMA 


WAZIRI wa Fedha na Mipango,  Dk. Mwigulu Nchemba, ameishauri Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kusimamia kikamilifu sekta ya mifugo kwa kubuni njia mbalimbali zitakazoongeza tija katika sekta hiyo.

Dk. Nchemba ametoa ushauri huo Jijini Dodoma, alipokutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Wizara hiyo pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii, kujadili masuala mbalimbali yanayohusu namna ya kuboresha sekta ya mifugo ili iweze kuongeza mchango katika ukuaji wa uchumi wa nchi na maendeleo ya watu.

“Tutakavyo weka mipango ya kisasa ya kukuza uzalishaji katika eneo hili la mifugo, tutatengeneza wigo mkubwa wa walipakodi, tutabadilisha maisha ya watu wetu, tutakuza uchumi na ajira,” alisema.

Dk. Nchemba alisema, kuwa maendeleo ya sekta ya viwanda yanayokwenda kwa kasi hapa nchini yanahitaji malighafi za kulisha viwanda hivyo na kwamba fursa zilizopo kwenye sekta ya mifugo ni kubwa na kushauri mbinu za kisasa za kuendeleza ufugaji ziwekwe bayana na kufanyiwa kazi ipasavyo.

Alisema utaratibu wa sasa wa wafugaji kuhamahama na mifugo kwa ajili ya kutafuta malisho na maji umepitwa na wakati na kuahidi kuwa Wizara yake iko tayari kutoa ushirikiano ili kufanikisha mipango ya kuendeleza sekta ya mifugo nchini.

Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki, alimshukuru Dk. Nchemba kwa kukutana na viongozi wa Wizara hizo mbili na kuahidi kuwa ushauri uliotolewa utafanyiwa kazi kikamilifu ambapo ameunda timu ya wataalamu kwa ajili ya kuchambua mapendekezo mbalimbali yaliyotolewa katika kikao hicho alichosema kilikuwa ni cha muhimu.

“Tutaangalia namna ya kupanua na kuwa na  maeneo maalum ya malisho ya mifugo yetu pamoja na kuboresha ufugaji ili ubadilike kutoka ufugaji wa kiasili kwenda ufugaji wa kisasa ili kuongeza tija,” alifafanua.

 Ndaki alisema, kuwa wafugaji watakaokuwa tayari kubadilisha namna ya ufugaji wao watapelekwa kwenye maeneo hayo yatakayowekewa miundombinu yote muhimu ya ufugaji ikiwemo maji na majani ya malisho.

Wakizungumza katika kikao hicho, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba, aliishauri Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuanzisha maeneo ya ufugaji (Ranch) kila mkoa na kujenga miundombinu itakayowasaidia wafugaji kufuga mifugo yao kisasa ili waweze kuongeza kipato chao, kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi na kuondokana na umasikini.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Elisante Ole-Gabriel aliiomba, Wizara ya Fedha na Mipango kuiwezesha Wizara yake kifedha kwa ajili kufanya utafiti katika sekta ya mifugo ili kuongeza mbinu za kisasa za kuongeza uzalishaji.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Allan Kijazi, alishauri kuwa ili sekta ya mifugo iweze kupiga hatua kubwa kuna umuhimu wa kutafuta masoko kwa ajili ya bidhaa za mifugo, kuongeza elimu kwa wafugaji, pamoja na kuwa na maeneo ya kimkakati ya viwanda vya kuchakata bidhaa za mifugo ni muhimu likafanyiwa kazi.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), kwenye kikao hicho Prof. Ole-Gabriel, Tanzania ni ya pili kwa kuwa na mifugo mingi barani Afrika kwa kuwa na ng’ombe milioni 33.4, mbuzi milioni 21.29, Kondoo milioni 5.65, Punda 657,380, lakini tija yake bado ni ndogo.


Wazazi, wadau, Serikali watakiwa kuwekeza kwenye riadha ya vijana

$
0
0

Muasisi wa Arusha Youth Athletic Championship, Juliana Mwamsuva akielezea kwanini ameamua kujikita katika eneo hilo la kuibua vipaji vya vijana wanaopenda riadha nchini. 

 

NA SULEIMAN MSUYA, ARUSHA


WAZAZI, wadau na Serikali wametakiwa kuwekeza kwenye mchezo wa riadha kuanzia ngazi ya chini kwa kuwa ni chanzo cha ajira.

Hayo yamesemwa na Muasisi wa Mashindano ya Arusha Youth Athletic Championship, Juliana Mwamsuva wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii.

Mwamsuva amesema ili mchezo wa riadha uweze kukuwa ni lazima kuwepo na uwekezaji kuanzia ngazi ya chini ili kupata wanariadha wengi.

Amesema wakiambiaji wenye rikodi nzuri za kimataifa mwanzo wao umeanzia ngazi ya chini hivyo familia, wadau na Serikali inapaswa kuwekeza katika eneo hilo.

Muasisi huyo amesema wazazi na familia kwa ujumla wanapaswa kubadilika kuhakikisha wanawashawishi watoto kushiriki riadha.

"Mchezo wa riadha unalipa iwapo maandalizi yataanza utotoni kwa kila mzazi na familia kuwa chachu," amesema.

Mwamsuva amesema iwapo mwamko utakuwa mkubwa wadau wengi watajitokeza kufadhili riadha nchini.

Aidha, amesema mafanikio ya Arusha Youth Athletic Championship yanawasukuma kuandaa mashindao ya vijana ya Kimataifa.

Amesema baada ya mashindano ya mwaka jana uhitaji wa washiriki kutoka mikoa mingi ni mkubwa hivyo watahakikisha hitaji hilo linapatiwa ufumbuzi kwa kuandaa mashindao yenye sura ya nchi.

WAKANDARASI ACHENI UBINAFSI UNGANENI TUWAPE KAZI- WAITARA

$
0
0

 

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Iddy Kimanta (kulia), akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mwita Waitara walipokutanamjini Arusha. 

 


Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Mwita Waitara amewataka wakandarasi nchini kuungana na kuacha chuki, ubinafsi na fitna ili wanufaike na miradi mingi ya ujenzi inayotekelezwa na Serikali.

Amesema hayo leo jijini Arusha wakati akifungua mkutano wa pili wa mashauriano wa wadau wa sekta ya ujenzi kwa mwaka 2021 ulioandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB), na kusisitiza nia ya serikali kufanya kazi na wakandarasi walioungana, waadilifu na wenye gharama nafuu.

“ Miradi mingi mikubwa ya Serikali inafanywa na wakandarasi wageni kutokana na wakandarasi wazawa kushindwa kuungana na kuitekeleza kwa ubora na kwa muda unaotakiwa”, amesema.

Serikali imejipanga kutoa kipaumbele kwa wakandarasi wazawa watakaojiunga ili kuwajengea uwezo wa kimtaji na kuwawezesha kumudu  kujenga miradi mikubwa na hivyo kubakisha fedha nyingi za miradi hiyo hapa nchini.

“Mkipewa miradi wekeni gharama nafuu na ikamilisheni kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa ili kujenga imani kwa Serikali na wananchi kuwa wakandarasi wa ndani wanaweza”, amesisitiza Waitara.

Amewataka wakandarasi kupambana na rushwa katika miradi na pale wanapoungana kuwa na nidhamu ya ushirika ili kuwezesha miradi wanayopata kukamilika kwa wakati, ubora  na kwa gharama nafuu.

Naibu Waziri Waitara amewataka wadau wa ujenzi kufanya tathmini kuhusu gharama za ujenzi nchini ili kuja na bei nafuu itakayowezesha miradi mingi ya Serikali  kufanywa na wakandarasi wazawa na hivyo kuongeza fursa za ajira na kukuza uchumi.

Naye Mwenyekiti wa CRB,  Mha. Consolatha Ngimbwa ameiomba Serikali kutumia wakandarasi waliosajiliwa ili kuwezesha ujenzi nchini kuwa wa viwango vya juu na kutoa fursa za ajira kwa watu wengi.

“ Hali ya wakandarasi nchini ni mbaya kutokana na matumizi ya force account kwenye miradi mingi ya serikali na hivyo kuwafanya wakandarasi wengi kukosa kazi amesema Mha. Ngimbwa.

Amesema CRB imewafundisha wakandarasi wake namna bora ya kutayarisha zabuni na kusimamia miradi ya ujenzi ili ikamilike kwa wakati.

“Wakandarasi tuko tayari tunaomba tupewe tujenge mji wa serikali na tulipwe kwa wakati”, amesisitiza Mha. Ngimbwa.

Naye msajili wa wakandarasi nchini Bw, Reuben Nkori ameiomba serikali iweke vituo vya kukodisha mitambo ili kuwawezesha wakandarasi kupata vifaa kwa urahisi, ipambane na rushwa katika usimamizi wa miradi na kuwalipa wakandarasi kwa wakati ili kuwezesha miradi kuwa nafuu.

Mkutano huo wa siku mbili wa mashauriano unaoongozwa na kaulimbiu “ juhudi za makusudi za wadau kuwezesha ukuaji wa wakandarasi wa ndani”, pamoja na mambo mengine utajadili na kutoka na ufumbuzi wa namna bora ya kuwezesha wakandarasi wazawa na sekta ya ujenzi nchini kukua.

Takriban wakandarasi 11,600 wamesajiliwa nchini na kati yao asilimia 3.5 ni wakutoka nje na 96.5ni wazawa ambao wako tayari kufanya kazi kwa ubora unaozingatia thamani ya fedha.


GST - WACHIMBAJI WADOGO WA WAMADINI WANACHUKUA SAMPULI ZA UCHUNGUZI KIHOLELA

$
0
0

 


Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Moses Machali akiangalia kitabu cha mwongozo wa namna bora ya
uchukuaji wa sampuli kwa ajili ya uchunguzi na uchenjuaji wa madini kilicho andaliwa na Taasisi ya
Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) mara baada ya kufungua mafunzo hayo Wilayani Masasi,

Mkoani Mtwara.

 

 

 

Na Projestus Binamungu, Idara ya Habari Maelezo

 

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) inaendesha mafunzo ya siku tatu kwa wachimbaji wadogo wa madini mkoani Mtwara juu ya namna bora ya uchukuaji wa sampuli za uchunguzi na uchenjuaji wa madini, kama sehemu ya kuwawezesha wachimbaji hao kufanya shughuli zao kisasa na kisayansi zaidi, ili kuongeza tija na mapato katika kazi yao.

 

Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Masasi,  Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Moses Machali aliwataka wachimbaji wadogo wa madini kuungana ili waweze kumudu gharama mbalimbali zinazohitajika katika shughuli za uchimbaji madini ikiwa ni pamoja na ununuzi wa vifaa vya kisasa, kupata mikopo na kumudu vipimo mbambali vya madini kabla hawajaanza kuchimba.

Alisema “Tutoke kwenye uchimbaji wa madini kama mtu na sasa tuwe kampuni, au kikundi kikubwa kinachoweza kuaminika mbele ya taasisi za fedha na hata kukopesheka kiurahisi.”

“Kuna baadhi ya wachimbaji wamechimba  madini miaka 10 mpaka 20, wengine mpaka kifo bila kuyafikia mafanikio au ndoto zao, hii kwa sehemu kubwa inatokana na kufanya uchimbaji kwa imani tu bila vipimo, jamani madini siyo uchawi wala majini, lazima tukubali kuitumia taaisi yetu  ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ili itupemie ardhi na kutufanyia tathimini ya thamani ya kilichopo chini ya ardhi tunayotaka kuichimba kabla hatujawekeza nguvu na pesa yetu” alisema Machali.

Awali akiongea kwa niaba ya wachimbaji wadogo Katibu Mkuu wa Chama cha Wachimba Madini Mkoa wa Mtwara- MTWAREMA Abdallah Esmail alisema, mafunzo hayo wanayahitaji karibia wachimbaji wote wa madini nchi nzima na kiomba GST iweke utaratibu angalau wa kutoa mafunzo hayo kila baada ya miezi mitatu ili kuwajengea uwezo zaidi wachimbaji na kuwakumbusha juu ya taratibu zinazo hitajika kufuatwa kitaalam katika uchukuaji wa sampuli.

“Tunaishukuru Serikali kwa kugharamia mafunzo ya uchukuaji wa sampuli za madini na miamba bure kwa wachimbaji wadogo hapa kwetu Mtwara, mara ya mwisho mafunzo ya aina hiyo yaliendeshwa mkoani Lindi kwenye kanda yetu ya kusini na washiriki tuligharamia shilingi laki tano, Kwakweli ahsanteni GST. Alisema Esmail

Katika mafunzo hayo yaliyowakutanisha wachimbaji wa madini zaidi ya 100 mjini Masasi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mtwara Mjiolojia Zortosy Mpangile ambaye ni mmoja wa wawezeshaji katika mafunzo hayo alisema GST imegundua wachimbaji wengi wa madini wanachukua sampuli kiholela pasipo kuzingatia taratibu za uchukuaji wa sampuli inayokwenda maabara, na kwakufanya hivyo tayari wanakuwa wameathiri majibu ya vipimo vya sampuli zao.

Mkoa wa Mtwara ni miongoni mwa mikoa yenye aina mbalimbali za madini na wataalam kutokaGST wameyainisha maeneo yenye madini katika mkoa huo kuwa ni pamoja na Lupaso, Chipite, Nanyumbu, Naugoo, Chikundi, na Mbaju.

RATIBA MAZISHI YA TEDDY MAPUNDA

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 07 Mei, 2021. (Picha na Ikulu).



NMB yaboresha bima ya faraja, yatambulisha bima ya vikundi

$
0
0


Mkuu wa Kitengo cha Bima cha Benki ya NMB, Martine Massawe akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam kuhusiana na Bima ya Maisha. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Metropolitan Life (CEO), Amani Boma na kulia ni Meneja Mkuu wa Biashara ya Makampuni Sanlam, Nura Masood. (Na Mpiga Picha Wetu).

 

Na Mwandishi Wetu

 

KWA mara nyingine Benki ya NMB imedhihirisha kauli mbiu yake kuwa ipo karibu na wateja, imekuja na maboresho ya huduma zake za bima ili kuhakikisha Watanzania wanapata faraja wakati wa matatizo.

Benki hiyo inashirikana na kampuni mbili za bima, Metropolitan Life na Sanlam Life ambapo watakuwa na utaratibu wa kutoa bima za maisha na vikundi kwa wateja na wasio wa NMB, katika kuangalia matarajio ya wateja wao baadae ikitokea hatari katika maisha yao na hivyo kusaidia malengo ya wateja kufikiwa hata kama wao hawapo au wamepata ulemavu.

Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya NMB jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Bima NMB, Martine Massawe alisema wameiboresha huduma ya bima ya NMB Faraja kwa kuongezea kiasi cha fedha kinachotolewa lakini pia kuongeza kpengele cha ulemavu wa kudumu atakaopata mteja pia atalipwa lakini pia wamekuja na hudma mpya ya bima kwa vikundi.

“”Katika kuchangia maendeleo ya bima nchini na kuisaidia serikali katika mikakati ya kuongeza idadi ya watumiaji wa huduma za bima, tumekuja na maboresho ya NMB Faraja lakini pia tuna aina mpya ya bima zitakazopatikana kwenye matawi yetu yote nchini,” alisema Massawe na kuongeza:

“Kuanzia Mei Mosi, 2021 NMB kwa kushirikiana na Sanlam tumefanya mabadiliko kwa kuongeza faida zaidi kwa wateja wetu. Mkono wa pole sasa ni mpaka Shilingi Milioni 2 kwa mteja, Sh Mil 2 kwa mwenza na pia Sh Mil 2 kwa mteja wetu atakapopata ulemavu wa kudumu. Hii ina maana kuwa unapomiliki akaunti ya NMB unapata faida ya kuwa na bima hii ya maisha na ulemavu wa kudumu (Faraja) bia gharama yoyote.”

Aidha, akizungumzia bima ya vikundi, Massawe alisema bima hiyo ni mpya sokoni ambayo itasaidia vikudi vyote ambavyo ni rasmi na visivyo rasmi: “Kikundi chochote kinaweza kuja na kukata bima na ikiwa mwanakikundi amefariki bima italipa gharama zote za mazishi ya mwanakikundi na familia yake, ikiwemo mwenza na watoto wasiozidi wanne. Mfano kikundi cha shule, Vikoba, Vikundi vya Whatsapp, Vikundi vya ukoo, vya familia na vikundi vingine vingi.”

Alibainisha, kikundi kinatakiwa kuwa na wanachama wasiopungua 10, mchango kwa mwezi upo wa aina tatu kuanzia Shilingi 500, Sh 1200 na Sh 2000 kwa kila mwanachama.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya bima ya Metropolitan Life, Amani Boma alisema wamefikiria aina hiyo ya bima ya vikundi ili kuingia kwenye viatu vya watu wengi. Kwa kuwa vipo vikundi vinachangishana fedha nyingi kwa mwaka lakini kupitia utaratibu walioshirikiana na Benki ya NMB wanachama watalipa fedha kiasi kwa huduma kubwa.

“Tumeamua kuangalia nyanja zote za maisha katika vikundi, kama tunavyofahamu kinaweza kumkuta mtu yeyote wakati wowote, unaweza kuwa hujajiandaa lakini bima hii itakusaidia. Tena tumeamua iwe inalipwa ndani ya saa 48, kwa kuwa tunafahamu wapo wanavikundi wa imani mbalimbali za dini ambao utaratibu wao wa kuzikana unatofautiana,” alisema Boma.

Naye Meneja Mkuu wa Kampuni ya bima ya Sanlam (General Manager - Corporate Business), Nura Masoud alisema wamekuwa na ushirikiano na benki ya NMB katika bima kwa miaka zaidi ya 10, hivyo anaamini maboresho haya yatawavutia zaidi wateja wao.

Katika hatua nyingine benki ya NMB imeangalia kwa jicho pana sekta ya bima nchini kuwa na mchango mdogo kwenye pat la taifa, hivyo kwa ubunifu huu itasaidia kukuza sekta ya bima na kuruhusu watu wengi zaidi wa vipato mbalimbali kuwa na bima.

WALIOWABEBESHA MIMBA WANAFUNZI KUSAKWA

$
0
0

 


Mwenyekiti wa kamati ya elimu afya na maji na diwani wa kata ya Rulanda Evart Ernest Tilwetwa.

 

Na Lydia Lugakila, Muleba

Madiwani katika Halmashauri  ya Muleba mkoani Kagera wameendelea na taarifa rasmi za kuwatafuta wahusika waliowabebesha mimba wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani humo huku watu  16 wakiwa wanasakwa na mmoja kukamatwa kwa matukio hayo.

Ikiwa jumla ya kesi 32 zimeripotiwa na mtu mmoja kutoroka, tayari kesi 3 ziko mahakamani na kesi moja imehukumiwa ambapo shule wanazotoka wanafunzi hao waliobebeshwa mimba  ni jumla ya  shule 23 zikiwemo msingi na sekondari.

Akieleza taarifa hiyo katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya muleba Evart Ernest Tilwetwa ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya elimu afya na maji  pia diwani wa kata ya Rulanda amesema kuwa kutokana na uwepo wa wimbi la wanafunzi kubeba mimba kwa shule za msingi na sekondari katika baadhi ya  wilaya mbalimbali mkoani Kagera wilaya  hiyo iliunda kamati maalum ambayo kazi yake kubwa ni kuhakikisha inafuatilia kuzuia na kudhibiti mimba shuleni, ikiwa ni pamoja na watu wanaohusika  kubebesha   mimba wanafunzi walifuatiliwa na kukamatwa na baadhi yao kupelekwa katika vyombo kisheria.

Amesema kuwa kamati hiyo ilifanikiwa kukamatwa kwa mtu mmoja na mmoja kutoroka huku 16 wakiendelea kusakwa.

Evert ameongeza kuwa, kufuatia mikakati kabambe waliyonayo madiwani hao kwa kushirikiana na wadau pamoja  wananchi wameendelea kuhamasisha na kuonyesha madhara ya mimba  idadi ya wanaobeba mimba mwaka baada ya mwaka imeendelea kupungua toka mwaka 2019 hadi Aprili 2021.

" shule za msingi kwa mwaka 2019 walibeba mimba wanafunzi 7, sekondari wanafunzi 22 jumla 29 ambapo mwaka 2020 shule za msingi walipungua hadi kufikia 5  sekondari 18 jumla yake 23 na hadi mwaka 2021 mwenzi aprili shule za msingi hakuwepo mwanafunzi hata mmoja aliyebeba mimba huku sekondari wakiwa 5" alisema diwani huyo.

Aidha amesema kuwa jitihada hizo zimeleta ufanisi mkubwa katika wilaya hiyo  licha ya ugumu huku akitaja changamoto kubwa inayosababisha kufifisha jitihada hizo  kuwa ni pamoja na wazazi wa mabinti kwani pale inapotokea mtoto kabeba mimba na wakaonekana ofisini viongozi uchukua hatua za kuwapeleka katika vyombo vya sheria,  ambapo baadae wahusika waliombebeshwa mimba mwanafunzi upita mlango wa nyuma na kukutana na wazazi wa familia ya mwanafunzi ili wakatoe chochote na kesi ipuuzwe au wakati mwingine binti anakuwa hajulikani halipo na yule aliyembebesha mimba hapatikani jambo linalosababisha ushirikiano kukosa.

Hata hivyo diwani Ernest amesema madiwani hao wataendelea kutoa elimu katika jamii ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za kuwabaini na kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wote wanaohusika na matukio hayo na kuongeza kuwa tayari wamebaini kundi la  waendesha pikipiki maarufu BODA BODA na vijana wa kawaida wenye uwezo na wamiliki wa vioski wanafanya ushawishi kubwa kwa watoto hao.

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AMSALIMIA ASKOFU PENGO NA ASKOFU RUWA'ICHI'

$
0
0

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akisalimiana na kuzungumza na Askofu Mkuu Msataafu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Kardinal Poycarp Pengo wakati alipomtembelea Ofisini kwake katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Dar es Salaam leo Mei 07,2021.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akisalimiana na kuzungumza na Askofu Mkuu wa Dar es Salaam + Jude Thaddaeus Ruwa'Ichi' wakati alipomtembelea Ofisini kwake katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Jijini Dar es Salaam leo Mei 07,2021. kulia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Bachwezi Mpango.

SIMBACHAWENE AFUNGUA KIKAO CHA BARAZA KUU LA WAFANYAKAZI, AKABIDHIWA MAKOMBE YA MEI MOSI

$
0
0

UFUNGUZI WA MAONESHO YA MAKISATU DODOMA

$
0
0

 

HAMIDA RAMADHANI, DODOMA


WAZIRI wa Elimu Sayansi na Techinologia Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia imetenga Jumla ya Shilingi Bilioni 3.2 kwaajili ya kuwaendeleza wabunifu walioshinda mashindano ya kitaifa ya kisayansi na Teknolojia (MAKISATU) 2019 mpaka 2020.


Profesa Ndalichako ameyasema hayo leo wakati akifungua Maonesho ya Mashindano ya Kisayansi,Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) yaliofanyika kitaifa Jijini Dodoma.


Aidha amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongoza na Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kutenga fedha kwaajili ya kuendeleza Ubunifu nchini kupitia vituo vya kuendeleza Teknolojia na Ubunifu.


"Niwaombe wabunifu wote nchini kujitokeza ili Ubunifu wao uweze kuonekana na uweze kutambulika msijifiche jitokezeni tuone Ubunifu kwani mkitambulika mtaendelezwa,"amesema Profesa Ndalichako.


Hata hivyo amezitaka Taasisi zinazohusika na masuala ya Teknolojia na Ubunifu nchini kuongeza kasi ya kuwatambua na kuwaendeleza wabunifu wote nchini na kuhakikisha kwamba Ubunifu wao unalindwa ipasavyo.


Amesema kwamba anatambua  kunamuongozo wakutambua wabunifu katika Halmashauri  hivyo wasimamie kuona muongozo huo unafanya kazi.


"Ninaimani kwamba tunawabunifu wengi hapa Nchini kwetu Tanzania kuliko wale ambao tumeweza kuwainua au kuwaibua katika Mashindano kama haya ya kitaifa,"amesema .


Na kuongeza kuwa " Mashindano ya kitaifa ni njia mojawapo lakini mfumo ambao tumeshautengenezea muongozo na upo katika Halmashauri tuakikishe tunausimia vizuri ili wabunifu wote waweze kutambuliwa na kuendelezwa," amesema.


Pia ameiagiza Tume ya Sayansi na Teknolojia kuhakikishe vikwazo vyote vinavyowekwa katika usajili wa bunifu za watanzania vinaondolewa ili kuwezesha Bunifu hizo zinaleta faida kwa nchi na zinafahamika kimataifa.

Amesema kuwa Serikali Pamoja na wadau kwa Pamoja wanatumia Fedha nyingi ili kuendeleza Bunifu zinazobuniwa na watanzania na Lengo lake ni kuhakikisha zinafika Mbali na kuisaidia jamii na wabunifu kwa Ujumla.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Dkt Leonard Akwilapo amesema Tangu kuazishwa kwa Mashinda no hayo ya Ubunifu, Bunifu 130 zilizoshinda zinaendelezwa na Serikali huku Bunifu 26 zikiwa zimefikia hatua ya kubiasharishwa.


Naye Mussa Dotto ni Miongoni mwa wabunifu waliopo katika Mashindano hayo ambaye ni Muhitimu kutoka chuo cha Mzumbe aliwahi kushiriki maonyesho hayo na baadae kuboresha bunifu yake ambapo amesema yupo hapo kwaajili ya kuonyesha bunifu yake na atakapo shinda atengeneze nyingine zaidi.

" Mimi niko hapa kwenye Maonesho hii ni mara yangu ya pili na nimekuja kuonyesha bunifu yangu ya gari shamba na ninaimani nitashinda na kushinda kwangu itakuwa ni mkombozi kea Mkulima wa Jembe la mkono,"amesema Mussa.

Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>