Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

TUTAONGEZA MISHAHARA MWAKANI-RAIS SAMIA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Jijini Mwanza leo tarehe 01 Mei, 2021 kwa ajili ya kuhudhuria kilele cha Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ambayo Kitaifa imefanyika mkoani Mwanza.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Wafanyakazi mbalimbali katika Kilele cha Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi Kitaifa ambazo zimefanyika Jijini Mwanza leo tarehe 01 Mei, 2021 katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.


Sehemu ya Wafanyakazi waliohudhuria kilele cha Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ambayo Kitaifa imefanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini  Mwanza. PICHA NA IKULU.


JAMII YA KIZANZIBAR YATAKIWA KUTILIA MKAZO ELIMU YA MADRASA

$
0
0

Makamu  wa Kwanza wa Rais Othman Masoud Othman ameitaka Jamii ya Kizanzibar  kutilia mkazo elimu ya Madrasa hasa Qur an  kwani ni msingi mkubwa wa mafanikio ya duniani na akhera.

Alitoa wito huo katika  mashindano ya kuhifadhi qur an huko Vitongoji Kibokoni Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba

Makamu alisema kuwa Elimu ya Madrasa ni Msingi wa maandalizi ya mtoto hasa za kiafrika kiakili, kimwili, kijamii hata kimadili.

Alieleza  kuwa suala kuhifadhisha Qur an  humsaidia mtoto katika kumjenga na  kuwatayari kusoma elimu nyengine.

Kutokana na umuhimu huo Serikali imeweka elimu ya Madrasa kuwa sehemu ya elimu ya maandalizi Visiwani Zanzibar.

alisema watoto wengi ambao hujisomea elimu hiyo wanapofika kutafuta elimu skuli huwa ni wenye kufahamu sana.

Aidha aliwata wazee kusaidiana na waalim wa Madrasa  kwa kuhakikisha watoto wanafika kwa wakatii ili kuwapatia hamu waalimu katiika kuwasomesha.

Alisema kama wazee watawabidiisha watoto wao katika kutafuta elimu hiyo basi Zanzibar itakuwa na kizazi chema baadae.

Alimuomba Allah kuwapa barka waalimu hao kwa kuwahifadhisha watoto Qur an kwa kile alichosema malipo yao watataona kesho akhera.

BODI YA MAJI BONDE LA KATI YAZINDUA JUMUIYA ZA WATUMIA MAJI BWAWA LA SONGWA NA NHUMBU MKOANI SINYANGA

$
0
0

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa  wa Shinyanga, Joackim Otaro (kulia) kwa niaba ya mkuu wa mkoa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa jumuiya za watumia maji wa Bwawa la Songwa na Nhumbu yaliyopo mkoani  Shinyanga, akikabidhi pikipiki mbili kwa  viongozi wa jumuiya hizo katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika Ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shinyanga hivi karibuni.

Mkurugenzi Bodi ya Maji Bonde la Kati, William Mabula, akizungumza katika hafla hiyo.

Viongozi wa Jumuiya ya watumia maji wa Bwawa la Nhumbu na Songwa wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na viongozi wa Bodi ya Maji ya Bonde la Kati.


Na Dotto Mwaibale, Shinyanga


WANANCHI  mkoani Shinyanga wameombwa kutumia rasilimali za maji vizuri kwa kuwa ndio tegemeo katika ustawi wa kiuchumi, kijamii na kimazingira.

Ombi hilo limetolewa hivi karibuni na Kaimu Katibu Tawala wa mkoa huo, Joackim Otaro kwa niaba ya mkuu wa mkoa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa jumuiya za watumia maji wa Bwawa la Songwa na Nhumbu yaliyopo mkoani humo.

"Ndugu zangu wana Shinyanga niwaombe tutumie rasilimali zetu za maji vizuri maana maji hayana mbadala, maji ni uhai na ndio tegemeo letu katika ustawi wa kiuchumi, kijamii na kimazingira." alisema Otaro.

Otaro alisema madhumuni ya kuzindua Jumuiya za Watumia maji wa Bwawa la Nhumbu na Bwawa la Songwa ambazo zimeundwa kwa ufadhili wa Bodi ya Maji ya Bonde la kati  kwa sheria namba 11 ya mwaka 2009 na Sera ya maji ya mwaka 2002 ni kutunza vyanzo vya maji. 

Alisema Jumuiya za watumia maji ni chombo cha chini katika ngazi ya jamii kinachoundwa kwa lengo la kuiwezesha na kuiunganisha jamii ya watumia maji wa chanzo husika kwa pamoja, ili kujadili changamoto zao na kuandaa mipango ya usimamizi na uhifadhi wa chanzo chao cha maji kwa lengo la kupunguza vitendo vya uchafuzi, uharibifu wa miundo mbinu, migogoro ya matumizi ya maji. 

"Suala la usimamizi na uhifadhi wa vyanzo vya maji ni jukumu la kila mtu si jukumu la Serikali peke yake, hivyo linahitaji nguvu ya pamoja katika kupanga na kusimamia mipango mbalimbali ya kuendeleza uhifadhi na utunzaji wa vyanzo vya maji." alisema Otaro.

Aidha,  Otaro aliongeza kuwa Bodi ya Bonde la Kati kama chombo chenye dhamana na Usimamizi wa Rasilimali kwenye eneo la bonde lake, waendelee kutoa hamasa, elimu na hata kuunda jumuiya za watumia maji kwenye maeneo mengine yenye changamoto za namna hiyo hususan katika mkoa huo wa Shinyanga na alieleza juhudi hizo walizozianzisha ziwe endelevu pamoja na kuhakikisha kuwa vyanzo vya maji vinatambuliwa, kuwekewa mipaka na kuhifadhiwa vizuri ili visiharibiwe na kuchafuliwa na shughuli zozote za kibinadamu. 

Mkurugenzi Bodi ya Maji Bonde la Kati, William Mabula alisema kuna umuhimu mkubwa mno wa jumuiya hizo kwa ajili ya kutunza vyanzo vya maji.

Alisema tukisiliza sekta ya maji inavyojadiliwa katika ngazi ya kimataifa na hata ngazi za Serikali kumekuwa na msisitizo kwenye lile tone la maji linalotoka lakini si habari ya chanzo chake na jinsi yanavyohifadhiwa.

"Serikali imeendelea kuhimiza utunzaji wa vyanzo vya maji kama tulivyomsikia hivi karibuni Rais Samia Suluhu Hassan alipokuwa akihimiza utunzaji wa vyanzo hivyo kuanzia ngazi za chini na ndio kama hizi jumuiya tulizozianzisha." alisema Mabula.

Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi, Bodi ya Maji Bonde la Kati, Nelea Bundala, alisema mchakato wa uundaji wa jumuiya hizo mbili ulianza Septemba mwaka 2020 baada ya maagizo ya kamati ya Taifa ya ufungaji migodi ya kuitaka Bodi ya maji Bonde la Kati kutembelea mabwawa yote ya Williamson na kuangalia changamoto zilizopo zinazopelekea kuharibika kwa ubora wa maji na kupungua kwa wingi wa maji. 

Alisema Bodi ilitekeleza agizo hilo na ilitembelea na kutathmini hali ya vyanzo hivyo na ilionekana kwamba kuna umuhimu wa kutoa elimu kwa watumia maji wa mabwawa hayo yote, pamoja na kuwezesha kuunda chombo cha kijamii yaani Jumuiya za watumia maji kwa Mujibu wa  sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za maji namba 11 ya mwaka 2009 inavyoelekeza. 

" Katika mchakato huo mikutano ilifanyika kila kijiji na wawakilishi wa kila kijiji walipewa mafunzo yatakayowawezesha kusimamia vyanzo hivyo vya maji vizuri." alisema Bundala.

Bundala alisema kwa Jumuiya ya Nhumbu vijiji vinavyohusika ni Mwamalili, Bushora, Songwa, Buchachi, Buganika, Mwigumbi, Seseko na Mpumbura na kwa Bwawa la Songwa jumuiya inahusisha vijiji vya Songwa, Buganika, Buchambi, Mwigumbi, Maganzo, Ikonongo na Masagala. 

Aidha Bundala alisema kuwa wawakilishi hao walitengeneza katiba ambayo ndani yake kuna sheria ndogondogo ambazo zitatumika kuzuia uharibifu mbalimbali unaoendelea katika mabwawa hayo, ikiwemo kulima karibu na mabwawa, kunywesha mifugo kiholela bwawani, uvuvi haramu, uchenjuaji madini bwawani, kuosha vyombo, kufua ndani ya vyanzo vya maji. 

Alisema mambo hayo yote yanayoharibu ubora na wingi wa maji na kuwa madhara ya uharibifu huo ni makubwa kwani kina cha maji kinapungua siku hadi siku na matokeo yake yanakua ni mafuriko. 

Katika uzinduzi huo Bodi ya Maji Bonde la Kati ilitoa pikipiki mbili aina ya Yamaha, simu za mkononi, katiba na baadhi ya vifaa vya ofisini kwa ajili ya kusaidia jumuiya hizo katika kazi  za kila siku za kutunza vyanzo vya maji.

WANAONYONYESHA WAOMBA MAREKEBISHO SHERIA YA LIKIZO

$
0
0

Mama akiwanyonyesha watoto wake mapacha  huku akiwa anafurahia na kutafakari jambo lake moyoni. 


Na Abby Nkungu, Singida


WAKATI leo dunia inaadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani maarufu kama “Mei Mosi”, wanawake waliopo kwenye utumishi wa umma na sekta binafsi wameiomba Serikali kuvifanyia marekebisho baadhi ya vipengele vya Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini ili  kutoa  haki na kukidhi mahitaji ya  kiafya kwa malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto.

Wakizungumza na Mwandishi wa Blog hii kwa nyakati tofauti, baadhi yao walisema kuwa Sheria hiyo  imekuwa kikwazo  katika utekelezaji wa  miongozo, kanuni na taratibu nyingine za kiafya;  hivyo kuathiri suala zima la malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto.

Walisema kuwa wakati miongozo ya afya inataka mtoto mchanga anyonyeshwe  maziwa ya mama pekee  kwa miezi sita mfululizo bila kumchanganyia chakula kingine, Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini inatoa siku 84 tu za likizo ya uzazi ambazo hazizidi miezi mitatu na ni hatari kiafya kwa mtoto mchanga.

“Hebu fikiria Serikali hiyo hiyo kupitia Wizara ya Afya inatutaka tunyonyeshe miezi sita mfulilizo halafu Utumishi wanatupa likizo ya miezi  mitatu tu, hii sio sawa. Ni kumnyima haki mtoto na mzazi wake lakini pia  inaweza kuathiri makuzi ya mtoto” alisema Halima John  mkazi  wa Mwenge  mjini Singida.

Neema Omari,  mkazi wa Ginnery mjini hapa alisema kutokana na siku za likizo kuwa chache huwa wanalazimika kukamua maziwa  yao na kuyahifadhi kwenye chupa ya chai ili mtoto aweze kupewa na yaya au mtu mwingine anayebaki nyumbani pindi yeye awapo kazini.

Kaimu  Mganga Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk Ernest Mugeta alisema kuwa ingawa  mtindo huo umezoeleka kwa akinamama watumishi wanaonyonyesha, njia hiyo sio sahihi kwani mbali na maziwa hayo kupungukiwa baadhi ya virutubisho yanapohamishwa kutoka kwa mama kwenda kwenye chombo kingine pia inatenganisha mahusiano mema baina  ya mama na mtoto.

“Usafi wa maziwa hayo baada ya kutoka kwenye titi la mama ni wa kutiliwa shaka. Pia, joto na ladha ya maziwa yanayotoka moja kwa moja kwenye titi la mama kwenda kwa mtoto haiwezi kulinganishwa na joto la chombo chochote cha kuhifadhia maziwa hayo… iwe chupa ya chai au vinginevyo” alieleza Dk Mugeta na kuongeza;

Kimsingi, uhusiano wa karibu wa mama na mtoto hutokana na mtoto kunyosha titi la mama, anazoea harufu ya mama na ndio maana mtoto humjua mama zaidi kuliko baba. Hivyo, inashauriwa pale inapowezekana mama apewe ruhusa ya kwenda kunyonyesha hata baada ya likizo yake ya uzazi kumalizika”.

Kutokana na hali hiyo, akinamama walisema kuwa kuna haja kwa Serikali kuvifanyia marekebisho baadhi ya vipengele vya Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini  ili kutoa muda zaidi wa likizo kwani kumruhusu mama mzazi kwenda nyumbani kunyonyesha kisha kurudi kazini inaleta usumbufu na haitekelezeki mahali pengine kama Dar es Salaam.

Kwa Mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini Namba 6 ya mwaka 2004, mtumishi hupewa siku 84 za  likizo kwa anayejifungua mtoto mmoja, siku 100 kwa anayejifungua mapacha na siku tatu kwa baba wa mtoto huyo.

Ofisa Kazi Mfawidhi mkoa wa Singida, Bibi Eunice Mmari anasisitiza kuwa likizo hiyo inatosha kwa mama kumlea mtoto na kuweka mazingira mazuri ya usalama na ulinzi wake baada ya  yeye kuanza kazi likizo inapomalizika; hiyo ikizingatia pia kutoathiri tija mahali pa kazi. 


WAFANYAKAZI SINGIDA WATAKA MASLAHI YAO YABORESHWE

$
0
0

Wafanyakazi kutoka Vitengo, Idara, Taasisi na Mashirika mbalimbali ya Umma na Binafsi kutoka wilaya zote za Mkoa wa Singida wakiingia kwa maandamano maalumu kwenye uwanjawa Liti,huku wakionesha mabango yenye jumbe mbalimbali zinazohusiana na siku ya wafanyakazi kwa mwaka huu.

Wafanyakazi wakifurahia Mei Day 2021.
Mkurugenzi waHalmashauri ya Ikungi Justice Kijazi akionesha cheti baada ya Halmashauri hiyo kuibuka mshindi kwa nafasi yaMwajiri Bora wa mwaka kupitia sherehe hizo. Kushotoni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi.
Mamlaka ya Maji  Safi na Mazingira Singida (SUWASA) wakishiriki sherehe hizo kikamilifu.
Wafanyakazi wakiimba wimbo  wa Mshikamano.

Mkuu  wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akihutubia wafanyakazi kupitia sherehe hizo zilizofanyika kwa ngazi ya mkoa.

Katibu wa TUGHE Mkoa waSingida, Ethel Kahuluda akisoma risala iliyo sheheni mafanikio, changamoto na mapendekezo ya wafanyakazi kwa niaba ya wafanyakazi wote wa mkoa.

Wafanyakazi wa Shirikalisilo la kiserikali la Maendeleo mkoani hapa SEMA wakionyesha juzi na stadi zinazotokana na matundayakazi yao, hususani kwenye eneo la karakana.


Na Dotto Mwaibale, Singida


MKUU wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi amesema tunu, fahari, tuzo na kila aina ya sifa iliyo nayo Tanzania kuanzia Awamu ya Kwanza ya uongozi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mpaka Awamu hii ya Sita chini Rais SamiaSuluhu Hassan, ni matunda ya kazi za wafanyakazi.

Nchimbi alitoa kauli hiyo wakati akihutubia sherehe za siku ya Mei Mosi kimkoa, mkoani hapa juzi, ambazo kwa mwaka huu zimebeba Kauli Mbinu isemayo ‘Maslahi Bora, Mishahara Juu-Kazi Iendelee.’ 

“Jeuri yote tuliyonayo kama taifa, msimamo, kujivunia kwetu, uwezo wa kuthubutu, kasi ya maendeleo na ukuaji wa Tanzania hii kiuchumi ni kwa-sababu ya wafanyakazi,” alisema.

Aliwasihi wafanyakazi kuitazama kizalendo na kuibeba kiuaminifu dhamana hiyo kubwa waliyonayo bila ya manung’uniko wala kubaguana kwa namna yoyote ile, lengo hasa ni kuongeza tija na ufanisi, ili kazi iendelee. 

“Niwaombe sana tunapoadhimisha Mei Mosi hii tukiri kwa umoja na pamoja kwamba popote alipo Rais wetu Samia na sisi wafanyakazi tupo...na tutamuunga mkono. Na katika hili naomba kila mmoja kwa nafasi na dhamana aliyonayo amfanye Rais wetu wa Awamu ya Sita aonekane,” alisisitiza Nchimbi na kuongeza:

Tunataka Mkoa wa Singida uwe ni nyumba ya amani kwa wafanyakazi na wanaofanyiwa kazi…nyumba ya furaha, usalama, na daima tuchape kazi ili kuonesha na kudhihirisha kweli sisi wafanyakazi wa mkoa huu ni watu ambao tunastahili maslahi bora, ili utumishi wa tija uendelee.

Awali akiwasilisha risala ya wafanyakazi mkoani hapa, pamoja na mafanikio kadhaa yaliyofikiwa chini ya Shirikisho la Vyama hivyo (TUCTA), Katibu wa TUGHE Mkoa wa Singida, Ethel Kahuluda, alieleza changamoto kadhaa zinazokwamisha ustawi wa wafanyakazi mahali pa kazi, ikiwemo suala la maslahi duni na kukosekana nyongeza ya mshahara.

Alisema changamoto nyingine ni kucheleweshwa kwa madai ya fedha za likizo, uhamisho, na malimbikizo ya mishahara sambamba na ucheleweshaji wa Pensheni  kwa wastaafu.

“Tunaomba serikali ilipe madeni ya watumishi kwa wakati ili kurudisha imani ya watumishi kwa serikali yao. Na suala hili la uhamishwaji watumishi tunaomba liendane na ulipwaji wa stahiki zao,” alisema Kahuluda.

Aidha, kwa niaba ya wafanyakazi mkoani hapa aliomba mamlaka husika kuzingatia kwa wakati suala la upandishaji wafanyakazi madaraja pamoja na marekebisho yake, sanjari na kupunguza kodi kwenye mishahara ili kuongeza ari ya utendaji.

Zaidi Kahuluda alipendekeza Waajiri wa Sekta Binafsi watoe mikataba ya kudumu, likizo na kima cha chini cha mishahara kizingatiwe kulingana na takwa la sheria No 5 ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004.

Pendekezo lingine lililowasilishwa ni kutaka ‘Mabaraza yaWafanyakazi’ yafanyike kwa wakati na malipo ya posho yatolewe kwa mujibu wa sheria na sio kwa hisani ya wakurugenzi.

Hata hivyo, waliomba pia wafanyakazi wote wanaolipwa kwa mapato ya ndani ‘GF’ walipwe mishahara yao kwa wakati na wawekwe kwenye akiba katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na wapatiwe Bima ya Afya.

“Baadhi ya waajiri hawawasilishi michango ya bima ya afya kwa wakati na hivyo kupelekea waajiriwa kujigharamia ikiwa ni sawa na kulipa mara mbili,” alisema Kahuluda.

Hata hivyo, kupitia hotuba ya kitaifa ya kilele cha sherehe za wafanyakazi kwa mwaka huu iliyotolewa na Rais Samia jijini Mwanza juzi, tayari serikali imeanza kuchukua hatua za utekelezaji, ikiwemo kushusha PAYE kutoka asilimia 9 hadi 8.

Aidha Samia alisema suala la utegemezi wa ukomo wa bima ya afya kwa umri wa watoto limeongezwa kutoka miaka 18 mpaka 21, huku akiagiza madeni yote ya watumishi yaanze kulipwa.

Kuhusu makato ya HESLB aliagiza kufutwa kwa asilimia 6 ya juu na kubakiza asilimia 15 ya mshahara, huku suala la stahiki kwa watumishi wa darasa la saba waliositishiwa ajira zao lizingatiwe.

Hata hivyo kuhusu suala la nyongeza ya mshahara wafanyakazi wametakiwa kusubiri kwanza mpaka ifikapo mwezi Mei mwakani.

DANIEL CHONGOLO NA SHAKA WATAKIDHI KIU YA WANA CCM NA WANANCHI

$
0
0

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida Dk. Denis Nyiraha.


Na Dotto Mwaibale


MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  (UVCCM) Mkoa wa  Singida,  Dkt. Denis Nyiraha amesema Katibu Mkuu wa chama hicho aliyechaguliwa juzi Daniel Chongolo na Katibu wa Itikadi na Siasa, Shaka H.Shaka kuwa ni viongozi ambao watakidhi kiu ya wana CCM na wananchi kwa ujumla.

Nyiraha aliyasema hayo juzi baada ya kumalizika kwa  mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika jijini Dodoma.

" Viongozi hawa ni wazoefu katika chama chetu na kazi zao zilikuwa zikionekana kwa kukitumikia chama chetu na Serikali hivyo kuchaguliwa kwao kutakidhi kiu za wananchi." alisema Nyiraha.

 Dkt. Nyiraha alisema kuwa viongozi hao watashusha kiu ya wananchi katika majukumu yao ya kila siku na kuongeza ari ya utendaji kwa kuwa wanauzoefu na uwezo na kuwa wamekuja wakati sahihi.

Nyiraha amewahikishia wananchi  kuwa chama kimepata viongozi sahihi chini ya Mwenyekiti wao wa Taifa Rais Samia Suluhu Hassan na akaomba wapewe ushirikiano.

NMB ILIVYOSHIRIKI MEI MOSI

$
0
0

 

 Afisa  Mkuu Rasilimali Watu wa Benki ya NMB,  Emmanuel Akonaay, akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka baada ya maadhimisho ya Mei Mosi Kitaifa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. (Na Mpiga Picha Wetu).

 

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB wakiwa katika maandamano ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza.

BASATA, BODI YA FILAMU NA COSOTA Zaagizwa Kuratibu Vyema Suala la Uhakiki wa Wasanii

$
0
0


Waziri ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Innocent Bashungwa.

 

Na Richard Mwamakafu, Arusha

 

Waziri ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Innocent Bashungwa amezitaka taasisi za Barazala la Sanaa la Taifa (BASATA) Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) na Bodi ya Filamu (TBF) kufanya uhakiki wa kazi za sanaa kwa utaratibu ambao haukwamishi kazi za wasanii nchini.

 

Mhe. Bashungwa amesema hayo Mei 02, 2021 Jijini Arusha ambapo ameeleza kuwa uhakiki unaofanywa na taasisi hizo lengo lake ni kulinda maadili kwa kuhakikisha maudhui ambayo yapo kinyume na mila na desturi za Mtanzania bila kuathiri ubunifu wa wasanii wetu, maendeleo ya sanaa nchini na kudumaza ukuaji wa ajira.

 

“Kwa upande wa filamu, uhakiki unasaidia kujua maudhui yaliyopo kwenye filamu husika ili kuamua ipangiwe daraja gani na unasaidia kuepusha maudhui mabaya ya kuharibu maadili ya jamii yetu, yadhibitiwe kabla ya kufika kwa mtazamaji/msikilizaji” amesema Waziri Bashungwa.

 

Waziri ameongeza kuwa Wizara inaendelea kupokea maoni na kukutana na wadau ikiwa ni sehemu ya namna ya kuboresha chambuzi na hoja zilizowasilishwa ambazo zitasaidia kuziunganisha BASATA, COSOTA na Bodi ya Filamu ili kuleta tija na kusimamia kazi za Sanaa na Wasanii nchini.

 

Vilevile amewasisitiza wadao ambao hawajawasilisha maoni yao, kuendelea kutoa maoni yatakayosaidia kuwa na Sheria na Kanuni zinazosimamia maudhui ya kazi za Sanaa kupitia taasisi hizo ili yasiende kinyume na mila, desturi na utamaduni wa Mtanzania. 

 


MAZAO YA KILIMO HAI YANA UHAKIKA WA SOKO

$
0
0
Sehemu ya vijana wanachama wa vikundi vya Tugende na Twiyunde vya Morogoro Vijijini wakiwa kwenye kitalu cha miche ya  mikarafuu wakati wa ziara ya watalaam wa Wizara ya Kilimo hivi karibuni.
Mkurugenzi wa SAT Bi. Janet Maro akitoa maelezo kuhusu zao la pilipili manga kwa wajumbe watoka Wizara ya Kilimo walipotembelea kikundi cha Vijana Tugende Kata ya Msufini Morogoro Vijijini hivi karibuni. Katikati ni Mratibu wa Mkakati wa Vijana kushiriki kwenye kilimo  Bw. Revelian Ngaiza.
 


Vijana nchini wameshauriwa kujikita kwenye uzalishaji wa mazao ya kilimo kwa njia ya kilimo hai kwa kutotumia kemikali hali inayowapatia uhakika wa masoko kutokana na ubora wa mazao hayo kiafya.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi wa kikundi cha vijana Tugende na Twiyunde vya  Kata ya Msufini wilaya ya Morogoro wanaolima mazao ya viungo kwa kutumia kilimo hai Mkurugenzi wa shirika la Kilimo Endelevu Janet Maro aliwahakikishia soko vijana hao.

“Bidhaa za kilimo hai zina uhakika wa soko kutokana na faida zake kiafya na pia kuwa na mwonjo mzuri unaovutia walaji  kutokana kuzalishwa bila kutumia kemikali za viwandani .SAT tutanunua mazao yenu kwa ajili ya kuongeza thamani na kuyafikisha kwa walaji ndani na nje ya nchi“ alisema Janet.

Taarifa ya vikundi hivyo iliyotolewa na Meneja miradi wa SAT Morogoro Vijijini Joel Paul ilisema tayari katika mwaka huu 2021 jumla ya tani 146 za tangawizi iliyozalishwa na vikundi kwa njia ya Kilimo hai inatarajiwa kuvunwa na kunuliwa na shirika hilo tofauti na tani 28 zilizozalishwa mwaka 2018 wakati mradi wa Kilimo cha viuongo ulipoanza.

Joel alisema vijana hao wapatao 368 katika kata ya Mkuyuni wanazalisha mazao ya viungo ikiwemo karafuu kwenye safu za milima ya Urugulu, tangawizi, mdarasini, pilipili, pilipili manga, hoho,binzari ambapo uzalishaji umeongezeka kufuatia elimu ya kilimo hai waliyopatiwa na watalaam wa shirika la SAT.

Kuhusu vikundi vingi kuwa na wasichana kuliko vijana wa kiume , Mkurugenzi huyo alisema shirika la SAT limechagua kusaidia vijana hususan wasichana wakina mama wadogo kuwafundisha kilimo hai na ujasiliamali ili wajiajili na kutunza familia zao.

Janet alisema kwa mujibu wa utafiti waliofanya ulionyesha mkoa wa Morogoro na Dodoma zina wasichana wengi waliozaa mapema na kukosa uhakika wa matunzo kwa watoto wao hivyo kupitia mradi wa Skills for Employment Tanzania (SET) unatoa fursa ya ujasiliamali, kilimo hai hususan mazao ya bustani ,mpunga na viungo.

Kwa upande wake Mratibu wa Mkakati wa Vijana Kushiriki kwenye Kilimo kutoka Wizara ya Kilimo Revelian Ngaiza aliwapongeza vijana kwa kujiunga kwenye vikundi kwa ajili ya kazi za kilimo zenye uhahika wa ajira kutokana na uhitaji wa mazao ya chakula na biashara.

Ngaiza alisema vijana ndio nguvu kazi hivyo wakitumia fursa ya uwepo wa ardhi na teknolojia rahisi ya Kilimo hai watazalisha kwa tija na kuwa na uhakika wa kipato hivyo kuzalisha ajira mbapo ndio lengo la mkakati huo.

“Serikali inapenda kuona vijana wakijiunga pamoja kwenye vikundi ili kutumia fursa ya nguvu walizonazo kuzalisha mazao ya kilimo kwa lengo la kujiajili, ndio maana kupitia halmashauri vikundi vya vijana na akina mama vinapatiwa mikopo kwa ajili ya ujasiliamali ikiwemo kazi za kilimo” alisema Ngaiza.

Shirika la SAT la Morogoro linafanya kazi ya kutekeleza mkakati wa Taifa wa Vijana kushiriki kwenye sekta ya kilimo unaotekelezwa na Wizara ya Kilimo ambapo lengo ni kuwafundisha kufanya kilimo kinachozingatia afya ya mimea, wanyama, mazingira na baionowai (Kilimo hai) na matumizi ya mbegu bora zenye kuwahakikishia mazao mengi na bora.

Waandishi wa Habari waaswa

$
0
0

NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA

KATIKA kuadhimisha siku ya uhuru wa Vyombo vya habari waandishi wa habari nchini wametakiwa kujiendeleza na  masomo, ili kuweza kukuza ufanisi wa utendaji kazi jambo ambalo litasaidia kuondoa uholela wa watu ambao hawana taaluma. 

Aidha taaluma yoyote ni lazima iwe na misingi ambayo itamuongoza mwana taaluma katika utekelezaji wa majukumu yake awepo kazini.

Akizungumza leo jijini hapa Katibu mkuu wa chama cha waandishi  wa habari mkoani Dodoma Central Press Club (CPC) Ben Bago amesema waandishi wasipojiendeleza hawawezi kuwa na Taaluma.

"Imekuwa ni mtindo kawaida kwa kila mtu ambaye anaweza kupiga picha za harusi basi naye anakuwa mwandishi jambo ambalo ni kinyume na misingi na sheria ya taaluma ya habari lakini kupitia sheria hii ya habari ya mwaka 2016 ya waandishi kurudi kusoma sheria italindwa ," .

Na kuongeza kuwa "Nikweli maslahi ni duni lakini suala zima la kujiendeleza ni muhimu ili kupunguza utitiri wa watu wasiokuwa wanataaluma kwenye tasinia ya habari," amesema Bago

Aidha akizungumzia siku ya uhuru wa vyombo vya habari amesema siku ya uhuru wa vyombo vya habari ni kioo na inapofika siku hiyo waandishi wote wanapaswa kujiangalia wapi walipotoka na wanapokwenda sasa.

Amesema lengo kubwa la kuwepo kwa siku hiyo ni kumsaidia mwandishi wa habari kuweza kutafuta habari ,kufanya habari bila kunyimwa uhuru wake.

Sambamba na hayo akizungumzia suala la baadhi ya viongozi kutotoa ushirikiano kwa waandishi mpaka wengine kufikia maamuzi ya kuwaweka ndani waandishi wa habari amesema huo ni ulevi wa madaraka.

"Mfano mzuri ni kile kitendo alichokifanya yule mkurugenzi wa halmshauri  ya Temeke ule ni ulevi kama mtu anashindwa kutoa taarifa atafute mtu ambae atakua ndio mtoa taarifa ndio maana ya uwepo wa maafisa habari "amesema Bago

Naye Ronald Sonyo mwandishi wa habari jijini hapa amesema inapoadhimishwa siku hii ya uhuru wa vyombo vya habari waajiri pia watumie  siku hii kutambua mchango wa wana habari kwa kutoa mikataba na ajira.

"Tunasema hakuna vyombo vya habari bila mwandishi wa habari,hakuna mwandishi wa habari bila vyombo vya habari na hakuna habari bila mwandishi wa habari,kwahiyo waajiri wetu tunategemeana mtujali kwenye maslahi ili mtutengenezee mazingira rafiki ya ufanyaji kazi"amesema Sonyo


Hata hivyo Chama cha Waandishi wa Habari kwa Mkoa wa Dodoma kimepanga kufanya maadhimisho hayo Mei 8 ambapo watakutana na wadau mbalimbali kuzungumzia mipango, changamoto  yanayowahusu waandishi wa habari.





MHE RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MSTAAFU WA NIGERIA MHE OLESEGUN OBASANJO IKULU CHAMWINO LEO

$
0
0

 

Rais Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Rais mstaafu wa Nigeria, Olesegun Obasanjo Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

RAIS SAMIA AZUNGUMZA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA IMF KWA NJIA YA MTANDAO

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Kristalina Georgieva, akizungumza kwa njia ya mtandano na Rais Samia Suluhu Hassan.
Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo kwa njia ya simu ya mtandao (VIDEO CONFERENCE) na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Kristalina Georgieva, Ikulu Chamwino Kleo Mei 3, 2021.

SERIKALI KUINGILIA KATI PAMBANO LA DULLA MBABE NA TWAHA KIDUKU

$
0
0


Kapteni Selemani Semunyu (kushoto) akichukua futari akifuatiwa na katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dk Hassan Abbas na Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam wakati wa Ftari ya Mabondia Jana Jijini Dar es Salaam. 


Baadhi ya wadau wa Mchezo wa Ngumi waliohudhuria  Ftari ya Mabondia iliyoandaliwa na kapteni Selemani Semunyu kwa ajili ya mabondia wakifuatilia matukio katika ukumbi wa JWTZ 361 Mwenge Jana Jijini Dar es Salaam.  




Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dk Hassan Abbas (katikati) akizungumza na Kapteni Selemani Semunyu ( Wakwanza kulia) na Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Musa ( wakwanza  kushoto)  juu katiaki ni Bondia Dulla Mbabe wakati wa Ftari ya Mabondia Jana Jijini Dar es Salaam. 


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dk Hassan Abbas (katikati) akiwa katika Picha ya pamoja na Baadhi ya wadau wa Mchezo wa Ngumi waliohudhuria  Ftari ya Mabondia iliyoandaliwa na kapteni Selemani Semunyu Jana Jijini Dar es Salaam. 


 

 Na Mwandishi Wetu


SERIKALI imeahidi kutoa ushirikia kufanikisha Pambano la Masumbwi kati ya Mabondia Mahiri Nchini Twaha Kiduku na Dulla Mbabe litakalofanyika Julai 24, 2021 Jijini Dar es Salaam.


Hayo yalisemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dk Hassan Abbas wakati wa Futari kwa Mabondia iliyoandaliwa na Wakala wa Michezo wa PeakTime jijini Lugalo Jijini Dar es Salaam.

" hili tunalibeba hakuna kusubiri na natoa wito kwa wadhamini kujitokea kutumia nafasi hii kujitangaza kwa kuleta maslahi kwa washiri. Alisema Dk. Abbas.

Aliongeza kuwa mbali na kutoa ushirikiano pia aliahidi kufikisha ombi kwa Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa kuwa mgeni rasmi katika pambano hilo.

Kwa upande Mwingine alisema wameanza kutenga fedha kidogo kidogo ili kusaidi wanamichezo wanaosafiri nje ya nchi kuwakilisha Taifa.

 Upande wake Mwakilishi wa Peaktime walioandaa Futari hiyo Kapteni Selemani Semunyu alisema maandalizi kuelekea Pambano hilo yako sawa na uwepo wa Waziri mkuu utaupa hadhi mchezo na kufungua fursa nyingi kwa wachezaji ambao wengi hutoka familia duni.

Tunaendelea kutafuta Wadhamini ili ikifanikiwa Waziri Mkuu aje kukabidhi gari zawadi ambayo tunaamini itakuwa chachu katika Mchezo huo na tunaamini wadhamini watajitokeza. Alisema Kapten Semunyu.

Kwa Upande wake Mwakilishi wa
Kamisheni ya Kusimamia ngumi za kulipwa Tanzania TPBRC Yahaya Poli ameipongeza Peaktime na kuwaomba wadau wengine kuiga mfano huo kwani unaipa heshima tasnia.

Kwa upande wake Mwakilisho wa Mabondia Hussuen Itaba alisema hatua kubwa sasa imefikiwa katika mchezo wa Ngumi na Kuitaka peaktime kuendeleza ilikofikia.

Mmoja wa Wadhamini wa Iftari hiyo Peter Kinabo kutoka Euromax alisema Majukumu ya Kijamii ni matukio muhimu yanayotakiwa kuendelezwa nao Eoroma wameamua kusaidia katika Ngumi.


Rais Samia Suluhu Hassan awasili nchini Kenya

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya kwa ajili ya ziara ya siku mbili. 

Mtafiti: Zinagatia ulaji huu katika mfungo wa Ramadhani

$
0
0

NA ASHA MWAKYONDE, DAR ES SALAAM

AFISA Lishe Mtafiti kutoka  Taasisi ya Lishe na Chakula Tanzania (TFNC), Fatuma Mwasora amesema kuwa Kama mtu atakula futari, daku nikuhakikisha chakula hicho kinakuwa ni mlo kamili ambao unatokana na makundi matano ya vyakula.

Futari ni kile chakula au mlo ambao mara nyingi hutayarishwa katika kipindi cha kufunga mwezi Mtukufu wa Ramadhani  na daku ni mlo ambao hupaswa kuliwa wakati wa usiku kabla ya funga inayofuatia.

Akizungumza jijini Dar es Salaam  leo, Mwasora amesema kuwa wanasisitiza ulaji huo kwani kumekuwa na tabia katika kipindi cha mfungo wa Ramadhani watu wengi huwa wanaangalia vyakula kutoka kundi moja ambalo linahusisha nafaka na  mizizi.

Afisa huyo Mtafiti amefafanua kuwa kwenya kundi la mizizi ni viazi vitamu, mviringo mihogo  na ndizi mbichi kisayansi hilo ni kundi moja.

" Hata vile virutunishi ambavyo tunavipata vinatokana na kundi moja hivyo hukosekana vingine vinavyotokana na makundi mengine ya vyakula," ameongeza.

Imekuwa ni mazoea kwa Waislamu katika mfungo akili yetu futari ni chakula kinachotokana na mizizi au nafaka," amesema Mwasora.

Ameongeza kuwa vyakula hivyo  mara nyingi vinapoliwa mwili hupata nishati lishe au wanga kwa ajili ya kuupatia mwili nguvu na joto.

" Vyakula hivi sisi tunaona ndio vyakula vya futari ukiangalia uji unatokana na nafaka, jwenye futari utakuta tambi wakati nayo imetoka katika kundi hilo hilo tunapata virutunishi vya aina moja vya nishati lishe, " amesema Mtafiti huyo.

Amesema kuwa athari zake Kama mtu atakula kundi moja la chakula ambavyo ni vyakula vya vinavyotokana na nafaka na mizizi atakosa vyakula vya aina ya Protini.

Aidha amewataka Waislamu kula vyakula vinavyotokana na makundi matano ili kukamilisha mlo ambayo ni  nafaka na mizia, nyama na vile vinavyotokana na jamii ya mikunde, mboga mboga, matunda na vile vinavyotokana na sukari.


Prof. Mkumbo: nimefurahishwa na utendaji wa TBS

$
0
0

 


Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo. (Picha na Eliud Rwechungura).

 

 

NA ASHA MWAKYONDE, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limepongezwa kwa kasi ya utendaji kazi wa kuhakikisha bidhaa zinazoingia kutoka nje ya nchi na zile zinazozalishwa nchini zinakuwa na ubora unaokubalika.

Haya yamesemwa jijini Dar es Salaam jana, na Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo wakati alipotembelea Shirika hilo, halina rekodi ya bidhaa ambayo hazifai kwa matumizi ya binadamu.

Prof. Mkumbo alisema kwa hali hiyo inamaanisha kwamba kuna wafanyakazi wanadhibiti uingizwaji wa bidhaaa za kutoka nje ya nchi na zinazozaliehwa hapa nchini.

Alisema shirika hilo linatekeleza mambo yake vizuri na kuahaidi kulipatia  ushirikiano kuona kwamba  linanafasi nyingine za kushiriki kikamilifu katika kuwezesha biashara ndani ya Sheria zilizopo katika ubora unaotakiwa na serikali.

"Nawapongeza TBS kwa kazi Nzuri waliyofanya za  kuhakikisha bidhaa zinazoingia kutoka nje na ambazo zinazalishwa  hapa zinazingatia Ubora  hivyo mafanikio yao ni makubwa hapa nchini,"alisema.

Aliongeza kuwa baada ya kukutana na wafanyabiashara leo (jana), pale Bandarini TBS ilitajwa kwa uchace  katika malalamiko yao na kwamba hatua hiyo ilintia moyo kwa kuona wanafanyakazi nzuri.

Alisema wamekubaliana na TBS kuongeza Bodi katika kuhakikisha mnafanya kazi kwa spidi kubwa ili wafanyabiashara wanaofanya biashara waweze kulewa huduma mapema iwezekanavyo.

"Nimewasisitiza watu wa TBS umuhimu wa huduma bora kwa wateja kwa kuwa wanafanya kazi na wafanyabiashara ni muhimu kuboresha huduma kwa wateja hilo ni jambo la Msingi,"alisema.

Aidha aliaidi kuyafanyia kazi kwa haraka iwezekanavyo mambo mawili yanayohusu Shirika hilo ikiwemo suala la uundwaji wa  bodi ya wakurugenzi na kuhakikisha wanafanya marekebisho ya Sheria mapema ambayo unahitajika kuboresha utendaji kazi.

Benki ya Stanbic yashiriki hafla ya futari iliyoandaliwa na Silent Ocean kwa ajili ya wafanyabiashara

$
0
0

 

Maneja wa Benki ya Stanbic Tawi la Kariakoo, Said Saleh, akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na kampuni ya Silent Ocean kwaajili ya wateja wao iliyofanyika Dar es Salaam jana. Benki ya Stanbic ilithibitisha kuongeza ushirikiano na Kampuni ya Silent Ocean ili kuwawezesha wafanyabiashara nchini. 
Baadhi ya wadau walioshiriki hafla ya futari iliyoandaliwa na Kampuni ya Silent Ocean.

NMB yaandaa kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu Zanzibar

$
0
0

Mapokezi ya Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Lela Mohamed Mussa (kushoto) aliyefungua kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Lela Mohamed Mussa akifungua kongamano la wanafunzi wa vuo vikuu lililofanyika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein, Tunguu Zanzibar mwishoni mwa wiki. 

Beatrice Mwambije wa NMB (kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri Lela (kulia).
Ofisa wa NMB, Hesbon Mpate (kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Utalii na mambo ya kale, Lela Mohamed Mussa (wa pili kulia).
Picha ya pamoja kati ya Waziri (wa tano kulia) na maofisa wa benki ya NMB baada ya ufunguzi wa kongamano mwishoni mwa wiki.

 

Na Mwandishi Wetu

 

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Leila Muhammed Mussa amewataka wanafunzi wa vyuo vikuu kisiwani humo kuzitumia fursa zinazotolewa na Benki ya NMB ili kujenga msingi mzuri wa kuweza kujiajiri na kuajiriwa pindi wanapomaliza masomo yao.

Aliyasema hayo alipokuwa akifungua kongamano la kusaidia safari ya wanafunzi mbalimbali wa vyuo vikuu katika kufikia malengo yao katika kutafuta fursa za kujiajiri na kuajiriwa pindi wanaomaliza masomo “NMB Career fair”  lililofanyika katika ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein wa chuo kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA mwishoni mwa wiki.

“Wanafunzi wengi wanaohitimu vyuo wanashindwa kuzitumia taaluma zao hivyo kupitia kongamano hili itawasaidia vijana hawa kuzifikia fursa za ajira na kujiongezea ujuzi ambao watautumia katika majukumu yao ya kazi,” alisema Mhe. Leila

Pia amewaomba waandalizi wa kongamano hilo benki ya NMB kuangalia uwezekano wa kuwasaidia wanafunzi wanaomaliza elimu ya sekondari kwani wengi wao wanapomaliza masomo hawajui masomo ya kuchukua ambayo yatawasaidia kukamilisha ndoto zao za baadae.

“Serikali ya awamu ya nane ipo tayari kushirikiana na taasisi mbalimbali zinazolenga kuwasaidia vijana hususani katika mbinu za kuwasaidia kupata ajira ili kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira nchini,” alisema Mhe. Leila.

Naye, Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya NMB, Juma Kimori amesema lengo la kuwakutanisha wanafunzi hao ni kuwapa mbinu mbadala za kutambua fursa za kuweza  kujiajiri na kuajiriwa ambazo watazitumia pindi watapomaliza masomo yao.

Amesema mbali na hilo pia NMB inaunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya 8 chini ya Rais Dkt Mwinyi ambayo imelenga kutengezeza fursa za ajira laki tatu, hivyo kupitia taaluma hiyo itawasaidia vijana kupata ujuzi wa kuzifikia ajira hizo.

Kwa upande wake Rais wa asasi ya vijana ya AIESEC, Michael Chacha amesema asasi yao imekuwa ikiwasaidia vijana mbalimbali kwa kuwajengea uwezo ili kubadilisha mitazamo na fikra zao hivyo wataendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali ili kuona vijana wanasaidiwa na wanaondokana na dhana ya  kusubiri ajira serikalini.

Nao baadhi ya wanafunzi waliopatiwa taaluma katika kongamano hilo la “NMB Career fair” wameipongeza benki ya NMB kwa kuwapatia mbinu ambayo itawasaidia kujiajiri na kuondokana na kusubiri kuajiriwa.

Zaidi ya wanafunzi elfu 1000 kutoka vyuo vikuu mbalimbali vya Zanzibar wameshiriki katika kongamano hilo.

RC NDIKILO AKUTANA NA UGENI WA WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI KWA AJILI YA UJENZI WA VIWANDA 200

$
0
0

 

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi  Evarist Ndikilo wa kati kati aliyenyoosha mikono akizungumza na baadhi ya  wawakilishi (Delegation) kutoka Chemba ya Wafanyabiashara wa China Tanzania (Chinese Business Chamber in Tanzania) kwa ajili ya kujadili mambo mbali mbali ikiwemo kupanga mikakati ya ujenzi wa viwanda katika Mkoa huo.

Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Pwani wakiwa katika kikao hicho cha pamoja na Wawakilishi (Delegation) kutoka Chemba ya Wafanyabiashara wa Kichina Tanzania (Chinese Business Chamber in Tanzania) ambao walifika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kupata ardhi kwa ajili ya ujenzi uwekezaji wa viwanda. 

 

NA VICTOR MASANGU, PWANI

 

SERIKALI ya Mkoa wa Pwani katika kuhakikisha inatekeleza kwa vitendo  azma ya kuwa na uchumi wa viwanda na kuwapa fursa wawekezaji  wa ndani na nje ya nchi imekutana na baadhi Wawakilishi (Delegation) kutoka Chemba ya Wafanyabiashara wa Kichina Tanzania (Chinese Business Chamber in Tanzania) kwa lengo la kujadili na kupanga mikakati ya kupata ardhi kwa ajili ya ujenzi wa viwanda.

Katika kikao hicho ambacho kiliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani na kuhudhuliwa na baadhi ya viongozi mbali mbali wa Mkoa lengo ikiwa ni kufanya mazungumzo na wawakilishi hao kwa ambayo yataweza kuleta mabadiliko chanya  ya kimaendeleo kupitia sekta ya uwekezaji wa viwanda mbali mbali ambavyo vikikamilika vitaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi katika  kutoa fursa za ajira na kukuza uchumi.

 Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo alibainisha kwamba lengo kubwa la ujio wa wawakilishi hao ni kuweza  kutafuta eneo la ardhi kwa ajili ya Ujenzi wa Viwanda ikiwa ni kutekeleza maombi waliyowasilisha kwa Mhe Rais walipokutana na kufanya mazungumzo Aprili, 21 mwaka  2021.

 

“Tumepokea ugeni huu  na katika mazungumzo yao ujumbe huo umekuja kwa lengo kutafuta Ardhi kwa ajili ya Ujenzi wa Viwanda ikiwa ni kutekeleza maombi waliyowasilisha kwa Mhe Rais walipokutana na kufanya mazungumzo hivi karibuni kwa hiyo sisi kama Mkoa wa Pwani suala hili tutalifanyia kazi ili kuwapatia ardhi ya kujenga viwanda,”alisema Ndikilo.

Aidha katika hatua nyingine  Ndikilo  amewatoa hofu kwa kuwahakikishia wawakilishi hao wa wafanyabiashara kuwa Mkoa  bado una maeneo ambayo tayari yametengwa  maalumu kwa ajili ya Ujenzi wa Viwanda hivyo watahakikisha wanawapa ushirikiano wa kutosha katika kila hatu ili waweze kutimiza malengo waliyojiwekea,


Pia Ndikilo  amependekeza  kwa Wawekezaji hao kuwekeza  kwenye eneo la Kwala ambalo Jumla ya Hekta 500 wanazohitaji zitapatikana, na kuwaeleza kuwa  eneo la Kwala linafaa kwa Uwekezaji huo wa ujenzi wa Viwanda (Industrial Park).

Katika hatua nyingine alifafanua kuwa katika eneo la Kwala kwa sasa lina Miundombinu mbinu yote Muhimu ikiwemo, Maji ya uhakika, Barabara, Umeme wa uhakika ukaribu na Bandari kavu, ukaribu wa Reli ya Mwendokasi, na ukaribu na Jiji la Dar es salaam.

Wawekezaji hao wakiongozwa na Bw. Janson Huang  wameeleza kuwa wanategemea kujenga na kuanzisha viwanda  zaidi ya 200 vya kuzalisha bidhaa mbali ikiwemo madawa, Kuunganishia pikiki, Viyoyozi, simu za mikononi  hivyo hitaji lao la kwanza ni Ardhi ila waendelee na michakato mingine ya Uwekezaji

                                                   

WIZARA YA AFYA YAANZA KUTEKELEZA KWA KASI MAELEKEZO YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN KATIKA SEKTA YA AFYA NCHINI

$
0
0


Na Jasmine Shamwepu, Dodoma


Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeanza kutekeleza kwa kasi maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ikiwa ni sehemu ya maboresho ya utoaji huduma katika Sekta ya Afya.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya - Idara Kuu Afya Prof. Abel Makubi
(pichani) katika kikao na Watumishi wa Idara Kuu ya Afya Makao Makuu kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.

Katika kutekeleza maagizo hayo Prof. Makubi amesema kuwa, Wizara inategemea kuwasilisha Bungeni mchakato wa kuridhiwa kwa Bima ya Afya kwa wote ili uweze kupitishwa na kuwezesha wananchi wote kuwa na Bima ya Afya hali itakayosaidia kupunguza gharama za matibabu kwa wananchi wote.

"80% ya Watanzania ni watoto wa wakulima, Wizara imepeleka mchakato huu haraka bungeni ili uweze kupitishwa, ambapo utasaidia wananchi wote kuwa na Bima ya Afya, jambo litalosaidia kupunguza gharama za matibabu kwa wananchi," amesema Prof. Makubi.

Aliendelea kusema kuwa, Serikali inaendelea kuweka mikakati mizuri itayosaidia wananchi ambao hawatakuwa na uwezo wa kulipa kiasi hicho ili kupata Bima ya Afya kwa kutafuta vyanzo vingine vya fedha ili kuwalipia huduma hiyo.

Hata hivyo, Prof. Makubi amesema kuwa, katika miaka mitano iliyopita Serikali imejenga vituo vya kutolea huduma za Afya vya kutosha ikiwemo Hospitali za Kanda, Hospitali za Wilaya, Hospitali za Rufaa za Mikoa, Vituo vya Afya na Zahanati, na hivyo katika kutekeleza agizo hilo amesema Wizara inaendelea kuhakikisha maboma yote yanakamilika na kuanza kutoa huduma za Afya kwa wananchi kwa kiasi kidogo cha fedha ndani ya miundombinu yenye ubora.

Kwa upande mwingine amesema kuwa, licha ya malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya hali ya upatikanaji wa dawa kutoridhisha nchini, Wizara ya imepokea jumla ya Tzs.Bilioni 80 kutoka Serikalini ili kuboresha hali ya upatikanaji wa dawa kwa wananchi. Ameonya kuwa Serikalini haitakubali kuona fedha hizi zinatumiwa vibaya au dawa kuibiwa katika vituo vya kutolea huduma.

Aliendelea kusema kuwa, katika kuimarisha zaidi eneo hilo, Wizara imekutana na Wazabuni ili kuendelea kuimarisha hali ya upatikanaji wa dawa, jambo litalosaidia kupunguza changamoto za malalamiko yanayotokana na ufinyu wa huduma za dawa katika vituo vya kutolea huduma.

Kuhusu masilahi ya watumishi, Profesa Makubi alisisitiza maelekezo ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha “motivations” zinatolewa , hasa kwa kazi nzuri zinazofanyika. Ameelekeza Taasisi zote chini ya Sekta ya Afya kuwa na moyo wa shukurani na pongezi kwa watumishi wanaojituma kupitia haki zao, mapato ya ndani, na miradi mbalimbali pale ambapo miongozo inaruhusu .

Aidha, Prof. Makubi amesema kuwa, moja kati ya kipaumbele cha Wizara ya Afya ni kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kuleta kiumbe kipya Duniani, hivyo kuwataka Watumishi wa Wizara ya Afya kwa kushirikiana na OR TAMISEMI kusimamia huduma bora ili kupunguza vifo hivyo ikiwezekana kuviondoa kabisa.

"Ni wajibu wetu kupunguza vifo vya mama na mtoto, naomba hili tulisimamie wote, nisingependa kuona vifo vya mama, wakati analeta kiumbe kipya Duniani," alisema Prof. Abel Makubi.

Kwa upande mwingine, Prof. Makubi amesema kuwa, Wizara imeendelea kuhamasisha wananchi kushiriki katika mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza kwa kuboresha mtindo wa maisha ikiwemo kufanya mazoezi, kula mlo unaofaa na kupata elimu juu ya kujikinga dhidi ya magonjwa hayo.

Aliendelea kwa kutoa maelekezo ya kuongeza kasi katika kutoa elimu kwa wananchi hususan watoto ili kujenga tabia ya kupenda kufanya mazoezi na kufuata mlo kamili, huku akiwaasa Watumishi wa Afya kuwa mstari wa mbele kwa kufanya mazoezi na kutoa elimu kwa wananchi.

Aliendelea kwa kuwapongeza Watumishi wote wa Sekta ya Afya kwa namna walivyoshiriki katika mapambano dhidi ya magonjwa ya kuambukiza ikiwemo magonjwa ya mlipuko kama vile ugonjwa wa Corona, huku akiwataka kuendelea kujikinga dhidi ya ugonjwa huo kwa kuchukua tahadhari zote muhimu kama kunawa mikono kwa sabuni na maji safi yanayotiririka, kuvaa barakoa pale panapohitajika na kuepuka msongamano isiyo ya ulazima.

Hata hivyo, Prof. Makubi amesisitiza juu ya kuongeza kasi katika kuboresha huduma za tiba asili, huku akielekeza kuwa na kituo cha Kisasa cha Tiba Asili kitachorahisisha shughuli zote ikiwemo tafiti kuhusu tiba asili na kuweka wazi kuwa dawa za tiba asili ziweze kupatikana katika maduka ya dawa (famasi).

Huduma kwa wateja, ni sehemu nyingine ambayo Prof. Makubi amesisitiza iongeze kasi kwa Watumishi, huku akielekeza Huduma kwa Wateja (Customer Care) zianze kutolewa kwa wateja mara wanapoingia getini au mlango mkuu mpaka wanapomaliza kupokea huduma na kuondoka.

"Huduma nzuri kwa wateja zianze kwetu ndani ya Wizara, wageni wapokelewe vizuri kuanzia getini, hatupendi kusikia malalamiko ya watu hawajapokelewa vizuri, wote tuna nafasi ya kupokea na kuwasikiliza wateja pindi wanapokuja kuhitaji huduma," amesema.

Pia, Prof. Makubi ameagiza kuongezeka kwa kasi ya kushughulikia kero kutoka kwa wananchi ili waweze kupata huduma kwa haraka, aliendelea kusema kuwa kila mtumishi kwa nafasi yake ahakikishe anashughulikia kero za wananchi ili zisifike ngazi ya viongozi wa juu.  

Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>