Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

MTOTO WA SHILOLE APATA DARAJA LA KWANZA KIDATO CHA NNE

$
0
0
Na Mwandishi Wetu


Mwanamuziki na mjasiriamali kutoka nchini Tanzania Zuwena Mohammed maarufu kama Shilole, ameonyesha furaha baada ya binti yake wa kwanza Joyce kufaulu vizuri katika mtihani wake wa kuhitimu kidato cha nne.

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Shilole ameandika “ Mwenyenzi Mungu asante, leo ni kati ya siku nilizowahi kuwa katika kiwango cha juu kabisa cha furaha na shukrani kwa Allah: MUNGU AMENITENDEA WEMA.

 

Mimi kama binti mwingine yeyote, nilikuwa na ndoto za kufanya vizuri shuleni lakini sikuwahi kufanikiwa katika hilo, njia yangu ilikuwa na miiba na mapito mengi, sifahamu hata cheti cha darasa la 7 kinaonekana vipi. Nilipokosa hayo nikaapa, nikamuomba Mungu na kuwekeza nguvu zangu kuhakikisha watoto wangu wanapita kwenye ile njia ambayo mimi sikuweza.

 

Joyce kama mtoto wangu wa kwanza ambaye kuzaliwa na kukuwa kwake kulikuwa kwa tabu zaidi, ninamuombea usiku na mchana aje kupita katika hizi njia za kisomi na kuwa mwanamke niliyewahi kuota. Mungu anaanza kujibu:

 

MWANANGU AMEFAULU VIZURI SANA, NIMEAMBIWA KAPATA ‘DIVISION ONE (1) YA POINT 16.

 

Nimelia, nimecheka, nimesimama, nimekaa ninamshukuru Mungu, nimshukuru binti yangu kwa kuendelea kunitoa aibu. I am proud of her. Nakupongeza sana mwanangu, nakupenda na kukuombea mafanikio zaidi, safari yako ndio kwanza inaanza. Allah azidi kukujalia.

 

Nawashukuru sana waalimu na wafanyakazi wa St.Christina kule Tanga, nawashukuru na kuwapongeza wanafunzi wote walioshirikiana na mwanangu kwenye masomo na Maisha ya shule”. Ameandika Shilole.

 

Aidha Shilole amewashukuru wateja wake wa shishifood na mashabiki wake wa muziki wanaomuwezesha na kupata fedha za kuwasomesha watoto wake.


AWESO KUWAONDOLEA KERO YA UPATIKANAJI WA MAJI WANANCHI WA WILAYA YA KIBITI

$
0
0


 Waziri wa Maji Juma aweso akiwa katika moja ya ziara zake za kikazi kwa ajili ya kuweza kuzungumza na viongozi mbali mbali wa serikali wataalamu wa maji pamoja na wakandarasi kwa lengo la kujadili jinsi ya kuweza kuwaboreshea huduma ya maji wananchi.

 

 

 NA VICTOR MASANGU,PWANI 

 

Waziri wa maji Juma Aweso ameahidi kulivalia njuga  changamoto ya baadhi ya wafugaji wenye tabia ya kutitisha mifugo yao katika vyanzo mbali mbali vya maji kwani kufanya hivyo kunasababisha   kuchafua maji  ambayo  yanatumiwa na binadamu hivyo kunaweza  kuhatarisha usalama wa afya za wananchi na kuibuka kwa mlipuko wa magonjwa.

Aweso aliyasema  wakati wa ziara yake ya kikazi katika wilaya mbali mbali za  Mkoani Pwani  kwa lengo la kuweza kuzungumza na watendaji, viongozi wa serikali, wakandarasi  pamoja na kutembelea miradi mbali mbali ya maji ambayo inasimamiwa na Dawasa pamoja na Ruwasa ili kuweza kujionea shughuli zinazofanyika na kubaini changamoto zilizopo iloi kuweza kuzitafutia ufumbuzi hasa katika maeneo yaliyopo vijijini.

Pia aliongeza kwamba serikali ya wamu ya tano lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba inawasaidia wananchi   kuondokana  na  changamoto  ya  kutembea umbari mrefu kwa ajili ya kwenda kutafuta maji katika maeneo mengine kwa kuboresha huduma za maji pamoja na kuchimba visima.

“Serikali ya awamu ya tano nia yake kubwa ni kuboresha huduma ya maji safi na salama katika maeneo mbali mbali hususan ya vijijini, ili waweze kupata fursa ya kuweza kuchota maji kwa urahisi kutokana na huduma hiyo kuwepo karibu kwa hivyo jitihada kubwa bado zinafanyika katika sehemu mbali mbali zenye changamoto ya ukosefu wa maji,”alisema Aweso.

Pia Awezo aliongeza kuwa kwa sasa serikali imeweka mipango madhubuti ya kuongeza zaidi wataalamu wa maji ambao wataweza kusaidiana na Wizara husika kwa lengo la kuweza kusimamia miradi mbali mbali ambayo itaweza kuleta chachu zaidi na kuwasaidia wananchi kuondokana na adha ambayo wamekuwa wakikumbana nayo.

Aidha Waziri Awezo aliongeza kuwa upatikanaji wa maji safi na salama kutaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuondokana na changamoto ya wananchi kupatwa na magonjwa mbali mbali ya mlipuko kama vile kuumwa na matumbo hasa katika maeneo ya vijijini  na badaala yake serikali inajikita zaidi katika kuwapatia huduma ya maji  ambayo yapo salama kwa matumizi ya binadamu.

“Wananchi kwa kweli wanapata tabu na Rais wetu  mpendwa wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli  ameweza kutupa  dhamana kwa ajili ya kuweza kuwatumikia wananchi hivyo nitahakikisha kwamba wakandarasi ambao wamepewa kazi ya kusimamia miradi yote ya maji inatekelezeka kwa kiwango na wakati,”alibaisha Waziri Aweso.

Katika hatua nyingie Waziri aweso alibainisha kwamba endapo watalaamu wa maji na wakandarasi wakitimiza wajibu wao ipaswavyo kwa kushirikiana na Wizara basi kutaweza kuleta mabadiliko makubwa katika maendeleo ya maji na kuwakomboa wananchi kuondokana kabisa na kutembea umbari mrefu kutafuta maji na baadhi yao kuondokana na kunywa maji machafu ambayo sio salama kwa afya yao kwani yanaweza  kupelekea kupata magonjwa ya milipuko.

       

Museveni ashinda Urais Uganda

$
0
0


Na Mwandishi Wetu


Tume ya Uchaguzi Uganda (EC) imemtangaza Yoweri Museveni kuwa mshindi wa kiti cha Urais wa nchi hiyo baada ya kupata kura 5,852,037 sawa na asilimia 58.64 ya kura zote zilizopigwa.

 

Naye mpinzani mkubwa wa Museveni ambaye pia ni mwanamuziki Robert Kyagulani maarufu kama Bobi Wine ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura 3,475,398 sawa na asilimia 34.83 ya kura zote zilizopigwa katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Januari 14 mwaka huu.

 

Pia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli amempongeza Museveni kwa kutangazwa kuwa mshindi na kusema kuwa Tanzania itaendeleza urafiki na nchi hiyo kwa maslahi mapana ya wananchi.

 

“Nakupongeza Mhe.Yoweri Kaguta Museveni kwa kutangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Uganda kuwa mshindi wa kiti cha Urais. Tanzania itaendeleza urafiki na undugu wetu kwa maslahi mapana ya wananchi. Hongera Waganda kwa kukamilisha Uchaguzi Mkuu, endeleeni kudumisha amani na upendo”. Ameandika Rais Magufuli katika ukurasa wake wa Twitter.

MHANDISI KASEKENYA AWAPONGEZA UCHUKUZI KUKUZA VIPAJI

$
0
0

 

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akionesha umahiri wake katika kuuchezea mpira kwa kichwa baada ya kuzinduwa rasmi Bonanza la Sekta ya Uchukuzi lililofanyika katika viwanja vya Sigara jijini Dar es Salaam.

 

 Na Mwandishi Wetu


NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ameipongeza sekta ya Uchukuzi kwa kukuza vipaji katika michezo na hivyo kuiletea heshima Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi katika mashindano ya kitaifa.

 

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kuzindua Bonanza la Sekta ya Uchukuzi, Naibu Kasekenya amesema michezo licha ya kuburudisha na kuwaweka watu karibu hujenga afya ya mwili na akili na hivyo kuleta tija mahali pa kazi.

 

"Nawataka wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya kuendeleza michezo na kuibua vipaji miongoni mwa watumishi ili kuwawezesha kuwa wenye afya njema na kufanyakazi kwa bidii," amesema Mhandisi Kasekenya.

 

Aidha ameitaka kamati ya maandalizi kuhakikisha Bonanza  la Tano linafanyikia mjini Dodoma ili kuongeza idadi ya washiriki.

Naye Mwenyekiti wa maandalizi ya bonanza hilo, Bw. Alphonce Mwingira amesema uwepo wa tamasha hilo ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dk. Leonard Chamuriho, kuhusu umuhimu wa michezo mahali pa kazi ili kujenga umoja na ushirikiano. 

 

Mbali na michezo na burudani, katika bonanza hilo washiriki pia walipata fursa ya kupima afya zao na kupata ushauri wa kitabibu.

 

Zaidi ya taasisi 14 za sekta ya Uchukuzi, zikiwemo TAA, TMA, TCAA, LATRA, TASAC, TAZARA, TRC, TPA, KADCO, ATCL, MSCL, SINOTASHIP, NIT na DMI zimeshiriki bonanza hilo lilokuwa na michezo mbalimbali, ikiwemo mpira wa miguu, pete, kuvuta kamba, mpira wa wavu, kucheza bao na riadha.

DKT. NDUGULILE AKUTANA NA BODI, TAASISI ZAKE KUJIPANGA KUENDESHA WIZARA MPYA

$
0
0

 

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wenyeviti wa bodi na wakuu wa taasisi za Wizara yake (hawapo pichani) wakati wa kikao chake na viongozi hao cha kujipanga kuendesha Wizara hiyo kilichofanyika Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula na kulia Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Jim Yonazi

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Justina Mashiba akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani) na wenyeviti wa bodi na wakuu wa taasisi zake, Dodoma. Kutoka kushoto ni Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Hassan Mwang’ombe na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Waziri Kindamba.

 

Na Prisca Ulomi, WMTH

 

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile amekutana na wenyeviti wa bodi na wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara yake ikiwemo na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Shirika la Posta Tanzania (TPC), Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Tume ya Taifa ya TEHAMA (ICTC) na Baraza la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA – CCC) na Menejimenti ya Wizara yake kwenye ukumbi wa Dodoma Convention Centre, Dodoma

 

Dkt. Ndugulile amesema kuwa malengo ya kikao hicho ni kufahamiana, kuwa na mtazamo mpya, uelewa wa pamoja na kujipanga kuendesha Wizara mpya ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Wizara na kudhihirisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa alifanya maamuzi sahihi kuunda Wizara hii

 

Ameongeza kuwa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ni njia kuu ya uchumi wa kidijitali kama ilivyo miundombinu mingine ya barabara ambapo taasisi za Serikali, sekta binafsi na wananchi wanatumia TEHAMA kuendesha shughuli za kila siku na kuifanya TEHAMA kuchangia ukuaji wa uchumi na kuongeza pato la taifa hivyo taasisi za Wizara zifanye mabadiliko ya kiutendaji, kuboresha sheria, kanuni na miongozo ili kufanikisha utekelezaji wa suala la Tanzania ya uchumi wa kidijitali

 

Amesisitiza kuwa taasisi za Wizara zinazofanya biashara zijiongeze na kuwa wabunifu kwa kufanya utafiti ili kubaini mahitaji ya wateja na kuwafikishia huduma mahali walipo kwa njia ya TEHAMA badala ya wateja kupoteza muda kwa kutafuta ofisi za taasisi ili kupata huduma

 

Aidha, amezitaka taasisi kuandaa mipango mikakati ya taasisi zao ambayo inapimika na inayoenda sambamba na Ilani ya CCM ya mwaka 2020 – 2025, hotuba ya Mhe. Rais Dkt. Magufuli  na Mpango Mkakati wa Wizara ili kuwa na majukumu yanayopimika na utekelezaji wa majukumu kwa matokeo kwa kuwa sio muumini wa michakato

 

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainabu Chaula amesema kuwa Waziri Dkt. Ndugulile ametoa dira na mwelekeo wa kiutendaji kwa Wizara na taasisi zake ili kuhakikisha kuwa Wizara hii mpya inakuwa Wizara ya wananchi kwa kuwa TEHAMA ni ya wananchi

 

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA, Dkt. Jones Killimbe amemshukuru Dkt. Ndugulile kwa kuitisha kikao hicho cha kusisitiza utendaji kazi kwa ushirikiano ili kuthibitisha kuundwa kwa Wizara mpya na taasisi ziko tayari kushirikiana ili kufikia malengo yaliyowekwa na Wizara

 

Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Justina Mashiba amesema kuwa taasisi yake imejipanga kutumia teknolojia rahisi ili kufikia malengo ya kufikisha mawasiliano bora na ya uhakika kwa watanzania waishio vijijini

 

Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba amesema kuwa Shirika lake litaendelea kuboresha kituo cha huduma kwa wateja kwa kuwa kila siku wanapokea malalamiko ya wateja na wanayashughulikia kwa haraka na TTCL inatumia mitandao ya kijamii na tovuti ili watanzania waweze kupata huduma za TTCL mahali walipo badala ya kwenda kwenye ofisi za TTCL

 

Dkt. Ndugulile amesema kuwa Wizara yake itaendelea kufanya vikao na wenyeviti wa bodi na wakuu wa taasisi zote za Wizara hiyo kila baada ya miezi mitatu ili kupata taarifa, mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu na kujadili taarifa ya mapato na matumizi ya taasisi hizo.

Hospitali ya Uhuru yaanza kutoa Huduma

$
0
0


Katibu wa kuratibu shughuli za Serikali kuhamia Dodoma Meshack Bandawe akizungumza jambo na manesi wanaofanya kazi katika hospital ya uhuru iliyopo Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.Hospitali hiyo ambayo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99.8, imeanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje.

  

Katibu wa kuratibu shughuli za Serikali kuhamia Dodoma Meshack Bandawe akikagua vifaa mbalimbali vilivyopo katika hospitali ya Uhuru ambayo imekamilika na kuanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje.

 


Jengo la Hospitali ya Uhuru lilikamilika kwa asilimia 99.8 na kugharimu bilioni 3.9 limeanza kutoa huduma kwa wananchi. Picha na MAELEZO.

 

 

 

 

Na Mwandishi Wetu

 

Hospitali ya Uhuru inayojengwa kwa gharama za bilioni 3.9 imeanza  kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje.

 

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Dkt. Dkt.Eusebius Kessy alipokuwa akiongea  na waandishi wa habari wakati wa ukaguzi wa hospitali hiyo

 

“Hospitali yetu imeanza kutoa huduma tangia tarehe 21 Desemba 2020 na mpaka sasa imeshahudumia wateja takribani 300”amesema Dkt Kessy

 

Ameongeza kuwa ujenzi wa hospitali hiyo ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa chamwino na maeneo ya karibu na kusema kuwa watahahakisha kwamba huduma zinakuwa bora kama ilivyokusudiwa

 

Dkt kessy amesema kuwa hospitali iyo inatoa huduma kwa wagonjwa wenye bima ya afya ya Taifa NHIF na Mfuko wa afya ya jamii (CHF) na pia wale ambao hawana bima ya afya.

 

Akizungumzia huduma zinazotolewa kwa sasa Dkt.Kessy amesema kwa sasa huduma za maabara,clinic za macho na meno,mionzi ,clinic za mama na mtoto na huduma za wagonjwa wa nje (OPD).


 

Kwa upande wake Katibu wa kuratibu shughuli za Serikali kuhamia Dodoma Meshack Bandawe ambae alifanya ziara maalum kukagua imaendeleo ya Hospitali hiyo amesema kuwa kuwa ujenzi wa hospitali iyo umekamilika kwa asilimia 99.8.

 

Amebainisha kuwa maagizo yaliyotolewa na Waziri mkuu alipofanya ziara Novemba 20,2020 yametekelezwa ikiwemo kukamilisha ujenzi wa jengo ifikapo tarehe 5 Desemba 2020,vigae vya chini,miundombinu muhimu na ukamilishaji wa ukuta kuzunguka hospitali hiyo ambao umekamilika kwa asilimia 99 na ujenzi wa miundombinu ya barabara hospitalini hapo unaendelea chini ya TARURA na utakamilika hivi karibuni.

 

Pamoja na hayo amesema mifumo ya maji na umeme na miundombinu mbalimbali imekamilika pamoja na vifaa tiba vya Utra sound, X-ray,ECG na baadhi ya samani ambavyo vimeshawasili hospitali hapo.

 

Amesema siku ya sherehe za mapinduzi ya Zanzibar kulifanyika uchangiaji wa damu salama na kufanikiwa kupata unit 48 za damu.

 

Aidha amelipongeza Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) kupitia SUMA JKT ambae ndio mkandarasi wa hospitali iyo,mshauri mwelekezi  wakala wa majengo Tanzania(TBA),Mkurugenzi wa halmashauri ya Chamwino,Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dodoma na Ofisi ya Rais- TAMISEMI kwa usimamizi wa ujenzi wa hospitali hiyo.

 

Lengo la ujenzi wa Hospitali ya chamwino ni kuboresha huduma za kijamii Dodoma ikiwamo afya ili kutimiza azma ya Serikali kuhamia Dodoma ambayo ndio makao makuu ya nchi.

 

Ujenzi wa Hospitali ya Chamwino ni agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwamba Fedha  zilizotengwa kwa ajili ya sherehe ya miaka 57 ya Uhuru wa Tanzania bara za tarehe 9 desemba 2018 zitumike kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Chamwino.

 

FOMMA KUSHUSHA NEEMA KWA MAKUNDI YA WAHITAJI

$
0
0

NA DANSON KAIJAGE, DODOMA


JAMII imeshauriwa kuwekeza kwa watu wenye shida mbalimbali,ikiwemo wajane,yatima,wazee na wasiojiweza badala ya kuwekeza kwenye starehe na hanasa.


Ushauri huo umetolewa leo 17 Januari 2021 na mwanzirishi wa umoja wa kuwasaidia wajane,yatima,wazee na makundi ya watu wasiojiweza Mc John Mwangata ujulikanao kama Friends of Mc Mwangata Association(FOMMA) wakati wa afla ya kutimiza mwaka mmoja iliyofanyik Msalato Jijini Dodoma.


Mc Mwangata akizungumza mbele ya wanachama wa umoja huo amesema kuwa ili kuweza kuwa na taifa la watu wenye furaha na upendo ni vyema wale wenye kujariwa kuwa na uwezo kujenga tamaduni ya kuwakumbuka ambao ni wahitaji.


"Watanzania Mungu katijalia kwa kiasi kibubwa cha kuonesha upendo kati ya mtu na mtu, lakini tujue kuwa hatulingani kwa kipato wapo watu ambao wanauhitaji mkubwa na kwa kulitambua hilo ni vyema kuwakumbuka watu wa aina hiyo.


"Na kutoa kwa wahotaji siyo jambo baya wapo watu wanatumia mali zao kwa kustarehe na kufanya anasa za kutisha lakini wanawasahau watu wenye uhitaji,sasa kwa kuliona hilo ndugu zangu naombeni tuwekeze kwa kada ya watu Wa aina hiyo na hakika Mingu atatuongezea na tutaongeza furaha na maisha marefu kwa watu wa aina hiyo"amesema Mc Mwangata.


Katibu wa Umoja huo Godbless Kisanga,akisoma Risala amesema Umoja huo( FOMMA) ulioanzishwa mwaka 2019 na umejipanga katika mwaka 2021 kuhakikisha wanawafikia watu wenye uhitaji ndani ya mkoa wa Dodoma na nje ya Dodoma kwa kutoa huduma mbalimbali kwa watu wenye wahitaji.


Kisanga amewasilisha risala hiyo wakati wa  tafrija fupi ya kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa umoja huo ujulikanao kama (FOMMA).


Kisanga amesema kuwa Mc Mwangata alianzisha umoja huo kwa maono ya kuwasaidia watu wenye uhitahi sambamba na kuwatembelea na kuwasaidia waliopo magerezani.


Kisanga ambaye ni Katibu katika Umoja huo amesema lengo la umoja huu ni kufahamina, kusaidia wasio jiweza na kusaidiana wao Kwa wao huku  lengo kuu likiwa zaidi ni kuwasaidia yatima,wajane,wazee pamoja na wale waishio katika maisha magumu.


Kwa upande wa Mwenyekiti wa Umoja huo Dk.Gaspaer Kisenga,amesema umoja huo umeanzishwa mahususi kwa lengo la kuwafanya watu wasiokuwa na uwezo nao kujiona hawajasahaulika katika Jami.


"Mimi kitaaluma ni Daktari katika kituo cha Afya Makole ninaona jinsi watu wanaohitaji huduma wanavyotesema na wengine hata kupata matibabu inakuwa shida.


"Kwa kuliona hilo kikundi chetu ambacho mwanzilishi ni Mc Mwangata tuliona jambo muhimu zaidi ni kujikita katika kuwasaidia wahitaji ambao wapo katika makundi ya wajane,yatima,wazee na wanaoishi katika mazingira magumu"amesema Dk.Kisenga.

MWAKALINGA AAGIZA ZOEZI LA UTOAJI MCHANGA MTO MSIMBAZI LIWE ENDELEVU

$
0
0

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga (kati kati), akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mkoa wa Dar es salaam, Mhandisi Ngusa Julius (kusoto), wakati alipotembelea eneo la Jangwani, jijini Dar es salaam, kukagua maendeleo ya ukarabati wa miundombinu katika neo hilo.

 

 

Na Mwandishi Wetu


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, amemtaka Meneja wa  Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Dar es salaam, Mhandisi Ngusa Julius,  kuhakikisha anendelea na shughuli za utoaji mchanga katika mto Msimbazi eneo la Jangwani, jijini Dare es salaam, ili kudhibiti changamoto zinazoweza kujitokeza hususani kipindi  cha mvua.

Akizungumza mara baada ya kukagua na kuridhishwa na kazi inayoendelea katika eneo hilo, Mwakalinga amemwagiza Meneja huyo kuandaa mchoro ambao utasaidia ufanisi wa kazi hiyo ili kutambua na kuyatafutia ufumbuzi maeneo yote yenye changamoto kubwa hasa kipindi cha mvua.

"Sisi kazi yetu si kupambana na maji, kazi yetu ni kuchimba eneo hili na kuelekeza maji sehemu ya kwenda, tunafanya hivi ili kupunguza athari za maji katika eneo hili", amesema Mwakalinga.

Mwakalinga, pia amemuagiza Mhandisi Ngusa kufanya matengenezo mara kwa mara ili kuepusha Serikali kutumia gharama kubwa ya kufanya matengenezo ya miundombinu mara baada ya matatizo kutokea.

Kuhusu suala la mpango wa ujenzi wa daraja kubwa katika eneo hilo, Mwakalinga, amesema kuwa mpango huo unaendelea vizuri na mchoro huo ukikamilika basi kazi hiyo itaanza mara moja.

Aidha, Mwakalinga amesisitiza kuwa kwa sasa mpango wa Serikali ni kuhakikisha kuwa inakagua miundombinu yake yote ili kuhakikisha kunakuwa na usalama wakati wote.

Katika hatua nyingine, Mwakalinga, amekagua daraja la Pugu Kinyamwezi, Manispaa ya Ilala, ambapo amemtaka Meneja wa TANROADS mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na uongozi wa Manispaa hiyo kuhakikisha wanapata ufumbuzi kuhusu kalvati la daraja la Pugu Kinyamwezi ambalo linatiririsha maji kwenye makazi ya watu.


Kwa upande wake, Meneja wa TANROADS mkoa wa Dar es salaam, Mhandisi Ngusa Julius, ameahidi kuyafanyia kazi maelekezo ya Katibu Mkuu huyo na kusisitiza kuwa bado wanaendelea kusubiri ufumbuzi wa kudumu katika eneo hilo mara baada ya mchoro kukamilika.


"Hapa tunachokifanya kwa sasa ni kufanya matengenezo ya dharura ili kupunguza athari kwa wananchi na watumiaji wa barabara hii, wakati huo huo tukisubiri mwarobaini katika eneo hili", amesema Julius.

Arch. Mwakalinga, amemaliza ziara yake ya siku moja mkoani Dar es salaam ambapo pamoja na mambo mengine amekagua barabara ya Pugu- Manerumango (Km 60.14) ambayo inajengwa kwa kiwango cha lami.


Zimamoto wakusanya Bilioni 81

$
0
0


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo (watatu kushoto) akimsikiliza Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Gilbert Mvungi (wanne kushoto)  akimpa maelezo ya chanzo cha maji kinachoonekana pichani kinachotumika  wakati wa tukio la kuzima moto  na uokozi wakati wa ziara ya kikazi ya naibu waziri huyo kutembelea Makao Makuu ya jeshi hilo leo jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 

 

Na Mwandishi Wetu

 

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limekusanya jumla ya Shilingi Bilioni 81,336,956,451 katika kipindi cha miaka mitano ikiwa ni gharama za ukusanyaji wa tozo za ukaguzi wa kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto katika majengo 356,845 nchi nzima ikijumuisha viwanda, mahoteli, mashule, masoko, migodi, maduka, hospitali, maofisi, matenki ya mafuta, nyumba za kuishi na vyombo vya usafiri.

 

Hayo yamesemwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, John Masunga wakati akitoa taarifa ya jeshi hilo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo wakati wa ziara ya kikazi Makao Makuu ya jeshi hilo,leo jijini Dodoma.

 

“Kwa kuwa ukaguzi huo wa king ana tahadhari ya moto huenda sambamba na ukusanyaji wa maduhuli ya serikali,Jeshi limefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi 81,336,956,451,aidha,Jeshi la Zimamoto linaendelea na jitihada za kuboresha maduhuli ikiwa ni Pamoja na kuanzishwa kwa mfumo mpya wa makusanyo ambao utasaidia kupunguza upotevu wa maduhuli ya serikali” alisema Kamishna Masunga.

 

Akizungumza wakati wa ziara hiyo,Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Khamis Hamza Chilo alilipongeza jeshi hilo huku akitaka waongeze ufanisi ikiwepo kufika kwa haraka katika matukio ya moto ili kuweza kunusuru Maisha na mali za wananchi.

 

“Kumekuwepo na malalamiko juu ya askari wetu kuchelewa kufika katika maeneo ya moto au ajali yoyote ili kufanya maokozi,nawasihi kufika haraka katika matukio mbalimbali kwani wananchi wanawategemea na uwepo wenu unasaidia mambo mengi kwa kuwa nyie ndio mna utaalamu na udhibiti wa majanga ya moto na uokozi” alisema Naibu Waziri Khamis Hamza Chilo.

 

Sambamba na mafaniko hayo jeshi hilo pia limefanikiwa kukamilisha ujenzi wa Jengo la Makao Makuu jijini Dodoma,Kituo cha Zimamoto na Uokoaji katika Wilaya ya Chato mkoani Geita,linaendelea na ujenzi wa kituo cha zimamoto wilayani Chamwino na ujenzi wa nyumba za askari wake katika eneo la Kikombo jijini Dodoma.

MAHABUSU 126 WAFUTIWA MASHTAKA MKOANI KAGERA

$
0
0

Lydia Lugakila, Muleba

Jumla ya mahabusu 126 kutoka Wilaya ya Biharamulo, Muleba na Bukoba mkoani Kagera wamefutiwa mashitaka mbalimbali yaliyokuwa yanawakabili na Mkurugenzi wa Mashitaka hapa nchini DPP.

Akizungumza na waandishi wa habari wilayani Muleba Mkurugenzi wa Mashitaka hapa nchini, Biswalo Mganga, amesema kuwa waliofutiwa mashitaka hayo kwa wilaya ya Muleba ni 26, Bukoba 52 na Biharamulo ni 48 na wote walikuwa na makosa mbalimbali.

Mganga amesema kuwa sababu iliyosababisha kuwepo kwa maabusu hao ni wao kwa wao kubambikiziana  kesi, migogoro ya ardhi, wivu wa kimapenzi pamoja na migogoro ya kifamilia ambapo amewataka Wananchi Mkoani humo kutatua migogoro yao ngazi ya serikali za vijiji badala ya kwenda ngazi ya Mahakama.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango ameshukuru Mkurugenzi huyo DPP kwa kufuta mashitaka hayo ambapo Wilaya ya Muleba ilikuwa na maabusu 126 na kufanya kupunguzwa na kubaki 100 katika gereza la wilaya  Muleba.

RAIS MAGUFULI KUZINDUA MIRADI YA MAENDELEO-KAGERA

$
0
0

 Na Lydia Lugakila, Bukoba

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli anatarajiwa kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo na uwekaji mawe ya msingi katika miradi mkoani Kagera.

Akizungumza mbele ya Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Kagera na  waandishi wa habari  juu ya ujio wa Rais Dk. John Magufuli Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco, Gaguti amesema ziara hiyo itaanza Januari 18, 2021 ambapo Rais Magufuli atafanya matukio yatakayohusisha uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa chuo cha ufundi Veta mradi wenye thamani ya shilingi bilioni 22, uzinduzi wa shule ya sekondari ya Ihungo wenye thamani ya shilingi takribani bilioni 11.1.


Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema kuwa licha ya shughuli hizo Rais Magufuli atapata fulsa ya kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa uchimbaji wa madini aina ya Nikel ambapo pia atatembelea na kujionea  ufugaji wa kisasa mradi ambao ukikamilika utakuwa na thamani ya shilingi bilioni 15.

Aidha kwa mujibu wa mkuu huyo wa Mkoa pia Rais Magufuli atawahutubia wananchi Mkoani humo katika uwanja vya michezo wa shule ya sekondari Ihungo na baadae ataelekea wilayani Karagwe Mkoani humo kwa ajili ya kutembelea na kuweke jiwe la msingi katika mradi wa ufugaji wa kisasa ambao utaishia kuwa na kiwanda Cha kisasa Cha maziwa.

Hata hivyo Brigedia Gaguti ametumia fulsa hiyo kuwataka wananchi Mkoani Kagera kujitokeza kwa wingi ili kumpokea kiongozi huyo

DIWANI KATA YA TANGINI AWEKA MIKAKATI YA KUPAMBANA NA UCHAFU WA MAZINGIRA

$
0
0


Diwani wa Kata ya Tangini Mfalme Kalanguti aakiwa katika zahanati alipotemnbelea na kufanya ziara kwa ajili ya kuweza kujionea shughuli mbali zinazofanywa pamoja na suala zima la utunzaji wa mazingira sambamba na usafi katika maeneo ya kazi. (Picha na Victor Masangu).

 

 

NA  VICTOR MASANGU, PWANI 

 

KATIKA kuunga mkono juhudi za Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu katika suala zima la  kupambana na usafi wa mazingira Diwani wa kata ya Tangini Mfalme Kalanguti kupitia tiketi ya (CCM) ameahidi kuanzisha kampeni maalumu kwa kushirikiana na wananchi wake yenye lengo la kuendesha zoezi la kufanya usafi  nyumba kwa nyumba kila mwishoni wa juma ili kuthibiti kuibuka kwa magonjwa mbali mbali ya milipuko.

Kalanguti aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mahojiano maalumu kuhusiana na mikakati yake aliyojiwekea katika kuhakikisha anapambana vilivyo ili kuweza kuwasaidia wananchi waweze kuondikokana kabisa na magoinjwa mbali mbali ya mlipuko amabyo  yanaweza kujitokeza kutokana na kuwepo kwa kuzagaa kwa uchafu katika maeneo ya makazi ya watu.

“Kwa upande wangu mimi kama Diwani wa kata ya Tangini pamoja na kuweka mipngo madhubuti ya kushirikiana na wananchi wangu katika masuala mbali mbali ya kimaendelea lakini moja katika ya mipango yangu ni kuunga juhudi za serikali katika suala la mambo ya usafi wa mazingira hivyo mimi zoezi langu nitakalolianzisha litakuwa endelevu na kwamba litakuwa likifanyika kila mwisho wa  wiki ambapo kila mwananchi ataweza kushiriki kikamilifu lengo ikiwa ni kutbitibinna kupambana na magonjwa ya milipuko,”alibainisha Kalanguti.

Pia Diwani huyo alisema kuwa pamoja na kuendesha kampeni hiyo pia atashirikiana bega kwa began a wataalamu mbali mbali wa masuala ya afya ili kuweza kutoa elimu zaidi kwa wananchi wake kuhusina na umuhimu wa kufanya usafi wa mara kwa mara katika maeneo ambayo wanayoishi hasa katika kipindi cha mvua zinapokuwa zinanyesha.

“Suala la usafi wa mazingira ni jukumu la kila mmoja wetu hivyo wananchi wanapaswa kuliangalia kwa jicho la tatzu zaidi na kushiriki kikamilifu bila ya kutegea kwani  magonjwa ya milipuko yanatokana na kuwepo kwa kuzagaa kwa uchafu mbali mbali hivyo nina imani tukishiriki kikamilifu kwa pampoja tutaweza kukabiliana na hali hii ya magonjwa ya milipuko.,”aliongeza Kalanguti.

Pia aliongeza kuwa katika kukabiliana na wimbi la magonjwa mbali mbali ya mlipuko wananchi wote wanapashwa kuendesha shugghuli zao kwa kuzingatia sheria za na taratibu ambazo zimewekwa na kuheshimi miongozo yote ambayo inatlewa na wataalamu wa afya lengo ikiwa ni kuweza mazingira yawe katika hali ya usafi.

Kalanguti pia aliweza kuiasa jamii kwa ujumla kujenga tabia ambayo ni endelevu ya kuhakikisha kwamba wananawa mikono yao kwa kutumia maji  safi na salama ambayo ni tiririka ili kusaidia kupambana na magonjwa hayo ya mlipuko na kutoa pongezi kwa serikali ya wamu ya tano kuweza kuwahamasiha wananchi katika suala zima la kufanya usafi katika kila mwisho wa mwezi.

WATEMBEA UMBALI MREFU KUFUATA HUDUMA ZA AFYA

$
0
0

 Na Lydia Lugakila, Muleba

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Katembe wilayani Muleba mkoani Kagera wameomba halmashauri ya wilaya hiyo kuwakamilishia ujenzi wa zahanati yao ambayo waliianzisha kwa nguvu zao kwa kushirikiana na shirika la Tanapa Rubondo tangu mwaka 2020.

Wakizungumza mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo baada ya kutembelea jengo hilo  wananchi hao wamesema kuwa kwa sasa wanapata huduma za afya katika kijiji jirani cha Nyakabango na kata jirani ya Kimwani hivyo baadhi yao wanapata adha ya kutembea umbali mrefu.

Wananchi hao wamesema kuwa endapo ikikamilika zahanati hiyo itawaondolea adha hiyo huku wakiiomba halmashauri ya Wilaya hiyo kukamilisha ujenzi uliobaki kutokana kwani wameishatumia nguvu nyingi katika ujenzi huo.

Kwa upande wake mtendaji wa Kijiji hicho cha Katembe Bwana Ulimwengu Richard amesema ujenzi wa zahanati hiyo umekwisha ghalimu zaidi ya shilingi milioni 76  ambapo kwa sasa wapo katika ujenzi wa nyumba ya waganga na vyoo kwa thamani ya zaidi ya shilingi milioni 30 na tayari halmashauri hiyo imeishaweka zaidi ya shilingi milioni 18 ili kukamilisha ujenzi uliobaki .

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandis Richard Ruyango amewashukuru wananchi hao pamoja na wadau mbalimbali wa Maendeleo kwa kushirikiana kuanzisha ujenzi huo ambapo amewataka Wananchi pamoja na wadau kuendelea kushirikiana kukamilisha ujenzi huo kwa kipindi hiki ili wananchi waweze kuondokana na adha hiyo.

Benki ya CRDB yatangaza Ufadhili wa Masomo wa Sh. Milioni 50 kwa Wachezaji 26 wa Mashindano ya Taifa Ya Mpira Wa kikapu. “CRDB Bank Taifa CUP"

$
0
0

 Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Abdallah Ulega, akizungumza katika hafla fupi ya kutangaza ufadhili wa masomo kwa wachezaji wa mashindano ya Taifa ya mpira wa kikapu “CRDB Bank Taifa Cup” iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mjumbe wa Bodi ya Benki ya CRDB, Martin Warioba.
 Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Abdallah Ulega (wa pili kulia), akimkabidhi, Abdul-aziz Abdulla  (katikati) kutoka Arusha cheti cha udhamini wa masomo ‘Scholarship’ uliotolewa kwa vijana waliofanya vizuri katika mashindano ya ligi ya taifa ya mpira wa kikapu CRDB Bank Taifa Cup yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile, Mjumbe wa Bodi ya Benki ya CRDB, Martin Warioba na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania, Phares Magesa. Benki ya CRDB imetoa udhamini wa masomo kwa vijana 26 wenye jumla ya shilingi milioni 50.

 

 Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Abdallah Ulega (wa pili kulia), akimkabidhi Nuru Mbaraka (katikati) kutoka Arusha cheti cha udhamini wa masomo ‘Scholarship’ uliotolewa kwa vijana waliofanya vizuri katika mashindano ya ligi ya taifa ya mpira wa kikapu CRDB Bank Taifa Cup yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile, Mjumbe wa Bodi ya Benki ya CRDB, Martin Warioba na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania, Phares Magesa. Benki ya CRDB imetoa udhamini wa masomo kwa vijana 26 wenye jumla ya shilingi milioni 50.


  Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Abdallah Ulega, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya vijana waliopata ufadhili wa masomo ‘Scholarship’ kupitia mashindano ya mpira wa kikapu ya CRDB Bank Taifa Cup yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana. Benki ya CRDB imetoa udhamini wa masomo kwa vijana 26 wenye jumla ya shilingi milioni 50.

 

 

Na Mwandishi Wetu

 

 Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Abdallah Ulega ameipongeza benki ya CRDB kwa hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Benki hiyo katika kuunga mkono jitihada za Serikali za kuleta hamasa kwa vijana katika michezo .

Naibu Waziri huyo ametoa pongezi hizo katika hafla fupi ya kutangaza ufadhili wa masomo kwa wachezaji wa mashindano ya Taifa ya mpira wa kikapu “CRDB Bank Taifa Cup” iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) na wadau wengine  ikiwamo Azam TV, Sanlam Insurance, Mayfair Insurance na Cool Blue.

Naibu Waziri Abdallah amesema pamoja na Serikali na wadau binafsi kuweka juhudi kubwa katika kuboresha sekta ya michezo nchini  lakini ipo haja ya kuweka mikakati endelevu ya kukuza vipaji vya mpira wa kikapu kuanzia ngazi ya chini.

“Nitoe rai kwa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) kuweka mikakati endelevu ya kukuza vipaji vya mpira wa kikapu kuanzia ngazi ya chini. Tutumie shule zetu kufundisha mchezo huu mashuleni. Lakini pia tuanzishe na kuziendeleza shule za mchezo wa mpira wa kikapu (basketball academy). Sisi kama Wizara tumejipanga kikamilifu kushirikiana nanyi ilikuweza kufikia lengo”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Bi. Tully Mwambapa alisema udhamini huo wa masomo kwa wachezaji ni muendelezo wa jitihada za Benki ya CRDB katika kuwawezesha vijana wa Kitanzania kupitia michezo. Aliongezea kuwa Benki hiyo kupitia sera yake ya Uwezeshaji katika Jamii (CSI Policy) imekuwa ikiwekeza katika michezo ya vijana kwa kuamini kuwa inasidia kuongeza ushiriki wao katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika jamii.

 

“Kwa kutambua haya Benki ya CRDB kupitia sera yake ya uwekezaji katika jamii “Corporate Social Investment Policy” iliona ni vyema kuambatanisha suala la elimu na michezo na hivyo kutangaza ufadhili wa masomo kwa vijana ambao wameonyesha uwezo mkubwa katika mashindano ya CRDB Bank Taifa Cup. Hii ilikua ni mbali ya zawadi zilizotoloewa kwa timu zilizofanya vyema pamoja na wachezaji binafsi”.

Akizungumzia kuhusu msukumo uliopelekea Benki hiyo kudhamini masomo ya wachezaji wa mpira wa kikapu Tully alisema mchezo wa mpira wa kikapu umekuwa haupewi sana kipaumbele kulinganisha na michezo mingine, Hivyo kupelekea kuwakatisha tamaa vijana wengi ambao wamekuwa wakionyesha vipaji katika mchezo huo.

“Baada ya mchakato mrefu wa kufanya tathimini ya uwezo uliooneshwa na vijana pamoja na kufatilia taarifa zao za kielimu, tumefanikiwa kukamilisha zoezi hilo na leo tupo hapa kwa ajili ya kutangaza vijana waliofanikiwa kupata nafasi hizo za ufadhili wa masomo kwa mwaka 2020/2021”. Alisema Tully.

Kwaupande wake Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania, Phares Magesa ameishukuru Benki ya CRDB kwa kuendelea kuwekeza katika mpira wa kikapu huku akisema udhamini huo wa masomo utakwenda kuleta hamasa zaidi kwa vijana wengi kushiriki katika mchezo huo.

Hafla hiyo ya kutangaza udhamini wa masomo kwa vijana hao ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa mchezo wa kikapu ikiwamo Mjumbe wa Bodi ya Benki ya CRDB na mchezaji wa zamani wa timu ya mpira wa kikapu ya Pazz, Martin Warioba, Afisa Uendeshaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile, Mkurugenzi Mkuu wa Sanlam Insurance, Khamis Suleiman, Msimamizi wa Vipindi vya Michezo Azam TV na wawakilishi wa Mayfair Insurance na Cool Blue ambao wote walikuwa wadhamini wa mashindano hayo.

Mashindano ya CRDB Bank Taifa Cup yakiwa yamebeba kauli mbiu ya “Ni Zaidi ya Game, Ni Maisha” yalizinduliwa tarehe 7 mwezi wa kumi mwaka jana na kufanyika kwa mafanikio makubwa jijini Dodoma katika viwanja vya Chinangali kuanzia tarehe 12 hadi 21 mwezi Novemba mwaka jana ambapo timu 36 za mpira wa kikapu kwa upande wa wanaume na wanawake zilichuana.

TARURA SINGIDA YAOKOA ZAIDI YA BILIONI 1.8 UJENZI WA DARAJA WILAYANI MANYONI

$
0
0

Watendaji wa  Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Manyoni wakikagua daraja hilo.

Wananchi na vyombo vyao wakivuka mto Nkonjigwe kwa kutumia daraja hilo.
Wananchi wanaozunguka maeneo ya daraja Nkonjigwe wakifurahia kutokana na kujengewa daraja hilo.


Na Dotto Mwaibale, Singida


SERIKALI ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk. John Magufuli kupitia watendaji waaminifu wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) imeokoa zaidi ya bilioni 1.8 kwenye ujenzi ambao tayari umekamilika wa daraja la Mto Nkonjigwe Wilayani Manyoni mkoani hapa.

Kabla ya kuanza kwa ujenzi huo kati ya Juni na Septemba upembuzi yakinifu wa mradi huo kupitia wazabuni mbalimbali ulikadiriwa kufikia zaidi ya shilingi bilioni 2, kabla ya Tarura kufanya maamuzi magumu ya kutumia mfumo wa Force Account.

Kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo kunakwenda kufungua fursa za uhakika wa upatikanaji wa huduma za afya hususani kwa akina mama wajawazito sambamba na kuimarisha wigo wa kibiashara kwa wakazi wa kata takribani tano zinazotumia njia inayounganishwa na daraja hilo yenye urefu wa km 76.2.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wanaozunguka eneo hilo akiwemo Halima Abdallah mkazi wa Kijiji cha Chikuyu alisema wamefurahishwa na ujenzi wa daraja hilo ambalo litawasaidia akina mama wajawazito kuvuka na kwenda kujifungua kwenye Zahanati za Kilimatinde na Chikuyu kwani awali wengi walikatisha maisha yao kwa kushindwa kuvuka mto huo.

Halima alisema walikuwa wanatoa shilingi elfu 2 hadi elfu 3 kuvushwa kwenye Mto huo na watu wenye uzoefu wa kuogelea jambo ambalo halikuwa salama kwao kwani kuna wakati licha ya uzoefu wao hushindwa kuvuka na kupelekwa na maji pamoja na aliyekuwa anavushwa.

"Tulikuwa tukifika hapa tunavua nguo halafu ndio tunavushwa, tunatoa shilingi elfu 2 za mtu kuvushwa na shilingi elfu 3 za nguo.watu wamekufa wengi sana hapa hasa Wanawake wajawazito." alisema  Halima.

Thomas Minaloganawenda mkazi wa Kijiji cha Chinyika kilichopo Kata ya Sasajila alisema moja ya shughuli kubwa ya kiuchumi kwenye maeneo haya ni uchimbaji wa chumvi lakini kuna wakati ilikuwa ikiharibikia kwenye mto kutokana na kukosa daraja.

Alisema amefanya kazi ya kuwavusha watu kwenye mto huo kwa muda mrefu licha ya kujipatia ujira lakini ilikuwa inaumiza anapoona wengi wakipoteza maisha hakuwa anafanya kazi hiyo kwa raha ila ni katika kujaribu kuokoa maisha ya watu waliokuwa wanafika hapo na kuhitaji kuvuka kwenda kupata huduma.

Awali Mratibu wa TARURA Mkoa wa Singida Mhandisi Boniphace William alisema ujenzi wa daraja hilo umegharimu shilingi milioni 122,415,500 hadi kukamilika kwake ambapo limetumia mfumo wa raslimali za ndani 'Force Account' 

Aidha, William alisema daraja hilo linatoa fursa ya upatikanaji wa huduma mbalimbali kuzunguka Vijiji vya Chikuyu,Chibumagwa, Sasajila, Majiri na Sanza.

"Nawaomba wananchi wanaohudumiwa na daraja hili na miradi mingine sehemu mbalimbali kutambua miradi hiyo ni kwa ajili yao, hivyo ni wajibu wao kuitunza na sio suala la Tarura pekee, wakijenga tabia hiyo miradi mingi itadumu kwa muda mrefu." alisema William.

Kwa upande wake Meneja wa Tarura Wilaya ya Manyoni Mhandisi Yose Mushi alisema daraja hilo ambalo lina urefu wa mita 53 na mita 25 eneo la kupitisha maji, kadhalika lenye tuta mita 28 linatarajia kuchagiza kasi ya ustawi wa uchumi kwa wakazi wanaozunguka maeneo hayo. 


Kipanga ataka Chuo cha Veta Korogwe kikamilike kwa wakati

$
0
0

 

Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga akisisistiza jambo  wakati wa ziara yake ya siku moja ya kukagua ujenzi wa Chuo cha Veta wilayani Korigwe mkoani Tanga mradi unaojengwa chini ya Usimamizi wa Chuo cha Veta Kihonda mkoani Morogroro wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa wa kwanza kushoto (aliyevaa tisheti nyeupe) ni Mkuu wa Chuo cha Veta  Kihonda Morogoro na Msimamizi wa Mradi huo Maganga Kashinde

Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga akisisistiza jambo  wakati wa ziara yake ya siku moja ya kukagua ujenzi wa Chuo cha Veta wilayani Korigwe mkoani Tanga mradi unaojengwa chini ya Usimamizi wa Chuo cha Veta Kihonda mkoani Morogroro wa pili kulia Mkuu wa Chuo cha Veta  Kihonda Morogoro na Msimamizi wa Mradi huo Maganga Kashinde.
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga katikati akikagua ujenzi wa chuo cha Veta wilayani Korogwe wakati wa ziara yake kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa.
Muonekano wa ujenzi wa baadhi ya majengo ya Chuo cha Veta wilayanu Korogwe.
Fundi akiendelea na ujenzi kwenye Chuo cha Veta wilayani Korogwe kama alivyokutwa.




Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Kipanga amefanya ziara ya kutembelea Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) wilayani Korogwe Mkoani Tanga huku akitoa wito kwa kamati inayosimamia mradi wa ujenzi huo kuhakikisha unakamilika kwa wakati uliopangwa.

Akiwa katika katika ziara ya kukagua mradi huo ambao unasimamiwa na chuo cha VETA Kihonda cha mkoani Morogoro alionesha kuridhishwa na hatua iliyofikiwa na kushauri matumizi ya jeshi la akiba kama vibarua ili kuharakisha utekelezaji wa mradi huo.

Kipanga alisema kwamba amekagua mradi huo na kuridhishwa na hatua ya ujenzi iliyofikiwa hadi sasa na kuwaagiza wasimamizi wa mradi kuhakikisha unakamilika kwa wakati uliopangwa ikiwemo kuwashauri kutumia vibarua kutoka Jeshi la Akiba kwa kuwa wapo wengi ambao wanaweza kufanya kazi hizo.

Hata hivyo Naibu Waziri huyo alitoa wito kwa wasimamizi wa mradi huo kuhakikisha vifaa vya upauaji vinapatikana mapema ili ujenzi uweze kukamilika kwa muda uliopangwa.

“Kwa kuwa majengo karibu yote yamefikia hatua ya upauaji, nitoe rai kuwa vifaa vya upauaji vipatikane mapema ili ujenzi uendelee na kukamilika kwa wakati,” amesisitiza Mhe. Kipanga.

Awali Akisoma taarifa ya ujenzi wa chuo hicho, Mkuu wa chuo cha VETA Kihonda, Kashindye Maganga amesema ujenzi wa mradi huo unagharimu kiasi cha Bilioni 1.6 huku kiasi ambacho walikwisha kupokea ni Tsh.Milioni 940.2 na hadi sasa wametumia kiasi cha Tsh.Milioni 917.9 na kiasi kilichobakia ni milioni 22.2 hivyo fedha ambazo imetumika ni sawa na asilimia 57.37 ya fdha ya mradi wote.

Alisema mpaka sasa mradi huo umefikia 34 ya kazi zote na kazi iliyobakia kwa sasa ni kumalizia kufunga lenta,kupaua na kazi ya umaliziaji ambapo tayari walikwisha kuomba fedha kwa ajili ya kumalizia kazi hizo na wanategemea kukamilisha kazi ya mradi huo ifikapo Machi 31 mwaka huu endapo fedha walizoomba watapatiwa mapema.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Kissa Gwakisa akizungumza katika ziara hiyo alionyeshwa kufurahishwa na hatua ya Serikali kujenga chuo hicho katika Wilaya yao na kwamba anaamini chuo hicho kikikamilika kitatoa vijana mahiri watakaotumika kiuzalishaji katika viwanda mbalimbali nchini .

Mkuu huyo wa wilaya aliahidi kushirikiana na Kamati ya ujenzi kuhakikisha vijana wa jeshi la akiba wanapatikana haraka ili kuweza kukamilisha ujenzi huo kwa wakati uliopangwa.

NMB yapongezwa kudhamini Tamasha la Biashara Zanzibar

$
0
0


 Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Zanzibar, Abdalla Duchi (kushoto), akipokea cheti kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Mudrik Soraga, ikiwa ni kutambua mchango wa benki hiyo katika kudhamini Tamasha la Saba la Biashara la Zanzibar lililofanyika kuanzia Januari 6 hadi 17. (Na Mpiga Picha Wetu).


Meneja wa benki ya NMB Tawi la Zanzibar,  Abdalla Duchi, akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kufungwa rasmi Tamasha la 7 la Maonyesho ya Biashara, Maisara mjini Zanzibar.

 

Na Mwandishi Wetu 

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Mudrik Soraga, amewataka wafanyabiashara kusajili biashara zao hatua itakayowawezesha kutambuliwa rasmi na kuwa walipa kodi ili kuchangia maendeleo ya Taifa.

Alisema hayo alipokuwa akifunga Tamasha la Saba la Biashara la Zanzibar kwenye viwanja vya Maisara Jijini Zanzibar, tamasha ambalo hufanyika kila mwaka kwa ajili ya kusherehekea Maadhimisho ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ambayo kwa mwaka huu yametimiza miaka 57.


 Soraga aliwasihi wafanyabiashara kuwa na utamaduni wa kushiriki matamasha mbalimbali ya biashara ya ndani na nje ili kuwaongezea uzoefu hatua itakayowawezesha kupanua wigo wa soko la bidhaa zao  na kujiongezea kipato wao binafsi na taifa kwa ujumla.


“Tuna adhma ya kuwaalika wafanyabiashara wa mataifa mengine kushiriki tamasha hili katika miaka ijayo hatua itakayolifanya kuwa la kimataifa na kuongeza wigo kwa wafanyabiashara wa ndani kujifunza zaidi” alisema Soraga.

Aidha katika hafla hiyo, Soraga alikabidhi tuzo kwa Benki ya NMB na taasisi kadhaa ambazo zilidhamini Tamasha hilo la Saba la Biashara la Zanzibar.

Akizungumza baada ya kupokea Tuzo, Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Zanzibar, Abdalla Duchi, alisema kuwa benki hiyo itaendelea kutoa huduma bora zaidi kwa lengo kukidhi mahitaji ya wateja wake ili kwenda sanjari na sera ya Zanzibar ya uchumi wa Buluu.

“Benki yetu ni wadau wakuu wa viwanda na wafanyabiashara wadogo wadogo hivyo ili kuboresha mustakabali wao tunalazimika kuwa na huduma bora zaidi kwa wateja na hata taasisi hususani za kijamii” Alisema Duchi.


Pamoja na hayo, aliishukuru Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar kwa kuandaa Tamasha hilo kwa kuwa limetoa fursa kwao (NMB) kujifunza zaidi pamoja na kupata wigo mzuri wa kuonesha huduma zao.

Tamasha la Biashara la Saba la Zanzibar lilikuwa na washiriki 360 ambalo ilifunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan Januari 6 na lilifungwa Januari 17 mwaka huu.

Rais Magufuli mgeni rasmi kilele siku ya sheria

$
0
0

Rais wa Tanzania, John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini  yatakayofanyika mkoani Dodoma, Februari Mosi, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Januari, 18 2021, Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma amesema kuwa siku hiyo ya Sheria itatanguliwa na Wiki ya Sheria ambayo ni mahususi kwa ajili ya utoaji wa elimu ya sheria na taratibu za kimahakama kwa wananchi.

Amesema wiki ya Sheria itaanza Januari 23 hadi 29, 2021 katika viwanja vya ‘Nyerere Square’ jijini Dodoma na kuongeza kuwa wiki hiyo itazinduliwa na matembezi maalum.

“Matembezi hayo ambayo yataanzia Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma na kuishia katika Viwanja vya Nyerere Square yatakayofanyika Siku ya Januari 24, 2021, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan,” amesema

Amesema kutakuwa na wiki nzima ya maonesho katika viwanja vya Nyerere Dodoma na kwenye maeneo mbalimbali ya mahakama nchini lakini kilele cha maadhimisho hayo itakuwa Februari Mosi mwaka huu katika viwanja vya Chinangali Dodoma.

“Mgeni rasmi siku hiyo anatarajiwa kuwa Rais Magufuli, hivyo tunaomba wananchi wajitokeza kwa wingi katika maadhimisho hayo kwa sababu kuna mambo mengi watajifunza  na watapata huduma na taratibu za ufunguaji wa mashauri, Sheria na taratibu zinazotumika katika kuendesha mashauri,” amesema

Aidha amesema kuwa maudhui ya maadhimisho haya yanaashiria kuanza rasmi kwa mwaka mpya wa shughuli za Mahakama na yameambatana na miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Mahakama Kuu.

“Kauli mbiu ya maadhimisho hayo inalenga kuonesha maudhui ya kuonesha ufanisi wa utoaji haki katika kipindi cha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Mahakama Kuu, kwa hiyo kauli mbiu itakuwa ‘Miaka 100 ya Mahakama Kuu, mchango wa mahakama katika kujenga nchi inayozingatia uhuru, haki, udugu, amani, ustawi wa mwananchi kati yam waka 1970 na mwaka 2020,” amesema

Amesema maudhui hayo yanakumbusha mchango wa mahakama ya Tanzania kuanzia enzi za ukoloni mpaka sasa.

Hata hivyo Jaji Mkuu amesema kuwa sheria, utawala wa sheria na mfumo wa utoaji haki kwa wakati ni nyenzo muhimu katika kufanikisha na kurahisisha biashara, uwekezaji, ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi.

KAGERA YAJIVUNIA MAFANIKIO SEKTA YA ELIMU

$
0
0

 

Rais John Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti.

 

 Na Lydia Lugakila, Bukoba

Mkoa wa Kagera umefanikiwa katika sekta ya elimu kwa kupungua kwa utoro kwa asilia 3 huku ongezeko la wanafunzi ikiwa ni asilimia 16 na 30 Kati ya shule za awali msingi na sekondari.

Akielezea mafanikio hayo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa mkoa huo umefanikiwa katika sekta ya elimu tofauti na miaka ya nyuma ambapo kwa sasa wamefanikiwa kuthibiti utoro kwa asilimia 3.

Brigedia Jenerali Gaguti amesema kuwa shule za msingi ufaulu umeongezeka kwa asilimia 88.8 na shule za sekondari ni asilimia 90.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa amempongeza Rais Magufuli kwa miradi mbalimbali ya kimaendeleo aliyoitekeleza katika mkoa huo ukiwa ni pamoja na uwekezaji, maji, miundombinu ya barabara usafiri na usafirishaji.

Akizungumza suala la uwepo wa hifadhi ikiwemo hifadhi ya Burigi Chato eneo la msitu wa Biharamulo mkuu huyo wa mkoa amemshukuru Rais Magufuli kwa kuimarisha ulinzi na usalama kwani eneo la msitu huo lilikuwa korofi kiusalama ambapo Kati ya mwaka 2010 - 2015 matukio ya kiuharifu yapatayo 124 ya kutumia siraha yamepungua yapata miaka miwili sasa.

Rais wa Magufuli yupo ziarani mkoani Kagera kwa shughuli ya uwekaji mawe ya msingi na uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

WADAU WA USAFIRISHAJI WALILIA ADA YA LESENI MAGARI YA KUKOD

$
0
0


Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Uchukuzi-Uchukuzi, Mhandisi Aron Kisaka, akifafanua jambo kwa wadau (hawapo pichani), wakati wa kikao cha kujadili ada ya leseni za magari maalum ya kukodi, kilichofanyika mkoani Arusha.


Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Uchukuzi-Uchukuzi, Mhandisi Aron Kisaka (wa tano kulia), katika picha ya pamoja na wadau wa usafirishaji, baada ya Mkutano wa siku moja wa kujadili ada ya leseni za magari maalum ya kukodi, kilichofanyika Mkoani Arusha.

 

 

 Na Mwandishi Wetu

 


Wamiliki na Madereva wa Magari maalum ya kukodi Mkoani Arusha wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi-Uchukuzi, kuitazama upya ada ya leseni ya magari hayo ya shilingi milioni 1 iliyopendekezwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) ili kuwezesha watoa huduma hao kuendelea kufanya biashara.

 

Wakizungumza katika kikao cha siku moja kilichofanyika mkoani humo cha kujadili ada hiyo wamesema wasafirishaji wengi hawakatai kutoa huduma lakini ni vyema Serikali kupunguza kiwango kwa kufanya utafiti wa kina sokoni.

 

“Kama watoa huduma tunapenda kuendelea kutoa huduma lakini ada iliyopendekezwa ni kubwa sana kulingana na aina ya biashara tunayofanya na kupitia biashara hii tunaendesha maisha yetu, ikipita hii tunaweza kufunga biashara” amesema Brian Fadhili.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wasafirishaji abiria (AKIBOA) mkoani Arusha, Locken Masawe amesema wasafirishaji wanapashwa kujenga hoja ambazo zitaifanya Serikali kufanya maamuzi ya kupunguza au kubakiza ada hiyo.

 

“Hoja tutakazojenga ndio zitaamua kupunguza au kubakiza ada hiyo maana Serikali hii ni sikivu na inafanya maamuzi kwa kuzingatia maoni ya na ndio maana wako hapa japo wana uwezo wa kufanya maamuzi na ada hii ikabaki kama ilivyo” amesema Masawe.

 

Masawe ameongeza kuwa Wizara izungumze na halmashauri ya majiji nchini ili kutenga maeneo maalum ambayo magari haya yanaweza kupatikana ili kupunguza changamoto ya kutokuwa kwa watumiaji kujua sehemu za kupata huduma.

 

Kwa upande wake Meneja Leseni kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), LeoNgowi amesema lengo la Mkutano huo na kusikia maoni ya wadau na kuboresha utoaji wa huduma za usafirishaji nchini.

 

“Maoni  mtakayowasilisha katika Mkutano huu tuangalie maeneo yote yanayohusisha makundi yote yaliyoainishwa tusijikite tu kwenye maeneo machache manake maoni yenu yataborehsa kanuni hizi na kuboresha mazingira ya usafirishaji’ amesema Ngowi.

 

Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Uchukuzi (Uchukuzi) amewahakikishia Wadau hao kuwa maoni yao yatazingatiwa na kufanyiwa kazi kabla ya utekelezaji wake na kuwasisitiza wasafirishaji kutoa maoni kwa maandisi kupitia barua pepe ya Katibu Mkuu-Uchukuzi ili kuharakisha mchakato huo.

Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>