Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

WAKULIMA WAFUNDISHWE KILIMO BORA CHA UMWAGILIAJI-KUSAYA

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya akikagua skimu ya umwagiliaji zao la mpunga ya kijiji cha Kagugu wilaya ya Mvomero leo. Skimu hiyo yenye ukubwa wa hekta 250 imejengwa miundombinu ya umnwagiliaji yenye urefu wa mita 2880 kupitia mradi wa kuongeza tija kwenye zao la mpunga (ERPP).

 

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya ametoa wito kwa maafisa kilimo wa halmashauri za mkoa wa Morogoro kuwafundisha wakulima kanuni bora za kilimo cha umwagiliaji ili waongeze tija na uhakika wa kipato kufuatia serikali kuboresha miundombinu.

Ametoa wito huo leo wilayani Mvomero wakati alipokagua utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa ghala na skimu yaumwagiliaji ya kijiji cha Kagugu inayotekelezwa na Mradi wa kuongeza thamani zao la mpunga (ERPP).

" Wakulima lazima waoneshe kilimo bora kwa kutumia mbegu kidogo na maji kidogo kufuatia mafunzo waliyopatiwa na wataalam wa kilimo cha umwagiliaji ili tija ipatikanae na kuwasaidia kuongeza kipato kupitia zao la mpunga" alisema Kusaya.

Katibu Mkuu huyo ameagua mashamba ya mpunga kijiji cha Kagugu na kuwaelekeza maafisa kilimo wa halmashauri kuwafundisha wakulima kilimo cha kisasa ili mradi wa umwagiliaji uwasaidie kuongeza tija kwa kutumia eneo dogo kisasa.


Kusaya anafanya ziara ya kufuatilia utekelezaji wa mradi wa ERPP unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi huu Januari ili ukabidhiwe kwa wakulima kupitia halmashauri baada ya Wizara yake kukamilisha miradi yote kumi na moja.

Katibu Mkuu huyo wa Kilimo aliongeza kusema Mradi wa Kuongeza tija na uzalishaji wa zao la Mpunga (ERPP) unaotekelezwa kwa ubia na Benki ya Dunia umefanikiwa kujenga maghala (5),skimu za umwagiliaji (5) na ujenzi wa maabara moja ya kilimo kwa lengo la kusaidia wakulima kuongeza tija katika zao la mpunga hatimaye nchi ijitosheleze kwa chakula na kipato kwa wakulima.

"Lengo la Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli ni kuona miradi hii ya kilimo cha umwagiliaji inamnufaisha mkulima,hivyo tutapenda kuona mara baada ya kuikabidhi kwa wakulima inakuwa endelevu" alisisitriza Kusaya.

Kusaya aliongeza kusema wizara yake inaamini kuwa kilimo cha umwagiliaji ndio mkombozi kwa mkulima kwani atakuwa na uhakika wa kuzalisha mazao yake zaidi ya mara moja katika mwaka kutokana na uwepo wa mabonde yenye maji na miundombinu ya kisasa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Albinius Mugonya alisema wanaishukuru wwizara ya kilimo kwa kufanikisha kukamilisha miradi mitatu ya  ujenzi wa maghala mawili kijiji cha Mbogo Kwamtonga na Kagugu pamoja na skimu ya umwagiliaji ya Kagugu ambazo zitakuza kiapato cha wakulima.

" Sisi wana Mvomero tuna miradi hii mitatu ambapo wakulima 5,673 watanufaika kwenye vijiji vya Mbogo Kwamtonga na Kagugu kwani tayari tija imefikia wakulima wanazalisha tani 5 hadi sita za mpunga kwa hekta" alisema Mugonya .
Mkuu huyo wa wilaya alisema mkakati wa wilaya yake ni kuhamasisha ujenzi wa viwanda vikubwa na vidogo ili kuongeza thamani ya zao la mpunga na kuwafanya wakulima wauze mchele badala ya mpunga ili wapate kiapato kikubwa.

Naye mratibu wa mradi wa ERPP Mhandisi January Kayumbe alisema kwa sasa miradiyote 11 katika wilaya za Mvomero, Kilosa na Ifakara ipo kwenye hatua za ukamilishaji na kuwa ifikapo mwisho wa mwezi huu itakakuwa tayari kukabidhiwa kwa wakulima.

Mradi wa ERPP ulianza kutekelezwa mwaka mwaka 2015 kwa gharama ya Dola za kimarekani milioni 22.91 toka Benki ya Dunia ukijusisha Tanzania Bara na Zanzibar.

 Jumla ya miradi 11 ikiwemo ujenzi wa skimu 5 za umwagiliaji,ujenzi wa maghala 5 na ujenzi wa maabara moja ya mbegu  inatekelezwa katika mkoa wa Morogoro chini ya ERPP.


RAIS DKT. MAGUFULI AMETOA MWELEKEO MPYA WA KIUCHUMI NA KIUTAWALA-MAJALIWA

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametoa mwelekeo mpya wa kiuchumi na kiutawala nchini ambao umesababisha Tanzania iingie kwenye kundi la nchi za uchumi wa kati miaka mitano kabla ya muda uliopangwa wa 2025.

 

Pia, Waziri Mkuu ametoa wito kwa Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ziendelee kutoa elimu ya uchumi wa viwanda kwa wananchi ili waweze kushiriki kikamilifu kujenga na kukuza uchumi wa viwanda.

 

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Januari 14, 2021) katika ukumbi wa Chimwaga, Chuo Kikuu cha Dodoma alipozindua kitabu cha “The Game Changer: President Magufuli’s First Term in Office”. Kitabu hicho kimehaririwa na Profesa Ted Maliyamkono na Dkt. Hugh Mason.

  

Amesema mpangilio na muktadha mzima wa kitabu hicho unabeba dhamira ya kukifanya kuwa kimbilio la rejea kwa watunga sera, wafanya maamuzi, wanataaluma na hata wananchi wa kawaida katika masuala mazima ya maendeleo ya nchi yetu.

 

“Kitabu hiki tunachokizindua leo, The Game Changer, kimeonesha namna sera na mipango ya Serikali ya Awamu ya Tano ilivyobadili mwelekeo wa Taifa letu kimaendeleo. Nitoe rai kwa waandishi wa kitabu hiki, waangalie uwezekano wa kutoa chapisho kwa Kiswahili ili Watanzania wengi waweze kukisoma na kunufaika na maudhui yake.”

 

Waziri Mkuu amesema kitabu kimefafanua kuwa Tanzania ni nchi yenye kuendeshwa kidemokrasia na kimeondoa shaka waliyonayo wadau wa maendeleo na wawekezaji kwa lengo la kuwawezesha kuongeza uwekezaji wao hapa nchini.

 

Naye, Katibu Mkuu Kiongozi na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Balozi Mhandisi Dkt. John Kijazi amesema: “Kitabu hicho kiwe chachu kwa Maprofesa wa vyuo vingine, wakae chini wafanye tafiti na kuandika vitabu vya aina hiyo ili kusaidia kuhifadhi historia ya nchi.”

 

Amesema vitabu vya aina hiyo vitasaidia vijana kutambua kazi zilizofanywa na viongozi mbalimbai nchini pamoja na kuenzi historia ya nchi.

 

Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema kazi ya fasihi andishi ni kutunza kumbukumbu na kitabu hicho kitasaidia kuhakikisha mambo mazuri yaliyofanywa na Rais Dkt. Magufuli yanadumu kwa vizazi vijavyo. “Hakika kazi yake imetukuka.” 

 

Naye, Mhariri Mkuu wa kitabu hicho, Profesa Maliyamkono akisoma muhtasari wa kitabu hicho, amesema kimeelezea namna Rais Dkt. Magufuli alivyoingia madarakani, hali aliyoikuta na hatua alizochukua pamoja na mafanikio ya Serikali.

 

“Rais Dkt. Magufuli wakati anaingia madarakani aliikuta nchi ikiwa katika wakati mgumu kiuchumi, amefanya kazi kubwa ya kurekebisha mikataba mibovu ya madini, amedhibiti rushwa na kwa sasa nchi inafaidika na rasilimali zake. Hakuna kiongozi wa Afrika ambaye aliweza kuziwajibisha kampuni kubwa za madini lakini Rais Dkt. Magufuli ameweza.”

 

Awali, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akitoa maoni kuhusu utendaji kazi wa Rais Dkt. Magufuli alisema amefanya mambo mengi katika miaka 20 ya utumishi wake Serikalini na miaka mitano ya urais. “Rais Dkt. Magufuli ni muasisi wa wazo la ujenzi wa barabara kwa kutumia fedha za ndani.”

 

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka alisema Rais Dkt. Magufuli ni mwanamageuzi wa kweli na ameipambanua nchi katika miradi mikubwa kama ya ujenzi wa reli ya kisasa inayowawezesha Watanzania kushindana katika uchumi. Alishauri kuwe na maandiko mengi yahusuyo viongozi.

 

Kitabu kimetayarishwa kwa lengo la kuweka kumbukumbu ya kazi zilizofanyika na zile zilizotegemewa kufanyika katika kipindi cha miaka mitano ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano (2015 - 2020) chini ya Rais Dkt. Magufuli.

 

WAKRISTO WATAKIWA KUPANDA MBEGU BORA WAPATE MAVUNO MENGI

$
0
0

Mtumishi wa Mungu Mwalimu Joyce Mwakalasya  baada ya kutoa mafunzo ya upandaji wa mbegu kwa waumini wa Kanisa la Moravian Usharika wa Kijichi jijini Dar es Salaam Jumapili.

Mchungaji wa Kanisa la Moravian Usharika wa Kijichi jijini Dar es Salaam, Raphael Mwampagatwa (kulia) akiwa na  Mtumishi wa Mungu Mwalimu Joyce Mwakalasya  (katikati) baada ya kutoa mafunzo ya upandaji wa mbegu. Kushoto ni mke wa mchungaji huyo.
Waumini wa kanisa hilo wakifurahi.
Waumini wa kanisa hilo wakibadilishana mawazo baada ya mafunzo hayo. Katikati ni mmoja wa Wazee wa kanisa hilo, Mwalimu Mary Anyitike.

Na Dotto Mwaibale

WAKRISTO wametakiwa kupanda mbegu bora kwa kumtolea Mungu sadaka ili waje wavune mavuno mengi.

Ombi hilo limetolewa na Mtumishi wa Mungu Mwalimu Joyce Mwakalasya wakati akitoa mafunzo ya upandaji wa mbegu kwa waumini wa kanisa la Moravian Usharika wa Kijichi jijini Dar es Salaam Jumapili.

Mwakalasya alisema suala la upandaji wa mbegu ni la muhimu wakati wa kumtolea Mungu sadaka kwani huwezi ukatoa sadaka ndogo wakati unayo kubwa ukategemea kubarikiwa.

"Hata kabla ya kwenda kutoa sadaka yako Mungu anakuwa anaijua hivyo tunapokwenda kuitoa mbele ya madhabahu tutoe kwa uaminifu ili uje uvune mavuno mengi baada ya kuipanda." alisema Mwakalasya.

Alisema kabla ya kupanda mbegu yako hiyo unapaswa kujua unaipanda eneo gani na kwa wakati upi na si kila eneo utakapo ipanda itastawi.

Mwakalasya alitaja uvivu na uzembe kwa mkristo kuwa ni adui mkubwa wa upandaji mbegu hivyo alitoa rai ya kufanya kazi kwa bidii kwani huwezi kumtolea Mungu sadaka bila ya kuwa cha chanzo cha mapato.

Alitaja vitu vingine ambavyo vinakwamisha kupanda mbegu  ni mtu kuwa na imani haba, wivu usiofaa, uchoyo, ubinafsi, kutosamehe, kufanya kazi isiyo halali na kutolipa kodi ya serikali.

Alitaja changamoto nyingine zinazo changia kuzolotesha upandaji wa mbegu kuwa ubinafsi, hofu, kutokuwa na moyo wa kuthubutu kufanya jambo, kiburi,  ushirikina na kuwaza kinyume cha matokeo.

Alisema mkristo akifanikiwa kuyashinda mambo hayo ni lazima atapata mafanikio Mungu ni zaidi ya yote kwani aliweza kuwa saidia akina Eliya na wengine wengi hivyo ukimtolea sadaka kamilifu kwa kupanda mbegu atakubariki.

Mwakalasya alitumia nafasi hiyo kuwaambia waumini hao kuwa mara baada ya kuvuna mavuno yao yaliyotokana na upandaji mbegu wayatumie kuwa saidia watu wenye uhitaji.

UZINDUZI KIJANISHA WILAYA YA IKUNGI-SINGIDA YASHIKA KASI

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akiongoza zoezi la maadhimisho ya uzinduzi wa upandaji miti kitaifa kwa ngazi ya wilaya mkoani Singida hivi karibuni.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi akishiriki zoezi hilo kikamilifu.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo (kulia)na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi kwa pamoja wakiwajibika kwenye maadhimisho hayo.

Mkuu wa Idara ya Usafishaji na Mazingira, Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Onesmo Rwehumbiza akipanda mti.

Mtendaji wa Kata ya Dung’unyi Yahaya Njiku na Kamanda wa Jeshi la Akiba wilaya ya Ikungi Massawe wakishiriki zoezi hilo.
Askari wa Jeshi la Akiba wakisikiliza hotuba ya DC Mpogolo kabla ya kuanza zoezi la kupanda miti kwenye maadhimisho hayo.
Watumishi wa Vitengo na Idara mbalimbali wakisikiliza hotuba ya DC Mpogolo kabla ya kuanza zoezi la kupanda miti kwenye maadhimisho hayo .
Maadhimisho ya uzinduzi wa upandaji miti yakiendelea.
Maadhimisho ya uzinduzi wa upandaji miti yakiendelea.
Maadhimisho ya uzinduzi wa upandaji miti yakiendelea.
Kazi ikiendelea.
Kazi ikiendelea.
Afisa Tawala wa Wilaya ya Ikungi akishiriki ipasavyo zoezi hilo..
Mhifadhi Misitu wa TFS kutoka Wilaya ya Ikungi, Wilson Pikoloti akishiriki maadhimisho hayo.

Mwonekano wa mradi wa ujenzi unaoendelea wa Majengo ya itakayokuwa Hospitali ya Wilaya ya Ikungi.

Afisa Tarafa wa Ikungi, Josephina Kadaso, akishiriki kupanda miti.
 



Na Dotto Mwaibale, Singida


MKUU wa Wilaya ya Ikungi mkoani hapa, Edward Mpogolo ameongoza mamia ya watumishi katika maadhimisho ya uzinduzi wa upandaji miti kiwilaya, ikiwa ni safari ya mwendelezo wa shabaha iliyopo ya hitaji la kufikisha idadi ya miti isiyopungua 709,000, huku kila kaya ikitarajia kupanda miti 10 kwa msimu wa 2020/2021.

Katika uzinduzi huo uliofanyika hivi karibuni, jumla ya miche ya miti 400 ilipandwa eneo la kijiji cha Muungano, mahali unapotekelezwa mradi wa ujenzi wa majengo ya itakayokuwa hospitali ya Wilaya ya Ikungi, huku miti mingine takribani elfu 30 inayozalishwa na TFS ikitarajiwa kusambazwa na kupandwa kwenye taasisi nyingine zote ndani ya wilaya hiyo.

“Shabaha yetu kwa mwaka huu kwanza ni kupanda zaidi ya miche laki saba lakini pia tunatarajia kupanda zaidi ya miche ya korosho milioni moja. Na kuhusu miche ya korosho tayari Jeshi la Kujenga Taifa hapa wilayani wameshazalisha zaidi ya miche laki 3…kikubwa tuendelee kuhamasishana,” alisema Mpogolo

Aidha, aliwataka wakazi wanaoishi ndani ya wilaya hiyo kuhakikisha idadi iliyopangwa ya kupanda miti 10 kwa kila kaya inatekelezwa kikamilifu kwa kiwango cha kuchanganya aina mbalimbali za miti ikiwemo ile ya mbao, lakini bila kusahau kupanda nje ya nyumba zao miti ya kivuli, miembe, korosho na palachichi.

Hata hivyo, aliwataka TFS kuongeza idadi ya uzalishaji miche kutoka elfu 30 iliyopo kwa sasa na kufikia angalau elfu 50 ili kukidhi hitaji la miti hiyo kwa kuzingatia jiografia ya ukubwa wa maeneo yanayozunguka wilaya hiyo ikiwa ni kubariki jitihada zinazoendelea katika kukabiliana na ukame.

“Kwa mwaka huu sitarajii tena kuona kuna upotevu wa miti, nikuombe Mkurugenzi tusimamie kikamilifu sheria zetu ndogondogo ili kutunza hii miti ambayo tumeanza kuipanda leo na tutakayoendelea kuipanda kwa mwaka mzima. Msiruhusu mifugo iwe sababu ya upotevu wa miti yetu,” alisema Mpogolo na kuongeza:

“Tumeamua kufanya uzinduzi huu kwenye hospitali hii sababu tunataka wagonjwa wetu wanapofika hapa wapumzike vizuri na wapate kivuli na hewa safi. Rais John Magufuli ametupatia jumla ya shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa majengo haya ya hospitali yetu ya wilaya…tunataka siku akija kuizindua basi akute kuna mazingira rafiki na uoto wa miti ya kutosha.”

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Wilaya aliagiza kuhakikisha wale wote waliovamia maeneo ya misitu ya Minyughe na Mlilii wanaondoka mara moja ili kuokoa bionuai za misitu hiyo iliyopo ndani ya wilaya ya Ikungi, ambayo siku hadi siku imeendelea kuathiriwa na uvamizi huo unaenda sambamba na shughuli za kibinadamu.

“Kwa bahati nzuri TFS kwa kushirikiana na Halmashauri wameanza kutenga baadhi ya maeneo na tumeshaanza kuangalia athari zilizojitokeza kwenye misitu hiyo ili kukamilisha taratibu zote kuwezesha msitu kupimwa na kupata GN ili tuweze kuumiliki kisheria,” alisema.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ikungi Justice Kijazi alisema uoto wan chi yetu ni kitu muhimu na ili tuweze kurithisha uoto huo kwenye kizazi kinachokuja tunapaswa kutengeneza mazingira mazuri ya upandaji miti kama zoezi endelevu kwa mfano wa tukio la uzinduzi huo.

Alisema kwa Halmashauri ya Ikungi kuanzia mwaka 2016/2020 imefanikiwa kupanda miti 1,385,900 lakini kati ya hiyo iliyopona mpaka sasa ni 145,860 sawa na asilimia 63.

“Tatizo kubwa linalosababisha uharibifu wa miti inayopandwa ni mifugo inayozunguka kwenye maeneo yetu. Natambua mifugo ni neema lakini wengi wetu tunaifuga kiholela,” alisema Kijazi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Usafishaji na Mazingira, Halmashauri ya Ikungi, Onesmo Rwehumbiza, alimweleza Mkuu wa Wilaya kwamba kuna misitu miwili ya asili ya Hifadhi, yaani Miili na Minyughe, lakini misitu hii kwa sasa imevamiwa na watu zaidi ya 1200 kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya wilaya ya ikungi.

“Pamoja na halmashauri ya wilaya kujitahidi kuweka mabango ya kukataza mtu yeyote kuingia kwenye hifadhi hizo lakini bado wananchi wanakaidi agizo hilo kwa kuendelea kuingia hifadhini na kufanya uharibifu mkubwa kwenye misitu hiyo ya asili,” alisema Rwehumbiza.


MAENEO YENYE MIFUMUKO YA MADINI LAZIMA YARASIMISHWE - PROF. MANYA

$
0
0

Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya akingumza jambo na baadhi ya wadau wa Madini pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu.

 Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya katikati, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka na kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula  wakiwa kwenye kikao kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo

Baadhi ya wadau wa Sekta ya Madini wakifuatilia kikao cha Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya.
Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya akitoa ufafanuzi mara baada ya kikao baina yake na wadau wa madini.
Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya akitoa ufafanuzi mara baada ya kikao baina yake na wadau wa madini.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula akizungumza jambo katika kikao cha Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya, kushoto ni Naibu Waziri wa Madini Prof. Manya.

 
Na Tito Mselem Simiyu,

Imeelezwa kuwa mfumuko wa madini (Rush) ni dharura tu, lazima sehemu zote zenye mifumuko ya madini zirasimishwe ili maeneo hayo yaweze kuchangia maduhuli ya Serikali.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya kwenye kikao baina yake na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo.

Prof. Manya amesema mfumuko wa madini ni kitu cha mpito hakitaachiwa kiendelee kwa muda mrefu na badala yake kirasimishwe ili kisadie kwenye ushirikishwaji wa watanzania kwenye rasilimali ya madini ambayo watanzania wote wanatakiwa kunufaika nayo.

“Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alisema wachimbaji wadogo watafutiwe maeneo ya kuchimba ila lazima wazingatie taratibu na sheria ikiwa ni pamoja na kuwa na leseni ya uchimbaji madini husika”, alisema Prof. Manya.

Prof. Manya aliongeza kuwa, Mkoa wa Simiyu umebarikiwa kuwa na madini mbalimbali ikiwemo madini ya metali kama dhahabu, shaba na nikeli, madini ya ujenzi kama mawe, kokoto, moramu na mchanga, madini ya vito kama amethyst na madini ya viwandani kama chokaa na chumvi.

Aidha, Prof. Manya amesema baadhi ya wachimbaji na wadau wengine wa shughuli za madini hawaelewi vyema Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na Marekebisho yake ya mwaka 2017 kuhusu haki ya leseni ya madini na haki ya ardhi hivyo kupelekea wamiliki wa ardhi kutowaruhusu waliopewa haki ya leseni madini kutofanya makubaliano ya fidia katika maeneo yao na kupelekea shughuli za uchimbaji kutofanyika katika maeneo yaliyotolewa leseni.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula amesema Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini imeshafanya mazungumzo na baadhi ya mabenki ili wapatiwe mikopo wachimbaji wadogo wa madini na kuwatoa hofu ya kwamba wachimbaji wadogo hawakopesheki.

“Tuliziambia taasisi za kibenki kwamba wale ambao wana leseni hai wakopeshwe, hivyo wachimbaji wanapaswa kujiunga ili wapatiwe leseni na waondokane na mfumo walionao wa mifumuko ya madini ambapo wanachimba bila leseni, lazima leseni zitolewe na Rush zikome mara moja”, alisema Prof. Kikula.

Naye, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Mhandisi Yahya Samamba, amewataka wachimbaji wa mkoa wa Simiyu kupendana na kuachana na wivu, majungu, chuki na fitina na badala yake wachimbe kwa kushirikiana ili walete tija kwenye shughuli zao.

Pia Mhandisi Samamba amewapongeza watumishi wa Ofisi ya Madini ya Mkoa wa Simiyu kwa kuvuka lengo la makusanyo ya maduhuli ya Serikali ambapo walipangiwa wakusanye kiasi Tsh milioni 250 na badala yake wamekusanya Tsh bilioni 2.3 ambapo wamevuka lengo kwa zaidi ya asilimia 1700 ndani ya miezi sita.

Vyama vya siasa vyatakiwa kutii katiba na sheria za nchi

$
0
0

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi.

 

NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA

 

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, ametoa wito kwa vyama vya siasa nchini kuendelea kutii Katiba ya Nchi na sheria zinginezo za nchi .

Pia amevitaka vyama vya siasa viendeleze siasa za kistaarabu na kuheshimu katiba zao ikiwa ni njia ya kukuza demokrasia nchini lakini pia itachangia katika kupunguza migogoro ndani ya vyama vyao.

Jaji Mutungi ameeleza hayo leo jijini hapa kupitia taarifa yake kwa umma ambayo ni mahususi kwa ajili ya kuwatakia heri ya mwaka mpya watanzania wote, viongozi wa vyama vya siasa na wadau wa siasa za ushindani nchini. 

“Mwezi Oktoba 2020 ulifanyika Uchaguzi Mkuu wa kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani, na kwa upande wa Zanzibar uchaguzi ulihusisha Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Baraza la Wawakilishi na Madiwani ambapo Vyama vyote 19 vyenye usajili wa kudumu vilishiriki uchaguzi kwa kuweka wagombea katika nafasi mbalimbali,” alisema . 

Na kuongeza kuwa “Vyama 15 viliweka wagombea wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku Vyama 17, vikiweka wagombea wa Kiti cha Urais Zanziba na vyama vyote 19 viliweka wagombea wa Ubunge, Baraza la Uwakilishi na Udiwani kwa idadi tofautitofauti,’’amesema Jaji Mutungi.

Aidha ametoa pongezi kwa vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu  kwa kuridhia kwao kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwezi, Oktoba 2020.

“Nanavipongeza vyama vyote vya Ssasa kwa kutilia maanani suala la utulivu na utii wa sheria za nchi ikiwemo sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kwani suala hili siyo tu limedhihirisha ukomavu wa kisiasa bali limechangia mchakato mzima wa uchaguzi kumalizika kwa amani na utulivu,’’amesema . 

Na kuongeza kuwa“Ni matarajio ya mzalendo yeyote kuipenda na kuilinda nchi yake, Ni kwa dhamira hiyo hiyo sisi kama Wananchi wa Tanzania tunashukuru kwamba Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 umemalizika salama na kwa amani na kuacha nchi yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikisalia na umoja na mshikamano kama ilivyo desturi na utamaduni wetu,” amesema  Jaji Mutungi.

Hata hivyo Kwenye taarifa hiyo Jaji Mutungi ameendelea kusisitiza Watanzania kuendelea kuunga mkono maono ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyoyatoa mara baada ya kuapishwa kwa kuwa uchaguzi sasa umekwisha badala yake wananchi wote bila kujali itikadi za vyama vyao wajikite katika harakati za kuleta maendeleo ya taifa na ustawi wa wananchi wake kwa ujumla.

“Ni kwa kuzingatia haya maono hayo aliyotoa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nimeona nito rai kuwaomba  Watanzania hususan Vyama vya Siasa kwa umoja wetu, tuzingatie na kuyatekeleza kwa vitendo maono haya ya Mhe. Rais,”

Katika hatua nyingine Jaji Mutungi ametoa pongezi kwa Vyama vya CCM, ACT – Wazalendo na ADA TADEA kwa kuonesha dhamira njema kisiasa na maendeleo kwa kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar kwa maslahi ya Wanzanzibari wote.

Ameongeza kuwa ukomavu huo wa kisiasa waliouonesha uwe endelevu na mfano wa kuigwa na vyama vyote vya siasa nchini bila kujali itikadi zao pindi linapojitokeza suala linalohusu utaifa na maendeleo ya nchi kwa ujumla.

NMB yatoa msaada wa mabati kutekeleza agizo la Waziri Mkuu

$
0
0

 

Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Angelina Nkwingwa akipokea msaada wa mabati yenye thamani ya Shilingi Milioni 15 kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Sospeter Magese kwa ajili ya kumaliza ukarabati wa shule tatu zilizopo wilayani humo. Hii ni sehemu ya jitahada za benki hiyo kuunga mkono utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alilolitoa kwa mikoa yote nchini yenye upungufu wa vyumba vya madarasa kutatua tatizo hilo. Kulia ni Mbunge wa Urambo Margaret Sitta. 

 

Na Mwandishi Wetu

 

Benki ya NMB imetoa msaada wa mabati 400 kwa Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora, lengo likiwa kuhakikisha inaunga mkono utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alilolitoa kwa mikoa yote nchini yenye upungufu wa vyumba vya madarasa kuhakikisha ifikapo Februari 28, 2021 vinajengwa.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo Disemba 7, 2020 wakati akizungumza na Wakuu wa Mikoa, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI ili kuhakikisha wanafunzi wa kidato cha kwanza wanaanza masomo.

Katika kikao hicho Waziri Mkuu Majaliwa Waziri Mkuu aliagiza Ofisi ya Rais-TAMISEMI ihakikishe kazi hiyo inakamilika kwa wakati na aliwataka watendaji hao wahakikishe ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa na utengenezaji wa madawati vinafanyika usiku na mchana.

Ili kuhakikisha agizo hilo la Waziri Mkuu linatakelezwa kwa haraka, Benki ya NMB imetoa msaada huo jana kwenye Wilaya ya Urambo, ambapo thamani ya mabati hayo ni sh. Milioni 15.

Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya hiyo Angerina Nkwingwa , Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi Sospeter Magese, alisema kuwa mbali na kurejesha sehemu ya faida kwa jamii benki hiyo imeona kuna haja ya kuunga mkono utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu.

Magese alisema mara baada ya kusikia wito wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akisisitiza kwamba wanafunzi wote waliofaulu kuingia kidato cha kwanza lazima waanze masomo hawakusita kutoa msaada kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa.

“Kupitia msaada huu ambao benki ya NMB imetoa kwenu, ni matumaini yetu kuwa wilaya hii inaenda kutekeleza agizo la Waziri Mkuu, kwa wakati na kwa haraka kama ambavyo aliagiza na wanafunzi waweze kuanza masomo,” alisema Magese.

Akipokea msaada huo Mkuu wa Wilaya hiyo, Angerina Nkwingwa ameishukuru benki hiyo kwa kuendelea kuwasaidia wananchi na kueleza kuwa NMB imemwondolea aibu kwa kumvika nguo, na kuwa msaada huo umefika wakati mwafaka na kuwataka wadau wengine kuiga benki ya NMB.

Mkuu huyo wa Wilaya amewaonya wanafunzi kutotumia meza na viti  ili vidumu kwa muda mrefu kutokana na tabia ya baadhi yao kupanda juu yake na kusababisha kuharibika.

Wakati huo huo, Benki hiyo imetoa msaada wa dharura wa vifaa mbalimbali kwa wakazi wa kijiji cha Kipera na Kitongoji cha Kinyenze kata ya Mlali Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro baada ya kaya 54 kuathirika na mvua iliyoambatana na upepo mkali kuezua mapaa na kubomoa nyumba Januari 9, 2021.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo kwa mkuu wa wilaya hiyo katika kijiji cha Kipera mkoani hapa, Meneja wa benki hiyo kanda ya mashariki, Dismas Prosper alisema kuwa baada ya kupata taarifa ya wakazi hao kupata janga hilo, benki hiyo imetoa msaada wa dharura wenye thamani ya sh. Milioni tano.

Dismas alisema kuwa vifaa hivyo ni pamoja na madogoro 54, mashuka 110, mchele kilo 540, lita 110 ya mafuta ya kula na sukari 160 kwa ajili ya kugawiwa kwa walengwa katika kipindi hiki kigumu.

“NMB imekuwa ikitoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa jamii hasa wanapopata janga mbalimbali na leo tumetoa vifaa muhimu vyenye thamani ya sh5milioni ambapo tunaamini uongozi utawagawia walengwa katika kipindi hiki kigumu,alisema Dismas.

Afisa mtendaji wa kata ya Mlali wilaya ya Mvomero, Anuciata Mpina alisema kuwa Januari 9 mwaka huu mvua kubwa iliyoambatana na upepo ilinyesha na kusababisha madhara kwa kaya 54 ambapo nyumba zimebomoka na kuezuliwa mapaa huku watu 318 wakikosa makazi.

Mkuu wa wilaya ya Mvomero, Albanus Mgonya alisema kuwa baada ya kutokea kwa janga hilo kamati ya ulinzi na usalama ilitembelea nyumba za waathirika 318 na kuwataka watu wote ambayo wamekumbwa na janga hilo wasirejee katika nyumba ambazo zimebomoka upande mmoja.

Mgoya aliishukuru NMB kwa msaada huo ambao unaenda kuwaokoa wananchi ambao walikumbwa na janga hilo, ambalo alieleza limewaacha bila ya chakula ambacho walikuwa wameweka akiba.

Watumishi nane wa VETA Pwani wasimamishwa kazi

$
0
0

Ukiukwaji wa taratibu  katika kutunuku zabuni za upatikanaji mafundi jamii wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA Rufiji umesababisha kusimamishwa kazi kwa watumishi nane wa chuo cha VETA Pwani ambao walikuwa katika Kamati ya ujenzi wa chuo hicho.

Hatua hiyo imefikiwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga alipokuwa akikagua mradi wa ujenzi wa chuo hicho hivi karibuni ambapo aligundua kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa utaratibu wa kutunuku mafundi ujenzi kupitia force akaunti uliopelekea ujenzi wa chuo hicho kuzorota.

"Kuanzia leo nawasimamisha kazi wote waliokuwa kwenye Kamati ya ujenzi na nawaagiza Takukuru kuwafanyia uchunguzi ili kubaini kilichofanya wakakiuka utaratibu kwa kiwango kikubwa hivi," amesema Kipanga.

Kamati hiyo ya ujenzi yenye jumla ya watu nane ilimtunuku fundi jamii mmoja aliyejulikana kwa jina la Phillipo Urasi, zabuni ya kujenga majengo 16 kinyume na utaratibu unaotaka fundi mmoja kupewa zabuni ya kujenga jengo moja tu.

Aidha,  Kipanga amemsitisha fundi huyo kuendelea na ujenzi na kuagiza  wachaguliwe mafundi wengine mara moja kutoka kwenye orodha ya wazabuni waliotuma maombi awali ili kazi iweze kumalizika kwa wakati.

"Naagiza pia huyo fundi Urasi asimame kazi kuanzia leo na nataka Mkurugenzi wa VETA Makao Makuu usimamie kuhakikisha wanapatikana mafundi wengine haraka, kutoka kwenye orodha ya mafundi walioomba kazi mwanzo ili kazi iendelee na kukamilika kwa wakati uliopangwa," amesisitiza  Kipanga.

Akisoma taarifa ya ujenzi, Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Pwani, Clara Kibodya amesema kuwa mpaka sasa wameshapokea jumla ya Sh. Bilioni 1.1 na kwamba ujenzi mpaka sasa umefikia asilimia 33 na unatarajiwa kukamilika mwisho wa mwezi Machi mwaka huu.

Waliosimamishwa kazi ni Leonard Mwandumbya
Mwalimu wa  Umeme, Aibu Issa Mwalimu wa Maabara, Haji Sinani Mwalimu wa majokofu na viyoyozi, David Thobias Mwalimu wa Magari, Erasto Thomas Mwalimu wa useremala na msimamizi wa ujenzi, Tumaini Magina Mwalimu wa Electronics, Paul  Kimaro Mwalimu wa Engineering Science na Kubri  Mkwanda Afisa Manunuzi.


NECTA yatangaza matokeo, asilimia 85 waliofanya mtihani kidato cha nne wafaulu

$
0
0

Katibu Mtendaji NECTA, Dk. Charles Msonde.

BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) leo Januari 15, 2021 limetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la nne, kidato cha pili na cha nne mwaka 2020 huku yakionyesha kuwa asilimia 85 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne wamefaulu.

Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji NECTA, Dk. Charles Msonde amesema katika mtihani wa kidato cha nne jumla ya watahiniwa wa shule na kujitegemea 490,213 wakiwemo wasichana 258,323 ndio waliosajiliwa kufanya mtihani huo.

Amesema watahiniwa wa shule 434,654 waliofanya mtihani huo, 373,958 wamefaulu katika madaraja mbalimbali.

Hata hivyo amesema katika upimaji wa darasa la nne jumla ya watahiniwa 1,828,268 ndio waliokuwa wamesajiliwa kufanya mtihani huo na kati ya hao wa 917,940 sawa asilimia 50.21, huku wavulana wakiwa 910,328 sawa na asilimia 49.79.

“Kati ya wanafunzi hao waliosajiliwa wanafunzi Milioni 1.4 ndio walifanikiwa kufanya mtihani huo huku wanafunzi 123, 864 sawa na asilimia 6.77 hawakufanikiwa kufanya mtihani huo wa darasa la nne,” amesema.

Amesema katika mtihani wa kidato cha pili jumla ya watahiniwa 646,200 ndio waliosajiliwa kufanya mtihani huo ambapo kati ya hao wasichana walikuwa 344,339 sawa na asilimia 53.29 huku wavulana wakiwa 301,861 sawa na asilimia 46.71.

WAZIRI LUKUVI: WALIOPIMIWA ARDHI, WENYE OFA WAKACHUKUE HATI OFISI ZA ARDHI

$
0
0

Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Singida, Shamim Hoza (kulia) akiwasilisha taarifa ya mpango wa usimamizi wa matumizi ya ardhi kimkoa na hatua za utekelezaji wake wakati Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alipofanya ziara ya kikazi kutembelea mkoa huo.

Mkuu wa Wilaya ya Singida, anayesimamia Halmashauri za Singida Manispaa na Singida Vijijini, Mhandisi Paskas Muragiri akizungumzia mambo kadhaa yanayohusu maboresho kwenye sekta ya ardhi mbele ya Waziri Lukuvi.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akikagua mafaili na nyaraka zote zilizohifadhiwa ndani yake kwenye Masijala ya Ardhi Singida Vijijini alipofanya ziara kwenye eneo hilo, sanjari na kutoa maelekezo ya namna bora ya utunzaji wa kumbukumbu hizo kwa faida ya wananchi.
Waziri Lukuvi akitoa maelekezo juu ya maboresho kadhaa yanayopaswa kufanywa ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, alipofanya ziara kwenye ofisi za ardhi ndani ya halmashauri hiyo. Kushoto ni Afisa Ardhi na Kaimu Mkuu wa Idara hiyo, Ambroce Ngonyani
Waziri Lukuvi akitoa maelekezo juu ya maboresho kadhaa yanayopaswa kufanywa ndani ya Manispaa ya Singida, alipofanya ziara kwenye ofisi za ardhi ndani ya Manispaa hiyo. Kulia ni Afisa Ardhi Mteule, Christian Kasambala.

Waziri Lukuvi akiwa kwenye ziara ya kukagua mashamba makubwa ya mradi wa Kilimo cha Pamoja cha Korosho ‘Block Farming’ yaliyopo eneo la Masigati Wilaya ya Manyoni. Kupitia ziara hiyo aliagiza wakulima wote kwenye maeneo hayo wapatiwe hati kwa ustawi zaidi wa maisha yao.

Baadhi ya Watendaji Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Singida wakiwa na Waziri Lukuvi (hayupo pichani) kwenye ziara hiyo. Kutoka kushoto ni Naibu Kamishna wa wa ofisi hiyo Shamim Hoza, Msajili wa Hati Msaidizi Jamila Awadhi, Mpima Ardhi Mkoa Sesaria Lusingu na Afisa Mthamini Angelina Bauleni.


Na Dotto Mwaibale, Singida


WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameagiza Wakurugenzi nchini kuanza mara moja kuwapa wajibu Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji kufanya kazi ya kuratibu na kusimamia masuala yote yanayohusu shughuli za uendelezaji ardhi kwenye maeneo yao-isipokuwa kugawa na kuuza, ili kupunguza changamoto ya migogoro na kurahisisha ukusanyaji wa kodi na taarifa.

Lukuvi aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani hapa juzi, alipotembelea ofisi zote za ardhi kwenye Halmashauri za wilaya Singida Vijijini, Singida Manispaa, Ikungi na Manyoni.

“Nataka Wakurugenzi wote muwape wajibu kwa maandishi Maafisa Watendaji wote wa Mitaa na Vijiji kufanya kazi kama ‘Land Administrators’ kwenye maeneo yao. Na lazima tushirikiane nao kwa karibu kama jicho letu kule chini, fanyeni haraka jitihada ya kuwakutanisha pamoja na kuwapa uelewa kujua mambo gani ya kwenda kusimamia, hii itasaidia sana katika usimamizi wa pamoja wa ardhi,” alisema Lukuvi na kuongeza:

“Nataka ieleweke huyu Mtendaji wa Mtaa sio jukumu lake kumilikisha wala kugawa ardhi, sababu hilo ni jukumu la kamati ya wilaya ya Manispaa. Yeye atahusika tu katika usimamizi wa kila kitakachofanyika na kwa kufanya hivyo tutapokea taarifa nyingi na kwa haraka sana juu ya uendelezaji holela, ukwepaji kodi na uvunjifu wa sheria. Tukiheshimu na kufuata utaratibu huu tutapiga hatua kubwa kwenye makusanyo.

Aidha, aliwataka wananchi wote kutofanya chochote kinachohusiana na uendelezaji wa shughuli yoyote ya ardhi bila kwanza kuripoti kwa Afisa Mtendaji wa Mtaa au Kijiji hata kama umepewa kibali toka wilayani lengo ni kwanza kumfanya Mtendaji ajue ni kitu gani kinataka kufanywa kwenye mtaa wake lakini pia kama kweli kina baraka zote kisheria.

“Makamishna wa mikoa simamieni hili sababu lengo la serikali hapa ni kutaka kudhibiti ujenzi holela ndani ya miji na kuhakikisha kila kinachoendelezwa kipo kwenye taratibu za michoro ya mipango miji na kimefuata sheria hata kama eneo ni lake. Na hao watendaji watengeneze mtandao na wajumbe wao ndani ya serikali za mitaa ili kupeana taarifa nani anajenga wapi na kwa wakati gani,” alisisitiza Lukuvi.

Katika hilo aliagiza kila Mtendaji wa Mtaa apatiwe jedwali maalumu litakalokuwa na orodha ya kutambua wangapi kwenye mtaa wake wamemilikishwa ardhi kwa hati, na wanamiliki nini, nani anastahili kulipa kodi ya pango la ardhi, na zile hati wanazomiliki wameendeleza nini ijulikane!-azma ni kusaidia namna ya kuwakumbusha na kuchukua kodi kwenye maeneo hayo.

Hata hivyo, Lukuvi aliwataka maafisa ardhi wa wilaya kutoficha taarifa badala yake wahakikishe kila mmilikaji mpya wa ardhi anayepatikana ndani ya wilaya basi taarifa zote zinamfikia Mtendaji wa Mtaa husika, lengo ni pamoja na mambo mengine, kurahisisha uhakiki wa taarifa na utunzaji kumbukumbu katika muktadha wa kuwatambua wote wanaomiliki ardhi kwenye mitaa mbalimbali nchini.

Hata hivyo, Waziri alishauri vitolewe vipande vidogo-vidogo ndani ya Mpango wa Matumizi ya Ardhi (Masterplan)kwa kila Manispaa na Halmashauri ‘Final Draft’ vinavyohusu mpango wa kila mtaa na akabidhiwe Mtendaji ili kumwezesha kuoanisha kama kinachoendelezwa kwenye ardhi kinafanana na mpango uliopo.

“Agizo na maelekezo haya nataka kabla ya bajeti yawe yametekelezwa na taarifa hizi ziwe mitaani kwa maana ya taarifa za wamilikishwaji wote kwenye mitaa ziwe zimeshapatikana na zipo kwa watendaji wa mitaa nchi nzima. Makamishna simamieni hili nitapita kukagua,” alisisitiza Lukuvi.

Katika hatua nyingine, akiwa wilayani Manyoni  mbali ya kupongeza juhudi kubwa zilizofanyika katika mpango wa matumizi bora ya ardhi kwenye eneo la Masigati na Kinangali unapotekelezwa Mradi wa Kilimo cha Pamoja cha zao la Korosho kupitia mashamba makubwa (Block Farming), aliagiza wakulima wote wanaotekeleza mradi huo wapatiwe hati mara moja ili ziwasaidie kuweza kukopesheka. 

 

Hawa ndio wanafunzi 10 bora kitaifa waliofanya vizuri

$
0
0

BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne na kutoa orodha ya wanafunzi 10 bora waliofanya vizuri katika mtihani huo.

Akitangaza wanafunzi hao na shule zao za sekondari kwenye mabano leo Januari 15,2021 jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa baraza hilo Dk. Charles Msonde amewataja kuwa ni Paul Luzinga (M) (Pandahili Mbeya), Justina Gerald (F) (Canossa-Dar es Salaam), Timothy Segu (Mzumbe-Morogoro), Isaya Rukamya (M) (Feza Boys- Dar es Salaam).

Wengine ni Ashrafu Ally (M) (Ilboru- Arusha), Samson Mwakabage (M) (Jude-Arusha), Derick Mushi (M) ( Ilboru-Arusha), Layla Atokwete (F)(Canossa- Dar es Salaam), Innocent Joseph (M) (Mzumbe-Morogoro) pamoja na Lunargrace Celestine (F) (Canossa-Dar es Salaam).

Hata hivyo katika matokeo hayo, Shule ya Sekondari Cannosa ndiyo iliyong’ara zaidi kwa kuingiza wanafunzi watatu kwenye orodha ya wanafunzi 10 bora kitaifa.

WAZIRI CHAMURIHO ARIDHISHWA NA UJENZI WA DARAJA LA SIBITI

$
0
0

 

Muonekano wa sasa wa Daraja la Sibiti ulivyokamilika, lenye upana wa mita 81,ambapo mita 41 zipo katika Mkoa wa Singida na mita nyingine 41 zipo katika mkoa wa simiyu na limegharimu takribani shilingi bilioni 28.


Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Leonard Chamuriho, ameridhishwa na ujenzi wa daraja la Sibiti linalounganisha mkoa wa Simiyu na Singida.

Waziri Chamuriho ameyasema hayo mkoani Singida wakati alipokagua daraja hilo lililokamilika kujengwa na mkandarasi Hainan International na kuimarisha usafirishaji wa mazao na huduma za usafiri kati ya wilaya ya Meatu na Mkalama.

"Daraja limekamilika hivyo basi naagiza Wakala wa Barabara (TANROADS), kukamilisha ujenzi wa barabara za maungio ya daraja zenye urefu wa kilometa 25, ili daraja liwe imara na usalama zaidi", alisema Waziri Chamuriho.

Aidha, ameiagiza TANROADS kulitunza daraja hilo ili liweze kutumika kwa muda mrefu.

Awali akitoa taarifa, Meneja wa TANROADS mkoa wa Singida, Mhandisi Masige Matari, amemueleza Waziri Mhandisi Chamuriho kuwa Daraja hili lina upana wa mita 82, ambapo mita 41 zipo katika mkoa wa Singida na mita nyingine 41 zipo katika mkoa wa Simiyu.

Mhandisi Masige, amefafanua kuwa ujenzi wa daraja na barabara zake za maungio utafungua uchumi wa wananchi wa Kanda ya Kati na Kanda ya Ziwa na pia itapunguza kilometa 200 ambazo zilikuwa zikitumika kutoka Singida hadi Musoma kwa kupitia Nzega, Shinyanga, Mwanza hadi Musoma.

"Ukipita njia ya Nzega, Shinyanga, Mwanza hadi Musoma ni kilometa 720 lakini ukitokea Singida, Simiyu mpaka Musoma ni kilometa 520 hivyo basi barabara hii ni njia fupi kwa wasafiri na wasafirishaji", amesema Mhandisi Masige.

Vile vile wananchi wanaopita katika Daraja hilo wameishukuru Serikali kwa ujenzi wa Daraja hilo la Sibiti na kufanya usafirishaji uwe wa haraka tofauti na hapo mwanzo, mvua zikinyesha usafiri ulikuwa wa shida sana.

Takriban shilingi bilioni 28 zimetumika katika ujenzi huo.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI, MHANDISI KASEKENYA AIPONGEZA TMA

$
0
0

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya (katikati) akizungumza na uongozi na menejimenti ya Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA) katika ziara yake kuitembelea taasisi hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Dkt. Buruhani Nyenzi pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agness Kijazi (kulia).
Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agness Kijazi (kulia) akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya (katikati) katika ziara yake kuitembelea taasisi hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Dkt. Buruhani Nyenzi. 

Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agness Kijazi (kulia) akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akitembelea shughuli anuai za taasisi hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Dkt. Buruhani Nyenzi. 

Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri – TMA, Bw. Samwel Mbuya akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akitembelea shughuli za TMA.

Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA, Dk. Hamza Kabelwa (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya (katikati) alipofanya ziara ofisi za TMA. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agness Kijazi.

Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi wa TMA, Dk. Ladislaus Chang'a (wa pili kulia)  akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya (kulia) alipotembelea TMA.

Sehemu ya menejimenti ya TMA wakifuatilia maelekezo ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya.

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, ameipongeza Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA) kwa ufanisi na utendaji mzuri wa kazi zao kiasi ambacho taifa linatambuliwa na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na shughuli zake kutegemewa na nchi za jirani.

 

Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema hayo jana katika ziara yake alipotembelea na kujionea shughuli na majukumu ya TMA ofisi kuu za mamlaka hiyo zilizopo Jengo la Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam, kupokea taarifa ya utendaji na kuzungumza na menejimenti ya TMA. 

 

"...Kwanza niwapongeze sana kwa kazi nzuri mnayoifanya, sasa endeleeni kuboresha zaidi. Kimsingi nimefarijika sana kusikia Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agness Kijazi pia ni Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) hii ni hatua kubwa. Kutambulika kwa Dkt. Kijazi kimataifa ni sifa kwa taifa letu hivyo nawapongeza sana.

 

"Nimesikia pia Tanzania, imepewa jukumu na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) kusaidia mataifa takribani matano jirani zetu upande wa hali ya hewa hii pia ni sifa kwa taifa letu na kukubalika," alisema Naibu Waziri Mhandisi Godfrey Kasekenya alipokuwa akizungumza na uongozi wa TMA. 

 

Aliitaka TMA kutambua mchango wa wafanyakazi wanaofanya vizuri na hata kuwapongeza na wale wasiowajibika kuwajibishwa ili kuongeza ari ya utendaji ndani ya mamlaka. Aidha ameitaka TMA kuhakikisha taarifa zao zinasaidia katika ujenzi wa miundombinu nchini na pia kuwa na utaratibu mzuri wa kuziifadhi kisasa ili ziendelee kulisaidia taifa leo na hata hapo baadae zitakapo hitajika.

 

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Kasekenya ameviomba vyombo vyote vya habari nchini kusaidia kusambaza taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na TMA kwa wananchi ili ziweze kuwasaidia wananchi kujua na kufuata ushauri wa mamlaka. Alisema licha ya mamlaka hiyo kuchakata taarifa nzuri za hali ya hewa itakuwa kazi bure kama hazitawafikia wananchi mapema na ama kujihami au kujipanga kulingana na ushauri wa wataalam hao.

 

Awali akitoa taarifa kwa Naibu Waziri, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agness Kijazi alisema viwango vya utoaji wa taarifa sahihi vya TMA vimeendelea kuboreshwa mwaka hadi mwaka na kuishukuru Serikali kuongeza vifaa na wataalam pamoja na kuwaongezea ujuzi kielimu mara kwa mara.

 

"...Tunaishukuru Serikali kwa kutuwezesha kuanzia vifaa vya kisasa, wafanyakazi pamoja na kutuongezea ujuzi kielimu hii yote ni kutuwezesha kufanya kazi zetu vizuri zaidi. Tuna kuhakikishia tutaendelea kufanya kazi kiufanisi zaidi na kuzingatia maelekezo ya Serikali ili kulisaidia taifa," alisema Dkt. Agness Kijazi.

DKT. NDUGULILE AIPONGEZA TTCL KWA KUJIENDESHA KWA FAIDA

$
0
0


Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo kwa Mameneja wa Mikoa wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (hawapo pichani) wakati akifungua kikao cha utendaji kazi wa Shirika hilo, Dodoma.  Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Waziri Kindamba.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akizungumza kumkaribisha Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Faustine Ndugulile (aliyeketi katikati) kabla ya kufungua kikao cha utendaji kazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Dodoma. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Waziri Kindamba.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Waziri Kindamba akifafanua jambo kwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (aliyeketi katikati) kwenye kikao cha utendaji kazi wa Shirika hilo kilichowakutanisha Mameneja wa Mikoa wote wa Shirika hilo (hawapo pichani), Dodoma. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi.

 

 

  

Na Prisca Ulomi, WMTH

 

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile amelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa kujiendesha kwa faida na kupunguza hasara kwa kipindi cha miaka mitano na kuacha kuacha TTCL kwa hasara

 

Dkt. Ndugulile ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha utendaji kazi wa Mameneja wa mikoa yote wa Tanzania Bara na Zanzibar wa TTCL na Menejimenti ya Shirika hilo kilichofanyika kwenye ukumbi wa Jeshi la Zimamoto, Dodoma

 

Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba amemweleza Dkt. Ndugulile kuwa Shirika lake limeweza kujiendesha kwa faida kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita kuanzia mwaka 2016/2017 kwa kutengeneza faida ya shilingi bilioni tano kwa mwaka tofauti na miaka mitano iliyopita kuanzia mwaka 2016 kurudi nyuma ambapo Shirika limekuwa likijiendesha kwa hasara

 

Dkt. Ndugulile ameitaka TTCL kuacha kufanya biashara kwa mazoea bali wawe wabunifu, wafanye utafiti wa masoko ili kubaini mahitaji ya wateja, kuongeza wateja na kwenda sambamba na ushindani kwa kuwa mpaka sasa TTCL ina asilimia mbili ya wateja wa simu za mkononi kwenye soko ukilinganisha na kampuni nyingine na jumla ya wateja milioni 1.3 wa simu za mkononi

 

Amewaita Mameneja wa Mikoa yote ya TTCL nchi nzima ili wajadaliane na kuweka malengo yanayopimika kwa kuwa hivi sasa kiasi cha shilingi trilioni 12 zinazunguka kwenye huduma ya fedha mtandao kwa mwezi na miamala isiyozidi milioni 300 kwa mwezi zinapita mtandaoni ili TTCL itumie fursa hii kufanya biashara na kutoa gawio

 

Amesisitiza kuwa kila Meneja wa Mkoa wa TTCL apewe malengo ya kuongeza wateja, kushughulikia malalamiko ya wateja kwa wakati, kutoa huduma nzuri kwa wateja na kuhakikisha kuwa ukuaji wa kuridhisha wa TTCL unaonekana

 

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi amewaeleza Mameneja hao kuwa watumie mbinu za kuongeza wateja na kutengeneza mazingira ya kukubalika katika maeneo wanayotoa huduma kama ilivyo kwa waganga wa tiba za asili na wahubiri wa dini ambapo wamejenga imani na wanatoa huduma kwa wafuasi wao

 

Pamoja na kikao hicho, washiriki wamepatiwa mada kuhusu Mkakati wa Kurahisisha Uongozi na Ushirikiano na Ofisi za Serikali Mikoani na Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoka kwa Johnson Nyingi wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI na mada kuhusu utawala bora kutoka kwa Apolinari Tamayamali, Mkurugenzi wa Utawala Bora, Ofisi ya Rais – Ikulu

Magereza waokoa Bilioni 11 za Chakula cha Wafungwa

$
0
0

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya  Nchi, Khamis Hamza Chilo(watatu kushoto), akimsikiliza   Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee (kulia) akimpa maelezo ya mashine ya kukatia chuma,leo  wakati naibu waziri huyo alipotembela Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Samani cha jeshi hilo kinachojengwa Msalato jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 

 

Na Mwandishi Wetu

 

Jeshi la Magereza nchini limeokoa jumla ya Shilingi Bilioni 11, ikiwa ni gharama ya chakula cha wafungwa tangu lianze kujitegemea kwa chakula ikiwa  ni maelekezo ya Rais  Dkt. John Pombe Magufuli ya kulitaka jeshi hilo litumie nguvu kazi ya wafungwa ilionao kuzalisha chakula.

Akizungumza leo katika ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,iliyofanyika katika Makao Makuu Mapya ya Jeshi hilo ,Msalato jijini Dodoma, Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee amesema walikuwa wanatumia Shilingi Bilioni Moja kila mwezi kulipa wazabuni wa chakula waliokuwa wanaliuzia chakula  jeshi hilo.

“Sasa hivi tunajitegemea asilimia kubwa kwa chakula, Serikali kabla ya mwezi wa tatu mwaka jana kila mwezi kulikua kuna deni la Bilioni Moja, lakini baada ya mwezi huo wa tatu sasa tunaokoa kiasi hicho cha fedha shilingi bilioni moja na mpaka sasa tuna miezi kumi na moja tunajilisha wenyewe kupitia shirika la magereza” alisema CGP Mzee.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Naibu Waziri, Khamis Hamza Chilo alilipongeza Jeshi la Magereza kwa kutekeleza vyema agizo la Rais Magufuli ikiwa sambamba na ujengaji wa kiwanda kikubwa cha samani ambapo mpaka kukamilika kwake kitagharimu shilingi Bilioni 1,101,743,123/=

“Niwapongeze kwa hatua mbalimbali za maendeleo ambazo zingine nimeshuhudia mwenyewe,lakini kubwa kuweza kujitegemea kwa chakula cha wafungwa hali iliyopelekea kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho kinabaki humu humu ndani na mnakitumia kwa shughuli zingine za maendeleo hongereni sana” alisema Naibu Waziri Chilo.


MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIORI IKULU CHAMWINO DODOMA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo Januari 15,2021 ameongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kilichoketi Ikulu Chamwino Jijini Dodoma kwa ajili ya kupita Mapendekezo Makuu matatu.
 

Kikao hicho cha Baraza la Mawaziri kilichoketi chini ya Mwenyekiti wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kimepitia Mapendekezo ya Mpango wa Tatu  wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/2025/26. 

 

Aidha Kikao hicho pia kimepitia Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti  ya Serikali kwa Mwaka 2021/22 na Mapendekezo ya Mpando wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22.

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR HAWATAKA WAZANIZAR KUWA NA MSHIKAMANO

$
0
0

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman akitoa salamu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya kukamilika ka Ibada ya Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Amani.

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla alisema mshikamano wa pamoja kati ya Viongozi, Waumini wa Dini pamoja na Wananchi mahali popote walipo ndio njia ya msingi itakayorahisisha kulijenga Taifa imara.

Akitoa salamu mara baada ya kukamilika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Ijumaa pembezoni mwa Uwanja wa Michezo wa Aman Mheshimiwa Hemed Suleiman aliwakumbusha Waumini hao kwamba kila Mwananchi ana nafasi yake katika kujenga Nchi si lazima ame Mtumishi wa Umma.

Mheshimiwa Hemed alisema hatua hiyo ya mshikamano wa pamoja ambayo Serikali Kuu tayari imeshaonyesha muelekeo wa mfano katika ngazi ya Uongozi itawezekana na kufanikiwa ipasavyo endapo jamii nzima itaendelea kuhamasishana katika usimamizi wa masuala ya Amani.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitahadharisha kwamba yapo Mataifa Duniani baadhi ya Waumini wake wenye Imani ya Uislamu wameshindwa kutekeleza Ibada ya sala ya Ijumaa kutokana na machafuko yaliyosababishwa na Itikadi za Kisiasa au Kidini.

Mheshimiwa Hemed Suleiman alihimiza umuhimu wa Waumini na Wananchi kuendelea kuzingatia Uadilifu katika matendo yao kama ulivyosisitizwa katika Hotuba ya Ijumaa ili kuleta utulivu wa moyo ndani ya vifua vya Watu katika maeneo yao.

Alieleza kwamba changamoto za Kijamii kwa asilimia kubwa zinaweza kuondoka au kupungua kabisa kama ulafi wa baadhi ya Watu hasa katika masuala ya Fedha utadhibitiwa jambo ambalo hivi sasa Serikali Kuu imekuwa ikiendelea kuchukuwa hatua za kukabiliana nalo.

Aliwahimiza Wananchi pamoja na Waumini wa Dini kuvumilia kipindi hichi ambacho Uongozi wa Serikali umekuwa ukichukuwa hatua hizo zinazoonyesha mwanga kwa baadhi ya Washirika wa Maendeleo ndani na Nje ya Nchi kwa kutaka kuungwa mkono jitihada hizo za Serikali.

Mapema akitoa Hotuba ya sala ya Ijumaa Mwanachuoni Maarufu Ustaadh Rajab Mohamed Shaali aliwakumbusha Waumini wa Dini ya Kiislamu kuhakikisha kwamba suala la uadilifu linapewa nafasi yake ili Jamii Mitaani iendelee kuishi kwa upendo.

Ustaadhi Rajab alisema Utamaduni wa baadhi ya Watu kupenda kujilimbikizia Mali za dhulma sio malengo ya uwepo  wao Duniani katika kufanya ibada bali unazidisha chuki na uhasama miongoni mwa Jamii  katika ngazi ya ufukara, umasikini na utajiri.

Mapema asubuhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla alikutana na Uongozi wa Jumuiya Wazee Wastaafu Zanzibar ili kubadilishana mawazo  mazungumzo yaliyofanyika Afisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Katika mazungumzo hayo Mh. Hemed alisema Serikali itaendelea kuwaheshimu Wazee wote Nchini kwa kuwapatia huduma stahiki ikitimiza wajibu wake ili waendelee kupata utulivu wa maisha yao  huku ikizingatia kuwa mchango wao ndio uliosababisha Taifa hili kufikia hatua kubwa ya maendeleo.

Mheshimiwa Hemed alisema Serikali inaelewa changamoto na matatizo mengi yanayowakumba Wazee katika maisha yao ya kawaida na ndio maana hulazimika kufanya utafiti wa kutosha unaosaidia kupata muelekeo wa kuwajengea mazingira rafiki.

Alisema katika hatua ya kuyakidhi mahitaji yao ya lazima Wazee , Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wote imekuwa na mfumo wa kuangalia mazingira ya hali ya uchumi inavyozunguuka na pale inaporuhusu haioni tatizo nguvu hizo kuzielekeza kwa Wazee hao waliotoa mchango mkubwa kwa Taifa wakati wa utumishi wao.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akitoa ushauri kwa Viongozi hao wa Jumuiya Wastaafu alisema ipo haja ya kuendelea kutoa Elimu kwa Watumishi wanaokaribia kustaafu ili pale watakapofikia muda waendelee na maisha yao bila ya wasi wasi wowote.

Mheshimiwa Hemed alisema Watumishi wengi wanapopata barua ya kumaliza muda wao wa Utumishi huchanganyikiwa huku wakijisahau kwamba wapo Vijana wengi waliomaliza masomo yao ambao wanahitaji kuziba nafasi zao  kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma Serikalini.

Mapema Katibu wa Jumiya ya Wastaafu Zanzibar Bibi Salama Kombo Ahmed alisema Wazee wengi Nchini wamefuharia uwepo wa Sheria iliyowashirikisha moja kwa moja wazee wenyewe ingawa bado haijawa na Kanuni zake.

Bibi Salama alisema Jumuiya ya Wastaafu Zanzibar iliyoasisiwa mnamo Mwaka 2001 pamoja na mambo mengine inaendesha mradi wa kuwaelimisha Wazee kupitia Mabaraza yao ya shehia Unguja na Pemba ili kutambua kwamba Miaka 60 ya ustaafu sio mwisho wa Maisha yao.

Katibu wa Jumuiya hiyo ya Wastaafu Zanzibar kwa niaba ya wanajumuiya wameishukuru Serikali Kuu kwa uamuzi wake wa kuendelea kuwapatia Pencheni kila mwezi sambamba na ile ya Shilingi 20,000 kwa Wazee wa Zaidi ya Miaka Sabini.

 Hata hivyo Bibi Salama alisema zipo baadhi ya changamoto zinazoendelea kuwasumbua Wazee akizitaja kuwa ni pamoja na ukosefu wa Kitambulisho ili kuwapa uangalizi wa huduma za Afya na Hospitali pamoja na Uwakilishi wa Wazee katika Mabaraza ya Kutunga Sheria.

UHAKIKI WA WASTAAFU MIKOA YA MWANZA, KAGERA NA GEITA WAKAMILIKA

$
0
0

 


Afisa Tehama kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Shafii Halfan, akihakiki taarifa za mstaafu Bi. Theresia Makomu, wakati wa zoezi linaloendelea la uhakiki wa Wastaafu wote nchini wanaolipwa pensheni na Hazina, mkoani Mwanza.

 

 

 Na Josephine Majura, WFM, Mwanza


Wizara ya Fedha na Mipango imekamilisha zoezi la uhakiki wa wastaafu wanaolipwa pensheni na Hazina katika mikoa mitatu ya Mwanza, Kagera na Geita ikiwa ni hatua inayochukuliwa na Serikali kuhuisha taarifa za wastaafu hao ili kuboresha kanzidata ya wastaafu kwa lengo la kuwaboreshea huduma.


Mratibu wa zoezi hilo ambaye ni Mhasibu Mkuu, upande wa Pensheni kutoka Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, Bi. Scola Mafumba, amesema kuwa zoezi hilo limekwenda vizuri ambapo wastaafu wamejitokeza kwa wingi na kuitikia wito wa Serikali licha ya kwamba baadhi yao hali zao zilikuwa na changamoto za kiafya.


“Kumekuwa na changamoto ya hali za wastaafu ila tumejipanga vizuri ambapo baadhi yetu walienda kuwahakiki wastaafu nyumbani, tumefanya hivyo ili kuhakikisha kila mstaafu anapata huduma kama ilivyokusudiwa”, alieleza Bi. Mafumba.


Alisema kuwa timu ya wataalam wanaohakiki wastaafu itaondoka kesho kuelekea mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu ambapo zoezi hilo litaanza Jumatatu tarehe 18 hadi 22 Januari, 2021 kwenye makao makuu ya Halmashauri za Wilaya wanazoishi na kutoa wito kwa wastaafu hao kujitokeza kuhakikiwa wakiwa na nyaraka muhimu zinazotakiwa.


Bi. Mafumba alizitaja nyaraka hizo kuwa ni pamoja na Barua ya Tunzo la kustaafu au Kitambulisho cha kustaafu, Barua ya kustaafu au kustaafishwa, Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Kadi ya Mpiga kura, Kadi ya Bima ya Afya, Hati ya Kusafiria au Leseni ya Udereva na Kadi ya Benki anayopokelea Pensheni.

 

Wakati wa zoezi likiendelea timu ya wataalamu imekuwa ikipokea ushauri na maoni kutoka kwa baadhi ya wastaafu waliofika kwenye eneo la uhakiki mkoani Mwanza kwa ajili ya kufanya maboresho kwa zoezi lijalo la uhakiki.


Baadhi ya wastaafu hao akiwemo Bi. Apiah Mayagi, wameiomba Serikali kufikiria namna ya kuweka wawakilishi bungeni kwa kundi la wastaafu ili mwakilishi huyo aweze kuzisemea kero na changamoto zao kama ilivyo kwa makundi mengine likiwemo kundi la vijana, watu wenye ulemavu na wanawake.


Kwa upande wake Mstaafu Bw. Abdallah Mlima, aliiomba Serikali kuwaongezea pensheni angalau ifike kiwango cha kima cha chini cha mshahara wa mtumishi kwa kuwa wanatozwa riba kubwa benki hivyo kupunguza kiwango wanacholipwa na kuwasababishia kushindwa kumudu maisha.


Bi. Mariam Murusuri, aliipongeza Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuendesha zoezi hilo la kuwahakiki kwani itaokoa fedha nyingi za Serikali kwani anaamini kuna baadhi ya wastaafu walikuwa wanalipwa pensheni wakati wamefariki dunia na kuiomba Wizara iendeshe zoezi la uhakiki kila mwaka.


Hadi sasa Wastaafu wanaolipwa pensheni zao na Hazina wamehakikiwa katika mikoa kumi ya  Dodoma, Singida, Manyara, Tabora, Rukwa, Katavi, Kigoma, Geita, Kagera na Mwanza na kwamba zoezi hilo linatarajiwa kukamilika mwezi Machi, 2021.

 

MAKAMU WA RAIS AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI CHAMWINO DODOMA

$
0
0

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kilichoketi leo Januari 15,2021 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).




UTATA BABA MZAZI WA DIAMOND

$
0
0


Naseeb Abdul 'DiamondPlatnumz' 

 

 

 

Na Mwandishi Wetu

 

MSANII wa muziki kutoka nchini Tanzania Naseeb Abdul maarufu kama DiamondPlatnumz ameendelea kushika headlines katika vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii baada ya mama yake kusema ukweli kuhusu baba yake mzazi.

 

Kupitia kipindi cha Mashamsham kinachorushwa na redio ya Wasafi, Mohamed Salum maarufu kama ‘ricardomomo’ alijitambulisha rasmi kuwa yeye na Diamond ni mtu na kaka yake na kusema kuwa baba yao ni mmoja lakini mama ni tofauti.

 

“Nilitambulishwa kuwa Naseeb ni mdogo wangu na baba yetu mzazi ambaye ni marehemu kwa sasa, Mzee Salum Iddi Nyange hivyo mimi na Naseeb ni mtu na kaka kabisa” Alisema Ricardomomo.

 

Pia aliendelea kusema “watu wengi wamekuwa wakitaka sana kujua undugu wangu na Diamond umetoka wapi lakini nilikuwa nikisubiri wakati sahihi ufike ndio niseme ukweli, Naseeb ni mtoto wa Salum Iddi Nyange na sio mzee Abdul kama wengi wanavyojuwa, yule ni baba yake mlezi tu”.

 

Akithibitisha taharifa hizo kwa njia ya simu mama mzazi wa Diamond, Sandrah (Mama dangote), alisema taarifa hizo ni za kweli kwani aliolewa na mzee Abdul akiwa na ujauzito wa Diamond na baada ya kujifungua Abdul alikataa kumlea mtoto na kumpelekea yeye kumlea peke yake.

 

“Niliolewa na Abdul nikiwa na ujauzito wa Naseeb, na alikuwa analijua hilo na hata mtoto alivozaliwa alikataa kumlea kwa sababu sio wa kwake, baba yake na Naseeb anaitwa Salum Iddi Nyange alikuwa akiishi Kariakoo ambaye ni  marehemu kwa sasa”. Alisema mama Dangote.

 

Baada ya kumtafuta mzee Abdul ambaye anafahamika kama baba mzazi wa Diamond na kumuuliza juu ya taarifa hiyo alisema amesikitishwa sana na uamuzi wa mama Diamond kutoa kauli kama hiyo kwenye vyombo vya habari bila kumshirikisha na kusema amemdhalilisha.

 

“Mimi nimeumia sana lakini kama ndio ameamua kusema hivyo basi, ninachokijua  mimi Nasseb ni mtoto wangu na ndio maana anatumia jina langu, kama alikuwa na baba yake kwa nini aliamua kutumia jina langu?, Najua mama yake amesema haya kwasababu ya mali lakini atambue kwamba sisi sote ni marehemu watarajiwa na mali zote tutaziacha duniani”. Alisema mzee Abdul

 

Pia aliendelea kusema kuwa “Kuanzia leo sitaki Naseeb atumie tena jina langu, kama ana baba mwingine basi atumie  jina lake na akiendelea kulitumia nitamfungulia mashtaka”.

Viewing all 19659 articles
Browse latest View live