Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

Watu Milioni 100 mpaka150 utumia kiswahil

$
0
0


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili katika Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma leo Januari 19, 2021. (Picha na VPO).


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua Vitabu vya Mkakati na Muongozo wa kufundishia Lugha ya Kiswahili kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili yaliyoadhimishwa leo Januari 19, 2021 katika Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi, Wajumbe, Wadhamini na Wafanyakazi wa  Taasisi za Kiswahili baada ya Kufungua Maadhimisho ya Siku ya kiswahili katika Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma leo Januari 19, 2021.

 

 

Na Hamida Ramadhan, Dodoma


MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya watu milioni 100 mpaka 150 utumia Lugha ya kiswahili kwa ajili ya mawasiliano  na kuzitaka taasisi binafsi kuendeleza kutumia lugha hiyo.

Aliyasema hayo jana Jijini Dodoma wakati  alipokuwa kwenye Maadhimisho ya siku ya kiswahili Kitaifa yaliyoandaliwa na mabaraza ya Tanzania bara (BAKITA) na Tanzania Zanzibar (BAKIZA)huku kauli mbiu ikisema"Bidhalisha Kiswahili kwa maendeleo endelevu ya Tanzania".

Aidha alisema kuwa lugha ya kiswahili imekuwa na matumizi mapana huku ikitumika ndani na nje ya nchi kwa kufundishia kwenye vyuo vikuu vya kimataifa  mbalimbali pamoja na shule za sekondari na msingi .

Alisema kuwa lugha ya kiswahili imekuwa ikisikika kwenye Radio za kimataifa ikiwemo BBC na Radio Amerika huku kiswahili kikitumika kama bidhaaa ya kukuza kiuchumi.

Hata hivyo alisema katika kukuza kiswahili, Awamu hii ya tano kupitia Rais John Magufuli  ameweza kukiwekea mkazo kukitumia kwenye mikutano mbalimbali na hata kukitumia nje ya nchi wawapo kwenye mikutano.

"Hapo awali hakukuwa na msisitizo kwenye mikutano kuongea kiswahili lakini kupitia Rais wetu John Magufuli ameweza kuimarisha ambapo mikutano inaendeshwa kwa lugha ya kiswahili na sio kiingereza kama mwanzoni  "alisema 


"Nawaomba Taasisi binafsi wasikionee haya Kiswahili kukitumia katika ofisi zao,kwani hiyo ni.mojawapo ya kuendeleza matumizi ya lugha yetu ya Kiswahili kwani Taasisi binafsi asilimia kubwa wanaofanya kazi ni Watanzania amabo wanaongea lugha ya Kiswahili,hivyo wasione ubaya kukitumia lugha ya mawasiliano hivyo Baraza la Kiswahili Tanzania BAKITA na lile la  Zanzibar BAKIZA kuongeza wigo wa misamiati inayoeleweka"alisema

Makamu huyo wa Rais alitolea mfano neno kusimikwa ambalo alisema kwa upande wa Zanzibar ni neno Kali lenye maana tofauti limitamkwa huku Tanzania Baram.

" Nimekuwa nikiingiwa na ukakasi katika kutamka neno la kusimikwa kwa maaskofu, kwani neno Hilo kwetu Zanzibar si neno la kutamkwa hadharani", alisema Suluhu.

Aidha Makamu wa Rais alisema kuwa Serikali inaendelea kufanya jitihada za kuendeleza Kiswahili kwa kuandaa kamusi yenye maneno Millioni 50, lakini mpaka Sasa umefikia maneno Millioni 1.5.

Suluhu pia aliwataka Wakurugenzi wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo kutoa fungu kwa kuendeleza lugha ya Kiswahili kwa kuangalia maeneo ambayo Kiswahili hakitumiwi Sana.

Alisema kuwa BAKITA na BAKIZA wapewe Rasimali Watu,Fedha na watalaamu na kutoa machapisho yachapishwe kwa wingi ili yasambazwe sehemu mbalimbali.

Naye Naibu Waziri wa Habari Utamaduni.na Michezo Abdallah Ulega alisema Lugha ya Kiswahili inaenea kwa Kasi, kwani Leo lugha hiyo imekuwa si Mali ya pekee imekuwa ikitumiwa nchi nyingi Duniani.

" Hivi Sasa Duniani Kiswahili no bidhaa ambayo, Watangazaji,waandishi wa habari, watafsiri Wana soko kubwa la kupata kazi"' alisema Ulega.

Katika maadhimisho hayo Makamu wa Rais alizindua kitabu chenye muongozo wa kufundishia watu kutoka nje .



ZAIDI YA MILIONI 58 ZAOKOLEWA NA TAKUKURU MKOA WA PWANI

$
0
0

 


Naibu mkuu  wa Takukuru Mkoa wa Pwani Sadiki  Nombo akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake akitoa taariga  kuhusiana na utekelezaji wa kazi amabzo wamezifanya katika kipindi cha kuanzia mwezi Octoba hadi disemba mwaka huu. (Picha na Victor Masangu).  

 

VICTOR MASANGU, PWANI   

 

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU ) Mkoa wa Pwani imefanikiwa kuokoa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 58 ambazo zimetokana na malalamiko yaliyowasilishwa yakiwemo ya wimbi la ubadhilifu wa fedha ambazo wamedhulumiwa  wakulima  wa  zao  la  korosho ikiwemo na vikundi vya vijana wanawake na walemavu.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Naibu mkuu  wa Takukuru Mkoa wa Pwani Sadiki  Nombo kwa ajili ya kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ambayo yameyafanya kwa kipindi  cha   miezi mitatu iliyopita kuanzia mwezi Octoba hadi kufikia Disemba mwaka 2020 pamoja na mikakati waliyojiweke katika kukabliana na wimbi la rushwa.

Aidha alifafanua kuwa katika robo ya kuanzia mwezi octoba  hadi disemba mwaka 2020 Ofisi ya Takukuru iliweza kupokea mamalamiko yapatayo 196  ambapo kati ya hayo  malalamiko 113 uchunguzi wake bado endelea kufanyika ili kuweza kuwabaini wale wote waliohusika na sheria iweze kufuata mkondo wake.

Pia aliingeza kuwa katika utekelezaji huo Takukuru Wilaya ya Mkuranga waliweza kukoka kiasi cha shilingi milioni 18 ambazo zilizotoka na baadhi ya wakulima kudhulumiwa na viongozi wa bodi ya Amcos ya kimanzichana kusini.

Kadhalika katika Wilaya ya Kibiti Takukuru iliweza kuokoa kiasi cha shilingi zaidi ya shilingi milioni 18 ambazo ziliweza kuokolewa kutoka katika vikundi mbali mbali ikiwemo kwa vijana, wanawake pamoja na walemavu ambavyo vilikopeshwa na halmashauri hiyo kushindwa kurejesha mikopo hiyo.

Aidha alifafanua kuwa kupitia katika Ofisi ya Wilaya ya Kisarawe waliweza kufanya uchunguzi wa kina na kuweza kuokoa jumla ya kiasi cha  zaidi ya shilingi milioni nne amabzo ziliweza kuchangwa na wananchi wa kijiji cha Marui Ngwata kwa ajili ya kufanya ujenzi wa mradi wa zahanati ya kijiji hicho.

Kwa upande wa Ofisi ya Chalinze katika kipindi cha mwezi octoba hadi disemba mwaka 2020 iliweza kufanikia kurejesha kiasi cha shilingi milioni moja zikiwa ni sehemu ya shilingi milioni tano amabzo zimetokana na mikopo amabyo ilitolea kwa vikundi vya wanawake vijana pamoja  na watu wenye ulemavu.

Ofisi ya Takukuru Wilaya ya Kibaha waliweza kufanya uchunguzi na kuweza kuokoa kiasi cha  zaidi ya shilingi milioni tisa kutoka kwa wanunuzi wa dawa za kituo cha afya cha mlandizi ambapo manunuzi hayo yalikiukwa na utaratibu  haukuzingatiwa ipaswavyo kwani dawa ziliozagizwa kutoka kampuni binafsi ya Astra Pharma Limited.

Katika hatua nyingine Naibu huyo alibainisha kwamba Takukuru katika  kupambana vilivyo  na wimbi la rushwa ya ngono ambayo imeonekana kuwa ni chngamoto  kubwa katika baadhi ya maeneo hususan kwa wanafunzi wameanzisha kampeni maalumu ambayo itaweza kusaidia  kwa kiasi kupunguza  hali hiyo.

Takukuru Mkoa wa Pwani katika robo ya tatu kuanzia mwezi octoba hadi disemba mwaka 2020  imeweza kupokea  kesi zipatazo 27 ambazo zinaendelea kusikilizwa katika mahakama mbali mbali  pamoja na  kupokea malalamiko   yapatayo 196 ambapo kati ya hayo malalamiko 113 yapo katika hatua ya uchunguzi.

MKOA WA RUVUMA WASHIKA NAFASI NZURI KITAIFA UKUSANYAJI MAPATO

$
0
0

Mkuu  wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme.


Na Mwandishi Wetu

 

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Chritina Mndeme amewapongeza Wakurugenzi watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kusimamia ukusanyaji wa Mapato kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ambapo Halmashauri zote nane zimevuka  asilimia 80 na kufanya Mkoa kuwa katika nafasi nzuri Kitaifa.

Mndeme pia ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Mkoa wa Ruvuma kwa kufanya kazi nzuri ya kukusanya Mapato ya ndani  ya Mkoa  katika kipindi cha mwaka 2019/2020 na kuweza kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 15 sawa na asilimia 94.

“Naipongeza Halmashauri ya Tunduru  kwa kukusanya Mapato ya Ndani kwa asilimia 121.87,pia naipongeza Halamashauri ya Manispaa ya Songea tangu  imeanza kutumia stendi kuu ya Shule ya Tanga Januari1,2021  imeongeza mapato kutoka shilingi 200,000 mpaka  970,000 kwa  siku”,alisema.

Mndeme amesema Mkoa unatarajia kuimarika kiuchumi kwa kuongezeka kwa mapato yatokanayo na kodi pamoja na ushuru kwasababu Barabara ya Ushoroba wa  Mtwara imefunguka na kupelekea kutoa fursa nyingi za kibiashara na kiuchumi.

Hata hivyo amesema biashara ambazo zinapatikana maeneo mengine Nchi Jirani za Malawi na Msumbiji yanaunganishwa kwa kupitia usafiri wa Ndege kupitia Uwanja wa ndege wa Songea na barabara ya lami ya Mtwara corridor.

Amesema Meli katika Ziwa Nyasa zimeanza kazi za Usafirishaji baada ya kuzinduliwa rasmi kwa Meli ya abiria ya MV Mbeya  II Januari 5,2021 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Kassim Majaliwa ambayo inabeba abiria  300 na Mizigo tani 200.

Hata hivyo Mndeme amewaagiza Wakurugenzi kusimamia Mapato yatokanayo na Kodi pamoja na Ushuru amesema fedha hizo hutumika katika kujenga miradi ya maendeleo ikiwemo vituo vya Afya,Barabara,Ununuzi wa Ndege,Ujenzi wa Reli na  huduma nyingine za kijamii.

Ameziagiza Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma kubuni na kupanua wigo wa mapato kwa kuhimiza watu kudai Risiti na wafanyabiashara  kutoa risiti kila wanapouza  bidhaa mbalimbali.

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI DODOMA

$
0
0

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Khamis Hamza Chilo, akiwasili katika ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Nchini zilizopo Dodoma, Katika ziara hiyo amelipongeza Jeshi la Polisi nchini kwa kuendelea kutekeleza majukumu yake ipasavyo ya kudumisha Usalama wa Raia na mali zao.

     Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Khamis Hamza Chilo, akisalimiana na Makamishna wa Jeshi la Polisi baada ya kuwasili katika ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dodoma.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro kuhusu Jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Nchini lililopo Dodoma ambapo ameaidi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha Jengo hilo linakamilika kwa asilimia mia moja ili Watendaji wake waweze kutekeleza majukumu yao katika mazingira mazuri.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Khamis Hamza Chilo, akisaini kwenye kitabu cha wageni katika ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Sirro Dodoma.

WALIMU WAKUU LUDEWA WAUKUBALI MRADI WA DARASA JIFUNZE

$
0
0
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Shaurimoyo, Senebius Mtega akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni.

Mwalimu Mkuu Msaidizi Shule ya Msingi Maholong'wa, Bw. Chefasi Mdessa akizungumza ofisini kwake hivi karibuni.

Mwalimu Mkuu Msaidizi Shule ya Msingi Matika, Ludan Njuu (kushoto), kulia ni mmoja wa walimu maalum wa kujitolea wa darasa la jifunze shuleni hapo.  

Na Joachim Mushi, Ludewa

 

BAADHI ya walimu wakuu wa shule za msingi zinazotekeleza mradi wa majaribio wa Darasa Jifunze ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, mkoani Njombe wameomba mradi huo uwe endelevu ili kuwasaidia wanafunzi wanaokubwa na changamoto ya ujifunzani hadi kufika darasa la tatu na kuendelea wakiwa hawajui kusoma na kuandika. Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni wilayani Ludewa kwa nyakati tofauti na walimu hao katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi kuzungumzia maendeleo ya mradi wa darasa jifunze uliokuwa ukitekelezwa kwenye shule zao.

Mwalimu Mkuu Msaidizi Shule ya Msingi Maholong'wa, Bw. Chefasi Mdessa akizungumza amesema kuna mafanikio makubwa ya mradi huo unaotekelezwa kwa majaribio katika shule hiyo, jambo ambalo limeleta matumaini kwao na hivyo kushauri ikiwezekana mradi huo uendelee kutekelezwa katika shule za msingi zenye changamoto ya ujifunzaji. 

Alisema tathimini iliyofanywa kubaini wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika kuanzia darasa la kwanza hadi la sita katika shule hiyo, ilibainini wanafunzi 83 wakiwa hawajui kusoma vizuri na hivyo kuingizwa rasmi katika mradi wa Jifunze uliotekelezwa kwa awamu tatu zenye siku 10. Alisema ndani ya siku 30 za utekelezaji mradi huo ilifanikisha kuwawezesha idadi kubwa ya wanafunzi na kusalia 9 tu ambao walikuwa bado na changamoto hiyo.

"...Mapendekezo mengine binafsi natamani mradi huu uwe wa kudumu shuleni hapa na utumike kwa kufundishia darasa la awali, darasa la kwanza na kwa darasa la pili, naamini mafanikio tulioyapata kwa muda mfupi tukiingiza mfumo huu ukawa wa kudumu tutapunguza kwa kiasi kikubwa wanafunzi waliojua kusoma na kuandika katika shule zetu," alisema Bw. Chefasi Mdessa.

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Shaurimoyo, Senebius Mtega alisema mradi wa darasa la Jifunze ulianza kutekelezwa katika shule hiyo tangu mwezi Agosti 2020 ukiwa na wanafunzi 78 wasiojua kusoma na kuandika katika hatua mbalimbali ulikuwa na mafanikio makubwa ndani ya kipindi kifupi. Alisema wapo wanafunzi ambao walikuwa wanashindwa kusoma herufi, wengine pia kushindwa kusoma maneno na pia wapo ambao walishindwa kusoma aya; ambapo waligawanywa kulingana na changamoto zao za ujifunzaji lakini idadi kubwa ilifanikiwa.

"...Tulianza kutekeleza mradi tukiwa na wanafunzi 78, kimsingi mradi huu umetusaidia sana kwani wanafunzi wengi wamefaulu kutoka katika changamoto ya awali ya kutokumudu kusoma na kuandika kwa ufasaha. Ni mradi mzuri tunaupenda na tunapenda hata uwe endelevu hapa kwetu na hata kwenye shule zingine," aliongeza Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Shaurimoyo, Bw. Mtega.

Naye Mwalimu Mkuu Msaidizi Shule ya Msingi Matika, Ludan Njuu anasema hadi wanaanza kutekeleza mradi wa Jifunze walikuwa na jumla ya wanafunzi 75, waliokuwa na changamoto za usomaji kwenye madaraja ya aya, maneno na silabi, lakini hadi mwisho wa mradi zinakamilika siku 30 ni wanafunzi 13 pekee ndio walikuwa na changamoto hiyo, huku wengine wote wakifanikiwa kuvuka katika changamoto hiyo.

"...Kimsingi zoezi hili kama litaendelea watoto wengi walio na changamoto hiyo tunaweza kuwapunguza. Alishauri viongozi sekta ya elimu kwa kushirikiana na Uwezo Tanzania kuangalia namna ya kuufanya mradi huo uwe endelevu na kutekelezwa shule zote kwa madarasa ya awali, darasa la kwanza na la pili ili kumaliza kabisha changamoto hiyo ambayo ipo katika maeneo kadhaa," alisema mwalimu huyo.

WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI PWANI WAASWA KUJIKINGA NA MAGONJWA YA MLIPUKO

$
0
0

 Mbunge wa viti maalumu wa Mkoa wa Pwani Hawa Mchafu (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanawake wa Mkoa wa Pwani. 


 

 NA VICTOR MASANGU, PWANI 

 

MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Pwani kupitia tiketi ya Chama cha mapinduzi Hawa Mchafu amewahimiza wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuhakikisha kwamba wanajenga tabia ya kula matunda ambayo yameoshwa na maji safi na salama  pamoja na kunawa mikono yao  kwa lengo la kuweza kuthibiti hali ya mlipuko wa magonjwa mbali mbali ambayo wanaweza kuyapata.

 

Mchafu aliyasema hayo wakati akizungumza kuhusiana na mikakati yake aliyojiwekea katika  masuala  mbali mbali ya kuboresha sekta ya elimu ambapo alibainisha kuwa wanafunzi wanapaswa kuwa ana afya njema wakati wote hivyo wanatakiwa kuzingatia taratibu zote ambazo zinatolewa na wataalamu wa afya ili kuepeukana na mlipuko wa magonjwa hayo.

“Kwa sasa hivi katika baadhi ya maeneo kuna shule ambazo zina miti ya matunda mbali mbali hivyo wakati mwingine yanawez kuanguka chini na baadhi ya wanafunzi waneweza kuyaokota na kula pasipo kuyaosha lakini mimi nichukue fursa hii kuwaasa wawe na utaratibu wa kuosha mikono yao pamoja na kuosha matunda hayo hii itasaidia zaidi katika kujikinga na magonjwa,”alisema Mchafu.

Pia Mchafu aliongeza kuwa katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na mlipuko wa magonjwa mbali mbali atashirikiana bega kwa began a walimu pamoja wataalamu wa afya ili waweze kutoa mafunzo juu ya umuhimu wa kunawa mikono wakati wa kula pamoja na kuachana na tabia ya kula matunda au vyakula ambayo hayijaoshwa.

Kadhalia aliongeza kuwa lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha kwamba wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanasoma katika mazingira ambayo ni rafiki na wakiwa katika afya nzuri hivyo ni vema kukawa na mipango madhubuti katika suala zima ya usafi wa mazingira katika maeneo mabali mbali hususan katika ulaji wa vyakula.

Katika hatua nyingine aliwakumbusha wanafunzi hao pia kuhakikisha kwamba wanakunywa maji ambayo yamechemshwa ili kuondokana na kupata magonjwa  mbali mbali ikiwemo kuumwa na matumbo na ambayo mengine yanakuwa na uchafu ambao unaweza kupelekea kusababisha madhara makubwa ya kiafya.

Pia  Mbunge  mchafu  aliahidi kuendelea kushirikiana na wananchi pamoja na wataalamu wa afya katika kuweka mipango madhubuti ya kutoa elimu ya mara kwa mara hasa katika maeneo ya vijijini ili kuweza kutoa elimu ambayoitaweza kuwa ni moja ya msaada na mkombozi mkubwa wa kuwasaidia wananchi kujikinga na magonjwa ya mlipuko.

WASHINDI NMB MastaBATA WAJINYAKULIA MAMILIONI

$
0
0

 Meneja Mahusiano wa Idara ya Biashara na Kadi wa Benki ya NMB, Yusuph Achayo, akizungumza wakati wa kuchezesha droo ya Saba ya Promosheni ya Mastabata iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam. kushoto ni Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha, Pendo Albert Mfuru na kulia ni ofisa huduma kwa wateja wa Benki ya NMB, Yvette Nkhoma.


Meneja Huduma za Kadi kwa Wateja wa Benki ya NMB, Yuette Lupilli akizungumza na mmoja wa washindi wa promosheni ya mastabata wakati wa kuchezesha droo ya saba iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha, Pendo Albert Mfuru na katikati ni  Meneja Mahusiano wa Idara ya Biashara na Kadi wa Benki ya NMB, Yusuph Achayo.


Na Mwandishi Wetu

  

KIASI cha Shilingi Milioni 56.8 kimenyakuliwa na washindi kwa droo ya NMB MastaBATA, ikiwa ni fedha taslimu na bidhaa nyingine zinazoshindaniwa katika droo hiyo inayoendeshwa na Benki ya NMB.

Hadi jana jumla ya washindi 280 wa kila wiki wamepatikana ambapo kila mmoja alishinda Shilingi 100,000 fedha taslimu tangu kuanza kwake Novemba 2020.

NMB MastaBATA, ni Kampeni ya miezi mitatu iliyozinduliwa Novemba 24, 2020 na itadumu hadi Februari mwaka huu, ambako zawadi mbalimbali zinatolewa zikiwamo pesa, simu janja, jokofu, runinga na safari ya kwenda kupumzika Zanzibar, Serengeti na Ngorongoro.

Aidha, jana walipatikana washindi 40 wa kila wiki waliojinyakulisha Shilingi 100,000 kila mmoja, ambapo idadi ya washindi hao imefikia 280 katika Droo iliyosimamiwa na Pendo Albert, kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), ambapo kigezo cha ushiriki ni matumizi ya Kadi za NMB Mastercard na Masterpass QR.

Akizungumza kabla ya kufanyika kwa droo hiyo, Meneja Uhusiano wa Biashara ya Kadi ya NMB, Yusuph Achayo alisema jana ilikuwa ni droo ya saba iliyotoa zawadi za jumla ya Shilingi Milioni 4 ambapo ni Shilingi 100,000 kwa kila mshindi kwa washindi 40.

"Tumeshuhudia watu wengi wakijinyakulia zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu na vifaa vya nyumbani. Tunawashauri wateja wetu waendele kutumia kadi zao kwenye manunuzi na huduma nyingine za kifedha," alisema Achayo.

Aliongeza kuwa, ukiondoa droo za kila wiki, pia NMB MastaBATA imewazawadia jumla ya washindi 12 kati ya washindi 15 wa droo za kila mwezi ambao wao wamekuwa wakijishindia simu janja aina ya Samsung Galaxy Note20, yenye thamani ya Shilingi Milioni 2.4

"Wito wetu kwa wateja wa NMB wenye kadi za NMB Mastercard na Masterpass QR, kufanya manunuzi na malipo mbalimbali ili kujiwekea nafasi ya kushinda droo zijazo za kila wiki, kila mwezi na ile zawadi kuu ya Grand Finale," alisema Achayo.

Aidha, zawadi kuu ya Grand Finale ambayo ni utalii Zanzibar, Ngorongoro ama Serengeti, inawapa washindi uhuru wa kuchagua zawadi mbadala kama runinga iliyolipiwa DSTV miezi mitatu, Jokofu, Laptop, Simu (Samsung A70), Water Dispenser na Microwave.

Kwa upande wake, Pendo, Ofisa wa GBT, aliwataka wateja wa NMB kuendelea kutumia kadi zao ili kujishindia zawadi zinazotolewa na NMB MastaBATA, na kwamba mchakato wa kuwapata washindi unafanyika kwa kufuata sheria na taratibu.

ZIARA YA RAIS MAGUFULI MKOANI KAGERA

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bukoba iliyopo Bukoba mjini mkoani Kagera muda mfupi mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Mkataba wa makubaliano kati ya Serikali na Kampuni ya LZ Nickel limited leo tarehe 19 Januari 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kyaka Misenyi mkoani Kagera wakati akielekea Wilayani Karagwe.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bukoba mara baada ya kuzungumza nao.
Sehemu ya Wananchi wa Kyaka Wilayani Misenyi wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakati aliposimama kuwasalimia leo tarehe 19 Januari 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bukoba mara baada ya kuzungumza nao.


WAGONJWA WAPYA WA SARATANI WAONGEZEKA TANZANIA

$
0
0

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Njisia,Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima. 

 

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

 

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Njisia,Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amesema Tanzania kuna ongezeko kubwa la wagonjwa wapya wa Saratani wapatao 50,000.


Nainakadiriwa kuwa, ifikapo mwaka 2030 kutakuwa na ongezeko la asilimia 50 ya wagonjwa wapya wa saratani.

Hayo yameelezwa leo na Waziri huyo wakati wa uzinduzi wa idara ya magonjwa ya saratani,huduma za patholojia na mkataba wa mteja  kwenye hospitali ya Benjamin mkapa

Dkt. Gwajima amesema kuwa ongezeko hilo kwa mujibu wa Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Tafiti za Saratani (IARC)  na kuongeza kuwa Takwimu za hapa nchini  za 2018 zinaonyesha kuwa idadi ya wagonjwa wapya wa Saratani ni 14,028 sawa na asilimia 33.3 ya wagonjwa wote nchini.

“Saratani kama moja ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza inashika nafasi ya tano kwa wanaume na ya pili kwa wanawake kwa kusababisha vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyo ya kuambukiza nchini.

Kwa ujumla Saratani zinazoongoza kwa wanawake ni mlango wa kizazi na Saratani ya Matiti. Kwa wanaume, Saratani zinazoongoza ni Saratani za Tezi Dume, Koo pamoja na  Kichwa na Shingo.

Aidha, Dkt. Gwajima amesema Magonjwa ya Saratani yanatibika iwapo tu mgonjwa atawahi kupata tiba katika Vituo vya Afya vinavyotoa huduma hiyo. Zaidi ya asilimia 75 ya wagonjwa wa Saratani hufika katika Vituo vya Matibabu wakiwa wamechelewa sana na kuwawia vigumu madaktari kutibu na kuponya ugonjwa huo. 

“Nitoe rai kwa wananchi, tujenge tabia ya kupima afya zetu mara kwa mara ili ikibainika kuwa tuna changamoto za kiafya basi tuanze matibabu bila kuchelewa”Alisisitiza Dkt. Gwajima

Aidha, amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau na mashirika yasiyo ya Kiserikali imeendelea kuhakikisha inapambana na magonjwa ya saratani, ambapo katika kukabiliana na hilo Serikali imefunga mashine mbili za kisasa za tiba ya saratani kwa njia ya mionzi aina ya LINAC katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ambazo zimeanza kutoa huduma tangu Septemba, 2018. 

Dkt. Gwajima aliongeza kuwa Serikali imeanzisha vituo takribani 624 ambavyo huweza kugundua na kutibu mapema saratani ya mlango wa kizazi.

Hata hivyo Dkt. Gwajima alifurahishwa na wataalamu wazawa wa Hospitali ya Benjamin Mkapa na wale wa Chuo Kikuu Dodoma kwa kujituma, kuwajibika na kuthubutu  kuanzisha na kutoa huduma za kibobezi katika upandikizaji wa Figo. 

“wagonjwa 16 wamepandikizwa Figo ndani ya kipindi cha miaka mitatu, kati yao wagonjwa 5 wamepandikizwa na wataalamu wetu wazawa. Hakika hili ni jambo la kijasiri kwani mmesaidia kupunguza mzigo wa gharama kwa Serikali na kwa Wananchi ambao walilazimika kufuata huduma hii nje ya nchi’.

Hata hivyo amesema uwepo wa Kitengo cha Patholojia ni faraja pia katika kuharakisha matibabu kwani hapo awali ilibidi sampuli zipelekwe Dar es Salaam ili kubaini kama ni saratani au la. Utaratibu huu ulikuwa unachelewesha kupata kwa zaidi ya wiki moja hadi mbili.

"Sampuli inatolewa na majibu yanatoka ndani ya kipindi kifupi na wanaobainika kuwa na saratani wanaanzishiwa tiba mapema. Vitengo hivi viwili lazima vifanye kazi kwa karibu kwani vinategemeana sana".

Naye Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Aliphonce Chandika amesema takwimu za shirika la IARC chini ya WHO zinaonyesha kwamba mwaka 2018 jumla ya watu 18.1 waligundulika kuwa na aina mbalimbali za saratani duniani,kati yao watu milioni 9.6 walifariki kutokana na magonjwa ya saratani.

Dkt. Chandika amesema kuanzishwa kwa daftari maalum la kuratibu maradhi ya saratani kanda ya kati  mwaka 2018,saratani ya malango wa kizazi ndio inaongoza  kwa saratani zote zilizoratibiwa ikiwa na jumla ya wagonjwa 778 sawa na asilimia 32 ya saratani zote na asilimia 50 kwa saratani za wanawake huku saratani ya tezi dume ikiongoza kwa wanaume ambapo wagonjwa 265 waliratibiwa sawa na asilimia 39 kwa upande wa wanaume.

Dkt. Chandika ameongeza kuwa umri unaoathirika zaidi na maradhi hayo ni kati ya miaka 50 hasi 69 ambapo jumla ya wagonjwa 1089 sawa na asilimia 42.2 ya wagonjwa wote.

Serikali ilijenga Hospitali  ya Benjamin Mkapa, yenye uwezo wa kutoa huduma bobezi na za kisasa kwa kiwango cha kimataifa katika magonjwa ya Figo, Moyo na Matibabu ya Saratani, ili kuwezesha upatikanaji wa huduma hizo hapa nchini na hivyo kupunguza idadi ya wagonjwa wanaopewa rufaa kwenda kupata matibabu haya nchi za nje kama India na Afrika Kusini.

ASKARI POLISI AJINYONGA HADI KUFA-KIBAHA

$
0
0


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na tukio hilo.


Aliyekuwa askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani mwenye  namba E 6472  marehemu Yusuph Said (52), ambaye alijinyonga katika  nyumba yake aliyokuwa anaijenga katika maeneo ya Kata ya Kongowe akiwa katika picha na wenzake enzi za uhai wake. (Picha na Maktaba). 

  

 

NA VICTOR MASANGU, PWANI 

 

ASKARI wa Jeshi la   Polisi aliyekuwa anafanyakazi katika Kituo cha Polisi wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani  namba E 6472   Yusuph Said  mwenye umri wa miaka (52)  amekutwa  amejinyonga hadi kufariki dunia  katika  nyumba yake anayoijenga katika maeneo ya miembe saba   kata ya Kongowe wilaya ya Kibaha.

 

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo limetokea katika eneo la Miembe saba B  kata ya Kongowe wilayani Kibaha ambapo alisema tukio hilo lilitokea Januari 18 majira ya saa 12 jioni.

 

Kamanda Wankyo alisema Yusuph alikua akitumikia katika kituo c anaishi Picha ya Ndege lakini siku ya tukio alienda Kongowe eneo ambalo anaendelea na ujenzi na ndipo alipokutwa amejinyonga na kamba.

 

Kamanda alibainisha kwamba uchunguzi kuhusiana na tukio hilo unaendelea wakati taratibu za kumsafirisha marehemu kwenda kwao Lindi kwa maziko zikiendelea.

 

Msaidizi wa balozi kwenye eneo hilo Imelda Kitosi alisema akiwa nyumbani alipigiwa simu kuwa kuna tukio la mtu kujinyonga ndipo akaenda kushuhudia akiwa na baadhi ya majirani.

 

Imelda alisema alipofika alielezwa na wazazi wa watoto waliokuwa karibu ya eneo hilo kuwa kuna watoto waliokuwa wanacheza kombolela nje ya nyumba hiyo ambao walisema walisikia mtu anajipiga ndani ya nyumba na walipochungulia wakamkuta tayari yupo chini akiwa na kamba shingoni na walikimbia kwenda kutoa taarifa.

 

Wazazi hao walipofika katika nyumba hiyo ambayo bado inajengwa walimkuta askari huyo tayari ameshafariki ndipo walipoanza kutoa taarifa kwa viongozi na kumpigia msaidizi huyo wa balozi.

 

"Mimi sasa baada ya kupigiwa simu niliingia hapa pamoja na baadhi ya watu waliokuwa karibu tulimkuta yuko kwenye chumba ambacho kilikua kinajengwa kama bafu au choo kamba kaifunga juu na chini kulikua na tofali ambalo baada ya kuhangaika sana mguu mmoja tulikuta kama umepiga goti na mwingine umeegemea tofali huku kamba ikiwa shingoni" alisema.

 

Balozi huyo alieleza kuwa baada ya kushuhudia tukio hilo ndipo walipiga simu Polisi kutoa taarifa na walifika na kuchukua mwili wa marehemu.

DAWASA YAKABIDHIWA MRADI MKUBWA KILIMANJARO, AFISA MTENDAJI MKUU ASEMA WANANCHI KUNYWA MAJI NOVEMBA 30

$
0
0
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akiwa ameongozana na viongozi mbalimbali wakiwemo wataalamu kutoka taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maji wakati akitembelea maeneo mbalimbali kujionea sehemu ya mradi wa maji wa Same -Mwanga -Korogwe uliokua umesimama.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akitizama moja ya chujio la maji katika mradi mkubwa wa Maji wa Same- Mwanga- Korogwe alipotembelea pamoja na wataalamu kutoka katika wizara hiyo.
Waziri wa maji Jumaa Aweso akiwa katika eneo la kupolelea maji kutizama namna ambavyo wataalamu wa ndani wanaweza kuendeleza kazi hiyo ambayo kwa sasa imekabidhiwa rasmi kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) 
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza wakati wa hafla fupi ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji wa Same -Mwanga -Korogwe ,mradi ambao sasa umekabidhiwa kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) .
Baadhi ya Watendaji kutoka Wizara ya Maji wakiwa katika hafla fupi ya utekelezaji wa mradi huo ,hafla iliyofanyika katika ofisi za Mamlaka ya Maji ya Same Mwanga .
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akizungumza katka hafla hiyo ambapo aliwanyooshea kidole wahandisi watakao suasua katika utekelezaji wa miradi ya maji kote nchini ,
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa ,Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza katika hafla hiyo ambapo amewatoa hofu wakazi wa wilaya za Mwanga na Same kuhusu huduma ya Maji na kwamba ifikapo Novemba 30 mwaka huu wateja 100 kwa wilaya ya Mwanga na wateja 100 kwa wilaya ya Same watakua wanatumia maji safi na salama.
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria hafla hiyo wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na viongozi .
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akikata utepe kuashiria kuanza rasmi kwa utekelezaji wa mradi wa MAji wa Same -Mwanga -Korogwe muda mfupi baada ya kukabidhiwa kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) .
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akiunganisha moja ya mabomba  yaliyoanza kusambazwa katika mji wa Mwanga mara baada ya mradi huo sasa kikabidhiwa Dawasa.
Wakuu wa wilaya za Mwanga  na Same Thomas Apson na Rosemery Senyamule wakishirikiana na wananchi wengine kufukia mitaro ambayo tayari bomba za maji zimewekwa.
Baadhi ya Wananchi wakishiriki katika kazi ya kujitolea kwa kufukia mtaro kulikolazwa Bomba mara baada ya mrad huo kukabidhiwa Dawasa.

Sehemu ya Mradi wa Maji wa Same Mwanga Korogwe unavyoonekana kwa juu ,mradi ambao sasa umekabidhiwa Dawasa.

 
Na Dixon Busagaga-Mwanga
 

 WIZARA ya Maji imekabidhi mradi wa maji wa Same –Mwanga –Korogwe (SMK) kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) baada ya kusitisha mikataba na kampuni za M .A Kharafi & Sons na Badr East African Enterprises Ltd .

 Maamuzi ya Wizara ya Maji yanatokana na kusuasua kwa mradi huo kwa muda mrefu sasa huku wananchi katika maeneo ya wilaya za Mwanga ,Same na Korogwe mkoani Tanga wakiendelea kukabiliwa na changamoto ya huduma ya maji.

 Katika mradi huo ambao chanzo chake ni Bwawa la Nyumba ya Mungu ,kampuni ya ukandarasi ya M.A Kharafi &Sons iliingia mkataba wa kujenga chanzo na mtambo wa kusafisha maji katika kijiji cha Njiapanda wilayani Mwanga pamoja na ujenzi wa miundombinu ya kupeleka maji hadi katika tanki la Kisangara.

 Katika hafla ya kukabidhi mradi huo kwa Dawasa Waziri wa Maji Jumaa Aweso alisema mkataba na kampuni hiyo ulisainiwa Nevemba 2014  ulitarajiwa kukamilika Julai 16,2017 na kwamba mkandarasi amekuwa akisuasua katika utekelkezaji .

 “Hadi mkandarasi anasitishiwa mkataba Desemba 29,2020 uteklezaji wa kazi hii ilikuwa imefikia asilimia 64”alisema Aweso.

 Waziri Aweso alisema mkataba mwingine ulikua ni usambazaji wa maji katika mji wa Mwanga na kujenga miundombinu ya kutoa maji Kisangara hadi kiverenge na kutoka Kiverenge hadi Mwanga mjini,kazi iliyokuwa ikifanywa na Mkandarasi BADR East African Enterprises Ltd.

 “Kama alivyo mkandarasi wa kwanza huyu naye alisuasua katika utekelezaji wa mradi lakini pi aligushi nyaraka muhimu za kimkataba nakujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na hadi kufikia mwisho wa mwaka 2020 alikua amefikisha asilimia 60.

 “Wizara ninayoiongoza imechukua maamuzi magumu ya kumsimamisha mkandarasi huyu Desemba 30,2020 “aliongeza Aweso

 Alisema mkataba namba nne unahusisha kazi za usambazaji maji katika mji wa Same na kujenga matenki manne na miundombinu ya kutoa maji Kiverenge hadi Same mjini kupitia mkandarasi BADR East African Enterprises Ltd ,mkataba ulionesha mkandarasi alipaswa kumaliza kazi Desemba 1,2019.

 “Ni kwa sababu hii tuliona kuwa upo umuhimu wa Serikali yenyewe kupitia taasisi yake ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) yenye uzoefu wa utekelezaji na usimamizi wa miradi mikubwa ikamilishe kazi hii.” Alisema Aweso.

 “Baadhi ya kazi kama Electro-mechanical works zitafanywa kupitia wakandarasi wenye uzoefu zaidi na kazi nyingine zitatekelezwa moja kwa moja na Dawasa” aliongeza Waziri Aweso.

 Aweso alimtaka Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja ahakikishe kuwa mradi unatekelezwa kwa wakati na kwa ubora kama ilivyo katika makabrasha ya usanifu .

Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cypriani Luhemeja alisema kazi ya ulazaji wa miundombinu ya maji katika maeneo hayo imeanza na kwamba wananchi katika wilaya ya Mwanga na Same wataanza kupata huduma ya maji ifikapo Novemba 30 mwaka huu.

 “Kwa unyenyekevu kabisa mimi pamoja na timu yangu pamoja na Bodi inayoongozwa na Jenerali Davis Mwamnyange ,mkuu wa majeshi mstaafu,kazi hii tunaiweza na itakamilika tarehe 30 Novemba ,ninakuomba katika ratiba zako tarehe 19 Desemba tutakualika kuja kuzindua huu mradi”alisema Mhandisi Luhemeja .

 Mwisho  


Serikali yajipanga kuondaoa majitaka Jijini Dodoma

$
0
0

 NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA


SERIKALI ipo kwenye hatua za mwisho za kuhakikisha kunakuwepo na uondoshaji mkubwa wa maji taka katika jiji la Dodoma unaojumuisha ujenzi wa kilomita 250 za mabomba pamoja na mabwawa 16 yatakayojengwa katika eneo la Nzuguni.

Hayo yamesemwa  leo Jijini hapa na Naibu Waziri wa Maji Maryprisca Mahundi alipokuwa akifungua Baraza la Sita la wafanyakazi wa DUWASA ambapo amesema lengo ni kuifanya Dodoma kuwa na sura ya Makao Makuu ya nchi.

Amesema ili mradi huo ufanikiwe kwa malengo yaliyokusudiwa lazima wananchi wapatiwe elimu ya kutosha kwani ni wachache wanaofahamu kuwa wanaweza kuunganishiwa mfumo huo kutoka  kwenye makazi yao hadi kupeleka maji taka kwenye mabwawa.

"Duwasa inatakiwa kutatua kero kwani kero nyingine zimekuwa zikisababishwa na baadhi ya watu ambao wanashindwa kufanya kazi kwa ufanisi,".

Na kuongeza kusema" Baadhi ya wananchi wamekuwa wakilalamika kutokana na huduma wanazozipata hivyo kupitia baraza hili hakikisheni mnafanya kazi ya kuzitatua kero hizo ili wananchi wafurahie uwepo wa mtandao wa maji," amesema Waziri Maryprisca.

Amesema kuna kila sababu ya Duwasa kuendelea kuujenga mtandao wa maji kwa kuwafikishia wananchi huduma za maji kwani wanauhitaji huo .

"Wizara itaendelea kuiwezesha ili iweze kutoa huduma bora kwa Wananchi," Amesema Waziri huyo.


Kwa upande wake Mhandisi Aron Joseph Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira DUWASA amesema wao kama Mamlaka wataendelea kutoa huduma bora ya maji safi na Usafi wa Mazingira kwa wanchi wote wa Dodoma.

"Licha ya Dodoma kuongezeka kwa watu kutokana na kutambulishwa rasmi kuwa ni jiji ili kukabili tatizo la ukosefu wa maji kwa wananchi miradi ya muda mfupi na miradi ya muda mrefu ambapo katika mradi wa muda mfupi jumla ya visima 20 vimeanza kuchimbwa,".

Na kuongeza kusema "Mradi mkubwa katika Ziwa Victoria utakaopitia Mkoa wa Singida mpaka Mkoa wa Dodoma na kuwanufaisha wakazi wa mikoa hiyo," amesema Muhandisi Aron.

Naye Mwenyekiti wa Bodi Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira DUWASA Faustine Bee amesema wamejipanga  kupunguza malalamiko kwa wakazi wa Dodoma juu ya upatikanaji wa maji na Usafi wa Mazingira katika makazi yao.

Pia amesema wamejipanga kuhakikisha wanadhibiti upotevu wa maji kutoka asilimia 26 mpaka kufikia 10 au kumaliza kabisa tatizo hilo.

MSAJILI AWA 'MBOGO' KWA WAFAMASIA WANAOKIUKA MAADILI

$
0
0


 

Na Rayson Mwaisemba WAMJW- Dom

Msajili wa Baraza la Famasi nchini, Elizabeth Shekalaghe (pichani), ametoa siku 14 kwa wafamasia wanaosimamia famasi ambazo hazipo katika maeneo yao ya kazi kujisalimisha katika Baraza hilo.

Bi. Shekalaghe ametoa agizo hilo leo wakati akiongea na maafisa habari wa Wizara ya Afya katika ofisi zake zilizo katika jengo la Bima ya Afya Jijini Dodoma.

"Kwa wale wafamasia ambao, wanasimamia famasi ambazo hazipo ndani ya  maeneo yao ya kazi, natoa siku 14 kuanzia leo, kujisimisha Baraza la Famasi, mtu anakaa Morogoro anasimamia famasi Dodoma, lakini taarifa alizotuletea sisi yupo Dodoma, sasa tumeshaanza kufanya ufuatiliaji maalum ili kuwabaini" alisema Bi. Shekalaghe.

Bi Shekalaghe alisema kuwa, Baraza la Famasi limeanza kufanya ufuatiliaji maalum ili kuwabaini wafamasia wote wanaokiuka maadili na Sheria kwa kutoa taarifa za uongo za kuonekana yupo kwenye kituo fulani, wakati uhalisia anakuwa katika kituo kingine.

Kwa upande mwingine Bi Shekalaghe alisema kuwa, “Kifungu Na. 43 cha Sheria ya Famasi, Sura 311 kinaelekeza kwamba, hairuhusiwi mtu yoyote kujihusisha na biashara ya famasi kama sio mfamasia, huku akisisitiza endapo mtu huyo atahitaji kufanya hivyo, atalazimika kutafuta mfamasia ili asimamie huduma hiyo " alisisitiza Bi. Shekalaghe.

Alisema pia kuwa, Kanuni ya 10  ya Kanuni za Utendaji wa Taaluma za Mwaka 2020, zimeelekeza kwamba mfamasia atawajibika na usimamizi wa huduma katika famasi hiyo kila siku, huku akiweka wazi kuwa, kwa kiasi kikubwa bado wafamasia wengi hawawajibiki kwa kiwango cha kuridhisha katika maeneo yao ya kutolea huduma.

Aliendelea kusema kuwa, hivi karibuni kumekuwa na tabia ya wafamasia kuingia mikataba na wamiliki wa maduka ya famasi, huku wakishindwa kutekeleza majukumu yao, jambo ambalo ni kinyume na Kanuni za utendaji wa taaluma na bado wakipokea mishahara ya usimamizi wa famasi hizo bila kufika na kutekeleza majukumu yao ya msingi.

Aidha, Bi Shekalaghe ametoa rai kwa wafamasia wote nchini, kufika katika maeneo yao ya kazi.
"Nitoe rai kwa wafamasia kwamba, hakikisha unakwenda katika famasi unayosimamia kwasababu kanuni ya utendaji wa taaluma inakuelekeza kwamba, una wajibu  wa kufanya shughuli za usimamizi wa huduma za kila siku katika eneo hilo " alisema Bi Shekalaghe.

Mbali na hayo, amewaeleza wamiliki wa famasi kuwa, ni kosa kwa mfamasia kutokufika katika eneo la kazi, huku akisisitiza kuwa Kanuni ya 13 ya Kanuni za Usajili wa Famasi imeelezea kuwa,  kutofika kwa mfamasia katika famasi ni moja ya sababu za kufutwa kwa kibali cha uendeshaji wa huduma hizo kwa sababu ya kukosa usimamizi.  

Pia, Bi Shekalaghe amesisitiza kuwa, dawa si biashara, bali ni huduma ambayo inapaswa kusimamiwa kwa weledi wa hali ya juu na mtaalamu aliyepewa jukumu hilo kisheria na  mwenye vigezo na maadili ya utoaji huduma hiyo.

“Sitakubali kuona uzembe na kutowajibika kwa wafamasia wachache huku wakiendelea kuwaweka wananchi katika hatari ya kupata athari dhidi ya matumizi holela ya dawa. Hilo halikubaliki”

Amewakumbusha wanataaluma wote kusoma Sheria, Kanuni na Miongozo inayosimamia taaluma ya famasi na kuitekeleza pasipo shuruti wakati wanatekeleza majukumu yao.

SHERIA ITUMIKE KUWABANA WANAOHUJUMU MIUNDOMBINU YA BARABARA

$
0
0

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, akisisitiza jambo kwa watumishi wa Mfuko wa Barabara (RfB), alipotembelea ofisini hapo jijini, Dodoma ili kujitambulisha na kukagua utendaji kazi wa Mfuko huo.

 

Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mfuko wa Barabara (RfB), wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea ofisini hapo jijini, Dodoma ili kujitambulisha na kukagua utendaji kazi wa Mfuko huo. PICHA NA WUU.

 

 

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, ameitaka Bodi ya mfuko wa Barabara (RfB) kutumia vifungu vya sheria vitakavyowabana watumiaji wa barabara wanaoegesha magari kwenye mabega ya barabara, wanaoiba alama za barabarani pamoja na wanaopitisha mifugo kwenye barabara.

Mhandisi Kasekenya ameyasema hayo, alipotembelea ofisi za Mfuko huo zilizoko Njedengwa, jijini Dodoma ili kujifunza shughuli zinazofanywa na mfuko huo.

“Simamieni sheria na muwachukulie hatua wale wote wanaoujumu miundombinu ya barabara kwa namna moja ama nyingine ili tuzilinde barabara zetu na kutotumia fedha nyingi katika matengenezo”. amesema Mhandisi Kasekenya.

Aidha, amewataka Mameneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) na wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuhakikisha wanaziba mashimo barabarani ndani ya masaa 48 kama sheria inavyoelekeza ili kupunguza ajali zinazoweza kutokea kutokana na uwepo wa mashimo hayo.

“Hakikisheni mnakuwa na uwezo wa kupata taarifa kwa kuambiwa au kukagua ili kubaini mashimo yaliyopo barabarani na kuziba mashimo haya ndani ya masaa 48, Sheria itachukua mkondo wake kwa yeyote asiyetii sheria hii’’, amesisitiza Kasekenya.

Naye, Meneja wa Bodi ya Mfuko wa Barabara Eliud Nyauhenga, pamoja na mambo mengine  amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa Mfuko unafanya shughuli mbalimbali ikiwemo kukusanya fedha, kugawa fedha kwa Taasisi husika pamoja na kufuatilia matumizi ya fedha hizo.

Aliongeza kuwa, asilimia 70 ya makusanyo inapelekwa kwenye ukarabati wa barabara za kitaifa ambazo ziko chini ya wakala wa Barabara nchini (TANROADS) na asilimia 30 inapelekwa kwenye ukarabati wa barabara zilizoko chini ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).

Nyauhenga, amefafanua kuwa mfuko huo unategemea vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwemo tozo za mafuta na barabara, tozo za magari ya kigeni (Transit fees) pamoja na tozo inayolipwa na wanaozidisha uzito wa magari barabarani.

Kasekenya, ametembelea Bodi ya Mfuko wa Barabara ambayo imekuwa ikitoa fedha kwa ajii ya matengenezo ya barabara nchini zinazosimamiwa na TANROADS pamoja na TARURA na kuhakikisha kuwa hali ya mtandao wa barabara nchini inakuwa bora.

WIZARA YA ARDHI KUANZA UHAMASISHAJI UTEKELEZAJI MPANGO KABAMBE JIJI LA DODOMA

$
0
0


Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maeandeleo ya Makazi Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Imaculate Senje akizungumza na Wenyeviti wa Mitaa ya Kata za Mpunguzi na Matumbulu katika halmashauri ya jiji la Dodoma (hawapo pichani) wakati wa kutangaza mpango wa uhamasishaji utekelezaji Mpango Kabambe wa jiji la Dodoma tarehe 20 Januari 2021.

 

 

 Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA

 

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inatarajiwa kuanza utekelezaji Mpango Kabambe wa jiji la Dodoma kwa kuanza kuhamasisha wananchi wa kata za Mpunguzi na Matumbulu kufanya maendeleo kwa kuzingatia mpango huo.

Timu ya Wataalamu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na  Halmashauri ya Jiji la Dodoma ikiongozwa na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Makazi Wizara ya Ardhi Bi. Imaculate Senje ilikutana na Wenyeviti wa Mitaa iliyo kwenye kata hizo kwa lengo la kuwajengea ufahamu kuhusiana na utekelezaji Mpango Kabambe.

Akizungumza na Wenyeviti hao leo tarehe 20 Januari 2021 katika ofisi ya Mtendaji Kata ya Matumbulu jijini Dodoma, Bi Imaculate alisema Wizara kwa kushirikiana na halmashauri ya jiji la Dodoma imeamua kuanza uhamasishaji wa utekelezaji wa mpango huo ili wananchi waulewe  na kuachana na ile dhana ya kusema Serikali inapora maeneo.

Mkurugenzi huyo Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Makazi Wizara ya Ardhi aliongeza kwa kusema kuwa, zoezi la utekelezaji Mpango Kabambe wa jiji la Dodoma unalenga maendelezo ya eneo hilo kufanyika kwa kuzingatia mpango huo.

Kwa mujibu wa Bi. Imaculate, kwa kuanzia utekelezaji Mpango Kabambe utaanzia kata ya Mpunguni na kuhusisha maeneo ya Mashamba na Viwanda na baadaye katika maeneo ya makazi ya wananchi ambapo zoezi litakalofanyika huko ni la urasimishaji.

‘’Kipaumbele kwa sasa katika zoezi la utekelezaji mpango kabambe wa jiji la Dodoma litakuwa katika maeneo ya mashamba na viwanda na hapa tunataka tuepuke ujenzi holela katika maeneo hayo na kuzingatia mpango kabambe uliopo’’ alisema Imaculate.

Alisema, wakati wa utekelezaji zoezi hilo hatua ya awali wataalamu watachukua taarifa za wamiliki wote kwenye maeneo yaliyopangwa kwa ajili ya mashamba na viwanda ambapo maeneo hayo yatapimwa na wamiliki wake kumilikishwa na kusisitiza kuwa, baada ya kumilikishwa hawataruhusiuwa kufanya maendelezo kinyume na mpango kabambe.

Kwa upande wake Afisa Mipango Miji wa halmashauri ya Jiji la Dodoma Aisha Masanja alisema lengo la kukutana na wenyeviti wa mitaa kabla ya kukutana na wananchi ni kuwataka wenyeviti hao kuwa mabalozi wazuri wa kuwaelimisha wananchi kuhusiana na zoezi hilo na kuongeza kuwa inachotaka serikali kupitia zoezi hilo ni kuhakikisha kila mwananchi anabaki katika eneo lake na kusisitiza kuwa baada ya hapo itatolewa ramani ya msingi itakayoainisha shughuli ya kila eneo kulingana na mpango.

Mpango Kabambe wa jiji la Dodoma ulizinduliwa Februari mwaka 2020 na Waziri Mkuu Mhe. Kasim kwa ajili ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa bora na la Kisasa.

WAZIRI MKUU ATOA AGIZO UENDELEZAJI ZAO LA MKONGE

$
0
0

 *Halmashauri zinazolima mkonge zatakiwa kuanzisha vitalu vya miche

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameziagiza Halmashauri zinazolima mkonge nchini pamoja na wakulima wakubwa wa mkonge watenge ekari 10 kwa akili ya kuanzisha vitalu vya kuzalisha miche ya mkonge ili kupunguza tatizo la upungufu wa mbegu.

 

Pia, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Kilimo itenge fedha katika bajeti yake kwa ajili ya kituo cha TARI Mlingano ili kukiwezesha kupanua eneo la uzalishaji miche kwa kununua vitendea kazi yakiwemo matrekta.

 

Ametoa maagizo hayo leo (Jumatano, Januari 20, 2021) baada ya kukagua kitalu cha miche ya mkonge la TARI Mlingano lililopo wilayani Muheza, Tanga na kufungua zoezi la ugawaji wa miche kwa wakulima wa zao hilo.

 

Waziri Mkuu amesema ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa miche ya mkonge nchini kila halmashauri na wakulima wakubwa wanatakiwa watenge ekari 10 kwa ajili ya kuandaa vitalu vya miche ya mkonge na kugawa kwa wananchi kwenye maeneo yao.

 

Amesema kituo cha TARI Mlingano kinatakiwa kijikite katika kufanya  utafiti wa mbegu bora pamoja na dawa za kudhibiti magonjwa katika zao hilo na suala la uzalishaji wa mbegu lifanywe kwa ushirikiano katika ya kituo hicho na wadau wa zao hilo.

 

Kadhalika, alisema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha mpaka ifikapo mwakani kuwa na ongezeko la uzalishaji wa miche zaidi ya Milioni mbili ya sasa kwani mahitaji ni makubwa kwa sasa.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Mlingano, Dkt Catherine Senkoro amesema hadi kufikia Januari, 2021 jumla ya hekta 32.6 sawa na ekari 81.5 zimepandwa miche ya mkonge katika maeneo ya TARI Mlingano.

 

Amesema kituo chao kwa kushirikiana na Bodi ya Mkonge Tanzania imetoa mafunzo kwa wakulima na Maafisa Ugani katika baadhi ya mikoa inayofaa kwa kilimo cha mkonge ambayo ni Tanga, Morogoro, Pwani, Kilimanjaro, Lindi, Simiyu, Shinyanga na Mara. “Kufikia Desemba 2020, wakulima 422 na Maafisa Ugani 840 katika mikoa hiyo walipatiwa mafunzo.”

 

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2020/2021 Wizara ya Kilimo kupitia kituo cha TARI Mlingano imepanga kuzalisha miche 4,000,000 katika vitalu vyake, pia itapanua maabara ya uzalishaji wa miche kwa njia ya chupa  ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa miche. Utaratibu huo unakadiriwa kuchangia miche milioni 10 kwa mwaka.

 

TTCL CORPORATION YAANZA NA WABUNGE

$
0
0

 

Mhe. Humphrey Polepole (mwenye tai), akipatiwa maelezo na Meneja Mahusiano TTCL, Bi. Puyo Nzalayaimisi juu ya vifurushi vinavyotolewa na TTCL CORPORATION alipotembelea viwanja vya Bunge leo asubuhi.

 

Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima, Mb (kushoto) akikabidhiwa zawadi ya kalenda ya mwaka 2021 na Meneja Mahusiano wa TTCL Bi. Puyo Nzalayaimisi (Kulia) mapema leo asubuhi katika viwanja vya Bunge.

 

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile (katikati), akifafanua jambo kwa watoa huduma wa TTCL waliotembelea viwanja vya Bunge mapema leo.

 

 Na Mwandishi Wetu, Dodoma 

 

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL CORPORATION), limeanza kutekeleza baadhi ya maagizo ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma. Baadhi ya maagizo yaliyotolewa na Mhe. Ndugulile alipozungumza katika kikao kazi cha Shirika hilo kilichojumuisha viongozi wa Shirika na Mameneja wa Mikoa mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dodoma. Miongoni mwa maagizo yaliyotolewa ni pamoja na Shirika kuendelea kujitangaza, kuboresha bidhaa, kuboresha huduma kwa wateja  na kuongeza ubunifu.

Katika utekelezaji huo, baadhi ya watumishi wa Shirika hilo wakiongozwa na Meneja wa Mahusiano Bi.Puyo Nzalayaimisi, wameanza utekelezaji wa maagizo hayo katika viwanja vya Bunge kwa kutangaza zaidi bidhaa zao kwa kipindi chote cha Bunge. Huduma zinazotolewa kwa Waheshimiwa Wabunge ni pamoja na Usajili wa laini za TTCL, Huduma za T-PESA na Uuzaji wa bidhaa zinazotolewa na Shirika hilo.

Mmoja wa wabunge waliohudumiwa ni Waziri wa Afya na maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (Mb) ambaye alilitaka Shirika kuendelea kutoa na kuboresha huduma ya mawasiliano katika sekta ya Afya Nchini.

Naye Meneja wa Mawasiliano wa Shirika hilo Bi. Puyo Nzalayaimisi aliahidi kuendelea kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na Waziri wa Mawasiliano, “Kama Shirika la Mawasiliano Nchini tutaendelea kutoa huduma zetu zenye viwango bora na kulitangaza Shirika letu ili kufikia malengo pamoja na kutimiza maazimio yaliyotokana na kikao kilichopita” alisema Bi.Puyo.

Mwanaume ambaye hajafanyiwa tohara anauwezo mkubwa wa kusambaza Virusi vya HPV

$
0
0
Na Asha Mwakyonde

DAKTARI wa Magonjwa ya Binadamu kutoka Hospitali ya Marie Stopes, Mwenge , Dkt. Mashingo Lerise amesema kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume ambaye hajafanyiwa tohara kunaweza kusababisha mwanamke kupata Saratani ya mlango.was kizazi kutokana na maambukizi ya aina ya virusi vijulikqnavyo kama Human Papilloma Virus (HPV)

Amesema  maambukizi ya kirusi  kinachojulikana kama (HPV), husababisha saratani ya mlango wa shingo ya kizazi._

Akizungumza ofisini kwake jijini Dar es Salaama jana daktari huyo amesema kuwa mwanaume ambaye hajafanyiwa tohara anauwezo mkubwa wa kusambaza virusi vya HPV pamoja na maambukizi ya magonjwa mengine ya zinaa.

"Kutofanya tohara kwa mwanaume kuna tengeneza mazingira rafiki ya kuvisambaza Virusi hivyo ambavyo vinapatikana zaidi kwenye maji maji ya kwenye viungo vya uzazi " anesema Dkt. Lerise.

Ameeleza kuwa serikali na taasisi mbalimbali imekuwa ikipiga kelele ili wanaume ambao hajawatahiriwa wafanyiwe tohara kwa lengo la kupunguza maambukizi ya magonjwa ya zinaa pamoja na Virusi hivyo ambavyo husababisha saratani ya shingo ya mlango wa Kizazi.

Daktari huyo amesema kuna vihatarishi vingine vinavyomuweka mtu kwenye hatari ya kupata saratani ya mlago wa shingo ya  kizazi ikiwa ni pamoja na kuanza vitendo vya ngono mapema, mimba chini ya umri wa miaka 16, kuwa na mahusiano na wanaume wengi na historia ya ugonjwa huu kwenye familia.
 
Pia kuwa na idadi kubwa ya watoto, kuzaa mara kwa mara, umri zaidi ya miaka 30 na  mahusiano ya kimapenzi na mwanaume ambaye mwenza wake amefariki kwa ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi..

Ugonjwa wa  saratani una aina zaidi ya 200 tofauti kutegemeana na kiungo kilicho athirika kama vile seratani ya matiti,mlango wa uzazi, tezi dume, koo, damu na nyingine.

Tandale kukuza vipaji vya vijana sekta ya michezo

$
0
0

Na Asha Mwakyonde

DIWANI wa Kata ya Tandale iliyopo Wilaya  ya Kinondoni Chifu Abdallah  Saidi wanatarajiwa kuandaa mashindano yenye lengo la kukuza vipaji vya vijana wa kata hiyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaama leo Januari 21, 2021 Chifu  Saidi amesema michezo ni ajira kwa vijana wenye vipaji na wanaojituma kwa kile wanacho kifanya.

Diwani huyo amefafanua kuwa mashindano hayo yatahusisha mpira, Pet, rede na mingine ikiwa ni pamoja na ngumi.

" Niliahidi kutengeneza nyumba ya kukuza vipaji vya vijana wa Tandale ( House of Talent), ili vijana hao waweze kupata ujuzi zaidi," amesema Chifu Saidi.

Amesema mbali na kujitenenezea ajira vijana hao kupitia michezo pia wataweka afya zao katika hali nzuri kutokana na michezo hiyo.

Diwani huyo ameongeza kuwa vijana wapo vijana ambao wamejituma kwa kucheza kwa bidii katika mchezo anaoupenda na kufanikiwa katika maisha yao na kuzisaidia familia zao kiuchumi.

Chifu Saidi ametolea mfano kwa mchezaji Mbana Samatta ambaye amepata mafanikio makibwa ya kucheza nje ya nchi na kuitambulisha Tanzania vema.

Amewataka vijana wa Kata ya Tandale kujitokeza kwa wingi mashindano hayo yatakapoanza ili waonyeshe vipaji vyao na baadae waweze kusaidiwa.

NMB yajipanga kusaidia kufufuliwa zao la Mkonge nchini

$
0
0

   

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi akizungumza katika mkutano wa wadau wa zao Mkonge uliofunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jijini Tanga.

 


Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi, akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Horticultural Association (TAHA), Jaqueline Mkindi, wakati wa mkutano wa wadau wa zao la Mkonge uliofunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  jijini Tanga. (Na Mpiga Picha Wetu).

 

Na Mwandishi Wetu, Tanga

 

Benki ya NMB imesema kuwa itahakikisha inaendelea kutoa huduma za kifedha kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kufufua zao la Mkonge na kuboresha uchumi wa wakulima wa zao hilo nchini.

Hatua hiyo inakuja baada ya serikali kuanza mikakati ya kuhakikisha zao hilo linafufuliwa na kuwanufaisha wakulima na taifa kwa ujumla kama ambavyo ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Akizungumza mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa kikao cha wadau wa Mkonge kilichofanyika jana mkoani Tanga, Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi  na Biashara wa Benki hiyo, Filbert Mponzi, alisema kuwa NMB itaendeleza jitihada za kufufua zao hilo ambazo imezianza.

Alisema kuwa tangu serikali imeanza kulifufua zao hilo benki hiyo imekuwa ikitoa ushirikiano ambapo imetoa zaidi ya Bilioni 1 kwa ajili ya ununuzi wa matrekta 11 na trela 22 vifaa ambavyo vitapunguza gharama ya uendeshaji na kuongeza tija na pato la wakulima wadogo wa mkonge.

Aidha aliongeza kuwa Benki hiyo imeendelea kutoa mikopo ya pembejeo na uendelezaji wa mashamba ya Mkonge kwa wakulima wadogo, kati na wakubwa ili kuongeza uzalishaji na mapato ambapo zaidi ya shilingi bilioni 6 zimeshatolewa kwa wakulima wa mkonge.

Alisema kuwa NMB imefanikisha kufungua akaunti kwa wakulima zaidi ya 1,500 ambapo akaunti hizo zinajumuisha wakulima mmoja mmoja na wale wanaozalisha kupitia Vyama vya msingi.

“ Uwepo wa akaunti hizi unajenga utamaduni wa wakulima kutumia huduma za benki kwa usalama wa fedha zao na mazingira sahihi katika kupata huduma zaidi ya kifedha ikiwemo Mikopo” alisema Mponzi.

 

"Mheshimiwa Waziri Mkuu ili kuendelea kuwajengea uwezo wakulima wadogo na kupata mitaji NMB kupitia taasisi kanzu ya NMB Foundation inaendelea kutoa mafunzo kwa wakulima kupitia vyama vya vya msingi na kikundi ili kuimarisha utendaji na kuongeza soko," alifafanua.

Mponzi alibainisha kuwa Benki ya NMB itaendeleza jitihada hizo, ikiwemo kutoa mikopo mikubwa, midogo na ya kati ili kuhakikisha wakulima wa zao wanazlisha kwa tija.

“NMB tutaendelea mikopo katika ngazi zote za uzalishaji wa zao la mkonge, ikijumuisha mikopo ya muda mfupi na muda wa kati (yaani uwekezaji). Mikopo hii inajumisha pembejeo, upanuzi na miundo mbinu ya mashamba, matrekta, mashine za uchakataji wa mkonge, viwanda vya mkonge pamoja na huduma mbalimbali katika sekta,” alisema.

Akizungumza katika kikao hicho cha wadau wa zao la Mkonge, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kuwa mpaka kufikia mwaka 2025 Tanzania inatarajia kuzalisha tani 120,000 za Mkonge kwa mwaka.

Majaliwa alisema kuwa zao la Mkonge ni miongoni mwa mazao ya biashara hapa nchini ambayo mikakati yake ikitekelezwa vizuri itawezesha serikali kupata fedha za kigeni lakini pia kukuza pato la mwananchi mmoja mmoja.

"Kilimo cha zao la mkonge na mchikichi unatuondolea mzigo mkubwa sana kwa kupunguza gharama mfano baada ya kuhamasisha kulima mchikichi tunaokoa zaidi dola za marekani 470 milioni za kuagiza mafuta kutoka nje ya nchi," alisema Waziri Mkuu.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, alisema kuwa kwa sasa Wizara tayari imeshatenga shilingi Bilioni 175 kwa ajili ya kufanya utafiti ili kuzalisha mbegu bora na zenye gharama nafuu.

Bashe alisema kuwa Wizara imeweza kuandaa utaratibu wa hati ya dhamana (LC) utakaowezesha wakulima wadogo kuchukua mkopo kwenye taasisi za fedha kwa riba ya asilimia mbili tu.

Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>