Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

WAZIRI CHAMURIHO AWATAKA WAFANYAKAZI KUZINGATIA MIKATABA YA KAZI

$
0
0

 

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Leonard Chamuriho (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na  wajumbe wa baraza la wafanyakazi la sekta ya Uchukuzi, mara baada ya kulifungua Mkoani Mwanza.

 

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,  Mhandisi  Leonard Chamuriho,  amewataka wafanyakazi wa sekta ya uchukuzi kuhakikisha wanatekeleza makubaliano yaliyosainiwa kati yao na wakuu wa taasisi ili kuwe na ufanisi na thamani ya fedha.

Waziri Chamuriho ameyasema hayo mara baada ya kufungua baraza la wafanyakazi wa sekta hiyo, lilifanyika katika ukumbi wa chuo cha Benki Kuu (B.o.T) Mkoani Mwanza na kusisitiza kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua kwa mtumishi atakayekiuka makubaliano hayo.

"Hatutasita kuchukua hatua pale tutakapobaini kuwa kazi zinafanywa kwa mazoea na kusahau malengo tuliyojiwekea kwa utendaji wa kazi za kila siku. "alisema waziri Chamuriho.

Aidha waziri chamuriho amesisitiza umuhimu wa taasisi za sekta ya uchukuzi kushirikiana ili kuwa na matokeo chanya hususani katika miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa kwenye miundombinu.

Hata hivyo waziri Chamuriho ameeleza changamoto ya vishiria vya uwepo rushwa na kuwataka watumishi wa sekta ya uchukuzi kujiepusha kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi.

"Zipo rushwa za aina nyingi, ikiwemo za kuomba fedha, zawadi, mapenzi  na hata kuwanyima haki watu haki zao, unyanyasaji wa kijinsia, na  ukiukaji wa haki za binadamu ". Alisema Waziri Chamuriho.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye ni Kaimu Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi, Gabriel Migire amemuhakikishia Waziri Mhandisi Chamuriho kuwa maelekezo yote yatafanyiwa kazi na kutoa mrejesho kwa kuzingatia

Katika hatua nyingine Mwenyekiti, Gabriel Migire amempongeza Waziri Chamuriho kwa utendaji uliotoa matokea chanya kwenye miradi ya ki  mkakati ya sekta ikiwemo ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR, Ununuzi na Ukarabati wa Meli za Mv Viktoria na Butiama, ujenzi wa Chelezo, Ujenzi wa Meli Mpya ya MV. Mwanza na Ununuzi wa Ndege.


Msimamizi wa Bandari ya Katembe matatani

$
0
0

 

Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Mhandisi Richard    Ruyango, akitoa maagizo ya kukamatwa kwa msimamizi wa Bandari ya Katembe Magarini, Maduhu Makajanga.

 

 

Na Lydia Lugakila, Muleba

Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera, Mhandisi Richard Ruyango, ameagiza kukamatwa kwa  msimamizi wa bandari ya Katembe Magarini, Maduhu Makajanga, kutokana na tuhuma ya kuwatoza tozo kubwa ya ushuru wafanyabiashara wa samaki kinyume na utaratibu wa Serikali baada ya wafanyabiashara hao kulalamikia kitendo hicho.

Hayo yamejiri baada ya mkuu wa wilaya huyo kutembelea bandari hiyo na kuzungumza na wafanyabiashara hao katika mwaro huo.

Wakilalamikia Hali hiyo wamesema kuwa awali walikuwa watozwa ushuru wa Kawaida unaoendana na maelekezo ya Serikali licha ya bandari hiyo kuanza kupadisha tozo hivyo na kuwalazimu kutumia badari Nyingine ya Mngaza iliyopo Wilayani chato.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango baada ya kusikiliza malalamiko hayo ameamuru msimamizi huyo wa bandari akamatwe ili ahojiwe  na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU).
 
Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera Mhandisi Richard Ruyango ameagiza kukamatwa kwa  msimamizi wa bandari ya Katembe Magarini Bwana Maduhu Makajanga kutokana na tuhuma ya kuwatoza tozo kubwa ya ushuru wafanyabiashara wa samaki kinyume na utaratibu wa Serikali hii ni baada ya wafanyabiashara hao kulalamikia kitendo hicho.

Hayo yamejiri baada ya Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango kutembelea bandari hiyo na kuzungumza na wafanyabiashara hao katika mwaro huo.

Wakilalamikia Hali hiyo wamesema kuwa awali walikuwa watozwa ushuru wa Kawaida unaoendana na maelekezo ya Serikali licha ya bandari hiyo kuanza kupadisha tozo hivyo na kuwalazimu kutumia badari Nyingine ya Mngaza iliyopo Wilayani chato.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango baada ya kusikiliza malalamiko hayo ameamuru msimamizi huyo wa bandari akamatwe ili ahojiwe  na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa. (TAKUKURU).

NYAVU HARAMU ZATEKETEZWA MULEBA

$
0
0

Nyavu haramu 1565 zenye thamani ya Sh. Bilioni 1.4 zikiteketezwa mkoani Kagera.


 

Na Lydia Lugakia, Muleba
 

Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Muleba mkoani Kagera imefanikiwa kuteketeza nyavu haramu zipatazo 1565 zenye thamani ya bilioni 1.4 katika mwaro wa magarini uliopo katika kata ya Nyakabango.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Wilayani humo ambaye pia ni mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango  nyavu hizo zipo zilizo salimishwa na nyingine kukamatwa katika  zoezi la doria iliyoendeshwa kwa kipindi cha mwaka 2019/2020.

Mhandisi Ruyango amesema kuwa nyavu hizo zilizokamatwa na kusalimishwa ni kokoro 538, nyavu ndogo za dagaa 12, timba 305, nyavu ndogo za makila 705 na katuli 5 .

Kufuatia Hali hiyo kamati hiyo imesema haitomfumbia macho mvuvi yoyote ambaye atavua kinyume na sheria katika ziwa  victoria.

Kwa upande wake Afisa Uvuvi Wilaya ya Muleba, Wilfred Tibendelana, amesema katika kuendelea kudhibiti uvuvi usiokubalika kisheria huku halmashauri hiyo ikiahidi kuendelea kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama pamoja na viongozi wa vijiji na kata ili kulinda rasilimali za ziwa victoria na Burigi.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wilayani Muleba wameshukuru kamati hiyo kwa zoezi hilo licha ya uwepo wa changamoto ya baadhi ya viongozi waliopo katika maeneo yao kujihusisha na vitendo vya rushwa baina yao na wavuvi hivyo kuishauri ofisi ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo kufanya doria za mara kwa mara ili  kuwachukulia hatua Kali za kisheria viongozi hao.

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR ASISITIZA UMOJA NA MSHIKANO KATIKA IDARA ZOTE ZA OFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR

$
0
0

Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ameendelea kuhuubiri umoja na  mshikamano katika Nchi ya Zanzibar kwa muda mrefu sasa, na leo ilikuwa ni zamu ya watendaji wake wa Idara kutoka Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Maalim ameyasema hayo aliporipoti rasmi katika Ofisi yake iliyopo Migombani Mkoa wa Mjini Magharib Unguja leo tarehe 11/01/2021.

Maalim Seif amepokelewa na Watendaji wa Ofisi hio wakiongozwa na Kaimu Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Dr. Khalid Salum Mohammed.

Baada ya kuwasili na kukagua maeneo yote ya Ofisi Makamu wa kwanza wa Rais alipata fursa ya kukutana na kuzungumza na Wakuu wa Idara mbali mbali zilizopo chini ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais.

Katika nasaha zake kwa wakuu wa Idara hao Maalim Seif amewataka Watendaji  wote wa Ofisi hio kuwa nadhifu kuanzia mavazi mpaka maeneo yao ya kazi kwani Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais ni miongoni mwa Ofisi kubwa katika Serikali, na muonekano wake pamoja na utendaji mzuri wa kazi unatakiwa kuwa mfano bora.

Maalim Seif pia amesisitiza uwepo wa nidhamu na uwajibikaji  kwa kusema;
”Suala la nidhamu ni suala muhimu sana kwani bila nidhamu hatuwezi kufanya mambo yetu tukapata mafanikio, na Wakuu wa idara musimuonee mtu muhali katika hili na kama mtu asipokuwa na nidhamu aadhibiwe kwamujibu wa sheria ila nasisitiza zaidi asionewe mtu’’.

Sambamba na hilo Maalim Seif amesema  Suala la Mashirikiano ni miongoni mwa jambo la muhimu sana,  na ushirikiano huu uwepo kwa mtu mmoja mmoja lakini pia kwa taasisi kwa ujumla,  na katika kusisitiza hilo Maalim amesema yeye anawakaribisha watendaji wote katika ofisi yake kwa ushauri na ufafanuzi kwa maslahi mapana ya taasisi na Taifa kwa ujumla

Jambo la mwisho  Maalim Seif amezungumzia suala la kujiwekea malengo kama taasisi kwa kuwaambia watendaji yakwamba;

”Tunahitaji tukamilishe majukumu yetu yote yanayotupasa kufanya tena kwa ufanisi mkubwa,  na hili litafanikiwa kama tutajiwekea malengo katika utendaji wetu, niwaombe Wakuu wa Idara na watendaji wote muwe na mikakati ya malengo yetu ya muda mfupi na ya muda mrefu ili kuhakikisha hakuna kitu tutakachokiwacha nyuma’’.

Kwakumalizia Maalim amewaambia Wakuu wa Idara zote zilizopo chini ya Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais kwamba ataanza Ziara Rasmi ya kupitia Idara hizo kuanzia siku ya Jumaatano ili kujua Changamoto na kubadilishana mawazo.

HALMASHAURI YA WILAYA YA MULEBA YATOA MADAWATI 836 KWA SHULE ZA MSINGI 26

$
0
0

 


Na Lydia Lugakila, Muleba


Halimashauri ya Wilaya ya Muleba mkoani Kagera imegawa madawati 836 katika shule za msingi  zipatazo 26 kupitia mapato yake ya ndani ambayo yamesaidia  kuondoa changamoto ya uhaba wa madawati shuleni.

Akigawa madawati hayo Mkurugenzi Mtendaji wa halimashauri ya Wilaya ya Muleba Bwana Emmanuel Sherembi amesema katika mwaka huu wa fedha halmashauri hiyo ilikuwa na mahitaji ya madawati 51,534 na kulikuwa na madawati 49,576 upungufu ukiwa ukiwa ni madawati 1948.

 sherembi amesema kuwa halmashauri ya Wilaya ya Muleba kupitia mapato yake ya ndani imetengeneza madawati 1,036 katika awamu mbili ambapo awamu ya kwanza madawati 200 yalitengenezwa na kusambazwa katika shule za msingi tisa.

Aidha Mkurugenzi huyo ameagiza walimu wakuu kuhakikisha wanakarabati madawati yote ndani ya siku saba kwani ofisi ya Mkurugenzi imetoa kibali cha utengenezaji wa madawati mabovu katika shule zilizoomba 58 ikiwa ni jumla ya madawati 1074 na hivyo kiumaliza kabisa changamoto ya madwati katika Wilaya hiyo.

Awali akisoma taarifa  kaimu afisa elimu msingi Wilaya ya Muleba Bi. Restuta Stephano amesema Wilaya ya Muleba ina jumla ya shule za msingi 241 ambapo shule 227 ni za serikali na shule 14 ni shule binafsi jumla yake wakiwa wanafunzi   154,604.

MBUNGE MTATURU AENDELEA KUWAKUMBUKA WANAFUNZI JIMBONI MWAKE

$
0
0

Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu akigawa sare za shule,madaftari na kalamu zenye thamani ya shilingi zaidi ya milioni 30 kwa  wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wapatao 1161 zilizopo jimboni kwake leo hii.

Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Ikungi, Mwalimu Ngwano Ngwano akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo, Justice Kijazi na Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo amempongeza na kumshukuru Mtaturu kwa dhamira yake ya kusaidia maendeleo ya wananchi kwenye sekta mbalimbali katika jimbo hilo.

Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu, akizungumza na wananchi wakati akitoa msaada huo.
Msaada wa daftari ukitolewa.
Msaada wa daftari, kalamu na sare za shule  ukitolewa.
Vifaa hivyo vikipokelewa.
Msaada wa daftari ukitolewa.
Vifaa vilivyotolewa


Na Dotto Mwaibale, Ikungi


MBUNGE wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu ameendelea kuwa kumbuka wanafunzi katika jimbo lake kwa kuwanunulia vifaa mbalimbali vya shuleni.

Vifaa alivyotoa ni sare za shule, madaftari na kalamu vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 30 ambapo wanufaika ni wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wapatao 1161 kutoka katika familia zisizo na uwezo zilizopo jimboni humo.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa ahadi yake ya kuwasaidia wanafunzi katika jimbo hilo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. John Magufuli za kutoa elimu bure kuanzia shule za msingi hadi sekondari.

Akizungumza wakati akigawa vifaa hivyo leo hii Mtaturu alisema amekuwa akifanya hivyo tangu alipo chaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.

“Serikali yetu ya awamu ya tano imewekeza kwenye elimu, inatoa elimu bila ya malipo nami kama mbunge wa jmbo hili nimeona niunge mkono jitihada hizo kwa kusaidia sare na vifaa vya shule ili kusiwepo kikwazo na hivyo kuwezesha lengo la serikali kutimia,” alisema Mtaturu.

Alisema katika utendaji kazi wake kipaumbele chake cha kwanza ni elimu kwa kuwa ndio msingi wa maendeleo hasa kwa watoto.

Mtaturu alisema dhamira yake hiyo ya kuwasaidia wanafunzi hao inaenda sambamba na kauli mbiu yake isemayo  'ElimuYetu, Maendeleo Yetu' inayochochea upatikanaji wa elimu kwa wote ili iwe njia ya kupatikana kwa maendeleo.

Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Ikungi, Mwalimu Ngwano Ngwano akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo, Justice Kijazi na Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo amempongeza na kumshukuru Mtaturu kwa dhamira yake ya kusaidia maendeleo ya wananchi kwenye sekta mbalimbali katika jimbo hilo.

Wakulima wa choloko wapewa mbinu ya kukwepa hasara

$
0
0

NA DANSON KAIJAGE, SHINYANGA


MKUU  wa Mkoa wa Shinyanga  Zainab Telack ameagiza Maafisa Kilimo Mkoani Shinyanga kutoa elimu ya mfumo wa stakabadhi gharani kwa wakulima wa zao la choroko ili waache tabia ya kuuza mazao yakiwa bado kuepuka kuwanufaisha wanunuzi badala ya wakulima ambao wanatumia nguvu nyingi kuandaa mazao hayo.


Kiongozi huyo wa Mkoa amesema hayo jana wakati wa ufunguzi wa kikao cha siku moja kilichowakutanisha  wadau wa zao la choroko Mkoani Shinyanga ili kujadili namna bora ya matumizi ya mfumo wa stakabadhi gharani kwa lengo la kuhakikisha unaleta tija kwa wakulima wa zao hilo na taifa kwa ujumla.


Aidha  Telack aliongeza kuwa kwa kutumia mfumo wa stakabadhi gharani itawezesha wanunuzi wa zao la choroko kujua sehemu sahihi ya kupata zao hili likiwa katika ubora na kuepuka kuibiwa fedha zao na matepeli.


 Telack amesema  kuwa ni agizo la serikali kuhakikisha mazao ya aina ya kunde yanatumia mfumo stakabadhi gharani kama ilivyo kwa zao la korosho na sasa Shinyanga kwa kuanzia inaanza na zao la Choroko na baadae itahamishia nguvu zake kwenye zao la dengu na mpunga lengo likiwa kuahakikisha wakulima wa mazao haya wanapata faida ya jasho lao na kujiletea maendeleo.


 ‘’Nataka kuona wakulima Mkoani Shinyanga wakiwa na uwezo wa kusomesha watoto, kujenganyumba bora na kufaidika na jasho lao sio mkulima analima mpunga katika maji mengi lakini mnunuzi ananunua mpunga bado ukiwa shambani nakuvuna gunia sitini kwa kumlagai mkulima kwa kumpatia bodaboda.’’Amesema Mkuu wa Mkoa huo.


Pis  Telack alimwagiza Kaimu Mrajisi wa Vyama Vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga,Hilda Simon kukutana na viongozi wa vyama vya msingi na Cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga(SHIRECU) kuweka mikakati ya pamoja ya kutoa elimu kwa wakulima ili wajue faida za kutumia mfumo wa stakabadhi gharani.


Naye Kaimu Mrajisi wa Vyama Vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Hilda Simon alisema kuwa changamoto ya kushindwa kutumia mfumo wa stakabadhi gharani inapelekea kushindwa kuwa na takwimu sahihi za zao hilo, kuendelea kuwepo kwa utoaji vibali holela vilivyokuwa vikitolewa na Halmashauri bila kupitia vyama vya Msingi.


Hilda aliongeza kuwa vibali hivyo vilikuwa vikitolewa kwa wanunuzi wa kati ambao kimsingi ndio wapinzani wa mfumo wa stakabadhi gharani na hivyo kuendelea kumyonya mkulima kwa kununuoa choroko kwa bei za chini akitaja pia changamoto ya wakulima kukosa uvumilivu wa kusubili malipo kuwa ni sababu pia ya kushindwa kutumia mfumo wa stakabadhi gharani.


Wakati huo huo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa aliwaambia wadau wa kikao hicho kuwa viongozi wa vyama msingi mkoani humo ni tatizo sana kwakuwa hawajui uchungu wa wakulima kwani hawana hata shamba moja kazi yao imekuwa ni kuongea maneno maneno tu nakuwataka wakulima kuchagua viongozi ambao pia wana mashamba ya zao hilo.


Suala la Mfumo wa Stakabadhi Shambani sio jipya lakini kumekuwepo changamoto mbalimbali za utekelezaji wa mfumo huo ndio maana Mkoa unajipanga upya kuhakikisha unaondoa changamoto zilizopo na kutafuta namna bora ya uendeshaji mfumo huo kwa kushirikisha wadau wa zao hilo.

ASEKENYA: JIPANGENI KUTOA WATALAAM WENGI WA RELI

$
0
0


Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, akitoa maelekezo kwa uongozi wa Chuo cha Reli cha Tabora na watalaamu wa karakana ya reli iliyopo mkoani humo.

 

 

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya, amezungumzia umuhimu wa Chuo cha Reli Tabora kuongeza kozi za reli zinazoendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ili kuzalisha wataalam wengi wa reli wataohudumu katika miradi mikubwa ya reli inayoendelea kujengwa nchini. 

Ameyasema hayo mkoani Tabora, wakati alipokagua chuo hicho na karakana ya reli ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza kuwepo kwa mikakati madhubuti ya kulisaidia Taifa katika usimamizi na ujenzi wa miundombinu ya reli mpya ya kisasa na ile ya reli ya kati inayoendelea kuboreshwa.

"Huu ni wakati wa Shirika la Reli nchini ( TRC), pamoja na Taasisi zake kuja na mtazamo mpya utakaowezesha juhudi za Serikali za kufufua Sekta ya Reli kufanikiwa", amesema Mhandisi Kasekenya.

Aidha ameitaka TRC kuhakikisha inaboresha mifumo ya ukusanyaji wa mapato ili fedha inayopatikana iwezeshe kuboresha huduma zake na kupata faida.

Kasekenya ameeleza lengo la Serikali ni kuhakikisha mizigo mizito inasafirishwa kwa reli nchini kote ili kulinda barabara.

Aidha, Naibu Waziri Kasekenya amesisitiza umuhimu wa watumishi wa reli waliopo kazini kupata mafunzo ya mara kwa mara ili kuondoa kufanya kazi kwa mazoea.

Amewataka watumishi wa reli kuwa waadilifu na kuacha vitendo vyote vya rushwa na uhujumu ili kuiwezesha reli kuwa salama wakati wote.

"Hakikisheni huduma za reli zinakuwa za haraka na uhakika, punguzeni urasimu kwa wafanyabiashara", amesisitiza Mhandisi Kasekenya.

Naye Mkuu wa Chuo cha Reli Tabora, Bw. Damas Mwajanga, amemhakikishia Naibu Waziri huyo kuwa chuo hicho tayari kimepata ithibati ya NACTE na hivyo kimeanza kuongeza udahili wa wanafunzi ili kuweza kuhudumia soko la reli katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

Zaidi ya wanafunzi 200 wa ngazi za cheti na diploma wanasomea mafunzo ya reli katika kampasi zake  za Tabora na Morogoro.

Chuo cha Reli cha Tabora kilianzishwa mwaka 1947 ikiwa ni kituo kikuu cha kuhudumia reli katika Ukanda wa Afrika Mashariki na kimekuwa kikitoa mafunzo ya ufundi wa treni, udereva wa treni, umeme, watalaam wa mawasiliano ya treni na wakaguzi wa mabehewa.


NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, GEKUL ATEMBELEA WAKALA YA MAABARA YA VETERINARI WILAYANI KIBAHA MKOANI PWANI

$
0
0

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu, Wakala ya Maabara ya Veterinari (TVLA), Dkt. Stella Bitanyi akimuonesha Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul moja ya chanjo wanazozalisha alipotembelea Kituo cha Wakala hiyo cha kutengeneza chanjo kilichopo Wilayani Kibaha, Mkoani Pwani Januari 11, 2021.


Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha TANCHOICE, Selo Luwongo (wa pili kutoka kushoto) akimuonesha Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (wa pili kulia) maroli yaliyopakiwa minofu ya nyama ya mbuzi zaidi ya Tani 40 kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi alipotembelea Kiwanda hicho Januari 11, 2021. Kulia ni Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama, Imani Sichwale.
Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha TANCHOICE, Selo Luwongo (kushoto) akimuonesha Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (wa tatu kutoka kushoto) mbuzi waliochinjwa na kuhifadhiwa katika chumba chenye baridi kali kwa ajili ya kusafirishwa kuuzwa nje ya nchi. Gekul alitembelea kiwanda hicho kilichopo Wilayani Kibaha, Mkoani Pwani Januari 11, 2021.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu, Wakala ya Maabara ya Veterinari (TVLA), Dkt. Stella Bitanyi (kulia) akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (katikati) alipotembelea Kituo cha Wakala hiyo kilichopo Wilayani Kibaha, Mkoani Pwani Januari 11, 2021. Kushoto ni Kaimu Msajili, Bodi ya Nyama, Imani Sichwale.


 Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu, Wakala ya Maabara ya Veterinari (TVLA), Dkt. Stella Bitanyi (kulia) akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (katikati) alipotembelea Kituo cha Wakala hiyo kilichopo Wilayani Kibaha, Mkoani Pwani Januari 11, 2021. Kushoto ni Kaimu Msajili, Bodi ya Nyama, Imani Sichwale. 

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK. HUSSEIN ALI MWINYI APOKEA MAANDAMANO YA WANANCHI NA VIKOSI VYA ULINZI YA AMSHA AMSHA NA MAPINDUZI VIWANJA NA MNAZI MMOJA ZANZIBAR

$
0
0

 

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwapungia mkono Wananchi wakati akiyapokea Maandamano ya Maadhimisho ya sherehe za Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilizofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Zanzibar na kushirikisha Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar Amsha Amsha Mapinduzi.(Picha na Ikulu).


WANANCHI wa Zanzibar wakishiriki katika Maandamano ya kuadhimisha sherehe za Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizoadhimishwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar.

ASKARI wa JWTZ wakishiriki katika Maandamano ya Amsha amsha na Mapinduzi wakati wa Maadhimisho ya sherehe za Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja na kupokelewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Zanzibar.

WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI MKOANI PWANI WAASWA KUZINGATIA USAFI WA VYOO

$
0
0

 


Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani Dk. Gunini Kamba akizungumza jambo katika moja ya mkutano na wadau mbali mbali wa sekta ya afya kwa ajili ya kujadili masuala mbali mbali yanayohusiana na utoaji wa huduma za afya.

 

 

NA VICTOR MASANGU, PWANI 

 

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani  Gunini Kamba amewawatahadharisha na kuwaonya vikali  baadhi ya  wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari  kuachana kabisa na vitendo vya kujisaidia  katika maeno ya vichake kwani kufanya hivyo kunaweza kusababisha madhara makubwa ya  kutokea kwa mlipuko wa magonjwa mbali mbali ikiwemo kipindu pindu.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake kuhusiana na   mikakati waliyojiwekea katika ngazi ya Mkoa katika kupambana na kudhibiti katiba hali ya kuwepo kwa magonjwa ya mlupiko katika maeneo mbali mbali hususana katika mkusanyiko wa wtu wengine kama vile mashuleni.

“Kwa sasa hivi tupo katika msimu mpya wa mwaka wa 2021 ambapo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari tayari wamefungua shule zao na kuanza masomo lakini pamoja na mambo mengine yote ni lazima sisi kama wataalamu wa afya tuweke mipango madhubuti ya kuwalinda watoto wetu hasa katika kipindi hiki na kuwatahadharisha na kutojisaidia ovyo ovyo katika maeneo ya vichaakni kwani hii ni hatari sana kupata magonjwa ya mlipuko.

Aidha Kamba alifafanya kubwa kwa kipindi hiki cha ni lazima viongozi wa shule pamoja na mamlaka zinazohusika kuhakikisha kwamba wanazingatia maagizo ambayo yanatolewa na wataalamu wa afya ikiwemo kuzingatia usafi wa mazingira pamoja na kuweka mafi safi na salama katika maeneo ya shule ili wanafunzi wanapotoka kujisaidia waweze kusafisha na kunawa mikono yao kwa lengo la kuthibiti milipuko ya magonjwa hayo.

Pia aliongeza kuwa katika kupambana na wimbi la mlipuko wa magonjwa wanaendelea kushirikiana bega kwa bega na walimu wa shule mbali mbali zilizopo katika Mkoa wa Pwani juu ya kuwaelimisha umuhimu  wa usafi wa mazingira katika maeneo yao ya kazi na kuwapa mafunzo ambayo yataweza kuwasaidia katika kuwaelimisha watoto wao katika kujikinga na magonjwa ambayo yanatokana na uchafu.

“Suala la baadhi ya wanafunzi au jamii yoyote kuwa na tabia ya kujisaidia katika maeneo ya vichakani hii sio sahii kabisa hata kidogo kwani ni hatari zaidi kutokea kwa magonjwa ya milipuko kama vile kuumwa na tumbo,kuhara na  kuibuka kwa  ugonwa wa kipindipindu na kitu kingine mtu anaweza kujisaidia na mvuaikaja kunyesha hivyo ikikisomba kinyesi kunaweza kuleta madhra makubwa katika jamii ambayo ipo karibu na maeneo hayo.

Katika hatua nyingine Kamba aliongeza kuwa serikali ya awamu ya tano lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba inaboresha sekta ya afya na kuwapatia huduma ya matibabu wananchi wake hivyo isingependa kuona hali ya kuwepo kwa magonjwa ya milipuko ambayo yanaweza kuthibitiwa endapo jamii ikizingatia kanuni na taratibu zote  ambazo zinatolewa na watalaamu wa sekta ya afya ili kuondokana kabisa na hali hiyo.

Washindi 40 Droo ya 6 NMB MastaBATA wavuta mkwanja

$
0
0

 Meneja kitengo cha Biashara ya Kadi Benki ya NMB, Sophia Mwamwitwa akizungumza kwenye droo ya MastaBata leo katika ofisi za Benki ya NMB Makao Makuu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Pendo Mfuru akisimamia droo hiyo na kulia ni Afisa Huduma kwa Wateja, Yvette Nkhoma. Hii ni droo ya wiki ya sita hadi sasa tumepata washindi 200 waliojishindia shilingi 100,000/- kila mmoja.

Afisa Huduma kwa Wateja wa Benki ya NMB, Yvette Nkhoma (kulia) akibofya kitufe kumpigia simu mmoja wa washindi wa droo ya Mastabata si Kikawaida, alioibuka mshindi katika droo ya wiki ya sita iliyoendeshwa leo. Kushoto ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Pendo Mfuru akisimamia droo hiyo na katikati ni Meneja kitengo cha Biashara ya Kadi Benki ya NMB, Sophia Mwamwitwa.


Afisa Huduma kwa Wateja wa Benki ya NMB, Yvette Nkhoma (kulia) akizungumza na mmoja wa washindi wa droo ya Mastabata si Kikawaida, alioibuka mshindi katika droo ya wiki ya sita iliyoendeshwa leo. Kushoto ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Pendo Mfuru akisimamia droo hiyo na katikati ni Meneja kitengo cha Biashara ya KadiBenki ya NMB, Sophia Mwamwitwa.




NA MWANDISHI WETU

DROO ya sita ya Kampeni ya NMB MastaBATA, inayoendeshwa na Benki ya NMB, imefanyika jijini Dar es Salaam, ambako washindi 40 wamepatikana na kufanya idadi yao tangu kuanza kwake Novemba 2020, kufikia 240.

NMB MastaBATA, ni Kampeni ya miezi mitatu iliyozinduliwa Novemba 24, 2020 na itadumu hadi Februari mwaka huu, ambako zawadi mbalimbali zinatolewa zikiwamo pesa, simu janja, jokofu, runinga na safari ya kwenda kupumzika Zanzibar, Serengeti na Ngorongoro.

Droo hiyo imesimamiwa na Pendo Albert, kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), ambako washindi wamejinyakulia Sh. 100,000 kila mmoja, kigezo cha ushiriki kikiwa ni matumizi ya Kadi za NMB Mastercard na Masterpass QR.

Akizungumza kabla ya kufanyika kwa droo hiyo, Meneja wa Idara ya Kadi ya NMB, Sophia Mwamwitwa, alisema jumla ya washindi 200 walishapatikana katika droo tano za kila wiki, na kwamba kampeni nzima inalenga kuzawadia washindi 400.

Aliongeza kuwa, ukiondoa droo za kila wiki, pia NMB MastaBATA imewazawadia jumla ya washindi 12 kati ya washindi 15 wa droo za kila mwezi ambao wao wamekuwa wakijishindia simu janja aina ya Samsung Galaxy Note20, yenye thamani ya Shilingi Mil. 2.4 

"Wito wetu kwa wateja wa NMB wenye kadi za NMB Mastercard na Masterpass QR, kufanya manunuzi na malipo mbalimbali ili kujiwekea nafasi ya kushinda droo zijazo za kila wiki, kila mwezi na ile zawadi kuu ya Grand Finale," alisema Mwamwitwa.

Aidha, zawadi kuu ya Grand Finale ambayo ni utalii Zanzibar, Ngorongoro ama Serengeti, inawapa washindi uhuru wa kuchagua zawadi mbadala kama runinga iliyolipiwa DSTV miezi mitatu, Jokofu, Laptop, Simu (Samsung A70), Water Dispenser na Microwave.

Kwa upande wake, Pendo, Ofisa wa GBT, aliwataka wateja wa NMB kuendelea kutumia kadi zao ili kujishindia zawadi zinazotolewa na NMB MastaBATA, na kwamba mchakato wa kuwapata washindi unafanyika kwa kufuata sheria na taratibu.


NAIBU WAZIRI KASEKENYA AWATAKA WATENDAJI KUFANYA MAAMUZI

$
0
0

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya (aliyevaa suti ya kaki) katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Uchukuzi, lililofanyika kwa siku mbili mkoani Mwanza.

 

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ameitaka menejimenti na viongozi wa taasisi wa Sekta ya Uchukuzi kufanya maamuzi ili kutochelewesha maendeleo kwa wananchi katika utekelezaji wa miradi.

 

Ametoa kauli hiyo wakati akifunga Mkutano wa siku mbili wa baraza la Wafanyakazi la sekta ya Uchukuzi lililofanyika Mkoani Mwanza na kusema kuwa awamu hii imejikita katika matokeo na sio mazoea.

 

“Katika awamu hii watendaji wengi wamekuwa wakichelewa kutoa maamuzi katika maeneo mbalimbali sababu ya kutojiamini hii inafanya utekelezaji wa miradi kuchelewa kukamilika na kuchelewesha maendeleo kwa wananchi” amesema Mhandisi Kasekenya.

 

Mhandisi Kasekenya ametabaisha umuhimu wa kuwa na ratiba ya ukaguzi wa miradi kwa kila muhula na kusisitiza kuwa ukaguzi huo utawezesha kupunguza changamoto zinazojitokeza kwenye utekelezaji wa miradi.

 

“Namna bora ya kutatua changamoto zinazojitokeza kwenye miradi ni kuwa na ratiba ya kukagua miradi hiyo mara kwa mara, na ratiba hizo zipangwe kwa miradi yote inayotekelezwa chini ya Sekta’ Amesisitiza Mhandisi Kasekenya.

 

Aidha, Mhandisi Kasekenya amesema kuwa ni muhimu wataalam wa sekta walio kwenye miradi kuchukua ujuzi wakati huu ambapo miradi inaendelea ili utaalam huo uwasaidie kusiimamia vizuri miradi itakapokamilika.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza na Kaimu Katibu Mkuu Gabriel Migire ameahidi kutekeleza maagizo hayo na kusisitiza kuwa kitengo cha Ufatiliaji na Tathimini-Uchukuzi kitaboresha zoezi hilo na kuhakikisha linafanyika na kuleta matokeo chanya.

 

Baraza la Wafanyakazi la sekta ya uchukuzi lililofanyika kwa siku mbili mkoani Mwanza limejumuisha menejementi na watumishi wa kila idara katika sekta na wakuu wa taasisi zilizo chini yake ambapo pamoja na mambo mengine limepitia utekelezaji wa miradi ya sekta na kuweka mikakati mbalimbali ya kuboresha utendaji wa sekta.

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI, MHANDISI KASEKENYA TANROADS NA ERB

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya (wa kwanza kulia) akizungumza na viongozi na watendaji wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) jijini Dar es Salaam alipofanya ziara kutembelea taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya (wa kwanza kulia) akizungumza na viongozi na watendaji wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) jijini Dar es Salaam alipofanya ziara kutembelea taasisi hiyo.


Baadhi ya viongozi na watendaji wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), wakiongozwa na Mkurugenzi wa Miradi wa TANROADS, Eng. Chrispianus Ako (wa kwanza kulia) wakifuatilia maelekezo ya Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya (hayupo pichani) alipofanya ziara kutembelea taasisi hiyo.


Mkurugenzi wa Miradi wa TANROADS, Eng. Chrispianus Ako (kushoto)  akitoa taarifa fupi ya utendaji wa taasisi hiyo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya (kulia) alipofanya ziara TANROADS.


Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya (wa kwanza kushoto) akizungumza na viongozi na watendaji wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania jijini Dar es Salaam alipofanya ziara kutembelea taasisi hiyo.


Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania (ERB) Mhandisi Prof. Ninatubu Lema (aliye simama) akitoa taarifa fupi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya alipofanya ziara kutembelea taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania(ERB) Mhandisi Prof. Ninatubu Lema akitoa taarifa fupi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya (kushoto) alipofanya ziara kutembelea taasisi hiyo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania, Injinia Patrick Barozi akifuatilia.

Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania, Injinia Patrick Barozi (wa kwanza kulia) akitoa taarifa ya utendaji kwa ujumla wa taasisi hiyo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya alipofanya ziara kutembelea taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania(ERB) Mhandisi Prof. Ninatubu Lema (katikati) akimkabidhi kitambulisho kipya cha uanachama wa ERB Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya (kushoto) alipofanya ziara kutembelea taasisi hiyo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania, Injinia Patrick Barozi akifuatilia tukio hilo.

AJINYONGA JUU YA MTI KWA KUTUMIA KHANGA

$
0
0

 Na Lydia Lugakila, Karagwe

Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Muombe Martin (20), mkazi wa kata ya Nyaishozi wilaya ya Karagwe mkoani Kagera amefariki dunia kwa kujinyonga juu ya mti wa muembe kwa kutumia kipande cha Khanga huku chanzo cha kujinyonga kikiwa hakijafahamika.

Akizungumza  katika eneo la tukio Ofisa Mtendaji wa Kata ya Nyaishozi, Jastus Vedasto, amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia januari 13, 2021.

Amesema kuwa mwili wa marehemu umegundulika baada ya wapita njia kupita katika eneo hilo na kubaini mwili huo ukiwa unaninginia juu ya mti huo katika sehemu ya shamba la jirani yake.

Vedasto ameongeza kuwa baada ya kupokea taarifa za wananchi, uongozi wa kata umefika katika eneo la tukio na kutoa taarifa katika kituo cha Polisi Nyaishozi kilichopo wilayani Karagwe ambapo baada ya Jeshi la Polisi kufika eneo la tukio wameruhusu mwili wa marehemu kuzikwa.


MAMA LISHE KIBAHA WAPEWA SOMO JUU YA KUJIKINGA NA MAGONJWA YA MLIPUKO

$
0
0


Mbunge wa Jimbo la Kibaha vijijini Michal Mwakamo kupitia tiketi ya Chama cha mapinduzi (CCM) akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari hawapo pichani kuhusina na mipango yake katika kuboresha sekta ya afya na kupambana na magonjwa ya mlipuko. (PICHA NA VICTOR MASANGU).

 

NA VICTOR MASANGU, PWANI

 

Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini, Michael Mwakamo, ameiasa jamii pamoja na kundi la  mama lishe kuhakikishe wanazingatia maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya ikiwemo suala zima la unawaji wa mikono kwa kutumia maji safi na salama yanayotiririka kwa kutumia sabuni  ili kuepukana kabisa na wimbi la  magonjwa ya milipuko ambayo ni hatari kwa afya za wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mikakati  aliyojiwekea katika suala zima la  kuboresha sekta ya afya  Mwakamo alibainisha kwamba kwa sasa ameweka mikakati madhubuti ya kuweza kushirikiana na wataalamu wa afya kwa lengo la kutoa elimu na mafunzo  juu ya umuhimu wa kunawa mikono hasa katika maeneo yenye mikusanyiko mingi ya watu.

 “Mimi kama Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini napenda kuchukua fursa hii kuwahimiza wananchi wangu wote pamoja na mama lishe kuweka mazingira ya kufanya usafi katika maeneo ambayo wanafanyia kazi lengo ikiwa ni kujilinda wao wenyewe pamoja na walaji kuondokana na magonjwa ya mlipuko,”alisema Mwakamo.

Pia Mbunge huyo aliongeza kuwa suala la uchafuzi wa mazingira ni hatari sana katika jamii ambayo inatuzunguka kwani linaweza kuleta madhara makubwa kwa baadhi ya wananchi kujikuta wanapata magonjwa hayo ya mlipuko ambayo chanzo chake kikubwa  kinatokana na baadhi ya wananchi kutupa taka ovyo kitu ambacho sio kizuri kabisa kwa afya ya binadamu.

Pia aliipongeza serikali ya awamu ya tano pamoja na wataalamu mbali mbali wa masuala ya afya kwa kuelekeza nguvu zao kubwa katika kuhakikisha suala la usimamizi wa usafi wa mazingira linafanyiwa kazi kuanzia katika ngazi za chini hadi juu na kuwepa kuwapa fursa wananchi waweze kuendsha shughuli zao mbali mbali katika hali ya usafi.

Aidha Mwakamo alisema kuwa katika kuunga  mkono juhudi za serikali ya awamu yatano katika mpango wake wa kufanya usafi wa mazingira atahakikisha kwamba anashirikiana bega kwa began a wananchi wa jimbo lake la kuendesha zoezi la mara kwa mara katika maeneo ya makazi ya watu ili kuweza kusafisha mazingira yawe katika hali ya usafi.

“Kitu kikubwa mimi nitaweka utaratibu mzuri wa kuendelea kushirikiana na wananchi wa jimbo langu kuanzia ngazi za vijiji kuendesha zoezi la usafi wa mara kwa mara pamoja na kuchoma taka zote ambazo zinakuwa zimezagaa lengo ikiwa ni kufanya kuondokana kabisa na magonjwa ya milipuko ambayo yanaweza kujitokeza kama vile kuumwa na matumbo, kuhala pamoja na mengineyo,”alisisitiza Mwakamo.

Katika hatua nyingine aliongeza kuwa wananchi wanapaswa kunywa maji safi na salama  ambayo tayari yanakuwa  yamechemshwa na kuuwa vijidudu ambayo vipo na kwamba itaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kuendelea kujishughulisha katika kazi zao mbali mbali bila ya kuwa na changamoto ya kuumwa na magonjwa ya aina mbali mbali.

WAZIRI MSTAAFU MIZENGO PINDA AWAAGIZA WABUNGE NA MADIWANI WA CCM KUTATUA KERO ZA WANANCHI

$
0
0
Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda akizungumza na madiwani na wabunge wa CCM mkoa wa Iringa wakati wa semina elekezi.
Mwenyekiti wa Ccm mkoa wa Iringa Abel Nyamahanga akizungumza kwenye Semina hiyo.


 
NA DENIS MLOWE, IRINGA

WAZIRI MKUU Mstaafu na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Mizengo Pinda amewaagiza viongozi katika ngazi mbalimbali mkoani Iringa ambao walichaguliwa kwa tiketi ya chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita kwenda kuisimamia Ilani kwa kushughulikia changamoto za wananchi waliowachagua.

Akizungumza katika Semina Elekezi iliyohusisha wabunge wote na madiwani wote wa CCM Mkoa wa Iringa na kufanyika katika ukumbi wa CCM mkoa wa Iringa, Mizengo Pinda alisema imani ambayo wananchi wamekionyesha chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu na kuwapa ushindi mkubwa ni kubwa na ina stahili kulipwa kwa kuwatumikia wananchi kama ambavyo imeainishwa kwenye Ilani ya chama.

Alisema kuwa wananchi wamekipa imani chama cha Mapinduzi na sasa ni zamu ya waliochaguliwa kuwaletea maendeleo ambayo wananchi wanayasubiri kwa hamu kubwa na ikumbukwe kwamba mbunge au diwani ambaye hatafanya kazi kwa misingi ilani ya chama katika kuwaletea maendeleo wananchi anawapa kazi kubwa chama kuweza kushinda katika chaguzi zake.

Aidha Pinda alisema kuwa chama kinatakiwa kutembelea miradi yote ambayo serikali inatekeleza kwenye maeneo ya wananchi kwani usipofanya hivyo huko kwenye kata wananchi kuna malalamiko mengi na unakuta diwani hata kwenye mradi mmoja hajafika hapo utakuwa diwani wa ajabu sana.

"Lazima twende kutembelea miradi kuona ile ilani ambayo wananchi walielezwa kwenye kampeni inakwenda  inavyotakiwa? tukifanya hayo ndugu zangu tutaona sehemu kubwa kabisa tutafanya kazi ya chama kuwa nyepesi na kurahisha shughuli katika chaguzi zinazofata" alisema

Aliongeza kuwa wabunge au madiwani kufanya ziara kwenye maeneo yao ni lazima isitokee kiongozi anasema kuwa asipangiwe shughuli za kufanya kumbuka chama kina taratibu zake na chama kikiona hufanyi kazi vizuri hakiwezi kukuacha hivi hivi kwani lazima chama kimbane mbunge kuhakikisha anafanya ziara kwenda kusikiliza changamoto za watu ,kuyapatia ufumbuzi na aweke utaratibu wa kusikiliza kero za watu kila wiki au kila anapopata muda.

Alisema kuwa kama mbunge au diwani hafanyi kazi yake ipasavyo ndio chanzo cha rais Magufuli kufikishiwa barua nyingi ambazo hazina sababu kwa sababu wa chini yake hawafanyi kazi ipasavyo hivyo ni wajibu wa kila mbunge na diwani kufanya hivyo kusikiliza kero za wananchi.

Alisema kuwa ukifanya wajibu wako wa kukutana na makundi ambayo yamesaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha ushindi na kusikiliza kero zao na sio kama ilivyo kuwatafuta kipindi cha uchaguzi kisha wakati huku mwanzo ulikaa kimya hiyo safari hii kama chama hakiwezi kuvumilia.

Pinda alitoa wito kwa viongozi kuhakikisha sekta binafsi kutoiweka pembeni katika maendeleo ya nchi hivyo ndani ya chama tawala tuone namna gani sekta binafsi inapata nafasi ya kusikilizwa kila mara kwa lengo la kuona changamoto wanazokabiliana nazo ili kuziondoa.

Aidha alitoa wito kwa viongozi kuhakikisha wanasoma ilani kwa umakini ili kuweza kubaini ahadi za wananchi katika kuwaletea maendeleo hivyo wananchi wanategemea mengi kutoka ndani ya chama cha Mapinduzi walichokipa madaraka ya kuongoza dora.

akizungumzia kuhusu mapato ya chama Pinda alisema kuwa bado inahitajika nguvu kubwa katika kukiletea mapato chama kwani inahitajika kazi kubwa na kuwataka makatibu kusimamia makusanyo ya mapato kila mkoa ili kukifanya chama kiweze kujitegemea iwe ajenda ya watu wote wakiwemo wabunge na madiwani kiwe kinajitegemea.

Aliwataka kuhakikisha miradi iliyopo inasimamiwa vizuri kila kinachopatikana kiende kikafanye kazi ya kujenga chama hivyo wale wenye tabia ya kukusanya fedha na kuingia mfukoni waache mara moja kwani hadi majuzi hapa kuna taarifa kuna baadhi wanakula fedha za chama hivyo lazima kuwe na miradi katika ngazi ya kata,ngazi ya tawi lazima hata kama midogo itasaidia.

Aidha alisema kuwa mafunzo kwa viongozi na makada ni muhimu sana yanasaidia kukumbushana mambo mbalimbali ya uongozi kuliko kukaa bila mafunzo na kuwaacha viongozi kutoelewa suala zima la kuongoza.

Kwa upande wake Mwenyekit wa CCM Mkoa wa Iringa Dk Abel Nyamahanga alisema wao kama chama watapita katika maeneo mbalimbali kuangalia utekelezaji wa ilani na kamwe hawatakuwa na simile na kiongozi atakayeshindwa kutekeleza kwa vitendo ahadi alizozitoa kwa wananchi kipindi cha uchaguzi.

Kwa upande wao baadhi ya wabunge akiwemo Justin Nyamoga Mbunge wa jimbo la Kilolo alisema kuwa maagizo waliyopewa na watayafanyia kazi kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi na kuhakikisha ahadi zote zinafanyiwa kazi.

Nyamoga alisema kuwa semina hiyo imewejenga kwa kiasi kikubwa kwani inawakumbusha kwamba wale wote waliochaguliwa wana deni kubwa kwa wananchi na endapo wakizembea katika kuwatumikia wananchi kutakuwa na kazi kubwa sana katika chaguzi zijazo,

"wananchi wametupa imani kubwa sana na ndio maana tukaibuka na ushindi wa kishindo katika chaguzi iliyopita hivyo deni hili linalipwa kwa kuwaletea maendeleo wananchi waliotuchagua na kumpa kura za kishindo rais Magufuli" alisema.

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA ZANZIBAR PAMOJA NA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR CHATO MKOANI GEITA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amewashika mikono Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad mara baada ya kuzungumza na Wanahabari katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita leo tarehe 14 Januari 2021.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad mara baada ya mazungumzo yao katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita leo tarehe 14 Januari 2021.

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad   akizungumza na Wanahabari mara baada ya kikao chao cha pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari mara baada ya mazungumzo yao ya pamoja na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad. PICHA NA IKULU.

KASEKENYA: ONGEZENI UBUNIFU NA KUZINGATIA MAADILI

$
0
0

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, akizungumza na uongozi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), (hawapo pichani), wakati wa ziara yake kwa wakala huo, mkoani Dar es Salaam. 

 

Dar es Salaam, Tanzania

 
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, amewataka wahandisi, wakandarasi, wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi kuongeza ubunifu na kuzingatia maadili katika majukumu yao ya kazi ili kuliwezesha Taifa kunufaika na thamani ya fedha katika miradi ya ujenzi inayoendelea.
 

Akizungumza mkoani Dar es Salaam, mara baada ya kutembelea taasisi za Wakala wa Barabara nchini (TANROADS),  Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB), Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), amewataka wataalamu hao kufahamu kuwa maendeleo na ukuaji wa uchumi unategemea sana taaluma zao.

"Tumieni fursa za miradi mikubwa inayoendelea nchini kujifunza ili kuliwezesha Taifa kuwa na watalaam wake watakaomudu kujenga miradi mikubwa katika siku zijazo", amesema Naibu Waziri Kasekenya.

Aidha, amezitaka taasisi binafsi na umma kuweka mipango madhubuti ya kuwapokea wanafunzi wa fani za kihandisi katika mazoezi ya vitendo ili kuwajengea uwezo.

Kwa upande wake, Kaimu Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Crispianus Ako, amesema TANROADS imejipanga kuhakikisha barabara zote kuu na za mikoa zenye urefu wa KM 36,258 zinapitika katika kipindi chote cha mwaka.

Amesisitiza kuwa katika kuhakikisha barabara zinalindwa ili ziweze kudumu kwa muda mrefu TANROADS inasimamia mizani 82 katika maeneo mbalimbali nchini.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Bodi ya ERB, Prof. Ninatubu Lema, amesema bodi hiyo inaendelea kusajili na kusimamia shughuli za kihandisi nchini ambapo zaidi ya wahandisi elfu thelathini (30,000) wamesajiliwa hadi  sasa.

Katika kuhakikisha wahandisi wazingatia maadili, Msajili wa ERB, Mhandisi Patrick Barozi, amesema bodi hiyo imekuwa ikitoa leseni ya uhandisi na imekuwa ikiwachukulia hatua kali wahandisi wanaokiuka maadili.

Mhandisi Barozi ametoa rai kwa wanafunzi wa kike kusoma masomo ya sayansi ili idadi ya wahandisi wanawake iongezeke ambapo hadi sasa kati ya wahandisi elfu thelathini (30,000) walisojaliwa nchini wanawake ni asilimia 11 tu.

Naye Msajili wa Bodi ya Wakandarasi (CRB), Rhoben Nkori, amemuhakikishia Naibu Waziri Kasekenya kuwa bodi hiyo inaendelea kuhakikisha wakandarasi wazawa wanaongezeka na kupata miradi mingi ili uwekezaji mwingi wanaoufanya uwe wa  hapa nchini.

"Tunahakikisha wakandarasi wazembe wanafutiwa usajili ili wakandarasi waliopo wawe wale wanaofanya kazi kwa ubunifu na uzalendo", amefafanua Nkori.

Kwa upande wa Msajili wa Bodi ya AQRB, Mkadiriaji Majenzi Edwin Nnunduma, amesema kuongezeka kwa idadi wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi kutaboresha sekta ya ujenzi hapa nchini na kuwezesha miradi mingi ya ujenzi kuwa ya uhakika na yenye viwango vya ubora.

Naibu Waziri Kasekenya yupo mkoani Dar es Salaam katika ziara ya kukagua taasisi zilizo chini ya Wizara yake ambapo ametembelea na kuzungumza na uongozi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS),  Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB), Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB).

MBUNGE NYAMOGA AWAHAKIKISHIA UMEME WANANCHI WA MGOWEKO NDANI YA MIAKA MITANO

$
0
0


 

NA DENIS MLOWE, IRINGA

 

MBUNGE wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Justin Nyamoga amesema atahakikisha ndani kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake wanakijiji cha Mgoweko kilichoko kata ya Nyanzwa wilaya ya Kilolo wanapatiwa umeme

 

Akizungumza wakati wa mkutano wa kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge uliofanyika katika kijiji cha Mgoweko, Nyamoga alisema kuwa kitendo cha wananchi hao kukipatia kura za kutosha chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu kimewapa deni kubwa la kuhakikisha wanaleta maendeleo.

 

Alisema kuwa kura za kishindo alizopata rais na wabunge zimekuwa deni kubwa kwao hivyo watahakikisha ndani ya kipindi cha miaka mitano vijiji hivyo vinapata umeme wa REA kwani atasimamia hilo kwa karibu zaidi.

 

“Ndani ya hii miaka mitano nitahakikisha kwamba tunashirikiana katika kutatua kero ambazo zipo zinatatuliwa na wananchi wanaendelea kuwa na maisha bora zaidi katika kipindi hichi ambapo nchi ipo katika uchumi wa kati na kuhakikisha kwamba mwananchi mmoja mmoja anafurahia maisha katika awamu hii ya tano chini ya Rais John, Magufuli” alisema

 

Aidha Nyamoga alisema kuwa katika sekta ya afya atahakikisha ujenzi wa zahanati ulioanzishwa na wanakijiji cha Nyawegete ndani ya kipindi cha miaka mitano wanakamilisha ili iweze kuhudumia wananchi na kuwapongeza kwa hatua hiyo.

 

Aliongeza kuwa changamoto ya maji wanayokabiliana nayo wananchi wa kijiji hicho atahakikisha anashirikiana na RUWASA ili kuondoa tatizo hilo na vitongoji 17 ambavyo havijapata huduma ya umeme wanapata huduma hiyo.

 

Aidha alichangia mifuko 10 ya saruji ili kukamilisha ujenzi wa matundu ya choo katika shule ya msingi Nyawegete na kuendelea kuwaahidi suala la mawasiliano ya simu ili kupata kampuni ambayo itawekeza kata ya Masisiwe ili kuondokana na tatizo la mawasiliano.

 

Nyamoga ambaye mbunge kwa mara ya kwanza katika jimbo hilo alisema kuwa kwa kushirikiana na wananchi wa kata ya Masisiwe atahakikisha anafanikisha adhama ya wananchi kuwa na jengo la ofisi ya kata ya Masisiwe .

Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>