Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

SERIKALI YA CHINA YATOA ZAIDI YA MILIONI 350 KUBORESHA MAFUNZO CHUO CHA VETA-CHATO

$
0
0

 

 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, akionyesha kitabu chenye hundi ya zaidi ya Sh. milioni 350 zilizotolewa na serikali ya China kwa ajili ya kuboresha mafunzo katika Chuo Cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) cha Wilayani Chato, mkoani Geita kilichozinduliwa jana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi kwa siku mbili.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi wakizindua Chuo Cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kilichopo wilayani Chato mkoani Geita, jana.


 


TCRA yatekeleza agizo la Waziri Ndugulile

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Joannes Karungura, akizungumza na wakuu wa makampuni ya Mawasiliano juu ya kuboresha huduma hiyo katika Kikao kilichofanyika Makao Makuu ya Mamlaka hiyo ikiwa ni agizo la Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari  Dkt. Faustine Ndugulile ya Mamlaka hiyo kukutana na wadau kujadili kuhusiana vifurushi vya Bando uliofanyika Makao Makuu Jijini Dar es Salaam.

MRADI WA VIUNGO KUFUNGUA FURSA KWA WAKULIMA ZANZIBAR

$
0
0


Picha ya kumbukumbu ikiwaonyesha washiriki wa Mkutano wa utoaji elimu dhidi ya mradi mpya wa viungo unaofadhiliwa na umoja wa Ulaya  (EU) kwa usimamizi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. (Picha na Talib Ussi).

Baadhi ya akinamama kutoka shehia ya Bandamaji mkoa wa Kaskazini Unguja wakionesha karatasi ilioashiria umuhimu wa kuweka akiba ambayo ni miongoni mwa ajenda kuu ya katika mradi wa viungo.

 

 

Na Talib Ussi,  Zanzibar 

 

Baadhi ya Wanananchi wa Shehia mbali mbali Unguja wameleza matarajio yao juu ya ujio wa mradi wa Viungo kuwa mradi huo utakwenda kufungua fursa zaidi za wakulima pamoja na kuongeza kipato sambamba na upatikanaji wa lishe bora na uwekaji wa akiba.

 

 

Wananchi hao waliyasema hayo katika shehia ya Bandamaji mkoa wa kaskazini Unguja na baadhi ya shehia nyengine mbali mbali  kwa nyakati tofauti walipokua wakipatiwa elimu juu ya mradi huo utakao jikita na kilimo cha matunda,mbogamboga pamoja na viungo na kufanyika zaidi ya shehia 50 za Unguja na Pemba.

 

Walisema kwa miaka mingi wamekua wakijishughulisha na shughuli za kilimo tofauti lakini hadi leo hii bado kama wakulima hawajafikia malengo yao ipasavyo.

 

Mmoja miongoni mwa wananchi hao Kidume Juma alisema licha ya kuwa  shughuli kubwa kwao ni kilimo lakini hadi leo hii bado wakulima walio wengi wamebaki kuwa masikini wanati wao ndio walipaswa kuwa kama walivyowakulima wengine ulimwneguni.

Alisema imefika wakati wakulima katika eneo hilo na maeneo mengine wanafanya shughuli hizo kama mazoea lakini si kwa kutegemea mafanikio kama wengine.

 

‘’Kuna wakati tunajikuta shamba zima la mananasi ama bidhaa nyengine baad aya kumaliza mavuno tumekula hasara au tunapata kile tulichokitoa tu kwa ajili ya uandaaji wa shamba na mambo mengine huku tukiwa tumepoteza nguvu na muda mwingi.

 

Nae Chapa Mkali Juma alisema licha ya uwepo wa changamoto hio lakini pia wamekua wakikabiwa na tatizo kubwa la uhaba wa masoko kwa bidhaa zitokananzo na kilimo chao.

 

Alisema katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar wananchi walio wengi hususani mashamba wamehamaisika na kilimo lakini wamekua wakikata tamaa wanapoona bidhaa zao zinakwenda sokoni bila kununuliwa kama walivotarajia.

 

Alieleza kuwa kikawaida mkulima hutumia nguvu nyingi kuzalisha mazao lakini matunda ya nguvu hizo ni madogo sana na yasioendana na uhalisia wa kazi wenyewe.

 

‘’Kwa mfano ulanguzi unaofanywa na baadhi ya watu masokoni wanaojiita madalali kushusha bei kwenye mazao yetu kwa sababu tofauti  ikiwemo kukosa ubora wa bidhaa huku wao wakiuza bei za juu kwa wanunuzi suala hili linatuumiza sana na lazima lifanyiwe kazi’’aliongezea.

 

Akitolea ufafanuzi wa changamoto hizo afisa Afisa maendeleo biashara  kutoka mradi wa viungo  Zanzibar Mwanaidi Mussa Shembwana alisema katika jamii kumekuepo na wakulima wengi wanaoendelea kulalamikia kukosa manufaa ya jasho lao kutokana na sababu tofauti.

 

Akitaja miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na wakulima kutojua mbegu sahihi za matunda ambazo zingeweza kuwasaidia kupata kipato zaidi kufuatia uhitaji wa wananchi sokoni.

 

Alisema kwa mfano hadi leo hii katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar licha ya kuwa ardhi yake kukubali kilimo cha nanasi lakini bado wakulima hawana taaluma ni aina gani ya matunda hayo yanahitajika zaidi katika masoko ya ndani na ya kimataifa.

 

Sambamba na hayo alisema  wakulima wanahitaji kupatiwa elimu ni wakati gani na sahihi kwao kufanya kilimo na mbegu gari ni bora zaidi  kwa kuwa kuna mazingira kikawaida si sahihi kuazisha baadhi ya vilimo kutokana na kukosa uhitaji wa bidhaa katika kipindi hicho.

 

 

Kuhusu suala la uhaba wa masoko aliwataka wakulima hao kuamini kuwa kila bidhaa iliobora inauzika sokoni hivyo kupitia mradi huo watahakikisha wanufaika wote wale iwe wa vikundi au mtu mmoja mmoja wanazalisha bidhaa bora na zenye viwnago vya kimataifa.

 

‘’Kwa hili la masoko naomba niwatoe wasiwasi tuna wenzetu ambao wapo Canada jukumu lao kwa kushirikiana na sisi nikuhakikisha tunapata masoko ya kimataifa kwa bidhaa zote zinazozalishwa Zanzibar kupitia mradi huu na ninaamini mutaweza’’aliongezea.

 

Awali afisa  fedha kupitia mradi huo  Agnes Nicodemas Msengi alisema licha ya mradi huo kunufaisha wakulima kupitia kilimo lakini pia utasaidia wakulima kuwa na utaratibu maalumu wa kujiwekea akiba.

 

Alisema kuna mkakati maalumu wa taaluma ambayo watapewa wakulima wote hususani wenye vikundi vya akinamama waweze kuweka akiba ya kujipatia mikopo katika benki mbbali mnali hapa Zanzibar.

 

Mradi wa huu wa viungo ni wa miaka mine na unaendeshwa na taasisi  ya People Development Forum, Community Forest in Pemba pamoja na TAMWA-Zanzibar kwa kuufadhiliwa na umoja wa Ulaya chini ya usimamizi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

 

 

HALMASHAURI ZASHAURIWA KUTUMIA BMU KUKUSANYA MAPATO YA UVUVI

$
0
0

Mratibu wa Mradi wa Usimamizi wa Rasilimali za Bahari Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFish), Dkt. Nichrous Mlalila akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (kushoto) alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Kikundi cha Ulinzi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi (BMU) inayojengwa katika Kata ya Dunda, Wilayani Bagamoyo jana.

Mwenyekiti wa Kikundi cha Ulinzi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi (BMU), Kata ya Dunda, Wilayani Bagamoyo, Isihaka Hudi (kulia) akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (kushoto) alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya BMU hiyo.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mratibu wa Mradi wa Usimamizi wa Rasilimali za Bahari Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFish), Dkt. Nichrous Mlalila ( kulia) alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Kikundi Cha Ulinzi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi (BMU) katika kata ya Dunda, Wilayani Bagamoyo.

 


Na Mbaraka Kambona, Bagamoyo

 

Mratibu wa Mradi wa Usimamizi wa Rasilimali za Bahari Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFish), Dkt. Nichrous Mlalila ameziomba Halmashauri kuvitambua Vikundi vya Ulinzi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi (BMU) na kuzipa uwezo wa kukusanya mapato yatokanayo na shughuli za uvuvi ili ziweze kusaidia vikundi hivyo kujiendesha na kuendeleza sekta ya uvuvi nchini. 

Dkt. Mlalila alitoa rai hiyo katika ziara ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya BMU inayojengwa na Mradi wa SWIOFish katika Kata ya Dunda, Wilayani Bagamoyo jana. 

Kwa mujibu wa Dkt. Mlalila sehemu kubwa ya mapato yanayokusanywa kwa sasa na Halmashauri hayarudishwi kwa Jamii ya wavuvi kwa ajili ya kuendeleza shughuli za sekta na uchumi wa jamii husika. 

Dkt. Mlalila alisema anatambua kuwa kuna changamoto ya kisheria ambayo baadhi ya Halmashauri zimetumia kuzizuia BMU kukusanya mapato yanayotokana na rasilimali za uvuvi. 

“Tunahamasisha Halmashauri kuwapa uwezo BMU kukusanya mapato ili kuziwezesha kupata kipato cha uhakika cha kuendesha shughuli zao za kulinda rasilimali za Uvuvi lakini pia mapato hayo yatawezesha kuendeleza sekta ya uvuvi tofauti na ilivyo sasa,” alisema Dkt. Mlalila. 

Katika baadhi ya Halmashauri ambazo wamewapa kazi BMU ya kukusanya mapato kama vile Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Mkoani Tanga, Mapato yanayotokana na uvuvi yameongezeka kutoka shilingi milioni 9 kwa robo mwaka hadi milioni 51 na kutoka shilingi milioni 36 hadi milioni 256 kwa mwaka. 

“Nazishauri Halmashauri nyingine zichukue mfano wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani kwa sababu sisi tumezipa mafunzo ya kina hizi BMU katika kusimamia fedha na ukusanyaji wa mapato, hivyo tunaamini hilo ni suala la mchakato na tumewasilisha andiko TAMISEMI ili kuangalia namna ya kuzifanya BMU kuendelea na shughuli zake hata pale ambapo mradi wa SWIOFish utakapokwisha muda wake,” aliongeza Dkt. Mlalila. 

Akizungumzia suala hilo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul alisema kuwa BMU ya kata ya Dunda na zingine zikajifunze Pangani kuona wao wanafanyaje na sisi kama Wizara tutaangalia kama kuna chanzo ambacho wataalam wa Halmashauri wanakusanya na hakifanyi vizuri na kuna BMU mahali inakusanya vizuri basi tutaibua hiyo hoja tuone tutafanyaje. 

“Ukweli ni kwamba kwenye vyanzo hivi vya leseni na ushuru wa rasilimali za uvuvi katika halmashauri zetu nyingi hazifanyi vizuri na hivyo kuna haja ya kuviangalia vizuri hasa wataalam wetu wanaotumika kukusanya hayo mapato kwa sababu kuna baadhi yao wamefanya hapo ndio maeneo yao ya kupatia pesa zao,” alisema Gekul. 

Alisema Wakurugenzi wanaweza kuwa na nia njema kabisa lakini wale wanaotumwa kukusanya hayo mapato wanarudisha maduhuli hayo kama walivyotumwa? Kama kuna watu wanauwezo wa kukusanya zaidi ya wataalam wa Halmashauri sidhani kama kuna haja ya kuwa na kigugumizi cha kuwatoa hao watu ili kazi hiyo apewe anayeweza kukusanya vizuri. 

“Kwa sababu mwisho wa siku sisi wananchi tunachotaka ni maendeleo hivyo nisingependa niseme moja kwa moja hapa kuwa BMU wapewe kazi hiyo isipokuwa Halmashauri ziangalie kama sheria inawaruhusu kuwatumia BMU kukusanya mapato,” aliongeza Gekul. 

Gekul alisema kuwa wao kama Wizara watawasiliana na TAMISEMI kuona maelekezo yakoje kwa sababu anasema kuna vyanzo Halmashauri zenyewe zinakusanya na vingine vinaruhusiwa kukusanywa na wakala na pale ambapo BMU itaonekana inafaa ipewe uwezo wa kukusanya. 

Mradi wa SWIOFish unafadhiliwa na Benki ya Dunia kuhamasisha ulinzi na usimamizi wa rasilimali za bahari na ndio umeimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi wa rasilimali za bahari (BMU) kwa ajili ya kulinda na kuhamasisha uvunaji endelevu wa rasilimali za bahari katika Wilaya za Mkinga, Pangani, Bagamoyo, Lindi Vijijini na Tanga Jiji.

WAKUU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI WAASWA KUPAMBANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO

$
0
0


 Afisa Elimu Mkoa wa Pwani, Hadija Mcheka, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake  kuhusiana na maandalizi ya kufunguza shule za msingi na sekondari na kuwahimiza wakuu wote wa shule kuhakikisha wanazingatia usafi wa mazingira.(PICHA NA VICTOR MASANGU).

 

 

VICTOR MASANGU, PWANI

 

Afisa Elimu Mkoa wa Pwani, Hadija Mcheka, amewataka wakuu wote wa shule za msingi na sekondari kuhakikisha wanaweka vizuri  miundombinu  ya mazingira ya shule zao kuwa safi na salama ikiwemo uwepo wa vitakasa mikono ambavyo vitaweza kuwasaidia wanafunzi kunawa ili kuondokana na magonjwa ya mlipuko.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini Kwake kuhusiana na maandalizi ya kuelekea katika kufungua shule  Afisa elimu huyo alibainisha kwamba walimu wote kwa sasa wanatakiwa kuweka mikakati ambayo itaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi pindi wanapofungua shule zao waweze kusoma katika mazingira masafi.

“Kipindi cha likizo kwa sasa ndio kimemalizika kwa wanafunzi wetu wa shule mbali mbali za msingi na sekondari katika Mkoa wetu wa Pwani kwa hivyo mimi napenda kutumia fursa hii kwa ajili ya kuweza kuwakumbusha walimu wakuu wote wa shule husika kuweka mazingira ya ufasi katika maeneo yote ya shule ikiwemo kuwa na vitakasa mikono ili wanafunzi waweze kuepukana na magonjwa mbali mbali ya mlipuko,”alisema Hadija.

Pia aliongeza kuwa serikali ya awamu ya tano lengo lake kubwa ni kihakikisha kwamba wanafunzi wanasoma katika mazingira ambayo ni salama na rafiki hivyo kunahitajika kufanyike usafi wa mara kwa mara  katika maeneo mbali mbali ikiwemo kufyaka nyasi, kusafisha madarasa pamoja na kusafisha katika maeneo ya vyooni.

“Shule zetu zilikuwa zimefungwa lakini zinafunguliwa siku ya jumatatu, kwa hivyo natambua baadhi ya maeneo kutakuwa na uchafu hivyo ninawahimiza tena wakuu wote wa shule kulitilia mkazo suala hili kwani likifumbiwa macho linaweza kusababisha kutokea kwa mlipiko wa magonjwa mabi mbali ikiwemo kuumwa na matumbo pamoja ana kipindpindu,”alisema.

Kadhalika Afisa elimu huyo alisisitiza kuhusiana na usafi wa vyoo vya shule pamoja na vyoo vya walimu viwe katika hali ya usafi, na kwamba kwa kufanya hivyo kutaweza kusaidia kwa kiasi kukubwa kupunguza au kuamaliza kabisa changamoto ya magonjwa ya milipuko kwa wanafunzi pamoja na walimu na kuweza kusoma  katika hali nzuri.

Katika hatua nyingine aliongeza kuwa kuwepo kwa milipuko ya magonjwa mbali mbali kunatokana uchafu hivyo pia amewataka hata wamiliki wa shule binasfi kuliangalia hilo kwa jicho la tatu katika kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yote yanayozunguka shule pamoja na ndani ya madarasa ambayo wanasomea wanafunzi.

Pia alifafua kwamba changamoto nyingine ambayo inaweza kusababisha watoto kutokwenda shule ni kwa ajili ya kupata magonjwa mbali mbali ya milipuko hivyo ana imani kwamba mazingira ya mashuleni yakiwa masafi kwa asilimia kubwa pia kutasaidia katika kuwafanya wanafunzi waweze kusoma vizuri na kuongeza kiwango cha ufaulu.

Waziri Wang: China Inakaribisha Samaki kutoka Tanzania

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia utiaji Saini wa mkataba wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga km 341 kati ya Shirika la Reli Tanzania TRC kupitia Mkurugenzi wake Mkuu Masanja Kadogosa na
Ubia wa Kampuni mbili za Kichina, China Civil Engineering Construction Corporation CCECC na China Railway Construction Corporation Limited CRCC kupitia Mtendaji Mkuu wa CCECC Zhang Junle katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita leo tarehe 08 Januari 2021.

 

 

Na Immaculate Makilika- MAELEZO, Chato

 
Waziri wa Mambo ya Nje wa China,Wang Yi amesema kuwa
nchi yake inakaribisha samaki kutoka Tanzania kuuzwa moja
kwa moja nchini humo ili kusaidia sekta ya maendeleo ya
uvuvi nchini.


Akizungumza jana (Januari 8, 2021) wakati alipotembelea
Mwalo wa Chato beach uliopo katika Wilaya ya Chato mkoani
Geita, na kukutana na wavuvi Waziri huyo wa Mambo ya Nje
wa China alisema kuwa soko la samaki China ni kubwa na
hivyo anakaribisha samaki kutoka Tanzania kuuzwa nchini
kwake.


“Nimeambiwa wakati wa mvua Tanzania hali inakuwa ngumu
sana na soko la samaki huko China ni kubwa. Kwa hiyo
ningependa kutangaza kwamba China inakaribisha samaki
kutoka Tanzania na pia tungependa kuwasaidia kuongeza
mapato na kuboresha maisha yenu”.


Alisisitiza “Tunapenda kusaidia kuuza bei ya samaki watanzania
kupitia mkataba husika ili mazao kutoka Ziwa Victoria yaende
China kwa urahisi zaidi.”
Vilevile, Waziri Wang alisema kuwa Ubalozi wa China nchini
utatoa kiasi cha dola za Marekani 20,000 kwa ajili ya kusaidia
wavuvi wa mwalo wa Chato kununua vifaa vya uvuvi.
Aidha, alionesha kufurahishwa na zawadi ya samaki aliyopewa
na wavuvui wa mwalo huo .

“ Leo nyinyi mmenizawadia samaki wazuri na wakubwa sana,
nimefurahi sana na nashukuru sana, kitendo hili kinaonesha
hisia zenu na urafiki wa kweli.”
Kwa upande wake, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashamba
Ndaki alisema kuwa Tanzania imejaliwa rasilimali za uvuvi
katika maeneo mbalimbali ya maziwa, mito na bahari ambazo
zinachangia pato la taifa, ambapo asilimia 75 ya mazoa ya
uvuvi yanayozalishwa hapa nchini yanavunwa kutoka Ziwa
Victoria.


Waziri Ndaki alitaja mazao hayo matatu ya kibiashara kuwa ni
samaki aina ya sangara, sato na dagaa. “Mazao yatokanayo na samaki aina sangara yanayojumuisha minofu na mabondo ndio husafirishwa kwa wingi kwenda kwenye soko la kimataifa ikiwemo China, kwa kupitia Hong Kong. 

Ni lengo la serikali yetu kuuza zao hili moja kwa moja
nchini China.”alisema Waziri Ndaki Alifafanua kuwa matarajia ya Serikali ni kusaini mkataba utakaowezesha kuuza bidhaa hizo moja kwa moja katika soko la China.


“Tunaomba mheshimiwa Waziri Wang mara tutakapowasilisha
rasmi maombi ya soko la mabondo tuungwe mkono na Serikali
ya China. Tuna imani kwamba kufunguliwa kwa soko hilo
kutasaidia sana jitihada za wananchi kujikwamua na umasikini”
alisisitiza Waziri Ndaki.


Tanzania ina mialo 1,373 ikiwamo mwalo wa Chato licha ya
Serikali kufanya juhudi za kuendelea mialo hiyo hapa nchini
bado kuna fursa ya kuboresha miundombinu ya kupokea,
kuhifadhi na kuchakata mazao ya samaki.

Aidha, Waziri Ndaki aliiomba Serikali ya China kuhamasisha
makampuni binafasi kutoka nchini humo kuja kuwekeza katika
viwanda na miundombinu ya vuvuvi ili kuongeza uzalishaji
kupunguza upotevu wa rasilimali za uvuvi na kuongeza ubora na
usalama wa mazao ya uvuvi hapa nchini.


“Zaidi ya wananchi milioni 4.5 wanajishughulisha na shughuli
mbalimbali katika mialo, na sekta ya uvuvi inawapatia kipato na
lishe wananchi na kuchangia pato la taifa.”alisema Waziri Ndaki
Asilimia 85 ya mazao ya uvuvi yakiwamo yale yanayosafirishwa nje ya nchi yanatokana na wavuvi wadogo wadogo ambao hutumia vyombo vidogo vya kuanzia mita tatu hadi mita 10.


Naye, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wavuvi katika mwalo wa
Chato Beach, Kamese Kalima alisema mwalo huo umeanzishwa mwaka 1999 ukiwa na wavuvi 500 na mitumbwi 125, na kati ya hiyo mitumbwi 110 ni ya makasia na mitumbwi 15 ni ya injini.


Bw. Kalima aliiomba Serikali ya China kuwasaidia kutatua
changamoto za miundombinu zinazowakabili ambazo ni
vyombo vya uvuvi, jengo ambalo litajumuisha soko la uvuvi,
mitambo ya kuzalisha tani 5 za barafu, chumba cha ubaridi
chenye uwezo wa kuhifadhi tani 10 za samaki, na mashine ya
umeme yenye uwezo wa kukaushia tani 5 za dagaa kwa siku.


“Tunatambua China ni vinara wa viwanda vya samaki duniani,
hivyo tunaomba miundombinu ya uchakataji samaki na China
kuja kuwekeza viwanda vya kuchakata samaki angalau tani 35
kwa siku.” Alisema Bw. Kalima.

Mwalo wa Chato na Mkoa wa Geita kwa ujumla unazalisha
zaidi ya tani 23,844 za samaki kwa mwaka ambao husafirishwa
umbali mrefu kwenda viwanda vilivyopo Kagera na Mwanza
kwa ajili ya kuchakata samaki.

VIONGOZI TENDENI HAKI: MAALIM SEIF

$
0
0

 Makamu  wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amewata viongozi kutenda haki kwa Wazanzibar wote bila ya kujali tofouti zao.

 

Alisema  kama wananchi na viongozi wao watashirikiana itakuwa chachu ya kusukuma mbele gorudumu la Maedeleo miongoni mwa Wazanzibar.

 

Maalim Seif alisema hayo katika msikiti wa Jumuiya ya waarabu uliopo Rahaleo Unguja akiungana na waimini wa Dini ya Kiislam kuswali swala ya Ijumaa.

 

Aliwataka viongozi wote waliochaguliwa na wale wateule kupiga vita ubaguzi wa aina yoyote katika kuwahudumia wananchi.

 

“Tukifanyakazi kwa pamoja nakuhakikishieni maendeleo ni rahisi sana” alisema Malim Seif.

 

Sambamba na hilo amewataka waumini Dini ya Kiislam kuiombea Dua Zanzibar ili umoja uliopo udumu.

 

Akizugmzia kuhusu ajira uwepo wa utulivu ni muhimu kwa ushiriiana an sekta binafsi kuondoa changamoto ajira Viwani Zanzibar.

Kama tikuvutana tutachelewa kupata maedeeo lakini sisi Wazanzibar tumelijua hilo ndio maana tukawa na SUK.

 

Alieleza kuwa changamoto ya ajira ni kubwa ambayo huipata wahitimu wa vyuo vya elimu ya Juu mbali mbali Tanzania.

Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipaga kutatuwa Changamoto inayowakabili akina mama na Vijana ya ajira na kuwataka wananchi wote kushiriki kwa hali na mali katika shuhuli za Maendeleo hapa nchini.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AWAHIMIZA WAHITIMU CHUO CHA MIPANGO KUJIAJIRI

$
0
0



Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mwanaidi Ali Khamis (katikati) na  Mkuu wa Wilaya ya Magu, Bw. Salumu Kali, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) baada ya hafla ya uwekaji jiwe la Msingi la ujenzi wa miundombinu ya Chuo  Kituo cha Mafunzo  cha Kanda ya Ziwa Mwanza.

 

 

 Na Walace Ng'wandu na Farida Ramadhani, WFM, Mwanza


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mwanaidi Ali Khamis,  amewataka wahitimu wa Vyuo Vikuu nchini wakiwemo wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, kutumia vizuri ujuzi walioupata kuleta ufumbuzi wa changamoto za kimaendeleo zinazoikabili jamii pamoja na kutafuta ajira katika sekta isiyo rasmi ili kujiletea maendeleo.

 

Hayo ameyasema wakati wa Mahafali ya 34 ya Chuo cha Mipango ya  Maendeleo Vijijini yaliyo fanyika kwa mara ya 8 katika Kituo cha Kanda ya Ziwa - Mwanza kwa Wahitimu wa Shahada na Stashahada na Astashahada.

 

Mhe. Mwanaidi Khamis alisema kuwa hakuna shaka vyuo vinatoa elimu bora ambayo kama ikizingatiwa kikamilifu inatoa fursa ya kujiajiri na kuajiliwa, hivyo kuwa chachu ya maendeleo yatakayoleta tija katika nyanja mbalimbali.

 

“Serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kuweka mazingira mazuri ya kujiajiri hususani kwa kuboresha mazingira ya kufanya biashara na hivyo kuongeza fursa za vijana wasomi kujiajiri na hatimaye kupunguza tatizo la ajira”, alieleza Bi. Mwanaidi Khamis.

 

Alisema kuwa baadhi ya hatua zilizokwisha kuchukuliwa na Serikali ni pamoja na kutenga fedha kwa ajili ya utoaji mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa, kupunguza riba ya mikopo ya mabenki pamoja na kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda ili kuongeza ajira na kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao yanayozalishwa nchini.

 

Naibu Waziri huyo amewaasa vijana wasomi nchini kufanya kazi kwa bidii na kwa weledi na kuzitumia fursa  mbalimbali zilizopo hususani katika sekta binafsi kujipatia kipato na kuwa na mchango kwa taifa.

 

Aidha amekitaka Chuo cha Maendeleo Vijijini kuyafanyia kazi maelekezo ya Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango, Mh. Dkt. Phillip Isdor Mpango aliyoyatoa Jijini Dodoma tarehe 22 Desemba, 2020 alipokutana na Watendaji Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma ambapo alizielekeza Taasisi za Elimu ya Juu kutumia vyema fursa zilizopo katika kuongeza mapato ya taasisi husika hususani kwa kuimarisha vitengo vya Ushauri na Utafiti ili viweze kuchangia angalau asilimia 10 ili kupunguza utegemezi katika Serikali Kuu.

 

 Alisema kuwa Chuo Cha Mipango kinatakiwa kuwa mfano kwa Taasisi nyingine za Elimu ya Juu ikizingatiwa kuwa kipo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango.  

 

Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), Prof. Martha Qorro, alisema kuwa jukumu la taasisi za elimu ya juu hususani Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijini ni kuendelea kuchapa kazi kwa bidii, maarifa na weledi wa hali ya juu ilikutoa huduma zinazo tatua changamoto za maendeleo katika jamii.

 

Alisema kuwa Chuo cha Mipango Tumewezesha kuendelea kutoa mchango kwa jamii kwa kuendesha na kutekeleza miradi ya maendeleo yenye kuwakwamua wananchi wengi kiuchumi hususani katika eneo la mifugo, uvuvi na kilimo.

 

Pia alimuahidi Naibu Waziri Mhe. Mwanaidi Khamis kuwa Chuo kinaendelea kupata hati safi ya ukaguzi ambayo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na Serikali kuanzisha mifumo mbalimbali ya udhibiti, utunzaji, na usimamaizi mapato na matumizi ya fedha za umma.

 

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa -Mwanza Prof. Juvenal Nkonoki, alisema kuwa idadi ya watunukiwa wa tuzo mbalimbali katika mahafali ya 34 yaliyofanyika kwa mara ya nane katika Kituo cha Mafunzo Kanda ya Ziwa Mkoani Mwanza ni 2571 wakiwemo wanaume 1009 na wanawake 1562.

 


TASAF YABORESHA MAISHA YA WANANCHI KIJIJI CHA BWITI

$
0
0

Na James Mwanamyoto-Mkinga

  

Wananchi wanaoishi katika kaya maskini Kijiji cha Bwiti, wilayani Mkinga wanaonufaika na ruzuku inayotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wamewezeshwa kuboresha makazi yao, kufanya shughuli za ufugaji, ujasiliamali, kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii, kujishughulisha na kilimo ikiwa ni pamoja na kumudu
gharama za mahitaji ya shule kwa watoto wao.


Wananchi hao wametoa shuhuda za mafanikio waliyoyapata kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi, wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma mkoani Tanga.


Mmoja wa wanufaika Bi. Fatuma Mohamed Hamza amemueleza Mhe. Ndejembi kuwa, ruzuku aliyoipata kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini imemuwezesha kununua bati 40 alizoziezeka katika nyumba yake na hatimaye kuondokana na adha ya kunyeshewa na mvua aliyokuwa akikabiliana nayo kwa kipindi kirefu.


Naye, mjane Bi. Mwajuma Ayubu Bakari amesema, baada ya kupokea ruzuku yake kwa vipindi vitatu mfululizo aliwekeza kidogo kidogo na hatimaye kuweza nununua mbuzi ambapo mpaka hivi sasa amefanikiwa kuwa na mbuzi wapatao 14 na kuongeza kuwa, ruzuku pia inamuwezesha kugharamia mahitaji ya watoto shuleni.


Mnufaika mwingine, Bi. Mwajuma Said Kidevu amemthibitishia Mhe. Ndejembi kuwa, kabla ya kupokea ruzuku alikuwa na mbuzi 6 lakini baada ya kuanza kupokea ruzuku ameweza kuongeza idadi ya mbuzi anaowafuga hadi kufikia 12.


Akizungumzia mafanikio aliyoyapata, Bi. Mwansaada Radoda Ramadhani amemueleza Mhe. Ndejembi kuwa, kupitia ruzuku anayoipata ameweza kujenga nyumba bora yenye choo bora, anajishughulisha na kilimo cha mazao ya chakula na ameweka umeme nyumbani kwake, hivyo anaishukuru Serikali kwa kuanzisha Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao kwa kiasi kikubwa umeboresha maisha yake.

Kwa upande wake, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi mara baada ya kupokea shuhuda hizo, amewataka walengwa wote wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini kutumia vema ruzuku wanazozipata kujikwamua katika umaskini ili kutimiza lengo la Serikali kuwa na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

Ndejembi amesisitiza kuwa, matumizi mazuri ya ruzuku ni sehemu ya kuunga mkono azma ya Mhe. Rais ya kuuendeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ili kuboresha maisha ya wanyonge nchini.
 

Sanjali na hilo, Mhe. Ndejembi amewataka waratibu wa TASAF nchini kuhakikisha wanatoa elimu ya namna bora ya kutumia ruzuku wanazopatiwa walengwa wa TASAF na kufanya ufuatiliaji wa karibu ili kuhakikisha ruzuku wanazopatiwa zinatumika kuboresha maisha yao na kuweza kuhitimu kwa lengo la kutoa fursa kwa kaya nyingine kunufaika na
ruzuku inayotolewa na TASAF.

Dk.Jingu : Wasajili wa NG'Os fanyeni kazi kwa maslahi ya nchi

$
0
0

KATIBU  Mkuu Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dk. John Jingu, akifafanua jambo.

Na Asha Mwakyonde


KATIBU  Mkuu Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dk. John Jingu, amewataka Wasajili wa Wasaidizi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO'S), kufanya kazi kwa uadilifu, uwajibikaji kwa kuzingatia maslahi ya Taifa.

Dk. Jingu ameyasema hayo leo kupitia UFM wakati akizungumza mafunzo ya Wasajili Wasaidizi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO'S), ambayo yameanza juzi  kwa ngazi ya mikoa na Halmashauri yanayotarajiwa kufanyika nzima.

Dk. Jingu amesema mafunzo hayo yana lengo kubwa la kuwafanya wasajili hao  wayajue majukumu yao.

Amesema kilichowasukuma kufanya mafunzo hayo ni kwamba maofisa hao wengi ni wapya ambao wamepewa majukumu siku za hivi karibuni.

KATIBU huyo ameongeza kuwa kwa utaratibu wa kawaida maofisa hao wakishakabudhiwa majukumu yao  lazima waeleweshwe, wapewe ufahamu  wa nini wanatakiwa kufanya na mipaka ya majukumu yao.

"Kiufupi wanatarajiwa wao Kama maofisa wa Serikali waliopewa jukumu la kuratibu shughuli za mashirika hayo katika maeneo yao mikoani,kwenye  Halmashauri, Wilaya wanatakiwa wafanye kazi zao kwa uadilifu, uwajibikaji kazi , kujitoa  kwa kuzingatia maslahi ya Taifa," amesema Dk. Jingu.

Amesema maofisa hao wameteuliwa hivi karibuni lakini wanafanya kazi vizuri, wanaelewa sheria inataka nini, kanuni ya GN ya 687  inaeleza vizuri majukumu yao.

Dk. Jingu ameeleza kuwa mafunzo hayo wamezungumza mambo mengi likiwamo la kusimamia sheria.

Amesema sheria inalazimisha Mashirika hayo kufanya kazi kulingana na katiba ambazo wamesajili nazo.
Mwisho

SIMAMIENI MAADILI NA WELEDI - DKT. GWAJIMA

$
0
0

Waziri wa Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima akiongea na Viongozi wa Vyama,Bodi na Mabaraza ya kitaaluma vilivyopo chini ya sekta ya afya nchini.

Naibu Waziri wa Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel akizungumza wakati wa kikao kazi na mabaraza, bodi na vyama vya  kitaaluma kwenye ukumbi wa hospitali ya Benjamin Mkapa.
Washiriki wa kikao kazi hicho kwenye ukumbi wa hospitali ya Benjamin Mkapa
 


Na Catherine Sungura, WAMJW-Dodoma


Vyama, Mabaraza pamoja na bodi za kitaaluma nchini  vimetakiwa kudhibiti maadili na weledi katika utendaji kwa  watumishi wa sekta ya afya nchini ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima wakati wa kikao na viongozi hao kwenye ukumbi wa hospitali ya Benjamin Mkapa jijiji Dodoma.

Dkt.Gwajima amesema kuwa vyama, bodi na mabaraza ya kitaaluma ndio wasimamizi wakuu na wadhibiti wa maadili na weledi ambapo wananchi bado wanakutana na changamoto nyingi za maadili na weledi wakati wa upataji  huduma za afya.

"Kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya uchaguzi  kurasa 137 imeandikwa kushirikiana na vyama vya kitaaluma vya kada ya afya katika kusimamia uzingatiaji wa maadili na weledi katika utendaji wa watumishi hilo ndio tunalotekeleza. "Amesisitiza Dkt. Gwajima.

Amesema wanapofanya ziara kwenye mikoa mbalimbali wanakutana na kero zitokanazo na kufifia kwa maadili na weledi wa utendaji, huku akiweka  wazi kuwa, haya yote yanadhibitiwa na vyama, bodi na mabaraza ya kitaaluma.

"Ili tuweze kuhuisha hayo yote, lazima tukae pamoja na kuangalia mifumo yao ya utendaji kazi ukoje hadi unatoa mianya ya baadhi ya wanataaluma kukosa maadili na kuleta malalamiko mengi kutoka kwa wananchi?,Aliuliza Dkt. Gwajima

Aidha, Dkt. Gwajima amesema kutokana na malalamiko hayo inafanya kuonekana kukosa meno ya vyama hivyo vya kitaaluma, hivyo kikao hicho kikubwa ni kuambina ukweli na kuwakumbusha majukumu yao na wafahamu kuna tatizo kwa wanataaluma wao ndio mana hawashtuki na hata wengine kuvunja maadili bila kujali kama kuna mabaraza ya kitaaluma na kubadilika ili kuondoa kero kwa wananchi.

Kwa upande wa kuwa na mwamvuli mmoja wa mabaraza yote ni kwamba itasaidia kuwa na timu moja na matumizi ya fedha ya kuendesha mabaraza yote yatapungua na kuongeza ufanisi na tija ya wataalam wengine ili wakae kwenye maadili.

Naye Naibu Waziri Dkt. Godwin Mollel amewataka viongozi hao kuwajibika ili kuondoa matatizo ambayo ama wao kama mabaraza hawayaoni au yanaonwa na viongozi wa wilaya eneo husika.

Dkt. Mollel aliendelea  kusema kuwa, wataalamu wengi hivi sasa hawafanyi kazi kwa kuzingatia maadili na hivyo kusababisha makosa mengi ya kitaaluma yanafanyika kwenye vituo vya  kutolea huduma na wananchi wengi kupoteza maisha na wengine kupata athari kwenye jamii.

"Tunakuta makosa kwenye taaluma mfano dawa zinaibiwa lakini  wewe mwenye baraza lako na unasimamia maadili hulioni hili hivi hujioni kwamba na wewe unatakiwa kuadhibiwa? Aliuliza Dkt.Mollel

Hatahivyo amewataka viongozi hao kujitafakari kama wanatosha kwenye mabaraza yao kama wanashindwa wao kugundua matatizo yaliyopo chini kwani wanakuwa wameshindwa kusimamia na kufanya kazi zao vizuri kwa kutoa adhabu kwa wanaofanya makosa na kusababisha matatizo kwa wananchi.

ATCL YAZINDUA SAFARI ZA NDEGE KUTOKA DAR ES SALAAM HADI GEITA

$
0
0


Ndege ya Shirika la Ndege la ATCL aina ya Bombardier Q-400 likiwasili katika uwanja wa Ndege wa Geita, Chato leo tarehe 09 Januari 2020 ikiwa ni uzinduzi wa safari yake ya kwanza mkoani Geita.

Ndege ya Shirika la Ndege la ATCL aina ya Bombardier Q-400 likiwasili katika uwanja wa Ndege wa Geita, Chato leo tarehe 09 Januari 2020 na kupewa heshima yakumwagiwa maji Water Salute mara baada ya kuwasili wakati ikitokea jijini Dar es Salaam.
Abiria wakishuka katika ndege hiyo ya ATCL aina ya Bombardier Q-400 mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Geita.
 
Ndege ya Shirika la Ndege la ATCL aina ya Bombardier Q-400 ikiondoka katika uwanja wa Ndege wa Geita, Chato kuelekea Mwanza mara baada ya uzinduzi wa Safari yake ya kwanza ya kutoka jijini Dar es Salaam.

Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo wachangia damu

$
0
0

 Na Talib Ussi, Zanzibar

 

Wananchi wa Zanzibar wameshauriwa kujitokeza kwa wingi katika kuchangia Damu ili kuokoa maisha ya watu.

 

Ushauri huo umetolewa na Katibu Mkuu Ngome ya Wanawake Chama cha ACT Wazalendo, Janet Fussi wakati alipoungana na viongozi Pamoja na wanachama wa Ngome hiyo kuchangia damu katika kituo cha Damu Salama kiliopo kwa wazee Sebleni Zanzibar ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 

Alisema hivi sasa mahitaji ya damu ni makubwa katika hospital za Zanzibar hivyo ni vyema wananchi wakajitokeza kuchangia damu ili iwe sababu ya kuhami maisha ya wenzao ambao wanahitaji damu.

 

Alisema hakuna ambaye atawaletea damu kama wazanzibar wenyewe hawajachangia Damu.

 

Aliwaomba wale wote ambao wanaafya njema hasa Vijana kujenga utamaduni wa kuchangia damu mara kwa mara  ili hospitali za zanzibar  ziwe na damu ya kutosha.

 

Aliwataka watu kuacha kuwa na ghofu katika kufanya jambo alililoita jema hasa kiimani kwa kile alichosema kuwa unapookowa maisha ya mtuu na kwa mwenyezi unapata fungu kubwa.

 

Alisema wahitaji wakubwa wa damu ni wanawake na Watoto kwa hiyo  kila mmoja anawajibu wa kuhakikisha maisha yao yanakuwa salama kwa kujitolea kuchangia damu.

 

Kwa upande wake Daktari Mkuu wa kituo cha Damu Salama Bakar Hamad Magarawa alisema kipindi hiki kuna mapungufu makubwa ya damu na kuwaomba wananchi wengine waige Ngome ya Wanawake wa ACT wazalendo ili kuondoa upungufu huo.

 

Alisema  asilimia 70 ya wahitaji wa damu ni wanawake wajawazito Pamoja na wale wenye ugonjwa wa matumbo na kueleza kuwa watu wakijitokeza kuchangia damu basi inaweza kuwahami akina  mama na wahitaji wengine.

 

“Natoa wito kwa wazanzibar wote tujitokeze kwa wingi kuchangia damu kwani Chupa moja ya Damu ni sawa na kuokowa maisha ya watu watatu” alisema Magarawa.

 

Alisema kituo hicho hakiwezi kuwa na damu kama wananchi hawajahamasika kuchangia damu.

 

“Changia Damu kwa kuokoa maisha ya watu” alisema Magarawa.

 

Attiye Ali Salim mwenyekiti wa Ngome hiyo mkoa wa Mjini Kichama alisema anajisikia furaha kuwa miongoni mwa wale waliochangia damu kwa ajili ya ustawi afya wa Zanzibar wanahitaji damu.

Alisema unapochangia damu hata mwenyewe anaweza kuja kuitumia mara akipata maradhi ya kuongezewa damu.

 

“Tusione kama tunachangia watu tuu hata sisi wenyewe inaweza ikatumika” alisema Attiye.

Rais Abdallah Mussa mwenyekiti wa Ngeme hiyo Wilaya ya Magharibi A alisema nchi yoyote haiwezi kuwa na maendeleo kama wananchi wake hawana afya njema kwa hiyo kuchangia damu sehemu kuchochea maendelea ya nchi.

 

“Na sisi kama wanachama wa ACT Wazalendo tunawajibu wa kuisaidia Serikali yetu ka juhudi za kufikia maendeleo kwa kusaidi kutoa damu kwa ajili kustawisha afya za wengine” alisema Bi Raisa.

 

Alisema havi sasa Viongozi wakuu wa Serikali wako kitu kimoja katika kuhakikisha maendeleo ya Zanzibar yanakuwa kwa haraka hakuna na wananchi wake kuwa kitu kimoja kwa kusaidia shida mbali mbali ikiwe Damu.

 

Sambamba na hilo Bi Raisa aliiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwajenga wananchi wao kuwa na moyo wa kujitolea kwa kila jambo hasa hilo la kuokowa maisha ya watu.

 

Viongozi hao Ngome ya Wanawake Miko ana Taifa wameshiriki tukio la kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 57 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.

WAZAZI LUDEWA WAOMBA SOMO LA HISABATI KUINGIZWA KWENYE MRADI WA JIFUNZE

$
0
0
Mzazi Alpha Samuel Melele mkazi wa Kijiji cha Shaurimoyo akizungumza na mwandishi wa habarihizi hivi karibuni wilayani Ludewa.


Baadhi ya Wazazi ambao watoto wao wamenufaika na programu ya Jifunze wakiwa na mmoja wa walimu wa darasa la Jifunze Shule ya Msingi Shaurimoyo, Castory Muagama (wa kwanza kulia) mara baada ya mahojiano kuzungumzia programu ya jifunze.

Na Joachim Mushi, Ludewa

BAADHI ya wazazi ambao awali watoto wao walikuwa na changamoto ya kujua kusoma na kuandika na hatimaye kuingizwa kwenye mradi wa jifunze kutatua changamoto hiyo, wameiomba taasisi ya Twaweza kuingiza somo la hisabati katika mradi huo ili kutatua changamoto ya ujifunzaji wa somo hilo kwa baadhi ya watoto.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni, Wilayani Ludewa katika mahojiano na baadhi ya wazazi hao kwa nyakati tofauti kuzungumzia changamoto za watoto wao katika ujifunzaji na mafanikio na mradi wa Darasa la Jifunze uliokuwa ukitekelezwa baadhi ya shule kusaidia watoto wasiojua kusoma kuanzia darasa la tatu hadi la sita. 

Mzazi Alpha Samuel Melele mkazi wa Kijiji cha Shaurimoyo akizungumza aliiomba taasisi ya uwezo kwa kushirikiana na wadau wa elimu kukubaliana kuliingiza somo la hisabati katika mradi wao wa darasa la Jifunze ili kusaidia kutatua changamoto inayowakabili baadhi ya watoto kwenye somo hilo.

"...Mwanangu yupo darasa la tatu Shule ya Msingi Shaurimoyo ni miongoni mwa wanafunzi walionufaika na darasa la Jifunze, awali alikua hajui kusoma na kuandika lakini baada ya kuhudhuria darasa hilo amebadilika hadi nashangaa...anajua kusoma na kuandika tena kwa kujiamini tofauti na mwanzo. Hata hivyo kwenye hesabu bado hayupo vizuri sana ndio maana naomba somo hili pia liingizwe katika darasa la Jifunze," alisema Bw. Samuel Melele.

Naye mzazi Fausta Mtitu amepongeza ujio wa programu ya darasa la Jifunze kwenye Kata ya Lugarawa kwani imesaidia watoto waliokuwa na changamoto ya kusoma eneo hilo na kuomba somo la hisabati kujumuishwa katika programu hiyo ili kuwasaidia watoto wao. 

"Somo la hesabu bado ni tatizo sana kwa watoto wetu, mimi mwanangu licha ya sasa kumudu kusoma na kuandika lakini bado hesabu zinamtatiza ndio maana tunahoji kwanini mradi huu pia usijumuishe hili somo kuwasaidia watoto wetu," alihojia Bi. Fausta Mtitu katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi.

Aidha aliongeza kuwa wamejaribu kuhoji kwa walimu wanaofundisha mradi wa Jifunze kwanini wasiingize somo hilo lakini wamejibiwa halimo katika programu hiyo, hivyo kuamua kuomba kwa asasi husika ili iangalie namna ya kujumuisha somo hilo la hesabu kwani bado linawatatiza wanafunzi hata wale ambao tayari wamenufaika na mpango wa Jifunze.


Baadhi ya wanafunzi wa darasa la jifunze waliofanya vizuri kwenye kipindi wakiwa wamevishwa kofia kupongezwa na walimu wao, ikiwa ni moja ya mbinu zinazotumika kuwavutia wengine kufanya vizuri darasani.

Kwa upande wake, Bi. Agnes Daniel Mtweve mwalimu wa darasa la Jifunze ameunga mkono maombi ya baadhi ya wazazi hao na kuongeza kuwa wapo tayari kuwasaidia wanafunzi hao hata kwenye somo la hisabati kama wataongezewa ujuzi na watekelezaji wa programu hiyo kama walivyoomba wazazi hao. 

"Ukiangalia kuna mafanikio makubwa katika muda mfupi wa kutekeleza mradi huu, watoto wengi wameweza kusoma vizuri na kuandika hivyo naamini hata kwenye somo la hisabati likiingizwa kutakuwa na mafanikio hivyo kujikuta tunawasaidia pia watoto hawa," alisema mwalimu huyo akizungumza na mwandishi wa habari hizi.

Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Njombe kwa kushirikiana na taasisi ya Uwezo Tanzania ni miongoni mwa wilaya zinazotekeleza mradi wa Darasa Jifunze kimajaribio kwa baadhi ya kata kusaidia wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika kwa darasa la tatu hadi la Sita, ikiwa ni kutatua changamoto ya ujifunzaji kwa wanafunzi walio na changamoto hiyo. Imekuwa ikiwatumia walimu waliopata mafunzo kufundisha kwa muda wa ziada kuwasaidia wanafunzi wenye changamoto hiyo, ukitekelezwa kwa siku 30, kabla ya kufanya tathmini kila baada ya siku 10.


SERIKALI YATOA ONYO KWA MSIMAMIZI WA UJENZI WA SOKO LA KIMKAKATI MWANZA KWA KUCHELEWESHA KAZI

$
0
0

Mwanza, Tanzania

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Mwanaidi Ali Khamis, amemwagiza Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa Soko la Kisasa la Mjini Kati Jijini Mwanza  kuwepo eneo la ujenzi muda wote ili mradi huo ukamilike kwa wakati.


Mheshimiwa Mwanaidi Ali Khamis, ametoa maagizo hayo alipotembelea na kukagua ujenzi wa Soko hilo pamoja na Kituo cha Mabasi cha Kisasa cha Nyegezi kilichoko Wilaya ya Nyamagana jijini humo.


“Nimepata taarifa kwamba msimamizi mmoja anasimamia miradi yote miwili jambo ambalo halikubaliki na linasababisha miradi hii kuchelewa na kuna hatari itatekelezwa chini ya kiwango kutokana na kukosa usimamizi makini” Alisema Mhe. Mwanaidi


Alisema kuwa nilazima msimamizi huyo awepo eneo la ujenzi saa 24 kuangalia ufanisi wa kazi ili kupata majengo na miundombinu imara itakayosadifu juhudi za Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, za kujenga miundombinu bora itakayochochea maendeleo ya wananchi kwa ujumla.


“Kama msimamizi hakai eneo la ujenzi basi aondolewe awaachie wengine ambao wanaweza kufanya kazi hiyo, iwapo msimamizi hayupo ni vema Serikali ikajulishwa ili iweze kuchukua hatua stahiki bila kuchelewesha miradi”, alieleza Mhe. Mwanaidi Ali Khamis.


Aidha Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, ametoa siku mbili kwa uongozi wa Wilaya ya Nyamagana kuhakikisha changamoto ya uhaba wa saruji katika miradi hiyo miwili ya kimkakati inayopewa fedha na Hazina ili kuziwezesha halmashauri kujitegemea kimapato, inatatuliwa haraka.


Awali Mkandarasi kutoka Kampuni ya Mohamemedi Builderrs anayejenga miradi hiyo, Mhandisi Taher Jafferji, alilalamikia changamoto ya upatikanaji wa Saruji licha ya kulipa fedha nyingi kwenye viwanda vya Saruji, jambo ambalo linapunguza kasi ya ujenzi.


Alisema kuwa, amepewa mkataba wa ujenzi wa miezi 18 ambapo anatarajiwa kukamilisha ujenzi wa Soko hilo Aprili, 2022, hivyo ni vema Serikali ikalitafutia ufumbuzi suala hilo kwa kuwa yeye anamorali wa kazi na ni mzalendo wa kweli.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Dkt. Phillis Nyimbi, amesema kuwa uongozi wa Wilaya hiyo utahakikisha maagizo yote yaliyotolewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango yatatekelezwa kikamilifu, kwa kuwa lengo lao ni miradi hiyo ikamilike kwa wakati na kuchangia maendeleo ya Jiji na Mwanza na kutatua changamoto ya ajira kwa wananchi.


Naye Mkurugenzi wa Wilaya ya Nyamagana Bw. Kiomoni Kibamba alisema kuwa  mradi wa ujenzi wa Soko la kisasa la Mjini Kati utagharimu shilingi bilioni 20.7 wakati Ujenzi wa Kituo cha Mabasi cha cha Nyegezi kitagharimu shilingi bilioni 15.8 ambapo ujenzi wa soko umefikia asilimia 8 na ujenzi wa Kituo cha mabasi umefikia asilimia 10 ambapo Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imetoa kiasi cha shilingi bilioni 7.13.




BASHUNGWA AAHIDI KUPIGANI HAKI ZA WAANDISHI, ASISITIZA UZALENDO

$
0
0

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa.

 

NA SULEIMAN MSUYA


WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amesema atatumia nafasi yake kutetea haki za waandishi wa habari nchini huku akisisitiza uzalendo na utaifa kwa kada hiyo.

Kauli ya Waziri Bashungwa inakuja baada ya kuwasikiliza waandishi walioshiriki mjadala wa pamoja kuhusu changamoto wanazopitia katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Wakiwasilisha maelezo yao waandishi walimueleza Waziri Bashungwa kuwa pamoja na wao kuwa na sifa za kitaaluma  asilimia 80 ya wamiliki wa vyombo vya habari  wahatoi mikataba ya ajira, wenye mikataba utekelezaji wake ni wakusuasua, sheria za kazi hazizingatiwi.

Aidha waandishi walimueleza waziri kuwa waandishi wengi wanafanya kazi kama vibarua kwa muda mrefu huku wakidhibitiwa kama waajiriwa.

Akijibu hoja hizo za waandishi Waziri Bashungwa amesema uamuzi wa kukutana na waandishi ni kutoa fursa kueleza hali halisi ili ajue anaanzia  wapi.

Amesema sekta ya habari ni muhimu kwa maendeleo ya nchi hivyo ni jambo la aibu na kusikitisha iwapo kuna haki zinakiukwa bila hatua kuchukuliwa.

"Nimewaita hapa ili tuelezane hali halisi mnayopitia ili sisi kama wizara tuweze kuchukua hatua stahiki," amesema.

Bashungwa amesema haingii akilini watu wanafanya kazi hatarishi na wamesomea ila hawana mikataba hivyo kuahidi kushirikiana Ofisi ya Waziri Mkuu Ajira na wadau wengine ili muafaka uweze kupatikana kwa haraka.

Waziri huyo amesema wizara ina jukumu la kutatua changamoto wanazopitia waandishi kwa kuzungumza nao ili kuwa kitu kimoja kwani ni wadau muhimu kwa nchi na wananchi.

 Aidha, amewataka wamiliki wa vyombo vya habari kuzingatia sheria ya kazi inavyotaka katika kutekeleza mikataba ya wafanyakazi na kwamba hawatosita kuchukua hatua za kisheria kwa mwajiri anayekiuka taratibu.

Halikadhalika Waziri Bashungwa amemtaka Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuhakikisha baraza la habari na bodi ya habari vinaundwa ili waandishi waweze kupata eneo la kufikisha matatizo yao.

Pamoja na kuahidi kutetea haki za waandishi Waziri Bashungwa amewataka waandishi wajiendeleze kielimu ili kukidhi hitaji la Sheria ya Habari namba 12 ya mwaka 2016 inayotaka sifa ya mwandishi wa habari awe na elimu ya diploma.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Abdallah Ulega amesisitiza uzalendo na utaifa kwa waandishi wa habari.

Ulega amesema waandishi wanapaswa kuandika mazuri ambayo yanafanyika hapa nchini ili yaweze kujulikana na kuvutia wawekezaji ikiwemo sekta ya wanayoisimamia.

"Nyie ni watu muhimu sana katika kusukuma gurudumu la maendeleo naomba mtumie kalamu zenu kuyalezea mazuri yanayofanywa na Serikali  inayoongozwa na Rais John Magufuli.

Lakini kwa umaalum zaidi sekta hii tunaomba muitangaze sana kwani ina kundi kubwa ambalo linahitaji mchango wenu kwa mfano Januari 12, 2021 tunacheza na DRC Congo tunaomba mtangaze nachambua mchezo huo," amesema Naibu Waziri Ulega.

NHIF SINGIDA MBIONI KUNUFAISHA WAKULIMA 300 KUPITIA ‘USHIRIKA AFYA

$
0
0


Meneja wa NHIF  Mkoa wa Singida,, Dk. Mohamedi Kilolile.


Na Dotto Mwaibale, Singida


MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kupitia fao lake mahsusi kwa wakulima wa Pamba linalojulikana kama ‘Ushirika Afya’ unatarajia kuanza kutoa huduma ya matibabu kwa wakulima takribani 300 wa zao hilo kwa gharama ya shilingi mia mbili (200) kwa siku ambazo ni sawa na 76,800 kwa mwaka.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa (NHIF) mkoani hapa, Dk. Mohamedi Kilolile, alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, hivi karibuni.

“Niwaombe wakulima wa pamba wachangamkie fursa hii kwa kujiandikisha ili kupata huduma ya fao hili la ‘ushirika afya’ sababu maradhi hayapigi hodi. Sifa za kupata huduma hii ni sharti kwanza uwe mkulima wa pamba na pili uwe mwanachama wa amcos,” alisema Kilolile. 

Alisema gharama ya fao hilo kwa mkulima mmoja ni shilingi 76,800 kwa mwaka huduma ambayo imetajwa kuwa na gharama nafuu zaidi ambayo kwa mgawanyo wa malipo ya gharama husika kwa mwaka ni sawa na mkulima kulipia shilingi 200 tu kwa siku.

Kilolile alieleza kuwa kwa sasa huduma hiyo imekwishaanza kutolewa kwa maeneo mengine, ambapo NHIF kwa kushirikiana na Benki ya Posta nchini (TPB) vimeungana ili kurahisisha utoaji wa fao hilo kwa utaratibu wa benki husika kumuazima huduma husika mkulima na kisha kurejesha malipo ya huduma hiyo baada ya kuuza mazao yake.

“Mpaka sasa mkoa wa Singida tumekwisha tembelea Amcos 31 na kufanikiwa kuandikisha wanachama wake 300 wanaojishughulisha na kilimo cha zao la pamba na zoezi bado linaendelea kabla ya mfuko kwa kushirikiana na TPB kuanza kuwanufaisha na fao hili,” alisema.

Aidha, akizungumzia huduma nyingine zinazoendelea kutolewa mpaka sasa kwa watanzania wote na zilizofanyiwa maboresho, Kilolile alisema mpaka sasa mfuko huo unatoa huduma ya vifurushi vya aina 3 vinavyoendana na ngazi ya uchumi wa kila mteja kuweza kumudu gharama yake kwa ubora stahiki.

Alivitaja vifurushi hivyo kuwa ni kile cha ‘Najali’ ambacho gharama yake kwa mtu mmoja ni shilingi 192,000 kwa mwaka, pia kifurushi kingine ni ‘Wekeza’ ambacho gharama yake kwa mtu mmoja ni shilingi 384,000 kwa mwaka na ‘Timiza’ ambacho huduma yake kwa mwaka kwa mtu mmoja  ni shilingi 516,000.

Pia alisema huduma ya vifurushi vyote hivyo hutolewa kwa mgawanyo wa makundi rika kwa kati ya umri wa miaka 18-35, 36-59 na zaidi ya 60. Aidha, fursa nyingine ya vifurushi hivyo mathalani ‘Najali’ pamoja na kugharamia huduma ya Bima ya Afya kwa mwaka mzima pia hutoa fursa ya mgonjwa kupatiwa huduma ya kulazwa wodini kwa siku 30, huku ‘Wekeza’ ikitoa siku 45 na ‘Timiza’ kikitoa siku 60 kwa huduma hiyo ndani ya mwaka. 

“Chaguo ni lako. Niwasihi wana-singida na watanzania kwa jumla changamkieni huduma hizi kwa ustawi wa afya katika muktadha wa ujenzi imara wa taifa letu. Ugonjwa huwa haumuandai mtu…unaweza kuazima nauli ya kwenda mahali fulani na ukapewa lakini huwezi kuazima fedha ya kwenda kwenye matibabu kwa sababu hujui matibabu hayo yatagharimu kiasi gani cha fedha,” alisema Kilolile. 

Maalim Seif afungua kituo cha kukeshea na kumkafini maiti

$
0
0

 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amewataka Mashekhe nchini kuwashirikisha na kuwafundisha vijana katika masuala ya kumuaandaa maiti hadi kuzikwa kwake ili kuendeleza utaratibu huo katika jamii.

 

Alisema kuwa wakifundishwa vijana utamaduni huo wa dini ya  Kislamu utasaidia sana kwani wazee wakiwa hawapo vijana wanaweza kufanyakazi hiyo.

 

Maalim Seif aliyaeleza hayo jana huko Masjid Barza Mji mkongwe wakati akifungua kituo cha kukoshea na kumkafini Maiti kilichojengwa na msaada ya wazanzibar wanaoishi nje ya chini kupitia Jumuiya yao ya Tears Joy.

 

“Hivi ssa kila mkosha maiti utamuona ni mtu mzima vijana wakiwa pembeni sasa hili tuliondosheni” alisema Maalim Seif.

 

Aliwasihi Mashekhe hao kuelekeza juhudi zao yingi kwa vijana kwa sababu watu wanakufa kila siku.

 

Madrasa zetu zina mchango mkubwa katika malezi na makuzi kwa maisha ya vijana hapa  dunia na akhera”.

 

Makamu wa kwanza alieleza kuwa kwa sababu waalimu wa Madrasa hutumia nguvu na nafasi kubwa katika kuwafundisha vijana na Serikali kwa nafasi yake inaandaa mpango nzuri dhidi ya waalimu hao.

 

“Hatuwezi kufanikiwa katika dunia hii kama elimu ya dini tutaipa mgongoo” alisema

 

Aliwafahamisha Mashekhe hao kuwa wengine wawalee ili waweze kuvaa viatu vyao vya uongozi.

 

Sambamba na hilo Maalim Seif aliwashukuru sana wazanzibar  hao kwa mchango huo na kwaeleza kuwa wamefanya jukumu lao la kuondoa shida kwa jamaa zao.

 

“Kituo hichi walichokijenga kitaisaidia sana kwa watu wa mji mkongwe na kwa yeyote yule anayetaka kutayarishiwa maiti wake, kwani hii si kwa watu mji mkongwe ni kwa waislamu woote” alieleza.

Alisema fikra ambayo ilizaliwa na Tears Of Joy ni nzuri na kuwataka mitaa mengine kuiga jambo hilo hasa mjini kuondoa kikwazo cha kumkosha maiti.

 

Mapema akizungumza mwakilishi wa Jumuiya hiyo ya wazanzibar wanaoishi nje Suleiman Ahmed Sadikk alisema jumuiya yao iiaza na watu kumi katika nchi Uingereza lakini iko dunia nzima na iliaza mwaka 2019.

 

Alisema lengo kuu la kuunda jumuiya ni kuona wanapata nafasi ya kusadia nchi yao ili kuondoa baadhi ya kero zinazowakabili

 

Alisema katika kituo hicho wametuma milioni 26 za kitanzania mpaka kukamilika kwake.

 

“Tulipoletewa wazo hili la kujenga kituo cha kukoshea na kukafini maiti tulikaa na tukaona ni jambo jema mnoo kwa hapa duniani na kesho akhera” alisema Sadikk.

 

Alisema kuwa wamejenga kituo hicho kwa ajili ya waislamu wa aina zoote hata wale wanaotaka kusafirisha maiti zao kwa boti.

 

Akimkaribsha  makamu wa Kwanza Profesa Hemed Hikman Rashid Mwenyekiti wa Bodi ya Alnour Islam Center alisema Uislamu unamuheshimu sana binaadamu tangu kuzaliwa hadi kufa kwake.

 

Alisema kituo hicho kittumika bure na hakutakuwa na malipo yoyote kwa nayetaka kuayarishiwa maiti.

BARABARA YA NYAHUA - CHAYA KUKAMILIKA MACHI

$
0
0


Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, akisisitiza jambo kwa watalaamu wa Mhandisi Mshauri kutoka kampuni ya AECO  na Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora, mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Nyahua – Chaya (km 85.4).


Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Mhandisi Damian Ndabalinze, akifafanua jambo kwa Mhandisi Mshauri kutoka kampuni ya AECO, Mhandisi Adel Alkhateeb, wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Nyahua – Chaya (km 85.4) kwa kiwango cha lami. Kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akifatilia.

 

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, ameelezea kuridhishwa kwake na kasi ya ujenzi wa barabara ya Nyahua - Chaya (km 85.4) inayojengwa kwa kiwango cha lami na mkandarasi China Henan International (CHICO).

Amesema kukamilika kwa barabara hiyo ambayo ni sehemu ya barabara kuu ya Tabora – Nyahua – Chaya – Itigi – Manyoni yenye jumla ya urefu wa kilometa 259 kutapunguza urefu wa safari kwa kilometa 191 kwa magari yanayopitia barabara ya Tabora - Nzega - Singida hadi Manyoni na hivyo kuleta tija kwa wasafiri na wasafirishaji wa mikoa ya Tabora, Kigoma na Katavi.

“Hakikisheni sehemu ya kilometa sita zilizobaki kuwekwa lami zinakamilika kabla ya mwezi machi ili kuwezesha wananchi kunufaika na barabara hii”, amesema Mhandisi Kasekenya.

Amewataka wakazi wa mkoa wa Tabora kuilinda miundombinu ya barabara, madaraja na taa za barabarani ili zidumu kama ilivyokusudiwa.

Naye Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Mhandisi Damian Ndabalinze, amemhakikishia Naibu Waziri Kasekenya kuwa mkoa huo umejipanga kuhakikisha unalinda barabara zake na kuziwekea taa sehemu nyingi ili kuongeza usalama na kupendezesha mji huo.

Zaidi ya shilingi bilioni 117 zimetumika katika ujenzi wa barabara ya Nyahua - Chaya ambayo imehusisha ujenzi wa madaraja makubwa mawili ya Nyahua na Kizengi ambapo mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Machi mwaka huu.

Naibu Waziri Kasekenya yupo mkoani Tabora kwa ziara ya siku mbili ya kukagua miundombinu inayoendelea kutekelezwa mkoani humo.

ZIARA YA RAIS WA MSUMBIJI CHATO GEITA

$
0
0


Ndege ya Rais wa Jamhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa SADC Mhe. Filipe Jacinto Nyusi ikiwasili katika uwanja wa Ndege wa Geita Chato kwa ajili ya ziara ya siku moja ya kikazi nchini leo tarehe 11 Januari 2021.

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa SADC Mhe. Filipe Jacinto Nyusi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Geita Chato kwa ajili ya ziara ya siku moja ya kikazi
nchini leo tarehe 11 Januari 2021.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa SADC Mhe. Filipe Jacinto Nyusi mara baada ya kuzungumza na Wanahabari.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa SADC Mhe. Filipe Jacinto Nyusi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa SADC Mhe. Filipe Jacinto Nyusi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa SADC Mhe. Filipe Jacinto Nyusi kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda -Chato mkoani Geita.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa zawadi ya picha ya Wanyama watano (The Big Five) mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa SADC Mhe. Filipe Jacinto Nyusi mara baada ya kuwasili katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa SADC Mhe. Filipe Jacinto Nyusi.


 

Rais wa Jamhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa SADC Mhe. Filipe Jacinto Nyusi akiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda -Chato mkoani Geita.


Hospitali ya Rufaa ya Kanda -Chato mkoani Geita ambayo imewekwa jiwe la msingi na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa SADC Mhe. Filipe Jacinto Nyusi mara baada ya kuwasili Chato mkoani Geita leo tarehe 11 Januari 2021.

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa SADC Mhe. Filipe Jacinto Nyusi mara baada ya kuzungumza na Wanahabari.
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>