Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

SAME WAMPOKEA KWA KISHINDO MGOMBEA MWENZA WA CHADEMA

$
0
0

Wanachama na wafuasi wa CHADEMA wakimpokea mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais kupitia chama hicho, Salum Mwalimu wakati akiwasili katika jimbo la Same Mashariki kuhutubia mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Maore Standi.


Wanachama na wafuasi wa CHADEMA wakimpokea mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais kupitia chama hicho, Salum Mwalimu wakati akiwasili katika jimbo la Same Mashariki kuhutubia mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Maore Standi.

Wanachama na wafuasi wa CHADEMA wakimpokea mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais kupitia chama hicho, Salum Mwalimu wakati akiwasili katika jimbo la Same Mashariki kuhutubia mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Maore Standi.

 

Mgombea mwenza kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu, akisalimia na viongozi na wanachama wa chama hicho alipowasili katika Kata ya Maore jimbo la Same Mashariki mkoani Kilimanjaro.

Mgombea mwenza kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu, akihutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Same Mashariki mkoani Kilimanjaro.

Mgombea mwenza kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu, akihutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Same Mashariki mkoani Kilimanjaro. Kulia ni mgombea wa ubunge katika jimbo hilo, Kaboyoka Naghenjwa.

Mgombea mwenza kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu, akiwanadi  wagombea udiwani  jimbo la Same Mashariki, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kata ya Maore mkoani Kilimanjaro.

Mgombea mwenza kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu, akimnadi  mgombea ubunge jimbo la Same Mashariki, Kaboyoka Naghenjwa, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kata ya Maore mkoani Kilimanjaro.


AGUSTINO SULE, FAILUNA MATANGA VINARA NMB BIMA MARATHON 2020

$
0
0

 

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi hundi ya sh. Milioni 100 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Maseru, (kushoto) wakati alipohitimisha  Mbio za NMB Marathon kwenye viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam, Septemba 12, 2020. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Uwekezaji) Angellah Kairuki, wa tatu kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, wa pili kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sanlam  East Africa, Julius Magabe na wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB, Dkt.Edwin Mhede. Fedha hizo zilizotolewa na Benki ya NMB zitatumika kuwasaidia watoto wenye ugonjwa saratani wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. 

 

NA MWANDISHI WETU

 

MBIO za NMB Bima Marathon 2020, zimefanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, huku Agustino Sule wa Arusha akiibuka kinara wa nusu marathon (kilomita 21 wanaume), sawa na Failuna Matanga wa Arusha pia, aliyeibuka mshindi wa umbali huo kwa wanawake.

 

NMB Bima Marathon ni mbio zilizogawa nywa katika kategori tano (nusu marathon – kilomita 21, kilomita 10, kilomita 5 na za watoto, ambazo zilizadhaminiwa na Benki ya NMB, zikilenga kutoa elimu ya bima pamoja na kuhamasisha mazoezi ya viungo kwa jamii.

 

Katika kinyang’anyiro hicho kilichovuta hisia za wengi miongoni mwa wakimbiaji nchini, kikianzia na kumalizikia katika Viwanja vya Mlimani City, huku washindi wakikabidhiwa medali na hundi za mfano na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyekuwa mgeni rasmi.

 

Katika kilomita 21 wanaume, Sule aliyekimbia kwa saa 1:05:10), alifuatiwa kwa ukaribu na Nestory Steven wa Singida (1:06:35), huku Faustine Mussa akikimbia kwa saa 1:07:53. Sule alipata kitita cha Sh. Mil. 1, Nestory Sh. 750,000 na Faustine Sh. 500,000.

 

Kwa upande wa wanawake, Failuna aliyetwaa kiasi cha Sh. Mil. 1 za ushindi wa kwanza, alifuatiwa na Nathalia Elisante (zawadi Sh. 750,000), huku nafasi ya tatu ikikamatwa na Sara Iti, aliyejinyakulia kiasi cha Sh. 500,000 za ushindi wa tatu wa mashindano hayo.

 

Gabriel Gerard alikuwa wa kwanza kilomita 10 wanaume, akifuatiwa na Elisante Elibariki na Marco Joseph, huku upande wa wanawake, Grace Jackson akiibuka kinara mbele ya Fadhila Salum na Glory Makula. Washindi walipewa Sh. 700,000, wa pili Sh. 350,000 na wa tatu Sh. 200,000.

 

Katika Kilomita 5 wanaume, Basil Sule, alitwaa ushindi juu ya Meshack Daniel na Paul Masenza, huku kwa wanawake Caterina Moshi aliibuka kidedea mbele ya Amoure Love na Sara Nyello. Washindi kilomita 5 walipewa Sh. 100,000, washindi wa pili 50,000 na wa tatu Sh. 40,000.

 

Katika mbio za watoto za NMB Bima Marathon 2020, Rayan Nuhu aliibuka mshindi akizawadiwa Sh. 100,000, huku akifuatiwa na Juma Laizer (wa pili Sh. 50,000) na Joe Mutunzi (wa tatu Sh. 30,000).

MGOMBEA MWENZA WA CHADEMA AFIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU DK. PHILEMON NDESAMBULO KUHANI KABURI LAKE

$
0
0

 

 Mjane wa aliyekuwa mwasisi wa CHADEMA, marehemu Dk. Philemon Ndesamburo, akimpa zawadi mgombea nafasi ya Makamu wa Rais kupitia Chadema, Salum Mwalimu, alipokwenda kuhani kaburi la marehemu Dk. Ndesamburo leo Septemba 13, 2020 mjini Moshi. 

 

Ndehorio Moshi ambaye ni mjane wa mwasisi wa CHADEMA, marehemu Dk. Philemon Ndesamburo, akimvisha skafu ya chama hicho mgombea mwenza kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu, kama ishara ya kumtia nguvu alipofika nyumbani kwake Moshi, Kilimanjaro kuhani kaburi la marehemu Dk. Ndesamburo.  


Mjane wa aliyekuwa  mwasisi wa Chadema marehemu Dk. Philemon Ndesamburo akimuongoza mgombea mwenza kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu, kwenda kuhani kaburi la marehemu Dk. Ndesamburo.  

Mgombea mwenza kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu (katikati), akiongoza dua ya kumuombea mwasisi wa chama hicho marehemu Dk. Philemon Ndesamburo, nyumbani kwake Moshi Kilimanjaro, Septemba 13, 2020.  Kushoto kwake ni mjane wa marehemu, Ndehorio Moshi.
Mgombea mwenza kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu, akiagana na mjane wa aliyekuwa mwasisi wa CHADEMA, marehemu Dk. Philemoni Ndesamburo, baada ya kuhani kaburi lake leo Septemba 13, 2020, Moshi Kilimanjaro.

MGOMBEA MWENZA CHADEMA APOKELEWA KIFALME MJINI MOSHI

$
0
0

 Mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu, akiwapungia mkono wananchi waliojitokeza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Manyema Kata ya Njoro Mjini Moshi leo Septemba 13, 2020.

Mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu, akihutubia wananchi waliojitokeza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Manyema Kata ya Njoro Mjini Moshi leo Septemba 13, 2020.
Mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu, akihutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Moshi Mjini leo Septemba 13, 2020.
Mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu, akipeana mkono na mgombea ubunge jimbo la Moshi Mjini, Raymond Mboya, katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Manyema Kata ya Njoro Mjini Moshi leo Septemba 13, 2020.
Mgombea ubunge jimbo la Moshi Mjini, Raymond Mboya, akiwapungia mkono wananchi waliojitokeza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Manyema Kata ya Njoro Mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro leo Septemba 13, 2020.
Mgombea mwenza nafasi ya Makamu wa Rais kupitia Chadema, Salum Mwalimu, akimnadi mgombea ubunge jimbo la Moshi Mjini, Raymond Mboya, katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Manyema Kata ya Njoro Mjini Moshi leo Septemba 13, 2020.

Umati wa watu uliofika katika kampeni za mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu.
Umati wa watu uliofika katika kampeni za mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu.
Wagombea udiwani kwa tiketi ya CHADEMA katika jimbo la Moshi Mjini.

RAIS DKT MAGUFULINA RAIS. MUSEVENI WA UGANDA WATILIANA SAINI MKATABA WA MAKUBALIANO WA KUANZA RASMI MRADI WA BOMBA LA MAFUTA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakishuhudia mawaziri wa Nishati wa nchi zao ( Mhe. Mary Goretti Kitutu wa Uganda na Dkt. Medard Kalemani wa Tanzania) wakitia saini mkataba wa kuanza haraka mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania) kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita leo Jumapili Septemba 13, 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakishuhudia mawaziri wa Nishati wa nchi zao ( Mhe. Mary Goretti Kitutu wa Uganda na Dkt. Medard Kalemani wa Tanzania) wakitia saini mkataba wa kuanza haraka mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania) kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita leo Jumapili Septemba 13, 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea mbele ya mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kutia saini Waraka wa Pamoja Unaoagiza kuanza haraka mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania) kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita leo Jumapili Septemba 13, 2020.
Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akiongea baada ya kutia saini Waraka wa Pamoja Unaoagiza kuanza haraka mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania) kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita leo Jumapili Septemba 13, 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akimsindikiza mgeni wake anayeagana na mawaziri wa Tanzania wakati akiondoka kurejea nyumbani baada ya kutia saini Waraka wa Pamoja Unaoagiza kuanza haraka mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania) kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita leo Jumapili Septemba 13, 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akimlaki mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni  alipowasili kutia saini Waraka wa Pamoja Unaoagiza kuanza haraka mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania) kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita leo Jumapili Septemba 13, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akimlaki mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni  alipowasili kutia saini Waraka wa Pamoja Unaoagiza kuanza haraka mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania) kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita leo Jumapili Septemba 13, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akimlaki mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni  alipowasili kutia saini Waraka wa Pamoja Unaoagiza kuanza haraka mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania) kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita leo Jumapili Septemba 13, 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulina Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakipunga mikono kumuaga Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakati akiondoka kurejea nyumbani baada ya kutia saini Waraka wa Pamoja Unaoagiza kuanza haraka mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania) kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita leo Jumapili Septemba 13, 2020. (Picha na Ikulu).

TUTAANZISHA MAMLAKA YA MAJI CHEMBA- MAJALIWA

$
0
0

 

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM  Taifa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Kelema, kata ya Paranga, wilayani Chemba, baada ya kuwasili katika mkutano wa kampeni, Septemba 13, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM  Taifa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kelema, kata ya Paranga, wilayani Chemba , katika mkutano wa kampeni, Septemba 13, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM  Taifa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kelema, kata ya Paranga, wilayani Chemba , katika mkutano wa kampeni, Septemba 13, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).  
 


Chemba, Dodoma

 

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali inapanga kuanzisha Mamlaka ya Maji Chemba hivi karibuni. 

 

Ametoa kauli hiyo leo (Jumapili, Septemba 13, 2020) wakati akizungumza na wananchi katika eneo la Mnadani, Kijiji cha Kelema, Kata ya Paranga, wilaya ya Chemba mkoani Dodoma kwenye mkutano wa kumuombea kura Rais Dkt. John Pombe Magufuli na mgombea ubunge jimbo la Chemba, Mohammed Moni na wagombea udiwani wa CCM.

 

“Wilaya hii haina mamlaka ya maji. Kwa hiyo tutaanzisha Mamlaka ya Maji ili watumishi wawepo wilayani. Wasimamie kwa karibu na waweze kufuatilia vyanzo vya maji kutokea hapa Chemba wakati tukiendelea kutatua tatizo la maji wilayani hapa. Tutaunda Mamlaka ya maji hivi karibuni.”

 

Amesema Serikali ilitoa sh. bilioni 1.688 za kutafuta vyanzo vya maji huko Orada, Kisanga, Moi, Mondo na Ndaki. “Pia Serikali ya Awamu ya Tano imetoa sh. milioni 677 za kuchimba visima huko Mondo, Mrijo Juu, Chambalo, Hamai na Chemba.”

 

“Tuna uhakika tukipata lita za maji za ujazo 4,700 zinatosha kabisa kujenga mtandao wa maji. Kazi ya kuboresha miundombinu ya maji inaendelea. Zimetengwa fedha nyingine, sh. milioni 150 za kusambaza maji Kelema, Msaada na Bumbu.”

 

Akizungumzia sekta ya afya, Mheshimiwa Majaliwa amesema zimetolewa sh. bilioni 1.8 za kujenga hospitali ya wilaya ya Chemba ili wananchi wapate huduma za tiba wakiwa hapohapo badala ya kwenda Kondoa kama ilivyokuwa awali.

 

“Nia yetu ni kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma hukohuko aliko kwa kuweka zahanati katika kila kijiji, vituo vya afya kwa kila kata. Wakimaliza ujenzi, tumetenga shilingi milioni 500 za vifaa vya hospitali kwa majengo yote saba.”

 

“Tumepeleka sh. milioni 400 za kituo cha afya kule Hamai, shilingi milioni 500 kule Mrijo na shilingi milioni 400 kule Kwa Mtoro. Kazi ya ujenzi ikiisha, kila kimoja kitapata shilini milioni 250 za vifaa vya tiba.”

 

Ninawaomba mumpe kura Rais Dkt Magufuli, Mbunge na madiwani wa CCM ili tukamilishe kazi hizi kwa sababu Serikali hii ni ya watekelezaji. Tunasema na tunatenda.”

 

Wakati huohuo, Mheshimiwa Majaliwa amesema Rais Magufuli anataka umeme usambazwe kote nchini na ndiyo maana akaamua kupunguza bei ya kuunganisha umeme.

 

“Rais wetu kasema anataka kuona kila nyumba ya Mtanzania inawaka umeme. Amepunguza gharama za kuunganisha umeme kutoka shilingi 380,000/- hadi shilingi 27,000/-. Rais wetu kasema ni marufuku kulipia nguzo za umeme.  Mwananchi hutakiwi kulipia nguzo yoyote ile. Atakayekuuzia nguzo, mwambie akupe risiti, leta risiti tumlipue huyo Afisa., amesisitiza.

MKUTANO WA KAMPENI ZA CCM JIMBO LA MASASI MJINI

$
0
0
                   
Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana Viongozi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi na Wananchi Jimbo la Masasi Mjini alipowasili katika uwanja wa Sabasaba Wilayani Masasi kwa ajili ya kuhutubia Mkutano wa Kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM leo Septemba 13,2020. 
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM na Wananchi wa Jimbo la Masasi Mjini wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akiwahutubia kwenye Mkutano wa Kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM katika Uwanja wa Sabasaba Masasi Mkoani Mtwara leo Septemba 13,2020. 

Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia  Wanachama wa Chama cha Mapinduzi na Wananchi Jimbo la Masasi Mjini mkutano wa kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM katika Uwanja wa Sabasaba Wilayani Masasi Mkoani Mtwara leo Septemba 13,2020.  

Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mtoto chipukizi wa Usanii wa Nyimbo za kizazi kipya Wilayani Masasi Mkoani Mtwara Shamsa Amani (3) baada ya kutumbuiza kwenye Mkutano wa Kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM katika Uwanja wa Sabasaba Wilayani Masasi Mkoani Mtwara leo Septemba 13,2020. 
Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na  Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM na Wananchi wa Jimbo la Masasi Mjini baada ya kuwahutubia mkutano wa kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM katika Uwanja wa Sabasaba Wilayani Masasi Mkoani Mtwara leo Septemba 13,2020.   (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).       

Kimei aiombea Himo kuwa Makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Moshi

$
0
0

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, akimnadi mgombea wa nafasi ya ubunge katika jimbo la Vunjo kupitia Chama cha Mapinduzi, Dkt. Charles Kimei katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho katika jimbo la Vunjo. Uzinduzi huo ulifanyika katika viwanja vya Polisi Himo Septemba 12, 2020.

Maelfu ya wakazi wa Himo wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa kampeni wa chama cha Mapinduzi katika Jimbo la Vunjo Uzinduzi huo ulifanyika katika viwanja vya Polisi Himo Septemba 12, 2020.  

 

 

Himo, Kilimanjaro.

 

 MGOMBEA Ubunge wa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la VunjoMoshi Vijini, Dkt. Charles Kimei  amewaomba wananchi wa Jimbo hilo kumpa ridhaa ya kuwa Mbunge wao ili aweze kuwaletea mapinduzi ya kiuchumi. Aliyasema  hayo katika Mkutano wa uzinduzi wa kampeni zake  uliofanyika katika Mji mdogo ya Himo na kuratibiwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Pinda na  kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa Jimbo hilo.

 

Katika hotuba yake, Dkt. Kimei alisema  kuwa Jimbo hilo lina changamoto nyingi ikiwamo miundombinu mibovu ya barabara, Elimu, Afya na ukosefu wa masoko thabiti kwa mazao yazalishwayo na wakazi wa jimbo hilo.

 

Alisema kuwa, ikiwa wananchi watamchagua kuongoza jimbo hilo, atatumia uzoefu wake katika sekta ya Fedha, kuanzisha Mfuko wa Ujasiliamari wa Jimbo ambao utahusika kutoa mikopo nafuu kwa wanachi ili kuwapa mItaji na hivyo kuwajengea uwezo wa kujiajiri na kuajiri ili kuwapaisha kiuchumi. “Kwa kushirikiana na wadau wengine, tunakamilsha mchakato wa kuanzisha mfuko wa Wajasiliamari Vunjo. 

 

Mimi mwenyewe nitatoa andiko la mradi  yaani (Project write-up) ili kupata fedha za uwezeshaji wa makundi maalum ya Wakulima, Wafugaji, Vijana, Wanawake, Bodaboda  na mafundi makenika kwa kuwapa mikopo nafuu”.

 

Kuhusu Kilimo na mazao ya shamba, Dokta Kimei alizungumzia kuhusu kuanzishwa Kilimo cha umwagiliaji ili kuongeza tija, sambamba na kuwawezesha wananchi kuanzisha viwanda vya usindikaji hivyo kuongeza thamani ya mazao. Jambo kubwa la msingi ni kuanzisha viwanda vya usindikaji ili kuongeza thamani ya mazao yetu. Badala ya kuuza Mpunga, tutaanza kuuza mchele wetu uliofungwa vizuri. Badala ya kuuza nyanya ambazo huharibika kirahisi, viwanda hivi vitasindika nyanya hizo na tutauza Tomato paste yetu wenyewe hivyo kuongeza thamani na vipato vya wananchi wa Himo. Tutafanya hivyo pia kwa mazao ya Kahawa na mengineyo’ alisema Dkt. Kimei.

 

Aliongeza kuwa, eneo lingine ni kuboresha miundombinu ya Barabara ili kurahisisha usafarishaji wa mazao hayo ili kufikia masoko kwa urahisi  kutokana na hali hiyo, maisha ya wananchi yatabadirika na kupiga hatua za kimaendeleo.

Kwa upande wa changamoto sekta  ya afya, Dkt. Kimei alisema kuwa vituo vingi vya afya vinahitaji ukarabati mkubwa wa haraka huku vikikosa vifaa vya kisasa kama XRAY na Ultra sound. “Tutasimamia kukamilisha ujenzi wa hospitali wa wilaya ya Himo ambao ulisimama. Pia tutashughulikia masuala ya Bima za afya na matibabu kwa Wazee. Kuhusu ukosefu wa gari la Wagonjwa, Dokt. Kimei alisema ‘Kwa sasa, Jimbo letu halina gari la uhakika la kubebea wagonjwa, Naahidi kutoa gari  langu mimi mwenyewe, lifanye kazi hiyo wakati tunaendelea na mchakato wa kuongeza mengine”alisema.


"Nimejipanga kuhakikisha wananchi wa 
Himo wanapata maendeleo kama inavyosema ilani ya Chama cha Mapinduizi. Nitashirikiana na Serikali kila nyanja ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo na kunufaika na rasilimali zao." alisema Dkt. Kimei


Aidha, pia
 Kimei mbali ya kujiombea kura, pia aliweza kumuombea kura nyingi na za kishindoi kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Madiwani wote wa CCM ndani ya jimbo hilo la Vunjo. 


ZITTO AHUTUBIA MKUTANO WA KAMPENI KIGOMA

$
0
0

Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, akizungumza na wakazi wa Kigoma Mjini kata ya Mwanga, wakati wa mkutano wa mgombea wa udiwani wa kata hiyo, Clayton Chipantu 'Baba Levo'. (Picha na Said Powa).

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU RUFAA ZA WAGOMBEA UBUNGE NA UDIWANI 13 SEPTEMBA 202

$
0
0


 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera Charles akisoma taarifa kwa umma kuhusu rufaa za wagombea Ubunge na Udiwani Jijini Dar es Salaam leo tarehe 13 Septemba 2020.

AJALI YA MOTO YAUA WANAFUNZI 10

$
0
0

 Na Lydia Lugakila Kagera

Jumla ya wanafunzi 10 wamefariki dunia katika ajali ya moto iliyotokea  katika Shule ya Msingi Islamic (Byamungu) iliyopo kata ya Itera wilayani Kyerwa mkoani Kagera.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ambaye ni Mkuu wa wilaya hiyo, Rashid Mwaimu, amesema kuwa Moto huo umetokea usiku wa kuamkia leo.

Amesema kuwa chanzo cha moto huo hakijajulika na tayari vyombo vya ulinzi na usalama vimefika katika eneo la tukio.

Mabaki ya shule ya  Shule ya Msingi Islamic (Byamungu).

LISSU ANGURUMA IRINGA MJINI

$
0
0

 

Mgombea urais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Tundu Lissu, akihutubia mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Mwembetogwa Iringa Mjini.

Wananchi wa Iringa wakiwa katika mkutano wa kampeni za mgombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Tundu Lissu.


Mgombea urais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Tundu Lissu, akihutubia mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Mwembetogwa Iringa Mjini.



MGOMBEA MWENZA WA CCM AKIWA NANYUMBU MTWARA

$
0
0


 Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kuagana na Viongozi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi na Wananchi wa kijiji cha Nanyumbu Jimbo la Nanyumbu Mkoani Mtwara alipokuwa njiani akielekea mkoani Ruvuma kuendelea na Ziara zake za mikutano  ya Kampeni ya Chama cha Mapinduzi CCM baada ya kukamilisha ziara yake katika Mkoa wa Mtwara leo Septemba 14, 2020. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais). 


CHADEMA KUBORESHA IDARA YA UHAMIAJI

$
0
0

 

Mgombea wa nafasi ya umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu, akihutubia katika mkutano wa kampeni katika viwanja vya Shule ya Msingi Namanga jimbo la Longido, mkoani Arusha Septemba 14, 2020. Mgombea huyo ametoa ahadi ya kufanya mabadiliko makubwa katika uboreshwaji wa idara ya uhamiaji hasa katika kitengo cha utoaji hati za kusafiria ambapo amesema CHADEMA itakapoingia madaraka itahakikisha ndani ya siku 21 taratibu za kumpatia mtu hati ya kusafiria zitakuwa zimekamilika tofauti na ilivyo sasa.
Baadhi ya viongozi wa CHADEMA jimbo la Longido.
 
Mgombea wa nafasi ya umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu, akihutubia katika mkutano wa kampeni katika viwanja vya Shule ya Msingi Namanga jimbo la Longido, mkoani Arusha.
 Wakazi wa Namanga wakimsikiliza mgombea wa nafasi ya umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu, wakati akihutubia mkutano wa kampeni katika viwanja vya Shule ya Msingi Namanga jimbo la Longido, mkoani Arusha.

Madiwani wa kata tofauti katika jimbo la Longido.
Mgombea wa nafasi ya umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu, akimnadi mgombea ubunge jimbo la Longido, Paulina Laizar.
Mgombea wa nafasi ya umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu, akivishwa vazi la kitamaduni na mmoja wa viongozi wa Chadema jimbo la Longido.

Mgombea wa nafasi ya umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu, akiwashukuru wakazi wa Namanga mkoani Arusha baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Longido. 

Mgombea nafasi ya umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu, akipeana mkono na mgombea ubunge jimbo la Longido, Paulina Laizar, mara baada ya kuhutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Namanga Shule Septemba 14, 2020.


WAKAZI WA KIKATITI WASIMAMISHA MSAFARA WA MGOMBEA MWENZA CHADEMA


WAKAZI WA KIKATITI WASIMAMISHA MSAFARA WA MGOMBEA MWENZA CHADEMA

$
0
0


Mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Salum Mwalimu, akihutubia wakazi wa Kikatiti waliosimamisha msafara wake wakati akielekea Namanga katika mkutano wa kampeni Septemba 14, 2020.

Mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Salum Mwalimu, akimnadi mgombea wa ubunge jimbo la Arumeru Mashariki.
Mgombea wa nafasi ya Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Salum Mwalimu, akimnadi mgombea wa ubunge jimbo la Arumeru Mashariki.


MGOMBEA MWENZA CHADEMA AHUTUBIA MKUTANO WA KAMPENI ARUMERU MAGHARIBI

$
0
0

 

Mgombea wa nafasi ya umakamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Salum Mwalimu, akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Sokoni, Kisongo jimbo la Arumeru Magharibi.

Mgombea wa nafasi ya umakamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Salum Mwalimu, akimnadi mgombea ubunge jimbo la Arumeru Magharibi, Gibson Ole- Meiseyeki,  wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Sokoni, Kisongo jimbo la Arumeru Magharibi.
Madiwani Chadema wanaogombea katika kata tofauti katika jimbo la Arumeru Magharibi.

MGOMBEA URAIS WA CCM RAIS DKT MAGUFULI AFURAHIA MKUTANO WAKE CHATO, AAGA KWA TABASAMU NA BASHASHA BAADA YA KUMALIZA KUHUTUBIA

$
0
0

Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Tawala na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amejawa furaha na bashasha akiondoka katika viwanja vya Mazaina mjini Chato mkoa wa Geita baada ya kuhutubia maelfu kwa maelfu ya wananchi kwenye mkutano wake wa hadhara wa kampeni leo Septemba 14, 2020.


KATIBU MKUU DKT AKWILAPO AAGIZA KUFANYIKA TATHMINI YA MAZINGIRA NA MIUNDO MBINU YA SHULE ZOTE

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo.

 

Na Mwandishi Wetu


Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt Leonard Akwilapo amewataka Wathibiti Ubora wa shule nchini kufanya tathmini ya mazingira na miundombinu ya shule katika kudhibiti majanga ya moto yaliyokithiri katika siku za hivi karibuni.

 Dkt Akwilapo amesema hayo kufuatia tukio la moto lililosababisha vifo vya wanafunzi 10 na kujeruhi wengine lililotokea katika shule ya Msingi Byamungu Islamic iliyoko Kyerwa Mkoani Kagera.

Akwilapo amewataka Wathibiti ubora wa shule kushirikiana na wataalamu kubaini vyanzo vya moto katika shule  na amesema sheria zipo na pindi shule itakapogundulika kukiuka taratibu wasisite kuzichukulia hatua.

 “Asubuhi ya leo tumepokea taarifa ya kuungua kwa shule ya msingi ya Byamungu  na watoto wamepoteza maisha, lakini matukio haya yamekuwa yanaongezeka hivyo kama Wizara tunawajibu kuhakikisha hili linapatiwa suluhisho kwa kutumia wataalamu,"aliongeza Dkt. AKwilapo

Aidha Dkt.Akwilapo amesema Wathibiti Ubora wa shule zaidi ya 400 wameajiriwa mmepewa ofisi na vitendea kazi, nataka kuona mabadiliko ya namna tunavyosimamia shule”alisisitiza Dkt. Akwilapo.

Katibu Mkuu Akwilapo ametumia fursa hiyo kutoa pole kwa wazazi, walezi na Shule ya Msingi Byamungu iliyopo mkoani Kagera kwa kuondokewa na wanafunzi na kuwatakia uponyaji wa haraka majeruhi sita ambao wanaendelea na matibabu.

TAMNOA washiriki warsha kujadili mbinu za kudhibiti utapeli kwa njia za simu za mkononi

$
0
0


Katika warsha hiyo iliyoandaliwa na GSMA, kupitia mtandao au webinar, wawakilishi kutoka makampuni ya simu waliweza kuchangia mada mbali mbali.
 
 Kutoka Tigo alikuwepo Nkata Kagoma, wengi walikubaliana kwamba utapeli ni tatizo kubwa barani Afrika, na wateja wanahitaji kupata elimu kuhusu tahadhari mbali mbali wanazo weza kutumia kuzuia utapeli kwa njia za simu za mkononi.pia wengi walikubaliana kuwa teknolojia ya dijitali inaweza ikasaidia kutatua matatizo mbalimbali ya kiuchumi na kijamii katika jamii ikiwa itapewa msukumo wa aina yake.

Viewing all 19659 articles
Browse latest View live