Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

Wataalamu wapewa mbinu za uhifadhi mali za kale

$
0
0

Na Asha Mwakyonde

 
VIJANA na wataalamu wa makumbusho wamepatiwa  mafunzo ya kuwajengea uwezo  wa utafiti lengo likiwa ni kuwapatia  mbinu mpya za uhifadhi wa mali za kale.


Akizungumza jijini Dar es Salaam Agasti 7, mwaka huu wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu Rasi wa Ndaki ya Insia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Rose Upor, amesema mafunzo hayo ni mradi mkuu wa utafiti ulifadhiliwa na tàasisi mbalimbali za vyuo.


Amezitaja taasisi hizo kuwa ni  makumbusho ya ujermani ya ujermani Ethinelico missio na chuo kikuu Humboji cha Ujermani na chuo kikuu cha Dar es Salaaam cha Tanzania idara ya historia.


Amesema Makumbusho ya Taifa itaendelea kushirikia na wadau mbalimbali kusaidia makusanyo yaliyopo kwenye makumbusho hayo Dkt. Rose ameongeza kuwa mwisho wa mafunzo hayo wanatarajia wataalamu hao watatumia ujuzi huo kufanyakazi kwa ufanisi mkubwa na kuupeleka ujuzi huo kwa wengine ambao hawajashiriki warsha hiyo.


Naye Mkurugenzi Mkuu makumbusho ya taifa Dkt. Noel Lwoga amesema mafunzo hayo ya kujenga uwezo wa vijana wawezo kufasiri baadhi ya nyaraka zilizopo makumbusho na kubaini sayansi iliyotumika kupata makusanyo na kuweka kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.


Kwa upande wake Mratibu wa warsha hiyo muhadhiri mwandamizi wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dkt. Oswad Masebo, amesema tafiti zinazofanywa ni kupitia makusanyo zilizopo kwenye makumbusho ili kubaini asili ya nchi,ujenzi wa Taifa na maendeleo ya nchi wapi tulipotoka na tunapikwenda .


TMA yatabiri ukame

$
0
0

Na Irene Mark

HALI ya ukame inatarajiwa kuwepo kwenye maeneo mengi ya nchi hasa mikoa inayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.

Akizungumzia na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Septmba 7, 2020; Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya  Hali ya Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi, alisema msimu wa mvua za vuli mwaka huu zinatarajiwa kuwa za chini ya wastani na wastani kwenye maeneo mengi ya nchi.

Mvua za vuli hutarajiwa kunyesha kuanzia Oktoba, Novemba na Desemba (OND) kwenye mikoa ya kaskazini mwa nchi ambayo hupata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.
 
Akitoa utabiri wa msimu wa vuli unaotarajiwa kuanza wiki ya pili ya Septemba mwaka huu hadi mwanzoni mwa Januari,2021 Dk. Kijazi alisema mifumo ya hali ya hewa inaonesha mwelekeo wa upepo na unyevunyevu kuwepo zaidi kwenye Bahari ya Pasifiki huku Bahari ya Hindi ikionekana kukosa upepo na unyevu.

“Mvua hizi za vuli zinatarajiwa kuwa chini ya wastani hadi wastani zikiambatana na vipindi virefu vya ukavu katika maeneo mengi ya nchi.

“Tunatarajia pia zitaanza kwa kuchelewa kati ya wiki ya pili na ya tatu ya Novemba, mwaka huu kwenye mikoa ya nyanda za juu kaskazini mashariki, ukanda wa pwani ya kaskazini na kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro,” alisema Dk. Kijazi.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, athari zitakazojitokeza ni upungufu wa unyevu katika udongo, maradhi ya mlipuko, malisho ya mifugo na upungufu wa maji safi na salma.

Alizishauri mamlaka zinazohusika kuchukua tahadhari ya kudhibiti majanga yanayoweza kutokea yakiwemo matukio ya moto kwenye mapori na misitu.

Aliitaja mikoa ya Kanda ya Ziwa itakayopata mvua chini ya wastani na wastani kuwa ni Kagera, Geita, Mara, Mwanza, Simiyu, Shinyanga na Kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma ambako mvua zitaanza wiki ya pili ya Septemba mkoani Kagera na kusambaa.

Kwa ukanda wa pwani ya kaskazini mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Unguja, Pemba na kaskazini mwa Morogoro mvua  hizo chini ya wastani na wastani zitaanza kwa kuchelewa kati ya wiki ya pili na ya tatu ya Novemba mwaka huu.

MAREKANI YAWATAKA WATANZANIA KUSHIRIKI UCHAGUZI, KUMCHAGUA KIONGOZI BORA

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Kabudi akimkabidhi zawadi ya picha Balozi wa Marekani hapa nchini Mhe. Dkt. Donald Wright. Kulia mwa Waziri ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi, Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge.

 


Balozi wa Marekani hapa nchini Mhe. Dkt. Donald Wright
amewataka Watanzania kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Octoba 28 mwaka huu ili kumchagua kiongozi bora atakayeweza kutekeleza malengo yao kimaendeleo.


Dkt. Wright amesema hayo wakati alipokutana na kufanya
mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi leo jijini Dar es Salaam ambapo wamejadili masuala ya ushirikiano wa maendeleo baina ya Tanzania na Marekani pamoja na kugusia harakati za kampeni za uchaguzi mkuu unaoendelea hapa Nchini.


Katika mazungumzo hayo Prof. Kabudi akiwa ameambatana na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge
amemhakikishia Balozi wa Marekani Dkt. Wright kuwa Tanzania ni sehemu salama ya kuwekeza hususani katika sekta za utalii, kilimo,na biashara na kumhakikishia kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu utakuwa huru,haki na wa amani.
 
Prof. Kabudi ameongeza kuwa katika sekta ya utalii serikali ya
awamu ya tano imedhibiti kwa kiasi kikubwa uwindaji haramu
ikiwa ni pamoja na kupambana na ujangili jambo ambalo
limeiwezesha serikali kuanzisha hifadhi za Taifa mpya nane ikiwa ni pamoja na kuimarisha hatua za usalama kwa watalii baada ya janga la corona kumalizika nchini.
 
Kwa upande wake Balozi wa Marekani hapa Nchini Dkt. Donald
Wright amemhakikishia Waziri kabudi kuwa atahamasisha wafanyabiashara na wawekezaji kuja nchini kuwekeza katika
sekta za kilimo,biashara,huduma za afya na viwanda pamoja na
kuhamasisha watalii kutoka marekani kuja nchini.
 

"Natumia pia fursa hii kuwasihi Watanzania kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba mwaka huu ili kumchagua kiongozi bora atakayeweza kutekeleza malengo yao kimaendeleo" Amesema Dkt. Wright.

Mama Samia awataka walioshindwa kura za maoni Kigamboni kuacha nongwa

$
0
0

NA JANETH JOVIN

Mgombea Mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Samia Suluhu Hassan amewataka  wagombea wa nafasi mbalimbali walioshindwa katika Jimbo la Kigamboni kuacha nongwa bali warudi kunduni  na kuungana kwa pamoja kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi.

Mama Samia amesema yeyote atakayebainika  kuwa anakihujumu chama kwa kuzunguka mitaani basi hatachukuliwa hatua na kusisitiza kuwa chama hicho kipo macho na kitamtambua mtu huyo atakayefanya hujuma.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Mjimwema Kigamboni wakati wa muendelezo wa kampeni zake, Mama Samia amesema wale wote walioshindwa katika kura za maoni Kigamboni anawaomba kundini na endapo wakigundua kuwa wanafanya nongwa au kukihujumu chama basically watakula saa moja na yeye.

Amesema mashikamano katika uchaguzi ni kitu muhimu na endapo wanachama wataruhusu wagawanyike basi wapinzani watashinda kirahisi uchaguzi Mkuu.

"Tusijaribu kuruhusu jambo hilo, najua wanaKigamnoni mpo imara hivyo tushikamane na kwa umoja wetu twende tukapige kura na hatimaye tupate ushindi," amesema.

Amesema katika jimbo hilo la Kigamboni ndani ya miaka mitano ijayo watakomesha tatizo la ukosefu wa maji ya Dawasa na kuongeza kuwa wataendelea kujenga hospitali na kusambaza umeme vijijini.

Aidha Mama Samia amesema kuwa katika miaka mitano ijayo watatekeleza mradi maalum wa kukomesha tatizo la mafuriko eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam.

"Tutaendelea kukarabati miundombinu ya elimu na kuhimarisha elimu ya watu wazima, hakika kote nilipopita katika jiji la Dar es Salaam nimeona yamefanyika mambo makubwa, hakuna kitu ambacho tuliahidi hatujakifanya bali vipo vilivyoanza kujenga na tukipewa mingine mitano tutamalizia, " amesema

Naye mgombea ubunge Jimbo hilo la Kigamboni,  Dk. Faustine Ndugulile amesema  katika kipindi cha miaka mitano mambo makubwa yamefanyika Kigamboni  kwani kwa sasa umeme kwenye jimbo hilo haukatiki ovyo.

Amesema katika miaka mitano ijayo watahakikisha Kigamboni inakuwa eneo la viwanda litakalotoa ongeza idadi ya ajira kwa Vijana na kuongeza kuwa wameshatenga Bilioni 75 kwa ajili ya kujenga soko la samaki Pemba Mnazi.

"Wananchi wa Kigamboni  mlinipa imani yenu na mimi nawaahidi kuwapatia maendeleo,  hakikisheni mnaichagua CCM ili kuleta maendeleo ya kweli," amesema

KONGAMANO LA NGOME YA VIJANA ACT-WAZALENDO LAFANYIKA ZANZIBAR

$
0
0


Naibu Katibu Mkuu wa chama cha ACT- Wazalendo, Nassoro Ahamed Mazrui akizunguma kwenye Kongamano la Ngome ya Vijana iliyofanyika Unguja Zanzibar leo Septemba 8.

MAJALIWA: WANAHAI MSICHAGUE VIONGOZI KWA VIGEZO VYA UKABILA, UDINI

$
0
0

 MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wasichague viongozi kwa kutumia vigezo vya udini, ukabila, itikadi za vyama na badala yake wachague viongozi watakaokuwa tayari kushirikiana nao katika kuboresha maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

 

Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumanne, Septemba 8, 2020) wakati akimuombea kura Rais Dkt. John Pombe Magufuli, mgombea ubunge wa jimbo la Hai, Saasisha Mafuwe na wagombea udiwani kwa tiketi ya CCM kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Masama Kusini kwenye uwanja wa Kwa Sadala wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro.

 

“Ndugu zangu Watanzania, ndugu zangu wanaHai na wanaKilimanjaro mnatambua uwezo na uelewa mkubwa alionao Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli wa kutambua na kuona nini Watanzania wanahitaji, nawaomba siku ya kupiga kura itakapofika tujitokeze kwa wingi bila kujali itikadi zetu tumpigie kura nyingi ili akaendeleze miradi ya maendeleo aliyoianzisha.”

 

Amesema wakati umefika kwa wakazi wa Hai kuchagua kiongozi mwenye kujali na kutambua changamoto zinazowakabili katika maeneo yao na kushirikiana nao katika kuzitafutia ufumbuzi na kamwe wasikubali kupiga kura kwa ushabiki au kufuata mkumbo. “Mchague Rais Dkt. Magufuli kwa nafasi ya urais na Saasisha nafasi ya ubunge pamoja na wagombea udiwani wote wa CCM.”

 

Mheshimiwa Majaliwa amesema Rais Dkt. Magufuli ni kiongozi anayetokana na Chama Cha Mapinduzi chenye utaratibu wa kuratibu miradi yote inayotakiwa kutekelezwa katika maeneo yote nchini kupitia ilani ya uchaguzi na kina mipango mizuri ya kuboresha maendeleo ya wananchi.

 

Wakati huo huo, Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika wilaya hiyo kupitia mradi mkubwa wa maji unaojengwa kwa sh. bilioni 520 kutoka Machame hadi Arusha. Visima vimekamilika kuchimbwa na usambazaji wa mabomba umeanza.

 

“Katika mradi huu wananchi wa Hai walio katika kilomita 12 kushoto na kulia kando kando ya maeneo ambayo bomba la maji litapita tutahakikisha Mamlaka ya maji AWSA inaweka matanki kwa ajili ya kusambaza maji kwa wananchi katika ukanda wa chini.”

 

Amesema sh. bilioni 3.3zimetumika kukamilisha mradi waujenzi na upanuzi wa skimu ya maji LOSAA – KIA. Maeneo yanayonufaika ni pamoja na kata ya Masama Magharibi, Masama Kati, Masama Kusini na kata ya KIA.

 

Mheshimiwa Majaliwa amesema sh. milioni 844 zimetumika kukamilisha ukarabati na ujenzi wa mifereji ya maji katika skimu za Nsanya, Musa Mwinjanga na Kikavu Chini.Skimu ya Uroke – Bomang’ombe imekamilika na inahudumia maeneo ya Machame Uroki, Kwa Sadala, Kware, Romu na Mji wa Hai.

PICHA ZA KAMPENI NZERA-GEITA

$
0
0
Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Wananchi wa Nzera mkoani Geita katika Mikutano ya Kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM wakati akitokea Buchosa Sengerema mkoani Mwanza.

NMB yafanya mapinduzimakubwa ya malipo nchini

$
0
0

 Benki ya NMB kwa kushirikiana na kampuni ya Mastercard imezindua matumizi ya kadi za kisasa zaidi za kieletroniki ambazo zinatarajiwa kuwa chachu ya mapinduzi makubwa ya malipo nchini, na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa watu wengi.
 
Kadi hizo zinazowezesha malipo ya kabla (prepaid card) na malipo kwa mkopo (credit card) zimezinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam katika hafla iliyoshuhudiwa na wadau mbalimbali akiwemo Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Bernard Kibesse, ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi.

Naibu Gavana wa Benki ya Tanzania, Dk. Bernard Kibesse (Katikati) akimpongeza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB Dkt. Edwin Mhede baada ya kuzinduliwa rasmi kwa kadi za NMB Prepaid na NMB Credit. Wakishuhudia kutoka kushoto ni Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara, Filbert Mponzi Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna na Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha, Benedict Baragomwa.


Kwa mujibu wa viongozi wa benki hiyo, ushirikiano na Mastercard kutoa huduma hizi mbili utakuwa wa manufaa mengi na mafanikio makubwa si kwa wateja wa NMB tu bali pia kwa sekta ya kifedha na Watanzania wote kwa ujumla.


Hii inatokana na kadi hizi kuweza kutumiwa na wateja na wasio wateja wa NMB ambayo huduma zake zinapatikana nchi nzima kutokana wigo mpana wa matawi zaidi ya 220, mawakala zaidi ya 7000 na mapinduzi ya huduma za kibenki kwa kutumia njia mbadala za kidijitali kama vile NMB Mkononi.

Hizi ndizo aina ya kadi mpya za NMB Prepaid (Nyekundu) na NMB Credit.

 
Katika mkakati wake wa kutoa huduma kupitia kadi za kielektroniki za Mastercard ambazo pia zina uwezo wa kutunza fedha, kufanya malipo kwa intaneti au kwenye point of sales (POS), Benki ya NMB imepanga kuzisambaza

kwa zaidi ya watu milioni tatu ndani ya miaka mitano. Dkt. Kibesse alisema litakuwa jambo jema kama lengo hilo litakuwa maradufu ili huduma hii mpya iweze kuchangia kwa kiasi kikubwa kuwepo na uhakika wa Watanzania wengi kuwa na huduma za kibenki muda wote na mahali popote.
 
Naibu Gavana huyo pia alisisitiza umuhimu wa kadi hizo kusambazwa hadi vijijini na maeneo ya pembezoni kwa kuwa faida yake ni pamoja na kuwasaidia wakulima kujiwekea akiba hata kabla ya kufungua akaunti. Hilo likifanikiwa, alifafanua, Tanzania itakuwa imepiga hatua kubwa katika jitihada zake za kuwa uchumi usiotegemea malipo ya fedha taslimu.
 
Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna, alisema huduma ya kadi za malipo ya kabla na zile za malipo kwa mkopo ni moja ya miradi mikubwa ambayo taasisi hiyo imefanya na Mastercard. Mwaka 2015, washirika hao wawili walizindua Mastercard debit cards ambazo zimesambazwa kwa wateja zaidi ya milioni tatu.
 
Mradi wa pili ulikuwa ni uzinduzi wa Mastaboda ambayo inawawezesha waendesha pikipiki kupokea malipo kupitia
simu za mkononi. Bi. Zaipuna alisema mradi huu mpya na wa tatu na Mastercard ni ushirikiano wa muhimu sana na wa faida kwa sekta ya fedha nchini na kwa Watanzania wote kwa ujumla.
 
Aidha, mpango huu unaenda sambamba na mkakati endelevu wa NMB wa kuwajumuisha wananchi wengi zaidi kwenye huduma za kibenki na kuwaingiza kwenye mfumo wa malipo kwa kadi. Pamoja na urahisi na usalama katika kufanikisha miamala, kadi hizi zitakuwa msaada mkubwa kwa wafanyabiashara ambao shughuli zao zinahitaji fedha za kigeni. Hatua hii ni muhimu sana kwa Tanzania na tunaamini itaongeza tija na thamani kwa wateja wetu kuanzia makampuni mpaka wateja binafsi.
 
Naye Mkurugenzi Mkazi wa Uendelezaji Biashara wa Kampuni ya Mastercard Afrika Mashariki, Frank Molla, alisema ubia wa kampuni hiyo na NMB ni sehemu ya mkakati wao wa kuwafikia watu bilioni moja duniani na kuwaingiza kwenye uchumi wa kidijitali mpaka ifikapo mwaka 2025.


ICVA yazitaka NGOs za msaada wakibinamu kushirikiana

$
0
0

Katibu Mkuu wa Tanzania Refugee and Migration Network (TAREMINET), ABEID Kasaizi akielezea warsha ya siku moja ya wadau wa msaada wa kibinadamu iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 
Mhadhiri Mwandamizi wa Shule Kuu ya Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Khoti Kamanga akifafanua jambo kuhusu dhana ya ushirikiano katika mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs).
 
 
 
NA SULEIMAN MSUYA

MASHIRIKA yasiyo ya Kiserikali nchini Tanzania (NGOs) yanayojihusisha na kutoa msaada wa kibinadamu yameshauriwa kushirikiana ili yaweze kufikia malengo waliyojiwekea.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Program wa  International Councils of Volunteers Agency (ICVA), Michael Hyden wakati akitoa mada kwenye warsha ya siku moja kuhusu dhana nzima ya ushirikiano kwa wadau wa masuala ya msaada wa kibinadamu jijini Dar es Salaam.

Warsha hiyo iliandaliwa na Mtandao wa Mashirika yanayoshughulika na kutoa msaada wa kibinadamu la Tanzania Refugee and Migration Network (TAREMINET).

Hyden alisema popote kwenye mafanikio msingi mkubwa ni ushirikiano wa wadau husika na kwamba dhana ya kila mtu kujipendelea itakuwa changamoto.

Mkurugenzi huyo alisema umoja na ushirikiano utaweza kuishawishi Serikali, Mashirika yaliyopo chini ya Umoja wa Mataifa (UN) na mengine mengi kuwasaidia kutimiza malengo ya msaada wa kibinadamu.

"Niwe muwazi kuwa iwapo mnataka kufanikisha malengo yenu mnatakiwa kuwa pamoja ili muimbe pamoja jambo ambalo litawarahisishia kufikia wadau wote katika muhimu na sisi tutasaidia ambapo mnakwama kama ni masuala ya kisheria iwapo kuna changamoto hiyo," alisema.

Alisema nchi ambazo NGOs zinafanya kazi pamoja mafanikio ni mengi tofauti na zile ambazo zinafanya kila mtu mwenyewe.

Alisema ICVA wanapromoti kanuni za msaada wa kibinadamu ziweze kutekelezwa katika nchi husika kwa kuwa wamesaini mikataba mbalimbali ya Kimataifa.

Mkurugenzi huyo alisema ushirikiano huo utafanikishwa na uongozi bora, usimamizi, uratubu, ushirikishwaji, uwazi na mengine muhimu kwenye taasisi.

Mwenyekiti wa TAREMINET, Janemary Ruhundwa warsha hiyo imejikita kujadili dhana nzima ya ushirikiano katika ngazi ya NGOs za ndani ya nchi katika utoaji wa msaada wa kibinadamu nchini.

Alisema kumekuwepo na mjadala mpana duniani tangu mwaka 1990 ila dhana hiyo haijatekelezwa kisawasawa na kuonekana kwa jamii husika.

"Warsha hii itatupa muongozo wa nini kifanyike hapa nchini kutekeleza dhana ya ushirikiano katika eneo la msadaa wa kibinadamu kwani makubaliano yalifikiwa bado tupo nyuma kiutekelezaji," alisema.

Ruhundwa alisema bado NGOs nyingi zinaamini katika kusubiri mashirika ya kimataifa kusambaza dhana hiyo jambo ambalo linawachelewesha.

Katibu Mkuu wa TAREMINET, Abeid Kasaizi alisema mtandao huo ni muunganiko wa mashirika 12 ya msaada wa kibinadamu Tanzania.

Alisema warsha ya leo imelenga kuona ni namna gani wanaweza kutumia nguvu ya pamoja katika kutatua majanga yanayopata nchi kwa pamija.

"Kuna majanga kama mafuriko, tetemeko na mengine ambayo yanahitaji NGOs zinazojihusisha na msaada wa kibinadamu kutoa msaada bila kubaguana.

" Sisi tumeamua kupigania msaada wa kibinadamu kwa miaka mingi hivyo tunapswa kuwa pamoja kupitia jukwaa la TAREMINET ili tusisambaze rasilimali zinazopatikana na wahanga watapata kilichobora zaidi,"alisema.

Kwa upande wake Mhadhiri Mwandamizi wa Shule Kuu ya Sheria na Kituo cha Wakimbizi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Khoti Kamanga alisema tatizo la wakimbizi ni kubwa duniani na njia sahihi ya kukabiliana nayo ni wadau wote kushirikishwa.

Prof.Kamanga alisema dhana ya ushirikiano inataka kuwe na lugha moja shirikishi na sio watu fulani kufanya maamuzi kwa niaba ya kundi fulani.

Alitolea mfano janga la wakimbizi pamoja na kwamba asilimia 83 wanatoka nchi maskini lakini sera kuhusu kundi hilo zinatungwa na nchi tajiri jambo ambalo sio sahihi.

"Pia mgawanyo wa fedha unafanyika huko katika nchi tajiri jambo ambalo halileti dhana ya ushirikiano inakosekana kwa nchi maskini ambazo ndizo zenye tatizo," alisema.

Mhadhiri huyo alisema changamoto nyingine ambayo inaonekana kutokana na kukosekana kwa ushirikiano ni nchi maskini kushindwa kufanya utafiti wa kina wa hali halisi ya tatizo.

Alisema ni wakati muafaka kwa mashirika ya kimataifa na wadau wa maendeleo kuwezesha wataalam ili wafanye utafiti wa hali halisi ya wakimbizi nchini na wahitaji wa msaada wa kibinadamu.


Benki ya CRDB yapewa dhamana ya bil.110/- kuboresha miundombinu

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
 
 
Na Mwandishi Wetu

BENKI ya CRDB imepokea dhamana ya Sh. Bilioni 110 kutoka kwa Kampuni ya GuarantCo ambayo ni dhamana ya maika mitano kwa ajili ya maboresho ya utendaji hasa kwenye miundombinu ya sekta mbalimbali kiuchumi.


GuarantCo ni Kampuni ya Maendeleo ya Miundombinu (PIDG) yenye maskani yake Nchini Uingereza.

Akizungumza na wanahabari kuhusu dhamana hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema dhamana hiyo itaongeza uwezo wa benki ya CRDB kuwekeza kwenye miradi ya kimkakati na mipango ambayo inalinufaisha taifa ambayo inalinufaisha taifa na watanzania wote.
 
Alisema lengo la dhamana hiyo ni kujenga mazingira wezeshi ya uwekezaji kwa kushirikiana ili kuchichimua ukuaji wa uchumi hususani kwenye uwekezaji mkubwa wa miundombinu na nishati.

Nsekela alisema ushirikiano wa Benki ya CRDB na GuarantCo utasaidia mipango ya serikali katika kufadhili miradi mikubwa ya miundombinu kwa kupanua mitaji na mikopo ya gharama nafuu kwa wakandarasi.

“Mbali na kuongeza upatikanaji wa fedha kwa wafanyabiashara, miradi inayofadhiliwa chini ya makubaliano ya GuarantCo itakuwa katika sarafu ya ndani, inayoepuka hatari ya kupoteza fedha za kigeni.

"Ushirikiano wetu unaonesha utayari yetu kwenye kujitolea kwetu katika kusaidia ukuaji wa uchumi wa nchi…"tunafurahi tunashirikiana kimkakati kuchunguza miundombinu ya ubunifu wa kifedha na kufadhili miradi ya miundombinu hapa nchini,” alisema Nsekela.

MATATANI KWA KUDAIWA KUSABABISHA KIFO CHA MTOTO WAKE

$
0
0

 Mtoto wa darasa la saba, Veronica Anthony (17) ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na baba yake mzazi Anthony Costantine (50) baada ya kudai kuwa amechelewa kurudi nyumbani.

Akidhibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mwandamizi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro, amesema tukio hilo limetokea saa mbili usiku maeneo ya Kayenze kata ya Kayenze wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.

Kamanda Muliro amesema mtoto huyo aliuawa kwa Kupigwa na Kitu Kizito Kichwani na Baba yake Mzazi  Costantine baada ya Kile kinachodaiwa  kurudi nyumbani Kwao akiwa amechelewa majira ya usiku kitendo kinachodaiwa kumkasirisha baba yake mzazi na kuamua  Kutoa  adhabu ya Kikatili kwa binti yake Iliyosababisha mauaji.

Amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa uchunguzi wa daktari na kuongeza kuwa mtuhumiwa ambaye ni Baba mzazi wa marehemu amekamatwa na atafikishwa Mahakamani kwa hatua za Kisheria.

Kamanda Muliro amesema katika tukio jingine,  Septemba 9, mwaka huu majira ya saa moja usiku huko maeneo ya Mhonze “a”, Kata ya Shibula, Wilaya Ya Ilemela, Mkoa Wa Mwanza, Emmanuel Joseph (49), Msukuma, Mkulima na Mkazi Wa Kijiji Cha Mhonze ‘a”, aliuawa baada Ya kupigwa na kitu Kizito Utosini na ndugu yake Mussa  Majuto, Miaka 35, Msukuma, Mkulima Na Mkazi Wa Mhonze

Amesema kiwa inadaiwa marehemu alikua akimtuhumu mtuhumiwa kumwibia Simu Yake aina ya Tecno ya Batani yenye thamani ya Tsh 40,000/=. Mwili Wa Marehemu umehifadhiwa Hospitali Ya Rufaa Ya Mkoa Ya Sekou Toure Kwa uchunguzi wa Daktari. Aidha  Mtuhumiwa amekamatwa Upelelezi unakamiliswa na atafikishwa Mahakani Haraka Iwezekanavyo

Hata hivyo amesema Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza linatoa wito kwa wazazi, walezi na familia Kwa Ujumla kuwa makini na adhabu wanazotoa kwa watoto kwani zinaweza kuwapelekea Kutenda Ukatili dhidi ya Watoto na kuleta madhara makubwa katika familia na baadae kufikishwa Mahakamani Kwa makosa ya Jinai.

"Pia Polisi Itaendelea kuwachukulia hatua kali Za Kisheria Watu  Wote Wasioheshimu Sheria Za Nchi na Kutaka kuvuruga zoezi zima la Uchaguzi Mkuu kwa aina yoyote," amesema Muliro .

Mgombea Urais wa CCM Rais Dkt. Magufuli ahutubia wananchi wa Geita katika Uwanja wa Kahangalala mkoani Geita

$
0
0


 Sehemu ya Wananchi wa Geita mjini wakisikiliza hotuba ya Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika uwanja wa Kalangalala mkoani Geita.

Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Wananchi wa Geita mjini katika mkutano wa Kampeni za CCM zilizofanyika leo tarehe 9 Septemba 2020 katika uwanja wa Kalangalala mkoani Geita.
 

HESLB YAFUNGA DIRISHA LA MAOMBI YA MIKOPO 2020/2021

$
0
0


Maombi 92,947 yapokelewa na kusajiliwa

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul- Razaq Badru (katikati) akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari Agosti 31 mwaka huu kuhusu kuongezwa kwa muda katika dirisha la maombi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu katika mwaka wa masomo 2020/21. Kushoto ni Meneja Masoko wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Joseph Kimaro na kulia ni Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Mwanaisha Said. (PICHA NA BODI YA MIKOPO- HESLB).

 
 

Na Mwandishi Wetu, HESLB, DAR ES SALAAM


 

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza kufungwa kwa dirisha la maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao kwa mwaka wa masomo 2020 ambapo hadi kufikia leo Septemba 10, 2020 imepokea na kusajili jumla ya maombi ya wanafunzi 92,947.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi (Septemba 10, 2020) Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa (HESLB), Abdul-Razaq Badru imesema mfumo wa maombi hautaweza kuruhusu usajili wa maombi mapya ya waombaji isipokuwa kwa waombaji 7,500 waliopo mtandaoni ambao hawajakamilisha maombi hayo.

Badru amesema HESLB ilifungua dirisha la maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao kwa muda wa siku 40 kuanzia tarehe 21 Julai mwaka huu, ambapo hata hivyo kufuatia maoni na maombi ya wazazi, walezi na wanafunzi  iliongeza muda wa siku 10hadi leo Alhamisi Septemba 10, 2020 ili kutoa fursa kwa waombaji kukamilisha maombi hayo.

Leo Alhamisi (Septemba 10, 2020) saa 6:00usiku dirisha la upokeaji wa maombi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2020/2021 kwa njia ya mtandao, litafungwa rasmi. Baada ya muda huo, usajili mpya kwa ajili ya maombi mapya hautaruhusiwa’alisema Badru

AIdha, Badru alisema Oktoba Mosi mwaka huu HESLB itaanza zoezi la uchambuzi wa maombi hayo na baadaye itaorodhesha maombi yote yenye mapungufu na kuwatangazia waombaji husika kwa ajili ya kurekebisha kasoro zilizojitokeza.

Akifafanua zaidi, Badru aliwataka wazazi, walezi na wanafunzi kuendelea kufuatilia vyanzo rasmi ikiwemo tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz) kuhusu taarifa muhimu na orodha ya watakaopangiwa mikopo kwa mwaka wa masomo 2020/2021 kwa mujibu wa kalenda ya mwaka wa kitaaluma (academic almanac) ya mwaka huu.

Serikali kupitia HESLB, imetenga kiasi cha TZS Bilioni 464kwa ajili ya wanafunzi 145,000,ambapo kati yao wanafunzi wanufaika 54,000watakuwa wa mwaka wa kwanza na 91,000ni wanafunzi wanufaika wanaoendelea na masomo.

Benki ya NMB yadhamini CDF Trophy Cup 2020 kwa Sh. Mil. 40

$
0
0

 Benki ya NMB imetangaza kudhamini Michuano ya Gofu - Kombe la Mkuu wa Majeshi ‘CDF Trophy Cup 2020’, inayotarajia kufanyika siku ya Septemba 19 na 20 mwaka huu, kwenye Viwanja vya Gofu Lugalo jijini Dar es Salaam.


Akitangaza udhamini huo wenye thamani ya Shilingi Milioni 40, katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Klabu ya Gofu Lugalo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB, Omary Mtiga alisema udhamini wao unatokana na kutambua thamani ya michezo ikiwemo gofu.

Mwenyekiti wa Klabu ya Lugalo Brigedia Mstaafu Michael Luwongo (wa pili kutoka kulia) akipokea mfano wa hundi ya shilingi Milioni 40/- kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Omari Mtiga, iliyotolewa na Benki hiyo kwa ajlli ya udhamini wa michuano ya Gofu  ya Mkuu wa Majeshi. Kushoto ni Nahodha wa timu ya Gofu ya NMB, Michael Misabo na kulia ni nahodha wa timu ya Gofu Lugalo, Captain Japhet Massawe.


Alisema ya kuwa, NMB kama taasisi kinara ya kifedha nchini, inafurahishwa na aina ya ushirikiano uliopo kati yao na Klabu ya Gofu Lugalo inayoandaa michuano hiyo na kwamba udhamini wao huo ni wa sita mfululizo tangia mwaka 2014 na unaakisi nafasi ya Benki hiyo katika maendeleo ya michezo Tanzania.


“Tunafurahishwa na aina hii ya ushirikiano baina yetu na waandaaji, ambao hauishii tu katika kudhamini CDF Cup, bali pia unaoifanya NMB kuwa na nyota wengi wa gofu wanaounda timu yetu, ambayo nayo itashiriki michuano hiyo,” alisema Mtiga.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo, aliishukuru NMB kwa namna inavyojitoa katika kusaidia ukuaji wa michezo nchini, hasa CDF Cup inayoratibiwa na kuendeshwa na klabu yake. Alisema wanatarajia kuwa na washiriki wengi mwaka huu, kutokana na mwitikio aliouona, kwani hadi wanakabidhiwa hundi ya udhamini na NMB, kuna jumla ya washiriki 110 waliojiandikisha, ikiwa imesalia wiki moja kabla ya kuanza kwa michuano hiyo.


“Tayari washiriki 110 wamejisajili hadi sasa kutoka klabu mbalimbali nchini, zikiwemo Lugalo, Dar Gymkhana, Arusha Gymkhana, Zanzibar Gymkhana, NMB na nyinginezo, na tunatoa wito washiriki wajitokeze zaidi na wazazi wawalete watoto wao kushiriki,” alisema Luwongo.


Naye nahodha wa Klabu ya Gofu ya NMB, Michael Misabo, alisema kuwa nyota wa timu yake wako tayari kushindania na hatimaye kutwaa ubingwa wa CDF Trophy, kwani wamejiandaa vya kutosha kuhakikisha wanafanya vyema katika kinyang’anyiro hicho.


“Katika CDF Cup 2020, NMB sio tu wadhamini wakuu wa mashindano, bali pia ni washiriki tuliojiandaa kuchuana na tunaingia tukiwa na uhakika wa kufanya makubwa na kutwaa ubingwa wa jumla,” alisema Misabo mbele ya wanahabari waliohudhuria hafla hiyo.


Kwa upande wake, nahodha wa Klabu ya Gofu Lugalo, Japhet Masai, alisema kama timu wamejiandaa vya kutosha
na kwamba maandalizi ya jumla ya michuano yanaendelea vyema na kwamba Ijumaa Septemba 18 kutafanyika
utangulizi kwa nyota wa kulipwa kuchuana.


“Nyota wa kulipwa watatangulia kuchuana Ijumaa ya Septemba 18, kisha ufunguzi rasmi Jumamosi na kuhitimisha
michuano Jumapili kwa nyota wa ngazi mbalimbal kutoana jasho katika Divisheni za A, B na C kwa watoto, wanaume na wanawake, pamoja na nyota wa ridhaa,” alifafanua.

MGOMBEA MWENZA MHE; SALUMU MWALIMU ATIKISA TANGA

$
0
0

Mgombea Mwenza kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Salum Mwalimu, akihutubia mkutano wa kampeni katika Kata ya Genge jimbo la Muheza mkoani Tanga leo Septemba 11, 2020. (Na Mpiga Picha Wetu).

Mgombea Mwenza kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Salum Mwalimu, akihutubia mkutano wa kampeni katika Kata ya Genge jimbo la Muheza mkoani Tanga leo Septemba 11, 2020. 
Mgombea Mwenza kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Salum Mwalimu, akihutubia mkutano wa kampeni Kata ya Genge jimbo la Muheza mkoani Tanga.
Mgombea Mwenza wa kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Salum Mwalimu, akimnadi mgombea ubunge jimbo la Muheza Yosepha Komba, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika  katika eneo la Teule wilayani Muheza mkoani Tanga.
Wagombea udiwani jimbo la Muheza.
 
 Mgombea ubunge jimbo la Muheza, Yosepha Komba, akihutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika  katika Kata ya Genge jimbo la Muheza. Kulia ni mgombea mwenza wa CHADEMA, Salum Mwalimu.
Baadhi ya wakazi wa Muheza wakimsikiliza mgombea nafasi ya Makamu wa Rais kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu.

Mwendesha bodaboda (katikati), akimsikiliza kwa makini mgombea nafasi ya Makamu wa Rais kupitia Chadema, Salum Mwalimu katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kata ya Genge jimbo la Muheza mkoani Tanga.
Baadhi ya viongozi wa chadema wakiwa katika mkutano uliofanyika Hedalu mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya viongozi wa chadema wakiwa katika mkutano uliofanyika Hedalu mkoani Kilimanjaro.
Mgombea mwenza kupitia Chadema, Salum Mwalimu, akiwaaga wananchi waliofika katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Muheza mkoani Tanga. 
Mgombea Mwenza wa kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Salum Mwalimu, akimnadi mgombea ubunge jimbo la Korogwe Vijijini, Aminata Saguti, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kata ya Hale mkoani Tanga. 

Mgombea Mwenza wa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Salum Mwalimu, akimnadi mgombea ubunge jimbo la Korogwe Mjini, Wynjones Mwakolo, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kata ya Korogwe mkoani Tanga. 
Mgombea Mwenza kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Salum Mwalimu, akihutubia mkutano wa kampeni katika Kata ya Hedaru jimbo la Same Magharibi mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Hedaru wakimsikiliza mgombea wa Mwenza kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Salum Mwalimu.

Mgombea Mwenza wa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Salum Mwalimu, akimnadi mgombea ubunge jimbo la Same Magharibi, Gervas Mgonja, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kata ya Hedaru.


UCHAGUZI UKIFANYIKA LEO JPM ANASHINDA KWA ASILIMIA 88 - POLEPOLE

$
0
0
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndg Humphrey Polepole akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) mjini Chato, mkoa wa Geita, Ijumaa Septemba 11, 2020.
                                     
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndg Humphrey Polepole akiongea na wanahabari mjini Chato, mkoa wa Geita, Ijumaa Septemba 11, 2020.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndg Humphrey Polepole akiongea na wanahabari mjini Chato, mkoa wa Geita, Ijumaa Septemba 11, 2020.

Na Joachim Mushi

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Humphrey Polepole amesema kwa namna ambavyo mgombea wa nafasi ya Urais kupitia tiketi ya CCM, Rais Dk. John Pombe Magufuli anavyokubalika na wananchi tangu wameanza kampeni zao, wananchi wakipiga kura leo anaibuka mshindi kwa asilimi 88.

Ndg. Polepole ameyasema hayo leo mjini Chato, mkoani Geita alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni mapumziko yao mafupi kabla yakuendelea na kampeni baada ya kufanya kampeni kwa siku 10 mfululizo mikoa kadhaa wakinadi ilani ya CCM kwa wananchi maeneo hayo.

"...Yaani ikitokea kura zikapigwa leo hii, mgombea wetu ambaye pia ni Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anaibuka na ushindi kwa asilimia zaidi ya 88. Hii ni kutokana na mambo makubwa ya kihistoria ambayo amelifanyia taifa hili na namna alivyopokewa na kuungwa mkono na wananchi katika kampeni zake tangu tumeanza...," alisema Ndg. Polepole akizungumza na wanahabari.

Amesema mgombea wa CCM, Rais Dk. John Pombe Magufuli amefanya mambo mengi katika sekta mbalimbali tangu aingie madarakani jambo ambalo limeiwezesha nchi sasa kuingia katika orodha ya nchi ya kipato cha kati.

Alisema Serikali ya awamu ya tano mbali na kutoa elimu bure na kuboresha huduma za afya mara dufu kuanzia madawa, vifaa tiba, ujenzi wa zahanati, hospitali na vituo vya afya kuanzia ngazi ya kata, wilaya, mkoa, kikanda na taifa kwa ujumla mpango wa sasa kuleta huduma za bima kwa wananchi wote.

Aliwashangaa wanaopinga ujenzi wa viwanja vya kisasa vya ndege mikoa mbalimbali unaofanywa na Serikali ya JPM na kudai watu hao hawana nia njema na taifa. Aliongeza kuwa Serikali imenunua ndege ambazo zinapaswa kutoa huduma kwa Watanzania wote sasa ujenzi wa viwanja vipya vya kisasa vya ndege na ukarabati utawezesha ndege hizo kutoa huduma kila mkoa tofauti na hapo awali.

Amesema Serikali ya CCM tangu JPM aingie madarakani imejenga viwanja vye ndege vya kisasa takribani 11 mikoa mbalimbali na kukarabati baadhi, ikiwemo mikoa ya Tabora, Mtwara, Kigoma, Shinyanga na pamoja na Bukoba. Aidha alitolea mfano kuwa ujenzi wa uwanja wa ndege wa kisasa mkoani Mwanza umeufungua mkoa huo kibiashara za kimataifa jambo ambalo limeleta mabadiliko makubwa kiuchumi.

"...Kwa mambo makubwa aliyoyafanya mgombea wa nafasi ya Urais kupitia tiketi ya CCM, Rais Dk. John Pombe Magufuli yanamfanya Mtanzania mpenda maendeleo na mzalendo anayelitakia taifa letu maendeleo kumpigia kura ya ndio ili aendelee kufanya makubwa zaidi," alisema Polepole.

Umati wa wananchi wakimpokea mgombea wa nafasi ya Urais kupitia tiketi ya CCM, Rais Dk. John Pombe Magufuli njiani kabla ya kufanya mkutano wake wa kampeni.

Maelfu ya wananchi wakimsikiliza mgombea wa nafasi ya Urais kupitia tiketi ya CCM, Rais Dk. John Pombe Magufuli (hayupo pichani) kwenye moja ya mikutano yake ya kampeni mikoani.

Maelfu ya wananchi wakimsikiliza mgombea wa nafasi ya Urais kupitia tiketi ya CCM, Rais Dk. John Pombe Magufuli kwenye moja ya mikutano yake ya kampeni mikoani.

Asilimia 80 ya uharibifu wa misitu hufanyika katika ardhi za vijiji

$
0
0
Na Ghisa Abby,Lindi

Afisa toka Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) Shaban Mafita ameeleza kuwa asilimia 80 ya uharibifu wa misitu nchini hufanyika katika ardhi za vijiji na shughuli kubwa inayofanya uharibifu huo ni kilimo cha kuhama hama ambapo hekta 17.6 milioni za misitu zilizopo kwenye ardhi hizo za vijiji bado hazijarasimishwa kisheria.

Aidha afisa huyo amesema hekta 1.4 milioni pekee ndizo zilizorasimishwa huku hekta 3 milioni kati ya hekta hizo 17.6 zipo kwenye halmashauri za serikali za mitaa.

Ameeleza hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuutambulisha mradi wa Haki katika Misitu awamu ya pili wenye lengo la kampeni ya misitu kwa kila kijiji na hiyo ni baada ya kuona kuwepo kwa changamoto zinazotokea kwenye usimamizi shirikishi wa misitu ambayo inasimamiwa TFCG pamoja na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA).

Mafita amesema wakati Tanzania ikiwa na hekta 48.1 milioni sawa na asilimia 54.4 ya maeneo Tanzania bara, misitu inayohifadhiwa katika ardhi za vijiji ni hekta 22 milioni.

“Shughuli za uanzishwaji wa mashamba kupitia kilimo cha kuhama ndizo zimekuwa zikifanya uharibifu wa mazingira na hii ni takwimu kwa mujibu wa ripoti ya Nafoma na kwa kiasi kikubwa zinaonyesha kuwa hekta 460,000 zinaharibiwa kila mwaka na kwa kiasi kikubwa eneo hilo linatokana na kutorasimishwa hasa maeneo ya vijiji,”amesema Mafita.

Amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine katika masuala ya Misitu lazima itoe kipaumbele kwenye misitu ambayo haijarasimishwa ili iweze kurasimishwa na vijiji vinavyofanya usimamizi shirikishi ya misitu kwa pamoja isimamiee kwani imekuwa na manufaa kwa jamii kwa kupata mapato kupitia usimamizi na uvunaji endelevu ambao unafanyika kupitia utatibu wa uvunaji wanaouanzisha katika maeneo yao, ikiwa ni pamoja na fedha wanazozipata kufanyia shughuli za maendeleo kama ujenzi wa shule,madarasa na kupata bina za afya.

“Faida hizi za misitu tunataka kupeleka mbali kuona kwamba ile misitu ya hekta 17.6 milioni na yenyewe inasimamiwa katika utaratibu ili kunusuru misitu kuendelea kuharibiwa katika namna ambayo inaonekana kama uchomaji wa mkaa, uvunaji mbao na ukataji miti kiholela,”amesema.

Mafita amesema kampeni hiyo  isiishie kwa viongozi wa kiserikali lakini viongozi wa kisiasa wana nafasi kubwa ya kuhakikisha mafanikio ya usimamizi shirikishi wa misitu yanaingizwa katika Ilani na program za serikali ambazo zitachukua hatamu hivyo kwenye miaka mitano ya utekelezaji shughuli zinazohimizwa na mafanikio yaweze kuingizwa ili jamii ziweze kunufaika na misitu yao.

Naye Afisa Uraghabishi na Mawasiliano wa TFCG Revocatus Njau amesema kwa miaka miwili 2020 – 2021 TFCG inatekeleza mradi wa Haki Misitu kwa Kanda za Kusini, Kasikazini na Nyanda za Juu Kusini na shughuli ya mradi huo ni kuhamasisha kuhusu uhifadhi wa mistu ya vijiji, na kwamba tangu kuanzishwa kwa sera na sheria ya misitu namba 14 ya mwana 2002 imeweza kuleta mafanikio kwa vijiji zilivyorasimishwa na wanajamii wamekuwa wakiitunza misitu yao kutokana na kupatikana na faida wanayoipata na hiyo imeleta hamasa ya kuendelea kuhifadhi misitu.

“Lakini hii ambayo haijahifadhiwa tumeendelea kuhamasisha kwa sababu  misitu ambayo haijaifadhiwa imekuwa na migogoro kwa sababu haina mpango wa matumizi bora ya ardhi, hasa kwa migororo ya mipaka wafugaji na wakulima na masuala mbalimbali ambayo maeneo yameingiliwa kutokana na kutokuwa na mpangilio rasmi,”amesema Njau.

Meneja Mradi wa Kuongeza Usimamizi wa Misitu ya Jamii katika misitu ya Pwani amesema kwa kuangalia kiwango cha misitu ambayo haijahifadhiwa mradi utawezesha jamii kwenye halmashauri ya Mtama kwa vijiji 10 kuweza kuhifadhi na hekta kati ya 2,500 hadi 5,000 mpaka kumalizika kwa mradi hiyo ni katika kupunguza hekta ambazo hazijahifdhiwa.

“Katika uhifadhi huo tumeanza kusaidia jamii kufanya shughuli nyingine ili kuwajengea utayari jamii kushiriki uhifadhi wa misitu ikiwemo ya kuanzisha mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji na tumenza katika kijiji cha Nteni,”amesema.

Yahaya alisema jamii itasaidiwa kuweza kupima ardhi yao na itawezesha kila kijiji kwenye vijiji 10 kupata hati miliki za kimila na kila kijiji kitapata hati 150 sawa na hati 1500 kwa vijiji vyote kama sehemu ya jamii kujifunza kwamba uhifadhi wa ardhi unawasaidia vyema kupata faida moja kwa moja ikiwa ni pamoja na kupanda miti mbalimbali ya asili na matunda ipatayo 20,000.

MGOMBEA UDIWANI KATA YA MAKURUMLA ATOA AHADI YA KUTATUA KERO ZA WANANCHI KWA MUDA MFUPI

$
0
0

 NA ASHA MWAKYONDE

 
MGOMBE udiwani Kata ya Makurumla kwa tiketi ya Chama cha
Mapinduzi (CCM), Bakari Kimwanga ametaja vipaumble vyake  endapo atapata ridhaa ya kuchaguliwa na wananchi  kuiongoza kata hiyo.


Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kampeni zake
zilizofanyika katika viwanja vya Kwa Jongo Mburahati  mgombea huyo alisema akipata ridhaa ya wananchi atahakikisha chanagamoto za kijamii zinazowakabili wananchi wa kata hiyo zinapungua kwa kipindi cha muda mfupi.


Mgombea huyo alisema kata hiyo ina changamoto nyingi ambazo zinahitaji watu makini kuzitatua na lengo la chama hicho ni kuleta ufumbuzi wa muda mfupi kutatua changamoto hizo.
 

Alivitaja vipaumbele vyake kuwa ni elimu, afya, miundombinu, mikopo kwa akina mama, vijana na kwa watu wenye ulemavu.
Mgombea huyo alisema kwa upande wa sekta ya elimu miundombinu yake bado hairidhishi  hasa katika shule ya msingi Mianzini baadhi ya madarasha ni hatarishi kwa  afya za  watoto.


Alisema kituo cha Afya cha Mianzini bado kuna masononeko ya wananchi kutotoa huduma bora na kwamba endapo atachaguliwa atahakikisha vifaa tiba vinapatikana kwa wakati pamoja na madakrari. Kimwanga alieleza kuwa wakiangalia suala la uwekezaji wa mikopo inayotolewa  inaangalia undugu  hivyo endapo watapata ridhaa wataenda kusimamia asilimia 10 ya mikopo inayotolewa na Halmashauri.


"Tutasimamia mikopo hii iende kwa makundi ya akina mama, vijana na watu wenye ulemavu bila kuangalia undugu kama inavyotolewa kwa sasa tutatoa kwa wote na kila mtu afye na chake,"alisema.


Alisema kwa upande wa miundombinu watajenga kingo za mifereji inayosababisha mafuriko kwa baadhi ya maeneo na kwamba barabara zilizopo haziendani na hadhi ya watu wanaoishi katika kata hiyo.
 

Mgombea hiyo alieleza kuwa kukosekana kwa uongozi thabiti ni
kukosekana kwa uwajibikaji kwa watu waliopewa ridhaa  hivyo wanahitaji kuleta utabuzi ndani ya muda mfupi.


"Wananchi chagueni CCM mafiga matutu ili tuweze kuongea lugha moja ya maendeleo ya kata hii kupitia Rais, mbunge na diwani kero zenu nitazifikisha kwa kaka yangu Profesa Kitila Mkumbo ambaye atakuwa bungeni ili aweze kunisaidia," alisema.


Aliongeza kuwa wanaposema suala la kusukuma  mbele maendeleo linahitaji watu makini ili kuweza kutatua changamoto  hizo hivyo wananchi hao wakiwachagua madiwani  wote wa chama hicho  katika jimbo la Ubungo kutakuwa namaendeleo makubwa.


"Mkituchangua madiwani wote takaingia Halmashauri hakika maendeleo mtayaona maana tutafanikiwa kuwa na Meya anayetoka CCM hivyo fedha zote za miradi tutakuwa nazo, " alisema mgombea huyo.
 



CAPT
Mbombea Udiwani kwa tiketi ya CCM katika Kata ya Makurumula, Dar es Salaam, Bakari Kimwanga akiwaomba kura wananchi aliponadi sera za CCM katika Mkutano wa ufunguzi wa Kampeni za CCM, jana  katika Kata hiyo

KAMPENI ZA ACT-WAZALENDO KIGOMA

$
0
0


 Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa ACT-Wazalendo, Abdul Nondo, akihutubia mkutano wa ufunguzi wa kampeni za mgombea Ubunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.

Waziri Mkuu aipongeza NMB kuchangia Mil. 100 wagonjwa wa saratani

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi hundi ya sh. Milioni 100 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Maseru, (kushoto) wakati alipohitimisha  Mbio za NMB Marathon kwenye viwanja vya Mlimani City jijini Dar es salaam, Septemba 12, 2020. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Uwekezaji) Angellah Kairuki, wa tatu kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, wa pili kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sanlam  East Africa, Julius Magabe na wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB, Dkt.Edwin Mhede. Fedha hizo zilizotolewa na Benki ya NMB zitatumika kuwasaidia watoto wenye ugonjwa saratani wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Badhi ya washiriki wa Mbio za Kilomita 5 za NMB Bima Marathon 2020, wakianza mbio hizo jijini Dar es Salaam.

 

 

NA MWANDISHI WETU

 

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, ameipongeza Benki ya NMB kwa kutoa kiasi cha Sh. Mil. 100 kuchangia matibabu ya watoto wenye saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), huku akikiita kitendo hicho kuwa kinachopaswa kuigwa na wadau wa afya nchini.

 

NMB imetoa kiasi hicho Jumamosi Septemba 12, kikitokana na ada ya usajili wa washiriki wa Mbio za Kilomita 5 za NMB Bima Marathon 2020, zilizodhaminiwa na benki hiyo, zikilenga kutoa elimu ya bima, sambamba kuhamasisha mazoezi ya viungo kwa jamii.

 

Akizungumza wakati wa kupokea hundi ya kiasi hicho, Majaliwa alisema licha ya jitihada za Serikali katika kumaliza changamoto kwenye Sekta ya Afya, bado kuna uhitaji mkubwa miongoni mwa wagonjwa, hospitali na vituo vya afya na kwamba NMB imeliona hilo na kujitoa kusaidia.

 

‘‘Niwapongeze NMB kwa kuyatoa makusanyo ya Sh. Mil. 100 na kuchangia matibabu ya watoto wanaougua saratani. Hii maana yake ni kuwa mnaungana na kasi ya Serikali ya Rais John Magufuli sio tu katika kutatua changamoto za afya, bali pia kuhamasisha mazoezi.

 

‘‘Jamii isiishie hapa, mahitaji ya kitiba kwa wagonjwa mbalimbali ni mengi, kama ilivyo kwa hospitali zetu, vituo vya afya na zahanati zetu. Ndio maana natoa wito kwa wadau wa afya, zikiwemo taasisi na mashirika, kuiga mfano huu walioufanya NMB,’’ alisema Majaliwa.

 

Waziri Mkuu Majaliwa  Kassim Majaliwa, ametoa wito kwa Hospitali za Rufaa zinazotoa huduma kwa wagonjwa  wenye Saratani kutenga wodi  maalumu kwa ajili ya watoto wenye saratani.


Aliongeza kuwa mbio hizo zimekuja wakati muafaka, kwani zinaendana na mwezi maalum wa uhamasishaji na uelewa kuhusu magonjwa ya saratani kwa watoto duniani na kwamba matumaini yake ni kuwa hamasa iliyofanywa na NMB, itakuwa na mafanikio makubwa kwa jamii.

 

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, mbio za NMB Bima Marathon ni zao la ushirikiano wa kikazi baina ya NMB na mashirika ya bima nchini, ulioanzia Februari mwaka huu – pale benki hiyo ilipozindua huduma ya NMB BancAssurance.

 

‘‘Kwa ushirikiano huu, NMB sasa tunaweza kusambaza na kuuza bima kupitia matawi yetu yote na hivyo kuwafikia wananchi wenye uhitaji wa huduma za Bima kwa urahisi zaidi. Lengo kuu ni kusaidia kuleta huduma za bima karibu na Watanzania.

 

‘‘Kimsingi huduma hii imesaidia kusisimua soko la bima kwa kiwango kikubwa, ambako Watanzania hata wa vijijini, ambako huduma za NMB zinapatikana, sasa wanaweza kupata huduma za Bima kwa urahisi na haraka zaidi,’’ alisema Zaipuna.

 

Alitoa wito kwa wadau nchini kuunga mkono jitihada za Serikali na benki yake katika kuyajali makundi yenye uhitaji, kwa kujenga utamaduni wa kuchangia gharama za matibabu, sambamba na kuhamasisha umuhimu wa bima za afya kwa jamii.

 

Naye Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru, aliishukuru NMB kwa mchango wao kwa watoto wanaougua saratani na kwamba anaamini washiriki wa NMB Bima Marathon, watakuwa mabalozi wema wa utamaduni wa kusaidia makundi maalum.

Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>