Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU AONGOZA MAZISHI YA HAYATI BOMANI KWA NIABA YA RAIS DKT. MAGUFULI

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza mazishi ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hayati Mark Bomani kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli na amewataka Watanzania wamuenzi kwa kuuishi utumishi wake uliotukuka wakati wa kupindi chote cha uhai wake.

 

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Septemba 14, 2020) wakati alipowaongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Hayati Bomani kwenye viwanja vya Karimjee na baadaye katika mazishi yaliyofanyika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Serikali imepokea msiba huu kwa huzuni na mshtuko mkubwa.

 

“Wote sisi ni mashahidi wa mchango mkubwa wa Mzee wetu Hayati Mark Bomani alioutoa katika tasnia ya sharia na katika nafasi mbalimbali alizotumikia ndani na nje ya Tanzania. Alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa kwanza mzalendo, alisaidiana na Mwanasheria Mkuu wa kipindi hicho Roland Brown katika kutayarisha nyaraka zote za kisheria za Muungano.”

 

Waziri Mkuu amesemma kati ya mwaka 1965 hadi 1976 aliteuliwa kushika nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa kwanza mzalendo nafasi ambayo aliitumikia kwa uaminifu, uadilifu na umahiri mkubwa na alifanikiwa kufanya jitihada kubwa za kuhakikisha sekta ya sharia inaimarika.

 

Amesema Hayati Bomani aliwezesha kupatikana kwa Jaji Mkuu wa Tanzania kutoka nchini Trinidad and Tobago na Mahakimu kutoka Nigeria ili kupunguza uhaba wa watendaji Waafrika katika mhimili wa Mahakama.

 

Amesema Watanzania watamkumbuka Hayati Bomani kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kamati mbalimbali zilizolenga kupitia sheria na keleta mabadiliko katika sheria. Alikuwa Mjumbe wa Tume ya Rais iliyoundwa kutoa mapendekezo ya mfumo wa demokrasia wa chama kimoja.

 

Pia, Hayati Bomani alikuwa alikuwa Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi, Mwenyekiti wa Tume ya Utangazaji, Mwenyekiti wa Kamati ya Kupitia Sera ya Madini ambayo iliwezesha kutungwa kwa sheria ya madini. Alikuwa mmoja wa Wajumbe wa Bodi ya Kwanza ya Udhamini ya CCM hadi umauti ulipomkuta.

 

Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasihi wanafamilia na waombolezaji wote waendelee kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo na kila mmoja kwa Imani yake wamuombe Mwenyezi Mungu ampumzishe Hayati Bomani mahala pema.

 

Hayati Bomani alizaliwa Januari 2, 1932 Bunda mkoani Mara na alikuwa kati ya watoto 10 wa Mzee Bomani na alisoma shule ya msingi Mwamanyili, Nassa ambapo baba yake mzazi ndiye alikuwa mwalimu wake. Alipomaliza shule ya msingi alijiunga na shule ya Wavulana ya Bwiru ambapo alisoma hadi darasa la 10.

 

Alifaulu na kujiunga na shule ya sekondari ya wavulana ya Tabora na ambako pia alifaulu  na kuchaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Makerere cha nchini Uganda mwaka 1953 hadi 1957 ambako alipata shahada ya kwanza ya masuala ya Siasa, Uchumi na Historia. Mwaka 1957 hadi 1958 alijunga na Taasisi ya Ustawi wa Jamii ya The Hague na alitunukiwa diploma ya masuala ya jamii.

 

Mwaka 1958 hadi 1961 alijiunga na chuo Kikuu cha London nchini Uingereza na kutunukiwa shahada ya kwanza ya sheria. Hayati Bomani mwaka jana aliugua na kupata matibabu nchini Afrika Kusini na India, hali yake ilikuwa nzuri na aliweza kurejea katika kazi alizozipenda za sharia lakini hali yake ilibadilika ghafla na alifariki dunia Septemba 10, 2020 na ameacha mke, Watoto watatu na wajukuu sita.

 

Mazishi hayo yamehudhuliwa na viongozi mbalimbali akiwemo Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi na mkewe Mama Sitti, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete, Jaji Mkuu Mstaafu, Mohamed Chande Othman, Jaji Mstaafu Damian Lubuva, Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Samatta na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Adelardus Kilangi. 

 


Waliofanya vizuri masomo ya sayansi wapewa tuzo

$
0
0


NA ASHA MWAKYONDE

 
KATIBU  Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto profesa Mabula Mchembe amelitaka Baraza la Mitihani Tanzania NECTA kutoa mwendelezo wa taarifa za wanafunzi wanaofanya vizuri kitaifa hata baada ya kumaliza masomo yao yote  elimu ya juu ili kusaidia kujua maendeleo yao na mchango wao katika ujenzi wa Taifa.


Akizungumza  jijini Dar es Salaam Septemba 14, mwaka huu wakati wa ghafla ya utoaji tuzo za wanafunzi na waalimu bora kitaifa  mwaka 2018 na 2019 katika masomo ya kemia,fizikia na baoilojia kidato cha nne na sita iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa serikali, amesema  kuna umuhimu wa kujua maendeleo ya vinara hao hata baada ya kumaliza masomo.


Mchembe ameshauri  shule kuongeza jitihada za kuboresha mazingira ya kusomea wanafunzi ikiwemo maabara za kujifunzia kwa kuhakikisha vifaa na kemikali zinazohitajika zinakiwepo za kutosha ili wanafunzi waeweze kusoma kwa vitendo zaidi na zaidi na idadi ya wanaofaulu kwa kiwango
cha juu kuongezeka.
 

Naye Mkemia mkuu wa serikali Dkt. Fedelice Mafumiko amesema  toka kuanza kwa tuzo hizo mwaka 2007 mpaka sasa wameshatoa tuzo kwa wanafunzi 288 na waalimu 22,ambapo utoaji wa zawadi hizo umekuwa ukiongeza moralali kwa wanafunzi na waalimu kuendelea kufanya vizuri
zaidi.


Amesema kuwa wanafunzi waliotunukiwa tuzo ni 36 na walimu wao 6 hivyo kufikisha jumla ya wanafunzi 288 na walimu 22 tangu kuanza kwake.


Dkt. Mafumiko amesema kuwa lengo la utoaji tuzo hizo kwa masomo hayo ni kuwashawishi wanafunzi wengi kupenda masomo ya sayansi ili kusaidia taiafa kutatua changamoto za majanga mbalimbali yanayotokea ikiwamo la ajali ya moto, maji. "Niwahakikishie wananfunzi mliotunukiwa tuzo za vyeti siku hii ya leo ni kumbukumbu tosha ya historia ya taalamuma zenu muendelee kuongeza juhudi ya kusoma kwa bidii mfike mbali  "amesema Dkt. Mafumiko.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi wa mamlaka ya mkemia mkuu wa serikali   Profesa Hellen  Jason amewahimiza watoto wakike kusoma masomo ya sayansi na kuondokana na kasumba iiyopo jamii kuwa masomo hayo ni magumu huhusani kwa mabinti. 

"kumekuwa na kasumba kubwa sana kwa jamii kuwaambiwa wanafunzi wa jinsia ya kike kuwa hawawezi kusoma masomo ya sayansi ni magumu kufaulu kwa ni vigumu mimi nasema kasumba hiyo iondoke mara moja wanawake wanaweza kusoma masomo ya sayansi, "amesema Profesa Heleni.


Kwa upande wake mwananfunzi wa shule ya sekondari Tabora aliyemalizwa mwaka jana na kushika nafasi ya nne kitaifa kwa wasichana Vanesa Mtabana amesema kufanya vizuri ni kutokana na juhudi za mtu binafisi
na sio shule.
 

Amesema anashukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuwekeza zaidi katika elimu ambapo hadi sasa shule za serikali zinafanya vizuri. "Walimu pia wanamchango mkubwa katika kusukuma maendeleo ya wanafunzi kimasomo kwani juhudi na matunda yao zinaonekana, " amesema Vanesa.

MGOMBEA MWENZA CCM AHUTUBIA MADABA SONGEA

$
0
0

 Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia  Wanachama wa Chama cha Mapinduzi na Wananchi Jimbo la Madaba  katika Kijiji cha Mtyangimbole na Limbuka kwenye mkutano wa kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM katika Uwanja wa Wilaya kijiji cha Limbuka Songea Mkoani Ruvuma leo Septemba 15,2020.  
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM na Wananchi wa Jimbo la Madaba Wilayani Songea  wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akiwahutubia kwenye Mkutano wa Kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM katika Uwanja wa Wilaya Kijiji cha Madaba Songea Mkoani Ruvuma leo Septemba 15,2020. (Picha  na Ofisi ya Makamu wa Rais)
      

HUDUMA KWA WAGONJWA WA SIKOSELI ZAANZA KUTOLEWA RASMI KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA BAGAMOYO

$
0
0

Dk. Agnes Jonathan ambaye ni mratibu wa huduma ya Sikoseli kutoka Chuo cha Afya Muhimbili (MUHAS), akitoa elimu kwa baadhi ya wagonjwa waliokwenda kupatiwa matibabu juu ya ugonjwa wa sikoseli sambamba na kuwaelekea namna ya wazazi kuwahudumia watoto wao pindi wanapokuwa na ugonjwa huo.

 Dk. Agnes Jonathan ambaye ni mratibu wa huduma ya Sikoseli kutoka Chuo cha afya Muhimbili (MUHAS) akitoa elimu kwa baadhi ya wagonjwa waliokwenda kupatiwa matibabu juu ya ugonjwa wa sikoseli sambamba na kuwaelekea namna ya wazazi kuwahudumia watoto wao pindi wanapokuwa na ugonjwa huo.

 

 

NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO

 

Jopo la wataalam wa Afya kutoka Chuo cha Afya Muhimbili (MUHAS) kupitia program ya ya selimundu wakiongozwa na Dk. Agnes Jonathan, hatimaye  wameanza rasmi  zoezi la utoaji wa  huduma katika kliniki maalum kwa wagonjwa wa sikoseli katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo iliyopo Mkoa wa Pwani.

 

Lengo la kuanzishwa kwa utaoji wa huduma hiyo imekuja ikiwan imepita  miezi miwili tu tangu Serikali kuzindua mwongozo wa Taifa wa matibabu kwa watu wenye ugonjwa wa sikoseli mnamo Juni 19,2020  kwa lengo la kuweza kusaidia kutoa huduma kwa wagonjwa mbali mbali wanaosumbuliwa na sikoseli katika Wilaya hiyo.

 

Katika kukabiliana na ugonjwa huo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu aliagiza  kuanzishwa kwa kliniki maalumu za kuchunguza ugonjwa huo katika ngazi ya wilaya na mikoa ili kuhakikisha watu wengi hasa watoto wanafikiwa kwa urahisi kupatiwa huduma hiyo.

 

Akizungumza katika uzinduzi huo Kaimu Mganga mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mohamed Farah alisema kwamba anashukuru sana kwa kuzinduliwa kwa mpango huo ambao utaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa wagonjwa ambao wamekuwa wanasumbulia kwa kipindi kirefu  na kusumbuliwa kwa  sikoseli.

 

“Kwa kweli napenda kutoa shukrani zangu za kipekee kwa kuanzishwa kwa utoaji wa huduma hii katika hospitali yetu ya Bagamoyo kwani kutaweza kutoa fursa ya kipekee kwa wananchi wa Bgamoyo kupitia wataalamu ambao wamefika kupata huduma ya matibabu  ya sikoseli ambapo wataondoka  na changamoto ya kwenda kutibiwa sehemu nyingine,”alisema Dk. Farah.

Pia alifafanua kuwa kuzinduliwa kwa kliniki hiyo katika Hospitali ya Bagamoyo kupitia mpango ambao umeanzishwa na serikali kutawapa urahi kwa wagonjwa mbali mbali ambao wanasumbulia na sikoseli kupata matibabau yao kwa uharaka zaidi kuliko na ilivyokuwa katika  kipindi cha mwanzoni.

Naye mratibu wa program ya sikoseli kutoka Chuo kikuu cha afya Muhinbili (MUHAS) Dk.Agnes Jonathan alibainisha kwamba jamii hususan wazazi kuwapelekea watoto wao mapema kupatiwa matibabu ya sikoseli endapo watabaini kuwa anadalili za ugonjwa huo lengo ikiwa ni kumpatia matibabu ya haraka.

“Kumekuwepo kwa baaadhi ya jamii kuwa na mwennendo wa tabia ya kuwa na dhana ptofu kuhusiana na ugonjwa huu wa sikoseli lakini ni vizuri tukajiwekea utaratibu wa kuwapeleka wagonjwa hospitalini ili waweze kupatiwa matibabu ikiwemo sambamba na kwenda kupima afya zao mara kwa mara,”alisema Dk. Agnes.

Bi. Arafa Said ni Mwanzilishi na Rais wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali inayojulikana kwa jina la Sickle cell Disease Patiebts Community of Tanzania amewaomba wazazi na kuwatia moyo wenye watoto ambao wanasumbuliwa na ugonjwa huo waondoe hofu na mashaka kwani wakizingatia ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya wanawezeza kusihi maisha marefu bila tatizo.

Mwongozo wa Taifa wa matibabu kwa watu wenye ugonjwa wa Sikoseli ulizinduliwa rasmi Juni 19 mwaka huu na Waziri wa afya maendeleo jinsia wazee na watoto Mh. Ummny Mwalimu katika hospitali ya Taifa ya muhimbili ukiwa na kauli mbiu inayosema “Huduma bora kwa kila mhitaji, chukua hatua panua wigo.

MGAWE - CHADEMA TUNAENDA KUMALIZA CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI WA MAJI JIMBO LA KIBAMBA

$
0
0


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika (kulia) akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Kibaha, Ernest Mgawe, akimwombea kura kwa wananchi  wakati wa ufunguzi wa kampeni zilizofanyika katika viwanja kimara stop over.


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kibamba kupitia CHADEMA, Ernest Mgawe, akizungumza jambo na kuwaomba  wananchi ridhaa ya kumchagua wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni hizo ambazo zilihudhuliwa na viongozi mbali mbali kutoka ngazi za chini hadi ngazi ya Taifa kwa ajili ya kuomba kura.

 

 

NA VICTOR MASANGU, MBEZI 

 

Mgombea wa  ubunge katika jimbo la Kibamba Ernest Mgawe kupitia tiketi ya Chadema  amesema kwamba  endapo atapata nafasi ya kuchaguliwa na wananchi  katika uchaguzi  wa mwaka huuu atahakikisha kwamba analivalia njuga changamoto ya  upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama ili kuwaondolea   wananchi kero na adha kubwa ya kutembea umbari mrefu kwenda kutafuta maji hususan kwa wakinamama.

Mgawe aliyasema hayo wakati wa uzinduzi rasmi wa kuanza kwa kampeni yake iliyofanyika katika viwanja vya kimara stop over kwa ajili ya   kuwaomba ridhaa wananchi kumpatia nafasi hiyo ili kuwawakilisha bungeni kwa ajili ya kupeleka kero  na  changamoto mbali mbai  ambazo zinawakabili lengo ikiwa kuzitafutia ufumbuzi.

Aidha Mgombea huyo alisema kwamba lengo lake kubwa ni kushirikiana na viongozi wake  kwa lengo la kuweza kuhakikisha kwamba wanatatua changamoto na kero mbali mbali ambazo zinawakabili wananchi wake ikiwemo kusimamia miradi ya maendeleo katika sekta ya maji, miundombinu ya barabara pamoja na mambo ya afya.

“Katibu wangu wa Chama Mnyika ameongelea mambo mbali mbali lakini nipende kuwaambia wananchi kitu kikubwa ambacho kinatakiwa ni kunichagua mimi ili niwe Mbunge wa Jimbo la Kibamba na zile changamoto mbali mbali za mambo yanayohusina na sekta ya ardhi upatikanaji wa maji safi na salama ikiwemo suala la asilimia 10 ambazo zinatolewa katika makundi ya vijana, wakinamama na walemavu zinatolewa kwa usawa ili ziweze kuwanufaisha wate,”alisema Magawe.

Katibu Mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Taifa  (CHADEMA) John Mnyika amewataka wagombea wa nafasi za udiwani na ubunge  endapo wakishinda katika uchaguazi mkuu wa mwaka huu kuhakikisha wanasikiliza kero na changamoto mbali mbali ambazo zinawakabilia wananchi katika sekta mbali mbali ikiwemo suala la urasimishaji wa ardhi ili wananchi wapate hati zao miliki.

“Sasa hivi ndugu zangu tupo kwenye kampeni na tunaelekea kipindi cha uchaguzi kwa hiyo mimi nilipokuwa Mbunge wa Jimbo la Kibamba nililete mabadiliko makubwa ingawa kuna baadhi ya vitu vingine ilikuwa bado sijavimalizia ikiwemo ule mpango wa urasimishaji wa ardhi kwa wananchi na kupata hati zao hivyo ninamuomba sana Mgawe atachagulia jambo hili alifanyia kazi haraka,”alisema Mnyika.

Naye mmoja wa watoto wa Mgombea ubunge huyo Preshezeli Mgawe  hakusita kuonyesha hisia alizonazo mara baada ya kupanda  jukwaani na kumwombea kura baba yake mzazi na kuwaomba wananchi kumuamini kwani alipokuwa diwani wa kata ya kibamba aliweza kuleta chachu ya maendeleo kwa wananchi wake.

 

“Nimepanda katika jukwaa hili mimi napennda kumwombea baba yangu mpendwa haweze kuchaguliwa katika nafasi ya Ubunge jimbo la Kibamba ili aweze kushirikiana na viongozi na wananchi ili kuweza kuleta maendeleo nina waombeni sana kumpatia baba yangu kura nyingi ili aweze kuwaletea mabadiliko zaidi,”alisema Mtoto huyo.

Kwa upande wake Meneja wa mgombea huyo  Hunfrey Sambo aliwataka wanachama wa Chadema kuhakikisha wanazingatia sheria na taratibu zote  wakati wa kipindi cha kampeni pamoja na kuelekea katika uchaguai mkuu na kuwahimiza kwamba wawachagua viongozi wa nafasi zote tatu kuaniza udiwani, Ubunge na nafasi ya Urais kupita tiketi ya Chadema.

MAELFU WAJITOKEZA KUMLAKI MGOMBEA MWENZA WA CHADEMA 2020

$
0
0

 

Mgombea wa nafasi ya umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Mhe. Salum Mwalimu, akipanda jukwaani kuhutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Monduli leo Septemba 15, 2020.
 

Mgombea wa nafasi ya umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu, akihutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Monduli leo Septemba 15, 2020.


Mgombea wa nafasi ya umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu, akihutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Monduli leo Septemba 15, 2020.

Mgombea wa nafasi ya umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu, akimnadi mgombea ubunge jimbo la Monduli, Cecy Ndossi, leo Septemba 15, 2020.
Mgombea wa nafasi ya umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Mhe. Salum Mwalimu, akimnadi mgombea ubunge jimbo la Monduli, Cecy Ndossi, leo Septemba 15, 2020.
Mgombea ubunge jimbo la Monduli, Cecy Ndossi, akizungumza wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Mto wa Mbu, leo Septemba 15, 2020.
Baadhi ya viongozi wa CHADEMA wakiwa katika mkutano wa kampeni jimbo la Monduli.

Ulinzi ukiwa umeimarishwa.
Baadhi ya viongozi wa CHADEMA wakifuatilia mkutano wa kampeni za mgombea nafasi ya umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Salum Mwalimu uliofanyika katika jimbo la Monduli.

Mgombea wa nafasi ya umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu, akizungumza na wakazi wa Karatu Mjini baada ya kusimamisha msafara wake wakati akielekea kuhutubia mkutano wa kampeni katika viwanja vya Bassodawishi jimbo la Karatu mkoani Arusha leo Septemba 15, 2020.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa CHADEMA.

Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa CHADEMA.
Mgombea wa nafasi ya umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Mhe. Salum Mwalimu, akihutubia mkutano wa kampeni katika viwanja vya Bassodawishi  jimbo la Karatu mkoani Arusha leo Septemba 15, 2020.
Mgombea wa nafasi ya umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Mhe. Salum Mwalimu, akihutubia mkutano wa kampeni katika viwanja vya Bassodawishi  jimbo la Karatu mkoani Arusha leo Septemba 15, 2020.
Diwani wa Kata ya Endamararieck jimbo la Karatu akiomba kura.
Mgombea wa nafasi ya umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Mhe. Salum Mwalimu, akimnadi mgombea ubunge jimbo la Karatu, Cecilia Paresso, uliofanyika katika viwanja vya Bassodawish.

Mgombea Urais kupitia tiketi ya CCM Rais Dkt. Magufuli akizungumza na Wananchi wa Muleba mkoani Kagera

$
0
0

Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya Wananchi wa Wilaya ya Muleba mkoani Kagera leo tarehe 15 Septemba 2020.

Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya Wananchi wa Wilaya ya Muleba mkoani Kagera leo tarehe 15 Septemba 2020.



Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya Wananchi wa Wilaya ya Muleba mkoani Kagera leo tarehe 15 Septemba 2020.
 Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya Wananchi wa Wilaya ya Muleba mkoani Kagera leo tarehe 15 Septemba 2020.
 Sehemu ya Wananchi wa Muleba mkoani Kagera wakishangilia mara baada ya Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili Muleba mjini leo tarehe 15 Septemba 2020.

Wanahabari watakiwa kutoa habari sahihi za Uchaguzi

$
0
0

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa Uchaguzi Dkt. Wilson Mahera akizungumza mbele ya Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni wakati akifungua Mkutano kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

 

Na Asha Mwakyonde
 

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka watoa huduma ya habari mitandaoni kuhakikisha kuwa vyombo vyao haviwi chanzo cha kuleta taharuki ndani ya jamii kwa kutoa taarifa zisizokuwa na uhakika.


Akizungumza katika warsha  iliyofanyika
jijini Dar es Salaam kwa watoa huduma hao, Mkurugenzi wa Tume hiyo Dkt. Wilson Mahera amesema njia muafaka ya kuepukana kusambaza  taarifa zisizo kuwa sahihi ni kuzingatia misingi ya maadili ya kazi zao.


Mkurugenzi huyo amesema kuwa Tume taari imeshafanya maandalizi mbalimbali ya uchaguzi  na kwamba ili zoezi hilo lifanikiwe  kwa kiwango kikubwa linategemea  ushirikiano wa wanahabari.
 

"Nitoe rai kwenu watoa huduma za mtandaoni kutenda haki sawa kwa vyama vyote na kuhakikisha mnawapa wagombea nafasi ya kutangaza na kunadi sera na ilani za vyama vyao," amesema.


Aidha amesema NEC bado inaendelea kushughulikia rufaa walizokatiwa wagombea kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu za uchaguzi na sio kufuata matakwa ya mtu.


Sambamba na hayo amesema katika maandalizi ya uchaguzi mwaka huu hakukuwa na marekebisho ya yeyote ya sheria za uchaguzi bali wamefanya maboresho ya kanuni za uchaguzi wa Rais na wabunge na kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa (madiwani) kwa mwaka 2020.
 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Habari na Mawasiliano ya Tume ya Uchaguzi NEC Asina Omari amewataka wamiliki wa mitandao ya Kijamii kuhakikisha taarifa wanazozitoa zinatoka katika vyanzo husiki.


"Ni muhimu kupata uhakika zaidi wa taarifa kabla ya kuandika taarifa ili kuepusha kusambaa kwa taarifa zisizo za kweli ambazo zinaweza kuleta taharuki ndani ya jamii" amesema Mwenyekiti Asina.


Aidha amesema watoa huduma ya Habari  mitandaoni ya Kijamii wanajukumu la kuelimisha wengine na pia kujielimisha ikiwemo kujua msingi ya habari hizo pamoja na kufuata sheria na kanuni zake ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea pale ambapo jamii itapata taarifa ambazo
sio sahihi.
 

Naye mshiriki wa mafunzo hayo mmiliki wa mtandao wa habari kutoka mkoani Kahama Shija feslishiani amesema elimu kwa waandishi wa habari za mitandao ya Kijamii ni muhimu kutolewa kutokana na idadi kubwa ya watu kupata taarifa mbalimbali kupitia mitandao hiyo.

 

Hata hivyo amesema elimu hiyo isipotolewa kwa wahusika inaweza kusababisha madhara makubwa kutokana na taarifa zake kusambaa kwa haraka na kwa idadi kubwa ya watu.


MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA KAMPENI - WILAYA YA MKALAMA

$
0
0

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Singida watafakari ni aina gani ya kiongozi wanamtaka aiongoze nchi hii.

 

Ametoa wito huo leo (Jumanne, Septemba 15, 2020) wakati akizungumza na wananchi waliohudhuria mkutano wa kuwanadi wagombea wa CCM uliofanyika kwenye viwanja vya CCM, kata ya Ilongero,  wilayani Singida.

 

"Uongozi wa nchi siyo jambo la mchezo, siyo jambo la kujaribiwa wala haliendi kwa upepo na ushabiki. Ni lazima mkae na kutafakari ni nani anafaa kuongoza nchi hii," amesema na kuongeza: “Tukae tuangalie tulipo na tunapotaka kwenda. Tujiulize je, ni nani anaweza kutupeleka huko?”

 

Amewataka wakazi hao wajihadhari na wagombea ambao wanatumia majukwaa kuanza kuwatukana wenzao. "Huu siyo wakati wa kutukanana bali ni wakati wa kuelezea sera na mambo gani atawafanyia."

 

Ametumia fursa hiyo kuwaomba wakazi hao wamchague Dkt. John Pombe Magufuli ili aongoze tena kwa miaka mitano na aweze kumalizia kazi zilizopangwa na CCM kwenye Ilani yake.

 

"Nawaomba wana-Ilongero, wana-Singida Kaskazini na wana-Singida wote ikifika tarehe 28 Oktoba mchagueni Dkt. Magufuli. Sababu za kumuombea kura ni nyingi hasa kutokana na kazi kubwa aliyoifanya kwa nchi hii. Wote mmeona na kusikia yaliyofanyika kwenye maeneo yenu."

 

"Yeye ni mzuri wa kutabiri na kuyapangilia na kuyafuatilia. Yeye ni mzuri wa kutambua kero za wananchi wake na kuzitatua. Amejipambanua sana na kuwasihi wasaidizi wake wazingatie kuwatumikia Watanzania. Sote tumeona, maendeleo yaliyopatikana ndani ya miaka mitano hayajapata kutokea," amesema. 

 

Pia alitumia fursa hiyo kuwaombea kura, mbunge mteule wa jimbo la Singida Kaskazini, Bw. Ramadhani Ighondo na mgombea udiwani wa kata ya Ilongero, Bw. Issa Mwiru.

Wakati huohuo, Mheshimiwa Majaliwa amempokea aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Singida, Bw. Frank Petro Akunay ambaye ameamua kuhamia CCM.

 

Bw. Akunay amehamia CCM akiambatana na mkewe, Betina Ibrahim pamoja na mdogo wake Bw. Daniel Petro Akunay. 

 

Akizungumza katika mkutano huo, Bw. Akunay alisema ameamua kurudi nyumbani kwa sababu zamani alikuwa CCM lakini alipotea njia.

 

"Nimeamua kurudi nyumbani na nitachanja mbuga kuhakikisha CCM inashinda sababu mimi ni mtu wa field. Hapa Singida Kaskazini tuna vijiji 84, vitongoji 435 na kata 21. Ninavijua vyote. Nakuhakikishia tutashinda kwa asilimia 98 sababu sijarudi kwa bahati mbaya," alisisitiza.

 

"Tuna uhakika wa kupata ubunge kwani anayegombea hatusumbui kabisa. Kwa madiwani, tumebakiza kata 19 kwani wawili walishapita bila kupingwa."

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi   nakala ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 mgombea ubunge wa CCM wa jimbo la Iramba Mashariki (Mkalama), Isack Francis, katika mkutano wa kampeni, uliyofanyika kwenye viwanja vya Stendi Gumanga, mkoani Singida, Septemba 15, 2020. Kulia ni Diwani wa Kata ya Gumanga, James Mkwega. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Mkalama wakati akiwahutubia, katika mkutano wa kampeni, uliyofanyika kwenye viwanja vya Stendi Gumanga, mkoani Singida, Septemba 15, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Mkazi wa Mkalama, Bi. Grace Andrew akisoma Ilani ya CCM, mbele ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati alipowahutubia wananchi, katika mkutano wa kampeni, uliyofanyika kwenye viwanja vya Stendi Gumanga, mkoani Singida, Septemba 15, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

MGOMBEA MWENZA WA CHADEMA AHUTUBIA MKUTANO WA KAMPENI MKOA WA MANYARA

$
0
0

 

Kaimu Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Nyanki Emmanuel, akizungumza katika mkutano wa kampeni kabla ya kumkaribisha mgombe wa nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Salum Mwalimu katika viwanja vya Mbulu Mjini, mkoani Manyara.

MGOMBEA URAIS WA CCM RAIS DKT MAGUFULI AUNGURUMISHA SERA MBELE YA MAELFU YA WANANCHI MJINI BUKOBA

$
0
0

Wasani wa TMK wakiwa na alama kuu za CCM bnaada ya kutumbuiza kwenye mkutano wa kampeni viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba leo Septemba 16, 2020.

Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi ambaye ndiye
Mwenyekiti wa Chama hicho Tawala na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na maelfu kwa maelfu ya wananchi katika mkutano wake wa kampeni  katika viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba leo Jumatano Septemba 16, 2020.
Maelfu kwa Maelfu ya Wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa
Chama cha Mapinduzi ambaye ndiye Mwenyekiti wa Chama hicho Tawala na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia  katika mkutano wake wa kampeni  katika viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba leo Jumatano Septemba 16, 2020.

Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi ambaye ndiye Mwenyekiti wa Chama hicho Tawala na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mbunge wa Bukoba mjini na Waziri wa Maliasili na Utalii Mstaafu Balozi Khamis Juma Suedi Kagasheki akimnadi Bw. Stephen Byabato (aliyejishika mikono) kugombea ubunge wa jimbo hilo huku Meya Mstaafu wa Manispaa ya Bukoba Dkt. Anatory Amani (kulia) akingoja kufanya hivyo katika viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba leo Jumatano Septemba 16, 2020.

Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi ambaye ndiye Mwenyekiti wa Chama hicho Tawala na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo Bukoba Vijijini Mhe. Jason Rweikiza huku wabunge wateule wa CCM Viti maalum wakingoja zamu zao baada ya kuhutubia maelfu kwa maelfu ya wananchi katika mkutano wake wa kampeni  katika viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba leo Jumatano Septemba 16, 2020.

Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi ambaye ndiye Mwenyekiti wa Chama hicho Tawala na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaga baada ya kuhutubia maelfu kwa maelfu ya wananchi katika mkutano wake wa kampeni  katika viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba leo Jumatano Septemba 16, 2020.

NEC YATANGAZA UAMUZI WA RUFAA 67 ZA WAGOMBEA UBUNGE NA UDIWANI NA KUWAREJESHA WAGOMBEA 31

$
0
0

 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera Charles akisoma taarifa kwa umma kuhusu rufaa za wagombea Ubunge na Udiwani Jijini Dar es Salaam leo tarehe 16 Septemba 2020.

Wananchi waishukuru Serikali baada ya kusambaziwa maji vijijini

$
0
0


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo (kulia) akiongea na baadhi ya wataalamu baada ya kuona ujenzi wa tenki la maji katika mradi wa P4R katika kata ya Mtowisa.

 

Na Mwandishi Wetu, Rukwa 

 

Wananchi wa vijiji vya Ng’ongo na Mtowisa katika Kata ya Mtowisa, Wilayani Sumbawanga, Mkoani Rukwa wameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli baada ya mradi wa maji wa lipa kulingana na matokeo (P4R) katika vijiji vinne vya Kata ya Mtowisa utakaohudumia wakazi zaid ya 11,000.

Wanachi hao wamesema kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakipata shida ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji hali ambayo imekuwa ikiwazuia kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo na hivyo ukamilifu wa mradi huo ambao umegharimu Zaidi ya shilingi milioni 464 utakuwa mkombozi kwa wananchi wa kata hiyo.

Abedi Saidi ni Mkazi wa Kijiji cha mtowisa aliyekuwa akitembea kwa masaa kadhaa kutafuta maji alisema, “Ni mbali kutoka Mtowisa hadi hapa Ng’ongo kuna kaumbali kidogo kwa miguu ni masaa mawili, mradi huu ukikamilika wananchi watafurahi sana, kwasababu mradi waliokuwa anatumia ni wa zamani halafu umechakaa yani watu wanahangaika sana, yaani huu mradi tumeufurahia na tutautunza sana.”

Aidha, Mwanakijiji Christian Kapele aliorodhesha faida zitakazopatikana baada ya mradi huo kuisha ikiwemo kupata maji ya uhakika katika hospitali mpya ya Wilaya Sumbawanga iliyopo katika kata ya Mtowisa Pamoja na kufikisha maji katika vijiji vinne ambavyo kwa muda mrefu vimekuwa vikihangaika kutafuta maji.

“Tunamwombea Muheshimiwa Magufuli, Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wanakijiji wa Ng’ongo tunaahidi kwamba tutafanya chini na juu apite nafasi kwa kura zote ili aweze kutuendeleza kwenye hii miradi yet una tunashukuru sana huyu mzee wetu ametusaidia maji katika kata yetu, na umeme na hivyo tunamuombea aweze kushinda katika uchaguzi huu,” Alisema.

Wakati alipomaliza kutemebelea mradi huo wa P4R Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewasisitiza wananchi kuendelea kutunza vyanzo vya maji kwani ndio uti wa mgongo wa maendeleo ya wananchi kwakuwa maji hayo hayatumiki tu majumbani lakini pia yanatumika katika mradi wa skimu ya umwagiliaji katika kata hiyo ya Mtowisa.

“Niwaombe wanakijiji wa vijiji hivi vinne watunze mradi huu, watunze mazingira, msifugie na kulisha katika vyanzo hivi, lakini pia huko juu kwenye vijiji vilivyopo kweny ukanda wa Sumbawanga watunze vyanzo vya maji wasichome misitu hovyo, wasifyeke misitu wala wasifuge katika maeneo ya vyanzo vya maji, vinginevyo watu wanaoishi katika bonde hili la ziwa Rukwa watapata athari kubwa ya kutopata maji safi na salama lakini pia ziwa Rukwa litakuwa katika hatari ya kutoweka, tutunze vyanzo ili maji yatutunze,” Alimalizia.

International Israeli-based NPO sets a positive pulse for children’s cardiac care in Tanzania

$
0
0

  

JKCI-Dar-es-Salaam


Tanzania, 16 September 2020– Congenital heart disease (CHD) is an enormous problem in low and middle-income countries, and particularly in sub-Saharan Africa, where children who are afflicted may struggle to receive the proper treatment. The journal Frontiers in Pediatrics reports that there is an estimated 500,000 children born in Africa with CHD each year, with a major proportion in sub-Saharan Africa.

Rheumatic heart disease (RHD) is the leading cause of acquired heart disease and is an ongoing concern in sub-Saharan Africa, affecting especially the younger population. Proper treatment is essential to improve the outcomes for these children, as both conditions contribute substantially to morbidity and mortality during infanthood and childhood. However, treatment for conditions like CHD and RHD can be prohibitively expensive for families without governmental or humanitarian organisations being involved.

Microsoft Israel has been working closely with the entire healthcare industry to provide new cloud-based solutions to meet the hospitals and HMO’s specific needs, with activities including everything from collaboration to Data, Machine Learning and AI solutions. The solutions provide better collaboration, facilitate remote work, making information accessible for healthcare workers, patients and citizens, and innovating the entire healthcare system. During the COVID-19 pandemic, there has been a focus on providing remote work as well as remote patient care for healthcare facilities.

With a footprint spanning over 60 countries across the Middle East and Africa, Asia, Eastern Europe and the America’s, Save a Child’s Heart (SACH) has treated more than 5,000 children for congenital and rheumatic heart disease. Founded by Dr Ami Cohen in 1995 at the Wolfson Medical Centre in Holon, Israel, SACH aims to improve the quality of paediatric cardiac care for all children; creating local centres of competence in developing countries. Working with the Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI) in Tanzania, this Israeli non-profit organisation is reaching new frontiers in the treatment and care of children across the country.

In Tanzania, the organisation has deployed two main modes of operation to support the diagnosis, treatment and recovery of children who are admitted to the JKCI. After diagnosis at the Institute, selected children and their caregivers are flown to the Wolfson Medical Centre in Israel for final diagnosis and subsequent surgery. In these cases, the Medical Centre’s Legacy Heritage Children’s Home, a fifteen-minute drive from the Centre, provides both counsel and accommodation to the children, escort nurse and their caregivers during this time. To date, 65 cardiac paediatric patients have benefited from this programme.

For treatment in Tanzania, SACH also sends surgeons, nurses, surgeons, anesthesia, doctors and perfusionists to the JKCI for a months-long deployment to fast-track the surgical treatments for children most in need. SACH also provides scholarships for nurses, surgeons, anesthesia, doctors and perfusionists from JKCI who are going to Israel for further study.

Through these collaborations, SACH and the Wolfson Medical Centre realised that there was an opportunity to develop a new approach based on digital transformation to better support JKCI. The partnership with Microsoft through the 4Afrika Initiative, initiated the development of an exciting and innovative model for SACH operations going forward. Through remote participation via Microsoft Teams collaboration tools including video call, document collaboration and the security of data, the teams envision Israeli surgeons being able to collaborate remotely and in real-time with surgeons at the JKCI, having access to a full suite of cutting-edge technology solutions at their fingertips during surgeries. The Microsoft Israel team has worked closely with the Wolfson Medical Centre to deploy the solution, implement security capabilities and provide technical guidance.

“Once implemented, this innovative approach will allow us to help deliver more precise diagnoses, and will help to limit the number of children needing to fly to Israel for treatment. On the social side, there are also the added benefits for the children at JKCI, who will be able to enjoy the comforts of familiar surroundings and family networks in their home country,” says Dr. Lior Sasson from the Wolfson Medical Centre.

“Our surgeons are in constant contact with our Israeli counterparts for consulting, coaching and mentorship. We are excited that this partnership with SACH and Microsoft will allow more precise diagnosis using remote, real-time digital collaboration tools that will immensely benefit the children in our care. We are stepping boldly into medical collaboration in the digital era, and we look forward to being at the leading edge of this innovation,” Prof. Mohamed Janabi Executive Director of JKCI.

“As Microsoft, we are encouraged by the collaboration and drive shown by the Wolfson Medical Centre and the Jakaya Kikwete Medical Institute in the area of paediatric cardiac treatment. Being part of their digital transformation journey is a real privilege, and we are confident that their efforts will serve as a template for similar partnerships in other countries, paving the way for innovation that drives collective action,” concludes Gustavo Raiter, Business Development Lead, Microsoft 4Afrika.

MGOMBEA MWENZA CHADEMA AHUTUBIA MIKUTANO YA KAMPENI MKOANI SINGIDA LEO

$
0
0
 
Mgombea nafasi ya umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Salum Mwalimu, akihutubia mkutano wa kampeni katika Kata ya Makiungu jimbo la Singida Mashariki.
Mgombea nafasi ya umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Salum Mwalimu, akimnadi mgombea ubunge jimbo la Singida Mashariki, Noel Hema.
Mgombea nafasi ya umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Salum Mwalimu, akiwanadi wagombea udiwani wa jimbo la Singida Mashariki.
Wakazi wa Kata ya Puma wakiwa katika mkutano wa kampeni jimbo la Singida Mashariki.
Mgombea nafasi ya umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Salum Mwalimu, akihutubia mkutano wa kampeni jimbo la Singida Mashariki.

Kukusanya michango.
Wakazi wa Kata ya Puma wakimsikiliza Mgombea nafasi ya umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Salum Mwalimu.
Mkazi wa kata ya Puma jimbo la Singida Magharibi akifuatilia mkuatno wa kampeni.
Wananchi wa Kata ya Puma jimbo la Singida Magharibi.

Wakazi wa Kata ya Makiungu wakifuatilia mkutano wa kampeni katika jimbo la Singida Mashariki.
Mwanachama wa CHADEMA akichangia chama hicho.
Mgombea nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Mhe. Salum Mwalimu, akihutubia mkutano wa kampeni katika eneo la Majengo jimbo la Singida Mjini leo Septemba 17, 2020.
Baadhi ya wananchi wakisikiliza sera za mgombea nafasi ya umakamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA.
Mgombea nafasi ya umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Mhe. Salum Mwalimu, akihutubia mkutano wa kampeni katika eneo la Majengo jimbo la Singida Mjini leo Septemba 17, 2020.
Baadhi ya wananchi wakisikiliza sera za mgombea nafasi ya umakamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA.
Mgombea nafasi ya umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Mhe. Salum Mwalimu, akiwaombea kura madiwani wa jimbo la Singida Mjini.
Mgombea nafasi ya umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Mhe. Salum Mwalimu, akimnadi mgombea ubunge jimbo la Singida Mjini, Rehema Koha wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Majengo, Stendi ya zamani.
Mgombea ubunge jimbo la Singida Mjini, Rehema Mkoha, akizungumza na wananchi waliojitokeza katika mkutano wa kampeni uliofanyika Majengo, Stendi ya zamani.
Mgombea ubunge jimbo la Singida Mjini, Rehema Mkoha, akionesha alama ya chama chake wakati akitoka katika mkutano wa kampeni uliofanyika Majengo, Stendi ya zamani.

NCHI YA TANZANIA INAJENGWA NA WAZALENDO - MAGUFULI

RT YATAKIWA KUIPOKEA RASIMU YA KATIBA

$
0
0

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, ameliomba Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), kupokea kwa moyo mkunjufu rasimu ya mabadiliko ya Katiba ya shirikisho hilo kwani imebeba mambo mengi mazuri.

 

Dk. Mwakyembe alitoa wito huo wakati akipokea rasimu hiyo kutoka kwa Katibu wa Kamati Maalumu ya mabadiliko ya Katiba ya shirikisho hilo, Henry Tandau, juzi jijini Dar es Salaam.

 

Waziri Mwakyembe, alisema chanzo cha kuunda Kamati hiyo ya mabadiliko ya Katiba ya RT, ni kutokana na malalamiko ya wadau wa mchezo huo kuhusiana na Katiba ya awali, mara baada ya kukutana nao wakati wa mbio za Kili Marathon mwaka huu.


Alisema kwa jinsi mambo yaliyopendekezwa na kamati hiyo yalivyo, yataleta mabadiliko chanya katika mchezo wa riadha na kuipongeza kwa kufanya kazi kwa kujitolea bila posho.

 

Aliwataka RT kuipokea rasimu hiyo na kuifanyia kazi, kasha kwa kushirikiana na Baraza la Michezo la Taifa (BMT), waandae mkutano mkuu wa kupitisha mabadiliko hayo, kisha isajiliwe na Msajili wa Vyama na Klabu za Michezo.

 

Awali kabla ya kukabidhi rasimu hiyo, Tandau alieleza sehemu kubwa walizozigusa ni pamoja na muundo wa Kamati Tendaji ya RT, ambako hivi sasa itakuwa na Rais, Makamu wa Rais mmoja badala ya wawili, Katibu na Mweka Hazina wa kuajiriwa na Wajumbe sita wa Kamati Tendaji watakaotokana na kanda.

 

Mabadiliko mengine, Tandau alisema ni kuundwa Kamati ya Nidhamu, Kamati ya Rufaa ya Nidhamu, Kamati ya Uchaguzi na Bodi ya Wadhamini.

 

Aidha mabadiliko mengine ni kiwango cha elimu kwa wagombea wa nafasi ya Rais na Makamu ambapo kitakuwa ni angalau kuanzia Diploma, huku ukomo wa kugombea ni miaka 70 badala ya mihula.

 

Kwa upande wake, Makamu wa Pili wa Rais-Ufundi RT, Dk. Hamad Ndee, alipongeza rasimu hiyo na kumuahidi Waziri Mwakyembe wataifanyia kazi.

 

Wajumbe wa Kamati hiyo maalumu ni Filbert Bayi (Mwenyekiti), Henry Tandau (Katibu), huku wajumbe ni Kanali mstaafu Juma Ikangaa, Meta Petro, Mwinga Mwanjala, Mahona Milinde, Abel Odena na Tullo Chambo.

 
Katika hatua nyingine, Kamisheni ya Wanariadha Tanzania (KAWARITA), imepata viongozi wapya watakaoiongoza kwa miaka minne ijayo.

Waliochaguliwa ni Benjamin Michael (Mwenyekiti), Andrew Rhobi (Katibu), huku wajumbe ni Alphonce Simbu, Wambura Ryoba, Angelina Tsere na Mariam Abubakar.

“CHAGUENI VIONGOZI WENYE MTAZAMO MMOJA”

$
0
0


Mjumbe wa Kamati Kuu, Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi wa Kata ya Nkololo,  jimbo la Bariadi, katika mkutano wa kampeni uliyofanyika, wilayani Bariadi, Septemba 17, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Wananchi wa Kata ya Nkololo, wilayani Bariadi, wakimshangilia Mjumbe wa Kamati Kuu, Kassim Majaliwa, wakati akiwahutubia, katika mkutano wa kampeni uliyofanyika katika Kata ya hiyo, Septemba 17, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Wananchi wa Kata ya Nkololo, wilayani Bariadi, wakimshangilia Mjumbe wa Kamati Kuu, Kassim Majaliwa, wakati akiwahutubia, katika mkutano wa kampeni uliyofanyika katika Kata ya hiyo, Septemba 17, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mjumbe wa Kamati Kuu, Kassim Majaliwa, akimkabidhi nakala ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 mgombea ubunge wa CCM wa jimbo la Bariadi, Injinia. Kundo Andrea (katikati), , katika mkutano wa kampeni uliyofanyika katika Kata ya hiyo, Septemba 17, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

 

 

 MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Bariadi wachague viongozi wenye mtazamo mmoja ili kuleta maendeleo ya haraka. 

 

"Ili upate uongozi unaoweza kuleta maendeleo, usichanganye viongozi wenye mitazamo tofauti. Ni vema tukaweka viongozi wanaozungumza lugha moja," amesema.

 

Ametoa wito huo leo (Alhamisi, Septemba 17, 2020) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Nkololo, wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu kwenye mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Nkololo 'A'.

 

Alitumia fursa hiyo kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi, Injinia Kundo Mathew, mgombea udiwani wa kata ya Nkololo, Nyamwela Sinda na wagombea udiwani wa kata zote za wilaya ya Bariadi waliokuwepo kwenye mkutano huo.

 

Akizungumza na wakazi hao, Mheshimiwa Majaliwa amesema Chama cha Mapinduzi kimetekeleza ahadi yake ya kuboresha miradi ya maji kwa kutoa sh. bilioni 3.2 zilizotumika kwenye vijiji vya Nkololo, Igaganulwa, Mwamlapa, Kasoli, Sengerema, Sanungu, Mahina, Nyangokolwa Masewa, Nyakabindi na Bupandagila.

 

"Serikali chini ya Chama cha Mapinduzi ilifanya ukarabati wa visima 120 na kununua pampu 64 na kuzifunga kazi ambayo imefikia asilimia 90 ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya Mheshimiwa Rais ya kumtua Mama ndoo kichwani ambayo ilikuwepo kwenye Ilani ya 2015-2020."

 

Kwenye sekta ya afya, amesema ujenzi wa vituo vya afya unaendelea na vituo hivyo vina uwezo wa kupima magonjwa yote, kufanya upasuaji na kutoa huduma kwa akinamama wajawazito. "Nia yetu ni kuvisambaza hadi huko wananchi waliko, Rais wetu anataka wananchi wasipate shida ya kulipa nauli kufuata huduma za afya."

 

Akielezea yaliyofanyika chini ya Ilani ya CCM iliyopita, Mhe. Majaliwa alisema sh. bilioni 1.8 zimetolewa kwa ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) ambalo sasa linatumika na majengo ya utawala, famasi, kufulia, maabara, mionzi, wodi ya wazazi ambayo yapo katika hatua ya ukamilishaji ya kuweka milango.

 

Alisema sh. milioni 450 zimetolewa kwa ujenzi wa kituo cha afya Byuna ambacho kina wodi ya wazazi, maabara, nyumba ya kuhifadhia maiti na nyumba ya mtumishi na tayari kinafanya kazi.

 

Kuhusu ujenzi wa zahanati, Mheshimiwa Majaliwa alisema sh. milioni 150 zimetolewa na kukamilisha ujenzi wa wodi za wazazi katika zahanati za Sakwe, Igegu, Dutwa, Mwasinasi na Ikungulyambesi.

 

Kuhusu ununuzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi, Mheshimiwa Majaliwa alisema sh. bilioni 2.2 zimetolewa kwa ajili ununuzi wa dawa na vifaa tiba ambapo fedha kwa wastani fedha iliyokuwa inatolewa kila mwezi ni sh. milioni 37. “Tumepeleka magari ya kubeba wagonjwa kwenye Hospitali ya Wilaya Dutwa (moja) na Kituo cha Afya cha Byuna (moja).

 

Mapema, mbunge aliyemaliza muda wake, Andrew Chenge aliwataka wakazi wa Bariadi waendelee kuziamini sera za CCM sababu ndiyo zinazoaminika na zinatekelezeka. 

 

"Wana Bariadi tuhakikishe tarehe 28 mwezi ujao tunafanya kazi ya uhakika kwa kuchagua viongozi waliosimamishwa na CCM tupate mafiga matatu ili maendeleo ya wilaya yetu yaende kwa kasi," alisisitiza.

 

Aliwaombea kura Dkt. John Pombe Magufuli, Injinia Kundo Mathew na madiwani 24 kati ya 31 wa wilaya ya Bariadi kwa sababu wagombea saba wameshapita bila kupingwa.

 

MAMIA WAJITOKEZA KAMPENI ZA DK. MAGUFULI KASULU MJINI

$
0
0

Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mamia ya wananchi wa Kasulu mkoani Kigoma katika Mikutano ya Kampeni za CCM leo tarehe 17 Septemba 2020.


 

MKOA WA KILIMANJARO WAIMARISHA HALI YA ULINZI KATIKA KIPINDI HIKI CHA KAMPENI

$
0
0

MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira amewataka Wanasiasa kutumia majukwaa yao ya kisiasa kutoa matamko ya matumaini kwa wananchi ili kuisadia nchi isonge mbele zaidi badala ya kutumia majukwaa hayo kutoa lugha za matusi.

Akizungumza na Amsha Amsha ya Uhuru FM 2020 nyumbani kwake alisema kipindi hiki kikitumiwa vizuri na wanasiasa kinasaidia kuwaweka wananchi pamoja lakini kikitumika vibaya kinaleta mfarakano na vurugu.

“Jukumu la wanasiasa kipindi hiki ni kuwaambia wananchi wataongeza thamani gani katika mambo yanayowagusa,maana vitu tayari vipo kinachotakiwa sasa ni kuboresha na kukarabati,”alisema.

Alisema dhamira ya serikali Mkoa ni kuhakikisha Uchaguzi wa Oktoba 28 unafanyika kwa amani na utulivu na kusisitiza kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vipo imara  kuhakikisha amani inakuwepo kabla na baada ya uchaguzi.

Aliongeza kuwa hali ya usalama kwa sasa ni nzuri na hakuna vitisho vyovyote na kusisitiza kuwa wamejiandaa kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu na kwamba hadi sasa hakuna vitisho vyovyote vya uvunjifu wa amani.

“Matamanio ya wanasiasa ya jukwaani yatafsirike kwenye maeneo watakayokuwa wanayaongoza, watambue kuwa hawaji kuongoza watu wapya bali ni watu wale wale waliokuwepo,”aliongeza.

Akizungumzia kuhusu mafanikio yaliyopatikana kwenye mkoa huo kupitia uongozi wa serikali ya awamu ya tano alisema kiasi cha Sh Bilioni 40.3 kimetumika kwa ajili ya kugharamia elimu bila ya malipo mkoani humo.

Aidha alisema kiasi cha zaidi ya Sh Bilioni 19 na sekondari zaidi ya Sh Bilioni 43 kimetumika katika ukarabati wa miundombinu katika shule.

“Upande wa miundombinu ya barabara kiasi cha Sh Bilioni 17 kimetolewa kwa ajili ya ukarabati wa barabara,ujenzi wa hospitali mpya ya Rombo na Siha na Sh Bilioni 12 kimetumika kukarabati pia jengo la mama na mtoto,”aliongeza.

Mkuu huyo wa mkoa alisema pia wanafuatilia viwanda ambavyo havijaendelezwa mkoani humo na kusisitiza kuwa mali za watanzania zitarudi kwa watanzania.

Akielezea upande wa sekta ya maji alisema kiasi cha Sh Bilioni 18 zimetumika katika kuhakikisha wananchi wanapata maji.

“Upande wa mifugo na kilimo tuna mpango wa kuwachimbia visima wafugaji ili mifugo yao ipate maji,ukiangalia wilaya ya Mwanga ndio inaongoza kwak uwa na idadi kubwa ya wafugaji hivyo maji ni muhimu kwao,”alisema.
Wakati huo huo, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi, Jonathan Mabihya, amesema ushindi wa Chama hicho kwa Mkoa huo mwaka huu ni zaidi ya asilimia 99 kutokana na wananchi kuielewa serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli ilivyofanga maajabu makubwa kwa kipindi kifupi tu.

Akizungumza na Amsha Amsha ya Uhuru FM Mjini Moshi, katibu huyo wa CCM Mkoa amesema Imani ya ushindi huo inatokana na utekelezaji mzuri  wa ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020.


Kutokana na Hali hiyo amewaomba wananchi kujitokeza katika mikutano ya kampeni ya CCM na hatimaye siku ya Jumatano ya tarehe 28 Oktoba kunipigia Kura za ndio CCM.

Miongoni mwa miradi inayoipaisha CCM katika ushindi wa mwaka huu amesema Ni Sera ya elimu bure, Afya kwa kuboresha na kukarabati Hospitali ya Mawenzi ya Mkoa wa Kilimanjaro, Miundombinu pamoja na mradi wa Maji ya Mwanga, Same na Korogwe ambayo wananchi wamekubali na kuipongeza.

Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>