Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU KANDA YA ZIWA YAENDELEA VIZURI

$
0
0
 Mwanasheria wa tume ya uchaguzi Bw.Mtibora Seleman akifafanua jambo wakati wa semina hiyo.
 Wanasemina wakifatilia kwa karibu mafunzo hayo yanayofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
 Wanasemina ya masuala ya Uchaguzi kanda ya ziwa wakiwa darasani.
 Bi. Jescar Mongi kutoka tume ya uchaguzi hapa akionesha mfano wa utaratibu wa upigaji kura utakavyokuwa.

Na Mwandishi Wetu, Kanda ya Ziwa

Imefahamika kwamba maandalizi muhimu ya uchaguzi mkuu kwa mikoa ya kanda ya ziwa yanaendelea vizuri huku, waratibu wa uchaguzi, wasimamizi na maafisa uchaguzi kutoka mikoa ya Mwanza na Mara wakiaswa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu wakati wa zoezi la mchakato kuelekea Octoba 25 mwaka huu ili kuepusha malalamiko yanayoweza kujitokeza mara baada ya uchaguzi kumalizika.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina ya siku mbili iliyo andaliwa na Tume ya taifa ya uchaguzi na kuhusisha Waratibu wa uchaguzi wa mikoa, wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi, na maafisa uchaguzi kutoka katika mikoa ya Mwanza na Mara Kaimu mkuu wa mkoa wa Mwanza Manju Msambya, amesema watumishi hao wanayo dhima ya kuhakikisha zoezi la uchaguzi linakwenda vizuri kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Msambya amesema nilazima dhamana waliopewa watumishi hao watambue  ni muhimu kwakua inakwenda kutoa mustakabali wa taifa letu na wapi tunako taka kuelekea kwa kuchagua viongozi kwa nafasi za udiwani, ubunge na urais. “Ndugu wanasemina tambueni kwamba, madhumuni ya semina hii nikuwajenge uwezo katika mchakato mzima wa uteuzi wa wagombea, upigaji kura, kuhesabu, kujumlisha pamoja na kutangaza matokeo ya uchaguzi” hivyo suala la umakini ni muhimu sana.
Msambya amesema, kwakutumia uzoefu walionao watumishi hao katika mazoezi mbali mbali ya kitaifa wataweza kufanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa hasa ikizingatiwa kwamba wengi wao walishiriki katika zoezi kama hilo kwa mwaka 2010.

Awali akimkaribisha kufungua semina hiyo Mratibu wa uchaguzi wa kanda ya ziwa Deogratius Nsanzugwanko alisema tayari maandalizi kadhaa kuhusiana na uchaguzi yamekwisha kamilika ikiwapo madaftari ya mikoa ya kanda ya ziwa pamoja na vifaa vyote muhimu kuwa tayari vimekwisha anza kusafirishwa kwenda kwenye mikoa husika.

Kanda ya ziwa inayoundwa na mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Geita, Kagera, Simiyu na Mara, ambapo kwa mkoa wa Mwanza pekee inakadiriwa kuwa na wapiga kura 1,442,391 sawa na asilimia 103% ya lengo lililokuwa limewekwa hapo awali na bodi ya takwimu ya mkoa wa Mwanza ya kuandikisha wapiga kura 1,403,763.

 Imeandaliwa  Na: Atley Kuni- The Power of Media grew.

NHC YAZINDUA UUZAJI WA NYUMBA ZA BIASHARA NA MAKAZI ZA MOROCCO SQUARE,Waziri Kiruki aipongeza NHC kwa ufanisi

$
0
0

 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mauzo ya nyumba za biashara na makazi-Morocco Square uliofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. (Picha na Francis Dande)
 Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo.
  Naibu Wazriri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu. 
 Wageni waalikwa.
 Wageni waalikwa.
  Naibu Wazriri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu. 
 Burudani ya muziki.
Burudani ikiendelea.
  Naibu Wazriri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu.  
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akizungumza katika hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akizungumza katika hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akizungumza katika hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akizungumza katika hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akizungumza katika hafla hiyo.

Na Francis Dande

NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki, amelipongeza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa mpango wake wa kujenga nyumba bora na kuwauzia wananchi kwa ajili ya  makazi na biashara.

Waziri Kairuki aliyasema  hayo juzi  jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua  mauzo ya nyumba  za biashara  na makazi zilizojengwa eneo la Morocco Square,  Kinondoni,  jijini Dar es Salaam.

Aliwapongeza Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu na wenzake kwa  kazi nzuri wanayoifanya kwa kiasi kikubwa katika kuleta  uhai na taswira nzuri ya  shirika hilo.

Alisema kuwa serikali inatambua kuwa  makazi  ni jambo  muhimu kwa maendeleo ya taifa, ndiyo  maana imekuwa ikichukua hatua  mbalimbali ili kuwezersha sekta  ya nyumba kuwa endelevu na yenye  tija kwa wananchi  na uchumi wa nchi.

Alibainisha kuwa moja ya mambo yaliyofanyika katika kukuza sekta hii ni kuwa  na Sheria ya Mikopo ya nyumba (The Mortgage Financing (Special Provision Act) ya  mwaka  2008,  iliyoanzishwa  kuweza kuwafanya wadau wa sekta ya  nyumba wakiwemo waendelezaji, wanunuzi wa nyumba  na taasisi za fedha  kushiriki kikamilifu katika kukukuza sekta hii muhimu.

Aidha , alisema tangu kuwapo kwa  sheria  hiyo, tangu mwaka 2008 kumeshuhudiwa benki 19 kati ya  zaidi ya benki 50 zilizopo nchini zikitoa  mikopo ya nyumba kwa  Watanzania, 16  kati ya  hizo zikiwa zimesaini makubaliano na  na Shirika la Nyumba la Taifa ili kuweza  kutoa mikopo kwa Watanzania wanao nunua nyumba zinazojengwa na NHC.

Naibu waziri huyo alisema kuwa  kutokana na  kuwepo kwa  changamoto  ya riba kubwa  ya  mikopo ya nyumbva inayotozwa  na benki mbalimbali ambayo ni kati ya asilimia 18  na 25, serikali itaendelea  kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania ili kuona namna bora ya kuewezesha  benki  kupunguza riba  katika  mikopo ya nyumba ili Watanzania wengi waweze kukopa na kununua  nyumba.

Aliwahimiza Watanzania  kutumia  fursa zilizopo za mikopo ya Benki kununua  nyumba zinazojengwa na NHC, ikiwamo kujitokeza  kwa wingi kununua nyumba hizo za  za mradi wa  Morocco Square ambao una nyumba za ofisi hoteli, makzi na maduka makubwa.

JK kuongoza maelfu kuombea amani Jumapili Oktoba 4,Makhabane, Mahlangu watua kukoleza utamu

$
0
0
 Msanii wa nyimbo za Injili raia wa Uingereza, Ifheanyi Kelechi (katikati) , akiwasili leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam, tayari kutumbuiza katika Tamasha la Amani linalofanyika leo Uwanja wa Taifa Dar. Kulia ni Mkurugenzi wa Msama Promotions wanaoratibu tamasha hilo, Alex Msama. Kushoto ni Mratibu, Hudson Kamoga. (Picha na Francis Dande)

NA MWANDISHI WETU

RAIS Jakaya Kikwete kesho Jumapili Oktoba 4 anatarajiwa kuwaongoza maelfu ya watanzania katika Tamasha la kuombea amani Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, linalofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaamchini ya uratibu wa kampuni ya Msama Promotions.

Akizungumza jijini Dar es Salaamjana, Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama alisema maandalizi yote yamekamilika ikiwemo kuwasili kwa waimbaji wa kimataifa Sipho Makhabane na Solly Mahlangu kutoka Afrika Kusini na Ifeanyi Kelechi kutoka nchini Uingereza.

Alisema waimbaji hao nguli wa muziki wa injili Afrika, wamekuja kuungana na wengine mahiri wa hapa nchini kupamba Tamsha hilo la kihistoria litakalohudhuriwa na viongozi wa kiroho wa ndani na nje ya nchi wakiwamo wachungaji zaidi ya 200 na maaskofu 50.

“Hili ni tukio la aina yake kwani tunaingia katika kipindi kigumu cha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa pengine kuliko yote iliyopita, hivyo tuna kila sababu ya kumtanguliza Mwenyezi Mungu, tuweze kuvuka salama,” alisema Msama.

Alisema lengo la kuandaa Tamasha hilo ni kutokana na kutambua umuhimu wa tunu ya amani kwa ustawi wa nchi iwe kijamii hata kiuchumi na kuongeza kuwa amani iliyopo inapaswa kulindwa na kila mmoja kwa nafasi yake.

Msama alisema kwa vile Mungu ni wa wote bila kujali dini, jinsia wala kabila na amekuwa akisikia maombi ya watu wake na kuyajibu, wananchi hawana budi kujitokeza kwa wingi katika tamsha hilo  kuomba nchi ivuke salama katika uchaguzi huo wa Oktoba 25.

Kwa upande wa buruidani, mbali ya Mahlangu na Makhabane kutoka Afrika Kusini, waimbaji wengine wanaotarajiwa kupamba tamasha hiloni Ephraem Sekeleti kutoka Zambia, Sarah K kutoka Kenya na Solomon Mukubwa, raia wa DRCongo anayeishi nchini Kenya.

Waimbaji wa Tanzania, ni Rose Muhando, Upendo Nkone, Jesca BM, Martha Mwaipaja, Christopher Mwahangila, Bonny Mwaitege, John Lissu, Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama, St. Andrew Anglican ya Dodoma na AIC Chang’ombe ya jijini Dar es Salaam.

Msama alisema viingilio kwa viti maalumu ni shilingi 5,000, jukwaa kuu shilingi 3,000 kwa wakubwa na watoto watalipa shilingi 1,000 na kuongeza ameweka kiwango hicho kutoa nafasi wengi kushuhudia na baada ya uwanja wa Taifa, litahamia katika mikoa mingine.

Kwa kutambua umuhimu wa amani kwa mustakabali wa taifa, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimepongeza uwepo wa tamasha hilo na kusema litumike pia kumwombea Rais Kikwete akubali kuyapokea matokeo ya aina yoyote yatakayoamuliwa na wananchi kupitia sanduku la kura.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika alisema wanatoa angalizo hilokutokana na baadhi ya viongozi wa chama tawala (CCM) kwa nyakati tofauti kusema hawatakubali kuachia upinzani Ikulu.

Mnyika amesihi Tamasha hilolitumike pia kuombea Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Chini ya Jaji Mstaafu, Damian Lubuva, isimamie uchaguzi huo kwa mujibu wa sheria na taratibu ili uweze kuwa wa huru na haki.

MAMA SAMIA AMALIZA ZIARA SIMIYU

$
0
0
 Kinamama wa mkoa wa Simiyu, wakimtawaza kuwa Mama Kiongozi wa Wasukuma, kwa kumvalisha mavazi rasmi Mgombea Mwenza wa Urais kwa timeti ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Maswa Mashariki mkoani humo leo. Jimbo hilo lilikuwa chini ya Mbunge wa Chadema, Kasulumbai
 Kinamama wa mkoa wa Simiyu, wakimtawaza kuwa Mama Kiongozi wa Wasukuma, kwa kumvalisha mavazi rasmi Mgombea Mwenza wa Urais kwa timeti ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Maswa Mashariki mkoani humo leo. Jimbo hilo lilikuwa chini ya Mbunge wa Chadema, Kasulumbai
 Kinamama wa mkoa wa Simiyu, wakimtawaza kuwa Mama Kiongozi wa Wasukuma, kwa kumvalisha mavazi rasmi Mgombea Mwenza wa Urais kwa timeti ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Maswa Mashariki mkoani humo leo. Jimbo hilo lilikuwa chini ya Mbunge wa Chadema, Kasulumbai
 Kinamama wa mkoa wa Simiyu, wakimtawaza kuwa Mama Kiongozi wa Wasukuma, kwa kumvalisha mavazi rasmi Mgombea Mwenza wa Urais kwa timeti ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Maswa Mashariki mkoani humo leo. Jimbo hilo lilikuwa chini ya Mbunge wa Chadema, Kasulumbai
  Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, baada ya kutazwa kuwa Mwanamke Kiongozi wa Wasukuma, kwa kuvalishwa mavazi rasmi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Maswa Mashariki mkoani humo leo. Jimbo hilo lilikuwa chini ya Mbunge wa Chadema, Kasulumbai
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, baada ya kutazwa kuwa Mwanamke Kiongozi wa Wasukuma, kwa kuvalishwa mavazi rasmi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Maswa Mashariki mkoani humo leo. Jimbo hilo lilikuwa chini ya Mbunge wa Chadema, Kasulumbai
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, baada ya kutazwa kuwa Mwanamke Kiongozi wa Wasukuma, kwa kuvalishwa mavazi rasmi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Maswa Mashariki mkoani humo leo. Jimbo hilo lilikuwa chini ya Mbunge wa Chadema, Kasulumbai
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, akihutubia umati wa wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Maswa Mashariki mkoani humo leo. Jimbo hilo lilikuwa chini ya Mbunge wa Chadema, Kasulumbai
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, akiwasili kuhutubia mkutano wa kampeni leo katika jimbo la Maswa Mashariki mkoani Simiyu leo
Aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la Nkenge na kushindwa katika kura za maoni za CCM, Mama Asupta Mshama, akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Maswa Mashariki mkoani Simiyu leo
Wananchi wakimshangilia mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipohutubia mkutano wa kampeni leo katika jimbo la Maswa Mashariki leo
Mwananchi akiwa amembeba mtoto wake ili kumuona Mama Samia Katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo jimbo la Maswa Mashariki mkoani Simiyu leo
Mgombea Ubunge jimbo la Meatu, Salum Hamis Salum, akiomba kura wakati wa mkutano wa kampeni wa Mama Samia uliofanyika leo katika jimbo hilo mkoani Simiyu
Kijana akimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Meatu
Baadhi ya wananchi wakiwa juu ya mti ili kumuona vizuri mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Meatu mkoani Simiyu
Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Meatu mkoani Simiyu
Wananchi wakifikisha ujumbe kwa Mama Samia kwa njia ya mabango, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Meatu mkoani Simiyu
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Meatu  Salum Hamis Salum katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimsikilza kwa makini Fatuma Maselle, baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni leo katika jimbo la Meatu mkoani Simiyu leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

RAIS KIKWETE AMTEUA MWAKAPALILA KUWA MHASIBU MKUU WA SERIKALI

$
0
0
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais waJ amhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Francis M. Mwakapalila kuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali kuanzia juzi, Alhamisi, Oktoba 1 , 2015.

Ndugu Mwakapalila anachukua nafasi ya Bibi Mwanaidi Mtanda ambaye amestaafu kazi kwa mujibu wa sheria.

Kabla ya uteuzi wake kuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali, Ndugu Mwakapalila alikuwa Naibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

03 Oktoba, 2015

MAHAFALI YA SITA YA BODI YA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI

$
0
0
PS1
Mwenyekiti wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi, Dk. Sr Hellen Bandiho akifungua rasmi kusanyiko la mahafali
..............................................................................
Wataalam wa Ununuzi na Ugavi nchini wameaswa kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kuzingatia miiko na maadili inayoongoza taaluma yao ili kuleta tija kwenye matumizi ya fedha za watanzania. Aidha Bodi imeagizwa kusimamia kwa ukaribu zaidi mienendo ya wanataaluma waliosajiliwa. 

Hayo yalisemwa na Dk. Hamis Mwinimvua Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha akimwakilisha Mgeni Rasmi Waziri wa Fedha Mheshimiwa Saada Mkuya Salum kwenye sherehe za mahafali ya sita ya wataalam wa ununuzi na ugavi (PSPTB).

Aidha Bodi imepongezwa kwa kuzindua mtaala mpya wa masomo utakaonza kufundishwa kuanzia Januari 2016 na kutahiniwa mwezi Novemba 2016. “ni matumaini yangu pia kuwa mtaala huo utawajengea uwezo wataalam wote wa ununuzi na ugavi ili wazidi kuwa mahiri na wenye weledi mkubwa katika kufanya kazi zao” alisisitiza.

Mheshimiwa Waziri wa Fedha aliipongeza Bodi kwa kuongeza masomo ya maadili, ujasiliamali, utafutaji wa masoko na usimamizi wa mikataba kwani eneo hili ni mahsusi katika kuleta maendeleo na tija katika matumizi ya rasilimali fedha.

 “ni matumaini yangu kwamba masomo haya yatakuza ajira kwani yatafungua wigo kwa wahitimu kuanza kujiajiri” alisema Mheshimiwa Waziri. Pia aliongeza kusema, serikali kwa upande wake imeboresha na itaendelea kuboresha zaidi mazingira ya ajira binafsi kwa minajili ya kuwawezesha wananchi kujipatia kipato halali cha kuendesha maisha yao.

Mheshimiwa Waziri wa Fedha aliwaagiza waajiri wote kuhakikisha kwamba wanazingatia mahitaji ya sheria juzuu Na 179, inayowataka kuhakikisha kwamba wanaajiri watumishi waliosajiliwa na Bodi.

Alihitimisha kwa kuwapongeza wahitimu 494 walitunukukiwa vyeti katika ngazi za cheti cha awali, msingi na taaluma.
PS4
Mgeni Rasmi, wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na baadhi ya wahitimu katika picha ya pamoja
PS5
Sehemu ya wahitimu wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi
PS3
Dk Hamis Mwinimvua akitoa hutuba kwa niaba ya mgeni rasmi
PS2
Dk Hamis Mwinimvua katikati aliyemuwakilisha Mgeni Rasmi, Mwenyekiti wa Bodi, Dk Sr Hellen Bandiho na Mtendaji Mkuu Clemence Tesha wakimshuhudia Mgeni Rasmi akizidua mtaala mpya.

LOWASSA AFUNGA KAZI JIJINI ARUSHA

$
0
0
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa akiwa ameambatana na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Mh. Godbress Lema, wakiwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Sinoni, Unga LTD, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni, leo Oktoba 8, 2015. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, ARUSHA
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akihutubiwa wananchi, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Sinoni, Unga LTD, Jijini Arusha leo Oktoba 8, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa akimnadi kwa wananchi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Mh. Godbress Lema, wakati wa Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Sinoni, Unga LTD, Jijini Arusha leo Oktoba 8, 2015.
Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye akiwahutubia wananchi wa Mji wa Arusha wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Sinoni, Unga LTD, Jijini Arusha leo Oktoba 8, 2015.
Mwanasiasa Mkongwe Nchini, Mzee Kingunge Ngomale Mwiru, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Arusha wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Sinoni, Unga LTD, Jijini Arusha leo Oktoba 8, 2015.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Arusha wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Sinoni, Unga LTD, Jijini Arusha leo Oktoba 8, 2015.
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Mh. James Mbatia, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Arusha wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Sinoni, Unga LTD, Jijini Arusha leo Oktoba 8, 2015.




















OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU (NBS) YASEMA PATO LA TAIFA LIMEONGEZA KWA AILIMIA 7.9

$
0
0
 Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.
 Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Wapiga picha wakichukua picha katika mkutano huo.


Na Dotto Mwaibale

OFISI ya Taifa ya Takwimu imesema pato la taifa limeongezeka kwa asilimia 7.9 huku sekta ya madini na uzalishaji umeme ikifanya kuongezeka kwa pato katika kipindi cha robo mwaka 2015 ikilinganishwa na kipindi cha mwaka 2014.

Akizungumza  Dar es Salaam leo asubuhi wakati wakati akitoa taarifa za pato la taifa robo ya pili ya mwaka kuanzia mwezi Aprili hadi Juni 2015, Mkerugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Morrice Oyuke alisema ongezeko hilo la takwimu ni la miezi mitatu ya mwaka huu.

Oyuke alisema ongezeko hilo la pato la taifa linaenda sanjari na matokeo ya thamani ya pato la taifa kwa mwaka huu ambalo lilikuwa ni trilioni 89.0 ambapo  katika robo ya mwaka ni trilioni 45.5 ikilinganishwa na trilioni 39.0 katika mwaka 2014.

Alisema thamani ya pato la taifa ya robo mwaka ya trilioni 45.5 ni kubwa hivyo kusababisha  pato la taifa la mwaka mzima linaweza kukuwa kama uchumi hautotetereka.

"Kama uchumi hautaweza kuguswaguswa na matatizo mingene inaweza ikasababisha pato la taifa la mwaka huu likaongezeka badala ya ile iliyotegemewa hapo mwanzo,"alisema.

Alisema ongezeko hilo la pato la taifa limechangiwa na sekta mbalimbali kufanya vizuri katika kipindi cha robo mwaka.

Alisema sekta ambazo zimeongoza katika kipindi cha robo mwaka ni sekta ya madini,umeme,kilimo na mifugo,viwanda na ujenzi na huduma za kitaalamu.

Alisema sekta ya uzalishaji umemere imekuwa kwa asilimia 18.5 huku bidhaa za viwandani ni asilimia 6.9 madini mawe na kokoto  zimeongezeka asimilia 8.3 limeongezeka kutokana na shghuli za kiuchumi.

"Kutokana na taarifa hii ya pato la taifa kwa robo mwaka taarifa hizi zitumike katika kupanga na kurekebisha sera mbalimbali za maendeleo ya nchi," alisema.

WAFANYAKAZI BOA BENKI KUPEPERUSHA BENDERA YAO NA CCBRT MLIMA KILIMANJARO KUANZIA OKTOBA 11

$
0
0
Naibu Mkuruenzi wa BOA benki, Wasia Mushi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na wanao kwenda kupeperusha bendera ya benki hiyo pamoja na bendera ya CCBRT katika kilele cha mlima wa Kilimanjaro ikiwa ni kukamilisha mchango wao kama benki kwaajili ya watoto waliozaliwa ikiwa miguu yao imepoza ili wapatiwe matibabu katika Hospitali ya CCBRT, ikiwa ni mchango wao kama benki kusaidia jamii inayosumbuliwa na ugonjwa wa kupinda miguu unaojulikana kwa jina la (KIBWIKO) benki ya BOA imekusanya kiasi cha USD 100,000  kwaajili ya kuchangia matibabu ya wanaopatwa na matatizo hayo, ameyasema hayo jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya BOA ambao wateenda kupererusha bendera ya benki hiyo pamoja na bendera ya hospitali ya CCBRT katika kilele cha mlima Kilimanjaro  kuanzia jumapili hii. 
 Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Naibu Mkuruenzi wa BOA benki, Wasia Mushi .
 Naibu Mkuruenzi wa BOA benki, Wasia Mushi  akimkabidhi bendera ya BOA benki Mwenyekiti wa wafanyakazi wa benki ya BOA, Bruno Ngooh leo jijini Dar es Salaam.
 Naibu Mkuruenzi wa BOA benki, Wasia Mushi  akimkabidhi bendera ya Hospitali ya CCBRT Mwenyekiti wa wafanyakazi wa benki ya BOA, Bruno Ngooh leo jijini Dar es Salaam, ambapo itatia moyo kwa makampuni binafsi kuchangia jamii kama walibyofanya benki hiyo.
Naibu Mkuruenzi wa BOA benki, Wasia Mushi  akimkabidhi bendera yenye nembo ya BOA benki  pamoja na nembo ya Hospitali ya CCBRT Mwenyekiti wa msafara wa wafanyakazi wa benki ya BOA, Bruno Ngooh leo jijini Dar es Salaam,ikiwa Mkurugenzi huyo akiwatakia kila raheri wafanyakazi wa benki hiyo kufanikiwa kufika katika kilele cha mlima Kilimanjaro na kurudi wakiwa na kumbukumbu kwao pamoja na ushindi katika jamii ikiwa ni faida na hata kwenye afya zao kwa ujumla alisema.

BENKI KUU YA TANZANIA YAANZISHA MFUMO MPYA WA MALIPO KWA MASAA 24 UTAJULIKANA KAMA TISS

$
0
0
 Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bernard Dadi (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, kuhusu benki hiyo kuanza kutumia mfumo wa malipo baina ya benki na benki kwa masaa 24 kwa siku saba za wiki kwa mwaka utakajulikana kama TISS. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki, Marcian Kobello.
 Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki, Marcian Kobello (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
 Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea. Walioipa kamera mgongo kutoka kushoto ni Meneja Msaidizi wa Idara ya  Uhusiano wa benki hiyo, Vicky Msima na kulia ni Kaimu Meneja Huduma za Kibenki, John Kayombo.

Na Dotto Mwaibale

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imesema kuanzia mwakawa fedha ujao itaanza kutumia mfumo wa malipo baina ya benki na benki kwa masaa 24 kwa siku saba za wiki kwa mwaka ambapo utakuwa ukijulikana kama TISS.

Hayo yamesemwa Dar es Salaam leo  mchana na Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo BoT, Bernard Dadi na kuongeza mfumo huo utaweza kufanya kazi kwa ufanisi iwapo wafanyabiasha na wananchi kwa ujumla watauchangamkia kwani kwa sasa inapatikana kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa mbili usiku kwa benki za kibiashara zilizojiunga.

"Kwa sasa kuna mfumo huu wa TISS ambao umekuwa ukifanya kazi siku za kazi hadi saa mbili usiku na siku za mapumziko na sikukuu unafanya kazi kuanzia saa tatu hadi saa nane, ila tunatarajia mwaka wa fedha ujao utakuwa unafanya kazi kwa masaa 24," alisema.

Alisema kimsingi mfumo huo una lengo la kuondoa mfumo wa kutumia hundi ambao unatumia muda mrefu na wakati mwingine kuna makosa ambayo yanatokea ya mtu anavyoandaa hivyo kuchelewa.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki wa BoT, Marcian Kobello alisema uhaba wa sarafu ya shilingi 500 mitaani unachangiwa na wananchi wenyewe ambao wakienda benki hawachukui fedha hizo hivyo kusababisha zibakie huko kwenye mabenki.

Alisema sarafu za shilingi 500 zipo zaidi ya milioni 100 BoT lakini hadi sasa ni milioni 20 ndizo zipo katika mzunguko hali ambayo inachangia kuadimika kwa fedha hizo.

Alitoa mwito kwa wananchi na wafanyabiashara kuchukua sarafu hizo katika mabenki ili ziweze kufika katika mizunguko na dhana kuwa sarafu hiyo ina madini ya fedha ni uongo kwani asilimia 94 ni chuma na asilimia 6 ni nikoni.

Aliwataka Watanzania kujenga utamaduni wa kupeleka fedha ambazo zimechakaa katika mabenki ili waweze kubadilishiwa kwani utaratibu wa kuuza fedha haupo kisheria pamoja na ukweli kuwa hakuna sheria inayokataza.

BOA yazindua huduma mpya ya Wari

$
0
0

Afisa Masoko wa Bank Of Africa (BOA), Daniel Sarungi akielezea huduma mpya ya Wari iliyozinduliwa na benki hiyo kwa ajili ya utumaji na upokeaji wa fedha kimataifa.
Mkuu wa ICT wa BOA, Bwana Willington Munyaga akitoa ufafanuzi kuhusu huduma mpya ya Wari

Katikati ni Meneja huduma za Kielectronic wa BOA Editha Jumbe


Bank Of Afrika imezindua huduma mpya ya kutuma na kupokea fedha kutoka mahali popote duniani kwa gharama naafuu.

Kwa mujibu wa Afisa masoko wa Benki hiyo, Daniel Sarungu huduma hiyo itakuwa ikiwahudumia watu wote wenye akaunti kwenye benki hiyo pamoja na wale wasio na akaunti.

“Ni benki ambayo itawahudumia watu wote wenye akaunti hapa kwentu na wasio na akaunti,”alisema.

Mkuu wa ICT wa benki hiyo, Willington Munyaga aliwataka watanzania kuitumia huduma hiyo kwa madai kuwa ni njia salama na rahisi na kwamba, itakuwa ikitolewa katika matawi yote 21 ya benki hiyo yaliyo Dar es salaam nan je ya jiji la Dar es salaam.

Meneja wa huduma za kielectronic Editha Jumbe alisema kuwa, wateja wa huduma hiyo watakuwa wakipokea ujumbe wa simu mara wanapotuma fedha zao na wakati zinapotolewa na kuondoa gharama ya kupita simu au kutuma email hasa kwa wateja wa ughaibuni ili kujua kama wamepatiwa huduma hiyo.

LOWASSA AFUNIKA KWA NYUMBANI KWA DK. SLAA

$
0
0
Sehemu ya wananchi wa Mji wa Karatu, wakionyesha furaha yao baada ya kuiona Chopa inayotumiwa na Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, wakati ikiwasili kwenye Uwanja wa Mkutano, Mjini Karatu, Mkoani Manyara
Kikundi cha Ngoma ya Asili kikitoa Burudani katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mbowe, Mjini Karatu, Mkoani Manyara leo Oktoba 9, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akivishwa vazi rasmi la kimila la kabila la wa Iraki, wakati wa Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mbowe, Mjini Karatu, Mkoani Manyara leo Oktoba 9, 2015.

Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akihutubia wananchi katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mbowe, Mjini Karatu, Mkoani Manyara leo Oktoba 9, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiteta jambo na baadhi ya Wagombea Udiwani wa Kata mbali mbali za Mji wa Karatu, Mkoani Manyara leo.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, akihutubia wananchi katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mbowe, Mjini Karatu, Mkoani Manyara leo Oktoba 9, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akisikiliza kwa makini Houba ya Mwenyekiti wake, Mh. Freeman Mbowe (hayupo pichani), aliyokuwa akiitoa kwa wananchi wa Mji wa Karatu, Mkoani Manyara leo.
Mwanasiasa Mkongwe nchini, Mzee Kingunge Ngomale Mwiru, akisisitiza jambo katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mbowe, Mjini Karatu, Mkoani Manyara leo Oktoba 9, 2015.
Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye akihutubia wananchi katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mbowe, Mjini Karatu, Mkoani Manyara leo Oktoba 9, 2015.



Meza Kuu.

Lowassa akisalimiana na mzee Kingunge Ngombale Mwiru.
Kusalimia
Umati wa watu.


Mbowe akihutubia.



























BUZWAGI YAWAZAWADIA WAFANYAKAZI BORA WA MWAKA

$
0
0
Meneja wa Idara ya Maboresho ya Biashara wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Richard Ojendo wa kwanza kushoto akipokea tuzo ya heshima ya utumishi uliotukuka ya meneja wa mgodi, “General Manager Prestegious award” kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Bwana Benson Mpesya,(katikati) anaeshuhudia upande wa kulia ni Eng. Philbert Rweyemamu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini aliyekuwa Shinyanga.
Meneja wa Idara ya Maboresho ya Biashara wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Richard Ojendo wa kwanza kushoto, mkuu wa wilaya ya Kahama bwana Benson Mpesya na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi wakiwa katika picha ya pamoja na Bwana Ojendo mara baada ya kutunukiwa uzo ya  akipokea tuzo ya heshima ya utumishi uliotukuka ya meneja wa mgodi, “General Manager Prestegious award”.
Meneja wa Idara ya Madini wa Mgodi wa Buzwagi Eng. Muganda Mutereko wa kwanza kushoto akipokea tuzo ya Meneja Bora wa Mwaka ”Best Manager of the year” kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Bwana Benson Mpesya,(katikati) anaeshuhudia upande wa kulia ni Eng. Philbert Rweyemamu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi.
Meneja wa Idara ya Ufanisi wa Kampuni wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Saimon Sanga wa kwanza kushoto akipokea tuzo ya ya mshindi wa pili kwa nafasi ya Meneja Bora wa Mwaka ”Best Manager of the year” kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Bwana Benson Mpesya,(katikati) kulia ni Eng. Philbert Rweyemamu.
Mkuu wa kitengo cha Uchenjuaji wa Dhahabu wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Festo akimpokelea Tuzo ya Mshindi wa tatu Bwana Karel Schultz ambaye ni meneja wa Kinu cha Uchenjuaji wa Mgodi wa Buzwagi mara baada ya kutangazwa mshindi wa tatu katika nafasi ya Meneja Bora wa Mwaka ”Best Manager of the year” tuzo hiyo ilikabidhiwa na mkuu wa wilaya ya Kahama Bwana Benson Mpesya.
Washindi wa Tuzo ya Meneja bora wa mwaka wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi.(kutoka kushoto ni Saimon Sanga Meneja wa Idara ya Ufanisi, wa pili ni Eng. Muganda Mutereko Meneja wa Madini, wa tatu ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Bwana Benson Mpesya na wa nne ni Eng.Philbert Rweyemamu aliesimama upande wa kulia ni bwana Festo aliyepokea tuzo hiyo kwa niaba ya bwana Karel Schultez
Mkuu wa kitengo cha Load and Haul Bwana Marco Peter wa kwanza kushoto akipokea tuzo ya Mfanyakazi bora wa mwaka ”Best employee of the year” kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Bwana Benson Mpesya,(katikati) aliyesimama upande wa kulia ni Eng. Philbert Rweyemamu.
Bwana Gulam Fazal Mkuu wa kitengo cha Ghala(warehouse) wa kwanza kushoto akipokea tuzo ya mshindi wa pili wa nafasi ya Mfanyakazi bora wa Mwaka “Best employee of the year” anaekabidhi tuzo hiyo ni mkuu wa wilaya ya Kahama Bwana Benson Mpesya,(katikati) kulia ni Eng. Philbert Rweyemamu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi.
Waziri Selemani Mkuu wa kitengo cha Huduma za Nje (Outside Services) wa kwanza kushoto akipokea ngao ya mshindi wa yatu baada ya kuibuka mshindi wa nafasi hiyo katika kundi la wafanyakazi bora wa Mwaka anaemkabidhi tuzo hiyo ni mkuu wa wilaya ya Kahama bwana Benson Mpesya ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.
Washindi wa tuzo za mfanyakazi bora wa Mwaka “Best Employee of the Year” wakiwa katika picha ya pamoja na meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Eng, Philbert Rweyemamu na Mgeni Rasmi mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Benson Mpesya.
Washindi wa tuzo za mfanyakazi bora wa Mwaka, meneja bora wa mwaka na mshindi wa tuzo ya heshima ya utumishi uliotukuka ya meneja mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Eng, Philbert Rweyemamu na Mgeni Rasmi mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Benson Mpesya.
Bwana Amos John(Kushoto) ambaye ni Meneja wa Idara ya Biashara Mgodi wa Buzwagi akimkabidhi cheti Bwana James Jisena kama sehemu ya kutambua mchango wake kwa kampuni kwa utumishi wa muda mrefu.
Bwana Amos John(Kushoto) ambaye ni Meneja wa Idara ya Biashara Mgodi wa Buzwagi akimkabidhi cheti mmoja wa wafanyakazi wa Idara yake kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi kirefu.
Meneja wa Idara ya Uendelevu  wa Mgodi wa Buzwagi Bwana George Mkanza  akimkabidhi cheti Bwana Abdalah kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi kirefu.
Meneja wa Idara ya Madini wa Mgodi wa Buzwagi Eng. Muganda Mutereko  akimkabidhi cheti Wilbert Masawe kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi kirefu
Meneja wa Idara ya Huduma za kitaalamu za madini Bwana Sam Eshun akimkabidhi cheti mmoja wa watumishi katika idara yake kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi kirefu.
Meneja wa Idara ya Madini wa Mgodi wa Buzwagi Eng. Muganda Mutereko  akimkabidhi cheti Cosmas Joseph kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi kirefu.
Meneja Mkuu wa Idara ya Ufanisi wa Kampuni ya Acacia Bi. Janet Ruben akimkabidhi mmoja wa wafanyakazi cheti  kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi kirefu katika idara ya Ufanisi wa Kampuni katika Mgodi wa Buzwagi
Meneja Mkuu wa Idara ya Ufanisi wa Kampuni ya Acacia Bi. Janet Ruben akimkabidhi Victor Mtutwa kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi kirefu katika idara ya Ufanisi wa Kampuni katika Mgodi wa Buzwagi.

Meneja Mkuu wa Idara ya Ufanisi wa Kampuni ya Acacia Bi. Janet Ruben akimkabidhi Shamsa Mohamed kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi kirefu katika idara ya Ufanisi wa Kampuni katika Mgodi wa Buzwagi
Meneja wa Idara ya Assets Reliability Eng. Peter Mbawala akikabidhi cheti Agness Joseph kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi cha miaka mitano
Mkuu wa kitengo cha Idara ya Raslimali watu Bwana Ivocatus Masanja akitangaza majina ya washindi wa Tuzo mbalimbali ambazo zilitolewa wakati wa halfa ya siku ya familia ya Mgodi wa Buzwagi.
Mshauri Mkuu wa Idara ya Uendelevu wa kampuni ya Acacia Steve Kisyaki (kushoto) akimkabidhi cheti Bwana Franco Eliya Mwakalinga kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi kirefu.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Eng.Philbert Rweyemamu akizungumza na wafanyakazi wa Mgodi wa Buzwagi pamoja na familia zao mara baada ya kuwatunuku tuzo mbalimbali na vyeti baadhi ya wafanyakazi waliofanya vizuri katika kipindi cha mwaka 2015
Kutoka kulia ni Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa Mgodi wa Buzwagi Bi Blandina Munghezi na Magesa Magesa Afisa Mawasiliano wa Mgodi wa Buzwagi (Kulia) wakifafanua jambo kwa mshereheshaji wa shughuli hiyo MC kalinga. (katikati)
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya (wa kwanza Kulia) akifurahia jambo na meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Eng.Philbert Rweyemamu (katikati) wakati wa hafla ya kutoa tuzo kwa wafanyakazi bora pamoja na kuadhimisha siku ya familia ya wafanyakazi wa Buzwagi.
BURUDANI YA KUKATA NA SHOKA NAYO HAIKUKOSEKANA VIJANA WA JJ BAND KUTOKA MWANZA WAKAUFANYA USIKU WA FAMILIA YA BUZWAGI KUWA WA AINA YAKE.

BENKI YA CRDB YASAIDIA UJENZI VYUMBA VYA MADARASA MKOANI GEITA

$
0
0
Benki ya CRDB kupitia tawi lake la mjini Geita imechangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika  Shule za Msingi Mwatulole na Shule ya Msingi Geita ambayo baadhi ya majengo yalibomolewa na mvua kubwa iliyoambata na upepo mkali mwanzoni mwa mwake huu mkoani Geita. 
Sambamba na kusaidia ujenzi na ukarabati wa madarasa Benki ya crdb ilichangia maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyofanyika mjini Geita kwa sababu benki hiyo inawajali wateja wake. Maadhimisho ya wiki Huduma kwa Wateja ilianza Oktoba 5 na kumalizika Oktoba 10 ambapo Benki ya CRDB ilishiriki kikamilifu katika kazi za kijamii. Benki ya CRDB imewashuru wateja wake kupitia tawi la Geita.
Meneja wa CRDB Geita, Amini Mwakang'ata (kushoto) akimkabidhi hundi ya shilingi milioni moja Mkuu wa Shule ya Msingi Mwatulole iliyopo Mkoani Geita, Catherine Mugusi  kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mwatulole akipokea msaada wa vitabu vya ziada na kiada kutoka kwa Meneja wa CRDB Geita, Amini Mwakang'ata.
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mwatulole akipokea msaada wa vitabu vya ziada na kiada kutoka kwa Meneja wa CRDB Geita, Amini Mwakang'ata.
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mwatulole akipokea msaada wa vitabu vya ziada na kiada kutoka kwa Meneja wa CRDB Geita, Amini Mwakang'ata.
Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela (kushoto) akipokea maoni kutoka kwa mteja wa wa Benki ya CRDB tawi la Geita wakati wa Maadhiisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja mjini Geita.
Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela akizungumza na wateja wa benki hiyo (hayupo pichani) katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika tawi la Geita.

KAYUMBA JUMA AZOA MILIONI 5O ZA BONGO STAR SEARCH

$
0
0
 Mshiriki wa Shindano la Bongo Star Search, Angela Marry Kato akiimba wakati wa fainali ya shindano hilo. 
 Mshiriki wa BSS, Jacky akiimba.
  Mshiriki wa BSS, Jacky akiimba.
 Nassib Fanabo.
 Majaji.
 Kelvin Gerson.
 Wadau wa muziki.
 Wadau.
 Angela Marry Kato.
Angela Marry Kato.
 Mwimbaji Nassib Fonabo akiimba moja ya nyimbo zake katika fainali ya Bongo Star Search iliyofanyika jijini Oktoba 9 jijini Dar es salaam.
 Frida Amani.
 Mashabiki wakishangilia kwa kuonyesha alama ya vidole viwili.
 Mashabiki wakishangilia kwa kuonyesha alama ya vidole viwili.
 Wasanii kutoka Nigeria wakitumbuiza.
  Wasanii kutoka Nigeria wakitumbuiza.
 Mshindi wa shindano la Bongo Star Search, Kayumba Juma akipiwa amepiga magoti huku akiangua kilio baada ya kutangazwa mshindi na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 50.
 Mshindi wa shindano la Bongo Star Search, Kayumba Juma akipiwa amepiga magoti huku akiangua kilio baada ya kutangazwa mshindi na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 50.
Mshindi wa shindano la Bongo Star Search, Kayumba Juma akimshukuru mungu baada ya kutangazwa mshindi na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 50. 
Mshindi wa shindano la Bongo Star Search, Kayumba Juma akimshukuru mungu baada ya kutangazwa mshindi na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 50.  
 Madam Rita akimtuliza Kayumba Juma.
  Madam Rita akimtuliza Kayumba Juma.
  Madam Rita akimtuliza Kayumba Juma.
  Madam Rita akimbembeleza mshindi wa Bongo star search, Kayumba Juma.
 Kayumba akilia.
 Kayumba akipongzwa na Madam Rita.
 Rita Paulsen akimfuta machozi Kayumba.
 Rita Paulsen akimkabidhi kitita cha milioni 50 mshindi wa BSS msimu wa 2015, Kayumba Juma.
 Kayumba akipokea mkoba yenye kiasi cha shilingi milioni 50.
 Kayumba akionyesha furaha yake baada ya kuibuka mshindi wa BSS 2015. 
 Ni furaha tupu..........

NSSF YASHIRIKI MAONYESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA ABITAT JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Ofisa Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mselem Mwanamsoga akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Edward Sungura (kulia), wakati wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yaliyoandaliwa na Umoja wa Wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki (Abitat), yanayoendelea katika Ukumbi wa Diamond Jubilee. (Picha na Francis Dande).
 Ofisa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Aisha Sango (wa pili kulia), na Ofisa Uwekezaji wa NSSF, Mselem Mwanamsoga wakitoa maelezo kuhusu huduma wanazotoa, ikiwemo uuzwaji wa viwanja vilivyopimwa katika eneo la Kiluvya, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, kwa watu waliofika katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yaliyoandaliwa na Umoja wa Wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki (Abitat), yanayoendelea katika Ukumbi wa Diamond Jubilee. 
 Baadhi ya watu wakipata huduma katika banda la NSSF.
 Ofisa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Aisha Sango (kulia), akigawa vipeperushi kwa watu waliotembelea banda la NSSF vyenye maelezo kuhusu huduma wanazotoa, ikiwemo uuzwaji wa viwanja vilivyopimwa katika eneo la Kiluvya, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, wakati wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yaliyoandaliwa na Umoja wa Wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki (Abitat), yanayoendelea katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Ofisa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Aisha Sango (kulia), akigawa vipeperushi kwa watu waliotembelea banda la NSSF vyenye maelezo kuhusu huduma wanazotoa, ikiwemo uuzwaji wa viwanja vilivyopimwa katika eneo la Kiluvya, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, wakati wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yaliyoandaliwa na Umoja wa Wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki (Abitat), yanayoendelea katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.

MGOMBEA MWENZA WA CHADEMA JUMA DUNI HAJI AHUTUBIA MKUTANO MJINI DODOMA

$
0
0
 Mgombea mwenza wa Chadema, Juma Duni Haji akihutubia wananchi  kwenye mkutano wa kampeni kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Chang’ombe mkoani Dodoma. 
Wakazi wa Dodoma wakimsikiliza mgombea mwenza wa urais Chadema anayeungwa mkono na Ukawa akizungumza katika mkutano wa kampeni kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Chang’ombe.
 Waendesha Bodaboda wakimsindikiza mgombea mwenza wa urais, Juma Duni Haji wakati alipomaliza kuhutubia wakazi wa Dodoma katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chang’ombe.

Kikundi cha ngoma cha Moto Kali kutoka Ibiwa wakicheza ngoma ya kumkaribisha mgombea mwenza wa urais wa Chadma Juma Duni Haji kwenye mkutano wa kampeni kwenye Viwanja vya Kongogo mkoani Dodoma.
 Mgombea mwenza wa Chadema, Juma Duni Haji akimnadi kwa wananchi wa Bahi mgombea wa Ubunge Jimbo la Bahi, Mathias Lyamundu kwenye mkutano wa kampeni kwenye Viwanja vya Kongogo mkoani Dodoma.
  Mgombea mwenza wa Chadema, Juma Duni Haji akimnadi mgombea wa Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Benson Kigaila kwenye mkutano wa kampeni kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Chang’ombe mkoani Dodoma.
Aliyekuwa mbunge wa Mkanyageni Zanzibar, Habibu Mohamed Mnyaa akihutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Chang’ombe mkoani Dodoma.
 Wakazi wa mjini Dodoma wakifuatilia mkutano huo.
 Wazee katika mkutano.

CHADEMA YATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA MWANASIASA MKONGWE JONAS MALLAH

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Arusha Mjini kimesikitishwa na kuhuzunishwa na kifo cha mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini, Ndugu Estomih Jonas Mallah ambaye alipata kuwa Mwanachama na Diwani Kata ya Kimandolu kupitia CHADEMA katika Wilaya hii.

Tumepokea kwa masikitiko makubwa na huzuni kubwa taarifa ya kifo cha Ndugu Estomih Jonas Mallah ambaye tumejulishwa kuwa aliaga dunia usiku wa kuamkia Ijumaa, Oktoba 9, 2015, katika Hospitali ya Rufaa- KCMC, Mkoani Kilimanjaro. Ni dhahiri Wanademokrasia tumeondokewa na mtu muhimu katika kipindi

muhimu.


Tunatuma salamu za dhati kuomboleza kifo cha Ndugu yetu Estomihi Jonas Mallah kwa familia, Viongozi na Wanachama wa chama cha ACT- Wazalendo.

Kwa pamoja tunamwomba Mungu mwenyeenzi, Mwingi wa Rehema, atupe subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya Marehemu Estomih Jonas Mallah. Amen

Lewis Emmanuel Kopwe

Kaimu Mwenyekiti
Wilaya ya Arusha Mjini
10/09/2015

UFAFANUZI WA IDADI YA VITUO VYA KUPIGIA KURA OKTOBA 25

$
0
0
Ndugu,

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ndugu Kailima Ramadhani  amefafanua jinsi mabavyo Tume ya taifa ya uchaguzi ilivyo gawanya vituo vya wapiga kura kote nchini. Katika ufafanuzi huo amefafanua mambo makuu Mawili.

1. Namna ambayo siyo sahihi ya kuhesabu vituo vya wapiga KURA kama walivyo fafamua baadhi ya watu, Ambayo ni namna ya KUPOTOSHA NA NI UWONGO, na

2. Namna SAHIHI  ya kuhesabu vituo kama tume ye taifa ya uchaguzi ilivyo hesabu. Nia hii inazingatia mambo yafuatayo.
i). KUTUO HAKITAZIDI WATU 450
ii). KITUO KINAWEZA KUWA NA IDADI CHINI YA WATU 450
ILI WATU WALIOJIANDIKISHA KITUO KIMOJA WASIHAMISHWE KWENDA KUJAZIA ENEO JINGINE.

Itakuwa hivi.
Endapo kuna eneo ambalo watu waliojiandikisha ni 1900 Tume ya taifa ya uchaguzi itagawanya watu kama ifuatavyo:-
450+450+450 = 1300
1900-1300 = 550
550 gawanya kwa 2 = 275

KWA HIYO MAHALI PENYE WAPIGA KURA 1900
PATAKUWA NA VITUO VITANO (5)

1. KITUO CHA KWANZA WATU 450
2. KITUO CHA PILI WATU           450
3. KITUO CHA TATU WATU        450
4. KITUO CHA NNE WATU          275
5. KITUO CHA TANO WATU       275
JUMLA                                            1900

ZINGATIA
Kutokana na kuwepo kwa vituo vyenye idadi ya watu chini ya 450 kumefanya idadi ya vituo iwe kubwa.

LOWASSA APATA MAPOKEZI YA NGUVU MJINI TARIME

$
0
0
Vijana wa Mjini Tarime wakiongoza mapokezi ya Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, alipowasili mjini Tarime kwa Mkutano wa Kampeni. PICHA NA OTHMAN MICHUZI.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Tarime katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba, Tarime Mjini, Mkoani Mara. 
Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akiwasalimia wananchi wa Mji wa Tarime waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Sabasaba, Tarime Mjini, Mkoani Mara.
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mara, Mh. Vicent Nyerere, akizungumza wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba, Tarime Mjini, Mkoani Mara.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tarime Vijijini kupitia CHADEMA, Mh. John Heche, akihutubia wananchi wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba, Tarime Mjini, Mkoani Mara.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tarime Mjini kupitia CHADEMA, Mh. Ester Matiko akihutubia wananchi wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba, Tarime Mjini, Mkoani Mara.

Sehemu ya wananchi wa Mji wa Tarime, walioshiriki Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba, Tarime Mjini, Mkoani Mara leo Oktoba 10, 2015.

Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwapungia wananchi wa Mji wa Tarime Mkoani Mara.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa na Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye, wakiwa pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mara, Mh. Vicent Nyerere, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tarime Mjini, Mh. Ester Matimo pamoja na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mh. John Heche, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba, Tarime Mjini, Mkoani Mara leo Oktoba 10, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, asikiliza jambo kutoka kwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tarime Mjini, Mh. Ester Matimo, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba, Tarime Mjini, Mkoani Mara leo Oktoba 10, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Tarime katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba, Tarime Mjini, Mkoani Mara leo Oktoba 10, 2015.
Umati wa watu ukiwa katika mkutano huo.
Mkazi Tarime akisikiliza sera za mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.
Mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassaakitoa akiwahutubia wananchi mjini Tarime.
Lowassa akiwanadi wagombea ubunge wa Musoma Vijijini na Tarime mjini.
Lowassa akisalimiana na wazee.
Akipokea hati ya ushujaa kutoka kwa mzee.
Akionyesha cheti cha ushujaa.
Lowassa akiondoka baada ya kumalizika mkutano.
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>