Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

MAGUFULI AENDELEA NA KAMPENI ZAKE,KESHO KUUNGURUMA LIVE UWANJA WA JAMHURI MKOANI DODOMA

$
0
0
 Pichani kati ni Mgombea Urais wa CCM Dkt John Magufuli akiwa sambamba na Mgombea Ubunge wa jimbo la Mtera Ndugu Livingstone Lusinde kwa pamoja wakiwapungia wananchi wa jimbo la Mtera (hawapo pichani),ndani ya mji wa Mvumi wilayani Chamwino mkoani Dodoma. PICHA NA MICHUZI JR-DODOMA
 Wakazi wa jimbo la Mtera,mjini Mvumi,Wilayani Chamwino wakishangilia jambo wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake za kuomba kura za Urais jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Mvumi wilaya ya Chamwino mkoani Dododma.

Mgombea Urais kupitia CCM, Dk. John Magufuli akiwahutubia  wakazi wa jimbo la Mtera  kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Mvumi wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
 Mgombea Ubunge wa jimbo la Kibakwe,Wilayani Mpwapwa,Ndugu Dkt.Simba Chawene akimuombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kwa wananchi wa kijiji cha  Chipogolo (hawapo pichani),wakati akitokea Iringa vijijini akielekea mkoani Dododma kuanza kampeni zake mkoani humo,kulia kwake ni Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwatazama wananchi waliokuwa wakimuuunga mkono kuwa watampa kura za ndio 
 Dkt Magufuli akiwapungia Wananchi wa kijiji cha Chipogolo Wilayani Mpwapwa,mara baada ya kuwahutubia mapema leo mchana kwenye mkutano wa kampeni,shoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma,Alhaji Adam Kimbisa.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Kada mkongwe wa chama cha Mapinduzi (CCM),Mh.John Samuel Malecela akimuombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwa wakazi wa jimbo la Mtera,mjini Mvumi,Wilayani Chamwino jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni.
Wakazi wa jimbo la Mtera,mjini Mvumi,Wilayani Chamwino wakishangilia jambo wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake za kuomba kura za Urais jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni  uliofanyika mjini Mvumi wilaya ya Chamwino mkoani Dododma.
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Isimani Ndugu William Lukuvi akiwahutubia wakazi wa Kijiji cha Idodi na Pawaga kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mjini humo mapema leo asubuhi mkoani Iringa wakati wa kumnadi Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli
  wakazi wa Kijiji cha Idodi na Pawaga wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia mapema leo asubuhi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni
  Mgombea Ubunge wa Jimbo la Isimani Ndugu William Lukuvi akiwahutubia wakazi wa Kijiji cha Idodi na Pawaga kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mjini humo mapema leo asubuhi mkoani Iringa wakati wa kumnadi Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli 
 Wanannchi wakifuatilia mkutano wa Dk. Magufuli katika kijiji cha Pawaga na Idodi mapema leo asubuhi.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia  wakazi wa Kijiji cha Idodi na Pawaga mapema leo asubuhi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni akimalizia kiporo cha baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Iringa aliyoanza kampeni zake hapo juzi mkoani humo,ambapo leo amewasili mkoani Dodoma na kuanza kampeni zake wilayani Mpwapwa katika jimbo la Kibakwe na baadae jimbo la Mtela. 


MAKAMU WA RAIS DK. BILAL AONGOZA MAZISHI YA WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS MENEJIMENTI YA TUMISHI WA UMMA MAREHEMU CELINA KOMBANI LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Udongo kwenye kaburi la Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma marehemu Celina Kombani wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo shambani kwake katika kijiji cha lukobe mkoani Morogoro. (Picha na OMR)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Shada la maua kwenye kaburi la Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma marehemu Celina Kombani wakati wa mazishi yake yaliyofanyika shambani kwake katika kijiji cha lukobe mkoani Morogoro.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka Shada la maua kwenye kaburi la Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma marehemu Celina Kombani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mgombea Mwenza wa Urais CCM Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka Shada la maua kwenye kaburi la Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma marehemu Celina Kombani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Bw. Hamadi Pungurani Mume wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma marehemu Celina Kombani Baada ya kumalizika mazishi yake.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Watoto wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma marehemu Celina Kombani Baada ya kumalizika mazishi yake yaliyofanyika shambani kwake katika kijiji cha lukobe mkoani Morogoro. 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu Pinda wakitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma marehemu Celina Kombani.
Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma marehemu Celina Kombani.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka shada la maua kwenye kaburi la Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma marehemu Celina Kombani wakati wa mazishi yake.

EMIRATES YAPATA MENEJA MPYA-TANZANIA

$
0
0
Meneja mpya wa Shirika la ndege la Emirates nchini Tanzania, Husain Alsafi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati alipokuwa akijitambulisha, Dar es Salaam jana. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Meneja mpya wa Shirika la ndege la Emirates nchini Tanzania, Husain Alsafi akizungumza na waandishi wa habari (kushoto), wakati alipokuwa akijitambulisha, Dar es Salaam jana.  
Meneja mpya wa Shirika la ndege la Emirates nchini Tanzania, Husain Alsafi akizungumza na waandishi wa habari, wakati alipokuwa akijitambulisha, Dar es Salaam jana.  
Meneja mpya wa Shirika la ndege la Emirates nchini Tanzania, Husain Alsafi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, alipozungumza nao, kuhusu mafanikio na matarajio ya shirika, wakati akijitambulisha, Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Ndege la Kimataifa Emirates lenye makao yake makuu Dubai, jana lilimtangaza Meneja wake mpya wa Tanzania Bw. Husain Alsafi.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafLa fupi ya utambulisho wake Mtendaji huyo mpya wa Emirates Bw. Husain Alsafi alisema kwamba, Emirates imefanikiwa kufikia wastani wa asilimia 12% wa idadi ya wateja wake wa Tanzania kwa kipindi cha miaka mitatu.

Mtendaji huyo mkuu aliongeza kuwa katika kuhakikisha kuwa Shirika hilo la Ndege la kimataifa linatimiza matakwa ya abiria wake hasa kwa soko la Tanzania na kwingineko, hivyo basi wameahakikisha kuwa na safari za kila siku kutoka Tanzania kwenda nchi za nje kupitia Dubai, hivyo watanzania wengi wananufaika pale wanapotumia kusafiri na shirika hilo ambapo pia wanapata faida Zaidi endapo watapanga safari zao mapema ili kupata punguzo la bei/nafuu Zaidi.

Katika kushiriki kwake Tanzania Mtendaji huyo MKuu alisema kuwa wametoa kipaumbele kikubwa kwa wazawa ambapo katika kuajiri wamefanikiwa kuwa na watanzania Zaidi ya 30 katika shirika hilo na pia wanazidi kuongeza  idadi ya Watanzania ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi Zaidi.

“ Emirates Tanzania imefanikiwa kuajiri watumishi wengi sana kutoka hapa hapa nyumbani ikiwa ni mojawapo ya vipaumbele vyetu katika kila nchi husika na pia tunaendelea kutoa nafasi  mbali mbali Zaidi”, alisema Bw. Alsafi.

Kuhusu kupanua vituo Mtendaji huyo alisema kuwa Emirates imeendelea kuwa kivutio cha utalii duniani kwote kwa njia mali mbali ikiwa ni pamoja na kuongeza/kupanua vituo vyake sehemu mbali mbali ambapo kwa mwaka huu hali hiyo imepelekea kukua kwa soko lao hasa kwa nchi kama vile India, UK, Amsterdam, China na France, sehemu ambazo watalii wengi wamekua wakivutiwa Zaidi pindi wanapofanya safari zao kupitia shirika hilo la Ndege.

Akizungumzia kwa upande wa kusafirisha mizigo mbali mbali aliongeza kuwa Emirates imekua ikifanya kazi kwa ukaribu sana hasa na wakulima wa Tanzania kwa muda mrefu sana, ambapo kupitia kitengo cha Sky Cargo kimekua mstari wa mbele katika kutimiza hilo na kuhakikisha usalama wa mizigo ya watu pia kuwafikishia kwa muda uliopangwa, kuwaunganisha wafanya biashara kutoka Tanzania na wale walioko nchi zingine kama Arabuni (UAE) n.k. kudhamini Watanzania wanaozalisha na kusafrisha bidhaa zao za chakula katika maonyesho Dubai. 

Wanawapatia nafasi ya kukutana na kuzungumzia maendeleo a wanunuzi mbalimbali ulimwenguni..

MGOMBEA MWENZA WA UKAWA KUPITIA CHADEMA AFANYA MIKUTANO KILWA KUSINI

$
0
0
 Mgombea mwenza wa urais Chadema, Juma Duni Haji akiwapungia mikono wananchi wakati akielekea jukwaani kuwahutubia kwenye mkutano wa kampeni katika kiwanja cha Mandawa Jimbo la Kilwa Kusini mkoani Lindi. (Na Mpigapicha Wetu)
 Mgombea mwenza wa urais Chadema, Juma Duni Haji akimkabidhi kadi ya CUF aliyekuwa mwanachama wa CCM baada ya kurudisha kadi ya chama hicho kwenye mkutano wa kampeni katika kiwanja cha Mandawa Jimbo la Kilwa Kusini mkoani Lindi.
 Mgombea mwenza wa urais Chadema, Juma Duni Haji akimkabidhi kadi ya CUF aliyekuwa mwanachama wa CCM baada ya kurudisha kadi ya chama hicho kwenye mkutano wa kampeni katika kiwanja cha Mandawa Jimbo la Kilwa Kusini mkoani Lindi.
 Mgombea mwenza wa urais Chadema, Juma Duni Haji akimkabidhi kadi ya CUF aliyekuwa mwanachama wa CCM baada ya kurudisha kadi ya chama hicho kwenye mkutano wa kampeni katika kiwanja cha Mandawa Jimbo la Kilwa Kusini mkoani Lindi.
Mgombea mwenza wa urais Chadema, Juma Duni Haji akiwaaga  wananchi baada ya kumaliza kuwahutubia kwenye mkutano wa kampeni katika kiwanja cha Mandawa Jimbo la Kilwa Kusini mkoani Lindi.

MAMBO YA KATUNI

TASOI YAZINDUA KAMPENI YA SARATANI KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO BILA MALIPO YOYOTE

$
0
0
Katibu Mkuu wa TASOI, Belinda Mlingo akizungumza na waandhishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati endelevu wa kuendesha kampeni ya Mshikamano dhidi ya Saratani kwa kutumia technolojia ya mawasiliano bila malipo yoyote katika ukumbi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road leo jijini Dar.
Dk. Dominista Kombe ambaye ni Mshauri kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road akitoa takwimu ya wagonjwa wanaofika kutibiwa katika hospitali hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Kinga Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage  akizungumza akieleza jambo mbele ya waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road leo.
 Waandishi wa habari wakiendelea kuchuka habari
 Mkutano ukiendelea

Na Michael Maurus, Dar es Salaam

ASASI isiyo ya kiserikali ya Tanzania Social Outreach Initiative (TASOI), imezindua kampeni rasmi mpango mkakati endelevu wa kuendesha kampeni ya Mshikamano dhidi ya Saratani kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano bila malipo yoyote.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TASOI, Belinda Mlingo, alisema kuwa kampeni hiyo itatoa elimu, uhamasishaji na kutoa ushauri nasaha kwa wananchi kwa kupitia ujumbe mfupi wa simu (SMS).

Alisema kuwa katika kampeni hiyo, TASOI inashirikiana na wadau mbalimbali katika masuala ya afya, teknolojia na uhamasishaji wa jamii ili kutoa huduma hii muhimu bila malipo au gharama yoyote kwa watumiaji wa simu za mikononi.

“Kwa kumnukuu Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Yasiyoambukiza Wizara ya Afya, Profesa Ayoub Mgimba, ‘Hali halisi inadhihirisha kwamba magonjwa yasiyoambukiza kama saratani hivi sasa yamekuwa ni tatizo kubwa hasa katika nchi kama yetu ambapo ufahamu na mwamko ni mdogo sana juu mazingira hatarishi, viashiria, matibabu na matunzo ya wahanga wa magonjwa haya. Saratani inasababisha madhara makubwa ambayo yanaelekea kuwa majanga kwa jamii na kiuchumi kwa Taifa.”

Akielezea jinsi kampeni hiyo itakavyoendeshwa, Hellen alisema kuwa kwa muda wa miezi sita, watumiaji wa simu za mkononi za mitandao yote nchini, wataweza kupata taarifa za saratani kwa kupitia namba 15774 kwa kutuma neno CANCER au SARATANI kwenda namba hiyo na kuchagua lugha anayotaka kupokea taarifa hiyo, iwe ni Kiswahili au Kiingeza.

“Hapo utapokea ujumbe wenye elimu juu ya saratani, kati ya za viungo vya uzazi, yaani tezi dume, saratani ya matiti na shinga ya kizazi. Huduma hii itapatikana kupitia mitandao yote ya simu nchini, Vodacom, Airtel, Tigo, Zantel na TTCL,” alisema.

Aliongeza: “Tungependa pia kuwashirikisha wananchi wote kuchangia kwa hiyari ili tutimize malengo haya kwa pamoja. Na hii unaweza kuchangia Sh 1200 kwa mwezi au Sh 300 kwa wiki. 


“Hili utaweza kulifanya kwa kukubali kupokea ujumbe mfupi kutoka kwetu ambao utakuwa na gharama ndogo ya Sh 150 tu. Pia unaweza kuchangia kupitia ezypesa, m-pesa, tigopesa, airtel money. Uchangiaji huu ni wa hiyari na hauzuii kupata huduma ya elimu ya saratani.”

Kwa upande wake, Daktari bingwa wa kwanza wa saratani mwanamke Tanzania, Dominista Kombe wa Ocean Road Cancer Istitute, alisema kuwa ni kweli saratani ni janga la jamii, hali halisi hapa Tanzania, saratani ni tatizo kubwa na linaongezeka kwa kasi, ni jumla ya ugonjwa wa HIV na ugonjwa wa TB, tatizo la saratani lilitakiwa kupewa kipaumbele zaidi.

“Tatizo jamii huwa haipo tayari kuweka wazi juu ya uginjwa huu kwa kuogopa aibu ya kutengwa, haya yote yakitokana na uhafamu mdogo juu ya ugonjwa huu,” alisema.




Alisema kuwa serikali imekuwa ikijitahidi kupambana na ugonjwa huu kwa kutoa huduma bure, lakini hata hivyo imejikuta ikishindwa katika kukabiliana nalo kwani tatizo ni kubwa mno, akiitaka jamii kusaidia katika vita hiyo kama walivyoamua kufanya TASOI waliokuja na mpango wao wa kampeni kupitia simu kuiwezesha jamii kujua juu ya viashiria vya janga hilo.



Alisema kuwa tatizo la saratani ni la dunia nzima, hivyo kuna ulazima wa jamii kujenga utaratibu wa kupima afya mara kwa mara kama ilivyo kwa nchi za Ulaya ambako imesaidia kupunguza ukubwa wa janga hilo kupitia chanjo.

Alisema kuwa Ocean Road hupokea wagongwa wapya 5000 kwa mwaka, kati yao asilimia 80, wanafika wakiwa katika hali mbaya kiasi kwamba hupewa tiba ya kuwaongezea siku tu, huku asilimia ndogo sana, huwahi na kupewa tiba inayowawezesha kuishi.

NAMELOK SOKOINE AZINDUA KAMPENI ZAKE JIMBO LA MONDULI

$
0
0
MGOMBEA jimbo la Monduli kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Namelok Sokoine, akihutubia mkutano wa hadhara wakati wa uzinduzi wa kampeni zake zilizofanyika katika viwanja vya Nanja Mnadani Monduli mkoani Arusha Septemba 28,2015 ambapo pamoja na mambo mengine ameahidi kuendeleza yote aliyoasisi, kusimamia na kutekeleza aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Edward Lowassa.

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro akihutubia mkutano wa  uzinduzi wa Kampeni za Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli Mkoani Arusha kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Namelok Sokoine.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Namelok Sokoine akihutubia wananchi katika mkutano huo wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni zake.
 Namelok Moringe Sokoine akiwasili katika uwanja huo wa Nanja tayari kwa uzinduzi wa kampeni.
 
Wazee wa Kimila wa Jamii ya Kimaasai wa Monduli wakiongoza dua maalim ya kumuombea Binti yao Namelok.
 Mwalimu Lorinyu Nkoosi, mmoja wa waliochuana na Namelok Sokoine katika mchakato wa uteuzi ndani ya CCM akiongea.
 Wananchi wa Monduli wakiwa katika mkutano huo.
Wajane wa Waziri Mkuu wa Zamani wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine ambao ni mama za Namelok Sokine wakitambulishwa mkutanoni hapo na Mwenyekiti wa kamati ya kampeni za CCM jimbo la Monduli, Paul Kiteleki.
 Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro (kulia) akimkabidhi ilani ya Chama cha Mapinduzi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli Mkoani Arusha kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Namelok Sokoine wakati wa uzinduzi wa jkampebni zake uliofanyika Monduli jana.
 Dk Asha-Rose Migiro akisalimiana na wamama wa kimaasai alipowasili mkutanoni hapo.

LOWASSA APATA MAPOKEZI MAKUBWA JIMBO LA BUMBULI, MKOANI TANGA

$
0
0
Wananchi wa Mji wa Soni katika Jimbo la Bumbuli, wakimlaki kwa shangwe Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Kisiwani, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo leo Septemba 28, 2015.
Umati wa Wananchi wa Mji wa Soni katika Jimbo la Bumbuli, wakisikiliza sera za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, wakati Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Kisiwani, leo Septemba 28, 2015.
Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye akihutubia wananchi kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Kisiwan, Mji wa Soni katika Jimbo Bumbuli, Mkoani Tanga leo Septemba 28, 2015.



TEA YAIPA TET MKOPO WA SHILINGI BILIONI TATU KUANDAA MITAALA NA KUCHAPISHA VITABU VYA ELIMU YA MSINGI

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Sifuni Mchome (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na Mamlaka ya Elimu (TEA) zilipotialiana saini mkataba wa makubaliano ambapo TEA itaipatia TET Mkopo wa Sh Bilioni 3 kwaajili ya kuandaa mitaala na kuchapisha vitabu vitakavyotumiwa na wanafunzi shule za msingi nchini kuanzia darasa la tatu hadi la sita. Prof Mchome, amewataka TET kuhakikisha wanakamilisha kazi hiyo kwa weledi ili kuweza kusaidia mabadiliko ambayo yatachangia kuwa na elimu inayokidhi viwango vya kimataifa.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa TEA, Joel Laurent na Kaimu Mkurugenzi wa TET, Dk Leonard Akwilapo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dk Leonard Akwilapo (kushoto) na Kaimu MkurugenziMkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Joel Lauren (kulia) wakitiliana saini hati za makubalino ya mkopo wa Sh Bilioni 3 ambazo TEA itaipatioa TET. Katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Sifuni Mchome.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dk Leonard Akwilapo (kushoto) na Kaimu MkurugenziMkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Joel Lauren (kulia) wakionesha hati za makubalino ya mkopo wa Sh Bilioni 3 ambazo TEA itaipatioa TET baada ya kutiliana saini jana mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Sifuni Mchome.Picha: Father Kidevu Blog.

Picha ya pamoja ya Wakurugenzi wa TEA, TET, Katibu Mkuu pamoja na watumishi wao.
 **************
Na Father Kidevu Blog
MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA) imeipatia mkopo wa shilingi Bilioni 3 Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) katika makubaliano yaliyofikiwa leo Septemba 30, 2015 jijini Dar es Salaam.

Makubaliano hayo yalifikiwa mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya Eklimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Sifuni Mchome ambapo TET itatumia fedha hizo katika kuandaa mitaala na kuchapisha vitabu vitakavyotumiwa na wanafunzi shule za msingi nchini kuanzia darasa la tatu hadi la sita.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Joel Laurent amesema mkopo huo nafuu utakaolipwa katika kipindi cha miaka sita, umetolewa katika kutekeleza sera mpya ya elimu ya mwaka 2014.

“Mamlaka kwa kuzingatia Sera mpya ya Elimu ya mwaka 2014, imeridhia maombi ya mkopo ili kuhakikisha uwepo wa mitaala, muhtasari na vitabu vya kiada kwa darasa la tatu hadi la sita vinavyoendana na mahitaji na wakati,”alisema Laurent.

Utaratibu huo utaiwezesha TET kuandaa vitabu vya kiada kwa hatua ya kwanza ya elimu msingi, kutafanya uwepo wa mitaala inayoendana na kuwa kuboresha mfumo wa upatikanaji wa vitabu sahihi kulingana na mitaala nchi nzima kupitia TET hivyo Sasa nchi itakuwa na kuwa na kitabu kimoja cha kiada kwa shule nzima tofauti na ilivyo sasa kila shule zinavitabu vyake vya kufundishia.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dk Leonard Akwilapo alisema mkopo huo watautumia kufanya utafiti na kubaini mahitaji ya maboresho kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali wa elimu wakiwamo wanafunzi, walimu, wazazi na waajiri na kuandaa mitaala ya Elimu ya awali na Elimu ya Msingi kuanzia darasa la tatu hadi sita na kuandika vitabu vya kiada.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Sifuni Mchome aliwataka TET kuhakikisha wanakamilisha kazi hiyo kwa weledi ili kuweza kusaidia mabadiliko ambayo yatachangia kuwa na elimu inayokidhi viwango vya kimataifa.

SIMBA YAIFUNGA STAND UNITED 1-0, YANGA YAIPIGA MTIMBWA SUGAR 2-0

$
0
0
Beki wa Simba, Murshid Juuko akiwatoka wachezaji wa Stand United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Taifa leo. Simba imeshinda 1-0. (Picha na Francis Dande)
Mshambuliaji wa Simba, Simon Sserunkuma akimtoka beki wa Stand United, Abuu Ubwa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

2nd PAN-AFRICAN MOSQUITO CONTROL ASSOCIATION (PAMCA) ANNUAL SCIENTIFIC CONFERENCE, 6-8th OCTOBER 2015

GLOBAL TV ONLINE:MPOTO AFUNUKA KUHUSU SABABU YA YEYE KUTEMBEA PEKU

WAGOMBEA UBUNGE NA UDIWANI USO KWA USO NA WAPIGA KURA WAO MUFINDI , WAULIZWA MASWALI MAZITO JUU YA AJENDA YA WATOTO

$
0
0
       Ndg Patrick Lalika, akiuliza Swali kuhusu Mazingira hatarishi kwa Watoto katika mdahalo uliofanyika katika Shule ya Msingi Igowole wilayani Mufindi, ambao ulishirikisha wanafunzi kutoka Shule za Msingi Igowole, Ibatu na Kisalasi, pamoja na walimu, wazazi na walezi ambao waliwahoji wagombea wa Ubunge

Mwalimu  Nico Mgala, Akiuliza swali kuhusu mrundikano wa wanafunzi madarasani katika .mdahalo uliofanyika katika Shule ya Msingi Igowole wilayani Mufindi, ambao ulishirikisha wanafunzi kutoka Shule za Msingi Igowole, Ibatu na Kisalasi, pamoja na walimu, wazazi na walezi ambao waliwahoji wagombea wa Ubunge


 
Ndg Castory Boniface Masangula Mgombea Udiwani kata ya Igowole kupitia CCM akijibu Swali  katika mdahalo uliofanyika katika Shule ya Msingi Igowole wilayani Mufindi, ambao ulishirikisha wanafunzi kutoka Shule za Msingi Igowole, Ibatu na Kisalasi, pamoja na walimu, wazazi na walezi ambao waliwahoji wagombea wa Ubung    



Ndg Israel Mpina Msalilwa, mgombea Udiwani kata ya Igowole kwa tiketi ya CHADEMA akijibu swali katika mdahalo uliofanyika katika Shule ya Msingi Igowole wilayani Mufindi, ambao ulishirikisha wanafunzi kutoka Shule za Msingi Igowole, Ibatu na Kisalasi, pamoja na walimu, wazazi na walezi ambao waliwahoji wagombea wa Ubunge




 Wazazi wakifuatilia  mdahalo uliofanyika katika Shule ya Msingi Igowole wilayani Mufindi, ambao ulishirikisha wanafunzi kutoka Shule za Msingi Igowole, Ibatu na Kisalasi, pamoja na walimu, wazazi na walezi ambao waliwahoji wagombea wa Ubunge

Baadhi ya wanafunzi walioshiriki kwenye mdahalo

 Frank Timothy Malata, mgombea Ubunge Jimbo la Mufindi Kusini. Kwa tikeki ya Chadema akitoa maelezo.




Mwanafunzi Mangula akiuliza swali juu ya huduma bora ya Umeme



Thabiti Msofe Afisa Ustawi wa Jamii Mufindi, Akichangia mada kuhusu Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na Lishe Bora katika  mdahalo uliofanyika katika Shule ya Msingi Igowole wilayani Mufindi, ambao ulishirikisha wanafunzi kutoka Shule za Msingi Igowole, Ibatu na Kisalasi, pamoja na walimu, wazazi na walezi ambao waliwahoji wagombea wa Ubunge
Zikiwa zimebaki siku 23 kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, hapo jana wakazi wa Jimbo la Mufindi kusini wamewataka wagombea Ubunge na Madiwani watakaopata nafasi ya kuwaongoza katika kipindi kinachofuata  kutafuta suluhisho la ukatili dhidi ya watoto ikiwa ni pamoja na adhabu kupita kiasi kutoka kwa walimu na wazazi, Mimba za utotoni na kukatishwa masomo kwa watoto kwa ajili ya ndoa ama ajira.

Hayo yalisemwa katika mdahalo uliofanyika katika Shule ya Msingi Igowole wilayani Mufindi, ambao ulishirikisha wanafunzi kutoka Shule za Msingi Igowole, Ibatu na Kisalasi, pamoja na walimu, wazazi na walezi ambao waliwahoji wagombea wa Ubunge Frank Timothy Malata (CHADEMA) pamoja na wagombea udiwani Castory Boniface Masangula (CCM) na Israel Mpina Msalilwa (CCM).

Aidha walisisitiza suala la upatikanaji wa viwanja vya michezo kwa watoto na kudai kuwa michezo ni njia mojawapo ya kumbadili mtoto kimwili na kiakili.

Akijibu hoja kutoka kwa wananchi, Mgombea Ubunge katika Jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Frank Timothy Malata ameahidi kupatikana suluhisho la adha hizo na kukomesha ukatili dhidi ya watoto. Mgombea huyo pia ameahidi kuinua michezo kwa kuanza na upatikanaji wa viwanja bora vya michezo mbalimbali zaidi ya mpira wa miguu. 

Kwa upande wake Mgombea Udiwani Kata ya Igowole kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Castory Boniface Masangula ameahidi kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa kamati za ulinzi za watoto na sekta nyingine zinazojihusisha na ulinzi wa mtoto ili kuhakikisha watoto wanalindwa dhidi ya ukatili wowote.

Naye Israel Mpina Msalilwa ambae ni mgombea Udiwani wa kata hiyo kupitia CHADEMA aliahidi kushirikiana na serikali pamoja na wadau mbalimbali kuondoa tatizo la mrundikano wa wanafunzi madarasani pamoja na kupiga vita ukatili dhidi ya watoto zikiwemo adhabu kupita kiasi zinazotolewa na wazazi, walezi ama walimu.

Katika hatua nyingine, watoto ambao ndio walengwa wakuu wa Midahalo hii walitoa maoni yao kuwa nini kifanyike baada ya viongozi hao kushika nyadhifa wanazogombea ambapo walitaja kuwa wanakerwa na uhaba wa vitabu, vyoo, huduma bora za afya, umeme na usafiri na kupambana na mimba za utotoni hasa hasa kwa wanafunzi.

Wakati huo huo, Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Mufindi Navoneiwa Mfinanga amewataka wagombea hao kuwa karibu na kamati za watoto ili kuhakikisha wagombea wanatimiza ahadi zao

Midahalo hii ni muendelezo wa midahalo ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto kinachoandaliwa na Kampuni ya TRUE VISION Production chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ikishirikiana na UNICEF yenye lengo la kuibua ajenda ya watoto kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015. 

Unaweza kusikiliza kipindi cha Walinde Watoto mahali popote kupitia redio shiriki 19 ikiwemo TBC inayorusha matangazo hayo siku ya Jumamosi kuanzia saa tisa mchana na pia kupitia tovuti ya www.walindewatoto.org nawww.facebook.com/WalindeWatoto

“Tuwape nafasi viongozi wanaojali watoto kwa kutetea haki zao” – Baraza la Watoto.

WAIMBAJI TAMASHA LA AMANI KUANZA KUWASILI IJUMAA

$
0
0
Mwenyekiti wa Tamasha la Kuombea Amani, Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Oktoba 4 kwenye Uwanja wa Taifa, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Jakaya Kikwete. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Hamisi Pembe. (Picha na Francis Dande)
Na Mwandishi Wetu

WAIMBAJI watakaoshiriki katika tamasha la kuombea Amani Uchaguzi Mkuu 2015 wanaanza kuwasili Ijumaa Oktoba 3.

Aklizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama amesema kuwa maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika kwa asilimia 100 huku waimbaji kutoka nje ya nchi wanatarajiwa kuwasili kuanza Ijumaa.

Aliwataja waimbaji hao kuwa ni Sipho Makhabane, Solly Mahalangu (Afrika Kusini), Ephraim Sekereti (Zambia), Solomon Mukubwa (DR Congo), Sarah K (Kenya).

Aidha kutakuwa na waimbaji wadhawa akiwemo malkia wa muziki wa injili Afrika Mashariki na Kati, Rose Muhando, Upendo Nkone, Jesca BM, Bonny Mwaitege, Christopher Mwangira, John Lissu.

Kwa upande wa kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama, Kweaya ya AIC Chang'ombe na Kwaya ya St. Adrew Aglikana ya Dodoma.

Wakati huohuo Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), limeipongeza Kampuni ya Msama Promotions kwa kuwa wabunifu wa kuinua vipaji vya waimbaji wa muziki wa Injili Tanzania ambao wanapata nafasi ya kutambulika kimataifa.

Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza, alisema kuwa ufanikishaji huo wa kazi za waimbaji inayofanywa na Msama ni baada ya kukamilisha taratibu zote ikiwemo ufuatiliaji wa vibali vya kufanikisha tukio hilo la kuombea amani Oktoba 4.

Mngereza alisema tamasha hilo ni lenye maana kubwa kutokana na maudhui yake, hasa ikizingatiwa nchi inakabiliwa na Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani utakaofanyika Oktoba 25.

Alisema tamasha hilo linasisitiza kuwa amani ni kitu cha msingi hasa kwa masuala ya kisiasa na kiuchumi, ambavyo havitapata mwelekeo wake iwapo amani hiyo ikikosekana.

“Kama hakuna amani vitu vyote havifanyiki, tamasha hilo limekuja wakati muafaka kwamba sisi ni wamoja, Watanzania tuzingatie misingi ya amani.

“Tumekuwa ndugu bila kubaguana kwa hali yoyote, amani tuliyopewa na Mungu, tuileee na kuitunza tunu hiyo kwa sababu ndiyo chachu ya maendeleo yetu na taifa kwa ujumla,” alisema.

Mkurugenzi wa Msama Prmotions, Alex Msama alisema maandalizi ya kuelekea tamasha hilo yamekamilika kwa kiasi kikubwa, hivyo alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kufanikisha tamasha hilo.

“Nawasihi wapenzi na mashabiki wa muziki wa Injili na wengine wenye mapenzi mema kwa nchi yao, wajitokeze kwa wingi katika Uwanja wa Taifa katika tamasha la kuombea amani Uchaguzi Mkuu,” alisema Msama.

Aidha, ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kukubali kubeba jahazi la tamasha hilo, kwa kukubali kuwa mgeni rasmi ambapo atatumia tukio hilo kuwaaga mashabiki wa muziki wa Injili.

LOWASSA ATIKISA DAR

$
0
0
Waangalizi kutoka Jumuiya ya Ulaya (EU), wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea urais wa Chadema uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwembe Yanga leo majira ya saa tano asubuhi, mgombea huyo anaungwa mkono na vyama vinne vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD. (Picha na Francis Dande)
 Tambwe Hiza akihutubia katika mkutano huo.
 Mgombea ubunge jimbo la Temeke, Abdalah Mtolea.
 Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Mwembe Yanga Temeke Dar es Salaam.
  Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Mwembe Yanga Temeke Dar es Salaam.
Umati wa watu ukiwa katika mkutano huo.
 Mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na umoja wa vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, Edward Lowassa akiwasili katika viwanja vya Mwembe Yanga majira ya saa tano asubuhi.
 Mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na umoja wa vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, Edward Lowassa akihutubia umati wa watu uliojitokeza majira ya saa tano asubuhi katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.
 Mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na umoja wa vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, Edward Lowassa akihutubia umati wa watu uliojitokeza majira ya saa tano asubuhi katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.
 Mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na umoja wa vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, Edward Lowassa akihutubia umati wa watu uliojitokeza majira ya saa tano asubuhi katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam. 
 Mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na umoja wa vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, Edward Lowassa akihutubia umati wa watu uliojitokeza majira ya saa tano asubuhi katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam. 
 Mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na umoja wa vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, Edward Lowassa akihutubia umati wa watu uliojitokeza majira ya saa tano asubuhi katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam. 
  Umati wa watu ukiwa katika mkutano huo.
 Umati wa watu ukiwa katika mkutano huo.
 Mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na umoja wa vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, Edward Lowassa akimtambulisha mgombea ubunge jimbo la Temeke, Abdallah Mtolea.
  Mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na umoja wa vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, Edward Lowassa akitoka katika viwanja vya Mwembe Yanga.
  Mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na umoja wa vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, Edward Lowassa akitoka katika viwanja vya Mwembe Yanga.
  Mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na umoja wa vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, Edward Lowassa akitoka katika viwanja vya Mwembe Yanga.

UJENZI WA MSIKITI KIMBANGULILE , MKURANGA PWANI

$
0
0
 Msikiti mpya wa Kitongoji cha Kimbangulile, Mkuranga Pwani
 Msikiti wa zamani wa Kitongoji cha Kimbangulile Wilaya ya Mkuranga mkoni Pwani.
Tunamshukuru Mungu kwa wale wote walio tuunga mkono katika harakati hizi Mungu awabariki.

Zaidi pia Mungu awabariki waendeshaji wa blog hii ya Jamii kwa kutuunga mkono katika kupeleka habari kwa Jamii na kutuunga mkono katika harakati zetu.

Ndugu zangu Wapendwa Michango tuliyo kusanya toka mwanzo Program PROJECT zetu za kheri hizi ni Tshs 6,000,000 ( Milioni Sita ) .

Pesa hizi zimetumika katika kuwezesha kufanya Mambo Mawili katika sehemu tofauti , Sehemu ya Kwanza ni Mkoa wa Pwani , Wilaya ya mkuranga , Kijiji cha Mlamleni , kitongoji cha Kimbangulile hapa tumewezesha kuubadilisha ki ujenzi Msikiti kutoka katika hali ya Nyasi kuwa hali ya bati kama mnavyo ona katika Picha . 

Hii ilikuwa ni Project yetu namba Moja .

Matumizi ya hapo tuliweza nunua Tofali 1500 katika Tofali 2000 zilizo tumika kujenga Jengo jipya.

Pesa yote iliyo baki tuli amishia Project namba mbili ambayo ipo mbezi Salasala ambapo tulinunua pesa zote tofali na wakatokea Wahisani wengine walituongezea Tofali ambazo idadi yake zilifikia 10,000/= pamoja na Mifuko 100 ya Cement .

Kwa Mchango huo tuliweza kufanya yafutayo:-

1.Tumejenga Msikiti ambao mnao uona katika Picha .

2.Madarasa Matatu .

3.fremu 3 . 

Na tofali zimebaki kwa ajili ya kujenga uzio.

Mdau katika kheri kwa Michango yenu ndio tumeweza kufika hapa .

Mungu awabariki zaidi na zaidi ili mpate kulikamilisha hili na mengine ya kheri .

 Project ya pili
Katika Project Site namba mbili tumechimbiwa kisima na Mfadhili , kisima kina Mita 120 ametutaka katika Mita hizo tutoe Tshs Milioni Nne ambapo mpaka sasa nina Tshs 125,000/=

Tunawakaribisha wale wote ambao wapo tayari kuchangia kwa lolote katika harakati hizi za kheri.

Mahitajio 

1.bati 
2.mbao
3.Nondo
4.Kifusi 
5.Madirisha na Milango 
6.Na vifaa vyote ambavyo vinaweza kutusaidia katika Mambo ya Ujenzi .

Nawashuru saana na saana kwa kutoa muda wako na kusoma maelezo haya , furaha yetu zaidi itakuwa pale utakapo kuwa na muda na utayari wa kututembelea site ilitupate muongozo zaidi kutoka kwako.

NAMBA ZA MAWASILIANO YA KUTUMA MCHANGO.

TIGO - PESA 

+255715800772 
+255673800772 

AIRTEL - MONEY

+255689604780 

Kwa wale walio nje wanaweza tuma kupitia 

WESTERN UNION :

Receiver Name :- GHALIB NASSOR MONERO.

Tafadhali naomba nijulishe mara tu utakapo tuma Mchango wako au kabla kwa Namba hizo za Simu.

Au face book : Kijana wa Kiislam Dsm .

SSRA yatoa elimu kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi (TUCTA) mkoani Dodoma

$
0
0
*Wafanyakazi watakiwa kufuatilia makato yao

Mkurugenzi wa Utafiti, Tathmini na Sera wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ansgar Mushi.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WANACHAMA wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii wametakiwa kufuatilia makato yao kwa kuwa baadhi ya waajiri wanachelewa kupeleka makato yao. 

Mbali na hilo, waajiri wa metakiwa kutowalazimisha wafanyakazi wao, kujiunga na mfuko wasio upenda badala yake wapewe nafasi ya kujieleza. 

Kauli hiyo, ilitolewa jana na Ofisa Tehama wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Kenneth Batanyita alipokuwa akitoa elimu kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi (TUCTA), mkoani Dodoma.


Mkurugenzi wa Utafiti, Tathmini na Sera kutoka SSRA, Ansgar Mushi aliwatoa hofu wanachama wa mifuko hiyo, ya jamii kwa madai kuwa haiwezi kufa. 

Katibu wa Chama cha Wafanyakazi, Mkoa wa Dodoma,Ramadhani Mwendwa aliwataka wafanyakazi kujenga hoja wanapodai stahiki zao badala ya kulalamika.

Msama Promotions yamshukuru Rais JK

$
0
0
NA FRANCIS DANDE

 MWENYEKITI wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la kuombea amani Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, Alex Msama  (pichani) amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika tukio hilo lenye umuhimu na uzito mkubwa kwa mustakabali wa taifa.

 Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Msama ambaye kupitia kampuni yake ya Msama Promotions ndiye amekuwa mwasisi wa matamasha ya muziki wa injili tangu mwaka 2000, alisema hatua ya Rais kikwete kukubakli mwaliko wao, kumewapa ari na nguvu zaidi. “Unajua Rais ni mtu mwenye majukumu mengi sana, hivyo hatua yetu ya kupeleka ombi la kumtaka awe mgeni wetu na kukubali, ni jambo la furaha sana kwetu kama Msama Promotions,” alisema Msama. 

 Msama alisema mbali ya Rais Kikwete kujumuika na watanzania katika tukio hilo la kuombea amani uchaguzi mkuu, pia kwake Tamasha hilo litakuwa na kumbukumbu kubwa kwake kabla ya kuondoka madarakani baada ya uchaguzi mkuu. 

 “Tunajua Rais Kikwete anakwenda kumaliza muda wake na kukabidhi madaraka kwa mwingine ajaye, hivyo kwa namna yoyote ile huenda likawa tukio la mwisho la aina hii akiwa ndani ya madaraka ya urais,” alisema Msama. 

 Alisema wapenzi, mashabiki na wapendwa katika kristo na wananchi kwa ujumla wana kila sababu ya kujitokeza kwa wingi katika tamasha la kesho Uwanja wa Taifa kuombea amani uchaguzi Mkuu. 

 Msama alisema wanapaswa kufanya hivyo sio tu kutokana na umuhimu wa tukio hilo kwa maslahi ya taifa, pia kumtia moyo Rais Kikwete ambaye amekuwa mdau mkubwa wa muziki wa injili kwani si nmara ya kwanza kukubali mwaliko wa Msama Promotions. Alisema alikwenda mbali na kusema hata mwaka 2011, Rais Kikwete alikubali kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka ambalo lilifanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni kielelezo cha umoja na mshikamano kwa kitaifa. Msama alisema kwa mazingira hayo, wao Msama Promotions wana kila sababu ya kutoa shukrani kwa Rais Kikwete na kumpongeza kwa kuwa karibu na muziki wa injili, akisema amesaidi kuupa hadhi na heshima kubwa, hivyo kutimia kwa malengo mbalimbali.

KATUNI YA LEO

MGOMBEA MWENZA WA CHADEMA JUMA DUNI HAJI AFANYA MKUTANO RUFIJI

$
0
0
 Mgombea mwenza wa urais Chadema anayeungwa mkono na Ukawa, Juma Duni Haji akikaribishwa na mkazi wa Chumba, Futa Bakari wakati wa mkutano wa kampeni katika Viwanja vya Muhoro, Rufiji mkoani Pwani.
Wakifuatili mkutano..............
 Mgombea mwenza wa urais Chadema anayeungwa mkono na Ukawa, Juma Duni Haji akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Kibiti CUF, Abdallah Ismail wakati wa mkutano wa kampeni katika Viwanja vya Jaribu mkoani Pwani.
 Mgombea mwenza wa Chadema anayeungwa mkono na Ukawa, Juma Duni Haji akihutubia na wananchi wakati wa mkutano wa kampeni katika Viwanja vya Jaribu mkoani Pwani.
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>