Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

Mgombea wa Urais wa CCM Dk Shein Awahutubia Wananchi wa Mtambwe: Ahaidi Mwaka wake wa Kwanza Elimu ya Sekondari Bure: Matibabu ya Afya Nayo Bure katika Miaka Miwili ya Mwazo ya Uongozi Wake

$
0
0
Kikundi cha Taarabu cha Kangagani Pemba cha Profesa Gogo kikitowa burudani wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, uliofanyika katika Jimbo la Mtambwe Kisiwani Pemba na kuhudhuriwa na Wananchi wengi. 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na viongozi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati akiwasili katika viwanja vya mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika viwanja vya Makoongeni Mtambwe Pemba.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akiwapungia mkono Wananchi wa Kijiji cha Mtambwe alipowasili katika viwanja hivyo kuhudhuria mkutano wa Kampeni ya mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Mtambwe wakiwa na mabango yenye ujumbe huo wakati wa mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika viwanja vya makoongeni Mtambwe Kisiwani Pemba. 
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya CCM Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Ndg Merwa Hamad Mberwa wakati akiwasili katika viwanja vya mkutano vya Makoongeni Mtambwe kuendelea na mikutano yake ya kampeni kisiwani Pemba.
Wanachama wa CCM Pemba wakimshangilia Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, alipowasili katika viwanja vya Makoongeni kwa ajili ya mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika Jimbo la Mtambwe Pemba na kuhudhuriwa na Wananchi wengi wa maeneo hayo ya mtambwe.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Wete Pemba Kombo Hamad akitowa salamu za WanaCCM wa Wilaya yake wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, na kuwataka Wananchi kumpigia Kura Dk Shein, kuzidi kuleta maendeleo kwa Visiwa vya Unguja na Pemba. 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mhe Mohammed Aboud Mohammed akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Mtambwe na kutowa Sifa za Mgombea wa CCM Dk Shein, kwamba ni Mchapa Kazi na Uongozi wake Imara kwa Maendeleo ya Wazanzibar ili kuijenga Zanzibar Mpya katika kipindi chake cha Uongozi wa miaka mitano ijaya. ili kuendeleza adhima yake ya maendeleo kwa Wananchi wa Zanzibar.
 Mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa CCM wakati wa mkutano wake wa Kampeni katika viwanja vya makoongeni mtambwe Pemba.
Mjumbe wa Malmashauri Kuu ya CCM Balozi Ali Karume akiwataka wananchi wa Jimbo la Mtambwe kumpigia Kura ya Ndio Dk Shein, ili kumchagua kuiongoza Zanzibar kwa maendeleo na kusema Uchaguzi sio kitu cha kujaribu   
Kada wa CCM Balozi Amina Salum Ali akizungumza na Wananchi wa Mtambwe wakati wa mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya makoongeni, amewataka Wanawake wa Mtambwe kuwaelimisha Kina Baba jinsi ya mafanikio ya CCM kwa kuipigia kura CCM ili kuendeleza wimbi la nmaendeleo katika kisiwa cha Pemba katika sekta mbalimbali za Uchumi CCM ndio chama pekee kinacholeta amani na upendo kwa wananchi wake.
Wanachama wa CCM wakimshangilia Balozi Amina Salum Ali wakati akihutubia katika mkutano huo wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein uliofanyika katika jimbo la Mtambwe Pemba. 
Kada wa CCM Dk Sira Ubwa Mwaboya akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Mtambwe na kuwataka kukipigia kura CCM kwa maendeleo ya Wazanzibar na kusema Mtambwe ya sasa siyo ile ya zamani  imekuwa na mabadiliko makubwa katika kipindi cha miaka ya sasa katika sekta zote za maendeleo kwa wananchi wake.
Wananchi wa Jimbo la Mtambwe wakiwa katika viwanja vya Mkutano wa Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, wakisikiliza sera za CCM kwa miaka mitano ijayo dhidi ya Uongozi wa Dk Shein. 
Mkalimani wa Lugha za Alama kwa Watu wasionikia akitowa ishara kwa vitendo kutowa ujumbe wa Watu wenye mahitaji maalum waliohudhuria katika mkutano wa kampeni ya mgombea wa Urais wa Zanzibar Dk Sheim Jimbo la Mtambwe.
Balozo Seif Ali Iddi Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Mtambwe wakati wa mkutano wa kampeni wa mgombea wa Urais wa Zanzibar Dk Shein, uliofanyika viwanja vya makoongeni mtambwe na kuwataka kukipigia kura Chama cha Mapinduzi ili kumchagua Dk Shein kwa Maendeleo ya Zanzibar kutimiza ahadi za Ilani ya CCM kwa kipindi chake cha Pili cha Uongozi wake. 
Wanachama wa CCM Jimbo la Tambawe wakimshangilia Balozi Seif Ali Iddi wakati akiwahutubia katika mkutano wa kampeni ya mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe Mberwa Hamad Mberwa akiwahutubia wananchi na kutoa historia ya iliokuwa mtambwe ya zamani hadi mafanikio yaliopatika kwa sasa kabla ya kumkaribisha Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, kuwahutubia Wananchi hao.
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Mtambwe wakati wa mkutano wake wa kampeni kisiwani Pemba uliofanyika katika viwanja vya makoongeni mtambwe na kuhudhuria na wananchi wengi wa jimbo hilo. 
 Wananchi wa Mtambwe Pemba wakimsikiliza Dk Shein, wakati akiwahutubia na kuomba kura kwa wananchi hao ili kuleta maendeleo kwa Wanamtambwe katika sekta mbalimbali za kiuchumi.

Wanachama wa CCM wakimsikili Mgombea Urais wa CCM Dk Shein, akiwahutubia wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya makoongeni Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Mtambwe katika mkutano wake wa kampeni kisiwani Pemba uliofanuika viwanja vya makoongeni na kutoa ahadi katika kipindi chake cha Pili cha Urais wa Zanzibar, akiingia madarakani mwaka wake wa kwanza Elimu ya Sekondari itakuwa bure na miaka miwili ya Uongozi wake Matatibabu Zanzibar yatakuwa Bure kwa Wananchi wa Zanzibar.
Wanachama wa CCM wakimsikili Mgombea Urais wa CCM Dk Shein, akiwahutubia wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya makoongeni Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba.
Vijana wa Jimbo la Mtambwe wakifuatilia hutuba ya Mgombea wa Urais wa Zanzibar Dk Shein wakati wa mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya makoongeni mtambwe Pemba.

Wanachama wa CCM wakimsikili Mgombea Urais wa CCM Dk Shein, akiwahutubia wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya makoongeni Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha Wagombea Ubunge wa Wilaya ya Wete Pemba wakati wa Mkutano wake wa Kampeni uliofafanyika katika viwanja vya mpira makoongeni Jimbo la Mtambwe Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha Wagombea Uwakilishi wa Wilaya ya Wete Pemba wakati wa Mkutano wake wa Kampeni uliofafanyika katika viwanja vya mpira makoongeni Jimbo la Mtambwe Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha Wagombea Udiwani wa Wilaya ya Wete Pemba wakati wa Mkutano wake wa Kampeni uliofafanyika katika viwanja vya mpira makoongeni Jimbo la Mtambwe Pemba
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa CCM wakiitikia dua baada ya kumaliza mkutano wake wa kampeni ya kugombea Urais wa Zanzibar uliofanyika katika viwanja vya mpira makoongeni Jimbo la Mtambwe Pemba.
Imetayarisha na OthmanMapara.Blogspot. zanzinews.com
Email othmanmaulid@gmail.com
Mobile No 0777424152 Or 0715424152.


JAPANI YAKUBALI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KATIKA KUCHANGIA BAJETI YA MAENDELEO

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile katika majadiliano na Bw. Hiroshi Kato ambaye ni Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo ya Japan (JICA).
 Ujumbe wa Tanzania na Ujumbe wa JICA wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile wakati wa majadiliano ya kuwekeza katika sekta ya umeme, utalii na kuboresha mazingira ya biashara.
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile wa kwanza kulia akiendelea  kufanya majadiliano na ujumbe wa JICA ukiongozwa na Rais wa JICA Bw.  Hiroshi Kato wa pili kulia.
Baadhi ya Ujumbe wa Tanzania na Ujumbe wa Japan wakiwa kwenye majadiliano. Katikati ni Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile, kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Bw. Khamis Mussa na Kamishna wa Fedha za Nje Bw. Said Magonya na kulia kwake ni Rais wa JICA Bw. Hiroshi Kato. Katibu Mkuu Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali

xxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Serikali ya Jumhuri ya Muungano wa Tanzania yapata dola milioni 280 kutoka Benki ya Dunia na Japani, fedha hizo zitatumika kusaidia mipango mbalimbali nchini Tanzania. 

Akiongea  na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia ukanda wa Afrika Bw. Makhtar Diop na Rais wa Shirika la Maendeleo ya Japan-JICA Bw. Hiroshi Kuto, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius  Likwelile alisema dola milioni 230 zimetolewa na Benki ya Dunia. 

Kiasi cha  Dola milioni 100 ni kwa ajili ya kuhimiza mambo ya uwazi katika utawala, dola milioni 80 ni kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara na dola milioni 50 ni kwa ajili ya kuboresha sekta ya hifadhi ya jamii yaani  pensheni.

Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) wamethibitisha kuendelea kuunga  mkono Serikali ya Tanzania  katika mipango ya maendeleo. Wakiwa katika kikao na ujumbe kutoka Tanzania, Bw. Hiroshi Kato ambaye ni Makamu wa Rais wa shirika hilo alisema  kuwa , Serikali ya Japan kupitia shirika lao la maendeleo ( JICA) lina mipango ya kuunga mkono Tanzania   na Kenya watajenga barabara ambayo itaunganisha  Arusha na Mombasa kwa kiwango cha juu ili kuweza kurahisisha mazingira ya biashara na utalii. Bw. Kato katika mazungumzo yake aliongeza kuwa bado wao wako tayari kusaidia kupitia bajeti kuu ya Serikali kama vile ambavyo wamekuwa wakifanya  miaka ya  nyuma.

Akifafanua kuhusiana na sekta ya hifadhi ya jamii Dkt. Likwelile alisema kuwa uboreshaji wa pension umeahirishwa kwa sasa na wameomba Shirika la kazi la Kimataifa (ILO) wafanye mapitio ya sekta hiyo na baada ya mapitio hayo ndio tutajua ni masuala gani tunaweza kuyazingatia ili kuboresha sekta yetu ya hifadhi ya jamii.
Katika majadiliano na viongozi wa benki ya Dunia  Dkt. Lilkwelile aliwaeleza kuwa, Tanzania kuna changamoto kubwa kwasababu uzalishaji wa umeme kupitia maji umepungua kutokana na kina cha maji kupungua katika maeneo ya uzalishaji hivyo tunategemea gesi.
“Tunategemea gesi ya Kinyerezi One ambayo inatupatia megawatts 405-407, na vilevile tunapata umeme kutokana na matumizi ya mafuta ambapo ni gharama kubwa na uzalishaji haujafikia lengo ambalo ni mahitaji yetu ya siku ambayo tunapata. Tuna mapungufu ya megawatts160, suala hili limeleta shida sana  kwenye bajeti yetu”. Alisisitiza Likwelile

Benki ya Dunia watashirikiana na Idara ya Serikali ya Uingereza ya maendeleo ya Kimataifa (DFID) pamoja na Japan kuwekeza katika reli ya kati ili kuunga mkono jitihada zetu za kuboresha huduma ya reli nchini Tanzania, Likwelile aliendelea kufafanua.

Kwa upande wa maendeleo ya uchumi wa Tanzania ni kwamba uchumi bado unakuwa kati ya asilimia 6.5 mpaka 7, mfumuko wa bei umeshuka japokuwa unapanda kidogo kufikia asilimia 6.4, akiba ya fedha za kigeni bado inawezesha Tanzania kuingiza bidhaa za karibu miezi minne, aliongeza Dkt. Likwelile.

Katika majadiliano hayo Rais wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Bw. Diop alisisitiza kuwa Tanzania iweke msisitizo mkubwa kwenye kilimo chenye tija na cha kibiashara pamoja  na kuwekeza kwenye miundombinu ambayo itasaidia uchumi kuimarika hasa kwenye nishati, reli, barabara, mawasiliano pamoja na kuwekeza kwa vijana  kwani ni wengi sana na  wanahitaji uhakika wa kupata ajira. Tukiweza kufanya kilimo kikawa cha tija na kuwekeza kwenye viwanda vidogovidogo na kuwapa vijana elimu ambayo itawasaidia kuweza kujitegemea, Tanzania itaweza kusonga mbela.

Akiendelea kufafanua Bw. Diop alisema, kutokana na uchumi wa Tanzania ulivyo hakuna sababu ya kukusanya mapato yetu ya kodi kwa kiwango cha sasa, tuna uwezo wa kwenda hadi asilimia 12 ya pato la Taifa. Naye Dkt. Likwelile alimuhakikishia Rais wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Bw. Diop kuwa lengo la Tanzania ni hili ila tunahitaji uwekezaji ili tuweze kufikia lengo tuulilokusudia,  maana tumeweka ukomo wa fedha angalau tufikie mpaka asilimia14.5 lakini tunaweza kwenda mpaka asilimia 17 – 20 katika miaka mitatu ijayo.

Katika kuhitimisha majadiliano hayo Dkt. Likwelile alisema kwamba ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya Dunia ni mzuri na mkubwa sana. Kiwango cha fedha ambacho tunakipata kutoka kwao kinazidi kuongezeka na wameweza kuturuhusu kuwekeza kutumia mlango  mwingine mfano kwenye Chama cha Maendeleo ya Kimataifa(IDA) na pia kwa sasa tumeweza kupata fedha kupitia Benki ya Kimataifa ya ujenzi na maendeleo(IBRD) kwa ajili ya upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam.
Hali ya hewa mjini hapa ni baridi sana. 

Imetolewa na: Bi. Ingiahedi Mduma
     Msemaji wa Wizara ya Fedha
                                                                    Peru – Lima

                                                              10/10/2015

WATUHUMIWA WA MAKOSA YA MTANDAO WAFIKISHWA MAHAKAMANI

$
0
0
Mtuhumiwa wa makosa ya mtandao anayetuhumiwa kusambaza katika mitandao  taarifa za uongo zinazomhusu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama,  Benedic Angelo Ngonyani (24) (wa kwanza Kulia) akiwa katika mahakama ya hakimu mkazi ya Kisutu akisubiri kusomewa mashtaka. 

Wengine ni watuhumiwa wa wizi kwa kutumia mitandao ya simu (fraud and use of telecommunication network) Ally Hamze (53) raia wa Afrika Kusini(wa Pili kulia), Huang Kun Bing (26)Raia wa China (wa Tatu Kulia) Irfan Mirza Baig (46) (wa kwanza Kushoto) Hefeez Irfan (32)(wa pili kushoto) na Mirza Rizwan Baig(41) (wa tatu kushoto) wote watatu raia wa Pakistani wakiwa katika Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu wakisubiri kusomewa mashtaka ya Uwizi kwa kutumia mitandao ya simu (fraud and use of telecommunication network). 

KATUNI YA LEO

MAMA SAMIA AMALIZA KAMPENI MKOA WA MWANZA NA KUANZA SHINYANGA KWA KISHINDO

$
0
0
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, akiwa katika Kivuko cha mv Misungwi, wakati akitoka Mwanza kwenda Sengerema mkoani humo.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi (Hawapo Pichani) aliosafiri nao katika Kivuko cha Misungwi, wakati akienda Sengerema kutoka jijini Mwanza, kwenda Sengerema kuendelea na kampeni zake leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan (wapili kushoto), akiwa katika Kivuko cha mv Misungwi, wakati akitoka jijini Mwanza kwenda sengerema kuendelea na kampeni zake leo. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Kampanei za CCM Kitaifa, Christopher Ole sendeka na watatu pia i Mjumbe wa kamati hiyo, Angela Kizigha na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza Baraka Konisaga ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mwanza
 Wananchi wakimsubiri kwa hamu Mgomea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan wakati Kivuko ca Mv Misungwi kilipokuwa kiliwasili katika eneo la Busisi wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akilakiwa na Mkuu wa wilaya ya Sengerema, alipowasili kwenye Kivuko cha Busisi,wilanai humo leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi wakati akitoka kwenye Kivuko cha mv Misungwi baada ya kuwasili Busisi wilayani Sengerema.
 Kina Mama wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan wakati akipita kwenye Kijiji kimoja wakati msafara ukienda Jimbo la Sengerema mkoani Mwanza.
Wananchi wakiwa wameusimamisha msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan katika eneo la Nyasenga, wakati ukienda Sengerema mkoani Mwanza.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM,Mama Samia Suluhu Hassan, akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni aliofanya katika jimbo la Sengerema mkoani Mwanza.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge jimo la Sengerema, William Ngeleja wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo.
Baadhi ya wagombea Udiwani katika jimbo la Sengerema, mkoani Mwanza wakiwasalimia wananchi waliponadiwa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo.
Magombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia umati wa wananchi katika mkutnao wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Buchosa mkoani Mwanza.
Umati wa wananchi ukimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM,Mama Samia Suluhu Hassan alipouhutubia kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Buchosa mkoani Mwanza
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Buchosa, Charles Tizeba, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo mkoani Mwanza
Baadhi ya wagombea Udiwani katika jimbo la Buchosa, wakisalimia wananchi baada ya kunadiwa na mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika Uwanja wa Sabasaba, eneo la Maganzo katika jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga.
Wananchi wakimshangilia mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimkabidhi  kitabu cha Ilani ya CCM, Mgombea Ubunge jimbo la Kishapu Suleiman Nchambi baada ya kumnadi katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo mkoani Shinyanga.
Mgombea  Ubunge jimbo Shinyanga mjini Steven Masele akiomba kura kwa wananchi wakati wa mkutano wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Chuo Cha Biashara mkoani Shinyanga.
Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Shinyanga mjini mkoani Shinyanga
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea bunge jimbo la Shinyanga Mjini, Steve Masele, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

RAIS WA NAMIBIA AANZA ZIARA YA SIKU MBILI NCHINI TANZANIA

$
0
0
 Bendera ya Tanzania na Namibia.
 Ndege ya Rais wa Namibia ikiwasili.
  Rais wa Namibia, Hage Geingob akilakiwa na Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kuwasili leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili.
 Rais Jakaya Kikwete akimkaribisha mgeni wake Rais wa Namibia, Hage Geingob.
  Rais wa Namibia, Hage Geingob akisalimiana na mke wa rais Jakaya Kikwete mara baada ya kuwasili nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili.
 Rais wa Namibia, Hage Geingob akipokea maua kutoka kwa mtoto, Elizaberth Jackson mara baada ya kuwasili leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili.
  Rais wa Namibia, Hage Geingob akipeana mkono na mtoto Elizaberth Jackson mara baada ya kupokea maua. 
 Rais wa Namibia, Hage Geingob akipigiwa mizinga 21.
 Gwaride la heshima.
 Rais wa Namibia, Hage Geingob akikagua gwaride la heshima mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Rais wa Namibia, Hage Geingob akikagua gwaride la heshima mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Rais wa Namibia, Hage Geingob pamoja na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete wakicheza muziki wa Brass Band walipokuwa wakiangalia vikundi vya burudani vilivyokuwa vikitumbuiza leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)

RAIS KIKWETE AZINDUA KIWANDA CHA SARUJI CHA DANGOTE MTWARA

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Halima Denengo na mmiliki wa kiwanda kipya cha Saruji cha Dangote Alhaj Aliko Dangote (nyuma yao) wakati wa sherehe za kuzindua kiwanda hicho kikubwa kuliko viwanda vyote vya saruji Afrika Mashariki huko Mtwara.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na  Alhaj Aliko Dangote na ujumbe wake kutoka Nigeria wakipata picha ya kumbukumbu wakati wa sherehe za kuzindua kiwanda hicho kikubwa kuliko viwanda vyote vya saruji Afrika Mashariki huko Mtwara Jumamosi Oktoba 10, 2015
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na  Alhaj Aliko Dangote na familia yake na ujumbe wake kutoka Nigeria wakipata picha ya kumbukumbu wakati wa sherehe za kuzindua kiwanda hicho kikubwa kuliko viwanda vyote vya saruji Afrika Mashariki huko Mtwara Jumamosi.
  Sehemu ya wafanyakazi wa kiwanda kipya cha Saruji cha Dangote Alhaj Aliko Dangote  wakati wa sherehe za kuzindua kiwanda hicho.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na  Alhaj Aliko Dangote wakikata utepe kuashiria  kuzindua rasmi kiwanda cha saruji cha Dangote ambacho ni kikubwa kuliko viwanda vyote vya saruji Afrika Mashariki huko Mtwara.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na  Alhaj Aliko Dangote wakifunua pazia kuashiria  kuzindua rasmi kiwanda cha saruji cha Dangote ambacho ni kikubwa kuliko viwanda vyote vya saruji Afrika Mashariki.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa uzalishaji Bi. Mbumi Mwampeta (23) kuhusu uzalishaji wa satuji kwa njia za kisasa baada ya  kuzindua rasmi kiwanda cha saruji cha Dangote ambacho ni kikubwa kuliko viwanda vyote vya saruji Afrika Mashariki huko Mtwara Jumamosi Oktoba 10, 2015.  PICHA NA IKULU.

BENKI YA CRDB YAADHIMISHA KILELE CHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto) akikata keki na mmoja wa wateja wa Benki hiyo tawi la Oysterbay wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimlisha keki mmoja wa wateja waliofika kupata huduma katika tawi la CRDB Oysterbay jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki, wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja. Kushoto ni Meneja wa Benki hiyo tawi la Oysterbay, Juliana Mhimbira.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimlisha keki mmoja wa wateja waliofika kupata huduma katika tawi la CRDB Oysterbay kama ishara ya kuwashukuru wateja wa Benki hiyo wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto) akisikiliza maoni ya mteja mkubwa wa Benki ya CRDB tawi la Oysterbay jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki, wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza na wateja wa Benki ya CRDB tawi la Oysterbay jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki, wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB akipokea zawadi ya maua kutoka kwa Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Lumumba Upendo Assey wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
 Dk. Charls Kimei akisalimiana na wateja.
 Dk. Charles Kimei akizungumza na wateja wa Benki ya CRDB.
 Dk. Kimei akizungumza na waandishi wa habari.
 ‘Tumerejesha bil. 1.3/- kwa jamii’

Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei amesema benki yake imetumia sh bilioni 1.3 ikiwa ni sehemu ya faida yake, kurejesha kwa jamii kupitia sekta ya elimu, afya na mazingira.

Alizungumza hayo akiwa na baadhi ya wateja wa benki hiyo Tawi la Oysterbay mwishoni mwa wiki wakati wa hitimisho la Wiki ya Huduma kwa Wateja wa CRDB nchini kote.

“Oktoba ya kila mwaka tunatumia wiki hii kurejesha asante yetu kwa jamii, tumegawa madawati katika shule mbalimbali za msingi yenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 40 kwa shule mbalimbali za msingi hapa nchini.

“Manispaa ya Kinondoni tumepeleka dawa na vitendanishi kwa ajili ya kipindupindu vyenye thamani ya sh. milioni 15 pamoja na shughuli nyingine nyingi zilizofanywa na watumishi wetu kwenye matawi yetu yote,” alisema Dk. Kimei.

Alisema umuhimu wa wiki ya huduma kwa wateja ni kuboresha ufanisi wa utendaji na huduma kwa kuwa ni kipindi cha wateja kueleza kero, maoni na ushauri wao kwa uwazi.

Wiki ya huduma kwa wateja wa CRDB huadhimishwa kuanzia Oktoba 5 hadi Oktoba 11 ya kila mwaka ambapo wafanyakazi wa benki hiyo hufanya shughuli mbalimbali za kijamii.

LOWASSA AZIDI KUVUTA HISIA ZA WATU WENGI, MAELFU WAJITOKEZA KATIKA MKUTANO WA MUSOMA LEO

$
0
0
 Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mara na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Musoma Mjini, Vicent Nyerere, wakiwasili kwenye Uwanja wa Mkendo, Jimbo la Musoma Mjini, Mkoani Mara leo Oktoba 11, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni.Picha na  Othman Michuzi, Musoma. (Picha na Othman Michuzi)
 Umati mkubwa wa watu ukiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea wa urais wa Chadema.
 Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mara na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Musoma Mjini, Vicent Nyerere, akihutubia wananchi katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mkendo, Jimbo la Musoma Mjini, Mkoani Mara leo Oktoba 11, 2015.Picha na  Othman Michuzi, Musoma.
 Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Musoma katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mkendo, Jimbo la Musoma Mjini, Mkoani Mara leo Oktoba 11, 2015.Picha na  Othman Michuzi, Musoma.
 Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Musoma katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mkendo, Jimbo la Musoma Mjini, Mkoani Mara leo Oktoba 11, 2015.Picha na  Othman Michuzi, Musoma.
 Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Musoma katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mkendo, Jimbo la Musoma Mjini, Mkoani Mara leo Oktoba 11, 2015.Picha na  Othman Michuzi, Musoma.

STARS YAWASILI, KOCHA AAHIDI KUFANYA VIZURI KATIKA MCHEZO WAO DHIDI YA ALGERIA

$
0
0
 Wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars wakiwasili kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo wakitokea Malawi katika mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018 zitakazofanyika Urusi. Katika mchezo huo Stars ililala kwa bao 1 na kufanikiwa kusonga mbele kutokana na mchezo wa awali Stars kushinda bao 2-0 na hivyo kusonga mbele kwa jumla ya mabao 2-1 ambapo itapambana na timu ya taifa ya Algeria. (Picha na Francis Dande)
 Wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars wakiwasili kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo wakitokea Malawi katika mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018 zitakazofanyika Urusi. Katika mchezo huo Stars ililala kwa bao 1 nakufanikiwa kusonga mbele ambapo itapambana na timu ya taifa ya Algeria.  
 Wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars wakiwasili kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo 
Kocha wa Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa akiwa na tabasamu baada ya kuwasili leo akityokea Malawi ambapo Stars ilipambana na Malawi. 

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAKUTANA NA VYAMA VYA SIASA

$
0
0

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi jaji mstaafu, Damian Lubuva akitoa hotuba yake.

  HOTUBA YA UFUNGUZI YA MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KATIKA MKUTANO WA TUME NA VIONGOZI  WA VYAMA VYA SIASA KATIKA UKUMBI WA NEW AFRICA HOTEL TAREHE 12/10/2015.
Viongozi wa Vyama vya Siasa,
Mheshimiwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa Ya Uchaguzi,
Waheshimiwa Makamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,
Mkurugenzi wa Uchaguzi,
Inspekta Jenerali wa Polisi,
Msajili wa Vyama vya Siasa,
Viongozi wa Serikali,
Watendaji wa Mradi wa Uimarishaji wa Demokrasia (DEP),
Watendaji wa Tume,
Waandishi wa Habari,
Mabibi na Mabwana.
Kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, napenda kuchukua nafasi hii kuwakaribisheni wote katika Mkutano huu wa kujadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali  ya  Uchaguzi pia  kupeana taarifa kuhusu maandalizi ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 25 Oktoba 2015.

Pamoja na kwamba mna majukumu mengi na ya muhimu mmetambua umuhimu wa mkutano wetu na mmekuja kuhudhuria mkutano huu kama ilivyotarajiwa. Tume imefarijika  sana kukutana nanyi siku ya leo na tunawashukuru kwa moyo mliyoonyesha katika mchakato huu wa maandalizi ya Uchaguzi na wa kututhamini na kuja kuhudhuria Mkutano wetu.

Viongozi wa Vyama vya Siasa,
Pamoja na changamoto mbalimbali mnazokabiliana nazo  katika kutekeleza majukumu yenu kisiasa  ni ukweli ulio dhahiri, kuwa Viongozi wa Vyama vya Siasa ni Wadau  muhimu wa  Uchaguzi ambapo  mkishirikiana kutekeleza majukumu yenu kwa ufasaha mtaleta mafanikio katika uendeshaji wa Uchaguzi.

Viongozi wa Vyama vya Siasa,
Vyama vya Siasa vina nafasi kubwa katika kuelimisha na kuhamasisha jamii, Tume inaamini kwamba ili Mpiga Kura aweze kufanya maamuzi sahihi ni muhimu kwake kupate Elimu sahihi. hivyo basi, Tume inatarajia kuona mkitumia majukwaa yenu vyema katika kuhamasishaji na kuelimishaji si tu wanachama wenu bali jamii nzima ya watanzania

Viongozi wa Vyama Vya Siasa
Kuelekea Uchaguzi Mkuu, Tume imeaandaa vituo vya kupigia kura 64,736, ambapo, Tanzania Bara ni Vituo 63, 156 na Zanzibar ni Vituo 1,580. Kila kituo kitakuwa na uwezo wa kuhudumia  Wapiga Kura  450 na wasiozidi 500. Hata hivyo Kituo kinapokuwa na  wapiga Kura zaidi ya 500 kinabidi kigawanywe ili viwe viwili yaani Kituo “A” na Kituo “B” na namba ya Wapiga Kura itakuwa nusu kwa nusu.  Wapiga Kura wanashauriwa kwenda katika vituo walivyojiandikishia kupiga kura siku nane (8)  kabla ya siku ya kupiga kura ili kuweza kujua Vituo vyao halisi vya kupigia kura. 
Sambamba na hilo wananchi wataweza kupata taarifa zao zilizoko kwenye kanzidata (Database) kwa kutumia simu zao za kiganjani kupitia ujumbe mfupi wa maneno ‘sms’ bila wao kulazimika kufika vituoni, namba hiyo ni *152*00# na kufuata maelekezo. Au kupitia Tovuti ya Tume ambayo ni (www.nec.go.tz)

MDAHALO WA TAASISI YA MWALIMU NYERERE WATAKA AMANI, UMOJA NA HAKI KATIKA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 25, 2015

$
0
0
Mtoamada katika Mdahalo kuhusu Amani, Umoja na Haki Tanzania, Bw. Humphrey Polepole akielezea mawazo yake mbele ya washiriki katika ukumbi wa Ubungo Plaza Dar es Salaam jana nyuma ni Balozi Getrude Mongela. Mdahalo huo uliorushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha ITV. Picha na Said Ng’amilo.
Washiriki waliohudhuria katika mdahalo kuhusu Amani Umoja na Haki uliofanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza Dar es Salaam jana.
Mwendesha mdahalo.
Watoto waliohudhuria katika katika Mdahalo kuhusu Amani Umoja na Haki.

LAFARGE TANZANIA YAZINDUA SARUJI MPYA “TEMBO SUPASET 42.5”

$
0
0
 Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Lafarge Tanzania, Allan Chonjo (wa kwanza kulia) akizungumza machache mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa chapa mpya ya saruji iitwayo “Tembo Supaset 42.5”leo Oktoba 12, 2015 katika ofisi zao jijini Dar es Salaam. Anayemfuatia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania, Catherine Langreney pamoja na Mkurugenzi wa Mauzo, Stanslaus Mmbaga. Picha zote na Cathbert Kajuna.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania, Catherine Langreney (katikati) akishangilia pamoja na Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Lafarge Tanzania, Allan Chonjo (wa kwanza kulia) pamoja na akiwa na Mkurugenzi wa Mauzo, Stanslaus Mmbaga mara baada ya uzinduzi wa chapa mpya ya saruji iitwayo “Tembo Supaset 42.5” katika ofisi zao jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Lafarge Tanzania, Allan Chonjo (wa kwanza kulia) akizungumza machache mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa chapa mpya ya saruji iitwayo “Tembo Supaset 42.5” katika ofisi zao jijini Dar es Salaam. Anayemfuatia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania, Catherine Langreney pamoja na Mkurugenzi wa Mauzo, Stanslaus Mmbaga.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania, Catherine Langreney (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa chapa mpya ya saruji iitwayo “Tembo Supaset 42.5” katika ofisi zao jijini Dar es Salaam. ambapo alisema Tembo Supaset ni matokeo ya utafiti makini uliofanywa na wataalamu wetu na imetengenezwa mahususi kukidhi mahitaji ya soko.
 Waandishi wa habari pamoja na wageni walioungana katika uzinduzi wa chapa mpya ya saruji iitwayo “Tembo Supaset 42.5”
---
Ikiwa ni jitihada mahususi kuwapa saruji imara zaidi wakandarasi na wafyatuaji matofali Lafarge Tanzania imezindua chapa mpya ya saruji iitwayo “Tembo Supaset 42.5” ambayo ni imara na mahususi kwa ufyatuaji matofali, zege, majengo makubwa pamoja na miradi mikubwa ya miundombinu kama madaraja, barabara na majukwaa ya michezo.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo leo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania, Catherine Langreney alisema kwamba Tembo Supaset 42.5 ni saruji maalum iliyobuniwa ili kukidhi ongezeko kubwa la mahitaji ya saruji imara na inayokauka haraka katika soko la ufyatuaji matofali na zege na ujenzi mkubwa “Tembo Supaset ni matokeo ya utafiti makini uliofanywa na wataalamu wetu na imetengenezwa mahususi kukidhi mahitaji ya soko.”alisema.
Akizungumzia kuhusu maendeleo katika sekta ya ujenzi Langreney alisema kwamba kwa ujumla thamani ya sekta ya ujenzi nchini Tanzania inakadiriwa kuwa dola bilioni. Sekta hiyo ilikua kwa asilimia 7.8 mwaka 2014 na ni sawa na asilimia 8.6 ya pato la taifa ikiwa ni kutokana na ujenzi binafsi, usafirishaji na miradi mikubwa ya ujenzi. Tanzania ina idadi ya zaidi ya milioni 44 kufikia mwaka 2014 na inatarajiwa kuongezeka sambamba na ongezeko la mahitaji ya nyumba na miundombinu.”
Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Lafarge Tanzania, Allan Chonjo alisema kuwa Tembo Supaset ambayo itauzwa kwenye soko la jumla na rejareja ikiwa katika ujazo wa kilo 50 ni saruji imara zaidi ikiwa na ubora kuliko saruji nyingine zilizopo kwenye soko kutokana na uimara pamoja na bei shindani ambazo zimepangwa na itakidhi mahitaji ya watumiaji kama vile:
• Kuimarika mapema jambo ambalo litawaongezea tija wazalishaji bidhaa zinazotokana na zege
• Ukaukaji wa haraka jambo litakaloyafanya matofali yaweze kuhamishika haraka na kuongeza tija wazalishaji
• Mchanganyiko mzuri wa zege na matumizi kidogo ya maji kuimarisha.
Chonjo alisema kwamba Tembo Supaset imezinduliwa ili kukidhi mahitaji ya soko kuwa na saruji imara zaidi huku akitarajia saruji hyo kupanua soko la Lafarge Tanzania hususani kwa wafyatuaji ambao hutegemea saruji inayoimarika haraka katika kazi yao. “Mbali na uimara, faida nyingine ya Supaset ni kuweza kudumu kwa muda mrefu ikiwa na maana kwamba majengo yatakayojengwa kwa saruji hiyo yatadumu zaidi”
Alisema neno Supaset linamaanisha uimara kutokana na kukauka mapema na kukaa muda mrefu zaidi katika uimara na saruji hiyo ni sehemu ya saruji za chapa ya Tembo.

KAMANDA MPINGA AKABIDHI TBL,RIPOTI YA UPIMAJI AFYA ZA MADEREVA

$
0
0
 KAMANDA wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Kamishna Mohamed Mpinga (katikati), akikabidhi Ripoti ya upimaji wa Afya za Madereva kwa Meneja Mahusiano ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Emma Oriyo, Dar es Salaam jana, baada ya zoezi la kupima Afya za madereva lililofanyika Mikese, mkoani Morogoro, Msata mkoani Pwani na Segera, mkoani Tanga. Kushoto ni Kamanda wa Kikosi cha Afya cha Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi, Paul Kasabago.
 KAMANDA wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Kamishna Mohamed Mpinga (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, baada ya kukabidhi Ripoti ya Upimaji wa Afya za Madereva kwa Meneja Mahusiano ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Emma Oriyo. (Kushoto ni Kamanda wa Kikosi cha Afya cha Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi, Paul Kasabago.
 Meneja Mahusiano ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Emma Oriyo, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana baada ya kupokea Ripoti ya Upimaji wa Afya za Madereva kutoka kwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Mohamed Mpinga (katikati), ambaye pia aliipokea kwa Mkuu wa Kikosi cha Afya cha jeshi hilo, Kamishna Msaidizi Paul Kasadago (kushoto).
KAMANDA wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Kamishna Mohamed Mpinga (katikati), akionyesha Ripoti ya upimaji Afya za MAdereva, baada ya kuipokea kutoka kwa Kamanda wa Kikosi cha Afya cha Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Paul Kasabago, Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Mahusiano ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

MABADILIKO KATIKA UPASUAJI WA UVIMBE WA SARATANI

$
0
0
Dk. Umanath Nayak, mshauri mkuu wa  magonjwa ya saratani ya kichwa na shingo pamoja na upasuaji kwa njia ya roboti katika hospitali ya saratani ya Apollo Hyderabad nchini India

Na Mwandishi Wetu
 
Sekta ya afya duniani imeshuhudia mapinduzi yanayolenga kuongeza umri wa kuishi, ubora wa maisha, njia mbadala za uchunguzi, njia bora za matibabu, na pia ufanisi na ubora katika huduma za afya. Teknohama imekuwa na mchango mkubwa sana katika maendeleo ya ndani ya sekta hii muhimu. Makampuni yanayohusika na kutengeneza vifaa vya tiba hivi sasa yanalenga katika kutengeneza roboti ambazo hufanya upasuaji kwa ufanisi zaidi bila madhara makubwa kwa mgonjwa.

Kuna matumaini sana katika upasuaji kwa kutumia teknolojia ya Roboti. Teknolojia hii ni ishara ya mapinduzi katika sekta ya afya, na ni moja ya mambo muhimu yanayoongelewa sana katika upasuaji hivi leo. Mfumo wa upasuaji kwa kutumia roboti umeletwa ili kusaidia katika upasuaji mgumu, ambao hufanyika kwa shida, au unaohusisha maeneo ambayo ni magumu kufikika na hatari. Kwa kutumia mikono maalumu inayopatikana katika Roboti hilo upasuaji huo urahisishwa zaidi.

Mikono ya Roboti hudhibitiwa na kompyuta inayoendeshwa na mpasuaji kwa kutumia mikono na miguu. Udhibiti huu ni sawa na ule wa mchezo wa video, maarufu kama ‘video game’ ambao huwezesha upatikanaji kwa usahihi zaidi wa maeneo magumu kufikika ikilinganishwa na njia iliyokuwa ikitumika awali ya  ‘laparoscopic’. 

Kutumia matundu madogo sana, upasuaji wa aina hii unaweza kuondoa uvimbe uliojificha pasipo uharibifu wa tishu na pia humsaidia mgonjwa kutokaa hospitalini muda mrefu pamoja kupona ndani ya muda mfupi. Teknolojia hii inapunguza hatari ya uharibifu wa mishipa na tishu katika eneo husika.

Upasuaji kwa kutumia Roboti unaweza kutumika kutibu hali mbalimbali kama vile magonjwa ya kina mama (gynaecologic), ikiwa ni pamoja kuondoa mfuko wa uzazi (hysterectomy), kutibu maambukizi kwenye leya ya ndani katika mfuko wa uzazi (endometriosis), uvimbe kwenye mfuko wa uzazi (fibroids uterine), saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya mfuko wa kizazi, fistula na viungo katika nyonga kutoka nje (pelvic organ prolapsed). 

Utaratibu wa upasuaji na ushonaji unaweza kufanyika kwa usahihi zaidi kupitia teknolojia hii. Kulingana na huduma ya afya inayoitajika na umri wa mgonjwa, upasuaji kutumia Roboti pia unaweza kusaidia kuboresha afya ya uzazi na kumsaidia mgonjwa uwezo wa kuzaa.

Kwa wagonjwa wa saratani, mara nyingi upasuaji wa aina hii huusisha upasuaji wa  kichwa, shingo, ulimi, tezi dume, magonjwa ya wanawake, kuondoa uvimbe kwenye utumbo (colorectal surgery) na upasuaji unaohusisha nyonga.  

Mfumo huu wa upasuaji una msaada mkubwa kwa wagonjwa ambao wanahitaji upasuaji wa tezi upasuaji unaohusisha kuchana sehemu ya chini ya shingo. Kwa kutumia roboti sasa inawezekana kufanya upasuaji wa tezi bila kuchana shingo kwa sehemu kubwa na bila kuacha kovu inayoonekana.

Dk Umanath Nayak, mshauri mkuu wa wa magonjwa ya saratani ya kichwa na shingo pamoja na upasuaji kwa njia ya roboti kutoka hospitali ya saratani ya Apollo Hyderabad India ameelezea faida ya upasuaji kwa kutumia Roboti. Anasema kuwa,"teknolojia ya kutumia Robot katika upasuaji itadumu sana kama tunaweza kuona faida nyingi za teknolojia hii ikilinganishwa na njia mbalimbali za zamani za upasuaji. 

Ni hatua ya pili ya upasuaji kwa kutumia mashine maalumu huku ukiangalia kwenye Skrini ya computer (laparoscopic). Hii itapunguza haja ya kufanya upasuaji wa wazi kwa wagonjwa wenye matatizo ya uzazi "
Anaongeza kuwa, "Upasuaji wa kutumia Robot ni njia mpya ya upasuaji ya isiyo na madhara na inajumuisha upasuaji wa kawaida (Open surgery) na Upasuaji wa kutumia skrini ya computer (laparoscopic). Kwa msaada wa Mikono maalumu ya Robot inayodhibitiwa, daktari anaweza kufanya upasuaji kupitia mikato midogo sana. Teknolojia hii husababisha kutokuwa na makovu makubwa yatokanayo na kukatwa sana, kutokuwepo na upungufu wa damu, maumivu baada ya upasuaji na kupona kwa haraka zaidi ".
Aidha mtaalamu wa magonjwa ya saratani nchini Dk. Harrison Chuwa, anasema kuwa “upasuaji kwa njia ya roboti ni njia kuu ya kufanya upasuaji ambayo itapunguza mapungufu ya kibinadamu na hata kovu la operesheni kuwa dogo ambalo aliweze kufanya mwili wako kuonekana tofauti na ulivyokuwa awali. Faida nyingine ya upasuaji kwa njia ya roboti ni kwamba unahitaji rasimali kidogo ya binadamu ili kufanikisha kazi hii.
Teknolojia ya roboti haipatikani nchini Tanzania, lakini watanzania wengi wanasumbuliwa na saratani za kichwa na shingo na mfumo wa mkojo (mfano. kibofu), uzazi, upasuaji wa utumbo mkubwa, na matatizo mengine wamepata huduma hii mara kadhaa pale walipopata rufaa ya kwenda kutibiwa katika hospitali za Apollo nchini India.
Ishara nyingine nyingi bado zina mjadala kwa maana njia hii ni mpya tokea upasuaji wa laparoscopic uanzishwe. Muda unavyosogea, upasuaji kwa njia ya roboti unatarajiwa kuchukua nafasi za upasuaji wa kawaida wa saratani na utakuwa ni msaada na kimbilio kwa wengi wanaoteseka na saratani na mapungufu mengine.  Inaweza tokea siku hapo baadae wakati daktari wa upasuaji amekaa ofisini kwake na anamfanyia mgonjwa operesheni au upasuaji akiwa mbali kwa msaada wa mfumo wa roboti.
Mwaka jana, Hospitali Apollo mjini Apollo Chennai na Hyderabad imefanikiwa kufanya upasuaji mfululizo wa tezi kupitia teknolojia hii. Hakuna shaka kwamba upasuaji wa kutumia Robot ni kifaa muhimu katika masuala ya upasuaji, mchango huu muhimu unajidhihirisha hata katika nchi zinazoendelea.

Kuhusu Hospitali ya Apollo

Hospitali za Apollo ni za kwanza katika eneo Asia Pacific kutoa huduma za upasuaji kwa kutumia mfumo huu wa Robot, ambayo ni aina ya upasuaji isiyokuwa na madhara. Taasisi ya upasuaji kutumia Robot iliyopo hospitalini hapo wamejitoa kipekee katika kutoa huduma bora kwa wagonjwa.

Taasisi ina wataalamu waliobobea kwenye mafunzo ya upasuaji, upendo katika utoaji wa huduma vifaa vya matibabu vya kisasa vinavyolenga kutoa uzoefu bora kwa mgonjwa. Vifaa hivyo ni pamoja na vifaa Robot ya Da Vinci inayotumika katika upasuaji.

Mfumo huu wa upasuaji hutumika katika teknolojia ya upasuaji wa magonjwa yanayohusiana na mfumo wa mkojo (Urology), magonjwa ya wanawake (Gynaecology), moyo, utumbo, na magonjwa ya watoto na matatizo ya uti wa mgongo.

KIGODA KUZIKWA LEO

$
0
0
 Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, na Mgombea ubunge Jimbo la Handeni kupitia CCM, marahemu Dk Abdallah Kigoda wakati wa mapokezi ya mwili huo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam jana, ukitokea nchini India.

Na Mwandishi Wetu
 
 MWILI  wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda  leo unatarajiwa  kuzikwa  kijijini kwao huko Wilayani  Handeni  Mkoani Tanga.

Mwili huo ulipokelewa jana  katika Uwanja wa Ndege ukitokea nchini India alikokuwa amelazwa.

Mwenyezi Mungu ailaze Mahala Pema Peponi.
AMEN
 Dk Magufuli akimfariji mtoto wa marehemu Dk Kigoda kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam
 Mkuu wa Mkowa wa Tanga, Mwantumu Mahiza akimfariji mjane wa marehemu Dk Kigoda, Rasul Kigoda

Mkutano wa Baraza la Vyama Vya Siasa wafanyika Zanzibar

$
0
0
Viongozi wa Meza Kuu wakiwa wamesimama wakati wa kuomba Dua Mkutano huo wa Baraza la Viongozi wa Vyama vya Siasa Tanzania uliovikutanisha Viongozi wa Vyama 22 vya Siasa Tamzania uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya bwawani Zanzibar.wa kwanza Jaji Lubuva Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Mzirai na Msajili Msaidi wa Vyama vya Siasa Tanzani Mhe Ibrahim Mkwawa.
Mmoja wa Viongozi wa Vyama vya Siasa Tanzania akiuombea Mkutano huo wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Bwawani Zanzibar. ukizungumzia maadili ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 
 Viongozi wa Vyama vya Siasa wakiitikia dua kabla ya kuaza kwa mkutano huo kuutakia baraka 
 Katibu wa Baraza la Vyama vya Siasa Mhe. Jaji Francis S.K. Mutungi, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania Mhe Peter Mzirai kuaza kwa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Bwawani Zanzibar na kuwashirikisha Viongozi wa Vyama 22 vya Siasa Tanzania.
Viongozi wa Vyama vya Siasa wakimsikiliza Mtoa Mada Msaidizi Msaidi wa Vyama vya Siasa Tanzania Mhe Ibrahim Mkwawa, akiwasilisha mada ya Maadili iliotiwa saini na Viongozi wa Vyama vya Siasa kuhusiana na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
Msajili Msaini wa Vyama vya Siasa Tanzania Mhe Ibrahim Mkwawa akiwasilisha Mada ya Maadili ya Vyama vya Siasa kuhusiana na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya bwawani Zanzibar na kuwashirikisha Viongozi wote wa Vyama vya Siasa vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu mwezi huu. 
Viongozi wa Vyama vya Siasa wakifuatilia Mkutano Huo. katika ukumbi wa hoteli ya bwawani Zanzibar.
Viongozi wa Vyama vya Siasa wakiwa makini wakifuatilia mkutano huo wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania ukizungumzia Maadili ya Uchaguzi Mkuu wa Tanxzania unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
Viongozi wa Chama cha TADEA wakifuatila mkutano huo wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania. 
Viongozi wa Chama cha AFP wakifuatilia mkutano huo kwa makini unaozungumzia Maadilidi ya Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya bwawani Zanzibar.
Imetayarishwa na OthmanMapara. Blogspot Zanzinews.com

DK MAGUFULI AUNGURUMA KISARAWE, UKONGA

$
0
0
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akinyooshewa vidole gumba na wakazi wa Jimbo la Ukonga ikiwa ni ishara ya kukubali kumpigia kura ya ndiyo , wakati wa mkutano wa kampeni eneo la Moshi Bar, Ukonga Dar es Salaam.

 Dk Magufuli aiomba kura kwa wananchi wakati wa mkutano wa kampeni Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam leo.

 Dk Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Ukonga kupitia CCM, Jerry Silaa wakati wa mkutano wa kampeni jimboni humo leo.

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akiagana na wakazi wa Jimbo la Ukonga baada ya kuhutubia  mkutano wa kampeni eneo la Moshi Bar, Ukonga Dar es Salaam
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akiagana na wakazi wa Jimbo la Ukonga baada ya kuhutubia  mkutano wa kampeni eneo la Moshi Bar, Ukonga Dar es Salaam.

MAPOKEZI DIAMOND BALAAA

$
0
0
 Msanii wa muziki wa kizazi kimpya Nassib Abdul 'Dimond Platinumz' akiwa ameshika mojo kati ya tuzo tatu alizotwaa za Afrimma mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo akitokea Marekani. (Picha na Francis Dande)
Msanii wa muziki wa kizazi kimpya Nassib Abdul 'Dimond Platinumz' akisindikizwa na mashabiki kwa miguu mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul ‘Diamond Platinumz’, leo amepata mapokeza ya aina yake kutoka kwa mashabiki wake wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Diamond aliwasili majira ya mchana akitokea nchini Marekani ambako alitwaa tuzo tatu za Afrimma.

"Nawashukuru wale wote walionisapoti mpaka kufikia hatua hii" alisema Diamond wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuongeza kuwa atahakikisha anajituma zaidi ili kutoa nyimbo kali zaidi.

Msafara wa Diamond ulitoka Uwanja wa Ndege kwa miguu kuelekea nyumba kwao Tandale na baadae katika Ufukwe wa Esca One ambapo alitarajiwa kufanya mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya kuwashukuru mashabiki wake na watanzania kwa ujumla baada ya kutwaa tuzo hizo.

Hata hivyo msafara wake ulishindwa kuendelea na safari kwa miguu baada ya Polisi kuuzuia katika eneo la Vingunguti na kumolazimisha msaii huyo kupanda gari.

STUDIO YALETA BURUDANI DAR, MWANZA, ARUSHA NA MBEYA

$
0
0
 Ma Dj walikuwa wakifanya mambo kuhakikisha mambo yanakuwa mazuri.
 *************
Onyesho la muziki la Coke Studio ambalo linajumuisha Kolabo ya wanamuziki wa kitanzania kwa kushirikiana na wanamuziki wan je limeanza kurushwa nchini Jumamosi nchini kupitia luninga ya Clouds ikiwajumuisha wanamuziki Ally Kiba,Vanessa Mdee,Ben Pol na Fid Q ambao wanashirikiana na wanamuziki Wangechi,Maurice Kirya,Victoria Kimani na 2Face.
Baada ya uzinduzi huo zilifanyika party za kukata na shoka katika viwanja vya maraha sehemu mbalimbali nchini ikiwemo mikoa ya Dar es Salaam,Mwanza,Mbeya na Arusha zilzowajumuisha vijana kucheza muziki,kuimba na kufurahi na kujishindia zawadi mbalimbali za Coca Cola
 Wadau mbalimbali ndani ya Coce Studio Party
 Baadhi ya mayanki waliohudhuria Coke Studio party wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye ukumbi wa Maisha Club jijini Dar es Salaam.
 Ilikuwa ni burudani kubwa vijana wakicheza muziki kwa furaha ndani ya Maisha Club.
 Vijana wakishiriki kuimba Coke Studio Party mkoani Mwanza.
 zawadi mbalimbali zilitolewa katika party ya Mwanza kama anavyoonekana Masai akijichukulia zawadi katika party ya Mwanza.
 Ma Dj walikuwa wakifanya mambo kuhakikisha mambo yanakuwa mazuri.
Watu wa rika mbalimbali walifika CokeStdi party kupata burudani kama wanavyoonekana baadhi yao pichani mjini mwanza.
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>