Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

RAIS KIKWETE MGENI RASMI TAMASHA LA KUOMBEA AMANI UCHAGUZI MKUU

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandali ya Tamasha la kuombea Amani na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, Alex Msama akifafanua jambo Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki, wakati akimtangaza Rais Jakaya Kikwete kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo, litakalofanyika Oktoba  4  kwenye uwanja wa Taifa. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Hamisi Pembe. (Picha na Loveness Bernard)
  
NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Jamnuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha  maalumu la kuombea amani Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 25.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati inayoratibu tamasha hilo, Alex Msama alisema ni faraja kubwa kwao kuona Rais anakubali mwaliko wao wa kuwa mgeni rasmi.

“Tumefurahi sana kuona Rais wa nchi anakubali kuwa mgeni rasmi katika tukio hilo la kuombea amani Uchaguzi Mkuu kwa manufaa ya taifa letu, sisi tukiwa waratibu wa tukio hili tumefarijika mno,” alisema Msama.

Alisema tukio hilo litakalowaleta pamoja viongozi wa kada zote wakiwamo wale wa madhehebu na dini mbalimbali bila ubaguzi, litasindikizwa na burudabi ya nyimbo za injili kutoka kwa waimbaji wa ndani na nje ya nchi.

Msama alisema Kamati ya maandalizi iliamua kumuomba Rais Kikwete sio tu kwa kutambua nafasi yake katika taifa, pia moyo wake wa kuhimiza amani wakati wote wa utawala wake ikiwemo kushiriki matamsha ya injili.

Alisema, mbali ya kuwaongoza Watanzania kuombea taifa lao lipite salama katika uchaguzi mkuu, pia wadau wa muziki wa injili watalitumia tukio hilo kumuga na kumshukuru kwa mchango wake katika kukuza muziki wa injili.

Akifafanua nafasi ya Rais Kikwete kukuza muziki huo, Msama alisema katika harakati zake za kuratibu matukio ya muziki wa injili, kiongozi huyo amewahi kuwa mgeni rasmi katika tamasha la Pasaka mwaka 2011.

Msama alisema kitendo cha Kikwete kutokuwa mbaguzi wa dini, ndio maana Kamati ya kuratibu Tamasha la kuombea Amani Uchaguzi Mkuu imempa heshima kutokana na kuwa kielelezo cha amani na mshikamano.

Alisema ujumbe mahususi katika Tamasha hilo ni kwamba, suala la amani na utulivu, ni jukumu la kila mmoja kwa nafasi yake kwani thamani ya tunu ya amani haiwezi kuonekana kwa wepesi hadi pale inapotoweka.

Msama alisema Kamati yake imejitwisha jukumu hilo la kuhimiza amani katika uchaguzi mkuu kutokana na kuwepo kwa viashiria vya uvunjivu wa hiyo amani kutokana ushindani mkali uliopo katika uchaguzi wa safari hii.

Ushindani mkali katika uchaguzi huo umetuama kati ya mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa anayeungwa mkono na vyama vinne ninavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na Dk. John Magufuli wa CCM.

Msama alisema, baada ya uzinduzi kufanyika Uwanja wa Taifa siku hiyo ambapo kiingilio kitakuwa sh 5000; 3000 kwa wakubwa na sh 1,000 kwa watoto, tamasha hilo litaelekea katika mikoa 10 kuhamasisha amani.

Miongoni mwa waimbaji wa kigeni waliothibitisha kushiriki na nchi zao kwenye mabano ni Solly Mahlangu na Sipho Makhabane (Afrika Kusini), Ephraem Sekereti (Zambia), Anastazia Mukabwa na Solomon Mukubwa Kenya.

UZINDUZI WA KAMPENI WA KAMPENI JIMBO LA HAI

$
0
0
 Baadhi ya wafuasi wa Ukawa wakiwa katika mkutano wa kampeni  kwenye Uwanja wa Half London eneo la Bomang’ombe Wilaya ya Hai Moshi
 Mgombea urais wa Edward Lowassa, akimnadi Mgombea ubunge wa Jimbo la Hai Freeman Mbowe katika  mkutano wa kampeni  kwenye Uwanja wa Half London eneo la Bomang’ombe Wilaya ya Hai Moshi
 Mfuasi wa Chadema akitoka kwenye jeneza lilioandikwa mwisho wa CCM kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea urais wa chama hicho , Edward Lowassa, katika Uwanja wa Half London eneo la Bomang’ombe Wilayaa ya Hai Moshi.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro.
 Mgombea urais wa Edward Lowassa, akihutubia mkutano wa kampeni  kwenye Uwanja wa Half London eneo la Bomang’ombe Wilaya ya Hai Moshi.
Mgombea urais wa Ukawa, Edward Lowassa, akiwa amembeba mtoto Sayuni Nassari wa Mgombea ubunge Arumeru Mashariki Joshuaa Nassari wakata wa  mkutano wa kampeni  kwenye Uwanja wa Half London eneo la Bomang’ombe Wilaya ya Hai Moshi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, wakiwapungia wananchi wa mji wa Bomang'ombe, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro. (Picha na Othman Michuzi)

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZOKUFUATIA KIFO CHA WAZIRI CELINA KOMBANI MIKOCHENI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akisaini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo kufuatia kifo cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina Kombani kilichotoke Nchini India juzi, wakati Makamu wa Rais alipokwenda nyumbani kwa marehemu Mikocheni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akifariji watoto wa Familia ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Marehemu Celina Kombani wakati alipofika nyumbani marehemu Mikocheni     Dar es salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akizungumza na Mume wa Marehemu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina Kombani, alipokwenda nyumbani kwa marehemu Mikocheni Dar es salaam leo Sept 27,2015 kwa ajili ya kusaini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo na kuifariji familia ya marehemu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akizungumza na Mume wa Marehemu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina Kombani, alipokwenda nyumbani kwa marehemu Mikocheni Dar es salaam leo Sept 27,2015 kwa ajili ya kusaini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo na kuifariji familia ya marehemu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akifariji watoto wa Familia ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Marehemu Celina Kombani wakati alipofika nyumbani marehemu Mikocheni     Dar es salaam.

TANZANIA KUPATA BILIONI 992 KUBORESHA UMEME

$
0
0
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone:255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425




PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Sasa ni Rasmi: Tanzania kupata mabilioni mengine ya MCC
·         Yafaulu mtihani wa kupata bilioni 992.8 za kuboresha sekta ya umeme
·         Yafanikiwa baada ya kutimiza masharti yote likiwemo la kupambana na rushwa
·         Zitaanza kutolewa mwakani baada ya kupigiwa kura na Bodi ya MCC

Tanzania imetimiza masharti yote ya kupatiwa raundi ya pili ya fedha za maendeleo kutoka Shirika la Maendeleo ya Milenia la Millennium Challenge Corporation (MCC) la Marekani na itaanza kupata na kunufaika na mabilioni hayo ya fedha baada ya wajumbe wa Bodi ya MCC kupiga kura ya kuidhinisha kutolewa kwa fedha hizo chini ya Mpango wa MCC-2.

Habari hizo njema zimetangazwa Jumamosi, Septemba 26, 2015, kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, na Mtendaji Mkuu wa MCC, Bi. Dana J. Hyde katika mkutano uliofanyika katika Hoteli ya JW Marriot Essex House, New York, na kuhudhuriwa na watumishi waandamizi wa MCC akiwamo Bwana Kamran Khan, Makamu wa Rais wa Operesheni za MCC. Rais Kikwete yuko New York kuhudhuria shughuli za mwaka huu za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. 

“Hongera Mheshimiwa Rais kwa sababu nchi yako, Tanzania imetimiza masharti yote ya kupata fedha nyingine chini ya mpango wa MCC - 2, ikiwa ni pamoja na uongozi wa MCC kuridhika kuwa Tanzania inachukua hatua za dhati kupambana na rushwa,” Bi. Hyde amemwambia Rais Kikwete na viongozi wengine wa Tanzania akiwamo Waziri wa Nchi za Fedha wa Zanzibar, Mheshimiwa Yusuf Omar Mzee.

Bi. Hyde amemwambia Rais Kikwete kuwa Bodi ya MCC, katika mkutano wake wa Septemba 17, mwaka huu na chini ya Mwenyekiti wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Bwana John Kerry, imeafiki kuhusu kipengele pekee kilichokuwa kimebakia katika masharti ya kupata fedha za MMC kuwa ni kweli Tanzania inakabiliana ipasavyo na rushwa na kuchukua hatua stahiki kukabiliana na janga hilo la rushwa.

MCC imetoa taarifa ya kuthibitisha kuwa Tanzania imetimiza masharti ya kuiwezesha kufaulu kupata raundi ya pili ya fedha za maendeleo na pia imetoa taarifa ya kuthibitisha kuwa ni kweli Bodi ya MCC imeridhishwa na hatua zinazochukuliwa kukabiliana na rushwa.

Tofauti na fedha nyingi zinazotolewa na wafadhili wengi duniani, fedha za MCC hazitakiwi kurudishwa na nchi inayopewa fedha hizo na pia nchi husika hupewa uhuru wa kuchagua aina ya miradi ya maendeleo ambayo inaitaka igharimiwe na fedha hizo.

Miongoni mwa wajumbe wengine wa Bodi ya MCC ni pamoja na Waziri wa Fedha wa Marekani ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi, Mwakilishi wa Biashara wa Marekani duniani, Mwendeshaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), nafasi ambayo kwa sasa anaikaimu Bwana Alfonsi Lenhardt, Mtendaji Mkuu wa MCC Bi. Hyde na Rais wa Taasisi ya International Republican Institute (IRI) Balozi Mark Green.

Mabalozi Lenhardt na Green walikuwa mabalozi wa Marekani katika Tanzania wakati wa majadiliano, upitishaji na utekelezaji wa MCC–1. 

Bi Hyde amesema sasa linalobakia ni kwa wajumbe wa Bodi kupelekewa muhtasari wa kuidhinisha mabilioni hayo kwa Tanzania ambayo chini ya mpango wa uwekezaji wa MCC–2 yatakwenda katika kuboresha huduma za umeme katika Tanzania ikiwa ni pamoja na kusambaza umeme katika vijiji vingi zaidi nchini. Kiasi cha asilimia 46 ya Watanzania kwa sasa wanapata umeme kutoka asilimia 10 ya mwaka 2005 na sehemu kubwa ya asilimia hiyo imetokana na msaada wa MCC-1.

Chini ya Mpango huo wa pili wa MCC, Tanzania itapatiwa kiasi cha dola za Marekani milioni 472.8 (sawa na sh. bilioni 992.80). Kwa kutilia maanani kiasi cha dola milioni 698 (sawa na sh. trilioni 1.46) ambazo zilitolewa chini ya MCC-1 basi Tanzania itakuwa imepata jumla ya dola za Marekani trilioni 2.45 za maendeleo kutoka Marekani katika kipindi cha miaka 10 tu iliyopita. Fedha za MCC-2 zitaanza kutolewa mwakani, 2016.

Kiasi kilichotolewa kwa Tanzania wakati wa MCC-1 ndicho kilikuwa kiasi kikubwa zaidi ambacho kimepata kutolewa na Marekani chini ya Mpango huo wa Millennium Challenge Corporation na kwa kupita MCC-2 Tanzania itakuwa ni nchi ambayo itakuwa imepata kiasi kubwa cha fedha za maendeleo chini ya MCC duniani.

Fedha zilizotolewa chini ya MCC -1 zilitumika kujenga Barabara za Tunduma-Sumbawanga, Tanga-Horohoro na Namtumbo-Songea-Mbinga.
Aidha, fedha hizo zilitumika kujenga upya mfumo wa huduma za maji kwa ajili ya miji ya Dar es Salaam na Morogoro na zilitumika kusambaza umeme katika vijiji vya mikoa 10 ya Tanzania Bara. 

Fedha hizo vile vile zilitumika kutandaza njia ya pili ya kusafirisha umeme chini ya Bahari ya Hindi kati ya Bara na Tanzania Visiwani na pia zilitumika kujenga barabara zote kuu za Kisiwa cha Pemba na baadhi ya barabara za Unguja kwa kiwango cha lami. 

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
27 Septemba, 2015

UPENDO NKONE AZINDUA ALBAMU YA TANO

$
0
0
Mwimbaji wanyimbo za injili, Upendo Nkone akiimba kwa hisia wakati wa uzinduzi wa albamu yake ya tano iitwayo ‘Omba Yesu Anasikia’ uliokwenda sambamba na kutimiza miaka 10 tangu aanze huduma ya uimbaji. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Francis Dande)
Waimabji wa nyimbo za injili, Masanja Mkandamizaji na Bonny Mwaitege wakiimba wakati wa uzinduzi wa albumu ya tano ya mwimbaji, Upendo Nkone uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Kwaya ya Rivers of Joy International-TAG-VCCT Beach ikiimba wakati wa uzinduzi huo.
 Meza Kuu.
 Upendo Nkone akiimba wakati wa uzinduzi huo.
Baadhi ya watu waliohudhulia uzindui huo wakicheza nyimbo za Upendo Nkone.

LHRC YAADHIMISHA MIAKA 20 TANGU KUANZISHWA KWAKE

$
0
0
 Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Septemba 26,1995, Jaji Mstaafu Osebia Munuo (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu cha maadhimisho ya miaka 20 cha LHRC yaliyofanyika Makao Makuu ya LHRC Kijitonyama Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya LHRC, Geoffrey Mmari na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk.Helen Kijo-Bisimba.
  Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Jaji Mstaafu Osebia Munuo (kushoto), akikata keki maalumu ya Maadhimisho ya miaka 20 cha LHRC yaliyofanyika Makao Makuu ya LHRC Kijitonyama Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya LHRC, Geoffrey Mmari na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk.Helen Kijo-Bisimba.
 Wimbo wa taifa ukiimbwa kabla ya kuanza maadhimisho hayo.
 Waimbaji wa Kwaya ya LHRC ya Mwalusanya wakiimba wa wimbo wa Taifa.
 Wimbo wa Taifa ukiimbwa.

 Kwaya ya LHRC ya Mwalusanya ikifanya vitu vyake katika maadhimisho hayo.
 Hapa ni Kwaya ya Mwalusanya ikiserebuka kwa kwenda mbele. 'Jamaa wa mbele kushoto yupo vizuri kiuchezaji chezea maadhimisho ya miaka 20 ya LHRC wewe'
 Mwenyekiti wa Bodi ya LHRC, Geoffrey Mmari (katikati), akitoa hutuba fupi katika maadhimisho hayo. Kulia ni Mwakilishi kutoka Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Rehema Ntimizi na kushoto ni Mgeni rasmi wa hafla hiyo, Jaji Mstaafu, Osebia Munuo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk.Helen Kijo-Bisimba (katikati), akisoma hutuba yake ya maadhimisho hayo. Kushoto ni Mjumbe wa LHRC, Emeliana Mboye.
 Meza Kuu ikionesha Kitabu cha Maadhimisho ya Miaka 20 tangu kuanzishwa LHRC baada ya kuzinduliwa kwenye hafla hiyo. Kutoka kushoto ni Mdau wa LHRC, Profesa Chris Peter,  Mjumbe wa LHRC, Emeliana Mboye, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk.Helen Kijo-Bisimba, Mgeni rasmi wa hafla hiyo, Jaji mstaafu, Osebia Munuo, Mwenyekiti wa Bodi LHRC, Geoffrey Mmari na Mwakilishi kutoka Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Rehema Ntimizi.
 Mgeni rasmi Jaji Osebia Munuo akisoma hutuba yake.

MKUTANO WA KAMPENI ZA CCM MKOKOTONI MKOA WA KASKAZINI UNGUJA LEO

$
0
0
Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na WanaCCM na Wananchi na Wapenda amani katika Wilaya ya Kaskazini A Jimbo la Tumbatu katika Uwanja wa Sunrize Mkokotoni Mkoa wa kaskazini Unguja leo jioni. (Picha na Ikulu)

MAGUFULI AENDELEA NA KAMPENI ZAKE NDANI YA CHIMALA,MBARALI,MAKAMBAKO NA MAFINGA,KESHO KUUNGURUMA IRINGA MJINI

$
0
0
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mgombea Ubunge wa jimbo la Makambako Ndugu Deo Sanga wakiwaiambisha wananchi wa Mafinga katika uwanja wa Polisi Mwembetogwa mkoani Iringa leo Septemba 27 kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Mafinga katika uwanja wa Mafinga mkoani Iringa leo Septemba 27 kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni. 
 Mmoj wa Waangalizi wa Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu,akifuatilia mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli mjini Makambako jioni ya leo Septemba 27 mkoani Iringa
????????????????????????????????????
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mufindi Kusini Ndugu Mahmoud Mgimwa akipiga push up mbele ya wakazi wa Mafinga waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli  ambaye anashuhudia tukio hilo katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vyaWambi  mjini Mafinga mkoani Iringa na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi.

Dk. John Pombe Magufuli amewaambia wakazi hao wasihadaike na maneno ya kisiasa yanayotolewa na vyama vingine kuwa nchi ya Tanzania haijapiga hatua ikiwa chini ya utawala wa CCM wakati maendeleo yanaonekana wazi na nchi inazidi kusonga mbele kwa mambo mengi ikiwemo amani na utulivu wa nchi.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa  Chimala,Mbarali mkoani Mbeya alipokuwa akielekea mkoani Iringa kuendelea na kampeni zake.
 gombea Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli akionesha hisia zake mara baada ya kuonana uso kwa uso na Kada Mkongwe wa chama cha CCM Ndugu Samwel Malecela mjini Mbarali kabla ya kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Kada Mkongwe wa chama cha CCM Ndugu Samwel Malecela mjini Mbarali kabla ya kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni,huku Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Ndugu  Bulembo akifuatilia kwa makini
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Rujewa mjini katika viwanja vya Barafu mjini Rujewa,wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya leo Septemba 27 kwenye mkutano hadhara wa kampeni.
  Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Rujewa mjini wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya leo Septemba 27 kwenye mkutano hadhara wa kampeni.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Makambako Ndugu Deo Sanga a.k.a Jah People akimuombea kura  Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mjini Ilembula leo Septemba 27 mkoni Mbeya
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge wa jimbo la Wanging'ombe Injinia Gerson Rwenge,katika mji wa Ilembula
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasili kwenye mjini Makambako kwenye uwanja wa Polisi Mwembetogwa mkoani Iringa leo Septemba 27 kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 wakazi wa Makambako wakishangilia wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akipanda jukwaani kwa kuruka ruka kuonesha yuko fiti kuwatumikia wananchi kwa namna yoyote ile.

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Ndugu Abdalah Bulembo akiwahutubia wakazi wa Makambako kwenye mkutano wa kumnadi mgombea urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli leo Septemba 27 mkoani Iringa
 Dkt Magufuli akiwasalimia wananchi wa Makambako kabla ya kuanza kuwahutubia na kuwaomba kura
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Makambako gombea Ubunge wa jimbo la Makambako Ndugu Deo Sanga wakiwaimbisha wananchi wa Mafinga katika uwanja wa Polisi Mwembetogwa mkoani Iringa leo Septemba 27 kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Wananchi wa mji wa Makambako wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake na kuwaomba wajitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura Oktoba 27 kwa kumpiga kura ya ndio na hatimae aibuke mshindi kwa nafasi ya Urais.

WAFANYAKAZI WA MGODI WA BUZWAGI WASHEREKEA SIKU YA FAMILIA NA FAMILIA ZAO

$
0
0
Eng.Philbert Rweyemamu akifafanua jambo katika moja ya mabanda ya maonyesho kwa baadhi ya maafisa wa uhamiaji walipokuwa wakitembelea mabanda ya maonyesho.
Eng.Philbert Rweyemamu akifafanua jambo katika moja ya mabanda ya maonyesho.
Wageni wakijionea namna mradi wa matofali ya gharama nafuu ulivyowanufaisha wenyeji wanaozunguka mgodi wa Buzwagi.
Wageni wakipata maelezo kutoka kwa wataalamu wa kampuni ya KALTIRE ambayo imekuwa ikihudumia mgodi wa Buzwagi kwa kuwauzia matairi kwa ajili ya mitambo ya uchimbaji mgodini hapo.
Wageni pamoja na baadhi ya maafisa wa mgodi wa Buzwagi na wale wa serikalini wakijionea matairi makubwa yanayotumika katika mgodi huo.
Wageni wakipata maelezo wakati walipotembelea banda la PANAF
Sehemu ya familia za wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi wakiwa wameketi baada ya kutembelea mabanda mbalimbali
Kama vile hawaamini!!!! Ni kweli anacheza na nyoka hivyo?
Kuhakikisha kumbukumbu hii haipotei kamera za simu zikafanya kazi yake
Kikundi hiki cha Ngoma kutoka Shinyanga kilitia fola kwa burudani safi ya Ngoma waliyoitoa.
Baadhi ya maafisa wakuu wa kampuni ya Acacia wakifuatilia burudani ya ngoma
Michel Ash-Afisa Mkuu wa Masuala ya uendeshaji wa kampuni ya Acacia akizungumza na familia pamoja na wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi
Baadhi ya maafisa wa idara ya ufanisi wa Mgodi wa Buzwagi wakiwa katika picha ya pamoja katika banda lao wakati wa maonyesho
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi mwenye shati la bluu akiongozwa na mkuu wa kitengo cha ulinzi Jamal Rwambol kutembelea mabanda ya maonyesho
Azael Kitange-Mkufunzi wa idara ya ufanisi wa kampuni akitoa maelezo kwa wageni walipotembelea banda la idara ya Ufanisi katika kitengo cha Mafunzo.
Ufugali wa nyuki wa kisasa ni moja kati ya shughuli zinazofanywa na mgodi wa Buzwagi kupitia idara ya Mahusiano ya Jamii kwa kuwawezesha wenyeji wanaozunguka maeneo ya mgodi kujipatia shughuli zinazowaongezea kipato.
Wataalamu wa idara ya afya wakionyesha baadhi ya vifaa mbalimbali vinavyotumika kupima afya za wafanyakazi wakati wote ili kuhakikisha afya za wafanyakazi wa mgodi huo muda wote zinakuwa salama.
Wataalamu wa miamba wakionyesha aina mbalimbali za miamba yenye dhahabu na namna wanavyotumia vifaa vya kisasa kuitafuta dhahabu.
Kikundi cha Ngoma cha kabila la wasukuma kikitoa burudani ya ngoma wakati wa maadhimisho ya siku ya familia kwa wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi
Baadhi ya wanafamilia wa wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi.
Baadhi ya maafisa kutoka Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu wakifurahia moja ya burudani wakati wa sherehe hizo.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Eng. Philbert Rweyemamu (katikati) na Meneja wa Biashara wa Mgodi huo wakifuatilia kwa makini burudani zilizokuwa zikiendelea wakati wa sherehe hizo, kushoto kwao ni mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Kahama.

Meneja Ufanisi wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Saimon Sanga akizungumza na wafanyakazi wa Mgodi huo wakati alipokuwa akimkaribisha meneja Mkuu wa mgodi wa Buzwagi.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Eng.Philbert Rweyemamu akizungumza na wafanyakazi wa Mgodi huo pamoja na familia zao wakati wa sherehe za siku ya familia.
Watoto wakishiriki michezo mbalimbali iliyokuwepo maalum kwa ajili yao
Watoto wakishiriki michezo wakati wa sherehe hizo.

Graham Crew-Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu (kushoto) akiteta jambo na Michelle Ash-Afisa Mkuu wa masuala ya uendeshaji wa kampuni ya Acacia wakati wa sherehe hiyo
Mtaalamu wa masuala ya uchimbaji wa Mgodi wa Buzwagi akitoa maelezo kwa wageni waliotembelea banda la idara yake.
Mmoja wa wafanyakazi wa wa Idara ya masuala ya usalama wa Mgodi wa Buzwagi akitoa maelezo kwa baadhi ya familia za watumishi wa mgodi huo wakati walipo tembelea banda maalum la maonyesho la idara ya usalama mgodini.
Mmoja wa wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi Bwana Moses Msofe akiwa na familia yake kusherekea siku ya familia
Wazazi wakiwasimamia watoto wao walipokuwa wakishiriki michezo mbalimbali ya watoto.
Watoto wa baadhi ya wafanyakazi wa Mgodi huo wakifurahia michezo mbalimbali wakati walipokuwa wakiadhimisha siku ya familia mgodini hapo
Baadhi ya ndugu wa wafanyakazi wa Mgodi wa Buzwagi wakiangalia aina mbalimbali za mashine zinazotumika katika shughuli za uchimbaji katika mgodi huo.
Moja kati ya magari makubwa kabisa yanayotumika katika mgodi huo likiwa katika eneo la maonyesho.
Kutoka kushoto ni meneja wa uendelezaji wa Mgodi wa Buzwagi George Mkanda, katikati ni Graham Crew-Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu na  Michelle Ash-Afisa Mkuu wa masuala ya uendeshaji wa kampuni ya Acacia wakati wa sherehe za siku ya familia ya Mgodi wa Buzwagi.
Baadhi ya familia za watumishi wa Mgodi wa Buzwagi zikitambulishwa wakati wa hafla hiyo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyekuwa Kahama.

Buzwagi imeanzisha mkakati wa kukuza na kuboresha hali ya utendaji kazi kwa wafanyakazi wake kwa kuanzisha utaratibu wa kuwakutanisha wafanyakazi wa mgodi huo na familia zao mara moja kwa mwaka katika siku maalumu ya familia ambayo hutoa fursa kwa familia za wafanyakazi wa mgodi huo kuweza kujionea namna ambavyo shughuli za uchimbaji wa madini hufanyika na hivyo kuwa mabalozi wazuri wa kampuni kwa ujumla.
Mwaka huu wafanyakazi wa kampuni hiyo wamepata fursa ya kukutana na kujionea shughuli mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanyika mgodi hapo. Pamoja na mambo mengine wafanyakazi hao pia walipata fursa ya kutembelea eneo ambapo shughuli za uchimbaji zinafanyika.
Sherehe hizo zilihudhuliwa na Afisa mkuu wa masuala ya uendeshaji  Michelle Ash, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulur-Graham Crew na meneja mkuu wa masuala ya ufanisi wa kampuni Janet Ruben pamoja na meneja mahusiano na mawasiliano wa Acacia Nector Foya, pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali..

WAFANYAKAZI WA MGODI WA BUZWAGI WASHEREHEKEA SIKU YA FAMILIA

$
0
0
Eng.Philbert Rweyemamu akifafanua jambo katika moja ya mabanda ya maonyesho kwa baadhi ya maafisa wa uhamiaji walipokuwa wakitembelea mabanda ya maonyesho.

Michel Ash-Afisa Mkuu wa Masuala ya uendeshaji wa kampuni ya Acacia akizungumza na familia pamoja na wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi
Kikundi hiki cha Ngoma kutoka Shinyanga kilitia fola kwa burudani safi ya Ngoma waliyoitoa.
Baadhi ya maafisa wakuu wa kampuni ya Acacia wakifuatilia burudani ya ngoma
Baadhi ya maafisa wa idara ya ufanisi wa Mgodi wa Buzwagi wakiwa katika picha ya pamoja katika banda lao wakati wa maonyesho
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi mwenye shati la bluu akiongozwa na mkuu wa kitengo cha ulinzi Jamal Rwambol kutembelea mabanda ya maonyesho
Azael Kitange-Mkufunzi wa idara ya ufanisi wa kampuni akitoa maelezo kwa wageni walipotembelea banda la idara ya Ufanisi katika kitengo cha Mafunzo.
Ufugali wa nyuki wa kisasa ni moja kati ya shughuli zinazofanywa na mgodi wa Buzwagi kupitia idara ya Mahusiano ya Jamii kwa kuwawezesha wenyeji wanaozunguka maeneo ya mgodi kujipatia shughuli zinazowaongezea kipato.
Wataalamu wa miamba wakionyesha aina mbalimbali za miamba yenye dhahabu na namna wanavyotumia vifaa vya kisasa kuitafuta dhahabu.
Kikundi cha Ngoma cha kabila la wasukuma kikitoa burudani ya ngoma wakati wa maadhimisho ya siku ya familia kwa wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi
Baadhi ya wanafamilia wa wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi.
Baadhi ya maafisa kutoka Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu wakifurahia moja ya burudani wakati wa sherehe hizo.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Eng. Philbert Rweyemamu (katikati) na Meneja wa Biashara wa Mgodi huo wakifuatilia kwa makini burudani zilizokuwa zikiendelea wakati wa sherehe hizo, kushoto kwao ni mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Kahama.


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyekuwa Kahama

Buzwagi imeanzisha mkakati wa kukuza na kuboresha hali ya utendaji kazi kwa wafanyakazi wake kwa kuanzisha utaratibu wa kuwakutanisha wafanyakazi wa mgodi huo na familia zao mara moja kwa mwaka katika siku maalumu ya familia ambayo hutoa fursa kwa familia za wafanyakazi wa mgodi huo kuweza kujionea namna ambavyo shughuli za uchimbaji wa madini hufanyika na hivyo kuwa mabalozi wazuri wa kampuni kwa ujumla.
Mwaka huu wafanyakazi wa kampuni hiyo wamepata fursa ya kukutana na kujionea shughuli mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanyika mgodi hapo. Pamoja na mambo mengine wafanyakazi hao pia walipata fursa ya kutembelea eneo ambapo shughuli za uchimbaji zinafanyika.
Sherehe hizo zilihudhuliwa na Afisa mkuu wa masuala ya uendeshaji  Michelle Ash, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulur-Graham Crew na meneja mkuu wa masuala ya ufanisi wa kampuni Janet Ruben pamoja na meneja mahusiano na mawasiliano wa Acacia Nector Foya, pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali..

MAKAMU WA RAIS AWAONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA WAZIRI CELINA KOMBANI

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwasilisha salamu za Pole za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wa kuuaga Mwili wa Marehemu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Marehemu Celina Ompeshi Kombani Karimjee Jijini Dar es salaam. (Picha na Othman Khamis Ame, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar)
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Uratibu na Bunge, , Jenister Muhagama akitioa salama za Serikali wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, marehemu Celina Kambani. (Picha na Francis Dande)
 Baadhi ya wabunge wakiwa viwanja vya Karimjee katika kuaga mwili wa aliyekuwa  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, marehemu Celina Kambani.
 Mama Maria Nyerere akiwasili katika viwanja vya Karimjee.
 Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na mama Maria Nyerere. 
Makamu wa Rais (katikati) akiwa na viongozi wa Serikali.
Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili katika viwanja vya Karimje Dar es Salaam.
Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Blozi Seif Ally Idd akitoa heshima za mwisho.
Mke wa Rais mama Salma Kikwete akitoa heshima za mwisho.
Spika wa Bunge Anne Makinda akitoa heshima za mwisho.
Mama Maria Nyerere akitoa heshima za mwisho.

Baadhi ya ndugu na jamaa wakiwa huzuni.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx



Mwili wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celine Ompesh Kombani aliyefariki Dunia Alhamisi iliyopita katika Hospitali ya  Andra Prash Apolo ya Nchini India umeagwa rasmi kwa Heshima zote za Kiserikali.

Marehemu Waziri Celine Ompesh Kombani  alianza kuumwa Tarehe 26 Agosti mwaka huu ambapo Tarehe Mosi Septemba alipelekwa Nchini India kwa matibabu zaidi na kugundulika kuwa  na maradhi ya Saratani ya Kongosho iliyoathjiri ini lake.

Heshima ya kuuaga rasmi Kiserikali Mwili wa Marehemu Celine  ulioletwa kutoka Nchini India Juzi Mchana na kupokelewa na Viongozi mbali mbali wa Serikali, Vyama vya Siasa, marafiki na wana familia zilifanyika katika viwanja vya Karimejee Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Moh’d  Gharib Bilal aliuongoza Umma wa Watanzania katika kuuaga mwili wa Marehemu Celine  Ompesh Kombani  ambao baadaye utapelekwa  shambani kwake Lukole Jimboni Ulanga Mkoani Morogoro kwa Mazishi.

Kwa Upande wa Zanzibar  maombolezo hayo yaliongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyeambatana pia na baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Wabunge, Wawakilishi  pamoja na Wanasiasa.

Mh. Celina Ompesh Kombani alizaliwa Tarehe 19 Juni Mwaka 1959 katika Kijiji cha Kisewe Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro akiwa Mtoto wa Pili miongoni mwa  Watoto 16 wa Mzee Ompesh  Kombani.

Alianza kupata elimu yake ya Msingi kuanzia mwaka 1968 hadi mwaka 1974 katika Skuli ya Kwiro Mahenge na baadaye kuendelea na elimu ya Sekondari kuanzia mwaka 1975 hadi 1978 kwenye skuli ya Sekondari ya Kilakala Mkoani Morogoro.

Marehhemu Celine Ompesh Kombani aliendelea na masomo ya Kidato cha Tano hadi cha sita katika Shule ya Sekondari ya wasichana Tabora akiunganisha na Elimu ya juu katika chuo cha Uongozi  wa fedha cha IDM Mzumbe na kupata Stashahada ya Uongozi na Utawala na baadaye Shahada ya Juu ya Uzamili katika Chuo hicho cha Uongozi wa Fedha IDM Mzumbe.

Mwaka 1985 Marehemu Celine Ompesh Kombani aliajiriwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro  akiwa Afisa Utumishi  nafasi iliyomuwezesha kupanda Madaraka na kuteuliwa kuwa Meneja wa Rasilimali Watu katika Kiwanda kilichopo Morogoro.

Katika uhai wake Marehemu Celine aliwahi kuwa Afisa Utawala wa Chuo cha Kilimo Morogoro, Kiongozi wa Halaiki ya Vijana wa Chipukizi wa Chama cha TANU, Mwenyekiti wa Tawi la CCM Kilosa pamoja na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Morogoro.

Katika nyanja ya Kisiasa Marehemu Celine Ompesh Kombani alikuwa Mbunge wa Jimbo la Ulanga kwa vipindi viwili mfululizo kuanzia mwaka 2005 hadi 2015 nafasi iliyomuwezesha kuteuliwa kushika nyadhifa mbali mbali za juu za Uongozi Serikalini.

Marehemu Celine aliwahi kuwa Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa Katiba na Sheria   pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma nafasi aliyodumu nayo hadi kufariki kwake.

Wakitoa salamu za maombolezo ya Makundi mbali mbali, Wawakilishi wa Makundi hayo ikiwemo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Bunge la Jamuhuri ya Muungano  wa Tanzania, Taasisi za Kijamii walimuelezea Marehemu Celine Ompesh Kombani kuwa alikuwa Mtu wa Watu.

Walisema Marehemu Celine alikuwa Kiongozi mahiri aliyekubali na kuridhia kuwa karibu na Taasisi na Watu wa makundi ya aina yote bila ya kujali itikadi, jinsia au Dini ya mtu.
Mapema akiongoza sala maalum ya kumuombea safari njema Marehemu Celine Ompesh Kombani Mchungaji Wilfred Mmary alisema Muungu muweza na asili ya kila kitu amekausha  pumzi ya Mpendwa Celine akifanya hivyo bila kosa bali  ni kutekeleza utukufu wake kwa viumbe vilivyo chini ya himaya yake.
Mbele ninaendelea nnazidi kutembea. Maombi uyasikie. Bwana umpambe. Ebwana  uniinue ili nipande milima yote.  Ni shairi alilolikariri mchungaji Wilfred ambalo alisema lilikuwa likiimbwa  na kumjumuisha Pia Marehemu Celine  wakati wa Ibada zao za misa.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania { NEC } kupitia Mkurugenzi wake Bwana Kailina Ramadhan imeahirisha uchaguzi wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro kufuatia Kifo cha Waziri Celine  Ompesh Kombani aliyekuwa miongoni mwa wagombea nafasi ya Ubunge  wa Jimbo la Ulanga kupitia chama Tawala Cha CCM.
Marehemu Waziri Celina Ompesh Kombani ameacha Mume, Watoto Watano pamoja na Wajukuu Wanne. Muungu iweke roho ya Marehemu Celine  Ompesh Kombani mahali anapostahiki kwa mujibu wa amali yake. Amin.


Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
28/9/2015.

MAGUFULI CLUB YAZINDULIWA

$
0
0
 Mratibu wa Kampeni upande wa Vijana CCM kwa Mkoa wa Dar es Salaam na Vyuo Vikuu Bw. Daniel Zenda akizungumza na Zaidi ya Vijana 500 kutoka Jimbo la Mbagala wakati wa uzinduzi wa MAGUFULI Club jijini Dar es Salaam na. MAGUFULI Club imeanzishwa kama jukwaa la kuwakutanisha vijana nchini kote wanaomuunga mkono mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli. Picha na:  Frank Shija
 Mratibu wa MAGUFULI Club wilaya ya Temeke Bw. Peter Dafi akizungumza na vijana kutoka Jimbo la Mbagala wakati wa uzinduzi wa MAGUFULI Club jijini Dar es Salaam jana. MAGUFULI Club imeanzishwa kama jukwaa la kuwakutanisha vijana nchini kote wanaomuunga mkono mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli.
 Baadhi wa vijana wakifuatilia uzinduzi wa MAGUFULI Club katika Jimbo la Mbagala jijin Dar es Salaam.

MISA TANZANIA YASHEREKEA SIKU YA KIMATAIFA YA HAKI YA KUPATA TAARIFA

$
0
0
Mwenyekiti  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege (katikati) akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa chapicho la ripoti ya matumizi bora ya utoaji wa habari katika sekta za umma hapa nchini akisaidiwa na Ofisa Habari Umoja wa Mataifa (UN), Bi. Usia Nkhoma Ledama (kushoto) pamoja na Mwenyekiti msaidi wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Andrew Marawiti (kulia) 
Waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa(hawapo pichani) wakioneshwa kitabu cha ripoti ya haki ya kupata taarifa halali katika sekta za umma kwa mwaka 2015 kilichozinduliwa leo siku ya kupata habari iliyofanyika kwenye ofisi za MISA Tanzania.
 Mwenyekiti wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege akionesha tuzo ya cheti cha kufuri la Dhahabu kwa kubana sana taarifa kwa mwaka 2015 kwa umma iliyokwenda kwenye Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mwenyekiti wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege(kulia) akimkabidhi Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Anthony Ishengoma tuzo ya cheti cha kufuri la Dhahabu kwa wizara hiyo kwa kubana sana taarifa kwa umma mwaka 2015.
   Mwenyekiti wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege(kulia) akimkabidhi tuzo ya cheti cha funguo la Dhahabu walioibuka washindi wa mwaka 2015 Kaimu Mkuu wa Mawasiliano wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya kwa kutoa taarifa kwa uwazi kwa umma.

FAHAMU UGONJWA WA BAWASIRI AU KUOTA KINYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA NA NAMNA YA KUEPUKA NA UGONJWA HUU

$
0
0
FAHAMU UGONJWA WA BAWASIRI AU KUOTA KINYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA NA NAMNA YA KUEPUKA NA UGONJWA HUU(JAMIIMOJABLOG)
~watu wengi wanasumbuliwa na tatizo hili ambalo huwafanya kuwa na uoga na aibu wa kuelezea na kushindwa hata kwenda hospital kupata tiba
JE, UNAJUA BAWASIRI/HEMORRHOIDS NI NINI????!!
~Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na nnje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe
~ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu tunauita HEMORRHOIDS ilhali kwa lugha ya kingereza unafahamika kama piles
~tatizo hili huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50%ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 30_50
AINA ZA BAWASIRI
~Kuna Aina mbili za bawasiri
(A) BAWASIRI YA NDANI
~Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili
~Aina hii hutokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa
~Aina hii imegawanyika katika madaraja manne
(1)DARAJA LA KWANZA ~Hii ni bawasiri ambayo haitoki mahal pale panapohusika
(2)DARAJA LA PILI ~hii hutokea wakati wa haja na kurudi yenyew ndani baada ya kujisaidia
(3)DARAJA LA TATU :hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenywe
(4)DARAJA LA NNE :hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi
(B)BAWASIRI YA NNJE
~Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu Hilo pia husababisha mishipa ya damu (vena) kupasuka na damu kuganda na kasababisha Aina ya bawasiri iitwayo THROMBOSED HEMORRHOIDS
CHANZO CHA TATIZO
~chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijapatikana ila Kuna vitu ambavyo huwa chanzo cha kupata ugonjwa wa bawasiri ambayo ni ÷
👉KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE
👉KUHARISHA KWA MUDA MREFU
👉TATIZO LA KUTOPATA CHOO
👉MATATIZO YA UMRI
👉KUKAA KITAKO KWA MUDA MREFU
👉UZITO KUPITA KIASI
👉MATUMIZI YA VYOO VYA KUKAA KWA MUDA MREFU
DALILI ZA BAWASIRI
👉Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
👉kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia
👉kutokea uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
👉kujitokeza kwa kinyama katika eneo la tundu Hilo
👉kinyesi kuwa na damu na kunuka harufu mbaya sana
MATIBABU NA JINSI YA KUEPUKA TATIZO LA BAWASIRI
~matibabu ya bawasiri hutegemea na Aina ya bawasiri pia tiba iliyozoeleka ni kukatwa kinyama na kuendelea na lishe ya chakula hata hvyo tiba hii si nzuri kwasababu huwa haitibu chanzo cha tatizo hivyo huwa rahisi kujirudia hivyo tiba nzuri ni kutumia dawa na anion chip kubandika mahali penye tatizo na kuondoa tatizo Hilo
~Pamoja na hayo bawasiri ni ugonjwa unaoweza kuepukika kwa kuzingatia
👉KULA MBOGAMBOGA ZA MAJANI, MATUNDA, NA NAFAKA ZSZOKOBOLEWA
👉KUNYWA MAJI MENGI ANGALAU GRASS 6/12 Kwa siku
👉EPUKA KUKAA CHOONI KWA MUDA MREFU
MADHARA YA TATIZO LA BAWASIRI
👉kupata upungufu wa damu (anemia)
👉Kupata tatizo la kutokuweza kuhimil choo
👉hupunguza nguvu za kiume na kuondoa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake
👉kuathirika kisaikolojia
👉kukosa moral ya kufanya Kaz kutokana na maumivu makali
WASILIANA KWA 0717035770 AU 0753692612. KAWAIDA FAHAMU UGONJWA WA BAWASIRI AU KUOTA KINYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA NA NAMNA YA KUEPUKA NA UGONJWA HUU(JAMIIMOJABLOG) ~watu wengi wanasumbuliwa na tatizo hili ambalo huwafanya kuwa na uoga na aibu wa kuelezea na kushindwa hata kwenda hospital kupata tiba JE, UNAJUA BAWASIRI/HEMORRHOIDS NI NINI????!! ~Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na nnje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe ~ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu tunauita HEMORRHOIDS ilhali kwa lugha ya kingereza unafahamika kama piles ~tatizo hili huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50%ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 30_50 AINA ZA BAWASIRI ~Kuna Aina mbili za bawasiri (A) BAWASIRI YA NDANI ~Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili ~Aina hii hutokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa ~Aina hii imegawanyika katika madaraja manne (1)DARAJA LA KWANZA ~Hii ni bawasiri ambayo haitoki mahal pale panapohusika (2)DARAJA LA PILI ~hii hutokea wakati wa haja na kurudi yenyew ndani baada ya kujisaidia (3)DARAJA LA TATU :hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenywe (4)DARAJA LA NNE :hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi (B)BAWASIRI YA NNJE ~Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu Hilo pia husababisha mishipa ya damu (vena) kupasuka na damu kuganda na kasababisha Aina ya bawasiri iitwayo THROMBOSED HEMORRHOIDS CHANZO CHA TATIZO ~chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijapatikana ila Kuna vitu ambavyo huwa chanzo cha kupata ugonjwa wa bawasiri ambayo ni ÷ 👉KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE 👉KUHARISHA KWA MUDA MREFU 👉TATIZO LA KUTOPATA CHOO 👉MATATIZO YA UMRI 👉KUKAA KITAKO KWA MUDA MREFU 👉UZITO KUPITA KIASI 👉MATUMIZI YA VYOO VYA KUKAA KWA MUDA MREFU DALILI ZA BAWASIRI 👉Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa 👉kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia 👉kutokea uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa 👉kujitokeza kwa kinyama katika eneo la tundu Hilo 👉kinyesi kuwa na damu na kunuka harufu mbaya sana MATIBABU NA JINSI YA KUEPUKA TATIZO LA BAWASIRI ~matibabu ya bawasiri hutegemea na Aina ya bawasiri pia tiba iliyozoeleka ni kukatwa kinyama na kuendelea na lishe ya chakula hata hvyo tiba hii si nzuri kwasababu huwa haitibu chanzo cha tatizo hivyo huwa rahisi kujirudia hivyo tiba nzuri ni kutumia dawa na anion chip kubandika mahali penye tatizo na kuondoa tatizo Hilo ~Pamoja na hayo bawasiri ni ugonjwa unaoweza kuepukika kwa kuzingatia 👉KULA MBOGAMBOGA ZA MAJANI, MATUNDA, NA NAFAKA ZSZOKOBOLEWA 👉KUNYWA MAJI MENGI ANGALAU GRASS 6/12 Kwa siku 👉EPUKA KUKAA CHOONI KWA MUDA MREFU MADHARA YA TATIZO LA BAWASIRI 👉kupata upungufu wa damu (anemia) 👉Kupata tatizo la kutokuweza kuhimil choo 👉hupunguza nguvu za kiume na kuondoa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake 👉kuathirika kisaikolojia 👉kukosa moral ya kufanya Kaz kutokana na maumivu makali WASILIANA KWA 0717035770 AU 0753692612

USIKU WA ESTER DIANA NANA, ALIVYOMEREMETA

$
0
0
 Bi Harusi mtarajiwa Ester Diana Nana (kushoto) akigonisha glasi na msimamizi wake, Hellen, wakati wa sherehe ya kuagwa (Send off) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
 Ester akikata keki huku akisaidiana namsaidizi wake
 Bi Harusi mtarajiwa Ester Diana Nana (kushoto) akimlisha keki msimamizi wake, Hellen, wakati wa sherehe ya kuagwa (Send off) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
 Bi Harusi mtarajiwa Ester Diana Nana akimkabidhi keki, Naibu Katibu Mkuu wa Ofoso ya Makamu wa Rais, Bi. Angelina Madete, wakati wa sherehe ya kuagwa (Send off) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
 Mwendesha Shughuli Mc Bazil, akifanya yake katika sherehe hiyo
 Mama Mzazi wa Bi harusi mtarajiwa, akimkabidhi zawadi ya Biblia mwanae Ester
 Wakwe wakiandaa zawadi ya Bi harusi mtarajiwa kabla ya kumkabidhi
 Mc Bazil. akimkabidhi zawadi ya Cd Bi Harusi mtarajiwa ukumbini hapo
 Wakati wa zawadi.....
Bi harusi mtarajiwa akiwa na mumewe mtarajiwa wakielekea kupata chakula cha usiku ukumbini hapo. Watarajiwa hao wanatarajia kufunga ndoa jumamosi ya wiki hii.
Wakati wa mlo wa usiku

MGOMBEA UBUNGE TEMEKE (CCM) MTEMVU AHAIDI NEEMA AKICHAGULIWA TENA

$
0
0
 Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Abbas Mtemvu akizungumza na wananchama na wafuasi wa Chama hicho  Dar es Salaam jana wakati wa mkutano wa Uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi Kata 14 Temeke katika viwanja vya Shule ya Msingi Madenge sambamba na mashina 3 yalizinduliwa. (PICHA NA KHAMISI MUSSA)
  Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Abbas Mtemvu (wa tatu kulia) na Mgombea nafasi ya Udiwani kupitia cha hicho Feisal (wa pili kulia) wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Shina la wakereketwa no, 1. Tawi la Maghorofani na wakwanza kulia ni Mwenyekiti wa Jimbo hilo Amhad Mnamala.
   Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Abbas Mtemvu (wa kwanza kulia) na Mdombea nafasi ya Udiwani kupitia cha hicho Feisal (wa pili kulia) wakipandisha Bendera ya Chama hicho kuashiria uzinduzi wa Shina la wakereketwa no, 1. Tawi la Maghorofani
  Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Abbas Mtemvu akipokea Risala kutoka kwa Katibu wa Shina hilo Zuzana Manamba
 Shamra shamra za uzinduzi wa Kampeni kata ya 14 viwanja vya Shule ya Msingi Madenge Temeke.

MAELFU WAMLAKI EDWARD LOWASSA BUMBULI-TANGA

$
0
0
Wananchi wa Mji wa Soni katika Jimbo la Bumbuli, wakimlaki kwa shangwe Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Kisiwani, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo.
 Lowassa akiwasili Bumbuli.
 Lowassa akihutubia mkutano wa kampeni jimbo la Bumbuli leo.
Umati wa Wananchi wa Mji wa Soni katika Jimbo la Bumbuli, wakisikiliza sera za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, wakati Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Kisiwani, leo Septemba 28, 2015.

WASANII WA BONGO MOVIE WAIBUKIA MJINI IRINGA,WATANGAZA KUTEMBEA NCHI NZIMA KWA BAJAJ KUMUUNGA MKONO DKT MAGUFULI

$
0
0
Baadhi ya Wasanii nyota wa Filamu hapa nchini wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB wakiwa wamenyanyua juu mikono yao kwa pamoja ni Ushindi sambamba na Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli (wa tatu kushoto),kuonesha kuwa wasanii hao wanamuunga mkono Dkt Magufuli katika mbio zake za kuusaka Urais kwa kutembea nchi nzima kutumia Bajaji zao tano,ambapo Bajaj mojawapo itakuwa na kazi ya kukusanya kadi za wale wanaomua kurudi/kujiunga na chama cha CCM.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-IRINGA
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wananchi wa Iringa na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo septemba 28 ndani ya uwanja wa Samora mkoani Iringa.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wananchi wa Iringa na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo septemba 28 ndani ya uwanja wa Samora mkoani Iringa.

  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiwaeleza wananchi sababu zilizosababisha CCM kutomteua Lowasa kuwa mgombea urais kupitia CCM hasa kutokana na hasa kile kilichoelezwa kuwa na kadhia ya ufisadi ya rushwa,mbapo pia Nape amewaomba Wananchi kumuombea afya Mgombea huyo wa Urais kupitia Chadema, ili aje ashuhudie CCM ikishinda  nafasi ya Urais.
  Wananchi wa Iringa na vitongoji vyake wakishangilia wakati Dkt Magufuli alipokuwa akiwaomba wampigie kura ya ndio itakapofika Oktoba 25,mwaka huu (ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika )ili aweze kuibuka mshindi na kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano
 Dkt Magufuli akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mgombea ubunge Jimbo la Iringa mjini, Ndugu Frederick Mwakalebela wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja samora mjini Iringa.
 Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kazini kwenye mkutano wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,jioni ya leo kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa.
 Magufulika staili kama kawa,hata baadhi ya wasanii nyota wa Bongo Movie hapa nchini wakiongozwa na Nnape Nnauye (pili shoto) walikumbwa na zoezi hilo jioni ya leo mbele ya wakazi wa Iringa na vitongoji vyake waliokuwa wamefurika kwenye mkutano wa kampeni ndani ya uwanja wa Samora,zoezi hilo kwa sasa limeanza kujizolea umaarufu mkubwa hapa nchini,la kupiga push up kama ionekanavyo pichani.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Kilolo Ndugu Venance Mwamoto,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Ilula,mkoani Iringa.
  Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Ndugu Godfrey Mgimwa wakati wa mkutano wa kampeni katika Mji wa Ifunda
 Vimbwanga vya hapa na pale vilikuwepo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Ifunda mapema leo mchana
wazee wa kimila wa kabila la Wahehe wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Dkt Magufuli uliofanyika mapema leo mchana katika Mji wa Ilula Jimbo la Kilolo mkoani Iringa.
  Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM, William Lukuvi akitangaza wasifu wa mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja Samora mjini Iringa.
 Wananchi wakiwa wamefurika ndani ya Uwanja wa Samora wakisikiliza sera za Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo.
 Wananchi wa Iringa na vitongoji vyake wakifuatilia mkutano wa kampeni,wakati Dkt Magufuli alipokuwa akiwaomba wampigie kura ya ndio itakapofika Oktoba 25,mwaka huu (ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika )ili aweze kuibuka mshindi na kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano

WANANCHI WAFUNGA BARABARA - LOWASSA KAMPENI

$
0
0
 Mgombea Urais wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Muheza Mkoani Tanga, waliofunga barabara ili azungumze nao leo Septemba 29, 2015, wakati akiwa safarini kwa kuelekea Dar es salaam kwa njia ya barabara akitokea Mkoani Tanga. Picha na Othman Michuzi.


 Mgombea Urais wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwapungia wananchi wa Mji wa Muheza Mkoani Tanga, mara baada ya kuzungumza nao, wakati akiwa safarini kwa kuelekea Dar es salaam kwa njia ya barabara akitokea Mkoani Tanga. Picha na Othman Michuzi.
  Mgombea Urais wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwapungia wananchi wa Mji wa Muheza Mkoani Tanga, mara baada ya kuzungumza nao, wakati akiwa safarini kwa kuelekea Dar es salaam kwa njia ya barabara akitokea Mkoani Tanga. Picha na Othman Michuzi.
  Mgombea Urais wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwapungia wananchi wa Mji wa Muheza Mkoani Tanga, mara baada ya kuzungumza nao, wakati akiwa safarini kwa kuelekea Dar es salaam kwa njia ya barabara akitokea Mkoani Tanga. Picha na Othman Michuzi.

BENKI YA CRDB YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA NA KUTOA VIFAA TIBA KWA MANISPAA YA KONONDONI

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja uliofanyika jijini Dar es Salaam na kukabidhi vifaa tiba kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wa kipindupindu katika Manispaa ya Kinondoni.(Picha na Francis Dande).
 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja uliofanyika Dar es Salaam.
Baadhi ya Mameneja na Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akikabidhi msaada wa vifaa tiba kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty, kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wa kipundupindu, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Dk. Aziz Msuya na kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB anayeshughulikia Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyopadhayay. (Picha na Francis Dande).
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akikabidhi msaada wa vifaa tiba kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty, kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wa kipundupindu, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Dk. Aziz Msuya na wa pili kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB anayeshughulikia Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyopadhayay. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akikabidhi msaada wa vifaa tiba kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty, kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wa kipundupindu, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB anayeshughulikia Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyopadhayay na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Dk. Aziz Msuya.
 Maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja
 Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB
 Vifaa tiba vilivyokabidhiwa leo.


  Na Mwandishi Wetu

BENKI ya CRDB imekabidhi dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya sh. milioni 15 kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wa kipindupindu katika Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja.

Msaada huo ulitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Injinia Mussa Natty aliyeishukuru benki hiyo na kukiri kwamba kipindupindu kipo katika manispaa yake.

Akizungumza baada ya kupokea dawa na vifaa tiba hivyo, injini Natty alisema mpaka sasa ugonjwa huo umepoteza maisha ya watu 17 katika manispaa hiyo huku wengine 1194 wameugua kipindupindu. 

“Kata zote 34 za manispaa ya Kinondoni zimeathirika na kipindupindu kilichoanzia Mwananyamala Agost 15 mwaka huu kata nyingine zenye ugonjwa huo ni Mburahati, Kigogo, Sinza, Mabibo, Magomeni, Kimara na Manzese.

"Mpaka sasa kambini kuna wagonjwa 25 nawashauri watanzania waache kusalimiana kwa kushikana mikono sababu ugonjwa huu unaendezwa kwa uchafu,” alisema injinia Natty.

Dk. Kimei alisema wiki ya huduma kwa wateja huadhimishwa kila mwaka na benki hiyo viongozi wa CRDB kutoa huduma kwenye matawi mbalimbali huku akieleza kwamba kaulimbiu ya mwaka huu ni Asanteni Sana.

“Wateja wetu ndio jambo la kila jema linalotokea kwetu… tunaitumia wiki hii kufungua milango na kusogea karibu zaidi na wateja ili kusikiliza maoni, mahitaji na ushauri wao, lengo ni kuwahudumia kwa ubora zaidi,” alisema Dk. Kimei.
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>