Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

MADEE: TEMA MATE TUWACHAPE UJUMBE KWA WASIONIKUBALI

$
0
0

Na Elizabeth John


KIONGOZI wa kundi la Tip Top Connection, Ahmed Ally ‘Madee’ amesema wimbo wake wa ‘Tema Mate Tuwachape’ umetumika kufikisha ujumbe kwa wasanii ambao hawamkubali katika kazi zake.

Wimbo huo ni kati ya nyimbo ambazo zinafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio kutokana na ubora wa mashairi yaliyopo ndani yake licha ya jina la wimbo kuacha maswali kwa wapenzi wa muziki huo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Madee alisema wimbo hauna mafunzo yoyote katika jamii ila ni kufurahisha tu mashabiki wa kazi zake pia ametumia nafasi hiyo kutoa ujumbe kwa watu ambao hawapendi maendeleo ya wenzao katika jamii nzima.

“Binadamu wengi hatupendani, huu wimbo ni kwaajili ya watu ambao hawapendi maendeleo ya wenzao na nimeamua kuuita hivi kutokana na kwamba nawachapa wale ambao hawapendi maendeleo ya wenzao hivi huwezi kuuelewa ila unaposikia lazima uelewe,” alisema.

Alisema video ya wimbo huo anaizindua Jumapili katika ukumbi wa kimataifa wa Club Bilicanas, akiwa na wasanii kama Chege na Shilole anaomba sapoti kwa mashabiki wa muziki huo waje washuhudie watu wanavyochapwa.


“Video ya wimbo huo nimefanyia nchini Kenya, katika kampuni ya Ogopa video chini ya mtayarishaji mahiri Adam Juma, hii ni kazi yangu ya kwanza kufanyia nchini humo naimani itafanya vizuri kutokana na umahiri wa mtayarishaji huyo,” alisema Madee. 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>