
Na Elizabeth John
MWANADADA anayetamba katika tasnia ya filamu nchini, Wema Sepetu, amesema amechukizwa na kitendo cha waandishi kuandika habari za kumchafua bila kufanya mahojiano naye.
Akiandika katika ukurasa wake wa Instergram, Wem alisema anachukizwa sana na kitendo hicho kwani kinamfanya asikae kwa amani na watu waliokaribu yake na wengine wanamtenga kupitia vichwa vya habari tofauti vya magazeti hayo ambayo kwaasilia kubwa anasema vinatumika kuuzia magazeti hayo.
“Hivi karibuni kuna gazeti moja limeandika, ‘Ishu ya dawa za kulevya-Wema kunyongwa China, aomba Watanzania kumuombea’, jamani siwezi kusema kama nina furaha, sijawahi kufikiria kwamba magazeti yetu ipo siku yatakuja kuandika uongo wa namna hii kwasababu nakaaga kimya ndio wameonda ni njia ya kunionea muda wote, roho inaniuma sana,” aliandika mwanadada huyo ambaye amewahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2006.
Wema alifafanua kuwa, kutokana na kuona hapa nchini kuna maneno mengi yasiyokuwa ya msingi, aliamua kwenda China kwaajili ya kufanya mambo yake binafsi lakini watu ambao hawapendi maendeleo yake wamekuwa wakimfuatiliana na kuamua kumchafua katika magazeti.
“Sidhani kama nishawahi kumkosea yeyote katika maisha yangu, maskini ya Mungu naishi maisha yangu mwenyewe sina habari na mtu sijawahi hata kufikiria kufanya biashara kama hii, muda uliopita niliambiwa nina pepo la ngono, leo nina lia tena kwakuambiwa nauza madawa ya kulevya, eeee mungu nisaidie mimi,” aliongeza Wema.